Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

CHUO CHA DIPLOMASIA CHAWANOA MAAFISA SERIKALINI NA SEKTA BINAFSI


BENKI YA KCB TANZANIA YAMWAGA MISAADA JIJINI DAR

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir(wapili toka kulia)akimkabidhi msaada wa Mashine ya kupasha moto vifaa vya hospitali kabla ya matumizi na baada ya matumizi  kwa mgonjwa(Sterilizer) Mkurugenzi wa Zahanati ya Njia Heath Centre ya Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw.Stephen Mosha(wapili toka kushoto .Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyote vyenye thamani ya  shilingi Milioni 5,wengine wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya hiyo  Christina Manyenye.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye ,akimkabidhi  Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mabati na saruji  vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata  jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yake.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye akimkabidhi  Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mifuko ya  Saruji 28,Mabati 18   vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata  jijijini Dar es Salaam.Msaada huo utamsaidia kwa ajiri ya ukarabati wa nyumba yake.
 Mkuu wa Masoko na Mahusiano  wa benki ya KCB Tanzania,akisoma hutuba kwa wakazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati  wafanyakazi wa benki  hiyo walipofika kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 katika Zahanati ya NJia  Health Centre.Anayeshuhudia (kushoto)ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Njia  Health Centre,Bw. Stephen Mosha wakati walipofika katika kituo hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5.Katikati ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi,Hellen Olengailuva. 
 
Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Njia Heath Centre kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,Bw Stephen Mosha ,akiongea na waandishi wa habari wakati  Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania,walipofika Hospitalini hapo kutoa  msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki  hiyo Bw.Moezz Mir na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.

Pinda ataka watafiti wa ndani watumiwe zaidi

0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa jengo jipya la ghorofa tano katika Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa.  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kampasi hiyo, Prof. Andrew Mbwambo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi (kushoto).

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akisalimiana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Utawala na Fedha, Prof. Faustin Kamuzora (kulia) wakati wa uzinduzi rasmi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam na pia uzinduzi wa jengo jipya la ghorofa tano katika kampasi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Anayetabasamu katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa. 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi rasmi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam na pia uzinduzi wa jengo jipya la ghorofa tano katika kampasi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Wengine ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Daniel Mkude (mwenye tai ya njano) na Mkuu wa kampasi hiyo, Prof. Andrew Mbwambo.

