Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

WIZARA YA KILIMO YAANDAA MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WOTE WA MAZAO YA NAFAKA NDANI NA NJE YA NCHI.

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe anautangazia Umma kuwa, Wizara imeandaa Mkutano wa Wafanyabiashara wote wa mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi. Walengwa wa mkutano huo ni: – Wasindikaji, Wamiliki wa maghala ya kuhifadhi nafaka na Wasafirishaji wa nafaka.
Mkutano huo utafanyika kwa muda wa siku mbili, kuanzia tarehe 29 hadi 30 Agosti, 2019 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Jijini Dar es salaam kuanzia saa 2:00 Asubuhi. 
Ajenda kuu ya mkutano ni kujadili fursa zilizopo kwenye tasnia ya nafaka na jinsi ya kuzitumia ikiwa ni pamoja na masoko.
Mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa, Mheshimiwa, Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo.
Ili kushiriki Mkutano huo, wasiliana na Wizara ya Kilimo kupitia namba za simu 0744468044/0652424014/0735500220, kupitia baruapepe: ps@kilimo.go.tz au kwa kumwandikia Katibu Mkuu – Wizara ya Kilimo, S.L.P 2182 Dodoma. Thibitisha ushiriki wako kabla ya tarehe 21.08.2019. 
Kila mshiriki anaombwa kujigharamia.



OFISI YA TAKWIMU ZANZIBAR YATOA TAKWIMU ZA AJALI NA MAKOSA YA BARABARANI

0
0
Polisi Trafiki kutoka makao Makuu ya Zanzibar CPL. Said Ali Said akitoa maelezo kuhusu ajali zinazotokea barabarani katika mkuta wa kutoa elimu kwa wandishi wa habari.Baadhi ya wandishi wa habari na wakifuatilia tarifa ya takwimu za ajali na makosa ya barabarani zilizotolewa na Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Asha Mussa.
Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Salim Abdulla Salim akichangia kitu katika Mkutano huo wa takwimu za ajali na makosa ya barabarani.Picha na Makame Mshenga.


Na Mwashungi Tahir,Maelezo

Elimu inahitajika zaidi kutolewa kwa jamii ili kupunguza ajali za barabarani na kutambua makosa ya barabarani ambayo hujitokeza mara kwa mara na kusababisha athari .

Hayo ameyasema Koplo Ali Abdullah Juma Polisi Trafic kutoka Makao Makuu huko katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makosa ya barabarani .

Amesema lengo la kutolewa elimu hiyo kwa jamii ni kuona ajali zinapungua kila tukienda mbele na hatimae kumalizika kabisa ili kuweza kunusuru ajali zinazoweza kuepukika .Hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwa na mashirikiano katika kuelimisha jamii ikiwemo madereva, abiria , wanaoendesha baskeli,na wanaotembea kwa miguu.

Akiwasilisha mada ya toleo la Takwimu za Ajali na makosa ya barabarani kwa Zanzibar Julai,2019 Asha Mussa Mahfoudh Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali amesema takwimu za ajali barabarani hutoa taarifa za ajali zinazotokea.

Amesema lengo la kutolewa toleo hilo ni kutoa taarifa za ajali na makosa barabarani za ndani ya Zanzibar ambazo ni muhimu na hutumiwa na wapangaji , watunga sera , na watoa maamuzi.

Pia amesema Jumla ya makosa ya barabarani 1,749 yameripotiwa mwezi Julai, 2019 , ambapo makosa hayo yote yanaongozwa na wanaume hivyo kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.

Aidha amesema Wilaya ya Mjini ina idadi kubwa ya makosa ya barabarani ambapo makosa 401 sawa na asilimia 22.9 kati ya makosa yote yaliyoripotiwa na Wilaya ya Micheweni ina idadi ndogo ya makosa ya barabarani yaliyoripotiwa ni 15 asilimia 0.9.

Hivyo Wilaya ya Mjini , Magharibi ‘A’ na Magharibi ‘B’ zimeongoza zaidi kwa makosa ya kushindwa kuvaa sare na beji kwa utingo na dereva kwa gari za abiria, kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.

Vile vile makosa mengine ni pamoja na kuendesha chombo cha moto gari,vespa,pikipikififti bila ya leseni, bima na leseni ya njia, kuendesha chombo ca moto bila kuvaa helment na kuzidisha idadi ya abiria na mizigo.

ASAS za kiraia zatakiwa kufanya kazi na serikali kuhudumia jamii

0
0
NA Francis Godwin,Iringa .

WITO umetolewa kwa mashirika ya utetezi wa haki za binadamu nchini kuendelea kufanya kazi ya kuisaidia serikali katika masuala mbali mbali ya kijamii kama afya,elimu na mengine ambayo ambayo serikali imekuwa ikifanya .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka asasi za kiraia kanda ya nyanda za juu kutoka mkoa wa Njombe na Iringa jana . mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC), wakili Deogratias Bwire .

Kuwa ipo dhana potofu kwa jamii juu ya kazi za watetezi wa haki za binadamu kwa kumuona mtetezi kama ni mchochezi jambo ambalo si sahihi kwani mtetezi ni mtu yeyote anayefanya kazi ya kusaidia kuokoa maisha ya mwingine .

Alisema kuwa mwaka 1998 baraza kuu la umoja wa mataifa lilidhia azimio la haki za binadamu japo kwa vipindi tofauti tofauti matamko mbali mbali yalitolewa na hadi nchi mbali mbali ziliweza kuja na sera ya haki ya binadamu japo kwa Tanzania bado hatujawa na sheria ama sera ya kuwatambua watetezi .

Kuwa matamko ambayo yamepata kutolewa kikanda ni kama tamko la Grad Bay la mwaka 1999 ,tamko la Kigali la mwaka 2003 ,makubaliano 2004 (Mwakilishi wa watetezi ) , mpango wa kikazi wa Kampala ( KAPA 2009) huku kitaifa ni THRDC (makubaliano ya Newafrica Hotel)

“Nani mwenye jukumu kumlinda mtetezi ,azimio la watetezi wa Haki za binadamu linasisitiza kwamba nchi ndiyo ya kwanza katika kuwalinda watetezi wa Haki za binadamu “ alihoji Bwire

Aidha alisema kuwa makundi na miungano inayochangia katika kuboresha ukiukaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi hivyo basi ukiangalia ibara ya 12 ya tamko hiloinatamka wazi kwamba dola ina mamlaka ya kumlinda mtetezi wa haki za binadamu .Alizitaja haki za mtetezi kuwa ni kulinda na kustawisha haki za binadamu ,kulindwa , kuchunguza na kupata habari ,kutoa maoni ,kukusanyika kwa amani ,kuunda asasi na kupata fedha za miradi pamoja na kuweza kuifikia mahakama.

Bwire alisema kuwa watetezi wa haki za binadamu wanatambulika kote duniani na serikali inajukumu la kuwalinda watetezi ,lakini sote tuna jukumu hilo na THRDC ni mtandao kwa ajili ya watetezi .

Hivyo alisema kuwa mafunzo ya utetezi wa Kimkakati na usalama kwa Watetezi wanaofanya kazi za utetezi wa haki za Kijamii kwa mikoa ya Iringa na Njombe ambayo yameandaliwa na THRDC ni kuweza kuwajengea uwezo zaidi ili kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi .

“Haki za Kijamii zitakazofundishwa zinahusisha haki za elimu bora, afya bora, chakula, maji safi, malazi yenye staha na haki za hifadhi ya jamii (social security) pamoja na mambo mengine” alisema .

