Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA KILIMO HASUNGA AZINDUA BIMA YA MAZAO YA WAKULIM

$
0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akionyesha kitabu cha Bima ya Mazao wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao uliofanyika kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe bidhaa na muongozo wa Bima ya Mazao wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao uliofanyika kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019. Mwingine Pichani (Katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NIC Dkt. Elirehema Doriye, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Ushirika Dkt.Titus Kamani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka pamoja na viongozi wengine wa sekta ya kilimo na Ushirika wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vyama vya ushirika waliopata vyeti vya utambuzi kwa mchango katika Kilimo na Ushirika, jana tarehe 4 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Mazao kwenye Banda la NHC wakati wa maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, jana tarehe 4 Julai 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Katika miaka ya karibuni, Wizara ya Kilimo imebuni mbinu mbalimbali za kubadili wakulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuwa cha biashara. Kwa upande mwingine, kilimo ni biashara yenye vihatarishi vingi kwa wakulima wa Tanzania na Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ujumla. 

Hali hii imesababishwa na kutegemea mvua, mabadiliko ya hali ya hewa, moto, uharibifu wa ndege na wanyama, magonjwa ya mimea, upepo mkali, mbegu na dawa za wadudu nk. Mara nyingi, hakuna uwiano kati ya wakulima wadogo na wakubwa katika sekta ya kilimo katika matumizi ya teknolojia, ufikiaji wa soko, kusimamia hatari zisizodhibitiwa, utoaji wa elimu na uhamasishaji, mikopo na huduma za bima. 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 4 Julai 2019 wakati akizundua Bima ya Mazao ambapo alisisitiza kuwa, kuanzisha Bima ya Mazao ni muhimu kwa wakulima nchini Tanzania ili kukabiliana na hasara zitokanazo na vihatarishi vinavyoathiri uzalishaji. 

Mhe Hasunga alisema kuwa kuna kampuni kadhaa za Bima ambazo zimeanzisha bidhaa mbalimbali za bima kwa ajili ya kumkinga mkulima dhidi ya hasara kwa aina tofauti za mazao. Kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Bima ya Taifa (NIC), Jubilee na UAP. 

Hata hivyo, utoaji wa bidhaa za bima ya mazao umekuwa ukifanyika bila mwongozo thabiti ambao ungewanufaisha wakulimna wengi wadogo hususan maeneo ya vijijini. Hivyo, mwongozo huu unaolenga kubainisha namna bima ya mazao inavyoweza kuwakinga wakulima dhidi ya hasara una umuhimu wa kipekee kwa wakati huu wa mapinduzi makubwa ya sekta ya kilimo nchini.


Alisema kuwa Bima ya mazao aliyoandaliwa na NIC kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo iliyozinduliwa ni faraja kubwa kwa wakulima nchini. 

Uandaaji wa Bima ya mazao iliyozinduliwa pamoja na Mwongozo vimezingatia: Dira ya Maendeleo ya Taifa (Tanzania Development Vision 2025); Mpango wa Taswira ya Muda Mrefu wa Taifa (Long Term Perspective Plan -LTPP 2012-2021); Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (Five Year Development Plan II - FYDP II 2016-21); Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Program II – ASDP II ). Vilevile, Sheria ya Bima Namba 10 ya mwaka 2009 (Tanzania Insurance Regulatory Authority Act. No. 10 of 2009) imezingatiwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa Miongoni mwa manufaa yapatikanayo kutokana na kuwepo kwa mwongozo wa Bima ya Mazao ni pamoja na kutoa fursa kwa wakulima kupata aina sahihi ya bidhaa ya bima ya mazao kutoka kwa kampuni za bima zenye vibali na zilizosajiliwa, kuwapa wakulima uwezo wa kuchagua aina ya bima ya mazao waipendayo, na kuwezesha wakulima kubadili tabia ili kufuata kanunu bora za kilimo.

Zingine ni kudhibiti kampuni zinazotoa huduma za bima ya mazao ili kubuni bidhaa za bima ya mazao ambazo zina manufaa makubwa kwa wakulima, kujenga uaminifu miongoni na taasisi za fedha kwa kutoa mikopo ya kilimo na kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima katika taratibu za kujiandikisha, kuwasilisha madai, kinga ya mazao na taratibu za malipo pindi hasara inavyotolewa taarifa.

