Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

QNET KUDHAMINI WACHEZAJI CHIPUKIZI WA KIAFRIKA KUHUDHURIA SHULE YA MPIRA WA MIGUU YA CITY FOOTBALL ACADEMY

$
0
0
QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ambayo ni mshirika rasmi wa Timu ya mpira wa miguu ya Manchester City, Ikiwa kama sehemu ya ahadi yake ya kuendeleza vipaji na kama namna ya kampuni kurudisha kwa jamii, imedhamini wachezaji watatu chipukizi wa kiafrika kuhudhuria mafunzo ya mpira wa miguu ya jijini Manchester (City Football Language School in Manchester) .

 Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ya Manchester ni kozi ya wiki mbili ya mpira wa miguu na mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa wachezaji chipukizi (vijana). Kozi hii ilianza tarehe 28 Julai na itakamilika tarehe 12 August mwaka 2019. 

Wachezaji hao chipukizi walichaguliwa kutoka katika mchakato wenye ushindani mkubwa nchini Ghana, Cameroun na Ivory Coast, na ni kozi ambayo haina gharama yoyote kwa wachezaji hawa walio chaguliwa. 

Shule ya Lugha ya Mpira wa Miguu ni kozi ya lugha ya kiingereza na mpira wa miguu yenye hamasha kwa wachezaji chipukizi wenye umri wa kati ya miaka 12-17, ambayo inafanyika katika viwanja vya mafunzo vilivyoko huko katika jiji la Manchester. Wachezaji chipukizi waliochaguliwa wanapata fursa ya kupata falsafa ya mafunzo na mbinu za mpira wa miguu za manchester city kupitia katika vipindi vya mafunzo ambavyo vinaongozwa na makocha wa mpira wa miguu wa jiji la manchester. 

 Vile vile wanapata fursa ya kuendeleza uwezo na ujuzi wao wa kutumia lugha ya kiingereza kupitia majadiliano katika vipindi vya ulimwengu wa mpira (the world of football) kutoka kwa walimu wa vituo vya mafunzo ya lugha vya British Study Centres 

Wachezaji hao chipukizi wanajifunza na kupata mafunzo nyumbani au katika makao makuu ya machester city katika kitovu cha campus ya Etihad, sehemu ambayo watakuwa na nafasi ya kutumia miundombinu bora. Mafunzo ya Mpira wa miguu yenye ubunifu wa kiwango cha juu na Mtaala wa Lugha ya Kiingereza vimeandaliwa kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza uwezo wa kujifunza nje na ndani ya uwanja, ikiwa inagusa maeneo ya msingi ya maisha ya mtaalamu wa mpira wa miguu. 

Zaidi ya kutambuliwa na Shule ya Lugha ya kiingereza ya British Council, kozi hii vile vile inatambuliwa na Eaquals ambao lengo lao ni kuthibitisha kwamba viwango vya juu katika kufundisha lugha na mafunzo vinafikiwa duniani kote. 

Akiongelea kuhusu fursa hiyo, Bwana Biram Fall; Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara alisema: "QNET inaendelea kuwekeza katika kuendeleza na kukuza vipaji katika ngazi zote. Udhamini wa Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester City kama mshirika wa mauzo ya moja kwa moja ni moja kati ya majukumu yetu katika mpira wa miguu na ari ambayo mpira huo unaambatana nao duniani kote. 

Mchezo wa mpira wa miguu unaunganisha watu kutoka katika asili na maeneo mbalimbali. Mpira wa miguu vile vile unahamasisha kufanya kazi kwa pamoja kama timu, kuwa na ari ya timu, kufanya kazi kwa nguvu na hamasa. Hizi ni baadhi ya tunu za msingi za QNET kama biashara." 

Katika Afrika, QNET ni mshirika wa mauzo ya moja kwa moja Ligi ya mabingwa CAF, Kombe la Shirikisho la Total CAF na Kombe la Total CAF Supa Cup (Total CAF Champions League, Total CAF Confederation Cup and the Total CAF Super Cup) 

QNET inaendelea kupanua uwepo wake katika sehemu mbalimbali katika bara la Afrika, huku ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kuwasaidia kubadilisha maisha yao kuwa bora zaidi. Mbali na ushirika katika michezo, QNET vile vile ni kampuni ambayo imewekeza katika kuwajibika kwa jamii, kurudisha na kutoa kwaajili ya manufaa ya jamii na jambo hili linafanyika katika maeneo yote ambako QNET inaendesha shughuli zake. 

 Katika mwezi Novemba mwaka 2018, Kampuni ya QNET ilitunukiwa tuzo ya e-Commerce CSR Company kuwa ni kampuni bora ya biashara ya mtandao kwa mwaka huo, ambayo ilitolewa na Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirka kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for Corporate Social Responsibility West Africa.)


BAKWATA SINGIDA WAMPA POLE RAIS MAGUFULI KATIKA SWALA YA EID AL-HAJI

$
0
0

 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami, akiongoza kuomba dua katika Swala ya Eid Al-Haji iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa leo. 
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami (kulia), akiongoza kuomba dua katika Swala ya Eid Al-Haji iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa leo. Kushoto  ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau.
 Sheikh Shabani Mkanga akisoma hutuba katika swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
 Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
 Wanawake wa Kiislamu wakiwa kwenye swala hiyo.
 Watoto na wakishiriki na wazazi wao katika swala hiyo.
 Dua ikifanyika.
swala ya Eid -Al- Haji baada ya kumalizika

Na Dotto Mwaibale, Singida

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)  Mkoa wa Singida limetoa pole kwa Rais Dkt.John Magufuli kufuatia msiba wa watu 71 waliofariki kwa ajali ya kuungua moto mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.

Pole hiyo kwa Rais imetolewa na Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Burhan Mlau katika swala ya Eid- Al-Haji iliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa.

"Tunampa pole Rais wetu kwa msiba huu mkubwa tulioupata pamoja na wafiwa na tunawaombea majeruhi wote wapate nafuu waweze kurejea katika shughuli za ujenzi wa taifa" alisema Mlau.

Mbali ya Rais Magufuli wengine waliopewa  
pole hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe pamoja na wananchi wote wa mkoa huo na kuwa Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa.

Katika swala hiyo Mlau aliwataka Waislamu wa mkoa huo kuwa kitu kimoja na kuondoa utengano kupitia taasisi zao mbalimbali badala ya kutengana.

"Nawaombeni ndugu zangu waislamu tuendelee kushikamana na kupendana kupitia taasisi zetu jambo ambalo litadumisha uislam wetu na kumpendeza mwenyezi mungu" alisisitiza Mlau.

