Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

WAZIRI MWAKEMBE AFANYA UKAGUZI WA BEI ZA TIKETI ALFAFJIRI MAENEO YA VISIGA

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi,Dr Harisoni Mwakembe afanya ukakuguzi wa tiketi ilikubaini mabasi yaliyo toza gharama kubwa za nauli zakusafiria katika kipindi cha Xmass na mwaka mpya,badhi ya mabasi yalikamatwa nakuamuliwa kurudisha nauli zilizozidi abiria wao.zoezi hilo limefanyika majira ya alfajiri katika eneo la Visiga mkoani pwani na kila basi lilozidisha nauli lilitozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.


DR. JOSE CHAMELEONE ATUA MWANZA KUPIGA BONGE LA SHOW USIKU WA LEO TAREHE 24 CCM KIRUMBA MWANZA.

$
0
0
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na Tamasha lililopewa jina la 'Badilisha Concert' litakalofayika leo 24 dec 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo kama sehemu ya kuikaribisha sikukuu ya Christmass. Pembeni yake anaonekana meneja wake na mwisho kabisa kulia ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo Mr. James Njuu wa K Vant Gin.
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na mmoja kati ya wasanii wa Jambo Squard mbele kidogo ni Dogo Dee na mwisho kabisa (kushoto) katika mstari ni mwanamuziki Bob Haisa ambao wamefika kumpa sapoti katika show ya Badilisha Concert itakayofanyika leo CCM Kirumba Mwanza. 
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Denis (kushoto) kutoka Silver Intertainment amesema kuwa kampuni yake imeamua kuweka kiwango kidogo cha kiingilio ili watu wote wa Kanda ya Ziwa waipate zawadi ya mwaka kushuhudia burudani kali.
"Zawadi nyingi huwekwa kwenye boxi lakini hii yaani mimi ni zawadi iliyo nje ya boxi maalum kwa wakazi wa Mwanza" pia Jose Chameleone anasema kuwa najivunia kuwa Mwanza mji ambao kwangu ni sawa na nyumbani.
Jose Chameleone amekwepa kulizungumzia suala lake la hivi majuzi kukumbatiana na mdogo wake Weasal na binamu yake Radio ile hali walikuwa kwenye bifu kali akisema yote yatafanyika lakini undugu utabaki pale pale akisita kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema hawezi kuzungumzia masuala ya familia nje ya familia anaheshimu utamaduni wa kiafrika.
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza.

Mwimbaji nyota wa nyimbo za injili solly Mahlangu awasili jijini dar leo,kutumbuiza kesho tamasha la krisimasi uwanja wa taifa

$
0
0
 Mwanamzuki mwimbaji  wa Kimataifa wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu pichani kati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni ya leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krisimasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kuhusiana na ujio wa mwanamuziki wa Afrika Kusini,Solly Mahlangu aliyewasili jioni ya leo jijini Dar tayari kuungana na wanamuziki wengine wa nyimbo ya Injili kwa ajili ya kutumbuiza hapo kesho kwenye tamasha la Krisimasi,ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili,Solly Mahlangu akiwapungia mikono mashabiki wake waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni .Kulia kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Zawadi ya Xmas kwa wadau. Ngoma ya Taja Sevelle ya 'Love Is Contagious'

Salamu za Krismas kutoka Ngoma Africa Band

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni inawatakia Merry Christ-Mass na heri ya mwaka mpya 2014,wadau wote popote pale duniani. Msikose kufurahia Christ-mass kwa kusikiliza muziki at www.ngoma-africa.com

Rais Kikwete akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

$
0
0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani 24/12/2013.

Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.

Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwaajili ya kufanya mazungumzo nae.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani 24/12/2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.

salamu za krismas na Mwaka mpya toka CCM

SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA TOKA CCM - TAWI LA UINGEREZA

$
0
0
Kwa Niaba ya CCM Tawi la Uingereza tunapenda kuungana na Wanachama, Wapenzi na waTanzania wote kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu za Krismas na Ujio wa Mwaka Mpya wa 2014.

Uingereza sherehe hizi zimetukuta katika hali ya hewa yenye kimbunga kingi na mvua nyingi zisizoisha, na hivyo kuathiri maandalizi kwa namna moja au nyingine kutokana na vizuizi katika baadhi ya miundo mbinu hasa barabara na reli.

