Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Tukio zima la HAFLA ya kutimia mwaka mmoja toka kuanza Safari za Treni za Mizigo TANZANIA - UGANDA


WAZIRI MKUU ASHIRIKI TICAD7- YOKOHOMA, JAPAN IKITOA DOLA BILIONI 20 KUSAIDIA MAENDELEO KWA NCHI ZA AFRIKA

$
0
0


Japan imetangaza kutenga kiasi cha dola za kimarekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa Nchi za Bara la Afrika ili kuziwezesha Nchi hizo kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi katika Bara la Afrika huku Tanzania ikikazia mkakati wake wa uchumi wa viwanda.

Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shinzo Abe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo Internatinaol Conference on African Development TICAD7) uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Pacifico jijini Yokohama na kuongeza kuwa Serikali ya Japan itaendelea kuchangia maendeleo ya Bara la Afrika kupitia program mbalimbali za ushirikiano kwa kuimarisha rasilimali watu, elimu ya awali kwa watoto na kuboresha huduma ya afya kwa wote.
.

Mhe. Abe amesema kuwa, kupitia Mpango wa TICAD, ushirikiano kati ya Japan na Afrika umeimarika na kwamba nchi hiyo itaendelea kuhakikisha inahamasisha Kampuni za Japan kuwekeza Afrika ambapo hadi sasa sekta binafsi ya Japan imewekeza dola za marekani bilioni 20 katika nchi mbalimbali za Afrika.

Akizungumzia program mbalimbali zinazotekelezwa na Japan katika kuchangia maendeleo ya Afrika ikiwemo ile ya ABE-African Businness Education Initiative, Waziri Mkuu huyo amesema kuwa tayari vijana zaidi ya 350 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanafanya mafunzo kwa vitendo kwenye Kampuni mbalimbali kupitia mpango huo na wengine 3000 ambao walishapitia mpango huo kama wawezeshaji.

Mhe. Abe amesema kuwa, Japan itaendelea kuchangia kwenye sekta ya afya hususan kwenye masuala ya dawa, lishe na kutoa mafunzo ya ujuzi kuhusu masuala hayo kwa nchi mbalimbali za Afrika. Pia Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Afrika kwenye ujenzi wa miundombinu kama barabara na bandari pamoja kutoa wataalam kwani nchi yake haijawahi kupungukiwa wataalam.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anahudhuria mkutano huo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Afrika zinazozalisha malighafi zinazosafirishwa nje kwa ajili ya kuongezewa thamani jambo linalofanya Bara la Afrika Tanzania ikiwemo kujikuta ikisafirisha ajira na kutengeneza soko la bidhaa kutoka katika mataifa mengine na kwamba sasa Tanzania imedhamiria kupitia viwanda kutumia malighafi zake kuzalisha bidhaa mbalimbali na hivyo kutengeneza ajira kwa watu wake lakini pia kuuza nje ya nchi na kuzalisha fedha za kigeni.
Ameongeza kuwa kupitia mkakati wa Japan kwa nchi za Afrika Tanzania ni mojawapo ya nchi zitakazonufaika na mkakati huo na kuongeza kuwa mojawapo ya maeneo ya kuboresha ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda ni kujenga miundo mbinu imara itakayoweka msingi wa kufikia malengo hayo kwa kuwezesha usafirishaji wa bidhaa pamoja na malighafi zitakazotumika katika viwanda.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema tofauti na mikutano iliyotangulia Mkutano huu wa TICAD saba kwa mara ya kwanza umeweka fursa ya kuwa na mpango kazi wa Yokohama ambapo badala ya kuwa na maazimio pekee sasa kutakuwa na fursa ya kuweka malengo vilevile kupima utekelezaji wake na upatikanaji wa fedha.

Rais wa Misri, Mhe. Abdel Fattah el-Sisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa TICAD 7, Mhe. El-Sisi amesema kuwa Afrika kwa sasa inahitaji mapinduzi katika teknolojia na uvumbuzi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinalolikabili Bara hilo ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na mabadiliko ya tabia. Aidha, ametoa rai kwa nchi zinalizoendelea kutekeleza ahadi zao pamoja na Mkataba wa Paris kuhusu kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Mhe. Rais El-Sisi alitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha wawekezaji kutoka Japan kuwekeza Afrika pamoja na kuzitaka taasisi za kifedha za kimataifa kutoa masharti nafuu ya mikopo ili kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara barani Afrika.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guteres ameipongeza Japan kwa ushirikiano wake na nchi za Afrika hususan katika kuunga mkono jitihada mbalimbali za kudumisha amani na usalama baranii humo. Pia amezipongeza nchi za Afrika kwa kuanzisha Mpango wa Eneo Huru la Biashara barani humo ambao kwa kiasi kikubwa utaimarisha sekta ya biashara na uwekezaji na kuchangia maendeleo ya nchi hizo. Mhe. Guteres amesisistiza kuwa nchi za Afrika kwa kushirikiana na Japan ziwekeze kwenye elimu bora kwa vijana hususan kwenye maeneo ya sayansi, hesabu na teknolojia kwani yana mchango mkubwa katika maendeleo. 

Akizungumzia mabadiliko ya tabianchi, Mhe. Guteres amesema kuwa jitihada za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaziathiri nchi za Afrika. Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa ameitisha Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika jijini New York, Marekani mwezi Septemba 2019 ili kwa pamoja nchi zijadili namna ya kuendelea kutatua changamoto hizo.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Moussa Faki Mahamat ambao hushirikiana na Japan kuandaa mikutano ya TICAD, amesema kuwa, Mkutano wa Saba umekuja na suluhisho kwa vijana kuhusu masuala ya teknolojia na uvumbuzi na kusisistiza kwamba suala hilo ni la kipaumbele kwa nchi za Afrika.

Mkutano wa Saba wa TICAD ambao umebeba kaulimbiu ya Kuiendeleza Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi, umehudhuriwa na zaidi ya washiriki 4,000 pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 44 za Afrika.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama, Japan.
28 Agosti 2019
Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa kaaika Mkutano wa Kimataifa Tokyo kuhusu Maendeleo kwa Bara la Afrika. Nyuma yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb). Mkutano huo unafanyika Yokohama,Japan.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akisaliqmiana na Waziri Mkuu wa Mauritius Mhe Pravind Jugnauth walipokutana na kufanya mazungumzo katika Mji wa Yokohoma Japan.


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akisikiliza jambo kutoka kwa Waziri Mkuu wa Mauritius Mhe Pravind Jugnauth. Viongozi wote wawili walikutana na kufanya mazungumzo ya namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia baina ya Nchi hizo. wote wapo katika Mji wa Yokohoma,Japan kushiriki mkutano wa TICAD7.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akiwa na Waziri Mkuu wa Mauritius Mhe Pravind Jugnauth walipokutana na kufanya mazungumzo katika mji wa Yokohoma Japan. Kushoto kwa Mhe. Majaliwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (Mb).

