Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

TAKUKURU YAOMBWA KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA RUSHWA

$
0
0

Na Lydia Churi- Mahakama 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-Takukuru kuyafanyia uchunguzi wa kina malalamiko ya rushwa wanayopokea kutoka kwa wananchi. 

Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ludewa alipomtembelea Mkuu wa Wilaya hiyo, Bwn. Andrea Tsere ofisini kwake, Jaji Mkuu ameiomba Takukuru kuyafanyia uchunguzi malalamiko hayo ili kubaini kama yanatokana na wananchi kutofahamu taratibu za Mahakama au ni tuhuma kweli za rushwa. 

“Takukuru tunawashukuru kwa kuwa mmetupa ramani ya maeneo yenye viashiria vya rushwa lakini sasa tunawaomba muende hatua ya pili ya kuyachunguza malalamiko yanayoletwa kwenu ili kujua kama yanatokana na wananchi kutokujua taratibu au ni malalamiko ya kweli”, alisema Jaji Mkuu. 

Alisema hatua ya Takukuru kuyachunguza malalamiko hayo itairahisishia Mahakama ya Tanzania kufahamu idadi ya wananchi wasiofahamu taratibu za Mahakama pamoja na kujua kiwango halisi cha vitendo vya rushwa ndani ya Mahakama. 

Akizungumzia changamoto za utoaji haki nchini, Jaji Mkuu alisema Mihimili yote mitatu ya dola haina budi kushirikiana kwa karibu kwa kuwa wote wana lengo moja la kumhudumia mwananchi. Aliongeza kuwa huduma za mahakama zinatakiwa kusogezwa karibu zaidi na wananchi kwa ushirikiano wa mihimili yote. 

Alisema changamoto katika kusogeza huduma za mahakama karibu zaidi na wananchi bado ni kubwa na hasa kufikisha haki katika ngazi za chini zikiwemo Mahakama za Mwanzo na za wilaya. 

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania imeandaa Mpango wa miaka mitano unaotoa picha ya maeneo yanayohitaji huduma za Mahakama. Alisema, Mpango huo utaisaidia Mahakama kujipima katika kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. 

“Kuanzia sasa mpaka ifikapo mwaka 2020 tunataka kila mkoa uwe na Mahakama Kuu pamoja na Mahakama za Mwanzo katika kila tarafa nchini”, alisema. 

Aliongeza kuwa Mahakama imeshaandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa majengo yake na endapo kutakuwa na wilaya yenye fedha za ujenzi, Mahakama itashirikiana nayo kujenga. 

Akizungumzia utovu wa maadili, Jaji Mkuu alisema Mahakama haifichi changamoto hiyo na katika kupambana nayo, tayari imesambaza mabango ya kupambana rushwa nchi nzima ili kuimarisha Imani ya wananchi kwa mhimili huo. “Bila kuwa na Imani ya wananchi Mahakama hazitakuwa na maana”, alisema. 

Kuhusu uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati, Jaji Mkuu alisema taratibu za Mahakama hazina budi kuangaliwa upya kwa kuwa baadhi ni ndefu na haziendani na kasi ya ukuaji wa uchumi huku akitolea mfano wa mashauri ya ardhi na yale ya Mirathi kuwa huchukua muda mrefu na mwisho wake thamani ya mali husika hupotea. 

Aliwataka Majaji na Mahakimu kuifahamu jamii inayowazunguka na kuhakikisha wanamaliza mashauri mapema ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi.

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO WA CPA

$
0
0
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (katikati) akiongozana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said (kulia) na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akisalimiana na Watumishi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ndg. Raya Issa Mselemo 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid akisajiliwa kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho cha Mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid (kulia) akipokelewa na Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu alipowasili leo katika hoteli ya Madinalt Al Bahr Mjini Zanzibar, Tanzania ambapo alifika na kukagua maandalizi ya Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika unaotegemea kuanza tarehe 30 Agosti mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said 
(PICHA NA OFISI YA BUNGE) 

………………. 

Na Debora Sanja, Bunge 

Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa waliyoipata ya kuwa wenyeji wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kujitangaza kibiashara na kitalii. 

Mheshimiwa Maulid ametoa rai hiyo leo Kisiwani Zanzibar wakati akikagua maandalizi ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi septemba 5 mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business & Spa. 

Alisema mkutano huo kufanyika Zanzibar utafungua fursa katika sekta za biashara ikiwemo utalii na kuwataka Watanzania kuonyesha ukarimu kwa wageni hao. 

“Tuonyeshe ukarimu wakati kupokea wageni hawa, tuitendee haki nchi yetu, tukikaa nao vizuri wageni wetu itatosha kwa sisi kujitangaza, tutumie fursa hii kwa kadri tutakavyoona inaweza kuisaidia nchi” alisema. 

Alisema mkutano huo ni wa kihistoria kwa kuwa unaweza kuvunja rekodi ya mahudhurio ya wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi 18 wanachama ambao unajumuisha maspika, manaibu spika na wabunge. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPA, Tawi la Zanzibar, Mheshimiwa Simai Mohammed Said alisema mkutano huo mbali na kutoa fursa za kiuchumi lakini pia utawezesha wajumbe kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuisimamia Serikali katika mambo yanayogusa wananchi. 

