Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Prof.Kabudi aipongeza Tigo kwa huduma nzuri SADC

$
0
0


Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akisajili laini yeke kwa kutumia alama za vidole katika banda la kampuni ya simu ya Tigo ambapo Tigo alikuwa mdhamini mkuu wa intaneti ya bure katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, akisajili laini yeke kwa kutumia alama za vidole katika banda la kampuni ya simu ya Tigo ambapo Tigo alikuwa mdhamini mkuu wa intaneti ya bure katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam.

WIZARA YATOA NAFASI ZAIDI ZOEZI LA UHISHAJI NGO

$
0
0
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa mwelekeo wa zoezi la uhuishaji Mashirika amabayo awali yalijisajili chini ya Sheria nyingine.

Na Mwandishi Wetu Dodoma.

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imetoa muda zaidi wa zoezi la usajili na uhuhishaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalijisajili kwa Sheria ya Makampuni, Bodi ya Wadhamini na sheria ya Jumuiya za Kiraia chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambazo kwa sababu tofouti hazijakamilisha zoezi la uhuishaji kwa mujibu wa Sheria no. 3 ya mwaka 2019.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dodoma Msajili wa NGOs Nchini Bi. Vickness Mayao amesema kimsingi kazi hii inahusu yale mashirika ambayo hayajakamilisha zoezi la kuhuisha vyeti vyao kwa mujibu wa Sheria na Wizara imeona ni vyema kuendelea na zoezi hilo baada ya kuwa imefanya hivyo katika  Kanda tano hapa nchini.

“Tunaendelea na zoezi la usajili huu ambao kisheria unakamilika tarehe 30 Augusti 2019  kama Sheria no.3 ya mwaka 2019 inavyoelekeza ili kutoa nafasi zaidi kwa Mashirika yaliyosalia ambayo kwa namna moja au nyingine bado hayajakamilisha usajili wake na ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Shirika litabaki katika Sheria yake”. Aliongeza Bi. Mayao.

Aidha Bi. Mayao amesema kuwa Ofisi ya Msajili wa NGOs tayari imetoa orodha ya awali ya Mashirika ambayo yameondolewa kwenye Daftari la Msajili wa Mashirika Yasiyo kuwa ya Kiserikali ambayo pia yanatakiwa kuhamia katika Sheria nyingine akiongeza kuwa orodha hiyo tayari imewekwa kwenye tovuti ya Msajili wa NGOs.

Bi. Mayao ametaja idadi ya Mashirika hayo kuwa ni 158 na inatarajia kuongezeka kadili zoezi la kuyatambua Mashirika hayo linavyoendelea na kusisitiza kuwa orodha iliyopo ni ya wali na kuyataka Mashirika hayo kufanya haraka kuhuisha usajili wao kama Sheria mpya inavyosema kwani kushindwa kufanya hivyo maana yake shirika husika litakuwa limefutwa.

Msajili wa NGOs ameongeza kuwa zoezi la uhuishaji limefanikiwa kwa asilimia 85 baada ya kuwa limefanyika katika kanda tano ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati , Kanda ya Kaskazini, Pwani  na Nyanda za Juu Kusini na sasa zoezi hili linaendelea mjini Dodoma kwa ajili ya Mashirika ambayo bado yamesalia na zoezi hili linaendelea kwa kushirikiana na wale wanaosimamia Sheria nyingine.

Zoezi la uhuishaji Mashirika linafanyika kwa miezi miwili kwa mujibu wa Sheria no.3 ya mwaka 2019 na tayari limekamilika katika Kanda tano lakini linaendelea kukamilika Jjini Dodoma ili kutoa fursa ya ziada kwa Mashirika ambayo bado hajakamilisha zoezi la uhuishaji usajili kwake kabla ya kuondolewa usajili kama takwa la kisheria lilivyo katika Sheria hiyo.

kikundi cha Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) chamtembelea Mama Maria Nyerere jijini Dar

$
0
0
  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akiteta jambo na Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Aliyeketi kulia ni mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani, na wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.  
 Mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya Wanawake (MYWO), Rahabu Mwikali, akimkabidhi zawadi ya picha Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
 Mama Maria Nyerere (Katikati) akipeana mkono na mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani kama ishara ya kumshukuru kwa zawadi walizoleta kutoka Kenya, wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.
Mwanaharakati na Mpigania uhuru wa Kenya Muthoni Likimani (94) akiwa na Mama Maria Nyerere (kushoto) baada ya kumkabidhi zawadi ya kikoi wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kihistoria yaliyofanywa na  kikundi cha  Kenya Maendeleo ya Wanawake Organization (MYWO) ambacho kilianzishwa mwaka 1952 kwa ajili ya kuhamasisha umoja na maendeleo ya wanawake, nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Aliyeketi kulia ni mwanasiasa mkongwe kutoka kenya, Muthoni Likimani, na wa kwanza kushoto ni mwanasiasa mkongwe wa Tanzania na Rais wa kwanza wa Pan-African Parliament (2004-2009),Gertrude Mongella.  

TRA Tabora Yatoa Elimu kwa Wafanyabiashara

$
0
0

Na Editha Edward -Tabora

Mamlaka ya Mapato TRA mkoani Tabora imelewa jukumu na Serikali la kuhakikisha inakusanya mapato kiasi cha Shilingi Bilioni 29.3, wakati ambapo Sheria mpya ya ukusanyaji wa mapato imeanza kufanya kazi 

Meneja wa TRA mkoa wa Tabora Thomas Masese amesema kulingana na Sheria hiyo itaweza kusaidia ongezeko la kodi ndani ya mkoa huo ukilinganisha na mwaka uliopita na kutoa elimu kwa Wafanyabiashara katika wilaya ya Urambo, Kaliua na Tabora manispaa 

" Mwaka uliopita tulikusanya kodi kwa asilimia tisini kulingana na sheria hii itaweza kusaidia ukusanyaji wa mapato katika mkoa wetu zaidi ya asilimia tisini " Amesema masese