----------------------------------------
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametoa Changamoto kwa taasisi mbalimbali hasa za serikali nchini kuwaamini na kuwatumia watafiti wa ndani badala ya kukimbilia kutumia wale wa nje ambao amesema mara nyingi huwa na gharama kubwa.
Waziri Mkuu alisema hayo wakati alipokuwa akizindua rasmi Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam na pamoja na jengo la ghorofa tano la kampasi hiyo juzi jioni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo baada ya uzinduzi huo, Bw. Pinda alisema kuna tabia imejengeka kwa taasisi na idara za serikali kukimbilia watafiti wa nje pale mahitaji yanapojitokeza na kuwaacha wa ndani.
“Huu mtindo haufai...watafiti wetu wa ndani wana uwezo na wanajua mazingira ya nchi yetu vizuri...tuwasadie kwa kuwapa kazi,” alisema, na kuongeza kuwa serikali inaamini kuwa watafiti hao wanaweza kufanya kazi kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
Alisema watafiti hao wakitumika vizuri watakuwana uwezo wa kutoa majibu yanayolingana na mazingira ya nchi na hivyo kupata suluhisho la changamoto mbalimbali za maendeleo.
Akitoa mfano wa Mzumbe alisema chuo hicho kilichodumu kwa takriban miaka 60 sasa kimetoa mchango mkubwa wa wataalam na kujijengea uwezo katika nyanja mbalimbali ambao unaweza kuwa faida kwa nchi kuliko ilivyo sasa kama kitatumiwa vizuri.
“Tumieni uwezo wa chuo hiki katika tafiti zenu,” Bw. Pinda aliwaambia baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali walioandamana nae katika hafla hiyo.
Alisisitiza kuwa katika maswala ambayo vyuo kama hicho vina uwezo nayo hakuna sababu ya kutafuta wataalamu kutoka nje ya nchi.
“Tabia ya kuchua watalaamu kutoka nje ya nchi kwa maswala ambayo wataalamu wetu wana uwezo nayo haiingii akilini,” alisema Pinda.
Aidha  alitoa ushauri kwa chuo hicho kuanzisha kozi fupi amabazo zitasaidia kutoa elimu kwa viongozi wakiwemo mawaziri, wabunge, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya na wengine kupata weledi wa uongozi.
“Kuna matatizo mengi yanajitokeza hivi sasa na ukiyaangalia unakuta kuwa baadhi ya mambo yanahitaji tu weledi wa mbinu kidogo za uongozi,” alisema Bw. Pinda.
Alisema Chuo hicho kilipoanzishwa wakati wa ukoloni na baada ya uhuru kilikuwa kinatayarisha watu kuwa viongozi na kwamba pamoja na kuwa sasa masomo hayo yanatolewa katika programu za masomo ya chuo hicho, bado ipo haja ya kuanzisha kozi hizo fupi kwa ajili ya viongozi ambao hawakupata mafunzo hayo.
Alisifu uongozi wa chuo hicho kwa kupanua wigo wa elimu kwa watanzania kwa kuanzisha kampasi za Mbeya na Dar es Salaam na pia kwa kupanua miundombuni na udahili wa wanafunzi.
Alisema uamuzi wa chuo hicho kutaka kuanza kutoa mafunzo katika ngazi ya uzamili kuwezesha wahitimu kusimamia miradi mikubwa katika sekta za madini, gesi na mafuta ni mzuri na wenye manufaa kwa nchi.
“Kinachotakiwa sasa ni kwa chuo hiki kujenga mahusiano na nchi zenye uzoefu katika sekta hizi ili mjue zaidi undani wake na mboreshe kozi mtakazotoa,” alisema.
Alisema pamoja na kwamba uwiano wa wanawake na wanaume katika udahili wa wanafunzi si mbaya, bado juhudi zinatakiwa katika kuongeza idadi ya wanawake.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa alisema chuo chake kimejenga jingo hilo kutokana na mahitaji makubwa ya  watu wanaotaka kusoma katika kampasi ya Dar es Salaam.
“Jengo hili litasaidia kuboresha huduma zetu kwa wanafunzi na pia kurahisisha kazi ya waalimu wetu,” alisema, na kuongeza kuwa sasa chuo kitaokoa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika katika kukodisha kumbi za mihadhara.
Jengo hilo lina maktaba ya kisasa iliyochukua ghorofa mbili za jengo, ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na ya Mkuu wa Kampasi, kumbi tatu za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 132 kila mmoja pamoja na ukumbi wa mikutano.
Alisema chuo kina mipango ya kuongeza ujenzi wa miundombinu na rasilimali watu ili kuzidi kupanua wigo wa elimu kwa watanzania katika sehemu mbalimbali nchini katika juhudi za kuunga mkono nia ya serikali ya kupanua fursa za elimu kwa wananchi.
Kampasi ya Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na wanachuo 146 na programu mbili za uzamili.
Katika mwaka wa masomo wa 2013/2014, kampasi hiyo ilidahili wanafunzi 1052 ambao kati yao 504 ni wanawake na 548 ni wanaume wanaosoma shahada za uzamili katika programu zaidi ya 10.
Kukua kwa kampasi hiyo kumechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Chuo Kikuu Mzumbe ambayo idadi yake kwa sasa ni zaidi ya wanachuo 8,000.


uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa PPF  Bw. William Erio, Picha ya mji Mkongwe wa Zanzibar iliyotengenezwa kwa ubunifu wa kutumia majani makavu ya Mgomba,aliyonunua kwa shilingi za Kitanzania Millioni Tano, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi  Mlango wa Zanzibar  Dr.Rajeev Aggarwal,mtaalam wa mambo ya uwezeshaji katika Wizara ya uwezeshaji wananchi,mlango huo ulinadishwa kwa Shillingi za Kitanzania  Millioni moja na Laki moja,katika uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea maonesho ya wajasiria mali kutoka Vikundi mbali mbali vya Unguja na Pemba, katika uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar, katika ukumbi wa mikutano Zanzibar Beach Resort. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

SALAMU ZA MWAKA MPYA TOKA HOLLAND

0
0
Mwaka mpya unakuja,tuufanyeje?
Mabaya yaliyopita,tuyazikeje?
Neema Tuliyopata,tuienzije?
Neema tukiipata,tufurahije?
Huzuni ikitufika,tuishikeje?