Kadhalika Mhe Hasunga alisema kuwa utekelezaji wa Mwongozo huo kwa ukamilifu, utawezekana ikiwa kutakuwa na juhudi za pamoja kati ya Wizara ya Kilimo na wadau wengine wanaojishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, imeendelea kuimarisha na kuendeleza ukuaji wa Sekta ya Kilimo Nchini kutumia programu mbali mbali kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo ya kilimo. 

Uendelezaji wa sekta hii ya kilimo ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa, unaopelekea ukuaji wa sekta ya viwanda, upatikanaji wa chakula na lishe ya kutosha kwa Watanzania na uzalishaji wa kibiashara. Kwa sasa, sekta ya kilimo inachangia 29.1% ya Pato la Taifa, 65.5% ya ajira, 65% ya malighafi za sekta ya viwanda na 30% ya mapato yatokanayo na mauzo ya nje ya nchi.


“SERIKALI KUPITIA TASAF YAANDAA UTARATIBU MPYA WA KUWAPATA WALENGWA WA TASAF WENYE UFANISI ZAIDI” - DKT. MWANJELWA

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi  na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  katika kijiji cha Burugo (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.

 Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani).

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini (kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Miradi ya Ajira za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi  wakishuhudia nyumba iliyojengwa na mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.

 Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa  kijiji cha  Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akitoa ushuhuda wa namna alivyotumia ruzuku kuboresha makazi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). Picha ya chini ni mlengwa huyo akimuonesha naibu waziri shamba lake analoliendeleza kwa kutumia ruzuku ya TASAF. 



NA ESTOM SANGA---KAGERA 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa amesema Serikali kupitia TASAF imeandaa utaratibu utakaowezesha kuorodheshwa kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watakaokidhi vigezo vya umaskini. 

Akiwahutubia Wananchi na Walengwa wa TASAF katika vijiji vya Lukindo na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Dkt. Mwanjelwa amesema utaratibu huo mpya wa kuzitambua na kuziorodhesha kaya za walengwa kwenye Mpango utahusisha matumizi ya kielektroniki na kupiga picha kwa wahusika ili kuondoa uwezekano wa kuorodhesha kaya zisizostahiki. 

Aidha Naibu Waziri huyo amesema serikali kupitia TASAF inaendelea kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema haitawapa mwanya wananchi wenye uwezo kujumuishwa kwenye Mpango huo. 

Amesema Walengwa wa Mpango huo wenye uwezo wa kufanya kazi watawekewa utaratibu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao watakayoibua na kisha kulipwa ujira kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali katika halmashauri za wilaya kutenga muda wa kuwatembelea Walengwa wa TASAF na kuona namna wanavyotekeleza miradi yao na kuwashauri namna bora zaidi ya kutekeleza miradi hiyo ili waweze kupata matokeo bora na yenye tija. 

Wakati huo huo ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio waliyoanza kupata Walengwa wa TASAF katika Nyanja mbalimbali jambo linaloonyesha kuwa mkakati wa Serikali katika kupambana na umaskini unatekelezeka. 

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea vijiji vya Lukindo, na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera na kukutana na Walengwa ambako amekagua shughuli wanazozifanya kwa kutumia ruzuku wanayoipata kutoka TASAF. 

Naibu Waziri huyo amesema Walengwa hao wa TASAF wameweza kubadilisha maisha yao kwa kutumia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kuboresha maisha yao hususani katika Nyanja za makazi, uchumi huku wengine wakifanikiwa kujenga nyumba zao bora ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kupata ruzuku hiyo. 

TAEC YAFANIKIWA KUPATA MATOKEO CHANYA YA MBEGU BORA YA SUPER BC YENYE KULETA MAVUNO MENGI

$
0
0
Kulia ni Simon Mdoe, Mtafiti Mwandamizi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( TAEC) akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la  TAEC kwenye maonesho ya kilimo ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya TASO vilivyoko Njiro Jijini Arusha
Peter Ngamilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( TAEC) akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la  TAEC kwenye maonesho ya kilimo ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya TASO vilivyoko Njiro Jijini Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha

TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeeleza kuwa utafiti wa mbegu ya mpunga kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ya kununurisha vinasaba (viasili) umefanikiwa kupata matokeo chanya ya kupata mbegu bora ya Super BC yenye kuleta mavuno mengi zaidi visiwani Zanzibar.

