Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

KAMPENI YA KUTOKOMEZA UGONJWA WA VIKOPE YAZINDULIWA MKOANI PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa nchini, yenye idadi kubwa ya wagonjwa wenye vikope(Trachoma) huku wilaya inayoongoza ikiwa ni Mkuranga yenye wagonjwa hao 1,041,wilaya ya Rufiji 191,Kisarawe 243 na Kibiti 207. 

Hayo yalibainika katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa vikope iliyozinduliwa wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliiasa jamii kuachana na imani potofu na badala yake wajitokeze kupima ugonjwa huo ili kuweza kupatiwa matibabu na kuondokana na upofu .

Aidha, alitoa rai kwa viongozi wa kijamii kuwapeleka wagonjwa wenye vikope katika kambi za uchunguzi ili kupatiwa matibabu.

Nae meneja mradi wa IMA WORLD HEALTH, Alex Msumanje akielezea magonjwa yasiyopewa kipaombele aliyataja kuwa ni matende,mabusha,minyoo ya tumbo,kichocho,usubi na trachoma(vikope).

Kaimu mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele wizara ya afya Oscar Kaitaba alisema watu takribani 11,350 wameshafanyiwa urekebishaji wa kope katika wilaya 21.

Alifafanua, aliwaomba wananchi kujitokeza kufanyiwa urekebishaji wa kope zao kwani huduma hiyo ni bure na mradi huu unafanywa katika mikoa 6 ikiwemo Manyara,Lindi ,Pwani Arusha,Mtwara,na Dodoma.

Kampeni hiyo katika mkoa wa Pwani itafanyika kwenye wilaya nne ikiwa ni pamoja na Kibiti,Kisarawe,Mkuranga na Rufiji.



KAMPENI YA TWENDE PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KUZINDULIWA KESHO KIGAMBONI

$
0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni, kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu jamii kuachana na Mila na tamaduni zisizofaa zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mkutano huo uliolenga kuhabarisha umma kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni,kulia ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu Shetta
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal maarufu kwa jina la Shetta akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Taasisi yake ya Shetta Against Women Abuse (SAWA) katika Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Elias Barnaba akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu ushirki wa wasanii katika kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia itakayozinduliwa kesho katika wilaya ya Kigamboni.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi Wetu

Kampeni ya Twende Pamoja Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi inatarajiwa kuzinduliwa kesho jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.kwa lengo la kuunganisha nguvu pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Maendeleo ya Jinsia kutoka Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi wakati wa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja. 

Aidha Bw. Mbilinyi amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi zinazoripotiwa kuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na asilimia 67 ya kesi zinazoripotiwa za ukatili hutokea kwa wanawake na 33 kwa wanaume.

Ameongeza kuwa Serikali imeliona tatizo hilo na kwa kushirikiana na wadau wengine imeandaa kampeni hiyo itakayosaidia kutoa kwa elimu nchini na kubadilisha fikra hasa kwa wanaume na kwa kiasi kikubwa itapunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa kwa asilimia kubwa umasikini unachangia kutokea kwa vitendo vya kikatili kwa wnawake na watoto ingawa pia hata kwa wenye vipato vikubwa na vya kati wanakabiliwa na vitendo vya kikatili.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa tamaduni na mila zenye madhara zimekuwa ni sababu kubwa kwa jamii kuendeleza vitendo vya kikatili kwa kutolea mfano wa mkoa wa Shinyanga katika miaka ya nyuma vitendo vya mauaji ya wazee wenye macho mekundu vilishamiri ikiushishwa na imani za kishirikina.

Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya na Mwenyekiti wa Taasisi ya SAWA Bw. Nurdin Bilal (Shetta) amesema kuwa wao wasanii wameguswa na vitendo vya kukatili kuzidi kuongezeka na wameamua kutumia sanaa yao katika kufikisha ujumbe kwa jamii kuachana na vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

SERIKALI KUHAMISHA KITUO CHA POLISI MBALIZI KUTOKANA NA UFINYU WA ENEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni,akitoka kukagua Kituo cha Polisi cha Mbalizi ambacho Serikali imedhamiria kukihamisha kutokana na ufinyu wa eneo,kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Ulrich Matei.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Ulrich Matei(kushoto),akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua Kituo cha Polisi Mbalizi ambacho serikali imedhamiria kukihamisha kutokana na ufinyu wa eneo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

BAIDU KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA NCHINI CHINA

$
0
0
Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, kwa ajili yakutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadayekuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
Wataalam wa Masula ya film wa kampuni ya Baidu kutoka China wakipata
maelezo kutoka kwa kiongozi wao Prof.Li Kunruonan, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III, wataalam hao wako nchini kwa siki 11 kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Tanzania lengo likiwa ni kujionea na baadaye kuzalisha film na picha ya vivutio hivyo kwa ajili ya mtandao wa Baidu.
Baadhi ya Wataalam kutuka kampuni ya Baidu kutoka China wakicheza
ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
Wacheza ngoma wa Kikundi cha Nimujo wakitoa burudani kwa wageni wa
kampuni ya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.
Mpiga ngoma wa Kikundi cha Nimujo akipiga ngoma kwa wageni wa kampuniya Baidu (hawapo pichani), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege waKimataifa Julius Nyerere Terminal III leo Agosti 22, 2019.

********************

Na. Paschal Dotto-MAELEZO
22-08-2019

Katika Jitihada za kukuza utalii nchini Taasisi iliyopewa jukumu hilo yaani Bodi yaUtalii Tanzania(TTB) ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Nchini China, wamewezesha kampuni ya Beijing Pseacher Business na Baidu kuja nchini kutembelea na badaye kufanya kazi ya uzalishaji wa picha mjongeo(Film) na picha zitakazowekwa kwenye mtando wao wenye wafuasi takribani 700 kwa lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alisema kuwa ujio wa wageni kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii, kwani utawezesha kuwepo kwa mradi mkubwa wa kupiga picha na kutengeneza Film ya vivutio vya utalii Tanzania ambavyo vitatangazwa kwenye mtandao wa Baidu na kuwezesha watalii kutoka China kuja kutalii nchini.

“Tumefanya kazi kubwa kwa kushirikiano na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China, ambapo tumepata kampuni hii waliowasili leo kutembelea na baadae kuja kufanya mradi wa kupiga picha, kutengeneza makala ya vivutio vyetu, vyakula vyetu vya asili, lakini pia watapata fursa ya kutembelea Serengeti, Bonde la Mamlaka ya Ngorongoro, Zanzibar na bagamoyo na badae watafanya mradi huo ambao utaisaidia Tanzania kuliteka soko la utalii la China”, Geofrey Tengeneza.

Tengeneza alisema kuwa wataalam hao 12 kutoka Baidu wamekuja kwa lengo la kuona jinsi gani watafanya mradi huo mkubwa ili kuwezesha uzalishwaji Film, picha za kawaida na kuziweka kwenye mtandao wao ambao unawafuasi wengi na hii itasaidia kukuza soko la utalii wa Tanzania kwa upande wa soko la China.

