Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109939 articles
Browse latest View live

MBUNGE WA TEMEKE ABDALLA MTOLEA ATOA SOMO KATIKA KIlLELE CHA SIKU YA VIJANA DUNIANI

$
0
0

MBUNGE wa Jimbo la Temeke Jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea ametoa rai kwa vijana nchini ikiwa ni katika kilele cha maadhimisho siku hii ya vijana ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Agosti 12 kila mwaka ambapo amewaasa vijana hao kuacha kutumika vibaya katika nyanja mbalimbali huku akiwataka waweze kujitambua na kuzitumikia nafsi zao kwa faida zao binafssi na si kutumika.

Mbunge huyo wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jana katika kongamano lililoandaliwa kwa mara ya kwanza na Taasisi Open Mind ambayo iko chini ya Mwenyekiti Abel Otieno ambaye pia ni maarufu kwa jina la 'MC Rhevan',lililowakutanisha vijana na wasajasiriamali lililofanyika katika hoteli ya Lamada Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mtolea amesema kuwa vijana wengi wamekua hawana elimu ya kujitegemea hasa katika kujiajiri na kujiwekea malengo ya kuweza kupata ajira binafsi huku akiwataka vijana kuangalia nchi inakwenda kwapi ili wasiweze kuachwa njiani huku akiwataka vijana wajifunze kutenda mambo kwa viyendo kuliko kuwa wazungumzaji zaidi ili mwisho wa siku jamii iweze kuyaona matunda ambayo yamezalishwa na vijana wake.

"Usipojitumia kama wewe mwenyewe kijana basi wenzako waliokuzunguka watakutumia sisi wanasiasa tutakutumia na watu wengine watakutumia sababu watu wengi wanapenda kuwatumia vijana kwakuwa ndiyo kundi kubwa ambalo mtu akilitumia ataweza kufanikisha jambo lake hivyo tambueni kuwa mwisho wa siku unayoyafanya leo ndiyo utakayovuna kesho"alisema Mtolea.
 Aidha Mwenyekiti wa Taasisi ya Open Mind MC Rhevan amesema Taasisi hiyo watakua wakiandaa makongamano ya vijana ili kuweza kuamsha ari na kutoa elimu kwa vijana kila mwezi huku wakiwa wanazunguka n katika mikoa mbalimbali ambapo mwezi ujao wataanza na Jimbo la Temeke kwa kutoa elimu ya kujitambua, afya na namna matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za ujasiriamali na elimu ya uwekezaji kwa sababu vijana wengi bado hawajapata fursa ya elimu hiyo ili pindi inapotokea fursa ya kuwekeza katika nyanja yeyote ile vijana hao waweze kuchangamkia fursa hiyo baada ya kupatiwa elimu na mafunzo hayo bila bila malipo yeyote.

Baraka Jackson Bingwa Kenice 88 Pool 2019.

$
0
0
BARAKA Jackson kutoka Mkoa wa Manyara ameibuka kuwa Bingwa katika fainali za Mashindano ya Pool siku kuu ya nanenane yajulikanayo kama “Kenice 88 Pool Competitions 2019” yaliyomalizika jana jijini Dar es Salam katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyama kwa kumfunga Festo Yohana kutoka Mkoani Dodoma 7-4 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki saba(700,000/=).

Baraka alipata ushindi huo kutoka katika mkusanyiko wa wachezaji 64 kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania katika mchezo huo wa mfumo wa mchezaji mmoja mmoja (singles) ambao ni mwaka wa tano sasa ukiandaliwa na mdau wa mchezo wa Pooltable katika siku kuu nanenae kila mwaka, Michael Machela na kuratibiwa na Chama cha Pool cha Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni.

Festo Yohana(Dodoma) kwa kufungwa fainali hiyo alishika nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=).

Akizungumza na wachezaji,mashabiki pamoja na wadau wote waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni, Mathayo Mathemba aliishukuru Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya Kenice kwa kuendelea kudhamini mchezo huo na kuwaomba waendelee kuwashika mkono kwani kupitia wao wanaamini ipo siku watapata mdhamini wakuweza kuurudisha mchezo huo kwenye hadhi yake kama ulivyokua.

Mathemba alisema, Wachezaji tuigeni nidhamu ya mchezo aliyoionyesha Bingwa wa mwaka huu toka tumeanza mashindano ambaye kwa sasa yuko Kenya anaishi vizuri kwa kucheza mchezo huu nchini Kenya pamoja na kwamba familia yake iko Mkoani Manyara.

Nai Bingwa wa mashindano ya Kenice 88 Poool 2019, Baraka Jackson alimshukuru muandaaji, Michael Machela, wadhamini Kampuni ya kutengeneza meza ya Kenice, waratibu Chama cha Pool Mkoa wa Kinondoni(KIPA) pamoja na wachezaji wote waliojitokeza mwaka huu na akasema kilichomfanya mpaka apate ubingwa ni hasira ya kukosa ubingwa katika kipindi cha miaka mine yote iliyopita hivyo aliamua kwenda kuweka kambi Kenya kwa maandalizi rasmi ya ushindi alioupata alisema Baraka.

Baaraka alisema, katika mchezo wa Pool hakuna uchawi bali ni mazoezi sana na nidhamu ya mchezo ndio yatakayokufanya ufanye vizuri siku sote katika mchezo huu. 

HIVI NDIVYO WAZIRI KABUDI ALIVYOKABIDHIWA 'KIJITI' CHA UENYEKITI WA MAWAZIRI WA SADC LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Michuzi JR.