Akizungumza jana na Mwandishi wa habari hizi kwenye viwanja vya maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini yaliyopo Eneo la Themi jijini Arusha yenye ujumbe wa mchango wa teknoljia ya nyuklia kwenye kilimo, mifugo kwa ukuaji wa uchumi wa Nchi, Mtafiti mwandamizi wa teknolojia ya Nyuklia, Simon Mdoe alisema utafiti huo ulioanza 2009 umefanikisha matokeo chanya mara saba zaidi kwa mavuno ya mbegu ya mpunga ya Super BC huko visiwani Zanzibar ikilinganishwa na awali.

Mdoe alisema utafiti wa mbegu hiyo uliofanywa na Kituo cha utafiti wa kilimo cha Zanzibar, (ZARI) na pamoja na chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA), unaratibiwa TAEC kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la nguvu za atomiki duniani (IAEA) ambapo walinunurisha (kupitisha mionzi kitaalamu kwenye mbegu) ambayo ilibadilisha viasili (vinasaba) na kuwa bora zaidi kuweza kuzalisha mara saba ya mazao yaliyokuwa yakizalishwa awali.

“Katika utafiti wetu tulichukua mbegu za mmea wa mpunga na kupitisha miale ya nyuklia kwa hatua sita, huku kila hatua moja tukihamishia mbegu shambani na kupata matokeo tofauti, mara ya mwisho tulipata matokeo mazuri zaidi kuliko hatua nyingine tano na kugundua kuwa na mavuno yamefikia mara saba ya kawaida ya mbegu hizo…kama mkulima anavuna magunia 12 kama ambavyo imezoeleka kwa mbegu za zamani na alipotumia mbegu za super BC alipata gunia 70 za mpunga.alisema Mdoe.

Alisema baada ya matokeo ya utafiti ulishirikishwaji ulifanyika kwa mashirika ambapo mbegu hizo za Super BC zilitawanya kwenye maduka ya mbegu visiwani Zanzibar na kuwapelekea wakulima ambao walipata matokeo  hayohayo mazuri mara saba zaidi tofauti na awali kabla ya utafiti. Asilimia takriban 80 ya wakulima Zanzibar wanapendelea kutumia mbegu hii

Mdoe alisema pia matokeo mengine ya utafiti na kuboreshwa kwa mbegu kupitia mionzi ya nyuklia yamebaini kuongezekana kwa ladha ya mchele uliotokana na mpunga wa Super Bc, pamoja na harufu nzuri kwa walaji.

“Alisema pia matokeo ya tafiti yameonyesha mbegu hiyo kutoshambuliwa na wadudu wakati wa kuota na ukuaji wake”alisema Mdoe. Utafiti bado unaendelea ili kupata mbegu zingine bora zaidi zikiwemo za mahindi na shayiri

Mtafiti hiyo alisema TAEC kwa kushirikiana na Chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA) wanaendelea na utafiti ili kununurisha mbegu nyingine za mpunga, zaidi ya Super Bc kwa kuzingatia hali ya hewa na maeneo tofauti tofauti ya Nchi na aina ya udongo ili kupata ili kupata tija itokanayo na mavuno mengi kwa ustawi wa Uchumi wa Nchi.

Mdoe alisema utafiti wa kununurisha mbegu hizo  unafanyika pia kwenye kituo cha utafiti cha Ilonga Mkoani Morogoro na katika kituo cha Mati kilichopo eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Aidha alisema kuna Tafiti nyingine kama hizo za mbegu za Mahindi na shairi zinazofanyika katika Kituo cha utafiti wa mbegu za Kilimo cha SELIAN, Arusha ambazo ununurishaji umeshafanyika na tayari mbegu hizo ziko kwenye hatua za mpando wa awali ambapo hatua nyenye ubora wa juu utakapofiki tamati, zitasambazwa kupitia njia zilizofanyika Zanzibar kwa wakulima ili kuongeza mavuno na kukuza uchumi wa wakulima na Taifa kwa pamoja.

