Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

RC SHIGELLA ATOA AGIZO KWA WALIMU WANAOFUNDISHA TWISHENI KUFANYA KAZI HIYO NJE YA MAJENGO YA SHULE

0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kata ya Tangasisi wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake ya kawaida kufuatilia utekelezaji wa ilani ya CCM na kupata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ambayo inafanyika mkoa mzima kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Diwani wa Kata ya Tangasisi Mohamed Haniu 
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Diwani wa Kata ya Tangasisi (CUF) Mohamed Haniu akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye hayupo pichani wakati akizungumza nao
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Tangasisi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Tangasisi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ameagiza walimu wanaofundisha Twisheni wafanye kazi hiyo nje ya majengo ya shule na nje ya muda wa kazi ili watoto watumie muda mwingi zaidi kusoma na kufundishwa.

Shigella aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwakidila wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake ya kawaida kufuatilia utekelezaji wa ilani ya CCM na kupata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ambayo inafanyika mkoa mzima.

Alisema kwani walimu hao wanalipwa mshahara na serikali hivyo lazima wahakikishe wanatimiza majukumu yao ipasavyo kuwa kuwapatia elimu bora wanafunzi ambayo itakuwa chachu ya mafanikio kwao.

“Nimekuja hapa lakini nimesikia kuna baadhi ya watu wanalalamika juu ya twisheni, nimeelekeza kama kuna mwalimu anataka kufanya twisheni afanya nje ya majengo ya serikali na nje ya muda wa kazi”Alisemaq RC Shigella.

“Kwani lazima watoto wetu watumie muda mwingi zaidi kusoma na kufundishwa na walimu ambao wanalipwa mishahara na serikali wanapokuwa darasani muda wa masomo”Alisema RC Shigella

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya watoto kusoma na kuendelea kupeleka walimu ikiwemo kutatua changamoto za walimu ili wafundishe kwenye mazingira mazuri na hatimaye waweze kupata wataalamu wengi zaidi.

Alieleza kwamba kupitia elimu watakuwa na watalaamu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, maji,afya na miundombinu na ndio maana serikali ya awamu ya tano imewekeza sana kwenye suala la elimu kuona watoto wanapata fursa hiyo muhimu.

Alisema pia serikali imeendelea kuleta fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu kwenye shule mbalimbali huku akisifu juhudi zinazofanywa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kwa kuwasaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kwenye Jiji la Tanga.

“Waziri Ummy ni mwenzetu wana mwakidila kwa kutambua mchango ya shule yetu alikwenda kuongeza na ubalozi wa Japani na kusaidia madarasa sita hivyo hatuna budi kumshukuru kwa kazi nzuri ni Mbunge wa mkoa wa Tanga angeweza hayo madarasa kupelekea wilaya nyengine na ndio maana akaona aje kusaidia jitihada za wananchi kwenye eneo hilo”Alisema RC Shigella.

Hata hivyo alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy wanamshukuru huku akiwataka kuendelea kumuombea dua ili aweze kuendelea kutimiza majukumu yake.

VIJANA 60 KATI YA 100 WAWASILI NCHINI ISRAEL, WAZIRI WA KILIMO AWAFUNDA NIDHAMU NA KUJITUMA

0
0
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Israel wakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion Jijini Tel Aviv nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019 mara baada ya kuwapokea vijana kutoka Tanzania waliowasili nchini Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimo ya Agrostudies. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.
Sehemu ya vijana kutoka Tanzania waliowasili nchini Israel kwa ajili ya mafunzo ya kilimo ya Agrostudies wakipokea maelekezo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion Jijini Tel Aviv nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019 mara baada ya kuwapokea 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Balozi wa Tanzania nchini Israel wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya nje ya Israel, tarehe 5 Septemba 2019.


Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel


Kundi la vijana wa kitanzania 60 limewasili nchini Israel kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies katika kipindi cha mwaka mmojahuku wengine 40 wakitarajiwa kuwasili tarehe 11 Septemba 2019 kukamilisha idadi ya vijana 100.

Vijana hao wamewasili tarehe 5 Septemba 2019 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion Jijini Tel Aviv nchini Israel na kupokelewa na Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb).


Waziri Hasunga amewataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kama muarobaini wa kuendeleza sekta ya Kilimo watakaporejea nchini Tanzania hivyo kuwa chachu ya maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.


“Ninyi mmekuja Israel mkiwa katika mtazamo wa kujifunza hivyo mambo mengine yote wekeni pembeni mzingatie masomo na katika kipindi cha mwaka mmoja mhakikishe mmetumia muda wenu wa masomo vizuri kujifunza, kupata maarifa na ujuzi ili mtakaporejea nyumbani mlete mabadiliko makubwa kwenye kilimo” Alikaririwa Mhe Hasunga


Mhe Hasunga amewataka vijana hao kuwa waaminifu wakati wote wa masomo yao kwani wanaiwakilisha Tanzania hivyo vitendo vyovyote vya utovu wa nidhamu itakuwa ni sehemu ya kulizalilisha Tanzania.


Alisema kuwa vijana hao wanapaswa kuwa na bidii na kuweka pembeni tabia zisizofaa kwani kuwa na maadili mema itawarahisishia vijana hao kupata utaalamu jadidu ambao utakuwa na manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla wake.


“Tunataka mabilionea wanaoibuka Tanzania watokane na sekta ya kilimo hususani vijana ambao mmepata fursa ya masomo nchini Israel, Rais Magufuli alishatangaza kuwa wakati wa utawala wake lazima mabilionea wapatikane” Alisema


Aliongeza kuwa ni matarajio ya serikali kuona vijana hao watakaporejea Tanzania wanaanzisha viwanda mbalimbali kwani malighafi nyingi zinatokana na sekta ya kilimo.


Mhe Hasunga amewataka vijana hao kutojihusisha na siasa kwani hivi sasa ni kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Israel. “Acheni kabisa kujiingiza kwenye siasa maana siasa za huku haziwahusu, waacheni waendelee na mambo yao nanyi endeleeni na kilichowaleta” Alisisitiza Mhe Hasunga


Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima amewataka vijana hao kutekeleza maelekezo waliyopatiwa na Waziri wa Kilimo.


“Chochote mtakachofanya ni Mtanzania amefanya kwahiyo mkifanya mabaya mtasambaza sifa mbaya ya nchi katika Mataifa mengine jambo ambalo halitakiwi”


Balozi Masima hakusita kuwapongeza vijana 45 ambao wamerejea nyumbani Tanzania baada ya kuhitimu masomo yao kwani wameacha alama kubwa na nzuri inayoitangaza Tanzania.