NAIBU WAZIRI KANYASU AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU KWA MIAKA 10 MKOANI MOROGORO

$
0
0

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Gairo akiangalia huku akizungumza kwenye miti iliyopangwa kwa ajili ya  kuchoma mkaa mara baada ya kufanya ziara  katika Hifadhi ya Msitu wa Kumbulu kujionea miti iliyokatwa  kinyume na sheria katika Hifadhi hiyo  wilayani  Gairo mkoani Morogoro.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizumgumza na wananchi wa kijiji cha Kumbulu wakati akitatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 10 ambapo aliwataka wananchi waache kuharibu msitu huo wa hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikabidhiwa kabrashana Mkuu wa wilaya ya Gairo,  Siriel Mchembe  lenye vielelezo vya mgogoro wa ardhi kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka huu mbele ya wananchi wa kijiji cha Kumbulu wilayani Gairo mkoani Morogoro.
 Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kabla Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao kuhusu mgogori kati ya Wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Kumbulu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu  kwa muda wa miaka 10  kati ya wanakijiji wa Kumbulu na  msitu wa Hifadhi ya Kumbulu unaosimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya  Gairo kwa kushirikiana na  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Mhe. Kanyasu amesema mgogoro huo wa ardhi  ulianza  mwaka 2009 baada ya kijiji hicho kupanga matumizi bora ya ardhi ambapo kutokana na baadhi ya  viongozi wa kijiji hicho kutokuridhia uamuzi huo na kuanza kuwachochea wananchi kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya msitu huo.

Kufuatia hali hiyo, Kanyasu ameagiza  kamati iliyosheheni wataalam mbalimbali ambayo ilikwisha undwa na wilaya ya Gairo igawe upya maeneo hayo kwa kuzingatia idadi ya watu katika kijiji hicho  kwa kuongeza eneo la kilimo kutoka ekari 1,000 hadi ekari  2,314 kwa kulimega eneo la msitu wa hifadhi wenye ukubwa wa ekari 5,500 hadi 5000 ili eneo hilo  litumike kwa ajili ya kilimo.

Aidha, Kanyasu ameagiza eneo la malisho lipunguzwe kutoka ekari 1,641 hadi ekari 1,000 ili ekari 641 iweze kutumika kwa ajili ya  kilimo.

Ameyatoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi wa  kijiji cha Kumbulu  wilayani  Gairo katika mkoa wa  Morogoro.

Kutokana na  malalamiko hayo ya wananchi, Kanyasu aliwaeleza wananchi hao kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi  uliofanyika  mwaka 2008 ulibainika kuwa na  kasoro kwa vile  baadhi ya  wananchi walichukua ardhi kubwa na kuna wengine  walichukua na kuiuza na kuna wengine walihamia kijijini hapo kwa ajili ya kutafuta ardhi.

Akizungumzia kuhusu ugawaji  huo wa ardhi kwa kila kaya,  Mhe. Kanyasu amesema  kijiji hicho  kina  kaya 642 hivyo kila kaya itagawiwa   ekari mbili na hivyo kufanya  jumla ya ekari 1,284 kati ya ekari 2,314.

Awali,   mpango huo wa matumizi bora ya ardhi  ulitenga eneo la misitu wa hifadhi ekari 5,500,  eneo la kilimo ekari 1,000 pamoja na eneo la malisho la ukubwa wa  ekari 1, 600  lakini bado viongozi wa kijiji hicho licha ya kushirikishwa katika mpango  huo  waliendelea kuwahamasisha wananchi kuvamia misitu huo kwa madai kuwa hawayatambui maamuzi hayo.

Aidha, Mhe. Kanyasu amesema kwa vile Msitu huo wa Hifadhi unapakana na vijiji vitatu ni vyema na vijiji viwili mbali na kijiji cha Kumbulu kama navyo vina  uhitaji ya ardhi viwasilishe maombi yao ili kupunguza migogoro.

Katika hatua nyingine, Mhe, Kanyasu amezionya kaya hizo zitakazopata ardhi ziendeleze ardhi hiyo la sivyo zitanyang’anywa.

Pia, Kanyasu amevionya vikundi vya watu wenye maslahi binafasi  ndani ya kijiji hicho viache  tabia ya kuchochea migogoro ya ardhi la sivyo Serikali haitasita kuvichukulia hatua  kali za kisheria.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe Amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo wakati itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake ili kila kaya iweze kupata ardhi kwa ajili ya kilimo

‘’Lazima mpate ardhi ya kilimo lakini ni muhimu pia kutunza miti iliyopo kwa vile bila miti hakuna kilimo kwa sababu miti inasidia kuleta mvua. Alisisitiza Mchembe

Naye, Mbunge wa Gairo, Ahmed  Shabiby amewataka wananchi hao wakati wakisubili kugawiwa maeneo kwa ajili ya kilimo wajiepushe na ukataji miti ovyo katika msitu wa Hifadhi ya Kumbulu.

‘’ Kwa wale wanaotaka kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa kwa ajili ya kuupeleka sokoni ni lazima mfuate sheria, hata ukitaka kuukata miti uliopo nyumbani kwako lazima uombe kibali kwa mamlaka inayohusika.’’ Alisisitiza  Shabiby

UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA MTENDAJI MKUU-MAHAKAMA

$
0
0

 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akisalimiana na Bw. Denis Biseko, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Tanzania pindi yeye pamoja na wenzake waliowasili ofisini kwa Mtendaji. Katikati ni Bi. Deborah Isser Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Washington-Marekani.

 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
  Picha ya pamoja baada ya mazungumzo; Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Mahakama, wa tano kulia ni Bi. Deborah Isser, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, wa nne kushoto ni Bw. Waleed Malik kutoka Benki ya Dunia, wa nne kulia ni Bw. Denis Biseko-Benki ya Dunia-Tanzania, wa tatu kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Sollanus Nyimbi, wa tatu kulia ni Mhe. Zahra Maruma, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania (JDU) pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo.
 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
 Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Benki ya Dunia pamoja na baadhi ya Wasajili na Watendaji wa Mahakama mbele ya jengo la Mahakama Kuu Musoma-Mara. Jengo hili pia lilikaguliwa na Ujumbe huo.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu lililokaguliwa na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia.
Na Mary Gwera, Mahakama
Wataalamu kutoka Benki ya Dunia ‘World Bank’ wapo nchini kwa  lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki  hiyo.

Lengo la Ujumbe huo kutembelea Mahakama ni kusaidia kukwamua vikwazo mbalimbali ili kuongeza kasi na ufanisi wa utekelezaji wa Mradi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha; Wataalam hao ambao watakuwepo nchini kwa muda wa siku saba (7), waliwasili nchini  Agosti 23, 2019 na tayari wametembelea baadhi ya Miradi ya ujenzi ya Majengo ya Mahakama Kuu Musoma-Mara, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu pamoja na kukagua maendeleo ya ufanyaji kazi ya Mahakama inayotembea ‘Mobile Court’ mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kitengo cha Maboresho cha Mahakama (JDU), Ujumbe huo pia tayari umekutana na baadhi ya Ofisi/Kurugenzi mfano Kurugenzi ya Ugavi na Ununuzi na vilevile Wajumbe hao watapatiwa taarifa za hatua  za utekelezaji wa malengo mbalimbali yaliyowekwa kwa kila Idara/Kitengo.

Hali kadhalika, Agosti 27, 2019, Ujumbe huo ulipata wasaa wa kukutana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kufanya mazungumzo kuhusiana na utekelezaji wa Mradi huo.

Baada ya kukamilika kwa ratiba ya ugeni huo, watatoa maoni/mapendekezo ya maeneo ya kuyafanyia kazi zaidi ili kuboresha utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020).

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

$
0
0
WANANCHI kote nchini hasa wanawake wameshauriwa na kutakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ili kuweza kujiongezea kipato  binafsi na kuondokana na umaskini.