Wakizungumza na wafanaya biashara hao baadhi ya wakuu wa Wilaya mkoani humo, akiwemo mkuu wa wilaya ya manispaa ya Tabora Komanya Erick wamewasisitiza Wafanyabiashara umuhimu kwa kulipa kodi pamoja na utunzaji wa kumbukumbu 

"Kodi ndiyo roho ya nchi yeyote duniani kodi ndiyo kitu pekee ambayo inawez kukamilisha miradi mbalimbali ya ndani ya nchi kwa hiyo tunachotakiwa tulipe kodi kwa maendeleo ya Taif letu"Amesema Komanya

Kwa upande wao wafanyabiashara wa mkoani Tabora Patrick Chokara na Amina Ally .Wamesema licha ya sheria hiyo kuwa na manufaa kwa Wafanyabiashara lakini bado wana wasiwasi kulingana na wafanyabiashara wengi kutokuwa na Elimu ya Biashara

Aidha Serikali katika mwaka wa fedha 2019 /2020 ilifanya marekebisho ya mfumo wa kodi ikiwemo kurekebisha baadhi ya viwango vya kodi tozo na ada zinazotolewa chini ya sheria mbalimbali pamoja na taratibu za ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.
 Meneja wa TRA mkoani Tabora  Thomas masese  akizungumza nawa Wafanyabiasha mkoani Tabora.
Pichani ni Wafanyabiasha mbalimbali mkoani Tabora wakimsikiliza meneja wa TRA (pichani Hayupo).

Dkt. Mwakyembe Apongeza Vyombo Vya Habari kwa Kutangaza Vyema Mkutano wa 39 wa SADC.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki WHUSM- DODOMA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amevipongeza Vyombo vya Habari nchini kwa kazi kubwa ya kiuzalendo na weledi wa hali ya juu katika kutangaza Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwakyembe ametoa pongezi hizo jana Jijini hapo ambapo amesema kuwa uandishi wa habari wa kujenga na kukosoa ambao una lengo la kurekebisha unahitaji kupongezwa kwakua unasaidia jamii na Serikali katika kuleta maendeleo ya haraka kwa Taifa.

“Waandishi wa habari mbali na kuutangaza Mkutano wa 39 wa SADC lakini pia wametumia taaluma yao kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Uwekezaji katika viwanda, Utalii, Uchukuzi na nyinginezo,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa Uwenyekiti wa Tanzania ambao unaendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli umeleta ari na matumaini mapya ambayo yatasaidia nchi wanachama kuondoa vikwazo vingi vya kibiashara na mawasiliano ya karibu baina ya nchi wanachama  na kujenga ustawi wa uchumi kwa nchi hizo.

Aidha Mhe. Mwakyembe  amesema kuwa baada ya lugha adhimu ya Kiswahili kutangazwa rasmi kuwa miongoni mwa lugha nne zinazotumika ndani ya Jumuiya hiyo, amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kutangaza bidhaa za lugha hiyo ikwemo uandishi wa vitabu vya kiada, ufundishaji wa lugha hiyo, kuuza Sanaa zinazotokana na lugha hiyo kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.


Mkutano wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC kwa Wakuu wa nchi na Viongozi wa Serikali umefanyika kuanzia Agosti 17- 18,2019 ambapo mambo mbalimbali yanayohusu nchi hizo yalijadiliwa ikwemo namna bora ya kuimarisha biashara ndani ya nchi hizo  ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

FEMATA KUFANYA MKUTANO MKUU WA SITA JIJINI TANGA

$
0
0
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wadau wa madini, wapili kulia ni Rais wa FEMATA, John Bina
Ofisa habari na mawasiliano wa shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini FEMATA, Dk Bernard Joseph akizungumza na wadau wa madini ya dhahabu eneo la Bassotu Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.
Waziri wa Madini Dotto Biteko (katikati) akiwa na Rais wa FEMATA, John Bina (kushoto) na Kamishna wa Tume ya madini wa FEMATA, Haroun Kinega.

……………………..
SHIRIKISHO la vyama vya wachimbaji madini nchini (FEMATA) wakiongozwa na Rais wao John Bina wanatarajia kufanya mkutano mkuu wa sita jijini Tanga. 

Kwa mujibu wa afisa habari na mawasiliano wa FEMATA, Dkt Bernard Joseph mkutano huo mkuu wa sita unatarajia kufanyika Agosti 31 mwaka huu kwenye hotel ya kitalii ya Tanga Beach Resort jijini Tanga. 

Dkt Joseph alisema mgeni rasmi siku ya ufunguzi wa mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Dotto Mashaka Biteko. 

Alisema mambo mbalimbali yenye manufaa ya wadau wa madini yatajadiliwa na kupitishwa kwenye mkutano huo ambapo washiriki wanapaswa kuwasiliana na wenyeviti wa vyama vya wachimbaji madini wa mikoa au Mtendaji Mkuu wa FEMATA. 

Alisema FEMATA ni shirikisho la vyama vya wachimbaji madini nchini linalowaunganisha wachimbaji madini, wafanyabiashara na wadau wa madini na Serikali. 

“FEMATA huendesha mafunzo ya elimu na ujuzi wa madini, biashara ya madini, changamoto na athari za mazingira kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Madini,” alisema Dkt Joseph.

Alisema FEMATA imeundwa na vyama vya mikoa vya madini na Wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya wafanyabiashara na wadau wa Madini.

Alisema FEMATA ni uwakilishi katika vyama vya mikoa vya madini (REMAs) kwenye masuala mbalimbali ya madini.

Alisema FEMATA ni chombo cha utetezi wa wachimbaji madini katika kuongeza ufanisi na masilahi ya wachimbaji na haki zao.

Alisema FEMATA ni 
shirikisho linalowakilisha vyama vya kimkoa vya wachimba madini (REMAs) katika kuwaunganisha wachimbaji madini na wadau wa uchimbaji madini na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa kimaendeleo.