====  =====  =====  =====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti cha uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),Dkt.Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano wa baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo jijini Dar leo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
Meza kuu ikifuatilia jambo
Meza kuu ikifuatilia moja ya video maalum iliondaliwa katika mkutano huo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) akitoka nje ya Ukumbi kwa ajili ya tukio la kupiga picha. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya ukumbi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.Picha na Michuzi JR.

MABALOZI 42 KUTEMBELEA MRADI WA UFUAJI UMEME RUFIJI

$
0
0
* Nchi zote za jumuiya SADC kushiriki mkutano huo wa kihistoria

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MABALOZI 42 wanaoiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali kesho Agosti 14 watatembelea mradi wa ufuaji umeme wa Julius Nyerere Hydro power Project (JNHPP) uliopo Rufiji Mkoani Pwani ili kuweza kujionea mradi hu unaotekelezwa na serikali ili kuweza kufanya diplomasia ya kiuchumi katika mataifa wanayotuwakilisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa mabalozi hao wameitwa rasmi kushiriki mikutano ya SADC inayoendelea ambapo wanatarajiwa kuwa wenyeviti wa SADC katika mataifa wanayoiwakilisha nchi kwa muda wa mwaka mmoja na wanaamini baada ya kutembelea miradi mbalimbali ukiwepo mradi mkubwa wa kufua umeme wa Julius Nyerere Hydro power wataenda kutumia vyema kofia zao za ubalozi katika kutangaza vyema diplomasia ya uchumi wa Tanzania katika mataifa mengine hasa yale wanayotuwakilisha.

Dkt. Abbasi amesema kuwa baada ya Profesa. Palamagamba Kabudi kupokea uenyekiti wa baraza la mawaziri wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa muda wa mwaka mmoja, kesho Agosti 14, Rais wa kwanza wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini atawasili nchini kwa matukio makubwa mawili.

"Rais Ramaphosa atawasili nchini kesho jioni kwa matukio makubwa mawili kwanza atakuwa na ziara ya kitaifa kwa siku tatu ambapo pia atatembelea kituo cha wapigania uhuru kilichopo Mazimbu Mkoani Morogoro, baada ya kumaliza ziara hiyo tarehe 16 Rais Ramaphosa ataungana na wakuu wa nchi na Serikali katika mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu" ameeleza Dkt. Abbasi

Aidha amesema kuwa Agosti 15 mwaka huu Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ataongoza mhadhara wa wazi ambapo ataeleza uzoefu wake juu ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kueleza kuwa mhadhara huo ni wa wazi kabisa na kila mmoja anaweza kushiriki ili kuweza kupata uzoefu kutoka kwa mzee Mkapa.

Mkutano huo wa wakuu wa nchi, viongozi wa serikali na wafalme unatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 17 na 18 mwaka huu ambapo nchi zote wanachama zimethibitisha kushiriki mkutano huo na wawakilishi wa nchi hizo walianza kushiriki mikutano ya ndani na ile ya wiki ya nne ya viwanda ya SADC.
Msemaji mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akizungumza leo na Waandishi wa habari za mkutano wa SADC,katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijin Dar es Salaam,kuhusu uwepo wa Mabalozi 42 wanaoiwakilisha nchi katika mataifa mbalimbali kesho Agosti 14 watatembelea mradi wa ufuaji umeme wa Julius Nyerere Hydro power Project (JNHPP) uliopo Rufiji Mkoani Pwani, ili kujionea mradi huo unaotekelezwa na serikali ili kuweza kufanya diplomasia ya kiuchumi katika mataifa wanayotuwakilisha. Dkt. Abbasi amesema kuwa mabalozi hao wameitwa rasmi kushiriki mikutano ya SADC inayoendelea ambapo wanatarajiwa kuwa wenyeviti wa SADC katika mataifa wanayoiwakilisha nchi kwa muda wa mwaka mmoja

 Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa ukumbini humo.Picha na Michuzi JR.

SERIKALI YA TANZANIA YAWAPONGEZA WAANDISHI WA HABARI WANAOANDIKA MIKUTANO YA SADC

$
0
0
*Yaahidi kuwatunuku vyeti vya heshima kutambua mchango wao

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SERIKALI imesema inafurahishwa na kazi nzuri ya kizalendo inayofanywa na waandishi wa habari nchini Tanzania ambao wanaandika atika habari za mikutano ya Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrikka (SASC) na kuomba waendelee hivyo hivyo kwani sasa mikutano hiyo ndio imeanza kupamba moto.

Imesisitiza kiu kubwa ya Serikali ni kuona waandishi wa habari na vyombo vya habari vya Tanzania kwa ujumla wanaendelea kuandika habari za jumuiya hiyo zenye tija huku ikifafanua Tanzania kuwa nwenyeji wa Mkutano wa 39 wa SADC ambao utafanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu kuna faida lukuki na endelevu kwa nchi yetu.

Hayo yamesemwa leo Agosti 13,mwaka huu wa 2019 na Msemaji Mkuu wa Serkali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk.Hassan Abbasi wakati anazungumza na waandishi wa habari wanaoandika habari za SADC katika mikutano inayoendelea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kuhusu namna ambavyo waandishi wa habari wanaandika habari za jumuiya hiyo Dk.Abbasi amesema Serikali kila siku inaangalia, inatazama na inaona,hivyo imefurahishwa na kazi kubwa na nzuri ya kizalendo na kihistoria inayofanywa na waandishi wa habari na hakika wanastahili pongezi.

"Waandishi wa habari naomba nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwenu na vyombo vyenu vya habari,mnaandika habari za SADC kwa weledi mkubwa na uliojaa uzalendo kwa nchi yetu. Tunafuatilia kila siku na ninakilasabababu ya kuwaambia hadi sasa Serikali tunaridhishwa na habari mnazoandika.Kwa mujibu wa ratiba sasa ndio kasi imepamba moto kwani tuko katikati kuelekea kwenye mkutano wenyewe wa 39 wa SADC.

