Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TIMU 16 BORA ZAPATIKANA MSIMU WA TATU WA SPRITE BBALL KINGS

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSIMU wa tatu wa Mashindano ya Sprite Bball Kings hatua ya mtoano imefanyika leo kwa timu 43 kushuka dimbani kutafuta tu 15 zitakazocheza kwenye hatua ya 16 bora.

Mechi hizo zilizoanza majira ya saa 2 asubuhi kwenye Viwanja vya JMK Park zilikuwa na ushindani mkubwa sana huku timu ngeni zikionekana kujiandaa vizuri.

Msemaji wa mashindano hayo Goza Chuma amesema kwa mwaka huu ushindani umekuwa ni mkubwa sana, timu zimejiandaa kuja kusaka kitita Milioni 10 zitakazoshindaniwa kwa mshindi wa kwanza.

Goza amesema, msimu huu wa tatu wa Sprite Bball Kings umeleta fursa kwa vijana kwani mchezo wa kikapu ni ajira tofauti na mawazo ya zamani ya watu kuwa unachezwa na vijana waliosoma au mabishoo.

“Mwaka huu watu wanaweza kuona idadi ya timu zimepungua ila sio kama mashindano yamekosa ubora hapana ila msimu huu watu wamejipanga sana na unapoona hapa hakuna timu iliyopota kwa walk over kwani zote zimefika tofauti na misimu iliyopota,” amesema Goza.
“Sheria za mwaka huu zimebadilika, misimu miwili tuliweka sheria ya kuwa na wachezaji watatu wa ligi kuu ila kwa msimu huu ni wachezaji sita kwahiyo nyie wenyewe mtaona ni ushindani wa aina gani utakaokuwepo kwenye msimu wa mwaka huu,”

Teknolojia ya mawasiliano ni nguzo muhimu ya ukuaji wa biashara nchini

$
0
0
LENGO la taifa la maendeleo linaelezea namna ambavyo biashara ndogondogo na za kati (SMEs) ni muhimu katika uchumi. Inakadiriwa kuwa SMEs zina jumla ya biashara milioni 3 ambazo kwa pamoja zinachangia zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa (GDP).

Kutokana na hali hiyo, ni muhimu kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua.
Tunapojadili SMEs ni ukweli usiopingika kuwa sekta ya mawasiliano ni muhimu kwa ukuaji wake. Makampuni ya mawasiliano ya simu hutupatia huduma za vifurushi vya data, kutuwezesha kuwasiliana kibiashara, au na rafiki zetu na familia kwa urahisi, na programu tumishi (apps) za makampuni hayo hurahisisha maisha yetu.

Msingi wa biashara ni mawasiliano na taarifa kati ya mnunuzi na muuzaji na makampuni ya mawasiliano nchini Tanzania, kwa kiasi kikubwa yanasaidia jumuiya ya wafanyabiashara.

Kwa mfano, Tigo ilikuwa moja ya kampuni za kwanza kujiunga na mfumo wa malipo wa serikali (Government’s e-Payment Gateway). Kwa kushirikiana na serikali, Tigo imewarahisishia sana wafanyabiashara kulipa ankara zao.

Programu tumishi kama vile Tigo Pesa zimewasaidia pia wafanyabiashara kukusanya malipo ya bidhaa zao. Wateja sasa wanaweza kulipia bidhaa zao kwa kutumia programu ya Tigo Pesa, au hata kuwalipa wafanyakazi wao. Inakadiriwa kuwa zaidi ya kampuni 70,000 zinatumia huduma za tigo kwa minajili hii.

Pamoja na hayo, Tigo imezindua njia ya huduma kwa wateja kwa kutumia WhatsApp ambao ni pamoja na wateja wa kibiashara. Huduma hiyo inawawezesha wateja kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja kwa urahisi na haraka kuhusu tatizo lolote.

Kadiri idadi ya SMEs na mchango wake katika uchumi unavyozidi kuongezeka, ni jambo jema kuona makampuni ya mawasiliano yakifanya kazi kutoa huduma kwa pamoja.

KUTAFUTA MFANYAKAZI WA NDANI MARUFUKU TARAFA YA ITISO - AFISA TARAFA ITISO

$
0
0
AFISA Tarafa Itiso Remidius Emmanuel amesema kuwa tarafa hiyo siyo sehemu kutafuta wafanyakazi wa ndani hasa katika nyakati hizi ambazo wanafunzi wa darasa la saba wanahitimu masomo yao.

Akizungumza katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa Afisa tawala wa Itiso Remidius Emmanuel ameonekana kukerwa na  baadhi ya watu ambao wameendelea kuwekeza kwa wahitimu wa darasa la saba  kwa lengo la  kuwaandaa wakawe wafanyakazi wa ndani "House Girl".

"Nimewatazama wanafunzi wakati wote wakiimba hapa na kuagana na wenzao, nimesikiliza pia risala yao, lakini nilipouliza wangapi wanayo matumaini ya kufaulu wote wamenyoosha mikono, tafsiri yake ni kwamba wanayo ndoto ya kusonga mbele, sasa huwa ninakerwa sana na ile dhana ya watu kutoka maeneo mbalimbali wanapiga simu kutafutiwa wafanyakazi ndani ya tarafa yetu Itiso, wakiwambia muwatafutie wafanyakazi wa ndani wambieni Tarafa ya Itiso sio mahala pake, hatuwaandai kuwa wafanyakazi wa ndani bali tunahitaji wafaulu na kuendelea na elimu ya Sekondari na siku za usoni kupitia kwenu tupate wataalamu katika fani mbalimbali ili waendelee kulijenga taifa" Ameeleza.

Na amewaonya wazazi ambao kwa namna moja au nyingine  watakuwa kikwazo kwa wanafunzi hao kuendelea na Elimu ya Sekondari ikiwa wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo yao.
"Ninazo taarifa za baadhi ya wazazi kuwa kikwazo na kutamani watoto wao kufeli masomo yao, ole wao wabainike kuwa chanzo cha vijana hawa kutoendekea na masomo" Ameongeza.

Mapema akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mkuu wa shule ya Msingi Zajilwa  yenye jumla ya  wanafunzi 1,239 Mwalimu Joseph Lusambo ameeleza kuwa jumla ya wanafunzi 84 wanatarajiwa kuhitimu elimu yao ya msingi katika shule hiyo kwa mwaka 2019 na kwamba wanayomatumaini makubwa juu ongezeko la ufaulu kwa mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita kutokana na maandalizi ambayo yamefanyika shuleni hapo huku akizitaja sababu za matarajio ya ufaulu kuongezeka kuwa ni pamoja na  uwepo wa ufaulu bora kwa mitihani ya kujipima sambamba na ubora na juhudi za walimu waliopo.

