Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live

TANZANIA YATAJA MATATU MUHIMU YA KUANZA NAYO SADC

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu

TANZANIA ambayo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) imetaja mambo matatu muhimu ambayo itayapa kipaumbele katika kuyatekeleza ndani ya jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wakati anazungumza na waandishi wa habari leo Agosti 21,2019 jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine lakini ni vema wakaeleza mambo muhimu matatu yatakayopewa kipaumbele.Amesema jambo la kwanza ni kuhakikisha lugha ya Kiswahili inazungumzwa kwenye nchi za jumuiya hiyo na hiyo ni baada ya wakuu wa nchi hizo kuipitisha rasmi kuwa lugha ya nne ya jumuiya hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu Kiswahili, Profesa Kabudi amesema haikuwa kazi rahisi kukipigania Kiswahili kuwa rasmi kwenye nchi hizo na kwamba mkakati wake ulianza Machi mwaka huu.

"Mkakati wa kukipigania Kiswahili ni baada ya majadiliano ya muda mrefu kwenye kikao cha mawaziri wa nchi wanachama wa SADC, hatimaye Mwenyekiti wa Jumuiya alitoa ombi kwa wakuu wa nchi na hatimaye imepitishwa.

"Ni jukumu letu Watanzania kuhakikisha tunachangamkia fursa hiyo ikiwemo ya kufundisha Kiswahili.Kwa sasa nchi za Kenya na Congo wananufaika sana na lugha hii maana wengi wao wamekuwa walimu wa Kiswahili kwenye mataifa mengine.Nasi tuna kila sababu ya kutumia fursa hii,"amesema.

Ameongeza ni vema watanzania wakajifunza lugha za kigeni ikiwemo Kifaransa na Kireno kwani hiyo itapaua wigo zaidi maana utakuwa unajua Kiswahili na wakati huo huo unafahamu na lugha nyingine.Waziri Kabudi amesema jambo la pili ambalo litapewa umuhimu ni kuhakikisha mkakati wa viwanda kwa nchi wanachama unatekelezwa kama ambavyo wamekubaliana wakuu wa nchi hizo.

Amesema ambacho kitafanyika ni kuwepo kwa mpango mkakati kwa kila nchi kufanikisha uwepo wa viwanda kwa maendeo ya nchi hizo.Amefafanua ni matarajio yao kuona kunakuwa na kiwanda au viwanda vya mfano kwa nchi za SADC huku akifafanua namna ambavyo Serikali ya Tanzania imejipanga kikamilifu kwenye eneo hilo.

"Tanzania tumepiga hatua sana katika viwanda , na hata kwenye maonesho ya bidhaa kwa nchi za SADC bidhaa zetu zimekuwa kivutio kutokana na ubora wa bidhaa zetu.Waliotembelea viwanda vyetu wamethibitisha na kufurahishwa na teknolojia ya hali ya juu katika utengenezaji bidhaa,"amesema.

Wakati jambo la tatu ambalo watalipa kipaumbele ni kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinasimama kidete katika kushinikiza jumuiya ya kimataifa kuoindolea vikwazo nchi ya Zambabwe.Amesema na katika kutekeleza hilo wamekubaliana nchi zote za SADC Oktoba 25,2019 iwe ni siku ambayo kutakuwa na shughuli au mijadala kwa kila nchi inayozungumzia Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Waziri Kabudi amesema hakuna sababu ya nchi hiyo kuendelea kuwa na kuwekewa vikwazo wakati wananchi wamefanya uchaguzi na kupata Rais wao kwa uhuru na kusisitiza kuendelea kuiwekea vikwazo nchi hiyo ni kuendelea kuwatesa wananchi.

"Kama kulikuwa na sababu za nchi hiyo kuwekewa vikwazo kwa sasa tunaamini havipo tena.Jumuiya ya Kimataifa itoe vikwazo kwa Zimbabwe.Tumekubaliana katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka huu tutakwenda na ajenda hii, lazima Zimbabwe iondolewe vikwazo na kwa kuwa Tanzania ndio Mwenyekiti wa SADC tumedhamiria katika hili,"amesema Waziri Kabudi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akifafanua jambo kwa msisitizo mbele ya Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar, 
 Baadhi ya Wahariri wakuu wa Vyombo vya habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Kabudi .
Mmoja wa Wanahabari akiuliza swali kwa Waziri Kabudi
 Baadhi ya Wahariri wakuu wa Vyombo vya habari  na Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Kabudi . 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya wakamata watu wawili wakiwa na nyara za serikali