Akizungumza katika kongamano maalum la wanawake la malkia wa nguvu lililofanyika leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa taasisi isiyo ya serikali ya Nafanikiwa Inspiration Reuben Ndimbo  amesema kuwa  kuna kila aina ya fursa nchini ambayo ikitumiwa vyema itaeleta matunda, hivyo watanzania wanatakiwa kuzichangamkia ili ziweze kuwanufaisha wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kufungua ya uwekezaji katika sekta ya  viwanda  ni vyema sasa kila mwenye nafasi kuwekeza katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.

Kwa upande wake muandaaji na mwenyekiti wa umoja wa  Malkia wa nguvu, Grace Mpanduka amesema kuwa wanawake  ni walengwa wakubwa katika kongamano hilo kutokana na uchakalikaji wao wa na wanaaminika katika kuchangamkia na kuzitendea kazi fursa zinazopatikana hapa nchini.

Amesema  kuwa nafasi ya uenyekiti wa SADC kwa Rais Dkt John Joseph Magufuli  ni fursa kubwa sana kwa watanzania  na hatuna budi kuongeza ubunifu katika nyanja mbalimbali ikiwemo nyanja za utalii, na ubunifu katika mambo mengine mengi. 

"Mimi nimejitolea kuwafungua na kuwaelimisha watanzania  wenzangu hasa akina mama ili wafahamu nchi za wenzetu wanavyochangamkia fursa  kama hizi pindi zinapotokea katika nchi zao, mwaka huu mmoja wa uenyekiti wa Rais Magufuli katika nchi za SADC ulete mabadiliko nchini" Amesema.

Aidha amempongeza Rais Magufuli kwa uchapakazi na ufunguaji  milango ya fursa kwa wanawake kwa kuwataka kuchapa kazi kwa kuanzisha viwanda na biashara zingine zitakazo itangaza nchi yetu katika mataifa ya nje.

Pia amewaomba wanawake kutumia nafasi ya SADC  kufungua milango kwa kwenda nje ya nchi kujifunza jinsi wenzetu wanavyochangamkia fursa kama za namna hiyo pamoja na ubunifu wanaotumia katika kufanya biashara.

Mgeni rasmi wa kongamano la Malkia wa nguvu na muigizaji wa filamu nchini Hidaya Njaidi 
akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake katika njanja mbalimbali wakati wa kongamano hilo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti na mwandaaji wa umoja wa Malkia wa Nguvu,Grace Mpanduka (kulia) akizungumza na baadhi wa waandishi wa habari mara baada ya kufungua kongamano maalum la wanawake la malkia wa nguvu , ambapo amewashauri wanawake kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ili kujikwamua kiuchumi, leo jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa taasisi ya Nafanikiwa Inspiration,Reuben Ndimbo(katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la maalum la wanawake la malkia wa nguvu ambapo amewashauri wananchi kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi, leo jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi na muigizaji wa filamu nchini Hidaya Njaidi akiwasili katika ukumbi wa TGNP uliopo Mabibo jijini Dar es Salaam ili kuendelea na shughuli ya kongamano la Malkia wa nguvu


WAKAZI WA MLANDIZI-MBOGA KUONDOKANA NA SHIDA YA MAJI FEBRUARI 2020-MWAMUNYANGE

$
0
0
 Mkurgenzi wa Uzalishaji na Usambazaji DAWASA Aron Joseph akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange  baada ya kutembelea mtambo wa Ruvu juu unaozalisha maji Lita Milioni 196 kwa siku wakati wa ziara ya bodi ya DAWASA  kuangalia na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo
Mkurgenzi wa Uzalishaji na Usambazaji DAWASA Aron Joseph akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange  baada ya kutembelea mtambo wa Ruvu juu unaozalisha maji Lita Milioni 196 kwa siku wakati wa ziara ya bodi ya DAWASA  kuangalia na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo
Mkurgenzi wa Uzalishaji na Usambazaji DAWASA Aron Joseph  akimuoneshaMwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange  pampu zitakazotumika kusukuma maji kuelekea kwenye mradi wa maji wa  Mlandizi -Chalinze Mboga wenye urefu wa Km 59 wakati wa ziara ya bodi ya DAWASA kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumzia mradi wa maji wa Mlandizi -Chalinze Mboga wenye urefu wa Km 59 na utakapokamilika utahudumia wananchi 120,000 na maji yatakayosafirrishwa ni lita milioni 9 kwa siku.
Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange baada ya kutembelea mradi wa Mlandizi-Chalinze Mboga.
 
Mafundi na Wakandarasi wakiendelea na zoezi la kuondoa mawe makubwa kwa ajili ya ulazaji wa mabomba ya maji kutoka kwenye mtambo ws Ruvu Juu kuelekea Mlandizi Chalinze Mboga.
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
KUKAMILIKA kwa Mradi wa Maji Mlandizi -Chalinze Mboga kutaondoa kero ya maji kwa wananchi wa Chalinze, Mlandizi na maeneo mengine ya Karibu.

Mradi huo wenye thamani ya Bilion 16, unatarajia kumalizika ifikapo Februari 2020 na utahudumia wakazi 120,000.

Akiwa katika ziara ya kutembelea mradi huo , Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuondoa kero ya muda mrefu ya maji .

Amesema, mradi huo umeanza kutekelezwa Mwezi Juni mwaka huu na unakadiriwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2020 na ukikamilika utakuwa na uwezo wa kusafirisha maji Lota Milion 9 kwa siku.

“Kuna changamoto imeweza kujitokeza, tulikua tunajadiliana na wakandarasi tumeona miamba ikiwa ni mikubwa kwenye njia ya ulazaji mabomba na wameweza kuiondoa na kuendelea na zoezi la uchimbaji na kulaza mabomba,”amesema Mwamunyange

Naye Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi mradi wa Mlandizi-Chalinze Mboga ni mpango wa kuondoa tatizo la maji kwenye mji mdogo wa Mboga na maeneo ya Viwanda.

“Mradi huu unachukua maji kutoka Mtambo wa Ruvu juu na tutajenga kituo kidogo cha kusukuma maji kwenye eneo la Chamakweza na Msoga na utawanufaisha wakazi wa Vigwaza, Chalinze na maeneo yote yanayopita mradi huo na tutaweka vituo kwa ajili ya kutoa huduma ya maji,”amesema Mtindasi.

DAWASA wameweka mikakati ya kufikia asilimia 95 ya wananchi kupata maji safi na salama kufikia 2020 kwa mijini na asilimia 85kwa vijijini ambapo kwa sasa miradi mbalimbali inaendelea kujengwa na mingine kuboreshwa.

NANDY AWEKA BAYANA UHUSIANO WAKE NA DOGO JANJA, NITASAIDIA THT

$
0
0
Na Khadija seif, Michuzi tv
MSANII wakike wa Bongofleva anaefanya vizuri kimataifa Nandy (African princess) amesema hatosita kusaidia na kuwafikisha mbali wasanii chipukizi wa kundi la THT.

Nandy ameeleza kuwa moja ya ndoto za wasanii wengi wa Muziki nikuona wanashikwa mkono na kufika mbali kwani hata yeye anatambua mchango wa watu mbalimbali waliomuwezesha kufika alipo akiwataja Kama Msanii Dullysykse pamoja na Marehem Ruge Mutahaba.

"Wapo wasanii wengi ambao wanafanya vizuri kama Barnaba, linah, jaymelody, Benson, Amin pamoja na wengine wengi hao wato ni zao la tht waliweza kushikwa mkono hivyo nitajitahidi na Mimi niweze kuwashika mkono waliobakia,"

Aidha, Nandy amesema bado anaamini wakipewa fursa watafanya vizuri hivyo wakae tayari na waendelee kuvipigani vipaji vyao wasikate tamaa.