Alisema watetezi hao watajengewa uwezo juu ya mabadiliko ya 2019 ya sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikari ya mwaka 2002 na kuelekezwa namna bora ya kufuata sheria za Mashirika yasiyo ya kiserikali na sheria nyingine za nchi kama njia mojawapo ya kuhakikisha usalama wa Mashirika hayo.

Wakitoa maoni yao katika mafunzon hayo washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa wengi wao wamekuwa wakifanya kazi ya utetezi bila kujua wao wanafanya kazi ngani na wakati mwingine wanakuwa katika mazingira magumu pasipo kujua nani wa kumtetea .

Kuwa aliwataka watetezi hao kutoogopa sheria zilizotungwa badala yake kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi huku wakitambua sheria na mazingira ya kazi ya utetezi .

Hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi wanaweza kupiga hatua ya kuboresha kazi zao na hata kuisaidia jamii na serikali katika uwajibikaji wake wa kila siku wenye lengo la kusaidiana pamoja kuhudumia jamii. 
Mkufunzi kutoka THRDC wakili Deo Bwire akitoa mafunzo kwa washiriki wa mafunzo kutoka asasi za kiraia mkoa wa Njombe na Iringa jana
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia masomo
Washiriki wakiwa darasani kuendelea na mafunzo

MILANGO YA UWEKEZAJI TANZANIA IPO WAZI -RAIS MAGUFULI

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

RAIS Dkt. John Joseph Magufuli amesema kuwa milango ya uwekezaji nchini ipo wazi na wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini wanakaribishwa kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ili kuleta ukombozi wa kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika jukwaa la wafanyabiashara baina ya Afrika Kusini na Tanzania Rais Magufuli amesema kuwa wawekezajj wanakaribishwa nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa kuwa nchi Ina hazina ya rasilimali za kutosha zikiwemo pamba na kahawa na hata sekta ya viwanda hasa vya dawa mbalimbali jambo ambalo ni changamoto kubwa katika ukanda wa SADC.

"Ukanda wa SADC una changamoto kubwa katika sekta ya usambazaji wa madawa, Tanzania tunatumia zaidi ya shilingi bilioni 270 katika kununua dawa na vifaa tiba na zaidi ya asilimia 90 ya dawa zinazosambazwa na bohari ya dawa zinatoka nje hivyo hatuna budi kuelekeza nguvu kwenye ukombozi wa kiuchumi hasa kwa kuangalia masuala ya uwekezaji na biashara" ameeleza Magufuli.

Aidha amesema kuwa Afrika Kusini na Tanzania ni washirika wazuri katika masuala ya biashara na lazima nchi hizo zipambane na changamoto ya uzalishaji ambayo bado ipo chini na hiyo ni kwa kuanzisha viwanda vyao wenyewe ambavyo vitachakata malighafi zinazozalishwa ndani ya nchi hizo na sio kusafirisha malighafi hizo nje ya nchi hali inayopelekea kupoteza ajira nyingi.

Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameanza hotuba yake kwa kutoa pole kwa watanzania kufuatia ajali ya moto iliyotokea Mkoani Morogoro na kupoteza maisha ya watanzania zaidi ya 70, na amewaombea manusura wa janga hilo waweze kupona haraka, pia ameishukuru Tanzania kwa kuwa washirika wazuri wa kibiashara na kubwa zaidi ni kushirikiana nao katika kipindi cha kupigania Uhuru kwa kutoa mafunzo, makazi, ushirikiano na umoja walioonesha kipindi kile hadi sasa.

Ramaphosa amesema kuwa amani tuliyonayo tuitunze kwa gharama yoyote na hiyo ni pamoja na kuimarisha umoja na kupiga vita masuala ya rushwa pamoja na kuimarisha biashara hasa kwa kutengeneza mazingira wezeshi ya kibiashara kwa kutoa elimu na ujuzi ambao unaenda sambamba na mazingira yetu.

Aidha ameshauri kuwatengeneza vijana kwa manufaa ya baadaye na hiyo ni pamoja na kuwapa ujuzi na teknolojia hasa katika masuala ya uchumi, biashara na viwanda ili kwenda sambamba na soko la dunia ambalo Lina changamoto ya ushindani na hiyo ni pamoja na kushirikiana baina yao kwani wasipokuwa na umoja hawawezi kuyafikia maendeleo.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli akizungumza katika Kongamano la jukwaa la wafanyabiashara Tanzania na Africha kusini ambapo amesisistiza nchi za Tanzania na Afrika Kusini zijikite katika kuendeleza na kuimarisha mazingira ya ujenzi wa viwanda ili kutengeneza ajira na kuacha kuuza bidhaa ghafi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Waziri Jafo awataka vijana kuwa mabalozi wa amani nchini

0
0

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman Jafo amewataka vijana kutochezea amani ya Nchi na Badala yake wawe Mabalozi Wazuri wa kutunza na kuenzi amani hiyo kwani ni Tunu kwa Taifa la Tanzania.

Waziri Jafo amesema hayo leo Agosti 15,2019 jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambapo amesema amani iliyoasisiwa na Marais wa Tanganyika na Zanzibar ni vigumu kuirejesha ikipotea hivyo vijana ni nguzo Muhimu wa Kuitunza amani hiyo.

“Waasisi Wa Taifa letu ,Julius Kambarage Nyerere na Aman Karume walipambana sana na walitumia gharama kubwa kuhakikisha amani ya nchi yetu inapatikana na tukajipatia Uhuru ,kilichobaki ni kirahisi sana ni kuiendeleza ,kuienzi na kuitunza amani ya Nchi Yetu kwani ikipotea kuirudisha ni vigumu sana ,na wenye wajibu na nguvu kubwa wa kuinza ni ninyi vijana “amesema Jafo.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka vijana waliopewa nafasi za Madaraka kufanya kazi na kuacha maigizo ili waache historia ya Taifa la Tanzania.Waziri Jafo amesema ni vyema kwa vijana waliopewa dhamana ya kuliongoza taifa kuwajibika vyema kuwahudumia Wananchi .

Pia amewataka kuchangamkia fursa ya mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Halmashauri ambapo amedai kwa sasa kina mama ndio wamekuwa wakichangamkia fursa hiyo.

“Igeni mfano wangu mimi simwangushi Rais,bajeti ya nchi zaidi ya asilimia 20 inatoka kwangu,vijana mkipewa nafasi fanyeni kazi.Usikubali ukiwa kama kijana lazima uache alama ili wakukumbuke,kijana sio sifa kukaa kiti kirefu halafu unasema kunyweni mpaka mikono idondoke, acha alama wekeni mifano kwa watu wengine,”amesema .

“Vijana acheni maigizo fanyeni kazi ya kuwasaidia Watanzania fanya kazi kwa ajili ya kuwahudumia watu,fanya kazi yako itangazike,tukifanya maigizo hatuwezi kulisaidia Taifa letu.Niwaombe vijana wenzangu tupambane,”amesema.Jafo amesema vijana ambao wamepewa fursa wasivunje matumaini ya vijana wenzao.

Amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri mbalimbali nchini huku akidai kwamba wanawake wamekuwa wakijitokeza kwa wingi.

“Bado ni changamoto,lazima tuangalie namna ya kurejesha mikopo wengi wanaorejesha ni kina mama,vijana wanaokopa kurejesha ni shida,”alisema Jafo.Jafo amewataka vijana kulima kilimo cha kisasa kwani kimekuwa na faida kubwa ambapo alidai ekari moja ikipandwa vizuri inaweza kutoa mazao mengi.

“Ukiamua kufuga kuku wa mayai 10,000 ambao kila siku wanatoa trei 300 kwa shilingi 7000 ina maana kila siku wana uwezo wa kupata milioni moja.Vijana naomba niwaambie badilishaneni mawazo,wekezeni katika ujasiriamali,”alisema.