Mkuu wa shule hiyo amezitaja baadhi ya changamoto shuleni hapo kuwa  ni pamoja na ukosefu wa vitabu vya kutosha,vyumba vya Madarasa ambapo  vyumba vilivyopo ni 8 kati ya 27 vinavyohitajika, hatua inayopelekea baadhi ya wanafunzi kusomea nje.

Mbali na kuwahimiza wanafunzi wanaobaki shuleni hapo kuhakikisha wanasoma kwa bidii, Diwani wa kata ya Zajilwa Farida Ramadhani  amesema kuwa tayari  changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa imeanza kufanyiwa kazi kufuatia uwepo wa tofali 35,000 zitakazo saidia kufanikisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na tayari Serikali ya kijiji hicho  imepitisha  fedha kwa  ajili ya kuanza ujenzi wa awali na kinachosubiliwa  kuidhinishwa kwenye mkutano wa Wananchi na kushirikisha wataalam wa  Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kila hatua.

Katika hatua nyingine Afisa Tarafa huyo alitambua na kupongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge wa jimbo hilo la Chilonwa  Joel  Mwaka ambaye kwa nafasi yake amekuwa msaada mkubwa katika kufuatilia na kusimamia maendeleo ya shule hiyo.

Akihitimisha hotuba yake mbali na kuhimiza Wazazi,Walimu,Jamii pamoja  na wanafunzi kila mmoja kutimiza wajibu wake, Afisa tarafa huyo alisema kwa suala la upatikanaji wa Vitabu, Serikali inaendelea kutatua changamoto hiyo
 " ninazo taarifa kwamba  ndani ya kipindi hiki cha mwaka  huu 2019 takribani Vitabu 317  vimetolewa na Serikali katika shule hii, ingawa pamoja na juhudi za Serikali  bado upo umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali kuona namna ya kukabiliana na changamoto za namna hii na  jambo hilo  linawezekana" alieleza.

Mahafali hayo pia yalihudhuriwa na Afisa Elimu wa kata hiyo  Heri Justine Mhinda, Wataalamu kutoka ngazi ya kata na vijiji, Wajumbe wa Serikali ya kijiji, Viongozi wa dini pamoja na wananchi wa Kijiji hicho.

 Afisa Tarafa Itiso Bw.Remidius Emmanuel akihutubia wananchi waliojitokeza katika Mahafali ya Darasa la saba Shule ya  msingi Zajilwa.
AfisaTarafa Itiso Bw.Remidius Emmanuel akipata maelezo ya jambo flani kutoka kwa mkuu wa shule hiyo Bw. Joseph Nicholaus Lusambo katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa.
 Risala ya Mkuu wa shule kwa Mgeni rasmi ikikabidhiwa na Mwalimu Fatuma Abubakari katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa.
 Diwani wa Kata ya Zajilwa Mhe.Farida Ramadhani akizungumza na wananchi waliojitojeza katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa.



 Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa

Picha na baadhi ya wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi Zajilwa

Dkt Kalemani aagiza vyombo vya usalama kuwakamata wakandarasi wa umeme vijijini Katavi

$
0
0
Na Hafsa Omar, Katavi
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa agizo kwa vyombo vya usalama mkoani Katavi kuwakamata wakandarasi waliopewa  kazi ya kusambaza umeme vijijini mkoani humo kutoka kampuni ya CRCBEG baada ya kusuasua katika utekelezaji wa kazi.

Alitoa agizo hilo Agosti 25, 2019 wakati akielekea kwenye kijiji cha Ntibiri wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi ili kukagua kazi ya usambazaji umeme, mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji Kirida wilayani humo.

Waziri wa Nishati pia alitoa agizo la kushikiliwa  kwa  hati za kusafiria za wakandarasi hao mpaka watakapomaliza kazi zao za usambazaji umeme walizopangiwa na Serikali.

 “ Nilitoa mwezi mmoja eneo lote la kilometa 27 muwe mmeshawasha umeme lakini bado, Kijiji cha Majimoto bado hamjawasha, leo nimepita hapa sijaona vibarua wakihangaika, na wala nguzo hazijafika, nimefika Shule ya Sekondari kule nguzo hazijafika na wala hamjasambaza popote.”alisema Dkt. Kalemani.

Waziri Kalemani, pia aliwaagiza Mameneja wa TANESCO kutoondoka katika eneo hilo ili kuhakikisha kazi ya usambazaji umeme inafanyika kwa kasi zaidi, “ninataka umeme ufike Kijiji cha Majimoto, ifikapo tarehe 5 mwezi ujao  na mameneja wote mtabaki hapa kusimamia kazi.”

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Ntibiri, Dkt. Kalemani aliwaeleza wananchi hao kuwa, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 89 kwa ajili ya usambazaji umeme mkoani Katavi  na kuwahakikishia kuwa, mkoa mzima utapata umeme.

“Leo nimetoa maelekezo kuwa, eneo la Ntibiri na maeneo ya jirani, wakandarasi watamaliza kazi mwezi wa 12 mwaka huu, hakuna kijiji kitakachobaki, sasa kama eneo lako halijapitiwa na umeme, kuanzia sasa litapitiwa.” Alisema Dkt Kalemani

Akiwa wilayani Mlele, Waziri wa Nishati, pia aliwasha umeme katika Kijiji cha Society katika eneo la wachimbaji wadogo wa dhahabu hali itakayopelekea wachimbaji hao kufanya shughuli zao kwa tija.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi (hawapo pichani),katika  Kijiji cha Society wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi  kabla ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi Kijiji cha Ntibiri wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi  wakati alipofika kukagua kazi ya usambazaji umeme kwenye Kijiji hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika Kijiji cha Kirida wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi.

KLABU YA MPIRA YA MANCHESTER CITY YAONGEZA MUDA WA USHIRIKIANO NA QNET

$
0
0


· Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City imeongeza muda wa ushirikiano na mshirika rasmi wa mauzo ya moja kwa moja, QNET 

· Muhula huu mpya utasherehekea miaka kumi ya ushirikiano 

Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City imeongeza muda wa ushirikiano wake na kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ya Asia, QNET. Hii itadumisha ushirikiano huu kufikia miaka kumi. Ushirikiano huu wa muda mrefu utaifanya kampuni ya QNET kuendelea kuwa Muuzaji rasmi wa moja kwa moja wa timu ya wanawake na wanaume ya Manchester city. 