Hata hivyo amefafanua mafanikio aliyoyapata kwenye Tamasha lake la (Nandi festival ) kuwa limeweza kumjenga kiakili, kumkuza kisanii,limempa moyo sana na kumpa nafasi yakujua mashabiki wengi hasa mikoani.

"Imenipa nafasi kubwa sana ya kugundua kuwa wasanii wakike wanaweza kutoa burudani kisawasawa kutokana na kuwa na mashabiki wengi pamoja na hamasa katika kutoa burudani na ndio maana niliwakutanisha wasanii kama mwansiti, Rosa ree, Linah na Haitham pamoja na wengine,"

Hata hivyo ameweka wazi kuwa yeye na Msanii Dogo janja pamoja na Whozu ni rafiki zangu ambao  nashirikiana na kwenye vitu vingi hasa vya Muziki.

TIC YAJIDHATITI KUSHIKA MKONO WAWEKEZAJI ILI KUINUA SEKTA YA VIWANDA

$
0
0

Meneja wa kanda ya Mashariki wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Venance Mashiba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika katika kiwanda cha betri  Chakavu Rufiji Mkoani Pwani.
Meneja wa kanda ya Mashariki wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Venance Mashiba akingumza wakati wa uwekeji jiwe la msingi Rufiji Mkoani Pwani.

Mwamvua Mwinyi, Rufiji
MENEJA wa kanda ya Mashariki wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Venance Mashiba, ameeleza wanajikita katika uwekezaji wa viwanda ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kuinua sekta ya viwanda na uwekezaji.

Akizungumza baada ya shughuli za kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchakata betri chakavu ( China Africa Business Council) Rufiji ,mkoani Pwani, alisema wameelekeza jitihada hizo hususan viwanda vinavyotokana na malighafi za kilimo na inayopatikana kwa ndani kwa wingi ambapo hutoa ajira na kuongeza pato la Taifa.

"Leo tupo hapa kushuhudia hafla hii, ambapo ni sehemu ya juhudi za kituo cha uwekezaji katika kuhakikisha kiwanda hiki kinapata mahitaji yake hadi sasa kinafunguliwa "alieleza Mashiba.

Aidha Mashiba alibainisha, huduma za uwekezaji ni mtambuka ambapo zinatolewa na taasisi mbalimbali ambazo taratibu zake zikigongana inasababisha baadhi ya changamoto ya ucheleweshaji wa huduma kwa wawekezaji.

Alisema ,kutokana na hilo kituo hicho , kiliimarisha huduma zake kwa kuongeza taasisi za serikali ambazo zinatoa huduma mbalimbali, vibali na leseni ili mwekezaji apate huduma mahala pamoja na sio kuzunguka .

Akiweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho,mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alimuelekeza mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo kusimamia mpango wa matumizi bora ya ardhi .

Aliwataka wakulima waheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji na wafugaji waheshimu wakulima huku akiyasihi makundi hayo kuacha kuvamia maeneo ya uwekezaji.

Ndikilo aliipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyohudumia wawekezaji na kusema katika mkoa huo hadi sasa vipo viwanda vitatu vinavyojishughulisha na uchakataji wa betri chakavu jambo ambalo linahitaji kujivunia.

Awali mkurugenzi wa kiwanda hicho ,Rashid Xian Ding alisema wametoa ajira kwa watu 100,wanasaidia shughuli za kijamii,kusomesha watoto,kusaidia huduma za afya kwa watoto na kutoa maji kwenye jamii inayowazunguka.

KAMPUNI YA BILLNDILLA ENTERPRISES YAMKABIDHI MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MABATI 160 UJENZI WA MADARASA MBEZI NDUMBWI

$
0
0


MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akipokea mabati 160 kutoka kwa Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kama msaada wake katika ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akikabidhi mabati 160 kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule Judith Senkoro Kilimo baada ya kupokea mabati hayo kutoka kwa Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kama msaada wake katika ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akiwasili katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi juu kwa ajili ya kupokea vifaa vya ujenzi kutoka kwa wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.
Baadhi ya maofiza walioongozana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo katika shule hiyo.
Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTDakizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 kwenye shule ya Mbezi Ndumbwi jijini Dar es salaam.
MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi vilivyotolewa na wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya makabidhiano shuleni hapo.
Kwaya ya wanafunzi wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi wakiimba mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo.
Baadhi ya watendaji wa kata madiwani na walimu wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi wakiwa katika hafla hiyo.
MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akitoa maagizo kwa watendaji alipokagua ujenzi wa maradasa wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya ujenzi katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi Juu vilivyotolewa na wadau wa maendeleo Makampuni ya kampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD.
Afisa Elimu Wilaya ya Kinondoni Bw. Kiduma Mgeni akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo wakati alipokagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mbezi Ndumbwi kata ya Mbezi Juu wilaya ya Kiondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Judith Kilimo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi wakati alipkagua ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
MKuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Danial Chongolo akifuatana na Bw. Bill Ndilla Mkurugenzi wa Makampuni ya Billndilla Enterprises na MAK Consortiums LTD kabla ya kupokea msaada wa mabati 160 kutoka kwa mkurugenzi huyo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Msingi Mbezi Ndumbwi Kata ya Bezi Juu wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