Aliongeza kuwa leongo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka china na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradi huo wa kampuni ya Baidu.

Kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo, Prof. Li Kunrounan alisema kuwa wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo wa uzalishaji wa film kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa ili kukuza ushirikiano wa Tanzania na China kwenye Sekta ya Utalii.

“tumekuja kujionea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini Tanzania na baada ya hapo tutakuja sasa kufanya film na picha ambazo tutaziweka kwenye mtandao wetu unafuatiliwa na watu zaidi ya milioni 700 nchini China”; alisema Prof. Li Kunrounan.

Prof. Li Kunrounan alieleza kuwa Tanzania ina vivutio vingi sana ikiwemo wanyama, mabonde pamoja na fukwe mbaliambali hayo ni moja ya maeneo ambayo yanahitaji kuitangazwa, lakini pia watu wake ni wakarimu sana

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA VIJANA UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar, wakati wa kuwasilisha Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo,23-8-2019.(Picha na Ikulu).
WATENDAJI mbalimbali wa Idara za Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati ikiwasilishwa Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yao, Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe,. Balozi Ali Abeid Karume, akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, kulia Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Lulu Msham Abdalla na Mshauri wa Rais Sanaa na Utamaduni Mhe. Chimbeni Kheri.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Ndg Amour Hamil Bakari, akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, kushoto Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Bi. Saum Ali Said na Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg. Joseph Kilangi.
MSHAURI wa Rais Masuala ya Sanaa na Utamaduni Mhe Chimbe Kheri akizungumza wakati wa mkutano na Uongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar, kuzungumzia Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo uliofanyika Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Tanzania na BAIDU Kushirikiana Kutangaza Utalii wa Tanzania Nchini China

$
0
0
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza katika
Ugeni wa Wataalam wa Mtandao wa BAIDU (hawapo pichani) katika hafla fupi kuhusunamna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema Jijini Dares Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya TTB Richard Rugimbana akizungmza na wageni kutoka
matandao wa BAIDU (hawapo pichani), katika hafla fupi kuhusu uzalishwaji wa Film yavivutio vya Tanzania iliyofanyika mapema Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki(wa tatu kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Mtandao wa BAIDU katika hafla fupikuhusu namna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapemaJijini Dar es Salaam, wataalam hao wako nchini wa siku 11 kutembelea vivutio nabadaye kuzalisha Film na kupiga picha.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki(wa tatu kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Mtandao wa BAIDU katika hafla fupikuhusu namna ya uzalishwaji wa Film ya vivutio vya Tanzania iliyofanyika mapemaJijini Dar es Salaam, wataalam hao wako nchini wa siku 11 kutembelea vivutio nabadaye kuzalisha Film na kupiga picha.

*****************



Na. Paschal Dotto-MAELEZO
22-08-2019

Kampuni za Beijing Pseacher Business na Baidu toka nchini China wamejikita katika tafiti za hatua za mwisho ili kutengeneza picha mnato na mjongeo(Film)
zitakazowekwa kwenye mtandao wao wenye wafuasi takribani 700, lengo likiwa
kuinua utalii nchini.

Balozi wa Tanzania Nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, katika mahojiano mwishoni mwa wiki, Jijini Dar es salaam, amesema Tanzania ni nchi ya kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki yenye vivutio vingi vya kiutalii, na kwamba ujio wa wageni wanaoongezeka kutoka China ni neema kwa sekta ya utalii.

“Kampuni hizi ni mawakili, yaani Beijing Pseacher Business na Baidu wameanzishaprogramu maalum ya kutangaza vivutio vya utalii duniani na wameamua nchi yakwanza watakayoanza nayo katika kazi hii ni Tanzania”, Alisema Balozi Kairukiambapo tayari wameanza hatua za kuandaa andiko (script).

Hata hivyo Balozi Kairuki alisema kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa ya kwanzakwenye mradi huo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo binadamu wa kwanza kuwepo hapa Tanzania, mbuga kubwa za wanyama na maeneo mazuri ya kupumzikia kama vile fukwe.

Aliongeza kuwa lengo la Bodi ya Utalii, TTB kuhusiana na zoezi hili kutoka China nikuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka China kuja kutembeleaTanzania na pande hizi mbili zinatambua vivutio vitakavyochukuliwa kwenye mradihuo wa picha na itakuwa fursa kubwa kwa Tanzania.

“Hii ni fursa kubwa kwetu kujitangaza katika soko la utalii la China na kufahamikakwa wachina wengi na hatimaye idadi ya watalii kutoka china kuongezeka, tulikuwa tukipata watalii elfu 34 kwa mwaka, lakini program hii inalenga kufikisha watalii elfu 50, ifikapo mwaka 2020 na laki moja mwaka 2025”, Alisema Balozi Kairuki.

Aidha Balozi Kairuki alisema kuwa katika kutekeleza hilo Serikali imejipangakikamilifu huku Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) likiwa katika hatua za mwishokuanzisha safari za moja kwa moja kwenda China.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Utalii,Richard Rugimbana amesema kuwa tukio la uzalishaji wa filamu hiyo kubwa ya vivutio vya utalii Tanzania na baadayekufanikiwa kuiweka kwenye mtandao huo mkubwa litakuwa ni tukio la kihistoria kwa Tanzania na sekta ya utalii kwa ujumla.

“Tukio la leo (alhamisi) ni tukio la kihitoria kwa maana ya kwamba kampuni zakimataifa za Beijing Pseacher Business na Baidu wameamua kuichagua Tanzania kwa Afrika nzima na kuitangaza, kwani ni nchi pekee ambayo wataweza kupata vitu vizuri vya utalii”, Alisema Richard Rugimbana

Richard alisema kuwa mtandao huo wa Baidu una zaidi ya wafuasi milioni 700 kwa hiyo itakuwa ni rahisi kwa vivutio vya Tanzania kuwavuta watalii wengi kwenye soko la utalii wa Tanzania kama uwekezaji.

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUONGEZA FEDHA MPANGO WA TASAF

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (kushoto) akiangalia chungu kilichotengenezwa na wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha zaidi kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania kwa kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mpango huo umeonesha matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya watanzania kiuchumi.
Wanawake wajasiriamali waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, wakiwa na bidhaa za Shanga wakizionesha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (hayupo pichani), katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (kushoto) akiangalia chungu kilichotengenezwa na wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
Wanawake wajasiriamali, waliowezeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, katika katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam, wakishangilia baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (hayupo pichani) kuahidi Benki yake kuongeza fedha katika mpango huo, alipotembelea utekelezaji wake.
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Keko Machungwa, Bw. Uwesu Misanga, akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (hayupo pichani), alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia- WB, Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, na wadau wengine wa maendeleo alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa mpango huo, katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

******************

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Dunia imeahidi kutoa fedha zaidi kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini- TASAF, unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Tanzania kwa kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mpango huo umeonesha matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya watanzania kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 zilizopo Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wakati alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa TASAF awamu ya kwanza na ya Pili katika Mtaa wa Keko Machungwa Kata ya Miburani, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa ameshuhudia mwenyewe wanawake wakiwa wamezalisha bidhaa mbalimbali vikiwemo viatu, vikapu, shanga, mikoba, vyungu, urembo na nguozilizotengenezwa kupitia mpango wa TASAF, jambo linalodhihilisha manufaa yampango huo kwa Kaya masikini katika kukuza uchumi wao.

