Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUZUIWA KWA NDEGE YA AIR TANZANIA AFRIKA KUSINI,WAZIRI WA UJENZI ATOA UFAFANUZI


BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUJENGA RELI YA KISASA KWA FEDHA ZAKE ZA NDANI

$
0
0


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani.

Bi. Kabagambe anayewakilisha nchi 22 za Kanda ya Afrika katika Benki hiyo yenye Makao yake Makuu Washington DC nchini Marekani, ametoa kongole hiyo kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kutembelea na kukagua sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya Reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

Alisema kuwa amefurahishwa na kiwango cha kiufundi kilichotumiwa na Kampuni ya Yapi Merkez iliyopewa kandarasi ya kujenga Reli hiyo na kwamba mradi huo sit u utakuwa na manufaa kwa Tanzania peke yake bali katika ukanda wa nchi za Afrika ambazo hazipakani na bahari.

“Nimekuja kujionea hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kujenga Reli hii ya kisasa na ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza mradi huu mkubwa na wa kielelezo kwa kutumia fedha zake za ndani” alisisitiza Bi. Kabagambe.

Aliahidi kuwa wakati Benki ya Dunia ikiangalia namna ya kuongeza ufadhili wa miradi kwa Tanzania, ataishawishi Benki hiyo pamoja na taasisi nyingine za Kimataifa zinazotoa misaada na mikopo kutoa fedha ili Tanzania iweze kutimiza malengo yake ya kukamilisha ujenzi wa Reli hiyo ambayo itafungua fursa za kiuchumi na kijamii katika ukanda wa Afrika.

Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli, Kutoka Kampuni ya Reli-TRC, Mhandisi Felix Nlalio, aliezea kufurahishwa kwake na ziara ya kiongozi huyo wa Benki ya Dunia pamoja na ahadi aliyotoa ya kuipigia debe Serikali kwenye taasisi za kimataifa ili zitoe fedha za kukamilisha mradi huo.

Aliahidi kuwa kazi yao kubwa kama Kampuni ya Reli na Serikali kwa ujumla ni kuchapa kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa reli hiyo unaokwenda kwa kasi uweze kukamilika kwa wakati na kuiletea faida nchi pamoja na nchi jirani.

Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa unaohusisha awamu mbili, Kipande cha kwanza kati ya Dar es Salaam na Morogoro (kilomita 300), ambacho kilianza kujengwa Mei 2, 2017 na kitakamilika ifikapo Novemba 2, 2019 kwa gharama ya Sh trilioni 2.7, wakati kipande cha pili kinachoanzia Morogoro –Makutupora (Manyoni, Singida) (kilomita 422), kilianza kujengwa Februari 26, 2018 na kitakamilika baada ya miezi 36 yaani Februari 25, 2021 kwa gharama ya Sh trilioni 4.4.

Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuongeza mapato katika Bandari ya Dar es Salaam na pia kutaimarishara biashara hususani kati ya Tanzania na nchi zinazopitiwa na ushoroba wa kati (Central Corridor) za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda na Rwanda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (wa pili kushoto), akiangalia ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa –SGR,  kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, kulia ni  Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli , Mhandisi Felix Nlalio.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (kulia), akiongozwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli , Mhandisi Felix Nlalio (wa pili kushoto), kutembelea ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa –SGR,  kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.
 Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli, Mhandisi Felix Nlalio, akitoa maelezo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa-SGR  kwa kipande cha kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (katikati), alipofanya ziara katika miundombinu hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (wa pili kulia), akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wamiundombinu ya  Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa-SGR, kwa fedha zake za ndani, wakati   alipofanya ziara katika miundombinu hiyo, kushoto ni Mkurugenzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Reli , Mhandisi Felix Nlalio.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (kushoto), akizungumza jambo na msaidizi wake, wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa –SGR, kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.
Muonekano wa moja ya Kituo cha Treni  katika mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Reli ya Kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa –SGR,  kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

WAZIRI JAFO AITAJA NMB KATIKA MAFANIKIO SERIKALINI

$
0
0
Waziri Selemani Jafo,akizungumza kwenye ufunguzi wa Teachers day mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na benki ya NMB
Baadhi ya walimu Mkoa wa Dodoma wakishiriki Mkutano uliyoandaliwa na benki ya NMB

Waziri Selemani Jafo akikaribishwa na Meneja wa Kanda ya Kati NMB,Nsolo Mlozi.
Waziri Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja



………………….

Serikali imeitaja benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha makusanyo ya fedha kwa mwaka 2018/19 kwa kuwa benki hiyo haina tofauti na Wizara ya Tamisemi kwa kufika maeneo yote nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Seleman Jafo, wakati akizungumza na walimu zaidi ya 300 kutoka halmashauri za wilaya mkoani Dodoma katika siku ya mwalimu ambao walikutanishwa na benki ya NMB.

Waziri Jafo alisema uamuzi wa benki hiyo kwenda nchi nzima na kufungua matawi, mawakala pamoja na kuongeza ATM, ulisaidia kwa watu kuzifikia kwa urahisi huduma za kibenki pamoja na halmashauri kuitumia kwa makusanyo yake.

Hivi karibuni Jafo alitangaza mapato ya serikali kutoka katika halmashauri yakipanda kutoka asilimia 73 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 81 mwaka 2018, juzi kwenye za mapato katika mmalaka ya serikali za mitaa tumekusanya takriban billioni 664 sawa na asilimia 91 kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa. Ninyi NMB mmetusaidia kwa hili,” alisema Waziri Jafo.

Kuhusu benki ya NMB alisema ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri hapa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 3.5 milioni pamoja na matawi 229 ambayo ni zaidi ya halmashauri zilizopo ingawa aliwataka waongeze wateja na kuagiza kitengo cha utafiti kufanya kazi yake vizuri.

Kuhusu mikopo alisema kuna kilio kutoka kwa watumishi kuhusu riba kubwa ya mikopo kwenye mabenki yote nchini kwani wanatoza kiwango ambacho si rafiki kwa wafanyakazi jambo linalopekea malalamiko na wengine kujutia uamuzi wa kukopa.

“Naomba suala la riba mliangalie, haiwezekani riba ya mfanyakazi ikawa sawa na anayefanya biashara, ndiyo maana mnasababisha walimu kuingia madeni kwenye visaccos vingine hadi wanaacha kadi zao huko mwisho wa siku wengine wanataka kujinyonga, tafakarini ikibidi mfike hata kwenye single digit,” alisema Jafo.

Katika hatua nyingine aliwataka walimu kutumia mishahara yao kwa utaratibu na kuacha maisha ya kuiga kwani ndiyo yanayowapelekea kwenye madeni makubwa.

Meneja wa NMB Kanda ya kati Solo Mlozi alisema benki hiyo imejipanga kuwafikia Watanzania mahali walipo kwa kutumia mawakala wake na kuendelea kuboresha huduma zao kwa kadri iwezekanavyo.

Mlozi alimwomba Waziri kufikisha ujumbe wao serikalini ili waendelee kuiamini benki hiyo na kufanya nayo kazi kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 31 ndani yake hivyo na mambo yaliyozungumzwa watashauriana ili kuwapunguzia mzigo Watanzania.

Awali Meneja Mwandamizi wa wateja wadogo Ally Ngingite alisema benki hiyo imeweka utaratibu kuwafikia walimu kama sehemu ya wateja na kusikiliza changamoto zao.

Ngingite alisema mpango huo ulianzia Jijini Dar es Salaam,Pwani na jana Dodoma kabla ya kwenda mikoa mingine ikiwemo Zanzibar huku akitaja benki kusogeza huduma zaidi kw akutumia simu za mkononi.

Vodacom yadhamini Ligi kuu Tanzania bara

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (kulia) akimkabishi Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia (Kusho ), mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 9, fedha ambazo zimetolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania kudhamini ligi kuuTanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021), katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.  Anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza udhamini  wa ligi kuu ya Vodacom iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.  Kampuni ya Vodacom imetoa kiasi cha sh. bilioni 9 kudhamini ligi kuu ya Tanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021) kwa lengo la kuinua vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu nchini na kuchochea maendeleo kwa ujumla. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na Kulia ni  Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Hendi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhamini uliotolewa na  kampuni Vodacom kwenda TFF kwa ajili ya Ligi kuu ya Tanzania Bara, katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.  Kampuni ya Vodacom imetoa  kiasi cha sh bilioni 9 kudhamini ligi kuu Tanzania bara kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021) kwa lengo la kuinua vijana wenye vipaji mpira nchini na kuchochea mendeleo kwa ujumla. Kulia ni  Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia


Vodacom Tanzania kudhamini ligi kuu ya Tanzania kwa miaka mitatu

Agosti 23, 2019 – Dar es Salaam: Ligi kuu ya Tanzania yarudi kwa kishindo baada ya Vodacom Tanzania na shirikisho la soka TFF kufikia maridhiano na Vodacom kudhamini ligi hyo. Kampuni hiyo imesaini mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambao utawezesha shirikisho hilo la soka kupokea TZS bilioni 9 za udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu (2019/2021), na kupelekea Vodacom kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo.


Ushirikiano na udhamini huo ulitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za makao makuu ya Vodacom, jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, na umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya Vodacom Tanzania, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na bodi ya ligi.


Ligi kuu ya Tanzania ambayo sasa itaitwa Ligi kuu ya Vodacom itaanza tarehe 24 ya mwezi huu, ikitarajia kushuhudia jumla ya michezo 380 ikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini na kushirikisha timu 20 zilizoko ligi kuu ya Tanzania bara.


Akizungumza katika hafla hiyo Dk Mwakyembe alisema serikali imepiga hatua kubwa katika kuwezesha vijana wenye vipaji mbali mbali nchini na alisisitiza umuhimi wa kuwekeza katika Vijana ili kuleta Maendeleo nchini. Pia aliipongeza Vodacom kwa kutia chachu juhudi za serikali katika kufanikisha malengo hayo.


 “Ukweli ni kwamba tupo katika wakati ambao tunahitaji kushirikiana na vijana katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ambapo mpira wa miguu unaajiri mamia ya vijana hao. Uwekezaji uliofanywa na Vodaom siku hii ya leo ni moja ya ngao ya kuleta mabadiliko makubwa katika mpira wamiguu nchini, vile vile kuongeza ajira kwa vijana. Napenda kuwasihi wawekezaji kuwekeza katika michezo mbali mbali ili kufanya vijana wetu wawe wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya uchumi,” aliongeza Mwakyembe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bwana Hisham Hendi amesema kuwa kampuni ya Vodacom iko mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na shughuli za mpira wa mguu hapa inchini hivyo leo ni siku ya furaha sana kwao. 


 “Tumedhamini ligi hii kwa zaidi ya miaka 9 na tumeona vipaji vingi vikiibuka na ligi kuongezeka umaarufu nchini na nje ya nchi ikufuatiliwa na mamilioni ya washabiki. Wote tumekubali kuwa wanamichezo ni mabalozi wazuri wa nchi yetu kama tulivyoona katika michuano ya AFCON iliyoisha hivi karibuni. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao kadri tutakavyo weza” alisema Hisham .


