Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

JUMUIYA YA WAZAZI CCM KAHAMA YATOA TAMKO KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUWA MWENYEKITI WA SADC

$
0
0
Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi Agosti 24,2019 wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama. 

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba, na Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange. 

Akisoma tamko hilo,Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Kahama,Disco Wabare amesema kuchaguliwa kwa rais Magufuli kuongoza SADC inaonesha dhahiri imani waliyonayo viongozi wa SADC kutokana na umahiri na utendaji kazi wake kwa wananchi wa Tanzania na Jumuiya ya SADC. 

"Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa baraza la Wazazi la wilaya ya Kahama kwa pamoja tunatoa tamko la kumpongeza Rais wetu mpendwa,mwenyekiti wa CCM taifa,Amiri Jeshi Mkuu na mtetea wanyonge, Mhe. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa SADC",amesema. 

"Sisi kama Baraza la Wazazi Kahama tunategemea kuona mabadiliko makubwa katika uongozi wake hasa katika kukuza uchumi wa nchi za SADC na kuondoa tatizo la ajira ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana wa nchi hizo",ameongeza Wabare. 

Amebainisha kuwa Baraza la wazazi Kahama linaamini kuwa kwa kasi aliyonayo Magufuli katika kuendeleza nchi ya Tanzania kimaendeleo,ataitumia pia katika kuendeleza umoja wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja aliochaguliwa kuongoza SADC. 

Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba alisema pamoja na kumpongeza rais Magufuli ni vyema WanaCCM na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii. 

Simba ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo mkoani Shinyanga zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura litaanza Agosti 26,2019 hadi Septemba 1,2019. 

"Tusiishie kujiandikisha tu bali wakati wa uchaguzi ukifika,naomba tukapige kura,ili kuipa ushindi mnono zaidi naomba wanaCCM wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Kila mwanaCCM ajitahidi kuwa na marafiki, wawashiwi wapenzi wa CCM wajitokeze kupiga kura.Tukumbuke kuweka wagombea wanaokubalika kwa kwa wananchi",ameongeza Simba. 

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa uchaguzi mkuu ujao 2020,ili tushinde kwenye chaguzi hizi,ni lazima tushikamane,tuwe na umoja kwani Umoja ni Ushindi.Naomba wingu la makundi liyeyuke,tushikamane,fitna kwetu ni mwiko",amesema Simba. 

Baraza hilo pia limepokea wanachama wapya kutoka vyama vya Upinzani akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) ambaye ameahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama leo Jumamosi Agosti 24,2019 .Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akisoma tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akimkabidhi wenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akionesha tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akiwasisitiza wanaCCM kushikamana na kuachana na makundi ndani ya chama. Simba pia aliwataka Makatibu wa CCM kuwapokea wanachama wapya wanaohitaji kujiunga CCM bila kujali kama wametoka vyama vya upinzani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza katika kikao hicho.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akiwahamasisha wanaCCM kukijenga chama na kukitetea.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akizungumza katika kikao hicho.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange akisisitiza kuwa CCM itaendelea kupokea wanachama wapya wanaotaka kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Sipilaus Bijampola akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka wilaya ya Kahama Machimu Mshono Ndalo akiwashukuru wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama kumchagua kuchukua nafasi hiyo licha ya kwamba hakuwepo wakati wa uchaguzi huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM mkoa wa Shinyanga kutoka wilaya ya Kahama, Greyson Tito Obata Okuku akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akimhamasisha diwani wa kata ya Mwakata,Ibrahim Six kuendelea kufanya kazi ya kuimarisha CCM
Wajumbe wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama wakiwa ukumbini.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM wilaya ya Kahama na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Wigehe, Marco Luswaga Shija akielezea mikakati mbalimbali ya uchaguzi. Shija aliwataka wanaCCM kuweka wagombea wanaokubalika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) akikabidhi kadi ya CHADEMA na kujiunga CCM leo huku akiahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) aliyejiunga CCM leo akielezea sababu za kujiunga CCM "Nimerudi CCM kwa sababu sasa kumenoga".
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAPELEKA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI ZANZIBAR

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna kila sababu ya kuendelea kutolewa elimu ya usalama barabarani na matumizi sahihi ya barabara zetu ili kupunguza ajali zinazosababisha ulemavu na vifo kwa watu wasio na hatia nchini.

Pia amesema kwa sasa Wizara hiyo ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea ukali sheria hizo ili kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto na hasa bodaboda ambao wengi wao wamekuwa wakivunja sheria mara kwa mara na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Mhandisi Masauni ameyasema hayo wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi na shule za msingi ambazo zimeshinda michoro yenye ujumbe wa usalama barabarani visiwani humo kwa mwaka 2019, ambapo Shule ya Msingi Mkunazini imepata kitita cha Sh.milioni nne kutoka kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.

Mafunzo hayo ya elimu ya usalama barabarani yamefadhiliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania ndio mara ya kwanza kutolewa visiwani humo.

"Kuna umuhimu mkubwa wa jamii yetu ya Watanzania kwa upande wa Bara na Visiwani kuendelea kupatiwa elimu inayohusu uslama barabarani pamoja na matumizi sahihi ya barabara zetu.


"Hivyo nitumie nafasi hii kuipongeza Kampuni ya Puma Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa elimu hii ambapo kwa hapa Zanzibar shule tano za msingi zimepata elimu hiyo na tunaamini itasaidia kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika,"amesema Mhandisi Masauni.

Ameongeza kuwa kutolewa kwa elimu ya usalama barabarani kwa wafunzi kutasaidia kuokoa maisha yao na kuwapusha na ajali kwani watakuwa na uelewa mzuri wa kutumia barabara zetu.

Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mikakati ya Serikali katika kuendelea kukabiliana na ajali za barabarani nchini na moja ya mkakati ni pamoja na kusimamia sheria zilizopo na kuongeza wanaendelea na mchakato wa kupitia upya sheria za usalama barabarani ili ziwe kali zaidi.

"Ajali za barabarani zimeendelea kupungua siku hadi siku, lakini bado kunachangamoto ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto na hasa waendesha bodaboda wanavunja sana sheria za barabarani.

"Tumeamua atakeyakamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani awekwe mahabusu na kisha apelekwe mahakamani ili sheria ichukua nafasi yake.Wanavunja sheria kwa kuamini sheria sio kali sana, sasa tumeamua na tutawadhibiti ipasavyo kwa watakaoendelea kutoheshimu sheria zilizopo,"amesema.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Ltd Dominic Dhanan amesema kuwa elimu ya usalama barabarani imetolewa kwa shule tano za msingi za Zanzibar.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la michoro ya Usalama barabarani kwa mwaka 2019 kisiwani Zanzibar. 

"Tukio hili la utoaji zawadi linahitismisha prgramu iliofanywa na kampuni ya Puma kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la AMEND kupitia New vision Consortium trainers ya Zanzibar wa kutoa elimu ya usalama barabarani,"amesema.

Amefafanua programu hiyo ilihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani katika shule za Msingi Mwembeshauri, Kisiwandui, Shule ya Msingi Jang’ombe, Shule ya Msingi Nyerere na Shule ya Msingi Mkunazini.

"Wanafunzi wasiopungua 6500 wamapeta elimu hiyo ambayo imekwenda sambamba na uchoraji wa michoro inayohamasisha matumizi sahihi ya barabarani na kufuata sheria zilizopo,"amesema.

Ameongeza programu hiyo ya usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa na jumla ya wanafunzi 106,500 wamepata mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Ruvuma, Dodoma na sasa visiwani Zanzibar. 

Ametumia nafasi hiyo kueleza Kampuni ya Puma ya Tanzania imeamua kufika visiwani Zanzibar kwa sababu ya ukuaji wa shughuli za utalii na za kiajamii ambazo zimesababisha ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shule na kurudi nyumbani. 