“Kwa kuwa nawakilisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika Benki ya Dunia,Washngton Marekani, nimejionea kwa macho yangu bidhaa mbalimbalizilizotengenezwa hasa na wanawake, hivyo naenda kupeleka ujumbe huo muhimu ili Benki iweze kuongeza fedha zaidi kwa awamu zingine kwa ajili ya mpango huu wa TASAF kutokana na manufaa yake katika kupunguza umasikini nchini Tanzania”, alieleza Bi. Kabagambe.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Keko Machungwa, Bw. UwessuMisanga, alisema kuwa kuanzia mwaka 2015 hadi Februari, 2019, fedha walizolipwa walengwa wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo lake ni takribani Sh. milioni 86.1.

Alisema manufaa ya mpango huo ni pamoja na upatikanaji wa mahitaji muhimu kama Chakula, kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni na kuhudhuria Kliniki kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka Kaya Masikini.

Mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa kipato kwa walengwa kutokana na biashara ndogondogo zinazofanywa na kaya hizo lakini pia kuboreshwa kwa mahitaji muhimu ya wanafunzi kutokana na ruzuku.

Aidha Bw. Misanga, alibainisha changamoto za utekelezaji wa Mpango wa TASAFkuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali, baadhi ya Kaya kukosa fursa ya kuingia kwenye mpango, uhaba wa maeneo ya kufanyia shughuli za kuongeza kipato na pia uhaba wa mitaji katika vikundi vya wajasiriamali vilivyoanzishwa na Kaya hizo.

Alisema kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali inafanya tathmini namapitio ya mpango kwa awamu ya kwanza ili kuwezesha Kaya zilizoachwa kuingizwa katika mpango huo na pia Ofisi ya Halmashauri ya Temeke Jijini Dar es Salaam, imewaelekeza wanakikundi wa ujasiriamali kuwasilisha mahitaji ya eneo kwa kuzingatia shughuli wanazotaka kufanya ili kutatua changamoto zao.

Baadhi ya wanufaika wa TASAF waliotoa shuhuda zao mbele ya Mkurugenzi huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, wameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwawezesha kujikwamua kimaisha na pia wameomba kuendelezwa kwa mpango huo kwa kuwahusisha watu wengi zaidi na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa elimu kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo waliopo Hospitali ya Mnazi Mmoja

$
0
0

Na Ales Mbilinyi - JKCI

23/08/2019 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeiahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inatoa elimu kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo waliopo Hospitali ya Mnazi mmoja ili wananchi wanaotibiwa katika Hospitali hiyo wapate huduma za kisasa na za utaalamu wa hali ya juu .

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi alipokutana na wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.

Prof. Janabi alisema Taasisi hiyo imekuwa ikipokea wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali hapa nchini zikiwemo za Benjamini Mkapa, Bugando na KCMC ambao walijifunza jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo kwa njia za kisasa na utaalamu wa hali ya juu na baaada ya kumaliza mafunzo yao walikwenda kuyafanyia kazi katika maeneo yao waliyotoka kitu ambacho kimesaidia wananchi kupata matibabu ya moyo yanayoendana na wakati uliopo.

“Umefika wakati sasa uzoefu walionao wataalamu wa afya wa JKCI ukatumika kuwafundisha wataalamu wengine wa afya wakiwemo wa kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja. Kama mtakuwa tayari watumeni wataalamu wenu waje kujifunza kwetu japo kwa kipindi cha miezi mitatu nasi tutawafundisha utaalamu wote tulionao”.

“Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iko tayari kushirikiana na Hospitali ya Mnazi mmoja kwa kutuma wataalamu wake na kufanya matibabu ya pamoja kwa wagonjwa wa moyo wanaotiiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja”, alisema Prof. Janabi.

Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema tangu kusainiwa kwa mkataba wa kupokea wagonjwa kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jumla ya wagonjwa 26 wameshatibiwa katika Taasisi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri.

“Baada ya kusaini mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwishoni mwa mwaka jana tulianza kuwapokea wagonjwa wa moyo kutoka Zanzibar. Hadi sasa wagonjwa 26 wamepata matibabu ya upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na bila kufungua kifua, miaka ya nyuma wagonjwa hawa walikuwa wanapelekwa nje ya nchi lakini hivi sasa wanatibiwa hapa nchini na wataalamu wetu”, alisisitiza Prof. Janabi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo mwenyekiti wa kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la wawakilishi Mhe. Mwanaasha Juma amesema kupitia ziara waliyoifanya katika Taasisi hiyo wameweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika kuhakikisha huduma bora za matibabu ya moyo zinapatikana Zanzibar.

“Ujio wetu hapa utatuwezesha kuendelea kutoa rufaa kwa wagonjwa wa moyo walipo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuja kutibiwa hapa JKCI badala ya kuwapeleka nje ya nchi kupatiwa matibabu ambayo yanapatikana hapa hapa Tanzania. Kama kamati tumeridhika na huduma zinazotolewa kwani tumejionea kwa macho yetu na ni furaha kuwa wagonjwa wetu kutibiwa katika nchi yao kwa mazingira waliyoyazoea,” alisema Mhe. Mwanaasha

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman aliishukuru Taasisi hiyo kwa mapokezi mazuri waliyowapatia na kuahidi wataendelea kushirikiana zaidi katika kuhakikisha wananchi wanapata matibabu mazuri ili watoke hapo walipo na kusonga mbele zaidi katika huduma za matibabu ya moyo.

Mhe. Harusi aliuomba uongozi wa JKCI kuwapeleka mara kwa mara wataalamu wake katika hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kufanya matibabu ya pamoja bila kuchoka ili mafunzo yatakayotolewa yawe na tija kwa wataalamu hao na kwa wananchi waweze kupata matibabu ya kibingwa.
 Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) wa wodi ya  watoto Theresia Tarimo akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar jinsi wanavyowahudumia watoto wanaolazwa katika wodi hiyo.  Kushoto kwa Theresia ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman ambaye aliambatana na wajumbe hao ili kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo. 
 Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wa chumba cha Cathlab Rogers Kibula akiwaelezea wajumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamiii ya baraza la wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  jinsi upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua pamoja na uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo unavyofanyika katika kwa kutumia mtamo wa  Cathlab wakati wa ziara ya wajume wa baraza hilo ya kuona huduma  mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi, Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la wawakilishi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wafanyakazi wa JKCI mara  baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Picha na JKCI


 Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya baraza la wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yao ya kuangalia huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam

NEC yamteua Anna Kajigili kuwa Diwani Viti Maalum Chadema

WAWEKEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI WANACHANGIA ASILIMIA 13 KATIKA GRIDI – MGALU

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akiongoza kikao cha majumuisho kilichohusisha wataalamu wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake, mara baada ya kushiriki kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, jijini Dodoma, Agosti 23, 2019.