Bwana Hendi aliongeza kuwa amejivunia kampuni hiyo kurejea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine na kufafanua kuwa itaendelea kuwa mdau wa kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo hapa Tanzania.


Pia aliweka wazi kwamba ligi kuu ya Vodacom inakuja na ofa kabambe kwa wateja wao pamoja na mashabiki wa mpira kupitia huduma ya SOKA LETU. “Pale mteja anapojiunga na SOKA LETU anapata dondoo mbali mbali za michezo, ikiwemo VPL na si hayo tu, sasa anapata nafasi ya kujishindia dakika au tiketi ya kwenda kutizama michuano itakayokuwa ikiendelea na zawadi nyingie kabambe,” alisisitiza Hendi.


Kwa upande wake Rais wa TFF, Wallace Karia, ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania akisema kuwa anaamini, maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi. “Kwa niaba ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa kuonyesha nia na kuendelea kuunga mkono mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kuthamini vipaji vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio zaidi,” alisema Karia.



 “Ikiwa ni sehemu ya malengo yetu ya kuipeleka Tanzania katiza zama na malipo kwa njia ya kidigitali, Sasa wateja wetu wote na mashabiki wa mpira watanuua tiketi zao kupitia M-Pesa kutoka mtandao wowote hata mabenki. Kwa kweli ukiwa na Vodacom yajayo yanafurahisha,” alihitimisha Bw Hendi.


SERIKALI YAJIPANGA KUONGEZA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI-WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 uliofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam, leo tarehe 24 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 unaofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 24 Agosti 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 uliofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam, leo tarehe 24 Agosti 2019. 
Sehemu ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 unaofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 24 Agosti 2019. 



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali imesema kuwa imejipanga lkuongeza ushirikiano na Sekta binafsi katika kuhakikisha kuwa kero na vikwazo vinaondolewa ili kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 24 Agosti 2019 wakati akimuwakilisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kufungua Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 huku akiongeza kuwa serikali imefanya uamuzi mahususi mwaka huu wa kuondoa muingiliano wa utoaji wa huduma za mashirika ya TBS na TFDA ili kupunguza usumbufu kwa Wanyabiashara. 

Alisema kuwa hizo ni hatua za awali na ametoa mwito kwa TCCIA kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanafuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ili kuondoa usumbufu wote unaoweza kujitokeza wakati wa kufanya biashara.

Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) tarehe 4 Juni, 2018. Kwa kutambua umuhimu wa Sekta Binafsi, moja ya maboresho makubwa ya ASDP II ukilinganisha na ASDP I ni kuipa nafasi kubwa zaidi Sekta Binafsi. 

Aliongeza kuwa ni wakati muafaka wa kubaini maeneo maalumu ambayo Taasisi hiyo ya TCCIA itaendelea kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza programu hiyo ili iweze kufikia malengo yaliyowekwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuhakikisha uboreshaji wa Mazingira ya biashara nchini, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi iliandaa andiko maalumu “Blue Print” ambalo lilikwisha zinduliwa, pia mpango wa utekelezaji wake umeandaliwa na umeanza kutekelezwa. 

“Ni wajibu sasa wa kila pande yaani Sekta ya Umma na Binafsi kuhakikisha kuwa yale yote yaliyoainishwa katika andiko hilo yanatekelezwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Vile vile, amesema kuwa serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya ambapo tayari imeshaweka Mwongozo wa Mabaraza hayo ambayo TCCIA ni Sekretarieti. 

Waziri Hasunga amewataka washiriki hao kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini, hasa miundo mbinu ya reli ya Kisasa, mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere, barabara za kisasa, bomba la mafuta, manunuzi ya ndege n.k. 

Alisema kuwa Fursa hizo kwa kupitia sera ya “Local Content” nao wakiwa wazawa wana nafasi kubwa ya kunufaika nazo. 

Amesema, Miradi hiyo ni mingi na itachukua muda mrefu ikitekelezwa kwa awamu tofauti. “Endapo kwa sababu moja au nyingine haukuweza kupata fursa ya kushiriki kazi kwenye mradi mmoja kwa sababu fulani zikiwemo sifa kadhaa basi, nakushauri ujipange vizuri kwenye miradi inayokuja, msikate tamaa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema kuwa serikali inatambua ushirikiano mzuri wa TCCIA na taasisi mbali mbali za Umoja wa Mataifa (UN) zikiwemo UNDP, UNIDO, FAO, UNV, UNESCO, ILO, na ITC, pamoja na Wadau wengine wa kimaendeleo kama Trade Mark East Africa. 

Ushirikiano huo kwa kupitia mifumo ya kielektroniki ya kuripoti na kufuatilia vikwazo mbalimbali (NTBs Reporting and Monitoring System) na utoaji wa vyeti vya Uasili wa Bidhaa kwa njia ya kielektroniki (Electronic Certificates of Origin) umesaidia sana uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha (NTBs). 

Pia, TCCIA imeshirikiana na Wadau wengine kama vile VSO, ENGEN, USAID, East African Trade Hub, BMZ, KOICA, JICA, TRIAS na DANIDA kupitia Local Investment Climate (LIC) kuimarisha biashara na mfumo wa majadiliano na sekta ya umma. Kwa kipekee ninawapongeza sana kwa mashirikiano hayo.

AWESO ATAKA WAJUMBE BODI INAYOSIMAMIA MRADI WA MAJI WA MAKILENGA WILAYANI ARUMERU WAKAMATWE

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Meneja RUWASA Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Christine Kessy akikagua tenki la maji la Mradi wa Maji wa King’ori.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akikagua Mradi wa Maji wa Makilenga na kusikiliza kero za wanakijiji Oldonyong’iro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na wakazi wa Kijiji cha King’ori, wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongoza kikao kilichohusisha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, wajumbe ya Bodi ya Mradi wa Maji wa Makilenga na wananchi.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akionyeshwa nadharia ya utekelezaji wa mradi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kabla ya kuukagua.

…………….

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wajumbe wa Bodi ya Makilenga inayosimamia Mradi wa Maji wa Makilenga, wilayani Arumeru, mkoani Arusha akiwemo Mwenyekiti na Mhasibu wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya ubadhirifu wa fedha.

Mhe. Aweso amewachukulia hatua wajumbe hao kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na kusababisha wakazi wa Kijiji cha 
Oldonyong’iro kukosa huduma ya maji.

Ameelekeza timu kutoka Wizara ya Maji na Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru ifanye uchunguzi kwenye Mradi wa Maji wa Makilenga na kumpa ripoti haraka.

Wakati huo Mamlaka ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wasimamie mradi kwa kipindi chote cha mpito, mpaka viongozi wengine watakapopatikana.

Aidha, Naibu Waziri Aweso amekagua ujenzi wa mradi wa majsafi na salama wenye lengo la kuimarisha huduma endelevu ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi 50,000 kupitia teknolojia bunifu katika maeneo ya Lengijave, Olkokola, Ngaramtoni, Ekenywa na Seuri yaliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Pamoja na vijiji vya Lemanyata, Lenjani, Ilkerundeti, Ilikuroti na Lemanda kwa siku zijazo.Mhe. Aweso amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Assess kumaliza mradi huo uliofikia asilimia 97 ya utekelezaji haraka.

Mkandarasi huyo ametoa ahadi ya kukamilisha mradi huo ifikapo Septemba 1, 2019 na wananchi wataanza kupata maji.

RAIS DKT SHEIN AFUNGUA HOTELI YA MADINAT AL BAHAR,MBWENI ZANIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Bw Rustamali Merani Shivji wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo mara baada ufunguzi rasmi uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati waliokaa) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Bw Rustamali Merani Shivji (wa pili kulia) wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo mara baada ufunguzi rasmi uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi,(kushoto) Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini MagharibiBaadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi. [Picha na Ikulu]24/08/2019.

MILIONI 300 KUTUMIKA MRADI WA MAJI HOROHORO

$
0
0

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Msimamizi wa Mradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma katikati wakati alipotembelea eneo la Bwawa ambalo litatoa maji kupelekea kwa wananchi eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya mradi huo unaotekelezwa na mamlaka hiyo utakapomalika kushoto ni Msimamizi wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia jambo kwa Msimamizi wa Mradi Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma wakati alipotembelea na kukagua eneo ambalo kutajengwa kituo kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo hilo.
Msimamizi wa Mradi Tanga Uwasa Mhandisi Shame Juma kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia wakati alipotembelea eneo ambalo kutajengwa kituo cha kusafisha maji kabla ya kwenda kwa wananchi eneo la Horohoro
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakitazama eneo ambalo kutajengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kwenda kwa wananchi eneo la horohoro
Mafundi wakiendelela na shughuli za ujenzi wa kituo cha kusafishia maji eneo la Horohoro ambayo yatakuwa yakitoka kwenye bwawa kabla ya kwenda kwa wananchi.


Mabomba ambayo yatatumika kwenye mradi huo yakiwa kwenye gari kabla ya kushushwa eneo la Horohoro wilayani mpakani mwa Tanzania na Kenya 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akikagua mabomba hayo kabla ya kushuhwa eneo hilo la Horohoro
Sehemu ya viungio vya mabomba vikiwa vimeshushwa eneo hilo la Horohoro
Afisa Ugavi Msaidizi wa Tanga Uwasa Fatuma Salimini kushoto akifanya uhakika wa vifaa mbalimbali ambavyo vimefikishwa eneo la Horohoro akiwa na dereva wa mamlaka hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akitazama maji yanayotumiwa na wananchi wa Kijiji cha Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati alipotembelea bwawa ambalo litatumika kutoa maji na kupeleka kwa wananchi yakiwa safi na salama
Muonekano wa bwawa la maji lililopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya ambalo litatumika kuondosha kero ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo
Muonekano wa bwawa la maji lililopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya ambalo litatumika kuondosha kero ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akifurahia jambo na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Horohoro Peter Sebastian katikati kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Miliya Merieyer
Kazi ya uchimbaji ikiendelea kama inavyoonekana
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (tanga Uwasa) imeeleza kwamba mradi wa maji eneo la Horohoro lililopo mpakani mwa Tanzania na Kenya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utagharimu kiasi cha milioni 300. 


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati alipotembelea na kukagua bwawa la maji eneo hilo wakati wa makabidhiano ya mabomba 415 yenye thamani ya milioni 64.4 yatakayotumika kwenye mradi huo kwa uongozi wa serikali ya Kijiji cha Horohoro. 

Alisema kwamba mradi huo ambao utakuwa ni kutoa maji kwenye chanzo cha maji ambao ni bwawa na kupelekwa kwenye tenki ambalo litakarabatiwa na kusambazawa kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha Horohoro ili kuweza kuondosha kero ya maji kwa wananchi. 

Licha kutembelea bwawa hilo lakini pia alifika eneo ambako kunaendelea kujengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kuwafikia wananchi wanaoishi eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Kenya. 

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Hilly alisema kwamba alisema mamlaka hiyo wamepewa kazi na wizara ya maji kwa ajili ya kujenga mradi huo ambao utasaidia kuondosha shida ya maji. 

