Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

X-MAS REGGAE BEACH PARTY

$
0
0
....it's X-MAS REGGAE BEACH  PARTY..at One LOVE Lounge-ngonda BEACH-kigamboni....live REGGAE  performance by JHIKO MAN & afrikabisa band..also non stop reggae mixing by top REGGAE DJs..lot's of beach games & kids program...ALL on Christmas day-25 -DEC.. ALL from morning till late night....never miss dis...

mavituzzzzz ya DJ CHOKA & CO.

TAARIFA TOKA TFF LEO Desemba 23, 2013

$
0
0
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu TFF

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

 Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TBL YAENDESHA SHINDANO LA UONJAJI BIA KWA WANAHABARI MWANZA

$
0
0
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima,Sitta Tumma akionja bia kwenye shindano la kuonja bia lililoandaliwa katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.

 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuendesha zoezi la kuonja bia katika Kiwanda cha Bia cha TBL Mwanza juzi.

SEGEREA VETERANS WAANDA BONANZA YA KUMKUMBUKA MCHEZAJI MWENZAO ALIYEFIA UWANJANI

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kushinda fainali hiyo walielekea meza kuu ilipokuwa picha ya mchezaji mwenzao marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o na kumwombea mungu ampumzishe mahali pema.
 Hapa ni furaha  kwa timu ya Segerea Veterans Sports Club baada ya kuchukua ubingwa
Mmoja wa mashabiki wa timu ya Segerea Veterans Sports Club akiwa amebeba picha ya marehemu Jacob Arid kwa jina maarufu Oming'o baada ya kumalizika kwa bonanza hilo.

Article 14

Airtel, Baraza la Usalama Barabarani kuhamasisha Usalama barabarani msimu wa sikukuu

$
0
0
· Watanzania waaswa kutumia huduma ya 
bure ya Airtel Money kutuma na kutoa pesa Dar es Salaam

Kampuni ya mitandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza ushirikiano wake na Baraza la Taifa la Usalama barabarani katika juhudi za kuelimisha uma kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani hususani msimu huu wa sikukuu. 
Airtel imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kikosi cha Usalama Barabarani katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kudhamini kampeni mbalimbali.
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) akisisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kujikinga na ajali za barabarani kwenye msimu huu wa sikukuu leo wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.  Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akifuatiwa na Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi.Hawa Bayumi alisema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wananchi wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili kujikinga na ajali za barabarani.
“Hiki ni kipindi ambacho wananchi wanapaswa kuwa makini sana katika kuhakikisha wanajilinda na wimbi la ajali za barabarani ambazo husababisha asara kubwa kwa taifa, na pia madereva wajitaidi sana kuepuka ulevi wa kupindukia,” alisema Hawa.
Aliongeza kwa kusema pia katika msimu huu wateja wa Airtel wanaweza kutumia huduma ya Airtel money kutuma na kupokea pesa bure mahali popote nchi nzima kuepuka kutembea na viwango vikubwa vya pesa.
 Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya umuhimu wa kujikinga na ajali za barabarani  katika msimu huu wa sikukuu pia kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake wananchi watumie huduma ya Airtel money. Kushoto kwake ni Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi pamoja na Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi. Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam leoDCP Mohammed Mpinga alisema Lengo la kampeni hizi ni kupunguza ongezeko la ajali za barabarani pamoja na madhara yake kwa kipindi cha sikukuu za mwaka huu 2013/2014 na wanajitaidi kuhakikisha elimu inatolewa ipasavyo. 
“Tunashukuru Airtel kwa kuungana nasi katika kujali usalama wa watanzania, kazi ya  kuelimisha watumiaji wa barabara ni kubwa na hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutuunga mkono ili kusaidia kufikisha ujumbe. Lengo hili litatimia kwa kushirikiana na wadau katika kufanya operasheni mbalimbali pamoja na kutoa elimu.” Alisema DCP Mpinga.
Mpinga alitumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wote kote nchini kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake watumie huduma ya Airtel Money kutuma, kuweka na kutoa pesa.
Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi akizungumzia athari zinazotokana na ajali za barabarani na kuwaasa wananchi waziepuke hususani katika msimu huu wa sikukuu. Bw. Athumani Hamisi alisema Kuelekea mwisho wa mwaka, matukio ya ajali za barabarani yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi kutokiuka taratibu hizo.
“Ukiukwaji wa sheria husababisha sana ajali za barabarani, wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepusha ongezeko la ajali hizo ambazo hutokea mara kwa mara haswa katika msimu huu wa sikukuu.” Alisema Athmani.