Balozi Seif awataka wataalamu wa afya kusomea fani zenye upungufu wa watendaji

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya na Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwashawishi Wataalamu wake kujifunza fani tofauti ili kuziba mapengo alipofika kufanya ziara ya kukagua Vitengo tofauti vya Hospitali ya Mnazo Mmoja.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Msafari Marijani akimuelezeas Balozi Seif changamoto wanazopambana nazo Watendaji wake katika kutoa huduma kwa Wananchi.
Mkuu wa Kitengo cha Kuhudumia Wagonjwa mahututi {ICU} Dr. Salum Shaaban Salum akimpatia maelezo Balozi Seif huduma zinazotolewa katika Kitengo hicho kinachohitaji utulivu wa hali ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salum Ali akifafanua mpango wa Wizara ya Afya wa kutafuta suluhisho la kudumu la upatikanaji wa Gesi ya Oxgen kwa ajili ya Hospitali za Serikali. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuendelea kuwashawishi Wataalamu wake wa Afya kusomea fani nyengine zenye upungufu wa watendaji ili kuziba mapengo yanayojitokeza katika utoaji wa huduma za Afya.
Alisema lazima ifikie wakati Hospitali za Serikali ziwe na uwezo kamili wa kuwa na Wataalamu wa kutosha badala ya kuendelea kutumia mfumo wa muda mrefu uliozoeleka wa kutegemea Wataalamu wa Nje.
Akifanya ziara fupi ya kukagua uwajibikaji kwa Watendaji tofauti kwenye Vitengo mbali mbali vinavyotoa huduma za Afya kwa Wananchi ndani ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Balozi Seif Ali Iddi alisema hatua hiyo ya ushawishi inaweza pia kusaidia kuziba mapengo ya Wataalamu wanaostaafu kwenye Vitengo vya Fani hizo.
Balozi Seif alikitolea mfano Kitengo kinachohudumia Wananchi wanaopatwa na ajali  ambacho kinastahiki kuimarishwa zaidi kwa vifaa pamoja na Wataalamu wazalendo waliobobea kwa vile ajali za vyombo vya Moto hivi sasa zimeongezeka mara dufu bara barani kutokana na harakati za Kimaisha.
Alisema takwimu inaonyesha wazi kwamba Wagonjwa wengi wanaopelekwa Hospitali kwa ajili ya huduma za Afya ni wale wanaopatwa na ajali za bara barani ambao wengi kati yao hulazimika kupelekwa nje ya Zanzibar baada ya kesi zao zinazohusiana na mifupa kushindwa kuhudumiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba lazima Taasisi za Umma zijitegemee kwa kuwa na Wataalamu pamoja na Vifaa vya kutosha ili kuepuka tatizo la kuwapeleka wagonjwa nje Zanzibar sambamba na kuacha kusubiri Wataalamu wa misaada.
Alifahamisha kwamba upatikanaji wa huduma za uhakika katika Vituo na Hospitali za Umma ndio njia pekee itakayojenga imani na upendo kwa Watendaji wa Sekta hiyo kutoka kwa Wananchi walio wengi Nchini.
Mapema Mkurugenzi wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Msafari Marijani alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uwezo wa kutoa huduma kwa saa 24 kwenye Kitengo hicho bado haujakamilika kutokana na uhaba wa Wataalamu wa Fani hiyo inayohitaji kufanyiwa kazi ya kuwahamaisha Watendaji wake kuzidi kupata mafunzo zaidi ili kujaza pengo liliopo.
Dr. Marijan alisema Kitengo hicho hutoa huduma kuanzia asubuhi hadi majira ya Saa Tatu za Usiku kwa sasa. Lakini hata hivyo Watendaji wake hulazimika kuwajibika katika muda wa ziada pale inapotokea kesi ya dharura inayohitaji kufanyiwa kazi ili kunusuru maisha ya Mgonjwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salum Ali alisema Wizara ya Afya kupitia Uongozi wa Hospitali hiyo ina mpango  wa kuimarisha Miundombinu Mipya katika Hospitali hiyo  tegemezi kwa Wananchi walio wengi Kisiwani Unguja.
Dr. Ali alisema Majengo mengi ya Hospitali hiyo ni ya zamani yakiwa yameshapitwa na wakati ambayo  yanahitaji kufanyia matengenezo makubwa vikiwemo baadhi ya vifaa kwenye Vitengo tofauti.
Akizungumzia changamoto inayojitokeza ya Hewa ya {Oxgen} kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr. Ali alisema Timu ya Wizara ya Afya hivi sasa iko Jijini Dar es salaam kufanya mpango wa utafiti wa upatikanaji wa mfumo mwengine wa Liquid Oxgen badala ya ule uliozoeleka ambao hukumbwa na matatizo ya mara kwa mara.
Alisema mtambo wa kutengeneza hewa ya Oxgen uliopo Mnazi Mmoja uliopatikana kwa msaada wa ufadhili Kutoka Nchini Uturuki Mnamo Mwaka 2017 hivi sasa umeharibika na unafanyiwa matengenezo ili ubakie kuwa wa hakiba.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alifahamisha kwamba Wizara ya Afya imejipanga kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa hewa safi ya Oxgen linalozikumba takriban Hospitali zote Nchini katika kipindi cha Miaka 20 sasa.
Alisema Mpango huo umelenga kujengwa kwa Mtambo Mkubwa wa kuzalisha Oxgen katika kiwango cha Mitungi yenye ujazo wa Lita 10,000 utakaowezesha kusambazwa kwa Taasisi nyengine Nchini zitakazohitaji hewa hiyo katika matumizi yao ya kawaida.
Alieleza kwamba kiwango hicho kitakachozalishwa kwenye Mtambo Mpya huo utakaojengwa kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na hakiba ya hewa ya Oxgen kwa asilimia 25% ya ziada.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada ilizochukuwa za kusaidia upatikanaji wa Hewa ya Oxgen kwa Hospitali za Serikali ambapo kwa sasa mahitaji halizi ni Mitungi 43 kwa Siku.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

WIZARA YA AFYA YAJA NA MFUMO WA DHARURA NA UOKOZI

$
0
0
Na Englibert Kayombo, WAMJW - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara nchini TANROADS iko mbioni kuanzisha mfumo wa huduma za dharura na uokoaji katika barabara kuu nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) kati ya malengo 17 ya Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG’s) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kwenye ukumbi wa mikutano bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu amesema “mfumo huu una lengo la kusaidia kupambana na dharura au maafa pindi yanapotokea na kuweza kusaidia upatikanaji wa huduma kwa haraka na tutaanza na vituo 7 vya huduma za dharura katika barabara kuu toka Mkoa wa Dar Es Salaam mpaka Ruaha Mbuyuni Mkoa wa Iringa.

Amevitaja vituo vya huduma za dharura ambayo vitaanzishwa kuwa ni Kituo cha Afya Kimara (DSM), Hospitali ya Tumbi, Kituo cha Afya Chalinze (PWANI), Zahanati ya Fulwe (Mikese Morogoro), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Hospitali ya St. Kizito (Mikumi, Morogoro) pamoja na Zahanati ya Ruaha Mbuyuni Darajani (Iringa)

“Tumeweza kununua gari za kubebea wagonjwa (Ambulance) 12 ambazo tutazisamba katika vituo vya huduma za dharura” amesema Waziri Ummy na kuendelea “bado tuna lengo la kuongeza magari matatu ya uzimaji moto yenye uwezo wa kuinua na kukata vyuma ili kuwaokoa majeruhi na kuwapatia huduma eneo la tukio”

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa tayari watoa huduma 272 wamehitimu mafunzo ya huduma za dharura na uokoaji yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi ambao kati yao, 1212 ni “basic provider” huku 160 ni watoa huduma ngazi ya Vijiji.

Akitoa maoni yake juu ya mfumo huo, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa ameipongeza Wizara ya Afya kwa kuja na mfumo huo ambao utaokoa maisha ya watanzania wengi huku akitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuhakikisha kuwa mfumo huo unasambaa maeneo yote ya barabara kuu ili kusaidia upatikanaji wa huduma za uokozi kwa haraka zaidi.

Waziri Ummy amesema kuwa wameanza na eneo hilo kwanza kwakuwa limekuwa na athari za kutokea kwa ajali nyingi kulinganisha na maeneo mengine huku akisema kuwa huo ni mpango endelevu na wataendelea maeneo yote ya barabara kuu nchini huku akisema kuwa mfumo huo utazinduliwa mwishoni wa Mwaka 2019.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) la Malengo Endelevu ya Maendeleo SDG"s kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii wakipitia taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.

 Wataalam kutoka taasisi mbalimbali katika Sekta ya Afya wakisikiliza uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) la Malengo Endelevu ya Maendeleo SDG"s kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.
 Wataalam kutoka taasisi mbalimbali katika Sekta ya Afya wakisikiliza uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) la Malengo Endelevu ya Maendeleo SDG"s kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Umm Mwalimu akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekeleza wa  lengo namba tatu (AFYA BORA NA USTAWI) la Malengo Endelevu ya Maendeleo SDG"s kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii wakipitia taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika ukumbi wa mikutano Bungeni Jijini Dodoma.

