Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

WADAU WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI YA KEMIKALI BASHIRIFU

$
0
0
 Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias (kulia) akifungua Mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta Binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mkutano wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam. Mamlaka za udhibiti zilizoshiriki katika mkutano huo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Baraza la Famasia Tanzania, Bohari ya Dawa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba na kuhusisha wadau mia moja wanaojihusisha na shughuli kemikali.Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias (aliyekaa kulia) na Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai, Bertha Mamuya (aliyekaa kushoto) wakiwa pamoja na washiriki wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta Binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu uliofanyika leo, Dar es Salaam.Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano wakifuatilia mada wakati wa mkutano.Meneja wa Ukaguzi wa Kemikali, Fidelis Segumba (kulia) akiwasilisha mada kuhusu Sheria zinazohusiana na Udhibiti wa Kemikali Bashirifu.


 Baadhi ya washiriki wa mkutano wakiuliza maswali na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa wakati wa mkutano huo.
 Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai, Bertha Mamuya (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau walioshiriki katika mkutano huo.

WADAU wanaoagiza, kusafirisha na kutumia kemikali bashirifu nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya kemikali hizo ili kuepusha kuchepushwa na kutumika kinyume na matumizi yaliyolengwa ikiwemo kutengeneza dawa za kulevya.
Akiongea kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na wadau wa Sekta binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu, Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, David Elias, alisema Serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali ili kuongeza jitihada ikiwemo kutunga Sheria kwa lengo la kupambana na kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu ambazo zinaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
“Kama njia mojawapo ya kusimamia mwenendo wa biashara na matumizi ya kemikali bashirifu, Serikali kupitia Mamlaka za udhibiti imeunda Sheria na Kanuni mbalimbali za kusimamia na kudhibiti uingizaji, usambazaji, usafirishaji, utumiaji, utekelezaji na usafirishaji wa kemikali nje ya nchi. Hivyo, ni muhimu kwa wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na kemikalimmbalimbali ikiwa pamoja na kemikali bashirifu, kuelewa Sheria na kanuni ili kuzitekeleza.”
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias, alisema mkutano huo utatoa ufafanuzi juu ya uchepushaji wa kemikali bashirifu na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika udhibiti.
“Ni matumaini yetu kwamba wadau mliopo kwenye mkutano huu mtapata uelewa wa kemikali bashirifu ni nini na umuhimu wa kudhibiti, uelewa wa Sheria na kanuni za udhibiti na mbinu zinazotumika katika kuchepusha kemikali hizo, hivyo naomba muwe huru kujadiliana, kutoa mapendekezo ya namna bora ya kushirikiana kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta binafsi ili kufukia lengo la Serikali katika kudhibiti mianya yote inayoruhusu uchepushwaji wa kemikali bashirifu” alimaliza. 
Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya, akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali, alisema wanaamini ushirikishwaji wa wadau wa kemikali utaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali.
“Kama Serikali tunaamini ushirikiano na wadau wa kemikali katika kujisimamia na kushirikiana na Mamlaka husika kutaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu hivyo kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya. Ni matumaini yangu majadiliano katika mkutano huu yatachagiza nia njema ya uanzishwaji wa ushirikiano wa hiari kati ya wadau na Mamlaka za udhibiti ili kufanikisha lengo la Serikali katika upatikanaji wa dawa za kulevya.”
Mamlaka za udhibiti zilizoshiriki katika mkutano huo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Baraza la Famasia Tanzania, Bohari ya Dawa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba na kuhusisha wadau mia moja wanaojihusisha na shughuli kemikali na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam.


UTEKELEZAJI WA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI WAPOKELEWA VIZURI NA WANANCHI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema utekelezaji wa Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini umepokelewa na wananchi kwa mtazamo chanya na Serikali inaendelea kuratibu usimamizi wa katazo la Mifuko ya plastiki kikamilifu kwa kuweka usimamizi madhubuti wa matumizi ya mifuko mbadala.

Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki; mwitikio wa jamii kuhusu katazo la kutumia mifuko ya plastiki na mipango ya serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa mifuko mbadala ambayo ni imara na kwa bei mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Sima amewahihikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa agizo linaendelea kusimamiwa na Serikali kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo.

Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo wametoa pongezi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibu utekelezaji wa katazo hilo la mifuko ya plastiki hapa nchini.
Aidha wajumbe hao walipendekeza sheria iwabane zaidi wazalishaji wa mifuko iliyokatazwa pamoja na wafanyabiashara wanaowafungia bidhaa watumiaji wa mwisho.

Pamoja na kutoa pongezi pia walizungumzia ubora wa baadhi ya mifuko mbadala ya 'non woven' wakisema kuwa haiwezi kuhimili bidhaa zenye uzito mkubwa.
Kutokana na changamoto hiyo waliiomba Serikali kutoa maelekezo kwa wazalishaji wa mifuko hiyo kuzalisha yenye ubora unaotakiwa ambayo haichaniki kwa urahisi ili wananchi waweze kuitumia.

Mjumbe huyo pia aliiomba Serikali kushughulikia tatizo la kupaa kwa bei ya mifuko mbadalana kusema kuwa mwananchi analazimika kununua mifuko badala ya kununua bidhaa aliyokusudia.
Kwa upande mwingine wajumbe walitoa mwito kwa Serikali kuimarisha ulinzi katika mipaka ya nchi wakisema kuwa mifuko mingi ya plastiki imekuwa ikipita mipakani na kuingia nchini.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akifafanua jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Wengine pichani ni Naibu Katibu Mku Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Utekeleaji wa Katazo la Mifuko ya Plastiki, Balozi Joseph Sokoine na Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mwaifunga.
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. Mussa Ntimizi akiongoza Kikao cha Kamati hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia Kikao cha Kamati hiyo.

TRA MKOA WA KIKODI TEMEKE YATOA SEMINA ELEKEZI KWA WADAU MBALIMBALI

$
0
0
MAMLAKA ya mapato nchini [TRA] katika Mkoa wa kikodi wa Temeke jijini Dar es Salaam imewakutanisha wadau mbalimbali wa TRA  wa Mkoa huo na kuwapatia semina elekezi na kuwahabarisha kuhusu mabadiliko ya sheria ya fedha iliyopitishwa na Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha bajeti ya mwaka 2019/2020 kilichomalizika Juni, 30 mwaka huu. 
Semina hiyo iliwakutanisha wadau wa mamlaka hiyo, wahasibu, wanasheria, wakaguzi ( auditors), washauri wa kodi (tax consultants) na viongozi wa TCCIA Temeke.

 
Meneja wa kodi Mkoa wa Temeke, Paul Walalaze  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kufungua semina elekezi kwa wadau mbalimbali wa TRA, ambapo wadau hao walielezwa sheria ya fedha iliyopitishwa na bunge katika kikao cha bajeti ya 2019/2020 kilichofanyika 30, Juni mwaka huu. leo jijini Dar es Salaam.  
 Afisa Msimamizi Mkoa wa kikodi wa kodi Temeke, Paul Magembe akizungumza na wadau mbalimbali wa kodi katika semina elekezi kwa ajili ya kutambua sheria ya fedha iliyopitishwa na bunge kwa mwaka 2019/2020 leo,jijini Dar es Salaam.  
 Afisa Msimamizi Mkoa wa kikodi wa Temeke, Paul Magembe (kulia) akifafanua jambo.
Wadau wa mamlaka hiyo  wahasibu, wanasheria, wakaguzi ( auditors), washauri wa kodi(tax consultants) na viongozi wa TCCIA Temeke  wakimsikiliza  Afisa Msimamizi Mkoa wa kikodi wa Temeke, Paul Magembe.