$
0
0

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili ZUNGU PAULO @ TINYA [45] na BARAKA LAZARO @ TIMOTHEO [40], wote wakazi wa Kijiji na Kata ya Lupa wakiwa na nyara za Serikali vipande vitatu [03] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe 19.08.2019 saa 20:00hrs katika Kijiji na Kata ya Lupa, Tarafa ya Kipembawe Wilaya ya Chunya. Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Mbinu iliyotumika ni kuhifadhi pembe hizo kwenye mfuko wa Sandarusi na kutafuta wateja. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili IGELELE DANIEL [42] na NYIRENDA JOHN @ DAIMON [32], wote wakazi wa Kijiji cha Isangawana wakiwa na nyara za Serikali vipande kumi [10] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe 19.08.2019 saa 20:15hrs katika nyumba ya kulala wageni iitwayo UZUNGUNI chumba namba 113 iliyopo eneo la Sinjilili, Kata ya Itewe, Tarafa Kiwanja, Wilaya ya Chunya. Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA KIFO.
Jeshi la Polisi linamtafuta dereva mmoja ambaye alikimbia baada ya kutokea ajali na kusababisha kifo cha askari MT. 90399 CPL FRED GRAYSON @ MBALIZI [35] askari wa JWTZ Kikosi cha 44KJ – Mbalizi, mkazi wa Iwambi. 

Tukio hilo limetokea tarehe 20.08.2019 saa 21:15hrs eneo la ZZK – Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini katika baraaaaaabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma. Katika tukio hilo marehemu alikuwa akiendesha gari ndogo T.219 CSU Nissan akitokea Songwe Airport kuelekea Mbalizi na kugongana uso kwa uso na gari kubwa T.838 APZ Scania Lori ambalo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kueleka Tunduma hivyo kusababisha kifo chake papo hapo. Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo [marehemu] kujaribu kulipita gari linguine lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari. Jitihada za kumtafuta dereva ambaye alikimbia mara baada ya ajali zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali teule ya Ifisi. 

OPERESHENI DHIDI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni na ukaguzi wa vyombo vya moto katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya vinavyokiuka sheria za usalama barabarani. Hivyo wamiliki wa Bajaji na madereva ni vyema wakafuata na kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika. Zoezi hilo la ukaguzi na ukamataji wa vyombo vya moto kwa makosa mbalimbali ni endelevu katika mkoa wetu. 


WITO:
Natoa wito kwa jamii kutoa taarifa katika mamlaka husika juu ya mtu/watu/kikundi au mtandao unaojihusisha na matukio ya ujangili ili hatua kali za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Imetolewa na :
[ ULRICH O. MATEI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WAZIRI KABUDI AFAFANUA OMBI LA BURUNDI KUJIUNGA NCHI ZA SADC

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Burundi haijakataliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) ila bado haijakidhi vigezo.

Ameyasema hayo leo Agosti 21, 2019 jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wahariri na waandishi wa habari nchini ambao alikutana nao kwa ajili ya kuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wameifanya kwa kuandika vema habari za mkutano Mkuu wa 39 wa SADC.

Pamoja na kutoa shukrani kwa waandishi wa habari nchini Tanzania kwa kazi hiyo nzuri, ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ni vema akaliweka wazi suala la Burundi kuhusu kujiunga na SADC.

Amefafanua kuwa, wakuu wa nchi za jumuiya hiyo wamepokea ombi la Burundi la kutaka kujiunga na jumuiya hiyo lakini nchi hiyo imekidhi vigezo vya kujiunga kwa asilimia 70 na imebaki asilimia 30 ambayo watatakiwa kukamilisha.

"Waandishi wa habari ifahamike nchi ya Burundi haijakataliwa ila bado hawajakidhi viwango, ukiwa mwanachama kuna ada na katika kigezo hicho bado hawajakidhi, hivyo watajiunga baada ya kukidhi vigezo vilivyopo ndani ya jumuiya hiyo,"amesema Waziri Kabudi.

Wakati huo huo Waziri Kabudi amewashukuru waandishi wa habari, wahariri na vyombo vyote vya habari nchini kwa namna ambavyo wameungana kufanikisha jambo hilo kubwa la kitaifa.

"Tunawashukuru waandishi na wahariri wote wa habari nchini, mmefanya jambo kubwa kwa ajili ya nchi yetu. Mmehakikisha mkutano wa SADC unafanikiwa na kweli mmeonesha uzalendo mkubwa kwa nchi yetu.Tumeungana sote kwa umoja wetu na hapa nishauri kwenye mambo yanayohusu Taifa tuwe wamoja,"amesema Waziri Kabudi.

Amesisitiza waandishi wa habari wamehakikisha Afrika na Dunia inafahamu kila kinachoendelea kwenye mikutano ya SADC na kueleza kuwa sasa kazi ndio imeanza kwani Tanzania kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo kuna vikao 32 ambavyo vitafanyika nchini. 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akifafanua mbele ya Wakuu na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar,kuhusu  nchi ya Burundi  kukataliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),ambapo ameeleza kuwa nchi hiyo haijakataliwa, ila bado haijakidhi vigezo.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi leo Agosti 21, 2019 jijini Dar es Salaam akizungumza na wahariri na waandishi wa habari nchini ambao alikutana nao kwa ajili ya kuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wameifanya kwa kuandika vema habari za mkutano Mkuu wa 39 wa SADC.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi  akipewa mkono wa Pongezi  kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro  mara baada ya kuzungumza na  Wakuu, na Wahariri Wakuu wa Vyombo vya habari, leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar.Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe.

TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA BILIONI 1.7 KUTOKA BENKI YA DUNIA

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimkabidhi zawadi ya picha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki na Serikali ya Tanzania.
Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara hiyo, Bw. Shogholo Msangi, wakifuatilia mazungumzo kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na Serikali ya Tanzania
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagamba (wa pili kushoto), akieleza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), Jijini Dar es Salaam. (Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam


Uhusiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania umeimarika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia nchi 22 zilizoko Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kwa Tanzania fedha zote za mkopo wa masharti nafuu kiasi cha dola za marekani bilioni 1.7 zilizobaki katika mgao wa 18 wa IDA.

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutolewa kabla ya kuanza mgao mpya wa 19 wa IDA utakaoanza Julai 2020, baada ya kukamilisha taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo.

”Fedha hizi zitaelekezwa katika kutekeleza miradi kadhaa muhimu ikiwemo ya Elimu, Afya, Mradi wa kusaidia Kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Awamu ya Pili na Uendelezaji wa Miji na Masuala ya Uchumi Jumuishi Visiwani Zanzibar” alisema Bi. Kabagambe

Aidha, alipongeza hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupiga vita rushwa na ufisadi nchini pamoja na kutekeleza miradi ya jamii kwa umahili mkubwa ikiwemo miradi ya kimkakati ya reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa pamoja na mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya maji katika mto Rufiji wa Julius Nyerere.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameiomba Benki hiyo kuisaidia Serikali kwa kuipatia fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya umeme, reli, maji safi na salama, kuimarisha sekta ya kilimo, viwanda, bandari, rasilimali watu na masuala ya teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.

Alibainisha kuwa miradi hiyo itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini wa wananchi kwa kuwa nishati ya umeme itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda hivyo na kukuza ajira, wakati reli imara na ya kisasa itaimarisha mtandao wa reli na kuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya Tanzania na nchi za Ukanda wa Afrika kwa ujumla.

Amepongeza pia uamuzi wa Benki hiyo wa kuruhusu upatikanaji wa fedha kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.7 na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika sekta ya elimu, kusaidia kaya maskini kupitia TASAF, kuendeleza masuala ya uchumi jumuishi Visiwani Zanzibar, masuala ya ardhi na miundombinu ya barabara ili kuboresha shughuli za kiuchumi katika jamii.

Akitoa majumuisho ya mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Mgeni wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali inapongeza uamuzi wa Benki wa kuendelea kuipatia fedha serikali ya Tanzania kwa manufaa ya wananchi.

Mpaka sasa, Benki ya Dunia imefadhili miradi 28 ya Maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.0 sawa na takriban sh. trilioni 11.5, ambapo miradi 20 ni ya kitaifa yenye thamani ya dola 4.065 bilioni na miradi 8 ni ya kikanda yenye jumla ya dola za Marekani 938 milioni.

MBUNGE SINGIDA KASKAZINI APONGEZA UENYEKITI WA RAIS MAGUFULI NCHI ZA SADC

$
0
0
Na Ripota Wetu, Michuzi TV

MBUNGE wa Singida Kaskazini Justine Monko amempongeza Rais John Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) katika mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo uliomalizika Jumapili Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, Monko amesema hatua ya Rais Magufuli kuteuliwa katika nafasi hiyo ni faraja kwa watanzania wote wakiwemo wananchi wa Jimbo la Singida Kaskazini ambao siku zote wamekuwa wakimuunga mkono kwa juhudi zake za kulileta Taifa maendeleo.

Amesema yeye pamoja na wananchi wa Singida Kaskazini wana imani kubwa na Mwenyekiti huyo mpya wa SADC katika wadhifa wake huo mpya kutokana na kuonesha mafanikio mazuri ya uongozi wake katika Taifa tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa taifa hili katika uchaguzi wa Mwaka 2015.

"Tunaamini ataitendea haki SADC kama ambavyo amekuwa akifanya katika Taifa hili, kwani katika kipindi ambacho amekuwepo madarakani amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo na ujenzi wa uchumi kitu ambacho watu wengi hawakudhani kama kingafanyika, imani hiyo aliyotupa ndiyo tunayoamini kuwa ataiendeleza SADC,"amesema Monko.

Aidha amesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, pia mkutano huo wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo ulifana chini ya Uenyeji wake huku hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa Maendeleo ya Jumuiya hiyo na wananchi wake.

"Jambo hili litazidi kuhimarisha umoja na mshikamano wa nchi hizo kama alivyokuwa ameligusia katika hotuba yake alipokuwa akifunga mkutano huo.Kauli ya Rais Magufuli kusema Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonesha ni kwa namna gani ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania,"amesema.

Amefafanua kimsingi mambo mengi ambayo Rais Magufuli amegusia katika hotuba yake hiyo yana akisi yale anayoendelea kuyafanya hapa nchini ambayo kwa kiasi kikubwa matokeo yake yanaonekana kwa kadri siku zinavyozidi.

