Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

INTRODUCING : Habari Njema - E.Mbasha ft Bashando (official video)


WAZIRI KABUDI AMUAGA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI Posted: 22 Aug 2019 01:17 PM PDT

$
0
0

Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez iliyofanyika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi katika hotuba yake amempongeza Bwana Rodriguez kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chote akiwa nchini. Aidha, amemshukuru kwa kushirikiana na Serikali na kujitoa kwa dhati katika kuchangia juhudi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali nchini.

Bwana Rodriguez amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini Tanzania ambapo amefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano.
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, anayemaliza muda wake wa kuhudumu nchi wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga
Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Bw. Rodriguez Maratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini 
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakishirikishana jambo  wakati wa hafla hiyo
Bi.Ramla Khamis Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza katika hafla ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akikabidhi zawadi kwa Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wa kuhudumu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi kutoka wizarani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa.

MPANGO WA RC MAKONDA KUWASHUGHULIKIA MATAPELI WA MAPENZI WACHUKUWA SURA MPYA, AWAUNDIA KIKOSI KAZI

$
0
0
Baada ya Mfumo wa Kupokea Malalamiko ya Wananchi dhidi ya utendajikazi wa watumishi wa Umma kuonyesha mafanikio makubwa ambapo hadi sasa umekamilika 99% na unatarajiwa kuzinduliwa Rasmi mwishoni mwa mwezi huu, sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaita tena Wataalamu wa ICT kufika ofisini kwake kwaajili ya Kuunda Mfumo wa Kusajili ndoa zote zilizofungwa kwa lengo la kuwalinda wanawake dhidi ya Wanaume walaghai wenye mchezo wa kutoa ahadi ya kuoa na mwisho wa siku wanaingia mitini.

RC Makonda amesema mfumo huo utasajili ndoa zote zilizofungwa kidini ikiwemo za Kikristo,Kislamu na zile zilizofungwa Kiserikali pamoja na kuchukuwa taarifa za Idadi ya watoto ndani ya ndoa.

Aidha RC Makonda amesema lengo la jitiada zote hizo ni kumlinda mwanamke dhidi ya Matapeli wa Mapenzi ambao wamekuwa na mchezo wa kuwachezea kinadada kwa kuwaahidi kuwa watawaoa na pindi wanapopata kile wanachokitaka wanaingia mitini jambo linalowaumiza wanawake na kupelekea baadhi yao kutaka kujiua, kupunguza ufanisi wa kazi na pia wengine kujikuta wanawachukia wanaume bila sababu yoyote.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema mpango huo pia unalenga kuzilinda ndoa zilizofungwa zisivunjike jambo litakalosaidia ustawi bora wa familia.

Mhe. Makonda amesema Mpango huo haulengi kuwatetea wanawake pekee bali hata wanaume waliowahi kuwagharamikia wanawake kwa kuwasomesha, kuwajengea nyumba, biashara na kuwapatia magari wanayo haki ya kurudishiwa gharama walizotumia.

MKOANI PWANI BADO KUNA MAENEO YA KUTOSHA-NDIKILO

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alipotembelea Mkoa wa Pwani na Kuweka Mawe ya misingi katika kiwanda vitano vilivyopo katika wilaya ya Mkuranga. 

Na Mwamvua Mwinyi Mkuranga
MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ,amesisitiza kwamba Tanzania hususan mkoani Pwani ni salama kwa uwekezaji na amekemea propaganda na uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa kuwa hakuna uwekezaji unaoendelezwa.

Aidha amewaasa ,wawekezaji na wenye viwanda kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA )mkoani hapo ili hali kuongeza pato la mkoa.

Ndikilo alitoa rai hiyo, wakati alipokwenda kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitano vilivyopo wilayani Mkuranga.

"Rais Dkt.John Magufuli amekuwa akisisitiza uwekezaji na ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, sasa akitokea mtu kukwamisha jitihada hizo anakuwa halitakii mema Taifa, :"'Pia mkoa wetu kupitia halmashauri umetenga maeneo hekta 22,937 kwa ajili ya uwekezaji "nawaomba wawekezaji waje kuwekeza ."alifafanua Ndikilo.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wenye viwanda kujali mikataba,haki,maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia sheria pamoja na kuwapa likizo na kuwawekea vitendea kazi .

Awali mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha matofali yenye ubora (Shaffa Ltd) kitongoji cha Kiguza, Suleiman Amour amebainisha ,ujenzi wa kiwanda umeanza 2018 kinatarajia kitakamilika mwaka 2019.

