Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

$
0
0

        Na Khadija seif, Michuzi tv
CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke.

Akizungumza na waandishi wahabari Mwenyekiti wa chama hicho Fred sumari (Dile) amesema Ni wakati wa serikali kutambua kuwa kuna vipaji vingi vinazalishwa katika wilaya hiyo .

"Mzee jongo,Rashid Matumla,Joketi Mwegelo,Tmk wanaume,yamoto band pamoja na Mchezaji mpira anaefanya vizuri nchi za nje Mbwana samata wote Ni zao la wilaya ya Temeke,"

Aidha, Sumari ameeleza bila kificho Temeke ndio sehemu peke inayoleta chimbuko la watu maarufu na kuthibitisha Hilo wameamua kuandaa tamasha kubwa la waigizaji wa wilaya ya Temeke lengo ni kuwakutanisha wasanii wote wa wilaya hiyo pamoja na kujenga umoja,mshikamano na nguvu ili kuwapa ushirikiano wasanii chipukizi wenye vipaji.
Kwa upande wake Msanii wa Maigizo Madebe lidai amesema hata serikali inawasahau sana wasanii wa Temeke hasa likija swala la fursa .

"Kwa umoja wetu tumekusanyana na kuandaa tamasha kubwa la kazi za Sanaa linalotarajiwa kufanyika Agosti 25 mwaka huu katika ukumbi wa  harbours club uliopo mivinjeni kurasini,"

Sanajari na hilo lidai ameeleza kuwa kutapambwa na burudani mbalimbali kama kucheza Rede,kukuna Nazi kwa wakina Baba,kuimba,vichekesho pamoja na  filamu fupi itakayochezwa na wasanii elfu 1000 huku  muimbaji mkongwe wa Taarab Patricia Hillary kuupamba usiku huo.

Pia amesema lengo lingine la tamasha  hilo ni kukuza na kunyanyua soko la filamu kwa wasanii na wazalishaji kwa upande wa Temeke.

Dkt Kalemani aendelea kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini

$
0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Uswaya wilayani Igunga wakati alipofika kukagua kazi ya usambazaji umeme kwenye Kijiji hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi umeme katika Kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
Na Hafsa Omar, Tabora.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameendelea na ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo mwaka 2021 linafanikiwa.

Tarehe 21 Agosti, 2019, amekagua kazi hiyo katika Kijiji cha Mwisi, Uswaya na Isenegeja wilayani Igunga ambapo aliwasha umeme katika Kijiji cha Isenegeja.
Aidha, akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti, amesisitiza kuhusu  wananchi kulipia gharama ya shilingi 27,000 tu, na bila kujali aina ya nyumba wanazomiliki.
“ Umeme ndiyo nguzo kuu ya maendeleo,  hivyo nawasisitiza kuchangamkia huduma hii inayotolewa na Serikali ili muweze kujifanyia shughuli mbalimbali za kiuchumi, kama tulivyosema umeme hautachagua nyumba, umeme wa Serikali hii unapelekwa kwa watanzania wote bila kujali masikini, tajiri au mtanzania wa kawaida.”alisema Dkt Kalemani.
Aidha, Dkt Kalemani amewaagiza wakandarasi kuacha tabia ya kuchelewa kuwaunganishia umeme wananchi  “ nimeshasema ni marufuku kuchelewa kuunganishia umeme wananchi,  mtu akishalipia  muunganishie umeme ndani ya siku Saba bila kisingizio chochote.”
Kuhusu hali ya umeme nchini, amesema kuwa, hali ya umeme ni nzuri na endapo kunatokea kukatika kwa nishati hiyo, ni  kwasababu ya hitilafu tena ya dharura ama kwasababu ya matengenezo.
Kwa nyakati tofauti wananchi wa Vijiji hivyo wameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kusambaza nishati ya umeme vijijini na kueleza kuwa itawawezesha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashine za kukoboa nafaka ambapo hapo awali walilazimika kutumia dizeli ili kuziendesha lakini kwa sasa watatumia nishati ya umeme na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

NAIBU WAZIRI MGALU AONGOZA TIMU YA WIZARA NA TAASISI KUWASILISHA TAARIFA KWA KAMATI YA BUNGE

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akiongoza kikao cha majumuisho kwa wataalamu kutoka Taasisi zilizo chini yake, mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dodoma, Agosti 21, 2019. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Haji Janabi.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiongoza kikao cha majumuisho kwa wataalamu kutoka Taasisi zilizo chini yake, mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dodoma, Agosti 21, 2019.
Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika kikao cha majumuisho mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dodoma, Agosti 21, 2019.