Alisema kwamba hilo linatokana na eneo hilo kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa maji licha ya kuwa na bwawa ambalo lina uwezo wa kuhifadhi maji lakini wanapata maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu 

Alisema kwamba mabomba hayo ni hatua mojawapo ya ujenzi mradi wa maji Horohoro kwa ajili ya kusafisha maji na kusambaza kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo hilo.Aidha alisema kwamba sambamba na ujenzi huo lakini pia watawekwa vituo vidogo vya kuchotea maji (vioski) huku akieleza kwa mujibu wa takwimu za watendaji kwamba wananchi 5000 wanaishi maeneo hayo ndio watanufaika. 

“Lakini pia mradi huu utakapokamilika utakuwa mkombozi mkubwa sana kwa wananchi lakini hata watumishi waliopo eneo la mpakani kwani walikuwa wanapata changamoto ya maji safi ikiwemo TRA kutokana na maji kutokuwa salama walikuwa wakifuata maji Tanga mjini na kuyatumia kwenye ofisi zao “Alisema

Awali akizungumza wakati wa halfa ya upokea wa mabomba hayo Mwenyekiti wa Kijiji cha Horohoro Kata ya Duga Maforoni wilayani Mkinga mkoani Tanga Miliya Merieyer alisema kabla ya mradi huo changamoto ya maji ilikuwa kubwa sana kutokana na kulazimika kufuata maji kwenye mto Umba uliopo nchini Kenya.

Alisema kwamba licha yam to huo kutokea nchini Tanzania lakini ukifaka maeneo hayo unaingia kwenye nchi hiyo sasa ilikuwa wanatembea kilomita 8 kutoka mpakani hadi huko watu walikuwa wakinunua maji 500 hadi 1000 lakini alipochaguliwa 2015 ndio akaanza kuhangaikia suala hilo.

Alisema kwamba kulikuwa na bwawa hilo ambalo lilikuwa limechimbwa na watu wa TASAF lakini wakalitelekeza ikawa ikinyesha mvua maji yanapita na hivyo kukutana na wananchi kutaka kulitengeneza na kuziba eneo lililokwa likivuja mvua iliponyesha watu walikuwa wakichota maji walipoona maji yanazidi kujaa akalazimika kwenda wilayani kuomba fedha akaambiwa hawana fedha.

Alisema baadae aliomba Mhandisi wa maji wilayani kufika eneo hilo ili aweze kuwafanyia mahesabu ili waweze kuona namna ya kupambana kuhakikisha wanasaka vifaa vya kutoa maji kwenye chanzo hicho huku akieleza kutokana na juhudi hizo aliweza kupata mabomba ambayo yaliwaweza kupata maji kutoka bwawani mpaka kwenye meneo ya karibu wananchi wakafurahi na kuamua kuuza maji hayo kwa sh.100 mpaka kufikia milioni 6. 

Akizungumza adha ya maji waliokuwa wakikumbana nayo eneo hilo alisema suala hilo lilikuwa kama mtaji wa mtu kwamba wanatoa maji Tanga mjini hadi Horohoro kwenda kuwauzia wananchi.

Hata hivyo alisema kwamba baada ya waziri alivyokuja kukagua bwawa hilo akakuta maji yapo akwaambia wanaweza kuwaboreshea bwawa hilo baada ya waziri kuondoka wahandisi wakaanza kwenda eneo hilo na kuhaidi kupelekea mabomba huku ujenzi wa kituo cha kusafishia maji ukianza kujengwa.

“Kwa kweli niishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli tulilia muda mrefu msaada wa maji lakini halikuweza kufanikishwa lakini Waziri Mbarawa alivyokuja wakaaona kama ni stori za miaka ya nyuma lakin mambo yamekuwa tofauti tunaona jambo hili linashughulikiwa kwa vitendo “Alisema

TANZANIA YASHINDWA KUTAMBA MICHUANO YA FEASSSA ARUSHA

$
0
0
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Piliakimalizia mbio kama anavyoonekana katika mbio za mita 10,000


Na.Vero Ignatus,Arusha.


Wanariadha nchini wameshindwa kutamba katika katika mashindano ya riadha ya vyama vya michezo kwa shule za Sekondari Afika Mashariki (FEASSSA) yaliyofanyika Jijini Arusha.

Katika Matokeo ya jumla kwa wanawake na wanaume nchi Kenya iliongoza kwa kuondoka na jumla ya Medali 18 za Dhahabu, Medali 11 fedha na medali 10 za shaba na kufanya jumla ya medali 39 sawa na pointi 359.

Uganda ilifuatia mshindi wa pili kwa kukusanya jumla ya Medali 10 za dhahabu,Medali 14 za fedha na 10 za Shaba na kufanya jumla ya Medali 34 walizonyakua ambazo ni sawa na pointi 334 huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu kwa kuambulia Medali 2 za dhahabu, Medali 5 za fedha na medali 8 za shaba ambazo ni sawa na pointi 209 .

Nchi ya Rwanda ilishika nafasi ya nne kwa kupata jumla ya medali 2 pekee za shaba na Zanzibar haikupata kitu.Kwa upande wa wanawake walioshoriki riadha mbio tofauti tofauti Kenya ilifanikiwa kunyakua jumla ya medali 7 za dhahabu, medali 5 za fedha, medali 6 za shaba.

Nchi ya Uganda ilifuata kwa wanariadha wake kufanya kweli kwa kujikusanyia jumla medali 6 za dhahabu,medali 8 za Fedha na medali 4 za shaba huku wenyeji Tanzania wakiambilia medali 2 za fedha,2 za fedha na tano za Shava, huku Zanzibar na Rwanda hazikupata kitu.

Kwa upande wa wanaume Kenya ilijikusanyia jumla ya Medali 11 za Fedha, 6 za fedha na 4 za Shaba , Uganda ilifuata kwa kuwa na jumla ya Medali 4 za dhahabu,6 za fedha na 6 za Shaba ,Tanzania haikupata kitu katika dhahabu,ilipata medali 3 za fedha na tatu za Shaba huku Rwanda ikiondoka na medali 2 za Shaba na Zanzibar haikuambulia kitu.

Matokeo mengine mwanariadha Faith Kipsang kutoka Shule ya St. francis ya Kenya alichaguliwa kuwa mwanariadha Bora kwa wanawake huku mwanariadha Layeng Eric Sibryanda kutoka Gombe nchini Uganda aliibuka mwanariadha bora kwa wanaume.

Kocha wa timu ya Riadha ya Tanzania katika michuano ya FEASSSA Robert Kalyahe alisema ni kweli wanariadha kutoka Kenya wamefanya vizuri kwa kuondoka na medali za kutosha na Tanzania kupata vichache 

" Tumepigwa kwani pia tumeokoteza tu vijana kutoka mashindano ya Umiseta yaliyofanyika Mtwara na muda wa mafunzo ulikuwa mfupi,hali ya hewa pia ilituchanganya hapa Arusha lakini yote kwa yote tumejifunza kutoka kwa wenzetu Kenya na tutajua nini cha kufanya,"alisema Kalyahe.

Alisema Tanzania inapokosea ni kuweka muda mchache inatakiwa kuweka muda mrefu wa maandalizi vijana wachaguliwe mapema tena ikiwezekana wachezaji wawekwe katika shule moja ili kuwa na maandlaizi ya kutosha.

Naye kocha wa riadha na mjumbe wa kamati tendaji ya Riadha Tanzania Yohana Misese alisema katika riadha inasikitisha kwani watanzania wamekuwa wakienda kwenye mashindano na kurudi bila kufanya tathmini wapi wanakosea .

"Tumeona wenzetu wako makini katika maandalizi na timu wameandaa kwa muda mrefu tofauti na sisi tumeandaa kwa wiki mbili hali inayopelekea kuwa na maandalizi yasiyo na Matokeo mazuri," alisema Misese.

VIJANA KANISA LA ANGLIKANA WACHANGIA DAMU MLOGANZILA

$
0
0
Mwanasayansi wa Maabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila Bw. Jastus Silvester akimuhudumia Bi. Foibe Jackson kutoka Kanisa la Anglikana wilaya ya Ubungo ambaye ni mmoja wa vijana wa Kanisa la Anglikana ambao leo wamejitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Mloganzila.
Mwanasayansi wa Maabara Bw. Mbaruku Kisutu (kulia) akimsajili Bw. Fredrick Anderson (kushoto) kabla ya kuingia katika chumba cha uchangiaji damu.
Baadhi ya vijana kutoka Kanisa la Anglikana wilaya ya Ubungo ambao leo wamejitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Mloganzila.

……………….

Hospitali ya Taifa Muhimbili –Mloganzila imetoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kujitolea katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuchangia damu wagonjwa ambao wanauhitaji wa damu ili kuokoa maisha yao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi MNH-Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu wakati akizungumza kwa niaba ya Naibu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Julieth Magandi katika zoezi la uchangiaji damu kutoka kwa vijana wa Kanisa la Anglikana wilaya ya Ubungo.

Dkt. Sakafu amesema mahitaji ya damu katika Hospitali ya Mloganzila ni chupa 40 kwa siku lakini damu inayokusanywa ni kati ya chupa 15 mpaka 20 na kusisitiza kuwa pamoja na hali hiyo hakuna mgonjwa anayekosa damu.

“Napenda kusisitiza kwamba pamoja na kukusanya chupa 20 za damu kwa siku, hakuna mgonjwa anayekosa damu katika Hospitali ya Mloganzila kwasababu tunasaidiana na wenzetu wa Muhimbili-Upanga, kituo cha damu salama pamoja na Hospitali za Tumbi na Mlandizi’’ amesema Dkt. Sakafu.

“Pia nachukua fursa hii kushukuru Kanisa la Anglikana kwa matendo ya huruma unapochangia damu unaokoa maisha ya watu, kwani makundi yenye uhitaji wa damu ni mengi ikiwemo mama wajawazito, watoto, wagonjwa wanaohiaji kufanyia upasuaji na majeruhi wa ajali’’ amefafanua Dk. Sakafu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana Kanisa la Anglikana wilaya ya Ubungo Bw. Daniel Katumbi amesema kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kufanya matendo ya huruma kila mwaka kwa kutambua kuwa wapo watu wenye mahitaji mbalimbali hivyo ni wajibu wa kanisa kuwatambua na kutoa huduma.

Katika zoezi hilo takribani vijana 50 wamechangia damu.

Polisi wala rushwa kutimuliwa kazi

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

JESHI la Polisi mkoa wa Arusha,limesema kuwa litawafukuza askari wa jeshi hilo pamoja na maafisa wake bila kujali cheo chake ikiwa watabainika kuomba rushwa kutoka kwa madereva wa magari ya waongoza watalii pamoja na wamiliki wa makampuni hayo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shana ameyasema hayo kwenye kikao cha wadau wa utalii mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye hotel ya Gran Melia, jijini Arusha.kilichokuwa kikijadili changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.Akitoa salamu zake kwenye kikao hicho kilichoongozwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Costantini Kanyasu, Kamanda Shana amesema amepokea malalamiko ya baadhi ya askari kupokea rushwa .