Alisema dira na malengo ya FEMATA ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wachimbaji madini, wadau na serikali ili kuleta ufanisi katika sekta ya madini na ukuzaji wa pato la taifa.

“Sisi FEMATA dira yetu ni kuhakikisha nchi na wachimbaji madini wananufaika na madini yaliyopo,” alisema Dkt Joseph.

Dkt Joseph alisema wanachama wao ni wachimbaji au wamiliki wa migodi kutoka katika mikoa yote nchini, wafanyabiashara na wadau mbalimbali na wanaotaka kujiunga wanapaswa kuwasiliana kupitia info@femata.co.tz

Alisema faida za kujiunga na FEMATA,  zipo nyingi ikiwemo kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu madini, biashara ya madini, utatuzi wa changamoto mbalimbali, uwakilishi na utetezi kwa wanachama katika maeneo ya madini. 

Alisema FEMATA ni kiungo muhimu katika kuwaunganisha wachimbaji madini na serikali ili kuhakikisha shughuli zao zinakwenda vizuri kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

“FEMATA Ni Shirikisho linalowakilisha vyama vya kimkoa vya wachimba madini katika kuwaunganisha na serikali,” alisema Dkt Joseph.

VIKUNDI 12 KEREGE VYANUFAIKA NA MKOPO WA MIL.67-NGATIPURA

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, KEREGE

VIKUNDI vya Ujasiriamali vya vijana, wanawake ndani ya Kata ya Kerege wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, vimepata mkopo wa sh.milioni 67 kutoka halmashauri ya Bagamoyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Diwani wa kata hiyo Said Ngatipura alisema ,mikopo hiyo imetokana na asilimia kumi ya halmashauri hiyo ambayo ni utekelezaji wa agizo la serikali kwa halmashauri zote nchini kupitia makusanyo yake ya ndani ya kuvikopesha vikundi mikopo isiyokuwa na riba.

"Vikundi hivyo vipatavyo 12 vimepatiwa fedha hizo kulingana na maombi na kiasi cha fedha, huku akieleza kwamba vikundi hivyo vinaendelea na marejesho.

"Kati ya vikundi hivyo vya wanawake vilivyopatiwa mikopo ni 6 kikiwemo cha Tumaini Kilemela ambacho kimerejesha vizuri na kukopa tena, katika mikopo hiyo vikundi vya wanawake vimekopeshwa shilingi milioni 39.5 wakati vijana wakipata mkopo wa sh. milioni 28 " alisema Ngatipura.

Alifafanua, Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Mwambao Shumina Sharifu, ametafuta wafadhili waliowezesha kuchimba visima viwili vya maji safi, kimoja kipo shule ya msingi Kerege na kingine shule ya Mapinga.

Akizungumzia sekta ya elimu, Ngatipula alisema kuwa Kata ina shule moja ya sekondari yenye kidato cha kwanza mpaka cha nne na wanafunzi 1,105, kati yao wavulana 540, wasichana 565 ikiwa na walimu 75.

Nae Mbunge wa jimbo hilo ,alhaj Shukuru Kawambwa,alibainisha mfuko wa jimbo umeunga mkono juhudi za wananchi katika umaliziaji wa vyumba vya madarasa sekondari ya Kerege, jengo la utawala, vyoo shule ya msingi Mapinga, ununuzi wa bati ofisi ya Kitongoji cha Amani na mifuko 100 ujenzi wa vyumba vya madarasa.

WATUMISHI TRA WAJENGEWA UWEZO UKUSANYAJI KODI SEKTA YA UJENZI

$
0
0
Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Lewis Ishemoi (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati wa kufungua mafunzo ya utozaji kodi katika sekta ya ujenzi kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo yanafanyika katika Chuo cha Kodi. Waliokaa kutoka kulia:- Mkuu wa Kozi Fupi ITA, Dkt. Amos Ibrahim, Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Mipango, Fedha na Utawala Emmanuel Masalu, Mwakilishi kutoka JICA Ayako Hatori na Mkufunzi Prof. Ninatubu Lema
Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Lewis Ishemoi (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wakufunzi wa mafunzo ya utozaji kodi sekta ya ujenzi mara baada ya kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Kodi.
Washiriki wa mafunzo ya utozaji kodi katika sekta ya ujenzi wakifuatilia mada kutoka kwa mkufunzi Prof. Ninatubu Lema
Washiriki wa mafunzo ya utozaji kodi katika sekta ya ujenzi wakifuatilia kwa makini mafunzo ambayo yanafanyika katika Chuo cha Kodi

………………………

Katika jitihada za kuhakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakuwa na wataalamu waliobobea katika ukusanyaji wa kodi katika sekta ya ujenzi, Chuo cha Kodi (ITA) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Misaada la Japan (JICA) wameendesha mafunzo ya utozaji kodi katika sekta ya ujenzi kwa watumishi wa TRA.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Kodi, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma Dr. Lewis Ishemoi amesema kwamba mafunzo hayo yataisadia TRA kuongeza makusanyo ya kodi hususan kutoka katika sekta ya ujenzi.

“Mafunzo haya yatawajengea uwezo washiriki ambao ni watumishi wa TRA katika ukusanyaji wa kodi kutoka katika sekta ya ujenzi na kupata uzoefu wa sekta hiyo kutoka kwa wawezeshaji kutoka Japan”, amesema Dr. Ishemoi ambaye ameishukuru serikali ya Japan kupitia shirika lake la kimataifa la Misaada –JICA kwa kufadhili mafunzo hayo pamoja miradi mingine mbalimbali katika kuwajengea uwezo watumishi wa TRA.

Awali akielezea muhtasari wa mafunzo hayo, Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Mipango, Fedha na Utawala Emmanuel Masalu, amesema kwamba lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wakufunzi kuuelewa mfumo mzima wa ujenzi pamoja na shughuli muhimu katika sekta hiyo, kufahamu mnyororo wa thamani pamoja na kufahamu wadau wakuu katika shughuli za ujenzi.

