Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109572 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA KRISMAS MKOANI DODOMA KUFANYIKA LEO UWANJA WA JAMHURI

0
0
 Mratibu wa Tamasha la Krismas Mkoani Dodoma, John Banda akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri,Mkoani Dodoma, Kushoto ni Mmoja wa waimbaji kwenye tamasha hilo Beatrice Wiliam (BSS 2011) Maandalizi ya Tamasha la Chrismas ndani ya Dodoma Tayari yamekamilika wasanii kibao tayali wapo Dodoma na Asubuhi ya leo wameshiriki ibada ya pamoja katika kanisa la Mlima wa moto Sabasaba Dodoma.
 Josephine Sudai akionyesha uwezo wake wa kuimba ndani ya kanisa la mlima wa moto Dodoma kabla ya kuelekea uwanja wa Jamhuri kwenye tamasha hilo.
 Jubilee Lugobo toka jijini Dar es salaam nae yupo Dodoma kwa ajili ya tamasha hilo
  Lusekelo Mwandiga akiimba kwa mbwembwe ndani ya kanisa la mlima wa moto sabasaba Dodoma kabla ya kushiriki tamasha hilo
Mwanadada Rose Kimaro ndani ya tamasha hilo na hapa ni mlima wa moto sabasaba.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CCM DMV KUJIUZULU KWA KATIBU MKUU, JACOB KINYEMI

VODACOM INAKUKARIBISHA COCO BEACH MUDA HUU

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Huawei wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika baadhi ya simu zinazouzwa na kampuni hiyo katika Tamasha linalofanyika katika fukwe za Coco jijini Dar. Simu ambazo zinauzwa katika Tamasha hilo ni pamoja na Huawei Y210D, inayouzwa kwa Tsh. 162,000, Huawei W1 inayouzwa kwa 360,000, Huawei G510, 350,000 , Huawei Ascend W1 360,000, Simu nyingine zenye ofa ya GB 5 za internet ni Huawei Ascend P6 inayouzwa 800,000 na Huawei Ascend Mate kwa shilingi 900,000.
Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya, Bariki Makombe aka Black B akitoa burdani kwa mashabiki wa muziki huo waliojitokeza katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam. Vodacom na Huawei watatoa burudani kwa wakazi wa dar kwa siku mbili za tarehe 25 na 26 pamoja na kuuza simu na bidhaa nyingine.

LUKUVI AWATAKA WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA AMANI,UTULIVU NA UPENDO.

0
0
 
 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akizungumza mbele ya watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.Lukuvi amewataka watazamaji na washabiki wa tamasha hilo  na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa amani,upendo na utulivu,ameongeza kuwa pia Serikali itahakikisha usalama upo na wa kutosha kwa watu wake,pichani kati ni Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha hilo Bwa.Alex Msama.
 Mmoja wa wageni waalikwa katika tamasha la Krisimasi,Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pichani kati akiwatakia heri na fanaka Watazamaji na Watazania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya. 
 Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) wakati wa tamasha la krisimasi likiendelea jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini Dar.

 Baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka kikundi cha Living Waters wakitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.
 Pichani shoto ni Mwimbaji nyota wa muziki wa injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima,wakishambulia kwa namna ya pekee kabisa,huku miluzi na shangwe za watazamaji zikivuma kila kona ya uwanja,jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi.
 Rose Muhando akiimba wimbo wake wa Utamu kwa Yesu mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambako tamasha la Krisimasi likiendelea jioni ya leo.

 Baadi ya Waimbaji wa kundi la Glorious wakiimba jukwaani
Mwimbaji wa nyimbo za injili,Boni Mwaitege pichani kati na madansa wake wakiwaimbisha mashabiki wao jioni ya leo.
 Sehemu ya umati wa Watu wakifuatilia tamasha la Krismasi,linalofanyika jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,ambalo limejumuisha wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya 'Love Come Down' ya Evelyn Champagne King ilitamba

Mwimbaji nyota wa Injili kutoka Afrika kusini,solly Mahlangu afanya kweli tamasha la krismass uwanja wa Taifa jijini Dar

MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA

0
0
 
 Mtangazaji wa kipindi cha mboni show Mboni Masimba akimkabidhi zawadi mtoto yatima Ally Mustapha baada ya kuimba vizuri katika mlo uliandaliwa na Mboni katika ukumbi wa Highland hall
 baadhi ya watoto yatima wakiwa katika ukumbi wa highland hall  na mc wa shughuli hiyo Mc Zipompampa akiwa na mtoto Ally Mustapha. (Picha Zote na Denis Mlowe).
 Wageni rasmi katika hafla maalum ya mlo wa pamoja uliondaliwa na kipindi cha Mboni Show, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi (kulia), Mboni Masimba katikati akiwa na mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Asas Abri, mgeni kutoka Nigeria.