Alisema pia TAEC na taasisi ya mboga mboga, maua na matunda ya (TAHA) kwa pamoja wako kwenye upembuzi yakinifu ili kuona namna ya kununurisha mboga mboga, matunda na maua ili kuhifadhika kwa muda mrefu na unaofaa pindi bidhaa inapokuwa sokoni kwa muda ili isiharibike kwa urahisi kwani uzoefu unaonyesha asilimia 40 ya matunda na mbogamboga huharibika kwa kuoza kutokana na kukosa au kutokutumia teknolojia kama hiyo ya mionzi.

Alisema tafiti nyingine zinafanyika kwenye mbegu za wanyama kama Ng’ombe kwa njia ya uhimilishaji inayofanywa na Taasisi ya mifugo ya uhimilishaji ya NAIC iliyopo USA Liver ili kupata mifugo bora inayokidhi viwango vya ndani na nje kwa nyama bora.

Naye mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wanTAEC, Peter Ngamilo alisema TAEC ina matarajio ya kuwa na mtambo wa kuzalisha vyanzo vya mionzi (Linear Acceletor) vinavyotumika kwenye matibabu, viwanda, kilimo na utafiti (Radioisotopes)

Alisema Pia TAEC  ina matarajio ya kuanzisha mradi wenye kutumia teknolojia ya nyuklia katika kufanya tafiti mbalimbali (Nuclear Research Reactor) Zenye manufaa kwa Nchi.

Mtambo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na viwanda vya madawa ya tiba ya saratani pamoja na kutumika kama nyenzo ya kufundishia katika taasisi za elimu ya juu na utafiti.

Tume ya Nguvu ya Atomiki (Tanzania Atomic Energy Commission) ilianzishwa kwa  sheria ya Bunge no 7 ya Mwaka 2003, awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya taifa ya mionzi iliyoanzisha kwa sheria ya bunge no 5 Mwaka 1983. TAEC ina majukumu ya kuthibiti na kusimamia matumizi salama ya mionzi  Nchini, kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojia ya Nyuklia  na kufanya utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbali mbali juu ya Sayansi na Teknolojia ya nyuklia.

TEMESA YASHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE KITAIFA SIMIYU

$
0
0

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Bi. Theresia Mwami kulia akimpa maelezo kuhusu huduma za Wakala huo Meneja wa Tanesco mkoa wa Simiyu Mhandisi Rehema Mashinji wakati alipotembelea banda la TEMESA katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Bi. Beatrice Peter katikati akiwaelekeza watoto wa shule jinsi ya kuvuka barabara, kusoma alama za barabarani pamoja na jinsi taa za barabarani zinavyoongoza magari na watumiaji wake walipotembelea banda la Wakala huo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Mohamed Mohamed kulia, dereva kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akiwapa elimu kuhusu matumizi ya taa za barabara na alama zake baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Wakulima Nanenane waliotembelea banda la TEMESA katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Fundi mwandamizi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Luhende Matinde kushoto akiwaonyesha vijana wa shule jinsi ya kutambua vipuri feki na halali vya magari wakati walipotembelea banda la Wakala huo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji TEMESA Hans Goodluck.

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

TAASISI YA ISLAMIC HELP TANZANIA YAWAFUTA MACHOZI WANATANGA

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Taasisi ya Islamic Help Tanzania wakati alipotemblea Taasisi hiyo inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (kulia) akizungumza wakati alipotembelea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Mkuu wa miradi wa Taasisi Islamic Help Tanzania akieleza kazi zinazofanywa na Taaisis yake kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipotemblea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akishuhudia shughuli zinazofanywa na Taasisi Islamic Help Tanzania kwa njia ya video wakati alipotemblea Taasisi hiyo inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.
Wadau kutoka Taasisi ya Islamic Help Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu( hayupo pichani) wakati Waziri huyo alipotemblea Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini mkoani Tanga.

************* 

Na WAMJW- TANGA. 

Taasisi ya Islamic Help Tanzania inayojishughulisha na miradi ya kusaidia Kaya masikini imewafuta machozi wananchi wa mkoa wa Tanga kwa kuwasaidia kujenga miradi ya maji iliuohusisha visima 200 kwa Wilaya za Pangani, Mkinga, Handeni, Lushoto jambo lililosaidia kipunguza hadha kwa wananchi. 