“Lengo ni kuielewa vema sekta ya ujenzi ili kutambua vitovu vya kodi katika sekta hiyo kwani ujenzi ni miongoni mwa sekta maalum nchini ambazo zinakua kwa kasi”, amesema Masalu na kuongeza kwamba wakufunzi pia watapata uelewa wa kodi za kimataifa na hivyo kuwa na weledi wa kukusanya kodi za kimataifa kutokana na kuwepo na miradi mingi nchini ambayo inaendeshwa na makampuni ya kimataifa kama vile makampuni ya ujenzi kutoka China na Uturuki.

Pamoja na mafunzo hayo washiriki pia watapata uzoefu wa ukusanyaji kodi katika sekta ya ujenzi kutoka kwa wakufunzi wa Japan nchi ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta ya ujenzi.

Mafunzo hayo ya siku tano yanafanyika katika Chuo cha Kodi na kuwashirikisha watumishi wa TRA kutoka katika Mikoa mbalimbali ya kodi. Mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa TRA katika ukusanyaji wa kodi kutoka katika sekta maalum za ujenzi, mawasiliano, madini, mafuta na gesi ambazo zinakua kwa kasi na hivyo kuhitaji wataalamu wa kodi wenye weledi ili kuweza kukusanya kodi stahiki kutoka katika sekta hizo.

WAZIRI UMMY MWALIMU KUZINDUA CHAMA CHA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA (TCA) AGOSTI 26,2019

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) Agosti 26 mwaka 2019.

Akizungumza leo Agosti 19,2019 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Shekha Nasser amesema sekta ya urembo na vipodozi inakua kwa kasi na kutoa ajira nyingi kwa watanzania walio wengi.

"Tukio hilo la kihistoria la kuzindua chombo hiki muhimu ndani ya nchi yetu litafanyika Agosti 26, 2019 katika jengo la PSSSF –KISENGA, Kijitonyama . Mgeni rasmi ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu,"amesema.

Amefafanua wamekuwa wakishuhudia ongezeko la warembaji, wenye salons, watengeneza kucha, watengenezaji na wanaoingiza bidhaa za urembo na vipodozi,hivyo ni wakati muafaka kuwa na chama chao ambacho kitaaunganisha wadau wote.

Amesisitiza TCA ni chama kinachoanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuhudumia na kuunganisha wadau wote katika sekta ya urembo na vipodozi nchini."Chama hiki kitahusisha wadau wote kuanzia waelimishaji, wajasiriamali wakubwa na wadogo, wazalishaji wa viwanda vidogo na vikubwa.

"Pia watengenezaji wa bidhaa asilia, watoa huduma, wasambazaji na watabibu wa ngozi katika sekta nzima hii ya urembo na vipodozi,"amesema.
Amesema kupitia ndani ya ya TCA kutakua na mafanikio ya kukuza sekta ya urembo na vipodozi baada ya kuona changamoto nyingi wanazozipitia washikadau.

Ametoa mfano pamoja na Wizara ya Elimu kupitia NACTE kupitisha mtaala wa kwanza wa elimu ya Stashahada hivi karibuni, lakini vyuo vya kutoa NTA Level 4, 5 na 6 bado havipo. 

Ameongeza pamoja na VETA kuwa na mtaaala wa kozi ya cheti cha Cosmetology lakini changamoto kubwa ni walimu wenye sifa ya Diploma wa kufundisha wanafunzi ili wafanye mtihani wa Taifa na kupata walimu wenye Weledi na sifa nchini. 

Amesema kuwa ukosefu huo wa walimu wa Cosmetology nchini unasababishwa na mambo mengi yakiwemo ya sekta hiyo kutotambulika rasmi na kujengewa heshima yake inayostahili kama ilivyo katika nchi za jirani Kenya, Uganda na South Afrika.

"Watanzania wengi huenda kwenye nchi hizo kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu ya Cosmetology ngazi ya Stashahada,"amesema Nasser na kuongeza kutokana na muamko huo wameona ni wakati muafaka wa kuanzisha chombo kitakachowaunganisha wadau wote wa sekta hiyo.

Mwenyekiti huyo wa TCA ametumia fyrsa hiyo kuwakaribisha wadau wote wa sekta ya urembo nchini Tanzania kufika ili kushuhudia tukio hilo la kipekee kwa mara ya kwanza Tanzania lenye kauli mbiu " Urembo na vipodozi katika uchumi wa Viwanda". 

 Mwenyekiti wa Chama cha Urembo na Vipodozi Tanzania (TCA) ,Shekha Nasser  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu  uzinduzi  wa chama hicho, Agosti 26,mwaka 2019, ambapo Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Kulia ni Katibu wa TCA Braison Makena na kushoto ni Meneja Utawala TCA,Judy Charles  
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.

YANGA YATANGAZA MABADILIKO YA BEI YA JEZI ZAKE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wetu Dk Mshindo Msolla amesema awamu ya tatu ya shehena ya jezi za Yanga inatarajiwa kuwasili wakati wowote ambapo kutakuwa na mabadiliko ya bei ya jezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Yanga Kaloleni jijini Arusha jana, Dk Msolla amesema kutakuwa na punguzo la bei ili kuwawezesha mashabiki na wanachama kununua kufuatana na uwezo wao.

Amesema,” Zile jezi tulizozindua kwenye awamu ya kwanza zilikuwa toleo daraja la juu ambazo zilikuwa za wachezaji ziliuzwa kwa Tsh 35,000/- na baadae likaletwa toleo la mashabiki ambazo ziliuzwa Tsh 30,000/-".

Ameeleza kuwa wamefanya mazungumzo na GSM na kukubaliana kuwa jezi za awamu ijayo, lile toleo la juu zitauzwa kwa Tsh 30,000/- na zile za mashabiki zitauzwa Tsh 20,000/-.

Msolla amesema Lengo kuu ni kuwawezesha mashabiki na wanachama wa Yanga kununua jezi original kulingana na uwezo wa kila mmoja na kuiongezea timu mapato.