=======  ======  =======
MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA

Na Denis Mlowe,Iringa.

MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV,Mboni Masimba leo amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.

Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa Moyo.

Hafla  hiyo  ya  kula  chakula cha mchana na yatima  imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..

Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha  kipindi chake cha Mboni Show  kwaa kujumuika na watoto hao.
.

MWANAFUNZI WA CBE-DODOMA AFARIKI DUNIA.

0
0
MAREHEMU  SAMWEL P. KITULA

Ikiwa ni siku moja  imepita Tangu Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma  kiondokewe na aliye wahi kuwa Mwanafunzi wa Chuo hicho katika Level ya Diploma 2012/2013 Marehemu Zeinabu J. Kasenga (ODMK -2012/2013)

Simanzi zimezidi kutanda Chuoni  hapa baada  ya Mwanafunzi Mwingine  Bw. Samwel P. Kitula (37)  aliyekuwa  akisoma  Bachelor Degree  in  Procurement and Supplies Management  mwaka wa tatu (3) mkondo  "A"  Kufariki Dunia usiku wa  kuamkia Tarehe 26/12/2013  ( Mnamo saa 8 usiku)  katika hospitali ya  Mkoa wa Dodoma (General Hospital).

Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia   amesema  Marehemu   alikuwa akisumbuliwa na Matatizo  ya Ini mpaka kupelekea Mauti yake.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi  wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma Mhe. Remidius  M. Emmanuel  amesema  amepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa sana  na kuwataka wanafunzi wote kuwa wavumilivu  hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza  mwanafunzi mwenzetu. 
Rais huyo amewataka  wanafunzi  kuwa  watulivu  wakati taratibu mbalimbali  zinaendelea  na kila kitakachoendelea watafahamishwa  kupitia taratibu  mbalimbali za  mawasiliano hapa chuoni.
Amasema Marehemu amekuwa akiishi na familia yake eneo la Makole  karibu kabisa na Lodge ya ELGON, na amemtaka  kila mtu kwa nafasi yake kujongea  eneo hilo kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu.

news alert: Nyumba yateketea kwa moto mkoani Lindi

0
0
Nyumba ya moja mali ya Mzee Nampembe,Mkoani Lindi. imeteketea kwa moto jana Usiku na kupelekea baadhi ya mali zilizokuwemo ndani ya nyumba huyo kushindwa kuokolewa. Hali hiyo ilipekekea Wananchi wa eneo la jirani na nyumba hiyo kupiga mawe gari la zimamoto baada ya kuchelewa kufika eneo la Tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.
Mmoja kati ya wakazi wa nyumba hiyo amepoteza fahamu toka jana baada ya kupatwa na Mshituko. Chanzo cha Moto imeelezwa kuwa ni Mshumaa baada ya kukosekana Umeme mjini Lindi usiku wa jana.
Picha na Abdulaziz Video, Lindi
Wasamalia waliokuwepo eneo la tukio wakisaidiana kumbeba mtu mmoja aliepoteza fahamu baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Vilio vilitawala wakazi wa nyumba hiyo baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Sehemu ya mali zilizookolewa.

MOHAMED MATUMLA AMGALAGAZA NASSIBU RAMADHANI KWA POINT NA KUIBUKA NA BODABODA

0
0
Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akimwadhibu Bondia Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika usiku wa sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9. Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda hiyo.
Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akipambana na Bondia Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9.
Kwa upande wa Masumbwi ya kina Dada,Bondia Lulu Kayage (kushoto) akipambana na Bondia mwenzake Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas.Bondia Lulu Kayage alishinda kwa KO.
Bondia Hamis Ajari (kushoto) akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya krismas.Cheka alishinda kwa point.
Baadhi ya mashabiki waliouhulia mpambano huo uliokuwa mkali na wakuvutia.Picha na Super D Blog.