Hayo yamebainishwa leo mkoani Tanga na Mkuu wa miradi wa Taasisi hiyo Bw. Amjad Khan wakati alipopokea ugeni kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu aliyeongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Tanga. 

Bw. Amjad Khan amesema kuwa Taasisi ya Islamic Help Tanzania imejipanga katika kuisaidia Serikali kupambana dhidi ya umasikini kwa kuwasaidia wananchi katika nyanja mbali mbali hususan katika Elimu, Uchumi, Afya, Malezi ya Watoto yatima, Mazingira. 

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo inatoa msaada wa chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kila mwezi kwa miezi miwili kwa wilaya ya Pangani, na kwa eneo la Rufiji huwa wanapokea pesa taslim kwa ajili ya kununu chakula. 

Bw. Khan amesema mbali na misaada hiyo pia Taasisi yake inatoa huduma za afya hasa huduma za Afya ya macho kwa kuweka kambi za upasuaji wa mtoto wa jicho katika mkoa wa tanga na huduma hizo hutolewa bure kwa wananchi. 

Aidha Bw. Amjad Khan alisema kuwa Taasisi hiyo imesajiliwa kama Taasisi ya kiislam inayosaidia binadamu wote na sio kuwa lengo la kuwasaidia waislam pekee hasa kwenye ibada kwa misikiti, huku ikitoa chakula kwa masikini mwezi wa ramadan. 

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ameishukuru taaissi hiyo kwa kujikita katika kusaidia wananchi hasa wale wa hali ya chini kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya, maji, Elimu na malezi kwa watoto yatima. 

Waziri ummy ameongeza kuwa Serikali ipo pamoja na Taasisi hiyo na Taasisi nyingine zote zinazofanya mambo kama hayo ya kuisaidia jamii ya watanzania kujikwamua kiuchumi na kutoa huduma za kijamii. 

“ Niwapongeze Taasisi ya Islamic Help Tanzania amejitoa kusaidia kaya maskini naamini zitajitokeza Taasisi nyingine ziige mfano wenu huu bora wa kuisadia jamii ya watanzania” alisisitiza Waziri Ummy.

VULLU AKABIDHI KITANDA , VIFAA VYA KUJIFUNGULIA KATIKA ZAHANATI YA YOMBO HUKO BAGAMOYO

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO 


MBUNGE wa viti Maalumu Mkoani Pwani Zaynab Vullu, amekabidhi kitanda ,baadhi ya vifaa vya vinavyotumika wakati wa kujifungua (delivery kit) pamoja na pempas za watu wazima, katika zahanati ya kijiji cha Yombo ,jimbo la Bagamoyo . 

Akiambatana na mwenyeji wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Zainab alisema hatua hiyo inalenga kusaidia akinamama wanaokwenda kujifungua na wakazi wa kata hiyo kijumla. 

Alisema, akishirikiana na wabunge wenzake wa majimbo wamekuwa na ushirikiano katika kusaidia na kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi kwenye sekymta mbalimbali ikiwemo afya. 

“Nimekuja katika zahanati hii kwa ajili ya kukabidhi kitanda hiki kitachotumika kwa wagonjwa tunaopata huduma hii hapa,pamoja na vifaa vingine na pempas za watu wazima,” alisema Vullu. 

Nae Dkt. Kawambwa alimshukuru Zaynab kwa mapenzi aliyoyaonesha kwa wana-Yombo, kufuatia kukabidhi kitanda, godoro pamoja na mifuko yenye vifaa maalumu vya kuwasitiri wagonjwa wa kike na kiume wakati wanapatiwa huduma. 

Alisema ,vifaa hivyo vitawasaidia wagonjwa watakaohitaji huduma hizo,na amewaomba wadau wa sekta hiyo kuendelea kuiangalia sekta hiyo ili kuiunga mkono serikali. 

Kwa upande wake muuguzi wa zamu Anna Mzeru alibainisha ,vifaa vilivyotolewa na mbunge huyo vina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa watano. 