Ushirikiano huu unaashiria hatua kubwa sana katika mwezi Mei mwaka 2018 wakati klabu ya Manchester city ilipoikaribisha kampuni ya QNET kama mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeves) katika Ligi ya Wanawake ya Super League. Katika kipindi chote kijacho cha ushirikiano huu kampuni ya QNET itaendelea kutoa kliniki za mpira wa miguu zinazosimamiwa na klabu ya mpira a miguu ya Manchester city kwa jamii duniani kote, pamoja na kujihusisha na watumiaji na wasambazaji kupitia uhusiano huu na klabu ya City. 

Kusherehekea tangazo hili QNET imezindua toleo dogo la saa za mkononi inayojulikana kama 'QNETCity Champions' zinazoundwa na kuzalishwa na mafundi mashuhuri wa nchini Switzerland. 

Makamu wa Raisi Mwandamizi wa ushirikiano wa City Football Group, bwana Damian Willoughby, alitoa maoni yake na kusema "Tunafuraha kutangaza kwamba QNET imekuwa mshirika wa hivi karibuni kuongeza muda wa ushirikiano na Manchester City katika makubaliano ya muda mrefu ambayo yatashuhudia tukisherehekea miaka kumi ya kufanya kazi kwa pamoja. Ushirikiano huu uliweka historia pale QNET ilipokuwa mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi (sleeve) katika ligi ya wanawake ya Super League na tunafuraha kuingia katika ukurasa mwingine kwa pamoja". 

Mkurugenzi Mkuu wa QNET Bwana, Malou Caluza alisema: “Huu ni ushirikiano unaothaminiwa sana kwa QNET na Manchester City kwa sababu utendaji bora ni msingi wa chapa zote mbili. 

 Sote tunamsukumo kuelekea katika mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii, ari na kujitolea. Kupitia ushirikiano huu, tumeweza kuwa na fursa ya kuwapeleka watoto kutoka katika familia zenye kipato kidogo kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda manchester kwaajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa miguu na kozi ya lugha ya kiingereza, ambayo kweli imekuwa ni fursa nzuri sana ya kubadilisha maisha kwa watoto walio wengi. 

Tunatumaini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za kushirikiana na kuwafikia mashabiki wetu."

TCA KULETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA UREMBO

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukutembelea moja ya meza za vipodozi vilivyokuwepo katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea moja ya meza za vipodozi lipotemelea meza ya kutengeneza mawigi katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wadau wa urembo mara baada ya kukutembelea meza za vipodozi vilivyokuwepo katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa urembo wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa ongezeko la wagonjwa wa Kansa kutoka taasisi ya Kansa Ocean road imefikia wagonjwa 7649 mwaka 2018 ukilinganisha na wagonjwa 2416 mwaka 2015.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa chama Cha urembo na vipodozi nchini (TCA), Waziri Ummy amesema kuwa amesukumwa sana mapinduzi yanayofanywa katika sekta ya urembo na vipodozi na amesukumwa zaidi  kuhudhuria ufunguzi huo na akiwa mwanamke mwenye dhamana katika Wizara inayosimamia jinsia pia ameona hilo ni jambo jema la kuungwa mkono hasa sekta hiyo inahusisha afya pia.

Amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa ya ini, figo, moyo na saratani ambapo kwa mwaka 2015 wagonjwa wa kansa walikuwa 2416 hadi kufikia wagonjwa 7649 kwa mwaka 2018 na sababu mojawapo inayosababisha ni matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu vikali na amewashauri watengenezaji wa vipodozi kutengeneza mazingira bora ya biashara kwa kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango huku akiahidi ushirikiano katika suala zima la upatikanaji wa masoko.

Waziri Ummy amewapongeza waanzilishi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wao Shekha Nasser kufanikisha kuanzishwa kwa chama hicho na wao kama Wizara watahakikisha wanatengeneza mazingira bora ya biashara ili kuendeleza ujenzi wa viwanda pamoja na kuuza na kufanya biashara nje ya nchi.

Vilevile amewashauri Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) pamoja na baraza la taifa la elimu  ya ufundi (NACTE) kuweka sehemu ya mafunzo katika sekta urembo katika mitaala ya elimu ili hata watu kutoka nje ya nchi waweze kuja kujifunza masuala ya urembo nchini na kuzidi kuipa thamani sekta hiyo, pia amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali itaendelea kukuza sekta hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Vilevile ametoa rai watengenezaji na wauzaji wa vipodozi na urembo kufuata kanuni na taratibu pamoja na kuwashauri watanzania kukitumia chama hicho ili kuwe na sauti moja ya kuwasiliana  na kufanya maamuzi kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Awali akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa chama hicho Shekha Nasser amesema kuwa tasnia hiyo inakua haraka duniani, barani Afrika na nchini Tanzania na kwa mwaka 2017 pekee ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 532 duniani huku ikitegemewa kufikia dola bilioni 863 kwa mwaka 2024 kwa ukuaji wa asilimia 7 kwa mwaka.

Amesema kuwa kuanzishwa kwa chama hicho kumelenga kufanikisha malengo mbalimbali yakiwemo kuwaunganisha wadau wote wa sekta ya vipodozi na urembo pamoja na kukusanya maoni na kuyapeleka kwa serikali yakiwa na sauti moja na hiyo ni pamoja na  kuendeleza viwanda vidogo, vya Kati na vikubwa na vinachangia sana katika kukuza ajira kwa vijana, kulipa kodi na mapato kwa serikali.

Shekha amesema kuwa Tanzania inapata asilimia 3 pekee katika soko la dunia huku wanufaika wakubwa wakiwa ni nchi za Afrika kusini, Kenya na Nigeria.

RAIS DKT.SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WIZARA, KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi (kushoto) akichangia katika mkutano wa Wizara hiyo wa   utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)
Makamo wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) alipokuwa akichangia  wakati wa  mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara ya  Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi  uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Marium Juma Abdalla Saadalia chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Baadhi ya Maofisa katika Wizara ya Kilimo,Maliasilio,Mifugo na Uvuvi wakiwa katika mkutano wa Wizara hiyo wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati),[Picha na Ikulu.] 26/08/2019.