Awali akizungumzia maandalizi ya awali, Katibu Msaidizi wa CPA, Kanda ya Afrika, Said Yakubu alisema Nchi zote 18 wanachama zimethibitisha ushiriki na kwamba maspika 23 kutoka mabunge makubwa na madogo watahudhuria. 

Alisema nchi wanachama wa CPA, Kanda ya Afrika ni Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Siera – Leone, Afrika ya Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.

WAZIRI LUGOLA, WATENDAJI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAJADILI UTENDAJI KAZI, JIJINI DA R ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo, katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, jijini Dar es Salaam, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alipokua akimfafanulia jambo katika kikao kazi cha Watendaji wa Wizara hiyo (hawapo pichani), kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KESI YA UCHOCHEZI VIONGOZI WA CHADEMA,SHAHIDI ASEMA HAKUWAHI KUPOKEA MALALAMIKO YOYOTE KUTOKA KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

SHAHIDI wa saba katika kesi ya Uchochezi inayowakabili Viongozi tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hakuwai kupokea malalamiko yeyote kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa juu ya mawakala kunyimwa barua za utambukisho wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni.

Shahidi huyo ambae ni afisa Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni, Victoria Wihenge amedai hayo leo Agosti 29,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kujibu maswali ya mwakili wa utetezi.

Akijibu maswali ya Wakili Hekima Mwasipo, shahidi huyo amedai kuwa maneno kama 'Kesho patachimbika, hatuwezi kuendelea kuona watu wanauwawa na kutupwa kwenye mitaro' aliyasikia na yaliyokuwa yakitumika katika kampeni lakini hajawahi kupokea malalamiko kutoka kwa mtu yeyote juu ya maneno hayo. 

Amedai hata baada ya kuyasikia maneno hayo hakuweza kuchukua hatua zozote kwani wakati alipoyasikia kanuni za maadili za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ilikuwa hawezi kufanya kazi tena kwakuwa muda wa kutumika kwa kanuni hizo ulikuwa umeishaisha. 

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya vyama vya siasa yanapelekwa wapi amedai, malalamiko ya wadau wakati wa uchaguzi kwa maana vyama vya siasa, yanapelekwa kwa msimamizi wa uchaguzi ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya maadili.

"Amedai kama mratibu alikuwa anafahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea katika kamati ya maadili na kuongeza kuwa njia ya mawasiliano iliyokuwa inatumika kuanzia ngazi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi mpaka kwa msimamizi wa kituo cha kupigia kura ni ya maandishi yaani kuandika barua", amedai shahidi huyo.

Hata hivyo alidai kuwa ni sahihi barua za utambulisho za mawakala zilipelekwa Februari 17, 2018 katika kila kata ili zipelekwe kwenye vituo 613 vya kupigia kura.

"Barua hizi ziliwafikia mawakala wote waliopo katika vituo hivyo vya kupigia kura, sio sahihi barua hizi wakala anatakiwa kupewa na kusaini," alidai shahidi huyo.

Ameendelea kudai kuwa, hajawai kutoa nyaraka yoyote mahakamani hapo kudhibitisha kuwa mawakala wote walipewa barua na kuongeza kuwa Februari 17 ,2018 wakati wa zoezi la kupiga kura likiendelea yeye alikuwa ofisini kwake.

Akiongozwa na Wakili wa Utetezi John Mallya, Shahidi huyo alidai kuwa kwa mujibu wa kanuni ya uchaguzi vyama vinapaswa kuleta majina ya mawakala wao siku saba kabla ya uchaguzi. 

Amedai kuwa mgombea hawezi kuwa wakala na washtakiwa waliopo mahakamani hapo hakuna hata mmoja ambaye alikuwa kwenye orodha ya mawakala wakati huo wa uchaguzi. 

"Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, wabunge yaani waheshimiwa hawafai kuwa mawakala," alidai shahidi huyo,Aidha alidai hafahamu kuwa Februari 16, 2018 wafuasi wa Chadema walifanya kampeni ya nyumba kwa nyumba.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

SERIKALI INA NIA THABITI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA TASNIA YA NAFAKA KUKOMESHA CHANGAMOTO-WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumzia fursa zilizopo katika tasnia ya nafaka wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ina nia njema kabisa ya kuhakikisha kuwa inashirikiana na wadau wote katika kuhakikisha kuwa tasnia ya nafaka inaendelea na kuondoa changamoto zinazojitokeza. 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Agosti 2019 wakati akifungua mkutano na wafanyabiashara na wasindikaji wa mazao ya nafaka katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano JNICC Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, Serikali peke yake, haiwezi kuziondoa changamoto hizo bila wafanyabiashara, wasindikaji na wasafirishaji kushirikiana na Serikali.

Katika mkutano huo waziri Hasunga amezitaja fursa zilizopo kwenye tasnia ya Nafaka kama ambazo ni pamoja na eneo linalofaa kwa kilimo ambalo linakadiriwa kuwa hekta milioni 44. Kati ya hizo, hekta milioni 29.4 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Eneo hilo, linafaa kwa kilimo cha mazao yote ya biashara na chakula, yakiwemo mazao ya nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na mengineyo. 

Fursa nyingine alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inajitahidi sana kufikisha umeme vijijini ambako ndiko nafaka zinapatikana. Hadi sasa asilimia 70 ya vijiji nchini, vimepatiwa umeme. Umeme huo unatakiwa utumike pia katika eneo la usindikaji. Hadi sasa, sehemu ndogo ya maghala kwenye usindikaji wa mpunga na mahindi kupitia mashine za kukoboa mpunga na mahindi. 

