Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAGARI YANAYOTUMIA GESI YAONGEZEKA HAPA NCHINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
SERIKALI imebainisha kuwa matumizi ya gesi asilia katika magari nchini yamezidi kukua ambapo kwa sasa idadi imefikia 210 kutoka 65 yaliyokuwa yakitumia nishati hiyo, mwaka 2017.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, jijini Dodoma, leo Agosti 21, 2019 wakati akiwasilisha taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuandaa moduli ya miradi ya bei ya gesi asilia, uuzaji na usambazaji wake majumbani na viwandani.

Akieleza zaidi, Dkt. Mataragio alisema kuwa kutokana na ongezeko hilo, kituo cha majaribio kilichopo Ubungo Dar es Salaam, kinashindwa kuhimili matakwa ya matumizi hivyo shirika limejipanga kujenga kituo kikubwa eneo la Sam Nuyoma jijini humo, ili kuondoa changamoto husika.

“Kituo hicho kinachotarajiwa kukamilika Oktoba 2020, kitatumika kujazia gesi katika magari pamoja na kupeleka gesi maeneo ambayo miundombinu ya mabomba ya gesi bado haijafika, yakiwemo maeneo ya viwanda Kigamboni na Kibaha pamoja na maeneo ya Feri na Muhimbili.”


Aidha, alieleza kuwa, sambamba na ujenzi wa kituo husika, shirika limetangaza fursa kwa kampuni binafsi kuuza gesi kwa rejareja kwa watumiaji wa nishati hiyo katika magari nchini. Aliongeza kuwa, jumla ya shilingi bilioni 16.6 zimetengwa kwa ajili ya vituo vya kuongeza mgandamizo wa gesi (CNG) na kujazia gesi katika magari.

Ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za uwezeshaji matumizi ya gesi katika magari nchini, Dkt. Mataragio alisema TPDC inalenga kuupatia gesi asilia mradi wa mabasi ya mwendokasi (DART), ambapo kwa kuanzia, kituo cha kujazia gesi kwenye magari kitajengwa eneo la DART, depoti ya Ubungo na kinatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.

Alisema, shirika limekubaliana na DART kuwezesha kuweka vituo maalumu vya gesi katika depoti ya Gongo la Mboto na Mbagala ili kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi ya DART na kuongeza matumizi ya gesi asilia.

“Miundombinu hii pia itakuwa na matoleo ya kuwezesha usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi ya viwanda na majumbani katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mikakati mingine inayofanywa na shirika hilo katika kuwezesha ongezeko la matumizi ya gesi asilia nchini, Dkt. Mataragio alisema TPDC imepanga kuendeleza miundombinu ya usafirishaji gesi asilia ikiwemo kujenga bomba la gesi kutoka Tegeta hadi Bagamoyo katika eneo la viwanda.

Aidha, alisema shirika limepanga kujenga bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Tanga ambalo litakuwa na matoleo ya kwenda mikoa mingine pamoja na nchi za jirani kulingana na Mpango kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia Nchini (NGUMP).

Katika uwasilishaji huo wa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ujumbe wa serikali uliongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu. Wengine walioshiriki ni viongozi na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TPDC na taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio (kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia kuwaunganishia wateja wa viwanda maeneo ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, hivi karibuni. 

IGP SIRRO AKUTANA NA WANAFUNZI KUTOKA CHUO CHA POLISI

$
0
0
IGP SIRRO AKUTANA NA WANAFUNZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA POLISI NCHINI KOREA KUSINI.
22/08/2019 JIJINI DAR ES SALAAM
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akiiangalia zawadi aliyopewa na Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akifurahia jambo wakati akizungumza na Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini. Picha na Jeshi la Polisi.

MKUTANO MAALUMU NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA MAWASILIANO KUSINI MWA AFRIKA WAFANYIKA TANZANIA

$
0
0



Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL alipokuwa akifungua mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo.
Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
Meneja Maendeleo wa Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Enocent Msasi akichangia mada katika Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA).
Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa (kushoto) akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akiwasilisha mada katika mkutano huo.

Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani).
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Maalum wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakifuatilia mada anuai katika Hotel ya Landmark.
Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa akiwaonesha wajumbe picha ya Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli iliyokuwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo kwenye Hotel ya Landmark.

Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe.