"Lengo kubwa la mpango huu ni kuwafanya watoto hawa kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara wakiwa bado wadogo.Kwa kufanya hivyo tunawaongezea uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa waTanzania wengi zaidi,"amesema Dhanah.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mkunazini ambaye ameibuka ushindi wa kwanza kwa mwaka 2019 kwa kuchora mchoro bora wenye ujumbe wa usalama barabarani Raya Zuberi Hemed ambaye amejinyakulia Sh.500,000 ameishuku kampuni ya Puma kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi atakuwa balozi wa kueleza matumizi sahihi ya alama za barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma, Dominic Dhanah (watatu kushoto) na Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah (watatu kulia) wakikabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni Nne kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mkunazini baada ya mwanafunzi Raya Zubeir Hemed(kulia), kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani kwenye hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimpa zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini, Saidat Jumbe zawadi baada ya kujibu swali lililohusiana na Kanuni za Uvukaji wa Barabara ili kuepuka ajali.Hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi kikombe mshindi wa kwanza wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani mwanafunzi wa Shuke ya Msingi Mkunazini Rayah Zubeir Hemed.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili Salum Ali Khatib baada ya kushika nafasi hiyo katika Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani lililodhaminiwa na kampuni hiyo.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwandui,Salma Ali Seif baada ya kujibu swali lililohusiana na usalama barabarani, wakati wa Hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PROGRAMU YA MAFUNZO YA UJASIRIMALI NA USIMAMIZI WA BIASHARA KUWANUFAISHA VIJANA MKOANI GEITA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na vijana wa Mkoa wa Geita alipokuwa akizindua Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa vijana inayoratibiwa na kusimamiwa na ofisi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamim Gwiyama akitoa taarifa fupi kuhusu fursa zilizopo katika Mkoa wa Geita zinazoweza kuwanufaisha vijana wa mkoa huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akielezea kuhusu Programu hiyo ya ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Geita ambapo vijana 150 walihudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sehemu ya Vijana Wajasiriamali wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkoani Geita.
Baadhi ya vijana wajasiriamali wakimsikilza kwa makini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizindua awamu ya tatu ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa Geita.
Sehemu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Geita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akigawa cheti cha Ushiriki kwa mmoja wa vijana aliyeshiriki katika mafunzo hayo Bw. Daniel Ntigizu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana alipokuwa akizindua awamu ya tatu ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa Geita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawezeshaji wa Mafunzo ya Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamim Gwiyama mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo na Usimamizi wa Biashara kwa vijana wa Mkoa wa Geita. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Deogratius Kayango.

…………………………………………………..

Na; Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imedhamiria kuwawezesha vijana kupitia programu ya mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamaizi wa Biashara kwa lengo la kuwawezesha kukuza na kurasimisha biashara zao.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya mafunzo hayo katika Mkoa wa Geita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa mafunzo hayo ni mahususi kwa vijana na yatawawezesha vijana kupata elimu juu ya masuala mbalimbali ya ujasiriamali na biashara ikiwemo urasimishaji wa biashara, kutambua ushindani, upatikanaji wa mitaji, masuala ya uchambuzi wa masoko, mikakati na uendeshaji wa biashara.

“Mafunzo haya yanamanufaa sana kwenu ninyi vijana kwa kuwa yatawawezesha kukua kwa kasi katika biashara zenu mnazoziendesha na hivyo kuwajengea wigo mpana wa kuendeleza shughuli za kiuchumi mnazozifanya,” alisema Mhagama

Alifafanua kuwa Ujasirimali ni moja ya nguzo za sera ya taifa ya uwezeshaji ambayo inalenga kuinua viwango vya ujuzi na uzoefu wa masuala ya biashara nchini.

Alieleza kuwa, kupitia programu hiyo vijana 4,000 watanufaika na Mafunzo hayo ambayo yatawajengea uwezo vijana nchini kuwa na uelewa juu ya masuala ya biashara ikionesha utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli katika kuwawezesha vijana.

“Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuwajengea uwezo vijana kote nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kujiajiri, kuajiri wenzao kwa ujumla pamoja,” alisisitiza Mhagama

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali katika kuwawezesha vijana inatekelezwa kwa vitendo kupitia programu mbalimbali ikiwemo ya ukuzaji ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, mmoja wapo ikiwemo ya Mafunzo ya Ujasirimali kwa vijana.

Sambamba na hayo, Mhe. Mhagama aliwasihi vijana walioshiriki mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kuwa ni chachu ya mageuzi katika kuboresha biashara zao. Pia aliwataka vijana hao kueneza ujuzi waliopata kupitia mafunzo hayo kwa vijana wenzao.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa maagizo kwa viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha vijana wanashiriki kwa wingi katoka mafunzo hayo kwa kuwa yataleta matokeo chanya kwa jamii na yatakuwa ni chachu kwa vijana katika kujiletea maendeleo sambamba na kuwawezesha kuchangia pato la Taifa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamim Gwiyama ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana maana wao ndio nguvu kazi ya taifa, hivyo kijana akiwa na ujuzi wa mambo mbalimbali ya biashara ni faida kwake kutambua njia bora za kukuza shughuli zao za uzalishaji mali.

“Katika Mkoa wa Geita vijana walikuwa na mawazo kuwa dhahabu ndio biashara pekee itakayowapa faida, ila kupitia mafunzo haya wataweza kutambua kuwa biashara yoyote wakisimamia vizuri itakuwa na manufaa kwao,” alisema Gwiyama

Naye, Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Mafunzo hayo Bw. Salim Hassan aliweza kutoa shukrani zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yameweza kuwatoa katika sehemu moja na kuwapeleka hatua nyingine.

“Leo tumepata stadi za msingi katika masuala ya ujasirimali na biashara, tumeweza kuelewa umuhimu wa kutunza kumbukumbu, usimamizi wa fedha, taratibu za kurasimisha biashara na jinsi ya kutafuta masoko,” alisema Hassan

Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Jijini Dodoma Julai 29, 2019. Mafunzo hayo yanasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika Mikoa nane (8) ya Tanzania Bara ikiwemo Dodoma, Ruvuma, Geita, Mwanza, Lindi, Mbeya, Arusha na Tanga. Tayari vijana kutoka Mkoa wa Dodoma na Ruvuma wamekishwa nufaika na mafunzo hayo.

NAIBU WAZIRI ULEGA ASEMA UVUVI HARAMU UMEPUNGUA NCHINI.

$
0
0
UVUVI haramu wa kutumia mabomu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na takwimu kuonesha ndani ya mwaka wa 2019 hakuna tukio lolote lililojitokeza la uvuvi wa kutumia mabomu.

Hayo yamesemwa  leo na  Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo  Abdallah Ulega baada ya kutembelea Mnada wa uuzaji Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mnada huo  Waziri Ulega amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali na wavuvi ndo chanzo cha kutokomeza uvuvi wa kutumia mabomu hapa nchini.

"Hakuna mlipuko wa mabomu kwasasa hivyo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kuna watu wamebaki vilema kwaajili ya hayo mabomu, ninyi mnatakiwa mtuunge mkono kuhakikisha msirudi nyuma, serikali ya awamu ya tano ipo kwaajili ya kushirikiana na wananchi wake". Amesema Waziri .Ulega.

Pamoja na hayo  Ulega amewataka wavuvi kuwa kila mtu kuwa mlinzi wa mwingine ili kuhakikisha kila mmoja anafuata utaratibu na sheria zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu.