Wakizungumza kwa niaba ya vijana waliowasili nchini Israel kwa ajili ya mafunzo hayo ya Kilimo ya Agrostudie, Janeth Patrick na Simion Jalusi wamemuhakikishia Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kuwa wataiwakilisha vyema Tanzania ili liweze kufanikiwa kufika kwenye Taifa la Viwanda.



“Tutajifunza kwa bidii kubwa ili elimu tutakayoipata tuweze kuitumia vizuri kwa ajili ya kuboresha sekta ya Kilimo nchini Tanzania” Walikaririwa wakisema 


Vilevile, Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli moja serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.


MWISHO

RAIS WA ZAMANI WA ZIMBABWE AFARIKI DUNIA

0
0
RAIS wa zamani wa nchini Zimbabwe, Robart Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95 huko nchini Singapore alipokuwa akipata matiabu.

Hayati Mugabe aliongoza nchi ya Zimbabwe kuanzia mwaka 1980 hadi 2017 ambapo alipata mrithi wake ambaye ni Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.

Rais Mugabe ambaye alionekana akisema maneno mengi ya masihara katika mtandao ya kijamii na yenye ukweli ndani yake kama  "SOMETIMES YOU LOOK BACK TO YOUR AT GIRLS
 YOU SPEND MONEY ON RATHER IT TO YOUR MUM AND REALISE WITCHCRAFT IS REAL".

TANESCO YAMKUMBUKA KIJANA ANAYEPUMULIA MASHINE YA OXYGEN NA GESI

0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetoa msaada wa kiasi cha fedha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya matibabu na Mita (Luku) yenye umeme wa miezi sita sawa na Tsh Milioni Moja na Nusu kwa Kijana Hamad Awadh anayesumbuliwa na tatizo kupumua. 

Akizungumza baada yakumtembelea Hamad nyumbani kwake, Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji amesema kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Tito Mwinuka wameguswa na hali ya Hamad yakupumulia Oxygen. 

Leila amesema kutokana na matumizi makubwa ya Umeme kwa Mashine yake anayotumia kwa ajili yakupumua, wameona wamsaidie Mita ya peke yake, tofauti na wapangaji wenzake anaoishi nao nyumba moja. 

‘’Hamad ni Mtanzania mwenzetu ambaye alikuwa na shughuli zake anafanya kama kawaida, lakini kutokana na maradhi yanayomsumbua ameshindwa kuendelea na kazi zake, Sisi kama TANESCO tumeliona hili hatuwezi kumuona Mtanzania mwenzetu anateseka hivi’’, amesema Leila. 

Naye, Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo amesema Shirika hilo limeguswa na hali hiyo ndio maana linamsadia kwa hali na mali, Hamad Awadh. 

‘’Rais wetu anasisitiza Watanzania tuwe Wazalendo, sisi kama TANESCO tuemona tulibebe hili la Hamad kama Watanzania ili tumsaidie’’, amesema Mhandisi Sotco. 

Hamad Awadh ambaye kwa sasa anataka msaada kwa ajili yakupatiwa matibabu nchini India, ameshukuru kwa msaada huo kutoka TANESCO, amesema kwa sasa maisha yake ni umeme na endapo utakatika basi huwa anatumia Gesi, ameshukuru Hospitali ya Mloganzila kwa huduma walizompatia mpaka kufikia hatua hiyo. 

‘’Nasema kila siku moyoni mwangu, hata siku nikidondoka Mloganzila Hospital wamenifanyia kitu kama Mtoto wao, naishukuru pia Serikali kwa huduma zake, naomba sio ninyi tu (TANESCO) na wengine wakisikia kilio changu basi naomba msaada wao'', ameeleza Hamad. 

Kwa upande wake Abdul Athumani, Mjomba wa Hamad amesema changamoto kubwa kwa Hamad ni Umeme kutokana na kutumua Oxygen inayotumia zaidi umeme, amesema gaharama nyingine ni Gesi wanayotumia kwa Mgonjwa huyo inayonunuliwa Elfu 45 kila mwezi hivyo wanaomba msaada. 

Ugojgwa wa Hamad Awadh ulianza mwaka mmoja na nusu uliopita baada yakupata homa ambapo ilipelekea kupelekwa Hospitali ya Amana, Ilala baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo ilibainika Mapafu yake yamesinyaa na Moyo wake umehama kutoka kulia na kwenda kushoto.
Meneja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) mkoa wa Ilala, Mhandisi Sotco Nombo (katika) na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Mhaji
walimpotembelea Hamad Awadh nyumbani kwake Majumba Sita, Ukonga jijini Dar es Salaam. Hamad kwa sasa anapumua kwa kutumia Mashine ya Oxygen na Gesi anahitaji Msaada kupatiwa matibabu nchini India. 

BENKI YA MKOMBOZI YAMSAIDIA MGONJWA WA SARATANI

0
0
 Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya Biashara ya Mkombozi,  Nwaka Mwabulambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Bw,Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi na kutoa mchango wa sh. miloni moja kwaajili ya matibabu pia nakumfungulia akaunti ya pamoja (Joint Akauti) kulia ni Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid,Meneja Mikopo wa Benki hiyo Bw. Andrew Chimazi. (PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
 Bi-Fatuma Rashid (katikati) akiushukuru uongozi wa benki
 hiyo kwa mchango wao walioutoa (kulia) Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge, na Mkurugenzi wa Hazina wa benki hiyo ,  Nwaka Mwabulambo.
 Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge (kushoto), akimshuhudia, Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid (katikati) akijaza fomu kwa alama ya kidole kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akaunt) kwa ajili ya michango ya kumsaidia.Uongozi wa benki hiyo ulimtembelea, Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi baada ya kuona matangazo kwenye vyombo vya habari.
 Bi-Fatuma Rashid akiwa na mume wake Bw.Salim Rashid ayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
 Uongozi wa benki hiyo ukishauriana jambo ulipomtembelea Bw.
Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
 ........................................................
BENKI ya Biashara ya Mkombozi  imeahidi kuendelea kushiriki  shughuli mbalimbali za kijamii kwa kuchangia watui wenye mahitaji maalumu.
Hatua hiyo imefikiwa  baada ya uongozi wa benki hiyo kutoa msaada kwa  familia ya Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mara baada ya kutembelea familia hiyo Nwaka Mwabulambo Mkurugenzi wa Hazina wa Benki hiyo alisema kuwa  katika kuelekea miaka kumi ya benki hiyo bebki imeamua kushiriki na familia hiyo kwa kutoa maada wa kuwafungulia akaunti ili jamii iweze kuwasaidia.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka katika vyombo mbalimbali kuhusu uhitaji wa Rashid ambaye anasumbuliwa na saratani  uongozi wa benki uliamua kushiriki kwa vitendo kwa  kuisadia familia hiyo kwa kutoa mchango wa sh. miloni moja sambamba na kufungua akaunti ya pamoja ili kuirahisishia familia hiyo kwenye zoezi la ukusanyaji wa fedha za msaada kutoka kwa jamii.

