Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TANESCO YAMKUMBUKA KIJANA ANAYEPUMULIA MASHINE YA OXYGEN NA GESI

$
0
0

Meneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo (katika) na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji.walimpotembelea Hamad Awadh nyumbani kwake Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam. Hamad kwa sasa anapumua kwa kutumia Mashine ya Oxygen na Gesi anahitaji Msaada kupatiwa matibabu nchini India.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limetoa msaada wa kiasi cha fedha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya matibabu na Mita (Luku) yenye umeme wa miezi sita sawa na Tsh Milioni Moja na Nusu kwa Kijana Hamad Awadh anayesumbuliwa na tatizo kupumua.

Akizungumza baada yakumtembelea Hamad nyumbani kwake, Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji amesema kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Tito Mwinuka wameguswa na hali ya Hamad yakupumulia Oxygen.

Leila amesema kutokana na matumizi makubwa ya Umeme kwa Mashine yake anayotumia kwa ajili yakupumua, wameona wamsaidie Mita ya peke yake, tofauti na wapangaji wenzake anaoishi nao nyumba moja.

‘’Hamad ni Mtanzania mwenzetu ambaye alikuwa na shughuli zake anafanya kama kawaida, lakini kutokana na maradhi yanayomsumbua ameshindwa kuendelea na kazi zake, Sisi kama TANESCO tumeliona hili hatuwezi kumuona Mtanzania mwenzetu anateseka hivi’’, amesema Leila.

Naye, Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo amesema Shirika hilo limeguswa na hali hiyo ndio maana linamsadia kwa hali na mali, Hamad Awadh.

‘’Rais wetu anasisitiza Watanzania tuwe Wazalendo, sisi kama TANESCO tuemona tulibebe hili la Hamad kama Watanzania ili tumsaidie’’, amesema Mhandisi Sotco.

Hamad Awadh ambaye kwa sasa anataka msaada kwa ajili yakupatiwa matibabu nchini India, ameshukuru kwa msaada huo kutoka TANESCO, amesema kwa sasa maisha yake ni umeme na endapo utakatika basi huwa anatumia Gesi, ameshukuru Hospitali ya Mloganzila kwa huduma walizompatia mpaka kufikia hatua hiyo.

‘’Nasema kila siku moyoni mwangu, hata siku nikidondoka Mloganzila Hospital wamenifanyia kitu kama Mtoto wao, naishukuru pia Serikali kwa huduma zake, naomba sio ninyi tu (TANESCO) na wengine wakisikia kilio changu basi naomba msaada wao'', ameeleza Hamad.

Kwa upande wake Abdul Athumani, Mjomba wa Hamad amesema changamoto kubwa kwa Hamad ni Umeme kutokana na kutumua Oxygen inayotumia zaidi umeme, amesema gaharama nyingine ni Gesi wanayotumia kwa Mgonjwa huyo inayonunuliwa Elfu 45 kila mwezi hivyo wanaomba msaada.

Ugojgwa wa Hamad Awadh ulianza mwaka mmoja na nusu uliopita baada yakupata homa ambapo ilipelekea kupelekwa Hospitali ya Amana, Ilala baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo ilibainika Mapafu yake yamesinyaa na Moyo wake umehama kutoka kulia na kwenda kushoto.

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya Maendeleo

$
0
0
VIJANA wa wilaya ya Kinondoni wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya fedha zinazotengwa kwa ajili yao ili wajiajiri kwa kuanzisha na kuendeleza biashara za ujasiriamali waondokane na umaskini.

Akizungumza katika semina ya siku mbili ya Ujasiriamali iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana kutoka kata tatu za Makumbusho, Kijitonyama na Mwananyamala, Afisa Maendeleo ya Jamii na Vijana kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi Halima Chodry Kahema amesema vijana wengi wanakuwa wanaoga kuomba mikopo hiyo inayotolewa kwa masharti nafuu.

Vijana wa kiume ndio wanaokwepa zaidi mikopo hiyo, ukilinganisha wa wasichana, imeelezwa.

“Halmashauri inatenga sehemu ya mapato yake kwa ajili ya kuwakopesha vijana ili wajiajiri waondokane na umaskini,”

“Lakini, kuna kipindi fedha hizi huwa zinabaki kwa sababu ni vijana wachache wanajitokeza,” amesema Kahema, huku akiongeza kuwa kuna vijana, licha ya kuchukua mikopo, wanakuwa hawana nidhamu ya pesa wanayokopeshwa, huku akiwashauri kupata mafunzo ya ujasiriamali ili kutimiza malengo yao ya biashara.

Ameishukuru asasi ya Pakacha Group, iliyoandaa semina hiyo kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society, akisema wanaisaidia serikali kwa kuendana na falsafa ya mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli ya kuwataka vijana wawezeshwe kiuchumi.

Muwezeshaji Andrew Michael Mwaselela kutoka katika taasisi ya Fursa Connect Initiative amesema vijana wengi, hasa wale wasomi kutoka vyuoni ndio wanakuwa waoga zaidi, wakiamini wanahitaji mtaji mkubwa kuanzisha biashara, badala ya kuifanyia kazi ile dhana ya ujasiriamali inayosema ‘Fikiri zaidi, Anza kidogo’.

Amesema ujasiriamali una faida nyingi, kama vile kuendeleza uchumi binafsi, uchumi wa familia na uchumi wa nchi.

Ameongeza ili mtu awe mjasiriamali mzuri, inabidi aangalie fursa za kibiashara, awe na mtaji (kutunza na kukuza), awe mbunifu, awe na mawasiliano na wateja na kutoa huduma bora kwa wateja wapya na wale wa zamani.