Ametoa rai kwa nchi za SADC kuyatekeleza ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa na kuongez hatua ya Rais Magufuli kuzitaka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuweka mkazo katika usimamizi wa rasimali zake una maana kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Kuhusu lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa miongoni lugha ya nne za kutumika katika mikutano ya SADC, Mbunge huyo amesema kunaleta fahari kwa Tanzania kwa kuwa itazidi kulitangaza nchi yetu.

WANAOTUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUITANGAZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA NA PROFESA KABUDI

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAPANDA baiskeli kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo kwa lengo la kuitangaza jumuiya hiyo pamoja na na utengamano.

Wakizungumza leo Agosti 21,2019 jijini Dar es Salaa mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, wapanda baiskeli hao wamesema lengo lao ni kuhakikisha wanapeleka ujumbe kwa wananachi kuifahamu vema jumuiya hiyo.

Kiongozi wa wapanda baiskeli hao John Balongo amemueleza Waziri Kabudi wamekuwa wakifanya hivyo kwa nia njema na wanaamini hiyo itasaidia kuifanya jamii kuwa na uelewa kuhusu jumuiya hiyo.

Pamoja na kufafanua kwa kina kuhusu ziara hiyo kwa nchi hizo, amesema changamoto kubwa waliyonayo ni fedha kwani hawana wafadhili zaidi ya kutumia fedha zao mfuko au kupata msaada kutoka kwa nchi za Afrika Mashariki.

"Ombi letu kubwa ni kupata ufadhili kwani itatusaidia kufanikisha safari yetu hii.Tunaenda kwenye nchi zetu kwa kutumia fedha za mfuko, hivyo tutashukuru kama tutapata msaada wenu,"amesema Balongo.

Kwa upande wake Waziri Kabudi amewapongeza kwa uamuzi wao wa kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo na kuwataka waendelee na moyo huo.

"Ni jambo jema kuitangaza Afrika Mashariki na utengamano.Hata hivyo hili la kupata msaada wa kifedha Serikali inao utaratibu wake , hivyo nitalifikisha ili utaratibu wa Serikali utumike,"amesema Waziri Kabudi.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akimkabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mratibu wa Waendesha Baiskeli wa Tanzania, Morris Manyori, kwa ajili ya wapanda Baiskeli wa 'East African Bicycle Tour' wanaofanya Tour ya kuzunguka katika Nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Muungano na umuhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo walianzia Uganda, Kenya na sasa wamefika Tanzania.  Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. 
WAPANDA baiskeli kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo kwa lengo la kuitangaza jumuiya hiyo pamoja na na utengamano.Pichani waendesha baiskeli hao wakiwasili leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam,ambapo Waziri Kabudi aliwakabidhi bendera.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akimkabidhi Bendera ya Tanzania, Mratibu wa Waendesha Baiskeli wa Tanzania, Enock Bernad , kwa ajili ya wapanda Baiskeli wa 'East African Bicycle Tour' wanaofanya ziara ya kuzunguka katika Nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Muungano na umuhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo walianzia Uganda, Kenya na sasa wamefika Tanzania. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Idara ya Miundombinu  na Huduma  za Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Eliabi Chodota  akizungumza jambo mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi,leo jijini Dar
Kiongozi wa wapanda baiskeli hao John Balongo akisoma hotuba yao kwa Waziri Kabudi

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akifungua Mkutano wa kujadili utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuanzia mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019 na Uongozi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 21-8-2019. Kulia kwa Mhe. Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma. 
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Mshauri wa Rais Pemba Mhe Maua Abeid Daftari , wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani akingoza mkutano huo wa Utekelezaji wa Bajeti na na Mpango Kazi wa Wizara hiyo, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar. 
BAADHI ya Maofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar , wakifuatilia Mkutano wa kupitia Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Idrisa Muslim Hijja akiwasilisha Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, Ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. 

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati wa mkutano huo na Uongozi wa Wizara yake uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, 21-8-2019. (Picha na Ikulu)

OFISA UCHAGUZI NEC ATOA USHAHIDI WAKE KATIKA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA AKIWEMO MBOWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Januari mwaka jana alivitangazia vyama vyote vya siasi nchini kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Ofisa Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni, Victoria Wihenge ameeleza hayo leo Agosti 21,2019 wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, Wihege ambaye ni shahidi wa sita wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo amedai, taarifa ya tume ilielekeza kwamba uchaguzi huo unapaswa kufanyika Februari 17, 2018.

Amedai, baada ya taarifa hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi manispaa hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni aliitisha kikao cha wadau wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini.

Na kwamba jumla ya vyama vya siasa 19 vikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa Wilaya vilishiriki katika kikao hicho ambacho lengo lake lilikuwa ni kuwajulisha tarehe ya uchaguzi, siku ya kufanya uteuzi wa wagombea ubunge na kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

"Miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho ni Chadema, CCM, Ada Thadea, AFP, CUF, UND, Demokrasia Makini, TLP na NRA. Viongozi wa vyama hivi tuliwataarifu kuhusu uwepo wa uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kinondoni na ushiriki wao katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika," alidai Wihenge.