UKILIPISHWA NGUZO ‘NIBIPU’ NITAKUPIGIA – NAIBU WAZIRI NISHATI

$
0
0
Na Veronica Simba – Kilimanjaro
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa namba yake ya simu ya mkononi kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na kuwaelekeza ‘wambipu’ ili awapigie na kutatua kero husika, endapo wataambiwa kulipia nguzo, nyaya au mita wakati wakipeleka maombi ya kuunganishiwa umeme maeneo ya vijijini.

Ametoa onyo kali kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ngazi ya Wilaya na Mkoa ambao watakaidi agizo la serikali linaloelekeza kuwa wananchi wote wa vijijini waunganishiwe umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 tu pasipo kulipia kifaa chochote ikiwemo nguzo, nyaya au mita.

Alikuwa akizungumzia yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya nishati, kwenye Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mkoa wa Kilimanjaro, leo, Agosti 24, 2019, ambalo lililenga kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya.

“Rais Magufuli alisema tupunguze gharama za kuunganishia wananchi umeme vijijini kutoka shilingi 177,000 hadi 27,000 tu. Atakayekwenda TANESCO akashindwa kuunganishwa kwa bei hiyo au akaambiwa lipia nguzo, lipia waya, lipia mita; Namba yangu ni 0652558010. Nibipu, nitakupigia,” alisema huku akishangiliwa na umati wa wananchi.

Akitoa takwimu za waliounganishiwa umeme vijijini, mkoani Kilimanjaro kwa gharama hiyo ya shilingi 27,000 tangu agizo hilo lilipoanza kutekelezwa mwezi Mei mwaka huu, amesema mpaka sasa idadi imefikia 5,000 huku waliounganishwa kwa mwezi Julai pekee ni zaidi ya watu 2,000.

Amesema Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania kwa kuwa na umeme katika maeneo mengi ambayo ni asilimia 87.

“Mkoa una Kata 148 ambazo zote zina umeme. Una vijiji 519 ambavyo kati yake, 453 vina umeme. Bado vijiji 66 tu ambavyo vipo wilaya ya Hai (5), Siha (7), Rombo (8), Mwanga (4), Moshi (22) na Same (20).

Amesema, kati ya vijiji 66 vya Mkoa wa Kilimanjaro ambavyo bado havijaunganishiwa umeme, vitabaki 35 kufikia Desemba mwaka huu na kati ya hivyo, serikali imeiagiza TANESCO kuchukua vijiji 18 ili iviunganishe hivyo Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III – 2), utaunganisha vijiji 17 tu vitakavyokuwa vimesalia.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, pamoja na mambo mengine, amempongeza Rais Magufuli kwa kuwapa nafasi za uongozi wanawake ambao wameonesha kuwa wanaweza, akitolea mfano wa Makamu wa Rais, Mama Samia Hassan na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza katika Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika Agosti 24, 2019 mkoani Kilimanjaro kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Tawala na Serikali, wakishiriki katika Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika Agosti 24, 2019 mkoani Kilimanjaro kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika Agosti 24, 2019 mkoani Kilimanjaro kumpongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya.

56% YA VIFO VYA VICHANGA INASABABISHWA NA MAGONJWA YA HOSPITALI

$
0
0
Mfamasia kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando akitoa mafunzo kuhusu njia bora ya kujikinga na kudhibiti maambukizi wakati wa kumuhudumia mgonjwa kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline). 
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka kwa moja ya washiriki wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti maambukizi kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline). 
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akielekeza jambo wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti maambukizi kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline). 
Picha ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya na Timu ya Wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti maambukizi kwa taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline). 

***************** 



Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-KAGERA 

Asilimia 56 ya vifo vya watoto wachanga husababishwa na magonjwa yanayotokea wakati wa utoaji huduma za Afya (Healthcare Associated Infections) katika nchi zinazoendelea. 

Hayo yamesemwa na Afisa kutoka kitengo cha uhakiki ubora wa huduma kutoka Wizara Afya Dkt. Radenta Bahegwa kwenye semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa IPC Guidline) 

Alisema taarifa ya tafiti inasema kuwa 75% ya vifo hivyo vilitokea katika nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo nchi ya Tanzania, huku ukosefu wa huduma ya maji safi yakutosha katika baadhi ya zahanati ikionekana ni moja ya changamoto iliyosababisha tatizo hilo la vifo. 

“Tafiti zinaonesha kuwa, 42% ya Vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyo na wodi za kujifungulia havikuwa na maji na vifaa kwaajili ya kuoshea mikono, hali inayopelekea kuwa katika hatari yakupata maambukizi kwa vichanga, mama zao au Watoa huduma”. 

Aidha, alisema kutofuata kanuni na taratibu za utoaji huduma kwa wagonjwa kwa baadhi ya Watoa huduma ni moja kati ya visababishi vikubwa vya vifo vya vichanga vingi katika nchi zinazoendelea, jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya Sekta ya Afya katika nchi hizo ikiwemo Tanzania. 

Hata hivyo alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Watoa Huduma kufuata misingi na taratibu za kutoa huduma kwa Wagonjwa (IPC Standard) ikiwemo kunawa mikono ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi yanayotokea wakati wa utoaji huduma kwa Wagonjwa ikiwemo vichanga (Healthcare Associated Infections). 

“Usafi wa mazingira kwa kufuata kanuni za usafi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya, hauishii kusafisha maeneo tu, bali hata kupangilia kila kitu ili kikae katika eneo linalostahili”. Alisema Dkt. Radenta Bahegwa. 

Aliongeza kuwa kuweka mazingira safi kutasaidia kupunguza hatari za maambukizi kwa Mgonjwa au kwa Watoa huduma, pia kunaongeza hamasa ya kufanya kazi kwa bidi kwa Watoa huduma na kuvutia wagonjwa jambo litalosaidia kuongeza mapato katika Kituo cha Afya. 

Kwa upande wake Afisa Afya, Mazingira kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali (JBHN) Bw. Said Chibwana alisema kuwa, Lazima kuwe na choo angalau kimoja kwa kila watumiaji 20 kwa wagonjwa wa ndani, na watumiaji wote 25 kwa Wagonjwa wa nje. 