………………………………………………….

Na Veronica Simba – Dodoma

Serikali imeendelea kutoa fursa kwa wawekezaji binafsi katika kuzalisha umeme nchini ambapo hadi sasa wanachangia asilimia 13.5 katika gridi ya taifa.

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Aidha, amesema kuwa serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), imetangaza zabuni kwa ajili ya wawekezaji binafsi kuwekeza katika miradi mipya ya kufua umeme, ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 950.

Akifafanua, amesema mchanganuo wa megawati hizo unahusisha umeme jua (megawati 150), upepo (megawati 200) na makaa ya mawe (megawati 600).

Akizungumzia utoaji fursa kwa wawekezaji wadogo wenye nia ya kuzalisha umeme nchini, Mgalu amesema, ili kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji hao, serikali tayari imeandaa sheria na bei elekezi ambazo zilichapishwa katika gazeti la serikali Juni 21, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka ameiambia Kamati hiyo ya Bunge kuwa hali ya upatikanaji umeme nchini ni nzuri ukilinganisha mahitaji yaliyopo kwa sasa na uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Kuhusu hali ya uzalishaji umeme nchini, Dkt Mwinuka amesema hadi kufikia Agosti 6 mwaka huu, uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa katika mfumo wa gridi ya taifa ulifikia megawati 1, 565.72

Aidha, amesema, shirika linamiliki mitambo ambayo haijaunganishwa katika mfumo wa gridi ya taifa yenye uwezo wa kuzalisha takribani megawati 36.176 hivyo kufanya uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini kufikia jumla ya megawati 1,601.896

Ameongeza kuwa, mahitaji ya juu ya umeme katika gridi ya taifa yalifikia megawati 1,116.58 Novemba 30 mwaka jana ikilinganishwa na megawati 1,051.27 zilizokuwa zimefikiwa hadi Juni, 2018.

“Kwa mlinganisho wa uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme na mahitaji yaliyopo, kuna ziada ya wastani wa megawati 300 katika gridi ya taifa. Taifa litaendelea kuwa na umeme wa ziada kutokana na miradi ya ufuaji umeme inayotekelezwa,” amefafanua.

Kikao hicho cha Kamati ya Bunge kimehudhuriwa pia na viongozi na wataalamu mbalimbali wa Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini yake.

Waziri Jafo atangaza rasmi tarehe ya Uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo, ametangaza rasmi siku ya uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa kuwa utakuwa siku ya tarehe 24 Novemba, 2019, uchaguzi utakao fanyika kote hapa nchini.

Waziri Jafo ametangaza siku hiyo Jijini Dodoma, wakati wa mkutano na wakuu wa mikoa wakati wa kuwapa maelekezo na makabidhiano ya nyaraka zinazohusiana na uchaguzi huo amesema ametangaza uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria.

Amesema uchaguzi utafanyika novemba 24, 2019 kuanzia majira ya saa mbili kamili(12:00)hadi saa kumi kamili (10:00) jioni na tayari maandalizi yote tayari yamekamilika kwa ajiri ya uchaguzi huo.

“Tangu kurejeshwa kwa mamlaka za Serikali za Mitaa katika mfumo wa utawala kupitia sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 na sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya Mtaa, Kijiji na Kitongoji”

“Umekuwa ukifanyika katika kila kipindi cha miaka mitano, uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwezi Oktoba mwaka 2014 na hivyo uchaguzi mwingine unatakiwa kufanyika mwaka 2019, na tarehe hiyo ni Novemba 24, mwaka huu” amesema Jafo.

Amesema uchaguzi huu unaongozwa kwa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa katika mamlaka za Wilaya na mamlaka za Miji, kwa mujibu wa matangazo ya Serikali Na. 371, 372 373 na 374 ya mwaka 2019.

Amebainisha nafasi zitakazo gombewa katika uchaguzi huo, “Mwenyeviti wa Kitongoji katika mamlaka za Miji Midogo, kwa nafasi hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji katika mamlaka za Miji Midogo za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 371 la Mwaka 2019)”. Amesema.

Pia wengine ni wenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake) na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji, kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 372 la Mwaka 2019).

Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji (Kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na Wenyeviti wa Vitongoji katika mamlaka za Wilaya.

Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 373 la Mwaka 2019); na

Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wahalmashauri ya Kijiji (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake), Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake) na Wenyeviti wa Vitongoji katika Mamlaka za Miji.

Kwa nafasi hizo, Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2019 (Tangazo la Serikali Na. 374 la Mwaka 2019).

Waziri Jafo amewataka Wakuu wa mikoa kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya uchaguzi huo sambamba na kuhakikisha vifaa vinafika kwa wakati maeneo husika na kuratibu uchaguzi huo, na amebainisha kampeni zitaanza siku saba kabla ya uchaguzi huo.

Akiongea kwa niaba ya wakuu wa mikoa, Mkuu wa Mkoa wa Singida Rehema Nchimbi amesema kama wakuu wa mikoa wamepokea maelekezo yote na wataenda kuyafanyia kazi pamoja na kuhakikisha uchaguzi huo unaenda kama ulivyopangwa na kuhakikisha vifaa vinafika kwa wakati.

Mchezo wa Riadha Watia fora Mashindano ya FEASSSA Jijini Arusha

$
0
0

Baadhi ya wanariadha wa Tanzania walioshinda medali za dhahabu, fedha na shaba wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya riadha ya FEASSSA yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo.

Kocha wa timu ya taifa ya riadha na mshauri wa ufundi wa timu ya riadha ya Tanzania kwenye michuano ya FEASSSA Robert Kalyahe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa riadha kutoka Tanzania leo.


Washindi wa kwanza wa mchezo wa mbio za kupokezana kijiti mita 100 x 4 kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mbio zao leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha

…………………

Na Mathew Kwembe, Arusha

Mashindano ya michezo ya shule za Sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (FEASSSA) imeingia katika siku ya nane leo ambapo mbali na michezo mingine inayoendelea kulifanyika pia mchezo wa riadha ambapo wanariadha kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania walitia fora baada ya kujizolea pointi na medali nyingi katika michuano hiyo.

Hadi michezo hiyo inakamilika leo mchana, timu ya wanariadha kutoka nchini Kenya ndiyo inayoongoza kwenye mashindano hayo kwa upande wa riadha kwa kujishindia jumla ya pointi 345 kufuatia wanariadha wake kupata medali 18 za dhahabu, 9 za fedha na 10 za shaba na jumla kujizoelea medali 37.