Amour amesema, lengo la mradi huo ni kuongeza wigo katika sekta ya ujenzi ,na ujenzi utagharimu sh.bilioni 15.3 hadi kukamilika ambapo itatoa ajira 200 mradi ukikamilika.

Kwa upande wake, msimamizi usafirishaji wa kiwanda cha super meals (Cool Blue) kilichopo Vianzi, Charles Malini amesema, ujenzi wa kiwanda umegharimu bilioni 2.7, kuna ajira 50 ,kinalisha maji ya kunywa ya chupa kwa matumizi ya majumbani na ofisini ambapo wanazalisha ujazo mbalimbali kuanzia nusu lita hadi lita 18.

Ametaja changamoto zinazowakabili ni kukosa umeme wa uhakika na miundombinu ya barabara isiyo rafiki .

Ndikilo alizungumzia tatizo la barabara na kuwaeleza ,ataangalia namna ya kuingiza hoja hiyo katika kikao cha barabara kijacho ili kiweze kutetea ipandishwe hadhi ihudumiwe na Tanroads.

Meneja wa shirika la umeme-TANESCO wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema tatizo la kukosekana umeme wa uhakika hutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa mara.

Mmuni alieleza, kwa sasa shirika hilo limetenga sh.milioni 261 ili kusaidia kubadili nguzo na nyaya chakavu.

Viwanda vingine vilivyowekwa mawe ya msingi  katika wilaya hiyo ,ni kiwanda kinachozalisha zana za uvuvi Taxtrade T2 Ltd ,cha nyaya za umeme -Plug Ltd na kiwanda cha kutengeneza masufulia cha Maxima.

AGOSTI 23, SIKU YA KUMBUKUMBU YA BIASHARA YA UTUMWA NA KUKOMESHWA KWAKE DUNIANI KOTE

$
0
0
 Leandra Gabriel na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
BIASHARA ya utumwa ilikuwa biashara iliyodhalilisha utu wa binadamu, hasa Waafrika ambao ndio waliotumika kwa kiasi kikubwa katika biashara hiyo. 

Baadhi ya watu Ulaya waliweza kuona madhara mbalimbali yaliyotokana na biashara hiyo hatarishi, na kuamua kuanzisha tapo la kuikomesha. Wengi wao walikuwa watu wa dini waliosukumwa na sababu za ubinadamu.

Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa duniani kote ambayo huadhimishwa kila ifikapo Agosti 23 kila mwaka ili kukomesha biashara hiyo. Nasi kama Tanzania biashara ya watumwa ilikuwepo huko Bagamoyo na maeneo mbalimbali ambapo wanunuzi wa bianadamu walikuwa wakiwanunua binadamu wenzao kwajili ya kuwatumikisha katika kazi.

Baadaye mataifa kama Uingereza yaliongeza bidii katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa, kwa kiasi fulani ukomeshaji wa biashara ya utumwa ulikuwa una manufaa ya kiuchumi kwao, hasa kufuatia matokeo ya mapinduzi ya viwanda yaliyotokea.
Usiku wa tarehe 22 na 23 Agosti mwaka 1971 huko Santo Domingo na Haiti kama ijulikanavyo kwa sasa mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa ile ya kupitia bahari ya Atlantic (Transatlantic slave trade) ulianza.

Kutokana na kupingwa kwake ikatengwa siku maalumu ya kukumbuka kwa kila mwaka na siku hii ya Agosti 23 imelenga kukumbuka huzuni iliyotokana na biashara ya utumwa kwa watu wote.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la elimu, sayansi na teknolojia (UNESCO) Audrey Azoulay, ametoa ujumbe katika siku hii adhimu kwa kuwaalika mawaziri wenye dhamana ya utamaduni katika nchi zote wanachama kuadhimisha Agosti 23, kila mwaka kwa kuwashirikisha wananchi, vijana, wasanii na wataalamu mbalimbali.

Kupitia ujumbe wake ameeleza kuwa siku ya kukumbuka biashara ya utumwa na kukomeshwa kwake kwa mara ya kwanza iliidhinishwa na nchi nyingi zikiwemo Haiti (Agosti 23, 1998) na Goree Senegal (23 Agosti 1999) na matukio mbalimbali ya kitamaduni na midahalo ilifanyika.