$
0
0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Prof.Florens Luoga amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya ya Afrika (Africa Group 1), Bi.Anne Kabagambe ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Gavana Luoga amemwelekeza Bi.Kabagambe hatua mbalimbali ambazo BoT inachukua kuhakikisha kuna ukuaji wa uchumi,kuimarisha sekta ya mabenki,mifumo ya malipo na huduma jumuishi za kifedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Kuu ya Dunia aliipongeza BoT kwa hatua mbalimbali inazochukua kutekeleza sera ya fedha na na kueleza utayari wa Benki ya Dunia kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Manaibu Gavana wa BoT, Dkt.Yamungu Kayandabila na Dkt.Benard Kibesse na Mshauri Mwandamizi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji huyo, Bw.Zarau Kibwe, walihudhuria mazungumzo hayo.

JIJI LA ARUSHA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 20 MAPATO YA NDANI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imepanga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 20.7 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya ndani.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt Maulid Madeni amesema kuwa licha ya jiji hilo kuvuka malengo ya makusanyo mwaka wa fedha 2019/20 na kushika Namba moja kwa majiji yote nchini,amesema mpango wa jiji hilo ni kufikia makusanyo yanayozidi sh, milioni 30 kwa mwaka .

Dkt Madeni amesema kuwa pamoja na pongezi nyingi alizopata za kuvuka makusanyo ya ndani, amesema kipaumbele chake si kupongezwa na wala hapokei pongezi hizo bali ni kufikia malengo ya makusanyo aliyojiwekea .

"Mimi si mtu wa kusifiwa na wala sikubali pongezi hizo ninachotaka bado hakijafikiwa, lengo langu ni kufikia makusanyo ya bilioni 30 " Amesema Madeni.Katika hatua nyingine Dkt Madeni amesema kuwa jiji la Arusha limetenga bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi na ukumbi wa Mkutano.

Dkt Madeni amesema ujenzi wa jengo hilo unatarajia kuanza mapema mwaka wa fedha 2919/20 na litajengwa jirani na ofisi za sasa za halmashauri hiyo.

Pia Mkurugenzi huyo amedai kuwa jiji la Arusha limetoa kiasi cha shilingi milioni 140 kwa wakala wa barabara za mijini na vijiiini Tarura kwa ajali ya kuzifanyia ukarabati barabara zote za jiji hilo zilizoharibiwa na mvua kipindi cha masika.

Amesema barabara hizo zitafanyiwa matengenezo na kuondoa malalamiko yanayojitokeza kwa watumiaji wa barabara wakiwemo watumiaji wa vyombo vya moto ambao wamekuwa wakilalamika kuharibika kwa magari yao kutokana na mashimo yaliyopo.

Wakati huo huo jiji hilo limesaini mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 3.5 itakayojengwa kwa kiwango cha Lami kwa thamani ya shilingi bilioni 4.1.

Akiongea wakati wa kusaini mkataba huo baina ya jiji hilo na kampuni ya ujenzi ya Sinohydro kutoka nchini china Meya wa jiji la Arusha, Kalist Lazaro alisema kuwa mradio huo ni kazi ya nyongeza ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Kisongo Bypass inayotoka Olasiti jijini hapa.

Meya alisema kuwa mkandarasi huyo atafanyakazi yenye ubora kwa muda wa miezi minne kuanzia September 11/2019/hadi January 11/2020 atakapokabidhi mradi huo.
Mkurugenzi wa jiji hilo,Dkt Maulid Madeni Wa kwanza kushoto akimkabidhi mkataba huo waluisaini baina ya jiji hilo na kampuni ya ujenzi ya Sinohydro kutoka nchini china.

Balozi wa Korea atembelea Hospitali ya Mloganzila

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (aliyevaa shati jeupe) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mh. Tae-ick-Cho ambaye leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
Balozi Tae-ick-Cho akizungumza jambo wakati wa kikao hicho mapema hii leo katika Hospitali ya Mloganzila.
Baadhi ya viongozi wa MNH-Mloganzila pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Korea nchini , wakimsikiliza kwa makini Balozi Tae-ick-Cho ambaye ameahidi kushirikiana na Hospitali ya Mloganzila katika kutatua changamoto zilizopo.
Balozi Tae-ick-Cho (wa kwanza kulia) akiwa na ujumbe wake, wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao, wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
Balozi Tae-ick-Cho (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru (kushoto), kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.

Na Neema Wilson Mwangomo

Balozi wa Jamhuri ya Korea Tae-ick-Cho leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na kuahidi ushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo, Balozi Tae-ick-Cho pia amezungumzia jinsi ya kuboresha mfumo wa TEHAMA uliokuwepo katika kusimamia utoaji wa huduma za afya hospitalini.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema watanzania wanapenda kuona hospitali hii ikifanya kazi iliyokusudiwa ya kutoa huduma, elimu na utafiti na kusisitiza kuwa hilo ndio kusudio kubwa la Rais John Magufuli.