Amesema kuwa ikithibitika askari ameomba rushwa kutoka kwa wamiliki wa makampuni ya waongoza utalii au madereva wa magari hayo atawafukuza mara moja na endapo kama atakuwa ni polisi mwenye nyota ataomba kibali kwa mamlaka husika cha kumfukuza afisa huyo.

Wakichangia kwenye kikao hicho wadau wamelalamikia uamuzi wa kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Kilimanjaro, KIA, kuwalazimisha watalii kulipia malipo yao kupitia Control namb kwenye benki zilizopo nje ya uwanja huo.

Mwenyekiti wa Chama cha makampuni ya waongoza watalii, TATO, Wilbad Chambulo, amesema wageni wanapata usumbufu unaowalazimisha kutoka nje ya uwanja kwenda kulipia kwenye benki zilizoko nje ya uwanja huo halafu ndipo warejee tena uwanjani na kuiomba serikali kuboresha mfumo huo kwa kuweka benki ndani ya uwanja ili kuondoa usumbufu.

Kwa upande wake benki ya NMB imesema kuwa kuanzia Augosti 15 imesema tayari imepata meza na kuhamishia shughuli zake ndani ya uwanja huo na hivyo kuwaondolea usumbufu wageni.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Costantini Kanyasu,amesema Augosti 22 na 23 Wizara itafungua utalii nyanda za juu kusini mkoani Iringa.

MAKUNDI YA UCHAGUZI UKARA, UKEREWE YALIIANGUSHA CCM DHIDI YA CHADEMA

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na wanachama wa CCM (hawapo pichani) wa Kata ya Bwisya Tarafa ya Ukara wilayani Ukerewe jana.
………………….


NA BALTAZAR MASHAKA, UKARA

MAKUNDI ya viongozi wasaka vyeo wakiwemo wanachama ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Ukerewe, yaliigharimu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015.Imebainika

Pia wana CCM na wananchi wa Kisiwa cha Ukara na wa Wilaya ya Ukerewe kwa ujumla wao walipokea na kubeba msiba usio wao uliosababisha baadhi ya vitongoji, vijiji,kata na Jimbo la Ukerewe kuangukia mikononi mwa chama wasichokijua undani wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu MKuu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli, alipozungumza kwa nyakati tofauti na wana CCM wa kata nne za Bwisya,Nyamanga, Bukiko na Bukungu kisiwani Ukara.

Alisema kwenye chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa 2015 CCM iliangushwa na makundi ya wasaka vyeo waliokosa kura kutosha, kwenye uchaguzi wa ndani hivyo walinuna na kugeuka makuwadi wa CHADEMA na kusababisha CCM ikapoteza jimbo, baadhi ya kata, vijiji na vitongoji.

Alisema wanachama wa CCM wenyewe waliamua kuwapa kura CHADEMA wakishirikiana na wananchi wasio wana CCM kuuza jimbo kwa kumchagua mgombea wa CHADEMA ambaye hata hivyo alipokosa pa kuzikia msiba huo aliamua kuwaachia mliomsaidia kuubeba na kurejea CCM.

Kalli alidai CCM iliadhibiwa na wanachama wake walioshindwa kwenye kura za maoni kwa msemo wa bora tukose wote akaonya mwaka huu asitokee mtu ambaye kura hazitatosha aseme bora amwage mboga, yeye abaki na ugali, cha moto atakona kwa dhamana waliyo nayo wana CCM ni vitendo si maneno.

Katibu huyo wa CCM Mkoa aliwataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wa Kisiwa cha Ukara pamoja na Wilaya ya Ukerewe kutofanya makosa yaliyopita ya kukumbatia makundi ya wasaka vyeo badala yake washikamane na CCM kwa kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo na kuachana na wasaka vyeo.

“Simlaumu Mbunge, kura alizopata wana CCM walimpa wenyewe kwa sababu ya makundi ya wale ambao kura hazikutosha.Walihangaika na kuwa makuwadi wa vyama vingine, mchana walikuwa CCM,jioni NCCR-Magauni (Mageuzi) usiku CHADEMA.Ndiyo yaliyotokea Bukiko Ukara na Ukerewe,”alisema Kalli.

Alisistiza kuwa misiba waliyoibeba ya kuchagua wagombea nje ya CCM ilisababisha Mbunge huyo wa CHADEMA Josephat Mkundi aliuachia msiba huo katikati ya safari baada ya kubaini alidanganywa akajiunga na CCM.

“Nguvu kubwa ya wana CCM ilimsaidia kumbeba Joseph Mkundi kushinda Ubunge Ukerewe lakini kwenye tukio la ajali hakuna kiongozi wa chama chake alishiriki na kujikuta akipwaya.Pia kasi ya maendeleo ya Rais John Magufuli na nguvu kubwa CCM iliyombeba,aliamua kujiunga na timu ya kuleta maendeleo,”alisema Kalli.

Aidha, baadhi ya wana CCM akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Nyamagana walisema kuwa makundi yanayotokana na uchaguzi wa ndani bado yapo ili kushinda lazima makundi hayo yaliyokigharimu Chama 2014 na 2015 yatafutiwe dawa na yavunjwe, kwani tunahitaji maendeleo ili kupiga hatua.
Pia walisema wana CCM si wavumilivu, ni wagumu wa kutafuta kura zingine kutoka nje lakini pia uhusiano duni ndani na nje ya CCM, kuishi kwa kujibagua na kujitenga na jamii ni changamoto

MKUTANO WA 50 WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unategemea kuanza tarehe 30 Agosti, 2019 mpaka tarehe 5 Septemba, 2019 katika hoteli ya Madinat Al Bahr, Zanzibar
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

KUMBUKIZI YA BI KIDUDE.

$
0
0
NA Moshy Kiyungi,Tabora.

Ukipima kwenye mizani historia ya muziki wa taarabu na tamaduni za unyago Visiwani Zanzibar, ni wazi kwamba mizani hiyo lazima itaegemea upande wa Fatuma Binti Baraka ‘Bi.Kidude’.

Uzoefu na uelewa aliokuwa nao katika fani hiyo, alikuwa hana mpinzani.

Nyimbo alizoimba miaka michache kabla ya kufariki dunia za ‘Muhogo wa Jang’ombe na ‘Halaiti’, zilimuongezea umaarufu zaidi.

Inaaminika kwamba Bi. Kidude ndiye aliyekuwa mwanamke, mwimbaji mkongwe kupita wote Afrika Mashariki na Kati.

Bi. Kidude alikuwa mwimbaji wa taarabu tangu miaka ya 1920, akiwa mfuasi wa Sitti Bin Saad.

Sitti alikuwa amebarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji, alipokuwa akiimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali maili nyingi.

Alizaliwa mwaka 1880 katika kijiji cha Fumba huko Visiwani Zanzibar.

Sitti Binti Saad alikuwa mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu Visiwani humo.

Bi. Kidude alizifuata nyayo za Sitti, akatambulika na kuheshimika kama Malikia wa taarabu na mambo ya unyago asiye na mpinzani.

Jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa ni Fatuma Binti Baraka.

Lakini baada ya kupata umaarufu katika uimbaji, jina la Bi. Kidude likashika nafasi.

Bi. Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo katika familiya ya watoto saba.

Wakati wa uhai wake aliwahi kusema kuwa hafahamu mwaka aliozaliwa, kilichokuwa kinatamkwa na baadhi ya watu ni kwamba alikuwa na umri zaidi ya miaka 90 hadi alipofariki dunia.

Sio ajabu alikuwa ameshafikisha umri wa miaka 100!

Mtu yeyote iliyekuwa akimuuliza Bibi huyo kuhusu umri wake, alisema hawezi kuutaja, lakini alikuwa akitamka kuwa alizaliwa zama za sarafu ya rupia.

Rupia ilikuwa ni sarafu iliyotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki mpaka wakati wa vita vya kwanza vya dunia.

Bi Kidude si kwamba alikuwa na mvuto kwa sauti yake nzuri ya kuimba taarabu, lakini pia namna ya muonekano wake katika jukwaa.

Wazazi wake walikuwa ni wafanyabiashara ya kuuza Nazi enzi hizo za Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa Wakoloni wa Kiarabu.

Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni, marehemu Bi.Kidude aliwahi kusema alianza kuimba akiwa na umri mdogo wa miaka kumi.

Alivutiwa sana na utunzi na uimbaji wa Sitti binti Saad, wakati huo yu ngali kigoli.

Fatuma Binti Baraka alikuwa akijificha nje ya nyumba ili kumsikiliza Sitti binti Saad akiwaimbia wageni ambao mara nyingi walikuwa wakipelekwa pale.
Akiwa na umri wa miaka 13, alionesha ujasiri mkubwa wakati alipotoroka katika visiwa vya Zanzibar, akakimbilia Tanzania Bara (Tanganyika enzi hizo), ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu kukwepa ndoa ya lazima.

Baadaye Bi. Kidudue akawa mtu anaejihusisha sana na muziki wa taarabu, alizunguka sehemu mbalimbali za nchi, akiwa mwimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki huo likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab.

Aliambatana na kundi hilo walipofanya ziara mbalimbali za muziki wa taarab katika maeneo ya Afrika Mashariki.

Fatuma Bint Baraka ‘alikwea Pipa’ akaenda nchini Misri, ambako aliimba huko kwa kipindi kifupi, akaamua kurejea Kisiwani Zanzibar.Aliporejea Zanzibar 1940, pamoja na kuwa mtu mwenye umaarufu mkubwa, aliendelea kuishi katika nyumba yake iliyotengenezwa kwa udongo.

Mbali na muziki alikuwa akijihusisha na vyama vya kijamii na Mwalimu wa ‘Unyago’ ambapo alikuwa na chuo chake akitoa elimu ya unyago kwa wasichana katika Visiwa hivyo.

Wakati wa uhai wake alikuwa akijivunia kwamba kati ya wanafunzi wake wote hakuna ambaye ameshawahi kupewa talaka na mumewe.

Pengine hii ndio sababu mwaka 2004 ulipozuka uzushi kwamba Bi.Kidude amefariki dunia wakati alipokuwa katika ziara ndefu ya kimuzik, kila mtu Kisiwani Zanzibar, alishikwa na butwaa na majonzi! .

Wakati wazushi ‘wanapakaza’ yeye alikuwa Ulaya na nchi za Mashariki ya mbali. Ikabainika kwamba habari za kifo chake zilikuwa ni uzushi mtupu.


Aidha Bi. Kidude alikuwa mjasiliamali akiuza Wanjana Hina ambazo alikuwa akizitengeneza mwenyewe pamoja na utaalamu wa dawa za mitishamba.

Mwaka 2005 huko Gateshead, Newcastle nchini Uingereza, Bi.Kidude alipokea Tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX), kwa mchango wake katika muziki na Utamaduni wa Zanzibar.

Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo.

Bi. Kidude aliwahi kusema kwamba hawezi kuacha kuimba mpaka siku atakapoiaga dunia, kwani akiimba anajihisi kama ni binti wa miaka 14!

Mwaka 2006, Kampuni ya nchini Uingereza iitwayo Screen Station kwa kushirikiana na Busara Promotions, walitoa filamu inayoonesha hali halisi ya maisha ya Bi. Kidude, iitwayo ‘As Old As My Tongue-The Myth and Life of Bi.Kidude’.