NEWS ALERT: BAADA YA KIPIGO CHA 3-1 NA SIMBA JUZI KATIKA 'BONANZA' YA NANI MTANI JEMBE, YANGA YAMTIMUA KOCHA WAKE ERNIE BRANDTS

$
0
0
Masaa 24 tu baada ya  Yanga kupigwa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Simba, uongozi wa klabu hiyo umemfungashia virago kocha wake Ernie Brandts, kufuatia uamuzi wa kikao cha kamati ya utendaji ya Yanga iliyoketi muda mchache baada ya mchezo wao na Simba. 

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Binklebu amesema leo jijini Dar es salaam kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kupokea maoni ya wachezaji mbali mbali wa zamani kuhusu kiwango cha timu. 

 "Tumempa notisi ya siku 30 ili tuendelee kutafuta kocha mwingine, na tupo kwenye mchakato wa kumlipa stahiki zake, tuachane kwa amani. 
 “Mwanzoni alipandisha kiwango cha timu, kilipanda sana, lakini baadaye kiwango kikaanza kushuka, tukasema tumpe muda kidogo, lakini tunaona mambo yanazidi kuharibika, hivyo tumeamua kuachana naye kwa sababu hana jipya, sisi tunalenga michuano ya kimataifa zaidi sasa kwa kiwango hichi hatutafika mbali ni lazima tuchukue hatua za haraka zaidi,”alisema. 

 Kuhusu Wajumbe wengine wa benchi la Ufundi, Bin Kleb alisema kwamba taratibu nyingine zinafuata na ndani ya wiki hii kuna maamuzi mengi makubwa ambayo klabu yake itayafanya. 
 Hata hivyo tayari Brandts alikabidhiwa barua yake ya kusitishiwa mkataba rasmi juzi na jana baada ya mazoezi Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga alikutana na wachezaji na kuzungumza nao kwa zaidi ya nusu saa. 
Kocha Brandts amesema  kwa kifupi "Nasubiri notisi ya siku 30 imalizike. Kuna kitu nitaongea lakini sio sasa. Sasa hivi msikilizeni Abdallah (Binkleb) anachosema ukifika muda na mimi nitazungumza."

POLISI YAZINDUA BODI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI

$
0
0
Na  Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhia kuundwa kwa bodi ya Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi itakayosaidia kuongeza mapato ya Jeshi la Polisi ili kuendelea kuboresha huduma ndani ya Jeshi la Polisi na hatimaye kuongeza ufanisi katika kutoa  huduma bora kwa wananchi.
Akizindua bodi hiyo ya Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi yenye wajumbe nane, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mheshimiwa Pereira Silima alisema, moja kati ya vipaumbele ambavyo bodi inapaswa kuviangalia ni pamoja na kuboresha makazi ya askari ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Mheshimiwa Pereira alisema kuwa, kuwepo kwa shirika hilo kwa upande wa jeshi la polisi kutasaidia kuongeza kipato kwa Jeshi ili liweze kuboresha mazingira ya kazi kwa askari wake, huku akitolea mfano wa shirika la Suma JKT pamoja na J`eshi la Magereza 
Nae Mwenyekiti wa bodi hiyo, Bwana Emmanuel Umba alisema yeye pamoja na wajumbe wenzake wa  bodi hiyo, wataifanya kazi waliyokabidhiwa na Serikali kwa weledi na kuhakikisha kuwa wanaleta mrejesho wenye mafanikio ili watanzania wawe salama kwani kwa kuboresha mazingira ya kazi kwa askari wa jeshi la  polisi kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema alisema usalama, amani na utulivu vina gharama kubwa na kwamba majeshi mengine katika mataifa makubwa na yaliyoendelea, wanatumia mfumo huo wa kuwa na mashirika ya uzalishaji mali katika kujipatia kipato cha ziada ili kuboresha huduma katika majeshi yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.

WAZIRI WA UCHUKUZI, DK. HARRISON MWAKYEMBE AFUNGA MWAKA KWA KUWATAMBULISHA RASMI KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO KWA WAFANYAKAZI WA WIZARA LEO JIONI KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
             Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(kulia kwa Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe Katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo. Mkutano huo umefanyika leo jioni katika ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika utendaji kazi wa kila siku.
 Sehemu ya Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo pichani) wakati wa mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Dk. Shaaban Mwinjaka (wa tano kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kushoto) na Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi leo alipokutana nao ili kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na watumishi.
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kulia mstari wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na baadhi ya watumishi wa  Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Uchukuzi)

HAPPY BIRTHDAY ASIA IDAROUS KUFANYIKA DESEMBA 24, NDANI YA NYUMBANI LOUNGE, DAR

$
0
0

Na Andrew Chale. 

