Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA KILIMO AFANYA MAZUNGUMZO NA MTENDAJI MKUU KAMPUNI YA INNOVATION AFRICA JIJINI TEL AVIV

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 4 Septemba 2019 Jijini Tel Aviv nchini Israel akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 4 Septemba 2019 Jijini Tel Aviv nchini Israel akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 6. Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Balozi Job Daud Masima.






Na Mathias Canal, Telaviv-Israel

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 4 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari.

Katika kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Jijini Tel Aviv nchini Israel, Mhe Hasunga amemualika Bi Sivan kutembelea nchini Tanzania ili kuwekeza kadhalika kusaidia katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Alisema kuwa kampuni hiyo inatakiwa kuongeza mshikamano na serikali ya Tanzania ili kuendelea kutatua sehemu ya matatizo ya wananchi huku kuimarisha mpango wao wa kutoa suluhisho la Israeli na ujuzi kwa wale wanaohitaji kuishi katika vijiji vya Kiafrika. 

Waziri Hasunga amemuhakikishia Bi Ya’ari kuwa Tanzania ni nchi nzuri katika uwkeezaji na sehemu salama ya kuishi huku serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiendeleza juhudi za kuboresha maisha ya watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi.

Hata hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi za Afrika katika sekta ya nishati ya jua ikiwa ni pamoja na mchango wao katika kutekeleza miradi ya maji safi, na Kusaidia vituo vya watoto yatima.

Alisema kuwa Tanzania ni sehemu salama na imara katika uwekezaji, kwani serikali imeanzisha kituo cha uwekezaji (TIC) ambacho ni Taasisi ya msingi ya serikali yenye jukumu la kuratibu, kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji.

Tanzania inaongoza kwa uwekezaji katika Afrika Mashariki na imeweza kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda dola za Marekani bilioni 0.7 na Kenya dola za Marekani bilioni 0.67. “Kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuvutia uwekezaji nchini, hali ya uwekezaji imeimarika ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha kuwa Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki

Taarifa ya Uwekezaji ya Dunia (World Investment Report) ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imebainisha kiasi hicho kikubwa cha uwekezaji huku Taarifa nyingine ya“The Africa Investment Index (AII) 2018” inaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 za Afrika katika kutoa fursa za masoko na vivutio vya uwekezaji.”

Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovation Africa Bi Sivan Ya’ari akizungumza katika kikao kazi hicho ameridhia ombi la Waziri Hasunga la kuongeza uwezekano wa kuisaidia Tanzania na kusema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa atawasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuainisha maeneo ya uwekezaji.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo katika ziara ya kikazi ya siku sita nchini Israel ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania

MABONDIA NA VIONGOZI WA NGUMI NCHINI WATEMBELEA BUNGE

$
0
0
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson akifurahia jambo na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Bigwa wa Dunia wa WBO Asian Pacificc (wa tatu kulia) alipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na Kushoto ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi Bw. Joe Anea.
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Watatu Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson (katikati) akizungumza na Mabondia na Viongozi wa Ngumi walipotembelea Bunge Jijini Dodoma leo. Wakwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

PICHA NA BUNGE

WATAALAM KUENDELEA KUSHAURI SERIKALI KUHUSU SEKTA YA MELI NCHINI

$
0
0
Bw. Julius Nguhulla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kulia ni Joel Uronu Katibu wa Chama cha Mawakala wa Meli (ASAA). 

............................................................

MBOBEZI wa Kimataifa katika shughuli za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli ambaye pia ni Mtanzania pekee kati ya wawili waliopo Tanzania wenye ubobezi wa aina yake aliyepo kwenye bodi ya watalaamu wa biashara ya usafirishaji wa mzigo kwa njia ya meli Duniani( ICS,) Julius Nguhulla(FICS) amesema ataendelea kumshauri Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kuhusu sekta ya meli nchini kwa maslahi ya Watanzania wote.

Nguhulla amesema Juni 3 mwaka huu wa 2019 kwa nia njema alimuandikia barua ya kumpongeza Rais wetu kwa kazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwani pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Meli Tanzania(TASAC)ambapo pia aliomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.

Hata hivyo alitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli na bandari.

Nguhulla ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Salaam wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo amesisitiza amewahi kumshauri Rais Magufuli kuhusu sekta ya meli kupitia barua yake hiyo aliyomuandikia .

"Tangu mwaka 2016 nimekuwa nikijishughulisha na kazi za usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli.Mimi ni miongoni mwa watu Duniani waliokwenye Bodi ya wataalumu wa biashara ya usafiri wa mizigo kwa njia ya meli yaani shipping.

"Kutokana na ubobezi wangu katika usafiri wa mizigo kwa njia ya meli nimekuwa nikishiriki kutoa ushauri wa kitaalamu wa mambo ya meli na bandari ndani na nje ya Tanzania.Kupitia ubobezi wangu tarehe 03.06.2019 niliandika barua kumpongeza Rais wetu kwakazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa TASAC.

"Kadhalika , nilimwomba Rais aishauri mamlaka husika kuhusu umuhimu watozo za delivery order na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa yaani kodi.

"Hata hivyo nilitoa historia pamoja na umuhimu wa waraka huo na jinsi unavyopaswa kuzingatiwa kitaalamu ili kuendelea na ufanisi wa biashara ya meli,"alisisitiza Nguhulla.

Alifafanua zaidi kwa kutumia ubobezi wake katika sekta ya bandari na meli hatasita kutoa ushauri kwa wakuu wa nchi na hasa Rais Magufuli ambaye amekuwa mzalendo kwa nchi yake,hivyo kuna kila sababu za Watanzania wa kada mbalimbali akiwemo yeye kumshauri kwa kufuata taratibu za nchi bila kuvunja sheria.

Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumuandikia barua Rais, amesikitishwa na namna ambavyo mmoja ya wanaharakati kumtusi na kutoa maneno ya kejeli dhidi yake.

"Agosti 26, mwaka 2019 mtu mmoja alinitukana kwa kutumia moja ya televisheni nchini na kusema mimi nilimwandikia barua kumshauri Rais kuhusu waraka unaoitwa delivery order na tozo zake.Mtu huyo alinichafua na kunitukana kwa kutaja jina langu kwa kudai kwamba kwa uamuzi huo mimi nilioufanya mimi ni mjinga na mpuuzi kabisa na sijui chochote,.

"Waandishi wa habari ni kweli nilimwandikia barua Rais nikimshauri kuhusu mada kama nilivyotaja hapo juu nikiwa na haki ya kumshauri Rais wangu kwa lengo la maendeleo ya Taifa langu lakini, hata hivyo nimedhalilishwa kwa kutukanwa kama nilivyoainisha hapo juu huku nikitajwa Jina langu,"alisema.

Alifafanua kuwa ameambiwa amemdanganya Rais wetu kuwa shipping ni taaluma yake na kwamba hajawahi kufanya kazi ya aina hiyo popote.Hivyo alisema kwa sababu upotoshaji na udhalilishaji huu ulifanywa kwenye chombo cha habari umma wa watanzania ukasikia na yeye ameona atoe sikitiko lake la kutukanwa mbele ya Umma wa Watanzania.

Pia alisema amejitokeza hadharani kukanusha mbele ya umma wa watanzania kwamba yeye hakumdanganya Rais kwamba shipping ni taaluma yake,hivyo aliamua kutoa ufafanuzi hatua kwa hatua kuhusu shughuli ambazo amezifanya.

Nguhullla amewaambia waandishi wa habari kuwa anayo shahada ya heshima kutoka nchini Uingereza kuhusu mambo ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli yaani Shipping baada ya kusomea kwa miaka mitano na kuingia kwenye bodi ya wataalamu wa shiping wa dunia ambapo chao cha juu cha kitaalam kwenye masuala ya biashara ya meli ni cha mtu anayeitwa FICS ambapo kwa Tanzania imefanikiwa kumtoa mtu mmoja ambaye ni yeye kati ya watu 2000 duniani.