“Kama tunavyofahamu simu za mkononi zina ukomo wa utoaji fedha hivyo benki kwa kuliona hilo  tumeamua kuirahisishia jamii kazi hii kwa kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akauti) ambayo itawezesha jamii na taasisi mbalimbali kuchangia kiasi chochote cha fedha ili  kuirahisishia  familia hii  iweze kupata msaada wa fedha za matibabu,”alisema Mwabulambo

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushiriki shughuli za kijamii benki itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuchangia shughukli mbalimbali za kijamii kama njia ya kutoa shukrani kwa kile wanachokipata kutoka kwa wateja wao ambao ndiyo wadau

Aidha aliongeza kuwa tayari uongozi wa benki umewashawishi watumishi wake kuona umuhimu wa kuchangia matibabu ya Rashidi huku ikiwataka  watanzania wengine kuona umuhimu wa kutoa michango kwa familia hii na zinmgine zenye mahitaji .

Aliitaja akaunti namba ambayo watanzania wanaweza kutoa michango yao kwa familia hiyo kuwa ni  00420111912801 na kusema kuwa kufanya hivyo  kutarahisisha matibabu ya Rashid ambaye tayari alishaanza matibabu hapa  nchini na nje ya nchi.

Kwa upande wake Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid   aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa mchango wao na kuwaomba kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha matibabu zaidi ya Rashid.

“Nashukuru Benki ya Ukombozi kwa kuliona tatizo la mume wangu na kulichukulia uzito kwa kuchangia kiasdi hicho cha fedha sambamba na kufungua akaunti, hii imetupa moyo kuwa jamii ipo pamoja nasi,”alisema Fatuma.

 kufungua akauti kwa familia hiyo ili kuwezesha jamii kuweza kushiriki kucahngia gharama za matibabu.

“Kama Benki tumeitembelea familia hii ya Rashid ili  kuifariji na tumeshaifungulia akaunti ya pamoja itakayowezesha jamii kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwezesha matibabu ya Salim ambaye anasumbuliwa na saratani,”alisema na kuongeza kuwa hii pia itasaidia taasisi mbalimbali kuweza kuchangia zaidi matibanu hayo.

Hata hivyo aliwaomba watanazia wote wenye mapenzi mema kuwa karibu na familia hiyo ili kuwezesha matibabu yaanyike na kuimarisha afya ya mume wake.

DKT.ABBAS ATEMBELEA HOSPITALI YA MUHIMBILI NA KITUO CHA RADIO CITY FM

0
0
Dkt. Patrick akionesha mfumo unaotumika katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili wa kuingiza majina na maelezo ya wagonjwa na mpango wa
kuwahudumia kupitia kompyuta.
Mtaalam wa kutumia CT scan mashine akielezea jinsi mashine hiyo
inavyofanya kazi na idadi ya watu inayohudumia kwa siku katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifafanua jambo
katika ziara yake ya kutembelea kituo cha Radio City Fm, kinachomilikiwa
na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Itifaki, Uhusiano na Umma, Gaston
Makwembe akifafanua jambo katika ziara iliyofanywa na Msemaji Mkuu
wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ya kutembelea kituo cha Radio City Fm,
kinachomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Dkt. Hassan Abbas akifafanua jambo katika kitengo cha utalii cha
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Dkt. Hassan Abbas akiwafafanulia jambo Madaktari wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili leo Jijini Dar es salaam.
Dkt. Hedwiga Swai akielezea mfumo wa matumizi ya mashine ya
Imaging Resonance Magnetic (IMR) katika chumba maalum cha uchunguzi
wa magonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, leo Jijini Dar es
Salaam.

DC MUHEZA AWATAKA WATENDAJI KATA NA VIJIJI KUWA MAKINI WAKATI WA UTOAJI WA DAWA ZA MAGONJWA YA USUBI

0
0
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha kamati ya afya ya msingi wilaya hiyo kuhusu mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichofanyika mjini humo iliyokwenda sambamba na uhamasishaji wa kunywa dawa za kukabiliana na magonjwa hayo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wilayani humo kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Dkt Flora Kessy akifuatiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Nassoro Moyo 
Msimamizi wa zoezi la Kinga Tiba katika ngazi ya Jamii kutoka wizara ya Afya Fadhili Katula akizungumza wakati wa kikao hicho
Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilaya ya Muheza Julius Mgeni akisisitiza jambo kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Sehemu ya wataalamu waliohudhuria kikao hicho
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza Bakari Mhando kulia akiwa na Diwani wakifuatilia kikao hicho
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akipima urefu kabla ya kuanza kutumia dawa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Bakari Mhando kushoto akipatiwa dawa


MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha kwamba wanapotoa dawa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa usubi kwenye maeneo yao wahakikisha wanaziweka maeneo salama ili kuepusha kuwafikia walaji ikiwa imepoteza ubora wake.

Mhandisi Mwanasha aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi wilaya hiyo kuhusu mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichofanyika mjini humo iliyokwenda sambamba na uhamasishaji wa kunywa dawa za kukabiliana na magonjwa hayo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wilayani humo.

Alisema kwamba changamoto kubwa ya watoa dawa wengine wanawapelekea wanafamilia huku akiwataka watumie utaratibu wa mikutano ya hadhara ikiwemo kuwataka wasiwaachie viongozi wa vitongoji kuteuwa watu wenyewe bali mikutano ianze ili kutolewa elimu kwa wananchi wote waelewa manufaa ya kunywa dawa na madhara ya kuwa na ugonjwa huo ndio watatoa ushirikiano wa kunywa dawa hizo.