UJUMBE WA BENKI YA DUNIA WAKUTANA NA MTENDAJI MKUU-MAHAKAMA

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama
Wataalamu kutoka Benki ya Dunia ‘World Bank’ wapo nchini kwa  lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki  hiyo.

Lengo la Ujumbe huo kutembelea Mahakama ni kusaidia kukwamua vikwazo mbalimbali ili kuongeza kasi na ufanisi wa utekelezaji wa Mradi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha; Wataalam hao ambao watakuwepo nchini kwa muda wa siku saba (7), waliwasili nchini  Agosti 23, 2019 na tayari wametembelea baadhi ya Miradi ya ujenzi ya Majengo ya Mahakama Kuu Musoma-Mara, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu pamoja na kukagua maendeleo ya ufanyaji kazi ya Mahakama inayotembea ‘Mobile Court’ mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kitengo cha Maboresho cha Mahakama (JDU), Ujumbe huo pia tayari umekutana na baadhi ya Ofisi/Kurugenzi mfano Kurugenzi ya Ugavi na Ununuzi na vilevile Wajumbe hao watapatiwa taarifa za hatua  za utekelezaji wa malengo mbalimbali yaliyowekwa kwa kila Idara/Kitengo.

Hali kadhalika, Agosti 27, 2019, Ujumbe huo ulipata wasaa wa kukutana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na kufanya mazungumzo kuhusiana na utekelezaji wa Mradi huo.

Baada ya kukamilika kwa ratiba ya ugeni huo, watatoa maoni/mapendekezo ya maeneo ya kuyafanyia kazi zaidi ili kuboresha utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020).
 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akisalimiana na Bw. Denis Biseko, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Tanzania pindi yeye pamoja na wenzake waliowasili ofisini kwa Mtendaji. Katikati ni Bi. Deborah Isser Mtaalam kutoka Benki ya Dunia-Washington-Marekani.

 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
  Picha ya pamoja baada ya mazungumzo; Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Mahakama, wa tano kulia ni Bi. Deborah Isser, Mtaalam kutoka Benki ya Dunia, wa nne kushoto ni Bw. Waleed Malik kutoka Benki ya Dunia, wa nne kulia ni Bw. Denis Biseko-Benki ya Dunia-Tanzania, wa tatu kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Sollanus Nyimbi, wa tatu kulia ni Mhe. Zahra Maruma, Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania (JDU) pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mahakama walioshiriki katika mazungumzo hayo.
 Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakiwa ndani ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’ iliyopo mkoani Mwanza, lengo ni kujionea hali ya ufanyaji kazi wa Mahakama hiyo.
 Picha ya pamoja kati ya Ujumbe wa Benki ya Dunia pamoja na baadhi ya Wasajili na Watendaji wa Mahakama mbele ya jengo la Mahakama Kuu Musoma-Mara. Jengo hili pia lilikaguliwa na Ujumbe huo.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu lililokaguliwa na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia.

WAKULIMA WA ZAO LA MUHOGO MKURANGA WAPATA KIWANDA CHA KUCHAKAZA MUHOGO

$
0
0
VICTOR MASANGU, MKURANGA
KILIO cha muda mrefu ambao kilkuwa kinawakabili wakulima wa zao la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani hatimaye hivi karibuni wanatarajia kuondokana na changamoto sugu ya upatikanaji wa soko la uhakika kufuatia kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata zao hilo ambacho kitagharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.5

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima hao wakati wa Ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa halfa ya uwekeaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini China katika kijiji cha Mkenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga ambapo wamedai hapo awali walikuwa na tatizo la kuuza mihogo yao kwa bei ya hasara.

“Sisi kama wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilayah ii ya mkuranga tumefarijika sana kwa ujio wa mradi w akiwanda hiki ambacho kimejengwa na marafiki zetu wa kutoka nchini chini, na tunashukuru kwa jitihada ambazo zinafanywa na Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wetu Dk. John Pombe Magfuli kwa kuwaleta wawekezaji hawa ambao watatusaidia kuondokana na tatizo la kupata soko la uhakika,”walisema wakulima hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka maafisa kilimo wote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwasimamia vema wakulima wa zao hilo la muhogo kutonyonywa na walanguzi na kupata haki zao stahiki na kuahidi kuwaondoa kazini wale wote ambao watabainika kukwamisha juhudi za serikali katika uwekezaji sekta ya viwanda.

Aidha Ndikilo alisema kuwa lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawasaidia kwa hali na mali wananchi wake katika kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili ikiwemo ukosefu wa masoko ya ukakiha, ajaira hivyo aatahakikisha zao hilo la muhogo linapata soko kupitia viwanda ambavyo vinajengwa na waekezaji katika maeneo mbali mbali na kuwahimiza wasikate tama na badala yake waendelee zaidi kulima mazao ya biashar ikiwemo ufuta,muhogo na korosho.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amesema kuwa kipindi cha nyuma wakulima wengine walikuwa tayari wameshakata tamaa katika kilimo cha zao la muhogo,hivyo kumamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kuleta mabadili chanya kwa kuwapa fursa wananchi kuwa na soko la uhakika .

“Kwa kweli wananchi wangu hasa kwa wakulima wa zao hili la muhogo katika Wilaya ya Mkuranga baadhi yao walikuwa tayari wameanza kukata tama kabisa na kujikitza zaidi na kilimo cha zo la muhogo nah ii hali ni kutokana na mfumo ambao ulikuwepo wanauza mazao yao kwa bei ya hasara kweli lakini kwa sasa kiwanda hiki kinakamilika mwaka huu hivyo wataondokana kabisa na changamoto ya soko,”alismema Sanga.

Awali akisoma Risala ya ujenzi wa mradi huo mmoja wa vongozi wa kiwanda Leonard Jambeli kwa niaba ya Mkurugenzi amebainisha kwamba waanategemea kutoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa wazawa zaidi ya mia moja pindi uzalishaji utakapoanza kufanyika rasmi.

KUKAMILIKA kwa mradi huo wa ujenzi wa kiwanda mwishoni mwa mwaka huu kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa zao hilo katika halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ambao kwa miaka mingi walikuwa wanapata hasara kutokana na kunyonywa na walanguzi kununua zao hilo kwa bei ndogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo kushoto akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo mara baada ya halfa ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho amabcho kimejengwa katika kijiji cha Mgenge kata ya Beta Wilayani Mkuranga,(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelekezo kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha kuchakata muhogo wakati alipofanya ziaara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa kaatika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho cha kuchakata muhogo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi.
 Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kushoto Ramadhani Maneno akimshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ikiwa ni moja ya ishara ya kumpongeza katika juhudi zake za kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa viwanda
  Mmoja wa viongozi wa kiwanda hicho cha kuchakata zao la muhogo kulia Leonard Jambeli akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho pembeni yake kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na baaadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na watumishi mbali mbali wa serikalini, pamoja na wananchi wa wa kijiji cha Mkenge hawapo pichani katika halfa fupi iliyoandaliwa kwa lengo la uwekezaji wa jiwe la msingi kataika kiwanda hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

WANAFUNZI 13 WAPATA MIMBA JIMBO LA CHALINZE KWA KIPINDI CHA MIEZI NANE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete  akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Na Mwamvua  Mwinyi, Chalinze
WANAFUNZI 13 katika jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani wamepata mimba kwa kipindi cha miezi nane kuanzia Januai hadi  Agosti mwaka huu, ambapo wanafunzi 12 kati ya hao ni kata ya Msata.