Alisema upatikanaji wa huduma za maji safi katika Vituo vya kutolea huduma za Afya husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa, kulinda Afya za watoa huduma na Wagonjwa wakati wa utoaji wa huduma za Afya 

Wizara ya afya inafanya mafunzo kwa Watoa huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) katka Mkoa wa Kagera, lengo ni kuelekeza njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti maambukizi kwa kufuata taratibu na miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Guideline).

MGALU ATOA ONYO KALI KWA MKANDARASI WA UMEME VIJIJINI KILIMANJARO

$
0
0


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngarenairobi, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro alipokuwa katika ziara ya kazi, Agosti 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika shule ya msingi Gararagua, iliyopo wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara.
**************

Na Veronica Simba – Kilimanjaro

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa onyo kali kwa Mkandarasi Urban & Rural Engineering, ambaye anatekeleza mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu mkoani Kilimanjaro, kwa kumwambia asiijaribu serikali kwa kutikisa kibiriti kwani njiti zimejaa na kitawaka.

Alitoa onyo hilo kwa nyakati tofauti Agosti 25, 2019 akiwa katika ziara ya kazi kwenye Wilaya za Hai na Siha, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na viongozi wao kuwa kasi ya mkandarasi huyo hairidhishi.
Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Hai, Naibu Waziri Mgalu alikiri mbele yao kuwa utendaji kazi wa mkandarasi husika unasuasua na zaidi ameonesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa serikali kwa kutoitikia wito alipoitwa kushiriki kwenye ziara hiyo pasipo kutoa sababu yoyote.
Akielezea zaidi, Naibu Waziri alisema yeye binafsi alijaribu kuwasiliana na mkandarasi huyo kwa njia ya simu pasipo mafanikio na hata ujumbe mfupi wa maandishi aliomtumia kumtaka apokee simu, haukujibiwa; kitendo ambacho alikiita ni dharau.

“Sasa mimi nataka nitoe salamu kwake. Mkandarasi Urban & Rural Engineering naona unatikisa kibiriti, unataka ujue kama kina njiti au hakina, na kama njiti zimejaa au zina baruti. Nataka nikwambie kibiriti kimejaa, njiti zina baruti na kitawaka.”

“Ulichokifanya ni dharau na unatupelekea tufanye maamuzi ya kuanza mapitio; na ni kweli nathibitisha ameshindwa kazi,” alisema Naibu Waziri.
Kufuatia hali hiyo, alimwagiza Msimamizi wa Mradi husika kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kumjulisha mkandarasi huyo kwenda Dodoma mara moja kushiriki katika kikao kitakachofanya mapitio ya suala hilo ili ikibidi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

“Kama ameshindwa kazi, tutawapatia wakandarasi wengine au hata TANESCO wanaweza kumalizia kazi husika.”
Awali, Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, alimweleza Naibu Waziri kuwa, Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoani Kilimanjaro unagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania takribani bilioni 12.

Alisema, Mradi unahusisha ujenzi wa kilomita 150 za msongo wa umeme wa kilovoti 33, ujenzi wa kilomita 334 za msongo wa umeme wa kilovoti 400 na ufungaji wa mashine umba (transfoma) 132 na kwamba unatarajiwa kuunganishia umeme jumla ya wateja 3,572 katika vijiji 75 ndani ya mkoa.
Aliongeza kuwa, kwa ujumla utekelezaji wa mradi husika mkoani humo umefikia asilimia 43 hadi sasa.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri aliwasha umeme katika shule za msingi za Roo na Msamadi zilizopo wilayani Hai, pamoja na eneo la viwanda Mwangaza na shule ya msingi Gararagua wilayani Siha. Pia, alizungumza na wananchi wa Kata ya Ngarenairobi wilayani Siha.

TIMU ZA JESHI POLISI TANZANIA ZIKIWA MAZOEZINI NCHINI KENYA KABLA YA KUANZA KWA MASHINDANO YA EAPCCO GAMES

$
0
0
TIMU za Jeshi la Polisi Tanzania zikiwa katika mazoezi katika viunga vya
Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kuwasili
tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa
Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES), michezo
inayofanyika Nchini Kenya.

Katika mashindano hayo, Jeshi la Polisi Tanzania linashiriki katika
michezo ya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kareti, judo, taekwondo,
vishale, riadha, kuvuta kamba na ulengaji wa shabaha. Mwaka jana
2018 michezo hiyo ilifanyika nchini Tanzania, ambapo Jeshi la Polisi
Tanzania liliibuka mshindi wa pili katika matokeo ya jumla.
 Timu ya mchezo wa Judo ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa katia mazoezi
katika viunga vya Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya
baada ya kuwasili tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa
Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO
GAMES), michezo inayofanyika Nchini Kenya.
 Timu ya mchezo wa kareti ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa katia mazoezi
katika viunga vya Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya
baada ya kuwasili tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa
Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO
GAMES), michezo inayofanyika Nchini Kenya.
 Timu ya mpira wa kikapu ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa katia mazoezi
katika viunga vya Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya
baada ya kuwasili tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa
Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO
GAMES), michezo inayofanyika Nchini Kenya.
Timu ya wanariadha wa Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa katia mazoezi
katika viunga vya Chuo Kikuu cha Kenyata Jijini Nairobi nchini Kenya
baada ya kuwasili tayari kwa mashindano ya michezo ya Wakuu wa
Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO
GAMES), michezo inayofanyika Nchini Kenya.

Kiwanda cha Happy Sausage chailalamikia halmashauri kukwamisha uzalishaji

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
KIWANDA cha kusindika nyama cha Happy Sausage cha jijini Arusha kimeiomba serikali kuingilia kati mgogoro wao na Halmashauri ya jiji la Arusha unaokwamisha kukuwa kwa uzalishaji na hivyo kushindwa kufikia soko la kimataifa ikiwemo la Afrika mashariki.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya kiwanda hicho kiwandani hapo Andrew George wakati akizungumza na vyombo vya habari kiwandani hapo kuelezea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho pamoja na changamoto zao.

Amesema kuwa Halmashauri ya jiji la Arusha imeendelea kukwamisha juhudi za ukarabati wa kiwanda chetu kwa kukataa kutoa kibali cha ukarabati wa (Bulding Permit) wakati serikali kupia wizara ya mifugo na bidi ya nyama wameshatoa maelekezo ya kufanyika kwa ukarabati .