Katibu wa Pakacha Group, Haroun Jongo amesema wanategemea kuandaa semina kama hizo katika siku za usoni ili kufungua fursa nyingi za ujasiriamali kwa vijana, huku akiwashukuru The Foundation For Civil Society kwa ufadhili wenye lengo la kusaidia vijana waondokane na umaskini kwa maslahi ya taifa.

Mmoja wa wajasiriamali, Martin Bogwe kutoka kata ya Mwananyamala anayejishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa pilipili ya mbilimbi anasema fursa zipo nyingi , akiwataka vijana kuzichangamkia ili kuondokana na utegemezi.

Zaidi ya vijana wajasiliamali wapatao 60 wanaojishughulisha na ujasiliamali walishiriki katika semina hiyo, ambayo pia maafisa maendeleo kutoka katika kata za Makumbusho, Mwananyamala na Kijitonyama walishiriki.

TBS Yatoa Elimu Kuhusu Majukumu Yake Mapya

$
0
0
Ofisa Uhusiano, Neema Mtemvu, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Ally Hapi kwa kudhamini Kongamano la Vijana na Wanawake lilimalizika jana (Septemba 5, mwaka huu) wilayani Kilolo .TBS imedhamini na kutoa elimu kwa vijana na wanawake wilayani humo. Picha na Chalila Chibuda.

Na Mwandishi Wetu, Kilolo
ZAIDI vijana na wanawake 800 katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wameelimishwa jinsi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linavyotekeleza majukumu mapya ambayo awali yalikuwa chini ya iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

Wananchi hao walipatiwa elimu hiyo kupitia kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na wilaya na kudhaminiwa na TBS. Kongamano hilo la siku mbili lilianza Septemba 4 na kumalizika Septemba 5, mwaka huu.

Akitoa elimu kwa washiriki wa kongamano hilo kuhusiana na mabadiliko hayo, Ofisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, alisema TBS inatekeleza majukumu hayo kufuatia mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo yameleta mabadiliko katika sheria ya viwango Na: 2 ya mwaka 2009.

Kutokana na mabadiliko hayo, Mtemvu alisema majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi yanafanywa na TBS. 

Alitaja huduma zinazotolewa na shirika hilo kwa sasa kuwa ni pamoja na usajili wa jengo,  kusimamia masuala ya usalama na ubora wa chakula na vipondozi na upimaji wa bidhaa za vyakula na vipodozi kwa lengo la kudhibiti ubora.

Majukumu mengine ni utoaji wa leseni au cheti cha TBS kwa bidhaa za chakula na vipodozi na usajili wa bidhaa za vyakula na vipodozi vinavyotoka nje ya nchi.

Wakati huo huo, maofisa wa shirika hilo walitoa elimu ya viwango kwa washiriki wa kongamano hilo miongoni mwao wakiwa ni wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo kupitia kongamano hilo,  Mtemvu, alitoa wito kwa wajasiriamali kutumia fursa ya huduma ya bure ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao ambayo inatolewa na shirika hilo ili kuwainua wajasiriamali na hatimaye kuweza kushindana na kuuza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje ya nchi bila vikwazo vya kibiashara.

Alisema kinachotakiwa ni mjasiriamali kupata barua ya utambulisho kutoka Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) na akiipeleka TBS mchakato wa kumthibitishia ubora bidhaa zake unaanza mara moja.

Alitoa wito kwa washiriki wa kongamano hilo kutumia elimu waliyoipata kujitokeza TBS kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na kuwa mabalozi wazuri wa masuala ya viwango.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ali Hapi, alitoa wito kwa wajasiriamali kujiajiri na hatimaye kuwa wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vikubwa, hivyo kusaidia kutoa ajira kwa Watanzania.

Hapi alifafanua kwamba Serikali peke yake haiwezi kuajira kwa wananchi wote, hivyo alitoa mwito kwa washiriki wa kongamano hilo kuchangamkia fursa za kujiajiri.

HOFU YA KULIWA NA MAMBA YATOWEKA LIPINGO

$
0
0
Na Netho Nyasa
WAKAZI wa Kata ya Kijiji cha Lundo, kata ya Lipingo wameupongeza uongozi wa Wilaya ya Nyasa, kwa kuwajengea daraja katika daraja la mto Lwika.Daraja hilo linalounganisha, Kitongoji cha zambia na Kijiji cha Lundo na kumaliza kero ya wakazi hao kuliwa na mamba. 

Wakazi hao walitoa pongezi wakati wa Ziara ya kamati ya Siasa, ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyasa, walipokuwa wanatembelea na kukagua miradi ya maendeleo, iliyotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa hivi karibuni katika Kata ya Lundo.

Wananchi hao walifafanua kuwa, kwa muda mrefu walikuwa wakishuhudia vifo vinavyotokana na kuliwa na mamba, waliokuwa wakikaa katika mto huo ,na kuwaua wakazi waliokuwa wakivuka kwa kuwa walikuwa wakilazimika kuingia katika mto huo ili wavuke.

Waliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa daraja hakuna kifo chochote cha kuliwa na mamba kilichotokea katika kijiji hicho na wakazi wa kijiji hicho. Wamekuwa wakiishi kwa amani, bila hofu ya kuliwa na mamba katika daraja hilo linalounganisha kitongoji cha Zambia na kijiji cha Lundo.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Lipingo, Kuno Ntini alithibitisha daraja hilo ni Ukombozi katika kata yake kwa kuwa kumewafanya wanachi kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Awali walikuwa wakiwa na hofu ya kwenda shamba kwa hofu ya kuliwa na mamba katika daraja hilo lakini kwa sasa wanaendelea vizuri na shughuli za maendeleo.