Nafasi ya pili katika mchezo wa riadha ilichukuliwa na wanariadha kutoka Uganda ambao walijizolea pointi 316 baada ya kushinda medali 8 za dhahabu, 14 za fedha na 10 za shaba huku wenyeji Tanzania wakiambulia nafasi ya tatu baada ya kupata jumla ya pointi 197 kwa kupata medali 2 za dhahabu, 5 za fedha na 6 za shaba.

Mchanganuo wa matokeo hayo unaonyesha kuwa ushindi wa Kenya umechangiwa na wanariadha wake wasichana kwa wavulana kufanya vizuri katika mashindano hayo ambapo timu yake ya wasichana ilijizolea medali 7 za dhahabu, 4 za fedha, na 6 za shaba na hivyo kujinyakulia pointi 162, huku wanariadha wavulana kutoka nchi hiyo walifanikiwa kupata medali 11 za dhahabu, 5 za fedha na 4 za shaba,

Kwa upande wa Uganda ushindi wao ulitokana na mafanikio ya wanariadha wao wasichana ambao walipata medali 5 za dhahabu, 8 za fedha na 4 za shaba na kujizolea jumla ya pointi 165, huku wavulana walipata medali 3 za dhahabu, 6 za fedha na 3 za shaba

Tanzania kwa upande wao timu yao ilishika nafasi ya tatu kufuatia timu yao ya wasichana kujishindia medali 2 za dhahabu, 2 za fedha na 4 za shaba na jumla kupata pointi 104 huku wavulana kutoka Tanzania walipata medali 3 za fedha na 2 za shaba.

Waliofanikiwa kuiletea medali ya dhahabu Tanzania ni mwanariadha Carreen Philipo kutoka shule ya sekondari ya wasichana Kondoa iliyopo mkoani Dodoma, mwanafunzi wa kidato cha tano ambaye alifanikiwa kushinda medali hiyo baada ya kufanikiwa kurusha tufe umbali wa mita 12.71 na kuwashinda Penina Akoth wa Kenya na Alanyo Catherine wa Uganda ambao walishika nafasi ya pili na tatu.

Medali nyingine ya dhahabu ilitokana na ushindi wa timu ya wasichana ya Tanzania katika mchezo wa kupokezana vijiti mita 100 x 4 ambapo wasichana wanne kutoka Tanzania walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza mbele ya wanariadha wa Kenya na Uganda.

Akizungumzia michuano hiyo Kocha wa riadha wa Tanzania Taratibu Machaku amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yalikuwa magumu kuliko walivyodhani lakini amewasifu vijana wake kwa ushujaa waliouonyesha kwenye mashindano hayo licha ya ukweli kuwa wanariadha wengi wa Tanzania hawatoki kwenye shule za michezo kulinganisha na wanariadha kutoka Kenya na Uganda.

Hivyo Machaku amewataka wadau wa michezo nchini kujenga shule nyingi za kulea vipaji vya michezo nchini ili Tanzania iweze kuwa na timu imara ya kuweza kushindana na nchi za Kenya na Uganda.

Naye Mwanariadha Mathayo Sombi wa Tanzania, Mwanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya vipaji ya Alliance ya jijini Mwanza ambaye alifanikiwa kupata medali 2 za fedha baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio ndefu za mita 10,000 na mita 5,000 alisema kuwa hali ya hewa ya Arusha ilichangia kumuathiri kushinda nafasi ya kwanza na amesema anajipanga mwakani ili aweze kushinda mashindano hayo.

Kwa upande wake Felix Ogwang ambaye ni mwandishi wa michezo kutoka Uganda amesema kwa upande wake ameona vipaji vingi vya michezo kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania lakini kwa maoni yake ameona kuwa kinachowakosesha ushindi wanariadha wa Tanzania ni kuchukulia michezo kama kitu cha ziada cha kufanya baada ya masomo.

Amesema kuwa hali hiyo ni tofauti na Uganda kwani wanafunzi wanaoshiriki michuano mikubwa ya FEASSSA ambao hupewa cheti maalum na wizara ya elimu ya Uganda hupata alama 5 ambazo hujumlishwa kwenye matokeo ya kujiunga na elimu ya juu nchini humo jambo ambalo Ogwang ameliita kama motisha inayowavuta vijana wengi nchini humo kujituma zaidi katika michezo.

Mashindano ya 39 ya FEASSSA yanatarajiwa kukamilika tarehe 25 agosti 2019 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo jumla ya mataifa sita ya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na wenyeji Tanzania yalishiriki mashindano hayo.

Mama Amtahiri Mtoto Kwa Kisu

$
0
0

Na, Editha Edward-Tabora 

Mwanamke mmoja mkazi Wa Goweko wilayani Uyui mkoani Tabora amemtahiri mtoto wake Wa kiume mwenye umri Wa mwaka mmoja na nusu kwa Kutumia Kisu kwa kile anachodai kuwa huwa anawatahiri watoto yeye mwenyewe bila kupata matatizo na huwa anafanya hivyo bila Kutumia ganzi 

Kwa upande wao majirani zake walioshuhudia kitendo hicho walilazimika kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi Goweko ambapo amechukuliwa yeye na mtoto wake na kukimbizwa hospitali Ili kwenda kuokoa maisha ya mtoto Huyo ambaye tayari Alikuwa amevuja damu nyingi hali iliyotishia usalama Wa mtoto

Akiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa Wa Tabora kitete mtoto Huyo amepokelewa na kupatiwa huduma ya matibabu kwa haraka zaidi.
Pichani ni mama Wa mtoto aliyemtahiri mwanae Wa kiume kwa Kutumia Kisu.

NDALICHAKO AZINDUA KITUO CHA UMAHIRI CHA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akimpongeza Makamu Mkuu wa Taasisi ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga baada ya kuzindua Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe (Hawapo pichani) walioshiriki katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako pamoja na wajumbe walioshiriki katika uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakifatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa katika uzinduzi huo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako akijadili jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela Profesa Lughano Kusiluka wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Umahiri cha TEHAMA.
***************



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amezindua Kituo cha umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Afrika Mashariki @ Centre of Excelence for ICT in East Afrika kilichoanzishwa katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST )Arusha, Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa. Ndalichako amesema kituo hicho kilichofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kinalenga kuwajengea uwezo watanzania pamoja na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuleta maendeleo kwa ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya shahada za uzamili “Masters”.
Waziri Ndalichako amesema Mwongozo wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unatambua nafasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya viwanda, uchumi na maeneo mengine akitolea mfano mifumo ya fedha inayotumia TEHAMA inavyotumika afrika mashariki.