Aidha,  Ulega amesema kuwa suala la wavuvi kutumia nyavu za kisasa maarufu kama Ringnet wakati wa mchana amesema serikali italifanyia kazi katika kipindi hiki ambacho wanafanya uboreshaji wa kanuni  za uvuvi

Amesema lengo ni kuboresha mazingira katika sekta ya uvuvi na kuhakikisha mazingira ya bahari yanahifadhiwa pamoja na kutoathiri upatikanaji wa dagaa ambao ni biashara kubwa kwa wavuvi hao  na wakina mama ambao hufika hapo na kununua kwenda kuuza na kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao.

kuhusu leseni,  Ulega amewatoa wasiwasi kwamba mvuvi hapaswi kuwa na leseni zaidi ya moja na kwamba mvuvi anapokuwa na leseni moja inamtosha kuendesha shughuli  za uvuvi mahali popote

"Leseni ya uvuvi ni moja ukikata Mkuranga utatamba nayo mpaka Mtwara, ukikata Mtwara utatamba nayo mpaka Lindi mpaka Tanga".Amesema Ulega.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Daniel Chongolo amewaahidi wavuvi wa eneo hilo kushughulikia suala la ujenzi wa choo ambao utakamilika kufikia mwezi Disemba mwaka huu utakua umemalizika ujenzi huo.
Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi  waliofika katika eneo la mnada wa Samaki Kunduchi wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaomba Wavuvi hao  kufanya kazi  bila kuwa na wasiwasi  kwa kufuata sheria  kanuni  na taratibu.

Wavuvi  pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega baada ya kutembelea mnada wa  Samaki Kunduchi wilaya ya Kinodoni  Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (kushoto) akizungumza wavuvi  pamoja na wachuuzi wa samaki katika eneo la mnada  wa samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kuboresha miundombinu mbalimbali katika mnada huo,Kulia ni Naibu Waziri wa Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega wa pili kulia ni Diwani wa kata ya Kunduchi,Michael Urio

  Diwani wa kata ya Kunduchi   wilaya ya Kinondini Jijini Dar es Salaam,Michael Urio akimshuru  Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega kwa kufika endeo la mnada wa samaki Kunduchi na kufanya mkutano wa kusikiliza kero za wavuvi.
 Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam waliofika katika eneo mnada wa wa Samaki Kunduchi leo.
 Mwenyekiti wa B.M.U Kunduchi wilaya ya Kinondoni jiji Dar es Slaam,Zedi Mwinyi wa kwanza kushoto akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega namana kazi zinavyo fanyika katika mnada wa kuuzia Samaki.
  Naibu Waziri wa Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwasili katika mnada wa kuuzia Samaki wa Kunduchi wilaya ya Kinondino jijini Dar es Salaam.

 Mkutano ukiendelea 

TANZANIA, BURUNDI WASAINI MAKUBALINAO KUWAREJESHA WAKIMBIZI 2000 NCHINI MWAO KILA WIKI,

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kuhsoto), na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Burundi, Pascal Barandagiye wakisaini maazimio ya makubaliano ya kuwarejesha wakimbizi 2000 kila wiki katika nchi yao ya asili. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi nchini, Sudi Mwakibasi, wakati walipokua wametembelea Kituo cha Shirika la Kuwahudumia Wahamiaji (IOM), kilichopo Makere, Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma. Lugola alisema Serikali Tanzania na Burundi imesaini hati ya makubalinao ya kuwarejesha wakimbizi 2000 kwa kila wiki nchini mwao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, Kigoma (MOHA). 

TANZANIA na Burundi wamesaini makubaliano ya kuwarejesha Wakimbizi 2000 kwa kila wiki nchini mwao kuanzia Oktoba Mosi, 2019. 

Wakimbizi hao waliopo katika Kambi ya Nduta na Mtendeli wanatarajiwa kusafirishwa kuelekea katika nchi yao ya asili kutokana na amani iliyopo katika nchi hiyo. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Burundi, Pascal Barandagiye tayari wamesaini makubaliano hayo ambayo watahakikisha wakimbizi wote waliopo katika kambi hizo wanartejeshwa nchini mwao bila kukwamishwa na mtu au shirika lolote. 

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Kigoma jana, Waziri Lugola alisema makubaliano hayo yataanza rasmi Oktoba mosi na wakimbizi hao watakuwa wanarejeshwa nchini mwao na kupata mapokezi makubwa na Serikali ya Burundi. 

“Tunataarifa wapo baadhi ya watu, mashirika ya kimataifa wanawarubani wakimbizi wakiowatangazia kuwa Burundi haina amani, jambo ambalo si la kweli, nchi hiyo ina amani na wakimbizi wanapaswa kurejea nchini mwao,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kuwa, atawachukulia hatua kwa watakaokwamisha zoezi hilo la kuwasafirisha wakimbizi hao, kwa kuwa Serikali ya Wakimbizi inataka watu wao na Tanzania imeamua kuwapa watu wao ili waende wakaijenge nchi. 

“Natoa kauli hii sio kuwatisha au kutishia nyau, bali nasema, Serikali ya Magufuli haiwezi kuchezewa na mtu yeyote, hivyo tutawakamata wanaowarubani, wanaowashawishi wakimbizi wasiende nchini mwao,” alisema Lugola. 

Wiki iliyopita, katika mkutano wa hadhara katika Kambi ya Nduta, baadhi ya Wakimbizi walisema wanawekewa vikwazo na kucheleweshwa na baadhi ya watendaji wa mashirika ya wakimbizi kambini humo wakati wanapoomba kujiandikisha kurejeshwa kwao. 

Mkimbizi wa kambi hiyo, Nzoisa Bhainoje, alisema yupo tayari kurejea nchini Burundi lakini amefanya juhudi za kwenda eneo la kujiandikisha kambini hapo lakini hakufanikiwa kutokana na kusumbuliwa akiambiwa kuwa idadi wanaotakiwa kuondoka imekamilika. 

“Nakumbuka nilifika eneo la kuondoka siku ya Jumanne lakini ilishindikana kujiandikisha kutokana na kukwamishwa, wengi tunataka kuondoka lakini tunashindwa kuondoka kwasababu tunakwamishwa,” alisema Bhainoje. 

Bhainoje aliongeza kuwa, wanaomba watendaji hao wawaruhusu kwa wale wanaotaka kurejea nchini mwao kwa hiari, lakini kwa wale ambao hawataki kuondoka wanaweza kubaki kwa mipango yao. 

Baada ya wakimbizi hao kutoa kero zao kwa Waziri Lugola na Waziri Barandagiye, ndipo Lugola aliagiza kufanyika uchunguzi katika kambi hiyo kuwakamata wale wote ambao wanakwamisha wakimbizi hao kurejea nchini kwao kwa hiari. 

“Naagiza uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kwa yeyote atakayehusika anakwamisha zoezi hili la kuwarejesha wakimbizi hawa ambao wapo tayari kuondoka nchini kwao kutokana na amani iliyopo, awe Afisa kutoka Wizarani, awe afisa wa shirika lolote, awe yupo hapa kambini, lazima tutamkamata na kumpeleka mahakamani,” alisema Lugola. 

Aliongeza kuwa, muda umefika kwa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini mwao, kwasababu zile sababu ambazo zilikuwa zinazuia zoezi la kuwarudisha kwao wakimbizi hao kwa sasa havipo tena kwasababu nchi hiyo ina amani. 

Alisema Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli imejiridhisha sababu kubwa iliyowaleta wakimbizi hao wa Burundi nchini ya kutowepo kwa amani haipo tena na kwamba kwa sasa Burundi ipo salama kiulinzi na kiusalama pia kisiasa hivyo wakimbizi hao wanapaswa kurudi nchi mwao wote bila kuwepo kikwazo chochote. 

"Wanaosema Burundi haina amani wanaipaka matope nchi hiyo kwani jambo hilo halina ukweli wowote na Tanzania imefanya uchunguzi wa kutosha na kujiridhisha kuwa amani ya kudumu ipo nchini humo, Oktoba Mosi tutaanza kutekeleza mkataba wa pande tatu wa kurudishwa kwa wakimbizi 2000 kila wiki wa Burundi kwenda nchini mwao," alisema Lugola. 

Naye Waziri Barandagiye, kwa upande wake alisema Burundi iko tayari kutekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu ya kuhakikisha wakimbizi wote wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye makambi mbalimbali ya wakimbizi mkoani nchini wanarudi Burundi lakini wanashangazwa na namna Shirika la Kuhudumia Wakimbizi linavyoendesha zoezi hilo kwa kasi ndogo. 