“Kwani wakipatiwa elimu ya manufaa ya kunywa dawa hizo na madhara yanayoweza kuwakumba iwapo hawatakunywa itakuwa chachu ya wananchi wengi kuweza kujitokeza pia tumeambiwa magonjwa hayo yanaambukizwa na mbu,inzi lakini mbu hatuwezi kumtokomeza kama hatufanyi usafi tusienda tu kuhamaissha suala la kumeza dawa lakini tuhamasishe suala la usafi wa mazingira”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba ili kuweza kuondoa mazalia ya mbu kwenye maeneo yao lazima yawe safi na salama huku akieleza namna suala la usafi lilivyokuwa jambo muhimu mpaka Rais Dkt John Magufuli aliweka siku mahususi kwa ajili ya watu kufanya usafi.

Aidha alisema hiyo inaonyesha namna serikali inavyotaka maeneo yao yawe masafi hivyo tuhamasisha wananchi kuhakikisha wanakula dawa hizo ili kuweza kuondokana na suala hilo.

“Labda niwaambia kwamba hizi zote ni juhudi za CCM tunajua Serikali inaongozwa na CCM ni kutaka wananchi kuwa na afya njema kwa lengo la kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo “Alisema

Awali akizungumza kwenye kikao hicho Msimamizi wa zoezi la Kinga Tiba katika ngazi ya Jamii kutoka wizara ya Afya Fadhili Katula alisema kwamba hapa muheza wanafanya kwenye suala la tatizo la Usubi hiyo ni wilaya Kongwe ambayo imekuwa ikitoa dawa kwa miaka iliyopita mpaka sasa wanaendelea na juhudi hizo.

Alisema kwamba wanaendelea kuhamasisha lengo kufikia kiwango cha chini kwa kutokomeza kabisa usubi kwa hiyo nia pekee ni kumezesha dawa kwenye jamii ili kufikia kila mwananchi anapata dawa ili kuweza kuzuia na kumtibu kama anavimelea.

Alisema wanapambana lengo lao asilimia kuanzia 85 na kuendelea wawe wamemeza dawa ili m wisho wa siku wilaya hiyo isahau kuhusu ugonjwa huo na kuelekeza nguvu kwenye magonjwa mengine

Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Dkt Flora Kessy alisema kwamba ugonjwa wa Usubi upo kwenye wilaya hiyo hivyo wao kwa kushirikaana na wizara ya Afya na wadau wengine wameendelea kuwekeza kwenye idara ya afya ili kutokomeza au kupunguza kwa kiasi kikubwa janga hilo.

Dkt Flora alisema wanapambana kwa kiasi kikubwa kuweza kuhakikisha unamalizika kwani madhara yake ni makubwa na zaidi ni kusababisha upofu kwa watu ambao wanakabiliwa nao jambo ambalo limewafanya kuanza kuchukua hatua za makusudi kukabiliana nao

“Kwani mwananchi anapopata upofu shughuli za uendelezaji wa maendeleo ya nchi haupo tena anakuwa tegemezi kwa nchi na jamii inayomzunguka na ndio maana tumeamua kuanza kukabiliana na tatizo hilo kwa vitendo “Alisema Dkt Flora.

Naye kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilaya ya Muheza Julius Mgeni alisema kwamba hivi wanakusanya silaha kwa ajili ya kugawa dawa za usubi kwa wananchi ili kuweza kujikinga na magonjwa hayo.

Alisema kwenye wilaya yao walianza utekelezaji wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele miaka kumi na tisa iliyopita tokea 2000 wakiwa na mpango maalumu wa kutokomeza ugonjwa wa usubi.

Alisema lakini mwaka mwengine 2004/2005 wakaanza kutekeleza mpango wa kutokomeza magonjwa ya mabusa na matende baadae waliunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza hilo.

SERIKALI KUSHUGHULIKIA USHURU WA ZAO LA GUNDI WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu,akitoa maagizo juu ya uhumhimu wa kutunza mbuga ya Wembere pamoja na miti yake ya asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
Meneja Misitu Wilaya ya Iramba, Shaban Nyamasagara (wa kwanza kushoto) ,akitoa maeelezo juu ya utunzani wa miti aina ya migunga inayoongoza kwa kuzalisha gundi duniani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu (mwenye kombati). alipofanya ziara ya kukagua shamba la miti aina ya migunga wilani Iramba mkoani Singida hivi karibuni.
Wakala wa Kampuni ya Mohammed Enterpriseses Kija,akitoa maombi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza ushuru na tozo ili iweze kupata soko na kunufaisha wakulima,wafanyabiashara na serikali yenyewe.


Na Nathaniel Limu, Singida

SERIKALI imeahidi kuyafanyia kazi maombi ya mawakala na wanunuzi wa zao la gundi wilaya ya Iramba yanayohusu punguzo la ushuru unaotozwa kwa madai unachangia zao hilo likose wananunuzi.

Ahadi hiyo imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Costantine Kanyasu,muda mfupi baada ya kukagua shamba la miti aina ya migunga (vachellia drepanolobium) inayoaminika kuzalisha gundi nyingi zaidi duniani.

Alisema majukumu ya serikali ni pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili biashara zao ziwe na tija kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.“Maombi yenu nimeyapokea tutayafanyia kazi mapema iwezekanavyo na tukijiridhisa na hicho mnachokisema serikali yenu sikivu itafanya maamuzi ambayo yatazingatia pande zote za Serikali na wafanyabishara ili kunufaika na zao la gundi”, alisema.

Kanyasu alisema kuwa mbunga ya Wembere iliyopo katika mikoa ya Singida,Tabora,Shinyanga na Simiyu,itapandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya taifa hiyo italindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria.

“Nashukru kusikia uongozi wa vijiji vinavyoizunguka mbuga hii wameridhia iwe hifadhi na kwamba watailinda kwa nguvu zao zote miti hii ya asili migunga ili iendelee kunufaisha kizazi cha sasa na cha baadae ”,alisema.

Katika hatua nyingine Kanyasu aliagiza wavamizi wote waliovamia chanzo cha maji cha bwawa la Urughu watolewe haraka katika maeneo hayo ili kunusuru chanzo hicho kukauka.Kwa upande wake Meneja Misitu wa Wilaya ya Iramba, Shaban Nyamasagara, alisema mbunga ya Wembere ina umuhimu kulindwa na kutuzwa kwa kuwa ina uoto wa asili wa nyasi.

“Nyasi hizi zinasambaa sehemu kubwa ya mbunga na ni muhimu katika uwepo na uhai wa ziwa Kitangiri na Eyasi.Maziwa haya ni vyanzo vikubwa vya uchumi kwa jamii inayoyazunguka maziwa hayo”, alisema Nyamasagara.