Aidha Dk Msolla amesema ujio wa jezi hizo utamaliza changamoto ya kukosekana kwa jezi mpya za Yanga madukani,Kampuni ya GSM imeahidi kuwezesha upatikanaji wa jezi za Yanga nchi nzima na bei elekezi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla akizungumza na wanachama wa Yanga mara baada ya kuzindua tawi la Kaloleni Arusha na kuelezea mabadiliko ya bei ya jezi hizo kwa awamu ya tatu pindi itakapoingia

Dkt. Maleko: Andaeni Maandiko ya Miradi yenye fursa pana za kiuchumi

$
0
0
 Na Mwandishi wetu, Mtwara

Wataalam wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuandika maandiko bora yenye kuzingatia mkondo mzima wa ongezeko la thamani (value chains) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi nchini.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Dkt. Jilly Maleko wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo watalaam hao wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi.

Akizungumza na watalaam hao mkoani Mtwara, Dkt. Maleko alisema kuwa wataalam hao hawana budi kujiridhisha na ubunifu wa miradi yao kuwa inaweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

“Tunapobuni miradi ya kiuchumi ni muhimu kuzingatia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo husika kwa kuzingatia mkondo mzima wa ongezeko la thamani (value chains) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi,” alisema.

Dkt. Maleko aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujenga uchumi wa viwanda katika kufikia azma ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo uandishi bora wa maandiko ya miradi unaongeza tija kufika malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella alisema kuwa warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo wataalam hao ili kukabiliana na changamoto za uandishi wa maandiko bora yanayokopesheka.

Aliongeza kuwa warsha hiyo inayoendeshwa kwa ushirikiano kati Benki ya Maendeleo TIB na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imelenga kuongeza tija ya uwekezaji unaofanywa na Serikali za Mitaa nchini.

“Warsha hii inalenga kuwajenga watumishi katika nyanja mbalimbali kama kuandaa miradi ya kibiashara katika manispaa na wilaya kama vile vituo vya mabasi na maeneo ya viwanda, ili kuhakikisha maandiko hayo yanakopesheka,” alisema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, Bw. Rashid Kitambulio alisema takribani watumishi 150 wanatarajia kujengewa uwezo wa mambo mbalimbali kuhusiana na kuandaa miradi ya kimaendeleo ambayo italeta faida kwa wananchi, mbali na hilo pia watafundishwa jinsi ya kuomba mikopo ya miradi ya kimaendeleo.

Aliongeza kuwa watumishi hawa wanatoka katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

Warsha hii ni matunda ya makubaliano kati ya Benki ya Maendeleo TIB na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ikiwa ni moja ya makubaliano waliyoyafikia mnamo mwezi Septemba 2017 ambapo walikubaliana kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika uandishi bora wa maandiko ya miradi.

Hii ni warsha ya tano tangu warsha hizi kuanza rasmi mwaka 2018, tayari warsha kama hii imefanyika katika Kanda ya Kaskazini (Arusha), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Ziwa (Mwanza) na Kanda ya Kati (Dodoma) ambapo takriban watumishi 450 wamefaidika na mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Dkt. Jilly Maleko (aliyesimama) akifungua warsha ya kuwajengea uwezo watalaam wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, Bw. Rashid Kitambulio (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella akihimiza jambo wakati akifanya wasilisho kuhusu Programu maalum na Huduma za Fedha za Benki ya Maendeleo TIB.


Washiriki wa warsha ya kuwajengea uwezo watalaam wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi wakifuatilia mawasilisho wakati wa warsha hiyo.

Dkt. Maleko: Andaeni Maandiko ya Miradi yenye fursa pana za kiuchumi

$
0
0
 Na Mwandishi wetu, Mtwara

Wataalam wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuandika maandiko bora yenye kuzingatia mkondo mzima wa ongezeko la thamani (value chains) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi nchini.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Dkt. Jilly Maleko wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo watalaam hao wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi.

Akizungumza na watalaam hao mkoani Mtwara, Dkt. Maleko alisema kuwa wataalam hao hawana budi kujiridhisha na ubunifu wa miradi yao kuwa inaweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

“Tunapobuni miradi ya kiuchumi ni muhimu kuzingatia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo husika kwa kuzingatia mkondo mzima wa ongezeko la thamani (value chains) ili kuwezesha ukuaji wa uchumi jumuishi,” alisema.

Dkt. Maleko aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujenga uchumi wa viwanda katika kufikia azma ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo uandishi bora wa maandiko ya miradi unaongeza tija kufika malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella alisema kuwa warsha hiyo inalenga kuwajengea uwezo wataalam hao ili kukabiliana na changamoto za uandishi wa maandiko bora yanayokopesheka.

Aliongeza kuwa warsha hiyo inayoendeshwa kwa ushirikiano kati Benki ya Maendeleo TIB na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imelenga kuongeza tija ya uwekezaji unaofanywa na Serikali za Mitaa nchini.

“Warsha hii inalenga kuwajenga watumishi katika nyanja mbalimbali kama kuandaa miradi ya kibiashara katika manispaa na wilaya kama vile vituo vya mabasi na maeneo ya viwanda, ili kuhakikisha maandiko hayo yanakopesheka,” alisema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, Bw. Rashid Kitambulio alisema takribani watumishi 150 wanatarajia kujengewa uwezo wa mambo mbalimbali kuhusiana na kuandaa miradi ya kimaendeleo ambayo italeta faida kwa wananchi, mbali na hilo pia watafundishwa jinsi ya kuomba mikopo ya miradi ya kimaendeleo.

Aliongeza kuwa watumishi hawa wanatoka katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam.

Warsha hii ni matunda ya makubaliano kati ya Benki ya Maendeleo TIB na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ikiwa ni moja ya makubaliano waliyoyafikia mnamo mwezi Septemba 2017 ambapo walikubaliana kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika uandishi bora wa maandiko ya miradi.