Kutokana na idadi hiyo, madiwani wa halmashauri ya Chalinze pamoja na mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete wamelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wanaume kutia wanafunzi mimba za utotoni hali inayosababisha kukatisha masomo yao.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani katika taarifa za kata kwa kata, Ridhiwani alisikitishwa na namba hiyo na kudai ni kubwa kwa kipindi kifupi.

Alisema ,shule ya sekondari Msata imekuwa ya mwisho ,wanafunzi wamezidi utoro na mimba zimeshafika tisa suala ambalo si jema na halifurahishi.

"Kesi ya jinai haifi, haiozi ,haipotei ,kutembea na binti wa miaka 18, hata ikifika mwaka 2060 ndipo ukagundulika ulimpa mimba mwanafunzi 2019 ,sheria bado ina meno utakamatwa "alifafanua Ridhiwani.

Ridhiwani alibainisha kuwa ,polisi isimamie kesi hizo kwa kutoa haki na sheria ichukue mkondo wake.
Nae OCS WAMI ,Joseph Ogutu alitaka ushirikiano dhidi ya kesi hizo.
Aliomba jamii kishirikiana na polisi ,kwakuwa kuna changamoto ya wazazi kwenda kudokeza wahusika na kusababisha kukimbia.

Ogutu alieleza ,kati ya kesi hizo 13 ,wamekamatwa watuhumiwa watatu pekee hadi sasa .

Awali akisoma taarifa ya kata kwenye baraza la madiwani, Diwani wa viti maalum Msata na mwenyekiti wa kamati ya elimu,afya na maji Chalinze,Rehema Mno alisema kati ya wanafunzi hao 13 ,wanafunzi tisa ni wa sekondari na wanne ni wa msingi.

Alisema ,suala hilo linaumiza kwani wakati serikali ikipiga vita vitendo hivyo kumbe bado kuna maeneo wanaendelea kukatisha ndoto za wanafunzi wa kike.

Rehema alieleza ,wazazi na walezi wanachangia kukua kwa suala la mimba za utotoni kwakuwa wanaficha wahusika waliowapa mimba watoto wao na wakati mwingine wanakaa nao kuyamaliza mezani.

"Watuhumiwa wanakimbia ,tumejipangia mkakati kwamba watoto wakipelekwa kupimwa madaktari wasitoe majibu kwanza hadi watakapowaruhusu ndipo waende moja kwa moja polisi kuwataja wahusika na kwa kufanya hivyo watakamatwa kirahisi ,"

"Wakirudi majumbani watatoa siri na hapo ndipo watuhumiwa wanapokimbia"alifafanua Rehema.

Mtendaji wa kata ya Msata, Balthazary Miti ,alisema katika kata hiyo mimba ni 12 ,kati ya hizo tisa ni shule ya sekondari.

NAIBU WAZIRI KANYASU AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU KWA MIAKA 10 MKOANI MOROGORO

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu  kwa muda wa miaka 10  kati ya wanakijiji wa Kumbulu na  msitu wa Hifadhi ya Kumbulu unaosimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya  Gairo kwa kushirikiana na  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Mhe. Kanyasu amesema mgogoro huo wa ardhi  ulianza  mwaka 2009 baada ya kijiji hicho kupanga matumizi bora ya ardhi ambapo kutokana na baadhi ya  viongozi wa kijiji hicho kutokuridhia uamuzi huo na kuanza kuwachochea wananchi kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya msitu huo.

Kufuatia hali hiyo, Kanyasu ameagiza  kamati iliyosheheni wataalam mbalimbali ambayo ilikwisha undwa na wilaya ya Gairo igawe upya maeneo hayo kwa kuzingatia idadi ya watu katika kijiji hicho  kwa kuongeza eneo la kilimo kutoka ekari 1,000 hadi ekari  2,314 kwa kulimega eneo la msitu wa hifadhi wenye ukubwa wa ekari 5,500 hadi 5000 ili eneo hilo  litumike kwa ajili ya kilimo.

Aidha, Kanyasu ameagiza eneo la malisho lipunguzwe kutoka ekari 1,641 hadi ekari 1,000 ili ekari 641 iweze kutumika kwa ajili ya  kilimo.

Ameyatoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi wa  kijiji cha Kumbulu  wilayani  Gairo katika mkoa wa  Morogoro.

Kutokana na  malalamiko hayo ya wananchi, Kanyasu aliwaeleza wananchi hao kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi  uliofanyika  mwaka 2008 ulibainika kuwa na  kasoro kwa vile  baadhi ya  wananchi walichukua ardhi kubwa na kuna wengine  walichukua na kuiuza na kuna wengine walihamia kijijini hapo kwa ajili ya kutafuta ardhi.

Akizungumzia kuhusu ugawaji  huo wa ardhi kwa kila kaya,  Mhe. Kanyasu amesema  kijiji hicho  kina  kaya 642 hivyo kila kaya itagawiwa   ekari mbili na hivyo kufanya  jumla ya ekari 1,284 kati ya ekari 2,314.

Awali,   mpango huo wa matumizi bora ya ardhi  ulitenga eneo la misitu wa hifadhi ekari 5,500,  eneo la kilimo ekari 1,000 pamoja na eneo la malisho la ukubwa wa  ekari 1, 600  lakini bado viongozi wa kijiji hicho licha ya kushirikishwa katika mpango  huo  waliendelea kuwahamasisha wananchi kuvamia misitu huo kwa madai kuwa hawayatambui maamuzi hayo.

Aidha, Mhe. Kanyasu amesema kwa vile Msitu huo wa Hifadhi unapakana na vijiji vitatu ni vyema na vijiji viwili mbali na kijiji cha Kumbulu kama navyo vina  uhitaji ya ardhi viwasilishe maombi yao ili kupunguza migogoro.

Katika hatua nyingine, Mhe, Kanyasu amezionya kaya hizo zitakazopata ardhi ziendeleze ardhi hiyo la sivyo zitanyang’anywa.

Pia, Kanyasu amevionya vikundi vya watu wenye maslahi binafasi  ndani ya kijiji hicho viache  tabia ya kuchochea migogoro ya ardhi la sivyo Serikali haitasita kuvichukulia hatua  kali za kisheria.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe Amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo wakati itakapokuwa ikitekeleza majukumu yake ili kila kaya iweze kupata ardhi kwa ajili ya kilimo

‘’Lazima mpate ardhi ya kilimo lakini ni muhimu pia kutunza miti iliyopo kwa vile bila miti hakuna kilimo kwa sababu miti inasidia kuleta mvua. Alisisitiza Mchembe

Naye, Mbunge wa Gairo, Ahmed  Shabiby amewataka wananchi hao wakati wakisubili kugawiwa maeneo kwa ajili ya kilimo wajiepushe na ukataji miti ovyo katika msitu wa Hifadhi ya Kumbulu.