Katika kusherehekea sikukuu hiyo Mlau aliwaomba waislam wa mkoa huo kusherehekea kwa utulivu  na amani huku wakiwangalia watoto wao kwa ukaribu.

RAIS WA AFRIKA KUSINI KUTUA NCHINI JUMATANO,KUPOKELEWA NA RAIS DKT MAGUFULI.

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosa atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wa wakuu  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia Agosti 16, ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao
kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda

SADC YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI UJENZI WA MRADI MKUBWA WA UMEME RUFIJI,

$
0
0
Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),kuhusu uboreshaji wa miundombinu hasa kwa nchi wanachama wa SADC,Makoena amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzindua ujenzi wa mradi mkubwa uzalishaji wa umeme mtoto Rufiji,amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. Picha na Michuzi Jr.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), ,Calicious Tutalife akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari za SADC katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Kuhusu uwezeshaji wa biashara huria sambamba na uwepo wa upatikanaji wa ushindani na maendeleo ya Viwanda anuai,kuongezeka kwa uwekezaji wa viwanda na tija,kufuata ubora na viwango vilivyowekwa Kimataifa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),
Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Viwanda katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC),Calicious Tutalife,Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano- SADC Barbara Lopi na Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena .
 
Wanahabari wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo 



Ujenzi wa mradi wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia. 

Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar  leo na Wanahabari , Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena  amesema mradi huo mkubwa unaojengwa nchini ni wa kipekee, ambao unasimamiwa moja kwa moja na Serikali na unagharamiwa na fedha za ndani. 

“Mradi huu mkubwa wa Rufiji ni jambo la kujivunia, sisi SADC tunajivunia na si kwa SADC tu, lakini pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Mokoena amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo mkubwa wa umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi za SADC huku akisema SADC inamuunga mkono katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa umeme. 

Amesema mradi huo unaonesha unatoa funzo kwamba uongozi unahusika katika kuhakikisha miradi yenye tija inasimamiwa kwa nguvu zote ili kuzinasua nchi zetu katika matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa uwezo wa ndani. 

Mokoena amesema kutokana na uhaba wa nishati unaozikabili nchi nyingi wanachama wa SADC, juhudi za ziada zinahitajika kuboresha upatikanaji wa nishati, ambayo ni muhimu katika kutimiza malengo ya uwekzaji katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa. 

Amesema miongoni mwa mikakati muhimu ya SADC kwa sasa ni kuhakikisha kuwa na uhakika wa nishati rahisi, yenye uhakika, gharama ya chini, kupitia mpango maalumu uliowekewa ukomo wa mwaka 2027.

NMB YATOA MISAADA YENYE THAMANI YA MILLIONI 50 KWA SHULE NA VITUO VYA AFYA

$
0
0
Benki ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya zaidi ya sh 50 milioni kwaajili ya kusaidia sekta za afya na elimu katika wilaya za Musoma na Butiama mkoani Mara. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo meneja wa NMB kanda ya ziwa Agustino Abraham alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo nikutaka kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii hususan katika sekta ya elimu na afya. 

Alisema kuwa benki yake imeamua kusaidia sekta hizo hasa ikizingatiwa kuwa serikali ya awamu ya tano ina sera ya uchumi wa viwanda na kwamba sera hiyo haiwezi kufanikiwa endapo sekta za afya na elimu hazitakuwa imara. 

Alisema kuwa kutokana na umuhimu wa sekta hizo katika ukuaji wa uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla benki yake imekwisha tumia zaidi ya sh 550 milioni kuboresha sekta hizo nchini kati ya sh 1 bilioni ambazo zimetengwa na NMB kwaajili ya kutoa msaada katika sekta hizo mwaka huu. 

Alisema kuwa msaada uliokabidhiwa ni pamoja na madawati , vitanda kwaajili ya wagonjwa na vingine kwaajili ya akinamama kujifungulia pamoja na mabati huku akisema kuwa msaada huo itanufaisha shule tatu za Msingi na tatu za sek9dari pamoja n.a. vituo vitatatu vya afya katika wilayani Musoma na Butiama.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima aliishukuru benki hiyo ambapo alisema kuwa serikali imepanga kuboresha sekta za afya na elimu lakini juhudi hizi zinahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha. 

Malima alisema kuwa pamoja na kupokea msaada huo lakini serikali mkoani Mara bado inahitaji msaada na ushirikiano mkubwa kutoka kwa benki hiyo ili kuweza kuboresha mazingira ya elimu hususuan kwa watoto wa kike.

Alisema kuwa kutokana na mkoa wa Mara kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili , serikali mkoani humo imepanga kujenga makambi maalum maarufu kwa jina la nyumba salama kwa ajili ya kuwahifadhi watoto wa kike Ile waweze kuepukana na vitendo vya ukatili ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekuwa vikisababisha watoto wengi wa kike kuacha masomo na hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao za elimu.

Malima pia ameitaka benki hiyo kusaidia katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia mfumo wa NMB foundation kwa maelezo kuwa sekta ya kilimo ikiimarika ni dhahiri kuwa umasikini katika jamii utakuwa umetokomezwa na hivyo kufikia lengo la serikali la kuboresha maisha ya watanzania.

Akizungumza is niaba ya walimu walionufaika na msaada huo, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Buhare iliyopo manispaa ya Musoma, Jonas Zakayo alishukuru NMB kwa msaada huo ambao alismea kuwa uatsaid8a katika kuboresha elimu na taaluma katika shule hizo.

Alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha elimu lakini bado zipo changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa kushirikiana na wadau ili.elimu iweze kutolewa katika mazingira mazuri kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima (wa pili kulia),Katibu Tawala wa mkoa huo Caroline Mthapula (kulia) wakipokea moja ya madawati zilizotolewa na NMB kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa wa NMB Abraham Augustino (wa pili kushoto) na Meneja wa tawi la NMB Musoma Sebastian Kayaga (kushoto) , kwenye hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Buhare. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu mkoani Mara.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhare, wakibeba viti baada ya kukabidhiwa na Benki ya NMB, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh50 milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima (kulia) akipokea moja ya vitanda vya kawaida vya hospitali kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa wa NMB Abraham Augustino, kwenye hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Buhare. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhare wakijisomea kipeperushi cha Benki ya NMB shuleni hapo wakati wa hafla ya kupokea msaada. Benki hiyo imetoa msaada wa Sh 50Milioni ikijumuisha viti na meza 300 kwa ajili ya Shule sita, mabati 222 kwa ajili ya shule moja, vitanda vya kujifungulia, mashuka na vitanda vya kawaida vya hospitali kwa ajili ya vituo vya afya vitatu vyote mkoani Mara 


MKUTANO WA SADC NGAZI ZA MAWAZIRI KUENDELEA KESHO

$
0
0
Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuanza kufanyika jumanne ya Agosti 12,2019 ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi za Mawaziri.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa pikipiki mpya zinazotarajiwa kutumiwa katika mapokezi ya viongozi na wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa SADC unaoendelea Jijini Dar Es Salaam,waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema serikali imekuwa ikiendelea na maandalizi mbalimbali ya mapokezi ya viongozi hao ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki achilia mbali hotel watakazofikia viongozi hao.