“daraja hili lilikuwa kikwazo sana kjatika shughuli za kimaendeleo, kwa kuwa watu walikuwa wakishindwa kufanya kazi kwa hofu ya kuliwa na mamba lakini tangu daraja likamilike hakuna kifo cha mamba kilichotokea”

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo, Kaimu meneja wa wakala barabara za mijini na vijijini (TARURA) wilayani hapa Mageta Mteleke ,alisema serikali imetoa Shilingi milioni sabini na tisa nukta nne (79,400,000/=) mpaka kukamilika kwa mradi huu na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Katubu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani hapa Abasi Mkweta kwa niaba ya chama hicho Wilayani hapa alipongeza juhudi zilizofanywa na Halmashauri ya kujenga daraja hilo na kuwaomba waendelee kutatua kero za wananchi kwa wakati ili kuwawezesha wananchi hao kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.

“Napenda kuchukua fursa hii kukupongeza sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Bw.Jimson Mhagama kwa kutekeleza mradi huu ambao ulikuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo katika Kata hii wakazi walikuwa wakiliwa na mamba na hata wananchi wameufurahia sana mradi huu kwa kuwa tangu kukamilika kwake hakuna kifo cha mamba kilichojitokeza katika Daraja hilo” . 

Aidha aliwaomba wananchi kutunza miundombinu ya daraja la mto Lwika ili iweze kudumu na kusaidioa vizazi vijavyo.

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA SOKO LA SAMAKI KUNDUCHI

$
0
0
Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua mapema leo katika mnada wa kuuzia Samaki wa Kunduchi wilaya ya Kinondino jijini Dar es Salaam.
 Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua katika mnada wa kuuzia Samaki wa Kunduchi wilaya ya Kinondino jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UGANDA, JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tazania Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa kutembelea mabanda mbalimbali katika kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda, lililofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipotembelea mabanda kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Laurean Rugambwa Bwanakunu walipokuwa kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

VIBAKA HATARI 13 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

$
0
0





Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana katika matukio mbalimbali.

Jeshi LA Polisi  Arusha,linawashikilia vibaka hatari wa kundi la tatu mzuka wapatao 13 ambao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya uporaji, unyang'anyi na wizi wa kutumia nguvu huku wakiwalenga zaidi wanawake.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amewataja vinara watatu kati ya 12 ambao wakuwa wakiongoza kundi hilo kuwa ni Faisal Mbaraka(17),Emmanuel Bosco(20) na Mohamed Hussein (18)wote wakazi wa Sanawari jijini hapa.

Kamanda Shana ametaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na Pikipiki nne ,MC 504AHT aina ya Kinglion,MC262AXQ aina ya Boxer ,MC240AEB aina ya Boxer na MC 811BWG aina ya Haojue.

Vitu vingine ni Laptop tatu,TV kubwa tatu,Meza mbili za TV Friji moja aina ya Boss na Redio kubwa moja ikiwa na spika zake mbili aina ya Sonny vikiwa vinashikiliwa kituoni hapo.

Kamanda wa Polisi amewataka wananchi walioibiwa vitu vyao kufika kituoni hapo na kuvitambua.

Picha ikionyesha Kamanda Wa Polisi akionyesha baadhi ya vitu bilivyokutwa na vibaka hao

Chiguma kula sahani moja na madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Kikosi Cha Polisi cha Usalama Barabarani Gabriel Chiguma akizungumza na madereva katika Stendi Kuu ya mabasi Mjini Tabora mara baada ya kufanya ukaguzi wa mabasi.
 Askari wa Kikosi Cha Usalama barabarani akionesha abiria namna Mfumo wa gari kuwa kabla ya haijaanza safari.
Mkaguzi wa mabasi Hamis Mshihiri akizungumza na waandishi kuhusiana namna wanavyofanya ukaguzi katika mabasi kabla hayajaanza safari.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Tabora
KIKOSI cha Polisi cha usalama Barabarani  Mkoani Tabora kimesema kuwa madereva wafuate sheria za usalama barabarani katika kuepusha ajali zinazotokana na uzembe wa kibindamu.

"Nitakula sahani moja na madereva wazembe ikiwa ni kulinda usalama wa abiria pindi wanaposafiri kwenda katika shughuli mbalimbali"amesema Chiguma.

Hayo ameyasema Kamanda wa polisi wa Kikosi hicho Gabriel Chiguma wakati akizungumza na madereva katika Stendi Kuu ya Mabasi Mjini Tabora, Chiguma amesema kuwa madereva waachane na ulevi wakati wa kuendesha vyombo vya moto.

Amesema kuwa agizo la kutembea usiku madereva wanalitumia vibaya kwa kuongeza mwendo.

Chiguma amesema hakuna sababu yeyote itakayofanya dereva asichuliwe hatua kutokana kutumia vibaya agizo la serikali la kutembea usiku.

Aidha amesema kuwa madereva ni wajibu wao kuendesha mabasi kwa weledi ili kulinda usalama wa abiria na mali zao.

Chiguma kuwa Tabora isiyokuwa na ajali inawezekana na hivyo atasimamia katika kuhakikisha madereva wanafuata sheria za usalama barabarani na wataokwenda kinyume watanyanganywa leseni.