Pia anayo Masters ya Biashara ya meli yaani MBA in shipping aliyoisomea Cyprus na sasa anaendelea na utafiti( Global Business University).

Alisema anao uzoefu wa miaka 15 ya kazi za meli( uwakala wa meli) na amewahi kufanya kazi na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC wa sasa kwa muda wa miaka mitatu akiwa mwajiri wake na kuongeza kila mwaka huwa anaenda nje ya Tanzania kwa ajili ya mikutano ya shipping pamoja na kufundisha.

"Sisemi haya kujisifu ila namshukuru Mungu maana yeye peke yake ndio wakusifiwa. Kadhalika , Serikali yangu ya Tanzania imekuwa ikinihusisha sana na shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano ya kuelimisha kuhusu shipping na mengineyo. Ipo siku nilitoa somo nikiwa na CEO wa TICTS tulipoalikwa na serikali kueleza umuhimu wa Teknolojia katika Port Operations. Serikali imewahi kuniomba kuwafanyia interview wakurugenzi waliokuwa wanataka kuajiriwa kwenye ofisi ya Serikali inayohusika na shipping.

"Nimewahi kuombwa na TRA kufanya mafunzo kwa siku mbili katika kitengo cha enforcement kuhusu Bill of Lading. Pia Januari mwaka 2018 nilitoa Presentation Tanzania ikijumuisha watu wa Serikali , na wamiliki wa meli wa mataifa mbalimbali , idadi ya watu ikiwa ni 200 kuhusu matumizi ya bill of leading, manifest na mengine mengi,"alisema.

Alisisitiza bila uzoefu wake na taaluma aliyonayo Serikali yake isingempa heshima kama hiyo ambayo ameianisha na kumuomba mtu asitumie cheo chake ambacho amepewa na Mungu kuwatumikia watanzania kwa kutukana watu na taaluma zao.

"Namheshimu sana mtu huyu na nitaendelea kumheshimu na nina msamehe maana umri wake kwangu ni kama baba yangu. Na haya niliyosema si kwamba namshambulia ila naeleza ili Umma ufahamu kuhusu mimi na kupuuza upotoshaji uliofanywa dhidi yangu na heshima ya taaluma yan,"alisema Nguhulla.

Alisisitiza watanzania wanayofursa sawa ya kumshauri Rais pasipo kuvunja sheria na kwamba kama wameamua kuzungumzia maslahi yaTaifa ,basi waendelee na mtazamo huo huo badala ya kuhamia katika maslahi binafsi.

WANANCHI WILAYANI KASULU WAZIOMBA TAASISI ZA KIFEDHA KUONGEZA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA KIBENKI

$
0
0
Baadhi ya wananchi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameziomba taasisi mbalimbali za kifedha kuongeza vituo vya kutolea huduma za kibenki katika maeneo ya vijijini ili kupunguza changamoto ya wafanyabiashara kuvamiwa na kuporwa fedha zao pale wanaposafiri na fedha kwenda kununua bidhaa
mbalimbali hasa nafaka.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa biashara na wateja wa benki ya NMB wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wananchi hao walisema kuwa kumekuwepo na matukio ya mara kwa mara ya wafanyabiashara kuvamiwa na kunyang’anywa fedha zao jambo walilodai kuwasababishia usumbufu na kushindwa kufanya biashara kutokana na kuwepo kwa vitendo hivyo.

Bi.Emmakulatha Mazina ambaye ni mfanyabiashara wilayani humo alisema uwepo wa taasisi za kifedha katika maeneo ya vijijini itasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha na kukuza biashara hasa kutokana na baadhi ya wakulima na wanunuzi wa mazao wakifanya biashara kwa hofu ya kuvamiwa, huku pia wakiomba serikali na wadau wengine wa maendeleo kutoa elimu kwa wananchi wa vijijini juu ya namna bora ya kuhifadhi fedha kwenye mabenki ili kuepuka hasara zisizokuwa za lazima zinazoweza kujitokeza.

“Wafanyabiashara kusafiri na pesa kwa sasa ni hatari sana katika maeneo yetu, unakuta mtu anaenda kijijini kununua mahindi au mihogo na hata mazao mengine akiwa na pesa mikononi, majambazi wakijua tu anatafuta bidhaa wanaanza kupanga njama za kumvami”alisema.

Aidha wafanyabiashara hao waliipongeza benki ya NMB kwa kutoa huduma za kibenki katika maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma na kuomba benki hiyo kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wake pamoja na kuona haja ya kutoza viwango vya riba za mikopo kwa kuzingatia hali ya kipato cha maeneohusika.

Pia waliiomba benki hiyo kuharakisha mchakato wa utoaji mikopo mikubwa kwa wateja kwa kuwaruhusu mameneja wa matawi kufanya tathimini na kumuidhinisha mteja kukopeshwa mkopo mkubwa tofauti na ilivyo sasa ambapo mteja hulazimika kusubiri majibu kutoka ngazi ya kanda na makao makuu ya ofisi za benki hiyo hali waliyosema imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwao.

Kwa pande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse alisema benki hiyo inaendelea kutatua changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha malengo ya benki hiyo kuwahudumia wananchi yanafanikiwa kama ilivyokusudiwa.

Aidha alisema kuwa benki hiyo imeanza utaratibu wa kushusha madaraka ya kutoa mkopo hadi bilioni moja kwa mameneja wa benki ngazi ya tawi ili baada ya kupokea maoni kutoka kwa wateja wake katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tunajaribu kuweka mambo sawa yakiwemo ya kisheria ili kujaribu kulegeza vigezo na masharti, lakini pia tuna mikopo ya aina nyingi mfano unahitaji kukopa milioni sitini za kujenga kiwanda, hapo lazima taratibu zifanyike hata kuanzia ngazi ya chini hadi kwenye bodi yetu ya wakurugenzi na wao ndio wenyemamlaka ya kuruhusu mkopo huo utolewe”alisema meneja huyo.

Awali akiwasilisha mada katika mkutano huo mshauri wa masuala ya kibiashara kutoka kampuni ya TRUEMAISHA TRAINING COMPANY Bwana Erick Chrispin ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni hiyo aliwapongeza wafanyabishara wa wilaya ya Kasulu kuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wanaofanya vizuri katika biashara zao huku akiwashauri kuwa makini katika kufanya biashara kwa kutumia mbinu za kitaalamu ambazo zitawasaidia kuepuka kupata hasara na kuona biashara kama mzigo.

Bidhaa ya unga wa Ngano ya AZAM sasa kupatikana katika vifungashio vipya

$
0
0


Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Ahmed Jaruan, wakionyesha waandishi wa habari muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Said Bakhresa Group, Hussein Sufian akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa muonekano mpya wa vifungashio vya unga wa ngano wa Azam ujulikanao kama Ngano Bora, ikiwa ni mkakati wa kulinda ubora na kutambulisha bidhaa zake kwa wateja.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo



Uongozi wa kampuni ya kutengeneza vyakula inayomikiliwa na makampuni ya Said Salim Bakhresa &Ltd, inayozalisha unga bora wa ngano wenye jina la kibiashara la Azam, imetangaza kubadilisha muonekano wa bidhaa yake maarufu ya unga wa ngano unaojulikana kwa chapa ya Ngano Bora.

