Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Timu ya Tanzania Mashindano ya All African Games Yakabidhiwa Bendera ya Taifa

0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco, Gabriel Geay wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akimvalisha bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco, Gabriel Geay wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wachezaji watakaoshiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco katika mchezo wa judo na riadha wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco (hawapo pichani) wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini, Gulam Abdalla Rashid na kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco (hawapo pichani) wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo, Addo Komba na kushoto ni Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini (TOC), Gulam Abdalla Rashid.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

Mbunge, wananchi wachangia damu majeruhi wa moto Muhimbili

0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega pamoja na wananchi wa Jimbo la Mkuranga wakichangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Bi. Wema Msafiri akiwashauri wananchi wa Jimbo la Mkuranga kabla ya kuanza shughuli ya kuchangia damu.
Wananchi wa Jimbo la Mkuranga wakisikiliza maelekezo kabla ya kuchangia damu leo.
Mmoja wa wakazi wa Mkuranga akichukuliwa vipimo na mtaalam wa MNH.
Baadhi ya vijana wakiwa katika foleni ya kufanya vipimo mbalimbali kabla ya kuchangia damu hospitalini hapa.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wakazi wa Mkuranga katika eneo la MNH.
Vijana wakisubiri kufanyiwa vipimo kabla ya kuchangia damu leo.



Na John Stephen

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega pamoja na wananchi wa Jimbo la Mkuranga wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuchangia damu kwa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro Jumamosi iliyopita.

Akizungumza wakati akichangia damu, Mhe. Ulega amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa kuwa kiasi kikubwa cha damu kinahitajika kwa majeruhi hao pamoja na wagonjwa wengine wenye uhitaji.

Mhe. Ulega ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga amesema kuwa amefika MNH pamoja na zaidi ya wananchi 50 kwa ajili ya kuchangia damu majeruhi hao ambao wamelazwa katika wodi mbalimbali.

“Tupo hapa kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi waliopata ajali ya moto, lakini pia tunamuunga mkono Rais wetu aliyekuwa wa kwanza kufika hapa Muhimbili lakini pia alimuagiza Waziri Mkuu, mh. Kassim Majaliwa kushiriki msiba kwa siku tatu mfufulizo, hivyo sisi hatuna namna zaidi ya kuunga mkono jitihada za viongozi wetu,” amesema Mhe. Ulega.

Mhe. Ulega amewataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kuchangia damu kwa kuwa hospitali nyingi nchini zina upungufu wa damu hivyo watu wajitokeze ili kuokoa maisha ya majeruhi wanaopata ajali .

Juzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Magufuli alitembelea majeruhi wa ajali ya moto waliolazwa MNH na kuahidi kulipa gharama zote za matibabu, dawa na chakula kwa majeruhi wote.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

WACHONGA VINYAGO NA WACHORAJ WACHANGAMKIA FURSA MKUTANO WA SADC.

0
0
Wafanyabiashara ndogondogo na wachonga  Vinyago na Wachoraji wa picha mbalimbali wanaouza bidhaa zao kwa wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),katika  eneo la barabara ya chuo cha IFM, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, wakipanga biashara zao tayari kuwasubiri wateja.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)





MAVETERANI YANGA NA SIMBA KUNOGESHA TAMASHA LA MTAA KWA MTAA

0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAVETERANI wa timu za Yanga na Simba wanatarajia kunogesha Tamasha la Mtaa kwa Mtaa litakalofanyika Mkoani Lindi kwa kucheza Mchezo wa Kirafiki.

Tamasha hilo limeandaliwa na Mashujaa Fm ya Mkoani humo litawashirikisha wachezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba waliocheza miaka ya nyuma.

Akizungumzia Tamasha hilo, Mkurugenzi wa Masoko Maxmilian Luhanga amesema tamasha la mtaa kwa mtaa limehusisha timu za mpira wa miguu zaidi ya 100 kutoka vitongoji vyote vya mkoa wa Lindi.

Amesema, timu zimeshafikia hatua ya fainali na siku ya Jumapili Agosti 18 mwaka huu itapigwa mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

“Timu takribani 100 zimeshiriki, na fainali itakuwa ni tarehe 18 mwezi huu ila kabla ya mchezo huo kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya wachezaji wa zamani wa Yanga na Simba utakaopigwa Agosti 17, “ amesema.

Luhanga ameeleza kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubww, kikubwa amewaomba mashabiki wa mpira wa miguu mkoani Lindi kuja kuwashuhudia wachezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba pamoja na mechi ya Fainali itakayopogwa kesho yake.

Kwa upande wa wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘machinga’ amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanamfunga mtani wao Simba kwenye mchezo huo wakitaka kulipa kisasi kwa kufungwa kwenye mechi ya bonanza la Serebuka hivi karibuni.