Mhe Hasunga alisema kuwa Kuna baadhi ya maeneo, maghala mazuri yamejengwa kwa usimamizi wa Serikali ili kuwa na uhifadhi mzuri wa nafaka. Mfano, maghala mengi yaliyojengwa wakati wa BRN bado hayajaweza kutumika ipasavyo. 

Alisema Nchi yetu ina ikolojia tofauti tofauti, hali hii inasababisha baadhi ya maeneo kuwa na mvua za kutosha, na maeneo mengine kuwa na uhaba wa mvua. Maeneo yanayopata mvua za kutosha huzalisha chakula cha kutosha pamoja na ziada. Kwa maeneo ambayo yamezalisha ziada, wanayo fursa nzuri ya kupeleka ziada hiyo kwenye maeneo mengine ambayo hayazalishi vizuri. 

“Vilevile, nchi yetu imezungukwa na nchi ambazo hazina fursa kubwa ya kilimo kama tuliyonayo. Miongoni mwa nchi hizo ni kama Uganda, Kenya, Congo, Sudan na nyinginezo. Hii ni fursa nyingine ya soko kwani tukizalisha vizuri, uhakika wa soko la nje, ni mkubwa pia” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amezitaja mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Fursa ya biashara ya mazao ya nafaka katika soko la Afrika na uwezo wa Tanzania kuzalisha nafaka na wafanyabiashara kushiriki kikamilifu, Upotevu wa mazao ya nafaka baada ya mavuno, mkakati wa Taifa wa kudhibiti na matokeo ya utafiti wa hali ya maghala yalivyo hapa nchini, Uongezaji thamani katika mazao na kuboresha mazingira ya biashara ya nafaka na Mfumo wa masoko na uzoefu.

Alisema kuwa mada hizo zitatoa nafasi pia ya kuelewa vizuri tasnia ya nafaka ili kuwa na maazimio ambayo yatajibu changamoto mbalimbali hususani ya upatikanaji wa taarifa na utumiaji vizuri wa fursa zilizopo katika tasnia hiyo.

“Nitoe rai kwa washiriki wote, tusikilize kwa makini, tuwe wawazi, na kwa uhuru tujadili mada hizo kwa mapana na marefu, ili baada ya siku mbili hizi, tutoke na maazimio yatakayojibu changamoto za tasnia hii ya Nafaka” Alisisitiza Mhe Hasunga

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MKUTANO WA SITA WA JUKWAA LA UONGOZI AFRIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wastaafu katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Taasisi ya Uongozi baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Somalia Mhe. Hassan Mohamed alipowasili kuhutubia Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019. Wanaofuatia kulia kwake ni Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki na Mfanyabiashara mashuhuri wa Tanzania Bw. Ally Mufuruki

 
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikaribisha chakula cha mchana na viongozi wastaafu na na wageni wengine wakati wa mapumziko ya mchana katika Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2019 PICHA NA IKULU 

SIMIYU YAANDAA MKAKATI MAALUM WA MIAKA MITANO WA MAPINDUZI YA KILIMO CHA PAMBA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,

Akifungua Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.

“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani mazao hayo.

Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine zaidi ya kuchambua pamba.

Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru

“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.

Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo na akazitaka Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.

Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika ufunguzi wa Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James akitoa salamu zake kwa Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Miradi wa Gatsby Africa, Samweli Kilua akitoa taarifa ya namna shirika hilo lilivyoshiriki katika uaandaaji wa Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, kwenye mkutano wa kuboresha mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wwa Mataifa(UNDP), Amon Manyama akichangia hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
 Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akiwasilisha mkakati wa maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa Wawakilishi wa Wakurugenzi na wamiliki wa Viwanda vya Kuchambua pamba kutoka kiwanda cha Alliance Ginneries Ltd, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.

RC Wangabo ataka ujenzi wa VETA Sumbawanga kuharakishwa ili kuanza kudahili wanafunzi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Tender International kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA kilichopo Kata ya Sumbawanga Wenyeji Wilayani Sumbawanga ndani ya mwaka huu ili kufikia mwezi Januari mwaka 2020 kianze kudahili wanafunzi katika fani mbalimbali za ufundi.

Chuo hicho ambacho ujenzi wake ulitakiwa kumalizika Septemba 21, 2019 bado haujakamilika kutokana na Mkandarasi huyo kutegemea fedha za ujenzi kutoka serikalini na hivyo kuomba kuongezewa muda wa miezi minne ili aweze kumalizia ambapo hadi sasa ameshalipwa shilingi bilioni 2.6 kwaajili ya ujenzi wa majengo 22 ikiwemo karakana mbalimbali za mafunzo, mabweni, madarasa na nyumba za watumishi.

Mbali na changamoto hiyo Mh. Wangabo pia amepongeza kiwango cha ubora wa majengo hayo ambayo kwasasa yapo katika hatua ya kupauliwa na kuongeza kuwa kama kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imeridhishwa na kiwango cha majengo ya chuo hicho hadi hapo kilipofikia.

