Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 11,2019


MSD YAKABIDHI MADAWA MKOANI MOROGORO KWA AJILI YA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA LORI LA MAFUTA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa MSD Salome Mallamia na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam inayohudumia mkoa wa Morogoro Celestine Haule wakiendelea kupokea dawa zaidi za kukabidhi hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhudumia majeruhi

…………………………………………………

Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto, iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia umelenga kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.

Aidha, wajumbe hao, wamewasilisha msaada wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo.


LIVE: RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AKIWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA MOTO MUHIMBILI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AUNDA TUME KUCHUNGUZA AJALI MOTO MOROGORO

$
0
0
Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kasimu Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe wakati akifafanua jambao katika eneo la msavu mahali ilipotokea ajali ya moto.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa Akimbatana Viongozi Mbalimbali Wa Kiserikali Katika wakati alipokagua eneo la ajali Msamvu Mkoani Morogoro.
Mabaki ya Lori la mafuta lililopinduka jana asubuhi mjini Morogoro na kulipuka moto.
Wananchi waliojitokeza katika uwanja wa shule ya sekondari morogoro kwa ajili ya utambuzi wa miili ya ndugu zao waliopata ajali ya lori la mafuta lililolipuka katika eneo la Msavu.

……………………………………………………..

FARIDA SAIDY MOROGORO.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa ameunda tume itakayochunguza chazo cha ajali ya lori lililolipuka na kuwaka moto.

Tume hiyo imeundwa leo jumapili Agosti 11,2019 ili kuchunguza kama kuna mamlaka au mtu yeyote ambaye hakuwajibika vya kutosha katika kuchukua hatua kutokana na ajali hiyo na imetakiwa kukamilisha uchunguzi huo ijumaa agosti 16 mwaka huu.

‘’Ninaunda tume ianze kuchunguza kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha kufanya.’’amesema Majaliwa.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 maeneo ya , Msamvu mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya wananchi kuanza kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo..

Aidha mpaka sasa Waziri mkuu amesema kuwa watu waliofariki ni 69, na majeruhi zaidi ya 66 ambapo Mh Kassim Majaliwa amewataka wanahabri kutokutoa takwimu zisizo sahihi kwani swala hilo linawatia hofu watanzania.

‘’Naogopa msije mkaingia kwenye sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni takwimu sahihi kutoka vyombo vinavyohusika na za Mkuu wa Mkoa” Amesema Mh. Kassim Majaliwa.

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA AJALI YA MOTO MOROGORO

TessyChocolate ndani ya SADC na Billion Paints kuupendezesha ulimwengu...

MFUKO WA KILIMO WA PAMOJA MBIONI KUANZISHWA KWA NCHI ZA SADC

$
0
0
JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) imesema ipo kwenye mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa kanda kwa ajili ya kusaidia nchi wanachama wa jumuiya hiyo. 

Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2019 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa jumuiya hiyo Domingos Gove wakati anazungumza na waandishi wa habari za mikutano ya SADC inayoendelea jijini. 

“Kwa sasa tupo katika mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ambao lengo ni kuhakikisha tunasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC,” amesema Gove. 

Amefafanua katika mkakati huo pia watahakikisha kunakuwa na miundombinu itakayofanikisha nchi wanachama zinajikita kwenye kilimo kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha kwa nchi zao. 

Mkurugenzi huyo wa Kilimo,Chakula na Maliasili ameongeza kuwa kwenye mfuko huo ambao utaanzishwa kwa nchi za SADC utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la kilimo. 

Pia amesema mikakati mingine ni kuongeza ushindani na uzalishaji wa nafaka pamoja na kuhakikisha kunakuwa na sera ya kulinda usalama wa chakula. 

“Tumejipanga kuhakikisha kupitia mfuko huo wa kilimo tunazalisha chakula kwa wingi na pale ambapo nchi mojawapo itakuwa na tatizo la uhaba wa chakula basi tunasaidia kupeleka chakula kutoka kwenye nchi zenye chakula cha ziada,”amesema. 

Ameongeza vyakula ambavyo vitazalishwa pamoja na mambo mengine vitazingatia suala la lishe kuhakikisha walaji wanakuwa na afya njema na imara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo kwa nchi wanachama. 

Wakati huo huo jumuiya hiyo imeeleza namna ambavyo imejipanga kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinakuwa na miundombinu ya uhakika. 

Ambapo kwenye eneo hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC Zamarad Kawawa ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazi katika ujenzi wa miundombinu. 

“Tanzania tuko vizuri, katika eneo hilo, ukienda bandarini, viwanja vya ndege , reli, na barabara kote kumeimarika kwa kiwango kikubwa,”amesema Kawawa ambaye pia nia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO).

 Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari za SADC,kuhusu  mkakati wa kuanzisha mfuko wa kilimo wa pamoja wa kikanda ili kuhakikisha nchi hizo zinasaidiana katika chakula kwa nchi za SADC.
  Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove  akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), wanaoandika habari za SADC leo Katika moja ya Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Habari, Matangazo na Machapisho Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya SADC, Zamarad Kawawa akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari za SADC,leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar,ambapo alieleza namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyoweka mkazo katika ujenzi wa miundombinu. 
Mkurugenzi wa Kilimo, Chakula na Maliasili wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),Domingos Gove amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa kuanzishwa mfuko huo wa kilimo  ambao kwa nchi za SADC, utahakikisha kunakuwa na usambazaji wa mbegu bora zisizo na magonjwa , upatikanaji wa soko kwa malighafi zinazohusika kwenye suala la kilimo. Picha na Michuzi JR.
Waandishi wa habari wakisikiliza yaliyokuwa yakijiri  ukumbini humo.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAOMBOLEZAJI WA VIFO VYA WATU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA JALI YA LORI LA MAFUTA MOROGORO

$
0
0

WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA AJALI YA MOROGORO

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameunda tume maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 69 hadi mchana huu na wengine 70 kujeruhiwa wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka, mjini Morogoro.

“Hii tume inaanza kazi leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), Hadi ijumaa inipe taarifa yake na hata kama mimi sijawajibika initaje. Ajali ya namna hii si mara ya kwanza ilitokea Mbeya eneo la Mbalizi. Naomba niwasihi Watanzani pale gari linapoanguka tusitume kama fursa twende tukaokoe binadamu waliopo pale”.

Waziri Mkuu ameunda tume hiyo leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), wakati akizungumza na waombolezaji waliofika katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao. Niko mbele yenu nikimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli aliyenituma kuja kuungana nanyi kwenye siku hii ya huzuni”.

Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe kama Serikali ilitekeleza vizuri jukumu lake kwa sababu ajali imetokea saa mbili asubuhi katikati ya mji, hivyo tunataka kujua ajalj ilipotokea kila mmoja alitumiza jukumu lake.

Amesema ajali imetokea karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi na kuna polisi sasa je hawa wananchi waliopata ajali walienda na madumu ya kuchotea mafuta inamaana waliamka asubuhi wakijua ajali itatokea. “Najua pale ajali inapotokea trafiki wana wahi haraka hata kama kwa gari la kukodi. Watu walikuja na madumu, wengine kuchomoa betri nani aliwazuia.Je lilipoanza kuungua gari la zima moto lilikuja kwa wakati gani”.

Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe ndani ya Serikali kama wamewajibika. “Kuna vitu vingi lazima tuviangalie tujue nani hakutimiza majukumu yake. Nadhani ujumbe mnaupata si vyema tutakimbilia vitu badala ya watu. Tunasikitika sana kwa yaliyotukuta hata upande wa Serikali tunasikitika kuwapoteza Watanzania”.

Pia, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu jitihada za kuokoa waliopata majeraha kwamba zinaendelea vizuri na jukumu lao kubwa kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani na pia wawaombee wajeruhi waweze kupona.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Magufuli tayari ameshatoa kibali cha kutolewa fedha kwa ajili ya kununuliwa vifaa tiba na dawa zinazohitajika.

Akizungumzia kuhusu idadi ya vifo na majeruhi waliotokana na ajali hiyo ambayo inatangazwa kupitia vyombo mvalimvali vya habari, Waziri Mkuu amesema ni vema takwimu hizo wakaacha zikatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Stephen Kebwe.

“Kwenye vyombo vya habari tuelewane kwenye takwimu za vifo na majeruhi. Msiseme suala la takwimu anayetoa ni Mkuu wa Mkoa na matukio haya yapo chini yake. Nimeamua kusema hivi hizi takwimu zikitajwa nyinginyingi mnajenga hofu na taharuki kwa wananchi. Hili halikubaliki mkitaka taarifa mtafuteni mkuu wa mkoa”.

Wakati Huo huo, amesema Rais Dkt. Magufuli alipokea taarifa mapema ya ajali ya lori la mafuta na kusababisha vifo vya Watanzania 69, ambapo alimtaka aende mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pole kwa wananchi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla kufuati tukio hilo la kuhuzunisha.

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anawaombea marehemu na majeruhi lakini pia amawataka wafiwa na wananchi wote wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao.

“Mheshimiwa Rais amehuzunishwa sana na msiba huu ndio maana amenituma nilete ujumbe huu kwenu.Lakini pia nimekuja na salamu za pole kutoka kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Jambo hili si dogo ni kubwa kwani tumepoteza ndugu zetu wengi. Kwa idadi hii kubwa ya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki na wale waliopo kwenye maumivu si jambo la faraja”.