Mwaka 2001 Makumbusho ya Mulhouse Textile ya huko Ufaransa walishiriki kwa kuandaa maonesho yaliyojulikana "Indiannes de Traite"

Ili kuendelea kufunza vizazi kuhusiana na biashara hiyo waziri wa utamaduni anawaalika nchi wanachama kuadhimisha siku hiyo kila mwaka katika nchi zao kwa kuandaa midahalo ya wazi na tafiti zilizofanywa na wananchi wa kawaida ili kuinua uelewa kuhusiana na historia tuliyopiyia na kupinga kila aina ya utumwa wa kisasa.

Katika kukumbuka siku hiyo imeelezwa lazima masuala ya ukusanyaji wa taarifa yatupiwe macho na hiyo ni kupitia misafara ya watumwa kwa kuangalia sababu za kihistoria zilizosababisha, njia walizotumia pamoja na matokeo ya biashara hiyo ambayo iliunganisha mabara ya Ulaya, Afrika, Amerika na Caribbean.

Hata hivyo Uingereza ikiwa taifa kiongozi katika biashara hiyo, halafu katika zoezi hilo la kuikomesha, ulisaidia kwa kiasi kikubwa katika ukomeshaji wa biashara hii iliyopitia katika bahari ya Atlantiki na ile ya bahari ya Hindi.

Si mataifa yote yalikubaliana na matakwa ya Uingereza ya kukomesha biashara ya utumwa, hivyo Uingereza ilipata upinzani kutoka kwa mataifa mengine yaliyokuwa bado yananufaika na biashara hii.

MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA APONGEZA MAFANIKIO YA TASAF.

$
0
0
Na Estom Sanga -TASAF 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam. 

Amesema kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

‘’Tumejiridhisha pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha na kuondokana na umaskini wa kipato. 

Kwa Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya Ujasiliamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato chao. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 


Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
 

INTRODUCING;Tell Me By Nessa (OFFICIAL VIDEO ) 2019

SOMA TAARIFA HII MUHIMU KWAKO KUTOKA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA).


Article 1

$
0
0

            
PICHA NAMBA 1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu maamuzi ya Serikali katika utekelezaji wa madeni yanayodaiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa wadaiwa sugu mjini Dodoma.

PICHA NAMBA 2 
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa,   akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Sekta hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mjini Dodoma.
  
PICHA NAMBA 3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi mara baada ya kupokea taarifa  ya Utekelezaji wa Sekta hiyo, mjini Dodoma.
PICHA NAMBA 4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika kikao kilichohusisha uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kamati hiyo, mjini Dodoma.

NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AKUTANA MAAFISA MAZINGIRA WA MIKOA YA TANZANIA BARA JIJINI DODOMA.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Warsha ya Maafisa Mazingira wa mikoa ya Tanzania Bara ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine(aliyekaa) ili aweze kuzungumza na Maafisa hao. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika jijini Dodoma.


Maafisa Mazingira Nchini wametakiwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais ili kuhakikisha Katazo la mifuko ya plastiki linafanikiwa na kutekelezeka vema.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine alipokutana na Maafisa hao kutoka mikoa ya Tanzania Bara katika Warsha iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika ukumbi wa Nyaraka jijini Dodoma.

Alisema kuwa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ina lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wakatazo la mifuko ya plastiki na namna ya kuboresha ushirikiano na uratibu katika hifadhi ya mazingira kwa ujumla.

“Kwa ujumla, katazo la mifuko ya plastiki limeleta sifa na heshima kwa nchi yetu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa. Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi 60 duniani ambazo zimepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Hii ni hatua kubwa na ya kujipongeza kwa dhamira na msimamo wa Serikali katika
kukabiliana na changamoto za hifadhi ya mazingira” alisema Balozi Sokoine.

Aliongeza kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni kuibuka kwa matumizi ya mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa ambayo ni “transparent” na kupelekea mifuko hiyo kuzagaa na kutumiwa kama vibebeo vya kubebea bidhaa. Hivyo basi amewaagiza Maafisa hao wa Mikoa kuanza kufanya ukaguzi kwa kushirikiana na Baraza la Usimamizi wa Mazingira katika mikoa yao waliotoka.

Pia aliwasisitiza kuendelea kujenga uelewa kwa walio chini yao kuanzia ngazi ya
mkoa mpaka ngazi ya chini(kata,Tarafa,vijiji) ili elimu ya katazo la matumizi ya mifuko ya plstiki ifike mpaka ngazi ya chini.

Katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lilianza rasmi tarehe mosi ya mwezi juni 2019, ikiwa ni kufuatia agizo lilitolewa na Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bungeni jijini Dodoma.