Na Veronica Simba – Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, leo Agosti 21, 2019 aliongoza Ujumbe wa wataalamu kutoka wizarani na taasisi zilizo chini yake, kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Taarifa zilizowasilishwa katika kikao hicho ni zinazohusu miradi inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Akiwasilisha taarifa ya shirika lake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio, aliiambia Kamati husika kuwa usambazaji wa gesi asilia majumbani na viwandani umeanza katika maeneo ambayo tayari kuna miundombinu wezeshi. Ametaja maeneo hayo kuwa ni Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

“Uunganishwaji wa wateja mbalimbali umefanyika ikiwemo wa viwandani na majumbani ambao wote hutumia gesi kama nishati mbadala,” alieleza.

Dkt. Mataragio, alitaja viwanda ambavyo vimesambaziwa gesi katika mikoa mbalimbali pamoja na vilivyo mbioni kupatiwa huduma hiyo kuwa ni pamoja na Lodhia Steel, kiwanda cha vigae cha Goodwill, Knauf Gypsum, Shreeji Silicates Tanzania Ltd, LN Future Building Material Co. Ltd, Wuzhoe pamoja na Balstian Group of Companies vya Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kiwanda cha Coca Cola, Polypety, Interchick, Chemi & Cortex, ESTIM Construction pamoja na Hoteli zilizopo maeneo ya Mbezi Beach. Aidha, amesema kingine ni kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara.

Akizungumzia usambazaji wa gesi asilia majumbani, alisema zoezi hilo linaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi na kwamba lengo ni kufikia nyumba za awali 233, Dar es Salaam na 125 Mtwara ifikapo Oktoba mwaka huu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA, Erasto Simon, aliieleza Kamati hiyo ya Bunge kuwa matumizi ya gesi ya kupikia kwa hapa nchini yameongezeka kufikia tani 8,000 kwa mwezi kutoka tani 4,000 kwa mwaka mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Alisema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuboresha biashara na matumizi ya gesi ya kupikia hapa nchini ikiwemo hatua kubwa ya mpango wa kuagiza gesi hiyo kupitia mfumo wa uagizaji kwa pamoja.

“Mfumo huo utasaidia sana katika kupata gharama halisi za uagizaji hivyo kusaidia upangaji wa bei yake nchini, Vilevile, utaongeza ufanisi katika matumizi ya miundombinu ya kupokelea gesi hiyo. Pia, mfumo utasaidia kupungua kwa gharama kutokana na kuagiza kwa pamoja hivyo kupunguza bei yake,” amefafanua.

Kikao hicho ni mfululizo wa vikao vya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini vilivyoanza Agosti 20 na kutarajiwa kukamilika Agosti 24 ambapo Wizara ya Nishati na Taasisi zake zinawasilisha taarifa mbalimbali kuhusu miradi ambayo zinatekeleza.

KIGAMBONI KUENDELEA KUWALIPA FIDIA WANANCHI GEZAULOLE

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Michuzi TV
WILAYA Kigamboni jijini Dar es Salaam imesema inatarajiwa kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wa Gezaulole iliyopo Kata ya Somangila katika mwaka huu mpya wa bajeti ili kuondokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi wa kata hiyo kutokana na malipo hayo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Charles Lawiso wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo ya Kigamboni kililofanyika leo Agosti 22,2019 ambapo pamoja na mambo mengine lilipongezwa kwa ufanisi mzuri katika kuiletea maendeleo manispaa hiyo.

Wakati wa kikao cha baraza hlilo la madiwani, Fransis Masanja ambaye ni Diwani wa Kata ya Somangila alitumia kikao hicho kuuliza swali la kutaka kufahamu ni lini wananchi hao watalipwa fidia zao baada ya maeneo yao kuchukuliwa kwa ajili ya mradi wa upimaji viwanja miaka miwili iliyopita.

Hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema Manispaa hiyo imekuwa ikilipa fidia hizo kwa wananchi hao kila mwaka kwa kadri ambavyo fedha zimekuwa zikipatikana.

Ambapo amesema kwa mwaka huu malipo hayo yataanza kutolewa wakati wowote ikiwa ni baada ya mwaka mpya wa fedha kuanza.

"Taratibu kwa ajili ya ulipaji wa fidia hizo zinaendelea, kilichochelewesha hatua hiyo ni kuanza kwa mpango husika unaohusiana na mwaka huu wa fedha, ila kila kitu kipo sawa matarajio yetu wananachi hao watalipwa fedha zaoo,"amesema Masanja.

Katika hatua nyingine manispaa hiyo imesema changamoto ya kukosekana kwa huduma ya choo katika Shule ya Sekondari Kisota inatarajiwa kutatuliwa karibuni.

Akifafanua kwenye hilo la ujenzi wa choo, Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kigamboni Paskazia Tibalinda amesema wanatarajia kukamilika rasmi kwa moja ya chemba ya choo hicho yanatarajiwa kujulikana Jumatano.

Ameongeza uamuzi uliochukuliwa na Manispaa hiyo ni kumtaka Mkandarasi husika kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo hadi Jumatano vinginevyo manispaa itafanya kwa fedha zake kisha kumakata fedha mkandarasi huyo.