Na mdau Hija Saleh,
Holland.

MATOKEO MAZURI YA UFAULU SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAVUTIA BENKI YA WANANCHI MUFINDI

0
0
 Mkurugenzi  wa shule  ya kimataifa  ya  Southern Highlands Mafinga  Bi Mary  Mungai akimkabidhi  cheti mmoja kati ya  wahitimu wa mahafali ya 13  shule  hapo ,kulia  kwake ni kaimu meneja  wa Benk ya wananchi Mufindi (Mucoba) Bw Ben Mahenge 

Walimu na  wafanyakazi wa shule ya Southern Highlands Mafinga  wakiwa katika  picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai kushoto wa kwanza .
................................................................
Na Francis Godwin
MAENDELEO mazuri  ya ufaulu  wa  wanafunzi  wa shule  ya kimataifa  ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa iliyoisukuma benk  ya wananchi Mufindi (MUCOBA) kujitokeza kuunga mkono jitihada za  elimu  katika shule  hiyo .

Shule ya Southern Highlands Mafinga imeonekana kuivutia zaidi  benki hiyo ya MUCOBA  kutokana na rekodi  yake nzuri  ya kufaulisha vizuri wanafunzi wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.

Kiwango  cha  elimu  kinachotolewa katika  shule  ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga kinaisukuma benk ya  wananchi  wilaya ya  Mufindi (MUCOBA)   kuahidi  kutoa  kiasi  cha  Tsh milioni 2.5  kwa  ajili ya  kuwafungulia  akaunti  katika benk hiyo  wanafunzi  waliofanya  vema  matokeo ya  mtihani  huo  mwaka  huu.

Bw Ben Mahenge  anasema  kuwa  moja kati ya  sababu  iliyopelekea  benk  yake kujitokeza  kuunga  mkono  jitihada za  shule  hiyo  ni  kutokana na ufaulu  mzuri  wa  mitihani  ya Taifa  ya  darasa  la  saba  ambayo shule  hiyo  imeendelea  kuongoza na  hivyo  kutoa  heshima kwa  wilaya  ya  Mufindi na Tanzania  kwa  ujumla .

Kwani  anasema  kuwa  mbali ya  benk hiyo  kuendelea  kutoa  mikopo mbali mbali  ila imekuwa  karibu  zaidi na  shule  hiyo ya  Southern Highlands Mafinga  ambapo  mkurugenzi  wake Bi Mary A. Mungai  ni mmoja kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  hiyo  kutokana na

wazazi  wote  wanaosomesha  watoto  katika  shule hiyo  kulipia ada kupitia  benk  hiyo hivyo  kiasi  hicho cha fedha  kilichotolewa na  MUCOBA ni  kutambua mchango  wa  shule  hiyo katika  uendelezaji  wa  benk hiyo. 

" Kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  ya  MUCOBA ni  pamoja na  shule ya  Southern Highlands Mafinga na  wazazi ambao  wanasomesha  watoto hapo kutokana na   wazazi wa watoto  wanaosomesha  hapo  hulipa ada  kupitia  benk  yetu .....hivyo  kwa  ajili ya  kumpongeza  mkurugenzi  wa  shule hiyo kwa kuzidi  kuiunga mkono  benk  yetu  bado tunazidi  kuwahamasisha  wananchi  wa  wilaya ya  Mufindi na nje ya  mkoa  wa  Iringa kujiunga nasi"

Mahenge  anasema  kuwa  benk hiyo  imeendelea  kutoa  mikopo  mbali mbali  kwa  wateja  wake  ikiwemo mikopo ya  ujenzi  wa  nyumba  bora , ujasiliamali na mikopo  ya kuendeshea  biashara .