Hii ni warsha ya tano tangu warsha hizi kuanza rasmi mwaka 2018, tayari warsha kama hii imefanyika katika Kanda ya Kaskazini (Arusha), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Ziwa (Mwanza) na Kanda ya Kati (Dodoma) ambapo takriban watumishi 450 wamefaidika na mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Dkt. Jilly Maleko (aliyesimama) akifungua warsha ya kuwajengea uwezo watalaam wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa, Bw. Rashid Kitambulio (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella akihimiza jambo wakati akifanya wasilisho kuhusu Programu maalum na Huduma za Fedha za Benki ya Maendeleo TIB.


Washiriki wa warsha ya kuwajengea uwezo watalaam wa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uandishi bora wa maandiko ya miradi wakifuatilia mawasilisho wakati wa warsha hiyo.

MAOFISA TARAFA PWANI WAAGIZWA KUDHIBITI KESI ZA MIMBA ZA UTOTONI ZINAZOMALIZWA KIMYA KIMYA PAMOJA NA KUKAMATA WALE WAPIGA MIMBA-NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

SERIKALI Mkoani Pwani, imewaagiza Maofisa Tarafa mkoani humo, kudhibiti kesi za mimba za utotoni zinazomalizwa kimya kimya pamoja na kusimama kidete kuhakikisha wale wanaohusika kupiga mimba wanafunzi wa kike wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria bila kufanya ajizi.

Aidha amewataka maofisa tarafa hao kutatua na kutafutia ufumbuzi migogoro ya wakulima na wafugaji na ardhi ,kabla wananchi hawajapeleka malalamiko ngazi ya juu .

Akitoa maagizo hayo, wakati akikabidhi pikipiki 28 kwa maofisa tarafa na mkoa, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alieleza ofisa Tarafa ni kiongozi muhimu ndani ya serikali lakini cha kushangaza wapo baadhi yao wanashindwa kusimamia na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wanaowapa mimba wanafunzi.

"Tokeni maofisini nendeni mkasimamie majukumu yaliyo kwenye maeneo yenu, kasimamieni tatizo ambalo bado ni kubwa la mimba na utoro mashuleni ,kama haitoshi wapiga mimba ,mnawajua,kamata piga ndani,msiruhusu kesi hizo kuisha kimya kimya"alisisitiza Ndikilo.

Hata hivyo Ndikilo ,alisema haiwezekani kuhamasisha masuala ya uwekezaji na kuinua sekta ya viwanda wakati migogoro ya ardhi, imesheheni katika maeneo yao.

"Msikae maofisini, katafuteni ufumbuzi wa migogoro ya ardhi shambani, wakulima na wafugaji kakaeni nao pande zote mbili zenye migogoro ,kamalizeni migogoro ya kijiji kwa kijiji":File la malalamiko kwa mwezi unakuta migogoro ya ardhi ndio imejaa,sasa maofisa tarafa mpo huko kwanini watu wanafuata suluhu ngazi za juu kabla nyie hamjakaa nao"alisema.

Pia aliwaasa, kufuatilia miradi mikubwa ya maendeleo, kuimarisha ulinzi na usalama na kuhamasisha watu kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa ,katibu tawala wa mkoa ,Theresia Mbando alisema pikipiki hizo zinakwenda kuleta maendeleo chanya kwakuwa awali kulikuwa na changamoto kwenye baadhi ya maeneo ambapo wengine kutumia pikipiki chakavu za tangu miaka 17 iliyopita.

Nae ofisa tarafa wa Msoga, Mgeni Juma alisema kwa sasa tatizo la usafiri katika majukumu yake ya kikazi linakuwa historia kwani wamepata usafiri wa uhakika.

MZUMBE WASADIA VIFAA TIBA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO MOROGORO VYENYE THAMANI YA ZIADI YA TSHS. MIL 6

$
0
0
Mfamasia kutoka Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Frank Milanzi akikagua na kupanga baadhi ya vifaa tiba vilivyonunuliwa kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto kabla ya kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akizungumza wakati wa kukabidhi misaada ya vifaa tiba kwa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro eneo la Msamvu na kusababisha vifo vya watu 95. Katikati ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw. Noel Kazimoto na wa mwisho ni Bw. Twalib Muzakir Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Akitambulisha aina ya vifaa tiba vilivyonunuliwa kwa majeruhi wa ajali ya moto ni Dkt Bunini Manyilizu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Afya ya Chuo Kikuu Mzumbe, wakati ya hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Chuo hicho kutibu majeruhi wa ajali ya Moto. Wakishuhudia tukio hilo ni Bi. Prakseda (aliyeshika kipaza Sauti) kutoka TBC, akifuatiliwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka (katikati mwenye tai).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (kushoto mwenye suti) akipeana mkono na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kusirya Ukio baada ya kubabidhi vifaa tiba kwa majeruhi wa ajali ya moto. Katikati ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw. Noel Kazimoto.

*****************



Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro, leo kimekabidhi misaada ya vifaa tiba kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro Jumamosi ya tarehe 10 Agosti 2019 na kusababisha vifo vya watu 95.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo; Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka amesema, Jumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe wamechangia vifaa tiba vya thamani ya Tshs. 6,343,000/- vikijumuisha madawa, sindano, dripu, gozi za vidonda, madawa ya maumivu, maji, taulo za kike na madawa mengine baada ya kuonekana uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo kufuatilia hali ya majeruhi na matibabu wanayoendelea kupatiwa kwenye hospitali hiyo.

“ Vifaa tunavyokabidhi ni michango ya watumishi, wanafunzi na Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwakuwa na sisi tumeguswa na tukio hili, ni sehemu ya wananchi wa Morogoro hivyo hatuna budi kujitoa kwa hali na mali kuokoa Maisha ya wenzetu. Tunatamani kuona majeruhi wa ajali hii wanatibiwa na kurejea kwenye afya zao” alisema.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo; Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo amesema; Serikali ya Mkoa imefarijika sana kwa namna Chuo hicho kilivyojitoa tangu ajali hiyo ilipotokea kwa msaada wa haraka wa gari la Wagonjwa kuwakimbiza hospitali ya Rufaa Muhimbili na walivyojitoa kuchangia damu kabla ya msaada wa vifaa walivyokabidhi leo.