Ameendelea kudai kuwa, baada ya kikao hicho wajumbe walienda kufanya maandalizi ya kuchukua fomu na uteuzi ambapo fomu zilianza kuchukuliwa Januari 14 hadi Januari 20,2018 ambapo kila chama kilitakiwa kupeleka jina la mgombea mmoja wa ajili ya kulipeleka katika kamati ya maadili na kamati ya kampeni.

Aidha alitaja mambo ya kuzingatia katika uchaguzi ikiwamo kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na katiba kuanzia tarehe ya kutangazwa uchaguzi hadi kufanyika kwa uchaguzi.

Mapema akimalizia kutoa ushahidi wake, shahidi wa sita Koplo Charles amedai alipangiwa na bosi wake kuripoti mkutano wa kufunga kampeni jimbo la Kinondoni na kwamba katika video iliyooneshwa mahakamani hapo haikuwa na tarehe kwa sababu hakuseti kamera yake ionyeshe vitu hivyo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori shahidi huyo ameendelea kudai kuwa alishindwa kuendelea kurekodi matukio katika mkutano huo wa Chadema kutokana na kauli vya viongozi hao ambazo zilikuwa zinatishia amani.

Alidia hakukuwa na kibao wala alama ya utambuzi, na kwamba yeye alienda pale kwa ajili ya kuchukua matukio ya mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chadema.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

WANAWAKE WAWILI WAFIKISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MASHITAKA 7 IKIWEMO BIASHARA YA UPATU NA UTAKATISHAJI FEDHA.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, 

WANAWAKE wawili, Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka saba yakiwemo ya kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kati ya Aprili Mosi, 2017 na Juni 30, 2017 washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kusimamia na kuendesha biashara ya upatu.

Katika shtaka la pili imedaiwa, tarehe na mahali hapo, washitakiwa walikusanya fedha kutoka kwa watu mbali mali ambazo walikuwa wakichangia kwa kuwaahidi kuwapatia faida watakayopata.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kujihusisha na muamala wa USD 394,265 kwenye akaunti ya Magdalena na Halima kupitia Benki ya Equity Tanzania Ltd wakati wakijua kwamba fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kuendesha biashara ya upatu.

Inadaiwa Aprili 22, 2017 maeneo ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa kwa lengo la kuficha chanzo halali cha fedha hizo, walihamisha USD 12,309 kwa Benki ya Equity Uganda kwa jina la Smart Magara.

Pia Aprili 24,2017 washitakiwa hao wanadaiwa kuhamisha USD 29,890 kwenye akaunti ya jina hilo.

Aliendelea kudai Aprili 25,2017 maeneo ya jiji la Dar es Salaam washitakiwa hao walihamisha USD 58,743 kupitia benki hiyo ya Equity Uganda.

Pia inadaiwa Aprili 21,2017 washitakiwa walihamisha USD 83,718 kwenye benki ya Equity Uganda kwa jina la Magara huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la makosa ya kuendesha biashara ya upatu.Hata hivyo, wshitakiwa wamekana kutenda makosa hayo na kwa mujibu wa sheria mashitaka wanayoshitakiwa nayo washitakiwa hao hayana dhamana

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.Wakili wa utetezi, Peter Kibatala anayewatetea washtakiw aliomba mahakama kupanga tarehe fupi kwa ajili ya kutoa hoja za kisheria kuhusu uhalali wa hati ya mashitaka.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30, mwaka huu kwa ajili yakutajwa.

KENYA YACHAGULIWA KUWA MWAKILISHI BARA LA AFRIKA KWENYE BARAZA LA ULINZI NA USALAMA LA UN

$
0
0
KENYA imechaguliwa rasmi kuwa mwakilishi wa bara la Afrika kwenye baraza la ulinzi na usalama la UN kwa mwaka 2020/2021.

Rais waKenya Uhuru Kenyatta amepokea taarifa hiyo kutoka UN kwa nchi hiyo kuwa sehemu baraza la ulinzi la UN kwa kushirikiana na kuziwakilisha nchi za bara la Afrika.

Kenyatta amesema kuwa umoja wa nchi za Afrika ni alama inayoonesha imani kwa nchi hiyo katika uwezo wao wa kuliwakilisha bara la Afrika kimataifa.

Kenya imeshinda imeshinda uwakilishi huo kwa kupata kura 37 dhidi ya kura 13 walizopata Djibouti's uchaguzi uliofanywa na wanachama na wawakilishi wa umoja wa Afrika leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Kenyatta ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwa mwaka 2020/2021 na kuahidi kushirikiana katika kudumisha amani na ulinzi.

TANZANIA NI SALAMA KWA UWEKEZAJI,HUSUSAN MKOANI PWANI AMBAPO BADO KUNA MAENEO YA KUTOSHA-NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,amesisitiza kwamba ,Tanzania hususan mkoani Pwani ni salama kwa uwekezaji na amekemea propaganda na uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa kuwa hakuna uwekezaji unaoendelezwa.