Ofisi ya Makamu wa Rais ni wasimamizi wakubwa katika kampeni hiyo ya marufuku ya mifuko ya plastiki.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 53 WA UTOAJI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MSIMU WA MVUA ZA VULI 2019 KATIKA NCHI ZA PEMBE YA AFRIKA

$
0
0
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 53 wa Utoaji wa Utabiri wa Hali ya Hewa wa Msimu wa Mvua za Vuli 2019 “Fifty Third Greater Horn of Africa Climate Outlook Forum” (GHACOF 53) utakao fanyika katika  Hotel ya Kilimanjaro (Hyatt Regency) kuanzia tarehe 26 hadi 28 Agosti 2019 Dar es Salaam.

Lengo la mkutano huo ni kujadili na kuandaa kwa pamoja utabiri wa msimu wa mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi Desemba 2019, pamoja na kuandaa mikakati ya kukubaliana na hali mbaya ya hewa kwa msimu huo kwa kulenga sekta muhimu za kijamii na kiuchumi ambazo ni pamoja na afya, kilimo na usalama wa chakula, maji, nishati n.k.

Mkutano huo utajumuisha nchi za Pembe ya Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Somalia, Ethiopia, Sudan, Sudan ya Kusini, Uganda, Burundi, Rwanda, Djibouti na Eritrea

UONGOZI WA WIZARA YA KAZI,UWEZESHAJI,WAZEE,WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi,Uwesheji,Wazee,Wanawake na Watoto katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 23/08/2019.
Mshauri wa Rais Pemba Mhe.Bi Mauwa Abeid Daftari (kushoto) akichangia wakati wa mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara ya Kazi,Uwesheji,Wazee,Wanawake na Watoto uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe,Shadiya Mohammed Suleiman(kulia) [Picha na Ikulu.] 23/08/2019.
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee (katikati) akichangia wakati wa mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara ya Kazi,Uwesheji,Wazee,Wanawake na Watoto uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiwepo na Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe,Shadiya Mohammed Suleiman.

MWANAFUNZI DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI OSUNYAI JIJINI ARUSHA AKUTWA AMEJINYONGA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Osunyai Elibariki Lekine (12)ambaye ni Mkazi wa Muriet jijini Arusha amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani.

Akizungumza leo Agosti 23,2019 Kamanda wa Polisi mkoani hapa Jonathan Shana amesema mwanafunzi huyo amekutwa amejinyonga jana saa 11 jioni katika mtaa wa FFU uliopo Kata hiyo ya Muriet jijini hapa.

Kamanda Shana amesema mwili huo ulikutwa kwenye nyumba ambayo ujenzi wake unaendelea mali ya Emmanuel Thomas ambaye ni mkazi wa eneo hilo.

Aidha amesema mwili huo ulikutwa unaning'inia juu huku kamba iliyotumika iliyokuwa imefungwa kwenye mbao ya jukwaa linalotumiwa na mafundi ujenzi.

Amesema kwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kufanya upelelezi kuhusu tukio hilo ili kufahamu chanzo halisi cha tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.

MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA YAMPONGEZA RAIS DKT. JOHN MAGUFULI KUWA MWENYEKITI SADC

$
0
0
*Pia yaeleza inavyoshirikiana na nchi za jumuiya hiyo kukomesha dawa za kulevya

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imempongeza Rais Dk.John Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Mbali ya kumpongeza Rais Magufuli, pia Mamlaka hiyo imefafanua kwa kina inavyoshirikiana na nchi za SADC kukomesha biashara ya dawa za kulevya na wanavyosaidiana katika kutoa kinga na tiba kwa walioathirika na dawa hizo.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Michuzi Blog na Michuzi TV, Kamishina wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti  Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Dkt. Peter Mfisi ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa SADC.

"Kabla ya haya mahojiano yetu,sote tunatambua nchi yetu imetoka kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 39 wa SADC.Hivyo nitumie nafasi hii kumpongeza Rais wetu kuwa Mwenyekiti wa SADC.

"Rais wetu ni kiongozi makini na ukweli usio na mashaka nchi za jumuiya ya SADC zitakwenda kule ambako wakuu wa nchi hizo wanataka iende kwa manufaa ya wananchi wote,"amesema Dkt.Mfisi.

Kuhusu ushirikiano kwa nchi za SADC , amesema Tanzania kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekuwa ikishirikiana kwa karibu na nchi za jumuiya hiyo kukomesha biashara ya dawa za kulevya.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri na nchi nyingine za SADC katika kukabiliana na dawa za kulevya, hivyo tumekuwa tukipeana taarifa za kiintelijensia na kuzifanyia kazi,"amesema Dkt.Mfisi.