Aidha, kama inavyojulikana Ulimwenguni Ukata wa kifedha nao umeshika hatamu. Kuyumba kwa Uchumi wa Nchi nyingi kubwa na ndogo na kuyumba kumepelekea mfumuko wa bei za bidhaa hasa vyakula . Tatizo ambalo limeukumba ulimwengu mzima.

Licha ya vikwazo hivi na vingine ,hatuna budi kumaliza mwaka kwa kuangalia nyuma na kuona yale mengi yaliyofanikishwa. Kwa hali hii , CCM UK tunachukua nafasi hii kuipongeza kwa dhati Serikali ya awamu ya nne ya Jamahuri ya Muungano ya Tanzania kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Mfano ulio wazi ni katika miundo mbinu ya barabara ambapo asilimia kubwa ya Nchi sasa inaunganika kwa barabara na maeneo mengi sasa yanafikika kirahisi kwa barabara,ambazo nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami. Hii imesaidia sana kupeleka mahitaji muhimu vjijini na uvutiaji katika uwekezaji, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Tunapenda kuwasihi WaTanzania wenzetu , tutumie kipindi hiki cha mapumziko ni vyema pia kutafakari na kupongeza yale mazuri yaliyofanywa na serikali na vilevile kuungana pamoja na kuchangia katika kuleta Maendeleo ya Mtanzania na si kubeza juhudi za maendeleo kwa sababu ya tofauti za kiitikadi na za kisiasa .

Ni muhimu kwanza tujipongeze wenyewe kama watanzania kwa nafasi pekee tuliyonayo na tunayojivunia ya amani ya nchi yetu. Tusikubali kurubuniwa kwa namna au hali ya aina yeyote na hasa inapobidi tujiulize na kutafakari ni nini kinatufanya watanzania tukawa wamoja , vilevile kudumisha Amani, Umoja na Upendo wetu.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule. TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.

"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

TUBURUDIKE NA WIMBO HUU KATIKA SIKUKUU HII YA KRISMAS

Balozi Peter Kalaghe akutana na Msanii Shilole

$
0
0
Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe akiwa katika  mazungumzo na Msanii wa Muziki wa mduara nchini, Zuwena Mohamed 'Shilole' wakati alipotembelea Ubalozini nchini Uingereza.Shilole yupo nchini Uingereza kwa ajili ya shoo moja iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Ville 640 Ripple road ndani ya Barking IG11 0SR.kwa ushirikiano na Msanii mwenzake AT a.k.a Mfalme wa Mduara.
Balozi Peter Kalaghe akijungumza jambo na Mdau Ayoub Mzee wakati alipoongozana na Msanii Shilole ubalozini hapo.

WAKAZI WA MTWARA WAJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA USAFI WA MJI WAO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Mtwara,Willman Ndile amewahimiza wakazi wa Manspaa ya Mtwara Mikindani kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni ya kufanya usafi wa mazingira ya mji aliyoianzisha ili kuuweka mji uo katika hali ya usafi.

Ndile aliyasema hayo alipokuwa akiongea mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi jana katika eneo la Bima mjini hapa ambapo alisema, ni jambo jema wananchi wanapojitokeza kushiriki katika shughuli za kijamii kuoneshwa namna ambavyo serikali inajali mchango wao licha ya kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo.

Alisema katika siku ya kwanza ya kampeni hiyo wananchi wengi wamejitokeza hali inayomtia hamasa zaidi kuendeleza kampeni hiyo na sasa itakuwa ikifanyika kila siku ya mwisho wa wiki na kuwataka viongozi wa mitaa na kata kuweka mikakati na mipango mizuriya kutekeleza zoezi hilo katika maeneo yao.

Hatua hiyo ya Mkuu huyo wa wilaya kuanzisha kampeni hiyo inatokana na kukithiri wa uchafu kwenye maeneo ya Manspaa ya Mtwara Mikindani huku mamlaka husika zikitupiana lawama kati yao na wananchi na taasisi mbalimbali kuwa ndio wenye jukumu la kufanya usafi hali inayofanya kuwapo kwa vichaka katikati ya mjini na marundo makubwa ya takataka katika makazi ya watu.

