Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 304 | 305 | (Page 306) | 307 | 308 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Salome Kalinga(wanne toka kushoto)mkazi wa Iringa,akipokea funguo wa pikipiki yake aliyojishindia katika promosheni hiyo toka kwa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa.Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
  Meneja wa Vodacom Tanzania,Mkoa wa Iringa Bw.John Watosha,akimfungia kamba za kofia ngumu Bw.Aloyce Mboya ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi hapo jana,anaeshuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Mkoa huo Galus Baltazal.Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda Mkazi wa Mkoa wa Iringa Bw. Francis Mlelwa,akishuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa(watatu toka kushoto)pamoja na washindi wenzake akiwa juu ya pikipiki yake tayari kwa kuondoka nayo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Kaimu huyo,Ili kujiunga na Promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.
  Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa,akimkabidhi pikipiki Bw.Francis Mlelwa ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi mkoani humo hapo jana,Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
  Baadhi ya washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wa Mkoa wa Iringa,wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Mkoani humo hapo jana mara baada ya kukabidhiwa pikipiki zao za ushindi,ili kujiunga na promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.

  0 0

   Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17),akiwa mpiga chenga ya Mwili Beki wa Timu ya Simba,Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Hadi hivi sasa Simba wanaongoza kwa Bao 1-0 na tayari dakika 35 za mchezo zishakatika.Picha zote na Othman Michuzi.
   Golikipa Machachari wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiruka juu kudaka mpira uliokuwa unaelekea langini kwake.
   Simba wakiandika Bao la Kwanza mnamo dakika ya 19 ya mchezo.
   Mashabiki wa Simba.

  0 0

   Mchezaji wa Timu ya Simba,Hamis Tambwe akipiga Mkwaju wa Penati uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuiadikia timu yake bao la pili katika dakika ya 42 ya mcheo huu wa Nani Mtani Jembe unaoendelea hivi sasa hapa Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.
   Beki wa Yanga,Kelvin Yongani (kati) akiondoka na mpira mbele ya wapinzani wake.
  Golikipa wa Yanga,Juma Kaseja akiondosha moja ya hatari iliyokuwa inaenda langoni kwake.Dakika 45 za kipindi cha pili ndio zimeanza hivi punde huku mpira ukiwa ni wa kasi kwa pande zote.

  0 0

  Wachezaji wa Timu ya Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao baada ya kukabidhiwa kwa kuifunga Timu ya Yanga Mabao 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo.Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na Ramadhan Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.Picha zote na Othman Michuzi.
  Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98 milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
  Hundi ya Simba ilisomeka hivi pamoja na Ushindi Mkubwa walioupata dhidi ya wapinzani wao.
  Mgeni Rasmi katika Mchezo huo,Waziri wa Sheria na Katiba,Mh. Mathias Chikawe akikabidhi Kombe la Ushindi wa Nani Mtani Jembe kwa Nahodha wa Timu ya Simba mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akiwahutubiwa wananchi wake leo.
   
  HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013

  Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.

  Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995.


  0 0


  0 0
 • 12/21/13--11:29: UZINDUZI WA RIPOTI YA UWEZO
 •  Msanii Mrisho Mpoto akielezea kupitia mashairi
   Mama Zaida Mgalla akitoa ufafanuzi kwa ripota wa Uwezo TV Bi. Melania Mhagama
   Mgeni Rasmi akionyesha ripoti baada ya kuzindua.

  Wakati ambapo asilimia 100 ya watoto wa Darasa la 3 na kuendelea wanapaswa kuweza kusoma na kufanya hesabu za kiwango fulani, matokeo ya Uwezo yanaonyesha kwamba ni wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo.

  Katika Darasa la 3, mmoja kati ya watoto wanne anaweza kusoma Kiswahili kwa kiwango sahihi. Shule za binafsi zinafanya vizuri zaidi kidogo kulinganisha na zile za Serikali, ambapo asilimia 61 ya watoto walio na umri chini ya miaka 9 hawawezi kusoma Kiswahili na kufanya Hesabu za Kuzidisha kulinganisha na asilimia 85 ya wenzao walio katika shule za Serikali.

  Matokeo haya yalitangazwa na Twaweza, inayosimamia Tafiti ya Uwezo, katika ripoti yake ya tatu ya Tathmini ya Mwaka ya Ujifunzaji. Matokeo haya yamejikita zaidi kwenye tathmini kubwa kabisa ya mwaka kwa ngazi ya kaya inayopima stadi za kusoma na kufanya hesabu za msingi za watoto.

