Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 307 | 308 | (Page 309) | 310 | 311 | .... | 3285 | newer

  0 0

  KOCHA wa Sakatari,Innocent Mathew ameiomba Serikali kuanzisha Chuo cha mafunzo ya mchezo huo ili kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kupata ujuzi utakaofanikisha kujiajiri wenyewe.

  Akizungumza Dar es Salaam leo na waandishi wa habari, alisema Tanzania ina vijana wengi wenye vipaji katika michezo mbalimbali ila kinachowakwamisha ni kutokuwa na sehemu ya kuwaendelea ili kuwa na ufanisi mkubwa utakaoendana na ushindani kimataifa.

  Mathew ni miongoni mwa vijana 12 wanaounda kundi la Hakuna Matata ambalo linafanya shughuli za maonesho ya sanaa za jukwaani, ikiwemo uigizaji na Sarakasi katika visiwa vya Macau pamoja na nchi ya China, alifafanua kuwa ikiwa Serikali na wadau wa michezo watafanya hivyo itasaidia vijana wengi kupata fursa ya kujifunza na kuondokana na kuikaa vijiweni.

  "Naamini ikiwa Serikali na wadau wa michezo watatoa hudumu hiyo kwa kuwajengea vijana vyuo vya aina hiyo itafanya kuwapa fursa ya kujitengenezea ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo yao kwa kuna soko kubwa la mchezo huo nje ya nchi," alisema.

  Alisema mfmno unaoweza kutumia ni kwa kutumia kundi lao ambalo lilianzishwa mwaka 2000 na tangu mwaka 2003 walinza kusafiri katika nchi mbalimbali kama vile Ujerumani, Australia,Seoul Korea,Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Korea Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu na baadae kutua huko Macau, China.

  "Kama Tanzania inahitaji vijana wake wapate fursa ya kuondokana na umasikini ni vema ikawatengenezea fursa hiyo ili kufukia mafanikio katika malengo ya milenia mwaka 2015," alisema.

  Mathew hivi karibuni alirejea nchini kwa ajili ya mapumziko akitokea China alikokuwa katika mafunzo mbalimbali ya mchezo huo, amewaomba wadau wa mchezo huo kujitokeza kumpa sapoti ili kufikia malengo.

  0 0

  Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.


  Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

  Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa 
  kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

  0 0
 • 12/23/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • NGOMA YA ODYSSEY YA 'GOING BACK TO MY ROOTS' ILITURUSHA SANA MWAKA 1981

  0 0

  Mkurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa msimamizi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi,Haruna Mtandika.

  Hafla hiyo ilifanyika hapo jana kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini dar,vituo vitano vilinufaika na msaada huo ambavyo ni onorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.
   Baadhi ya Wanahabari mbalimbali waliofika kwenye tukio la Msama Promotions Ltd,ilipokuwa ikikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuuu za Krisimasi na Mwaka mpya kwa vituo vitano vya Watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu,jijini dar jana. 
  Mkurugenzi wa Msama Promotions,Inayoandaa tamasha la Krismasi linalotarajiwa kufanyika kesho Duniani kote,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta.

  Mwenyekiti wa Tamasha hilo Bwa.Msama amesema kuwa kama ilivyo ada ya kampuni yake,imeamua kutoa kiasi fulani cha mapato yake ya tamasha hilo na kununua vyakula kwa ajili ya kuwapa zawadi watoto yatima na wasiojiweza ili na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao.

  Vituo vilivyopata zawadi hizo ni Honorata Temeke,Mwandaliwa Boko,Malaika Kinondoni,Yatima Group Truts Fund ya Chamazi na Mahabusu ya Watoto Upanga,vyote vya jijini Dar.Makabidhiano yao yamefanyika jana kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kinondoni jijini Dar.