Filamu hiyo ilikuwa ikielezea historia nzima ya maisha yake Bi. Kidude.
Fatuma Binti Baraka alikuwa anakunywa sana pombe na kuvuta sigara katika jamii isiyopenda mabadikilo lakini aliweza kuishi.

Sauti ya Bi,. Kidude alikuwa ya juu, alikuwa ni mahiri wa kuimba bila kutumia kipaza sauti.

Taarabu ni nini:

Taarab ni mchanganyiko wa muziki wa Kiarabu na Kiafrika, Taarabu ni sehemu ya mchanganyiko wa muziki wa Kiswahili na wenye kuchanganyika na Kihindi na Kiarabu, inatumia ala za udi, fidla, filimbi na ngoma.

Kwa kiasi kikubwa muingiliano wa tamaduni za Kiswahili na Kiarabu unatokana Zanzibar kuwa mji wa uliokuwa chini ya Mamlaka ya Sultan wa Oman.

Zanzibar ilikuwa kituo cha biashara ya utumwa kwa mataifa ya rasi ya Kiarabu.Mwaka 1920, Bi Kidude alikuwa akiimba rasmi katika matamasha ya kitamadauni.Bibi huyo alionesha mfano kwa wanawake hasusan wanaovaa Baibui, vazi la kujisitiri kwa wanawake wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Bi. Kidude alionesha ujasiri mkubwa wakati alipotoroka katika visiwa vya Zanzibar kukwepa ndoa ya lazima akiwa na umri wa miaka 13.

Baadaye akawa mtu anaejihusisha sana na muziki wa taarab kwa kufanya ziara mbalimbali za muziki huo katika maeneo ya Afrika ashariki.

Baada ya kurejea Zanzibar 1940, pamoja na kuwa mtu mwenye umaarufu mkubwa lakini aliendelea kuishi katika nyumba yake iliyotengenezwa kwa udongo. Mbali na muziki alikuwa akijihusisha na 

vyama vya kijamii na kutoa elimu ya unyago kwa wasichana katika visiwa hivyo.

Taarabu ni maisha yake.

Kwa kutumia muziki wenye hisia na huzuni, Bi Kidude alikuwa akiimba kwa mtindo wa aina yake wenye mvuto.

Hakuweza kujali kuhusu miiko, aliolewa mara mbili japokuwa hakubahatika kupata mtoto.Wakati akiwa katika jukwaa alikuwa akipenda kubadili miondoko wakati wowote.

Kitendo hicho kilikuwa kikiwapa wakati mgumu sana wanamuziki wanaompiga vyombo mbalimbali katika bendi husika kwa wakati huo.

Washabiki wake walikuwa wakipenda sana mawazo yake ya kubadili miondoko au nyimbo akiwa katika jukwaa.Ingawa mwanamke huyo alikuwa mwenye umbo dogo lakini alikuwa akipiga ngoma katika kiwango cha kushangaza wengi.

Bi. Kidude alikuwa kikongwe, lakini alikuwa maarufu na mwenye kufurahisha watu wa umri tofauti hadi vijana kwa kuimba na kupiga ngoma kwa wakati mmoja.

Kila mara alikuwa akipinga kwa nguvu zote mitindo ya taarabu inayopigwa miaka hii ya karibuni, akitamka kwa kusema siyo taarab.

Bi. Kidude alikuwa akisisitiza kuwa taarab halisi wanamuziki wote huketi kwenye viti vyao, mwimbaji muongozaji ndiye aliyekuwa akisimama akishika kipaza sauti.

“toka linii taarab ikachezwa na steji shoo, kutamka matusi, kukata viuno hadharani” alilama Bi.Kidude. 

Taarab ya miaka hii imeboreshwa kutokana na wakati, siku hizi wanaita ‘Tara dance’

Mwenyezi Mungu akupe kauli thabiti, na kaburi lako liwe ni nuru miongoni mwa nuru za peponi Amina.



Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao mbalimbali.

Mwadaaji anapatikana kwa namba: 0713331200, 0784331200, 0736331200 na 0767331200.

DKT NDUGULILE AAGIZA UTEKELEZAJI MAJUKUMU KAMATI ZA ULINZI WA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimkabidhi kitabu cha Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri wakati wa uzinduzi wa Kamati ya ulinzi ya wa wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizindua Kamati ya ulinzi ya wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akiwasalimia wakazi wa Wilaya ya Kigambo wakati wa uzinduzi wa Kamati ya ulinzi ya wa wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatiliwa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kigambo ni wakati wa akizindua Kamati ya ulinzi ya wa wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akiangalia bidhaa zinazotengenzwa na wanawake wa wilaya ya Kigamboni wakati wa uzinduzi wa Kamati ya ulinzi ya wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kigamboni wakifuatili hotuba za viongozi, mada na burudani wakati wa uzinduzi wa Kamati ya ulinzi wa wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri pamoja na wadau wengine mara baada ya kuzindua Kamati ya ulinzi wa wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 



Na Mwandishi Wetu WAMJW 

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Wilaya ya Kigamboni kuhakikisha Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto zinatekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuisadia jamii ya wanakigamboni kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia . 

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa akizindua Kamati ya ulinzi ya wanawake na Watoto ya Wilaya ya Kigamboni pamoja na Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa Kamati hizo ikisimamiwa vizuri itakuwa nuzo bora katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyozidi kushamiri kila siku nchini katika jamii na familia zetu. 

Ameongeza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi kikubwa kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo. 

”Ni matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa Kijinsia Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha kampeni’’ alisema Dkt. Ndugulile. 

Dkt. Ndugulile pia ameagiza kutafutwa kwa wale waonafanya vitendo vya kikatili katika wilaya ya Kigamboni na Tanzania kwa ujumla na vyombo husika kusimamia na kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki zao. 

Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia nchini Dkt. Ndugulile amesema taarifa ya hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha kuwa jumla ya watu 41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa kwenye vituo vya polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya hivyo mwaka 2016. 

Dkt. Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto, ukeketaji na kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya mataukio hayo 41,416 yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703 sawa na asilimia 67 yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto. 

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake wa umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri amesema kuwa Serikali ya Wilaya itahakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili na amewaomba wanawake kutoa taarifa ya vitendo hivyo na kuwataka kutofumbia macho vitendo hivyo na kuacha vipite kwa mwavuli wa ndoa. 

“Sisi Serikali tunaheshimu ndoa na dini zote ila tunaangalia uhai wa mwananchi hivyo wanawake wenzangu nawaomba ndoa zisiwe sababu ya kuendelea kufanyiwa vitendo vya kikatili na kuachana inawezekana” alisema Mhe. Sarah 

Naye mmoja wa wnawake aliyefanyiwa vitendo vya kikatili Bi. Lucy Sanga ameishukuru Serikali ya Wilaya ya Kigamboni kwa kumsaidia kupambana na vitendo vya manyanyaso ambavyo anafanyiwa na mume wake. 

“Mume wangu amekuwa akininyanyasa sasa kwa muda mrefu na imefikia hatua ya kuficha vyombo vya kupikia na kunihamisha chumba chetu cha kukaka na kumleta mama yake mzazi kutoka Musoma na yeye analala humo na me nalala kwenye chumba cha watoto” alilalama Bi. Lucy

JUMLA YA MASHAURI 14 YAFUNGULIWA NA KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT’

$
0
0
Gari likiwa eneo linapopaki Buhongwa mnamo Agosti 22, 2019.
Mhe Hakimu (aliyeketi mbele) akisikiliza kesi ndani ya Mahakama inayotembea 'Mobile Court' mkoani Mwanza.



Na Mary Gwera, Mahakama

Jumla ya Mashauri 14 yamefunguliwa na kusikilizwa na Mahakama inayotembea ‘mobile court’ mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya amesema kuwa mashauri hayo yamefunguliwa na kutolewa maamuzi katika kipindi cha mwezi Julai, 2019.

Mhe. Nkya alieleza kuwa Mahakama hiyo inayotembea inaendelea kutoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza huku Mahakama nyingine inayotembea iliyopo jijini Dar es Salaam inaendelea kutoa elimu kwa Wadau juu ya uendeshaji wa Mahakama hiyo. 

Kwa mkoa wa Mwanza, Mahakama hiyo inafanya kazi katika maeneo ya Igoma, Buswelu na Buhongwa na kwa upande wa Dar es Salaam Mahakama hiyo inatoa huduma katika maeneo ya Bunju ‘ A’, Kibamba, Buza na Chanika.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mahakama inayotembea inasikiliza mashauri yote yanayosikilizwa na Mahakama za Mwanzo kama vile migogoro ya ndoa, madai, mirathi na jinai, pamoja na rufaa kutoka Mabaraza ya kata, yakiwemo mashauri yanayojitokeza katika operesheni maalmu zinazofanywa na taasisi/vyombo mbalimbali vya serikali.

Huduma nyingine zitolewazo na Mahakama hiyo ni kutoa taarifa za mashauri, kutoa fomu za viapo na kuthibitisha nyaraka mbalimbali, kufanya usuluhishi kwa wadawa na kutoa elimu kuhusiana na masuala ya Mahakama.

Mnamo Februari 06, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizindua rasmi Mahakama inayotembea lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa wananchi na kutoa haki kwa wakati.

Aidha; lengo jingine ni kuwapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma za Mahakama mbali na maeneo wanayoishi.

Mahakama ya Tanzania ina mpango wa kutanua wigo wa utoaji huduma hii kwa kuanzisha vituo vingine katika mikoa iliyosalia kwa awamu tofauti

DEKULA KAHANGA ‘VUMBI’ ANAYEMILIKI BENDI YAKE SWEDEN.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam


Dekula Kahanga ameweza kuyasaka mafanikio hadi kuunda bendi yake anayojulikana kama Dekula band akiwa katika jiji la Stockholm nchini Sweden.

Kabla ya kwenda nchini humo Kahanga alikuwa mpigaji wa gitaa la solo katika bendi ya Maquis Original, iliyokuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Lang’ata, Kindondoni jijini Dar es Salaam, miaka ya 1990.

Dekula ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Vumbi’, aliwahi kutamka kwamba mafanikio yoyote katika maisha ni lazima mtu kuwa na malengo, na dhamira ya dhati, hatimaye kufanya maamuzi magumu.

Alisema baadhi ya maamuzi magumu aliyoyafanya mojawapo ni lile la kondoka katika bendi hiyo ya Maquis Original, na kutokomea kwenda Sweden bila kujua atakuwa mgeni wa nani huko Ughaibuni.

Vumbi alieleza kwamba hivi sasa hajutii maamuzi yake kwakuwa yamempata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kumiliki bendi yake.

Amesema bendi hiyo hupiga muziki kwa mkataba mara mbili kwa mwezi katika ukumbi wa Lala Vin, mjini Stockholm nchini Sweden.

Dekula Band ina wanamuziki mahiri toka nchi mbalimbali duniani, wakiwemo akina Luhembwe Mwanahita ‘Bobo Sukari’ ambaye ni mwimbaji na kunengua, Sammy Kasule, ambaye ni injinia pia huimba, kupiga gita la besi, drums na kinanda.