“Teknolojia na ubunifu kwa ujumla ni nyenzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na tunapozungumzia uchumi wa viwanda hatuwezi kufanikiwa kama hatutatoa kipaumbele katika teknolojia, lakini pia kama hatuta kuwa makini katika kutumia tafiti na uvumbuzi katika juhudi mbalimbali za maendeleo” amesisitiza Prof. Ndalichako

Waziri Ndalichako amewashukuru wafadhili wa kituo hicho serikali ya Ujemani ambao tayari wametoa kiasi cha Euro Milioni 1.384 ambayo ni takriban Shilingi Bilioni 3.5 za Kitanzania kati ya Euro Milioni 4 thamani ya mradi mzima utakaotekelezwa kwa miaka minne hadi 2021. Aidha amewashukuru washirika wote wa kituo hicho na kuwataka wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo katika kituo cha CENIT@ EA kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa bidii na kuonyesha vipaji vyao ili waweze kupata ujuzi katika fani ambaowataitumia katika kuleta maendeleo katika nchi wanazotoka.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza katika uzinduzi huo, ameishukuru Taasisi ya NM- AIST kwa kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Arumeru katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwa kuanzisha Kituo cha Umahiri cha TEHAMA. Wakati huohuo ameishauri taasisi ya Nelson Mandela kuhakikisha kituo hicho hakiwi cha wanawataalama pekee bali pia huduma zake zisaidie wananchi hasa wakulima katika kuongeza tija katika kilimo na mazao na kusaidia kutoa mbinu bora za kilimo kupitia tafiti zitakazokuwa zikifanyika.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza wa taasisi hiyo, Profesa Lughano Kusiluka amesema kituo hicho ni cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kitakuwa kikifundisha wanafunzi katika ngazi za shahada ya umahiri katika teknolojia ya mambo simu , hasa masuala ya usalama wa matumizi ya simu na mawasiliano. Amesema kwa sasa kimeanza na wanafunzi 27 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Masahariki ambapo Tanzania imetoa wanafunzi 10 kati ya hao.

Naye Meneja Mradi wa Kituo cha Umahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka giZ Simon Hochstein, amesema serikali ya ujerumani itaendelea kufadhili miradi mbalimbali katika Elimu ya Juu na kuwata wataalamu kuandaa maandiko ya miradi ili kupata fedha kama ilivyokuwa katika mradi wa Kituo hicho cha Umahiri.

EMAT yatoa mafunzo kwa wataalam wa magonjwa ya dharura Mbeya

$
0
0
Chama cha Wataalam wa Magonjwa ya Dharura na Tiba Tanzania (EMAT) kimetoa mafunzo kwa wataalam wa magonjwa hayo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalam wa magonjwa ya dharura wa hospitali hiyo ili waweze kutoa huduma za magonjwa ya dharura na kuepusha vifo vinavyosababishwa na kukosekana kwa huduma hiyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Kilalo Mjema amesema mafunzo hayo yaliendeshwa kwa siku nne na yametolewa kwa wataalam wa idara tofauti katika hospitali hiyo.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha watoa huduma kuweza kukabiliana na magonjwa ya dharura na kuzuia vifo vinavyoepukika kwa kupatiwa huduma hiyo, pia ni muhimu kila mtu kufahamu hatua za awali za kusaidia mgonjwa wa dharura,” amesema Dkt. Kilalo Mjema.

Dkt. Kilalo amesema kwamba katika mafunzo hayo watoa huduma wamejengewa uwezo wa kumsadia mgonjwa ambaye amepata mshtuko wa moyo (Cardiac Arrest)

Katika mafunzo hayo, watoa huduma wameshauriwa kuwa na uharaka wa kutambua mgonjwa na aina ipi ya uhuduma ya awali apatiwe kuokoa maisha yake, pia wamejengewa uwezo wa kushirikiana katika utoaji wa huduma kiufasaha
Dkt. Adyson Mpyambala akifanya mafunzo kwa vitendo namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo la kupua kwa kutumia kifaa maalumu cha kusaidia upumuaji kwa lugha ya kitaalamu bag valve mask ventilation.
 Wataalam wa magonjwa ya dharura wakimsikiliza Dkt. Kilalo Mjema wakati akifundisha mbinu mbalimbali ambazo wanapaswa kuzitumia kuokoa maisha ya wagonjwa.


WAKIMBIZI WA BURUNDI WALALAMIKA KUZUIWA NA MASHIRIKA KUREJEA NCHINI KWAO, WAZIRI LUGOLA AAGIZA WAKAMATWE WANAOWEKA VIKWAZO, ASEMA SASA WAKIMBIZI 2000 KUSAFIRISHWA KILA WIKI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumzakatika mkutano wa hadhara na maelfu ya Wakimbizi wa Kambi yaNduta (hawapo pichani) Wilayani Kibondo, Mkoani Kigoma, leo.Lugola aliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini
Burundi, Pascal Barandagiye, ambapo walitembelea katika Kambi za Nduta na Mtendeli mkoani humo, kwa lengo la kuhamasisha wakimbizi kurejea nchini mwao kwa hiari. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo, Pascal Barandagiye akizungumza katika mkutano wa hadhara na maelfu yaWakimbizi wa Kambi ya Nduta (hawapo pichani) Wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma, leo. Waziri huyo aliwaambia Wakimbizi hao, warudi
nchini mwao kwa kuwa sasa nchi hiyo ina amani na ipo tayarikupokea wakimbizi hao waliopo nchini. Lugola aliambatana na Wazirihuyo kutembelea Kambi za Nduta na Mtendeli mkoani humo, kwalengo la kuhamasisha wakimbizi kurejea nchini mwao kwa hiari.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumzakatika Kikao kilichoshirikisha pande tatu, Serikali ya Tanzania,Burundi na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),kilichofanyika katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Wilayani Kibondo,
Mkoani Kigoma, leo. Kikao hicho kilikua na lengo la kuhamasishaWakimbizi wa Burundi warejee nchini mwao kwa hiari. Watatukushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi, PascalBarandagiye. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwaWakimbizi nchini, Sudi Mwakibasi. Picha na Wizara ya Mambo yaNdani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizinchini, Sudi Mwakibasi, wakati alipokuwa anawasili katika eneo lamkutano wa hadhara, Kambi ya Nduta, Wilaya ya Kibondo MkoaniKigoma, leo. Lugola aliambatana na Waziri wa Mambo ya Ndanikutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, ambapo walitembeleakatika Kambi za Nduta na Mtendeli mkoani humo, kwa lengo la kuhamasisha wakimbizi kurejea nchini mwao kwa hiari. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sehemu ya Wakimbizi wa Burundi wakimshangilia Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), alipokuwaanazungumza na maelfu ya wakimbizi hao, katika Kambi ya Nduta,Wilayani Kibondo, Kigoma, leo. Lugola aliambatana na Waziri wa
Mambo ya Ndani kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, ambapowalitembelea katika Kambi za Nduta na Mtendeli mkoani humo, kwalengo la kuhamasisha wakimbizi kurejea nchini mwao kwa hiari.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

********************

Na Felix Mwagara, Kibondo (MOHA).