‘’ Kwa wale wanaotaka kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa kwa ajili ya kuupeleka sokoni ni lazima mfuate sheria, hata ukitaka kuukata miti uliopo nyumbani kwako lazima uombe kibali kwa mamlaka inayohusika.’’ Alisisitiza  Shabiby
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Gairo akiangalia huku akizungumza kwenye miti iliyopangwa kwa ajili ya  kuchoma mkaa mara baada ya kufanya ziara  katika Hifadhi ya Msitu wa Kumbulu kujionea miti iliyokatwa  kinyume na sheria katika Hifadhi hiyo  wilayani  Gairo mkoani Morogoro.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizumgumza na wananchi wa kijiji cha Kumbulu wakati akitatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 10 ambapo aliwataka wananchi waache kuharibu msitu huo wa hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikabidhiwa kabrashana Mkuu wa wilaya ya Gairo,  Siriel Mchembe  lenye vielelezo vya mgogoro wa ardhi kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka huu mbele ya wananchi wa kijiji cha Kumbulu wilayani Gairo mkoani Morogoro.
 Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akizungumza na wananchi wa kijiji cha kabla Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi hao kuhusu mgogori kati ya Wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Kumbulu.

DK. MWAKYEMBE AWAPONGEZA AY, MWANA FA KWA KUPIGANIA HAKI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu


WAZIRI wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrson Mwakyembe amewapongeza wasanii wa Bongo Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA na Ambwene Yeseya a.k.a AY kwa walivyosimama imara kupigania haki zao bila kuchoka.

Dk.Mwakyembe ameyasema hayo leo Agosti 28,2019 alipokutana na wasanii kwa lengo la kujadili haki za wasanii ikiwemo ya kupata gawio kutokana na kazi zao za sanaa, ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa wasanii hao.

"Nitumie nafasi hii kuwapongeza AY na Mwana FA kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha wanapata haki yao kwenye mgao unaotokana na milio ya nyimbo zao kwenye miito ya simu,"amesema.

Amesema "Mmeifanya kazi ninyi wenyewe, wengine tulijitokeza pale tu tulipohitajika. Mmepigania haki yenu hadi mkafanikiwa.Hongereni sana,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakiibiwa kazi zao na ikafika wakati wizi wa kazi za wasanii baadhi ya watu wameuhalalisha bila woga.

"Wezi wa kazi za wasanii wananuifa na wasanii wenyewe pamoja na wabunifu wakiishi maisha ya magumu na kutonufaika na kazi wanayoifanya,"amesema Waziri Mwakyembe.

Amefafanua haiwezekani wanaohangaika kubuni katika kazi za sanaa ikiwemo ya muziki wanabaki wakihaha tu na wanaonufaika ni wengine kabisa.

Hivyo amesema ili kuondoa dhulma kwa wasanii, Serikali pamoja na mikakati mingine inaendelea na kuangalia na kupitia upya sera ya utamaduni ili kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi wanayoifanya.

Amesema katika eneo hilo la sera ya utamaduni iliyopo ni ya muda mrefu na hivyo katika mchakato wa kuipitia upya wameomba ushauri kwa wabobezi wa utamaduni waliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili watoe ushauri wao katika eneo la sera.

Ameeleza katika kupigania haki za wasanii na maslahi yao kumekuwepo na mkwamo wa muda mrefu na matokeo yake hata mafanikio hayapatikani.

"Tunafahamu katika mazingira ya sasa ya kukua kwa teknolojia ya Tehama kunahitajika mageuzi makubwa ya mfumo mzima na sio kugusa eneo moja,"amesema Waziri Mwakyembe.

Wenyeviti wa Vijiji watakiwa kuhamasisha wananchi kutumia CHF iliyoboreshwa

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dk Dorothy Gwajima amewataka viongozi wa serikali za vijiji nchini kusaidia kuhamasisha wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ili waondokane na adha wanapokuwa hawana fedha mkononi.

Dk. Gwajima ameyasema hayo jana wakati alipotembelea Zahanati ya kikiji cha Chiboli wilayani Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia namna ambavyo Zahanati hiyo imeweza kuandikisha idadi kubwa ya kaya katika mfumo huo.

Amesema suala la kuhamasisha wanachi kujiunga na bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa siyo jukuu la wataalam wa afya kwani wanaotakiwa kulisimamia ni viongozi wa vijiji ambao ndiyo wenye watu.

"Hili suala la watu kujiunga na bima hii ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa ni suala la kushirikishana hawa viongozi wa vijiji kama mwenyekiti wa kijiji na afisa mtendaji wa kijiji ndiyo wenye watu na wenye mikutano ya hadhara ambayo ajenda hii wataifikisha kwa njia rahisi" amesema Dk Gwajima.

Dk Gwajima amesema kama viongozi wa serikali za vijiji watakuwa na ushirikano na wataalamu wa vituo vya afya nchini wataweza kuibeba ajenga hiyo kwa kuifikisha kwa wanachi na kuweza kuziandikisha kaya zote nchini katika mfumo huo wa CHF iliyoboreshwa.

"Hapa Chiboli wameweza na ni kijijini sana ni zaidi ya kilomita 90 kutoka mjini lakini wameweza kuandikisha zaidi ya kaya 315 toka walipoanza mwaka jana mwezi Novemba ambapo ndipo mkoa ulianza kuandikisha"alisema.

Naye Muuguzi wa Zahanati hiyo Shija Makeja,alisema kuwa kupata mafanikio ya kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kumetoka na kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali ya kijiji.

"Mwaka jana tulipata mafunzo juu ya mfumo huu tuliporudi tulishirikisha viongozi wa serikali ya kijiji pamoja na kamati ya uendeshaji wa zahanati na kulipeleka suala hili kwa wanachi kupitia mikutano ya hadhara ndipo watu walipo hamasika na kujiunga kwa idadi kubwa"amesema.

Kwa upande wake meneja mradi wa HPSS Tuimarishe afya Ally Kebby, amesema kuwa azma ya serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ambao mwanachi atatambuliwa na pesa anayochangia itarudi kwenye kituo.

Mradi wa HPSS Tuimarishe afya unafadhiriwa na shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi kwa kushirikana na serikali ya Tanzania ambao umechangia katika kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji waratibu na wasimazi wa CHF iliyoboreshwa nchini.
 Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dk Dorothy Gwajima akizungumza wakati alipotembelea Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, Dodoma.
Meneja Mradi wa HPSS, Ally Kebby akizungumzia umuhimu wa kutumia bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dk Dorothy Gwajima katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino.

Matokeo ya kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili yatangazwa

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ametangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili.

Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi hao waliopangwa kidato cha tano limefanyika kwa kuzingatia jumla ya wanafunzi wavulana 1,861 waliokua wamebaki kwenye uchaguzi wa awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi 1,861 waliochaguliwa ni wanafunzi 1,674 na wanafunzi 187 wamekosa tahasusi hivyo hawajachaguliwa. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 178 wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na 1,496 wamepangiwa Sanaa na Biashara.

" Niwashauri waliokosa nafasi waombe kozi mbalimbali katika vyuo vya elimu ya ufundi vinavyotambulika na NACTE, lakini pia waliochaguliwa wanapaswa kuripoti Septemba 2 hadi 16 mwaka huu watakaochelewa watakua wamepoteza nafasi, " amesema Waziri Jafo.

MAHAKAMA YATAKA NYARAKA MUHIMU KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOWAKABILI VIGOGO KAMPUNI YA MAWASILIANO, YATOA SIKU 14

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku 14 kwa upande wa Mashtaka kuwasilisha nyaraka muhimu  katika Mahakama Kuu Kitengo cha uhujumu uchumi dhidi ya kesi ya Uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, akiwemo wakili maarufu Dk. Ringo Tenga,

Hatu hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mahakamani hapo leo Agosti 28,mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa, kesi hiyo ililikuja kwa ajili ya kutajwa,  upelelezi umekamilika hivyo wanaomba wiki mbili ili kuweza kuwasilisha nyaraka hizo Mahakama ya mafisadi. 