Katika kikao cha baraza hilo, kimeelezwa kutokana na changamoto hiyo wanafunzi wa sekondari hiyo wanalazimika kwenda kujisaidia choo cha shule iliyojirani.

Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni, Maabad Hojja akizungumza na waandhi wa habari mara baada ya kumaliza kwa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilicho fanyika leo kililofanyika leo Agosti 22,2019 jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv).
Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kigamboni,Paskazia Tibalinda akifaafnua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilicho fanyika leo kililofanyika leo Agosti 22,2019.

Mkutano ukiendelea.

VIJANA MKOANI GEITA WAPATIWA ELIMU YA UJASIRIAMALI

$
0
0
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Silas Daudi akitoa mada kuhusu Mpango wa Biashara kwa vijana wanajihusisha na shughuli mbalimbali za biashara na ujasiriamali katika Mkoa wa Geita ikiwa ni awamu ya tatu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 yanayosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baadhi ya Wajasiriamali wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mmoja ya watoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Julius Tweneshe akielezea mada kuhusu taratibu za kufungua kampuni wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya wajasirimali kutoka Mkoa wa Geita wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bw. Halidi Mbwana akitoa mada kuhusu masuala ya utafutaji wa vyanzo vya mapato kwa vijana walioshiriki mafunzo hayo Mkoani Geita.
Baadhi ya Wajasiriamali walioshiriki kwenye mafunzo hayo wakijadiliana kazi kwenye vikundi.
Sehemu ya Sekretarieti wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wawezeshaji wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Geita Agosti 22, 2019.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

WAFANYAKAZI TBL WATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSITIRI WASICHANA WAKATI WA HEDHI MASHULENI

$
0
0
Meneja Ugavi wa TBL, Poul Canute akikabidhi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi kwa Afisa Mwandamizi kutoka taasisi ya Her Africa, Asnath Ndosi Wakati wa hafla hiyo,wengine pichani ni wafanyakazi wa TBL
 Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi (wa tatu kushoto) Akiongea Wakati wa hafla hiyo.
 Maofisa wa taasisi ya Her Africa wakifurahia msaada huo wa kusaidia wasichana kukabiliana na changamoto ya hedhi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.


Na Cathbert kajuna - Kajunason/MMG. 

Wafanyakazi wa kampuni yak Bia Tanzania (TBL Group), chini ya kampuni mama ya kimataifa ya AB InBev, wametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya  kuwasitiri wasichana wanafunzi wanaosoma shule za sekondari kupitia mradi wa kukabiliana na changamoto za hedhi unaoendeshwa na taasisi ya Her Africa.

Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika ofisi za makao makuu ya TBL zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi maofisa kutoka taasisi ya Her Africa na wafanyakazi wa TBL. 

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa msaada huo umetolewa kutokana na michango ya wafanyakazi baada ya  kuguswa  na changamoto ya vifaa vya hedhi mashuleni kwa wasichana, hususani wanaotoka kwenye familia zenye vipato vidogo na kuwapunguzia uwezo wao wa kufaulu vizuri kutokana na wengine kutohudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo.

“TBL tunayo sera ya kujenga ulimwengu maridhawa ambayo inatekelezwa pia na wafanyakazi, ambapo mara nyingi wamekuwa wakijitoa kukabiliana na changamoto za kijamii na sio kwa kutoa pesa tu bali pia wamekuwa wakitoa hata muda wao kushiriki katika kazi za kijamii kama ambavyo wamefanikisha kutoa mchango huu” alisema Mutiganzi.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya  Her Africa  nchini, Salha Kibwana, alishukuru wafanyakazi wa TBL kwa kulipa kuipa umuhimu changamoto ya vifaa vya Watoto wa kike wa sekondari kujisitiri wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi mashuleni, kwa kutoa msaada huo na amewahakikishia kuwa utawafikia walengwa “Nawashukuru kwa kujitoa na nina imani tukizidi kuunganisha nguvu tutafanikiwa kusaidia wanafunzi wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini” alisema.

UONGOZI WA YANGA WATANGAZA KAMATI YA SHERIA NA NIDHAMU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeteua wajumbe tisa watakaouunda kamti ya Sheria na nidhamu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla wa kuunda tume hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Adv Sam  Mapande.

Aidha, wajumbe  ni Cosmas Chidumule, Esther Cheyo, Sharifu Makosa, Benjamin Mgonja na Philipo Bura.

Wengine ni Seleman Jongo na Mary Mavula  ambapo wote kwa pamoja wataunda kamati hiyo itasimamia sheria na nidhamu ndani ya klabu hiyo.

Kwa sasa Yanga inaendelea kuboresha baadhi ya kamati zao ili kuboresha utawala bora ndani ya klabu hiyo.