“ Tunawashukuru sana Uongozi na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa michango yenu kwa hakika haitawasaidia majeruhi wa ajali hii tu lakini na wagonjwa wengine wenye uhitaji na hasa kwa kuzingatia Mkoa wetu uko katikati na hivyo kuwekuwa na wajeruhi wengi wa ajali ambao wanahitaji msaada wa haraka wanapofikwa na majanga kama haya” alisisitiza.

Amewataka kuendelea kujitoa kwa wananchi wa Morogoro kila inapobidi kufanya hivyo kwakuwa uwepo wao ni muhimu sana katika ustawi na maendeleo ya Wananchi.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kusirya Ukio ameeleza hali ya majeruhi wa ajali ya moto ambapo hadi kufikia leo idadi yao ni 17 (kumi na saba) wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa na kati yao baadhi wameanza kufanya mazoezi.

Hata hivyo matibabu yao bado yatachukua muda mrefu kutokana na aina ya majeraha waliyoyapata, hivyo misaada bado inahitajika vikiwemo vifaa tiba.

DODOMA KUWA KAMA ULAYA BAADA YA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KUTOA MKOPO WA SH. BILIONI 414 KUJENGA BARABARA ZA MZUNGUKO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Uzinduzi Nyumba Day NMB wafanyika Mwanjelwa Jijini Mbeya

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (pili kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi siku ya nyumba,kwanza kulia Mkuu wa wilaya ya Mbeya Paul William Ntinika na kwanza kushoto Kaimu Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati Ally Ngingite,na pili kulia Meneja na bank ya Nmb kanda ya Manda za juu kusini Straton Chilongola wakati wa hafla uzinduzi siku ya nyumba NMB Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka huu .
Baadhi ya wananchi na wateja wa Benki ya NMB Mwanjelwa ,wakifatilia hatoba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila hayupo katika picha wakati hafla ya uzinduzi wa siku ha nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB Katika eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka huu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizugumza na wateja wa benki ya NMB katika uzinduzi wa siku ya nyumba iliyoandaliwa na Benki ya NMB eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya Agosti 16 mwaka.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila katikati walioketi akiwa na wafanyakazi wa Bank ya NMB wakati wa uzinduzi wa siku ya nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB,hafla ambayo imefanyika katika Viwanja vya benki hiyo Mwanjelwa Jijini Mbeya Agosti 16,2019.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila (wa pili kulia) akimsikiliza kwa Makini Kaimu Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati kutoka Bank ya NMB Ally Ngingite (wa pili kushoto),wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya nyumba katika viwanja ya Benki ya NMB Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika wa kwanza kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akipewa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya nyumba na Steven Mohamed (katikati) amabaye ni Msanifu majengo Kampuni ya Malk Consultants(T) Ltd wakati wa hafla ya uzinduzi siku ya Nyumba iliyoandaliwa na benki ya NMB hafla ambayo imefanyika katika eneo la benki hiyo Mwanjelwa Jijini Mbeya.
 

USHAHIDI WA VIDEO KESI YA AKINA MBOWE YAONESHWA MAHAKAMANI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 19, mwaka 2019 imeangalia ushahidi wa video uliowasilishwa na shahidi namba sita, Koplo Charles, katika kesi ya jinai namba 112/2019 inayowakabili viongozi wa tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Mawakili wa pande zote mbili na watu mbalimbali wamepata kushuhudia video hiyo iliyooneshwa katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo mahakamani hapo kwa kutumia Projector mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Hata hivyo katika video hiyo inayodaiwa ni ya mkutano uliofanywa na viongozi hao, hakuna mahali popote ambapo palipomuonesha Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko akihutubia katika mkutano huo. 

Pia video hiyo haijaonesha watu wakirusha mawe wala viongozi hao wa Chadema wakiwa katika maandamano bali imeonesha baadhi ya viongozi hao wakihutubia katika mkutano wa kumnadi aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu na mwisho wafuasi wa chama hicho wakiandamana.

Mapema kabla ya kuangalia ushahidi huo wa video Hakimu Simba alisoma uamuzi na kuruhusu video hiyo kuoneshwa na kutupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi waliokuwa wakiponga ushahidi huo kuoneshwa mahakamani hapo wakidai kuwa, upande wa mashtaka hawakuwasilisha vifaa vya kusaidia kuonekana kwa video hiyo

Awali, upande wa mashitaka kupitia kwa shahidi wake namba sita uliiomba mahakama hiyo ikubali kuonyeshwa ushahidi wa video kutoka katika kamera ya Koplo Charles kwa kutumia vifaa vya nje.

Akisoma uamuazi huo, Hakimu aliridhia video hiyo kuoneshwa kwa kutumia vifaa vya nje (external device).

Katika zoezi hilo, shahidi namba sita, Koplo Charles alisaidiwa na mtaalamu wa IT Nazari Moshi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuunganisha kamera yake na vifaa vya nje vya mahakama hiyo kwa ajili ya kuonesha video hiyo aliyoigawa mara mbili (Min div 1 &2).

Koplo Carles alionesha video ya kwanza aliyoipa jina la Mkutano wa Chadema wa mwaka 2018 iliyoonesha baadhi ya viongozi na wabunge wa chadema wakiongozwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa na Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, wakimnadi Salum Mwalimu aliyekuwa Mgombea wa Jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio wa mwaka huo.

Video hiyo ya kwanza yenye dakika 56 na sekunde 37 ilionesha wabunge kadhaa wa Chadema akiwemo, John heche (Tarime Mjini), Cecil Mwambe (Ndanda), Halima Mdee (Kawe) Ester Bulaya (Bunda Mjini) Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) wakitoa hotuba zao za kumnadi Mwalimu.