“VETA hii ilianza kujengwa mwaka jana mwezi wa tisa na ilitegemewa iwe imemalizika mwaka huu, kipindi cha mwaka mmoja. Lakini kumekuwa na changamoto za hapa na pale upande wa mkandarasi n ahata upande wa wizara inayohusika, basi hizi changamoto zimefikia kwenye hatua ambayo sasa tunaweza kwenda vizuri, Mkandarasi ameomba kuongezewa miezi minne na hii mimi nitaifuatilia, kuhakikisha kwamba hii ‘extention’ inakwenda haraka ili ikamilike ili ianze kuchukua wananfunzi Januari 2020,” Alisema.

Ameyasema hayo leo tarehe 29.8.2019 alipotembelea katika eneo la Ujenzi wa Chuo hicho kinachotarajiwa kudahili wanafunzi 600 wa masomo ya muda mrefu na wanafunzi 2000 wa masomo ya muda mfupi katika fani za umeme wa majumbani, umeme wa magari, ushonaji, mapishi, ufundi wa kompyuta, ufundi wa magari, useremala, na usindikaji wa chakula.

Awali akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya ujenzi wa Chuo hicho karani wa Mradi Mhandisi Jeremiah Longido alisema kuwa endapo serikali italipa fedha za ujenzi kwa wakati wana uhakika kwamba majengo hayo yatakamilika katika kipindi hicho cha miezi minne waliyoiomba na hatimae kufikia mwezi January, 2020 kuanza kudahili wanafunzi.

“Kama ‘Cash flow’ itakwenda vizuri, hii miezi minne kama kazi itafanyika kwa nguvu tunaweza kumaliza kazi, kwasababi amelipwa ‘certificate’ namba nne ambayo ni kama milioni 130 lakini kuna ‘certificate’ namba tano kama milioni 640 amabyo ipo tayari ambapo mda wowote anaweza kulipwa kwahiyo kama hiyo atapokea inamaanisha tutakuwa vizuri,” Alisema.

Katika Hatua nyingine, Mh. Wangabo amesikitishwa na kasi ya konokono katika ujenzi wa hospitali za Wilaya ambazo kwa mujinbu wa tarehe za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, hospitali hizo ziliongezewa muda wa kuisha kwake na zilitakiwa kumalizika na kukabidhiwa tarehe 31.8.2019 kwaajili ya kuanza kutumika.

“Kasi yenu ni ndogo, kasi ya konokono, vifaa havipo hata ujenzi katika jengo hili la utawala hakuna, hali kwakweli ni hovyo na si nzuri ni mbaya muda umekwishaisha, kwahiyo nashindwa hata kuwaambia kuna siku za nyongeza kwasababu kuna ‘deadline’ ya TAMISEMI. Sasa fanyeni juu chini kwa siku zilizobakia mmalize hapa sasa sijui mtaweka hema ama mtafanyaje lakini fanyeni juu chini hii kazi iishe,” Alisisitiza

Ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, viongozi na wataalamu wa wilaya ya Sumbawanga ambapo kabla ya kufika hapo pia alitembelea hospitali ya Wilaya ya Nkasi na hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
  Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa Mbele) akikagua jengo la Utawala katika Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga iliyoko katika Kata ya Mtowisa, bonde la ziwa Rukwa
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia) akiongozana akiongozana na Karani wa Mradi wa ujenzi wa Chuo Cha Ufundi VETA Mkoani Rukwa Mhandisi Jeremiah Longido wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa chuo hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa mbele) pamoja na viongozi na wataalamu wengine wakitoka katika jengo la Maabara la hospitali ya Wilaya ya Nkasi.
Baadhi ya majengo ya Chuo Cha Ufundi VETA Mkoani Rukwa

Waziri Mwakyembe Akutana na Kujadiliana na Wahariri Juu ya Tamasha la JAMAFEST

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati alipokutana nao leo29 Agosti, 2019 jijini Dar es Salaam kuzungumzia Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.

  Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao leo 29 Agosti, 2019 jijini Dar es Salaam kuzungumzia Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akifafanua  jambo kwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati alipokutana nao leo29 Agosti, 2019  jijini Dar es Salaam kuzungumzia Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao leo29 Agosti, 2019  jijini Dar es Salaam kuzungumzia Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Mhariri Mkuu wa E. FM Radio, Scholastica Mazula akichangia mada wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alipokutana na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo  29 Agosti, 2019 jijini Dar es Salaam kuzungumzia Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA YAPONGEZWA KWA KUWA NA MFUMO WA UTOAJI VIBALI KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ameipongeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kuwa na mfumo wa utoaji vibali kwa njia ya mtandao.

Naibu Waziri, Dkt. Ndugulile ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipotembelea na kujifunza TMDA kuhusu mifumo ya udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa upande wa Bara.

Amesema mfumo wa mtandao umerahisisha wateja kuomba vibali huko waliko bila ya kufika ofisini na hivyo kuboresha utoaji huduma kwa jamii. 
Aidha, Dkt. Ndugulile amepongeza utayari wa TMDA katika kutoa msaada wa kiufundi kwa taasisi nyingine za kiudhibiti.

Dkt. Ndugulile amesisitiza ushirikiano kati ya TMDA na taasisi ya ZFDA ya zanzibar katika uboreshaji wa utoaji huduma bora za udhibiti wa dawa nchini.