Muonekano mpya wa kifungashio (mfuko) wa bidhaa hii umeboreshwa ili kuwapatia wateja wake kuitambua kwa urahisi na kuweza kuitofautisha na bidhaa zenye vifungashio vinavyofanana nayo.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Hussein Sufian , amesema kumekuwepo na wazalishaji ambao wanaiga na kubadilisha rangi za muonekano wa bidhaa zao zifanane na bidhaa za AZAM, hali ambayo imekuwa ikiwachanganya wateja kwenye masoko kutambua bidhaa za kampuni hiyo.

Alisema kutokana na kubadilisha vifungashio, wateja wa Ngano Bora, unaotengenezwa na AZAM kwa sasa wataweza kutambua bidhaa hizo kwa urahisi pia ametoa tahadhari kwa wazalishaji wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiiga muonekano wa bidhaa za kampuni hiyo kuacha kufanya hivyo kwa kuwa wanavunja sharia na tayari wameishatoa taarifa kwa mamlaka mbalimbali,watakaokamatwa kwa kufanya udanganyifu huu watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha kampuni imetoa tahadhari kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia vifungashio vya bidhaa za kampuni hiyo zilizotumika na kujaza bidhaa nyingine na kuziuza kwa wateja kama bidhaa za kampuni ya AZAM.

Sufian alisema kampuni inapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa itaendelea na ubunifu na uzalishaji wa bidhaa zenye kiwango cha juu ubora kukidhi matakwa ya wateja wote nchini na nje ya nchi.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na ujumbe kutoka China Academy of Building Research, ambao umekuja kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wa awamu ya pili, leo Septemba 4.2019. Mradi huo ni miongoni mwa matunda ya ziara ya Waziri Mkuu aliyoifanya nchini China Oktoba 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka China Academy of Building Research, ambao umekuja kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wa awamu ya pili, leo Septemba 4.2019. Mradi huo ni miongoni mwa matunda ya ziara ya Waziri Mkuu aliyoifanya nchini China Oktoba 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

HAYDOM YAPATA MASHINE MPYA YA CT SCAN

$
0
0
Mkurugenzi wa tiba wa hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, Dkt Emmanuel Nuwass akizungumza na waandishi wa habari, baada ya mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi wa mionzi CT Scan kufikishwa hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa tiba wa hospitali ya rufaa ya Haydom ya Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Dkt Emmanuel Nuwass (kushoto) akizungumza na madaktari wenzake.
Mkurugenzi wa tiba wa hospitalivya rufaa ya Haydom Dkt Emmanuel Nuwass akizungumza na madaktari wenzake wa hospitalini hapo baada ya kupokea mashine mpya ya mionzi ya CT Scan.

*********************

HOSPITALI ya rufaa ya Kilutheri ya Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, imenunua mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi ya mionzi (CT Scan) ambayo kwa miaka miwili hakukuwa na huduma hiyo baada ya iliyokuwepo awali kuharibika. 

Hospitali hiyo kwa mwaka uhudumia zaidi ya wagonjwa 105,296 wa nje na 14,020 wa ndani wa mikoa sita ya Manyara, Arusha, Tabora, Singida, Dodoma na Simiyu. 

Mkurugenzi wa tiba wa hospitali ya Haydom Dk Emmanuel Nuwass alisema sh800 milioni zimetumika kuinunua Ujerumani na kuisafirisha mashine hiyo ya kisasa hadi hospitalini hapo. 

Dk Nuwass alisema awali mashine waliyokuwa nayo iliharibika miaka miwili iliyopita hivyo kusababisha wagonjwa wengi kukosa huduma ya vipimo hivyo. 

Alisema kutokana na ukosefu wa mashine hiyo iliwabidi watu wa eneo hilo kufuata vipimo hivyo takribani kilomita 400 hadi 600 kwenye hospitali za kanda za KCMC Kilimanjaro na Bugando Mwanza. 

“Mashine hiyo ya kisasa itasaidia wagonjwa wengi hasa wasio na kipato kuweza kupata vipimo kwenye eneo la karibu na tunatarajia kumuomba Waziri wa Afya Ummy Mwalimu atuzindulie hivi karibuni,” alisema Dk Nuwass. 

Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, Catherine Faustine alisema wananchi wengi wameshindwa kupata huduma hiyo kutokana na umbali mrefu wa kufuata katika hospitali nyingine kubwa. 

“Kuna baadhi hata wamefariki kwa sababu hawana fedha za kwenda kupimwa katika hospitali za mbali ikiwemo KCMC Moshi au Muhimbili Dar es salaam, tunashukuru kwa kupata mashine hii,” alisema. 

Mtaalamu wa mionzi wa hospitali hiyo Paul Fissoo alisema mashine hiyo mpya ina uwezo mkubwa zaidi tofauti na ile ya awali iliyoharibika. 

Hospitali ya Kilutheri ya Haydom inayomilikiwa na KKKT Dayosisi ya Mbulu ilianzishwa na wamisionari wa Norway mwaka 1955 ikiwa na vitanda 50 na sasa ina vitanda 420.

Wagonjwa wanaopata huduma hospitali hiyo wanatoka wilaya za Mbulu, Hanang na Babati mkoani Manyara, Karatu mkoani Arusha, Igunga mkoani Tabora, Iramba na Mkalama mkoani Singida, Kondoa mkoani Dodoma na Meatu mkoani Simiyu.

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA,SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa utekelezaji wa mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/09/2019. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa utekelezaji wa mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/09/2019. 


Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Radhiya Rashid Haroub alipokuwa akisoma wa utekelezaji wa mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg. Khalid Abdallah Omar. [Picha na Ikulu.] 03/09/2019. 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Said Juma Ahmada alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Manispaa ya Mji wa Zanzibar wakati wa mkutano wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ,[Picha na Ikulu.] 04/09/2019.

Wimbo wa JAMAFEST2019 Wampa Dili Peter Msechu

$
0
0
Wimbo mpya wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msanii Peter Msechu, umeteuliwa kuwa wimbo maalum katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Masharikilinalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Septemba 21-28 mwaka huu katika Uwanjawa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za wimbo wa JAMAFEST2019 kuteuliwa kuwa wimbo rasmi wa Tamasha hilomaarufu Afrika Mashariki zilifahamika baada ya Msechu kuandika katika ukurasawake wa Instagram akimshukuru Mungu kwa wimbo wake huo kupitishwa.

Akiongea baada ya kupigiwa simu kutoa ufafanuzi juu ya kuchaguliwa kwa wakekuwa kuwa maalum katika tamasha la JAMAFEST, Msechu alisema kuwa alitungawimbo huo baada ya uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezokuwaomba wasanii mbalimbali kutunga wimbo ambao ungetumika kama wimbomaalum wa Tamasha.

“Wasanii tupo wengi sana kwa mimi kupata fursa hii ya kuimba katika ufunguzitamasha hili kubwa la JAMAFEST kwangu ni heshima kubwa sana. Tulikuwa wasaniiwengi tuliotunga nyimbo kwa ajili ya Tamasha lakini wimbo wangu umechaguliwani furaha kubwa”, alieleza Msechiu.

Amesema kwa sasa anaandaa video ya wimbo huo ili uweze kutumika kuhamasishawatanzania na watu wa Afrika Mashariki kushiriki katika Tamasha ambalo lengo lakudumisha uridhi wa utamaduni, Sanaa za mikono na ubunifu, biashara na kukuzaAkiongea kuhusiana na Wimbo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST, Bi. Joyce Fissoo alisema kuwa mchakato wa uteuzi wa wimbo rasmi kwa ajili ya Tamasha la JAMAFEST haukuwa rahisi kwani kulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na wasanii wengi wakujitokeza na kufanya utunzi wawimbo kwa ajili ya tamasha .

“Mchakato wa kupata wimbo wa Tamasha ulikua mgumu kutokana na wasaniikujitokeza na baada ya kusikiliza nyimbo zote ndipo Sekretarieti ya Maandalizi yaTamasha inayoundwa na Wajumbe kutoka nchi sita wanachachma wa Jumuiya yaAfrika Mashariki ikauchagua wimbo wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msechu kuwandio wimbo wa tamasha”, alieleza Bi. Fissoo.