Aidha,Jafo aliwataka vijana ambao watajadiliana katika kikao hicho kufanya tathmini ya yale watakayokubaliana nayo na kisha wanayapeleke Serikalini.“Tumepata fursa ya kukutana bahati nzuri kutoka katika mikoa yote nawaomba mfanye tathmini ya mambo yote na yale mtakayokubaliana yaleteni Serikalilini na tutayafanyia kazi.

“Zamani kulikuwa na kauli mbiu vijana ni taifa la kesho kauli hiyo tumeitoa na kwa sasa vijana ni taifa la leo,vijana sasa mnaweza kupewa fursa na mkapewa nafasi mkazitendea haki.

Jafo amesema wana kila sababu ya kujadiliana kuhusu elimu kwani imekuwa ni daraja la kuweza kufikia mafanikio.“Kumbukeni tuna kila sabbau ya kujadili ajenga ya elimu, tuna kila sababu ya kuboresha elimu yetu bila elimu vijana wa sasa hatuwezi kupasua tuna kila sababu ya kuitafakari elimu yetu.Niwaombe sana lazima vijana wa kitanzania tujikite katika elimu.

Aidha,Jafo amewataka vijana kujitambua kwa kuhakikisha wanakuwa na uzalendo wa kununua bidhaa zinazozalishwa na vijana.“Tuna agenda kubwa tupambane na adui wa roho mbaya kuna vijana wengine wana roho mbaya wapo kuwakwamisha kwanza tupendane,bidhaa hizo zote kama tutanunua tutaenda mbali kwani vijana ni timu kubwa,”amesema.

Kwa Upande wake,Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Vijana,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Zanzibar,Amour Hamil Bakari,ame sema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kuchukua juhudi kuhakikisha vijana wanapata kazi pamoja na kufanya kazi zenye staha. 

“Serikali zinaendelea kuchukua juhudi kuhakikisha vijana wetu wanapata kazi zenye staha pamoja na changamoto ya ajira.Niwakumbushe vijana kuendelea kulinda amani iliyopo, suala la kudumisha muungano wetu hili halina mjadala na sisi tutaendelea kuwakumbusha vijana kuhakikisha wanalinda muungano kwa nguvu zote,”amesema.

Naye,Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)Jacqueline Mahon amesema vijana wanatakiwa kusaidiwa kwenye mambo mbalimbali.

Pia amesema elimu ni Msingi wa Maendeleo endelevu kwa vijana ndio maana maadhimisho ya vijana duniani mwaka 2019 imelenga zaidi kuimarisha elimu kwa vijana na UNFPA imekuwa ikijikita zaidi kutatua changamoto mbalimbali za vijana ikiwa ni pamoja na changamoto ya elimu na Ajira Kwa Vijana.

Hivyo Maadam Mahon amesema UNFPA ina mkakati Kabambe wa kuwawezesha vijana kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Tanzania na ya Kimataifa huku akizungumzia mkutano Mkubwa wa Vijana utakaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na kuwaasa vijana kujitokeza kwa wingi kwani vijana ni chachu muhimu kwa Maendeleo ya nchi.

Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya vijana,Maadam Sophia Mbeyela ameshukuru serikali pamoja na asasi za kiraia kwa kujali vijana wa rika zote na aina zote wakiwemo wenye ulemavu na kusema kuwa wao kama vijana wenye ulemavu hawaachwi nyuma kwani ulemavu si ugonjwa.

Awali Afisa Maendeleo ya Jamii ,Idara kuu ya vijana jiji la Dodoma Mfungo Daniel Manyama ambaye alikuwa mwakilishi wa Afisa vijana Mkoa wa Dodoma , amewaasa vijana kuchangamkia Fursa ya Zao la Zabibu pia kuunga mkono vijana wenzao kununua zao hilo ili kuinua uchumi wa vijana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Suleiman Jafo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa jijini Dodoma leo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Suleiman Jafo akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya vijana kimataifa leo jijini Dodoma

RAIS MAGUFULI ,RAIS RAMAPHOSA WAZUNGUMZIA UMUHIMU WA NCHI ZA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI KUSHIRIKIANA KUKUZA UCHUMI

0
0


Na Said Mwishehe, Michuzi TV


RAIS Dk.John Magufuli wa Tanzania na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini  wameeleza umuhimu wa uwekezaji katika  miundombinu na kutumia fursa ya rasilimali zilizopo kukuza uchumi.

Marais hao wameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua Jukwaa la Biashara lililohusisha wafanyabishara, wawekezaji na maofisa wa serikali hizo.

Kwa upande wake Rais Cyril Ramaphosa, amesema kwamba uhusiano wa nchi yake na Tanzania ni wa muda mrefu na matarajio yao ni kuona ushirikiano unaendelezwa.

Amesema Afrika Kusini imaumia kwa tukio lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 walioungua kwa moto.Hivyo anatoa pole kwa familia na majeruhi na kwamba wanamuomba Mungu awaponye.

Kuhusu mafanikio yao ambayo wamefikia nchini kwao leo hii amesema yanatokana na   ushirikiano baina ya nchi zao na kwamba majadiliano ya Jukwaa hilo la Biashara yataonesha wapi waelekee kwa sasa.

"Tunapaswa kuwa na kauli moja ya wapi tunaelekea kibiashara ili kila nchi iweze kunufaika kwa maendeleo jumuisha," alisema.Alisema takwimu zinaonesha idadi ya watu itaongezeka siku zijazo hivyo ushirikiano huu unapaswa kuendelezwa kwa maslahi ya nchi zetu huku akieleza kuwa biashara itafanikiwa kama urasimu utaondolewa kwa kila pande.

Ametumia nafasi hiyo kueleza changamoto za kupata visa zinapaswa kuondolewa ili kuwavutia wafanyabishara na watalii.

Rais huyo wa Afrika Kusini amesema serikali yake imekuwa ikjadiliana na wafanyabishara kuhusu fursa zilizopo na kupata ufumbuzi.Pia amesema wanakaribisha kila mtu anayetaka kuwekeza kuingia kuwekeza ili kuchochea uchumi

Nchi zinatakiwa kuwekeza katika kukuza uchumi ili kusaidia huduma za jamii kwenye mitaa ambapo wawekezaji wanawekeza.Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania imejipanga kuelekea uchumi wa viwanda ndio maana imeamua kuwekeza kwenye miundombinu kama kivutio cha wawekezaji kuja kuwekeza.

" Serikali imejipanga kuleta  mapinduzi ya kiuchumi kwa kuwekeza kwenye miundombinu naomba wawekezaji waje wawekeze na nyie nawaomba mjadala wenu ujikite kwenye mipango yetu sio mpeane namba halafu hakuna kinaendelea. Tunataka matokeo ya nyie kukutana yaweze kuwa na adhari chanya kwa nchi zetu kiuchumi, kijamii na maemdeleo, "amesema.

Alisema jukwaa hilo linaonesha dhamira nzuri ya nchi zetu kukuza uchumi, biashara na uwekezaji hivyo likitumika vizuri nchi zetu zitanufaika na kuongeza Afrika Kusini ni taifa kubwa ambapo bidhaa nyingi za Tanzania zimekuwa zikiienda Afrika Kusini hivyo kulifanya taifa hilo kuwa la pili kwa kununua bidhaa.

Pia amesema.Tanzania inauza bidhaa nyingi Afrika Kusini ikiwemo madini hivyo na ni muhimu kuongeza uwekezaji wa viwanda kama vya usindikaji  nyama, samaki na sukari.Rais Magufuli amewakaribisha wananchi wa Afrika Kusini kuja kuwekeza katika viwanda vya kuchenjua madini na vya dawa ili kupunguza gharama za kuagiza kutoka  nje ya Bara la Afrika.