" Kama kuna kitu natamani ni kuona waandishi wa habari mnaendelea kuandika kwa uzalendo.Tutafurahi kama tutamaliza kama ambavyo tumeanza.Naamini kwenye uandishi wa habari unaowajibika kwa misingi ya taaluma ya habari,na mara zote kwenye mikutano yangu nimekuwa nikisisitiza hilo.Tuendelee kuandika habari kwa misingi ya uwajibikaji wenye weledi,"amesema Dk.Abbasi.

Alipoulizwa kuhusu faida ambayo nchi ya Tanzania inaipata kutokana na vikao vinavyoendelea vya Jumuiya hiyo, Dk.Abbasi amejibu kuna faida nyingi endelevu ambazo zimeanza kupatikana na zitaendelea kupatikana.

Amefafanua kuna faida ambazo zinaonekana moja kwa moja na zipo faida ambazo kila Mtanzania kwa nafasi yake anaziona na faida za jumla kwa nchi yetu."Kwenye wiki ya viwanda washiriki walipata nafasi ya kutembelea baadhi ya viwanda.

"Wamekiri na kuridhishwa na teknolojia ya hali ya juu ambayo wameiona kwenye viwanda vyetu.Ni matarajio wetu washiriki hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuielezea Tanzania yetu kwenye nchi zao na haswa tulivyojiimarisha katika eneo la viwanda.Hii faida kubwa kwa nchi yetu,"amesema.

Alipoulizwa kuhusu uhifadhi wa picha na historia ya Jumuiya ya SADC ,Dk.Abasi amejibu Tanzania inao utaratibu mzuri wa kuhifadhi picha,sauti na picha za video zinazohusu ukombozi wa Bara la Afrika na kufafanua uhifadhi huo unafanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Pia amesema Tanzania ni mwenyeji wa mradi wa kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika na makao makuu ya.mradi huo yapo hapa hapa nchini, huku akishauri Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo ambayo historia ya bara la Afrika imehifadhiwa.
 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk.Hassan Abbasi .

MWENYEKITI MPYA KAMATI BARAZA LA MAWAZIRI SADC PROFESA KABUDI ATAJA VITAKAVYOPEWA KIPAUMBELE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)Profesa Palamagamba Kabudi amesema kwamba nchi za Jumuiya hiyo zinapasaa kutumia sekta ya viwanda katika kuleta maendeleo na kuondoa umasikini.

Profesa Kabudi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,.ameyasema hayo leo Agosti 13,2019 baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo ya uenyekiti wa kamati ya baraza la mawaziri kwa nchi SADC . Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Netumbo Ndaitwah ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia.

Hivyo baada Waziri Kabudi kukabidhiwa nafasi hiyo pamoja na mambo mengine amesema nchi za SADC zinapaswa kufikia maendeleo kwa kasi, hivyo sekta ya viwanda ni njia muhimu kufikia lengo hilo na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake atakikisha sekta ya viwanda inapaswa kipaumbele.

"Nitahakikisha nashirikiana na wenzangu katika kamati na viongozi wa nchi kuchochea uanzishwaji wa viwanda kwa nchi wanachama kwani viwanda ndio chachu ya uchumi na maendeleo," almesema na Kuongeza anaamini iwapo kila nchi mwanachama itajikita kwenye uanzishaji wa viwanda na ujenzi wa miundombinu changamoto ya kiuchumi, ajira na huduma za jamii.

Aidha, amesema katika uongozi wao watapigania lugha ya kiswahili kutumika kama lugha rasmi ya SADC kwani Tanzania ina mchango mkubwa kwa jumuiya hiyo."Pia tutasimamia haki za watoto, wanawake na jamii kwa ujumla kwani hatutaki kumuacha mtu nyuma ndani ya jumuiya," amesema.

Wakati huo huowa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Ndaitwah amesema nchi wanachama ili zinufaike na SADC ni lazima zisimamie utekelezwaji wa Eneo Huru la Biashara (FRA).

Aidha amesema pia mkakati wa kiendeleza wajasiriamali na vijana ni njia muafaka ya kuchochea maendeleo ya wananchi wa nchi za SADC.Pia amesema katika mwaka mmoja wa Uenyekiti wake umekuwa wa mafanikio kwa kupata ushirikiano wa nchi zote hivyo kuwaomba wajumbe wenzake waendeleze ushirikiano kwa mwenyekiti mpya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa SADC, Dk. Stergomena Tax amesisitiza kuwa ili jumuiya iweze kuwa na tija ni lazima vijana washirikishwe kwenye maamuzi kwa kuwa ni nguzo muhimu ya uchumi na maendeleo.

SHIRIKA LA POSTA LAWATAHADHARISHA WATEJA WAKE DHIDI YA MATAPELI

TAKUKURU MKOA WA DODOMA YAOKOA ZAIDI YA MILIONI 135

$
0
0

Na EZEKIEL MTONYOLE, DODOMA.

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema kwa kipindi cha miezi sita wamefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi, Milioni 135, zilizokuwa zipotee kwa katika miradi mbalimbali.

Akizungumza na Fullshangwe Blog, mapema leo Agosti 13,2019 Ofisini kwake jijini Dodoma, amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.

“Kwa kipindi hicho pia tumefanikiwa kudhibiti zaidi ya sh.Milioni 322, na kunzia Januari hadi Juni ,2019 tumepokea jumla ya Malalamiko 231 ya vitendo vya rushwa” amesema.