  0 0
 • 12/23/13--21:33: KIJIWE CHA UGHAIBUNI LEO • 0 0


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfanyia mahojiano Mshindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda,Bi.Consolata Deogratius mkazi wa jijini Dar es Salaam huku washindi wenzake wakishuhudia baada ya kumkabidhi pikipiki yake aliyejishindia kupitia promosheni hiyo.Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mmoja wa washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam,Bi.Monica Saimoni akisukuma pikipiki yake(kushoto)huku akifurahia jambo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)baada ya kukabidhiwa pikipiki yake aliyejishindia katika promosheni hiyo na Meneja huyo,Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda,Bi.Consolata Deogratius mkazi wa jijini Dar es Salaam,akiwaonyesha waandishi wa habari kadi ya pikipiki yake aliyejishindia katika Promoshe hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania huku Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimshuhudia na kuongea nae.Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda, Lambert Paulo akiikagua Pikipiki yake huku Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(wa kwanza toka kusho)akimshuhudia pamoja na washindi wenzake mara baada ya kukabidhiwa pikipiki hiyo na meneja huyo aliyejishindia katika Promosheni hiyo.Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda Bw.Watson Ngimbusi,Mkazi wa jijini Dar es Salaam Kigamboni akimwelezea furaha yake Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kulia)kana kwamba haamini kama kweli anaondoka na pikipiki yake aliyekalia baada ya kukabidhiwa rasmi,Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Baadhi ya washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam,wakibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(aliesimama kulia)mara baada ya kuwakabidhi washindi hao bodaboda zao,Jumla ya Bodaboda(230)zimekabidhiwa kwa washindi wa promosheni hiyo nchi nzima na Milioni 142.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

  Baada ya kushuhudia washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakikabidhiwa zawadi zao zilizojumuisha Pikipiki maarufu kama Boda boda pamoja na fedha taslim kutoka katika Promosheni ya Timka na Boda Boda, Promosheni hiyo imeshuhudia kwa mara nyingine wakadhi wa jiji la  Dar es Salaam na sehemu zake nao wakikabidhiwa Bodaboda hizo hafla iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za kampuni ya Vodacom zilizoko Mlimani City.

  Wakizungumza punde baada ya kukabidhiwa Pikipiki zao baadhi ya washindi wamesema wamefurahi kuibuka wahindi katika Promosheni hiyo huku wakitoa wito kwa Watanzania kuendelea kushiriki katika pomosheni hiyo ambayo imebakiza siku chache kumalizika.

  "Nimefurahi ana na kufarijika kuwa mshindi wa Promosheni hiiya Timka na Boda Boda, Usafiri huu utanisaidia sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine watu wengi wanajua namna usafiri kwa jiji a dar ulivyo mgumu lakini sasa nimepata suruhisho la tatizo hili nitakuwa nafika mahala pangu pa kazi kwa urahisi na kuondoka bila matatizo na kwa gharama nafuu, alisema Mzee Mustapha Bai, Moja ya washindi wa Pikipiki.

  Kwa Upande wake Bwana, Steven Masawe ambaye ni Mwalimu wa VETA Amesema "Nimeshiriki promosheni hii kwa hari sana nikijua ipi siku nitashinda, na imekuwa kweli Pikipiki hii nitaipeleka kijijini kwetu migombani, Kibosho Moshi, ikawasaidie katika usafiri kwani kutoka kijijini kwetu hadi kufika mjini ni takribani kilomita 45 na usafiri ni wa tabu sana sasa kutokana na kuwa mteja wa Vodacom nimewatatulia tatizo la usafiri.

  Miongoni mwa washindi ambao walikuwa kivutio kwa watu katika hafla hiyo ni ambaye ni mfanyakazi wa kazi za ndani Bi. Anastazia Nyangige alipowaambia washindi wenzake kuwa ametumia mshahara wake kushinda Bodaboda hiyo.

   "Mimi ni dada wa kazi za ndani sasa nitaendelea kufanya kazi zangu na kumtafuta kijana ambaye ataiendesha Boda boda hii na kuniletea fedha ili niweze kujiendeleza zaidi na ninaamini baada ya siku sitaweza tena kuendelea kuwa dada wa kazi na nitakuwa mjasiriamali, alisema Nyagige.

  Akizungumzia juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema mpaka sasa kampuni yetu imekwishatoa bodaboda 230 huku  200 bado hazijatolewa mbali na hapo kuna kiasi cha shilingi milioni 142 tayari zimechukuliwa na milioni 178 zimebakia.

  "Promosheni hii imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwani wateja wetu wameonesha mwitikio wa hali ya juu, promosheni hii inamlenga kila mtu kwani tatizo la usafiri ni letu sote na pia kilio cha watu kutokuwa na fedha za kukuza au kuongeza mitaji yao ya kibiashara ni kwa kila mtu. Kampuni yetu ni sikivu siku zote, tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu na ndio maana tunawapatia kile wanachohitaji." Aliongezea Nkurlu

  Nkurlu aliongezea pia tunakabidhi bodaboda hizi kama sehemu ya sikukuu za Krisimas na mwaka mpya na huku tukiwaahidi kuja na huduma na ofa kemkem kwa ajili ya wateja wetu kwa mwaka ujao.