WAZIRI MBARAWA AITAKA BODI YA TANGA UWASA KUEPUKA MGONGANO WA MASLAHI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

$
0
0
 Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akizundua bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ambapo pia aliwataka kufanya kazi kwa uwazi isipokuwa pale mahitaji ya kisheria yanapolazimisha vinginevyo

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa halfa hiyo
 Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya
 Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya
 Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly  kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa uzinduzi huo
 Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya wakurugenzi wa Tanga Uwasa  kulia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Salum Shamte kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Shekifu
 Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Tanga Uwasa.
 Sehemu ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo
 Watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makambe Mbarawa  kulia ni PRO wa Tanga Uwasa Dorrah Killio
 Watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri wa Maji Proffesa Makambe Mbarawa
 Sehemu ya waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo
 Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akigawa vifaa vya utendaji kwa wajumbe wapya wa Bodi hiyo Mhandisi Zena Saidi ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga.
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akigawa vitendea kazi kwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa  Tanga Uwasa mara baada ya kuzindua bodi mpya ya wakurugenzi kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella


WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amewataka wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kuepuka mgongano wa kimaslahi katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Proffesa Mbarawa aliyasema hayo wakati akizundua bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ambapo pia aliwataka kufanya kazi kwa uwazi isipokuwa pale mahitaji ya kisheria yanapolazimisha vinginevyo 

Alisema pia lazima wazingatie sheria na taratibu za nchi katika mambo yote yanayohusu uendeshaji wa mamlaka hiyo huku akisisitiza matumizi ya sheria ya huduma za maji safi wa mazingira na 5ya 2019 ambapo majukumu ya bodi ya wakurugenzi wa mamlaka.

“Lakini matumizi sheria hii ya maji yaambnatane na matumizi ya sheria nyengine katika uendeshaji wa taasisi za umma kufikia dhana nzima ya utawala bora mfano sheria ya manunuzi ya umma, sheria ya mazingira, sheria ya fedha “Alisema Waziri Mbarawa.

“Pia bodi mhakikishe hesabu za mamlaka zimeandaliwa kutunzwa kwa usahihi kulingana na mifumo wa kimataifa wa ripoti za fedha (International Public Sector Accountin Standards (IPSAS).

Awali akizungumza Mwenyekiti kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi waliomaliza muda wao Salum Shamte alisema kwamba mafanikio yaliyopatikana wakati wao ni pamoja na kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa maji safi na majitaka ,kuboresha mipango,bajeti na utendaji ikiwa ni pamoja na kupata hati safi za mahesabu kila mwaka.

Alisema pia wamesaidia kuiwezesha mamlaka kuongeza mashine mbili za vifaa vya kupunguza matumizi ya umeme kwenye mtambo mkubwa wa kusukuma maji eneo la Mabayani ambapo vifaa hivyo vimepunguza gharama kwa kati ya asilimia 10 hadi 15 kwa mwezi

“Lakini pia kusimamia kuhuisha mkataba kati ya Tanga Uwasa na Taasisi ya wananchi wa Muheza ya Uwamakizi wa kutunza vyanzo vya maji yam to Zigi wa Shilingi milioni 180 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Novemba 2016 hadi 2019”Alisema

Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba mtandao wa maji taka unapatikana kidogo sana na wapo asilimia 9.7 kwa eneo la mjini huku akieleza changamoto ya kupasuka kwa mabomba za maji taka zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Fransis Barabara alisema kwamba katika kipindi cha bodi iliyomaliza muda wake wameshuhudia upanuzi wa mtandao wa majisafi ukienda sambamba na ongezeko la wateja hali iliyoweza kuongezeka kwa mapato ya mamlaka kwa ujumla ukilinganisha na hapo awali.

Alisema pia kodi kwenye mishahara na posho mbalimbali imeendelea kuwa juu na kuathiri maisha ya watumishi kimapato licha ya kupigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta za ajira bado suala hili halijapatiwa ufumbuzi na hivyo kufanya washindwe kumudu makali ya maisha.

“Sheria ya utumishi wa umma na 8 ya mwaka 2002 inaelekeza mtumishi wa umma kulipwa posho isiyo na makato ya kodi lakini kwa Tanga Uwasa bado posho za watumishi zinaendelea kukatwa kodi “Alisema.

Wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wauzaji wa nondo nchini wanolewa na TBS

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodgar Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na umuhimu wa viwango kwa bidhaa za ndono wakati wa semina iliyoandalisha na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 
Picha na Chalila Chibuda.

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewapatia elimu wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wauzaji wa nondo nchini kuhusiana na taratibu na mifumo ya ukaguzi wa bidhaa hizo nje kabla ya kuingizwa nchini ili kuhakikisha zinakidhi viwango.

Semina hiyo ambayo ilifanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, Ubungo, jijini Dar es Salaam ilifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya.

Amesema kupitia semina hiyo ambayo ni sehemu ya taratibu za shirika hilo kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali, wadau hao wataelimishwa utaratibu za uthibitishaji ubora wa bidhaa za nondo, matakwa ya viwango na taratibu za kupata huduma za shirika hilo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Hivi karibuni maofisa ukaguzi na udhibiti walifanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye masoko na kubaini kuwepo kwa nondo zenye dosari mbali mbali hasa kwenye viwango  vya urefu na upana.

Dkt. Ngenya, amewaambia washiriki wa semina hiyo kuwa nondo ni bidhaa muhimu kwa Taifa hasa kipindi hiki ambacho taifa lipo kwenye mkakati wa ujenzi viwanda. "Hivyo tumeona ni muhimu kukaa na wadau wote wa nondo na kukumbushana umuhimu wa kuzalisha, kuagiza, kusambaza na kuuza nondo zenye viwango," alisema Dkt. Ngenya.

Amekiri kwamba kuna kasoro ndogo ndogo wamezibaini kwenye uzalishaji wa nondo na kwamba hiyo ni moja ya sababu ya kuja na semina hiyo.  

Ametoa mwito kwa Watanzania kutonunua nondo bila kujua urefu na upana wake ni kiasi gani. Alifafanua kwamba wanatambua kwamba sio rahisi kwa mnunuzi kujua viwango vya nondo kwa macho, ndiyo maana shirika hilo linaweka msisitiza kwa wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wauzaji ili kuhakikisha wazalisha nondo zenye viwango. 

Amesema kwa kuzingatia kifungu cha 36 cha Sheria ya Viwango Na.2 ya mwaka 2009, Serikali ilipitisha kanuni za udhibiti wa shehena kupitia notisi ya Serikali Na. 405 ya Desemba 2009.

Kwa mujibu wa Dkt. Ngenya kanuni hizo ziliipa TBS mamlaka ya kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia nchini kabla ya kusambazwa kwenye soko la ndani.

Amesema Februali 1, mwaka 20012 shirika hilo lilianzisha mfumo wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuletwa nchini kama mpango wa udhibiti ubora wa bidhaa katika nchi zinakotoka ambao unasaidia kutatua changamoto zilizokuwepo wakati wa bidhaa zilipokuwa zinakaguliwa baada ya kufika nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodgar Tenga, aliipongeza TBS kwa kuandaa semina hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba viwango ni jambo la muhimu sana.

"Ni muhimu kwa wazalishaji wote kuhakikisha viwango vinaheshimika,"alisema Tenda. Amesisitiza kwamba ubora wa nondo zinazozalishwa nchini na zinazotoka nje ni muhimu sana, hivyo alitoa mwito kwa wadau wote kuzingatia viwango.