BUGANDO YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI TATU KWA MWEZI

$
0
0
Jengo lenye huduma za kibingwa ambalo linahudumia hadi wanachama 350 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanahudumiwa kwa siku. Limegharimu Shilingi Milioni 800 tulizowezeshwa na NHIF na tangu 2017 wameshamaliza kurejesha malipo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiongea na maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake
Maabara ya Vinasaba iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando
Wafamasia kitengo cha kuchanganya dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu ikiwemo magonjwa ya moyo,ngozi kwa akina mama na watoto

Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiwa na Maofisa Habari na Mahusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wapo mkoani Mwanza kujionea hali ya maboresho ya hospitali hiyo.

………………………


Na.Catherine Sungura, Mwanza


Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa mwezi baada ya kuimarisha mfumo wa makusanyo wa kieletroniki katika utoaji huduma.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akielezea mafanikio ya hospitali hiyo kwa maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake waliotembelea hospitali hiyo kujionea maboresho ya sekta ya afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.


Prof.Makubi alisema kuwa baada ya kuimarisha mfumo huo hospitali hiyo imeweza kukusanya kiasi hicho cha fedha tofauti na awali ambapo walikua wakikusanya shilingi milioni mia nane kwa mwezi.


“Licha ya makusanyo haya mfumo huu pia umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wepesi na kwa haraka kwani zamani kulikuwa na upotevu wa mafaili na hivyo kuleta malalamiko kwa wagonjwa”. Alisema Prof.Makubi.


Kwa upande kwa huduma za kibingwa na bobezi mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya Serikali kushusha huduma za kibingwa kwenye hospitali za rufaa za kanda hospitali hiyo imefanikiwa kununua mashine kadhaa za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo CT- SCAN ya kisasa, kwa mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na hivyo kuweza kuwaondolea adha wakazi wa mwanza na majirani zake.


“Pia tumeboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi ya nane kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali kwa muda wa masaa matatu kutoka masaa 12 yaliyokuwa yakitumika kutokana na vifaa vya zamani na hivyo imeleta faraja kwa wagonjwa kuongezeka kupata huduma hospitalini hapa tofauti na nyuma ambapo vipimo vingi walikua wanavipata nje ya hospitali yetu”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo Prof. Makubi alisema katika kuboresha miundombinu wameweza kujenga jengo zuri lenye huduma zote za madaktari bingwa ambapo wanapokea wagonjwa 350 kwa siku wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF) ambalo limegharimu shilingi milioni 800 walizowezeshwa na NHIF na tangu mwaka 2017 wamefanikiwa kumaliza kulipa mkopo huo.

Prof.Makubi ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na NHIF kuhamasisha wananchi kukata bima ya afya na hivyo kuongeza watumiaji wa bima hiyo kwa asilimia 70 tofauti na awali ambapo walikuwa wakipata wanachama hao kwa asilimia 30 hadi 40.

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (katikati), Bungeni jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 6.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Capital Dodoma, nje ya jengo la Bunge, jijini Dodoma, Septemba 6.2019.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 6.2019.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Trilioni 2.6 Yazinduliwa na Mwenge

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
JUMLA ya miradi 5,603 yenye thamani ya shilingi trilioni 2.6 imezinduliwa na Mwenge wa Uhuru kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2018.

Hayo yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa alipokuwa akijibu swali la Mhe. Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum kuhusu idadi ya miradi inayofunguliwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka.

"Uwiano wa miradi inayozinduliwa kwa mwaka na kuwekwa mawe ya mzingi ni 1,402 yenye thamani ya shilingi 651,849,585,126.64," amesema Ikupa.

Ameendelea kusema kuwa, miradi hiyo huendana na Kauli Mbiu mbalimbali. Mfano mwka 2017, Kauli Mbiu ilikuwa uwekezaji katika sekta ya viwanda. Mwaka 2018 Kauli Mbiu ilikuwa Uwekezaji katika Sekta ya Elimu, na mwaka 2019 Kauli Mbiu ni Maji ni Haki ya Kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Aidha, Waziri Ikupa amempongeza Mhe. Kadika kwa kukiri kuwa Mwenge wa uhuru umekuwa ukileta maendeleo makubwa nchini.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenyeulemavu, Mhe. Stella Ikupa akijibu swali wakati wa kikao cha Nne cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 06 Septemba 2019 jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa.
 (Picha na IDara ya Habari – MAELEZO)

WAKAZI WA KATAVI WASHIRIKI MBIO ZA RIADHA KUCHANGIA HOSPITALI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akizungumza na wananchi katika uwanja wa Azimio
Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa na viongozi wengine wakipasha misuli kabla ya mbio kuanza.
Mshindi namba moja wa mbio kilometa 20 Fillingson Singyi akiwa amekamilisha mbio hizo.


Na Ripota wetu, Katavi 

Wakazi wa mkoa wa Katavi kwa mara ya kwanza wamejitokeza kushiriki mchezo wa mbio za riadha za kilometa 20, kilometa 10, 5, 3 na 1 zinazojulikana kwa jina la Homera Marathon kwa lengo la kuchangia fedha za ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi inayokabiliwa na uchakavu mkubwa

Mbio hizo zimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ambaye amewataka wakazi wa mkoa huo kuchangia hospitali hiyo“Tuna namba za simu na akaunti za benki ambazo kila mwananchi anaruhusiwa kuchangia” alisema Homera

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wameeleza dhana nzima ya mbio hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha afya pia itaboresha miundombinu ya hospitali hiyo

Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo sasa inatumika kama Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ilijengwa tangu mwaka 1952 inakabiliwa na uchakavu mkubwa

BUGANDO YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI TATU KWA MWEZI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Prof. Abel Makubi akiongea na maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake.
  Wafamasia kitengo cha kuchanganya dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu ikiwemo magonjwa ya moyo,ngozi kwa akina mama na watoto.
Maabara ya Vinasaba iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya Bugando.