“Lengo letu ni kuhakikisha hospitali hii inafanya kazi kama inavyotakiwa hasa ukizingatia ni hospitali kubwa na ya kisasa hivyo tutaendelea kuboresha huduma zetu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Prof. Museru.Balozi Tae-ick- Cho mapema hii leo amefika MNH-Mloganzila kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na uongozi wa hospitali.

MAWAKILI UPANDE WA MASHITAKA NA WA UTETEZI KESI YA UCHOCHEZI VIONGOZI WA CHADEMA WARUSHIANA MANENO KORTINI

$
0
0
MAWAKILI wa upande wa Mashtaka na wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamejikuta wakirushiana maneno mahakamani kufuatia kitendo cha wakili wa utetezi, Hekima Mwasipo kunyanyuka mahali alipokuwa amekaa na kwenda kumchungulia shahidi mahali alipokuwa amekaketi wakati akitoa ushahidi wake.

Baada ya kuona kitendo hicho, wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliyekuwa akimuongoza shahidi huyo, alitoa taarifa kwa Hakimu

Mkazi Mkuu Thomas Simba juu ya tukio hilo akidai kuwa mawakili wa utetezi wanamtisha shahidi ambapo, wakili Peter Kibatala alidai walidhani shahidi huyo anasoma ushahidi wake kwenye simu ndio maana akaenda kumchungulia huku wakili Matata akihama mahali alipokuwa amekaa na kwenda kukaa karibu na kizimba cha shahidi kutolea ushahidi wake.

Baada ya wakili Wankyo kudai hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala alisimama na kutaka kutoa maelezo lakini wakili wa Serikali Faraja Nchimbi alionekana kutokubaliana na hilo na kuwafanya wrote kuanza kurushiana maneno hali iliyopelekea Hakimu kumuita askari aliyekuwa mahakamani hapo na kuwaambia mawakili hao "Nitaagiza askari awakamate" 

Hata hivyo, Hakimu Simba alifanikiwa kumaliza vurugu hiyo kwa kuwataka mawakili wote kukaa kimya na kumuonya Mwasipo kuwa haruhusiwi kusimama mahakamani bila ruhusa ya mahakama na Mwasipo akaomba msamaha. 

Hata hivyo, shahidi alilazimika kutoka kwenye kizimba na askari polisi aliamuriwa kumkagua shahidi na kukagua sehemu alipokuwa amekaa kama kuna simu au kitu chochote.

Askari polisi aliiambia mahakama kuwa hakuna kitu chochote na hivyo shahidi alirudi na anaendelea kutoa ushahidi.

Mbunge Kingu afunguka kuhusu miradi ya maendeleo jimboni kwake

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

UJENZI wa Reli ya Kisasa, ufufuaji wa Shirika la Ndege nchini, usimamizi makini wa ulipaji kodi, elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi kidato cha nne, vituo bora vya afya ni sababu ambazo zinatajwa kuipa ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh Elibariki Kingu wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika eneo la Sepuka wilayani Ikungi, Singida.

Mhe Kingu amesema tangu Rais Dk John Magufuli aingie madarakani amefanya mambo makubwa kwa Watanzania wakiwemo wananchi wake wa Singida Magharibi ambapo amepeleka miradi mingi ya maendeleo ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Amesema wananchi wa Jimbo lake wamenufaika na miradi ya ujenzi wa Kituo kikubwa cha Afya cha Sepuka kilichozinduliwa jana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally ambacho kinakwenda kumaliza adha iliyokua ikiwasumbua kwa muda mrefu.

" Sisi watu wa Singida Magharibi na Wilaya ya Ikungi tuna mengi ya kumshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyotukarimu, miradi mikubwa ya Afya ukiachilia mbali Kituo hiki cha Sepuka lakini pia tumeshapokea takribani Milioni 500 kwa ajili ya Kituo kingine cha Ihumba.

" Kwenye maji huko ndio usiseme kila Kijiji tumepanga kuhakikisha kinakua na Maji ya kutosha lengo likiwa ni kuakisi kwa vitendo Sera ya Rais Magufuli ya kumtua Mama ndoo, ndio maana tunaanza ujenzi wa miradi 14 ya maji na tayari tumeshanunua mitambo miwili ya Kisasa kwa ajili ya kumaliza changamoto ya maji pia, " amesema Mh Kingu.