DESEMBA 24 ‘kesho’ Jumanne kutakuwa hakutoshi ndani ya mgahawa na ukumbi wa kisasa wa Nyumbani Lounge kwenye bonge la ‘Party’ ya kuzaliwa kwa Mama Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous wa Khamsin, atakapokuwa akitimiza miaka 54. 
Party hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali wakiwemo wa filamu, muziki, mitindo na wabunifu. 
  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashion, na muandaaji wa onyesho kubwa la Kila mwaka la Mavazi lijulikanalo kama … Usiku wa Khanga za Kale, anasema kuwa tayari mandalizi yameshakamilika na wadau mbali mbali wanatarajia kuhudhuria kwenye ‘party’ hiyo itakayokuwa ya aina yake. 
“Kesho Desemba 24, Ni siku yangu ya kuzaliwa, Namshukuru Mungu kwa neema zake kufika hadi leo hii kwa ulinzi na muongozo wake, leo hii mimi kufikia hapa na kutimiza miaka hii 54” alisema Asia Idarous. 
Akitoa nasaha zake kwa wabunifu wa mitindo wanaochipukia hapa nchini, Asia aliwataka wasivunjike moyo kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na maalifa. “Namshukuru Mungu kwa kufikia hapa leo hii na hakika nitaendeleza fani hii pia nawaomba wabunifu na wanamitindo wanaochipukia kuwa na hali ya ushirikiano, kusaidiana, kuchapa kazi na kuwa na ‘tojo’ safi” alisema Asia Idarous Khamsin. 
Aidha, Asia Idarous alisema kuwa milango ipo wazi kwa wabunifu wa mitindo kupata ushahuri wake kwa watakaotaka huku akiwaombea wafike mbali katika kuendeleza gurudumu la mitindo hapa nchini.





REDDS MISS TANZANIA 2013 KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA X MASS NA WATOTO YATIMA KITUO CHA MGOLOLE MOROGORO.

$
0
0
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), tarehe 25 Desemba 2013 atajumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole Orphanage kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. 
Mrembo huo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tano Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013 ambaye ndie atakae kuwa mwenyeji wao wakati wote wakiwa mkoani hapo. 
Ni kawaida kwa Mrembo wa Taifa, Miss Tanzania kila mwishoni mwa mwaka kula X Mass na Watoto Yatima, wasiojiweza pamoja na wale waishio katika mazingira magumu. 
Baada ya shughuli hiyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa atajumuika pia na watoto wa aina hiyo jijini D’salaam siku ya Mwaka mpya tarehe 1 January 2014 katika vituo vingine atakavyopangiwa na  Kamati ya Miss Tanzania. 
Pamoja na shughuli hiyo, Mrembo Happiness Watimanywa pia anakusudia kusaidia jamii wenye matatizo ya Maji kwa kuwachimbia visima vya maji safi katika mikoa ya Dodoma na Singida. 
Miss Tanzania Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Dodoma na Miss Kanda ya Kati 2013, ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu  nchini Scotland ameahirisha masomo yake kwa muda wa mwaka mmoja hadi hapo atakapovua Taji la Mrembo wa Taifa mwishoni mwa mwaka ujao 2014.
  
HIDAN .O. RICCO.
PUBLIC RELATIONS OFFICER
LINO INTERNATIONAL AGENCY

SHAMRASHAMRA ZA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI: SEKONDARI CHASASA NA UTAANI A ZAZINDULIWA PEMBA LEO.

$
0
0

Wasomaji wa utenzi Asha Ali Omar,na Asha Ali Mbarouk,wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Utaani A,na Chasasa, Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra
za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar


Risala ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Chasasa Utaani A,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ,ikisomwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi Zaina Omar Othman,leo baada kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akiwasalimiana wanafunzi na walimu wa Skuli za Sekondari za Chasasa na Utaani A,baada ya kufunguliwa leo, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake kwa Walimu,Wananchi,na Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Chasasa na Utaani A, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu

--- Article Removed ---

$
0
0
***
***
*** RSSing Note: Article removed by member request. ***
***

JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LINAWASHIKILIA WATU SABAKWA MAKOSA MBALIMBALI WALIOKAMATWA KATIKA HARAKATI ZA KUFANYA UHALIFU

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA akionyesha baadi ya vitu walivyokutwa navyo watu saba wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa makosa mbalimbali. 
Sehemu ya vitu hivyo.

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu saba kwa makosa mbalimbali waliokamatwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Kamishna Msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA amesema tukio la kwanza limetokea tarehe 20/12/2013 majira ya saa 23:00 usiku eneo la Kizota Manispaa ya Dodoma ambapo watu sita wamekamatwa wakiwa wamevunja ghala kwa kung’oa bati moja la paa na kuingia ndani.