Aidha Prof. Kabudi kwa niaba ya serikali,ameeleza kuridhishwa na kufurahishwa kwa namna vyombo vya habari Nchini vinavyoripoti kizalendo Mkutano unaoendelea wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jambo ambalo limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu SADC na kuvitaka kuendelea kufanya hivyo katika masuala yote yanayohusu maendeleo ya nchi.

Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Denmark Nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet.

Katika mazungumzo yao Prof. kabudi amemkaribisha Balozi huyo mteule nchini na kumhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini huku Balozi Mteule Mette Norgaard Dissing-Spandet akiipongeza serikali kwa mageuzi ya haraka inayoyafanya ili kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuongeza uwajibikaji serikalini.

PROFESA KABUDI APOKEA NAKALA YA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA BALOZI MTEULE WA DENMARK NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anasalimiana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini, Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akiwatambulisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi baadhi ya maafisa aliongozana nao,wakati alipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhi nakala za hati za utambulisho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet. Walioko pembeni ni baadhi ya wakurugenzi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.

Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi nakala za hati za utambulisho. Tukio hilo limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet pamoja na Wakurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw Jestas Nyamanga na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Jestas Nyamanga wakipunga mkono kuagana na Balozi Mteule wa Denmark hapa Nchini,Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet

PROFESA KABUDI AKAGUA PIKIPIKI ZA KUONGOZEA MISAFARA YA VIONGOIZI WAKUU WA NCHI ZA SADC MKUTANONI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anashuhudia namna mojawapo ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam,Tanzania ikiunganishwa. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa Ikuli  Bw. Zuberi Kachingwa.
Baadhi ya pikipiki mpya zitakazotumika katika mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam zikiwa tayari kwa mapokezi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anajaribu moja ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu Bw. Zuberi Kachingwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa anajaribu moja ya pikipiki mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya mapokezi na kuongoza misafara ya viongozi,Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu Bw. Zuberi Kachingwa.

World Economic Form 2017 2018 Scorecard

Siwezi kuwa na amani moyoni huku mnalia -BITEKO

$
0
0

Na Issa Mtuwa “WM” Nanyumbu Mtwara
"Sikuzote katika sehemu ya maisha yangu nikiwa kama Waziri wa Madini, hakuna kitu kinachonisononesha na kunikosesha amani moyoni kama ninapofika mahali au kuona kwenye vyombo vya habari wananchi tena wanyonge wanalia na kunyanyasika kisa wanakosa  maeneo ya kuchimba, wanalilia leseni ama mwekezaji wana wanyanyasa wakati rasilimali hizo zinawazunguka kwenye maeneo yao..."
Haya yamesemwa na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko tarehe wakati akiongea na wananchi wa kata ya Michiga wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kufuatia ziara yake wilayani humo kukagua shuguli mbalimbali za sekta ya madini na kutatua wananchi wanamlilia na kumpigia magoti kuomba eneo baba chondechonde tunaomba tusaidie eneo lile tuchimbe.
Katika ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara Biteko amekutana na kilio cha wananchi karibu kila mahali kukosa maeneo ya kuchimba madini huku raslimali hizo zikiwa zimewazunguka.
“Mhe. Waziri kuja kwako leo tunakushukuru sana, Babaa kiliochetu sisi ni eneo la kuchimba baba tafadhali chondee tunaomba turuhusu tukachimbe, tupate riziki babaaaa, pale palipo fungiwa hata sisi tunaathirika kwa sababu palikuwa panatusaidia” alisema Mzee Faya Bozani Mussa  alipopata fursa ya kuongea mbele ya waziri Biteko.
Kufuatia kilio hicho akiwaangalia kwa huruma na kwa kuonyesha kuguswa na wananchi hao waziri Biteko papo hapo hakutaka kuwa chukuwa muda kutatua kero hiyo alitoa kauli na iliyo geuza huzuni kuwa furaha ya wananchi walio kusanyika kwa wingi katani hapo.
“Ndugu zangu, poleni sana, naumia sana moyoni kuwaona mnasononeka moyoni kwa ajili ya raslimali zinazo wazunguka. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anawapenda sana na mimi ameniteuwa kumsaidia lakini kazi yangu aliyo nituma ni kuja kutatua kero za wananchi katika sekta ya madini na ndio maana nipo hapa Michiga siku ya leo.” 
“Mimi ni mtumishi wenu, nipo hapa kuwatumikia sipo teyari kuondoka hapa huku bado machozi yakiwa yanaendelea kutiririka. Sasa nisikilizeni. Moja, naagiza Tume ya Madini ifikapo ijumaa ijayo tarehe 16/08/2019 leseni ya lile eneo iwe imeshafika kwa Mkuu wa Wilaya ili yeye na afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mtwara waje wakabidhi hiyo leseni. Pili, safari yangu nimeambatana na Mkurugenzi Ukaguzi Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga yule pale, yeye atabaki hapa hataondoka japo kesho ilibidi aondoke kwa ajili ya majukumu mengine lakini hataondoka ili yule mwekezaji wenu Arafati Mrope  amsaidie kuandaa mpango kazi wa lile eneo ili ikifika leseni kazi ianze. Dkt. Utabaki hapaa” alisema Biteko.
Maelezo hayo yaliibua shangwe, vigelegele, nderemo na vifijo kwa Wanamichiga na kusahau kilio chao.
Kufuatia kauli hiyoo Mwenye (Chief) Njawala alisimama na kuishukuru serikali na kuipongeza huku akisema kauli ya waziri imeondoa minong’ono iliyokuwa imetanda ikiwatuhumu viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa ndio waliokuwa wanawazuia wasichimbe wakati taratibu za kuchimba zilikuwa hazijazingatiwa.
“Mhe. Waziri Mimi ni Chief wa eneo hili, nakushukuru kwa kutatua tatizo hili na umeleta amani maana awali viongi mbalimbali ndio walio kuwa wanatuhumiwa kwamba ndio wanaozuia, binafsi nakushukuru sana” alisema Chief Njalawa.
Eneo  Michiga limezungukwa na madini ya Chuma eneo ambalo lilikuwa limechukuliwa na mwekezaji Arafati Omari Mrope aliekuwa anachimba na kununua madini hayo kutoka kwa wananchi na baadae eneo hilo kuzuiwa na serikali kwa kuwa waliokuwa wanafanya shuguli hizo walikuwa wanafanya kinyume cha sheria.
Kwa upande mwingine Waziri Biteko alimshukuru na kumpongeza mwekezaji Arafati kwa kwa utii kwa serikali kwani hata alipo simamishwa asiendelee na kazi ya uchimbaji wa madini hayo mpaka afuate utaratibu kwa maana apate leseni alikubali na hakuendelea huku akilipa madeni ya zaidi ya Tsh. 35,000,000/= kwa wananchi waliokuwa wanachimba mchanga wa madini ya Chuma na kumuuzia mwekezaji huyooo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alimshukuru Waziri wa Madini Doto Biteko kwa kufanya ziara hiyo na kutatua kero hiyo papo hapo bila kusubiri.
“Mhe. Waziri nakushukuru sana kwa ujio wako, na maamuzi ya papo kwa papo na hiyo ndio speed ya serikali ya awamu ya tano katika kutaatua kero za wananchi hasa katika kufanyaa maamuzi yanayogusa maisha ya wananchi  wetu moja kwa moja” alise Machali.
Kabla ya mkutano huo Biteko alikutana na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na mkuu wa wilaya Moses Machali ambapo alisomewa taarifa ya wilaya kuhusu hali ya sekta ya madini.
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (wa tatu kulia) na Mkuu wa Wilaya Nanyumbu Mhe. Moses Machali (kushoto) wakimsikiliza Bw. Arafati Omar Mrope mwekezaji wa madini ya Chuma Michiga