Bw.Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa[TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine, huku akiitaja wilaya ya Dodoma kuongoza kwa malalamiko.

Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.

YANGA KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI KABLA YA KUWAVAA WABOTSWANA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimesafiri asubuhi ya kuelekea Nyanda za juu kaskazini Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers utakaopigwa nchini Botswana.

Akizungumza na waandishi wa habari  Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mwakalebela amesema Kikosi chao kimeamua kuweka kambi mkoani Kilimanjaro ili kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa August 23.

Amesema mazingira ya nchini Botswana yanalingana na hali ya hewa ya Kilimanjaro kwahiyo wameonelea timu ikakae huko kwa muda pamoja na kucheza mechi mbili za kirafiki.

Mwakalebela amesema, watacheza mchezo wa kwanza na Polisi Tanzania iliyopanda ligi kuu msimu huu na pia watacheza mechi ya pili na AFC Leopard ya nchini Kenya ambayo ina historia kubwa na klabu yao katika miaka ya 1970 mechi iliyofanikisha kujenga jengo la Mtaa wa Mafia.

“kuelekea kwenye mchezo wa marudiano ya timu ya Township Rollers, kikosi kitaendelea na mazoezi na pia tutacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania (August 16) na AFC Leopards (August 18),”amesema Mwakalebela.

Amesema Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ameuhakikishia uongozi kuwa wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers na watahakikisha wanapata matokeo ugenini na kufuzu raundi ya kwanza.

Katika hatua nyingine Mwakalebela amesema wamefanya mawasiliano na CAF  ili waweze kupata  leseni za wachezaji wao watatu kabla ya kwenda kwenye mchezo wa marudiano nchini Botswana

Amesema lengo la Yanga ni kuhakikisha wanakwenda Botswana wakiwa na kikosi chao kamili.

Wachezaji  waliukosa mchezo wa kwanza ni mlinda mlango Farouk Shikalo, Moustafa Suleiman na David Molinga.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

WANA CCM SINGIDA MASHARIKI WAOMBWA KUSHIRIKIANA NA KUWA WAMOJA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu (kulia),akimkabidhi funguo ya pikipiki Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mika Likapakapa aliyotoa kwa Wana CCM wa Kata ya Siuyu baada ya kumchagua Mbunge na Diwani kupitia chama hicho katika mkutano uliofanyika hivi karibuni wilayani humo. Kushoto ni Diwani wa kata hiyo, Selestine Yunde.
Ofisa Mtendaji Kata wa Siuyu, Bakari Kaduguda, akiwatambulisha viongozi wa kata hiyo kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM Kata ya Siuyu, Tito Lissu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Siuyu, Yasin Dao, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu Muenezi na Itikadi wa CCM Wilaya ya Ikungi, Pius Sanga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Siuyu, Selestine Yunde akizungumza na Wana CCM wa Kata hiyo katika mkutano wa kuwapongeza baada ya kuchaguliwa kuongoza kata hiyo uliofanyika hivi karibuni.
Wataalamu wa Kata ya Siuyu wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Makofi yakipigwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Noverty Kibaji akizungumza na Wana CCM wa Kata ya Siuyu katika mkutano wa kuwapongeza baada ya kumchagua mbunge na diwani kupitia chama hicho uliofanyika katika kata hiyo hivi karibuni.
Usikivu kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mika Likapakapa (kulia), akimkabidhi funguo ya pikipiki iliyonunuliwa na Mbunge Kingu, Katibu wa CCM Kata ya Siuyu, Tito Lissu.
Hapa ni wimbo wa CCM inachachamaa chaaa ukiimbwa 
Mbunge Kingu akiwa na Diwani wa Kata hiyo
Mbunge Kingu akizungumza.
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mika Likapakapa akizungumza na Wana CCM wa Kata ya Siuyu katika mkutano wa kuwapongeza baada ya kumchagua mbunge na diwani kupitia chama hicho uliofanyika katika kata hiyo hivi karibuni.
Mmoja wa mwana chama aliyehamia CCM kutoka Chadema akila kiapo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Singida Mashariki wameombwa kuwa pamoja na kushirikiana ili kuliletea maendeleo jimbo hilo.

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa wakati akizungumza na Wana CCM wa Kata ya Siuyu katika mkutano wa kuwapongeza baada ya kumchagua mbunge na diwani kupitia chama hicho. 

"Nawaombeni wana CCM wenzangu wa Singida Mashariki tuwe kitu kimoja ili tuliletee maendeleo jimbo letu la Singida Magharibi ambayo yalichelewa kwa muda mrefu ukilinganisha na jimbo la wenzetu la Singida Magharibi linaloongozwa na Elibariki Kingu" alisema Likapakapa.

Alisema hivi sasa kata hiyo inaongozwa na viongozi kutoka CCM kuanzia Rais, Mbunge na Diwani hivyo wanakila sababu ya kupata maendeleo kwa kuwa tayari wanamafiga matatu na lugha itakuwa moja.

Katika mkutano huo Kingu alipata nafasi ya kukabidhi pikipiki yenye thamani ya sh.milioni 2 .2 aliyoinunua ikiwa ni zawadi kwa kata hiyo kufuatia ushindi mkubwa walioupata wa kumchagua Mbunge Miraji Mtaturu na Diwani Selestine Yunde wote kutoka CCM.

"Pikipiki hii ninayo wakabidhi niahadi yangu niliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani kuwa tukipata ushindi nitainunua ili itumike kwa shughuli za chama katika kata hii" alisema Kingu.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Noverty Kibaji alisema ushindi walioupata wa kumpata mbunge na diwani huyo ulitokana na maombi yao kwa mungu.