Wakati huo huo ,wakazi wa Kijiji cha Yombo Kata ya Yombo jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanatamani kubadilishana kopo la korosho na kilo ya unga, ili kujikimu kimaisha kutokana na kukabiliwa na hali mbaya kiuchumi. 

Hali hiyo imetokana na kutegemea kilimo cha korosho na mahindi, huku sekta hiyo ikikabiliwa na changamoto luluki, iliwemo kuchelewa malipo ya korosho na mifugo kula mazao yao mashambani.. 

Mkazi mzee Makorosho, akiwakilisha wenzake katika mkutano ulioitishwa na Mbunge Dkt. Shukuru Kawambwa, alieleza, kucheleweshwa malipo ya korosho wanaishi maisha magumu, huku wakitamani kubadilishana korosho na kilo ya unga. 

Akitolea majibu ya malalamiko hayo, Dkt. Kawambwa alibainisha ,kuhusu suala la uuzwaji wa korosho hawezi kulitolea taarifa kwani ni agizo kutoka serikali kuu linalowataka wakulima kupeleka katika maghala ili zinunuliwe na serikali na kudai atafuatilia suala hilo.

SIMANJIRO YAKABIDHIWA MRADI WA UBORESHAJO MIUNDOMBINU SHULE YA MSINGI LOSWAKI

$
0
0

Na Novatus Makunga,Simanjiro,Agosti 04,2019

Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imekabidhiwa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi Loswaki iliyopo katika kata ya Terrat.

Miundombinu hiyo iliyojengwa na mingine kukarabatiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la ECLAT Development Foundation kwa ufadhili wa shirika la Upendo Society la Ujerumani kwa gharama ya shilingi milioni 330.

Akipokea mradi huo,mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula aliwataka viongozi wa kimila la jamii ya kabila la Wamasai wanaofahamika kama Malaigwanani katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wametakiwa kutimiza kiapo chao kinachofahamika kama azimio la Namalulu kwa kuhakikisha kila mtoto wa kike anafikia elimu ya chuo kikuu.

Mhandisi Chaula aliwakumbusha Malaigwanani kutekeleza azimio lao la Namalulu ambapo alisema kuwa walikubaliana kuhakikisha kila mtoto wa kike anasoma hadi Chuo Kikuu.

Aidha Mhandisi Chaula alitoa ahadi ya kupeleka walimu katika shule hiyo mara tu wilaya hiyo itakapopokea walimu wapya.Alisema kuwa wilaya hiyo ina uhaba mkubwa wa walimu wapatao 460.

Aidha Chaula aliagiza kila shule wilayani humo kuandaa kambi za kitaalumu ambapo alisema zimeonyesha kuwa na mafanikio makubwa akitolea mfano wa shule ya Msingi Naisinyai ambayo ilikuwa inaburuta mkia lakini kwa sasa inafanya vizuri kutokana na makambi hayo.

Mhandisi Chaula pia aliwataka wazazi kuweka mpango wa kuwapatia chakula Watoto katika shule zote katika wilaya hiyo kwani alieleza kuwa wengi wao utembelea umbali mrefu hadi shule na hivyo upoteza usikivu darasani masomo kutokana na njaa.

Awali Mwenyekiti wa shirika la Upendo Dk.Fred Heimbach alimtaka mkuu wa wilaya ya Simanjiro kuhakikisha shule hiyo inapata walimu wanaohitajika ili wanafunzi waweze kupata elimu bora.Alisema kwa upande wao wamesaidia uboreshaji wa miundombinu lakini hawana uwezo wa kuchukuwa walimu kutoka Ujerumani na kuwapeleka Loswaki na hivyo akamtaka Mkuu wa wilaya Chaula kulingalia tatizo hili la walimu wa uzito mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya watoto wa Simanjiro.

Mwenyekiti wa ECLAT,Peter Kiroya Toima aliitaka jamii ya wafugaji wa Kimasai kutambua kwamba wakiendelea na mila zao bila kuzichuja wataachwa nyumba kimaendeleo na kuwataka kuhakikisha kila mtoto anahitimu baada ya kuanza shule.

“Tutaweza kutatua changamoto nyingi zinazotukabili endapo tu tutazingatia elimu kwa watoto wetu kwani mila ambazo tumekuwa tukizikumbatia kwa miaka mingi hazijatupeleka popote pale hivyo tuwe makini,”alisema.