Hata hivyo upande wa utetezi katika kesi hiyo haukuwa na pingamizi lolote kuhusu maombi hayo ya upande wa mashtaka.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba  10, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhandisi Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Dk. Tenga na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa  chini ya kiwango cha Dola za Marekani  0.25 kwa  dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Pia wanadaiwa  katika kipindi hicho  walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola za Marekani 466,010.07 kwa TCRA.


Pia washitakiwa hao  wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22 (sawa na Sh.bilioni 8).

POLISI PWANI YAKAMATA MAGUNIA TISA YA BANGI-WANKYO

$
0
0
MWAMVUA MWINYI, PWANI

JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia dereva Francis Deogratias (30) mkazi wa Mwananyamala Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kusafirisha bhangi magunia tisa kila moja likiwa na uzito wa kilo 50.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alisema kuwa bhangi hiyo ilikutwa kwenye gari alilokuwa akiendesha mtuhumiwa.

Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 27 majira ya saa 3:30 usiku eneo la Maili Moja askari wakiwa doria walikamata gari hilo aina ya Toyota Prado yenye namba za usajili T855CYP rangi ya Silver likitokea mkoani Morogoro.

"Mtuhumiwa alikuwa na wenzake watatu ambao walikimbia na msako mkali unaendelea kuwatafuta ili waje wajibu tuhuma zitakazowakabili za kusafirisha bhangi," alisema Nyigesa.

Alisema kuwa watu wanaojishughulisha na uhalifu kwa sasa hawana nafasi na waangalie shughuli halali kwani hawatavumiliwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na wananchi watoe taarifa za uhalifu.


BEI YA MBOLEA YASHUKA, WAZIRI HASUNGA ATANGAZA BEI ELEKEZI

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Kutokana na ushindani wa zabuni za BPS iliyofunguliwa Juni 21, 2019, bei za mbolea ya DAP katika chanzo ilipungua kwa asilimia 12 ikililinganishwa na bei za zabuni ya Julai, 2018. Sambamba na punguzo lililotokana na zabuni hiyo, Serikali ilifanya marejeo ya kikokotoo cha bei elekezi ambacho kimetumika kwa misimu ya kilimo 2017/2018 na 2018/2019. 

Waziri Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 28 Agosti 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ndogo za wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa Ushindani wa zabuni za BPS pamoja na marejeo ya kikokotoo umefanya bei ya mbolea kwa mkulima kupungua kwa wastani kimkoa wa Tshs 8,000/= hadi Tshs 10,000/ sawa na asilimia 13 - 17 kwa mfuko wa kilo 50 wa mbolea aina ya DAP.

Aidha, punguzo la Tshs 5,000/= 6,000/= sawa na asilimia 14 – 19 kwa wastani wa kimkoa kwa mfuko wa kilo 25. Kwa mfuko wa kilo 5, bei imepungua kwa Tshs 1,300/= 1,500/= sawa na asilimia 15 – 20 wastani wa kimkoa.

Kwa muktadha huo, bei elekezi ya mbolea ya DAP kwa mikoa ya Kanda ya Mashariki, Kati, Kusini na Kaskazini zitakuwa kati ya Sh. 51,900/= na 60,300/=. Aidha, kwa mikoa ya Kanda ya Magharibi, Nyanda za Juu Kusini na Ziwa, bei elekezi itakuwa kati ya Sh. 57,000/= na 63,200/=. Bei hizi zitaanza kutumika rasmi tarehe 1 Septemba, 2019 na zitaendelea kutumika hadi pale itakapotangazwa bei nyingine. 

Mhe Hasunga amesema kuwa bei hizo ni kikomo cha juu kwa Mkulima katika eneo husika. Hivyo, wafanyabiashara wanaweza kuuza chini ya bei elekezi bila kuathiri ubora wa mbolea. Kwa kuzingatia hilo, Wizara imetoa bei elekezi ya jumla na rejareja za mbolea kwa uzani wa kilo 50, 25, 10 na 5. 

Alisema kuwa ni kosa kisheria kuuza mbolea kwa bei ya juu ya bei kikomo kwa nia ya kujiongezea kipato.

Alisema ili kumwezesha mkulima mdogo kupata mbolea hizi zikiwa katika hali ya ubora unaokubalika, Wizara imetoa pia bei elekezi ya jumla na rejareja za mbolea kwa uzani wa kilo 50, 25, 10 na 5. Hivyo, wakulima wanashauriwa kununua mbolea katika mifuko maalum. 

Endapo kutakuwa na tofauti ya gharama za usafirishaji kwa baadhi ya sehemu katika baadhi ya maeneo ambayo itakuwa haiendani na bei elekezi, maelekezo ya suala hili yatatolewa kwa Wakuu wa Mikoa/Wilaya kuwapa Mamlaka ya kukaa na Kamati za pembejeo na kurekebisha bei elekezi ili ziendane na hali halisi kwa kuzingatia jiografia ya eneo husika ili kurahisisha usambazaji na upatikanaji wa mbolea kwa wakulima.

Mhe Hasunga alisema kuwa bei elekezi za mbolea hutegemea umbali wa sehemu inakopelekwa kutokea bandarini. Maeneo yote itakapopelekwa mbolea yana umbali kati ya kilometa 1 na 1,600 kutoka bandari ya Dar es salaam. 

Kwa Wastani, gharama ya kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea wa Kilo 50 kwa barabara kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi makao makuu ya Halmashauri kwa barabara ni Sh. 5,500/= kwa kilometa 1,000. Gharama hii hupanda na kushuka kutegemeana na hali ya barabara na hali ya hewa (masika au kiangazi). 

Aidha, usafiri kwa njia ya Reli ni nafuu zaidi kwa sababu gharama za kusafirisha mbolea kwa kilometa 1,000 kwa mfuko wa kilo 50 ni Tshs 4,160 (TRC) au Tshs 4,600 (TAZARA).

Katika kuhakikisha kwamba tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo inaongezeka kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula na kutoa malighafi za viwandani; Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja kama ilivyopendekezwa na wakuu wa nchi za Afrika kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2006. 

Waziri huyo wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa ili kufikia lengo hilo serikali ilianzisha Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS - Bulk Procurement System), kufuta tozo mbalimbali za mbolea, kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa mbolea na kuweka bei elekezi za mbolea kwa mkulima. 

Uingizaji wa mbolea kupitia BPS unahusu mbolea za Urea, DAP, NPK, CAN na SA. Hata hivyo, kwa sasa BPS inatumika kuingiza mbolea za DAP na Urea ambazo zinazotumika kwa zaidi ya asilimia 50.

MBUNGE SAME MAGHARIBI ATEKELEZA ILANI YA CCM JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi Afisa elimu Kata, Ruth Kisaka Mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata ya Msimbo wilayani Same, ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk. Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mshewa, Anastazia Clement kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslimu diwani wa CCM kata ya Mhezi wilayani Same John Kiure kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akihutubia wananchi. 
MBUNGE wa Jimbo la Same Magharibi CCM, Dk. Mathayo David Mathayo amewaomba wananchi wa Jimbo la Same Magharibi kumuunga mkono na kumuombea afya njema Rais John Magufuli ili aweze kuendelea kuiongoza Tanzania izidi kupata maendeleo na kurudisha nidhamu katika sekta mbalimbali nchini.