Akifafanua zaidi katika eneo hilo la ushirikiano na nchi nyingine za SADC, amesema baada ya Mamlaka hiyo kufanikiwa kudhibiti uingizwaji na usambazaji wa dawa za kulevya na kuwepo kwa sheria kali, wanaojihusisha na biashara hiyo wameona kwa Tanzania biashara imekuwa ngumu, hivyo wanatumia nchi nyingine kupitisha dawa hizo.

Amesema baada ya Mamlaka hiyo kudhibiti uingizwaji na usambazaji wa dawa hizo nchini katika viwanja vya ndege na Bahari ya Hindi, wanaojihusisha nayo wanatumia nchi za Afrika Kusini, Msumbiji, Malawi na Zambia kuingiza dawa nchini Tanzania.

"Baada ya kuanzishwa mamlaka hii kumekuwa na sheria kali za kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya, hivyo wachache wanaojihusisha nayo wamekimbia nchini na hata wanaoendelea kuifanya wanatumia nchi za Msumbiji na Afrika Kusini.

"Zikishaingia kwenye nchi hizo sasa ndio wanajaribu kutaka kuziingiza nchini kwa kutumia mipaka ya Msumbiji, Zambia na Malawi ambako nako tumeweka mfumo mzuri wa kudhibiti,"amesema Dk.Mfisi.

Kamishna huyo wa Kinga na Tiba amesema katika kuhakikisha wanashirikiana kukabiliana na dawa za kulevya kwa nchi za jumuiya hiyo tayari Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini kupitia mawaziri husika wameweka mkakati kuanzisha chombo maalumu cha kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

"Ofisi za chombo hicho zitakuwa Msumbiji na 

kila nchi itahusika kuchangia gharama za kukiendesha na wenzetu wa UN-ODC, Umoja wa Ulaya na DA ambacho ni chombo cha kupambana na dawa za kulevya nchini Marekani wameahidi kutusaidia,"amesema Dk.Mfisi.

Kuhusu eneo la tiba na kinga , amesema wamekuwa wakishirikiana vizuri."Tunashirikiana vizuri kwenye eneo la tiba na kinga na mamlaka yetu imekuwa ya mfano kwa nchi nyingine za jumuiya hiyo.Pia tumekuwa tukishirikiana na nchi za Kenya na Uganda ambazo hazipo SADC".

WAZIRI MKUU AAGIZA APELEKEWE TAARIFA ZA UTENDAJI WA DED LINDI

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga ampelekee taarifa za utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Waryoba Gunza baada ya kushindwa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji kata ya Rutamba.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Agosti 23, 2019) wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Rutamba akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo na huduma za jamii mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kumtaka Mkurugenzi huyo atoe maelezo ya namna gani walivyojipanga katika kutekeleza mradi wa maji kwenye kata hiyo ambayo wakazi wake wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji na kushindwa kutoa maelezo.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Lindi, alisema mradi wa kata hiyo unakabiliwa na tatizo la uchakavu wa miundombinu na ukarabati wake unahitaji bajeti sh. milioni 75 ambazo wameziomba kutoka Wizara ya Maji.

Waziri Mkuu amesema miradi yote ambayo gharama zake ziko chini ya sh. milioni 100 inatakiwa itekelezwe kwa kutumia fedha za ndani ya halmashauri husika. “Miundombinu hiyo ilitakiwa iwe imebadilishwa. Mradi wa sh. milioni 75 unaomba fedha wizarani ni uvivu.”

Waziri Mkuu amesema suala la huduma ya maji limewekewa msisitizo na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama karibu na makazi yao.

Waziri Mkuu aliwaambia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Hata, hivyo Waziri Mkuu amewahakikisha wananchi hao kwamba licha ya kuagiza mradi huo wa ukarabati wa miundombinu ya kusambazia maji ufanyike kwa haraka, pia Serikali inatekeleza mradi mwingine wa maji wa Milola ambao ukikamilika maji yatafikishwa hadi Rutamba.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini wahakikishe wanawasimia vizuri watumishi wa umma na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kushindwa kutekeleza majikumu yao ipasavyo.

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ana nia njema ya kuwapa huduma safi wananchi wote hadi wanyonge na ameelekeza wahudumiwe vizuri bila ya ubaguzi. Wananchi kama kuna mtumishi asiyewahudumia vizuri msisite kumtaja kwa sababu Serikali hii haitomvumia.”