 
 Waziri Biteko wa tatu kulia mstari wa mbele akiangalia mchanga wenye madini ya Chuma katika eneo la Michiga wilayani Nanyumbu.
Mkuu wa Wilaya Nanyumbu Moses Machali akiongea na wananchi wa Kata ya Nanyumbu kabla hajamkaribisha wazi wa Madini Dotto Biteko kushoto kwake ili azungumze na wananchi.

DKT BASHIRU ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA MOTO MOROGORO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally akizungumza na viongozi wa CCM na wananchi katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya viongozi wilayani Meatu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally katika kikao cha ndani kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis akitoa saamu kwa niaba ya wananchi, katika kikao cha ndani cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. BashIru Ally na viongozi wa CCM ngazi ya tawi hadi Mkoa, kilichofanyika Katika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Wilayani Meatu, Agosti 11, 2019.
Kutoka Kulia Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt.Joseph Chilongani wakiwa katika Daraja la mto Sibiti.
Sehemu ya Daraja la Mto Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally, akipewa maelezo na viongozi wa Chama na Serikali wilayani Meatu na Mkoani Simiyu wakati alipotembelea daraja la Sibiti mara baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Simiyu, Agosti 11, 2019.

*************



Na Stella Kalinga, Simiyu

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally ametoa salamu za rambirambi na kuwaombea majeruhi na waliofariki katika ajali ya moto Mkoani Morogoro, huku akitoa wito kwa wananchi kuwa zinapotokea ajali wawe wepesi wa kuokoa watu na mali za waliopata ajali badala ya kukimbilia kuchukua vitu ili kuepusha madhara.

Dkt. Bashiru ametoa salamu hizo wakati akizungumza na viongozi wa CCM wilayani Meatu katika kikao cha Ndani kilichofanyika Ukumbi wa CCM Mjini Mwanhuzi Agosti 11, 2019 ambapo amewaombea marehemu wote wapumzike kwa amani na majeruhi wapate afya njema ili waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.

“Natoa pole kufuatia vifo vya wenzetu waliofariki katika ajali ya moto kule Mkoani Morogoro tuendelee kuwaombea waliotangulia mbele ya haki wapumzike kwa amani na wale majeruhi waweze kupata afya na kurejea katika shughuli za kujenga Taifa”

“Kama Mwenyekiti wetu na Rais wetu alivyosema, tunapopata majanga kama haya ya ajali ni vizuri wote tuwe wepesi wa kuokoa waliopata ajali na mali badala ya kukimbilia kuchukua vitu kuepusha madhara makubwa” alisema Dkt. Bashiru.

Akizungumza na Viongozi wa CCM wilayani Meatu, Dkt. Bashiru amewataka viongozi hao kutoa taarifa za watu wanao nunua pamba kwa njia ya Umachinga, pasipo kutumia utaratibu unaotakiwa wa kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji na ujenzi huku akiwashukuru wabunge wa wilaya ya Meatu(Jimbo la Kisesa na Jimbo la Meatu) kwa namna wanavyojitoa binafsi na kupitia mifuko ya majimbo kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Magufuli kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Draja la Sibiti ambalo ujenzi wake umerahisisha mawasiliano na utachangia katika kukua kwa uchumi wa wilaya ya Meatu, mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.

Mara baada ya kuhitimisha kikao cha ndani na viongozi wa CCM Wilaya ya Meatu, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally alipata fursa ya kutembelea na kuona ujenzi wa Daraja la Sibiti ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo alipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo linaiunganisha mikoa ya Simiyu na Singida.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amesema kutokana na ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti Halmashauri ina mpango wa kupanua stendi ya Mjini Mwanhuzi kwa kuwa magari mengi yameanza kupita Meatu kupitia daraja hilo

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AONGOZA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA SALA YA EID EL HAJJ KATIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU BETRAS ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mshauri wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Abdalla Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa Kampasi ya Bertras, kuhudhuria Sala ya Eid El Hajj.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja Chuo Cha Taifa SUZA Kampasi ya Bertars Wilaya ya Magharibi A Unguja, (Picha na Ikulu).

BAADHI ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakifuatilia hutba ya Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Kampasi ya Betras Wilaya ya Magharibi A Unguja.(Picha Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakifuatilia hutba ya Sala ya Eid El Hajj katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kampasi ya Betras Wilaya ya Magharibi Unguyja ikisomwa na Sheikh Tawaha Huein Twaha baada ya kumalizika kwa Sala hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wa Dini na Serikali wakiitikia dua ikisomwa na Kadhi Dhamana wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Sheikh Othman Haji Chum.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, akihutubia Baraza la Eid El Hajj katika viwanja vya Dole Wilaya ya Magharibi A Unguja.
KADHI Dhamana wa Wiliya ya Magharibi A Unguja Sheikh Othman Haji Chum akisoma dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Hajj iliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Kampasi ya Bertras Wilaya ya Magharibi A Unguja.(Picha na Ikulu).