WANANCHI WA MTAA WA CHONGOLEANI KULIPWA FIDIA WANAYOSTAHILI KWA MUJIBU WA SHERIA

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Chongoleani Kata ta Chongoleani Tarafa ya Chumbageni Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kata kwa kata kusikiliza kero zinazowakabili wananchi
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
 MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Diwani wa Kata ya Mabokweni Jijini Tanga Njama akizungumza wakati wa ziara hiyo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akimsikiliza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati wa ziara yake
 Sehemu ya wananchi wa Mtaa wa Chongoleani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
SERIKALI mkoani Tanga imewahakikishia wananchi wanaoishi eneo la Chongoleani Jijini Tanga kunapojengwa mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta kutoka hoima nchini Uganda mpaka eneo hilo kwamba itahakikisha wanapata fidia wanayostahili kwa mujibu wa sheria

Huku akiwatoa hofu wananchi hao kwamba wawekezaji wengine ambao watafika kwa ajili ya kuwekeza kwenye maeneo hayo itahakikisha hakutakuwa na vikwazo vya aina yoyote kwenye utoaji wa fidia.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara yake ya Kata kwa Kata iliyoanzia kwenye Kata ya Chongoleani ambapo pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hao.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka wananchi hao kuacha tabia ya kuuza ardhi yote walionayo kwa sasa kwani wakumbuke inaweza kuwasaidia kwa ajili ya vizazi vyao vijavyo.

Alisema kwamba hawategemei kuona wananchi wa eneo la Chongoleani wakizulumiwa haki yao kwa misingi ya fidia na baadhi ya watu wanaotaka kupindisha sheria,

“Niwaambie kwamba kila mtu atapata fidia kwa mujibu wa sheria lakini nisema tu tutakuwa na wageni wengi ambao watakuja kwenye shughuli za mradi lazima tujipange vizuri ili isifike mahala tukakosa eneo la kujenga makazi yetu”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo wa Mkuu huyo wa mkoa, mtathimini wa Jiji la Tanga Victor Urassa alimueleza mkuu huyo wa mkoa kwamba fidia iliyolipwa imelipwa kwa mujibu wa sheria na kwa usimamizi wa Halmashauri ya Jiji hilo.

Urrasa pia aliwafafanulia wananchi hao kwamba wawekezaji wanapokwenda kwa Mkurugenzi wa Jiji kwa ajili ya kupatiwa ardhi hawajafanya udalali bali wanakwenda huko ili halmashauri iweze kuwasaidia.

“Labda niwaambie kwamba kwenye miradi mikubwa yenye manufaa ya umma halmashauri ndio inahusika kuja kwa wananchi kueleza taratibu “Alisema

Katika hatua nyengine wananchi hao wamelalamikia baadhi yao walitaka malipo ya fidia yaongezeke kutokana ukubwa wa maeneo yao wanayoyatoa kwa ajili ya kupisha shughuli za mradi huo.

Akizungumza mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Chongoleani Zuberi Waziei alisema pia kwamba wawekezaji wanapokwenda maeneo hayo wasipitia sehemu nyengine badala yake wafika kwa wananchi wenyewe ili waweze kuongea nao

“Kwa kweli wawekezaji wakija kuchukua maeneo yetu malipo ya fidia yaongezeke haiwezekani malipo ya Arusha na Tanga yawe tofauti leo ekeri moja ni milioni 2 jambo hilo ni uonevu mkubwa wakae kikao chao waone namna ya kurekebisha suala hili “Alisema mkazi huyo.

Naye kwa upande wake mkazi mwengine Daudi Rafael alieleza kwamba fidia imekuwa ni ndogo hawakufaidika kitu walichopewa wamenua kiwanja wamejenga na hatimaye hata cha kukidhi familia hakuna kitu chochoe.

Alisema mashamba yao yamechukuliwa ni sawa hawakatai ni suala la kimaendeleo lakini mengine yanachukuliwa wanahitaji gharama ziweze kuongezeka wanachohitaji ni kuongezwe fidia. 

TUTAPEKENYUA NA KUFUKUNYUA WAHAMIAJI HARAMU KILA SEHEMU -RC MAKONDA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LEO Agosti 29 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua mpango mkakati wa kudhibiti na kutokomeza wahamihaji haramu katika Mkoa wa Dar es salaam  na  kuwaagiza watendaji wa mitaa na kata kurejesha daftari la Mkazi ili kila mkazi kuanzia ngazi ya mtaa afahamike anapoishi na kazi anayofanya jambo litakalosaidia kutambulisha wakazi na kuzuia matukio ya  uhalifu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makonda amesema kuwa mpango huo ni dawa tosha ya kupambana na wageni wanaoishi nchini kinyume na sheria wameamua kuwahusisha watendaji wa kata, mitaa na wananchi ambao watakuwa na jukumu la kutoa taarifa kwa watu wanaowatilia mashaka kwenye makazi yao.

Vilevile amesema kuwa wahamiaji haramu wamekuwa sehemu ya kutekeleza matukio ambayo yanahatarisha usalama wa raia ikiwemo wizi, ubakaji, uporaji, kutumia rasilimali za nchi, kutumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo afya, elimu na ajira vilevile kusababisha msogamano katika magereza pamoja na kuwa chanzo cha migogoro hasa ya ardhi.

"Tunaelekea kwenye uchaguzi, kuna watu watatumia nafasi hiyo kuweka dosari tusiruhusu! mamlaka zote kwa kushirikiana na wananchi tuwe kitu kimoja ili tuweze kufanikisha hilo" amesema Makonda.


Awali akitoa taarifa ya mkakati huo Kamishina wa Uhamihaji Mkoa wa Dar es salaam  Novaita Mrosso amesema kuwa Mkoa huo ni kitovu cha uchumi lakini kumekuwa na ongezeko la wahamiaji haramu kila mwaka huku idadi kubwa ya wahamiaji hao wakitoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC,) Burundi, DRC, Somalia na Ethiopia na wahamiaji hao wamekuwa wakipendelea kuishi Mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa ni jiji lenye fursa nyingi za kibiashara.

"Idadi ya wahamiaji imekuwa ikiongezeka, kwa mwaka 2016 tuliwakamata wahamiaji haramu 1010, mwaka 2017 walikamatwa 1154 na mwaka 2018 walikua 1332 licha ya idadi kuongezeka  mamlaka bado inaendelea kupambana na kudhibiti hali hii" ameeleza.

Pia amesema kuwa mkakati huo wa kuwatambua wageni utapita kila mahali kama walivyofanya mwaka uliopita ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kulikua na wageni wanaotambulika 16,000 .
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto) akipokea mpango mkakati wa kudhibiti na kutokomeza wahamiaji haramu kutoka kwa afisa uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Novaita Mrosso (kulia) ambapo wamedhamiria kupita kila kona ya jiji hilo  kuwatambua na kuwadhibiti wahamiaji haramu leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maafisa Uhamiaji mara baada ya kupokea mpango mkakati wa kudhibiti na kutokomeza wahamiaji haramu jijini Dar es Salaam.