Dk.Mathayo ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo ambapo akizungumza na wananchi wa kata za Msindo,Mshewa na Mhezi, Mathayo amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio lukuki katika Nyanja mbalimbali.

Aidha Mbunge huyo amekabidhi vifaa mbalimbali alivyoahidi katika kata hizo zikiwemo Fedha, saruji na mabomba ya kusambazia maji huku akitoa rai kwa uongozi wa kila Kata kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Katika Kata ya Msindo Dk. Mathayo ametoa fedha ,mifuko ya saruji,mabomba ya maji,ambapo katika kata ya Mshiwa amekabidhi mifuko ya saruji na fedha taslimu kwa ajili ya shughuli za marendeleo kiasi cha shilingi milioni 13 laki 9 na Zaidi ya shilingi million tisa katika kata ya Mhezi Zaidi ya shilingi milioni tisa na mifuko ya saruji.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuendelea kuwashawishi Wataalamu wake

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya na Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwashawishi Wataalamu wake kujifunza fani tofauti ili kuziba mapengo alipofika kufanya ziara ya kukagua Vitengo tofauti vya Hospitali ya Mnazo Mmoja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya na Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwashawishi Wataalamu wake kujifunza fani tofauti ili kuziba mapengo alipofika kufanya ziara ya kukagua Vitengo tofauti vya Hospitali ya Mnazo Mmoja.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Msafari Marijani akimuelezeas Balozi Seif changamoto wanazopambana nazo Watendaji wake katika kutoa huduma kwa Wananchi.
Mkuu wa Kitengo cha Kuhudumia Wagonjwa mahututi {ICU} Dr. Salum Shaaban Salum akimpatia maelezo Balozi Seif huduma zinazotolewa katika Kitengo hicho kinachohitaji utulivu wa hali ya juu.Picha na – OMPR – ZNZ.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuendelea kuwashawishi Wataalamu wake wa Afya kusomea fani nyengine zenye upungufu wa watendaji ili kuziba mapengo yanayojitokeza katika utoaji wa huduma za Afya.
Alisema lazima ifikie wakati Hospitali za Serikali ziwe na uwezo kamili wa kuwa na Wataalamu wa kutosha badala ya kuendelea kutumia mfumo wa muda mrefu uliozoeleka wa kutegemea Wataalamu wa Nje.
Akifanya ziara fupi ya kukagua uwajibikaji kwa Watendaji tofauti kwenye Vitengo mbali mbali vinavyotoa huduma za Afya kwa Wananchi ndani ya Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Balozi Seif Ali Iddi alisema hatua hiyo ya ushawishi inaweza pia kusaidia kuziba mapengo ya Wataalamu wanaostaafu kwenye Vitengo vya Fani hizo.
Balozi Seif alikitolea mfano Kitengo kinachohudumia Wananchi wanaopatwa na ajali  ambacho kinastahiki kuimarishwa zaidi kwa vifaa pamoja na Wataalamu wazalendo waliobobea kwa vile ajali za vyombo vya Moto hivi sasa zimeongezeka mara dufu bara barani kutokana na harakati za Kimaisha.
Alisema takwimu inaonyesha wazi kwamba Wagonjwa wengi wanaopelekwa Hospitali kwa ajili ya huduma za Afya ni wale wanaopatwa na ajali za bara barani ambao wengi kati yao hulazimika kupelekwa nje ya Zanzibar baada ya kesi zao zinazohusiana na mifupa kushindwa kuhudumiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba lazima Taasisi za Umma zijitegemee kwa kuwa na Wataalamu pamoja na Vifaa vya kutosha ili kuepuka tatizo la kuwapeleka wagonjwa nje Zanzibar sambamba na kuacha kusubiri Wataalamu wa misaada.
Alifahamisha kwamba upatikanaji wa huduma za uhakika katika Vituo na Hospitali za Umma ndio njia pekee itakayojenga imani na upendo kwa Watendaji wa Sekta hiyo kutoka kwa Wananchi walio wengi Nchini.
Mapema Mkurugenzi wa Kitengo cha Maabara katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Msafari Marijani alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uwezo wa kutoa huduma kwa saa 24 kwenye Kitengo hicho bado haujakamilika kutokana na uhaba wa Wataalamu wa Fani hiyo inayohitaji kufanyiwa kazi ya kuwahamaisha Watendaji wake kuzidi kupata mafunzo zaidi ili kujaza pengo liliopo.
Dr. Marijan alisema Kitengo hicho hutoa huduma kuanzia asubuhi hadi majira ya Saa Tatu za Usiku kwa sasa. Lakini hata hivyo Watendaji wake hulazimika kuwajibika katika muda wa ziada pale inapotokea kesi ya dharura inayohitaji kufanyiwa kazi ili kunusuru maisha ya Mgonjwa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Ali Salum Ali alisema Wizara ya Afya kupitia Uongozi wa Hospitali hiyo ina mpango  wa kuimarisha Miundombinu Mipya katika Hospitali hiyo  tegemezi kwa Wananchi walio wengi Kisiwani Unguja.
Dr. Ali alisema Majengo mengi ya Hospitali hiyo ni ya zamani yakiwa yameshapitwa na wakati ambayo  yanahitaji kufanyia matengenezo makubwa vikiwemo baadhi ya vifaa kwenye Vitengo tofauti.
Akizungumzia changamoto inayojitokeza ya Hewa ya {Oxgen} kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr. Ali alisema Timu ya Wizara ya Afya hivi sasa iko Jijini Dar es salaam kufanya mpango wa utafiti wa upatikanaji wa mfumo mwengine wa Liquid Oxgen badala ya ule uliozoeleka ambao hukumbwa na matatizo ya mara kwa mara.
Alisema mtambo wa kutengeneza hewa ya Oxgen uliopo Mnazi Mmoja uliopatikana kwa msaada wa ufadhili Kutoka Nchini Uturuki Mnamo Mwaka 2017 hivi sasa umeharibika na unafanyiwa matengenezo ili ubakie kuwa wa hakiba.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alifahamisha kwamba Wizara ya Afya imejipanga kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa hewa safi ya Oxgen linalozikumba takriban Hospitali zote Nchini katika kipindi cha Miaka 20 sasa.
Alisema Mpango huo umelenga kujengwa kwa Mtambo Mkubwa wa kuzalisha Oxgen katika kiwango cha Mitungi yenye ujazo wa Lita 10,000 utakaowezesha kusambazwa kwa Taasisi nyengine Nchini zitakazohitaji hewa hiyo katika matumizi yao ya kawaida.
Alieleza kwamba kiwango hicho kitakachozalishwa kwenye Mtambo Mpya huo utakaojengwa kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na hakiba ya hewa ya Oxgen kwa asilimia 25% ya ziada.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada ilizochukuwa za kusaidia upatikanaji wa Hewa ya Oxgen kwa Hospitali za Serikali ambapo kwa sasa mahitaji halizi ni Mitungi 43 kwa Siku.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/08/2019.

WAFANYABIASHARA WA MADINI WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 125

$
0
0

 Wafanyabiashara wanne wa madini ya dhahabu na madereva wawili  wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu.