Waziri Mkuu asema ni lazima kila mtumishi wa umma anayelipwa mshahara kwa kutumia kodi za wananchi ahakikishe anatekeleza ipasavyo majukumu yake kwani asipofanya hivyo hatokuwa na nafasi ya kuendelea na kufanya kazi ndani ya Serikali.

“Watumishi fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya, ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”

Waziri Mkuu amesema kuwa watumishi wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Amesema watumshi wa umma hawapaswi kukaa maofisini bali wanatakiwa wapange siku nne katika juma kwa ajili ya kwenda kutembelea wananchi hususani waishio maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuwasikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Rutamba, akiwa mkoani Lindi katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutibia wananchi wa Kata ya Rutamba, kwenye mkutano wa hadhara, akiwa mkoani Lindi katika ziara ya kikazi ya siku mbili, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Samwel Gunza, kuhakikisha maji yanatoka katika Kata ya Rutamba, mkoani Lindi, Agosti 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za jamii ambazo zilikuwa zikiwakwaza wananchi zikiwemo za miundombinu ya barabara, tatizo la maji, elimu na afya, lengo likiwa ni kuwawezesha Watanzania wote waishi vizuri.

Awali, akizungumza kwaniaba ya wabunge wa mkoa wa Lindi, Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Lulida alisema wakazi wa kata ya Rutamba wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji licha ya kuwepo kwa vyanzo, hivyo aliiomba Serikali iwasaidie.

Hata hivyo alilalamikia kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira katika maeneo hayo ikiwemo uvamizi katika vyanzo vya maji pamoja na ukataji hovyo wa misitu unaohatarisha kuibuka kwa jangwa, ambapo Waziri Mkuu ameagiza viongozi wa wilaya hiyo kuzishughulikia suala hilo.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAA, AGOSTI 23, 2019.

Deni la JPM la shilingi milioni 5 lalipwa Muhimbili

$
0
0
Deni la shilingi milioni 5 kati ya Shilingi 5,364, 814.2 ambalo Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kulipa ikiwa ni gharama za matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita, leo limelipwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako Bi. Sabina alikuwa akipatiwa matibabu.

Fedha hizo ambazo zimechangwa na wananchi zimewasilishwa MNH na wakili Albert Msando kwa niaba ya wananchi hao.

Bi. Laila Kitwae ambaye ni mtoto wa marehemu Sabina Kitwae Loita alitoa ombi la kusaidiwa gharama za matibabu ili aweze kuchukua mwili wa marehemu mama yake Agosti 11 mwaka huu wakati Rais Magufuli alipotembelea Muhimbili kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo alipokuwa akikabidhi shilingi milioni 5 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru, Wakili Msando amesema kuwa amelipa fedha hizo baada ya kuchangisha katika mtandao wa kijamii na amewataka wananchi kulipa gharama za matibabu kwa kuwa MNH ina mahitaji mengi katika kujiendesha.

“Mimi binafsi kupitia akaunti yangu ya instagram nilihamasisha wananchi ili tuweze kulipa hili deni. Kwanza sababu kuu ya kufanya hivyo ni kuwahamasisha matumizi sahii ya mitandao ya kijamii, pili mheshimiwa rais ni binadamu kama nilivyo mimi na wewe ambaye naye anaguswa kama ambavyo aliguswa na tatizo hili na kuahidi kulipa deni hili, tatu wananchi wafahamu kuwa hospitali kubwa kama Muhimbili ina mahitaji mengi, hivyo wanatakiwa kuchangia huduma za matibabu”amesema Wakili Msando.

Akipokea kiasi hicho cha fedha, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amewashauri wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kusaidiwa kupata matibabu mara wanapohitaji huduma.

“Gharama za matibabu ni ghali, tunapoboresha huduma za matibu gharama ya kutoa tiba zinazidi kuongezeka kwa mfano utakuwa na CT-scan, MRI na kutakuwa na gharama za uchunguzi wa maabara, zote hizi ni gharama na kwa kawaida zinaongezeka hivyo Watanzania wanapaswa kuchangia huduma ili fedha zinazopatikana zitumike kutoa huduma,” amesema Prof. Museru.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea shilingi milioni 5 kutoka kwa wakili Albert Msando ikiwa ni fedha za gharama za kulipa matibabu ya marehemu Bi. Sabina Kitwae Loita. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Museru akitoa ufafanuzi kwa waandishi habari kuhusu deni hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Museru wa MNH.

IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KUTOKANA NA LORI LA MAFUTA KULIPUKA MORO YAFIKIA 101

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IDADI ya watu waliofariki kutokana na janga la moto lililotokea mkoani Morogoro Agosti 10, 2019 baada ya roli la mafuta kulipuka wamefikia 101 huku wengine wakiendelea kupata matibabu pamoja na kufanya mazoezi ya kusimama na kutembea.

Akizungumza leo Agosti 23,2019 jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema kuwa majeruhi mmoja katika ajali hiyo ya moto amefariki dunia alfajiri ya leo.

" Hospitali ya Taifa Muhimbili tulikuwa tumebaki na majeruhi 15, kwa bahati mbaya leo alfajiri ya saa 12:30 majeruhi mmoja mwanaume, Sadick Ismail Mganga amefariki dunia na kufanya idadi ya majeruhi waliobaki hospitalini hapo kufikia 14," ameeleza Aminiel.

Aidha amesema kuwa kati ya majeruhi 14, majeruhi 11 bado wapo katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na wagonjwa watatu wapo wodi namba 22 Sewahaji na wanaendelea na vizuri na matibabu pamoja na mazoezi ya kusimama na kutembea.

Pia amesema kuwa maiti zote zimesafirishwa mkoani Morogoro kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na kuongeza kuwa vifaa na wataalamu wapo wanaendelea kupigania maisha ya wagonjwa hao.

Tunaomba pia tuishukuru Serikali na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na hospitali ya Taifa Muhimbili katika kuhakikisha wagonjwa wetu hawa na wengine waliopo hospitalini hapo wanapata huduma stahiki,"amesema.

Ikumbukwe kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea majeruhi 47 kutoka Hospitali ya Rufaa Morogoro na kwa bahati mbaya majeruhi 33 wamefariki dunia hadi sasa na kufanya idadi ya majeruhi waliobaki kuwa 14.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha 

RC GAMBO ATAKA ZIFUNGWE KAMERA ZA USALAMA KATIKA VITUO VYA UKAGUZI WATALII KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi TV ,Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza kufungwa kamera za usalama (CCTV )katika vituo maalumu vya ukaguzi wa magari ya kusafirisha watalii ili kudhibiti matukio ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani yanayoweza kujitokeza wakati wa ukaguzi.

Gambo ameeleza hayo leo wakati anazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani wa Arusha, wakiwemo wa usalama barabarani katika hafla ya kutunuku motisha kwa askari waliofanikisha kukamata madini yaliyokuwa yakitoroshwa katika mpaka wa Namanga.

Amesema kuwa vituo hivyo ambavyo vimewekwa katika maeneo ya Kikatiti,Engikareti, Makuyuni na Karatu vimeanzishwa maalumu kwa ajili ya kukagua magari yanayosafirisha watalii ,ukaguzi wa vileo kwa madereva pamoja na usalama wa magari .

Amesema kuwa kufungwa kwa kamera hizo kwenye vituo vya ukaguzi wa vituo vya utalii ,kutasaidia kuondoa utata kwa baadhi ya matukio yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa askari wa usalama barabarani.

"Msimamo wa mkoa ni kuhakikisha watalii wetu hawabughudhiwi na trafiki kwani wanachangia kipato kikubwa kwa Mkoa wa Arusha ambapo mkoa wetu unachangia asilimia 86 ya pato la Taifa,"amesema Gambo.

WAUGUZI FANYENI KAZI KWA PAMOJA-DKT CHAULA

$
0
0
Na. Catherine Sungura, Dodoma 

Wauguzi wote nchini wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kuacha tabia za ubinafsi ili kuweza kuwasaidia wananchi wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata huduma bora na kwa wakati. 

Hayo yamesemwa na katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula aliposhiriki kikao cha kuwashirikisha wadau mwongozo wa utoaji huduma kwa kuzingatia utu,heshima na maadili kilichofanyika jijini hapa. 

Dkt. Chaula alisema kuwa taaluma ya uuguzi ni ya wito hivyo wanatakiwa kuzingatia weledi wa fani yao ili kuwa na mafanikio ya utoaji huduma za afya nchini ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wanahitaji msaada wa kuokoa kutoka kwa wataalam hao. 