Tamasha la JAMAFEST ni tamasha lililopitishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya yaAfrika Mashariki ili kuenzi na kulinda utamaduni wa makabila ya Afrika Mashariki.Tamasha hili hufanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi wanachama ambapomwaka huu tamasha hilo litafanyika nchini Septemba 21-28 katika Uwanja waTaifa.

HALMASHAURI JIJI LA ARUSHA,WADAU WAENDELEZA KAMPENI YA TALII KASKAZINI

$
0
0
Na Jusline Marco-Arusha

Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii imeendelea kuendeleza kampeni ya Talii Kaskazini kwa kushirikisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha School kwa kutembelea makumbusho ya elimu ya viumbe na makao makuu ya jiji la Arusha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa kutangaza utalii wa ndani Kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani kwa kujumuisha Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Tanga na Manyara ambapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kujifusa historia ya jiji la Arusha.

Afisa Utalii jiji la Arusha Michael Ndaisaba amesema kuwa kampeni hiyo ambayo imeanza katika jiji la Arusha kwa kuhamasisha wanafunzi licha ya kuwa ni sehemu yao ya mafunzo ni wadau wakubwa wa utalii wa ndani katika jamii.

Ndaisaba ameongeza kuwa kampeni hiyo pia imelenga kukuza mahusiano ya taasisi zinazohusika na utalii na zitakazoshiriki kutekeleza mkakati wa vivutio vya utalii kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini ili kuweza kuwekeza kwenye utalii kwa gharama nafuu na rahisi kufikika.

Sambama na hayo ameeleza melengo mengine ya kampeni hiyo ni kukuza utamaduni kwa vijana kupenda kutalii na hatimaye kuongeza idadi ya watalii wa ndani ifikapo mwaka 2021.

Vilevile amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini wakiwemo Tanzania Tourist Board(TTB),TANAPA na TAWA walengwa wa mkakati huo ni wakazi wa Kaskazini mwa Tanzania wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo bila kuwasahau wananchi wa kawaida,taasisi za fedha,vikundi mbalimbali vya kijamii pamoja na wafanyabiashara ambapo kauli mbiu katika kampeni hiyo ni UTALII WA NDANI UNAANZA NA WEWE,TWENDE TUKATALII.
 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha School walipotembelea Makumbusho ya elimu ya viumbe jijini Arusha katika kuendeleza kampeni ya Talii Kaskazini
Wanafunzi wa shule ya msingi Arusha School wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya jiji la Arusha wakipewa maelekezo katika kampeni ya Talii Kaskazini

Tuendelee kuliombea Taifa, Ndege yetu imeachiwa -Waziri Jafo

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhe. Selemani Jafo akifungu Mkutano wa Chama cha Madaktari wa
Kikristo Tanzania uliofanyika St. Gasper Jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania Dr. Bwire
Chirangi akiwasilisha risala kwa mgeni rasmi wakati wa kufunga
kikao cha madaktari hao wa Taasisi za Dini zinazotoa huduma za
Afya Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhe. Selemani Jafo(kulia) akiwa na Mkurugenzi wa CSSC Mr.
Maduku wakati wa kufunga Mkutano wa Chama cha Madaktari wa
Kikristo Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Chama cha Madaktari wa
Kikristo Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa
kufunga kikao cha madaktari hao wa Taasisi za Dini zinazotoa
huduma za Afya Tanzania.
Baadhi ya mshiriki wa Mkutano wa Chama cha Madaktari wa Kikristo
Tanzania akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa kufunga kikao
cha madaktari hao wa Taasisi za Dini zinazotoa huduma za Afya
Tanzania.

**************.

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewataka viongozi wa dini Nchini kote kuendelea
kuliombea Taifa hasa wakati huu ambao miradi mikubwa ya maendeleo
inatekelezwa.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 82 wa Chama
cha Madaktari wa Kikristo Tanzania unaofanyika chini ya Taasisi ya
Huduma ya Kijamii za Kikristo(CSSC) katika ukumbi wa St. Gasper Jijini
Dodoma.

Waziri Jafo amesema “Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi
mikubwa ambayo haijawahi kutokea tangu Uhuru, kila unapopita unaona
ujenzi wa miundombinu ya barabara inaendelea, halkadhalika ujenzi wa reli
ya kisasa (SGR), huku mradi wa ufuaji umeme wa mto Rufiji unatekelezwa
hatuna budi kuendelea kumuombea Rais wetu Dkt. John Joseph Pombe
Magufuli azidi kuwa na afya njema na aweze kusimamia miradi hii hadi
ukamilifu wake”.

Tunashukuru Mungu leo hii Mahakamu Kuu ya Gauteng, Africa Kusini
imetoa hukumu na kuamuru ndege yetu ya Air Tanzania iliyokuwa
inashikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi hizi
ni habari njema sana kwetu na haya ni matunda ya kufanya vitu kwa nia
njema na dhamira ya dhati ya kuwainua watanzania tusiache kuomba kwa
ajili ya Taifa hili aliongeza Jafo.

Wakati huo huo Waziri Jafo aliziagiza Halmashauri zenye Hospitali Teule
(DDH) kuhakikisha wanafanya vikao na Taasisi za kidini zenye
makubaliano ya uendeshaji wa Hospital hizo.

“Hizi tabia za Halmashauri kusema hawana hela za vikao sjui viburudisho
zisikwamishe ufanyikaji wa vikao, kutaneni hata saa nane mchana mpaka
kumi jioni cha msingi mjadiliane changamoto zinazokabili hospitali hizo na
kuzitaftia njia ya kuzitatua kwa pamoja” alisema Jafo.

Kuna changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kutatuliwa kwa
mashauriano tu lakini unapoziacha kwa muda mrefu zinakuwa tatizo
kubwa, mkiwa mnakutana ni vizuri katika uboreshaji wa huduma za Afya
kwenye Halmashauri husika aliongeza Jafo.

“Taasisi za Dini mnafanya kazi kubwa sana katika Sekta ya Afya na kwa
muda mrefu mmekuwa mkimiliki Hospital takribani 105 na Serikali tulikuwa
na Hospital 77 tu kabla hatujaanza ujenzi wa Hospital za Wilaya 67.
Mmekuwa msaada katika kuwafikia wananchi ambao Serikali ilikua bado
haijajenga Hospital niwapongeze kwa kuhakikisha huduma za Afya
zinapatikana karibu na wananchi na kwa haraka hakika mmewasaidia
watanzania wetu kupata huduma bora za Afya na mmeboresha afya zao
Alisema Jafo.

Halkadhalika Waziri Jafo aliweka wazi mpango wa Serikali kukamilisha
mchakato wa kuajiri Watumishi wa Afya takribani 400 ambao kwa kiasi
flani wataenda kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya katika Vituo vya
kiutolea huduma za Afya.

“Ninafahamu fika tatizo la uhaba wa watumishi katika hospital nyingi
Serikali tunalifahamu hilo na tumechukua hatua za makusudi za kutangaza
ajira za Afya na sasa tunakamilisha mchakato wa ajira hizo na muda si
mrefu mtaanza kuwapokea kwenye baadhi ya Hospital ambao wataongeza
nguvu katika utoaji wa huduma za Afya Nchini” Alisema Jafo.

Akizungumza katika Kikao hicho Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo
Tanzania Dr. Bwire Chirangi alitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja
na kukosa vikao vya mashauriano, uhaba wa watumishi wa Afya pamoja
na miundombinu duni ya kuzifikia huduma za Afya.