  "Nawaasa washindi watakaopokea bodaboda hizi leo kuzitumia ipasavyo kwa usafiri au kuwekeza katika biashara na kuleta manufaa katika maisha yao. Pia ambao mpaka sasa hamjajiunga na promosheni hii, wakati ni huu kwani Januari mwakani zoezi hili litakamilika na nitasikitika kuona kwa nini hamshiriki kujishindia zawadi hizi." Alimalizia Meneja huyo

  Ili kujiunga na promosheni ya Timka na bodaboda wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.

  0 0

  Bi. Shida Mapele akiwa hospitalini kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya na mchumba wake.

  Na Abdulaziz Video

  Huku Dunia ikiwa Imeazimisha Siku 16 za harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,huko Wilayani Liwale Mkoani Lindi, Mkazi Mmoja wa kijiji cha Naluleo aliefahamika kwa Jina la Shida Mapele amejeruhiwa vibaya kwa Mapanga na Mchumba wake na kumsababishia ulemavu wa kudumu baada ya kumkata mkono wa kulia na kumjeruhi katika baadhi ya viungo vyake.

  Hii ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na uvunjaji wa haki za binadamu licha ya Mtuhumiwa kufikishwa mbele ya Sheria,Wanawake wilayani Humo wametakiwa kutetea haki zao huku wakiomba sheria ichukue mkondo wake dhidi ya ukatili huo uliofanywa na Bw. Ally Burian ambae anashiliwa na Jeshi la Polisi.

  Akiongea na Ripota wa Globu ya Jamii Wilayani humo,Mratibu wa Asasi ya kutetea wanawake na watoto(Liwopac)Bi Hidaya Chikawe alieleza kuwa licha ya harakati zinazofanywa na wanawake kuelimisha jamii Bado Vitendo hivyo vinashika kasi wilayani humo.

  “Hakika kwa tukio hili ni Ishara tosha inayodhihirisha kuwepo kwa ukatili wilayani humu,Hapo Awali tulizoea kusikia katika mikoa ya wenzetu lakini sasa Dunia imebadilika tunashuhudia matukio haya mara kwa mara”alieleza Chikawe.

  Aidha aliwataka akina mama wa liwale kuanza kujitetea kwa kufichua uhalifu unaojitokeza kutokana na Takwimu ya mwaka jana inaonyesha matukio hayo kuwepo kwa 2% lakini sasa hali inaongezeka kila mara hususan kipindi hiki cha mauzo ya korosho.

  Kwa Upande wao baadhi ya akinamama walisema licha ya historia ya matukio mabaya kutokea wilayani humo tukio hili la kumsababishia ulemavu mwanamke huyo kutokana na kukatwa kwa mapanga.

  Walieleza walivyoguswa na tukio hilo huku wakitoa wito kwa jamii na serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wanaobanika na kukamatwa.

  Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo hivi karibu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi wa Polisi Bi Renatha Mzinga alianzisha kampeni ya kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matukio hayo katika maadhimisho ya siku 16 za ukatili dhidi ya Mwanamke ambapo walifanikisha kutoa misaada na usafi katika kambi ya wazee na walemavu

  0 0  0 0
 • 12/24/13--01:06: Article 12
 • At this festive season, we look back and turn to all who have made our progress and success possible. We wish you all a Merry x-mass and a prosperous 2014....
  Board, Management and staff of 
  Tanzania Education Authority. 
  TEA