Na.Catherine Sungura, Mwanza
HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa mwezi baada ya kuimarisha mfumo wa makusanyo wa kieletroniki katika utoaji huduma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi wakati akielezea mafanikio ya hospitali hiyo kwa maofisa habari wa Wizara ya Afya na Taasisi zake waliotembelea hospitali hiyo kujionea maboresho ya sekta ya afya katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Prof.Makubi alisema kuwa baada ya kuimarisha mfumo huo hospitali hiyo imeweza kukusanya kiasi hicho cha fedha tofauti na awali ambapo walikua wakikusanya shilingi milioni mia nane kwa mwezi.


“Licha ya makusanyo haya mfumo huu pia umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wepesi na kwa haraka kwani zamani kulikuwa na upotevu wa mafaili na hivyo kuleta malalamiko kwa wagonjwa”. Alisema Prof.Makubi.

Kwa upande kwa huduma za kibingwa na bobezi mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya Serikali kushusha huduma za kibingwa kwenye hospitali za rufaa za kanda hospitali hiyo imefanikiwa kununua mashine kadhaa za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo CT- SCAN ya kisasa, kwa mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 na hivyo kuweza kuwaondolea adha wakazi wa mwanza na majirani zake.

“Pia tumeboresha huduma za maabara kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi ya nane kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali kwa muda wa masaa matatu kutoka masaa 12 yaliyokuwa yakitumika kutokana na vifaa vya zamani na hivyo imeleta faraja kwa wagonjwa kuongezeka kupata huduma hospitalini hapa tofauti na nyuma ambapo vipimo vingi walikua wanavipata nje ya hospitali yetu”. Alisema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo Prof. Makubi alisema katika kuboresha miundombinu wameweza kujenga jengo zuri lenye huduma zote za madaktari bingwa ambapo wanapokea wagonjwa 350 kwa siku wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa (NHIF) ambalo limegharimu shilingi milioni 800 walizowezeshwa na NHIF na tangu mwaka 2017 wamefanikiwa kumaliza kulipa mkopo huo.

Prof.Makubi ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na NHIF kuhamasisha wananchi kukata bima ya afya na hivyo kuongeza watumiaji wa bima hiyo kwa asilimia 70 tofauti na awali ambapo walikuwa wakipata wanachama hao kwa asilimia 30 hadi 40. 

Jengo lenye huduma za kibingwa ambalo linahudumia hadi wanachama 350 wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanahudumiwa kwa siku. Limegharimu Shilingi Milioni 800 tulizowezeshwa na NHIF na tangu 2017 wameshamaliza kurejesha malipo.

Mradi wa VectorWorks wafikia tamati huku kiwango cha Malaria kikipungua nchini

$
0
0
MRATIBU wa Malaria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Stella Kajange, amesema ugonjwa wa Malaria umepungua kwa asilimia 50 akimaanisha kuwa kiwango cha maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo vimepungua kutoka asilimia 15 kwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa mkutano wa wadau wa masuala ya malaria alisema kupungua kwa ugonjwa huo wa Malaria kumetokana na mafanikio waliyopata kati ya Serikali, wadau na wahisani wakiwemo. Alisema Tanzania inaendelea vizuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao ugonjwa huo umekuwa ni tishio kwa jamii.

“Licha ya kupungua kwa ugonjwa huu nchini lakini ugonjwa huu bado ni tishio kwa jamii na hivyo serikali inaendelea na utekelezaji wa afua mbalimbali ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua,”alisema Kajange

Aidha aliongeza sera ya mwaka 2007 inaelezea muelekeo wa nchi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya njema ili waendelee na shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo tunatekeleza sera mbalimbali kwa faida ya wananchi wetu kuhakikisha wanakuwa na afya njema,”alisema na kuongeza kuwa 

“Serikali ya Tanzania inafanya kazi na wadau mbalimbali wa Maendeleo……tunawashukuru sana PMI kwa pamoja na USAID na wadau wengine kwa kutuunga mkono kwa miradi inayotekelezwa sehemu mbalimbali nchini,”alisema Kajange

Naye Msimamizi wa Kitengo cha Kupambana na Malaria Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP),Winfred Mwafongo alisema ugonjwa wa Malaria unaathiri zaidi kundi la wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Alisema katika mikakati yao waliyojiwekea ni kuhakikisha wanadhibiti Malaria nchini ambapo tayari wameweka utaratibu wa afua ambazo zinazohusika na udhibiti wa Malaria.

Alisema miongoni mwa afua hizo ni kuhakikisha kuna kuwepo na matumizi ya vyandarua vyenye dawa ,kuangamiza vijidudu na upuliziwaji wa viuadilifu kudhibiti mbu.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa VectorWorks Waziri Nyoni alisema mradi huo umedumu nchini takribani miaka mitano ambao ulijikita katika usambazaji wa vyandarua vyenye dawa katika mikoa mbalimbali.

“Mradi umedumu nchini ndani ya miaka mitano na mwaka huu mwezi September ndio mwisho wa mradi huu,tunaamini kwa ushirikiano tulioupata umeweza kuleta tija kwa jamii katika kuhakikisha wananchi wanatumia vyandarua vilivyowekwa dawa,”alisema. 