“Lazima turudishane kwenye mstari ili tuweze kuokoa maisha ya akina mama wajawazito,watoto na wagonjwa wengine ,tujiulize kwanini akina mama wajawazito wanafariki?nyinyi ndio chachu ya mabadiliko katika utoaji wa huduma”.Alisisitiza Dkt.Chaula. 

Aidha, katibu mkuu huyo alisema kuwa katika kutimiza wajibu wa wauguzi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya anatamani kusiwepo na kifo hata kimoja hususani upande wa akina mama wajawazito hivyo inahitajika nguvu ya pamoja na uelewa miongozi mwa wauguzi kote nchini ili ifikapo 2020. 

Mkakati wa kitaifa wa kupunguza vifo wa vitokanavyo na uzazi tanzania imekusudia ifikapo mwaka 2020 kupunguza vifo hivyo kufikia 292 katika vizazi hai laki moja ukilinganisha na mwaka 2015 vya vifo 556 kwa vizazi hai laki moja.

washiriki wa kikao cha wadau cha kuwashirikisha muongozo wa utoaji huduma kwa kuzingatia utu,heshima na maadili ya wauguzi nchini

Bi. Jane Mazigo kutoka baraza la wauguzi tanzania akichangia kwenye kikao hicho.

Aliyekua mganga mfawidhi wa zahanati ya uturo Wilson Chotamganga akielezea jinsi kijiji cha uturo kilivyofanikiwa kuondoa vifo vitokanavyo na uzazi

WAKILI MSANDO AIBEBA AHADI YA RAIS DKT. MAGUFULI, AKABIDHI MILIONI 5/- MUHIMBILI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAKILI wa kujitegemea na Mshauri Msaidizi wa masuala ya kisheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Albert Msando amekabidhi fedha Sh.milioni tano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Fedha hizo zilikuwa ni ahadi ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa ajili ya matibabu ya marehemu Sabina kitwae Loita aliyefariki dunia hospitalini hapo na mtoto wake kushindwa kulipa gharama hizo na hivyo akamuomba Rais msaidie kulipa na Rais alikubali kukulipa gharama hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo Wakili Msando amesema aliamua kutumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuhamasisha ndugu jamaa na marafiki kuchangia fedha hizo.

"Kuna sababu kuu tatu zilizosababisha kuchangiasha fedha hizi ikiwemo kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ya kijamii pamoja kuona mahitaji mengi na ninawasihi wote tutakaoguswa na kuwasaidia wagonjwa tufike Hospitali ya Muhimbili na kuchangia kile ambacho tumejaliwa" ameeleza Wakili Msando.

Pia amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma kufanikisha kupatikana kwa fedha hizo ni kumsaidia Rais ambaye ana majukumu mengi na wanaomlilia ni wengi.

" Rais Magufuli alipokuja Muhimbili kuwaona wagonjwa waliopata ajali ya moto mkoani Morogoro na akakutana na mama aliyempoteza mama yake mzazi na kushindwa kulipa bili ya Sh.milioni tano.

"Aliuambia uongozi wa hospitali "Nidaini mimi" hivyo basi kwa kuwa Rais ni binadamu na ana majukumu mengi hivyo tukaona tulibebe hili" ameeleza Msando.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrance Museru amesema kuwa gharama za matibabu ni ghali sana na ni haki ya kila mwananchi kupata matibabu.

"Ni vema wananchi wajiunge na mifuko ya bima ya afya kwa kuwa watanzania wenye mahitaji ni wengi na tunawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 500 hadi 600 hufutwa kwa mwezi kutokana na hali za kiuchumi za wananchi,"amesema.

Profesa Museru amesema kuwa waliandika barua Ikulu baada ya Rais kuchukua deni hilo na baada ya deni hilo kulipwa leo wataandika barua tena kwenda Ikulu ambayo itaeleza deni lililobaki.

Aidha amemshukuru Msando kwa kuona mahitaji ya hospitali hiyo na kutumia vyema mtandao wa kijamii kuhamasisha wananchi kuchangia gharama hizo za matibabu.
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya taifa Muhimbili profesa. Lawrance Museru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea fedha hizo za malipo kwa matibabu za Sabina Kitwae Loita ambaye alifariki dunia hospitalini hapo zikizochangwa na wananchi na kuwasilishwa na wakili wa kujitegemea na mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa CCM Albert Msando (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.
Wakili wa kujitegemea na Mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Albert Msando (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu za kiasi cha shilingi milioni tano ambazo ni gharama za matibabu ya Sabina Kitwae Loita ambaye alifariki dunia hospitalini hapo kwa Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Profesa. Lawrance Museru leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images