SERIKALI YA TANZANIA KUIMARISHA TAFITI KWA AJILI YA KUKUZA NISHATI ENDELEVU NA KUIMARISHA TEKNOLOJIA YA MAJI

$
0
0
Serikali imeendelea kuongeza ubora wa elimu na kukuza ujuzi ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza ajira nchini. Hii imewezekana kwa kuweka sera, mifumo na miundo mbinu wezeshi kwa watanzania kuweza kupata ujuzi na umahiri unaohitajika katika kuiwezesha Tanzania kufikia malengo ya mpango wa maendeleo 2025 na malengo endelevu ya milenia.

Kauli hiyo imetolewa Jiji Arusha na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa tatu wa Kimataifa wa Nishati endelevu na Teknolojia ya maji (International Conference on Energy, Aquatech and Sustainability 2019, ICEAS) )wenye lengo la kujadili changamoto zinazokabili sekta ya Nishati hususan kukuza nishati mbadala na Teknolojia ya Miundombinu ya maji na kuja na mapendekezo ya namna bora ya kutumia rasimali zilizopo katika jamii kukuza sekta hizo. 

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inajenga uchumi wa viwanda ni kuhakikisha kuwa elimu itolewayo inakuwa bora na kuendeleza ujuzi kwa watanzania ili waweze kuongeza thamani katika mazao kutumia teknolojia ya kisasa , ambapo maji na Nishati ni maeneo muhimu katika kutekeleza hili.

"Tunataka kuona kama ni mkulima anakuwa na uwezo wa kuongeza thamani ya mazao kwa kutumia Teknolojia za kisasa na hasa kutumia tafiti zilizofanywa," alisema Waziri Ndalichako

Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ameipongeza Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kuboresha kiwango cha utafiti katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na programu wanazotoa.

"Mwaka 2017 hapa NM-AIST tumefanya uzinduzi wa vituo vinne vya umahiri vya Sayansi na Teknolojia katika elimu ya juu kwa lengo la kuhakikisha tunaboresha elimu yetu na kunakuwa na wigo mpana wa kufanya tafiti, tunaona sasa mnafanya vizuri na kuendana na moto wa Chuo ambao ni Taaluma kwa jamii na viwanda, na hata maji ya kunywa yanayotumika katika mkutano huu ni moja ya kazi za tafiti zinazofanyika hapa"aliongeza Waziri Ndalichako

Waziri Ndalichako kabla ya kutoa hotuba yake ametumia fursa hiyo kutuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ndugu jamaa na marafiki kufuatia vifo vya watanzania vilivyosababishwa na ajali ya moto jijini Morogoro Agosti 10, 2019. 

Nae Makamu Mkuu wa Chuo katika Taasisi ya Sayansi Teknolojia ya Nelson Mandela ambae pia ni Mwenyekiti Mwenza wa ICEAS Profesa Emmanuel Luoga amesema mkutano huo umewaleta pamoja wataalamu wa nishati mbadala na endelevu na watafiti kutoka nchi mbalimbali ambapo mada 37 zitawasilishwa wataalamu kutoka nchi 11 zilizoshiriki mkutano huo.

Mada zitakazojadiliwa zitajikita katika maeneo ya mabadiliko ya tabia nchi, upatikanaji wa maji, nishati mbadala na endelevu.Aidha amesema Taasisi anayoingoza itaendelea kushirikiana na taasisi na vyuo vingine kutoka ndani na nje ya nchi kufanya tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii pamoja na kuendeleza viwanda.

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela na Chuo cha Taifa cha Seoul cha Korea chini ya uratibu wa Kituo cha Umahiri ambacho kinashughulika na miundombinu ya maji na Nishati endelevu na Kituo cha umahiri cha ubunifu na Teknolojia ya Nishati na unafanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 12, 2019 katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo ya tafiti zilizofanyika kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Mkutano wa ICEAS unaofanyika katika Taasisi ya NM-AIST jijini Arusha.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Nishati endelevu na Teknolojia ya maji (ICEAS) unaofanyika NM-AIST jijini Arusha.
Baadhi wa wajumbe wa Mkutano wa ICEAS wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Arusha.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa ICEAS mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya NM-AIST jijini Arusha

BI.MWANAMWEMA SHEIN ASISITIZA SUALA MATUNZO KWA WAZEE NA WATOTO

$
0
0

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama
Mwanamwema Shein amesema suala la matunzo ya wazee na ulezi wa
watoto linaendeana na utekelezaji wa Sera na Ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).

Amesema hayo katika hafla ya utoaji wa zawadi ya sikukuu ya Eid el
Hajj kwa wazee na watoto wanaoishi katika nyumba za Wazee Welezo
na Sebleni pamoja na vituo vya kutunzia watoto vya SOS na Mazizini,
alizozianda kwa kushirikiana na na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Asha Suleiman Idd.

Akizungumza kwa niaba ya Mama Mwanamwema, Waziri wa Wizara ya
Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake wa watoto Moudline Castico
alisema katika kufanikisha malengo hayo Serikali inatumia zaidi ya
shilingi Milioni 200 kwa mwezi, ikiwa ni malipo ya Pensheni jamii kwa
wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

Sambamba na hilo, alisema Serikali inaendelea kuyafanyia matengenezo
majengo ya makaazi ya wazee wasiojiweza ili kuleta ustawi bora wa
maisha yao, pamoja na kuwapatia huduma bure za afya ikiwa ni
kuthamini mchango mkubwa walioutowa wakati wa ujana wao.

Aidha alisema Serikali inakusudia kuifanya sheria dhana ya Pensheni
jamii, ili kuepuka athari za mabadiliko ya uongozi hapo baadae.
Alisema viongozi hao wameamuwa kutowa zawadi hizo ili kuhakikisha
wazee na watoto hao wanafurahi na kujumuika pamoja na wananchi
wengine.

Waziri Castico, aliwataka wazee hao kupitia sikukuu hiyo kuendelea
kuliombea dua Taifa, ili liweze kuepukana na athari zitokazo na majanga
mbali mbali.

Aidha, aliwataka wazazi na walezi kuzingatia malezi bora na maadili ya
ya watoto wao kwa kujiepusha na vitendo vya kikatili na udhalilishaji.

Alisema tukio la hivi karibuni la utupaji wa mtoto Kisiwani Pemba na
hatimae kuokotwa na mbwa, linathibitisha kwa kiasi gani jamii isivyojali
na kuthamini malezi na mtunzo ya watoto.