Amefafanua viwanda vya dawa vitaweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi zetu .Wakati katika sekta ya utalii bado haijafanya vizuri na kuweza kusaidia maendeleo ya nchi."Tanzania ni ya pili duniani kwa vivutio vya utalii baada ya Brazili napenda kuwaomba wajumbe wa SADC mtembelee vivutio vyetu," alisema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa mara baada kumaliza kusoma hotuba yake katika Jukwaa la Biashara lililohusisha wafanyabishara, wawekezaji na maofisa wa serikali hizo. lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.

MABALOZI WA TANZANIA KUTOKA NCHI 42 DUNIANI WAFURAHISHWA NA KASI YA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR

0
0
Shirika la reli Tanzania - TRC lapokea Ugeni wa mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC ambao wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.

Ugeni huo mkubwa ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa katika eneo ambalo stesheni kubwa ya reli ya kisasa inajengwa Stesheni jijini Dar es Salaam na kuwapa maelezo kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa - SGR ambao ulianza mwaka 2017 chini ya Mkandarasi Yapi Merkezi ambapo mradi unatekelezwa kwa kusanifu na kujenga.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja kungu Kadogosa alielezea faida za Mradi ikiwemo ajira zilizozalishwa kupitia mradi ambapo 96% ya wafanyakazi katika mradi huo ni Watanzania, pia Mkurugenzi ameeleza kuwa shirika linaendelea na mpango wa kuandaa vijana watakaosimamia na kuendesha shughuli za usafirishaji katika reli ya kisasa ambapo vijana wanapewa mafunzo ya nadharia na vitendo nje na ndani ya nchi ili mradi utakapokamilika kuwe na nguvu kazi ya kuweza kuendeleza mradi huo mkubwa.

“Katika miradi mikubwa inayosimamiwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mh. Rais Dr.John Pombe Magufuli Ujenzi wa Reli ya Kisasa ni mmoja wapo” alisema Ndugu Kadogosa.

Vivyo hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TRC alitolea ufafanuzi juu ya tofauti zilizopo kati ya Reli ya kisasa - SGR inayojengwa Tanzania na za nchi nyingine barani Afirka na kusema kuwa reli inayojengwa nchini ni ya kipekee kuwahi kujengwa Afirka 

“Reli ya kisasa ya Tanzania itakuwa na uwezo mkubwa wa ekseli 35 tofauti na nchi zingine ambazo nyingi ni 25, kwa hiyo itakuwa na uwezo mkubwa wa kubeba mizigo hasa madini kutoka Kongo na Msongati Burundi, pia mwendokasi kwa treni ya mizigo utakuwa 120 na 160 kwa treni za abiria ambayo kitaalamu ni ‘single truck’ hivyo ni tofauti na reli za nchi nyingine”

Mabalozi walipata Fursa ya kupanda treni ya majaribio ya mkandarasi kuanzia stesheni ya Soga hadi eneo la Kikongo mkoani Pwani ambapo mabalozi walifurahishwa na ubora na uimara wa reli ya SGR kwa kuwa hakuna mitikisiko kama ilivyozoeleka katika reli ya ‘Meter Gauge’, katika Safari hiyo Mkurugenzi aliwashukuru Mabalozi hao kwa kuwa anaamini watakuwa wawakilishi wazuri katika kuutangaza Mradi

“Najua mtakuwa mabalozi wazuri kwa nchi mnazofanyia kazi”, alisema Mkurugenzi Mkuu wa TRC.

Akizungumza na waandishi wa Habari Balozi wa Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kuwa Mabalozi ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchumi wa nchi hivyo uwepo wa Miundombinu imara ya reli, anga, barabara na bandari unaleta matumaini makubwa katika kuleta uchumi imara 

“Tunapotekeleza diplomasia ya uchumi, miundombinu ni lazima hivyo uwepo wangu kwenye treni hii ni ndoto iliyotimia, nampongeza Rais wa Jamhuri na Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa kwa usimamizi mzuri” alisema Dkt. Migiro

Halikadhalika Mabalozi pia walitembelea kiwanda cha kutembelea mataruma kilichopo soga kibaha mkoani pwani ambapo kiwanda hicho kinazalisha mataruma 1500 kwa siku na hivyo kipande cha Daresalaam - Morogoro yatatandikwa mataruma yapatao laki tano , mabalozi pia walisifu ubora wa mataruma hayo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akifafanua jambo kwa  mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC ambao wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
  Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC  wakiwa katika picha ya pamoja,wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
 Baadhi ya Mabalozi wakiwa ndani ya treni ya Wahandisi wakijadiliana jambo
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akiwaogoza mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,kushuka kwenye treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.
 Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,wakimisikiliza mmoja wa wahandisi wa ujenzi wa reli hiyo waliposimama kwenye moja ya kituo ili kupata ufafanuzi zaidi,wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019.

 Ujenzi wa Reli ya kisasa-SGR ukiendelea kwa kasi
 Mabalozi wa Tanzania takribani 42 kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwemo Mabalozi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika - SADC,wakisafiri kwa treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019. 
Mabalozi wakishuka kwenye treni ya Wahandisi wakati wa ziara yao ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 15, 2019. 

Naibu Waziri Mavunde aagiza uchunguzi wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi kiwanda cha Hong Wei

0
0

Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amefanya ziara ya ukaguzi katika kiwanda cha HONG WEI INTERNATIONAL kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na kuagiza kufanyika uchunguzi katika usahihi wa malipo ya mishahara ya Wafanyakazi iliyoandikwa kwenye mikataba na kiasi halisi kinachopokelewa ambapo imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Serikali ikawa inapoteza mapato ya kodi ya mshahara.

Naibu Waziri Mavunde amevitaka vyombo vya uchunguzi kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mufindi kujiridhisha na nyaraka mbalimbali za mishahara ya wafanyakazi na kuwasilisha taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ndani ya siku saba.

Wakati huo huo,Naibu Waziri Mavunde amekitaka Kiwanda hicho kuwapa Wafanyakazi wote mikataba kwa mujibu wa Sheria na.6/2004 ya Ajira na Mahusiano Kazini na pia kuagiza wafanyakazi wote warudishiwe fedha walizokatwa kinyume na sheria katika mshahara wao kwa ajili ya kununua vifaa kinga na kuwataka waajiri wasikwepe jukumu la kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa afya na usalama wao wakiwa kazini.

Akiwa wilayani  hapo Naibu Waziri Mavunde amepata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya HISOON Ltd kutoka China James Lee ambaye amevutiwa na sera na mazingira ya uwekezaji nchini na sasa anakamilisha taratibu za uwekezaji mkubwa wa kiwanda kikubwa cha Makaratasi ambacho kitakuwa uwezo wa kuzalisha tani laki tano za karatasi na ambacho pia kinatarajiwa kuajiri wafanyakazi wasiopungua 5000.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,  Vijana, Kazi na Ajira, Mhe Anthony Mavunde akizungumza na viongozi na watumishi wa kiwanda cha Hong Wei kilichopo wilayani Mufindi mkoani Iringa

Sakata la Ultrasound iliyoibiwa Simiyu, Waziri Jafo atoa maelekezo kwa RC Mtaka

0
0
Charles James, Michuzi TV

SIKU mbili baada ya mashine ya Ultrasound kuibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Suleiman Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka kuunda tume maalum ya kuchunguza tukio hilo.