Waziri Mkuu amesema wananchi wasipeleke miili kwanza makaburini ili waweze kupitia na kutambua ndugu na rafiki kwa ajili ya kuwa na kumbukumbu ya kudumu. “Hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana wapo wengine mnaweza msiwatambue lakini mnaweza kutambua kwa alama. Wapo wengine walivaa bangili, heleni, mkanda havijaungua”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kama hawajawatambua Serikali imeweka utaratibu wa vipomo vya vinasaba, ambapo kumbukumbu hizo zimechukuliwa na wataalamu wetu wa afya. “Kama ukipita ukishindwa kumuona bado tunakuruhusu kukupima vinasaba na kulinganisha na vyakwako. Bado haki ya kumpata ndugu yako iko pale pale madaktari wapo, mitambo ipo tutachukua vinasaba na kuainisha tutatoa nafasi leo hadi saa 10 kufanya utambuzi”.

Amesema Serikali inaratibu vizuri jambo hilo lakini kuanzia saa 10 itaruhusu wale waliotambuliwa kuchukua mwili lakini kama hawajajipanga vizuri itauzika na kama kuna jina litaliandika na kama hakuna jina wataandika namba ya vinasaba ili kutoa fursa kwa ndugu siku nyingine waende wakapimwe na kuoneshwa kaburi la ndugu yao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mahali ambapo lori la mafuta lilipinduka na kushika moto hatimaye kusababisha vifo vya watu 69 kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro wakati alipotembelea eneo hilo, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji wakati aliposhiriki katika maandalizi ya kutambua miili na maziko ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019.
Baadhi ya waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kushiriki katika maadalizi ya kutambua miili na mazishi ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alizungumza na waombolezaji hao kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Morogoro walioshiriki katika maandalizi ya kutambua miili na maziko ya watu 69 waliofariki dunia katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kushika moto kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Alikuwa kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogelisi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WALIOLETWA KUTOKA MOROGORO NA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILIRAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WALIOLETWA KUTOKA MOROGORO NA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya Lori la Mafuta kupinduka na kuteketea kwa moto.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati alipokuwa akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto ambao wameletwa kutoka mkoani Morogoro kwa ajili ya matibabu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto ambao wamelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kusafirishwa kutokea mkoani Morogoro.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kutoka kuwajulia hali majeruhi 43 wa ajali ya moto ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga kuhusu hali za majeruhi 43 ambao wanapatiwa matibabu mara baada ya kuungua miili yao katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kitengo cha Dharura na kuelekea katika Wodi za Wagonjwa kwa ajili ya kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika wodi ya Sewahaji mara baada ya kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAZISHI YA WALIOKUFA KWA AJALI MORO

$
0
0

*Huzuni, simanzi, majonzi na vilio vyatawala mjini Morogorogo

HUZUNI, simanzi, majonzi na vilio vimetawala mjini Morogoro leo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwaakiongoza umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, mkoani Morogoro katika mazishi ya wananchi waliofariki dunia kutokana na ajali ya moto wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 71 huku wengine 59 wakijeruhiwa.

Mazishi hayo yameanza kufanyika leo (Jumapili, Agosti 11, 2019) katika eneo la makaburi la Kola Hill mjini Morogoro ambapo Waziri Mkuu amemwakilisha Rais, Dkt. John Magufuli. Ametoa pole kwa wafiwa wote na amewaomba wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.

Akizungumza na wananchi katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Msamvu mjini Morogoro iliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano waliouonesha wakati huu wa amajonzi.

Kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana saa 2 asubuhi baada ya lori lenye shehena ya mafuta ya petrol kupinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu mjini Morogoro wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki. Rais Dkt, Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kuanzia jana Jumamosi Agosti 10,2019 na bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isac Kamwelwe, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Wengine ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, viongozi wa dini na wananchi wa mkoa wa Morogoro.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole , Shukuru Fabian ambye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali, Hans Kifah ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IGP SIRRO AWASILI MKOANI MOROGORO KUWAPA POLE WAFIWA NA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA JANA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewasili katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuwapa pole wafiwa waliokuwa wamekusanyika ili kuwatambua ndugu na jamaa zao pia na majeruhi waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo. (Picha na Jeshi la Polisi)

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimpa pole moja ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea juzi eneo la Msamvu Ndege wengi katika Wilaya ya Morogoro mjini baada ya kuwasili katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Mtafungwa baada ya kuwasili eneo la tukio ilipotokea ajali ya lori lililokuwa limebeba mafuata aina ya petrol na kusababisha vifo vya watu 62 na majeruhi 72.