Akizungumzia kuhusu uendelevu wa shughuli zilizokuwa zikitekelezwa na VectorWorks, Waziri Nyoni alisema kuwa “tumejenga mifumo thabiti ya kuhakikisha utaratibu wa ugawaji wa vyandarua kwa walengwa kupitia vituo vya kutolea huduma nchi nzima na kupitia shule za msingi katika mikoa 14, na uwajibikaji unaendelea bila changamoto yoyote, tumejenga uwezo wa bohari kuu ya dawa (MSD) kuendelea na utaratibu huu na pia watendaji ngazi za halmashauri wataendelea kusimamia utoaji wa huduma hizi hata bila uwepo wa VectorWorks ambayo ni mafanikio makubwa ya mradi” 

Aidha alisema nchini Tanzania mradi huo ulijikita katika maeneo matatu ikiwemo kushauri serikali juu ya sera zinazohusu masuala ya malaria, ,Utekelezaji wa afua ya ugawaji wa yyandarua vyenye dawa, kufanya tafiti juu ya ugonjwa wa malaria na upimaji wa matokeo ya program za malaria.

Mradi wa VectorWorks umekuwa ukifadhiliwa na USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti Malaria (PMI).
Mkurugenzi wa mradi wa VectorWorks Waziri Nyoni (kulia) akimkabidhi cheti maalum Msimamizi wa kitengo cha kudhibiti malaria nchini Winfred Mwafongo (kushoto) wakati wa halfa wa kumalizika mradi huo ambao umedumu kwa miaka mitano. VectorWorks imekuwa ikiendesha mradi wa kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu hapa nchini chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.

Airtel Africa appoints George Mathen as Managing Director for Airtel Tanzania PLC

$
0
0
Nairobi, September 6, 2019: Airtel Africa, a leading telecommunications services provider with operations in 14 countries across Africa, is pleased to announce the appointment of George Mathen as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. The appointment will take effect on the 1st of October, 2019.

Mr. Mathen has more than 20 years’ of experience in senior management roles, with experience in the telecommunications and FMCG sectors. Prior to joining Airtel Africa, he was CEO – Homes, at Bharti Airtel In India where he designed and implemented the Airtel Home strategy. Prior to taking up the role, he has also been the CEO of various circles within the India business. Before joining Bharti Airtel, George also spent ten years’ in Coca-Cola India in several capacities including Area General Manager and Sales Manager across various regions. He holds a Bachelor of Commerce degree and has done his Masters in Business Administration. 

Commenting on this appointment, Raghunath Mandava, Airtel Africa’s Chief Executive Officer, said: “We are excited to welcome George as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. He will be responsible for the profitable growth of the business and help Airtel be the preferred telecom brand to bridge the digital divide and preferred partner to grow financial inclusion. 

I would also wish to take this opportunity to sincerely thank Sunil Colaso, the outgoing Managing Director, leaving after 13 years’ of dedicated service to Airtel, including the last 6 years’ as Managing Director for Airtel Tanzania PLC. We wish him the very best as he starts a new chapter in his life.”


RAIS MAGUFULI AOMBWA KUINGILIA KATI YANAYOENDELEA NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu 

TAASISI tatu nchini Tanzania zisizo za kiserikali wamemuomba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Rais John Magufuli kuingilia kati kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Wakizungumza leo Septemba 6,2019 , na waandishi wa vyombo vya habari viongozi wa taasisi hizo ambazo ni Action for Change(ACHA), The Right Way(TRW) na Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika(SAHRINGON) wamesema kuna kila sababu ya viongozi kuchukua hatua ya kukomesha machafuko yanayoendelea Afrika Kusini.

Akizungumza kwa niaba ya taasisi hizo, Martina Kabisama kutoka SAHRINGON amesema kwa pamoja wanatoa mwito kwa Mwenyekiti wa SADC Dk.Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini humo dhidi ya watu wa mataifa mengine ya Afrika.

"Wimbi la kushambuliwa kwa watu wanaoitwa wageni si peke linatokea Afrika Kusini, bali pia limetokea katika nchi mbalimbali katika ukanda wetu.Mfano siku za karibuni kuna mbunge mmoja nchini Kenya alitoa kauli inayoumiza kwa wale aliowaita wageni.

"Uzalendo ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa ya Afrika na mababa wa Afrika umevamiwa na kuufanya uzalendo usinyae."Ni suala la kupiga kengele kwamba Waafrika kwa pamoja waungane na kuanisha zaidi chanzo cha ubaguzi huu mpya unaobagua watu wa mataifa mengine , miongoni mwa watu wa mataifa,"amesema.

Kabisama ameongeza ACHA, TRW na SAHRINGON wanatambua kuwa Tanzania ndiye Mwenyekiti wa SADC , hivyo wanayo imani kuwa Rais wetu mpendwa Dk.Magufuli anaweza kuitumia nafasi aliyonayo kumaliza sintofahamu inayoendelea nchini Afrika Kusini.

"Tunatoa mwito wa mikakati ya kuvunja minyonyoro ya utengano wa namna hii ya unyanyasaji wa aina hii ambavyo vyote ni dalili ya kutengana na siyo kuungana-Muungano wa Afrika.

"Viongozi wa Afrika budi warejee uongozi uliotukuka(uongozi wa pamoja na wa mmoja mmoja) kujiamini na weledi, kutengeneza mitandao na viongozi wenzao wa Afrika...

"Ili kupambanua vikwazo kwa pamoja na kupambana kwa pamoja dhidi ya ubaguzi wa watu wa mataifa unaoota mizizi katika ukanda huu wa dunia,"amesema.