Timu ya Yanga ina mchezo wa mkondo wa pili wa Klabu Bingwa dhidi ya Township Rollers nchini Botswana siku ya Jumamosi ambapo Yanga inahitajika kushinda mchezo huo au kupata sare ya kuanzia goli 2 na kuendelea ili kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.

DK.SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII NA MAMBO YA KALE

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale anayeshuhulikia Habari Dkt.Saleh Yussuf Mnemo (wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi wakati wa Mkutano wa Wizara hiyo wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale anayeshuhulikia Utalii na Mambo ya kale Dkt .Amina Ameir Issa (kushoto)
Baadhi ya Viongozi mbali mbali katika Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale wakisimama wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipoingia katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar kabla kuanza Mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo.
Baadhi ya Maafisa katika Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na Ungozi wa Wizara hiyo leo katika Mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. [Picha na Ikulu.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA KUHUSU UTEKELEZEJI WA MARUFUKU YA MIFUKO YA PLASTIKI KWA MAAFISA MAZINGIRA WA MIKOA NCHINI

$
0
0

Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa akiongea na Wajumbe wa kikao kinachohusu Katazo la mifuko ya plastiki, kilichoshirikisha Maafisa Mazingira wa Mikoa ya Tanzania kikao hiko kimeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma katika ukumbi wa Nyaraka.
Injinia Joseph Kiruki kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akitoa mada juu ya katazo la mifuko ya plastiki katika kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika jijini Dodoma
Mwanasheria kutoka Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) Bwana Vincent Haule akifafanua jambo wakati wa kikao cha Maafisa ya Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma
Sehemu ya Wajumbe waliohudhsuria kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa wakifuatilia mada kwa makini wakati wa kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI JIJINI DODOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Jijini Dodoma leo Agost 22,2019.

KMC WAAHIDI USHINDI DHIDI YA AS KIGALI LEO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Timu ya KMC inashuka dimbani leo kucheza mchezo wa Mkondo wa pili wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya As Kigali.

Mchezo huo utaanza majira ya saa 9 alasiri katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam .

Mchezo wa kwanza nchini Rwanda uliweza kumalizika kwa suluhu ya 0-0 ambapo KMC inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kuvuka hatua inayofuata.

Kocha Mkuu wa KMC Jackson Mayanja ameahidi ushindi kwa kuwa wachezaji wake wapo imara kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya AS Kigali utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Mayanja amesema mchezo huo wa leo utakuwa wa wazi kwa pande zote na wachezaji wamejiandaa kwa ajili ya  kupata matokeo chanya licha ya kutokuwa na washambuliaji halisi.

"Kuna baadhi ya majeruhi ambao wapo kwetu jambo linalotuumiza, Hatuna mshambuliaji kutokana na majeruhi ukimuangalia Salim Aiyee kwa sasa hayupo sawa ila tumejipanga kufanya vizuri kikubwa sapoti," amesema.

Kikosi cha KMC kitaongozwa na Golikipa mzoefu Juma Kaseja ambapo kwa pamoja wameendelea kujionea kuelekea mchezo wa kesho na wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi na wamewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo huo.


Kwa upande wa As Kigali wao watakuwa na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga na Simba Haruna Niyonzima ambaye kwa sasa anacheza kwenye timu hiyo.

FAROUK SHIKALO AITWA TIMU YA TAIFA KENYA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Benchi la Ufundi la timu ya Kenya limetangaza kikosi cha wachezaji wake kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia  Qatar 2022.

Kenya atacheza mchezo wa kirafiki na Uganda wakati wa mapumziko ya kalenda ya michuano ya Kimataifa

Timu hizo hazina majukumu ya michezo ya awali kusaka nafasi ya kutinga makundi ya Afrika katika kutafuta tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Qatar mwaka 2022

Wachezaji walioitwa ni pamoja Golikipa wa Yanga Faruk Shikalo , Patrick Matasi (St. George SC, Ethiopia ), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya),Timothy Odhiambo (Ulinzi ), Johnstone Omurwa (Wazito,Kenya), Brian Otieno (Bandari, Kenya) na David Owino (Mathare, Kenya)

Wengine ni Hillary Wandera (Tusker, Kenya), Dennis Odhiambo (KCB, Kenya),Lawrence Juma (Gor, Kenya), Nicholas Kipkirui (Gor Mahia, Kenya), Enosh Ochieng (Ulinzi, Kenya), Timothy Otieno (Tusker, Kenya),Michael Olunga (Kashiwa Reysol FC, Japan), Jesse Were (Zesco United, Zambia) na John Avire (Sofapaka, Kenya)

Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania, Burundi na Rwanda zinakabiliwa na michezo hiyo

Tanzania itacheza na Burundi, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa huko Burundi Septemba 02 na marudiano kufanyika uwanja wa Taifa Septemba 08

BENKI YA NMB YAAHIDI KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA GOFU

$
0
0
 Pichani wa tatu kulia ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki



WACHEZAJI wa mchezo wa Gofu zaidi ya 100 wanatarajia kushiriki mashindano ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu huku Benki ya NMB ikiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka.


Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo huwa ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Majeshi ya Wananchi wa Tanzania ambayo hufanyika Septemba 1 ya kila mwaka huu lakini kutokana na ufinyu wa ratiba mashindano hayo yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8 ambayo itakuwa Jumamosi na Jumapili.

Akizungumza jana Agosti 22, 2019 jijini Dar es Saalam kuhusu mashindano hayo Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai amesema mashindano hayo hufahamika kwa jina la CDF NMB 2019 ambao ndio wadhamini wakuu."Siku ya Septemba 1 ya kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya Siku ya Majeshi ya Wananchi Tanzania.Kutokana na ufinyu wa ratiba yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8,"amesema.

Kapten Masai amesema wanatoa shukrani kwa Chama cha Gofu Tanzania kwa kukubali mashindano hayo yawe chini ya usimamizi wa Chama cha Gofu Tanzania na kuongeza zamani yalikuwa ni mashindano ya ndani lakini safari hii yatakuwa mashindano ya wazi.

Amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa gofu kutoka wa ndani na nje ya Tanzania."Pia litajumuisha wachezaji wa kulipwa na wachezaji wa ridhaa.Kutakuwa na wachezaji chini ya miaka 18 na wachezaji kuanzia umri wa miaka 55 na kuendelea,"amesema Kapten Masai.

Ameongeza mwitikio wa mashindano haya ni mkubwa na kusisitiza wachezaji zaidi ya 100 wamethibitisha kushiriki kutoka vilabu mbalimbali vya nchini Tanzania.

"Tunatoa mwito kwa wachezaji wengine watambue mashindano hayo yatafanyika tarehe hiyo na hivyo muda bado upo wa kushiriki,"amesema Kapten Masai.
 
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponziamesema huu ni mwaka wa nne sasa benki hiyo imekuwa ikidhamini mashindano hayo na wataendelea kudhamini mwaka hadi mwaka.

"Benki ya NMB imekuwa ikidhamini kwa zaidi ya miaka minne sasa na tukaona tuendelee kusapoti na tutaendelea kwani benki yetu ni wadau wakubwa wa majeshi yetu.


"Katika mashindano ya mwaka tumetoa Sh.milioni 21 kwa ajili ya kuyadhamini na hatujaishia hapo kwani kwa kutambua umuhimu wa michezo."Pia tumedhamini mashindano ya majeshi yanayoendelea Nairobi nchini Kenya kwa kutoa Sh.milioni 15 ambazo zimetumika kununua vifaa ya wachezaji wetu,"amesema.

Amefafanua hiyo yote inaonesha ushirikiano mkubwa kati ya NMB na majeshi ya Tanzania na wajisikia faraja kuendelea kushirikiana na majeshi yetu.

 Pichani wa pili kulia  ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki

NDIKILO ASHUSHA 'RUNGU' ZITO KAMPUNI YA ULINZI YA ASLO-PA SECURITY LTD,KUFUATI TANI NNE ZA NONDO KUIBWA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ameagiza kampuni ya ulinzi ya Aslo-Pa security service ltd, iliyopewa kazi ya kulinda na mkandarasi katika kiwanda cha Hester Biosciences Africa Ltd, Kibaha,iache kazi hiyo mara moja baada ya kutokea wizi wa nondo tani nne zenye thamani ya milioni kumi.

Aidha ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo, lisaidie kuchunguza suala hilo kwani inaonekana kuna ushirikiano wa wizi baina ya baadhi ya walinzi wa kampuni na wengine .

Akitoa maelekezo hayo ,wakati alipokwenda kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuweka mawe ya msingi katika viwanda 13, Ndikilo ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Pwani ,alielekeza kazi hiyo ya ulinzi ikabidhiwe kwa SumaJkt .

Ndikilo alitoa rai kwa walinzi na mafundi wanaopewa nafasi ya kulinda na kujenga miradi mikubwa kuwa waaminifu na kuacha udokozi na wizi hali inayosababisha hasara na kuchelewesha kukamilika kwa miradi.

Akizungumzia kiwanda cha Hester alisema kinaenda kuondoa tatizo la ukosefu wa chanjo za mifugo nchini kwani ni kiwanda pekee Tanzania.

"Ni gharama kubwa tunapoteza kuagiza chanjo za wanyama nje ya nchi ,sasa kukamilika kwa kiwanda hiki itaokoa gharama kubwa tunazotumia na wafugaji wa mkoa na Tanzania watanufaika kupatikana kwa madawa haya hapa hapa nchini"alieleza Ndikilo.

Alifafanua ,magonjwa ya wanyama yamekuwa yakirudisha nyuma jitihada za wakulima na wafugaji kwakuwa wamekuwa wakikosa fursa ya soko nje ya nchi kutokana na mifugo kuathirika na magonjwa .