Alieleza kuwa Serikali imefanya juhudi kufanikisha upatikanaji wa
Mashine ya uchunguzi wa Vinasaba (DNA) ili kukabiliana na wimbi la
matukio mbali mbali ya udhalilishaji.

Mapema, Mkurugenzi wa kituo cha Kulelea watoto cha SOS, Asha Salim
aliwashukuru viongozi hao kwa muendelezo wao wa kila mwaka na
kuwatakia kheria na afya njema katika amisha yao.

Alisitiza umuhimu wa wazazi na walezi katika utunzaji wa watoto wao na
kuviomba vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na taasisi nyengine
zinazohusika na haki za watoto kuwachukulia hatua wote watakaobainika
kuhusika na vitendo vya udhalilishaji na utupaji watoto.

Nae, mtoto Salama Abdalla Ali wa kituo cha kulelea watoto Mazizini,
kwa niaba ya watoto wenzake aliwashukuru viongozi kwa imani na

mapenzi makubwa kwao na kuwakumbuka mara kwa mara, hatua
aliyosema inawapa faraja.

NAIBU WAZIRI KANYASU AIAGIZA TFS IDHIBITI WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI KUPANUA MAENEO YA UCHIMBAJI KATIKA SHAMBA LA MITI LA BIHARAMULO-CHATO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mataba ndani ya Shamba la miti la Biharamulo- Chato linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) kuhusu umuhimu wa kufuata sheria na taratibu za kuchimba madini ndani ya Hifadhi hiyo katika mkoa Geita.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ambao wanaendesha shughuli zao za uchimbaji madini katika Shamba la miti la Biharamulo-Chato wakinyoosha mikono juu ikiwa ni ishara kukubali maagizo aliyayatoa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuwa wanapaswa kufuata taratibu na sheria za uhifadhi wakati wanapochimba madini ndani ya hifadhi hiyo ya Misitu mkoani Geita.


Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa madini Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mataba ndani ya Shamba la miti la Biharamulo- Chato linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) kuhusu umuhimu wa kufuata sheria na taratibu kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri Mhe, Kanyasu kuzungumza nao.


Baadhi ya Wachimbaji wadogo wa madini ambao wanaendesha shughuli zao za uchimbaji madini katika Shamba la miti la Biharamulo-Chato wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuhusu umuhimu wa kuunda vikundi vya wachimbaji madini ili serikali iweze kuwatambua na wawe na leseni na kisha waombe kibali kutoka TFS.


Mkuu wa wilaya ya Chato. Eng. Mtemi Msafiri akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mataba ndani ya Shamba la miti la Biharamulo- Chato linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) kuwa hakuna Wawekezaji watakaowasumbua wakati wa kuchimba madini yao kwa sasa hadi pale trakapowapa taarifa rasmi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akizUngumza na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wa kanda ya Ziwa wanaosimamia Shamba la Miti la Biharamulo- Chato kabla ya kutembelea eneo la Mataba ambako Wachimbaji wa madini wamezuiwa kuanzisha makazi mapya pamoja na kuongeza maeneo ya uchimbaji mbali na yale waliyopo kwa sasa katika mkoa wa Geita.


( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)


**************



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kupitia Menejimenti ya Shamba la Miti la Biharamulo- Chato mkoani Geita idhibiti upanuzi wa Uchimbaji madini unaofanywa na Wachimbaji wadogo nje ya yale maeneo ambayo yanatambulika kwa shughuli hiyo katika Shamba hilo.

Aidha, Mhe.Kanyasu ameiagiza TFS idhibiti uanzishwaji wa makazi mapya pamoja na ukataji ovyo wa miti unaoendelea hadi pale Kamati ya Mawaziri nane itakapotoa ripoti iliyokuwa imeundwa na Rais John Pombe Magufuli kufuatia maombi yaliyokuwa yamewasilishwa na wilaya ya Chato kupitia Mbunge wao, Dkt. Medard Kalemani ya kuomba ardhi yenye ukubwa wa hekta 25 nje ya hifadhi hiyo ili kuwawezesha Wachimbaji hao kuanzisha makazi yao ya kudumu.


Hatua hiyo inakuja kufuatia uwepo wa leseni saba zilizotolewa na Wizara ya madini na kati ya hizo saba ni leseni moja tu ndo ambayo imeshalipiwa kibali cha kufanya shughuli hiyo ndani ya Shamba hilo

Agizo hilo amelitoa leo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wapatao 2000 katika eneo la Matabe ndani ya Shamba hilo, na kuwataka Wachimbaji hao wafuate sheria na taratibu zinazotakiwa za kuchimba madini ndani ya shamba hilo.

Katika shamba hilo Wachimbaji wadogo wamekutwa wakiendelea kuchimba dhahabu katika eneo la Matabe, Ilyamchele na Nyantimba ambapo wengi wao wakiwa hawana leseni wala kibali cha kuchimba kutoka TFS.


Amewataka Wachimbaji hao wajiunge katika vikundi visivyopungua watu watano ili waweze kukidhi vigezo vya kupewa leseni na badaye 
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) itoe kibali cha kuwawezesha kufanya tathmini katika maeneo ya leseni hiyo.


Amesema kitendo cha Wachimbaji hao kukosa vibali vya kuchimba madini ndani yua Shamba hilo kunaikosesha serikali mapato kwa vile hawatambuliki.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewaonya wachimbaji hao kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya shughuli za machimbo pasipo kuomba kibali kutoka TFS

” Tutakapokubaini unakata miti kwa ajili ya machimbo tutachukua sheria kali dhidi yako kwa kulipa faini au jela miaka miwili” alilisitiza Kanyasu.

Kwa upande wake Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt.Medard Kalemani amewaeleza Wachimbaji hao kuwa nia ya serikali sio kutaka kuwafukuza ila inawataka wafuate sheria na taratibu ili waweze kutambulika na serikali


” Serikali inataka ninyi Wachimbaji wadogo mnufaike wakati huo huo Serikali nayo inufaike hivyo lazima mjiunge kwenye vikundi ili mtambulike kisheria.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhandisi.Mtemi Msafiri amewaonya Iponya Nybihabi wanaodai kuwa wao ndo wamiliki wa leseni waache kuwasumbua Wachimbaji wadogo kwani ofisi yake haiwatambui

Kufuatia malalamiko mengi kutoka Wachimbaji wadogo kuwalalamikia Wachimbaji hao Wakubwa, Mkuu wa wilaya hiyo alilazimika kumuamuru Mkuu wa Polisi kuwakamata Wachimbaji hao wakubwa na kisha kuondoka nao.