Kabisama amesema kile kilichotokea kwa kaka na dada zetu nchini Afrika Kusini ambapo raia wetu wa Afrika wa damu wanaumia kwa kiwango kikubwa kwa kunyanyapaliwa uto wao, haki zao za binadamu a fursa ya maendeleo yao ni fedheha kwa wanaotekeleza vitendo hivyo.

"Kinachotokea nchini Afrika Kusini na sehemu zingine za bara letu ni cha kihistoria ambapo machafuko ya ukatilii yameachwa bila kushughulikiwa na wahusika."Kwa mshangao wetu Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zilizoridhia na kusaini mikataba na mapatano ya kimataifa.

"Mathalani mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ubaguzi na mkataba wa kuondoa aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake.Ziko wapi sheria za kimataifa huko Afrika Kusini?"

Ameongeza wakati wanatoa mwito huo kwa ajili ya kuvunja minyororo hiyo ya ubaguzi na kutengwa , pia wanatoa mwito kwa raia wa Afrika kusimama kidete kupigania amani endelevu na utulivu milele.

"Iwapo waafrika wanaota ndoto ya uzalendo wa Afrika , ndoto hiyo ni budi iwe kweli kupitia uhuru , usawa na mshikamano,"amesema Kabisama.
 Mratibu Taifa  wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu kusini mwa Afrika (SAHRINGON),Martina Mnenegwa Kabisama akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu kutoa mwito kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kuchukua hatua za haraka kukomesha ukatili unaofanywa nchini Afrika Kusini dhidi ya Watu wa Mataifa mengine.  Picha na Michuzi JR

RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WAFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA LA TANZANIA NA UGANDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda huku wakiongozwa na marais Dkt John Pombe Magufuli na Mhe. Yoweri Museveni. Picha zote na Matokeo Chanya+.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia hotuba za marais wa Tanzania na Uganda.
Rais wa Uganda Rais Yoweri Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akifuatilia hotuba ya Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi akiwakaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi,

SERIKALI HAINA NIA YA KUZIBANA NGOs-WAZIRI UMMY

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na watendaji wake katika kikao cha kujadili uboreshaji wa mifumo ya utoaji huduma kwa wadau wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Maendeleo ya jamii) Dkt. John Jingu akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(kulia) kuhusu Utekelezaji wa kazi ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao cha Waziri na Watendaji wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Zainabu Chaula akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) kuhusu uandaaji wa mfumo utakaosaidia kujua kazi na miradi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao cha Waziri na Watendaji wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma.
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(mbele mwenye kiremba cheusi) kuhusu uhuishaji wa Mashirika yaliyokuwa nje ya Sheria katika zoezi lililofanyika nchini mwezi uliopita katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Wizara kilichofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Ponsiano Mawazo akielezea kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(mbele mwenye kiremba cheusi) jinsi ya Mfumo wa Usajili na Uratibu wa NGOs utakavyokuwa unafanya kazi na kurahisha wadau kupata huduma ya Usajili na uwasilishaji wa ripoti mbalimbali wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Wizara kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata keki katika kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa kwake jana jijini Dodoma.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haina nia ya kuyabana Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kutekeleza majukumu yao bali inaweka utaratibu wezeshi wa kuyaratibu Mashirika hayo ili yaweze kuleta tija katika maendeleo ya nchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati alipokutana na watendaji wake kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na Idara Kuu ya Afya kwa lengo la kujadiliana na kupata namna bora ya kuboresha huduma ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha inaweka mazingira bora ya kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa ufanisi zaidi ili yaweze kuleta matokeo chanja katika jamii hasa matokeo yanayoonekana na kugusa hali ya maisha ya watu masikini tofauti na kuendesha semina na warsha kama ilivyozoeleka hapo awali.

Amesisitiza kuwa fedha za miradi zinazotumika katika miradi inayotekelzwa na NGOs nchini zitumike kama ilivyopangwana sehemu yenye uhitaji na sio kupeleka miradi sehemu moja na sehemu nyingine kukosa miradi ya maendeleo kutoka kwa wadau wa NGOs.

Waziri Ummy amesema kuwa ni muhimu kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwekeza fedha kwa kufuata vipaumbele vya Taifa ili kuisaidia Serikali katika kuhakikisha jamii inapata maendeleo.

“Kama Wizara tulishataka kufanya maadhimisho mkoa wa Katavi lakini hakukuwa na mdau hata mmoja eneo hilo anayejishughulisha na mradi wa kimaendeleo” alisisitiza Mhe.Ummy

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa watahakikisha wanaweka mazingira mazuri ya wadau kufanya kazi zao kwani wadau hawa ni kundi muhimu katika maendeleo ya nchi yetu katika kutekeleza majukumu ya kitaifa.

Amesisitiza kuwa kumekuwa na changamoto katika kufanya kazi na wadau wa NGOs hivyo Serikali inatengenza mazingira mazuri ya kutatua changamoto hizo ili kuendelea kufanya kazi na wadau hao katika ulekeo mzuri.

Naye Katibu Mkuu Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa Serikali inafuatilia na kujua wadau wa maendeleo wanafanya kazi wapi imeamua kuja na mfumo wa Wadau Portal utakaosaidia kuonesha wadau walipo nchini na wanatekeleza miradi ipi na wapi.