Amesema yeye kama Mbunge anaetokana na CCM ni lazima ahakikishe anasimamia Sera ya Elimu bure kwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa na Hostel ambavyo vyote viko mbioni kukamilika.
Amesema miradi yote hiyo imeweza kutekelezwa kutokana na namna Rais Magufuli anavyosimamia kwa uadilifu ukusanyaji wa kodi za Watanzania ambazo zimekua zikitumika kwenye miradi ya maendeleo.

" Kwa haya makubwa ambayo Rais Magufuli anatutendea njia pekee ya kumpa shukrani zetu ni kuhakikisha tunachagua wenyeviti wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hilo ndilo deni letu kwake," amesema Mh Kingu.

Aidha amesema Jumatatu ya Wiki ijayo wanatarajia kupokea Fedha za mfuko wa Jimbo takribani Milioni 46 ambazo zote zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
 Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe Elibariki Kingu (kushoto) akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Ikungi, Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh Elibariki Kingu akihutubia wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika eneo la Puma wilayani Ikungi.

WATANZANIA WATAKIWA KUWATUNZA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
Na Woinde Shizza,Michuzi Tv,Arusha

Watanzania wametakiwa kuwatunza watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi ,kwa kuwa watoto hao wengi wao Wana ndugu hapa nchini lakini pia baadhi  ya wazazi wao wapo hai.

Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha, Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi amesema kuwa dhana ya kuliacha kundi hili kutunzwa tu na wageni kutoka nje ya nchi haileti taswira nzuri.

Aidha Dkt.Ng'ondi alisema kuwa ni vyema watanzania wakajenga utaratibu wa kuchangia Kundi hili ili kupunguza baadhi ya changamoto badala ya kuwaachia wageni kutoka nje.

"Hii dhana haileti taswira nzuri Jamani tumekuwa tukiwaachia wageni tu kuchangia kuanzia masomo , chakula,na mengineyo kwanini hatujishughulishi na hawa watoto wakati ni watanzania "alihoji dkt.Ng'ondi

Hata hivyo aliitaka kamati ya ulinzi kwa watoto mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu Juu ya ukatili kwa mtoto kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa vitendo hivyo vimekidhiri katika mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani na Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani Mendert Schaap alisema kuwa kituo hicho kinalea watoto zaidi ya 300 na kuwapatia elimu na kuwakutanisha na wazazi wao.

Bw.Schaap alisema kuwa mbali na kuwawezesha watoto wanaoishi mitanii makazi hayo Salama,yatawawezesha watoto kupatiea misaada Mbali Mbali na kujiendekeza kiuchumi na kielimu.

Mmoja wa watoto aliyeokolewa mtaani anayefahamika kwa jina la Marry Christopher (19) alisema kuwa aliingia mtaani akiwa na miaka kumi tu na aliweza kuishi ndani ya miaka miwili mtaani Kama mtoto wa kiume ili aweze kukwepa vitendo vya ukatili.

Marry alisema kuwa kituo cha Amani kimeweza kumpatia elimu na Sasa ni mwalimu ambaye anafundisha kuchomelea vitu Mbali Mbali na kuwataka watoto wa mitaani pindi wanapokolewa kutumia vyema nafasi ya elimu na kupata ujuzi .
kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi akikata utepe ishara ya ufunguzi rasmi Wa kufungua kituo cha Amani Cha Makazi Salama na kuokoa watoto wa mitaani kilichopo kaloloni Jijini Arusha

 kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng'ondi  akiongea na waandishi Mara baada ya kituo hicho kufunguliwa
Mkurugenzi wa kituo cha Amani na  Makazi Salama Cha kuokoa watoto wa mitaani  Mendert Schaap akiongea na waandishi Mara baada ya kituo hicho kufunguliwa
Baadhi ya wafadhili kutoka nje waliochangia ujenzi huo Wa kituo cha watoto cha Amani

CHUPA 51819 ZAIDI ZA DAMU SALAMA ZAKUSANYWA KWA MWAKA 2018/2019

$
0
0
Meneja Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dkt. Magdalena Lyimo akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji wa damu salama nchini kwenye kikao.kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri unaondelea jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya TIba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiongea kwenye kikao.kazi hicho.
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishaji wa mada unaoendelea kwenye ukumbi wa CCM

……………………

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Mpango wa damu salama umefanikiwa kukusanya chupa 51819 sawa na asilimia ishirini zaidi ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka 2018/2019.