Alitaja changamoto za hifadhi hiyo kuwa ni baadhi baadhi ya watu kuvamia mara kwa mara kwa shughuli za kibinadamu na uelewa duni wa wananchi kuhusu mambo ya uhifadhi wa taifa na kuwa eneo la Wembere kukosa miundo mbinu ya barabara za kupitika kipindi cha masika na kiangazi.

Mawakala na wanunuzi wa zao hilo walisema kuwa hivi sasa soko la dunia la gundi bei imeteremka hivyo kununua kwa sasa na kulipa ushuru na usafirishaji ni lazima mfanyabiashara atapata hasara na kufilisika.

Wakala wa Kampuni ya Mohammed Enterprises, Zengo Kija, alisema biashara ya gundi kwa sasa inasuasua na mambo yasiporekebishwa haraka mvua zikianza kunyesha shehena za zao hilo zilizopo kwenye maghala na kwa wananchi itaharibika.


BARAZA LA JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM CHATO WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

0
0
Na Editha Karlo wa Michuzi Tv,Chato

BARAZA la Jumuiya ya wazazi wa chama cha apinduzi(CCM) WilayaniChato wamehamasishwa kujiunga na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu wanapougua wao na familia zao.

Meneja wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Geita Elias Odhiambo aliwaambia wajumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Chato kuwa ni muhimu kujiunga na bima ya afya wamehamasishwa kujiunga na Bima ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu na dawa pale wanapougua hata kama hawana pesa mfukoni.

"Ugonjwa huwa unakuja bila ya taarifa,unaweza kuugua mfukoni huna hata pesa,lakini unapokuwa na kadi yako ya bima ya afya unakuwa na uhakika wa kupata matibabu na dawa"alisema Odhiambo

Odhiambo aliwaomba wajumbe hao kujiunga na Bima ya Afya kwa uhakika wa matibabu pia ilani ya Chama Tawala inaelekeza wananchi kujiunga na Bima ya afya.

"Mkiwa kama wasimamizi wa ilani ya chama tawala niwaombe mjiunge na utaratibu wa Bima ya Afya, Kwani sasa wananchi wanawigo mpana wa kujiunga na Bima ya afya kupitia NHIF au CHF iliyoboreshwa"alisema Meneja

Alisema kuwa upande wa NHIF zipo huduma mbalimbali za bima kama Bima kwa watumishi, Ushirika Afya kwa Wakulima, Bima kwa Watoto na Wanafunzi,Vile vile hivi karibuni NHIF itaanzisha mpango wa Bima ya Afya kwa mtu mmoja mmoja.

Odhiambo aliongeza kwa kusema kuwa kujiunga na Bima ya Afya ni kuwekeza kwenye afya yako ili kukabiliana na changamoto ya ugonjwa kuja bila hodi na gharama kubwa za tiba. 

Amewaomba wajibu hao kupitia kauli yao ya uchungu wa mwana aujuaye mzazi kwa kujiunga na Bima ya afya sambamba wananchi wengine kujiunga na Bima ya afya.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Chato Acheny Mwinshehe Maulidi amewaambia wajumbe hao umuhimu wa Bima ya Afya akitolea mfano wa jinsi ambavyo yeye na familia yake wamekuwa wanufaika wa NHIF. 

Katibu huyo ameahidi kuwa balozi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya.

TAMISEMI QUEENS YAICHAPA MAKUTUPORA JKT MAGOLI 34 KWA 27

0
0
Na Mathew Kwembe, Dodoma

Michuano ya netiboli ligi daraja la kwanza imeendelea tena leo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo katika mchezo wa kusisimua uliochezwa jioni umeshuhudia timu ya netiboli kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ‘TAMISEMI QUEENS’ ikiwachapa maafande wa JKT Makutupora kwa magoli 34-27.

Mchezo huo ulilazimika kusimama kwa takribani dakika 40 baada ya kundi kubwa la nyuki kuvamia uwanja huo na kusababisha taharuki kwa wachezaji na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.

Magoli yote ya TAMISEMI QUEENS yalifungwa na mfungaji hodari wa timu hiyo Lilian Jovin, ambaye kutokana na umahiri aliounyesha katika ligi hiyo anatarajiwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo, timu ya TAMISEMI QUEENS ipo nafasi ya tatu baada ya kupata jumla ya pointi 12 katika michezo 8 iliyocheza ambapo timu hiyo ilifanikiwa kushinda michezo 6, na kufungwa michezo miwili.

Wanaoongoza ligi hiyo ni timu tishio ya JKT Mbweni iliyo na pointi 14 baada ya kucheza michezo 7 na kufuatiwa na Jeshi Stars ambao nao wana pointi 14, na nafasi ya tatu na ya nne zikichukuliwa na TAMISEMI QUEENS na Jiji la Arusha, huku timu zote zikiwa na pointi 12 isipokuwa timu ya TAMISEMI QUEENS ikiwazidi jiji la Arusha kwa wingi wa magoli ya kufunga.

Akizungumzia michuano hiyo Kiongozi wa TAMISEMI QUEENS Rose Makange alisema kuwa timu yake ipo vizuri kwani kufikia sasa imeshinda michezo 6 kati ya 8 waliyokwishacheza na akaahidi kufanya vizuri katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya wanaoongoza ligi hiyo JKT Mbweni.

Bi Makange ameongeza kuwa timu yake haiwaogopi timu yoyote na akawataka JKT Mbweni ambao watakutana nayo siku ya jumamosi tarehe 7 septemba, wajiandae kwa kipigo kitakatifu kutoka kwa timu yake.

Hata hivyo kiongozi huyo wa TAMISEMI QUEENS amelalamikia kukiukwa kwa kanuni za uendeshaji wa ligi hiyo kufuatia baadhi ya timu kuchezesha zaidi ya wachezaji watatu wa kutoka nje ya nchi kinyume na kanuni zinazotaka timu hizo kutochezesha zaidi ya wachezaji watatu.

Bi Makange amewataka viongozi wa chama cha mchezo wa pete Tanzania (Chaneta) kutofumbia macho ukiukwaji wa kanuni hizo, na akataka chama hicho kutenda haki kwa kutoa adhabu kwa timu zilizokiuka kwa makusudi kanuni hiyo ili ligi hiyo impate mshindi halali.