MBUZI 10,000 WACHINJWA KWA AJILI YA SIKUKUU YA EID MKOANI SINGIDA

$
0
0
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata ) Mkoa wa Singida, Sheikh, Burhan Mlau akiwa Machinjio ya Ng'ombe ya mkoa huo akiwa amesimama jirani na nyama ambazo zitatolewa sadaka katika kusheherekea Sikukuu ya Eid inayofanyika duniani kote kesho. 
Mratibu wa utoaji wa sadaka hiyo kutoka Taasisi ya Noor al-yaqeen Foundation ya Zanzibar, Abdul-hamid Khamis (kushoto), akizungumzia utoaji wa sadaka hiyo. Kulia ni Mratibu wa utoaji wa sadaka hiyo mkoa wa Singida, Hassan Hamad.
Pilika pilika machinjioni.
Ng'ombe wa sadaka wa Eid wakiwa machinjioni mkoani Singida wakisubiri kuchinjwa.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUZI na kondoo 10,000 wamechinjwa kwa ajili ya kitoweo cha Sikukuu ya Eid mkoani Singida.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata ) Mkoa wa Singida, Sheikh, Burhan Mlau alisema kiloweo hicho ni sadaka inayotolewa kwa ajili ya sikukuu hiyo.
" Ni kawaida kila mwaka katika sikukuu ya Eid kuchinja wanyama kama sadaka na kuwa wanyama hao hutolewa na taasisi mbalinbali za kiislam kutoka uturuki, na Misri ambao hufanya kazi ya kuchinja" alisema Mlau.

Alisema mwaka huu wamechinjwa kondoo na mbuzi 10,000 huku ng'ombe wakiwa 1300 na kuwa kitoweo hicho kinatolewa kwa jumuiya mbalimbali za kiislam mkoani humo.

Alisema sherehe za baraza la Eid mwaka huu zitafanyika katika wilaya zote za mkoa wa Singida ambazo amezitaja kuwa ni Mkalama, Manyoni, Itigi, Singida Mjini, Singida Vijijini, Iramba na Ikungi.Sheikh Mlau alitumia fursa hiyo ya Sikukuu ya Eid kuwaomba waislam mkoani humo kuwa na mshikamano na kupendana.

Mratibu wa utoaji wa sadaka hiyo kutoka Taasisi ya Noor al-yaqeen Foundation ya Zanzibar, Abdul-hamid Khamis amezishukuru taasisi za dini za mkoa wa Singida kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kufanikisha zoezi zima la kuchinja na kutoa sadaka hiyo.

Kampuni za Simu hazijatekeleza agizo za gharama za upigaji simu

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzichukulia hatua kampuni zote za mawasiliano nchini ambazo hazijatekeleza agizo la serikali la kuhakikisha gharama za kupiga simu kwa dakika kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine inakuwa Sh. 10 na Senti 40.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya uchukuzi na mawasiliano, Atashasta Nditiye wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kutoka Zanzibar Dk. Sira Mamboya. 

Alisema kuwa amekuwa akisikia matangazo ya kampuni mbalimbali za simu katika redio na televisheni ambayo yanasema kuwa kupiga simu ni Shilingi moja kwa sekunde jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

Nditiye amesema TCRA inapaswa kulifatilia suala hilo kwani gharama zilizowekwa na Serikali ni Shilingi 10 na Senti 40 kwa dakika kufanya Shilingi moja kwa sekunde ni sawa na Sh. 60 kwa dakika. 

"Mwishoni mwa mwaka jana niliutangazia umma wa Watanzania kuwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu zile gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine itakuwa ni Sh. 10 na Senti 40 lakini jambo hili wala halijatekelezeka mpaka sasa na kampuni za simu, kwahiyo nawataka TCRA wafatilie kampuni zote ambazo hazijatekeleza utaratibu huu maana vifaa vyote wanavyo," alisema na kuongeza 

"Mawaasiliano ni haki ya kimsingi ya kila mtu na tunahitaji wananchi waweze kumudu gharama za kupiga simu, natambua kuwa teknolojia hii inakua kila siku na watu ubuni vitu vipya ikiwamo wizi na ujanja ujanja ambao kiukweli TCRA wanapambana nao, ila katika suala hili la gharama kampuni hizi alijazitekeleza hivyo ni wajibu wa TCRA kulifuatilia na kuwachukulia hatua, " alisema. 

Aidha Waziri Nditiye amewataka wananchi wote nchini wanaomiliki simu za mkononi kuendelea kusajili laini zao kwa alama ya vidole. Mbali na hayo, Waziri Nditiye alisema katika wizara hiyo sekta ya mawasiliano ni ya muungano hivyo amejisikia faraja kwa waziri wa Zanzibar kuja kutembelea mamlaka hiyo kwa lengo la kujifunza vitu mbalimbali. 