Naye Thomas Kipese mchezaji wa zamani wa Simba amesema kuwa watani zao Yanga wanawafahamu vizuri tu na hata miaka ambayo wakiwa wanacheza waliwafunga ila katika mchezo huo wanataka kuendeleza historia yao ya kushinda kama kwenye mchezo uliopita.

Mshindi wa kwanza wa mechi hiyo ya fainali atapata gari aina ya Noah.
Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Fm Maxmilian Luhanga akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kirafiki wa maveterani wa Yanga na Simba pamoja na fainali ya tamasha la Mtaa kwa mtaa linalofikia tamati Agosti 18 Mkoani Lindi.
Wachezaji wa Zamani wa Yanga na Simba wakiwa kwenye picha ya pamoja pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Fm Maxmilian Luhanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar
Mchezaji wa Simba wa zamani Thomas Kipese akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga utakaofanyika Agosti 17 Mkoani Lindi
Mchezaji wa Yanga wa zamani Mohamed Hussein ‘Machinga’ akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya watani wao wajadi Simba utakaofanyika Agosti 17 Mkoani Lindi.

Muhimbili yashirikiana na Mkemia Mkuu kutambua ndugu wa majeruhi

0
0
Na Sophia Mtakasimba

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali wanaendesha zoezi la kuwapima vinasaba majeruhi ambao hawajitambui wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro ili kubaini ndugu zao halisi.

Katika taarifa aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa hospitalini hapo Bw.Aminiel Aligaesha alisema kuwa awali hospitali ilitoa wito wa ndugu kujitokeza kutambua majeruhi, lakini walijitokeza ndugu zaidi ya mmoja kwa majeruhi mmoja.

“Hii imeleta mkanganyiko hivyo tumeona tushirikiane na wenzetu wa Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili wachukue vinasaba vya wagonjwa na kulinganisha na ndugu waojitokeza ili kuhakikisha kwamba zoezi hili haliingii dosari,” alisema Bw.Aligaesha .

Kuhusu hali za majeruhi wa moto Bw. Aligaesha alisema kuwa kati ya majeruhi 46 waliopokelewa, 8 wamefariki dunia, 13 wapo katika wodi ya mahitaji maalumu na hawajitambui, 25 wanajitambua na wapo katika wodi za kawaida ambapo madaktari na wauguzi wanaendelea kuwapa huduma nzuri ya daraja la kwanza.

Akifafanua aina ya ndugu wanaohitaji kuchukuliwa vinasaba kwa ajili ya utambuzi Meneja wa Maabara ya Vinasaba kutoka Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bi. Hadija Said Mwema alisema ndugu wanaohitajika kulinganishwa vinasaba kwa urahisi ni wazazi wawili au watoto wa majeruhi. 

“Kwa wale ambao kwa bahati mbaya wazazi walishatangulia na hawakubahatika kuwa na watoto hapo sasa tutaomba ndugu wa karibu kwa mfano Kaka, Dada au Baba mdogo, lakini kitaalamu ningependa wananchi wafahamu kwamba urahisi wa ulinganifu ni kwa ndugu wa karibu,” alisema Bi. Hadija.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Bw.Aminiel Aligaesha akiongea na waandishi wa habari kuhusu utambuzi wa ndugu wa majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Kulia ni Meneja wa Maabara ya Vinasaba, Bi.Hadija Said Mwema kutoka Mamlaka ya Mkemia mkuu wa Serikali.

KIONGOZI MSAADA WA PICHA ZA SHEIKH MKUU WA TANZANIA

0
0
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Aboubakar Zubeiry bin Ally akifanya Dua fupi ya kuwaombea majeruhi waliolazwa wodini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na majeraha waliopata katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Muhimbili, Bw. Yassin Munguatosha. Sheikh Mkuuametembelea majeruhi wa ajali ya moto na kuwapa pole na kuwaombea Dua ili mwenyezi Mungu awape wepesi wa kupona haraka.
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Aboubakar Zubeiry bin Ally akielekea katika wodi walikolazwa majeruhi wa moto katika Hospitali ya Muhimbili.
Sheikh Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaidizi wake pamoja na wataalam wa Muhimbili baada ya kutembelea majeruhi wa ajali ya moto.