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa hatua hiyo imetokana na mgogoro wa muda mrefu unaofikia miaka name kati ya pande hizo kuhusiana na suala zima la umiliki wa Ardhi wa eneo ambalo hadi sasa kila upande unavutia kwake wakati halmshauri hiyo ni mbia kati ya wabia 12 wa uwekezaji wa eneo la kiwanda .

“Kiwanda kimeshindwa kufikia malengo ya uzalishaji inatokana na kujikuta ikikwamishwa kufanya ukarabati wa kiwanda hicho cha usindikaji wa nyama kwa hali hiyo ambayo serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikikitaka kiwanda hicho kufanya ukarabati imekuwa ndio changamoto yetu kufikia malengo ya uzalishaji”.alisema George

Amesema kuwa Kiwanda hicho Licha ya misukosuko hiyo katika kipindi cha miaka sita kimeweza kulipa wafugaji wanaokuja kuuza mazao ya mifugo kiasi cha tsh.bilion 9.3 na kuweza kilipa kodi ya serikali leseni tozo na vibali mbali kiasi cha bilion 2.2 katika kipindi cha miaka 6

Ameeleza kuwa masoko yao makubwa ya kuuza bidhaa wanazozalisha ni masoko ya ndani ya nchi katika mikoa yote nchi kupitia mahoteli mbali mbali ya kitalii na maduka ya rejereja ya nyama nchini ambapo mpango wa kwa sasa ni kuelekea kwenye masoko ya nje ya nchi yakiwamo ya Afrika ya mashariki pamoja na Soko la pamoja la jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC.

Amesema kuwa kuhusiana na uzalishaji wa kiwanda hicho unavyobeba wananchi wengi wenye kuzalisha mazao ya mifugo kwenye kanda ya kaskazini na nchini kwa ujumla unaweza kuzorota kutokana na wao kushindwa kuleta mashine mpya .

Amesema kuwa kiwanda hicho wawekezaji wapo 12 akiwemo halmashauri ya jiji la Arusha ,ambao uwekezaji wake ulitokana na Ardhi na kuridhiwa na baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Arusha wakati huo kwenye miaka ya 1990 ambacho kiwanda hicho kimejengwa ndani ya ardhi hiyo.

Ameeleza kwamba hapo awali kiwanda hicho kimekuwa kikifanyakazi na kiwanda cha Nyama cha Arusha Meat ambacho kwa sasa kinamilikiwa na halmashauri ya jiji la Arusha kwani hapo awali manispaa ilikuwa mbia kwa asilimia 49 wa kiwanda hicho ikiwa na asilimia 51

Amesema hatua ya mgogoro huo imesababisha kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji pamoja mabenki kukataa kuwapatia mkopo , hivyo ameiomba serikali kuingilia kati ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Mkurugenzi wake Dkt Maulidi Madeni kwa nyakati tofauti amekuwa akidai kuwa kiwanda hicho ni Mali ya halmashauri hiyo na kwamba wanaojiita wamiliki wanania ya kutaka kukitaifisha .

Dkt,Madeni amedai kuwa kwa muda mrefu amekuwa akimwita ofisini kwake mwenyekiti wa bodi ya Happy Sausage, Andrew George lakini ameshindwa kufika jambo ambalo ,George amedai si kweli kwa kuwa hakuwahi kuitwa na mkurugenzi huyo kwa mfumo rasmi wa kiofisi.

JUMLA YA MASHAURI 14 YAFUNGULIWA NA KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT’

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama
Jumla ya Mashauri 14 yamefunguliwa na kusikilizwa na Mahakama inayotembea ‘mobile court’ mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya amesema kuwa mashauri hayo yamefunguliwa na kutolewa maamuzi katika kipindi cha mwezi Julai, 2019.

Mhe. Nkya alieleza kuwa Mahakama hiyo inayotembea inaendelea kutoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza huku Mahakama nyingine inayotembea iliyopo jijini Dar es Salaam inaendelea kutoa elimu kwa Wadau juu ya uendeshaji wa Mahakama hiyo. 

Kwa mkoa wa Mwanza, Mahakama hiyo inafanya kazi katika maeneo ya Igoma, Buswelu na Buhongwa na kwa upande wa Dar es Salaam Mahakama hiyo inatoa huduma katika maeneo ya Bunju ‘ A’, Kibamba, Buza na Chanika.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mahakama inayotembea inasikiliza mashauri yote yanayosikilizwa na Mahakama za Mwanzo kama vile migogoro ya ndoa, madai, mirathi na jinai, pamoja na rufaa kutoka Mabaraza ya kata, yakiwemo mashauri yanayojitokeza katika operesheni maalmu zinazofanywa na taasisi/vyombo mbalimbali vya serikali.

Huduma nyingine zitolewazo na Mahakama hiyo ni kutoa taarifa za mashauri, kutoa fomu za viapo na kuthibitisha nyaraka mbalimbali, kufanya usuluhishi kwa wadawa na kutoa elimu kuhusiana na masuala ya Mahakama.

Mnamo Februari 06, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizindua rasmi Mahakama inayotembea lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa wananchi na kutoa haki kwa wakati.

Aidha; lengo jingine ni kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma za Mahakama mbali na maeneo wanayoishi.

Mahakama ya Tanzania ina mpango wa kutanua wigo wa utoaji huduma hii kwa kuanzisha vituo vingine katika mikoa iliyosalia kwa awamu tofauti.
Mhe Hakimu (aliyeketi mbele) akisikiliza kesi ndani ya Mahakama inayotembea 'Mobile Court' mkoani Mwanza.
Gari likiwa eneo linapopaki Buhongwa-Mwanza mnamo Agosti 22, 2019.
Wananchi wakisubiri huduma eneo la Buhongwa- Mwanza linapopaki gari.

MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI JULIUS NYERERE KATIKA MAPOROMOKO YA MTO RUFIJI UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI ULIASISIWA NA BABA WA TAIFA MWAKA 1975

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka za Waasisi wa Taifa zilizotunzwa katika maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uhifadhi mzuri wa nyaraka alipotembelea maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia baadhi ya watafiti wakipata huduma ya taarifa zitakazowawezesha kukamilisha tafiti zao. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.IMG_5001 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka muhimu zinazotunzwa na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo jijini Dar es Salaam

……………………….. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project ambao uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada kufanya ziara ya kikazi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kujionea kitabu cha Tanzania News Review cha mwaka 1977 kinachoainisha kuwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ndiye Muasisi wa mradi huo. 

Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa taifa yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere. 

“Hakika ule usemi wa zidumu fikra za Mwalimu Nyerere umetekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa mradi huu,” amefafanua Dkt. Mwanjelwa. 

Aidha, Dkt Mwanjelwa ameitaka Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuwa na utaratibu mzuri wa kuuhabarisha umma juu ya taarifa muhimu za kihistoria ambazo si za siri ili watanzania wajue maamuzi mbalimbali ya kizalendo yaliyofanywa na viongozi wao kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa. 

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amemhakikishia Dkt. Mwanjelwa kuwa Idara yake itaendelea kutunza vizuri na kwa uadilifu mkubwa nyaraka muhimu za nchi za kabla na baada ya uhuru kwani nyaraka hizo ni rejea muhimu katika utendaji kazi wa Serikali. 

Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022 na utakuwa ukifua megawati 2,115 kwa siku.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ZANZIBAR

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, wakatiu wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti kwa mwezi Julai 20 hadi Juni 2019 na Mpango Kazi Mpya kwa mwaka 2019 -2020, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
KAIMU Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019 na mpango kazi kwa mwaka 2019 -2020, wa Wizara hiyo, wakati wa mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kushoto Mshauri wa Rais Pemba Mhe.Dk. Maua Abeid Daftari na na kulia Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.
KATIBU Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Yakout Hassan Yakout, akisoma Utekelezaji wa Bajeti  na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi 2019, na kuwasilisha mpango kazi wa mwaka 2019-2020, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

WATENDAJI wa Idara za Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019 na Mpango kazi kwa mwaka 2019 hadi 2020, mkutano huo umefanyika ukumbi Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)   

TMA YAASWA KUTOA TAARIFA ZA TAHADHALI KWA MAPEMA

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifungua  mkutano wa 53 wa utabiri wa msimu wa vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Hayat Regency jijini Dar es salaam leo.
Meza Kuu
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) nchini, kutoa taarifa na tahadhari za mapema za hali ya hewa kwa vile ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu ya kijamii na uchumi katika nchi zetu na ukanda wote Wa pembe ya Afrika

Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasikiano Mhandisi Izack Kamwelwe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam alipofungua mkutano wa 53 wa utoaji wa utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika.

Mhandisi Kamwelwe amesema ni vema utabiri ukatolewa kwa wakati sababu nchi nyingi za ukanda huo ikiwemo Tanzania zinategemea sana hali ya hewa.

"Sekta Kama vile kilimo na usalama wa chakula, maji, Nishati, Afya, Mifugo, uvuvi na shughuli nyinginezo zinazofanyika baharini, usafirishaji na utalii na nyingine nyingi hutegemea sana hali hewa hivyo mabadiliko ya hali hewa yanayoambatana na vipindi virefu vya ukame na mvua yanaendelea kuufanya utabiri kuwa Wa umuhimu sana..

Aidha, Kamwele ameshauri kutumia pia njia za asili za kutabiri hali ya hewa kuliko kuachana nazo kabisa huku akisisitiza kwamba njia hizo zinaweza kuboreshwa.

"Hata wakati wa kubadili sheria kutoka kwenye Agency kwenda kwenye Authority tulipata ushauri kwamba hata kakakuona tunaweza kumtumia kuandaa utabiri," alisisitiza Waziri Kamwelwe.

Waziri huyo aliwataka washiriki 200 wa mkutano huo watatoka na maazimio yatakayochangia upatikanaji wa taarifa sahihi zaidi za hali ya hewa ili kuwasaidia watumiaji wa taarifa hizo kwenye shughuli zao za maendeleo kwa nchi shiriki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema wataalam hao pamoja na kujadiliana na kukubaliana na kufikia muafaka Wa pamoja juu ya utabiri wa hali ya hewa wa msimu ujao wa mvua za vuli Oktoba hadi Desemba watatoka na utabiri wa nchi wanachama kwa maendeleo ya nchi zao.

"Hii ni mikutano inayofanya mara kwa mara kabla ya kuandaa taarifa ya msimu kwenye nchi zetu huwa tunakutana na kutoa utabiri wa ukanda wetu huu na mwaka huu kauli mbiu yake ni utoaji wa tahadhari kwa hatua za haraka katika kukabiliana na athari za hali mbaya ya hewa.

"...Naamini mkutano huu utakuwa na matokeo chanya hivyo basi watumiaji wa taarifa zetu waendelee kusubiri," alisema Dk. Kijazi huku akifurahia Tanzania kupewa heshma ya kuandaa mkutano huo muhimu Afrika.

Amesema ingawa kuna changamoto kubwa upungufu wa hali ya hewa, Tanzania imejenga miuondombinu ya hali ya hewa ikiwemo kujenga rada na tayari mpaka sasa kina rada mbili na Tatu ziko katika hatua ya manunuzi ambapo mpango wa TMA ni kuwa na rada saba.

Akizungumzia mvua zinazoendele kunyesha, dk. Kijazi amesema kuwa zipo nje ya msimu huku akibainisha kwamba ni mabadiliko yanayosababisha kupungua kwa mkandamizo wa hewa baharini jambo linalosababisha unyevu kwenye anga.

"Sio mvua kubwa na hazitachukua muda mrefu, hizi zipo hasa ukanda wa Pwani na mikoa inayozunguka Ziwa Victoria... Wananchi wasihofu," alisema Dk. Kijazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TMA, Burhani Nyanzi alisema mkutano huo unalenga kuwasaidia watu wote wanaofanya shughuli zao wakitegemea hali ya hewa.

Kongamano hilo linahusisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi mbali mbali zikiwemo, Tanzania, Ethiopia, Sudan, Sudan ya kusini Burundi, Djibouti, Elitrea, Kenya, Somalia, Uganda nw Rwanda.

MAHAKAMA KUU imetupilia mbali mapingamizi ya awali La serikali

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam,  imetupilia mbali mapingamizi ya awali la serikali na Septemba 2, 2019 itaanza kusikiliza rasmi maombi  ya msingi ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki,Tundu Lissu, ya kuomba kibali cha kufungua shauri kupinga kukoma kwa ubunge wake.

Mapema, upande wa serikali uliwasilisha hoja tisa za pingamizi za kutaka maombi hayo yasisikilizwe kwa sababu yanamapungufu kisheria na kuiomba mahakama iyatupilie mbali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Jaji Sirillius Matupa kusoma uamuzi na kukubaliana na majibu ya hoja zilizotolewa na jopo la mawakili wa Lissu, linaloongozwa na wakili Peter Kibatala na kutupilia mbali mapingamizi hayo.