  Tathmini ilifanyika nchi nzima mwaka 2012; ikipima watoto 104,568 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 16 katika kaya 55,191, katika maeneo (vijiji) 3,752, kwenye wilaya 126 za Tanzania.

  Tathmini ya Uwezo inaonyesha kwamba utendaji uko duni nchini kote. Matokeo muhimu yalikuwa:

  Stadi ya kusoma Kiswahili
  Matokeo bado ni duni na hayajabadilika sana tangu 2011Mtoto 1 tu kati ya 4 (26%) wa Darasa la 3 anaweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

  Kwa Darasa la 7, mtoto 1 kati ya 4 (24%) bado hakuweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

  Stadi ya kusoma Kiingereza
  Matokeo yalikuwa mabaya zaidi kuliko katika Kiswahili

  Katika Darasa la 3, 1 tu kati ya watoto 10 (13%) aliweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.

  Hata katika Darasa la 7, ni watoto 5 kati ya 10 walioweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la 2.
  Kufanya hesabu
  Matokeo yamepanda zaidi kuliko mwaka 2011 lakini bado ni duni
  Katika Darasa la 3, zaidi kidogo ya watoto 4 tu kati ya 10 (44%) walioweza kufanya Hesabu za kuzidisha.

  Kufika Darasa la 7, mtoto 1 tu kati ya 10 (11%) aliweza kufanya Hesabu ya ngazi ya Darasa la 2.

  Matokeo haya yanaonyesha kwamba kundi kubwa kabisa la watoto halipati ujuzi muhimu katika elimu ya msingi. Hata wanapomaliza elimu ya msingi, watoto bado wanashindwa kufanya zoezi la ngazi ya Darasa la 2.

  Kuna tofauti kubwa nchini:
  Tathmini ya Uwezo inaonyesha jinsi tofauti ya kimatabaka inavyozidi kukua. Watoto katika maeneo ya mijini wanafanya vizuri zaidi kuliko wenzao wa vijijini katika masuala ya kusoma na kuandika.

  Watoto wanaotoka kwenye kaya zenye kipato cha juu vilevile walionekana kufanya vema zaidi katika stadi hizi za msingi, sawa sawa na watoto wanaosoma katika shule za binafsi. Ingawa matokeo ya kujifunza kwa ujumla wake ni duni, tofauti hizi zinazozidi kukua zinaonyesha kuwa mfumo wa elimu unawanufaisha zaidi wale wenye hali bora.

  Watoto wote, bila kujali umri, darasa au hadhi ya shule walijaribiwa kwa kutumia ngazi ya kusoma na kufanya hesabu ya Darasa la 2. Matokeo muhimu yalikuwa:

  Mahali Katika umri wa miaka 9, ni watoto 3 tu kati ya 10 (32%) wa mijini walio na ujuzi huo wa msingi, kulinganisha na mtoto 1 tu kati ya 10 (11%) wa vijijini.

  Utajiri Katika umri wa miaka 9, ni watoto 2 tu kati ya 10 (21%) kutoka katika kaya tajiri zaidi walio na ujuzi huo wa msingi, kulinganisha na chini ya mtoto 1 kati ya 10 (6%) kutoka kaya maskini.

  Aina ya Shule Katika umri wa miaka 9, ni zaidi kidogo tu ya mtoto 1 kati ya 10 (15%) katika shule za umma aliyefaulu majaribio hayo wakati ambapo ni watoto 4 kati ya 10 (39%) kutoka shule binafsi walioweza kufanya hivyo.

   “Kuna habari kuu mbili katika elimu ya Tanzania leo,” alisema Zaida Mgalla, Mratibu wa Nchi wa Uwezo Tanzania “Kwanza, watoto walio wengi hawajifunzi kitu. Pili, sisi ni jamii ya matabaka mawili – lile lenye utajiri zaidi au la mjini au linaloweza kumudu gharama za shule za binafsi na hivyo watoto wao kufanya vizuri zaidi shuleni kuliko watoto wengine.

  Linapokuja suala la elimu, Tanzania si nchi moja.” Tathmini ya Uwezo ya mwaka 2012 iliendeshwa na wananchi waliojitolea 7,560, ambao walisimamiwa na washirika katika wilaya 126 nchini (Wilaya za Mtwara hazikujumuishwa kwa sababu viongozi wa Mkoa hawakuruhusu utafiti kuendeshwa mwaka 2012). Lengo lilikuwa ni kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuhakikisha watoto wetu wanajifunza.

  Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, alisema “Kuinua ubora wa elimu ni jukumu la msingi la Serikali; hata hivyo jukumu hili inatuhusu sote. Hatua zichukuliwe katika ngazi zote, na kila mmoja – kuanzia wazazi hadi watunga sera, kuanzia walimu hadi maofisa wa wilaya – kila mmoja ana mchango wa kipekee katika kuhakikisha watoto wetu wanajifunza.”
  Mgeni Rasmi Salum Mjagila, Mkurugenzi, Elimu ya Watu Wazima MOEVT, akikabidhi ripoti kwa mwakilishi wa wanafunzi ambae pia ni ripota wa Uwezo TV, Bi. Fatma Bakari
  Rakesh Rajani, John Ulanga, Zaida Mgalla na waalikwa wakifurahia jambo

  0 0


  0 0

  Mbunge wa Nzega Mhe Dkt Hamisi Kigwangwalla katika bodaboda

  0 0

  *Asema ni fundisho kwa watakaolala
  *Ataka hatua zaidi zichukuliwe
  *ziara za Kinana zimesaidia sana kutatua kero
  *Bado moto wa ziara hizo haujapamba

  *2015 CCM kurejesha viti  vya ubunge, Udiwani vilivyoko upinzani

  NAPE NNAUYE
  NA BASHIR NKOROMO
  KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema amepokea kwa faraja kubwa, hatua ya mawaziri wanne kuenguliwa nyadhifa zao kwa ridhaa ya Rais Jakaya Kikwete.

  "Najisikia vizuri, maana kwa kitendo cha mawaziri hao wanne kuchuliwa hatua, ninaamini kitasaidia wale wengine waliolala nao waamke. Bila shaka sasa hakuna atakayelala na akilala anajua itakula kwake.", alisema Nape akijibu swali la mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Emmanuel Buhohela, kwenye kipindi cha 'mahijiano' cha televisheni hiyo, mjini Dar es Salaam, leo asubuhi.

  Mtangazaji huyo alitaka kujua, Nape kama kiongozi wa ngazi ya juu CCM,  amejisikia au kupokeaje hatua ya Bunge 

  kumuomba Rais kuwawajibisha mawaziri hao wanne na kisha Rais kuridhia ombi hilo kwa kutengua uteuzi wake wa nafasi za mawaziri hao jana.
  Mawaziri waliofutiwa uteuzi wao na Rais na nafasi walizotoka zikiwa kwenye mabano ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai (Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu akiwa Bungeni, jana.  Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni jana jioni, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua inayoaminika kuwa imetokana na shinikizo la bunge, baada ya Kamati yake ya Kudumu ya  Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini 'uozo' katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.

  Chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli, Kamati hiyo ilieleza kwamba pamoja na mambo kadhaa iliyoyaeleza kuwa ya hovyo yaliyojitokeza kwenye operesheni hiyo, vitendo vingi ikiwemo ubakaji na udhalilishaji vilifanyika ambapo ni kinyume na utu na haki za binadamu.

  Kufuatia kadhia hiyo, Kamati hiyo kupitia kwa Lembeli, iliwataka mawaziri wanaohusika kutazama kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao au wajiuzulu, na pia Kamati hiyo ikaenda mbali zaidi kwa kumuomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya kuwawajibisha.

  Akizungumzia zaidi hatua hiyo, Nape alisema, pamoja na mawaziri hao kuwajibika, lakini ipo haja ya kwenda mbali zaidi kwa kutazama mifumo na sheria zilizopo sasa kwa kuwa inaonekana navyo ni miongoni mwa vyanzo vya vikwazo katika utekelezaji wa utawala bora.

  "Kwa mfano leo hii, mawaziri wameng'oka, sawa ni jambo jema, sitetei, lakini inawezekana kabisa kuna mifumo na sheria ambazo zilimkwaza Waziri huyu kutimiza wajibu wake. Mfano, alihitaji kumfukuza mtu kazi kwa kuzembea jambo fulani, lakini malmaka ya kufukuza kazi mtumishi yapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, hapa atafanyaje!", alisema Nape na kuongeza;

  "La msingi hapa ni lazima sasa hatua hizi ziende mpaka chini huku kwa watendaji, ili isiwe mawaziri wanawajibishwa tu kwa sababu ya dhamana zao za kusimamia kisiasa, huku watendaji wanazidi kuvuta shuka bila hofu wakati baadhi yao ni sehemu ya matatizo".

  Akijibu swali kuhusu ziara za Katibu Mkuu na sekretarieti ya CCM mikoani, Nape alisema, ziara hizo ndiyo kwanza zimeanza, na mado moto wake mkubwa zaidi unakuja hasa itakapokaribia uchaguzi mkuu wa 2015.