Kamanda KAGANDA amewataja watu hao amabao ni:


VODACOM YAKABIDHI COMPUTER 3 NA ROUTER MOJA YENYE UWEZO WA KUUNGANISHA COMPUTER 7 KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI DODOMA

$
0
0
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa wilaya chamwino Fatma Ally (wapili kushoto waliokaa) mwakilishi wa vodacom Salum mwalimu (kushoto waliokaa) pamoja na waandishi wa habari mkoa wa dodoma muda mfupi baada ya vodacom kukabidhi msaada wa computer 3 na router ya kuunganisha computer na mtandao kwa chama cha waandishi wa habari mkoa wa dodoma Leo,msaada hug unathamani ya zaidi ya million 5.
Mkuu wa wilaya chamwino Fatma Ally kushoto akimkabidhi mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa dodoma CPC Joyce kasiki kulia computer zilizotolewa na vodacom kama msaada kwa chama waandishi wa habari mkoa wa dodoma ili kusaidia shuguli zao za uandishi wa habari, anayeshuhudia katikati ni mwakilishi wa vodacom Salum mwalimu.Kushoto.
Mkuu wa wilaya chamwino Fatma Ally akisisitiza waandishi wa habari wa dodoma kuboresha utendaji kazi, kufanya tafiti za mtandaoni na kutoa habari na taarifa zenye ubora wa hali ya juu kutumia msaada wa computer 3 na rooter ya kuunganisha mtandao vilivyotolewa na Vodacom kama msaada kwa waandishi hao, hafla yamakabidhiano ilifanyika ofisi za waandishi wa habari mjini dodoma Leo.Msaada.
Mwakilishi wa vodacom Salum mwalimu akielezea azma ya vodacom kusaidia vyama vya waandishi wa habari vya mikoa ili kusaidia kunyanyia ubora wa shughuli za uandishi wa habari hapa nchini, jumla ya computer 3 na rooter ya kuunganisha mtandao vyenye shaman ya zaidi ya milioni 5 vimetolewa na vodacom vodacom kama msaada kwa waandishi wa habari mkoa wa dodoma mapema Leo. (PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA)

MH. REHEMA NCHIMBI AFUNGUA MKUTANO WA UHAMASISHAJI AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOA WA DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akisisitiza kwa wadau mikakati ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) na vifo vitokanavyo na uzazi wakati akifungua mkutano wa uhamasishaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani Dodoma mapema jana. Kushoto ni kaimu katibu Tawala wa mkoa Dodoma Bw. Felix Mwedipando na kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Ezekiel Mpuya.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye mkutano wa uhamasishaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani Dodoma mapema Jana, kutoka Kushoto Mkuu wa wilaya kongwa Alfred Msovela, Mkuu wa wilaya kondoa Omary Kwaangw' Mkuu wa wilaya Bahi Betty Mkwassa na Mkuu wa wilaya Chamwino Fatma Ally.
Wataalam na wadau wa huduma za afya kutoka wilaya za mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Dodoma. Mkutano huo ulifanyika mapema Jana.
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa mkoa na wilaya za Dodoma na wadau wa kutoa huduma za afya mkoani Dodoma muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa uhamasishaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Dodoma.

ngoma azipendazo ankal

MNEC Magesa katika ziara ya kuimarisha Chama na kusimamia utekelezaji wa ilani Temeke

$
0
0
Mjumbe wa NEC Phares Magesa akiongea na viongozi wa Chama na Serikali kata ya Mbagala Kuu, jimbo la Kigamboni, Ndg. Magesa yuko katika ziara ya kuimarisha Chama na kusimamia utekelezaji wa Ilani , pamoja na mambo mengine MNEC alisisitiza umuhimu wa kushirikiana viongozi wote, kutokuwa na makundi, kutekeleza kwa haraka miradi yote ya maendeleo iliyoahidiwa kwa wananchi, kuwa na umoja ili kupata mafanikio ya haraka. UMOJA NI ISHINDI !

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA( TCAA) WATOA MSAADA WA VYAKULA MBALIMBALI KWA WATOTO YATIMA WANAOLELEA KATIKA KITUO CHA NEW LIFE ORPHANS HOME CHA KIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akiwakabidhi msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya ambao ni watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akiwakabidhi msaada wa mafuta ya kula Mohamed Achume ambaye ni miongoni mwa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwa kabidhi msaada wa vyakula mbalimbali yakiwemo mafuta ya kupikia , mchele na sukari.
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images