Ndikilo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kujitangaza ,kutangaza uzalishaji wa madawa hayo ya wanyama na chanjo ya magonjwa ya wanyama ili kutambulika.

Awali mratibu wa mradi, Tina Sokoine alisema, ujenzi wa kiwanda utagharimu kiasi cha dollar za kimarekani milioni 18, wanatarajia kuajili wafanyakazi 300 na chanjo itakuwa ikitolewa kwa magonjwa 26 ya wanyama .

Alibainisha, ujenzi umeanza mwaka 2019 na utakamilika Jan 2020 ambapo feb 2020 wanatarajia kuanza kuweka mitambo na kuifanyia majaribio na kutoa elimu kwa wafanyakazi.Aliomba waongezwe ardhi hekari mbili kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi ili kuepuka wafanyakazi kukaaa nje ya eneo la kazi.

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama alisema wana maeneo ya kutosha ,ambapo mji wa Kibaha pia kuna hekari 1,246 eneo la Zegereni.

Assumpter alisema wenye mashamba pori na maeneo yaliyotelekezwa ,taratibu zinafanyika kisheria kuwapokonya na serikali itaangalia shughuli za kufanya ikiwemo za uwekezaji.



BENKI YA DUNIA YAPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUTOA KIPAUMBELE KWENYE SEKTA ELIMU

$
0
0
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Kibasila ya Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara katika shule hiyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe.
Walimu wa shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati alipotembelea shule hiyo akiwa na ugeni kutoka Benki ya Dunia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Kibasila wakati alipotembelea shule hiyo. Ameipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila ya Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika shule hiyo akiwa na ugeni kutoka Benki ya Dunia.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ya Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.
Benki ya Dunia imepongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele  kwa sekta ya Elimu na kwamba ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa sana katika kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata nafasi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa jijni dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia ukanda wa nchi za Africa Anne Kabagambe alipofanya ziara katika shule ya Sekondari Kibasila akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Mkurugenzi huyo ametembelea shule ya Kibasila kwa sababu Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi zinazofanywa katika sekta ya elimu ikitambua kuwa elimu ni ndio chimbuko la maendeleo katika yoyote katika nchi. 
Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema Benki ya Dunia imekuwa ikishirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo  ikiwemo mradi wa Elimu unaojulika kama Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo Benki ya Dunia imetoa dola za kimarekani milioni 202 katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2014 na unategemewa kumalizika mwaka 2021.
Waziri Ndalichako amesema kupitia mradi huo takribani Sh bilioni 141 zimeshatumika kwa ajili ya kukarabati shule kongwe 62, kujenga vyumba vya madarasa 2,876, matundu ya vyoo 6,558, nyumba za walimu 59, mabwalo 76, majengo ya utawala 16, Mabweni 533 kwa ajili ya kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za mbalimbali, pamoja na kujenga mifumo ya maji safi kwenye baadhi ya shule ambazo hazikuwa na vyanzo vya maji.
Aidha Waziri Ndalichako alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari Kibasila  shilingi milioni 900 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya ukarabati na tayari wataalamu  wameanza kufanya tathmini ya majengo ya shule hiyo ambayo ukarabati wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa.
Awali akitoa taarifa ya shule Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Yasinta Matilya amesema moja ya changamoto inayokabili shule hiyo ni utoro wa wanafunzi unaotokana na changamoto za kifamilia ikiwemo watoto kulelewa na mzazi mmoja, kipato duni, umbali wa makazi ya wanafunzi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hiyo wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa saikolojia watakaowasaidia kujitambua ikiwa ni pamoja na kuwajengea mabweni ili kuepukana na vishawishi vya barabarani pamoja na usumbufu wa usafiri wa unaopelekea wanafunzi kuacha shule. 







DKT.KALEMANI AENDELEZA KUKAGUA KAZI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Hafsa Omar, Tabora

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameendelea na ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa na nishati ya umeme ifikapo mwaka 2021 linafanikiwa.

Tarehe 21 Agosti, 2019, alikagua kazi hiyo katika Kijiji cha Mwisi, Uswaya na Isenegeja wilayani Igunga ambapo aliwasha umeme katika Kijiji cha Isenegeja.

Aidha, akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti, alilisisitiza kuhusu wananchi kulipia gharama ya shilingi 27,000 tu, na bila kujali aina ya nyumba wanazomiliki.

“ Umeme ndiyo nguzo kuu ya maendeleo, hivyo nawasisitiza kuchangamkia huduma hii inayotolewa na Serikali ili muweze kujifanyia shughuli mbalimbali za kiuchumi, kama tulivyosema umeme hautachagua nyumba, umeme wa Serikali hii unapelekwa kwa watanzania wote bila kujali masikini, tajiri au mtanzania wa kawaida.”alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza wakandarasi kuacha tabia ya kuchelewa kuwaunganishia umeme wananchi “ nimeshasema ni marufuku kuchelewa kuunganishia umeme wananchi, mtu akishalipia muunganishie umeme ndani ya siku Saba bila kisingizio chochote.”