Baadhi ya Wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaoishi katika Kambi ya
Nduta, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wamesema wanawekewa
vikwazo na kucheleweshwa na baadhi ya watendaji wa mashirika ya
wakimbizi kambini humo wakati wanapoomba kujiandikisha kurejeshwa
kwao.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Waziri wa Mambo ya Ndani na
Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, wakimbizi
hao wamesema wapo tayari kurudi nchini mwao kwa hiari lakini
wanashindwa kujiandikisha kutokana na kukwamishwa na baadhi ya
watendaji wa mashirika hayo.

Mkimbizi wa kambi hiyo, Nzoisa Bhainoje, alisema yupo tayari kurejea
nchini Burundi lakini amefanya juhudi za kwenda eneo la kujiandikisha
kambini hapo lakini hakufanikiwa kutokana na kusumbuliwa akiambiwa
kuwa idadi wanaotakiwa kuondoka imekamilika.

“Nakumbuka nilifika eneo la kuondoka siku ya Jumanne lakini ilishindikana
kujiandikisha kutokana na kukwamishwa, wengi tunataka kuondoka lakini
tunashindwa kuondoka kwasababu tunakwamishwa,” alisema Bhainoje.

Bhainoje aliongeza kuwa, wanaomba watendaji hao wawaruhusu kwa wale
wanaotaka kurejea nchini mwao kwa hiari, lakini kwa wale ambao hawataki
kuondoka wanaweza kubaki kwa mipango yao.

Baada ya wakimbizi hao kutoa kero zao kwa Waziri Lugola na Waziri
Barandagiye, ndipo Lugola aliagiza kufanyika uchunguzi katika kambi hiyo kuwakamata wale wote ambao wanakwamisha wakimbizi hao kurejea nchini kwao kwa hiari.

“Naagiza uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kwa yeyote
atakayehusika anakwamisha zoezi hili la kuwarejesha wakimbizi hawa
ambao wapo tayari kuondoka nchini kwao kutokana na amani iliyopo, awe
Afisa kutoka Wizarani, awe afisa wa shirika lolote, awe yupo hapa kambini,
lazima tutamkamata na kumpeleka mahakamani,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, muda umefika kwa wakimbizi wa Burundi kurudi nchini
mwao, kwasababu zile sababu ambazo zilikuwa zinazuia zoezi la
kuwarudisha kwao wakimbizi hao kwa sasa havipo tena kwasababu nchi
hiyo ina amani.

Alisema Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli imejiridhisha
sababu kubwa iliyowaleta wakimbizi hao wa Burundi nchini ya kutowepo
kwa amani haipo tena na kwamba kwa sasa Burundi ipo salama kiulinzi na
kiusalama pia kisiasa hivyo wakimbizi hao wanapaswa kurudi nchi mwao
wote bila kuwepo kikwazo chochote.

“Wanaosema Burundi haina amani wanaipaka matope nchi hiyo kwani
jambo hilo halina ukweli wowote na Tanzania imefanya uchunguzi wa
kutosha na kujiridhisha kuwa amani ya kudumu ipo nchini humo, Oktoba
Mosi tutaanza kutekeleza mkataba wa pande tatu wa kurudishwa kwa
wakimbizi 2000 kila wiki wa Burundi kwenda nchini mwao”. Alisema Lugola.

Naye Waziri Barandagiye, kwa upande wake alisema Burundi iko tayari
kutekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu ya kuhakikisha wakimbizi
wote wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye makambi mbalimbali ya
wakimbizi mkoani nchini wanarudi Burundi lakini wanashangazwa na
namna Shirika la Kuhudumia Wakimbizi linavyoendesha zoezi hilo kwa kasi
ndogo.

"Tuko tayari kupokea wakimbizi 3000 kila wiki zaidi ya takwimu ya
wakimbizi 2000 iliyotolewa kwenye makubaliano ya pande tatu, maandalizi
na matayarisho ya kupokea wakimbizi hao yapo vizuri na wengi wanaorudi wamekuwa wakipata misaada mbalimbali ikiwemo miradi ya kiuchumi kwa ajili ya kuendesha maisha yao,"Alisema Barandagiye.

Barandagiye amewataka wakimbizi hao kutokubali kudanyanywa na
maneno ya wanasiasa kwamba hakuna amani nchini Burundi lakini kuwa
na tamaa ya kwenda kuishi Marekaani, Canada kuwa huo ni uongo hivyo
wqanapaswa kurejea nchini mwao kwakuwa ipo amani na pia mazingira
yanaruhusu kuppokelewa.

Waziri Lugola na Barandagiye walitembelea Kambi ya Nduta, Wiliyani
Kibondo na Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko mkoani humo, kwa lengo la
kuhamasisha wakimbizi katika kambi hizo kurejea nchini kwao kwa hiari.

AMIN SAMBO ASHINDA UNAIBU MEYA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGAMBONI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri  akizungumza na madiwani katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo leo jijini Dar es Salaam,ambapo amesema wananchi wanao jihusishisha na uharifu waache mara moja
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani ulifanya leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni,Maabad Hojja akizungumza na madiwani  katika mkutano wa baraza la Madiwani wa kuchagua naibu Meya na kamati mablimbali,ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo katika Halmashauri hiyo ambapo,Amin Mzuri  Sambo ameshinda Unaibu Meya.

Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Kigamboni wa kuchagua Naibu Meya  na kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Halmashauri  hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi,elimu na afya,miundombinu ukiendelea.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

OSHA WATOA MAFUNZO KWA MAKAMPUNI,TAASISI NA MASHIRIKA MBALIMBALI ILI KULETA TIJA KATIKA UZALISHAJI

$
0
0
Na.Khadija seif, Michuzi tv.

WAKALA wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) wafanyakazi wanahitaji ongezeko la mafunzo ya mahali pa kazi kwa kiwango Cha hali ya juu nchini.

Akizungumza na waandishi wahabari Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda alipokua akihitimisha mafunzo ya kozi ya Taifa ya usalama na Afya Mahali pa kazi (National occupational safety and Health course-) amesema kozi hiyo imetolewa kwa wiki tatu mfululizo katika ofisi za (OSHA) Kinondoni jijini Dar es salaam.

Aidha,Mwenda amefafanua kuwa jumla ya washiriki 107 kutoka taasisi, makampuni,mashirika na watu binafsi kutoka mikoa mbalimbali kote nchini.

"Kozi hii tulikua tunaitoa mara kwa mwaka lakini kutokana na uhitaji wa mafunzo hayo kuongezeka tumelazimika kutoa kwa awamu nne kwa mwaka,"

Mwenda aliongezea kuwa kimsingi kumekua na mwamko mkubwa sana miongoni mwa taasisi za umma, makampuni binafsi na mtu mmoja mmoja ambao wanafika ofisi za osha kupata mafunzo hayo muhimu kwa ajili ya kuandaa wataalam wa kusimamia masuala ya usalama na Afya katika sehemu za kazi.