  0 0

  Na Kiza Sungura-MAELEZO,Dar es salaam 
   Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho kikwete ametoa jumla ya kilo za mchele 1,200 , lita 220 za mafuta na mbuzi 25 kwa ajili ya zawadi ya sikukuu ya Krismas kwa makundi maalum. Zawadi hizo zilikabidhiwa jana (leo) na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bibi Beatrice Fungamo kwa niaba ya Rais Kikwete kwenye sherehe fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam. 
   Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum kama vile yatima, wazee wasiojiweza na watato walioko katika mkinzano na Sheria ili nao waweze kuungana na Watanzania wengine katika kusherekea sikukuu ya Krismas. Bibi Fungamo alisema kuwa nje ya kutoka zawadi kwa vituo mbalimbali vya Mkoa wa Dar es salaam pia ametoa katika makunndi mengine ya mikoa mingine hapa nchini. 
   Alisema kuwa kwa upande wa Dar es salaam ametao kwa vituo 11 vinavyosaidia kutoa huduma kwa watoto na wazee wasiojiweza ambazo ni Kituo cha Watoto Ibn Kathir, Tabata, Ilala, Makao ya Watoto Kurasini, Temeke, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Kituo cha Kwetu Mbagala Girls Home, Kituo cha Yatima Group, na Kituo cha CHAKUWAMA. Vingine vya mkoani Dar es salaam ni Mahabusu ya Watoto, Makao ya Watoto Yatima Mburahati, Kituo cha Tuwapende Watoto Bunju, Makao ya Wazee wasiojiweza Msimbazi na Vosa Mission Kongowe. 
   Alisema kuwa kwa vituo vya mikoani na maeneo mengine nje ya Dar es salaam zawadi zao watapatiwa katika maeneo yao . Bibi Fatuma alivitaja vituo vya nje ya Dar es salaam vilipatiwa zawadi na Rais Kikwete ni Kituo cha Mabaoni Chakeckale Pemba, Kituo cha Werezo cha Unguja, Mahabusu ya Wototo Moshi mkoani Kilimanjaro na Makao ya Wazee wasiojiweza Sukamaela mkoani Singida. Vingine ni Makao ya wasiojiweza Bukumbi, Misungwi mkoani Mwanza na Makazi ya Wazee wasiojiweza Msufini , Muheza mkoani Tanga. 
   Alisema kuwa Rais Kikwete ametoa zawadi hizo kwa kutambua kuwa watoto na wazee hao wanapaswa kujumuika na wanajamii wengine katika kusherehekea sikukuu hiyo vema. 
   Hatua hii ya Rais Kikwete ni sehemu ya utamaduni wake aliojijengea wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali .
   Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi  Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi  Beatrice Mgumiro mbuzi watatu, kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.

   Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia)  mbuzi wawili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu kwa furaha.
   Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi  Sister Maria Silvana  (kulia)  mbuzi watatu, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.
  Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Mkurugenzi WA  Kituo cha Vosa  Mission Hochimin Mugarura (kulia)  mbuzi wawili, kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerehekee sikukuu.  Picha na MAELEZO, Dar es salaam

  0 0

  Kampuni ya Transevents Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi  kutoka Uholanzi  yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayoanzia Tanzania.
  Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
  Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu  kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
  Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania
  Tazama Video za Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio  
  Tazama video ya Basi hilo Likiwa linafanya safari zake Nchi kavu na Baharini pamoja na abiria ndani. 

  0 0  0 0
 • 12/24/13--01:34: dereva bora wa basi duniani

 • 0 0

  Na Mwandishi Wetu.

  Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra “Sikinde” kesho  mchana zitachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.

  Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.

  Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.

  Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa muda wote.

  Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa hujuma.Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.

  Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera  alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.

  Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni  'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na  'Suluhu'.

  Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Athumani Kambi, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya,  James Mawilla,  Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roman Mng’ande `Romario’  na Hassan Moshi.

  Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.

  Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’,  'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.

  Sikinde inaundwa na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka,  Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard, Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.

  Pambano umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Nipashe, CXC Africa na Saluti5.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji waliojitolea kusaidia kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Nusu Karne hapo Serena Hoteli Jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Nchini uturuki kwenye chakula cha usiku kilichofanyika Serena Hoteli Mjini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuacha milango wazi kwa wawekezaji wa sekta tofauti kutoka Nchini Uturuki kuwekeza vitega uchumi vyao Visiwani Zanzibar kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Zanzibar za kuimarisha uchumi wake pamoja na kudumisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili.

  Fursa kadhaa za uwekezaji katika sekta ya Kilimo, Utalii na afya bado zipo kutokana na washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi kujengewa mazingira mazuri na Serikali ya miundo mbinu ya uwekezaji katika maeneo hayo.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa chakula cha usiku kilichojumuisha wafanyabiashara wa sekta tofauti ndani na nje ya nchi waliojitolea kuchangia harakati za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia nusu karne.