Aidha amewaasa ,wawekezaji na wenye viwanda kuhakikisha wanasajili namba za utambulisho ya mlipa kodi (TIN no) kwa meneja wa mamlaka ya mapato (TRA )mkoani hapo ili hali kuongeza pato la mkoa.

Ndikilo alitoa rai hiyo, wakati alipokwenda kuweka mawe ya msingi katika viwanda vitano vilivyopo wilayani Mkuranga.

"Rais dkt.John Magufuli amekuwa akisisitiza uwekezaji na ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati, sasa akitokea mtu kukwamisha jitihada hizo anakuwa halitakii mema Taifa, :"'Pia mkoa wetu kupitia halmashauri umetenga maeneo hekta 22,937 kwa ajili ya uwekezaji ,nawaomba wawekezaji waje kuwekeza ."alifafanua Ndikilo.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wenye viwanda kujali mikataba,haki,maslahi ya wafanyakazi kwa kuzingatia sheria pamoja na kuwapa likizo na kuwawekea vitendea kazi .

Awali mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha matofali yenye ubora (Shaffa Ltd) kitongoji cha Kiguza, Suleiman Amour alibainisha ,ujenzi wa kiwanda umeanza 2018 kinatarajia kitakamilika mwaka 2019.

Amour alisema, lengo la mradi huo ni kuongeza wigo katika sekta ya ujenzi ,na ujenzi utagharimu sh.bilioni 15.3 hadi kukamilika ambapo itatoa ajira 200 mradi ukikamilika.

Kwa upande wake, msimamizi usafirishaji wa kiwanda cha super meals (Cool Blue) kilichopo Vianzi, Charles Malini alisema, ujenzi wa kiwanda umegharimu bilioni 2.7, kuna ajira 50 ,kinalisha maji ya kunywa ya chupa kwa matumizi ya majumbani na ofisini ambapo wanazalisha ujazo mbalimbali kuanzia nusu lita hadi lita 18.

Alitaja changamoto zinazowakabili ni kukosa umeme wa uhakika na miundombinu ya barabara isiyo rafiki .

Ndikilo alizungumzia tatizo la barabara na kuwaeleza ,ataangalia namna ya kuingiza hoja hiyo katika kikao cha barabara kijacho ili kiweze kutetea ipandishwe hadhi ihudumiwe na Tanroads.

Meneja wa shirika la umeme-TANESCO wilayani Mkuranga, Octavian Mmuni alisema tatizo la kukosekana umeme wa uhakika hutokana na maboresho yanayofanyika mara kwa mara.Mmuni alieleza, kwa sasa shirika hilo limetenga sh.milioni 261 ili kusaidia kubadili nguzo na nyaya chakavu.

Viwanda vingine vilivyowekwa mawe ya msingi katika wilaya hiyo ,ni kiwanda kinachozalisha zana za uvuvi Taxtrade T2 Ltd ,cha nyaya za umeme -Plug Ltd na kiwanda cha kutengeneza masufulia cha Maxima.




DC Ikungi apongezwa kwa kusimamia miradi ya Maendeleo

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Edward Mpogolo amepongezwa kwa namna ambavyo ameweza kusimamia miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi ya maendeleo wilayani Ikungi.

Miradi mitano ya Maendeleo iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Darajani, Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Ighuka, Mnara wa Mwenge wa Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi ambapo miradi yote hiyo imegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.162.

Akizungumza Wilayani hapo Kiongozi huyo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuwafanya Watanzania waendelee kuiamini Serikali yao chini ya Rais Dk John Magufuli.

" Niwapongeze sana Wananchi wa Ikungi kwa namna ambavyo mmeendelea kumuamini Rais wetu Dk Magufuli, kipekee nikupongeze DC Mpogolo kwa uzalendo wako unaouonesha toka uteuliwe na Mhe Rais kuwa Mkuu wa Wilaya hii, nikuombe uendelee kuwatumikia wananchi wetu kwa kasi hii hii uliyoanza nayo.

" Niwaombe pia ndugu zangu wa Ikungi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muende kuwachagua viongozi ambao ni waadilifu na wenye kuichukia rushwa, msichague viongozi mafisadi, chagueni watu safi watakaoweza kuwatumikia bila kujali itikadi zenu," amesema Mzee Mtongea.

Kwa upande wake DC Mpogolo ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya Serikali kwa uadilifu pamoja na kuwatumikia wananchi hawa ambao walimuamini Rais Dk Magufuli na kumpa kura.

DC Mpogolo amesema atahakikisha wananchi wa Ikungi wananufaika na miradi ambayo imezinduliwa ndani ya Wilaya hiyo ili waweze kuona kazi kubwa ambayo Serikali inaifanya katika kuwahudumia.