Wengine amewataja kuwa ni Joe Gerald Nnaddibanga, ambaye huimba, kupiga konga na kucheza show, Christina Frank, na Marceline Kouakoua.

Mwenyewe Dekula Kahanga, hulicharaza gitaa la solo na rhythm pamoja na Arne Winald ambae hubofya kinanda.

Safu hiyo kwa pamoja huufanya muziki wao kukubalika kimataifa hadi kupelekea kupata mialiko lukuki ndani na nje ya Sweden zikiwemo nchi za Ulaya, Asia, Marekani, Japan, Falme za kiarabu na Afrika.

“ Hakuna kitu muhimu kama kuwa na mahusiano mema na baadhi ya watu toka nchi mbalimbali ninazotembelea. Nimefikia kuweza kuongea kwa ufasaha lugha tano tofauti za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Lingala na Kiswidish” Anajigamba Dekula ‘Vumbi’.

Historia ya Dekula Kahanga anailezea kwamba alizaliwa mwezi Aprili 02, 1962 katika kijiji cha Lumera, Wilaya ya Kivu Kusini huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ni baba wa familia akiwa na mke na watoto watatu. Dekula ni mtoto wa kwanza kati ya watoto kadhaa wa Mzee Aloyce Obeid Dekula, aliyekuwa mfanyakazi katika serikali ya Zaire iliyokuwa ikiongozwa na rais Mobutu Seseseko.

Alipata elimu ya Sekondari katika shule mbili tofauti za Bukavu na Uvira huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alihitimu kidato cha nne mwaka 1979. Mwaka uliofuatia wa 1980, safari yake katika muziki ilianza kwa kujiunga na bendi za Bavy National, na Grand Mike jazz, ambako alikutana na wanamuziki akina Kyanga Songa na Issa Nundu.

Akiwa huko kwao wilaya ya Kivu, ‘Vumbi’ alikuwa msikilizaji mzuri wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo ilikuwa ikisikika wakati huo na alizitamani sana nyimbo zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi za Morogoro Jazz, Jamhuri Jazz, Tabora Jazz, Nyamnyembe Jazz, NUTA Jazz, Mlimani Park, Maquis du Zaire na Orchestra Safari Sound.

Kamwe hatomsahau John Luanda katika historia ya maisha yake, huyo ndiye aliyekuwa chanzo cha yeye kuingia hapa Tanzania.

Luanda licha ya kuwa mtangazaji wa RTD, alikuwa akimiliki bendi ya Chamwino Jazz.

Aliwachukua toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiwa na wenzake akina Bwami Fanfan, Sisco Lunanga na Baposta kwa madhumuni ya kuimariisha bendi yake ya Chamwino.

Bendi hiyo wakati huo ilikuwa ikipiga muziki maeneo ya Tandale huko Manzese, jijini Dar es Salaam.

‘Vumbi’, mwaka 1980 alikutana na mwanamuziki Chimbwiza Nguza Mbangu ‘Viking’ katika ofisi za ubalozi wa Kongo hapa nchini.

Nguza wakati huo alikuwa mpiga gita la solo pia alikuwa ni mmoja kati ya wanahisa wa Orchestra Maquis Comapy (OMACO) na mmoja kati ya viongozi wa bendi ya Orchestra Maquis du Zaire. Katika maongezi yao, Chimbwiza Nguza alimpa mwaliko yeye na wenzake kwenda kuburudisha kwenye ukumbi wa White House, uliokuwa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Dekula alikubali mwaliko huo na Weekend moja walifika na kupewa nafasi ya kuburudisha kwa muda mfupi.

Walipopanda jukwaani waliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki waliokuwa wamefurika ukumbini humo pamoja na wanamuziki wa bendi hiyo ya Maquis du Zaire.

Dekula Kahanga baadaye aliitwa na uongozi wa bendi ya Maquis du Zaire akina Chibangu Katai ‘Mzee Paul’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Mbuya Makonga ‘Adios’ wakimtaka aandike barua ya kuomba kujiunga na bendi yao kwa mkataba usio na mshahara. Alitakiwa na bendi hiyo ili kuziba nafasi ya Nguza ambaye alikuwa tayari ameanza mgomo baridi. Vumbi alikubali na akajiunga na Maquis du Zaire.

Vumbi anaikumbuka siku mmoja wakipiga muziki katika ukumbi wa Temeke Stereo, alimuona Nguza akiwa amejibanza pembeni mwa ukuta ukumbini humo huku akisikiliza midundo inavyounguruma..

“Nilipomuona, nikaingiwa na hofu kubwa nikijihisi kama ninamvunjia heshima Nguza. Nikaomba nimpishe ili ashike nafasi yake” Anasema kwa kujiamini Dekula Kahanga.

Lakini viongozi wake akiwemo Chibangu Katai ‘Mzee Paul’ na Ilunga Lubaba, walimwamuru aendelee kushika ‘mpini’.

Kwa amri hiyo, ilikuwa kama Fisi aliyeachiwa Bucha kuilinda. Aliweza kuzicharaza kwa umahiri mkubwa nyimbo zote alizokuwa zikipigwa Field Marshal Nguza zikiwemo za Makumbele, Ngalula Seya Malokelee, Karubandika, Mage, Dora mtoto wa Dodoma, Clara, Mwana yoka ya Babote, Nimepigwa ngwala na nyingine nyingi pasipo kutofautisha kati yake na Nguza.

Aliachiwa kulivurumisha gitaa hadi mwisho wa onyesho hata mpiga solo Ilunga Lubaba hakutaka kuligusa siku hiyo. Baada ya hapo kwa adabu zote alikwenda kumsalimia na Nguza pale alipo naye hakusita kumpa hogera kwa kazi nzuri.

“Mungu mkubwa, siku hiyo Nyota yangu iling’ara kiasi kwamba hata mimi mwenyewe sikuweza kuamini nilichokuwa nikikifanya jukwaani hapo” Anasema Dekula Kahanga ‘Vumbi’ huku akitabasamu.

Baadhi ya nyimbo lizoweza kupiga gitaa ni katika nyimbo za Makumbele, Ngalula Seya Malokelee, Karubandika, Mage, Dora mtoto wa Dodoma, Clara, Mwana yoka ya Babote, Nimepigwa ngwala na nyingine nyingi pasipo kutofautisha kati yake na Nguza.

Kabla ya hapo gitaa hilo lilikuwa licharazwa na Nguza Vicking.

Baadae bendi hiyo ilisambaratika na kuzinduliwa upya ikiwa na majina ya Maquis Original. Bendi hiyo ilikuwa ikipiga muziki wake katika kumbi za Wapi Wapi’s Bar pale Chang’ombe, Temeka Kata ya 14 kabla ya kuweka makao yake makuu katika ukumbi wa Lang’ata Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazoezi makali katika bendi hiyo, Oktoba 10, 1989 walirekodi nyimbo za Mashoga, Tipwatipwa, Hali Ngumu, Ossa, Marusu, Mangolibo, Kisebengo na zingine nyingi zote hizo akilicharaza gitaa la solo.

Wakati huohuo Maquis Original aliwapata wanamuziki wengine watatu toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwamo waimbaji Bobo Sukari, Fred Butamu na mcharazaji gitaa la solo Kivugutu Moto na Chacho.

Vumbi wakati huo alikuwa na umri ambao unamruhusu kuhangaika kutafuta maisha yenye maslahi mazuri. Hivyo maamuzi magumu yakaanzia hapo Lang’ata baada ya kuamua kuicha bendi ya Maquis Original, iliyompa jina na kuchepukia katika jiji la Stockholm nchini Sweden.

Kabla haja Akiwa Stockholm, Vumbi alianza kuchacharika mitaani akitafuta bendi ya kupiga, hatimaye akakutana na mwanamuzi toka Uganda, aitwaye Sammy Kasule. Mwaka 1993 wakaamua kuanzisha bendi yao ikiitwa Makonde Group.

Mwaka 1999, Dekula Kahanga alifyatua Album iitwayo Bolingo Ekesemi iliyosheheni nyimbo za ‘Dunia kuna mambo’ na ‘mpenzi Asha’

Dekula Kahanga anajivunia kwamba yeye ni mwanamuziki wa kwanza toka Afrika huko Sweden, kufyatua album. Alitoa album iitwayo ‘Dekula Sultan Qaboos’ yenye nyimbo za Sultan Qaboos, Mon Amour, Babylon, Mayanga, Rozina, Mambo leo na Nostalgie nyimbo hizo anasema zinazopigwa mno katika vituo vingi vya redio Duniani.

Ili kupata unafuu wa maisha nchini Sweden, Dekula alilazimika kuomba uraia wa nchi hiyo hivyo ilifuata taratibu zote.

Alichukua maamuzi magumu mengine ya kuukana uraia wa nchi yake ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ili kupata uraia wa nchi hiyo.

Hivi sasa yeye na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo ni raia halali wa nchi ya Sweden na wanaweza kusafiri kwenda nchi za Marekani Ulaya Asia na kwingineko pasipo kuomba VISA.

Dekula ametoa mwito kwa wanamuziki chipukizi kujifunza kupiga ala za muziki ili wafikie viwango vya kuwa wanamuziki. Pia amewaasa kuacha kulewa sifa ndondogo pia kuepuka anasa zisizo na tija.

“Nawapenda sana Watanzania, walinipokea, wakanilea, wakanithamini na wakanipenda…” alisema Dekula.

Aidha alisema kuwa anatarajia kutoa zawadi endelevu kwa Watanzania siku za usoni kuanzisha bendi ya vijana, itakayokuwa ikitumia ala za muziki wa kisasa.




RASHIDI PEMBE ‘KULI’ MANZESE HADI KUMILIKI BENDI.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.


Mafanikio yoyote ya mwanaadamu hupatikana baada ya kukabiliana na changamoto nyingi, ambazo wengine hushindwa kuvumilia wakaishia kukata tamaa.

Rashidi Pembe ni mmoja kati ya watu waliokumbana na matatizo mengi, likiwemo la kufanya kazi ya ukuli maeneo ya Manzese, jijini Dar es Salaam.

“Kaka usinione hivi, mimi nimebeba mizigo ya abiria wanaotoka Mbeya na mikoa mbalimbali pale Manzese, hadi nikateguka shingo, jamani maisha ni kiboko…”

Haya ni baadhi ya maneno ya mwanamuziki huyo, wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa makala hii, nyumbani kwake Mwananyala, Dar es Saalam.

Pembe alisema hakuna silaha kubwa kwa mwanaadamu kama kutokata tama. Yeye baada ya kusota kwa kipindi kirefu, hivi sasa akiwa na wanamuziki wenzake, wanamiliki bendi yao waliyoipa jina la Orchestra Mark International.

Kufuatia muziki mzuri wa Kimataifa wanaopiga, wamewahi kupata mkataba mnono wa kupiga muziki Ughaibuni, ulioweza kuwafuta ‘jasho’ wanamuziki hao.Pembe alieleza kuwa maisha yake yalianzia baada ya kuzaliwa mwaka 1957, mkoani Pwani.