Dkt. Abbasi aipongeza Muhimbili kwa kuboresha huduma

0
0
Msemaji Mkuu wa Serikali akiwa katika wodi ya watoto wanaohitaji uangalizimaalumu (PICU) wenye umri wa siku 30 hadi miaka 14.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya MNH wakimsikiliza Msemaji Mkuu waSerikali.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (wa pili kushoto) akiwasili MNH,wa pili kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Dkt. Hedwiga Swai.Wengine ni wajumbe wa Tamati Tendaji ya Chama cha Maafisa MawasilianoSerikalini (TAGCO).
******************

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ameupongeza Uongozi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika utoaji huduma kwa wananchi.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali
akiambatana na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Chama cha Maafisa
Mawasiliano Serikalini (TAGCO) ili kuhamasisha utendaji kazi wa kitengo
cha Habari na Mawasiliano kwa Umma hospitalini hapa.

Katika ziara hiyo Dkt.Abbassi ameridhishwa na utendaji kazi wa kitengo
Habari na Mawasiliano kwa Umma na pia ameupongeza Uongozi wa
Hospitali kwa kutoa ushirikiano mkubwa unaokiwezesha kitengo hicho
kufanya kazi kwa ufanisi.

“Natoa pongezi kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
ushirikiano mkubwa mnaoutoa kwa kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa
Umma, nimemsikia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji anasema Mkuu wa kitengo
hiki anahudhuria vikao vyote vya Menejimenti, Bodi ya Wadhamini na pia
kitengo kinatengewa bajeti ili kufanya kazi na sisi huko nje tunaona utendaji
kazi wake,”amesema Dkt. Abbasi.

Awali akimkaribisha Dkt. Abbasi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Dkt.
Hedwiga Swai, amesema Hospitali imeboresha huduma kwa kiwango
kikubwa ikiwemo kuanzishwa kwa huduma mpya ya upandikizaji figo,
upandikizaji vya kusaidia watoto kusikia na tiba kwa njia ya radiolojia.

Dtk. Swai amesema tangu kuanzishwa kwa huduma hizo, wagonjwa 47
wamepandakizwa figo, watoto 30 wamepandikizwa vifaa vya kusaidia
kusikia ambapo wananchi 450 wamenufaika na huduma ya tiba radiolojia.

Aidha amesema Hospitali imeboresha kwa kiwango kikubwa miundombinu
ya kutolea huduma ikiwemo kuongeza vitanda vya ICU kutoka 25 hadi
vitanda 80, vumba vya upasuaji kutoka 13 hadi 20, kuongeza mashine za
kusafisha damu kutoka 17 hadi 42 na ununuzi wa mashine za kisasa za
radiolojia ikiwemo CT-Scan na MRI pamoja na kuongeza kiwango
upatikanaji wa dawa kwa asilimi 95.

Dkt. Swai amesema MNH ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya
kuanza kupandikiza ULOTO (bone marrow transplant) kwa wagonjwa
wenye saratani ya damu.

Dkt. Abbasi akishirikiana na Viongozi wa Kamati ya TAGCO, yupo kwenye
ziara maalum ya kutembelea baadhi ya taasisi na idara za Serikali ili
kuangalia hali ya utendaji kazi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano
Serikalini.

DC MURO AGUSA MAISHA YA WALEMAVU

0
0
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa kushirikiana na Taasisi ya walemavu wa Uti wa mgongo KASI imetoa misadaa mbalimbali kwa walemavu wenye matatizo ya Uti wa Mgongo walioko katika wilaya ya Arumeru

Dc Muro ambae ameamua kuonyesha juhudi binafsi katika kuwasaidia watu wenye ulemavu amesema wametoa misaada ya kuanza maisha ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu ili waweze kumudu maisha hatua itakayowasaidia kuwaondoa katika kundi la utegemezi katika familia jambo linalochangia watu kuwanyanyapaa

Misaada iliyotolewa ni vifaa vya kuanzisha biashara ya vifaa vya ujenzi, maji kwa ajili ya mradi wa kuuza maji ya jumla , vifaa vya majumbani zikiwemo chupa za chai , hotpot, mamia ya kuku wa kienyeji kwa ajili ya bishara ya mifugo, mbuzi pamoja na bidhaa mbalimbali

Wakizungumza mara baada ya Dc Muro kukabidhi misaada hiyo, kiongozi wa jumuiya ya watu wenye ulemavu wa uti wa mgongo kwa mikoa ya kilimanjaro na Arusha KASI Ndugu Deogratiua Chami ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu hatua inayowasaidia kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto walizonazo ambapi amesema wao kama KASI wanapambana kuwafikia walemavu wengi zaidi katika ukanda wa kaskazini

Kwa upande wao viongozi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya kichama ya Meru wakiongozwa na katibu mwenezi Comrade Joshua Hungura wamesema jitihada zinaonyeshwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru katika kuyafikia makundi mbalimbali yenye mahitaji maalum ni kielelezo tosha cha utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika kuwahudumia watu wenye ulemavu.

HUDUMA ZA BENKI YA WANAWAKE KUTOLEWA NA BENKI YA TPB PLC

0
0
Na. Farida Ramadhan na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imesema kuwa kwa sasa hakuna Benki ya Wanawake Tanzania baada ya iliyokuwa Benki ya Wanawake kuunganishwa na Benki ya TPB Plc.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Faida Mohammed Bakar, aliyetaka kujua sababu zilizokwamisha uanzishwaji wa Benki ya Wanawake kwa upande wa Zanzibar.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, huduma za iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania zinaendelea kutolewa na Benki ya TPB Plc ambapo imeanzisha dirisha maalum la wanawake katika matawi yake yote yakiwemo matawi ya Unguja na Pemba ili kukidhi mahitaji yao kote nchini.