Mashine hiyo inadaiwa kuibiwa pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer) ambapo ilikua maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina Mama wajawazito na iliibiwa ikiwa katika wodi hiyo.

Akizungumza jijini Dodoma, Waziri Jafo amesema hajafurahishwa na kitendo cha mashine hiyo kuibiwa kwa sababu kinarudisha nyuma maendeleo makubwa ambayo Serikali imeyafanya katika sekta ya Afya nchini.

" Kitendo cha mashine hii kuibiwa kinaonesha jinsi gani wapo watu wenye nia ovu ya kurudisha nyuma Uwekezaji ambao Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeufanya katika sekta ya afya, sasa nitoe maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa kuhakikisha anatuma Timu ya kwenda kuchunguza ili tujue mashine hiyo iliibiwaje,"amesema Waziri Jafo.

Aidha ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi aliyoagiza watumishi 137 wa Hospitali hiyo kuchangia kutoka kwenye mishahara yao ndani wiki moja ili kulipa machine hiyo iliyoibiwa.

" Maelekezo yangu ni kwamba kutokana na hali iliyojitokeza huko Timu itakayoundwa kuchunguza tukio hilo inapaswa ije na majibu ambayo tutawajua waliofanya wizi huo ambapo kwanza watapaswa kurudisha mashine hiyo kisha wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kupandishwa mahakamani.

" Kuhusu watumishi 137 kulipia mashine hiyo kutoka kwenye mishahara yao, nielekeze kuwa watumishi hawa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu kitendo cha kuwaambia walipe ni kuwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma," amesema Waziri Jafo.

Amezitaka mamlaka za Wilaya ya Bariadi kutowachangisha fedha watumishi hao na badala yake wajielekeze katika kuhakikisha wanawapata waliohusika na wizi huo ili wachukuliwe hatua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Suleiman Jafo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Dodoma juu ya kupotea kwa mashine ya Ultrasound katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi

CMSA YATAKIWA KUWEZESHA KAMPUNI NYINGI KUORODHESHWA SOKO LA HISA

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama, wakipeana mkono baada ya kumaliza Ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 ya CMSA, jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama, alipokuwa akieleza utekelezaji wa bajeti ya Mamlaka hiyo kwa mwaka wa Fedha 2018/19, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), kuhakikisha inaorodhesha Kampuni nyingi katika Soko hilo ili kuweka uwazi zaidi katika utendaji wao na kuchangia katika ongezeko la mapato ya Serikali kwa njia ya kodi.
Mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (mbele) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama (wa pili kulia), ukiendelea katika ofisi za CMSA jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka CMSA na Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kumaliza Ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 wa CMSA, jijini Dar es salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

…………………….

Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam 

Serikali imeitaka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuhakikisha Kampuni nyingi zinaorodheshwa katika Soko la hisa ili kuweka uwazi zaidi katika utendaji wa kampuni hizo na hivyo kuwezesha Serikali kukusanya kodi stahiki na kuchangia katika ongezeko la mapato ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alipofanya ziara katika Mamlaka hiyo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Kazungu, alisema kuwa CMSA iendelee kusimamia masoko ya Mitaji ya Dhamana kwa kuorodhesha Kampuni nyingi zaidi katika soko hilo la hisa kwa kuzingatia masharti ya kuorodheshwa kampuni ili kuongeza uwazi, utawala bora na ufanisi wa kampuni hizo kwa kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji na uwazi wa hesabu zao, hatua itakayochangia kukuza uwekezaji na mapato ya Serikali hususani katika eneo la kodi.

“Muendelee na kasi ya kutoa elimu kwa wananchi wengi ili waweze kujiunga na Masoko ya Hisa hususani kwa wananchi walio katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”, alieleza Dkt. Kazungu.

Alisema kuwa iwapo wananchi wengi watajiunga katika Masoko la Hisa kutawafanya kuongeza mapato yao lakini pia kushiriki katika umiliki wa uchumi wa nchi yao.

Dkt. Kazungu alisema kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa uchumi wa viwanda, uchumi unaotarajiwa kujengwa katika kipindi kifupi wakati wa kuelekea katika uchumi wa kati hivyo ni vema wawekezaji wakahimizwa kupata mitaji ya kuendeleza na kupanua uwekezaji kupitia masoko ya mitaji na kutoa fursa nyingi za uwekezaji kwa wananchi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama, amesema Mamlaka yake imeweka mkakati wa kutoa elimu kwa umma na wawekezaji mbalimbali jinsi ya kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo.

“CMSA inaendelea kutoa elimu kwa umma na kwa makundi mbali mbali ya wanataaluma, wanafunzi wa elimu ya juu, watunga sera ikijumuisha Kamati za Bunge. Elimu hii inalenga kuelimisha umuhimu na fursa ya masoko ya mitaji katika kukuza uchumi na ushirikishwaji wa wananchi katika Sekta ya Fedha hususani masoko ya mitaji” alifafanua Bw. Mkama.

Alisema kutokana na jitihada hizo, kwa sasa uhitaji katika uwekezaji katika Soko ni mkubwa, hii inawafanya kuongeza bidhaa zinazokidhi matakwa ya wawekezaji ndani na nje ya nchi.

“Hii imejidhihirisha hivi karibuni kwa kuongezeka kwa kampuni nyingi katika sekta ya fedha kuorodhesha hatifungani ikiwa ni njia sahihi ya taasisi hizo kupata fedha za mahitaji mbalimbali ya utoaji mikopo na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Alisema elimu hiyo pia imeleta matokeo chanya na mwitikio wa matoleo ya hatifungani za Kampuni ya Kuendeleza Sekta ya Nyumba – TMRC, Benki ya Biashara ya DCB na Benki ya Biashara ya NMB na unaonyesha wazi kuwa kuna ongezeko kubwa la uelewa wa wananchi kushiriki katika uwekezaji kwenye masoko ya mitaji.

Toleo la hatifungani ya NMB Bank limeweka historia kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini kwa kupata kiwango cha shilingi bilioni 83.3, ikiwa ni mafanikio ya asilimia 333 ikilinganishwa na shilingi bilioni 25 zilizotarajiwa kukusanywa.

Bw. Mkama alisema kuwa mauzo hayo yamekuwa na idadi na thamani kubwa kuliko mauzo yote ya hatifungani yaliyowahi kufanyika hapa nchini, ambapo jumla ya wawekezaji 2,264 wameweza kushiriki. Kati ya wawekezaji hao, asilimia 99.5 ni wawekezaji wadogo wadogo, na wawekezaji Kampuni ni asilimia 0.5.

“Tumeshatoa maelekezo kwa watendaji na washiriki (wanaotoa dhamana) katika Masoko ya Mitaji kuhakikisha wanakuja na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wawekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi watakao sababisha ongezeko la mapato yao na upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo jambo litakalochangia kushiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi”, alieleza Bw. Mkama.

Alisema kuwa katika utoaji wa elimu, CMSA inatumia mbinu mbalimbali za kibunifu ikiwa ni pamoja na kuweka mashindano kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania Bara na Visiwani kwa kuwezesha wanafunzi kujifunza elimu ya masoko ya mitaji kwa njia ya kujibu maswali na kuandika insha

Alibainisha kuwa, wanafunzi wanaofanikiwa kushinda nafasi ya kwanza hadi ya tatu wanapewa tuzo mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kuanzia shilingi milioni moja hadi milioni 1.8 kama kivutio cha ushiriki huku wanafunzi walioshika nafasi 20 za juu wanazawadiwa shilingi laki 2 kila mmoja na kwamba washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu wa mwaka huu (2019) watapelekwa nchini Namibia kwa ziara ya mafunzo.