Hayo yameelezwa leo na meneja mpango wa taifa wa damu salama Dkt. Magdalena Lyimo wakati akiwasilisha mada ya upatikanaji wa damu kwenye kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri kinachoendelea jijini hapa.

Dkt. Lyimo amesema kwamba kwa mwaka 2018/2019
wizara ya afya kupitia mpango huo uliweka malengo ya kukusanya kiasi cha chupa 309376 nchi nzima ikilinganishwa na chupa 257557 zilizokusanywa mwaka 2017/2018.

Hata hivyo Dkt. Lyimo alisema kuwa wameweza kukusanya chupa 309,376 sawa na,asilimia sitini ya mahitaji ya nchi kulingana na idadi ya wananchi waliopo “tumeweza kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya chupa za damu zaidi na hii ni kutokana na uelewa mkubwa wa wananchi wa kuelewa umuhimu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha hususani akina mama wajawazito na wahitaji wengine wa damu”.Alisema.

Aidha, Dkt. Lyimo alitaja makundi ya wachangia damu kuwa wanawake ni asilimia 14 pekee huku idadi ya wanaume ikiwa ni asilimia 86 hapa nchini.

Hata hivyo alisema hali ya maambukizi ya magonjwa kwa damu zinazobainika katika ukusanyaji huo ameeleza kuwa ugonjwa wa homa ya Ini ndio inayoongoza kwa asilimia 5.9 ikifuatiwa HIV kwa asilimia 2.8.

Dkt. Lyimo amewashukuru wananchi wanaoendelea kuchangia damu ikiwemo vijana watumishi wa umma, taasisi na mashirika mbalimbali kwa moyo wa kutekeleza zoezi hilo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

Mpango wa kuendeleza Miji nchini wazinduliwa na Waziri Jafo

$
0
0
MPANGO kazi wa kuendeleza Miji Tanzania umezinduliwa jana Jijini hapa, huku Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Seleman Jafo akiwataka Wakuu wa Mikoa kuusimamia mpango huo.

Akizindua jana Jijini hapa,Jafo aliwataka Wakuu wa Mikoa nchini kuusimamia mpango huo ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo."Niwaombe wadau tujipange kwenda kutekeleza mpango huu na niwaombe,Wakuu wa Mikoa kuanisha eneo kwa eneo ikiwa ni pamoja na kuusimamia," alisema.

Jafo alisema kwa sasa ongezeko la watu ni kubwa hususan katika Mikoa ya Dodoma na Dar es salaam hivyo akadai kwamba umekuja wakati muafaka.
"Bila kuwa na mpango kazi inawezekana tukaishi maisha sio azuri,mabadiliko haya ambayo yanafanywa sasa hivi ni muhimu sana katika upangaji wa miji," alisema.

Waziri Jafo alisema Mji wa Dar es salaam upo hovyo na haujapangika vizuri hivyo akataka isitokee tena kwenye miji mingine."Mji wa Dar upo hovyo,hata moto ukitokea hauwezi kuokoa tujiulize ni majanga mangapi yametokea tumeshindwa kuokoa sababu ya Miji kupangwa vipaya ?

" Jiji la Dar tumechelewa yaani unatamani uchukue Greda uvunje nyumba kwani zimekaa vibaya.Niwapongeze Dodoma angalau Jiji limekaa vizuri,"alisema Jafo.Aidha,alisema lazima Miji ipangwe vizuri kwani kwa sasa ile ambayo imepangwa vizuri imeweza kusababisha kuongezeka kwa mapato kutokana na Serikali kuweza kukusanya kodi.

"Sehemu zingine gari la zimamoto haliwezi kupitia,sehemu zingine kupitisha jeneza shida,msiba unakuwa nyumba ya tatu sababu kwenye msiba hakufikiki.Kuna vijana wana magari mazuri lakini yanakaa kwa jirani wanapokaa hakufikiki," alisema.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angelina Mabula alisema mpango huo ni muhimu na utasaidia katika ujenzi wa Miji iliyopangika pamoja na kuongeza thamani ya ardhi.

Mabula alisema Serikali imetayarisha Mipango kabambe 30 kwa mwaka 2018-2019 ambapo 20 imekamilika huku 10 ikiwa katika mipango mbalimbali.

Naye,Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Fedha na Mipango,Adolf Ndunguru alisema kwa sasa Miji inakuwa hivyo mpango huo umekuja wakati muafaka.