Hata  hivyo  Mahenge  anasema  kuwa  wanafunzi  watakaonufaika na msaada  huo  ni  yule  aliyefanya   vizuri katika matokeo  ya mtihami  wa  Taifa  wa darasa la  saba pamoja na mwanafunzi Aida  Mhagama  ambae  aliibuka  mshindi  wa  jumla katika masomo  mbali mbali  na  kupongezwa  wakati  wa  mahafali  ya  darasa  la  saba ya  shule  hiyo .
Anasema  fedha  hizo  zitaingizwa katika akaunti   zao baada ya  kufunguliwa na  benk hiyo  kwa  lengo la kusaidia  kuwasomesha  elimu  ya  sekondari pindi watakaojiunga na  elimu  hiyo ya  sekondari mapema  mwakani .

Mkurugenzi mtendaji wa shule  hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata   kuwa afisa  elimu shule za msingi anasema  kuwa shule  imekuwa  ikifundisha kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena mwaka  huu 2013 wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.

“…Tunawapa hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako. ….pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern Highlands School.”

Anasema pia uongozi  wa shule  hiyo hautaacha  kuwapongeza walimu, kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo ya kiwango cha juu.

“ Sisi  tunapokea watoto  kutoka pande zote za nchi  na watakaotaka  watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za english medium.”

Anasema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .

“Shule  yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”

Anasema katika  matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.

“  Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai

Hata  hivyo  anasema kila mwaka wanafunzi wote  wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.

“Mwaka  huu tena  wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari”

Mwenyekiti  wa bodi ya shule  hiyo Bw Omary Mahinya anasema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule  hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka  watoto wao hapo . 

Mama Asha Suleiman Iddi akabidhi bao, karata na busati kwa wanamichezo ya jadi Pemba

0
0
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Zawadi ya Bao miongoni mwa Mabao 12 Katibu wa mchezo wa Bao Wilaya ya Chake chake  Nd. Faki Salum Khamis aliyojitolea kuhamasisha mchezo huo ili wajiandae vyema katika mashindano ya bao kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.Kulia ya Mama Asha ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar {BTMZ } Sharifa Khamis, Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar Mama Asha Bakari Makame na Afisa Mdhamini Wizara inayosimamia Michezo Pemba Ali Omar.
Katibu wa Mchezo wa Karaka Wilaya Chake chake Bwana Amour Khamis Haji akipokea msaada wa Karata kutoka kwa Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi  tayari kujiandaa na vugu vugu la michezo ya kusherehekea nusu karne ya Mapinduzi ya Zanzibar.Mama Asha pia alikabidhi mabusati manane kwa vilabu hivyo vya michezo ya ndani kisiwani Pemba hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Gombani Kisiwani Pemba. Picha na Hassan Issa wa   OMPR – ZNZ.

Taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya ardhi, maliasili na mazingira kuhusu tathmini ya matatizo yaliyotokana na oparesheni tokomeza iliyosomwa jana bungeni mjini dodoma Chini ya Mwenyekiti wa Kamati James Lembeli

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya ardhi, maliasili na mazingira Mhe. James Daud Lembeli, Mb.
1.0 UTANGULIZI.
Mheshimiwa Spika, wakati Bunge likijadili hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili jambo muhimu la dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 47 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2013, iliyowasilishwa na Mhe. Said Nkumba, Mbunge wa Sikonge kuhusu Mgogoro kati ya Wafugaji na Wakulima, Hifadhi na Uwekezaji, Mheshimiwa Spika alitoa Uamuzi ‘Speakers Ruling’ kuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ishughulikie kazi ya kutathmini na kuangalia jinsi Mpango wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na kutekelezwa na Serikali kupitia ‘Operesheni Tokomeza’.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Taarifa Rasmi za Bunge za tarehe 1 Novemba 2013, wakati Bunge likihitimisha Hoja ya Kuairisha Shughuli za Bunge, Mhe. Spika alitoa uamuzi ufuatao:-