Aidha Dr. Chirangi alieleza kuwa Chama hiki kimeanza mwaka 1937 na
kinawakutanisha pamoja wataalamu wote wa Afya wanaohudumu katika Hospital za Dini na wamekuwa wakikutana kila mwaka kujadili changamoto na mafanikio mbalimbali ya huduma za Afya zinazotolewa na Taasisi za Dini ya Kikristo.

JESHI LA POLISI KIKOSI CHA RELI CHATOA ELIMU KWA ABIRIA WANAOTUMIA USAFIRI HUO.

$
0
0

***************

Jeshi la Polisi kupitia kikosi chake cha Reli leo kimetoa Elimu kwa Abiria
wanaotumia usafiri wa Treni juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na uhalifu
unaofanywa na baadhi wa matapeli, elimu hiyo imetolewa na SGT Michael,
eneo la kamata kariakoo jijini Dar Es Salaam mapema leo kabla abiria hao
kuanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma. Huku akisema kwa kipindi kifupi
ambacho safiri za treni zilisimama baadhi ya watu walitumia nafasi hiyo kamasehemu ya kujipatia kipato kwa kuwatapeli abiria kwa njia ya kukatisha tiketifeki.

Aidha katika hatua nyingine SGT Michael aliwataka wanandoa pamoja na
watu wengine wanaotumia usafiri huo kuacha kuwafanyia ukatili wa kijinsiawenza wao au watoto wao huku akisema kuna baadhi watu husafirisha familiazao hasa kwa wanawake wajawazito ambao wamekaribia kujifungua hali hiyohuwapelekea wanawake hao kujifungulia ndani ya Treni.

ASASI ZA KIRAIA ZINAITAKA SADC KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA JUU YA UKATILI UNAOENDELEA AFRIKA KUSINI.

$
0
0
ASASI ZA KIRAIA WANACHAMA WA TANGO, TUCTA NA CCT INAITAKA SADC KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA JUU YA UKATILI UNAOENDELEA NCHINI AFRIKA KUSINI.

Kuibuka kwa ukatili wa hivi karibuni nchini Afrika Kusini ni suala la kutia huzuni kubwa kwa nchi hiyo, kanda yote ya SADC na bara la Afrika kwa ujumla. Kwa bahati mbaya mashambulizi haya yaliyolengwa dhidi ya watu wanaotazamwa kama “wageni” sio matukio ya nadra yanayofanywa na
wahalifu wachache. 

Sasa ni wazi bila kupinga kuwa hali ya kibaguzi dhidi ya waafrika wenzao imeongezeka miongoni mwa raia nchini Afrika Kusini, jambo ambalo linakinzana na Sera za SADC zinazohimiza umoja, ushirikiano, usalama na uhuru wa raia kusafiri na kufanya shughuli za kiuchumi
katika nchi wanachama ili mradi wanazingatia sheria na taratibu zilizokubalika ndani ya SADC.

Inafikirisha pia kuwa vyama vya siasa nchini Afrika Kusini, karibu vyote, vimekuwa vikifungamana nahisia finyu, kejeli na zisizo-sahihi za utaifa kitu ambacho sio tu kinahalalisha uvunjaji haki na utengano bali kinatanua wigo wa chuki na ubaguzi. Ni wazi pia kuwa watu maskini nchini Afrika Kusini
wanapata tabu kwa kukosa kuthaminiwa, haki za binadamu na fursa za kujiendeleza kibinafsi. 

Tofauti zinazosababishwa na mfumo kati ya walionacho na wasionacho nchini humo inakuza saikolojia ya ukatili ambayo jamii nchini humo bado haijaishughulikia kwa zaidi ya miaka 20 tangu nchi hiyo ianze
kuwa na mfumo wa utawala wa walio wengi. 

Ukatili ulioenea na kulindwa kimfumo nyakati za Ubaguzi wa Rangi (Apartheid) na Ukoloni haujatafutiwa ufumbuzi wa kutosha na serikali ya kidemokrasia. Ukatili wa kila siku unaowakumba watu wengi waishio nchini Afrika Kusini – ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaume; ubaguzi wa kimfumo na kijinsia; ubaguzi wa makundi fulani kijamii - na ukatili dhidi ya maskini na kwa wale waliotengwa kijamii unaleta muunganiko ulio wazi na unachangia kuwaweka kafara Waafrika wengine kwa mateso na kero za watu maskini nchini humo.

Kwenye mkutano wetu wa hivi karibuni wa Jukwaa la AZAKI za SADC jijini Dar es Salaam, Tanzania –vyama vya wafanyakazi, AZISE, asasi za kidini za ukanda huo – zilitamka wazi: “Mkutano wa 15 wa Jukwaa la AZAKI unatanabahisha na kutahadhalisha ukatili unaondelea kwa raia/watu wa mataifa mengine, hasa nchini Afrika Kusini. 

Tunalaani mashambulizi hayo na kwa mara nyingine kuzitaka nchi
wanachama wa SADC kulaani kwa pamoja matamshi na mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni yanayoendelea nchini Afrika Kusini. Serikali ya Afrika Kusini na nchi nyingine wanachama za SADC, lazima zihakikishe usalama na kuthamini haki za binandamu za raia wote wa nchi nyingine wanaoishi
ndani ya mipaka ya nchi hizo.” (Agosti 15, 2019 Tamko la Jukwaa la AZAKI la SADC CSF).

Namna ambavyo ukatili huu wa hivi karibuni kabisa uliovyoandaliwa ni jambo la kutisha, ikiashiria ongezeko la kuwalenga watu ambao sio raia wa nchi hiyo.

 Dola nchini Afrika Kusini, wadau wengine na serikali lazima wakomeshe ‘ukanaji’ wa haki za binadamu kwa wageni ambao unaoneshwa na ukatili huu na watambue kuwa vitendo hivi vya kihalifu na udhalilishaji sio vya kuzuka, au vya nadra, kwa hakika hivi ni vitendo vya kupangwa vinavyotokana na chuki, umaskini na kukata tamaa ya maisha. 

Suala hili halina budi kuwekwa kwenye ajenda ya SADC ili kuisaidia Jamhuri ya Afrika Kusini kuweza kuingilia kati hali hii. Ni budi pia kuwakemea viongozi waliotamka kuwa'waliofanywa haya
wana upungufu wa akili' kwani kukubali mtazamo huo ni kukubali kutawaondoa wahalifu dhidi ya kuchukuliwa hatua za kuwashtaki mahakamani kwa makosa ya jinai kwa kudhaniwa tu kuwa ni
wendawazimu.

Pia kumewepo na matukio ya wanawake na wasichana kubakwa wakati vurugu, mashambulizi na ukatili huu ukiendelea. Huu ni ukikwaji mkubwa sana wa haki za binadamu. Tunatarajia hili likemewe kwa nguvu zote na SADC na kuitaka Serikali ya Afrika Kusini iombe radhi hadharani juu ya vitendo hivyo viovu hususan vya ubakaji na makosa yanayofanana na hayo yaliyofanywa kwa wanawake bila kujali rangi au utaifa wao.

AZAKI za Tanzania pia zinaitaka serikali ya Afrika Kusini na uongozi wa Jumuiya ya SADC kuhakikisha kuwa waliotekeleza mashambulizi na uhalifu huu wa kijinai wanatiwa nguvuni na kuchukuliwa hatua stahiki kisheria.
Baraza la Mawaziri la SADC linalohusika na Chombo cha Siasa, Ulinzi na Masuala ya Usalama lazima washtushwe na ukatili ulioikumba Afrika Kusini na kukutana haraka ili kupata taarifa ya uchunguzi wa kina kutoka kwa Serikali ya Afrika Kusini, waunge mkono juhudi na kukubaliana juu ya aina ya msaada unaotakiwa kutolewa kwa raia wa nchi za SADC na Afrika waliomo ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Tunaitaka serikali ya Afrika Kusini kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wa kigeni pamoja na mali zao.