FORMER PRESIDENT BENJAMIN WILLIAM MKAPA KEYNOTE SPEAKER AT PUBLIC LECTURE ON DEEPENING INTERGRATION IN SADC TOMORROW AT UDSM

STATEMENT ON ISSUES RAISED BY THE EAST AFRICAN NEWSPAPER OF 10TH 16TH AUGUST, 2019

0
0
cid:4ebc9837-d38d-42fa-ae49-c60d14275b56
EAC Secretariat

Our attention has been drawn to issues raised in a story by The East African Newspaper edition of 10th – 16th August 2019 headlined “EAC Staff desert stations over pay.” At the outset, I wish to clarify that this is a newspaper that we have a lot of respect for at the Community. However, there were glaring errors of fact and accuracy in the article. We wish to clarify the issues raised by the paper as follows:

1.     Alleged Desertion by Staff of their Duty Stations due to non-payment of salaries

We can confirm that staff salaries for all EAC Organs and Institutions for the month of July 2019 have been fully paid. 

On the issue of some members of staff being out of duty station, we wish to clarify that in accordance with Article 71 of The Treaty, EAC Programmes and Projects are coordinated by the EAC Secretariat with staff undertaking official missions within the Partner States. Judges of the East African Court of Justice and the Members of the East African Legislative Assembly come to Arusha as and when there is the business to be transacted as per the respective Organ’s approved Calendar of Activities.

Staff who are out of the station are either on annual leave or on official duties in the Partner States. Out of the 400 members of staff at the three EAC Organs based in Arusha, 14 are on annual leave, one is on maternity leave, while 11 are on official missions in the Partner States. It is therefore not true that some members of staff have moved back to their home countries due to non-payment of salaries. Contrary to the claims by The East African, the entire Community is operating normally with all staff of Organs and Institutions on duty.

2.     Delay by the Partner States in remitting their annual contributions to the Community

We wish to clarify that the EAC normally starts receiving disbursements from the Partner States from the month of August each financial year. This is occasioned by the budgeting processes such as debates in the National Assemblies and approvals for disbursements in the Partner States which in some cases takes up to three months after the commencement of the Financial Year.

At the start of every Financial Year, the Community usually experiences liquidity challenges as it awaits the finalization of the budget approval processes by the Partner States which dictates the disbursement of funds to the EAC through the Ministries responsible for EAC Affairs.  

Partner States are expected to make their respective disbursements after the finalization of their national budget approval processes. Further to this, the EAC Financial Rules and Regulations require that the Partner States should have disbursed the total financial year contribution by the end of the 2nd Quarter of the Financial Year (31st December every year). 

3.     The Community is on track towards attaining its vision of an integrated East Africa

The EAC Partner States with the foresightedness of the Heads of State are fully committed to the success of the regional integration agenda. The 19th Summit of the EAC Heads of State held in Kampala, Uganda on 23rd February 2019 deliberated on the status of the EAC integration and directed the Council of Ministers to take appropriate measures to: fully implement the Single Customs Territory; fast-track full implementation of the Common Market Protocol; fast-track implementation of the Monetary Union, and; make preparations for the drafting of the Constitution of the EAC Political Confederation as a transitional model to the Political Federation. The commitment of the Heads of State has enabled the EAC to attain several achievements including:

a)     good political will and climate within the EAC region;

                                      i.        the EAC regularly holds key statutory meetings of her governance Organs. The Heads of State Summit meets twice in a year, the Council of Ministers meets on a quarterly basis to give policy guidance, Sector-Specific Sectoral Councils meet twice a year.        at the bilateral level, Heads of State within the region meet to commission and launch regional projects e.g. the One Stop Border Posts, roads and railways, ports, energy, health, etc.
                                    iii.        joint cooperation initiatives in defence, small and micro enterprises (SMEs); arts and culture; sports; East African International e-passport; EAC One Area Mobile Network, etc.

b)    the continued financial support from Partner States –despite the financial challenges faced by each Partner State, Partner States have continued to fulfill their financial obligations to the EAC;

c)     continued collaboration and support from various Development Partners across all the four pillars of the integration process.

d)    the strides taken in attaining the four pillars of the integration process, namely Customs Union, Common Market, Monetary Union and Political Federation;

                                      i.        Customs Union – EAC is now a Single Customs Territory, 15 One Stop Border Posts operationalized, Authorised Economic Operator, Time-bound removal of Non-tariff Barriers, leading in the implementation of the EAC-COMESA-SADC Tripartite Free Trade Area in addition to the African Continental Free Trade Area (AfCFTA)
                                     ii.        Common Market – health projects, education, food security, international e-passport, Mutual Recognition Agreements, Single Tourist Visa, promotion of cultural industries, trade in services
                                    iii.        Monetary Union – enactment of two regional laws to support the establishment of institutions to implement the Monetary Union by 2024 (East African Monetary Institute and East African Statistics Bureau), Financial Sector Development and Regionalization, Payments and Settlements Systems Infrastructure in the Partner States ongoing in all Partner States
                                    iv.        Political Federation – the EAC is in the process of drafting a constitution for the EAC Political Confederation as a transitional model to the Political Federation. The 20th Summit of the EAC Heads of State held on 1st February, 2019 in Arusha, Tanzania appointed 12 Constitutional Lawyers (three from each Partner State) to draft the constitution for the EAC Political Confederation within a period of six (6) months. The Committee of Experts to draft the Constitutions for the Political Confederation will be launched in Kampala, Uganda on 19th August, 2019 by President Yoweri Museveni. The Summit further directed the Council of Ministers to report back to 21st Summit of Heads of State. 