…Kamati ile ya kawaida ya Maliasili itaendelea na kazi yake ya kufanya tathmini ya kuangalia jinsi mpango ule wa Kupambana na Majangili ulivyopangwa na ndani yake itashughulikia kama kulikuwa na uzembe ama kuna watu wanahusika katika kuondoa maisha ya watu kwa sababu za uzembe …






7 die and scores injured in Kibera Train Accident

0
0
In the wake of the train crash that left seven people dead in Kibera on Monday, concern is growing over settlements that have over the years encroached on land reserved for railway tracks. As Brenda Mulinya reports, more danger lurks in several crowded slum dwellings that have been constructed close to the railway line. Courtesy of MTN

MDAU FELIX MWAGARA NA MKEWE WALAMBA NONDOZZZZ CHUO KIKUU MZUMBE-KAMPASI YA DAR ES SALAAM

0
0
 Afisa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Felix Mwagara (kulia) na mai waifu wake  Lydia Mbonde baada ya kulamba Nondozzzz za  Uzamili ya MSc/HRM mara baada ya kutunukiwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ya Chuo Kikuu cha Mzumbe – Kampasi ya Dar es Salaam.

 Afisa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Felix Mwagara na mai waifu wake  Lydia Mbonde wakipokea zawadi mara baada ya kula Nondozzz ya  Uzamili ya MSc/HRM katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ya Chuo Kikuu cha Mzumbe – Kampasi ya Dar es Salaam.

Afisa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Felix Mwagara na mai waifu wake  Lydia Mbonde wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao mara baada ya kulamba Nondozzz za Uzamili ya MSc/HRM katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ya Chuo Kikuu cha Mzumbe – Kampasi ya Dar es Salaam.

BONGO LEGEND SHIRTS BY KAJUMULO THE BUSHMAN

0
0
I manufactured only a limited number of shirts.  These shirts are still worn today by some of the most powerful people in Tanzania. I am planning to manufacture another limited edition run of the Bongo Legend shirt in 2014 for release at the time of the celebration of his birthday.  I will be taking pre-orders, information will be released about this in early 2014.
The design of this shirt is owned by me, not BabuKaju records or Kajumulo World Soccer, or Soccer Monster.  
It is my personal design and is owned by me personally.  If anyone wants to license this design they need to come directly to me. Before I made this design, I obtained permission from the Nyerere foundation to use this image and the entirety of the design is copyrighted by me with full permission from the foundation for use of the image
Kajumulo, 
The Bushman
206-501-9778

MH. LOWASSA ASHIRIKI TAMASHA LA WAENDESHA BODABODA JIJINI DAR LEO

0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.

WAKONGWE WA DISCO DJ SEYDOU NA DJ JERRY KOTTO WAIBUKA UPYA

MSIBA ROME: MWILI WA MAREHEMU ABDULLI ABUU (HATIBU CLEAN HEART) WASAFIRISHWA

0
0
Mwili wamarehemu Abdulli Abuu ukiwa tayarii kuelekea uwanja wa ndege wa Rome kwa safarii ya mwisho nyumbani kwa mazishi

Wakiwa katika hatua za mwisho ni viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome ambao ndio walikuwa wenyeji wa msiba, wakisaidia kuingiza mwili wamarehemu ndani ya usafiri.
pichani ni Mh.Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania Rome ndugu Erasmus Pindu Luhoyo na katibu wake ndugu Endrew Mhella,wakisaidiwa na mjumbe wa Jumuiya y
a Watanzania ndugu Mohamed Mnodwa.


Kabla ya mwili kupandishwa ndani ya usafiri,(from L) Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Rome Erasmus Pindu Luhoyo, (c) Kaimu mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia mama FATUMA TANDIKA na katibu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Italia ndugu Kagutta N.Maulidi wakitoa heshima za mwisho. Mwili umeondoka leo na ndege ya shirika la kituruki TURKISH AIR kuelekea Istanbul- Dar. itafika Dar es salaam Tanzania saa 03:35 usiku.
Katika shughuli za maombi na kuaga mwili ubalozi wa tanzania Rome uliwakilishwa na Mh Mbilinyi ambae ni mkuu wa utawala ubalozi wa Tanzania Rome. Mh Mbilinyi aliwasilisha salaam za balozi wa Tanzania Rome ambae kwa sababu za kikazi hakuweza kufika na badala yake akatuma ujumbe.