" Miradi hii imegharimu Fedha nyingi upo ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanaakisi Sera ya Elimu bure inayosimamiwa na Rais wetu kipenzi, mradi wa Maji kama sehemu ya kampeni yetu ya kumtua Mama ndoo kichwani, yote hiyo ni katika kuwatumikia nyinyi wananchi wetu na zaidi kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa kwenu mwaka 2015.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally (wa mbele) akikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Darajani Wilayani Ikungi ambapo aliridhishwa na ujenzi huo na kuuzindua.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Edward Mpogolo (katikati) akizungumza mbele ya wakimbiza Mwenge Kitaifa wakati Mwenge ulipofika kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya yake
Sehemu ya wananchi wa Eneo la Puma wilayani Ikungi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru uliofika Wilayani hapo kukagua miradi ya maendeleo

WADAIWA SUGU NYUMBA ZA TBA DODOMA WAANZA KUONDOLEWA

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imewatolea uvivu wapangaji wake ambao wamekuwa sugu kwa kutolipa kodi ya pango kwa wakati hali iliyosababisha kuwatolea vitu vyao nje kutokana na kudai zaidi ya bil 1.5 huku wabunge wakitajwa kuhusika.

Pia wastaafu nao watakiwa kuhama katika nyumba hizo kwani TBA wanaamini kuwa mtu akishastaafu anauwezo wa kuwa na nyumba yake mwenyewe.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma Helman Tanguye baada ya kufanya zoezi hilo alisema kuwa wadaiwa hao wamelimbikiza madeni yao kwa miaka 10 sasa.

Amesema kuwa TBA imekuwa ikidai fedha nyingi sana na hasa katika mkoa wa Dodoma kwa wafanyakazi wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali ambazo wamezipangisha.

“Mpaka sasa tunadai zaidi ya bil 1.5 hivyo lengo kuu la TBA ni kuwaondoa wale watu walioshindwa kulipa kodi ya pango kwa wakati ili watu wanaohamia kutoka mikoa ya Dar es salaam na mingineyo nao waweza kupata nafasi”alisema Tanguye.

Akizungumzia zoezi zima walivyolianza alisema kuwa “tumelianza jana baada ya kufanya taratibu zote za kisheria na mikataba inavyosema kwahiyo tuliwapa notes ya siku 30 badaye tukaongeza Siku 14 lakini zilivyokwisha tulichukua vyombo ambavyo vinatambulika na mahakama ili tuweze kuwaondoa.

Amesema kampuni wanayoitumia katika zoezi zima la kuwatolea watu vitu vyao nje ni Yono Auction Mart ambayo wamekuwa wakiitumia mara kwa mara katika shughuli zao.

Wakati huo huo Tanguye alisema kuwa TBA ukiacha kazi yake yakujenga nyumba lakini pia inamiliki nyumba ambazo imewapangisha wananchi,taasisi,makampuni ,na wabunge lakini chakushangaza watu hao wamekuwa wakikaidi kulipa hata baada ya kupewa notes ya mwezi mmoja"

“Zoezi hili hapo awali lilifanyika jijini Dar es salaam lakini kwa sasa limehamia jijini Dodoma ambapo litakuwa endelevu kwa mikoa yote nchini”alisema.Pia wapangaji amabao hawajahuisha mikataba yao ya mwaka basi nao wanahusika kuondolewa kwani wanaonyesha kyuwa hawana nia ya kuishi katika nyumba hizo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Afisa miliki fredy mangala amesema kuwa mnamo juni 30 waliwasisitizia kuwa wametoa notes hivyo wanaodaiwa waende wakalipe lakini baada ya kuona wamekaidi agizo hilo wakaona bora kuchukua hatua hizo za kuwatolea vitu vyao nje.

“Wale wote wanaodaiwa na waliopata notes walipe madeni hayo kama inavyotakiwa hivyo zoezi hilo litakuwa endelevu kwani sheria inakataza kwa mtumishi wa umma kuwa na madeni.Amesema kuwa fedha zaidi ya bil.1.5 ni nyingi sana kwani wangeweza kuzitumia ongeza nyumba nyingine eneo la Nzuguni ambapo wana eneo la hekali 630.

Mangala alisema kuwa wabunge nimiongoni mwa watu wanao daiwa hivyo wanachotakiwa ni kutekeleza majukumu yao kama mikataba inavyosema nakusema kuwa wao kama wakala wataendelea kutekeleza wajibu wao.

“Lakini endapo pia kuna mbunge atafikia kiwango cha kutolewa basi itabidi atolewa ingawa kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakijitokeza na kutuonesha ushirikiano”alisema.Hata hivyo Malanga alisema kuwa mikataba hiyo inaelezea mtumishi akistaafu,akifariki au kuhamishwa mkoa mwingine inabidi kuachia nyumba ,hivyo katika zoezi hilo wanalolifanya pia wanaangalia watu hao.
Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma, Helman Tunguye akizungumza na wanahabari ofisini kwake Jijini Dodoma

TMDA YATOA UFAFANUZI KUHUSU UVUMI WA DAWA AINA YA P-500 (PARACETAMOL)

BODI YA WAKURUGENZI YA MAZIWA TANZANIA YAVUNJWA


MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI HAYA HAPA.