Pia ametoa wito kwa wahitimu wa mafunzo hayo kuzingatia na kutumia maarifa waliopata katika kuleta mabadiliko chanya kwenye maeneo ya kazi hususan katika kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza tija katika uzalishaji.Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo amesema ni muhimu sana kwa watanzania wote kuimarisha masuala ya afya na usalama katika maeneo ya kazi.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na Afya  Mahali pa kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya wiki 3 ya usalama Mahali pa kazi na kuwahimiza kutumia maarifa hayo ili kuleta tija katika uzalishaji

Naibu Waziri Dkt Ndumbaro afanya mazungumzo na Mabalozi

$
0
0
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mhe.Yonas Yosef Sanbe Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2019,Baloz Sanbe katika mazungumzo hayo ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna kuganishwa Mkutano wa SADC HAPA 
Mhe. Dkt Ndumbaro Naibu Waziri akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Sanbe walipokutana kwa mazungumzo. 
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akimsikiliza Mhe. Mousa Farhang Balozi wa Iran nchini, walipokutana kwa mazungumzo ofisi ndogo za Wizara jiji Dar es Salaam.Katika mazungumzo yao, waliwili hao walijikita kujadili masuala mbalimbali ya kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili. 
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akisalimiana na Mhe. Mousa Farhang Balozi wa Iran nchini Tanzania 
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akimsikiliza Mhe. Abdelilah Benryane Balozi wa Morocco nchini Tanzania 
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifanya mazungumzo na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane 
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akisalimia na Mhe. Abdelilah BenryaneBalozi wa MoroccoWakati huohuo Mhe. Pro. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke 
Sehemu ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa China wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea 
Mhe. Pro. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki akiwa katika mzungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Agosti 23, 2019 

TAEC YAENDESHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAMLAKA YA MAPATO NCHINI (TRA)

$
0
0



Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini akizungumza na washiriki wa wa mafunzo ya namna ya kujikinga na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mashine ya X-Ray.Picha zote na habari na Vero Ignatus,Michuzi Blog.
Dkt.Remugius Kawala mtafiti mwanadamizi na Mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC.


Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )
Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Nchini Profesa Lazaro Busagala akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano ya namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,

Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )katikati ni mwanadada pekee aliyeshiriki katika mafunzo hayo Devotha Mwenda kutoka TRA Makao makuu Dar es salaam.
Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nchini Profesa Busagala akimkabidhi cheti cha mafunzo hayo Afisa Usalama Mwandamizi Idara ya mambo ya ndani TRA kutoka makao makuu Jijini Dar es salaamMmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kutoka TRA Majid Lema akipokea cheti cha mafunzo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini Profesa Lazaro Busagala.


Albert Mwangila Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam akitoa neno la shukrani mara baada ya mafunzo hayo kukamilika.



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini imeendesha mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini lengo likiwa ni kujua namna ya kujilinda na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo ,kwa kutumi a mashine za X-RAY .

Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini,amesema lengo la nguvu za Atomiki Tanzania ni kuendesha mafunzo ya aina hiyo mara kwa mara, kwani ni muhimu ili kuweza kuhakikisha kwamba wananchi kwa ujumla wao wanakuwa salama kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza kwasababu ya mionzi au Teknolojia ya Nyuklia .

Profesa Busagala amesema kuwa hata katika viwango vya Kimataifa ,Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani International Atomic Energy Agency ( IAEA) linatumia kuwa ni kigezo kimoja wapo kuiweka nchi katika kundi la kuwa salama ikiwa kuuna mafunzo ,amesema kama hakuna mafunzo ni kwamba watu hawana uelewa wa kutosha na mambo yanakwenda bora yaende na watu wanatumia visivyo.

“Kwasababuhiyo pia tunabadilisha kanuni zinazowalinda wananchi kutokana na madhara ya mionzi tayari katika hatua za ndani ya Tume ya nguvu za Atomiki nchini Tanzania tumeshapitisha na tumeshapeleka kwa serikalini,na serikali sasa inaendelea kutumia kwa muda kuzipitia na mwanasheria mkuu wa serikali anazipitia,na zikishwa pitishwa tuweze kuweka mambo vizuri zaidi “Alisema Profesa.

Dkt.Remugius Kawala ni mtafiti mwanadamizi na mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa wale wanaoratibu mashine hizo,pamoja na uelewa wa jamii,na kuripoti namna ya watu wanaokwenda mipakani na Bandarini kutumia hizo mashine na kuwasaidia wadhibiti kuwa na watu ambao wanauelewa wakutumia hizo mashine.

“Mzigo unapoingia nchini kwa mara ya kwanza lazima ukaguliwe kwa mashine,kwahiyo ukiangalia tunamaeneo mengi sana ya hizo check point,bandari,mamlaka mbalimbali nchini,viwanja vya ndege,mahoteli makubwa,ila kwa sasa tumeanza na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na baadae tutaendelea na Mamlaka nyingine Nchini”Alisema Dkt.Kawala.

Dkt Kawala amesema kuwa wanashauri wakati mashine ya Scan ikiwa haijazimwa hawaruhusu mtu kuingiza mkono kwani mionzi inayotoka katika mashine hiyo husababisha baadhi ya seli za mwili kufa japo kuwa hawajui ni kwa kiwango gani kwa wakati huo ,amesema ikiwa inajirudia mara kwa mara kuna uwezekano wa kusababisha madhara mengine kama ya kansa.

“Mashine ikishamulika ule mzigo unatakiwa uache utoke kabisa kwenye mkanda uje uupokelee nje kabisa hata Yule operetta ukimuangalia kwa umakini utaona hawai kukimbilia lile begi,kwasababu kunavidhibiti vinaitwa leedsheets”alisema Dkt.Kawala.

Albert Mwangila ni Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam amesema kuwa mafunzo yalikuwa yakilenga namna ya kutumia mashine bila ya kuleta madhara kwa mtumiaji ,wakati huohuo kuweza kuwalinda wateja pamoja nawageniwanaotembelea ofisi za Mamlaka hiyo .

“ Mashine hizo tulizopatiwa elimu ni kwaajili ya ukaguzi,mashine zinazotoa mionzi ambazo ni X-Ray,na mashine ya kuskani mizigo “Alisema Mwangila.

amesema kuwa wanaishukuru TAEC kwa kuwapatia mafunzo hayo sambamba na mambo mengi ambayo Taasisi hiyo imeyafanya kwaajili yao wakati wa mafunzo,wamekuwa na wataalam tofauti kwa nyakati mbalimbali na wote walikuwa wamebobea katika maeneo yao.

Hata hivyo mafunzo hayo yamefungwa leo huku idadi ya wahitimu wakiwa ni watumishi nane kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA , na mmoja M

eneja usalama kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )

Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>