Alisema kuwa shirika lake lenye makao makuu yake wilayani Simanjiro tangu lianzishwe mwaka 2008 limeshatekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya shiriki bilioni tano katika sekta ya elimu,maji,afya na maendeleo ya wanawake katika mikoa ya Manyara,Arusha na Mtwara

Naye diwani wa Terrat Jackson Materi alimtaka mkuu wa wilaya kuchukuwa jukumu la kuhakikisha kwamba shule inapata walimu ili iweze kufanya vizuri na kujinasua kutoka miongoni mwa shule kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kuhitimu darasa la saba kwa msimu uliopita.

Alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 800 na walimu watano tu ili iweze kufanya vizuri inahitaji walimu zaidi ya 15.Akitoa taarifa ya uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo,Msimamizi wa miradi wa ECLAT,Bakiri Msham alisema ulihusisha ujenzi wa nyumba 4 za walimu,madarasa 3,ofisi 2,vyoo vya matundo 32 pamoja na ukarabati wa madarasa 7,ofisi 2 na kutoa madawati 46.
 Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula(kushoto) akifungua mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi Loswaki, wa kwanza kushoto aliyevaa mgolole ni mwenyekiti wa ECLAT Peter KIroya Toima
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Loswaki wakishuhudia makabidhiano ya mradi wa uboreshaji wa shule ya Msingi Loswaki. 
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Loswaki wakishuhudia makabidhiano ya mradi wa uboreshaji wa shule ya Msingi Loswaki. 
 Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula(katikati) akipokea hati za makabidhiano ya  mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi ya Loswaki kutoka kwa mwenyekiti wa ECLAT Peter Kiroya Toima(kushoto) na mwenyekiti wa Upendo Dkt.Fred Heimbach(kulia)
 Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula(kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani kwa uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi ya Loswaki mwenyekiti wa Upendo Dkt.Fred Heimbach(kulia).
 Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula(kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani kwa uboreshaji wa miundombinu ya shule ya msingi Loswaki mwenyekiti wa ECLAT Peter Kiroya Toima(kulia).
 Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula akimkabidhi rasmi hati ya mradi wa shule ya msingi Loswaki kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mwalimu Ayub Mshana(katikati),anayeshuhudia katikati ni mwenyekiti wa Upendo Dkt.Fred Heimbach.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula(kushoto),mwenyekiti wa Upendo Dkt.Fred Heimbach(kulia) na mwenyekiti wa EcLAT Peter Kiroya Toima wakitoa zawadi za vifaa vya masomo kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Loswaki.
Picha zote na Novatus Makunga

TANZANIA YALAANI MAUAJI NCHINI MAREKANI


MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2019 MKOANI SIMIYU

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za viatu ndani alipotembelea Maonesho ya Nanenane 2019 ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani Simiyu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akitazama Asali na bidhaa nyingine alipotembelea Banda la Maonesho la Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia mashamba ya mafunzo alipotembelea  Maonesho ya Nanenane 2019 ambayo yanafanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia mashine ya kupura mazao ya kilimo husuani Mahindi, Mtama,Dengu, Choroko na Kunde alipotembelea Maonesho ya Nanenane 2019 ambayo yanafanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za nguo alipotembelea banda la JKT kwenye Maonesho ya Nanenane 2019 mkoani Simiyu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia ufugaji wa kisasa wa Samaki kwenye Bwawa la Samaki la JKT wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Simiyu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akinywa maji safi na salama yaliyochujwa kitaalam kwa mashine za kuchujia maji zilizobuniwa na Watanzania wakati alipotembelea Maonesho ya Nanenane mkoani Simiyu leo Agosti 4, 2019.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akilima kwa jembe la kukokotwa na trekta lililobuniwa na mjasiriamali na mbunifu wa zana za Kilimo alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 4, 2019.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla atembelea maonesho hayo katika viwanya vya Nyakabindi mkoani Simiyu leo Agosti 4, 2019.