Baba yake mzee Pembe Rashid, alikuwa mzaliwa wa kijiji cha Kuruwi, tarafa ya Mzenga, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani wakati mama yake Bi. Frida Abel, mzaliwa wa kijiji cha Mihugwe, wilayani humo. Wote walikwisha tangulia mbele za haki.

Katika mahojiano hayo Rashidi Pembe alielezea historia ya maisha yake akisema."Nilianza kusoma shule ya msingi Chanzige iliyoko Kisarawe mwaka 1963, mama alikuwa Daktari, alihamishwa kwenda kuhudumia huku na kule, nasi ndio tulikuwa tukiishi na mama kwani wakati huo alikuwa amekwisha tengana na baba.

Mama alipenda sana nisome, ila baba hakuwa na msisitizo sana wa shule, sijui kwa kuwa alikuwa mbali na sisi, maana huduma ilikuwa kwa mbinde kidogo…”.Mwaka 1966 mama yake alihamishwa toka hospitali ya Kisarawe, akapelekwa hospitali ya Vikindu, nao wakalazimika kuhama kwenda kusoma hapo Vikindu, iliyopo wilaya hiyo ya Kisarawe wakati huo akiwa darasa la Nne.

Pembe alifaulu mtihani wa kuingia darasa la tano, mwaka 1967, akaingia shule ya kati hapo Vikindu. Huko ndiko alikokutana Joseph Benard wakiwa darasa na dawati moja.Joseph Benard ni mwanamuziki anayepuliza saxophoni katika bendi Mlimani Park Orchestra.

Joseph ambaye hivi sasa anaitwa Yusuph Benard, alikuwa ni mpiga filimbi bingwa shuleni kwao. Pembe alitamani sana aweze kupuliza ala hiyo, akamua kumuomba amfundishe.Pasipo kusita Yusuph alimfundisha kupuliza filimbi wakawa wote wapiga filimbi katika bendi ya shule.

“mwana 1968 nikiwa darasa la sita niliugua, mkono ulikuwa haukunjuki sijui ilikuwa ni nini. Hospitali ya Muhimbili waliamua wauvunje, nikakataa, wakanifukuza hosptalini hapo…” alisema Pembe.

Hakutaka mkono wake kuvunjwa halafu uungwe tena, akihofia kuwa atakuwa kilema wa mkono kutokukunja tena.

Kwa mapenzi ya mungu, mkono huo ulikunjuka siku hiyohiyo jioni, baada ya kusota kwa takriban mwaka mmoja. Pembe alikuwa akiugulia kwa maumivu makali, ukiwa umevimba na kwa kipindi chote hicho, alikuwa haendi shuleni.

Mama yake Bi. Frida mwaka huohuo wa 1968, alihamishwa kupelekwa katika hospitali ya Sotele, baadaye tena akapelekwa katika hospitalia ya Kisiju.Baada ya kukosa masomo kwa mwaka mzima, mama yake alimshauri arudie tena darasa la nne, kwenye shule ya Kisiju, ambayo ilikuwa mpya haikuwa na darasa la tano na sita.

Alisema kuwa wakati akiwa mdogo, alipenda sana ngoma, ilikuwa Mdundiko ukipita, mama yake alikuwa akiwaambia dada zake wamkamate.“Walifanya hivyo kwa kuwa nilikuwa naifuata ngoma ya Mdundiko nisijue waendako, mwisho wake nikuwa napotea” alisema Pembe

“mimi sikuwa napenda shule kabisa, kwenda ilikuwa hadi kwa viboko, kila siku nilipambana na mama hadi nilipomaliza darasa la saba mwaka 1972” alisema.Rashid Pembe hakuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, hivyo mama yake alimpeleka kwa mjombawe aliyekuwa akiishi Dar es Salaam, akatafute kazi.

Alifanikiwa kupata kazi katika kiwanda cha nguo cha Kilimanjaro Textile, kilichokuwa kinatengeneza Khanga na Vitenge hapo Gongolamboto jijini humo.Mara alipoanza kazi mwaka 1973, aliwekwa kitengo ambacho walikuwa wa wakishughulikia Pamba. Wakawa wanaziba pua kwa vitambaa, ili wasiathirike kutoka katika pamba wanazosindika kwenye mashine.

Pembe akiwa kazini humo, aliwashuhudia vijana wenzake wadogo, wakiwa wameshika mafaili na kuzunguka huku na kule na wengine wakiwa ofisini.
Akatamani kuwa na kazi kama ya hao vijana, ikabidi aulize mbona wale wana kazi nzuri, akajibiwa kuwa wale wamesoma hadi Kidato cha nne.

Nguli huyo akaikumbuka kauri ya mama yake akimsihi asome sana, baadaye ataiona faida yake.Rashidi Pembe akajutia ‘ujinga’ wake wa kutopenda shule, lakini kipindi hicho tayari akafahamu umuhimu wa elimu.

Akaona hakuna njia ya kujikwamua ila kwenda shule, hivyo alimuomba kaka yake amtafutie shule.Kaka yake akampeleka shule ya Ufundi ya Bagamoyo, iliyokuwa inamilikiwa na Umoja wa Wazazi (TAPA) wakati huo, hadi alipohitimu kidato cha nne mwaka 1978.

Wakati akiwa shule, Pembe aliipenda sana bendi ya Safari Trippers, iliyokuwa ikiongozwa na Marijani Rajabu, pale Princes Bar, ilikuwa Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.Akiwa likizo alikuwa akienda kuwaangalia wanamuziki wa bendi hiyo wakifanya mazoezi.

“Mimi nilikuwa nadhani muziki mtu anajuwa kupitia kipaji alicho zaliwa nacho, wala sikufahamu kuwa ni lazima mtu ujifunze. sasa pale nilimshuhudia Abdallah Gama akipiga gitaa huku akiwa na umri mdogo sana.Hata nilipokuwa shule alikuwa tayari nilikuwa na gitaa, jambo ambalo kaka yake aliyekuwa akimsomesha, alikasirika mno akamuamuru aliuze gitaa hilo, Rashid akakataa.

Brother akanifukuza nyumbani kwake, akaamua kwenda kwa dada yake. Lakini shemeji yake naye akamtamkia kuwa hawezi kuishi na watu lukuki nyumbani kwake.Rashidi Pembe akaondoka kwa kaka yake, akawa analala nje ya soko la Kariakoo.

Kuanzia hapo ndipo aliyaona machungu ya maisha ya shida. “nilitamani kufa lakini sikuuza gitaa langu. nilikubali yote, nikaanza kubeba mizigo ya abiria wanaotoka mbeya na mikoa mbalimbali pale Manzese hadi nikateguka shingo. Jamani maisha ni kiboko…” alisema Rashidi Pembe

Alimuamini sana Mungu, akiamuomba amuondoshee yale mateso aliyokuwa akiyapata hadi amalize shule.Wakati huo Kaka yake aligoma hata kumlipia karo ya shule, baba yake akawa anamlipia.

Matokeo yalipotoka, Pembe alichaguliwa kwenda kusomea ualimu wa ufundi chuo cha Mrutunguru kilichopo mkoani Mara, akakataa kwenda huko. Baba yake naye akashikwa na ghadhabu, akamwambia hatamsaidia kamwe kwa lolote lile.

Pembe bahati ilikuwa upande wake, mwaka 1979, alienda kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akitumaini kwamba cheti chake cha ufundi Uashi grade 1, kingempatia kazi. Kumbe JKT ni kujitolea, akatoroka kabla hata namba za jeshi hazijatoka.

Baadaye Jeshi la Polisi walikuwa wanahitaji mafundi waliotoka shule, hapo ndipo cheti chake ‘kilimbeba’, akachukuliwa akawa askari Polisi kwenye bohari kuu ya jeshi hilo, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Rashidi Pembe akiwa hapo ndipo alipokutana na TX Moshi William na Kassim Mapili, ambaye akaamua kumchukuwa ili alijiendeleze kupiga gitaa.

Akaomba kubadilishwa Idara Kikosi cha Ufundi na kuingia bendi ya Polisi.

“kwakuwa nilikuwa kama mwanafunzi wa kuendelezwa, marehemu mzee Mayagilo, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Brass band, aliamua kunipa saxophone, niache gitaa.

Sababu ni kwamba kuna mpiga ala hiyo, mzee Abdul Mwalugembe aliyekuwa anakaribia kustaafu. Hivyo niliingizwa shule ya palepale na kuanza kusoma Nota na kuanza kujifunza saxophone mwaka 1981….” alisema Pembe.

Mwaka 1985 alichaguliwa kwenda kufanya kozi ya cheo cha Coplo huko Zanzibar, ambako alifanya vyema akaweza kutunikiwa cheo cha Coplo.

Pamoja na kupata kazi hiyo ya Polisi, yeye hakuwa akiipenda kazi hiyo, lakini jeshi hilo ndilo limenifikisha hapa alipo, hususan kwa masomo ya muziki ambayo yamenifanya kuwa mwanamuziki kamili.

Aprili 1987 Rashidi Pembe ‘aliitosa’ kazi ya Polisi, akaamua kujiunga na bendi ya Vijana Jazz, ambako alipiga muziki hadi mwaka 2005, alipoamua kuacha.Nguli huyo akachukuliwa na Samba Mapangala, mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwenda katika ziara zake za Afrika.

Pembe alipofika mwaka 2006, alimuomba Mapangala aachane naye, akakubaliwa.Alifikia uamuzi huo baada ya kujikuta alikuwa tayari ameutumikia muziki kwa takriban miaka 26, hakuyaona mafanikio yeyote.

Wakati huo kuna baadhi ya wanamuziki waliokuwa wameunda bendi ya Orchestra Mark International, iliyoanzishwa kwa ajili ya kupiga muziki katika hoteli mbalimbali.Pembe akaungana nao, wakaanza kupiga muziki karibia hoteli zote kubwa jijini Dar es Salaam.

Bendi hiyo ya Orchestra Mark International, iliwahi kupata mkataba mnono, uliowapeleka nchi nyingi za Ulaya, zikiwemo za Ujerumani, Misri, Ufaransa na Sweden, ambako walikuwa wakipiga muziki kwa mkataba katika Meli ya Kitalii katika jiji la Stockholm.

Rashidi Pembe hadi sasa anakula ‘bata’ , katika bendi hiyo ambayo wakati wowote alisema itakwenda Ughaibuni kupiga muziki kwa mkataba wa kueleweka.Gwiji huyo alitamka kuwa amekumbana na changamoto nyingi alizokumbana nazo.

“maisha ya muziki ni magumu sana hasa kutokana na mpangilio wa haki za muziki na wanamuziki wa Afrika ni tatizo kubwa ambalo hakuna udhibiti, kitu ambacho ni kigumu kwa maisha yetu sisi wanamuziki…” alisema Pembe.

Kila la heri, songa mbele licha ya changamoto utakazo kumbana nazo. Usiache kukiendeleza kipaji cha muziki alichonacho binti yako.

Mwisho.

Mwandishi wa makala anapatikana kwa namba: 0713331200, 0767331200, 0784331200 na 0736331200.

WEMA SEPETU ASIYEFUTIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NCHINI.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.


Jina la Wema Sepetu ni maarufu lililojitokeza hususan baada ya kushiriki na kushinda mashindano ya Miss Tanzania ya mwaka 2006.