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wanne wa madini ya dhahabu na madereva wawili kulipa faini ya Sh. Milioni 125 milioni na iwapo watashindwa watatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani na pia wametakiwa kulipa fidia zaidi ya Sh. 216.5

Aidha mahakamani imetaifisha kiasi cha sh. Milioni 142 ambazo zilikutwa pamoja sh. 75,000 za kutoka nchini Rwanda ambazo zilikamatwa nyumbani kwa mshtakiwa mmojawapo.

Washitakiwa hao ni Faisal Ally (31) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa s Kariakoo, Isack Shija (28) dereva na mkazi wa Kiluvya na Abdulkarimu Doshi (25) Msimamizi  wa Kampuni ya FAA Truck Ltd  na Mkazi wa Gachuriro Rwanda.

Wengine ni Abas Said (23) dereva na mkazi wa Mtongani, Nassoro Sleyyum (23)dereva na mkazi wa Tandika na Ahmed Abubakari (32) mfanyabiashara na mkazi wa Upanga.

Hukumu hiyo imetolewa leo Agosti 27, 2019 na Hakimu Mkazi, Janeth Mtega Baada ya Washtakiwa hao kukiri makosa matano yaliyokuwa yakiwakabili  ikiwemo kusafirishaji madini yenye thamani ya Sh bilioni 2.9.

Akiwasomea hukumu hiyo hakimu Mtega amesema washtakiwa kwa pamoja  walishiriki genge la uhalifu, kusafirisha madini nje ya nchi, kuuza madini kinyume na sheria, kushindwa kulipa mrabaha na kuisababishia Serikali hasara.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mtega amesema Katika shtaka la kwanza kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 au kwenda jela miaka 20, katika shtaka la pili washtakiwa wote wanatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 5 au kwenda jela mwaka mmoja huku  katika shtaka la tatu la kuuza madini kinyume na sheria washtakiwa hao wote wametakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5  au kwenda jela mwaka mmoja.

Katika shtaka la nne linalomkabili Faisal Ally la kushindwa kulipa mrabaha zaidi ya Sh milioni 216.5 milioni hivyo alihukumiwa kulipa faini ya Shmilioni 5 au kwenda jela mwaka mmoja na katika shtaka la tano washtakiwa wote wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 au kwenda jela miaka 20 baada ya kuisababishia hasara Serikali zaidi ya Sh216.5 milioni.

Hakimu Mtega amesema washtakiwa wakishindwa kulipa faini kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 20 jela 

Hukimu Mtega amesema adhabu hiyo inakwenda kwa pamoja.
Hata hivyo, washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa faini na kukwepa kwenda jela.

Katika kesi hiyo, inadaiwa Januari Mosi na Mei 15, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rwanda, washitakiwa hao waliongoza na kufadhili genge la uhalifu kwa kusafirisha madini dhahabu  yenye uzito wa Kilogramu 30 yenye thamani ya Dola za Marekani 1,283,900 sawa na Sh 2,968,827,672.

Katika mashitaka ya pili, inadaiwa siku na mahali hapo, washitakiwa walisafirisha madini hayo ya dhahabu ya kilogramu 30 yenye thamani ya Dola za Marekani 1,283,900 sawa na Sh 2,968,827,672.

Pia inadaiwa kati ya Mei 4 na Mei 6, mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora walidisposition madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 1.99 yenye thamani ya Dola za Marekani 85,828.7 sawa na Sh 196,932,235.576 bila kuwa na leseni ya biashara hiyo.

Katika mashitaka ya nne, inadaiwa Mei 4 na Mei 6 mwaka huu, maeneo hayo walijipatia Sh milioni 80 ikiwa ni zao la makosa ya kusafirisha madini hayo  kinyume na taratibu.

NMB YAFUNDA WAJASIRIAMALI 1200 KUHUSU ELIMU YA FEDHA

DC MBONEKO AONYA WAPINGA MAENDELEO,ATAKA WANANCHI WASHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0

 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya serikali kuwatatulia matatizo yao ambapo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za serikali. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akionya watu ambao wamekuwa wakipinga maendeleo pamoja na kuwashawishi wananchi wasishiriki kuchangia shughuli hizo za maendeleo kuwa serikali itawachukulia hatua kali. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika kata ya Masengwa na Samuye zilizopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwaonya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikwamisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.Mboneko amefanya ziara hiyo leo Agosti 28, 2019 kwa akianzia wenye Kata ya Masengwa ambapo mkutano wake wa hadhara ameufanyia kwenye kijiji cha Bubale, huku kata ya Samuye akifanyia kwenye kijiji cha Ibingo. 
 
Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Mboneko aliwataka wananchi washiriki na kuchangia shughuli za maendeleo, na kuwapuuza watu ambao hupinga maendeleo. Alisema Serikali itaendelea kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo zinawakabili likiwamo suala la maji, huduma za afya, umeme, kilimo, miundombinu ya barabara pamoja na elimu. “Licha ya serikali kuendelea kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi, pia tunawaomba na nyie wananchi muwe mnashiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili kuunga juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo, na muwapuuze wale ambao hupenda kupinga maendeleo,”alisema Mboneko. 
 
“Naomba pia viongozi wa maeneo haya husika, pamoja na Diwani mtusaidie kutuletea majina ya watu ambao hupenda kupinga maendeleo na kukwamisha wananchi wasishiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili tushughulike nao,” aliongeza. Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika Novemba 24 mwaka huu,Mboneko aliwataka wananchi wasichague viongozi wasiopenda maendeleo, bali wachague wale ambao ni wapigania maslahi ya wananchi ili wapate kutatuliwa matatizo yao.
 
 Katika hatua nyingine amewataka maofisa ugani kuwatembelea wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa, ili pale watakapoanza kulima walime kilimo chenye tija, ambacho kitawapatia mavuno mengi na hatimaye kuinuka kiuchumi. Nao baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya mkuu huyo wa wilaya, wamepongeza kwa kusikilizwa kero zao pamoja na kutatuliwa, yakiwemo masuala ya umeme, maji, barabara, elimu, pamoja na kilimo hasa kwenye ununuzi wa pamba.  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali yao ambayo ni sikivu ambapo itaendelea kutatua changamoto zao zote ambazo zinawakabili. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko akizungumza pia na wananchi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya Serikali kuwatatulia kero hivyo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za Serikali. Diwani wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni, akiwahakikishia wapiga kura wake kuwa changamoto zao zote zitatatuliwa ikiwa serikali ya awamu ya awamu ya Tano ipo kwa ajili ya wananchi. Diwani wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga John Ngegeshi akiomba serikali kuongeza msukumo wa ukamilishaji wa mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme wa REA. Mtendaji wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Husein Majaliwa akisoma taarifa ya kata hiyo na kueleza changamoto ambazo zinawakabili wananchi, ikiwemo uhakika wa masoko ya mazao yao ambayo hulima likiwemo zao la pamba.
 
  Mtendaji wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Damiani Ndassa, akisoma taarifa ya kata hiyo na kuelezea changamoto ambayo ipo ni wananchi kugoma kuchangia shughuli za maendeleo mara baada ya serikali ya Kijiji cha Ibingo kufanya ufujaji wa fedha. Awali Mwananchi Jumanne Makanga mkazi wa kata ya Masengwa akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.  
 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bubale kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eliakimu Methew akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Mwananchi Ndeshema Nshimbi mkazi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
 
Kaimu Meneja wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) Emaeli Nkopi, akijibu maswali ya ukamilishwaji wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye Kata ya Masengwa na Samuye. Msimamizi wa umeme wa REA Hally Twaha akimwakilisha Meneja wa Tanesco mkoa wa Shinyanga, akijibu maswali ya umeme kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.  
 