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya amesema TCRA ni chombo cha muungano hivyo yeye kama Waziri ameamua kuja kujifunza na kuangalia jinsi kinavyofanya kazi. 
Amesema kila baada ya muda vikao vya baraza la wawakilishi ufanyika na kunakuwepo na maswali kuhusu TCRA hivyo kuja kwake anaamini atajifunza mengi yatakayomsaidia kuweza kujibu maswali hayo.
Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uendeshaji wa mamlaka hiyo wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia uendeshaji wa mawasiliano nchini katika Ofisi za Makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Connie Francis akizungumza kuhusiana na utendaji wa TCRA Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya na watendaji wake walipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Victor Kweka namna wanavyoangalia masafa katika gari maalum wakati waziri huyo alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa Makumbusho ya TCRA Jasmine Kiyungi wakati waziri huyo alipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

VYUO VYA UALIMU VYAAGIZWA KUZALISHA WALIMU WA FIZIKIA WENGI-DKT SEMAKAFU

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV


SERIKALI imesema kuwa walimu wa somo la Fizikia ni wachache na kutaka vyuo vya ualimu kuandaa walimu hao katika kwenda sambamba na malengo ya ya serikali.

Hayo ameseyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolijia Dkt. Evamaria Semakafu wakati wa kufunga ya kuwa na mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu lililofanyika jijini Dar es salaam,amesema kuwa walimu wa hisabati na Kemia hakuna tatizo lilopo ni walimu wa somo la Fizikia.

Amesema kuwa serikali inafanya mikakati mbalimbali katika kuhakikisha suala elimu linakwenda kutokana na mdau kutambua nafasi yake kutekeleza sekta ya elimu nchini.

Dkt.Semakafu anasema kuwa serikali iko katika mchakato wa kuwa na bodi ya walimu ambao watakuwa wasimamizi maadili na weledi wa kufanya kazi hata ikitokea kuna ukiukaji wa weledi huo kuweza kuchukuliwa hatua.

“Kuwepo kwa bodi itaondoa wale wanaokiuka maadili kutoendelea na kazi kwani wengi wamekuwa wakiuka na wakati mwingine anakwenda kuajiriwa sehemu nyingine au shule ya jirani sasa bodi itafanya kazi hiyo ni suala la muda tu na sheria katika hatua mbalimbali”amesema Semakafu.

Amesema wadau wa elimu kila mtu kutumia nafasi yake katika kupeana taarifa na sio taarifa zinaonekana mitandaoni kwa vitu ambavyo vinaweza kuzungumzika na serikal ikachukua hatua na kumaliza changamoto ambazo ziko katrika sekta ya elimu.

Aidha amesema kongamano hilo linafungua kwenda kuongeza ufanisi wa elimu katika maeneo yao ya kazi huku serikali ikichukua mapendekezo ya michango ya utoaji wa elimu kwa wanafunzi.

Amesema ADEM ifanye jukumu lao la msingi kwani wanatoka na kufanya majukumu mengine hivyo ni bora warudi kama ilivyokuwa dhamira ya uanzishaji wa hiyo ADEM.

Mwenyeki wa mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi Rais -Tawala Mitaa na Tawala za Mikoa Tamisemi) George Jidamva amesema kuwa wakiwa wasimamizielimu watafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa mkutano huo.

Amesema katika mkutano huo wamejifunza vitu mbalimbali kwani pasipo kuwepo na mikutono hiyo kuna baadhi ya vitu vinaweza visiende sawa.

Nae Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyuo Binafsi Mahmood Mringo amesema sekta ya elimu inazungumzwa na watu wasio wadau hivyo kila mtu atumie nafasi ya kuzungumza suala la elimu na sio watu wengine.

Amesema kuwa ukurasa mpya umfunguliwa katika hivyo na kuongeza nguvu katika kusukuma gurudumu la elimu. 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu akizungumza wakati wa kufunga mkutano la wadau wa Elimu ya Ualimu kuhusu usimamizi na uendeshaji bora wa Elimu ya Ualimu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Elimu ya Ualimu wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu wakati akifunga mkutano wa wadau hao uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Ualimu Augusta Lupokela akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu ambapo amesema matokeo ya Mkutano huo yatasaidia katika maandalizi ya mpango mkakati wa maboresho ya usimamizi wa mafunzo ya ualim uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyuo Binafsi Mahmood Mringo akitoa neno la wa Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu kuhusiana uwepo na ushirikishwaji wa sekta ya elimu kwa maendeleo ya Taifa uliofanyika jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Evamaria Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano wa wadau wa elimu ya ualimu baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam.