e)     growth of EAC to accommodate an expanded mandate – establishment of new institutions and Centres of Excellence e.g. the East African Health Research Commission, East African Science and Technology Commission, EAC Competition Authority, East African Kiswahili Commission, East African Centre for Renewable Energy and Energy Efficiency, among other institutions.
It is because of these many achievements that the EAC has been rated as the best performing regional economic bloc in Africa by the African Development Bank (2018) and the UN Economic Commission for Africa (2017).

The strides and successes the EAC has achieved over the years will be celebrated during the Community’s 20th anniversary which will be marked on the 30th November, 2019 under the theme EAC @ 20: Deepening

Integration; Widening Cooperation.

The EAC therefore holds an indispensable and critical position in leading the region to attain the Community’s Vision 2050, the UN Sustainable Development Goals and the African Union Agenda 2063. Hence, the EAC will continue to lead the integration agenda in Africa.

The EAC integration process as enshrined in the Treaty is therefore on track.


Eng. Steven Mlote, DSG
For: The Secretary General      


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela atatua mgogoro wa shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa na akiwa amezungukwa na wanafamilia pamoja na mashahidi waliohudhuria kutatua mgogoro huo. 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa familia ya mzee Mwenda iliyopo katika kata ya Nduli uliodumu kwa miaka mingi kutokana na kaka yao Ayubu Mwenda kwenda tofauti na wanafamilia wengine.

Akizungumza kwenye shamba la familia marehemu mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa kaka yao Ayubu Mwenda na wanafamilia wote kwa pamoja wamekaa na kufikia makubariano ya kugawana sawa ardhi ambayo ipo katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli.

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.

Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.

“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MBURAHATI

0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na wakazi wa Kata ya Mburahati, Kigogo jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Kata hiyo kwa lengo la kujua changamoto wanazokutananazo pamoja na namna wanavyoshirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia uhalifu na wahalifu katika maeneo yao wanayoishi.
Picha na Jeshi la Polisi.

WIMBO MAALUMU WA SADC 2019 NA TANZANIA ALL STARS

Timu ya Tanzania Mashindano ya Jumuiya ya Madola Yakabidhiwa Bendera ya Taifa

0
0
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji  wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco (hawapo pichani) wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini, Gulam Abdalla Rashid na kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo  akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji  wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wachezaji  wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco (hawapo pichani) wakati wa kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo, Addo Komba na kushoto ni Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini (TOC), Gulam Abdalla Rashid.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco, Gabriel Geay wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akimvalisha  bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco, Gabriel Geay wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wachezaji watakaoshiriki mashindano ya All African Games nchini Morocco katika mchezo wa judo na riadha wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