Naye ,Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo, Emanuel Juang amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa licha ya kusumbuliwa mara kwa mara na Wachimbaji Wakubwa katika eneo la Mataba lakini wapo tayari kufuata sheria na taratibu zinazotakiwa ikiwemo suala kununua miti kwa TFS kwa ajili ya uchimbaji madini.

Waislamu Tabora Wafanya Dua Kufuatia Vifo vya Watu 70 Waliokufa Ajali ya Moto Mkoani Morogoro.

$
0
0

Na, Editha Edward-Tabora 

Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Tabora leo wameungana na waumini wengine ulimwenguni kote kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha na kufanya Dua Kufuatia Vifo vya Watu zaidi ya 70 waliokufa kwa ajali ya Lori la mafuta kuwaka moto mkoani Morogoro na kuwaombea Majeruhi 46 wa ajali hiyo 

Katika Ibada hiyo muhimu iliyohudhuriwa na waumini wa kiislamu katika kwanja cha Alli Hassan Mwinyi, Sheikh mkuu wa Tabora Alhaj Ibrahimu Mavumbi akahudhurisha salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa wafiwa na majeruhi wa ajali ya moto Mkoani Morogoro 

"Msiba huu ni wa kitaifa umepunguza nguvu Kazi kwa jamii wote hawa walikuwa na ndoto zao lakini Mauti imewakatiza wengine wemeacha watoto, Wajane niwape pole wale wote waliofikwa na msiba huo na tudumu katika Imani " Amesema Mavumbi

Pia Sheikh Mavumbi amewataka wananchi wote kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nchini kote Kushiriki uchaguzi huo kwa Amani na utulivu Ili kuweza kupata viongozi kwa Amani 

Kwa upande wao viongozi wa Amani akiwemo zinduma kambwanga ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi ya kina mama wa kiislamu Mkoani Tabora amewataka waumini wenzake wadumishe Amani na umoja katika nchi 

"Tunapoona tukio kama hili ni vyema kuchukua tahadhari siyo kukimbilia eneo la tukio siyo la kwanza kutokea Mungu awatie nguvu wale wote waliofikwa na msiba "Amesema Zinduma

Hata hivyo katika suala hiyo waumini wa madhehebu mbalimbali Wametakiwa kumcha Mwenyezi Mungu na kutii Sheria za nchi kama vitabu vitakatifu vinavyofundisha Maadili Mema.
 Pichani ni Sheikh mkuu wa Mkoa wa Tabora Alhaj Ibrahimu Mavumbi Akiongea na waandishi wa habari.
 Pichani ni waumini wa dini ya kiislamu  mkoani Tabora wakiswali dua kuadhimisha sikukuu ya Eid Al Adha katika kiwanja cha Ally hassan Mwinyi.

Mwenge wa Uhuru watua Dodoma, kukagua miradi 47 ya Maendeleo

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

MKOA wa Dodoma umepokea rasmi Mwenge wa Uhuru 2019 unaotarajia kutembea umbali wa kilomita elfu 1,397 na kukagua miradi 47 yenye thamani ya shilingi bilioni 26.1.

Mwenge huo umepokelewa katika viwanja vya shule ya sekondari ya Pandambili wilayani Kongwa kutoka kwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Noel Kazimoto kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Kebwe S Kebwe.

Akipokea mwenge huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Dokta Binilith Mahenge, Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Maduka Kessy amesema kati ya miradi inayotembelewa, miradi 19 itawekwa mawe ya msingi.

Aidha miradi 19 itazinduliwa na miradi 9 itatembelewa katika wilaya 7 na halmashauri 8 zilizopo mkoani humo ambapo kwa kuanza unaanzia wilaya ya Kongwa.

Maduka amesema kiasi cha fedha kinachogharamia miradi hiyo kimetoka kwa serikali shilingi bilioni 19.3, halmashauri shilingi bilioni 477.5, wafadhili shilingi bilioni 1.4 na wananchi shilingi bilioni 5.2.

Miradi hiyo inayotembelewa imekidhi kauli mbiu ya Mwenge 2019 isemayo maji ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katika mkoa wa Morogoro Mwenge wa Uhuru 2019 umetembea kilomita elfu 1,520 na kukagua miradi 48 yenye thamani ya shilingi bilioni 81.5 iliyopo kwenye wilaya 7 na halmashauri 9 zilizopo mkoani humo.
 Mwenge wa Uhuru Umbria mkoani Dodoma na kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Maduka Kessy kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dk Binilith Mahenge ukitokea mkoani Morogoro.
Kaimu Mkuu wa Morogoro, Noel Kazimoto (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy (kulia) Mwenge wa Uhuru baada ya kutua mkoani humo

Naibu Waziri Ikupa achangia mabati 10 kwa ajili ya uwezeshaji wa Elimu bure

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa amesema watu wanaombeza na kupinga jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli watakuwa wanapingana na Mungu Mwenyewe.

Mhe Ikupa amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.

Amesema mambo Mengi yaliyokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa Chama Cha Mapinduzi yametekelezwa na kubainisha kuwa mtu ambaye hajaguswa na jitihada za Rais Magufuli atakuwa Muongo.

Aidha ametaja nyanja ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi uimarishaji wa miundombinu na umeme, barabara, reli na usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.

Awali akizungumza katika kikao hicho,mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule amesema tangu wanaingia madarakani waliahidi mambo matatu ikiwemo kujenga UWT yenye upendo,umoja na mshikamano na kupitia mikutano mbalimbali tuliyoifanya hilo wamefanikiwa.

“Kwa sasa tumebaini na kushughulikia upatikanaji wa viwanja vya uwekezaji,na hili tumelifanya kila wilaya nia yetu tujitegemee na tusiwe tegemezi,”alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku akiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo.
 Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akizungumza na wajumbe  wakati wa  kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma

Wilaya ya Kongwa yapongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mwenge wa Uhuru umekagua miradi saba ya kimaendeleo wilayani Kongwa mkoani Dodoma na kuipitisha yote huku Mkuu wa Mbio hizo za Mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally akimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Deo Ndejembi kwa namna alivyoisimamia na kumtaka kuongeza juhudi zaidi katika kuwatumikia wananchi wake.

Miradi hiyo saba iliyokaguliwa imagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.3 ambapo ipo miradi ya Maji, Hospitali, miradi ya Maendeleo ya vijana, Shule ya Sekondari pamoja na kiwanda cha kutengeneza maziwa.

Aidha Kiongozi huyo wa Mwenge alimtaka DC Ndejembi kuwachukulia hatua watumishi ambao wamekua wakikwamisha juhudi za Mhe Rais Magufuli za kuwatumikia Watanzania na kuagiza kuchukuliwa hatua kwa Mhandisi wa Wilaya hiyo, Christian Mlay ambaye aliyedharau ujio wa Mwenge huo.