MAOFISA WA TBS WABAINI KASORO ZA UZALISHAJI NONDO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameendesha ukaguzi wa kushtukizwa kwenye magodauni ya kuuza vifaa vya ujenzi jijini Dar es  Salaam na kubaini kuwepo kwa baadhi ya nondo zinazozalishwa na baadhi ya viwanda nchini zisizokidhi viwango vya ubora viliwekwa kwa mujibu wa sheria.

Ukaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika magodauni ya kuuza nondo yaliyopo Buguruni, Mbagala, Kariakoo na Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi huo mwishoni mwa wiki, Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ramadhan Shija, alisema hatua hiyo unalenga kujiridhisha kama wazalishaji wa nondo viwandani wanafuata matakwa ya viwango husika pamoja na kutoa elimu kwa umma.

Shija, alisema ukaguzi wao umebaini baadhi ya nendo ni fupi kulingana na kiwango husika. "Nondo nyingine tumebaini kuwa ni fupi, kwani badala ya kuwa na urefu wa futi 38 zina urefu wa futi 37.6, hivyo kuna udanganyifu unaofanyika," alisema Shija.

Kwa upande wake Mkaguzi Mwandamizi wa TBS, Donald Manyama, alisema 
ukaguzi wao ulilenga urefu wa nondo na kipenyo. Alisema kupitia ukaguzi wao wamebaini baadhi ya nendo zinafikia kipenyo husika na zingine hazifikii. Kwa mujibu wa Manyama baada ya kubaini kasoro hizo kazi inayofuata ni kwenda kwa wazalizaji na kuwaeleza kuhusiana na kasoro walizobainia ili wazirekebishe vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria. Pia Manyama alisema kasoro walizobaini kwenye baadhi ya nondo zinawasukuma kufanya ukaguzi huo nchi nzima na kutoa elimu kwa umma, umuhimu wa kuhakikisha bidhaa wanazotaka kununua zinakidhi vigezo kwa kuoneshwa nyaraka husika na wazalishaji au kufika ofisi za shirika hilo kupata ushauri.

Aliongeza kwamba wanafanya hivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata 
bidhaa wanazokusudia kulingana na mahitaji. alitaja madhara ya nondo 
hizo kutokidhi viwango kuwa ni pamoja na majengo kuweza kuanguka.
Alifafanua kwamba ukaguzi huo ni sehemu ya taratibu wa TBS kwa sababu 
wakishatoa leseni kwa mzalishaji mbali na kufanya ukaguzi kwenye eneo 

za uzalishaji kwa kushtukiza pia ununua sampuli za bidhaa katika masoko bila mzalishaji kuwa na taarifa na kwenda kuzipima kwenye maabara za shirika ili kujiridhisha kama anaendelea kufuata viwango. 
Zinapokuwa na kasoro mzalishaji anatakiwa kuzirekebishe au kutakiwa kuziondoa bidhaa hizo sokoni na kuziteketeza gharama zake pamoja na hatua nyingine za kisheria.

Meneja mauzo wa kampuni ya vifaa vya ujenzi la 92, Emmanuel Marongo, 
alipongeza utaratibu huo wa TBS akisema unalenga kuwawezesha wananchi 
kununua bidhaa zenye ubora kulingana na makusudio yao.

Alisema hata wao mteja akienda kununua aina fulani ya bidhaa wanamsaidia kumpa elimu ili aweze kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji yake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya 92 ya jijini Dar es Salaama wakisaidiana na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania TBS (hawaonekani pichani) kupima viwango vya nondo. Maofisa hao walifanya ukaguzi wa kushtukiza mwishoni mwa wiki katika magodauni mbalimbali. Picha Chalila Chibuda.

TAMASHA LA KUKATA NA SHOKA DAR LIVE KESHO

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

Waandaji wa Bonse Vibe Festival wamesema katika sikukuu ya Eid Alhaj wameanda burudani za asili kutoka kwa makundi mbalimbali ya wasanii ambao hawatawaungusha mashabiki wao.

Meneja wa Burdan wa Dar Live Rajab Mtenda amesema kuwa shoo ya kesho ni ya kukuta na shoka katika ukumbi wa Dar Live kutokana na walivyipanga wasanii watakaoshusha burdan hiyo.

Amesema kuwa tamasha hilo linaupekee linalotofautiana na matamasha mengine katika kuendeleza muziki wa asili nchini Tanzania.

Mkuu wa Uendeshaji wa LBM Victor Kaduma amesema kuwa tamasha hilo litabamba kwa siku kesho kwani hakuna tamasha lingine kwa siku hiyo.Nae Msanii Heri Samil (Mr Bluu)amesema kuwa katika sikukuu ya kesho mashabiki waje kuangalia show hiyo na kundi lake analosimamia.