IGP SIRRO AKUTANA NA WANAFUNZI KUTOKA CHUO CHA POLISI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akiiangalia zawadi aliyopewa na Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akifurahia jambo wakati akizungumza na Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza Sajin Kim (katikati) na Yujun Cho, wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Polisi nchini Korea Kusini, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo 22/08/2019, ziara ya wanafunzi hao, ni kuendelea kukuza ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi Korea Kusini. Picha na Jeshi la Polisi.

SERIKALI YA MAREKANI YAAHIDI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA SELI MUNDU (SICKLE CELL) NCHINI

$
0
0
Na WAJMW-Brazzaville

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Waziri wa Afya wa Marekani Amiral Brett Giroir na kufanya mazungumzo na kuona namna gani nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kupambana na ugonjwa wa Sickle Cell (Seli Mundu) hasa kwa watoto wachanga na wale walio chini ya miaka mitano.

Waziri Ummy amemueleza Waziri huyo kuwa watoto wapatao 11,000 wanazaliwa na ugonjwa huo Tanzania na wengi hupoteza maisha kwa sababu ya kuchelewa kufanyiwa vipimo na kugundulika mapema.

Waziri Ummy amemueleza kuwa muelekeo wa nchi sasa ni kuhakikisha kuwa kila mtoto anayezaliwa anapimwa Sickle Cell na watakaogundulika matibabu yaanze mapema ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mawaziri hao wamekubaliana kwa pamoja kushirikiana katika kudhibiti vifo vinavyoweza kutokea kwa sababu ya ugonjwa huo huku Waziri Amiral akiahidi kuimarisha upatikanaji wa vipimo, pamoja na matibabu kwa watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kuanzia ngazi ya zahanati na vituo vyote vya kutoa huduma za afya ya msingi nchini.

“Ni muhimu huduma hizi zikatolewa katika ngazi ya afya ya msingi mpaka taifa ili kuwapa huduma stahiki wananchi, hii ikiwa ni utekelezaji wa afya kwa wote. Suala la upimaji wa Seli Mundu, elimu kwa jamii na pia suala la matibabu katika ngazi zote za utoaji huduma ni muhimu vikapewa kipaumbele”. Aliongeza Waziri Ummy.

Hivi sasa huduma hii hapa nchini inapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Rufa za Mikoa za Amana na Temeke pekee kwa nchi nzima.

Kwa upande wake Waziri Brett amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kujenga viwanda vya dawa nchini ikiwa ni pamoja na za Sickle Cell. Pia ameahidi kutembelea Tanzania kuona na kujadiliana zaidi namna nchi hizi mbili zitavyoshirikiana katika kushughulikia ugonjwa huu nchini.

Mawaziri hao wanahudhuria mkutano wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaojumuisha Mawaziri wa Afya toka nchi mbalimbali za Afrika unaoendelea jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo.

FIFA And The RACISM Problem.

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI MBALIMBALI ZA NJE.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Kikao na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Kikao na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje mara baada ya kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi watano kutoka (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Damas Ndumbaro watano kutoka (kulia) pamoja na Mabalozi Wanawake wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU






ZAIDI YA MILIONI 81 ZATUMIKA KUBORESHA ELIMU YA MSINGI TARAFA YA KIBENGU

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa iliyopo katika tarafa ya kibengu alipotembelea kujua changamoto za shule hiyo. 
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akisalimiana na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisusa


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MBUNGE wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametumia zaidi ya shilingi 81,667,221 katika ukarabati na ujenzi wa shule za msingi za tarafa ya kibengu iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara katika tarafa hiyo Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Mapanda amesaidia ukarabati na ujenzi wa Madarasa mawili shule ya msingi Mtwivila Saruji 90 na fedha kiasi cha shilingi jumla ya shilingi laki sita na nusu,shule ya msingi ukami saruji 70 na rangi kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo.

“Saruji mifuko 220 imetumika katika ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi ya Chogo,Ihimbo na Uhafiwa pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya uingizaji wa umeme katika shule ya msingi Uhafiwa zote hizo ni juhudi zangu” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Kibengu amechangia jumla ya mifuko 210 ya saruji,bati 280,madawati 10 na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kuboresha elimu katika shule ya msingi Kibengu,Igomtwa,Kipanga,Igeleke,Usokami na Ilogombe.

Aidha Mgimwa alisema kuwa kata ya Ihalimba inajumla ya shule za msingi nne ambazo ni Vikula,Ugesa,Nundwe na Ihalimba ambapo ametoa saruji mifuko 50 bati 310 na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 44,932,221 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya msingi Ihalimba pamoja na utengenezaji wa madawati 60 kwa ajili ya shule zote za kata hiyo.