Video ya kwanza ilikwisha, ikawekwa ya pili yenye urefu wa dakika 25 na sekunde 55 ambayo nayo ilimuonyesha Mbowe akihutubia kisha kuhamasisha wananchi kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kinondoni.

kwa ajili ya kupata barua ya utambulisho za mawakala wao katika uchaguzi huo wa marudio.Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho

BAADA YA MKUTANO SADC SASA BAJAJI , BODABODA KAMA KAWA KATI KATI YA JIJI DAR ....WASEMA WALIENDA 'LIKIZO'

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAENDESHA bajaji na bodaboda katika Jiji la Dar es Salaam na hasa eneo la Mnazi Mmoja ya Posta Mpya wameanza kurejea kwa kasi kuendelea na shughuli zao kama kawaida yao.

Kurejea kwa huduma za usafiri huo ni siku moja tu baada ya kumalizika kwa kwa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) ambao ulifanyika Agosti 17 na Agosti 18 mwaka huu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kwa kukumbusha tu Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake Lazaro Mambosasa walipiga marufu usafiri huo kuingia kati kati ya Jiji hilo ili kupisha mkutano wa SADC.

Ambao ulianza kwa kutanguliwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za maonesho ya bidhaa ya viwanda kwa nchi za jumuiya hiyo.Hata hivyo baada ya Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam kupiga marufuku usafiri wale wote waliokaidi walikamatwa na bajaji na bodaboda zao kushikiliwa na jeshi hilo na kwa mujibu wa Mambosasa alisema waliokaidi katazo lao watapelekwa mahakamani.

Michuzi Blogu leo Agosti 19,2019 imeshuhudia usafiri huo wa bodaboda na bajaji ukiwa umeanza kurejea na hata kwenye maeneo ambayo bodaboda waliondolewa baadhi yao wamesharudi.

Hata hivyo baadhi yao wameonekana wakiwa na hofu na kuamua kuficha pikipiki zao na pale anapotokea mteja wanachukua walikoweka na kuendelea na safari.

Baadhi ya waendesha bodaboda wamesema pamoja na kuondolewa kwenye maeneo yao waliyokuwa wanafanya shughuli za utoaji huduma ya usafiri wanaipongeza Serikali kwa kufanikisha mkutano huo na kumalizika kwa uslama na amani.

Wengine wamesema kuondolewa kwao kwenye maeneo hayo ambayo wamekuwa wakiyatumia kusubiri wateja wao(wasafiri) imesababisha kuyumba kiuchumi lakini hiyo haiwapi shida kwani wamerudi na mambo yatakwenda sawa kwa madai nia ya Serikali ilikuwa njema.
"Kwangu kipindi chote cha SADC niliona kama vile nipo likizo ya muda mfupi maana nilikuwa naamini tutarejea na kweli leo tuko kwenye maeneo yetu.Bado tunahofu huenda tukafukuzwa lakini angalau baada ya siku kadhaa leo nimeingia mjini na bodaboda yangu,"amesema mwendesha bodaboda eneo la Posta Mpya Juma Kingimali.

Hata hivyo Jeshi la Polisi halijatoa taarifa ya kuruhusu bodaboda na bajaji kurejea kwenye maeneo waliyokuwa wameyazuia kwa muda kupisha mkutano wa SADC.

RC CHALAMILA AMTEMBELEA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB, JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akisaini kitabu cha wageni, wakati alipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ofisini kwake leo Agosti 19, 2019, jijini Dar es salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati alipomtembelea ofisini kwake leo Agosti 19, 2019, jijini Dar es salaam. 

CCM WILAYA YA ILALA YASHINDA NAFASI YA NAIBU MEYA...MASABURI ASHUKURU

$
0
0

NA Heri Shaban, ILALA

CHAMA Cha Mapinduzi( CCM ) Wilaya ya Ilala kimekibwaga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika nafasi ya Naibu Meya Ilala.

Katika uchaguzi huo CCM walimsimamisha Ojambi Masaburi aliyeibuka kidedea kwa kula 33 dhidi ya ya Elen Ryatula wa Chadema aliyepata kura 21.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabir Makame amesema kuliwa na wajumbe 57 na kati ya hao waliopiga kura ni 54.Hakuna kura iliyoharibika katika uchaguzi huo na uchaguzi huo umefanyika katika hali ya tulivu.

Akizungumza katika uchaguzi huo mara baada kuteuliwa Naibu Meya Mteule Manispaa ya Ilala Ojambi Masaburi amewapongeza wapiga kura kwa kumchagua kushika wadhifa huo.Pia amewapongeza viongozi wa CCM Wilaya kwa kumteua kwa kumpa tiketi ya CCM kugombea kiti hicho.

"Nashukuru kwa ushindi mnono uliotokana na madiwani wenzangu wa CCM kunichagua katika kiti hichi.Pia nawapongeza UKAWA kwani madiwani wake watano wamenipigia kura,"amesema Ojambi na kuongeza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi unaofanyika chini ya Mwenyekiti wao Rais John Magufuli umefanya hata upinzani nao kuunga mkono na ndicho ambacho wamekionesha kwa kumpa kura.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri ,awali alifungua kikao cha Baraza la madiwani Ilala alisema kikao hicho ni cha kawaida ,uchaguzi wa Naibu Meya kila baada ya mwaka mmoja .

Shauri amesema wapiga kura wajumbe wa kuteuliwa au kupiga kuratatibu Meya Mwenyekiti,Mkurugenzi Katibu utaratibu wa ushindi wa kiti mgombea anatakiwa kupat kura zaidi zilizopigwa na wajumbe.

Kwa upande wake Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto amechagua kamati zake za kufanya nao kazi ambazo ni Kamati za Mipango Miji na Mazingira na Kamati na Kamati za Huduma za Jamii.
 Naibu Meya wa Halmashauri ya Ojambi Masaburi akizungumza katika Baraza la madiwani Arnatogluo leo (Picha na Heri Shaaban)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya,Ilala Jumanne Shauri akisoma taarifa katika uchaguzi wa Naibu meya wa Ilala leo (Picha na Heri Shaaban)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images