“Nitoe wito kwa wanawake wa Tanzania watumie akaunti ya Tabasamu iliyopo katika Benki ya TPB Plc ili kunufaika na mikopo yenye riba nafuu bila kulazimika kuwa katika vikundi kama Benki zingine zinavyofanya”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Akaunti ya Tabasamu ilifunguliwa na Benki ya Posta kwa ajili ya Wanawake pekee kama Benki ya Wanawake ilivyokuwa ikifanya na pia inatoa mkopo kwa mwanamke mmoja mmoja kwa lengo la kumuwezesha kufanya shughuli zake za kijasiriamali, kiuchumi na za kijamii kwa maslahi yake na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mhe. Faida Mohammed Bakar, ameipongeza Serikali kwa majibu yake kwa kuunganisha Benki ya Posta na Benki ya Wanawake ili Wanawake waweze kuhudumiwa katika maeneo yote, ambapo awali huduma hizo zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache kutokana na ufinyu wa matawi ya Benki ya Wanawake.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

WATU ZAIDI YA 1,000 KUFAIDIKA NA LUGHA YA KOMPYUTA YA KIAFRIKA

0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akizungumza wakati wa kuzindua wiki ya Lugha ya Kompyuta kwa nchi za Afrika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa programu ya Lugha ya Komyuta kwa nchini za Afrika hasa Tanzania itasaidia watu wengi kulingana na mahitaji yao ikiwa Tanzania kwa sasa tunakampeni ya kuelekea uchumi wa viwanda tunamahitaji makubwa ya kompyuta hivyo programu hii itasaidia watu wengi zaidi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kilimo, elimu na nyanja mbalimbali zinazohitaji matumizi ta teknolojia hasa ya komyuta.

Amesema kuwa COSTECH pamoja na Ubalozi wa Ireland wawahimize watu kugundua na kutumia teknolojia na kuzielewa programu hizo na sio kutumia pekeyake.
Mkurugenzi mwenza wa  Application ya Girls App, Winnie Msamba akizungumza wakati wa ufunguzi wa Programu ya Lugha ya Kompyuta kwa nchi za Afrika, amesema kuwa watu wengi watafaidi sana kutumia lugha za kompyuta ambazo ni za Kiafrika.


 Baadhi ya wadau malilmbali wa teknolojia wakiwa katika uzinduzi wa Programu ya Lugha ya komyuta ya Afrika jijini Dar es Salaam.
 Mkuirugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), DK.Amosi Nungu akizungumza na wadau mbalimbali wa teknolojia jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua programu ya Lugha ya Kompyuta kwa nchi za Afrika amapo amesema kuwa watoto wawe na uwezo wa kujua lugha ya komyuta katika kuelekea uchumi wa Viwanda hapa nchini inahitajika teknolojia ya hali ya juu ili kuleta mawazo mapya ya ukuaji wa uchumi katika nchini za Afrika hasa Tanzania.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock akizungumza mara baada ya kuzindua Programu ya lugha ya Kompyuta kwa nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza umuhimu wa programu ya lugha ya kompyuta kwa nchi za Afrika zitakavyosaidia watu.
Amesema kuwa Lugha ya  Kompyuta inawapa wananchi uelewa wa kuelewa lugha inayotumiwa na waafrika.

KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) YAENDELEA KUFANYA VIZURI KIBIASHARA

0
0
LICHA ya changamoto za kibishara  zilizokuwepo katika kipindi cha mwaka uliopita, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, imeendelea kufanya vizuri kibiashara na kuchangia pato la serikali kupitia kodi sambamba na kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii.



Hayo yamebainishwa katika mkutano Mkuu wa 46 wa  wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo imeelezwa kuwa faida ya kampuni hiyo imeongezeka kwa asilimia 15 na kuwezesha wanahisa wake kupata gawio la shilingi 350 kwa kila hisa.
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Mh. Cleopa Msuya,(katikati) akifafanua jambo katika mkutano wa wanahisa,wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kulia)na Katibu wa bodi,Huruma Ntahena.
Baadhi ya wanahisa wakifuatilia ajenda za mkutano na kushiriki kutoa mapendekezo
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Cleopa Msuya na Mkurugenzi wa TBL, Philip Redman wakiongea na waandishi wa habari.

SACP MISIME ATOA SOMO KWA TAASISI YA KUTOA ELIMU YA AMANI TANZANIA

0
0
 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, SACP David Misime akizungumza na wajumbe wa Taasisi ya Kutoa Elimu ya Amani Tanzania hawapo pichani lengo likiwa ni kuwafundisha wajumbe hao juu ya namana ya kukabiliana na wavunjifu wa amani na namna ya kutatua matatizo yanayoweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii kabla hayajatokea, kikao hicho kilifanyikia eneo la Mbagara wilayani Temeke jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Fimbo Hotel.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, SACP David Misime akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Taasisi ya Kutoa Elimu ya Amani Tanzania njee ya ukumbi wa fimbo hotel na kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Jeshi la Polisi SACP Kiyondo na kulia kwa SACP Misime ni Rais wa Taasisi hiyo Willison George.
(Picha na Jeshi la Polisi)

KAMBI YA KITAALUMA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WENYE UFAULU HAFIFU YAZINDULIWA SIMIYU

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizindua kambi ya Kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne, walimu na wadau wa elimu mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
 Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu (daraja sifuri) katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia waweze kuongeza ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.

Akizindua kambi hiyo Septemba 05, 2019 Mtaka amesema wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu ambayo ni Kiswahili, Kiingereza ,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa kuwafundisha wanafunzi hao kwa moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata alama D na kuendelea katika mtihani wa Taifa.

“Hawa watoto wafundisheni masomo manne, Kiswahili, Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara kwa mara katika siku hizi 60 watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F wapate angalau D nao wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni angalau mtu awe na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa jamii ya Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo husika.

Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju amesema kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa  Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata daraja la kwanza hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo yote.

Aidha, Hinju ameongeza kuwa  kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu kwenye Mtihani ya Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita, ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74 mkoa ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka  2017 ufaulu asilimia 79.8 nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia 82.5  ukashika nafasi ya 9 kati ya mikoa 26.

Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini  wameshukuru kuwekewa kambi hiyo na wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa vema na mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.

“Tunawashukuru viongozi wetu na wazazi wetu kwa kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri kambi hizi zisiishie kwetu ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther Nashoni mwanafunzi shule ya sekondari Bariadi(Bariadi)

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema walimu wamejiandaa vema katika kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu ya kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika  vizuri.

Kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019 ilianza rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.

MIRADI YA NISHATI YAJADILIWA KWENYE MKUTANO WA TUME YA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA UGANDA

0
0
Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, ulioanza Septemba 3 mwaka huu, umehitimishwa jana, Septemba 5 jijini Dar es Salaam; ambapo miradi ya nishati ni miongoni mwa iliyojadiliwa.

Akifunga mkutano huo, ngazi ya Mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, aliwaeleza wajumbe kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda umeendelea kuimarika siku hadi siku kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa katika sekta kadhaa, ambayo ni pamoja na nishati.

“Kwa sasa tunatekeleza miradi kadhaa ya ushirikiano, ukiwemo wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), mradi wa kuzalisha umeme wa maji (megawati 14) wa Kikagati – Murongo, mradi wa umeme wa maji Nsongezi na mingine mingi.”