Waziri Lugola na Barandagiye walitembelea Kambi ya Nduta, Wiliyani Kibondo na Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko mkoani humo, kwa lengo la kuhamasisha wakimbizi katika kambi hizo kurejea nchini kwao kwa hiari. 


ASKOFU MAGWESELA AFUNGUA KANISA JIPYA LA AICT KAHAMA MJINI

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela amefungua rasmi nyumba mpya ya kuabudia (kanisa la jipya AICT Kahama Mjini) lililogharimu jumla ya shilingi milioni 900 (902,397,070/=).

Ufunguzi wa kanisa hilo bora na la kisasa lililopo Nyihogo Mjini Kahama umefanyika leo Jumapili Agosti 25,2019 na kuhudhuriwa na maelfu ya viongozi,waumini na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kuweka wakfu na kufungua jengo hilo jipya,Askofu Magwesela alisema ni jengo bora na la kisasa huku akiwasisitiza waumini na kutumia jengo hilo kumwabudu Mungu.

"Kwa heshima ya Mungu nalifungua na kuliweka wakfu jengo hili. Nyumba hii ni kwa ajili ya ibada pekee,naomba mlitumie kwa maksudi yaliyokusudiwa",amesema. 

Akisoma taarifa ya ujenzi,Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe amesema kanisa la AICT Kahama Mjini limeanzishwa tarehe 15 Novemba,1975 na mpaka sasa limefungua Pastoreti tisa mjini Kahama na Pastoreti mama ya Kahama,Mlima Sayuni,Mhongolo,Mhungula,Nyakato,Lugela,Majengo,Mbulu na Mwendakulima.

Amesema wamejenga jengo jipya kisasa la kuabudia lililotokana na michango ya waumini ambapo lina mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na ofisi sita,vyoo,sehemu ya kubatizia na maombi ya faragha,mabenchi,meza hivyo mpaka jengo linafunguliwa limegharimu jumla ya shilingi 902,397,070/=.

Amebainisha kuwa mbali na kujenga kanisa jipya pia wamejenga nyumba ya kisasa ya Mwinjilisti,madarasa mawili na ofisi zake,bwalo la kulia chakula na kanisa linaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi 'English Medium School',ujenzi wa shule ya sekondari na zahanati na ukamilishaji wa hosteli ya kanisa. 
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini leo Jumapili Agosti 25,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akiendesha ibada ya kufungua na kuweka wakfu jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Maaskofu wa kanisa la AICT wakiendelea na ibada ya ufunguzi na uwekaji wakfu jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini. Aliyeshikilia kipaza sauti ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota.
Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.
Muonekano wa jengo jipya la kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akikata utepe wakati wa kufungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua jengo jipya la kuabudia katika kanisa la AICT Kahama Mjini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akifungua mlango kuingia ndani ya jengo jipya la kuabudia/kanisa la AICT Kahama Mjini.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Katibu wa Kanisa la AICT Kahama Mjini,Charles Pambe akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 900.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini na kuwasisitiza waumini kutumia kanisa hilo kumwabudu Mungu pekee.


Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akizungumza wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.




Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, Zakayo Bugota akizungumza wakati wa ufunguzi wa kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.




Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Tabora, Silasi Kezakubi akiweka wakfu benchi katika kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.




Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT nchini,Musa Masanja Magwesela akizungumza baada ya kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.




Viongozi mbalimbali wa Kanisa la AICT wakiwa kanisani wakati wa kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini. Maaskofu wakiwa wamekaa jukwaa kuu wakati wa ibada ya Jumapili baada ya kufungua kanisa jipya la AICT Kahama Mjini.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

DKT MABULA AAGIZA KAYA 13 KUONDOKA ENEO LA WAFUGAJI TABORA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwasikiliza baadhi ya wafugaji na wakulima wanaoishi katika hifadhi ya Wembele iliyopo kijiji cha Makomelo wilaya ya Igunga mkoani Tabora alipokwenda kusuluhisha mgogoro baina yao wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi na kukagua masijala za ardhi katika mkoa wa Tabora jana
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafugaji na wakulima wanaoishi katika kijiji cha Makomelo wilaya ya Igunga mkoani Tabora alipokwenda kusuluhisha mgogoro baina yao wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi na kukagua masijala za ardhi katika mkoa wa Tabora jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo wakiwasili kijiji cha Makomelo wilaya ya Igunga mkoani Tabora alipokwenda kusuluhisha mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi na kukagua masijala za ardhi katika mkoa wa Tabora jana (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI)

…………………………………………………

Na Munir Shemweta, WANMM IGUNGA

Serikali imeagiza kaya 13 zilizopo eneo la wafugaji katika hifadhi ya Wembele kijiji cha Makomelo kitongoji cha Kitulo wilayani Igunga mkoani Tabora kuondoka katika eneo hilo kwenda eneo ililopangiwa la wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu kati ya wafugaji na wakulima.

Kauli hiyo ya serikali inafuatia wakulima kuvamia eneo la wafugaji katika kijiji hicho na kuzuia wafugaji kulisha mifugo yao jambo lililokiuka makubaliano ya awali ya kila upande kubaki katika eneo lake kwa ajili ya shughuli zake.

Akizungumza na pande mbili za wafugaji na wakulima katika kijiji cha Makomelo akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi na kukagua Masijala ya Ardhi katika mkoa wa Tabora jana tarehe 24 Agosti 2019, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema serikali haiwezi kuendelea kuona watu wanapigana na kuuana wakati mipaka ya eneo hilo ilishawekwa.

Alisema, eneo linalogombaniwa na pande hizo mbili linajulikana kama eneo la hifadhi ya Wembele chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii lakini kwa busara serikali iliamua kutoa matumizi kwa ajili ya wakulima na wafugaji na kuweka mipaka lakini wakulima wameamua kukiuka utaratibu na kuvamia eneo la wafugaji kitu alichokieleza kuwa hakikubaliki.

‘’Waliokiuka utaratibu wa awali waondoke, ziko kaya 13 hatuwezi kuendelea na vifo katika haya, serikali ishaweka mipaka kinachotakiwa ni kuheshimu maamuzi’’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kinachotakiwa kwa pande mbili zinazogombana ni kuheshimu makubaliano hadi hapo Wizara ya Maliasili na Utalii itakalichukua eneo lake.

Aliwataka wafugaji na wakulima wasiendelee kufanya vurugu na kuheshimu makubaliano waliyokubaliana awali ambapo alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora John Mwaipopo kuhakikisha anasimamia zoezi la kuondoka kwa kaya 13 katika eneo la wakulima.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kitulo katika Kata ya Igunga Zephania Ndassa alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, eneo hilo limekuwa na mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji pamoja na kuwepo makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2004 wakati wa uongozi wa Mkuu wa mkoa wa Tabora wakati huo Marehemu Abbas Kandoro.

Kwa mujibu wa Ndassa pande zinazopingana zinatambua kabisa kama eneo hilo ni hifadhi ya Wembele tangu mwaka 2002 na wao wanalitumia eneo hilo wakifahamu pindi litakapohitajika litachukuliwa na Maliasili lakini mgogoro huo umekuwa ukuwasumbua.

Naye Mkazi wa kijiji cha Makomelo Christopher Shigela alimuomba Dkt Mabula kunusuru mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu hasa baada ya juhudi za wilaya na mkoa kugonga mwamba na kubainisha kuwa, pamoja na uwepo alama zilizoainisha maeneo ya wakulima na wafugaji lakini wakulima wameendelea kufanya uvamizi jambo lililozusha mgogoro uliosababisha watu kuumia na wengine kupoteza maisha.

WAZIRI KAMWELWE AKAGUA ENEO LA MRADI UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MAFIA NYAMISATI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe katikati akikagua baadhi ya malighafi ambazo zimekwishawasili zitakazotumika katika ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati. Ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.3 za kitanzania na unatarajiwa kukamilika ifikaapo mwezi Februari mwaka 2020.






Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe katikati akisistiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, wafanyakazi wa kampuni ya Ms. Songoro Marine pamoja na TEMESA alipokuwa akifanya ukaguzi wa eneo la mradi wa ujenzi wa kivuko kipya ambacho kinatarajiwa kutoa huduma kati ya Nyamisati na Mafia. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Maselle na kulia ni Mbunge wa Mafia Mh. Mbaraka Dau.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Maselle akisoma taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati iliyowasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi Mh. Isack Kamwelwe wa pili kulia alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kivuko hicho utakaofanyika katika eneo la Kigamboni. Kulia ni Mbunge wa Mafia Mh. Mbaraka Dau.


Mbunge wa Mafia Mh. Mbaraka Dau aliyenyoosha mkono akimuonyesha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe katikati michoro itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha Mafia Nyamisati wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa eneo la mradi wa ujenzi huo ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 5.3 za kitanzania, kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Japhet Maselle. Zoezi hili limefanyika katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MRADI URAMBO VIPATIWE UMEME NDANI YA MIEZI SITA-DKT.KALEMANI

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji umeme katika Kijiji cha Mabundulu wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora. Wa Pili kushoto ni Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto), akitoa maelekezo wa wataalam wa TANESCO wanaosimamia ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo ambacho kinajengwa chini ya mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Kigoma.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mabundulu wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wakati alipofika kijijini hapo kuwasha umeme. Wengine ni viongozi mbalimbali kutoka wilayani Urambo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu) akikagua mradi wa umeme katika Kijiji cha Mabundulu wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wakati alipofika kijijini hapo kuwasha umeme. Wengine ni viongozi mbalimbali kutoka wilayani Urambo na wananchi.
………………..

Na Hafsa Omar, Tabora

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Meneja wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Tabora, kuwa vijiji vyote vinavyozunguka mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Urambo, vipatiwe umeme ndani ya miezi Sita.

Alisema hayo Agosti 24, 2019 wakati alipofanya ukaguzi kwenye mradi wa Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Urambo, Tabora hadi Kigoma na kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Uhuru kata ya Vumilia wilayani humo.

Akizugumza na wanachi wa kijiji hicho, Waziri Kalemani alisema “huwezi ukajenga kituo cha kupoza hapa, halafu vijiji vilivyozunguka hapa visiwe na umeme, kwahiyo vijiji vyote vinavyozunguka kituo hiki natoa miezi Sita viwe vimeunganishiwa umeme.”

Aidha, Dkt. Kalemani aliwapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa uvumilivu wao katika kipindi chote kwa kutopata umeme wa uhakika na kueleza kuwa “mmehangaika miaka mingi lakini, Serikali yenu ni sikivu ndiyo maana sasa inaleta umeme imara unaotabirika, na ninampongeza sana Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kutoa fedha za kutosha za kujenga mradi huu.”

Vilevile Dkt. Kalemani alisema kukamilika kwa mradi huo kutaokoa pesa nyingi zinazotumika kununua mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya umeme.Alitoa mfano kuwa, Mkoa wa Kigoma unatumia takribani shilingi bilioni 1.1 kwa mwezi kuendesha mitambo ya mafuta ambapo kwa mwaka inatumika bilioni 13.2 hivyo umeme wa gridi utaokoa fedha hizo.

Alieleza kuwa, mradi huo wa njia ya kusafirisha umeme unatekelezwa na TANESCO wenyewe na hawatatumia wakandarasi wa nje ya nchi.

Katika ziara hiyo, Dkt Kalemani aliwasha umeme katika kijiji cha Madundulu tarafa ya Usoke, wilayani Urambo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AENDA JAPAN KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 25, 2019 ameondoka nchini kwenda Japan kwa ziara ya kikazi ya siku saba. Pichani, Mhe. Majaliwa akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Avemaria Semakafu (wapili kushoto) kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Taasisi ya family Federation for world peace yaahidi kupunguza uhaba wa damu nchini

$
0
0
Baadhi ya wanachama wa federation wakichangia damu katika hospital ya taifa Muhimbili kitengo cha damu salama.
Mratibu wa taasisi ya family Federation Bw. Semeni Kingaru aliyefanikisha shughuli nzima ya uchangiaji damu 
Muuguzi  Mwandamizi katika Hospital ya  Taifa Muhimbili kitengo cha damu Judith Mayombo akizungumza jambo na baadhi Wadau waliojitokeza kujitolea damu 

*****************

Na Stahmil Mohamed

Taasisi ya family Federation for  World peace imeahidi kumaliza upungufu wa damu nchini kwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kila mwisho wa wiki ili kuokoa watu mbalimbali wenye uhitaji wa damu.

Akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa Taifa wa shirikisho hilo wakati wa uchangiaji damu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Bw Semeni Kingaru ambaye ni mratibu wa masuala mbalimbali ya taasisi hiyo amesema kuwa kutokana na uhaba wa damu uliopo nchini taasisi hiyo ambayo inawanachama zaidi ya elfu 80 wameanzisha utaratibu wa uchangiaji damu kila mwisho wa juma.

"Lengo hasa ni kupunguza changamoto hiyo pia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji Wa damu wakiwemo majeruhi wa ajali, wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungua hata watoto wenye uhitaji wa damu",alisema Kingaru

Imesema kutokana na hamasa waliyonayo wanachama wa taasisi hiyo katika suala la uchangiaji damu,wanaamini kuwa uhaba wa damu utapungua na watu mbalimbali wataweza kuokoa maisha kama ilivyo kauli mbiu yao ya 'ishi kwa ajili ya wengine' .

Wanachama wa family Federation Irene na Nasibu Mbarook  waliojitokeza kuchangia damu katika hospital ya Taifa ya Muhimbili ,wamesema kuwa wameamua kuchangia damu katika hospital hiyo Kwani wanajua uhaba wa damu uliopo katika hospital hiyo ya Taifa, Kwani kuna watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo majeruhi wa ajali.

Kwa upande wake Judith Mtayombo ambae ni Muuguzi mwandamizi katika kitengo cha damu Hospital ya Taifa Muhimbili amewaomba Watanzania kujijengea utaratibu wa kuchangia damu ili iweze kusaidia Wagonjwa mbalimbali waliopo wodini pia inapotokea majanga makubwa kusiwepo na changamoto ya upatikanaji wa damu.

WAZIRI WA NCHI HAJI OMAR KHERI AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA YA MAGHARIB A

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud (hawapo Pichani) walitembelea Eneo la kihinani  Wilaya ya Magharibi “A”zinapofanyika shughuli za kuanikwa Dagaa. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud aliyevaa (Shati jeupe) na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri wakiwa katika Ziara ya kutembelea eneo la Kihinani huko Wialaya ya Magharibi “A”.



****************

Na Mwashungi Tahir Maelezo 25-8-2019.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina dhamira nzuri kwa wananchi wake katika kujiendeleza maisha yao.

Ameyazungumza hayo wakati wa ziara ya Wilaya ya Magharib “A” alipokuwa akitembelea eneo la Kihinani la Ushirika wa maisha gemu akiangaliya shughuli za waaanika dagaa na kuwapongeza kwa kuendelea na shughuli zao.

Amesema Serikali haikusudii kumkandamiza mwananchi ila ina lengo la kumuwekea mwananchi mazingira mazuri katika kuendelea na harakati zake za kujitafutia rizki zake za kihalali .

“Serikali yetu ni Serikali inayowapenda wananchi wake wawe na amani katika ufanyaji wao wa kazi kwa kujiajiri wenyewe na kujipatia riziki zao za kihalali na kuendeleza maisha yenu”alisema Waziri Kheir.

Aidha amewapongeza kwa kufuata ushauri wa Serikali ya kuwaondosha katika eneo la Malindi na kuwaleta eneo la Kihinani kwa nia ya kuendeleza shughuli za biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Pia aliwataka wawe wastahamilivu baada ya kutoa changamoto zao ambazo zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi sehemu hiyo na kuwaahidi kuzitatua kwa awamu.