Kibaji alitumia mkutano huo kumshukuru Kingu kwa msaada wa pikipiki hiyo na kuwaomba wana CCM wa Kata hiyo kuitunza na itumike kwa kazi za chama na si vinginevyo.

Diwani wa Kata hiyo, Selestine Yunde alisema sasa anaanza kazi rasmi ya kuwatumikia wananchi na jambo atakalo anza nalo ni kushughulikia suala la mashine za kukusanyia ushuru ambazo zinalalamikiwa kutumika vibaya na kusababisha Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na kata hiyo ya Siuyu ambayo ni sura ya wilaya hiyo kupata mapato kiduchu.

MASAUNI AONGOZA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimuelekeza dereva bodaboda jinsi ya kufunga kofia ngumu wakati wa utoaji wa elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara, lengo la elimu hiyo ni kuwaepusha na ajali zinazoweza kuzuilika,zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akizungumza na dereva wa daladala wakati wa utoaji wa elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara, lengo la elimu hiyo ni kuwaepusha na ajali zinazoweza kuzuilika,zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Zanzibar,Kamishna Msaidizi Robert Patrick, akiwaonyesha wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani sehemu ambako hutumika kwa wavuka kwa miguu ikiwa imefutika alama za pundamilia,wakati wajumbe hao walipokwenda kutoa elimu kwa madereva na abiria juu ya usalama barabarani,watatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni aliyeongoza ujumbe huo,zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Kamishna Mwandamizi Msaidizi,Fortunatus Musilimu akiwaeleza wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ripoti ya ajali za barabarani nchini muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kutembelea vituo vya daladala kutoa elimu ya kujiepusha na ajali za barabarani,wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni aliyeongoza ujumbe huo,zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiwaongoza wajumbe wa baraza hilo kuelekea katika vituo vya daladala kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto,lengo la elimu hiyo ni kuwaepusha na ajali zinazoweza kuzuilika,zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza mwananchi wa Zanzibar wakati wa utoaji wa elimu kwa madereva na watumiaji wa barabara, lengo la elimu hiyo ni kuwaepusha na ajali zinazoweza kuzuilika, zoezi hilo limefanyika Visiwani Zanzibar.Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Anayedaiwa kumchoma mkewe, atoa vitisho kwa waandishi wa habari

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV,

MFANYABIASHRA Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani ametoa vitisho kwa waandishi wa habari wanaompiga picha akiwa mahakamani kuwa atawafanyia kitu kibaya ambacho mahakama haijakitarajia.

Mshtakiwa Said amedai hayo leo Agosti 13,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally, baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mbele ya Hakimu Mkazi Salim Ally kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo, mshitakiwa Said alinyoosha kidole na kuomba kuongea akasema, "Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu Waandishi wa Habari, wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama nitafanya kitu kibaya sana;

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ili akili yangu itulie wanakuja kunipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitafanya kitu kibaya ambacho mahakama haitatarajia,"

Kufuatia kauli hiyo ya vitisho kwa waandishi wa habari, Wakili Wankyo alimueleza mshitakiwa kuwa, kupigwa picha ni hali ya kawaida kwa mshitakiwa yeyote anayedikishwa mahakamani, wote wanapigwa picha, hivyo amemtaka awape uhuru Waandishi wa habari wafanye kazi yao.

"Lengo la Waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwahabarisha jamii, hivyo kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani,"

Hata hivyo, Hakimu Ally anayeendesha shauri hilo, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo, mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji Kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002

Katika kesi hiyo ya muaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu, mshtakiwa Meshack alisambaza tangazo magazetini na kwenye mitandao ya Kijamii kuwa anamtafuta mke wake ambae alitoweka ghafla lakini baadae jeshi la polisi kupitia Mkuu wa Upepelezi wa kanda hiyo, Camillius Wambura alitangaza kumshikilia Luwonga akidaiwa kumuua na kisha aliuchoma moto mwili wa mkewe.
MFANYABIASHRA Khamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani akifikishwa mahakamani.

UBALOZI WA CHINA NCHINI WAINUA VIJANA KUPITIA WUSHU

$
0
0
*Vijana wapata fursa ya kujifunza na kujiajiri wenyewe, waushukuru ubalozi wa China nchini

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BARAZA la michezo nchini (BMT) kwa kushirikiana na chama cha Wushu pamoja na vituo vya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam wameendesha mashindano ya kimataifa ya sita ya Wushu jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha washiriki 200 kutoka nchini Tanzania na washiriki 20 kutoka nchini Rwanda.

Akizungumza mara baada ya mashindano hayo  mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye ni mwakilishi wa katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa (BMT) Milinde Mahona amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa ukifanya jitihada za ziada katika michezo na chama cha Wushu kipo kwenye orodha ya vyama vinavyofanya vizuri na hiyo ni kutokana na uongozi bora na ameupongeza ubalozi wa China nchini kwa ushirikiano wanaoonesha kwa vijana hao.

Amesema kuwa ubalozi wa China nchini umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha na kushirikiana na  vijana katika suala la kujiajiri kupitia michezo na kusema kuwa ubalozi umekuwa ukileta walimu kutoka China ili kuwafundisha vijana hao.

Milinde amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kusaidia chama hicho ambacho hadi sasa wameanzisha chama chao cha ulinzi pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi na kuwashauri  viongozi wa chama hicho kupeleka mafunzo hayo mikoani ili waweze kuwafikia vijana wengi zaidi.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa China nchini Gao Wei amesema kuwa mashindano hayo yataendelea kila mwaka kwa kushirikisha nchi mbalimbali Afrika Mashariki kama yanavyofanyika nchini China.