MASAUNI AFUNGA SEMINA YA USALAMA WA MATAIRI NA MFUMO WA BREKI ILIYOTOLEWA KWA ASKARI WA USAMALA BARABARANI, VETA, SUMATRA, NIT NA TBS

$
0
0
Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi  ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa kufunga Semina ya Usalama wa Matairi na Mfumo wa Breki iliyotolewa kwa askari wa usalama barabarani na wadau wengine kutoka taasisi zinahusiana na usalama barabarani,lengo ikiwa kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na uchakavu wa vipuri kwenye vyombo vya moto, semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Washiriki wa Semina ya Usalama wa Matairi na Mfumo wa Breki iliyotolewa kwa askari wa usalama barabarani na wadau wengine kutoka taasisi zinahusiana na usalama barabarani, wakimsikiliza Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi  ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga semina hiyo iliyokuwa na  lengo la  kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na  uchakavu wa vipuri kwenye vyombo vya moto,semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Semina ya Usalama wa Matairi na Mfumo wa Breki iliyotolewa kwa askari wa usalama barabarani na wadau wengine kutoka taasisi zinahusiana na usalama barabarani, wakimsikiliza Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya Nchi  ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifunga semina hiyo iliyokuwa na  lengo la  kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na uchakavu wa  vipuri kwenye vyombo vya moto,semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi  ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Matairi ya Michelini,Marc Pasquet(kushoto), alipowasili kufunga Semina ya Usalama wa Matairi na Mfumo wa Breki iliyotolewa kwa askari wa usalama barabarani na wadau wengine kutoka taasisi zinahusiana na usalama barabarani,lengo ikiwa kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na uchakavu wa vipuri kwenye vyombo vya moto, semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi  ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (watano kulia),Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Matairi ya Superdoll, Seif A. Seif(wasita kulia) na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Matairi ya Michelini,Marc Pasquet(wasaba kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Usalama wa Matairi na Mfumo wa Breki iliyotolewa kwa askari wa usalama barabarani na wadau wengine kutoka taasisi zinahusiana na usalama barabarani,lengo ikiwa kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na uchakavu wa  vipuri kwenye vyombo vya moto, semina hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

SERIKALI KUWEKA VIFAA CHANGAMSHI KWA WATOTO KWENYE HOSPITALI NDANI YA JIJI LA DAR

$
0
0
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Dar as Salaam, Yudas Ndungile amesema kuwa, serikali inakusudia kuweka vifaa changamshi kwa watoto kwenye hospitali mbalimbali za Mkoa huo.

Vifaa hivyo ni pamoja na michoro ya picha mbalimbali ikiwamo picha wanyama, alfabeti na herufi ambazo zinabandikwa ukutani kwenye wodi za watoto ili viweze kuwasaidia katika malezi, makuzi na elimu ya awali ya watoto hata kama ni wagonjwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Dk Ndungile alisema kuwa kuwekwa kwa vifaa hivyo changamshi kwenye hospitali kunasaidia watoto kupata faraja pindi wanapougua na kupelekwa hospitali.

"Watoto hata kama wanaumwa, wanahitaji faraja na kushiriki kwenye michezo mbalimbali itakayowasaidia kukuza na kuimarisha ubongo wao katika malezi na makuzi yao, hivyo nasi uwepo wa vifaa changamshi kwenye hospitali ni muhimu kwa sababu zinawasaidia kujifunza hata kama ni wagonjwa," alisema Dk. Ndungile.

Aliongeza kuwa, mpaka sasa baadhi ya hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwamo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), hospitali ya Mloganzila na Mwananyamala kwenye wodi za watoto kuna vifaa changamshi ambavyo uwasaidia watoto kujifunza hata kama ni wagonjwa.

Alisema lakini pia vifaa hivyo uwasaidia kuwaondolea uoga watoto wakiwa hospitali na kujiona kuwa wapo salama na mazingira mazuri ya kucheza na kufurahi jambo ambalo linasaidia kuwapa faraja.

Aliongeza kuwa suala la kuwekwa kwa vifaa hivyo kwenye wodi hizo sio la Tanzania peke yake,bali ni mpango wa uboreshaji wa huduma za matibabu kwa watoto kwenye hospitali mbalimbali Duniani.

Alisema mikakati wake ni kuhakikisha kuwa, hospitali zote zilizopo Mkoa huo zinapata vifaa changamshi kwa watoto pamoja na kutoa huduma bora za matibabu kwa watoto chini ya miaka mitano.

Alisema lakini pia watahakikisha wanaendelea kutekeleza mpango wa serikali wa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma bora za matibabu ikiwamo ni pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba, uwepo wa madaktari, pamoja na kuweka mazingira bora ya utoaji wa huduma bora kwa watoto chini ya miaka mitano.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Denmark hapa nchini Mette Norgaard Dissing Spandet Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa nchini  Mette Norgaard Dissing Spandet mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Angola hapa nchini  Sandro Renato Agostinho De Oliveira mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Angola hapa nchini  Sandro Renato Agostinho De Oliveira mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Meja Jenerali Anselem Nhamo Sanyatwe Balozi mteule wa Zimbabwe hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Sanjiv Kohli Balozi wa India hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini Meja Jenerali Anselem Nhamo Sanyatwe mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AENDELEA NA MKUTANO WA TICAD 7

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (wapili kushoto) wakizungumza na Profesa Mark Rweyemamu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha SACIDS Foundation for One Health chenye makao yake mkoani Morogoro (wapili kulia) na Profesa Gerlad Masinzo ambaye ni Kiongozi wa Kituo hicho katika Mkutano wa Saba wa TICAD unaoendelea kwenye Hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RIDHIWANI NA MADIWANI CHALINZE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI NA CHALIWASA KWA KUTATUA KILIO CHA MAJI KATIKA BAADHI YA MAENEO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa jimbo hilo wamepongeza jitihada za serikali awamu ya tano inazofanya kutatua tatizo la maji lililodumu kwa miaka 16 Chalinze ambapo kwa sasa huduma hiyo imeanza kutolewa katika baadhi ya maeneo.

Aidha wameupongeza uongozi mpya wa CHALIWASA na kuushukuru kwa kusimamia kikamilifu mradi unaoendelea kwani awali walikuwa wakishihudia vijisababu ambavyo vilikuwa vinaondoa imani kwa jamii.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani ,Ridhiwani alisema ,mradi wa maji Wami-Chaliwasa sasa unakwenda vizuri na ameridhishwa na kasi ya utekelezaji unaoendelea.

"Itakuwa hatuna fadhila kama hatutomshukuru mheshimiwa Rais Dkt .John Magufuli kwa jitihada zake za kutuondolea ukosefu wa maji Chalinze,"Mimi nikiwa mwakilishi wa wananchi nachukua nafasi hii kumpongeza na serikali ya awamu ya tano kwa juhudi hizi"

"Wafadhili ambao ni kutoka India walikubali kutoa fedha nyingine ili kukamilisha mradi wa WAMI na mkandarasi karibu anaanza kazi hiyo huku mchakato wa manunuzi ukiwa umekamilika"alifafanua Ridhiwani.

Hata hivyo Ridhiwani alieleza , kutokana na shida ya maji ,serikali yetu ni sikivu chini ya DAWASA imetenga kiasi cha sh.bilioni 16 kwa ajili ya mradi mpya wa Ruvu-Kinonko-Ngerengere hadi-Mboga ambapo kwa eneo la Mboga litanufaika na mradi wa CHALIWASA na Ruvu.

Alifafanua ,katika mradi wa CHALIWASA awamu hii unakwenda kuviunganisha vioski vilivyojengwa ambavyo vilikuwa havijaunganishwa na vilivyokuwa havijajengwa katika vitongoji vinakwenda kujengwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA Mhandisi Honest Raymond Makoi alisema ,eneo la Chalinze lilikuwa na shida kubwa ya maji lakini wameanza mkakati wa kujua changamoto zilizopo ili kutatua kwa haraka.

Alisema ofisi yake ipo wazi kwa kubeba mahitaji na wameanza utarabu wa kusambaza maji majumbani.

Nao madiwani ,akiwemo viti maalum Rehema Mno aliwashukuru kutokana na juhudi zinazofanywa na mafundi kuwa kikazi zaidi,ila mabomba ya zamani yaangaliwe kwakuwa baadhi ya maeneo yanapasuka.


Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images