 Katika salaam za balozi alielezea jinsi gani anaungana na Watanzania wote Italy,ndugu wa marehemu na Wazazi katika kuombopleza msiba  huu.Mh Mbilinyi alisema msiba wa mtanzania ni msiba wa ubalozi.katika salaam zake aliwasisitiza zaidi Watanzania kuendelea na ushirikiano,umoja na upendo zaidi.
Katibu mkuu wa jumuiya ya Watanzania Italia alikuwa na mazungumzo mafupi na viongozi wa jumuiya ya Watanzania Rome,na wamekubaliana kuitisha kikao cha viongozi wa jumuiya zote za Watanzania nchini Italia ili kuweza kuongelea kwa mapana zaidi kuhusu matatizo ya 
Watanzania na kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na hayo kuna mambo zaidi ya muhimu ya kujadili na pengine kuyafikisha ngazi za juu. Kikao hicho kitakuwa mapema mwezi ujao.
Kama mwenyeji, Mwenyekiti 
Erasmus Pindu Luhoyo aliitumia nafasi ya kuutambulisha uongozi mpya wa Roma na kuongea kwa kirefu na Watanzania katika kuhimizana na kukumbushana mambo muhimu yanayozunguka jamii ya Watanzania ughaibuni.
katibu mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Italia

matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,alipokuwa akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar na Wanachama wa CCM Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,pamoja na kuyafungua Matembezi ya Umoja huo ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, (kushoto) Naibu Katibu Mkuu  wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(wa pili kushoto)akiongoza Maandamano ua Umoja wa Vijana CCM Zanzibar yaliyoanzia Michweni kelekea Wete Pemba,leo katika ufunguzi rasmi,Makamo wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa kamati Kuu Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,(katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC Dk.Mauwa Daftari
Vijana wa CCM Zanzibar,UVCCM wakiwa katika Matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)yaliyoanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba
 Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba Pich za Viongozi wa Chama katika Matembezi ya Madhimisho ya miaka 5o ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)kuanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba. 



 Kikundi cha Brass Band cha Umoja wa Vijana CCM Zanzibar,kikiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,leo kuanzia  Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba.Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu.


Article 24

Shekinah Garden Christmas Programe

0
0
Mbezi Beach
Makonde Opp. Engen Petrol Station
Tel: 022 2627116 / 0767 333 239 / 0655 627 116

VIJANA CCM WAMPONGEZA JK KUTEMA MAWAZIRI WANNE

0
0
NA BASHIR NKOROMO

UMOJA wa Vijana wa CCM, Kata ya Mabibo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, umempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa kuwavua uongozi mawaziri wanne mwishoni mwa wiki.

Mawaziri waliovuliwa uongozi kufuatia Rais Kikwete kutengua teuzi wao ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai (Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu akiwa Bungeni.

Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua iyotokana na mapendekezo ya bunge, baada ya Kamati yake ya kudumu ya  Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini 'uozo' katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.

Pongezi hizo ya UVCCM Mabobibo, ni miongozi mwa mazimio waliyofikia wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM kata hiyo, baada ya semina yao iliyomalizika jana kwa kufunguwa na Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.

Katika maazimio hayo, Vijana hao, Wamepongeza ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambazo amefanya hivi karibuni na sekretarieti yake, na kumuomba Kinana kuendeleza ziara hizo, kwa maelezo kwamba zimeonyesha manufaa makubwa kwa Chama.

Katika ziara iliyomalizika hivi karibuni Kinana alifanya ziara katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe akiambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye sasa pia ni Mbunge kufuatia kuteuliwa na Rais Kikwete.