Kuhusu hali ya umeme nchini, alisema kuwa, hali ya umeme ni nzuri na endapo kunatokea kukatika kwa nishati hiyo, ni kwasababu ya hitilafu tena ya dharura ama kwasababu ya matengenezo.

Kwa nyakati tofauti wananchi wa Vijiji hivyo waliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kusambaza nishati ya umeme vijijini na kueleza kuwa itawawezesha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashine za kukoboa nafaka ambapo hapo awali walilazimika kutumia dizeli ili kuziendesha lakini kwa sasa watatumia nishati ya umeme na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi umeme katika Kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Uswaya wilayani Igunga wakati alipofika kukagua kazi ya usambazaji umeme kwenye Kijiji hicho.

WALIOPATA SIFURI MTIHANI WA ‘MOCK’ KIDATO CHA NNE SIMIYU KUWEKWA KAMBI MAALUM YA KITAALUMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu walifanikisha wanafunzi kupata alama A katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2019 katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa wa Simiyu akichangia hoja katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Maafisa Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Maafisa Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), ya kufunga Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
…………………………

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia daraja la nne na kuendelea, katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.

Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019 katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri” alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani 2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI AIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUJENGA RELI YA KISASA KWA FEDHA ZAKE ZA NDANI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe amefanya ziara fupi kuona Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 22, 2019.

Katika ziara hiyo Bi. Anne alipata fursa ya kutembelea Stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa eneo la Stesheni jijini Dar es salaam pamoja na kutembelea eneo la Vingunguti kuona kipande cha reli ya kisasa kilichotandikwa eneo hilo ambapo Bi Anne alionesha kufurashishwa na kasi ya ujenzi.

“Nimekuja kuona hatua kubwa ambayo serikali imechukua ya kujenga reli ya kisasa ninachoweza kusema kwa niaba ya nchi ninazoziwakilisha ni kwamba huu si mradi wa Tanzania pekee bali ni mradi wenye manufaa kwa nchi zilizofungamana katika ukanda huu” alisema Bi. Anne

Aidha Bi. Anne ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kwa kutumia mapato ya ndani pia ameahidi kuwa Balozi kueleza yale aliyoyaona katika Mradi wa SGR

“Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kujenga mradi huu kwa kutumia vyanzo vya ndani" Nitafikisha ujumbe huu juu ya hiki tulichokiona leo” alisema Bi. Anne 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa taasisi za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia zinaweza kukamilisha Mradi huu kwa kuufadhili siku zijazo 
“Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo tutakapokuwa tunatafuta njia za kufadhili mradi huu taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia tutaweza kuja kukamilisha mradi huu” alisema Bi. Anne 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi na Miundombinu ya Reli Mhandisi Felix Nlalio amesema kuwa wameupokea ujio huo kwa furaha na kwa kuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia amejionea mwenyewe kasi ya ujenzi na amefurahishwa na ubora wa wa kazi. 

WALIOPATA SIFURI MTIHANI WA ‘MOCK’ KIDATO CHA NNE SIMIYU KUWEKWA KAMBI MAALUM YA KITAALUMA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau wa elimu katika mkoawa Simiyu katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
 Maafisa Elimu wa Wilaya, kata, wakuu wa shule na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika kikao cha tathmini ya ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi mmoja wa walimu walifanikisha wanafunzi kupata  alama A  katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mwaka 2019 katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa wa Simiyu akichangia hoja katika Kikao cha Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita mwaka 2019 na Matokeo ya Mtihani wa Mock kilichofanyika Agosti 22, 2019 Mjini Bariadi.

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
MKUU wa mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka amesema wanafunzi kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika mtihani wa Mkoa wa Kujipima ‘Mock’ watawekwa  katika kambi maalum ya kitaaluma na kufundishwa na walimu mahiri  kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu na kufikia  daraja la nne na kuendelea,  katika mtihani wa Taifa mwaka huu 2019.

Mtaka ameyasema hayo Agosti 22, 2019  katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa Mock kwa wanafunzi wa kidato cha nne na matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2019, ambapo mkoa wa Simiyu umekuwa miongoni mwa mikoa kumi bora Kitaifa.

Mtaka amesema lengo la Mkoa ni kuona wanafunzi wote waanafanya vizuri na hakuna mwanafunzi wa kidato cha nne anapata daraja sifuri hivyo wanafunzi wote wenye daraja sifuri na wale walipata daraja la nne alama za mwisho watawekwa pamoja na kutafutiwa walimu mahiri ili wawasaidie kupanda kitaaluma na kupata ufaulu mzuri.