Wasanii watakuwepa ni Mr Bluu, Hamisa Mobeto, Chid Benz, Easy Man pamoja na Mzee wa Bwaks.
Meneja wa Burdan wa Dar Live Rajab Mtenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha litakalofanyika Kesho katika Siku ya Eid Alhai katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.
Msanii Heri Samil (Mr Bluu akizungumza na waandishi wa habari alivyojipanga katika tamasha litakalofanyika Kesho katika Sikukuu ya Eid Alhai katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Uendeshaji wa LBM Victor Kaduma akitoa maelezo namna walivyojipanga kufanikisha Tamasha hilo katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

IGP SIRRO ATOA SALAMU ZA POLE

MILIONI MIA MBILI ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA KIHESA.

$
0
0
Diwani wa kata ya Kihesa manispaa ya Iringa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake Kihesa

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

Zaidi milioni mia mbili zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo Jully Sawani alisemakuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kwaushirkiano wa serikali,wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo katika kata hiyo.

“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni mchanga na mawe tu,mfano shule ya sekondari ya kihesa ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa majengo,viti,meza za walimu na miundombinu ya shule haikuwa rafiki kabisa katika namna ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule na hivyo hivyo katika shule za msingi ngome na Kihesa ambazo nazo zilikuwa zinakabiliwa na tatizo la vyoo na uchakavu wa miundombinu lakini tumefanikiwa kutatua tatizo hilo” alisema Sawani

Sawani alisema kuwa katika sekta ya afya amefanikisha zoezi la wazee na kupewa huduma bure,tatizo la madawa nalo wamefanikiwa kulitatua na kufanikiwa kuboresha huduma bora kwa kutoa elimu kwa wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wagonjwa na wateja wote ambao wamekuwa wanapata huduma katika kituo hicho.

“Saizi ukienda katika kituo cha afya cha ngome unahudumiwa vizuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali hiyo kutokana na elimu ambayo walipata wahudumu wote wa kituo hicho kutoka kwa wataalamu wa huduma makazini na ndio sababu ya sasa kutolewa huduma bora kabisa” alisema Sawani

Aidha Sawani alisema kuwa swala la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo kuharibika mara kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo lakini kuna barabra ya kutoka ngome kwenye shule sekondari ya Kihesa,mwachang’a kwenda kanisani na majengo mapya.

“Ili kurahisisha maendeleo lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano mkubwa na chama cha mapinduzi tumefanikiwa kutatua kero hiyo kwa kiasi chake” alisema Sawani

Sawani alisema kuwa tatizo la maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

VIJANA MKOANI RUVUMA WACHANGAMKIA FURSA YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika Mkoa wa Ruvuma, Agosti 10, 2019.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru akizungumza na vijana walioshiriki katika mafunzo hayo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika mkoa huo. (Kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw. Philliph Beno.
Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi wakifuatilia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa akielezea kuhusu Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali.
Sehemu ya wajasiriamali wanaomiliki biashara wakifuatailia maelezo ya Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo hayo katika mkoa huo.
Meneja wa Ufuatiliaji na Tathmini Bi. Flora Kajela akielezea kuhusu malengo ya Programu ya Mafunzo ya Ujasiriamali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Mkoa wa Ruvuma.
Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Daudi Sailasi akielezea kuhusu programu ya kuongeza ujuzi kwa vijana inayoratibiwa na ofisi hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara yaliyofanyika katika Mkoa huo. (Kulia) ni Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa.
Mwezeshaji kutoka Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Lucas Mafuru akitoa mada kuhusu uchambuzi wa ushindani na mikakati ya masoko kwa wajasiriamali (hawapo pichani).
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eliakim Mtawa akitoa mada kuhusu vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili kwa wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo.
Mmoja wa Wajasiriamali Bw. Richard Mpagala akielezea kuhusu mbinu anazotumia kuendesha biashara yake alipokua amejifunza kuhusu masuala ya mapato na matumizi katika usimamizi wa biashara.
Bi. Pudencia Msangawale akionesha bidhaa anazotengeza na akielezea mbinu anazotumia kutafuta masoko ya bidhaa zake katika eneo lake la biashara.
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya Ujasiriliamali kutoka kwenye Ofisi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi za Umma.
Katibu Mtendaji wa Balaza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’I Issa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara.

……………………………………………………..

Vijana Mkoa wa Ruvuma wamefurahia fursa ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamaizi wa biashara yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatawawezesha vijana hao kukuza na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi.

Akifungua Mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa alieleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni muhimu sana na yanalenga kuwawezesha vijana wanaomiliki biashara wanapata mbinu za kuendeshaji na kusimamia biashara zao.

“Mafunzo haya ya ujasiriamali yameleta tija kwa vijana na wameweza kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zenye faida,” alisema Issa

Alieleza kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa hizo zinapojitokeza ili waweze kuunganishwa na fursa za mitaji na mitandao ya huduma za biashara, pia kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kujiamini na kuweza kuweza kupata faida.