Vilevile, Naibu Waziri ameitaka TMDA kuanza mchakato wa kufuzu ngazi ya nne ya Shirika la Afya Duniani (WHO maturity Level 4) maana vigezo na uwezo upo kutokana na kazi kubwa inayofanyika katika katika udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Amesema TMDA hivi sasa imekuwa taasisi ya kwanza Barani Afrika kufikia ngazi ya 3 ya WHO (ML3) jambo ambalo nchi inajivunia kwakuwa usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaatiba na vitendanishi huakikiwa ipasavyo kabla ya kumfikia mtumiaji ili kulinda afya ya jamii nchini.

Ndugulile amesisitiza kuwa dawa zote zilizo nchini kutoka ndani na nje ya nchi ni salama na hakuna dawa yenye madhara kwa binadamu.Pia amekemea matumizi mabaya ya dawa hususani vijiua sumu (antibiotic ) na kuwataka wauzaji wenye maduka ya dawa kuacha kuuza dawa bila ya cheti cha daktari.

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika ziara yao imetembelea pia maabara ya TMDA ili kujionea uwekezaji mkubwa wa mitambo iliyopo na kuona namna ya kuboresha kwa upande wa visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mara baada ya kuwapokea Wajumbe wa Kamati ya Bajeti Bunge la wawakilishi  Zanzibar walipotembelea  ofisi za Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),leo jijini Dar .Picha na Emmanuel Massaka wa michuzi Tv).
 Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika maabara ya TMDA ili kujionea uwekezaji mkubwa wa mitambo iliyopo wakati wa ziara ya kujifunza mambo mbalimbali katika maabara hiyo, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa michuzi Tv)
 Picha ya pamoja

SHIRIKA LA FCS LATOA MILIONI 40 KUDHIBITI UKEKETAJI WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Washiriki wa mafunzo ya kupinga mila potofu ya ukeketaji wakionesha mshikamano wa mapambano dhidi ya vitendo hivyo baada ya kuunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida juzi.
Mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya akizungumza katika mkutano wa kuunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto wilayani Ikungi mkoani humo.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi, Haroon Haroon akiwasilisha mwongozo wa ( MTAKUWA) kwa kamati za ulinzi wa mama na mototo ngazi ya Kata sita za Ikungi,Ihanja, Iglanson, Iseke, Mhintiri na Minyughe.
Mwezeshaji, Daniel Saido akiwa na Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Ihanja, Sombi Majuta akizungumza katika mkutano
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo akizungumza katika mkutano huo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya mradi wa kupambana na mila potofu za ukeketaji mkoani Singida ambao umeanza mwezi Julai hadi Machi 2020. 

Fedha hizo zimetolewa kwa Shirika lisilo la kiserikali la Save the Mother and the Children of Central Tanzania (SMCCT), ambalo limeunda kamati za ulinzi wa mama na mtoto kwenye kata sita na vijiji 18 katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya mapambano hayo. 

Imeelezwa kwamba majukumu ya kamati hizo ni kumlinda mama na mtoto dhidi ya vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. 

Hayo yalisemwa na mwezeshaji wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu, Japhet Kalegeya wilaya ni hapa juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ambao utasaidi kupunguza vitendo hivyo au kuvimaliza kabisa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali. 

Alisema wamefikia uamuzi wa kuanzisha kamati hizo ili ziweze kuharakisha kutokomeza kabisa vitendo hivyo ambavyo vipo kinyume na haki za binadamu kama vile ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba za utotoni, ndoa za utotoni ,ubakaji ,ulawiti,ukeketaji na udhalilishaji wa kijinsia katika wilaya hiyo. 

“Mradi huu wa utetezi dhidi ya mila potofu ikiwemo ukeketaji na ukatili wa kijinsia unalenga kuwafikia wanawake na wasichana wapatao 7,200 katika wilaya ya Ikungi ambapo hali ya unyanyasaji wa kijinsia ni mbaya”, alisema Kalegeya.

Akitolea mfano wa hali hiyo alisema kuanzia Januari hadi oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 23 waliokuwa kati ya kidato cha kwanza na nne walipachikwa mimba wilayani Ikungi.

Naye mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Masinda, Rosemary Seith, amelishukru na kulipongeza shirika la SMCCT kwa kushirikisha baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwapa elimu juu ya madhara ya ukeketaji na ukatili wa kijinsia. 

“Sisi tuliohudhuria mafunzo haya yametusaidia kujua kwa mapana madhara ya vitendo hivyo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia sasa tunaenda kuwaelimisha na wenzetu ambao hawakubahatika kupata mafunzo haya hapa leo”, alisema. 

Mratibu wa mradi huo, Evaline Lyimo, ametaja baadhi ya malengo ya mradi huo kuwa ni kuongezeka kwa uelewa kwa jamii kuhusu kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji na kuimarisha mfumo wa utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii hadi ifikapo Machi mwaka 2021.

Kata zilizounda kamati hizo ni lkungi, Ihanja, Iglansoni,Iseke, Minyughe na Muhintiri.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE PROF JOHN KABUDI AFANYA MAZUNGUMZO NA MEYA WA NAGAI NCHINI JAPAN

$
0
0
Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Uchiya jarida linaloonesha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini 
 Prof. Kabudi akiagana na Mhe. Shigeharu Uchiya mara baada ya kumaliza mazungumzo kati yao 
 Prof. Kabudi akisalimiana na mmoja wa raia wa Japan aliyewahi kufanya kazi za kujitolea kwenye sekta ya afya nchini Tanzania miaka ya 1960.





Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Nagai nchini Japan 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuishirikisha Tanzania kikamilifu kwenye maandalizi ya Michezo ya Olympic inayotarajiwa kufanyika jijini Tokyo mwaka 2020 ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake kutoka Tanzania.

Mhe.Prof. Kabudi ametoa shukrani hizo wakati wa mkutano wake na Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya uliofanyika leo tarehe 29 Agosti 2019 jijini Yokohama pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika (TICAD 7).

Mhe. Prof. Kabudi alisema kuwa, anaishukuru Japan kwa kuwa imeonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania ishiriki kwenye Michezo hiyo muhimu ya Olympic ambayo itafanyika nchini humo mwaka 2020 na kuzishirikisha nchi zote duniani. Mhe. Waziri alifafanua kuwa tayari Serikali hiyo imesaini Hati ya Makubaliano na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwezi Julai 2019 kuhusu ushiriki wa Tanzania kwenye michezo hiyo pamoja na kufanikisha ziara ya Timu ya wanariadha kutoka nchini wakiongozwa na mkimbiaji wa mbio za marathon mstaafu, Bw. Juma Ikangaa iliyofanyika mwezi Oktoba 2018. Pia Japan imeahidi kutoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake yatakayotolewa jijini Nagai. 

“Ushikiano wa kirafiki kati ya Japan na Tanzania ni wa miaka mingi hususan kwenye medani za siasa, uchumi na diplomasia. Umefika wakati sasa nchi hizi mbili zishirikiane katika masuala ya kijamii na utamaduni ili kuwaunganisha mtu mmoja mmoja na kwamba ushirikiano huo ndio muhimu kwa ukuaji wa Taifa lolote” alisema Prof. Kabudi.

Aidha, alieleza kufurahishwa na ahadi kuwa Japan itatoa mafunzo kwa wanamichezo wanawake ili kuwajengea uwezo kwenye michezo mbalimbali ikiwemo ile ya Olympic itakayofanyika Tokyo mwaka 2020. “Tumepokea kwa furaha taarifa kwamba Nagai itatoa mafunzo kwa wanamichezo wetu wanawake. Hii itawajengea uwezo mkubwa wanamichezo hao wakati wakijiandaa na mashindano ya Olympic” alisisitiza Prof. Kabudi.

Kadhalika, Mhe. Prof. Kabudi alitumia fursa hiyo kumweleza Mhe. Uchiya kuwa Serikali ya Tanzania imehamishia shughuli zake jijini Dodoma ambako ni Makao Makuu ya nchi na kwamba ipo tayari kuanzisha ushirikiano wa kidada kati ya Jiji la Dodoma na Jiji la Nagai.

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Nagai, Mhe. Shigeharu Uchiya alisema kwamba jiji hilo litaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania na tayari limeanzisha program ya kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya michezo ambapo Mtanzania, Bw. Bahati Rogers ni miongoni mwa vijana wanaoshiriki program hiyo jijini humo. Pia alisema kuwa aliongoza ujumbe wa watu ishirini kutembelea Tanzania mwaka 2017 kwa ajili ya kubadilisha uzoefu kuhusu michezo.

Serikali ya Japan ambayo imeanza maandalizi ya Michezo ya Kimataifa ya Olympic itakayofanyika jijini Tokyo mwaka 2020, imetenga Jiji la Nagai kuwa kituo cha Wanamichezo wote wa Tanzania kitakachotumika kuwaadaa kabla ya kuanza kushiriki michezo hiyo rasmi. Maandalizi hayo ni pamoja na kuwawezesha wanamichezo kuzoea hali ya hewa, tamaduni, chakula na masuala mengine muhimu kuhusu Japan kabla ya ushiriki wao rasmi wa michezo hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasil
iano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Yokohama, Japan
29 Agosti 2019

MAHAKAMA YA TANZANIA YATOA ELIMU KUHUSU MAHAKAMA INAYOTEMBEA DAR

$
0
0


Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakisoma vipeperushi vya Mahakama Inayotembea wakati gari maalum la Mahakama hiyo lilipokuwa likitoa elimu kwa umma  kuhusu Mahakama hiyo.
 Dereva wa pikipiki akisoma kipeperushi cha gari  maalum la  Mahakama Inayotembea leo wakati wa utoaji elimu kwa umma kuhusu mahakama hiyo, huku wenzake wakiendelea kusikiliza matangazo yaliyokuwa yakitolewa  na gari hilo kwenye eneo la Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam 
 Wananchi wakipatiwa elimu kuhusu Mahakama Inayotembea na Karani Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba ndani ya gari hilo maalum lililokuwa limepaki eneo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju 
Karani wa Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(mwenye shati la njano ndani ya gari hilo maalum ) akitoa elimu  kwa umma kuhusu Mahakama Inayotembea na shughuli zitakazofanywa na Mahakama hiyo, kwa wakazi wa Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa elimu kwa Umma.

MEJA KUNTA AWAOMBA WASANII WASINGELI KUUMIZA KICHWA KUTUNGA NYIMBO ZENYE KUJENGA JAMII

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi tv


MSANII chipukizi wa Muziki wa Singeli Mwalami sadiki(Meja kunta) amewataka wadau wa Muziki kutoa ushirikiano na kuuchukulia o muziki wa Singeli wa kipekee sana.