“Hizi zote ni juhudi zangu binafsi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi tub ado hapo sijaelezea kuhusu shule za sekondari lakini unakuta watu wamekaa tu vijiweni wanasema mbunge hajafanya kitu sasa hivi wewe mwandishi umejine kwa macho na umewasikia wananchi wenyewe kwenye mikutano ya hadhara” alisema Mgimwa

Zaidi Ya Shilingi milioni 300 Zatengwa kuwafidia wananchi Wa wilaya ya Igunga waliopitiwa na Mradi wa Umeme wa REA

$
0
0
Na Editha Edward-Tabora 

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa shirika la umeme Tanesco mkoa wa Tabora kuanza kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vinne vya kata ya mwisi vilivyopo wilayani Igunga mkoani Tabora waliopitiwa na mradi wa umeme wa REA ambapo ameweka bayana kuwa zaidi ya Shilingi bilioni miatatu tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wananchi hao 

Dkt, Kalemani akiwa katika kijiji cha mwisi Wilayani Igunga mkoani Tabora amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho ambapo mmoja wa wananchi anaeishi katika kijiji hicho, Hamis Masinge amepewa fursa kueleza malalamiko yao ya kudai fidia kwa muda mrefu "Tumesumbuka sana sisi wananchi wa kata hii tumekutafuta sana waziri wa umeme lakini Bila mafanikio tumeshindwa kukarabati majumba yetu mabovu yako barabarani na wakati wote yanaweza kuvunjika kwa hiyo tunogopa kukarabati na tusipokarabati tunaweza kupondwa na hayo majumba waziri tunaomba utusaidie"Amesema Masinge

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Tabora Mhandisi Alvin Limo amesema Sababu ambayo ilikuwa inawakwamisha wananchi kutopewa fidia hizo ni uhakiki ambao walikuwa wanafanya shirika hilo"Tulikuwa tunafanya uhakiki kwa wananchi kwani Mwanzoni kulikuwa kuna watu ambao walijiingiza katika orodha hiyo ndo maana tulichelewa kuwalipa fidia zao kw waliopitiwa na mradi huo"Amesema Limo

Aidha pamoja na hayo Waziri Kalemani amezindua na kuwasha umeme wa REA katika kijiji cha Isenegeja wilaya ya Igunga huku akitoa wito kwa wananchi Kutumia nishati hiyo kwa Shughuli za maendeleo na Kutunza pia miundo mbinu Ili kuleta mabadiliko katika Sekta ya uchumi.
 Pichani ni waziri Wa nishati dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme wa REA katika kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
Pichani ni moja kati ya nyumba iliyopata umeme Wa REA   katika kijiji cha Isenegeja wilayani Igunga.
 Pichani ni waziri wa nishati Medard Kalemani Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwisi wilayani Igunga mkoani Tabora.

NYOTA WA ZAMANI TIMU YA TAIFA YA GHANA AFARAIKI DUNIA

$
0
0
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ghana, na Klabu za Nottingham Forest na Bristol Rovers, Junior Agogo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 40.

Agogo, alianza kucheza soka katika Klabu ya Sheffield Wednesday, ambapo alicheza Ghana michezo 27 na aliifungia mabao 12.

Alimaliza Soka lake katika Klabu ya Hibernian mwaka 2012 pia alicheza katika timu za United States, Cyprus na Egypt.

Agogo alipata Kiharusi mwaka 2015, Agogo alikuwa katika sehemu ya Kikosi hicho kilichoshika nafasi ya tatu katika Michuano ya AFCON 2008.

KUTOKA MITAANI KWETU LEO

$
0
0
Mamalishe wakiwa katika harakati za kuandaa maakuli, kando ya Barabara ya Kilwa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo .(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Kazi ikiendelea .

WAZIRI WA KILIMO JAPHET HASUNGA AZINDUA MINADA YA KAHAWA KANDA YA MBEYA /SONGWE

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wanunuzi na watumishi wa Bodi ya Kahawa wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifatilia jinsi mnada wa kahawa unavyoendeshwa mara baada ya uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe Leo tarehe 22 Agosti 2019 katika hafla iliyofanyika katika Mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Serikali imewataka wakulima wote nchini kwa kupitia vyama vya Ushirika kuweka mkakati wa kununua na kutumia mitambo ya kuchakata kahawa ili kuongeza na kuwa na mwendelezo (Consistency) wa ubora wa kahawa inayozalishwa ili kupata bei nzuri mnadani au kwenye soko la moja kwa moja. 