Jaji Matupa amesoma uamuzi huo baada ya kupitia na kuchambua hoja za Serikali za pingamizi hilo alilolisikiliza Ijumaa iliyopita na majibu na mawakili wa Tundu Lissu, dhidi pingamiizi hilo.

Lissu amefungua maombi Mahakama Kuu, Masijala Kuu, Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute  Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.

Katika maombi hayo dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu anaomba kibali cha kufungau shauri la maombi maalum kwa lengo la kupata amri mbalimbali kuhusiana na uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa juzi Ijumaa Agosti 23, 2019, lakini yalikwama baada ya Serikali kupitia kwa AG, waliwasilisha pingamizi la awali akiiomba mahakama iyatupilie mbali maombi hayo bila hata kuyasikiliza.

Katika pingamizi hilo la awali, Serikali iliwasilisha jumla ya hoja tisa, ikipinga kusikilizwa kwa maombi hayo kwa madai kuwa yana kasoro za kisheria. Katika uamuzi wake le Jaji Matupa ametupilia mbali pingamizi la awali la Serikali isipokuwa hoja moja tu ya kasoro katika viapo vinavyounga mkono maombi ya Lissu.

Kutokana na kasoro hizo Jaji Matupa amesema inapotokea kuwa kuna aya zenye kasoro za kisheria namna pekee ni kuziondoa aya hizo katika kiapo hicho na kuangalia kama aya zinazobaki zinaweza kusimama na kuthibitisha maombi.

Hivyo hoja zote za pingamizi la Serikali zimekataliwa isipokuwa hizo zenye upungufu kwenye hati za viapo. Ukiachilia mbali kasoro hizo za viapo, mambo mengine yote yataasikilizwa wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.”

Jaji Matupa amesisitiza kuwa pingamizi haliweza kuondoa haki za msingi kuwasikiliza wadaa kama kuna hoja za msingi za kusikilizwa.
Kuhusu hoja ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki,  Faraji Mtaturu, Jaji Matupa amesema kuwa sasa ni mapema mno kulitolea uamuzi na kwamba atalisikiliza ombi hilo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.

Juni 28, 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge Spika Job Ndugai alitangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA ASEMA HANA NIA YA KUGOMBEA URAIS ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kiongozi wa Banki ya NMB Vicky P. Bishubo alipotembelea maonesho kuangalia bidhaa za mbali mbali katika kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agost 26, 2019.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni wa Kituruki waliohudhuria katika maonesho ya kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agost 26, 2019.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Mabati kwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mtende Mndo Yusuf Abeid Haji kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa Tawi CCM Mtende Mndo yenye Jumla ya Shilingi Milioni Tano na Laki wakati wa kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agost 26, 2019.


Wazee wa Kijiji cha Kizimkazi wakishiriki kwenye Ngoma ya Kijadi maarufu kama Shomoo wakati wa kilele cha Sherehe ya siku ya Wakizimkazi inayofanyika kila Mwaka katika kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja leo Agost 26, 2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KESI YA TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE ,MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR YAKATAA MAPINGAMIZI YA SERIKALI

$
0
0


Na Karama Kenyuko,Michuzi TV

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya awali ya Serikali huku akieleza kwamba Septemba 2,mwaka huu wa 2019 itaanza kusikiliza rasmi maombi ya msingi ya Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu, ya kuomba kibali cha kufungua shauri kupinga kukoma kwa ubunge wake.

Mapema, upande wa Serikali uliwasilisha hoja tisa za pingamizi za kutaka maombi hayo yasisikilizwe kwa sababu yanaupungufu kisheria na kuiomba Mahakama iyatupilie mbali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Jaji Sirillius Matupa kusoma uamuzi na kukubaliana na majibu ya hoja zilizotolewa na jopo la mawakili wa Lissu, linaloongozwa na Wakili Peter Kibatala na kutupilia mbali mapingamizi hayo.

Jaji Matupa amesoma uamuzi huo baada ya kupitia na kuchambua hoja za Serikali za pingamizi hilo alilolisikiliza Ijumaa iliyopita na majibu ya mawakili wa Tundu Lissu, dhidi pingamiizi hilo.

Lissu amefungua maombi Mahakama Kuu, Masijala Kuu, Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.

Katika maombi hayo dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu anaomba kibali cha kufungau shauri la maombi maalum kwa lengo la kupata amri mbalimbali kuhusu uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa Agosti 23, 2019, lakini yalikwama baada ya Serikali kupitia kwa AG, waliwasilisha pingamizi la awali akiiomba Mahakama iyatupilie mbali maombi hayo bila hata kuyasikiliza.

Katika pingamizi hilo la awali, Serikali iliwasilisha jumla ya hoja tisa, ikipinga kusikilizwa kwa maombi hayo kwa madai kuwa yana kasoro za kisheria. Katika uamuzi wake le Jaji Matupa ametupilia mbali pingamizi la awali la Serikali isipokuwa hoja moja tu ya kasoro katika viapo vinavyounga mkono maombi ya Lissu.

Kutokana na kasoro hizo Jaji Matupa amesema inapotokea kuwa kuna aya zenye kasoro za kisheria namna pekee ni kuziondoa aya hizo katika kiapo hicho na kuangalia kama aya zinazobaki zinaweza kusimama na kuthibitisha maombi.

Hivyo hoja zote za pingamizi la Serikali zimekataliwa isipokuwa hizo zenye upungufu kwenye hati za viapo. Ukiachilia mbali kasoro hizo za viapo, mambo mengine yote yataasikilizwa wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.”

Jaji Matupa amesisitiza kuwa pingamizi haliweza kuondoa haki za msingi kuwasikiliza wadaa kama kuna hoja za msingi za kusikilizwa.

Kuhusu hoja ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki, Faraji Mtaturu, Jaji Matupa amesema kuwa sasa ni mapema mno kulitolea uamuzi na kwamba atalisikiliza ombi hilo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.

Juni 28, mwaka 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge Spika Job Ndugai alitangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NCHINI JAPAN

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, ambako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, ambako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya maofisa wa serikali ya Tanzania wakati alipowasili kwenye hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan Agosti 26, 2019, amabako anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa TICAD 7 na kufanya ziara ya kikazi nchini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images