WADAU WA LISHE WATAKIWA KUTOMEZA TATIZO LA UDUMAVU

0
0
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha.
Wadau wa Masuala lishe wakiwemo wazalishaji na wasindikaji wanaoongeza thamani  bidhaa za lishe wametakiwa kushiriki katika kutokomeza tatizo la udumavu nchini ambalo linawakabili watoto wengi hasa waishio maeneo ya vijijini.
Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la Infoy Laurent ,Sabuni alisema hayo  katika maonyesho ya bidhaa za lishe yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo la Sido mkoa wa Arusha  ,ambapo alisisitiza kuwa wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za lishe wanapaswa kushiriki kutatua matatizo ya lishe duni katika jamii na kuhakikisha kuwa wanazifikisha bidhaa hizo vijijini.
Sabuni alisema kuwa wamekua wakitoa mafunzo kwa wasindikaji wa bidhaa za lishe  juu ya namna bora ya kusindika na kuzifungasha ili ziweze kuwafikia wateja na kusaidia kupunguza tatizo la udumavu  linalowakabili watoto wengi licha ya uzalishaji wa nafaka ulioko.
Meneja wa Sido mkoa wa Arusha Nina Nchimbi aliwataka wasindikaji  watengeneza unga wenye virutubisho na viini lishe ili kukidhi afya ya mlaji   na kuhakikisha suala la viwango vya ubora  katika  bidhaa za lishe  wanazozalisha unazingatiwa.
Nina alisema kuwa Sido imefanya juhudi za kuwaunganisha wajasiriamali hao na taasisi za ubora ikiwemo TBS,TFDA ili bidhaa zao ziweze kuthibitishwa ubora na kupata masoko ya kitaifa na kimataifa.
Kwa upande wao Wasindikaji na Wajasiriamali wa bidhaa za lishe Dorice Assenga na Walter David  wameeleza kuwa wamekua wakitoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya unga wa lishe kwa watoto wadogo na kuzipeleka bidhaa za maeneo ya pembezeni na vijijini ambako kuna hitaji kubwa la lishe ili kuwasaidia kinamama  wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Mtaalamu wa Lishe Prisca Mwakalasi alisema kuwa mchango wa wadau wa lishe ni mkubwa kwani madhara ya udumavu huonekana hasa mtoto anapokua na kuwa mtu mzima inakua vigumu kufanya maamuzi sahihi kwani anakua amedumaa hadi akili hivyo masuala ya lishe kwa watoto na watu wazima yanapaswa yapewe kipaumbele kwani lishe ni kiini cha maendeleo
Msindikaji wa Bidhaa za Lishe Dorice Assenga akifafanua juu ya virutubisho na viini lishe vinavyopatikana katika unga wa lishe kwa Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY ,Laurent Sabuni katika maonyesho ya bidhaa za lishe jijini Arusha.Picha na Woinde Shizza 

WIMBO WA SADC SUMMIT 2019 TANZANIA BA DOKII WENCESLAUS

Wahadhiri, Wanafunzi, Chuo cha Ustawi Wa Jamii waongeza nguvu Kuhudumia familia za Wahanga wa ajali ya moto Msamvu

0
0
Timu ya wahadhiri na wanafunzi wa Chuo cha ustawi wa Jamii ikiongozwa na Mkuu wa taasisi hiyo Dkt. Joyce Nyoni wapo mkoani Morogoro kuanzia leo tarehe 13/08/2019 kuungana na timu ya maafa ya Mkoa wa Morogoro kutoa huduma za unasihi na huduma nyingine za awali za kisaikolojia kwa kuanzia na utambuzi wa mahitaji ya kisaikolojia ya wanafamilia hao.

Kwa kushirikiana na wataalamu wengine waliopo katika timu hiyo, Chuo cha Ustawi wa Jamii kitashiriki katika kupanga huduma na utekelezaji wa mpango wa huduma kwa familia hizo.

Katika kufanikisha zoezi hili timu ya maafisa ustawi inafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na serikali za mitaa kuhakikisha kila kaya iliyofikwa na msiba au kupata majeruhi ya ajali hii mbaya ya moto zinatambuliwa mahitaji yao ya kisaikolojia na kupata huduma stahiki.
Mhadhiri msaidizi wa Chuo cha ustawi wa Jamii Abigail Kiwelu kutoka idara ya taaluma ya ustawi wa jamii na Afisa ustawi wa Jamii Subisya Kabuje kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi (wenye makaratasi) wakizungumza na mama mzazi (wa kwanza kushoto) na dada (wa pili kushoto) wa mmoja wa wahanga aliyepoteza maisha kwenye ajali ya moto msamvu.

15 CYCLISTS ON EAC BICYCLE TOUR FLAGGED OFF IN ARUSHA

0
0



EAC Secretariat

 A group of 15 cyclists who are participating in the 3rd East African Community Bicycle Tour (Tour d’EAC) were today flagged off at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

Flagging off the group of volunteer cyclists, the EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote, hailed the cyclists for their efforts in complementing initiatives by the Secretariat to create awareness on the integration process.

Eng. Mlote noted that it was encouraging that the annual initiative which started with cyclists from Uganda only in 2016, had now expanded to include cyclists from Burundi, Kenya, Rwanda and Tanzania.

He urged the cyclists to mobilize more youth in the region to appreciate the importance of regional integration as a way of empowering East Africans and making East Africa united and stronger.

The DSG said that the movement of the cyclists across the region had been made possible by the free of movement of persons as enshrined in the EAC Common Market Protocol.

Eng. Mlote assured East Africans that the Community was growing stronger with each passing day, adding that it had recorded many achievements which were gradually beginning to trickle down to ordinary East Africans.

In her remarks, Ms. Joyce Kevin Abalo from the GIZ Office at the EAC Headquarters, assured the cyclists that the German Technical Cooperation would continue working closely with the EAC Secretariat to ensure that the event was a success.

Ms. Abalo urged the cyclists to endeavour to complete the journey noting that success can only be attained through discipline and perseverance.