  Balozi Seif aliwaeleza wafanyabiashara hayo aliojumuika nao pamoja katika ukumbi wa Serenna Hoteli Jijini Dar es salaam kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika jitihada za kunyanyua uchumi wake katika kubuni sekta mbali mbali ili kusaidia zao la Karafuu ambalo ndilo muhimili wa uchumi hivi sasa likisaidiwa na sekta ya Utalii.

  Akizungumzia maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamuwa kuzifanya sherehe za mwaka 2014 kuwa kubwa za aina yake kutokana na Mapinduzi hayo kufikisha Nusu karne.

  Alisema uamuzi huo wa Serikali umekuja ili kuwaenzi waasisi wa mapinduzi hayo ambao walipigania haki ya kujikomboa kitendo ambacho kimeleta faraja na mabadiliko makubwa ya kiuchumi miongoni mwa wananchi wake.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewashukuru na kuwapongeza wafanyabiashara waliojitolea na kuweka ahadi ya kuchangia mambo mbali mbali kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar.

  Balozi Seif alisema michango ya wafanyabiashara hao pamoja na washirika wa maendeleo imeleta faraja na matumaini makubwa kwa Serikali pamoja na Wananchi wote hapa Nchini.

  Mapema wafanyabiashara hao wakiwakilishwa na Mzee Bashir walieleza kwamba wataendelea kuyaeshimu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo ndio yaliyozaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Wafanyabiashara hao walisema wako tayari kuchangia kwa hali na mali kufanikisha sherehe hizo zinazotarajiwa kubwa na za aina yake mwaka ujao wa 2014.

  Zaidi ya shilingi Milioni 65,000,000/- zimeahidiwa kutolewa na wafanyabiashara hao kwa ajili ya kuchangia shsrehe hizo za Kihistoria.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  24/12/2013.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea pikipiki 44 zikiwa ni msaada kutoka Ubalozi wa China na Kampuni ya Fu-Tang ya kutoka China.

  Amekabidhiwa msaada huo leo mchana (Jumanne, Desemba 24, 2013) mbele ya viongozi wa wilaya ya Mlele katika hafla fupi iliyofanyika kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi na kushuhudiwa na wakazi wa kijiji hicho.

  Akizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wakazi wa kijiji hicho kabla ya kukabidhi msaada huo, Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing alisema anaamini kupatikana kwa pikipiki hizo kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka ya wilaya hiyo.

  “Tunataraji matumizi ya pikipiki hizi yatasaidia kuleta maendeleo ya haraka na hatimaye kuongeza kipato cha wakazi wa wilaya hii,” alisema Balozi Lu ambaye ofisi yake imekabidhi pikipiki 20.

   Alisema wakazi wa nchi yake wanafikia bilioni 1.3 na yeye anatamani kuona walau kila raia wa China akinunua walau kilo moja ya chakula kutoka hapa nchini ili waweze kuongeza soko kwa mazao yanayozalishwa na wakulima wa Tanzania.

   Naye Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza pikipiki cha FEKON ambayo ni kampuni tanzu ya Fu-Tang, Bw. Zheng Bing alisema mara taratibu zitakapokamilika, wana lengo la kujenga kiwanda cha kutengeneza pikipiki na kompyuta ili kuongeza ajira kwa Watanzania. Kampuni hiyo ilikabidhi pikipiki 24.

    Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi Lu pamoja na kampuni ya Futang kwa msaada huo na kuahidi kuzigawa ili ziwasaidie watendaji kusimamia kazi na hivyo kuharakisha kuleta maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo.

  Tuna kata 24, kwenye wilaya yetu kwa hiyo kila kata itapewa pikipiki moja. Hiyo pikipiki siyo ya Katibu Kata binafsi bali ni ya kata, kwa hiyo Katibu Kata atakuwa ndiyo msimamizi...,” alisema.   Waziri Mkuu ambaye yuko kijijini kwake Kibaoni kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, alisema pikipiki saba zitapelekwa kwenye vituo vitano vya afya vya Mamba, Usevya, Inyonga, Katumba na Kanoge na zahanati za Nsimbo na Kasansa.

  “Pia tutapeleka pikipiki nyingine nane katika shule za sekondari za Sitalike, Machimboni, Magamba, Nsimbo na Mtapenda. Nyingine ni Utende, Inyonga na Kasokola,”  aliongeza.