MASHINDANO YA MISS TANZANIA KURINDIMA AGOSTI 23 MWAKA HUU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania nchini, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akiwa na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na warembo hao (waliosimama) leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii, ambapo ameeleza kuwa maandalizi yapo tayari na mashindano yatakuwa ya aina take, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa shindano la Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKURUGENZI wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) Basila Mwanukuzi Shayo amesema kuwa fainali za mashindano hayo yatahitimishwa rasmi siku ya ijumaa, Agosti 23 huu katika ukumbi wa Millenium Tower LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwanukuzi amesema kuwa washiriki wapatao 20 kutoka Mikoa mbalimbali nchini wapo kambini tangu Agosti 12 wakijiandaa na kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

"Kufanyika kwa fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya Mikoa ambayo yalifanyika kuanzia mwezi April mwaka huu" ameeleza.

Ameeleza kuwa kwa kipindi walichokuwa kambini washiriki wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutembelea, kuwafariji na kucheza michezo mbalimbali na watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam  pamoja na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

"Washiriki wakiwa kambini pia walipata nafasi ya kufanya mashindano madogo madogo kwa mujibu wa mashindano ya dunia ambapo walifanya mashindano ya kumtafuta mrembo mwenye kipaji, mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu, na washindi watatangazwa siku ya tukio" ameeleza Mwanukuzi.

Mashindano hayo yanategemewa kuwa ya aina yake ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi zao ili waweze kumshuhudia mlimbwende ambaye ataliwakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya dunia.

Kamati ya ulinzi na usalama wa mwanamke na watoto kuzinduliwa

MPANGO KAZI WA UENDELEZAJI MIJI KUFANIKISHA HUDUMA ZA KIJAMII

$
0
0

Na. Josephine Majura, WFM, Dodoma
SERIKALI imezindua rasmi Mpango Kazi wa Uendelezaji Miji Tanzania ili kuhakikisha nchi inakuwa na miji iliyopangwa na makazi yenye huduma zote za kijamii ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21.

Mpango huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango kazi huo, Waziri Jafo alisema kuwa Serikali imejidhatiti kuandaa mipango miji madhubuti ambayo imezingatiwa katika miongozo ya kuandaa mipango ya taifa.

“Serikali inazindua rasmi Mpango huo ili kuleta mpangilio mzuri wa Miji wenye manufaa kwa Taifa na kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa nchi”, alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa mpango huo umejikita katika maeneo manne ambayo ni matumizi ya lugha ya mpango kazi, suala la utawala na kanuni, mkakati wa fedha pamoja na kuchunguza njia za kukuza uchumi kwa kutambua njia ambazo zitachochea ukuaji wa uchumi katika viwango vya juu.

Alisema kuwa maeneo hayo manne ni muhimu kufanya ukuaji wa miji kuwa mchakato wenye manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kuwa unatoa mapendekezo ya msingi kwa wakati ambayo ni muhimu kwa upangaji wa maendeleo ya miji nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula, alisema kuwa ukuaji wa miji ni suala pana ambalo linahitaji wadau wengi kuunganisha juhudi ili kuhakikisha ukuaji wa miji inayosimamiwa kikamilifu.

Dkt. Mabula amesema kuwa, wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano katika kuleta pamoja jitihada za kila taasisi ili kuepuka jambo moja kufanywa na wadau zaidi ya mmoja, lengo likiwa kufanikisha malengo ya nchi iliyojiwekea. 

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolph Ndunguru, aliwashukuru viongozi na wote waliohudhuria katika hafla hiyo muhimu kwa Taifa na kueleza kuwa mpango huo utasaidia kutatua changamoto za upangaji miji kwa maendeleo ya uchumi na Taifa kwa ujumla. 


Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa kiuchumi na Kijamii, Dkt. Tausi Kida, amesema Mpango huo utasaidia katika uandaaji wa mipango ya kitaifa ya uendelezaji miji pamoja na uandaaji wa sera kwa kuwa uliotokana na utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii kwa kuwa uliofanywa kwa kufuata kanuni za kisayansi za ufanyaji tafiti.

MKUTANO MAALUMU NCHI WANACHAMA JUMUIYA YA MAWASILIANO KUSINI MWA AFRIKA WAFANYIKA TANZANIA

$
0
0

Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL alipokuwa akifungua mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo.   

Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL alipokuwa akifungua mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo. 

Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark. 

Meneja Maendeleo wa Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Enocent Msasi akichangia mada katika Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA).

Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa (kushoto) akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Katibu Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA), Eng. Jacob Munodawafa akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani).

Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Maalum wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakifuatilia mada anuai katika Hotel ya Landmark. 

Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark. 

Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Alex Ntanguligwa akiwaonesha wajumbe picha ya Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli iliyokuwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) uliokutanisa wajumbe mbalimbali jijini Dar es Salaam kujadili masuala anuai ya mawasiliano kutoka nchi hizo ukiendelea katika Hotel ya Landmark. 

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano maalum wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mawasiliano ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Telecommunication Association-SATA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo kwenye Hotel ya Landmark. 


Viewing all 110105 articles
Browse latest View live




Latest Images