MBUNGE MGIMWA AKERWA NA UBOVU WA BARABARA ZA KATA YA MAPANDA

0
0
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mtwivila kilichopo kijiji cha Mapanda kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Ihimbo kata ya Mapanda juu ya masikitiko yake juu ya ubovu wa barabara



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kutokana na wananchi kutofanya kazi kwa uhuru.

Akizungumza wakati wa ziara yake kwenye kata ya Mapanda Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amekiwa kuwa tatizo la ubovu wa miundombinu hiyo imekuwa kero na ameanza kuifanyia kazi ili kuzikarabati ziweze kupitika kirahisi.

“Nimebaini kuwepo kwa uchakavu wa barabara katika kata ya Mapanda ambazo zimekuwa zikififisha maendeleo ya jimbo langu hivyo natakiwa kufanya kila niwezalo kuhakikisha barabara hizi zinapitika” alisema Mgimwa

Mgimwa amesema kuwa amefaikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutengeza barabara zote korofi ili ziweze kupitika kwa urahisi.“Nimefakisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia nane kuhakikisha tunakarabati barabara hii ambayo imekuwa inatumiwa na watu wengi kimaendeleo katika jimbo hili” alisema Mgimwa

Mgimwaalisema kuwa kuna barabara inayotoka kuanzia Kibengu,Kipanga,Ihimbo,Uhafiwa,Kisusa,Ukami hadi njia panda ya Mapanda inayokadiliwa kuwa na urefu wa kilometa sitini na moja imetengewa fedha kidogo tofauti na matengenezo yanayotakiwa kufanyika katika barabara hiyo.

“Nitakuja na viongozi wa TARURA huku kuhakikisha wanajionea ubo vu wa barabara hizi ili wanavyotenga fedha wajue wanakarabati wapi na wanaacha wapi haiwezekani barabara hii ikatengewa kiasi cha shilingi milioni thelethini tu” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa amewataka TANROAD na TARURA kuzikarabati barabara zote korofi kipindi cha kiangazi ili zipitike kirahisi na sio kipindi cha masika ambapo mara nyingi hutokea kero kwa wananchi.

Wakitoa kilio chao kwa mbunge huyo wanachi wa vijiji hivyo walimwambia hakuna maendeleo yanayoendelea katika vijiji hivyo kutokana na ubovu wa barabara hizo.Hakuna usafiri wa basi wala gari inayofika huku kutokana na ubovu wa barabara hizi hivyo tunakuomba uhakikishe unatusaidia kuzikarabati barabara hizo” walisema wananchi

MABALOZI WA TANZANIA WATEMEBELEA MRADI WA RELI NA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM

0
0
Baadhi ya Wafanyakazi wakiendelea na majuku ya kutengeneza zana za kujengea mradi wa SGR kwenye kiwanda kidogo kilichopo kambi ya Soga, Pwani. 
Mhe. Nahim Azizi Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika akisalimiana na mfanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam akiwa na ujumbe wa mabalozi wengine walipowasili bandarini hapo kwa ziara ya kikazi.

Wakiwa katika Bandari ya Dar es Salaam mabalozi walipata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa upanuzi wa bandari sambamba na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kuhudumia meli zinazobeba mzigo mkubwa. 

Mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, Bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kuhudumia mizigo ya kiasi cha tani milioni 28 kwa mwaka, ikiwa ni mara mbili ya kiwango cha sasa ambapo inauwezo wa kuhudumia mizigo kiasi cha tani milioni 13 pekee. Aidha, sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia mizigo mingi, pia mradi huo utapunguza muda wa kuhudumia meli kutoka masaa 80 kwa meli moja kama ilivyo sasa hadi masaa 30 mara mradi huo utakapo kamilika.

Wakati huo huo mabalozi walitembelea mradi wa ujenzi wa wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) ambapo walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kuanzia Stesheni jijini Dar Salaam hadi Soga mkaoni Pwani.

Mabalozi wamefurahishwa na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu kwa manufaa ya Wananchi. Mabalozi kwa nyakati tofauti wamesema licha ya miradi hii kuliongezea pato Taifa, mara baada ya kukamilika miradi hii itaiweka Tanzania katika nafasi nzuri zaidi ya ushindani wa kibiashara katika soko la Afrika Mashariki na katika ukanda wa Kusini mwa Afrika
Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni alipoambatana na mabalozi katika ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam. 
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza wakati wa ziara ya kikazi Bandari ya Dar es Salaam 
Mabalozi wakifuatilia wasilisho kuhusu mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam 

Mabalozi wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa Shirika la Reli kuhusu mchoro wa mradi mpya wa SGR 
Mabalozi wakipanda Treni tayari kwa safari ya kuelekea Soga mkoani pwani, ambapo pamoja na mambo mengine walijionea kiwanda cha kuunda baadhi ya vifaa vya kujengea mradi 
Sehemu ya mabalozi wakiangalia mandhari yanayozunguka eneo la mradi wa SGR wakiwa njiani kuelekea kambi ya mradi ya Soga 
Sehemu nyingine ya mabalozi wakifurahia jambo wakati wa ziara ya kikazi kutoka stesheni, Dar es Salaam kuelekea Soga, Pwani. 
Sehemu ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioambatana na ujumbe wa mabalozi wakati wa kutembelea mradi wa ujenzi wa SGR 
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara, Shirika la Reli na wafanyakazi wa ujenzi wa mradi wa SGR 



HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LAVUKA LENGO, LAKUSANYA MAPATO KWA ASILIMIA ZAIDI YA 100%

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imevuka lengo la kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 105%,ambapo limekusanya jumla ya shilingi bilioni 16.4 lengo lilikuwa ni shilingi bilioni 15.6

Hayo yameelezwa na mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuelezea pongezi zilizotolewa na waziri wa Tamisemi Suleiman jafo kufuatia Jiji la Arusha kuongoza kwa makusanyo kwa mwaka 2018/19 katika majiji yote Nchini.

Amesema haijawahi kutokea Jiji la Arusha likaongoza kwa mapato ya ndani na hivyo wameweka mkakati ambalo utaliwezesha Jiji hilo kuendelea kuongoza kutokana na ubunifu wa kuongeza vyanzo vingine vya mapato na kuimarisha usimamizi wake.

Amesema katika kuhakikisha wanaimarisha ukusamyaji wa mapato ya ndani halmashauri hiyo ya Jiji imekabidhi vyanzo 14 vya mapato kwa Suma JKT ikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na maliasili na machimbo ya Moramu kutokana na uadilifu wao.

Amesema kuwa halmashauri itaendelea kubuni vyanzo vingine vya mapato ikiwemo ujenzi wa maduka eneo la Ranger safari,kuboresha machinjio,kumaliza mgogoro wa Happy sausage.

Amesema kutokana na makusanyo hayo halmashauri imeweza kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani.utengenezaji wa madawati kwa kutumia karakana ya halmashauri hiyo ,wamekarabati kituo cha afya cha Moshono.

Amesema kuwa mwaka huu halmashauri inajenga shule za ghorofa kwenye shule za Moivaro,Muriet na Terati kupitia fedha za ndani.Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha Dakta Maulid Madeni amesema kuwa halmashauri imejipanga kukusanya shilingi bilioni 20 kwa mwaka 2019/20.

Amesema ukusanyaji huo utaiwezesha halmashauri hiyo kujitegemea kimapato ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi wote na hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kutoa ruzuku kwa halmashauri hiyo.

Katika hatua ningine Mkurugenzi huyo amewaonya wafanyabiashara wakubwa wa maduka wanaotumia vitambulisho vya machinga kuendesha biashara zao,kwa kudao kuwa atawachukulia hatua kali kwa kuwa wanaikosesha halmashauri mapato .
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro akiongea na waandishi wa habari.