Meja amesema ni wakati umefika tuwaaminishe kuwa tunaweza na tutaufikisha mziki wa Singeli mbali kwa ni wakipekee na unapatikana Tanzania tu.

Pia ametoa ushauri kwa waimbaji wasingeli kujaribu kujichanganya na kufanya kazi na wasanii wa miziki mbalimbali kama taarabu,bolingo, Bongofleva.

"Tusijitenge sana, tujichanganye na ndio maana Nina ndoto za kufanya kazi na Vanessa mdee,"Aidha amesema bado amekumbana na changamoto nyingi sana tangu aingie rasmi kwenye fani hiyo ya muziki wa Singeli.

"Bado kuna baadhi ya jamii wanaamini Muziki wa Singeli ni wakihuni haufai katika jamii kutokana na baadhi ya tungo nyingi kuhamasisha mambo ya kihuni,"

Hata hivyo amewashukuru mshabiki zake kumpokea vizuri kwenye Muziki huo wa Singeli na kibao chake cha "Mamu" kuendelea kutikisa kila kona.

"Bado naendelea kuumiza kichwa ili kuendelea kuwa pamoja na mashabiki zangu na nimelenga hasa kwenye tungo zenye kutufundisha na kutujenga zaidi kuliko kupotosha jamii yetu,"Nina ndoto za kufanya kazi na msau,"

WAPEWA MIEZI MITATU KULIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 500

$
0
0

Na Jusline Marco Arusha

Waziri wa ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.William Lukuvi ametoa muda wa miezi mitatu kwa wavamizi 110 waliovamia wa eneo la Bibi.Nancy Muruo kulipa gharama ya ardhi ambayo walijimilikisha kinyume na sheria na kuwataka kumlipa fidia ya shilingi milioni 500.

Ametoa agizo hilo katika Kata ya Sinoni Mkoani Arusha mara baada ya zoezi la upimaji wa eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 8 kukamilika kufuatia wataalamu wa ardhi kutoka wizarani kupima eneo hilo kutokana na kuwepo kwa mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka mingi na kusema kuwa kila mmoja atalipa kulingana na ukubwa wa eneo alilonalo ambapo kwa kila mita moja in apaswa kulipiwa shilingi elfu ishirini.

Waziri Lukuvi amesema kuwa gharama ambazo wavamizi hao wanapaswa kulipa ni makadirio ambayo yametolewa na serikali ya awamu ya tano badala ya kutekeleza amri ya mahakana ya kuyavunja makazi hayo na kurudisha eneo kwa bibi huyo kutoka na wengi wao kuonekana kutokuwa na kipato chochote.

Ameongeza kuwa pamoja na ulipaji wa gharama za ardhi pia zipo gharama nyingine ambazo kila mmoja aliyejimilikisha eneo la bibi huyo anapaswa kulipa ikiwemo ulipaji wa hati miliki ili kuweza kubadili jina kutoka kuwa mvamizi na kuwa mmiliki halali,kulipia gharama za kutengeneza hati,kodi ya mbele ya thamani ya ardhi ambayo imepunguzwa kutoka asilimia mbili na nusu na kuwa asilimia moja.

Hata hivyo hatua hiyo imefikiwa baada ya Bibi.Nancy Muruo mwenye umri wa miaka 98 kumfuata Rais John Magufuli Ikuli jijini Dar es salaam kwa lengo la kuomba msaada ili aweza kurudishiwa eneo lake hilo ambalo alidhulumiwa tangu mwaka 1979.

Sambamba na hayo bibi huyo alianza mchakato wa kurudisha ardhi yake ambayo aliyodhulumiwa na mmoja kati ya ndugu zake mnamo mwaka 1979 ambapo katika hatua zote alikuwa akishinda lakini amekuwa akinyimwa maeneo yake.
Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akimsalimia bibi Nancy Muruo mara baada ya kuwasili katika Kata ya Sinoni Mkoani Arusha kwa ajili ya kutoa maamuzi yaliyofanywa na serikali kupitia wizara ya ardhi kufuatia kuwepo kwa wavamuzi 110 waliovamia eneo la bibi huyo.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JICA NA AfDB WATIA SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI AFRIKA

$
0
0
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina na Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japani, Dkt. Shinichi Kitaoka wakipongezana mara baada ya kutia saini Marekebisho ya Makubaliano (Amendment of MoU) katika ushirikiano wao wa uwekezaji kwa pamoja barani Afrika. Wengine ni wadau mbalimbali kutoka Sekta za Umma na Binafsi waliohudhuria hafla hiyo.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina na Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japani, Dkt. Shinichi Kitaoka wakitia saini Marekebisho ya Makubaliano (Amendment of MoU) katika ushirikiano wao wa uwekezaji kwa pamoja barani Afrika. Wengine katika picha ni wadau mbalimbali kutoka Sekta za Umma na Binafsi waliohudhuria hafla hiyo
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, akiwa kwenye kikao na Kobe Nabuyuki kutoka Makao Makuu ya JICA ambaye ni msimamizi wa miradi ya Sekta ya Nishati nchini Tanzania. Katika Kikao hicho kilichofanyika Tokyo, Japani, walijadili kuhusu miradi mbalimbali ya Nishati nchini.

………………….