“Vijana mnapaswa kutambua ninyi ndio nguvukazi ya Taifa, hivyo kuwa wabunifu ni jambo la msingi katika biashara zenu mkitambua fursa mlizonazo ili muweze kushindana katika biashara,” alisema Issa

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali watakayopatiwa vijana hao yakiwemo masuala ya uchambuzi wa masoko, dhana ya ujasiriamali, uchambuzi wa mahitaji ya mteja, kutambua ushindani wa soko, mkakati na uendeshaji biashara, utambuzi wa masoko, usimamizi wa fedha, vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili, usimamizi wa biashara na rasilimali watu, urasimishaji wa biashara na vyanzo vya mitaji.

Aliongeza kuwa Programu hii ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana itawawezesha kutambua mapungufu waliyonayo na kutumia mwanya huo kuangalia fursa walizo nazo katika ushindani wa biashara zao.

“Ni muhimu vijana mkawekeza katika biashara mnazozimudu kimtaji, kiusimamizi kwa ushindani na kufanya maamuzi sahii,” alieleza Issa

Alieleza kuwa kila Mkoa una fursa zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali katika kujiendeleza kiuchumi, vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo ili waweze kunufaika kwa njia mbalimbali.

Alifafanua kuwa Ofisi yake imekuwa ikiendesha mafunzo ya aina hii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi za Umma, Wadau wa Mendeleo, Sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

“Zaidi ya Vijana 10,000 wameweza kufikiwa na programu mbalimbali za mafunzo ikiwemo Kijana jiajiri, Ajira yangu, Kliniki ya vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, mifuko ya uwezeshaji na watoa huduma,” alisema Issa

Aidha, alitoa shukrani zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona haja ya kuwekeza kwa vijana kwa kuwapatia ujuzi ili waweze kujiajiri, kuajiri na kuchangia katika pato la taifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru amewahimiza vijana wa Mkoa huo kuchangamkia fursa za mafunzo kama hayo yanayotolewa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa yatawawezesha kujitambua na kujisimamia wenyewe na kuongeza tija kwenye biashara zao.

Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Mafunzo hayo, Bi. Pudencia Msangawale alieleza kuwa mafunzo hayo yatajibu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kama wajisiriamali ikiwemo masuala ya ujuzi, maarifa, kurasimisha biashara, namna bora ya kuhudumia wateja na utafutaji wa masoko.

“Ninawashukuru Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa elimu waliyotupatia yametuwezesha kujitambua, kuwa wabunifu, waaminifu na kuweza kujisimamia katika biashara,” alisema Msangawale.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatafanyika katika Mikoa nane (8) ya Tanzania Bara ikiwemo Dodoma ambapo tayari yamekisha fanyika, Ruvuma, Geita, Mwanza, Lindi, Mbeya, Tanga na Arusha.

SMZ YATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisaini salamu za rambi rambi Kumpelekea Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kufuatia vifo vya Watanzania kadhaa Mkoani Morogogo vilivyosababishwa na mripuko wa Gari la Kubebea Mafuta.Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemtumia salamu za rambi rambi Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kufuatia vifo vya Wananchi kadhaa vilivyotokea huko Msamvu Mkoani Morogoro kufuatia ajali ya mripuko wa Gari la kubebea Mafuta ya Petroli.

Katika salamu hizo Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar alisema yeye binafsi pamoja na Wananchi wa Zanzibar wamekumbwa na jitimai zito lililotokana na ajali hiyo mbaya iliyogharimu uhai wa Makumi ya Watanzania.

Alisema huo ni msiba mzito kuwahi kutokea Nchini uliowagusa Watanzania wote Bara na Zanzibar na sio kwa Wana wa Morogoro pekee. Hivyo ametumia pia salamu hizo za rambi rambi kuwapa pole Wananchi na Familia za Jamaa waliofariki kutokana na janga hilo lililosababisha Maafa.

Balozi Seif amewaombea kwa mwenyezi Muungu wale Watanzania waliopata majeraha awajalie kupona haraka ili warejee katika harakati zao za kujitafutia Maisha na Familia zao.

Balozi Seif aliwataka Wananchi wote waliokumbwa na Maafa hayo kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kizito cha msiba wa wapendwa wao.

Halkadhalika Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Taifa ya kukabiliana na Maafa Zanzibar aliwatahadharisha Wananchi wote wa Tanzania kukimbilia majanga yanayoweza kuepukika.

Ajali ya mripuko wa Moto katika gari hilo la kubebea mafuta ya Petroli Mkoani Morogoro kwa taarifa za awali inaelezwa kusababishwa na cheche za moto zilizosababishwa na Mtu aliyetaka kuiba Betri ya Gari lililopata ajali.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images