NMB MOVES TO PROVIDE LACTACTING MOTHERS A NURSING & FIRST AID ROOM

0
0
NMB Bank has established a lactation room that will provide space for nursing mothers working with the Bank to breast feed their babies.

The room will among other things help working moms at the bank pump and preserve breast milk for their babies during working hours. 

The move, according to the NMB management, is to help mothers to transition well after maternity leave. 

Speaking during the launching ceremony of the nursing room at NMB headquarters in Dar es Salaam, the Chairperson of NMB Women Arise Network and the bank’s head of Trade Finance Ms Linda Tegisa, said the establishment of the room is an initiative set by the bank to support women in carrying up their roles at the workplace and nursing their babies. 

We are very grateful to the management of the bank for setting up the initiative to support women especially those with babies; she said adding that the move expresses strong commitment by the employer to support women in nursing their babies without missing at the workplace. 

Ms Tegisa urged other financial institutions and others to establish nursing rooms and help the working mothers express breast milk for their babies in order to avoid unnecessary misunderstandings that may arise between the working moms and their employer. 

Many working mothers face many challenges when it comes to balancing breastfeeding with tackling their job requirements; having a nursing room at the workplace is an important initiative to break the challenges; she said. 

On the other hand, the Head of Innovation of the Bank Ms Josina Njambi, said the launched nursing rooms contain all important facilities to enable moms at the bank meet and breastfeed their babies, pump and preserve milk. 

The rooms contains comfortable chairs that allow working mothers to sit up straight to pump milk, a refrigerator for storing breast milk and a sink to rinse out parts with soaps and towel among other necessities.
 Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Filbert Mponzi  na Meneja biashara, Abamwesiga Beneth  wakiwa chumba cha mapumziko kwa wagonjwa baada ya benki ya NMB kuzindua huduma ya kwanza.
 Wafanyakazi wa NMB wakizundua chumba za huduma ya kwanza kwa wajawazito na wanaonyonyesha. 

Morogoro yatoa utaratibu kwa wadau wa maendeleo kuchangia msaada wa vifaa tiba

0
0
Serikali ya mkoa wa Morogoro imetoa utaratibu kwa baadhi ya wadau wa maendeleo watakao penda kuchangia msaada wa vifaa tiba kwaajili ya majeruhi kupitia akauti ya bank ya NMB huku baadhi ya wadau hao wakiwemo shirika la hifadhi za taifa tanapa wakitoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya wathirika wa ajali ya lori lililolipuka kwa mato na kusababisha vifo zaidi ya 80 mpaka sasa.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk, Kebwe Steven Kebwe akipokea hundi ya shillingi millioni 10 kutoka kwa Mhifadhi mkuu wa hifadhi  milima ya Udzungwa, Donatus Dayona kwa niaba ya  shirika la hifadhi  za taifa TANAPA  kwa lengo la kusaidia  waathiriwa wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk,Kebwe Steven Kebwe akiwasikiliza kwa makini maofisa wa jeshi usu waliofika katika ofisi yake kwa mazungumuzo   mbalimbali ikiwemo  kutoa  hundi ya shillingi milion 10 kwa ajiri ya kusaidia maafa yaliyotokea mkoani humo.
 Mkuu wa mkoa wa morogoro Kushoto mwenye koti jeusi  Dk,Kebwe Steven Kebwe  akiongozana na maofisa wa jeshi usu mara baada ya kutoka kuona miili  ya marehemu iliyokuwa  nje ya chumba cha kuhifadhia maiti .

DC Ndejembi kula sahani moja na maafisa ugani wazembe wilayani Kongwa

0
0
Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mh Deo Ndejembi ametoa siku saba kwa maafisa ugani wilayani hapo kumletetea tathimini ya mpango kazi wao wa namna gani ya kuweza kuwainua wakulima wa Alizeti wilayani hapo katika kufanya kilimo cha biashara.

Amesema zao la Alizeti ni miongoni mwa mazao tegemezi katika kufikia malengo ya Rais Dk John Magufuli aliyoyaweka ya kuhakikisha Tanzania inakua Nchi ya viwanda.

Hayo ameyasema katika mkutano maalumu na wakulima wa zao hilo ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara nchini (TNBC) ambapo DC Ndejembi amesema maafisa ugani hao wana jukumu kubwa la kuhakikisha wakulima wanabadilika na kuacha kufanya kilimo cha mazoea.

" Tunaweza kuwalaumu wakulima kuwa hawachangamkii fursa na hawabadiliki lakini kiukweli maafisa ugani wetu ndio wamekua changamoto kwetu, hawaendi site kuwapa elimu wakulima, hawatembelei mashamba wao wanakaa tu mpaka wasikie DC ana ziara ndo wanaanza kukimbizana.

" Sasa natoa wiki moja waniletee mpango kazi wao na baada ya hapo nitaanza ziara ya Kata kwa kata kukagua mashamba yao na namna gani wametoa elimu kwa wakulima wetu, hatuwezi kuwa na watu wasiofanya kazi halafu wanalipwa mshahara huko ni kumhujumu Rais Dk John Magufuli na hilo siwezi kukubali likatokea Kongwa," amesema Ndejembi.

Amesema lazima maafisa ugani hao wawe sehemu ya kuwasaidia wakulima katika kufanya kilimo bora cha kibiashara lakini pia kuona fursa zingine zilizopo kwenye kilimo.

" Haiwezekani tukawa na maafisa ugani wanaofanya kazi Desemba mvua zibapoanza hadi Aprili zinapoisha, je miezi mingine wanafanya nini huku ni kula mshahara wa bure, tutawachukulia hatua wote ambao hawana mpango wa namna gani tunaweza kuongeza mavuno yetu," amesema DC Ndejembi.

Aidha Mh Ndejembi amewataka wakulima wa Alizeti kubadilika na kuacha kufanya kilimo cha mazoea badala yake wafanye kilimo cha kisasa wakijua kuwa Alizeti ni zao la biashara na viwanda nchini vinategemea pia zao hilo.

" Mimi nimejifunza kuwa Alizeti haiishii tu kwenye mafuta hata mashudu yale yana thamani kubwa sana, haya mashudu mnayoyadharau yanatengeneza hadi breki za gari. Ndugu zangu wakulima badilikeni ili muweze kuondokana na umaskini, kilimo kinalipa hasa hiki chetu cha alizeti," amesema DC Ndejembi.

Kwa upande wake Meneja wa Uboreshaji wa Mazingira wa Baraza la Biashara nchini (TNBC), William Magehema amesema wao kama Baraza wamelipa kipaumbele zao la Alizeti na kwamba kupitia kikosi kazi chao cha kilimo watahakikisha kilimo cha zao hilo kinakua ni tija kwa wakulima wa Kongwa ili kuongeza idadi ya mafuta nchini ambayo yatasababisha Serikali iache kumaliza Fedha nyingi kuagiza nje ya Nchi lakini kupitia kilimo hicho pia wananchi waweze kufaidika kiuchumi
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mh Deo Ndejembi akizungumza na wakulima wa zao la Alizeti na maafisa ugani wa Wilaya hiyo katika kikao cha pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa akiwa katika kikao cha pamoja na wakulima wa Alizeti na maafisa ugani wa Wilaya hiyo katika semina maalumu ya kutoa elimu ya jinsi gani wakulima hao wanaweza kuchangamkia fursa za zao hilo

TPA YAKABIDHI MASHINE MBILI KWA AJILI YA KUHIFADHI WATOTO NJITI KWENYE HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO ZENYE THAMANI YA MILIONI 25

0
0
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mashine mbili za incubator kwa ajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga vilivyotolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo akifuatiwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Abdiely Makange
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Witonde Philipo akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese 
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Abdiely Makange akizungumza wakati wa hafla hiyo
Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese akizungumza wakati wa halfa hiyo
PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Sehemu ya msaada wa vifaa vilivyokabidhiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga
Sehemu ya msaada wa vifaa vilivyokabidhiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ajili ya kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga
Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakiwa kwenye halfa hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese wakati alipowasili kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya kupokea msaada mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga. uliotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo




MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.