Meneja wa TARURA halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eng. Salvatory Yambi, akijibu maswali ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. DR Joseph Ngowi akimwakilisha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Amosi Mwenda, akijibu maswali ya sekta ya afya yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akijibu maswali ya Pamba yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwenye Kata zote za Masengwa na Samuye.  

 Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog

KUTANA NA MSANII ANAYETAMANI KUMFIKIA DIAMOND

$
0
0
MAFANIKIO ya Wasanii mahiri wa mziki wa Kizazi kipya maarufu kama Bongo fleva nchini Nassib Abdul (Diamond) imemuibua Yusufu Said ambaye naye ameamua kujikita kwenye sanaa hiyo ya mziki na kutamba na kibao chake cha NATAMBA. 

Amesema kuwa kutokana na kuvutiwa na wasanii hao alijikuta naye akiingia kwenye mziki na kuaza kuchana mistari ambapo hadi hivi sasa amefanikiwa kutoa singo moja ya NATAMBA ambapo anafanya kazi chini ya Mtayarishaji wa Muziki atamulikae kwa jina la 'Producer J. '

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar Es Salaam leo msanii Said amesema anaamini anauwezo mkubwa wa kufanya maajabu katika medani ya mziki endapo atapata mtu wa kuweza kumsimamia kwani hadi hivi sasa hana menejimenti.wa kuweza kumsimamia. 

Amesema kuwa hivi sasa anapambana kupata fedha za kutoa albam mzima ili kuweza kutimiza ndoto zake na mwisho wa siku kuwa mwimbaji mkubwa kama walivyo kundi la Wasafi linaloongozwa na Msanii Diamond Platinum. 

"Natamani sana kufika level za akina Diamond ,alkiba lakini nakosa Menejimeti kama nitapata uongozi naamini wapenzi wa mziki nchini watafurahia kazi zake kwani najiamini na ninatunga mwenyewe" amesema Said 

Aliongeza kuwa licha ya akina Diamond wanamuziki wengine walimvutia kuingia kwenye sanaa hiyo ni pamoja na Pepekale,Bongoman,Dogdog na wengine wengi hivyo anashukuru Mungu leo naye mwanamziki japo bado mchanga. 

Ameongeza kuwa anapenda kufanya kazi na Diamond kwani anatamani siku moja kufikia mafanikio kama ya Diamond, na anamuomba msanii huyo kama anasoma habari hii ajuwe kama kuna mtu anatamani kufanya naye kazi. 

"Namuomba Diamond hata kama hawezi kufanya na Mimi kazi basi msaada wake naomba aweze kunisaidia ili niweze kurekodi albam kwani nina nyimbo za kutosha na ninatunga mwenyewe lakini pia hata nikiwa chini yake nitashukuru Mungu." amesema Said. 

Stendi ya Mabasi Sumbawanga Kuwa ya Mfano Mikoa ya Nyanda za juu kusini

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mji wa Sumbawanga pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa stendi ya mabasi katika mji wa Sumbawanga kutohujumu miundombinu ya eneo hilo na badala yake wasaidie kuimarisha ulinzi na wakandarasi kujenga kwa uzalendo ili kituo hicho kiweze kuwa nembo ya mkoa wa Rukwa.

Amesema kuwa hajawahi kuona ndani ya jengo lastendi kukiwa na vyumba vya kulala wageni, migahawa,  mabanda ya mamalishe, sehemu ya kuegeshea bodaboda na bajaji pamojana mabasi  na kufananisha eneo hilo na kiwanda kwakutarajiwa kuzalisha ajira kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa.

“Stendi hii katika Manispaa ya Sumbwanga itakuwani nembo ya Mkoa wa Rukwa, Sisi Wana Rukwa tutajivunia sana hii stendi , stendi ambayo sijaona popote ambapo kuna vyumba vya kulala ndani ya stendi, iko hapa, kuna ‘restaurant’ kuna mabanda ya mama lishe kuna sehemu ya bodaboda, bajaji, kuna mabasi, kuna kila aina ya mambo inajitosheleza, hiki kitakuwa nikama kiwanda kidogo maana kitaajiri watu wengi sana hapa, wale wanaojenga hapa wasihujumu miundombinu hii,” Alisema. 

Ameyasema hayo leo tarehe 28.8.2019 alipotembelea stendi hiyo ya mabasi yam ji wa Sumbawanga iliyoanza kujengwa mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka 2019 na kutarajiwa kumalizika mwezi Disemba mwaka huu akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Wataaalamu wengine kutoka Ofisi ya mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Sumbawanga. 

Akitoa taarifa ya ujenzi huo Mhandisi wa Manispaa ya Sumbawanga Suleimani Mziray alisema kuwa kutokana na ufinyu wa fedha stendi hiyo itajengwa kwa awamu mbili na mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 40 na bado mkandarasi anaendelea na ujenzi na kuongeza kuwa katika jengo hilo kutakuwa na eneo la kuwahifadhi abiria zaidi ya 400 watakaokuwa wakisubiri safari zao za nje na ndani ya mkoa.

“Kutokana na Ufinyu wa fedha ujenzi wa kituo cha mabasi eneo la katumba Azimio utafanyika kwa awamu mbili ambapo mpaka sasa kazi zimekwishafanyika kwa asilimia 40 na bado inaendelea kwenye maeno tofauti kulinngana na Mkataba, jengo Kubwa litakuwa nae neo kwaajili ya kusubiria abiria ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba abiria 400,” Alisema

Aidha Msimamizi wa ujenzi huo kwa upande wa Mkandarasi Said Rajabu Mbelwa ameongeza kuwa ili kufika kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo hilo kutakuwa na Lifti ili kuwasaidia walemavu na wale ambao afya zao haziruhusu kutumia ngazi 
“Hapa kuna Lifti ambayo itatumika kwaajili ya Walemavu n ahata ukiwa mgonjwa kwasababu itakuwa siyo rahisi kupita kwenye ngazi ya kupanda kwa mguu kama una matatizo ya afya, kwahiyo imewekwa kwaajili ya walemavu na watu amba afya zao si nzuri sana,” Aliongezea. 

Hadi kufikia hatua hiyo mkandarasi SUMRY ENTERPRISES LTD tayari ameshalipwa Shilingi Bilioni 1.72 ambayo ni sawa na asilimia 28.89 ya Shilingi bilioni 5.95 ambayo ni gaharama ya ujenzi wa stendi hiyo, ambayo inategemewa kuwa na vyumba vya kulala waheni, vymba maalumu vya kufanyia mazoezi(Gym), kituo cha polisi, sehemu ya migahawa mikubwa na mama lishe na sehemu za kuegeshea Baiskeli, Bodaboda, Bajaji, Teksi na mabasi yanayosafirisha abiria ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa. 

 Mkuuwa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mwenye kaunda suti ya Kijivu) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa viongozi pamoja na wataalamu wengine wakikagua jengo kuu la stendi ya mabasi Sumbawanga linaoendelea kujengwa katika eneo la katumba azimia Sumbawanga Mjini.
 Mhandisi wa Manispaa Suleiman Mziray (T-shirt ya Zambarau) akitoa maelezo ya uzio unaozunguka stendi ya Mabasi Sumbawanga Kwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja na viongozi na wataalamu wengine waliofika kukagua ujenzi wa stendi hiyo. 
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images