Gao amesema kuwa maarifa ya Wushu yaliyotolewa nchini yanaweza kuwa hazina kwa kutoa mafunzo kwa nchi nyingine, na amewashauri vijana hao kuendelea kuzalisha miradi mingi zaidi ambayo inatoa ajira kwa vijana wengi zaidi.

Vilevile ameeleza kuwa michezo hiyo imelenga kukuza nidhamu ambapo wizara inayosimamia masuala hayo imeona umuhimu mkubwa wa kituo hicho na wao wataendelea kuwaunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali kupitia Wushu.

Mashindano hayo yalizikutanisha timu nane kutoka Tanzania bara kwa kuhusisha Mikoa mbalimbali nchini pamoja na timu ya Rwanda Kungfu Wushu Federation ya nchini Rwanda.
 Viongozi mbalimbali waliohudhuria mashindano hayo ya sita ya Wushu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha vijana kutoka Tanzania na Rwanda, ambapo wito umetolewa kuwa chama hicho Cha Wushu kipelekwe Mikoani ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika, leo jijini Dar es Salaam.
 Vijana wa Wushu kutoka Mikoa mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Rais wa Wushu nchini Salehe Muhindi akizungumza katika hafla hiyo ambapo ameushukuru ubalozi wa China nchini kwa ushirikiano na kuahidi kuendelea kuunganisha vijana kote barani Afrika kupitia Wushu, leo jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Wushu msimu wa 6 wakiwa kwenye picha ya pamoja.

UGENI WA SADC KULINDWA NA HELKOPTA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
*Vyombo vya moto 126 vyakamatwa kwa kukiuka sheria elekezi zipo pikipiki, bajaji na magari yenye ving'ora na taa sumbufu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMANDA wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga katika kuhakikisha wageni wote watakaoingia nchini wanakuwa salama katika kipindi chote watakachokuwa nchini kwa kuangalia usalama wao kuanzia watakaposhuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, watakapofikia na wawapo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mambosasa amesema kuwa wageni wanazidi kuja nchini na jeshi la polisi lipo makini katika kuhakikisha hakuna aina yoyote ya uvunjifu wa amani utakaotokea.

"Msako na doria wa askari watumiao magari, pikipiki, mbwa, farasi, na watembeao kwa miguu unaendelea katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam na kuanzia kesho helkopta zitatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya jiji la Dar es Salaam" ameeleza Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa baada ya kuzuia pikipiki, magari yenye ving'ora na gari zenye rangi za taa sumbufu na bajaji kutoingia katikati ya mji,bado kuna watu wameendelea kukiuka agizo hilo ambapo hadi sasa jumla ya vyombo vya moto 126 vimekamatwa na vinashikiliwa na jeshi la polisi.

"Tuliweka zuio la baadhi ya vyombo vya moto kutoingia katikati ya mji, Kuna baadhi wamekiuka hasa pikipiki (bodaboda) ambazo zimekuwa hazifuati sheria, wanabeba mishikikaki na hawavai kofia ngumu na kupitia msako uliofanywa na jeshi la polisi vyombo vya moto 126 vimekamatwa na hivyo vikihusisha pikipiki 87, bajaji 13 na magari yenye ving'ora na taa sumbufu barabarani 26 na baadhi ya wahusika wanashikiliwa na watapelekwa mahakamani" ameeleza Mambosasa.

Vilevile amewahakikishia wananchi na wageni usalama wa hali ya juu na bado wanaendelea na kazi ya kuhakikisha jiji hilo linaendelea kubaki salama salimini hata baada ya mkutano huo kumalizika

"Jiji lipo shwari kabisa tuna akiba ya askari zaidi ya 300, msako utaendelea na watakaojaribu kukaidi kile kinachoelekezwa na serikali pamoja na vyombo vya ulinzi  na usalama,watakutana na vyombo vya dola na ninazidi kuwahimiza wananchi kuunga mkono jeshi la polisi hasa kwa kutoa taarifa za uharifu na waharifu kwa kuwa mafanikio yatakayotokana na mkutano huo ni yetu sote" ameeleza.

Mwisho ameishukuru kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, wakuu wa Wilaya, madiwani, wenyeviti wa mitaa, vyama vya ulinzi shirikishi na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano wanaoonesha hasa katika kipindi hicho ambacho taifa linategemea kuupokea ugeni mzito kutoka mataifa 15.
KAMANDA wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akizungumza na Waandishi wa habari za SADC,kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam leo,kuhusu namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga katika kuhakikisha wageni wote watakaoingia nchini wanakuwa salama katika kipindi chote watakachokuwa nchini .Picha na Michuzi JR.

MAWAZIRI SADC KUENDELEZA HARAKATI KUITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUIONDOLEA VIKWAZO ZIMBABWE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMATI ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), imesema jumuiya hiyo itaendelea na harakati za kuishinikiza Jumuiya ya Kimataifa ili kuiondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2019 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Palamagamba Kabudi amesema kamati hiyo itaendeleza harakati za kuishinikiza jumuiya hiyo ya Kimataifa kuondolea vikwazo Zimbabwe.

Profesa Kabudi ambaye amekabidhiwa nafasi hiyo ya Uenyekiti leo ameeleza umuhimu wa Zimbabwe kuwa huru katika shughuli za kichumi kwa kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.

“Zimbabwe imewekwewa vikwazo vya kuichumi kwa muda mrefu , na sasa hakuna sababu ya vikwazo hivyo kuendelea.Hivyo umefika wakati wa kuondolewa vikwazo vya kiuchumi,”amesema Profesa Kabudi.