TANGO, TUCTA na CCT inaziomba kwa heshima na taadhima Serikali za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Zimbabwe kuchukua hatua stahiki za kiuongozi ndani ya SADC kuhakikisha suluhisho la haraka linapatikana. TANGO, TUCTA na CCT ziko pamoja na AZAKI ambazo juhudi zake za kuzuia,
kupatanisha na kuhudumia wahanga wa ukatili huo na kwa mshikamano na ndugu zetu wake kwa waume nchini Afrika Kusini na kuwahakikishia mfungamano wetu kamili kwenye juhudi hizo.

Tunatoa rai kwa Rais wa Afrika Kusini kukutana na wawakilishi wanaohusika kwenye jamii zilizoathiriwa na kukemea waziwazi ubaguzi na chuki dhidi ya wageni, kuweka mazingira ya kuwarejeshea maisha yao wahanga wa ukatili huu na kurejelea ahadi ya kukomesha kutokea tena kwa
mashambulizi haya kwa wasio-raia wa Jamhuri ya Afrika Kusini.

TANGO ni shirika mwavuli la asasi za kiraia nchini lililodumu kwa muda mrefu na kubwa zaidi Tanzania likiwa na dhamana ya uwakilishi wa mashirika zaidi ya 600 hapa nchini.

 Wanachama wa TANGO ni pamoja na mitandao ya kimkoa na kiwilaya ipatayo 28 na AZAKI moja moja; TANGO ina utajiri wa utofauti, upana na ujumuishi wa AZISE/AZAKI zinazofanya kazi kwenye sekta za ardhi, mazingira, madini, elimu, afya, kilimo, utamaduni, uwezeshaji kiuchumi, wanawake, watoto, vijana, wazee, watu wenye ulemavu na wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi (VVU).

Bolt yazidi kutanua huduma zake katika miji mikubwa Tanzania

$
0
0

  KAMPUNI inayokua kwa kasi katika utoaji wa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni barani Ulaya na Afrika- BOLT, inatarajia kuzindua huduma zake katika miji mikubwa miwili nchini Tanzania ikiwa ni hatua mojawapo ya kuendelea kupanua huduma za usafiri katika soko lake la ndani ya nchi.

Huduma hiyo imeanza kupatikana jana Septemba 4, 2019 katika jiji la Arusha na kuanzia wiki ijayo itaanza kupatikana Visiwani Zanzibar.

Uzinduzi huo wa Bolt katika jiji la Arusha na Visiwani Zanzibar unaongeza idadi ya miji ya Kitanzania inayohudumiwa na kampuni hiyo kutoka mikoa mitatu hadi mitano, na kuifanya Bolt kuwa mtoaji huduma mkubwa wa usafiri kwa njia ya mtandao katika ukanda huu wa Afrika.

Meneja wa Bolt Tanzania, Remmy Eseka alisema kuwa dhamira ya Bolt ni kufanya usafirishaji wa mijini kuwa rahisi zaidi na wa bei nafuu kwa watu wote na hivyo kufikia malengo ya kampuni katika utoaji huduma za usafiri na ajira ikiwa ni moja ya mchango Bolt kwa jamii.

"Baada ya miji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma kama ilivyo ada Bolt imeendelea kukua kwa kasi nchini kote. Sasa tunakusudia kujenga jamii mpya Arusha na Zanzibar kutokana na uaminifu tunaoendelea kuupata kwa Watanzania," alisema Eseka.

Alisema huduma hiyo ni rahisi kutumi kwani abiria wanatakiwa kupakua programu ya Bolt kutoka kwenye maduka ya programu ya iOS au ya Android na kujaza wasifu wa mtumiaji. Wakati wapo tayari kusafiri, watumiaji hufungua program na kuweka eneo lao walilopo na mahali walipokusudia kufika.

Pia Programu itatoa makisio ya gharama kwa safari hiyo.

"Mara baada ya abiria kuomba safari, programu humwonesha madereva wa karibu ambao wanakubali safari hiyo.Mara tu dereva anapokubali safari hiyo, abiria wataweza kuona jina la dereva wao, picha, muundo wa gari na usajili, na kuweza kufuatilia dereva anayewafuata kwa wakati muafaka na wa kweli lakini pia program hiyo hufanya iwe rahisi kuwa na uhakika kuwa wanaingia salama kwenye gari sahihi na dereva sahihi.

"Abiria pia wanaweza kutoa maelezo ya safari yao kwa kutumia program ‘ETA’ iliyomo katika kipengele cha ziada kwenye suala la usalama.

"Wakati safari imekamilika, malipo hufanywa na pesa taslimu, au kupitia kadi ya deni ya mpandaji aliyejiunga kwenye program hiyo. Abiria na madereva wanaweza kupima kila mmoja kati ya nyota tano na kutoa maoni kuhusu umahiri wa utumiaji programu ya Bol," alisema.

Aidha, alisema Bolt tayari imewasajili madereva katika miji ya Arusha na Visiwani Zanzibar, ambao wote wanapokea asilimia 80 ya nauli zote zinazolipwa na abiria.Hata hivyo, madereva wanaotumia Bolt wanaweza kuchagua masaa mangapi wanaendesha na wanaweza kufanya kazi katika maeneo yoyote wanayotaka.

"Magari ya Madereva lazima yawe yamesajiliwa kuanzia mwaka 2000 au mapya zaidi. Gari lazima iwe na milango minne (Toyota Corolla, aina ya Hyundai, Kia Rio, nk). Hii inamaanisha kuwa kila mtu akipanda safari kupitia Bolt anaweza kuwa na hakika kwamba watafika salama kwao na kwa raha," alisema.
Mwisho

Tumeshafuta Leseni 1,000 za madini kati ya 18,000 za watu ambao hatukuwahi kuwaona - Biteko


MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI BRELA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serilkali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Menejimenti ya wafanyakazi wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) alipotembelea kwa zira ya kikazi iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serilkali, Dkt.Hassan Abbasi, akisistiza jambo kwa Menejimenti ya wafanyakazi wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) alipotembelea kwa zira ya kikazi Septemba 4, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serilkali, Dkt.Hassan Abbasi, akifurahia jambo na wafanyakazi wa Wakala waUsajili wa Leseni na Biashara (BRELA) pamoja na Viongozi Chama cha Maafisa Mawasiliano na Mahusiano Serikalini(TAGCO) wakati wa zaira ya kikazi iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serilkali, Dkt.Hassan Abbasi, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA) pamoja na Viongozi Chama cha Maafisa Mawasiliano na Mahusiano Serikalini(TAGCO) wakati wa zaira ya kikazi iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2019.

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

BUNGE LINAWAALIKA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI Na. 6 MWAKA 2019

WALIOFICHA MENO YA TEMBO WAPEWA MWEZI MMOJA WAJISALIMISHE

$
0
0

Na. Aron Msigwa – WMU, Dar es Salaam.

SERIKALI imetoa muda wa mwezi mmoja (kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 4, 2019) kwa wananchi wote wanaomiliki meno ya Tembo kinyume cha sheria, kuhakikisha wanayasalimisha kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na kwamba watakaofanya hivyo kabla ya kuisha kwa muda huo hawatashtakiwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa muda huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada Kikosi Kazi cha Taifa dhidi ya Ujangili (NTAP) kukamata watuhumiwa 8 wa ujangili, vipande 338 na meno mazima ya Tembo 75 pamoja na meno mawili ya kiboko.