    Mbali na hao, wengine watakaofadika na mgao huo ni watendaji wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Mlele ambao watapatiwa pikipiki moja, jumuiya za chama katika wilaya hiyo zitapatiwa pikipiki tatu na moja iliyobakia itagawiwa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi.

  Waziri Mkuu aliwashukuru Balozi Lu na Bw. Tang Hulin kwa msaada huo ambao alisema anaamini utasaidia kusukuma maendeleo ya wakazi wa wilaya hiyo.

  Kuhusu uzalishaji wa chakula cha kutosha wakazi bilioni 1.3 wa China, Waziri Mku alisema itabidi Tanzania izalishe magunia milioni 13 ya nafaka ili iweze kufikisha lengo alilolisema Balozi Lu.

  Waziri Mkuu Pinda alishapokea msaada wa pikipiki 23 kutoka kwa wafadhili wengine na kugawa pikipiki sita kwa Jeshi la Polisi, pikipiki 13 kwa vikundi vya vijana na zilizobakia nne alizigawa kwa shule za sekondari.

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akizungumza na viongozi wa Jumuia hiyo katika Kata za wilaya ya Temeke, leo Mbagala, kuwashukuru viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za wilaya hiyo kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti katika uchaguzi uliopita. . Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
  Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akimvalisha kitenge cha sare maalum ya Jumuia hiyo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilakala, Henedi Fereji, alipogawa sare hizo kwa wajumbe 60 waliohudhuria kikao maalum kilichofanyika leo, Mbagala Kuu, kuwashukuru viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za Temeke, kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa mkoa huo katika uchaguzi uliopita. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega na Watatu ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  OFISA UHUSIANO MWANDAMIZ WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF BW. ABDUL NJAIDI (KUSHOTO) AKIKABIDHI ZAWADI MBALIMBALI KWA BW. OMARY KYARUZI WA NYUMBA YA KULEA WATOTO YATIMA YA MWANDALIWA. PSPF IMEJIWEKEA MPANGO WA KUWAKUMBUKA WATOTO YATIMA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU.
  OFISA UHUSIANO MWANDAMIZ WA MFUKO WA PENSION WA PSPF BW. ABDUL NJAIDI (KUSHOTO) AKIKABIDHI ZAWADI MBALIMBALI KWA MWALIMU RASHID ALI WA NYUMBA YA KULEA WATOTO YATIMA YA MWANDALIWA. PSPF IMEJIWEKEA MPANGO WA KUWAMBUKA WATOTO YATIMA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU.
  BW .MOHAMMED MADENGE AFISA KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF (KULIA) AKIMKABIDHI SISTA OLIVA PAULO WA KIJIJI CHA FURAHA ZAWADI MBALIMBALI KWA AJILI YYA WATOTO WANAOTUNZWA KATIKA KUTUO HICHO, HII IKIWA NI UTARATIBU WA PSPF KUWAKUMBUKA WATOTO YATIKA KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU MBALIMBALI.
  OFISA UHUSIANO MWANDAMIZ WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF BW. ABDUL NJAIDI (KUSHOTO) AKIKABIDHI ZAWADI MBALIMBALI KWA MWALIMU RASHID ALI WA NYUMBA YA KULEA WATOTO YATIMA YA CHAKUWAMA, PSPF IMEJIWEKEA MPANGO WA KUWAMBUKA WATOTO YATIMA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU.
  OFISA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF BW. MOHAMMED MADENGE (KULIA) AKIKABIDHI ZAWADI MBALIMBALI KWA JUMUIYA YA NYUMBA YA KULEA WATOTO YATIMA YA AL-MADINA CHILDREN HOME, PSPF IMEJIWEKEA MPANGO WA KUWAMBUKA WATOTO YATIMA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU.
  OFISA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF BW. MOHAMMED MADENGE (KULIA) AKIKABIDHI ZAWADI MBALIMBALI KWA SISTA GEUSALDIA WA NYUMBA YA FURAHA NA AMANI, PSPF IMEJIWEKEA MPANGO WA KUWAMBUKA WATOTO YATIMA KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Machano (122) mmoja kati ya Waasisi wa ASP wakati alipomtembelea kumjulia hali kijijini kwake Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Disemba 24-2013. (Picha na OMR).


older | 1 | .... | 307 | 308 | (Page 309) | 310 | 311 | .... | 3285 | newer