“ Tutaweka kambi ya wanafunzi wote waliopata sifuri kwenye mtihani wa ‘Mock’ lakini pia hata wale waliopata daraja daraja la nne alama zinazoashiria kuelekea kwenye sifuri, Siku sitini kabla ya mtihani wafundishwe masomo manne tu, Civics(Uraia), Kiswahili, Kiingereza na Historia ngalau wapate alama D ili wapate cheti; nia yetu kama mkoa ni kuona kila mwanafunzi anafanya vizuri" alisema

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wakuu wa shule kusimamia kwa karibu ufundishaji na kuhakikisha katika kipindi hiki kuelekea katika mitihani wa Taifa wa Kidato cha nne, kuongeza ufaulu kutoka nafasi ya tisa ya mwaka 2018 kwenda kwenye nafasi nzuri zaidi.

Afisa elimu wa mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju  amewataka wakuu wa shule na maafisa elimu kata na wilaya  kuendelea kusimamia ufundishaji ili wanafunzi waweze kufanya vizuri na wale ambao shule zao hazikufanya vizuri waimarishe usimamizi ili kuongeza ufaulu.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Itilima amezungumzia kambi maalum za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata sifuri kwenye mtihani wa Mock ambao wapo takribani  2000 kati ya wanafunzi zaidi ya 9000, kwamba zitakuwa msaada kwao na wanatarajia kuzifanya kwa ufanisi ili mkoa uwe kati ya mikoa tisa bora Kitaifa mwaka 2019(Single digit).

Mkuu wa mkoa ameahidi kutoa shilingi elfu 30 kwa mwalimu katika kila alama A itakayopatikana kwenye somo lake, shilingi milioni tano kwa shule itakayoingia kumi bora kitaifa, Milioni tano kwa Halmashauri itakayoingia kumi bora kitaifa, na milioni mbili kwa mwanafunzi atakayepata ufaulu  daraja la kwanza pointi saba na kuwa katika kumi bora kitaifa na ikiwa hatakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa atapewa shilingi milioni moja.

Mkutano wa tathimini ya matokeo ya kidato cha sita mkoani Simiyu unawakutanisha wakuu wa shule za sekondari,maafisa elimu wilaya ,wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri za wilaya na wenyeviti wa Kamati za Elimu za Halmashauri lengo likiwa ni kuangalia walipo na wanapoelekea katika maendeleo ya elimu mkoani Simiyu

Serikali kutumia watalaam wa ndani kutekeleza miradi ya Maji

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imedhamiria kutumia zaidi wataalam wake wa ndani katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kazi walizopewa.

Amesema maamuzi hayo yamekuja baada ya wataalam hao kufanya kazi nzuri, zinazochukua muda mfupi kukamilika, zenye viwango na kwa gharama nafuu ukilinganisha na wakandarasi ambao kazi zao zimekuwa na changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za Serikali kumaliza tatizo la maji.

Naibu Waziri Aweso amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini kutokana na ubabaishaji wa wakandarasi licha ya kutumia fedha nyingi kwa dhumuni la kufikisha huduma ya maji kwa kila mwananchi.

‘‘Tumekuwa na utaratibu wa kuwapa kazi Wataalam Washauri ya usimamizi wa ujenzi wa miradi kwa gharama kubwa, lakini wamekuwa wakishirikiana na wakandarasi kuihujumu Serikali kwa kutotimiza wajibu wao na kuingizia Serikali hasara kubwa’’, Naibu Waziri Aweso amefafanua.

‘‘Baada ya kugundua tatizo hilo tukaamua kutumia wataalam wa ndani waliopo kwenye mamlaka za maji, wahandisi wa mikoa na wilaya kwenye miradi mingi iliyokuwa imekwama au ujenzi wa miradi mipya kwa gharama ndogo na kupata mafanikio makubwa, Aweso ameeleza.

Akieleza kuwa baadhi miradi mingi iliyosimamiwa au kutekelezwa na wataalam wa ndani katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya na Kanda ya Ziwa imekuwa na mafanikio makubwa, jambo ambalo limeifanya Serikali kudhamiria kutumia zaidi wataalam hao na kuachana na wakandarasi wababaishaji kwa lengo la kupata matokeo mazuri.

Awali, Naibu Waziri Aweso alichukua hatua ya kumkamata Mkandarasi wa Kampuni ya Mbeso Construction Ltd kwa sababu ya kusuasua kwa ujenzi wa miradi ya maji ya Munge na Tella Mande iiliyopo katika Wilaya za Siha na Moshi, mkoani Kilimanjaro bila sababu za msingi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Aweso kukagua Mradi wa Maji wa Munge, wilayani Siha na kutoridhiswa na kasi ya mkandarasi na muda wa utekelezaji wake ukiwa umebaki mwezi mmoja na kazi ikiwa ni asilimia 25 hali akiwa hana madai yoyote ya fedha kwa Serikali.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images