“Nimewaita hapa ili mshuhudie kazi nzuri iliyofaywa na maafisa wa Serikali na Kikosi Kazi maalum cha kudhibiti ujagili, ninatoa huruma ya mwezi mmoja kwa kila aliye na meno ya Tembo ayasalimishe kwenye chombo chochote cha Serikali na atakayefanya hivyo ndani ya muda huo hatutamshtaki” Amesisitiza Dkt.Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla amesema kukamatwa kwa majangili hao kumetokana na kazi ya muda mrefu ambayo imezaa matunda na matokeo yake kuonekana kwa kukamatwa kwa majangili sugu 8 (nane) akiwemo Bw. Hassan shaban maarufu kwa jina la Nyoni aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa kujihusisha na mtandao wa ukusanyaji wa meno ya Tembo kutoka Tanzania na Msumbiji.

Amesema mtuhumiwa huyo wa ujangili amekamatwa na jumla ya vipande vya meno ya Tembo 338 na memo mazima 75 pamoja pamoja na meno 2 ya Viboko ambapo kwa mujibu wa Wataalam na Wanasayansi wa Uhifadhi wa Wanyamapori wanaeleza kuwa meno hayo ni sawa na Tembo 117 waliouawa.

Amebainisha kuwa meno hayo yalianza kutafutiwa soko mwaka 2015 wakati Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilipoingia madarakani, hivyo hatua ya Serikali kuimarisha Ulinzi wa Rasilimali za Taifa na kukiongezea uwezo Kikosi cha Kudhibiti Ujangili soko la meno hayo liliharibika.

Dkt. Kigwangalla amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya tano Majangili wengi wamekamatwa na mitandao yao kusambaratishwa akisisitiza kuwa yeyote atakayejihusisha na biashara hiyo kwa namna yoyote ile atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

“Mtuhumiwa huyu amehangaika na huu mzigo kwa zaidi ya miaka minne na hili nataka watanzania wajue ya kwamba yeyote atakayejihusisha na biashara hii ya kuuza nyara za Serikali tutamkamata tu maana, sababu ni moja wateja tumebaki ni sisi wenyewe popote utakapojaribu kuuza tutakukamata tu” 

Aidha, ametoa onyo kwa wananchi wanaojihusisha au kushiriki kwa namna yoyote ile na vitendo vya ujangili waache mara moja akibainisha kuwa kazi hiyo kwa sasa haina nafasi nchini Tanzania.

Amesema kuwa kuanzia mwaka huu Wizara yake itaweka Mkakati mpya wa kukomesha vitendo vya ujangili nchini hadi kufikia mwaka 2014 akieleza kwamba mkakati huo utaimarisha kikosi kazi cha kudhibiti ujangili, kuimarisha ushirikiano na wizara nyingine, kuimarisha Jeshi USU na kuweka muundo mzuri utakaozuia mauaji ya wanyama.

Aidha, amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka 3 katika Ikolojia ya Selous hakuna Tembo hata mmoja aliyeuawa na majangili akibainisha kuwa meno ya Tembo yaliyokamatwa Agosti 31 mwaka huu ni yale ya ujangili uliofanyika nyuma kabla ya kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano.

Amesema Kikosi Kazi hicho cha Serikali kimefanikiwa kuziba mianya yote ya biashara haramu za nyara za Serikali kwa kupambana na uharifu kwa kufuatilia na kusambaratisha mitandao yote ya ujangili ikiwemo mali na silaha za majangili.

Amebainisha kuwa kazi hiyo imefanikiwa kwa kuwa kinajumuisha maafisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama na taasisi za kisheria na kimekuwa kikifanya kazi nzuri ya kuratibu , kusimamia na kuchukua hatua za kupambana na uhalifu wa rasilimali za Wanyamapori na Mazao ya Misitu kwa kuendesha operesheni zinazoongozwa na taarifa za Kiintelijensia.

Dkt. Kigwangalla ameongeza kuwa Kikosi Kazi hicho kinafanya uchunguzi wa wahalifu na mali zinazotokana na uhalifu, kukamata, kupekua na kushikilia mali za wahalifu wanaojihusisha na ujangili. 

“Sasa hivi kupitia Kikosi Kazi chetu tumeziba mianya yote, anayefanya biashara tutamkamata, aanayewinda kwenye maeneo ya hifadhi tutamkamata na hata askari wote wanaoshirikiana na majangili tutawakamata kwa kuwa tukimpata jangili mmoja tunahakikisha na mtandao wake wote tumeuvunja” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 Kikosi Kazi hicho kimefanikiwa kukamata watuhumiwa zaidi ya 1072 silaha 539 zikiwemo siala 85 za Kivita na jumla ya risasi 37,921.

Aidha, nyara mbalimbali za Serikali zilikamatwa ikiwa ni pamoja na meno tembo, pembe za faru, ngozi za Simba, Chui na Duma, meno ya Kiboko, Kobe pamoja na mazao ya Misitu.

Pia Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa Kikosi kazi hicho hadi sasa kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakubwa wa ujangili wakiwemo Aloyce Francis Ayubu( Kamanda), Mateso Kassiani Albano (Mateso Chupi) na Jayzan George Kuchar (China), Haruna Kassa, Frank Silagei na Ojugu (Original).

Wengine ni Haong Nghia Trung, MS. Yang Feng Glan (Queen of Ivory) ambaye amekwishahukumiwa pamoja na Salvius Francis Matembo na Manase Julius Philemon, Boniface Maringo, (shetani), Juma Maringo (Yesu), Godfrey James Nyamicha (Papa), Haidari Omary Sharif, Oliva Lucas Mchua na Mrangilwa Emanueli.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia na kupata maelezo ya vipande 338 na meno mazima ya Tembo 75 pamoja  na meno mawili ya kiboko yaliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa 8 wa Ujangili na  Kikosi Kazi cha Taifa dhidi ya Ujangili (NTAP). Picha na Aron Msigwa - WMU.
 

WAZIRI WA MAMBO YA NJE PROF. KABUDI AWAAGA WANAFUNZI WANAOKWENDA ISRAEL KUSHIRIKI MAFUNZO YA KILIMO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi 44 kati ya 100 waliochaguliwa kwenda nchini Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Septemba 2019. Hafla hiyo imefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 4 Septemba 2019. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Ayoub Mndeme na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Emmanuel Buhohela. 
Prof. Kabudi akizungumza na wanafunzi hao 
Wanafunzi hao wakimsikiliza Prof. Kabudi (hayupo pichani) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe naye akiwaasa wanafunzi hao kuzingatia maadili na kuwa wazalendo wanapokuwa kwenye mafunzo nchini Israel 
Dkt. Mnyepe akizungumza 
Mhe. Prof. Kabudi akimkabidhi tiketi na hati ya kusafiri, Bi. Janeth Barnaba ambaye ni mmoja wa wanafunzi wanaokwenda kushiriki mafunzo ya kilimo nchini Israel 
Mwanafunzi mwingine akipokea tiketi na hati yake ya kusafiria tayari kuelekea nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019 kwa ajili ya kuanza program ya mafunzo ya kilimo 
Prof. Kabudi akiendelea na zoezi la kuwakabidhi wanafunzi hao tiketi na hati zao za kusafiria kama inavyoonekana pichani 
Zoezi la kukabidha tiketi na hati za kusafiria likiandelea 
Wanafunzi wakishuhuda mwenzao akikabidhiwa hati yake ya kusafiria na tiketi ya ndege 
Prof. Kabudi akikabidhi hati za kusafiria na tiketi za ndege kwa wanafunzi wanaokwenda Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo kwa vitendo 
mwanafunzi akifurahia kukabidhiwa hati ya kusafiria na tiketi ya ndege vitakavyomwezesha kwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo 
Prof. Kabudi akimkabidhi hati ya kusafiria na tiketi ya ndege mwanafunzi atakayeshiriki program ya mafunzo ya kilimo nchini Israel 
Wanafunzi wakiwa wameshikilia hati zao za kusafiria na tiketi za ndege zitakazowawezesha kusafiri kwenda Israel kushiriki program ya mafunzo ya kilimo 
Mhe. Prof. Kabudi akiwaasa wanafunzi hao mara baada ya kuwakabidhi tiketi zao na hati za kusafiria zitakazowawezesha kwenda Isarel kuanza mafunzo ya kilimo kwa vitendo. Prof. Kabudi aliwataka wanafunzi hao kuwa waadilifu, wasikivu, wachapakazi, wazalendo na warejee nyumbani wakiwa na ujuzi na maarifa kwa manufaa ya Taifa.
===============================================================