Ameongeza kuwa dhamira ya juhudi zinazofanywa na Wizara ni kuhakikisha kuwa panakuwepo miongozo na mifumo ya utoaji huduma kwa wadau itakayosaidia kuratibu, kusimamia na na kubaini kwamba ni kwa kiasi gani wadau wa maendeleo wanachangia katika juhudi za Serikali za kukuza maendeleo na ustawi wa maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

NMB YAWAPIGA MSASA WAFANYABIASHARA TABORA

$
0
0

Na Mwandishi wetu,Tabora

Wafanyabiashara katika Mkoa wa Tabora,wengi hawajilipi mishahara kutokana na kazi zao wanazofanya na hivyo kukosa fursa ya kufahamu namna biashara zao zinavyokua au zinavyodorora.

Haya yamebainishwa na Meneja wa NMB kanda ya Magharibi, Sospeter Magese,wakati akizungumza na wafanyabiahara wa Mkoa wa Tabora, alisema wengi huwa hawajilipi mishahara na kufanya mahesabu yao kutokuwa vizuri.

“Inashangaza mfanyabiashara anawalipa wafanyakazi wake mshahara lakini yeye akiwa mkurugenzi hajilipi mshahara na pia huchanganya matumizi binafsi na ya biashara jambo amvalo huyumbisha mitaji yao.

Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya wafanyabiashara juu ya huduma inayotolewa na NMB, Magese aliwaeleza kuwa kupitia mishahara yao ndio matumizi ya binafsi yanaweza kutoka huko na sio katika biashara.

Aliwaeleza kuwa benki ya NMB ni benki yao na waitume kwani imejipanga kushirikiana nao katika kukuza uchumi wa Taifa.Mwenyekiti wa wafanyabiashara wenye akaunti benki ya NMB,Ahadi Mviombo,aliwahimiza wafanyabiashara kutenga sehemu ya mauzo yao kwa ajili ya kulipa madeni wanayokopa.

“Kama ukiweza kutenga angalau shilingi elfu tano kila siku kwa ajili ya marejesho mtihani utakuwa umeshinda”AlisemaMfanyabiashara Mwalimu Mambo,aliipongeza NMB kwa utaratibu wake wa kuwafundisha wafanyabiashara namna ya kuweka mahesabu sawana kutafuta faida.

“Tunashukuru kwa elimu tunayopewa na benki hii ambayo kwa kweli inatusaidia sana katika biashara zetu”Alisema

Kikao hicho chenye lengo la kupokea maoni kutoka kwa wafanyabiashara ziadi ya 300 wenye akaunti NMB pia kilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki hiyo ambao walitoa elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifurahia jambo wakati wa kongamano la wanachama wa klabu ya wafanyabiashara mkoa wa Tabora uliolenga kuwapa mafunzo na nidhamu ya biashara. Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kuwapa elimu na fursa zakukuza biashara zao kupitia benki hio.

Walimu Wanaofundisha Lugha ya Alama Wapewa Mafunzo

$
0
0

Na, Editha Edward-Tabora 

Zaidi ya walimu mia moja kutoka shule za sekondari kumi na tisa nchini wameanza kupewa mafunzo ya Lugha ya Alama Ikiwa ni moja ya Mpango wa Serikali na wadau wa elimu nchini kufanya maboresho katika Sekta ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususani viziwi

Akizungumza katika mafunzo hayo maalumu ya kujadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili Watu wenye mahitaji maalumu yaliyofanyika katika chuo kikuu cha AMUCTA, naibu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia dkt. Avemaria Semakafu amesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamekuwa hawafanyi vizuri katika Masomo yao ya darasani na kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa kutokana na walimu wanaotoa elimu kwa wanafunzi hao kutokuwa na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wanafunzi hao wenyeahitaji maalumu

"Tunatakiwa suala hili tulichukulie kiuhalisia na Tunatakiwa tuwawekee hawa wanafunzi wenye mahitaji maalumu mazingira wezeshi ili waweze kufanya vizuri katika Masomo yao na waendelee mbele ili waweze Kushiriki katika kujenga Taifa hasa viziwi pindi wanapokuwa darasani sisi kama wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia na wadau wa elimu ambao tumepewa jukumu la kusimamia suala la sera na mustakabali Mzima wa elimu bado tunasema uziwi bado ni Tatizo"Amesema Semakafu

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Tabora Suzan Nusu amesema mafunzo hayo ya Lugha ya Alama yamekuja wakati muafaka kwani yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi hao wenye uhitaji maalumu hapa nchini

"Kupitia mafunzo haya watoto hawa sasa watapata maarifa ya kutosha na tutaepukana na ile adha na aibu ambayo ilikuwa inatunzunguka mara kwa mara kwamba watoto wenye wetu walikuwa hawafanyi vizuri hasa kwa hawa ambao wana matatizo ya kutosikia nina amini kabisa tukiyatumia ipasavyo mafunzo haya hii tabia tuliyokuwa tunaiona kama Siyo kuimaliza kabisa basi tutakuwa tumeipunguza kwa asilimia kubwa"Amesema Suzan

Hata hivyo mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku kumi na nne hapa mjini Tabora Ikiwa bado Lugha ya Alama ni changamoto kubwa katika Sekta ya elimu hapa nchini na, wadau wa elimu na jamii wanapaswa kuona umuhimu wa kuwasaidia Watu wenye uhitaji maalumu hasa walio na uziwi.
 Pichani ni naibu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu Akizungumza na walimu Wanaofundisha Lugha ya Alama nchini( Pichani hawapo).
Pichani ni walimu Wanaofundisha lugha ya Alama kutoka shule za sekondari kumi na tisa nchini walioudhuria mafunzo.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images