  Nape alisema, ziara hizo, zimeonyesha matunda makubwa sana, klwa kuwa zimesaidia kupunguza kero nhyingi katika maeneo zilikofanyika.

  Alitoa mfano wa ziara hiyo ilivyoweza kuondoa msongamano wa malori wilayani Tunduma mkoani Mbeya, akisema kwamba wakati Kinana na msafara wake wanaingia tunduma walikuta msongamano ni mkubwa sana kutokana na wafanyakazi wanaohudumia malori hayo kufanya kazi kwa mda mfupi.

  "Baada ya kuiagiza serikali isimamie wafanyakazi wa eneo hilo wafanya kazi kwa saa 24, kwa zamu, siku ya pili yake ya agizo hilo, msongamano ulionekana kupungua sana na kuleta nafuu kwa madereva na wafanya biashara kwa jumla pale Tunduma", alisema Nape.

  Nape alisema, pia kutokana na ziara hizo, mgogoro uliokuwa mkubwa baina ya wananchi na wenye mgodi wa machimbo Nyamongo, umepungua kwa asilimia 90 sasa, na hali imekuwa ya kuridgisha sana.

  Akizungumzia wabunge wanaodaiwa kulipwa posho bila kuzifanyia kazi, Nape alisema, kurudisha fedha pekee hakutatosha, kwa upande wa CCM ambayo ndiyo yeneye wabunge wengi itabidi ichukue hatua zaidi dhizi ya waliohusika na kadhia hiyo bila kuoneka mtu.

  Kuhusu ajira kwa vijana, Nape alaisema ili kutimiza hilo, ni lazima viwanda vifufuliwe kwa dhati kabisha, ikiwa ni kuchukua hatua za kuwanyang'anya wawekezaji waliochukua viwanda mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza lakini baadhi yao majengo ya viwanda hivyo wakayafanyia shughuli zingine tofauti ikiwemo kuyageuza maghala.

  Nape aliitaka pia serikali kupunguza au kuondoa kabisa urasimu katika kupokea wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini akisema, kwamba, kwa sasa vikwazo na urasimu bado ni vingi sana kiasi kwamba wawekezaji waanakwazika na hivyo kupunguza kasi ya uwekezaji ambao wakiongezeka haraka ajira kwa vijana nazo zitakua haraka.

  Alisema, hatua ya sasa inayofanywa na CCM kusimamia serikali ni ya kawaida kabisa kwa kuwa kazi hiyo haipaswi kufanya na wapinzani kwa kuwa sera inayotekelezwa siyo yao, na wahaijui.

  Nape aliahidi kwamba katika uchaguzi zijazo CCM itakomba viti vyote vya ubunge na udiwani vililivyopo sasa chini ya wapinzani, akisema, kwamba, baada ya wapinzani kujaribiwa wameshindwa kuonyesha matunda yoyote ya kusaidia wananchi na hivyo kutokuwa mbadala wa CCM.

  0 0
  HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013


  Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.

  0 0

  Balozi Phikllip Marmo (kulia) akiwa amepokelewa katika ukumbi wa Watu mashuhuri(VIP) katika Uwanja wa ndege wa Tigel jijini Berlin.alippowasili  kutoka Dar es salam kufuatia uteuzi wake kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani. Kushoto ni Balozi Osinde wa Kenya, katikati ni Balozi Gertze wa Namibia. Alipokelewa pia na Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania, Berlin ambao hawapo katika picha. 

  0 0

  Ankal salaam. 
   Kama ujuavyo, msimu huu ni msimu wa sikukuu ambapo wenzetu Wachagga hupendelea sana kwenda kwao kusheherekea sikukuu hiyo pamoja na ndugu na jamaa waliopo huko vijijini. 
   Nimetumiwa baadhi ya picha na rafiki yangu mmoja ambaye hivi sasa yuko kwao huko Rombo Kilimanjaro kwa ajili ya sikukuu.  Hakika ni taswira za kupendeza sana. 
   Tafadhali ukipata nafasi ziweke kwenye blog yetu ya jamii  ili Watanzania wengine waweze kuona sababu mojawapo ya hawa jamaa zetu kupenda sana kwenda kwao mwisho wa mwaka....... Ni pamoja na kufaidi mazingira yenye taswira mwanana kama hivyo.
  Mdau Rombo