Katika kampeni hizo watu mbalimbali walijitokeza wakiwemo wakazi wa manspaa, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, watendaji wa serikali na waandishi wa habari ambapo walishiriki kufanya usafi katika eneo ya kandokando ya barabara kuu itokayo Mnarani hadi bodi ya korosho.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara,Willman Ndile (Aliyeshika kidumu) akishiriki katika kampeni ya kufanya usafi wa mji ambapo viongozi wa siasa, watendaji wa serikali na wananchi wengine walishiriki kampeni hiyo inayofanyika kila mwisho wa wiki.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile, akikusanya takataka tayari kwa kuzichoma moto, kama anavyoonekana hapa eneo la CRDB mjini Mtwara.
Katibu tawala wa wilaya ya Mtwara mkoani hapa, Nuru Ringo, akishiriki katika kampeni ya usafi wa mji iliyoanzishwa na mkuu wa wilaya hiyo, Willman Ndile, hapa anaonekana akizoa matawi ya miti iliyopanguliwa pembezoni mwa barabara eneo la Bima.

SALAMU ZA MSIMU WA SIKUKUU KUTOKA TTCL

TFF yamtangaza Selestin Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo la soka nchini

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akimtangaza Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo,ambaye ni Selestin Mwesigwa (aliewahi kuwa katibu mkuu wa Yanga) (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF,Wakili Evodius Mtawala (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Afisa Habari wa TFF,Boniface Wambura.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria,Wakili Evodius Mtawala nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.kushoto ni Katibu Mkuu wa Mpya wa TFF,Selestin Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestin Mwesigwa nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

VODACOM YAENDELEA KUMWAGA BODABODA KWA WATEJA WAO NCHI NZIMA

$
0
0
Baadhi ya washindi wa Promosheni ya Timka na Boda Boda wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Mwanza baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi pikipiki zao walizojishindia kupitia promosheni hiyo,Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Meneja wa duka la Vodacom Mwanza,Bi.Jumeo Khamis akimkabidhi funguo ya pikipiki Godlove Kanyonga kwa niaba ya mkewe Vianey aliyeshinda kupitia Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Kaimu Mkuu wa kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania,Victoria Chale akimkabidhi funguo ya pikipiki mshindi wa chomoka na bodanoda kutoka Geita, Bijampola, Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania,Bi.Harieth Koka akimkabidhi kadi na kibao cha namba za pikipiki mshindi wa chomoka na bodaboda , Maneno Raamdhan kutoka Igoma Mwanza,Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

Mwanza. Washindi wa 5 kati ya wanane wa Timka na na Boda Boda wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wamekabidhiwa zawadi zao jana na Meneja wa Kanda Harieth Koka,hafla iliyofanyika Jijini Mwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo, Koka alisema kiasi cha shilingi milioni 236 kati ya 436 kimekwishatumika tangu kuanza kwa shindano hilo lilinaloendeshwa na kampuni ya simu ya Vodacom.

Alisema shindano hilo litafikia tamanti Januari mwakani hivyo akawataka wananchi kujitokeza kushiriki shindano hilo na kujinyakulia zawadii kwa ajili ya kuboresha vipato namaisha yao ambapo kila wiki kampuni hiyo inatoa shilingi milioni 5 kaa washindi.

Aidha wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao baadhi ya washindi hao walisema watatumia zaadi ya fedha n pikipiki hizo kwa ajili ya kuboresha vipato vyao na kuendesha maisha ya familia zao.

Godlove MKanyonga ambaye bni Afisa Taibu mkoa wa Mara ambaye akwa pmoja na mkewe wameshinda na kunyakua vitita vya shilingi milioni moja kil pmoja na pikipiki mbili alisema atatumia pikipiki hizo kuwekeza kwenye biashara ya usafiri.

Mwingine ni Bijampola kutoka Geita ambaye alitumia Sh300,000 kushinda zawadi hizo alisema anatarajia kufanyia biashara ya usafirishaji wa abiria.

Aidha Mwanafunzi wa wa mwaka wa nne katika Chuo cha Mtakatifu Agostino, Aloys Kimaro yeye alisema amepata mtaji wa kuanzisha kampuni ya Usafirishaji.