Speaking at the event, the Coordinator of the Tour D’EAC, Mr. John Balongo, requested the EAC Secretariat to include the tour in its Calendar of Activities in the future.

“We also want to request that in future events, all ministries support individual cyclists from their respective countries,” said Balongo, adding that the group’s aim was to educate EAC citizens on the importance of a united East Africa.

“We seek to stir up interest of groups and individuals in the understanding of the land, and people of East Africa. Subsequently, this results into growing personal and group relationships across the region multiplying out into travel, trade and many other beneficial linkages,” he said.

Also present at the event was the EAC Director General, Customs and Trade, Mr. Kenneth Bagamuhunda.

The 3rd Tour d’EAC was flagged off on 1st August, 2019 at the Independence Monument in Kampala by Uganda’s Deputy Prime Minister and Minister for EAC Affairs, Hon. Dr. Ali Kirunda Kivejinja, and the Tanzanian High Commissioner to Uganda, H.E. Aziz Ponary Mlima. The cyclists arrived in Nairobi on the evening of Wednesday, 7th August, 2019 where they were hosted by the Ministry of EAC and Regional Development in Kenya one day later. 

 The Tour d’EAC 2019 is expected to cover 4,300 km around East Africa over a period of 50 days. The aim of the Annual East African Bicycle Tour is to promote the spirit of East Africanness among the people of East Africa, the tourism and business potential of the Community while enhancing awareness about the social and cultural peculiarities of people and places in the EAC.

The ultimate goal of the initiative is to bring the citizens of East Africa to own the integration process as enshrined in the Treaty for the Establishment of the EAC. The tour is also one of the activities to mark the Community’s 20th Anniversary.
 EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote (right), flags off the cyclists at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. Standing third right is the Director General, Customs and Trade, Mr. Kenneth Bagamuhunda.
  Some of the cyclists after they were flagged off at the EAC Headquarters in Arusha.
EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Eng. Steven Mlote (right), Mr. John Balongo (Coordinator Tour d’EAC), Mr. Kenneth Bagamuhunda (centre) and Ms. Joyce Kevin Abalo (second left) after the DSG flagged off the cyclists in Arusha.


MKURUGENZI TRC AELEZEA UMUHIMU WA SEKTA YA USAFIRISHAJI WA RELI KATIKA NCHI ZA SADC

WAZIRI WA NISHATI DKT. KALEMANI ATAJA MIKAKATI YA KUUPELEKA UMEME WA TANZANIA NCHI ZA SADC

0
0


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

Dk.Kalemani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

Akifafanua zaidi ,Waziri Kalemani amesema kuwa katika eneo la nishati ya umeme kuna mambo manne makubwa na kwamba jambo la kwanza kama nchi ni kujihakikishia kuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuleta maendeleo kupitia uchumi wa viwanda.Mbili umeme unaotabirika, tatu wa uhakika na nne wa bei nauu.

"Kwa sasa upande wa Tanzania kuna mambo matatu likiwemo la makubaliano ya nchi za SADC kwamba kila nchi ijenge miundombinu ya umeme ambayo itaunganisha kati ya nchi na nchi. Kama nchi kwa upande wetu Tanzania tumeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha lakini wakati huo huo tumeangalia na malengo ya nchi za SADC na katika eneo hilo tumeweka majukumu ya kuzalisha umeme megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025,"amesema Waziri Kalemani.

Amefafanua katika kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuuza kwa nchi za jumuiya hiyo Serikali imeweka mkakati wa kutumia umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi asili na umeme unatokana na maji."Katika eneo la gesi asilia pamoja na gesi iliyopo , pia tunaendelea kuvumbua gesi na tunazo futi za ujazo trilioni 57 .54 na kati hizo futi za ujazo trilioni 8.8 zitatumika kuzalisha umeme.

" Pia kuna chanzo cha maji na kupitia utafiti ambao umefanyika kwa miaka mitano imeonekana tunaweza kuzalisha mpaka megwati 4,000 na tayari tumeanza na maporomoko ya mto Rufiji ambapo tutatalisha mgewati 2,115.Mradi wa umeme wa maporomoko ya Mto Rufiji ni wa kwanza na wa kihistoria kwa ukubwa nchini Tanzania, ni bwawa la kwanza la kuzalisha umeme Afrika Mashariki, ni bwawa la nne kwa Bara la Afrika na kwa dunia ni kati ya mabwawa 70 makubwa ya kuzalisha umeme mwingi,"amesema Dk.Kaleman.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mara ya kwanza katika nchi za SADC zimeingia kwenye historia ya kuwa na mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme."Tumeanza na mradi huu wa umeme wa maporomoko ya bonde la mto Rufiji kwasababu tunakwenda kuleta mambo manne ambayo ni ya umeme wa umeme, unaotosheleza, unbaotabirika na gharama nafuu,".