Aliongeza umaarufu zaidi baada ya kujikita katika tasnia ya maigizo katika filamu mbalimbali.

Pamoja na sifa zote hizo, Wema Sepetu amekuwa nyota asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii kila mara.


Kabla ya hapo hakuwahi kufikiria katika maisha yake kama angekuja kuwa mmoja kati ya ma-star wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje.

Wema ilitokea mpaka siku mmoja akiwa kwenye matembezi yake Slypway Masaki, alikutana na dada Mange Kimambi.Kimambi baada ya kumuona Wema Sepetu alivyo, akamshawishi kushiriki katika mashindano ya Miss Tanzania.

Wema aliukubali ushawishi huo akaamua kushiriki shindano hilo, ambapo aliibuka kidedea akawa Miss Tanzania mwaka 2006, akawagalagaza Jokate Kidote Mwegelo na Lisa Jensen.

Wasifu wa mlimbwede huyo unaeleza kuwa alizaliwa Septemba 28, 1988 akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne wa marehemu Balozi Isack Abraham Sepetu.

Balozi Sepetu alikuwa Mnyamwezi wa toka mkoani Tabora, aliyehamia Zanzibar miaka mingi ya nyuma.Wakati wa uhai wake Balozi Sepetu aliwahi kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo za Uwaziri na Ubalozi wa Tanzania nje ya nchi.

Mama Wema alikuwa ni mke wa pili, wa kwanza alikuwa mama Amani.
“Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu.
Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana familiya yake.

Dada yangu wa kwanza yuko Marekani anafanya kazi, amejaaliwa kupata mtoto mmoja. Wa tatu yuko huko huko Marekani anasoma na anafanya kazi” alisema Wema.

Wema alianza elimu ya msingi na hadi sekondari katika shulemoja pekee, iitwayo ‘Academic International’ iliyopo maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Pamoja na yote hayo, binti huyu amelelewa na kuishi kama mtu wa Magharibi (Ulaya).

Wema Sepetu ni mwanamitindo, mjasiriamali na mwigizaji wa Bongo movie kutoka nchini Tanzania.

Kabla ya kuwa Miss Tanzania, alikuwa na mwandani wake japo hakuwa super star.Hawakudumu katika mahusiano yao kwakuwa mara baada ya kushikilia taji la Miss Tanzania, Wema alikuwa na majukumu mengi yaliyokuwa yakimkabiri.

Jambo lililomfanya akose muda wa kukutana na mwandani wake huyo, lakini ni kipindi hicho ambapo alikutana na Steven Kanumba, wakaanza uhusiano mara moja.

Uhusiano wao ulikwenda vizuri, nyota zao zote zikang'aa sana.
Kanumba sasa akaonekana Kanumba wa ukweli, si yule wa kwenye maigizo ya kikundi cha Kaole tena.Wakashirikiana kutengeneza filamu zilizokuwa na ubora wa hali ya juu, zilizozidisha umaarufu wao mara dufu.

Hakuna ubishi kwamba Kanumba ndiye aliyegundua kipaji cha Wema Sepetu, pia ndiye aliyemuibua katika sanaa ya maigizo.Wema kwa sababu alizokuwa nazo mwenyewe, alimsaliti Steven Kanumba, akapata ‘mshikaji’ mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Jumbe.

Tabia za Jumbe hazikuwa nzuri kwa jamii, alikuwa akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, yaliyopelekea hadi kuswekwa rumande.
Juhudi kubwa alizifanya mama yake Wema kumnasua binti yake mikononi mwa Jumbe.

Heka heka za Wema wa Sepetu hazikuishia hapo akajikuta yuko mikononi mwa mwanamuziki Chalz Baba.Wazazi wa Wema baada ya kaona binti yao anapamba magazeti kwa habari mbaya, wakaamua kumpeleka nchini Marekani kwa mmoja wa dada zake, wakiwa na matumaini ya kubadilika kitabia.

Akiwa huko alikuwa anachati na watu kwa kutumia mitandao ya kijamii, chating ya kwanza ya Wema na Diamond ilikuwa kwenye Facebook.
Baadaye Wema Sepetu alirejea nchini akapanga nyumba na kumkaribisha mpenzi wake mpya Diamond Platnumz, wakaanza maisha ya pamoja kwa raha na mstarehe.

Baadhi ya watu walipigwa na butwaa kila mmoja akilalama kwanini Wema anamchukua mtu kama Diamond, asiye na mbele wala nyuma na mengi mabaya juu yao.

Ujasiri wa Wema uliweza kukomaza penzi lao baada kuweka pamba masikioni kwa yasemwayo na watu.Alitaka kudhihirisha kuwa Naseeb Diamond aliyempenda yeye, ni ‘Almasi’ ambayo inang'aa duniani kote.
Wakati huo Diamond Platinum alishatoka na nyimbo zake kama mbili hivi kali moja wako wa Mbagala.

Lakini hakuwa juu kiasi hicho na bila Wema. Yaelezwa kuwa Diamond angebakia kama wasanii wengine wanatesa na nyimbo kali ila nyota hazing'ai kivileee Ben Pol, Chid Benzi Barnaba na wengineo.

Wema Sepetu hakuona soni kuonesha pendo lake kwa Diamond popote wawapo, alidiriki kumpa mabusu mbele ya kadamnasi, maneno ya watu hayakuwastua wakazidisha mapenzi mara dufu.

Ndipo watu wakaanza kumuona Diamond akiwa katika muonekano wa pili, aling'aa sana akawa na swaga za Wema, Kiingereza kidooogo.

Baadhi ya mwanamke wakatamani wawe kama Wema na Diamond.

Wawili hao wakawa simulizi tamu midomoni mwa watu ukizingatia Wema anavyojua kudeka na kupenda, watu wakachanganyikiwa na mapenzi yao yalivyokuwa yamenoga.

Wema alimpenda kwa dhati Diamond japo alipigwa vita sana na jamii kuwa hafai eti si wa hadhi yake!

Lakini hakuvunjika moyo alimpenda zaidi Diamond nakutufanya watanzania wote na ulimwengu wote kumtambua Diamond na kipaji chake na hadi akaonekana kijana mtanashati, hadi kufikia leo hii amekuwa super star.



Wema aliwahi kuvalishwa pete ya uchumba na

Diamond Platnumz, baadaye uchumba ukapotelea mbali.



Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema kabisa katika filamu A Point of No Return, akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania Steven Kanumba.




Wema Sepetu amezidi kupata umaarufu japo magazeti mengi yakiendelea kumchafua usiku na mchana.

Licha ya fitna hizo, Wema ambaye kama akitamka kuwa leo atakuwa Jangwani ku-perfom, anayetaka kumuona aje, pasipo shaka maelfu ya watu watakusanyika.

Inaaminika kuwa nyota yake imepelekea kila atakaye mshika mkono, naye lazima awe juu na hii si kwa wanaume wake pekee bali hata mashoga zake wa kike mfano halisi ni Snura.


Pamoja na Wema na kusalitiwa mara nyingi na kusemwa vibaya na mashoga zake, bado yuko juu, anamiliki Kampuni yake ya Production inayoitwa Endless Fame.

Pia anakipindi chake ambacho hivi karibuni kinategemewa kurushwa hewani kitakachoitwa Reality Show, anamiliki nyumba na magari kadhaa.

Mlimbwende huyo anajiweza kimaisha na Mungu anazidi kumbariki kwani anajitoa sana kwa watu na mtoaji mzuri wa sadaka.

Kila la heri Wema Isack Sepetu.

Mwisho.

Habari hizi zimeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.

Mwandaaji anapatikana kwa namba: 0784331200, 0713331200, 0736331200 na 0767331200.

Mwakyembe Afunga Mashindano ya FEASSSA

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Arusha

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameyafunga Mashindano ya 19 ya michezo ya shule za Sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (FEASSSA) kwa kuahidi kuwa mwakani timu kutoka Tanzania zitaleta upinzani mkali kulinganisha na mwaka huu.

Akizungumza kwenye sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zilizofanyika leo leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mhe.Mwakyembe amewatahadharisha wenyeji wa mashindano hayo mwakani nchi ya Kenya kuwa wakae tayari kwani timu kutoka Tanzania zitakuja kwenye michuano hiyo kwa kishindo.

Amesema kuwa katika mashindano ya FEASSSA mwakani ambayo yamepangwa kufanyika katika mji wa Kakamega nchini Kenya, timu za kutoka Tanzania zitaleta upinzania mkali kwani zitakuja kwenye mashindano hayo zikiwa zimejiandaa vizuri.

“Napenda kukuhakikisha Rais wa FEASSSA kuwa tutaziandaa timu zetu vizuri ili mwakani ziweze kushinda makombe mengi,” amesema Mhe.Mwakyembe.

Aidha Mhe.Mwakyembe amezitaka timu za nchi wanachama zilizoshiriki mashindano haya kuhakikisha kuwa zinafanya maandalizi ya kutosha kwani bila hivyo zitaendelea kutofanya vizuri.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi Odilia Mushi amesema jumla ya washiriki 3600 wameshiriki mashindano ya FEASSSA, wakiwemo washiriki kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, Zanzibar,Tanzania na nchi ya Malawi walishiriki michuano hiyo kama mgeni mwalikwa.

Amesema michuano ya mwaka huu mbali na kuwashirikisha wanafunzi wa sekondari pia iliwahusisha wanafunzi wa shule za msingi, wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Bi Mushi ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha kuwa kuwa kila mwaka wawashirikishe wanafunzi walio kwenye mahitaji maalum.

“Natoa wito ushirikiano huu ambao tumeuonyesha Afrika Mashariki kwa kuuonyesha kwa wenzetu hawa wenye mahitaji maalum,” amesema.

Ameongeza kuwa michezo hii imefanyika kwa ufanisi mkubwa ambapo kila nchi ilipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao, na kuongeza kuwa changamoto zilizojitokeza mwaka huu zitakuwa kichocheo kwa ajili ya kufanya vizuri katika mashindano ya mwakani.

Naye Rais wa FEASSSA bwana Justus Mugisha amesema kuwa kuanzia mwakani jina la mashindano hayo litabadilika kutoka kuwa FEASSSA hadi FISSA na kuongeza kuwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo zimeongezewa siku moja zaidi ili kutoa fursa kwa wawakilishi wa kila nchi kwenda kwenye utalii wa ndani.

Aidha bwana Mugisha amezitaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa zinafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushiriki mashindano mengine ya FEASSSA kwani bila kufanya hivyo itakuwa ni ndoto kwa timu hizo kushinda michuano hiyo.

Akizungumzia michuano hiyo, bwana Mugisha amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yalikuwa ni magumu kulinganisha na mashindano yaliyopita na hivyo akataka timu ambazo hazikufanya vizuri mwaka huu ziende zikajiandae kwa ajili ya michuano mingine kama hiyo itakayo fanyika mwakani nchini Kenya.

Kabla ya kufunga mashindano hayo Waziri Mwakyembe alipata fursa ya kushuhudia pambano kali la fainali la mpira wa miguu baina ya timu mbili za Uganda.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images