Kwa upande wake Katibu wa Ushirika wa maisha gemu kihinani Nasib Abdullah Khamis alisema changamoto zinazowakabili ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ikiwemo barabara na kutengenezewa daraja la kudumu.

Akitembelea Kituo cha Mbuzini aliwataka viongozi wa Wilaya ya Magharibi “A” kukaa kwa pamoja na kutafutia ufumbuzi kituo hicho ili kiweze kumalizika kabla ya uchaguzi 2020 ikiwa ni Agizo la Rais la kutaka Hospitali hiyo iwe ya Wilaya.

Hata hivyo aliuomba uongozi wa Wilaya hiyo kutowaruhusu wananchi kuvamia katika sehemu hiyo kwani eneo hilo linatarajiwa kuwa hospitali ya Wilaya.

Vile vile ziara hiyo katika Mkoa wa mjini Magharibi, Wilaya ya Magharib “A” iliendelea kwa kutembelea sehemu mbali mbali ikiwemo Skuli ya Sharifu Msa, kituo cha Afya Chuini, na cha Afya Mbuzini.

SIMBA YAKUBALI SARE NYUMBANI, YAONDOSHWA KLABU BINGWA AFRIKA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Klabu Bingwa Timu ya Simba imeondolewa katika mashindano baaada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya UD songo ya Msumbini.

Mabingwa wa ligi ya soka ya TPL, wameondolewa kwa goli la ugenini baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Msumbiji kutoka suluhuya kutokufungana.

Katika daika ya 14, Luiz Misquissone aliifungia UD Songo goli la kuongoza baada ya kupiga faulo nje kidogo ya eneo la hatari.

Simba walishindwa kutumia nafasi walizozipata kwenye kipindi cha kwanza baada ya safu ya ulinzi ya UD Songo kuwa makini na kuondosha hatari hiyo.

Mpaka timu zinaenda mapumziko, UD Songo walikuwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Simba.

Kipindi cha pili kilianza kila upande wakitafuta nafasi, Simba wakizidisha mashambulizi langoni mwa wapinzani wao ila umakini unakuwa mkubwa kutoka kwa walinzi wa timu hiyo na kuondoa mipira ya hatari langoni mwal.

Penalti ya dakika za lala salama iliopigwa na Erasto Nyoni haikutosha kuisaidia timu hiyo ya Msimbazi Reds huku Songo ikifuzu katika raundi ya pili kutokana na goli la ugenini.

Kocha wa Simba Simba Patrick Aussems amesema kuwa, wameumia baada ya kushindwa kwenda hatua inayofuata ila kwa sasa watajipanga zaidi katika Ligi Kuu ili wafanye vizuri na kuchukua ubingwa tena.

Kwenye mchezo huo Simba walifanya mabadiliko katika dakika ya 41 kwa kumtoa kiungo wa kati wa Kenya Francis kahata na kumuingiza Hassan Dilunga, Shiboub na kuingia Miraji Athumani na Beki Gadiel Michael na kuingia Mohamed Hussein.

Kwa sasa Tanzania itaendelea kuwakilishwa na Yanga waliofanikiwa kutinga hatua inayofuata ya michuanoya Klabu Bingwa baada ya kuifunga Township Rollers kwenye mchezo wa mkondo wa Pili nchini Botswana goli 1-0 ambapo latika mchezo wa mkondo wa kwanza walitoka na sare ya 1-1 Uliochezwa dimba la Uwanja wa Taifa.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho, Azam wamefanikiwa kutinga raundi ya pili baada ya kuitoa Fesal Kenam kwa jumla ya goli 3-2.





Wakili Albert Msando Amlipia JPM Deni la Mil 5 Muhimbili

$
0
0
Na Sophia Mtakasimba GPL
Deni  la shilingi milioni tano kati ya Shilingi 5,364, 814.2 ambalo Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kulipa ikiwa ni gharama za matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita, leo limelipwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako Bi. Sabina alikuwa akipatiwa matibabu.
Fedha hizo ambazo zimechangwa na wananchi zimewasilishwa MNH na wakili Albert Msando kwa niaba ya wananchi hao
Bi. Laila Kitwae ambaye ni mtoto wa marehemu Sabina Kitwae Loita alitoa ombi la kusaidiwa gharama za matibabu ili aweze kuchukua mwili wa marehemu mama yake Agosti 11 mwaka huu wakati Rais Magufuli alipotembelea Muhimbili kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akikabidhi fedha hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru, wakili Msando amesema kuwa amelipa fedha hizo baada ya kuchangisha katika mtandao wa kijamii na amewataka wananchi kulipa gharama za matibabu kwa kuwa MNH ina mahitaji mengi katika kujiendesha.

“Mimi binafsi kupitia akaunti yangu ya Instagram nilihamasisha wananchi ili tuweze kulipa hili deni. Kwanza sababu kuu ya kufanya hivyo ni kuwahamasisha kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, pili Mheshimiwa Rais ni binadamu kama nilivyo mimi na wewe ambaye naye anaguswa kama ambavyo aliguswa na tatizo hili na kuahidi kulipa deni hili.
“Tatu, wananchi wafahamu kuwa hospitali kubwa kama Muhimbili ina mahitaji mengi, hivyo wanatakiwa kuchangia huduma za matibabu,” amesema Msando.

Akipokea kiasi hicho cha fedha Museru amewashauri wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kusaidiwa kupata matibabu mara wanapohitaji huduma.

“Gharama za matibabu ni ghali, tunapoboresha huduma za matibabu gharama ya kutoa tiba zinazidi kuongezeka.  Kwa mfano kutakuwa na CT-Scan, MRI na kutakuwa na gharama za uchunguzi wa maabara, zote hizi ni gharama na kwa kawaida zinaongezeka hivyo Watanzania wanapaswa kuchangia huduma ili fedha zinazopatikana zitumike kutoa huduma,” amesema Prof. Museru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea shilingi milioni tano kutoka kwa wakili Albert Msando ikiwa ni fedha za gharama za kulipa matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita.


Prof. Museru akitoa ufafanuzi kwa waandishi habari kuhusu deni hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza  Museru.


MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2019 ZAPITISHA MIRADI YOTE YA MAENDELEO WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wiyala ya Itigi kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika juzi Kijiji cha Mkiwa kabla ya  kuanza mbio katika wilaya yake na kukagua miradi ya maendeleo.
 Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Darajani yaliyojengwa na Serikali.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally akivuta pazia kuashiria kufungua madarasa katika Shule ya Msingi Darajani.
 Vijana wa Skauti wakiimarisha ulinzi wakati wa kuupokea Mwenge baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika Kijiji cha Mkiwa.