Amefafanua kuwa sehemu ya pili ni kwamba unapokuwa na umeme wa kutosha na gharama na fuu unaweza kusambaza sehemu nyingi na kwa gharama nafuu, hivyo mkakati ulipo ni kujenga miundombinu ya kuusafirisha .

"Kwa sasa katika nchi yetu tunajenga miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kona zote nne za nchi yetu.Tunafahamu ajenda hapa ni kuzalisha umeme wa uhakika na kusambaza, hivyo ni muhimu kujenga miundomboni ya kusambaza umeme huo,"amesema Dk.Kalemani huku akitaja baadhi ya kona hizo ni ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Kaskanini.

Wakati kona ya pili amesema ni kuutoa umeme kutoka Iringa, Mbeya, Sumbawanga, Kigoma mpaka Nyakanazi.Pia amesema kuna mradi wa umeme wa kilovoti 400 ambao unatoka Mkoa wa Iringa kwenda Mbeya ambao unaweza kwenda mpaka nchini Malawi na tayari wamepata fedha kutoka Benki ya Dunia."Makubaliano ya nchi za SADC ni kuuziana umeme kulingaa na mahitaji".

Amesisitiza kuna mkakati wa mradi wa kusafirisha umeme kati ya Zambia ,Tanzania na Kenya na tayari umeshaanza. "Na huu mradi ni muhimu katika kuunganisha umeme kwa nchi za SADC, hivyo mradi wa umeme bonde la Rufuji unatakapokamilika tutauuza kwa nchi nyingine za jumuiya ikiwemo nchi ya Malawi,Zambia na Congo DRC".

Hata hivyo amefafanua kukiwa na umeme wa kutosha maana yake maeneo mengi ya vijiji yatakuwa na umeme wa uhakika na hivyo kutaisaidia kupunguza uharibifu wa mazingira huku akieleza kuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha nishati ya umeme na gesi asili inatumika katika maeneo yote nchini.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa nchi za SADC kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya kuunganisha umeme kwenye maeneo ya vijiji ili kuondoa changamoto ya uharibifu wa mazingira.

WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.

Kalemani ameeleza kwa kina mkakati wa Serikali ya Tanzania kuhusu namna ambavyo imejipanga kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha, uhakika , gharama nafuu na unaotabirika huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kina namna ambavyo wamejipanga kuuza umeme kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani akisalimiana na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya SADC,Dkt . Stragomena Tax kabla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC
WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiyasoma baadhi ya majarida kabla uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC 

 WAZIRI wa Nishati Dk.Medard Kalemani (kulia) akimsikiliza wakati akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kabla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwemo wanahabari wakiwa ukumbini humo kushuhudia uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC .Picha na Michuzi JR.

KITUO CHA AFYA KEREGE CHAHITAJI GENERETA ,ILI KUKABILIANA NA TATIZO LA UMEME WA DHARURA WAKATI WA UPASUAJI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

KITUO kipya cha afya Kerege ,Bagamoyo, mkoani Pwani ,kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme mbadala hali inayosababisha hofu endapo itatokea umeme kukatika ghafla huku upasuaji mkubwa ukiwa unafanyika.

Kutokana na hali hiyo ,kunahitajika genereta ama solar ambalo litasaidia wakati itatokea dharula ya kukatika umeme.

Aidha ,kituo hicho kinakabiliwa pia na changamoto nyingine ya upungufu wa watumishi 19,kuongeza jengo la mama na mtoto,exray,uzio, na nyumba za watumishi.

Akitoa taarifa kwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo, alhaj Shukuru Kawambwa, wakati alipotembelea kituo hicho na kuzungumza na watumishi na wananchi katika ziara yake ya jimbo, kaimu mganga mfawidhi dkt.Asha Chanyeliela alisema, kwasasa wameshaanza kutoa huduma za upasuaji na kinalenga kuhudumia watu 8,921,tangu kituo kianze wazazi 400 wamejifungua kati yao 32 wamefanyiwa upasuaji.

Alieleza, wanashirikiana na shirika la umeme Tanesco ,wakati ikitokea umeme kukatika huku wakifanya upasuaji na wanashukuru haijawahi kutokea madhara ikitokea dharura ya aina hiyo.

"Umeme wa dharura utatusaidia,tupate genereta ama solar maana hadi sasa haijawahi kutokea madhara ,wakati umeme ukitokea na wakati huo huo ukifanyika upasuaji ,ila bora ya kinga kabla ya madhara"

Akizungumzia kuhusu watumishi ,Asha alisema ,wapo 20 mahitaji 39 na pungufu ni watumishi 19 ili kukidhi mahitaji.Nae ,alhaj Kawambwa alisema, ujenzi wa kituo cha afya kerege ulianza tarehe 20/10/2017 na lengo kuu la mradi likiwa ni kuboresha vituo vya afya nchini na kuwa na vituo vya afya vyenye ufanisi.