  0 0
  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akikata utepe kuzindua matumizi ya magari mawili ya kubebea wagonjwa yaliyonunulia na Ofisi ya Bunge. Pembeni ni Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi.
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa tume ya Bunge na katibu wa Bunge mbele ya mojawapo ya magari hayo ya kubebea wagonjwa yaliyonunuliwa na Ofisi ya Bunge.
  Katibu wa Bunge na Mhe. Spika wakikagua magari hayao. katikati ni muuguzi mwandamizi kutoka Hospitali ya mkoa wa Dodoma bi, Cecilia Sanya. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

  0 0

   Zikiwa zimebakia siku chache kwa Promosheni ya timka na bodaboda inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuisha, washindi kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameendelea kukabidhiwa pikipiki zao safari hii ilikuwa ni zamu ya washindi sita kutoka kanda ya Kusini (Iringa) kukabidhiwa zawadi zao. 
   Akikabidhi pikipiki hizo sita Kaimu Mkuu wa Kanda Kusini Magharibi wa Vodacom Tanzania, Benedict Kitogwa aliwahimiza wateja wa mtandao huo kuendelea kucheza promosheni hiyo kwa kasi zaidi ukizingatia shindano hilo linakaribia kuisha mapema mwezi ujao.
   “Promosheni hii ni yenye manufaa makubwa sana kwa wateja wetu ukizingatia inawasaidia kukabiliana na tatizo la usafiri linalowakabili watanzania na nchi kwa ujumla na pia kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato.” Alisema Kitogwa na kuongezea 
  “Timka na bodaboda ni mkombozi wa watanzania na nimelishudia hilo, sasa watu wanamiliki biashara zao, hawana tatizo tena la usafiri na pia watu wanajishindia fedha ambazo wanaongezea mitaji yao na kujikwamua kiuchumi.” 
   Awali Meneja Mauzo Galus Baltazal na Meneja wa Vodacom Iringa John Watosha wamewapongeza washindi hao na kuwahimiza kuendelea kutumia mtandao wa Vodacom kila wakati. Baadhi ya washindi wa Timka na Bodaboda waliopewa Pikipiki zao hapo jana ni Aloyce Mboya, Francis Mlelwa, Salome Kalinga na Hassan Ahmed Abdallah amboa kila mmoja alijishindia bodaboda moja. 
   Aloyce Mboya ambaye ni mshindi mmojawapo wa promosheni hiyo alibainisha kuwa sasa tatizo la usafiri kwake ni ndoto na pia anaweza kuitumia kama njia ya kujiingizia kipato. 
   “Ni furaha kubwa sana kwangu leo hii kukabidhiwa pikipiki hii kwani nimekuwa ni mteja wa Vodacom kwa muda mrefu na nimeshirika promosheni nyingi ikiwemo hii ya Timka na bodaboda. Nadhani kushinda kwangu leo naona ni kama zawadi kutoka kwa kampuni hii kwa kuwa mteja wa muda mrefu, nawataka wateja wa Vodacom kucheza promosheni hii na wasiojiunga na mtandao huu wafanye hivyo haraka kwani si tu wateja wake tunafaidi huduma bora za kimawasiliano bali pia tunaboreshewa maisha yetu.” Alihitimisha Mboya.
       Kujiunga na promosheni hii ni rahisi na mteja anachotakiwa kukifanya ni kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.
   Meneja wa Vodacom Tanzania,Mkoa wa Iringa Bw.John Watosha,akimfungia kamba za kofia ngumu Bw.Aloyce Mboya ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi hapo jana,anaeshuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Mkoa huo Galus Baltazal.Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
   Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda Mkazi wa Mkoa wa Iringa Bw. Francis Mlelwa,akishuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa(watatu toka kushoto)pamoja na washindi wenzake  akiwa juu ya pikipiki yake tayari kwa kuondoka nayo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Kaimu  huyo,Ili kujiunga na Promosheni hiyo  inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.
   Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa,akimkabidhi pikipiki Bw.Francis Mlelwa ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi mkoani humo hapo jana,Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544
   Baadhi ya washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wa Mkoa wa Iringa,wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Mkoani humo hapo jana mara baada ya kukabidhiwa pikipiki zao za ushindi,ili kujiunga na promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Salome Kalinga(wanne toka kushoto)mkazi wa Iringa,akipokea funguo wa pikipiki yake aliyojishindia katika promosheni hiyo toka kwa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi Bw.Benedict Kitogwa.Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.

  0 0


  0 0  0 0
 • 12/21/13--21:00: bei ya madafu


older | 1 | .... | 304 | 305 | (Page 306) | 307 | 308 | .... | 3283 | newer