 Wanawake wa Kijiji cha Issuna  na wabunge  kutoka wilaya ya Ikungi, Elibariki Kingu na Miraji Mtaturu na wakimbiza Mwenge wakiwa wamebeba vyandarua walivyo kabidhiwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Mzee Mkongea Ally wakati akikagua banda la kujikinga na malaria alipotembelea banda lao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kulia) akiwatanbulisha Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (kushoto) na Mbunge wa Singida Magharibi,  Elibariki Kingu wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika Kijiji cha Issuna.
 Mbunge Kingu akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Issuna.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Issuna wakiupungia kwa matawi ya miti Mwenge wakati ukipita barabarani.
 Mzee maarufu wa wilayani Ikungi, Said Mughwai (78) akizungumzia historia ya wilaya hiyo mbele ya wakimbiza Mwenge Kitaifa.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akikagua Mnara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere unaojengwa katika viwanja vya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo.
 Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakifurahi wakiwa wamekaa kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
  Taswira ya mnara huo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akipanda mti itakapo tengenezwa bustani kuzunguka mnara huo.
 Mwonekano wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi lililofunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa.
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mbele ya Ukumbi wa Wilaya hiyo wakati wa uzinduzi rasmi.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akimkabidhi kadi ya matibabu ya iCHF mwanafunzi, Ruth Allan wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko wakati wa Uzinduzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida juzi. Wanafunzi 143 walikabidhiwa kadi hizo walizo katiwa na halmashauri hiyo.
 Muonekano wa jengo la mradi wa maji katika Kijiji cha Ighuka.
 Wanafunzi wakiangalia ukaguzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ighuka.
 Wanawake wa Kijiji cha Ighuka wakiangalia ukaguzi wa mradi wa maji uliokuwa ukifanywa na wakimbiza Mwenge Kitaifa.
 Kijana Mohamed Katende aliyekuwa akitumia dawa za kulevya akizungumza mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge mafanikio waliyopata kupitia ujasiriamala baada ya kuacha kutumia dawa za kulevya na wenzake kufuatia elimu waliyoipata kutoka kwa maofisa wa Polisi wa Kituo cha Puma.
 Viongozi na wananchi wakiwa kwenye mkutano Kata ya Puma.
 Mbunge Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi wa Kata ya Puma.
 Mbunge Elibariki Kingu akizungumza na wananchi wa Kata ya Puma.
 Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano baada ya Mwenge kuwasili kukagua mradi wa Kituo cha Afya.
 Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano baada ya Mwenge kuwasili kukagua mradi wa Kituo cha Afya.
 Makada wa CCM wakiserebuka wakati viongozi wa mbio za Mwenge wakikagua mradi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Sepuka.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru kabla ya kutolewa kiapo cha Utii cha Mwenge katika eneo ulipokesha Viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Sepuka.
 Kiapo cha Utii kwa Rais kikisomwa.
 Mbunge Kingu akicheza sanjari wa Wasanii wa Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Mgungila.
 Baadhi ya Viongozi na Watendaji kutoka Manispaa ya Singida Mjini wakipasha wakati wakisubiri kukabidhiwa Mwenge kutoka Wilaya ya Ikungi katika eneo la Ititi mkoani hapa.
 Mkimbiza Mwenge Kitaifa kutoka Mkoa wa Lindi, Makugu Mwanganya akivikwa skafu na vijana wa Skauti wakati wa makabidhiano ya Mwenge katika eneo la Ititi.

 Wanafunzi wa Shule ya Awali ya Malaika Matumaini ya Singida wakionesha umahiri wa kuruka wakati wa makabidhiano ya Mwenge kutoka Wilaya ya Ikungi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kushoto) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Singida Pasacas Muragiri,  baada ya makabidhiano ya Mwenge.
 Taswira ya makabidhiano ya Mwenge eneo la Ititi.
 Makada wa CCM Wilaya ya Ikungi wakiwa pamoja baada ya Mwenge kukabidhiwa Manispaa ya Singida.
Crew nzima ya Wilaya ya Ikungi wakizungumza machache baada ya Mwenge kumaliza mbio zake wilayani humo  na kuukabidhi Manispaa ya Singida katika eneo la Ititi.

Na Dotto Mwaibale, Singida

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2019 , Mzee Mkongea Ally amepitisha miradi yote ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 1.162 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani 
Singida na kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo.

Pongezi hizo alizitoa juzi wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Miradi mitano ya Maendeleo iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Darajani, Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Ighuka, Mnara 
wa Mwenge wa  Kumbukumbi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi ambapo miradi yote hiyo imegharimu kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza Wilayani hapo Kiongozi huyo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuwafanya Watanzania waendelee 
kuiamini Serikali yao chini ya Rais Dk John Magufuli.

" Niwapongeze sana Wananchi wa Ikungi kwa namna ambavyo mmeendelea kumuamini Rais wetu Dkt. Magufuli, kipekee nikupongeze DC Mpogolo kwa uzalendo wako unaouonesha toka uteuliwe na Mhe Rais kuwa Mkuu wa Wilaya hii, nikuombe uendelee kuwatumikia wananchi wetu kwa kasi hii hii uliyoanza nayo.

" Niwaombe pia ndugu zangu wa Ikungi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muende kuwachagua viongozi ambao ni waadilifu na wenye kuichukia rushwa, msichague viongozi mafisadi, chagueni watu safi watakaoweza kuwatumikia bila kujali itikadi zenu," alisema Mzee Mkongea.

Kwa upande wake DC Mpogolo ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya Serikali kwa uadilifu pamoja na kuwatumikia wananchi hawa ambao walimuamini Rais Dk Magufuli na kumpa kura.

DC Mpogolo amesema atahakikisha wananchi wa Ikungi wananufaika na miradi ambayo imezinduliwa ndani ya Wilaya hiyo ili waweze kuona kazi kubwa ambayo Serikali inaifanya 
katika kuwahudumia.

" Miradi hii imegharimu Fedha nyingi upo ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanaakisi Sera ya Elimu bure inayosimamiwa na Rais wetu kipenzi, mradi wa Maji kama sehemu ya kampeni 
yetu ya kumtua Mama ndoo kichwani, yote hiyo ni katika kuwatumikia nyinyi wananchi wetu na zaidi kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa kwenu mwaka 2015.

 Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu  akihutubia wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru Kata ya Sepuka alisema tangu Rais Dkt. John Magufuli aingie madarakani amefanya mambo makubwa kwa Watanzania wakiwemo wananchi wake wa Singida Magharibi ambapo amepeleka miradi mingi ya maendeleo ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Alisema wananchi wa Jimbo lake wamenufaika na miradi ya ujenzi wa Kituo kikubwa cha Afya cha Sepuka kilichowekwa jiwe la msingi juzi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee 
Mkongea Ally ambacho kinakwenda kumaliza adha iliyokua ikiwasumbua wananchi wa kata hiyo kwa muda mrefu.

" Sisi watu wa Singida Magharibi na Wilaya ya Ikungi tuna mengi ya kumshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyotukarimu, miradi mikubwa ya Afya ukiachilia mbali Kituo hiki cha Sepuka lakini pia tumeshapokea takribani Milioni 500 kwa ajili ya Kituo kingine cha 
Iyumbu.

" Kwenye maji huko ndio usiseme kila Kijiji tumepanga kuhakikisha kinakua na maji ya kutosha lengo likiwa ni kuakisi kwa vitendo Sera ya Rais Magufuli ya kumtua Mama ndoo, 
ndio maana tunaanza ujenzi wa miradi 14 ya maji na tayari tumeshanunua mitambo miwili ya kisasa kwa ajili ya kumaliza changamoto ya maji pia, " alisema Kingu.

Alisema yeye kama Mbunge anaetokana na CCM ni lazima ahakikishe anasimamia Sera ya Elimu bure kwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa na Hostel ambavyo vyote viko mbioni kukamilika.

Alisema miradi yote hiyo imeweza kutekelezwa kutokana na namna Rais Magufuli anavyosimamia kwa uadilifu ukusanyaji wa kodi za Watanzania ambazo zimekua zikitumika kwenye miradi ya maendeleo kote nchini.

Vodacom yaunga mkono serikali usajili wa alama za vidole

$
0
0



Meneja wa Vodacom Tanzania Plc wilaya ya Kinondoni, Suleiman Amri akimsajili Mama Maria Nyerere kwa njia ya alama za vidole nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc inaendelea kuunga mkono zoezi hilo lililoainishwa na serikali na kuhamasisha watu wote kujisajili kwa njia ya alama za vidole ambayo ni ya haraka na haina gharama yeyote

NAIBU SPIKA DKT TULIA AKSON AWASILISHA KWA NIABA YA SPIKA MAMBO 15 YALIYOFANYWA NA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali alipowasili katika viwanja vya Majengo mjini Moshi kwa ajili ya Kongamano la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) lililofanyika mjini Moshi mwishoni mwa wiki. 


 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akipokelewa katika uwanja wa Majengo mjini Moshi na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro pamoja na serikali wakati wa Kongamano la Wanawake lililofanyika mkoani Kilimanjaro akimwakilisha Spika Job Ndugai.