" Nakuahidi nitamsaka popote alipo mhandisi huyu na nitamchukulia hatua za kinidhamu na kisheria kwa sababu kitendo cha kudharau Mwenge huu wa Uhuru ni kumdharau pia Rais wetu Dk Magufuli, " amesema DC Ndejembi.
Mhandisi huyo Christian Mlay alipaswa kuwepo katika eneo la ujenzi wa madarasa mawili aliyosimamia lakini alipotafutwa hakupokea simu na baadae hakupatikana kabisa. 

Akizungumza kabla ya kuzindua madarasa hayo Mkongea alisema hiyo ni dharau kubwa kwa Rais Dokta John Magufuli na dharau kwa Mwenge uliosisiwa na muasisi wa Taifa hili baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

"Nimesikitishwa sana kwa kitendo hiki, mkuu wa wilaya kwa mamlaka uliyonayo hao walioonyesha dharau wachukulie hatua kali ndani ya siku 4 kwa maandishi,

"Nilishatoa taarifa nilipofika tu Dodoma kwamba katika miradi yote tutakayoitembelea ni lazima wawepo wataalam na taarifa ya mradi, sasa hapa mtaalam hayupo wala msaidizi wake,"alisema mkimbiza mwenge huyo.

Akizungumza mara baada ya maelekezo hayo Ndejembi alisema ameyapokea na anayafanyia kazi ili muhusika apatikane mara moja.

Alisema mhandisi Mlay alipaswa pia kuripoti Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mwishoni mwa wiki yeye na wenzake watatu kwa kosa la kuisababishia hasara serikali kwenye ujenzi wa majengo katika shule ya sekondari ya Kongwa lakini hakufanya hivyo. 

"Wenzie waliripoti Takukuru na kwa afisa upelelezi wilaya wakalala ndani siku moja yeye hakutokea na tangu aliposikia maagizo yangu ndio hajaonekana kabisa, lakini tutamtafuta atapatikana na hatua zitachukuliwa, "aliongeza Ndejembi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika wilayani hapo kukagua miradi ya kimaendeleo
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkonge Ally akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi saba ya kimaendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru wilayani Kongwa mkoani Dodoma

JWTZ LAWAPA TAHADHALI WATAKAO VURUGA AMANI NA USALAMA WA NCHI

$
0
0
Na Editha Karlo,wa michuzi Tv,Kigoma

JESHI la wananchi wa Tanzania(JWTZ) limesema kuwa litawaadhibu wale wote watakaojaribu kuvuruga amani na usalama wa nchi na limetoa tahadhari kwa watu wote wanaotumia mapori vibaya kuacha kufanya hivyo mara moja.

Mkuu wa Brigedi ya kanda ya magharibi (202 Kikundi cha Vikosi) Brigedia Jenerali, Julius Mkunda alisema hayo mkoani Kigoma wakati akiahirisha zoezi la kijeshi la kujiweka tayari kwa wapiganaji wa jeshi kupambana adui pindi anapotokea na kusema kuwa amani na usalama wa Watanzania ni lazime upewe kiupaumbele.

katika zoezi hilo lililofanyika kwenye mapori ya wilaya za Kibondo, Kasulu na Kakonko na kutambulika kama kama Opereshini KIKAKA Brigedia Jenerali Mkunda alisema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mapori hayo, kutumika kwa shughuli za maficho ya ujambazaji, uwindaji haramu na kilimo mambo ambayo yanafanywa na wageni kutoka nchi jirani.

"Tanzania siyo shamba la bibi kwa kila anayetaka anakuja kufanya anachojisikia, hatutakubali tutawaadhibu wale wote wenye nia mbaya ya kutumia mapori yetu kwa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi yetu, lakini vinatishia amani na usalama wa raia na mali zao na kuwafanya waishi kwa woga,"Alisema Brigedia Jenerali Mkunda.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kutoka Brigedi ya kanda ya Magharibi, Kanali Wilbert Ibuge alisema kuwa mapori yote ambayo watu wanayaona nchini yana wenyewe na wenyewe ni jeshi la wananchi wa Tanzania ambao wana wajibu wa kuyatunza na kuyalinda na hivyo hakuna mtu yeyote ambaye ataingia kwenye mapori hayo akaachwa ayatumie anavyotaka.

Mkuu huyo wa mafunzo alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utimamu na utayari wa jeshi kujindaa kupambana pindi adui anapotokea na kwa sababu kwenye vita hakuna mahali pa kufanya majaribio hivyo kazi ya kuwasaka na kuwakamata wale wote ambao wataingia kwenye mapori hayo na kufanya vitendo vya uhalifu itatumika kama sehemu ya mazoezi kwa vitendo kwa wapiganaji.

Mkuu wa kikosi cha 24 KJ mkoa kigoma ambacho kimesimamia na kuratibu mafunzo hayo, Meja J.S.Luhonyva akisoma risala kuhusu mafunzo hayo alisema kuwa mazoezi hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na vijana wameonyesha kuwa tayari kukabiliana na adui pindi atakapotokea.
Meja Luhonvya alisema kuwa lengo la mazoezi hayo kwa kiasi kikubwa limefikiwa ambapo medani zote za mapambano kivita zimefanyika na vijana wapiganaji wameonyesha wako tayari wakati wowote watakapotumwa kwenda mstari wa mbele kulinda nchi yao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa kigoma,Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga Mkuu wa wilaya Kasulu, Kanali Simon Hanange alisema kuwa zoezi hilo kwao kama mkoa ni hatua kubwa kuelekea katika kuhakikisha kwamba mkoa unakuwa na amani na usalama lakini mapori yote yanatumika kwa manufaa ya Taifa badala ya watu wachache kwa maslahi yao.
Mkuu wa Brigedia ya magharibi 202KV Julius Mkunda akisoma risala yake wakati akihairisha zoezi la kujiweka tayari lililotambulika kama operesheni KIKAKA kwa wapiganaji wa jeshi pindi anapotokea adui.
Askari wakishangilia kwa morali baada ya zoezi walilokuwa wanafanya la kujiweka tayari kupambana na adui au oparesheni kikaka kufungwa leo
Askari wakiwa wanamsikiliza Mkuu.wa Brigedi ya kanda ya magharibi 202 KV Brigedia Jenerali Julius Mkunda (hayupo pichani)wakati akihairisha mafunzo ya oparesheni kikukuu yaliyofanyika kwa siku 14 kwa Wilaya za Kakoko,Kasulu na Kibondo
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images