Akikabidhi msaada huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa imetenga bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya elimu na afya.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Witonde alisema kwamba wao wanashukuru kupewa nafasi ya kujumuika kwenye mkoa wa Tanga kusaidia kuboresha maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Alisema kwamba walipata maombi ya kuwepo kwa changamoto hizo na wao wakaona wafanye jambo hilo hivyo wanaimani uongozi wa mkoa huu ungeweza kupata watu wengine lakini wakawaona wao.

Mhandisi Witonde alisema kwamba mamlaka hiyo imekuwa na utaratibu kila mwaka kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia jamii kwenye ameneo ya afya, elimu na maeneo mengine ya kijamii.

Alisema katika mwaka wa fedha walipanga kutumia kiasi cha milioni 50 kutoa huduma hizo huku akieleza kwamba vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto.

“Kabla ya zoezi hili siku chache tulikwisha kukabidhi mabati 378 shule ya sekondari Tanga School yenye thamani ya milioni 15 na yamekarabati nyumba tano lakini pia tutaendelea kuona namna ya kuwasaidia kwa kadiri mungu atakavyowajalia”Alisema 

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwashukuru TPA kwa kutenga fedha hizo milioni 50 kwenye mwaka wa fedha na kuwezesha kwenye katika mkoa wetu kuleta vifaa hvyo ambavyo vitakuwa ni chachu kuwasaidia kuboresha sekta ya afya.

Alisema kwani kutenga fedha ni jambo moja na kufanikisha ni jambo la pili hivyo niwapongeze TPA kwa kutekeleza wale walioyapanga na kuhaidi
“Nimshukuru MKurugenzi Mkuu wa TPA kwani Tanga imekuwa ni nyumbani kwenu kuja mara kwa mara na kuweza kuwasaidia tunatambua jitihada kubwa mnazofanya katika kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla”Alisema

Alisema wanatambua jitihada kubwa mnazofanya TPA kuhakikisha mnasaidia jamii na watanzania kwa ujumla ukiacha suala la kusimamia mapato na kujenga mazingira mazuri ya kuwa lango kuu la kibiashara kati ya nchi yetu na jirahi bandari imekuwa ni msaada kuwasaidia shughuli mbalimbali za kijamii na maelezo yako ulioyayatoa yanadhihiridha

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa huo, Abdiel Makange, amesema mashine hizo zitaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto njiti ambao wanazaliwa katika hospitali hiyo.

“Hospitali ilikuwa ina mashine mbili tayari, hivyo uwepo wa nyingine za ziada kutawezesha kupunguza changamoto ya vifo kwa watoto hao” amesema.

TAARIFA YA KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE

Waziri Simbachawene apiga stop vifungashio vya Plastiki

0
0
*Ataka wafanyabiashara wafuate sheria

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

Serikali imesema kuwa sheria ya zuio ya mifuko ya Plastiki itekelezwe kwa wafanyabiashara kwa kuacha kuuza vifungashio ambavyo ni vibebeo vya bidhaa mbalimbali.

Hayo aliyasema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene wakati alipotembelea soko la Kariakoo kwa wafanyabiashara wa mifuko waliomuomba kupata ufafanuzi wa mifuko na vifungashio katika Soko hilo jijini Dar es Salaam.

Waziri Simbachawene amesema kuwa wafanyabiashara kuacha kununua vifungashio kwa wazalishaji kutokana vifungashio hivyo havina utofauti na mifuko ya Plastiki.

Amesema sheria hata yeye inamfunga akikutwa na vifungashio hivyo ambavyo bado ni mifuko ya plastiki iliyowekewa marufuku tangu Juni Mosi mwaka huu.

Amesema vifungashio ambayo vinahitajika ni vile yenye lakiri alama na mfanyabiashara aonyeshe namna ya kufanya vifungashio hivyo kuweza kurudi mara baada ya kutumia ili kusiwepo na uharibifu wa Mazingira.

Nae Mwanasheria wa NEMC Heche Suguta amesema kuwa sheria imeshaeleza na hakuna kurudi nyuma kinachotakiwa ni utekelezaji wa sheria hiyo kwa wadau wote.

Amesema kuwa faini na vifungo vilishaelezwa hivyo mifuko ya plastiki ambayo inadaiwa vifungashio viondolewe katika mzunguko.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akionesha mifuko inayodaiwa vifungashio wakati bado inajulikana no mifuko ya Plastiki iliyopigwa marufuku kuanzia Juni Mosi Mwaka huu katika mkutano na wafanyabiashara hao jijini Dar es Salaam.Kulia ni kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Baraza laTaifa la  Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Heche Suguta.
 Mwanasheria wa NEMC Heche Suguta akizungumza namna sheria inavyotekelezeka katika marufuku ya mifuko ya Plastiki wakati walipokutana na wafanyabiashara wa mifuko katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akitoa ufafanuzi wa sheria ya mifuko ya Plastiki alipokutana na wafanyabiashara ya mifuko katika Soko dogo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akiangalia vifungashio vidavyodaiwa ni Plastiki kutokana na sheria ya marufuku ya mifuko ya Plastiki.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene akioneshwa mfuko ya kubebea taka na mfanyabiashara katika Soko dogo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Tamasha la mziki wa Rhumba festival kufanyika next Door Arena jijini Dar Agosti 30

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIST International Limited, Georgy Kytika kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha tamasha la kistaarabu lenye mahadhi ya kiafrika litakalofanyika katika ukumbi wa Next Door Arena Osterbay jijini Dar es Salaam Agosti 30 mwaka huu. Kushoto ni mzalishaji wa kampuni ya TIST, Neema Mbuya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIST International Limited, Georgy Kytika katikati, Kushoto ni mzalishaji wa kampuni ya TIST, Neema Mbuya na Meneja masoko wa kampuni ya TIST, Annie mosses wakisikiliza swali kwa mwandishi wa haari hayupo pichani.

KAMPUNI inayojishughulisha na Burudani nchini ya TIST inatarajia kufanya tamasha la kistaarabu la mziki wa Rhumba linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Next Door arena Osterbay jijini Dar es Salaam Agosti 30 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kutambulisha tamasha la Rhumba Festival jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIST International Limited, Georgy Kytika amesema kuwa siku hiyo watu wastaarabu waende wakajionee mziki wa kistaarabu wenye mahadhi ya Afrika jinsi utakavyotumbuizwa na wasanii mbalimbali wa hapa nchini wakiongozwa na SAUTI SOL kutoka nchini Kenya.

Amesema kuwa "Onesho la tamasha hilo ambalo litakuwa la kihistoria hapa nchini pia kutakuwa na utambulisho aina nyingine ya burudani ambapo mtanzania usiwaze kukosa katika tamasha hilo la Rhumba".

Amesema kuwa mziki utakuwa wakistaarabu watu waende wamependeza na suti zao kwani Burudani itakuwa ya kistaarabu na yenye kufurahisha kwa watakaohudhuria.

Kiingilio katika tamasha hilo Kyatika amesema kuwa itakuwa VIP shilingi 50,000/= na VVIP ni shilingi 100,000/=.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images