NEWS ALERT: POLISI MKOANI MOROGORO WAKAMATA GARI LENYE MAITI YENYE MADAWA YA KULEVYA

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefari ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari  hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar.

Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Mwili huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.

Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala.

Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.

Salaams from the Eastern Africa Diaspora Business Council

0
0
The team at the Eastern Africa Diaspora Business Council (EADBC) wishes you peace, joy and prosperity throughout the coming year.
Thank you for your continued support and partnership. As we look back upon the past year, we would like to acknowledge you for helping us shape our organization and business. Thanks for a great year, and wewish you all the best as you embark on 2014.
We look forward to working with you in the years to come.

Article 13

Yaliyojiri wakati wa ziara ya Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi Katika Jimbo la California

0
0
 Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Khadija Mwinyi wakifurahia mashada ya  maua wanayopewa baada ya kuwasili California.
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi katika picha ya pamoja na wadhamini wa sherehe za uhuru California zilizofanyika katika Jiji la Oakland.
 Rais Mstaafu akipeana mikono  na Meya wa Jiji la Vallejo Bw Osby Davis
  Rais Mstaafu katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jiji la Vallejo
Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mama Khadija Mwinyi katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika chuo kikuu cha Berkeley CA, kulia chini ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

TAARIFA KUTOKA TFF LEO Desemba 26, 2013


zahir ally zorro bado anadai

0
0

Gwiji la muziki nchini Zahir Ally Zorro akitumbuiza solo katika sikukuu ya Christmas hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam, ikiwa ni special request ya Ankal.

wadau wa michezo watoa vifaa vya michezo kunogesha sherehe za miaka 50 ya mapinduzi

0
0
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mhe. Mohamed Raza kusaidia mashindano ya Kombaini  za wanafunzi wa Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons Mhe Mohamed Raza  akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kutumika katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya mashindano ya kombe la Mapinduzi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA




WENGI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA

0
0
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. 
 Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kulia) akimfariji mdogo wa marehemu, Benny Kisaka, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MBUNGE FILIKUNJOMBE ATIMIZA AHADI ZAKE KWA KANISA LA ANGLIKANA ILELA LUDEWA

0
0
Mbunge  Deo Filikunjombe  akitoa  neno
Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa  Juma  Madaha  kulia akiwa na mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kati  na mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa Bw  Kolimba  wakati  wa ibada ya Krismas jana
 Mchungaji  wa kanisa  la Anglikana  mtaa wa Ilela  Canon Ngoye  akikabidhiwa  kinada na  mbunge Deo Filikunjombe
 Mchungaji  Ngoye  akikabidhiwa  saruji mifuko  20 kutoka kwa  mbunge  Deo Filikunjombe  wakati wa ibada ya Krismas.
Kwa habari kamili na picha na Francis Godwin

MUENDELEZO WA TAMASHA LA KRISMASI LAFANYIKA MKOANI MOROGORO LEO.

0
0
 Mmoja ya Waimbaji machachari katika anga ya muziki kiroho a.k.a Injili,Bone Mwaitege akionesha umahiri wake wa kucheza,na madansa wake kwenye uwanja wa Jamuhuri,mkoani Morogoro mapema leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krismasi,ambapo hapo jana limezinduliwa rasmi jijini Dar katika uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watu kibao.
 Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu,Upendo Kilahiro akiwaimbisha sehemu ya wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwenye muendelezo wa tamasha la krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja
wa jamuhuri mkoani Morogoro.

 Madansa wa mwimbaji nyota wa muziki wa Injili hapa nchini,Rose Muhando wakiwajibika vilivyo. 
 Sehemu ya mashabiki wakishangilia.
 Mwimbaji wa injili kutoka nchini Zambia,Eprahim Sekereti akiimba sambamba na kundi la Victoria singers,ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro jioni ya leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Krisimasi.
 Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za kiroho kutoka mkoani Morogoro,Tumaini Njole akiimba huku akiwa katika staili ya kipekee kabisa,huku mayowe na shangwe zikisikika kutoka kwa mashabiki.
Viewing all 109572 articles
Browse latest View live




Latest Images