Serikali ya Tanzania inaungana na Serikali ya Afrika Kusini kulaani vikali vitendo vya ubaguzi na mashambulizi vinavyofanywa na raia wachache wa nchi hiyo dhidi ya raia wa nchi zingine za Afrika na kuziasa nchi zingine kutolipa kisasi kutokana na vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi 100 kutoka Tanzania wanaokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo iliyofanyika leo tarehe 4 Septemba 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mhe. Prof. Kabudi amesema kuwa, vitendo vinavyofanywa na raia wachache wa Afrika Kusini vya kuwashambulia raia kutoka nchi zingine za Afrika na kuharibu mali zao vinasikitisha na kuivunjia heshima nchi hiyo. Hata hivyo, alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaunga mkono kauli ya Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa aliyoitoa hivi karibuni ya kukemea na kulaani vikali vitendo vinavyofanywa na raia hao wachache.

Aidha, ameongeza kuwa, vitendo hivyo ambavyo vinatokana na raia hao wengi kukosa ajira, ardhi na pia kutopenda kujishughulisha havihalalishi watu wengine wakiwemo watanzania kulipa kisasi kwa namna yoyote ile.

“Ni jambo la kusikitisha lakini Serikali ya Afrika Kusini inalisimamia kikamilifu na sisi tupo tayari kushirikiana nao ili kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.Nawasihi Watanzania wenzangu tusilipize kisasi na tutaendelea kuwalinda raia wa Afrika Kusini waliopo Tanzania kwani tunaamini kuwa Afrika ni moja na waafrika ni ndugu zetu” alisema Prof. Kabudi.

Kadhalika, Prof. Kabudi alieleza kuwa hadi sasa hakuna taarifa kuhusu Mtanzania kuuawa, kujeruhiwa au kuharibiwa mali kutokana na vurugu hizo. Pia alisema kuwa Wizara itaendelea kutoa taarifa za uhakika kadri zinavyopatikana kutoka kwenye vyanzo vya uhakika ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huohuo, Mhe. Prof. Kabudi amewaaga wanafunzi 44 kati ya 100 waliochaguliwa kwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia mwezi Septemba 2019. Wanafunzi hao ambao wengi wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Taasisi ya Kilimo ya Uyole ya Mbeya na Ukiriguru ya Mwanza wanakwenda kushiriki mafunzo hayo ya vitendo kwenye sekta mbalimbali za kilimo ikiwemo uzalishaji na teknolojia. Kati ya Wanafunzi hao, 16 wameondoka nchini tarehe 4 Septemba, 2019, kuelekea Israel, 44 wataondoka nchini tarehe 5 Septemba 2019 na idadi iliyosalia itaondoka tarehe 10 Septemba 2019.

Katika hotuba yake, Mhe. Prof. Kabudi amewataka wanafunzi hao vijana kuzingatia mafunzo hayo ili kuja kutoa mchango wao kwenye mapinduzi ya kilimo ambayo yatachochea mapinduzi ya viwanda nchini. Aidha aliwaasa kuwa waadilifu, kufanyakazi kwa bidii, kushikamana na kujiepusha na vitendo viovu. 

“Mnaenda Israel kutafuta ujuzi, uzoefu na ubunifu katika maeneo ya uzalishaji mazao. Hivyo tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuja kuibadilisha Tanzania katika eneo la kilimo na mtaleta mapinduzi ya kilimo kwani vijana mpo wengi nchini, mna ari na ni nguvu kazi ya Taifa” alisisitiza Prof. Kabudi.

Akiielezea Israel, Mhe.Prof. Kabudi amesema kuwa nchi hiyo ni nusu jangwa kama ilivyo baadhi ya mikoa hapa nchini. Hata hivyo Israel inaongoza kwa kuuza mazao ya mbogamboga na matunda kwenye nchi za Ulaya kutokana na watu wa nchi hiyo kutumia maarifa katika kugeuza ukame kuwa fursa. Hivyo aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanapata maarifa na kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa ili kuja kuendeleza kilimo kikiwemo kile cha umwagiliaji kwenye mikoa kama Singida, Manyara, Shinyanga na Dodoma.

Wanafunzi hao mia moja (100) wamechaguliwa kati ya wanafunzi 1,440 waliotuma maombi ya kwenda kushiriki program ya mafunzo ya kilimo nchini Israel ambayo hufanyika kwa kipindi cha miezi tisa. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliratibu zoezi la upatikanaji wa wanafunzi hao kwa maelekezo ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa mwezi Novemba 2018 alipofanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini, Mhe. Noah Gal Gendler.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam.

MAONYESHO YA PILI YA VIWANDA MKOANI PWANI KUFANYIKA OCTOBA 1-7 MWAKA HUU - NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

MKOA wa Pwani, kwa mara ya pili unatarajia kufanya maonyesho ya viwanda kuanzia tarehe 1-7 octoba mwaka huu, huku ukitarajia kuongeza idadi ya wawekezaji watakaoshiriki kutoka 166 mwaka 2018 hadi kufikia 500.

Maonyesho hayo yataambatana na kongamano la uwekezaji litakalofanyika octoba 3 ambapo yatafanyika katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),maarufu uwanja wa sabasaba uliopo ,Mkuza wilayani Kibaha mkoani hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu suala hilo na kusainishana mkataba baina ya mkoa na waratibu hao, mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema, waratibu wa maonyesho hayo watakuwa ni wabobezi wa masuala ya maonyesho kama hayo kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) pamoja na mamlaka ya maendeleo ya viwanda (TANTRADE) .

Alieleza, malengo ya matukio hayo ni kuonyesha kwamba mkoa wa Pwani ,umedhamiria kuwa ukanda wa viwanda,wenye viwanda kupata masoko ya uhakika,kupanua wigo wa soko la ndani ya mkoa kufikia kimataifa na ,kuvutia wawekezaji wapya.

Aidha Ndikilo alifafanua lengo la kongamano hilo ,kuwa ni kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii,uchumi,kijamii,kilimo,uvuvi na viwanda.

"Kufanyika kwa kongamano hili italeta picha halisi ya fursa zote zilizopo mkoani Pwani,na kuonyesha namna mkoa ulivyopiga hatua katika sekta ya viwanda,uwekezaji na fursa za miradi mikubwa ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa uzalishaji umeme megawatts 2,100 STIGO ,huko Rufiji"alibainisha Ndikilo.
Hata hivyo,mkuu huyo wa mkoa alisema wenye viwanda maonyesho ya mwaka jana walikuwa 166 mwaka huu wanatarajia kufikia 500 japo sio namba sahihi,na idadi ya watu watakaotembelea kuongezeka kutoka 18,000 hadi kufikia 100,000.
Nae Januarius Maganga wa TSN alisema ,wanakwenda kuratibu maonyesho hayo ikiwa ni maonyesho ya kumi .

Kwa upande wake ,mwakilishi wa mkurugenzi kutoka TANTRADE ,Victor Rugemalila aliwahakikishia wananchi na mkoa kwamba ,wamejipanga kuona namna bidhaa inakua na kuleta maendeleo ya wenye viwanda na kuratibu kwa ufanisi mkubwa maonyesho hayo.

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>