Pamaoja na kupongeza ziara hizo, UVCCM Mabibo pia wameazimia kuhakikisha mitaa mitatu iliyopo chini ya chama cha CUF, kati ya sita ya kata hiyo ya Mabibo inarejeshwa kwenye himaya ya CCM baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwakani.

Akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo, Cholage aliunga mkono maazimio hayo, akiyaeleza kwamba ni ya msingi. 

"Kwa kweli naunga mkono maazimio. Siyo kwamba tunafurahi mawaziri hawa kukosa kazi, la hasha, lazikini kinachotufurahisha zaidi ni kuona kwamba Mwenyekiti wa Chama Rais Kikwete amesimamia inavyostahili misingi ya uwajibikaji", alisema Cholage na kuongeza;

"Pia hii kazi inayofanywa na Mzee wetu Kinana na kina Nape, ni ya kupigiwa mfano ambayo sisi kama vijana, lazima kuiunga mkono kwa dhati ya mioyo yetu yote, lakini si kwa maneno tu bali kwa vitendo".

Cholage aliwahimiza vijana, kuwania nafasi za uongozi wa mitaa, uchaguzi utakapowadia, lakini akawataka kufanya hivyo kwa kujipima kwanza kama anatosha kila atakayekuwa anadhamira ya kugombea.

Aliwataka UVCCM kuwa imara katika kukilinda Chama akiwakumbusha kuwa wao ndiyo askari wa mstari wa mbele katika kazi hiyo.

Cholage aliwataka vijana wa CCM na vijana wote kwa jumla, kujiepusha na tabia ya kulalamika waliyonayo baadhi yao, badala yake wawe mstari wa mbele kukosoa katika njia zinazostahili na kisha kuonyesha njia wanazoona zinafaa kutumika katika utatuzi wa changamoto wanazoziona.

NSSF YACHANGIA MILIONI 100 MFUKO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZANZIBAR

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar (SMZ), Dk. Mohamed Shein akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa kutokana na kutambua mchango wa shirika hilo wa kuchangia sh. milioni 100 wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, uliokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo. Hafla hiyo ilifanyika mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa tatu kushoto), Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (wa pili kushoto) wakiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kulia), Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (katikati), wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar, iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko huo. 
Rais Dk, Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mashirika na Taasisi mbalimbali zilizochangia Mfuko wa Uwezeshaji Zanzibar.

WAWANAKE mkoani Iringa watakiwa kuzitambua haki zao

0
0
WAWANAKE mkoani Iringa wametakiwa kuzitambua haki zao sambamba na sheria za utawala bora ndani ya jamii katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika masuala ya utawala na mifumo ya maisha ihusuyo tamaduni mbalimbali zinachochangia kuchochea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi yao.
Hayo amesema Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (RUCO) Dk. Cephas Mgimwa wakati wa mafunzo ya juu ya haki za wanawake yaliyoandaliwa na Kitengo cha Haki za Binadamu na Utawala bora wa chuo hicho kwa wanawake wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa chuoni hapo.
Amesema kuwa wanamke anapaswa kupewa nafasi za kutoa michango yao katika maamuzi mbalimbali ndani ya jamii ikiwemo masuala ya ndoa, umiliki wa mali na masuala ya mirathi.
Amesema mafunzo hayo ya utawala bora yamelenga kuwajengea uwezo wanawake kufikia mifumo mbalimbali ya mahakama ili kupata msaada wa kisheria kwa lengo la kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake zikiwemo kupigwa, kubakwa, kuachika (talaka) na kunyimwa mirathi kutokana na baadhi ya mila potofu katika baadhi ya makabila.
Mgimwa amesema kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii nyingi za Kitanzania hasa watoto na wanawake walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa na kwa kukosa ufahamu wa sheria na haki za binadamu wengi wao wameshindwa kupeleka malalamiko yao sehemu husika.
Kwa upande wake Mhadhiri na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa chuo hicho Dk. Mary Livera amesema binadamu wote ni sawa na hakuna tofauti ya mwanamke na mwanaume katika kupata haki za msingi za binadamu kila mmoja anastahili kupata haki katika huduma za mifumo ya sheria katika mahakama.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images