WANAFUNZI WA CBE DODOMA WATOA MKONO WA KHERI YA KRISMASS KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA- MIYUJI

$
0
0
 Hii ni nembo ya kituo hiki iyonacho sadifu mazingira harisi ya watoto wanolelewa mahari hapa.
Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akikabidhi zawadi hizi kwa mlezi wa kituo hiki zilizopokelewa na mtoto katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji jana tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi, akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao.Vitu vilivyotolewa ni Mchele kilo 50, Ngano kilo 50, Mafuta kula lita 20, Mafuta ya kujipata  dazan 1 na Maji carton 2.
Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo akipoke ndoo mbili za mafuta ya kula.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DEATH ANNOUNCEMENT OF OUR TANZANIAN HAPPENED IN N.C

$
0
0
GREENSBORO, N.C. -- Greensboro police have identified the man who died in a wreck Monday morning on I-40 East in Greensboro. 

Officers say his name was Ghazal Mohamed Omar, of Burlington.According to the Greensboro Police Department, a woman driving a Ford Focus lost control of her vehicle. She hit a guardrail and a tractor-trailer hit her as she came back on the highway. 

Omar was the passenger in the Focus. EMS took him to Moses Cone Hospital where he died from his injuries. Police said the woman driver was seriously injured in the accident and went to a hospital for surgery.

The wreck happened before 9 a.m. Monday around mile marker 220.Police closed all lanes for more than 3 1/2 hours while they cleared and investigated the accident. The lanes reopened around 12:30 p.m. 

   R.I.P Our brother Ghazal Mohamed Omar, Ameen Ameen Ameen.

RAMBIRAMBI MSIBA WA JAMES KISAKA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.

Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.

Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.

Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Airtel yawatakia Watanzania heri ya sikukuu

$
0
0
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel imewaasa Watanzania wote kote nchini kulinda amani na utulivu wa nchi katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwa ni baada ya kuwatakia heri ya Christmas na mwaka mpya.

Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema sikukuu za Christmas na mwaka mpya ni sikukuu muhimu sana kwa wananchi wa taifa hili hivyo zinapaswa kusherehekewa kwa amani na utulivu.

“Ninawaomba wateja wa Airtel na watanzania wote kwa ujumla kutambua umuhimu wa sikukuu hizi na kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu wa taifa,” alisema Mmbando.

Aidha alisema katika msimu huu wa sikukuu bado Airtel inazidi kudhihirisha kuwa ni baba lao  kwa wateja wake kwa kutoa  huduma zilizo za gharama nafuu zinazowawezesha kutuma na kupokea pesa bure pia kutumia huduma mbalimbali za inataneti na kupiga kwenda mitandao yote.

“Airtel  bado ni baba lao kupitia huduma zetu mbalimbali, Wateja wetu bado wanaweza kunufaika na huduma zetu ambapo kwa sasa wateja wanaweza kupata vifurushi vya inataneti kwa gharama nafuu, kupiga simu kwenda mitandao yote na pia kutuma na kupokea pesa bure,” alisema Mmbando.

Ikumbukwe kuwa vifurishi vyote vya siku vya Yatosha vinadumu kwa masaa 25 tangu mteja anapojiunga ikiwa na lengo maalumu la kumfanya mteja aweze kufurahia huduma hiyo na kuwafaidisha watanzania waendelee kuokoa pesa nyingti walizokuwa wakizitumia kwenye mawasiliano na kuanza kuzitumia katika shughuli nyingine za uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.

HAPPY BIRTHDAY YA MAMAA WA MITINDO ASIA KHAMSIN IDAROUS YAFANA KWENYE KIOTA CHA NYUMBANI LOUNGE

$
0
0
DSC_1541
Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous jana alisheherekea siku yake ya kuzaliwa na ndugu, jamaa na marafiki katika mnuso wa nguvu uliofanyika kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam. Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio katika mnuso huo wa nguvu.
DSC_1543
Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous, akizungumza machache kabla ya kukata cake kwenye mnuso wake wa kumbukumbu ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye kiota cha Nyumbani Lounge.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU SHEIKH SULEIMAN AMOUR JENDELE ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) kwenye Makaburi alipozikwa kijijini kwake Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) aliyefariki Dunia hivi karibuni wakati alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.Picha na OMR
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images