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japani (JICA) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wametia saini Marekebisho ya Makubaliano (Amendment of MoU) katika ushirikiano wao wa uwekezaji kwa pamoja barani Afrika. 

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina na Rais wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japani, Dkt. Shinichi Kitaoka wametia saini Makubaliano hayo, Tarehe 30 Agosti 2019, katika Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) unaofanyika Tokyo, Japani na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha wa Japani, Keisuke Suzuki pamoja na Wadau wa sekta ya Umma na binafsi.

Katika Makubaliano hayo, Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika zitaendelea kunufaika na uwekezaji wa pamoja wa JICA na AfDB unaofanywa katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Nishati.

Kwa upande wa Tanzania, hadi sasa JICA na AfDB, wakishirikiana na Washirika wengine wa Maendeleo wamehusika katika ufadhili wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 673 (Backbone) ya kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Tabora. 

Vilevile, miradi mingine inayofadhiliwa kwa pamoja na JICA na AfDB ni pamoja na mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 514 kutoka Singida hadi Kenya kupitia Arusha na mradi wa upanuzi wa vituo vya kupoza umeme wa gridi vilivyopo Dodoma na Singida.

Aidha, katika Mkutano huo, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, alifanya kikao na Kobe Nabuyuki kutoka Makao Makuu ya JICA ambaye ni msimamizi wa miradi ya Sekta ya Nishati nchini Tanzania.

Katika kikao hicho, walijadili utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 300 kwa kutumia Gesi Asilia utakaojengwa mkoani Mtwara, mradi wa kuboresha miundombinu ya kusambaza umeme katika Jiji la Dodoma pamoja na mradi wa kuzalisha Umeme MW 200 kwa kutumia Joto Ardhi. 

Mkutano wa TICAD 7 ambao unajadili Maendeleo ya Afrika katika Sekta mbalimbali, unatarajiwa kufikia kilele leo tarehe 30 Agosti 2019.

RC Dodoma atoa onyo kwa watakaofanya ubadhirifu kwenye mradi wa maji Kondoa

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Binilith Mahenge amewatahadharisha wananchi pamoja na mkandarasi anayejenga mradi wa maji katika kitongoji cha Fai kijiji cha Ntomoko wilayani Kondoa kutoharibu mradi huo kwani yeyote atakaethubutu kufanya hivyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Imeelezwa kuwa mradi huo ambao Chanzo chake ni chemichemi yenye uwezo wa kuzalisha lita laki 5 na elfu 27 kwa siku pindi utakapo kamilika utahudumia wananchi elfu 21 kutoka katika vijiji vinne vya wilaya ya Kondoa na Chemba.

Dkt,Mahenge amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo na kisha kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Ntomoko ambapo mbali na kuwahakikisha maji kutoka mapema mwezi Octoba mwaka huu pia amesema kuwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametenga Jumla ya Shilingi Bilion 2.2 kwa ajili ya kuhakikisha wananchi hao wanapata maji, hivyo mtu yeyote atakaefanya ubadhilifu katika maradi huo atawajibishwa.

"Mimi ndio Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,nimekuja kuwahakikishia kuwa safari hii maji mnapata,sasa hivi tuna watu wa uhakika na nimeongea na mkandarasi amenihakikishia kuwa hadi kufikia mwezi wa kumi maji yatakuwa yanatoka hapa,watakaoharibu tunawasweka wote ndani,hakuna mtu kupona hapa,lazima wahakikishe mradi huu unakamilika"Alisema

Aidha pia Dkt,Mahenge amewaomba wazee na Serikali ya kijiji hicho kuwasimamia wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu jirani ya chanzo hicho ili kutosababisha maji kupungua

"Wazee wa eneo hili na Serikali ya Kijiji hapa naombeni muwaambie wananchi wenu waache kuharibu chanzo hiki cha maji,kwani itafikia kipindi maji yatapungua na mwishowe yatakauka kabisa,na kama ikitokea hivyo nyie wote mtakosa maji,kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake hakikisheni hamfanyi shughuli za kibinadamu kwenye eneo hili"Aliongeza

Kwa upande wake Mhandisi John Orest kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) yeye amesema kuwa mkandarasi wa mradi huo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuanzia June 7 mwaka huu na tayari amekwisha lipwa jumla ya Shilingi Milioni 680 sawa na asilimia 6.4 ya fedha zote

Wananchi wa eneo hilo wamempongeza Rais Dkt.Magufuli huku wakisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawaondolea adha kubwa walioyonayo ya kuasafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo muhimu ya Maji.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Fai wilayani Kondoa alipofika kukagua maendeleo ya mradi wa Maji unaojengwa

SPIKA WA BUNGE LA LESOTHO AWASILI NCHINI KWA AJILI YA MKUTANO WA 50 WA CPA

$
0
0
Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na kupokelewa na Maafisa Itifaki wa Bunge la Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika utakaofanyika tarehe 30 Agosti hadi tarehe 5 Septemba mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business and Spa

IGP SIRRO AKUTANA NA IGP WA SUDANI

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani. Picha na Jeshi la Polisi Nchini.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, wakati akitoa hotuba mbele ya Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi hilo (hawapo pichani) jijini Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea zawadi kutoka kwa  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, ambaye yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, ziara ambayo imelenga kuzidi kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Sudani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil  Mohamed Ahmed, wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi baada ya kumaliza kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi Nchini.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images