Alipokea changamoto zilizotolewa na kuahidi kuzifikisha katika eneo mamlaka husika, na kubeba tatizo la upungufu wa watumishi ili waweze kuongezewa wataalamu wa afya sio tu Kerege lakini na katika vituo vya afya vingine na zahanati za Bagamoyo.

Awali diwani wa kata ya Kerege ,Saidi Ngatipura alimshukuru mbunge huyo kwa kupigania na kushiriki kusogezewa huduma za afya katika kata hiyo ambapo kwa sasa imekuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi.Katika kata hiyo, mbunge huyo alifanya mikutano ya hadhara na wananchi eno la Kitonga,Manofu,Matumbi na kwa Kiwete.

DKT. KAZUNGU AKITAKA CHUO EASTC KUWAJENGEA UWEZO MAAFISA MIPANGO NCHINI

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akipeana mkono na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Frank Mkumbo, alipowasili katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya kuangalia changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19 na namna ya kuzitatua. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akitoa maagizo kwa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), kuhakikisha wanaongeza ubunifu kwa kuandaa program za kitaaluma zenye mvuto, ili kuongeza wanafunzi na kipato na kuondoa utegemezi wa Bajeti Kuu ya Serikali.
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Frank Mkumbo, akielezea changamoto mbalimbali za chuo hicho na namna walivyojipanga kuzitatua kwa mwaka wa Fedha 2019/20, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), katika Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa masuala ya Mipango kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Msabaha Msabaha (kulia) na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Tumaini Katunzi, wakifuatilia kwa makini, mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Khatibu Kazungu na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Frank Mkumbo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akikagua miundombinu ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Frank Mkumbo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akiagana na Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Frank Mkumbo, baada ya kumaliza ziara yake katika Chuo hicho, ziara iliyoangazia kufuatilia changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19 na njia za kuzitatua kwa mwaka huu wa fedha.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

………………

Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimetakiwa kutoa mafunzo ya takwimu rasmi za Serikali kwa maafisa mipango nchini ili kuwajengea uwezo wa kufuatilia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka Mitano katika maeneo yao ya kazi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alipofanya ziara katika Chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika Chuo hicho.

Alisema kuwa mafunzo ya takwimu rasmi za Serikali yanatakiwa kutolewa kwa Maafisa Mipango kuanzia ngazi ya Serikali Kuu hadi Serikali za Mitaa ili kuwezesha kufanya tathimini ya mipango ya maendeleo na kuweka mikakati yenye tija kwa taifa hususani kwa wananchi wa hali ya chini katika kukuza kiwango chao cha maendeleo katika nyanja ya uchumi, kijamii na masuala ya sayansi na teknolojia.

“Wizara ya Fedha na Mipango inayonafasi kubwa ya kuhakikisha Chuo hiki kinajiimarisha katika Sekta ya miundombinu na kuweza kutekeleza shughuli zake vizuri kwa maendeleo ya nchi”, alieleza Dkt. Kazungu

Aidha Dkt. Kazungu, amekitaka Chuo hicho kujikita katika ubunifu kwa kubuni program mbalimbali za kitaaluma zitakazowavutia wanafunzi, jambo litakaosababisha ongezeko la wanafunzi na kuimarika kwa kipato cha Chuo, hivyo kupunguza utegemezi kwa Bajeti Kuu ya Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Frank Mkumbo, alisema kuwa kuna utofauti kati ya takwimu rasmi zinazotolewa na chuo hicho na takwimu zinazotolewa na vyuo vingine, kwa kuwa EASTC hutoa takwimu rasmi za Serikali zikiwemo za mfumuko wa bei, idadi ya watu na hata kiwango cha uzalishaji wa bidhaa nchini.

Dkt. Mkumbo, ameahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Kazungu, yakiwemo ya kutoa mafunzo kwa maafisa mipango na kuanzisha kozi zitakazo ongeza idadi ya Wanafunzi lakini pia kuendelea kushirikiana na wizara katika kutekeleza shughuli mbalimbali.

Mkuu huyo wa Chuo amesema, ziara ya Naibu Katibu Mkuu Dkt. Kazungu, katika taasisi zilizopo chini ya Wizaya ya Fedha na Mipango, kikiwemo Chuo cha EASTC imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa utaimarisha upatikanaji wa mapato na kuongeza ufanisi wa utoaji elimu.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images