Waziri wa Kilimo amesema hayo Leo tarehe 22 Agosti 2019 wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe na kuzitaka Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya mapato kuendelea kuwekeza katika uendelezaji wa zao la kahawa ikiwemo uzalishaji wa miche, ununuzi wa CPU na kuwawezesha wakulima na maafisa ugani kupata mafunzo ya kilimo bora cha kahawa ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi.

Alisema kuwa ili kulinda ubora wa kahawa, matumizi ya mitambo ya kisasa ya kuchakata kahawa (CPU) hayawezi kuepukika. Alisema nchini kuna takribani mitambo 481 kiasi ambacho bado kipo chini ukilinganisha na kiasi cha kahawa inayozalishwa. "Hivyo nawasihi wadau wote muone umuhimu wa uwepo wa mitambo hii kwa kuwa ili upate kahawa nyingi zenye sifa za ubora unaofanana ni lazima kuwepo na matumizi makubwa ya CPU tena kwa kuzingatia hatua zote za uchakataji wa kahawa" Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga aliongeza kuwa Lengo la Serikali ni kuona kwamba kahawa zote zinaandaliwa katika mitambo ya kisasa (CPU) ili zipate bei nzuri katika masoko kwani dhamira ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuimarisha tija katika uzalishaji kadhalika kutafuta masoko ya mazao nje na ndani ya nchi.

Alisema kuwa Ili kuhakikisha tasnia ya kahawa inaondokana na changamoto ya tija ndogo na uzalishaji, Serikali kwa kushirikiana na Wadau imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo kuongeza kasi ya upatikanaji wa miche bora ya kahawa kupitia TACRI; Ruzuku ya miche inayotolewa na Bodi ya Kahawa na kuanzisha utaratibu wa upatikanaji wa mikopo ya mbolea kwa wakati kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Sekta Binafsi. 

Aliongeza kuwa hatua hizo zimewezesha kuongezeka kwa uzalishaji wa kahawa kutoka tani 43,625 za kahawa safi msimu wa mwaka 2017/2018 mpaka kufikia tani 68,147 msimu 2018/2019.

Waziri huyo wa kilimo Mhe Hasunga alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa tija katika uzalishaji wa kahawa kwa wakulima wadogo wa kahawa ni ndogo sana ukilinganisha na wakulima wa mashamba makubwa na wakulima wa kahawa wa nchi nyingine. Aliongeza kuwa Wastani wa tija kwa mti mmoja wa kahawa ya Arabika ni gramu 350 ikilinganishwa na kilo moja (gramu 1,000) kwa nzi za Brazil na Vietnam. 

Aliziraja Sababu kubwa zinazosabisha tija ndogo kwenye kahawa kuwa ni pamoja na Matumizi madogo ya mbolea na virutubisho kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji; na Wakulima kutokuzingatia kanuni za kilimo bora cha kahawa ambapo wakulima wengine hawatunzi kabisa miti yao ya kahawa na huvuna tu kile kitakachopatikana.

Sababu nyingine ni Uwepo wa magonjwa na wadudu waharibifu wa kahawa Miti iliyozeeka sana na kupoteza uwezo wa kuzaa vizuri; Badala ya kutumia miti iliyoboreshwa yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa na kuzaa sana. Nimeambiwa mti wa mmoja ulioboreshwa unao uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 3 – 5 za kahawa kavu (Parchment). 

Aidha, Mhe Hasunga amsema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya kahawa na kuhakikisha inaendelea kutoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini, kuongeza pato la taifa na kuongeza ajira kupitia viwanda mbalimbali vya kahawa. 

Moja ya lengo kuu la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Ili kufikia lengo hilo, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha matumizi ya miche bora ya kahawa ili kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima, kuimarisha mazingira ya biashara na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya kahawa ili kuiwezesha kutoa mchango unaohitajika katika kujenga Tanzania ya viwanda. 

Kuanza kwa minada ya kanda ya kahawa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuwa kuanzia msimu wa kahawa 2019/2020 Bodi ya Kahawa ianze kuendesha minada ya kahawa katika Kanda nne (4) za uzalishaji wa kahawa. Kanda hizo ambazo minada ya kanda itafanyika ni Kanda ya Mbeya/Songwe mnada unafanyika Mbozi, Kanda ya Ruvuma/ Njombe mnada unafanyika Mbinga Mkoani Ruvuma, Kanda ya ziwa mnada unafanyika Bukoba Mkoani Kagera na Kanda ya Kaskazini mnada unafanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images