Katika Mkutano huo wa siku tatu, pamoja na mambo mengine, ulipokea taarifa ya Wizara ya Nishati ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Mkutano wa Pili wa Tume husika, uliofanyika Agosti, mwaka jana, jijini Kampala, Uganda.

Mbali na miradi iliyotajwa awali; Taarifa hiyo ya Wizara ilijikita pia katika masuala ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika bonde la Eyasi Wembere, ujenzi wa bomba la kupeleka gesi asilia nchini Uganda, njia ya kusafirisha umeme ya Masaka – Mutukula – Mwanza, pamoja na miradi mingine ya umeme inayotekelezwa mpakani mwa nchi husika.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Katibu Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Haji Janabi, Kamishna wa Petroli na Gesi Adam Zuberi na baadhi ya maafisa waandamizi wa wizara na taasisi zake, walishiriki mkutano huo.

Aidha, sekta nyingine zilizoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Ulinzi na Usalama; Maendeleo ya Miundombinu na Usafirishaji; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Utalii; Kilimo, Uvuvi na Mifugo; Maji na Mazingira; Afya; Elimu na Mafunzo; Habari; pamoja na Utamaduni.

Mkutano ngazi ya Mawaziri ulitanguliwa na ngazi ya Wataalam Septemba 3, ukifuatiwa na Makatibu Wakuu Septemba 4, mwaka huu.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akizungumza wakati wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza – kushoto) akiwa na wajumbe wenzake kutoka Tanzania, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.   
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati-mstari wa mbele), akiwa na baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na wajumbe wengine kutoka Tanzania, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.  

  Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini na Wizara nyingine mbalimbali, wakiwa katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa kwanza kulia-mstari wa mbele), akiwa na wajumbe wenzake kutoka nchi hiyo, katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam. 
Wajumbe wakiwa katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, Ngazi ya Mawaziri, uliofanyika Septemba 5, 2019 jijini Dar es Salaam.  

UMMY: SERIKALI HAINA NIA YA KUZIBANA NGOs

0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na watendaji wake katika kikao cha kujadili uboreshaji wa mifumo ya utoaji huduma kwa wadau wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Maendeleo ya jamii) Dkt. John Jingu akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(kulia) kuhusu Utekelezaji wa kazi ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao cha Waziri na Watendaji wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Zainabu Chaula akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) kuhusu uandaaji wa mfumo utakaosaidia kujua kazi na miradi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao cha Waziri na Watendaji wa Wizara kilichofanyika jijini Dodoma.
 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(mbele mwenye kiremba cheusi) kuhusu uhuishaji wa Mashirika yaliyokuwa nje ya Sheria katika zoezi lililofanyika nchini mwezi uliopita katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. 
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Ponsiano Mawazo akielezea kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(mbele mwenye kiremba cheusi) jinsi ya Mfumo wa Usajili na Uratibu wa NGOs utakavyokuwa unafanya kazi na kurahisha wadau kupata huduma ya Usajili na uwasilishaji wa ripoti mbalimbali wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata keki katika kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa kwake jana jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haina nia ya kuyabana Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kutekeleza majukumu yao bali inaweka utaratibu wezeshi wa kuyaratibu Mashirika hayo ili yaweze kuleta tija katika maendeleo ya nchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati alipokutana na watendaji wake kutoka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na Idara Kuu ya Afya kwa lengo la kujadiliana na kupata namna bora ya kuboresha huduma ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha inaweka mazingira bora ya kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa ufanisi zaidi ili yaweze kuleta matokeo chanja katika jamii hasa matokeo yanayoonekana na kugusa hali ya maisha ya watu masikini tofauti na kuendesha semina na warsha kama ilivyozoeleka hapo awali.

Amesisitiza kuwa fedha za miradi zinazotumika katika miradi inayotekelzwa na NGOs nchini zitumike kama ilivyopangwana sehemu yenye uhitaji na sio kupeleka miradi sehemu moja na sehemu nyingine kukosa miradi ya maendeleo kutoka kwa wadau wa NGOs.

Waziri Ummy amesema kuwa ni muhimu kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwekeza fedha kwa kufuata vipaumbele vya Taifa ili kuisaidia Serikali katika kuhakikisha jamii inapata maendeleo.

“Kama Wizara tulishataka kufanya maadhimisho mkoa wa Katavi lakini hakukuwa na mdau hata mmoja eneo hilo anayejishughulisha na mradi wa kimaendeleo” alisisitiza Mhe.Ummy

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa watahakikisha wanaweka mazingira mazuri ya wadau kufanya kazi zao kwani wadau hawa ni kundi muhimu katika maendeleo ya nchi yetu katika kutekeleza majukumu ya kitaifa.

Amesisitiza kuwa kumekuwa na changamoto katika kufanya kazi na wadau wa NGOs hivyo Serikali inatengenza mazingira mazuri ya kutatua changamoto hizo ili kuendelea kufanya kazi na wadau hao katika ulekeo mzuri.

Naye Katibu Mkuu Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa Serikali inafuatilia na kujua wadau wa maendeleo wanafanya kazi wapi imeamua kuja na mfumo wa Wadau Portal utakaosaidia kuonesha wadau walipo nchini na wanatekeleza miradi ipi na wapi.

Ameongeza kuwa dhamira ya juhudi zinazofanywa na Wizara ni kuhakikisha kuwa panakuwepo miongozo na mifumo ya utoaji huduma kwa wadau itakayosaidia kuratibu, kusimamia na na kubaini kwamba ni kwa kiasi gani wadau wa maendeleo wanachangia katika juhudi za Serikali za kukuza maendeleo na ustawi wa maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Mkoani Songwe katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

0
0

 Wananchi wafurika katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.

 Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe. 
 Wananchi wakisoma kitabu cha Muongozo wa Mawasiliano cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
 Wananchi wakipata huduma za usajili wa vitambulisho vya Taifa katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa vipeperushi na vitabu  mbalimbali vya Elimu ya mawasiliano kwa Wananchi mkoani Songwe katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada inayofanyika katika Soko la Mlowo mkoani Songwe.

WAKAZI wa Mkoa wa Songwe  na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.


Mkuu wa nyanda za Juu Kusini wa TCRA na sio Kaskazini  Mhandisi  Asajile John amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe katika Soko la Mlowo na viunga vyake  kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 

John amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

John amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

John amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi John amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

John amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema John
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images