Naibu Spika wa JAmhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akizungumza katika Kongamano hilo. 

Baadhi ya Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotoklewa katika kongamano hilo. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza katika kongamano hilo. 

Baadhi ya Wanawake katika kongamano hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira ambaye alikuwa mwenyeji wa kongamano hilo akieleza juu ya miradio mbalimbali iliyotekelezwa katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020. 


Baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbalimbali za serikali wakiwa katika Konagamano hilo. 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro ,Patrick Boisafi akizungumza katika kongamano hilo. 


Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro Zuhura Chikira akizungumza katika Kongamano hilo. 


Naibu Waziri wa Nishati ,Mh Subila Mgalu akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ulivyofanyika katika sekta ya Nishati. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo njia ya Treni ya kutoka Tanga kuja Kilimanjaro ilivyofanyiwa marekebisho ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na mipango ya baadae ya shirika hilo. 

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa ,Esther Mmasi akizungumza katika Kongamano hilo. 

Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akizungumza katika Konagamano hilo.

Burudani ya muziki kutoka Bendi ya Chuo cha Polisi iliwakusanya wanawake hao kucheza muziki katika ya uwanja.




Na Dixon Busagaga,Moshi 




Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka watanzania kumuunga Mkono.


Ndugai ameyataja mjini Moshi, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).


Hotuba ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na wanawake wa mkoa huo.


Ndugai alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi.


Alisema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.


Akizungumza mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.






Mwisho

MKUTANO WA 50 WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unategemea kuanza tarehe 30 Agosti, 2019 mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr, Zanzibar
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

UONGOZI KIWANDA CHA NYAMA ARUSHA WAOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO KATI YAO NA HALMASHAURI YA JIJI

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

KIWANDA cha kusindika nyama cha Happy Sausage cha jijini Arusha kimeiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wao na Halmashauri ya Jiji la Arusha unaokwamisha kukuwa kwa uzalishaji na hivyo kushindwa kufikia soko la kimataifa ikiwemo la Afrika Mashariki.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda hicho kiwandani hapo Andrew Goerge wakati akizungumza na vyombo vya habari kiwandani hapo kuelezea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho pamoja na changamoto zao.

Amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Arusha imeendelea kukwamisha juhudi za ukarabati wa kiwanda chao kwa kukataa kutoa kibali cha ukarabati wa (Bulding Permit) wakati Serikali kupia Wizara ya Mifugo na bodi ya nyama wameshatoa maelekezo ya kufanyika kwa ukarabati .

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa hatua hiyo imetokana na mgogoro wa muda mrefu unaofikia miaka nane kati ya pande hizo kuhusiana na suala zima la umiliki wa Ardhi wa eneo ambalo hadi sasa kila upande unavutia kwake wakati halmshauri hiyo ni mbia kati ya wabia 12 wa uwekezaji wa eneo la kiwanda .

“Kiwanda kimeshindwa kufikia malengo ya uzalishaji inatokana na kujikuta ikikwamishwa kufanya ukarabati wa kiwanda hicho cha usindikaji wa nyama kwa hali hiyo ambayo serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikikitaka kiwanda hicho kufanya ukarabati imekuwa ndio changamoto yetu kufikia malengo ya uzalishaji,"amesema George.

Amesema kuwa kiwanda hicho licha ya misukosuko hiyo katika kipindi cha miaka sita kimeweza kulipa wafugaji wanaokuja kuuza mazao ya mifugo kiasi cha Sh.bilion 9.3 na kuweza kilipa kodi ya Serikali leseni tozo na vibali mbali kiasi cha Sh.bilion 2.2 katika kipindi cha miaka sita.

Alieleza kuwa masoko yao makubwa ya kuuza bidhaa wanazozalisha ni masoko ya ndani ya nchi katika mikoa yote nchi kupitia mahoteli mbali mbali ya kitalii na maduka ya rejereja ya nyama nchini ambapo mpango wa kwa sasa ni kuelekea kwenye masoko ya nje ya nchi yakiwamo ya Afrika ya mashariki pamoja na Soko la pamoja la jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC.

Amesema kuwa kuhusiana na uzalishaji wa kiwanda hicho unavyobeba wananchi wengi wenye kuzalisha mazao ya mifugo kwenye kanda ya kaskazini na nchini kwa ujumla unaweza kuzorota kutokana na wao kushindwa kuleta mashine mpya .

Amesema kuwa kiwanda hicho wawekezaji wapo 12 akiwemo Halmashauri ya Jiji la Arusha ,ambao uwekezaji wake ulitokana na ardhi na kuridhiwa na baraza la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Arusha wakati huo kwenye miaka ya 1990 ambacho kiwanda hicho kimejengwa ndani ya ardhi hiyo.

Ameeleza hapo awali kiwanda hicho kimekuwa kikifanyakazi na kiwanda cha Nyama cha Arusha Meat ambacho kwa sasa kinamilikiwa na halmashauri ya jiji la Arusha kwani hapo awali manispaa ilikuwa mbia kwa asilimia 49 wa kiwanda hicho ikiwa na asilimia 51

Amesema hatua ya mgogoro huo imesababisha kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji pamoja mabenki kukataa kuwapatia mkopo , hivyo ameiomba Serikali kuingilia kati ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Mkurugenzi wake Dk. Maulidi Madeni kwa nyakati tofauti amekuwa akidai kiwanda hicho ni mali ya halmashauri hiyo na wanaojiita wamiliki wanania ya kutaka kukitaifisha .

Dk.Madeni amedai kuwa kwa muda mrefu amekuwa akimwita ofisini kwake mwenyekiti wa bodi ya Happy Sausage, Andrew George lakini ameshindwa kufika jambo ambalo ,George amedai si kweli kwa kuwa hakuwahi kuitwa na mkurugenzi huyo kwa mfumo rasmi wa kiofisi.

MIKONONI MWA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MITATU

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Dismas Silyvester (35) kwa tuhuma za  kumbaka mtoto mdogo mwenye miaka mitatu(jina limehifadhiwa), huko Mlandizi A ,kata ya Mlandizi ,Kibaha .

Akithibitisha kutokea kwa tukio la kwanza ,Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa amewaambia waandishi wa habari kwamba, Dismas anatuhumiwa pia kumuiba mtoto wa miaka mitatu na kwenda nae kichakani na kumfanyia unyama huo. 

"Baada ya taarifa kutolewa kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema lilimkamata mtuhumiwa na mtoto mchanga huyo katika mashamba ya mbogamboga vichakani,"amefafanua Wankyo.


Wankyo alieleza ,uchunguzi unaonyesha mtoto huyo ambae jina limehifadhiwa ,ameingiliwa kimwili.

Katika tukio jingine,Kamanda Wankyo amesema Agosti 25, mwaka huu, saa saba mchana katika eneo la Msongola, Mariam Shomari aligundua kuibiwa mtoto wake mchanga Swaumu Sudi mwenye miezi mitatu.

"Mtoto huyo aliibiwa ndani akiwa chumbani alipokuwa amelala baada ya mama yake kutoka kwenda kuomba kibiriti kwa jirani umbali wa mita 200 na mwanamke ambae hajafahamika hadi sasa,"amesema.


Inadaiwa mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kuvizia mama wa mtoto kutoka na yeye kufika kwenye nyumba hiyo na kumwambia mtoto mdogo Fatima Sudi miaka mitatu aliyekuwa amebaki na mdogo wake kuwa ametumwa na mama yake kuja kumchukua mtoto huyo ili ampelekee na kufanikisha wizi huo.


Amesema jeshi la Polisi mkoani hapa linaendesha msako mkali wa kumtafuta mwizi wa mtoto ambapo ametoa mwito kwa viongozi wa Serikali za mitaa ,watendaji wa kata ,wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na jamii kutoa taarifa iwao watamtilia shaka mtu ambae anaonekana na mtoto asiye wake.



Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>