Prof. Kabudi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefafanua zaidi Zimbabwe imefanya uchaguzi mkuu wake na imempata Rais, hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kuondolewa vikwazo vya kiuchumi ili waendelee kuijenga nchi yao.

Kuhusu mambo mengine yatakayofanywa na kamati hiyo Mwenyekiti huyo wa kamati ya baraza la mawaziri amesisitiza namna Tanzania itakavyotumia nafasi hiyo kuzihamasisha nchi za SADC kutumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya mawasiliano kwa nchi wanachama.

Wakati huo huo Profesa Kabudi amezungumzia umuhimu wa kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinatafuta ufumbuzi wa changamoto ya uhaba wa ajira kwani asilimia 60 ya vijana katika nchi hizo wanakabiliwa na changamoto hiyo.

“Tutashirikiana kuweka nguvu kwenye eneo la viwanda ambalo tunaamini mbali ya kuleta maendeleo kwa nchi za SADC, pia tutapunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwani wananchi wetu,”amesema Profesa Kabudi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),Profesa Palamagamba Kabudi.Picha na Michuzi JR.

WATOA HUDUMA ZA AFYA MWANZA WAFUNDWA

$
0
0
Afisa Afya ya Mazingira kutoka Taasisi ya JBHN Said Chibwana akitoa Elimu kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akieleza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), inayoendelea Jijini Mwanza.
Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana akisisitiza jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), Semina hiyo inaendelea Jijini Mwanza.
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Seketoure wakifuatilia mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka kwa Wataalamu wa Huduma za Afya na baadhi ya Watumishi wa Sekta ya Afya wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline), mafunzo yanaendelea Jijini Mwanza.

…………………………………………………..

Na Rayson Mwaisemba WAMJW-MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yawafunda Watoa Huduma za Afya Jijini Mwanza kuwakumbusha namna ya utoaji elimu bora kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji huduma kwa Wagonjwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo visivyo na ulazima.

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kutibu magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na Wizara ya Afya imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Kwa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Aidha, Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Afisa Mkuu Uhakiki Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joseph Hokololo amesema kuwa zaidi ya watu milioni 1.4 Duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wakupata huduma ya afya, hii hutokana na Watoa huduma za Afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.

Aliendelea kusema kuwa Asilimia 15 ya Wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya pindi waendapo kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya, kutokana na kutofuatwa kwa taratibu, kanuni za miongozo ya kutoa huduma za Afya (IPC Guideline, SOP).

Kwa Upande wake Afisa kutoka Kitengo Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogane Justine amesema kuwa kufuata taratibu za utoaji huduma kama kanuni za uoshaji sahihi wa mikono kutamsaidia Mtoa huduma kuzuia kusambaza maambukizi ndani ya Kituo cha kutolea huduma za Afya na nje.

Licha ya changamoto za upatikanaji wa huduma za maji safi kwa baadhi ya Vituo vya Afya, Dkt. Chrisogone Justine German amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Mtoa huduma za Afya kuhakikisha ananawa mikono yake vizuri kwa sabuni na maji safi ili kuepuka kusambaza maambukizi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akitoa Elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi mapya yanayotokea wakati wa matibabu kutokana na baadhi ya Watoa huduma kutofuata taratibu na miongozo Dkt. Radenta Bahegwa amesema kuwa asilimia 40 ya magonjwa yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya nayosababishwa na kutofuata kwa taratibu za miongozo ya utoaji huduma.

“Asilimia 40 ya ya magonjwa yanayopatikana katika Vituo vya kutolea huduma za Afya husababishwa na kutofuata miongozo (IPC Guidline), ndiomaana asilimia 80 ya UTI zinazoibuka katika Vituo vya Afya zinatokana na kukosea kuweka kifaa cha kupitisha haja ndogo” alisema Dkt. Radenta.

Mtaalamu kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Dkt. Alex Sanga amesema kuwa katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo ametoa wito kwa Watoa huduma kuhakikisha wanafuata miongozo na taratibu wakati wa kutoa huduma ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi mapya katika jamii.

“Tafiti za Shirika la Afya Duniani zinonesha kuwa ndani ya miaka 3 (2015-2018) kati ya watu 33,421, watu 542 walipoteza maisha, huku katika watu 100, watu 5 hadi 10 wanakuwa katika hali mbaya ya ugonjwa wa kipindu pindu, hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa” alisema Dkt. Sanga.

Naye Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu.

Kwa upande wake Mfamasia kutoka Hospitali ya Kanda Bugando Francisco Chibunda ametoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kufuata miiko na taratibu na miongozo inavyoelekeza jambo litalosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata taratibu na miongozo wakati wakutibu ugonjwa.

“Tunapoteza nguvu kubwa, tunapoteza rasilimali nyingi kwenye dawa na matibabu, mwisho wa siku tunasababisha maambukizi mapya, nah ii hupelekea usugu wa magonjwa , kwa hiyo tubadilike” Alisema Chibunda.

BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) YAWALILIA WATANZANIA WALIOFARIKI KWENYE AJALKI YA MOTO WA GARI LA MAFUTA HUKO MOROGORO

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MBURAHATI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na wakazi wa Kata ya Mburahati, Kigogo jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Kata hiyo kwa lengo la kujua changamoto wanazokutananazo pamoja na namna wanavyoshirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia uhalifu na wahalifu katika maeneo yao wanayoishi. Picha na Jeshi la Polisi.

MALINZI AJITETEA, ADAI HANA UHAKIKA NA KIASI ANACHOIDAI TFF

$
0
0
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hana uhakika na kiasi cha fedha anachoidai hakika lakini anaimani kuwa anaidai kwani hata siku chache kabla ya kukamatwa kwake aliikopesha TFF Sh. Milioni 15.

Amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha mara kwa mara kwani wakati anaingia madarakani, shirikisho hilo lilikuwa na hali ngumu kiuchumi iliyosababisha madeni makubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha akaunti za shirikisho hilo kufungwa mara kwa mara.

Malinzi amedai hayo leo Agosti 13, 2019 wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde, dhidi ya kesi inayomkabili ya mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha baada ya kukutwa na kesi ya Kujibu.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza amedai, alikuwa akiikopesha TFF fedha zake binafsi na alikuwa akifanya hivyo kupitia akaunti waliyoifungua kati yake na shirikisho hilo.

Amedai kiasi hicho cha sh. Milioni 15, zilikuwa ni kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za Afrika kati ya Tanzania na Lesotho 

Amedai akiwa Rais, alihakikisha shughuli mbalimbali za timu zinakwenda hadi kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa ambapo ili kufanikisha hilo, mara nyingine ilikuwa ikinilazimu kutumia fedha zangu za mfukoni ili kuweza kuinusuru TFF hali ikiwa nzuri narudishiwa na wakati mwingine kukopa kwenye kamati tendaji na kwa watu binasfi" alidai

Malinzi alidai kuwa aliikopesha TFF kutokana na hali ngumu ya kifedha iliyokuwa ikiikabili na hivyo kulazimika kutumia fedha zake binafsi, kukopa kwa watu binafsi ama kamati ya utendaji ili kunusuru hali hiyo hasa katika matukio muhimu yanayoikuta TFF na timu ya Taifa Taifa Stars.

Akiendelea kutoa utetezi wake, amedai, baadhi ya matukio ambayo alilazimika kutoa fedha zake na kuikopesha TFF mojawapo ni ile ya kulikomboa basi la TFF ambalo lilikuwa linashikiliwa na kampuni ya udalali ya Yono kufuatia amri ya mahakama la kuilipa Kampuni ya Pachi Line iliyokuwa ikitoa huduma za tiketi uwanjani.

Ameendelea kudai kuwa, aliilipa sh milioni 20 kwa kampuni ya udalali ya Yono ambapo TFF ilikuwa ikidaiwa na TRA na walitaka kukamata basi ambalo lilitolewa na wafadhili wao, Kampuni ya Bia ya TBL,Pia alilipia sh.milioni 40 za tiketi za ndege Kampuni ya Ethiopia Airline, za wachezaji wa Tàifa Stars waliokuwa wanakwenda Nchini Nigeria katika Mashindano ya Afrika yaliyokuwa yakufuzu Misri

Aidha ameongeza kudai kuwa aliwahi kuikopesha TFF USD 7000 wakiwa Harale, Zimbabwe baada ya wachezaji waTaifa Stars kutolewa mizigo yao nje ya hoteli waliyokuwa wamefikia kwa sababu Shirikisho la mpira Zimbabwe lilikuwa likidaiwa na hoteli hiyo, hata baadhi ya mashahidi waliowahi kutoa ushahidi mahakamani hapa walithibitisha hilo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa TFF Daniel Masangi"alidai Malinzi

Amewataja mashahidi wa upande wa mashtaka waliodhibitisha jambo hilo Mahakamani akiwemo Katibu Mkuu Wilfred Kidao, Hellen Adam na Sareki Yonasi.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Selestine Mwesigwa
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya uwamuzi wa kupokelewa kwa kielelezo cha nyaraka ya taarifa ya madeni kati ya TFF na Malinzi ama laKesi hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.

Wananchi Rukwa kushiriki kuchangia Damu kusaidia Majeruhi Ajali ya Morogoro

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa mkoa huo kushiriki katika zoezi la kuchangia damu litakalofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 14 hadi 18.8.2019 katika halmashauri nne za mkoa, ili kusaidia majeruhi walioungua na moto uliosababishwa na kulipuka kwa lori la Mafuta katika ajali iliyotokea eneo la Msavu mkoani Morogoro, na kusababisha vifo vya watu 76 na majeruhi 54.

Mh. Wangabo amesema kuwa zoezi hilo litawajumuisha Waendesha Bodaboda na Bajaji, Madereva wa Magari, Vijana, Watumishi wa Serikali, Wanafunzi, Vyama za Siasa, Madhehebu ya Dini, Viongozi mbalimbali na wale wote wenye mapenzi mema na moyo wa kujitolea kwaajili ya majeruhi hao.

“Nafahamu kuwa mtu yeyote aliyeungua sehemu yoyote ya mwili, miongoni mwa madhara makubwa anayoyapata ni pamoja na kupoteza kiasi kikubwa cha maji mwilini (Dehydration) na kupungukiwa damu mwilini (Anaemia). Kwa hiyo natoa wito na kuwaomba Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuchangia Damu kwa ajili ya wenzetu majeruhi wanaoendelea na matibabu. Damu hiyo pamoja na salamu zetu za pole tutaiwasilisha kwa Dkt. Kebwe Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,” Alisema.

Aidha Mh. Wangabo kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa anaungana na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Viongozi wa Mkoa huo, Familia za Marehemu, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Wapendwa wao. Na kumuomba Mwenyezi Mungu awape Moyo wa Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.



“Mungu awape pumziko la milele waliopoteza uhai na awaponye Majeruhi wote wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro. ‘Bwana Alitoa na Bwana Alitwaa Jina lake lihimidiwe’.” Alimalizia.



Mh. Wangabo ametoa maelekezo hayo kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kilichohusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini.
Viewing all 109939 articles
Browse latest View live




Latest Images