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA AWATAKA WATAFITI NA WADADISI KUZINGATIA VIWANGO UKUSANYAJI WA TAKWIMU

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia) akizungumza
jambo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ofisi ya Dar es Salaam Ms Preet Arora(kushoto) muda mfupi baada ya kufungua mafunzo kwa wadadisi na wasimamiziwa utafiti wa sekta isiyo rasmi leo Jumapili (Agosti 4, 2019). Katikati niMtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu. 
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Ofisi ya Dar es Salaam, Ms Preet Arora
akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto
James, muda mfupi baada ya baada ya uzinduzi wa mafunzo kwa wadadisi nawasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi leo Jumapili (Agosti 4, 2019).
Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa pamoja na
Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu.(PICHA NA MAELEZO) 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (katikati waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na waddisi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchinimara baada ya kufungua mafunzo yao leo Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar esSalaam. Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa na kulia kwaMgeni rasmi ni Mkurugennzi Msaidizi- idara ya Ajira na Ukuzaji Ajira, Ofisi yaWaziri Mkuu, Bw. Ahmed Makbel. 
************* 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James amewataka wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchini kuzingatia viwango vya ubora katika ukusanyaji wa taarifa ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zenye kubaini mahitaji na changamoto za sekta hiyo nchini. 

Akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Sekta isiyo rasmi Nchini leo Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar es Salaam, Bw. James alisema matokeo ya utafiti huo yataisaidia Serikali kufahamu mchango halisi wa sekta isiyo rasmi katika Pato la taifa ikijumuisha ulipaji kodi. 

Aliongeza kuwa ni ukweli ulio dhahiri kuwa sekta isiyo rasmi imekuwa nguzo muhimu katika pato la taifa kwani kulingana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi uliofanyika mwaka 2014 ilibainika kuwa, asilimia 21.7 ya watu waliokuwa na ajira walikuwa katika sekta isiyo rasmi, na hivyo kuleta kiashiria kuwa sekta hiyo ina mchango muhimu katika pato la taifa. 

Bw.James alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejiwekea malengo mbalimbali katika kuinua uchumi wa wananchi wake ikiwemo kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta isiyo rasmi ikiwemo hali ya upatikanaji wa masoko, fursa za mikopo, ujuzi unaohitajika pamoja na matumizi ya teknolojia kwa nia ya kuongeza tija kwenye uzalishaji. 

“Sina shaka na ubora wa takwimu zitakazokusanywa kwa kuwa mnaendelea kufanya kazi hii kwa karibu sana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Benki ya Dunia (WB), tumieni uzoefu wenu ili na sisi Watanzania tunufaike kuifahamu zaidi sekta hii katika kukuza uchumi wa Tanzania” alisema Bw. James. 

Kwa mujibu wa Bw. James alisema utafiti wa kwanza wa kitaifa katika sekta isiyo rasmi ilifanyika nchini mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti kama huo katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1995, hivyo ni kipindi kirefu kimepita na kufanya kuwepo na mahitaji makubwa ya takwimu zinazoakisi hali halisi ya sasa ya sekta hiyo nchini. 

Kwa upande wake, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alisema hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kufanya utafiti huo ni uthubutu mkubwa kwa Tanzania kwa kuwa ni nchi chache za Bara la Afrika zimeweza kufanya utafiti huo kwa ajili ya kupima sekta yenyewe na upatikanaji wa rasilimali fedha sambamba na kubaini fursa za ajira kwa wananchi wengi wakiwemo wananchi maskini. 

“Kama mnayofahamu Serikali kwa sasa inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21 ambao unahitaji takwimu katika ngazi za chini za utekezaji, ili kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii kwa lengo la kufikia lengo la angalau asilimia 40 ya watu wenye ajira ifikapo mwaka 2020” alisema Dkt. Chuwa. 

Aidha Dkt. Chuwa alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeshakamilisha maandalizi yote ya kufanyika kwa utafiti huo, unaotarajia kuanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Mwezi Agosti hadi Novemba mwaka huu. 

Dkt. Chuwa alisema muundo wa utafiti huo umegawanyika katika ngazi kuu mbili, ikiwemo ngazi ya ukusanyaji wa taarifa katika ngazi ya kaya na ngazi ya pili ni ngazi ya biashara (uchumi), ambapo katika ngazi ya kaya, utafiti huo umejikita katika maeneo ya taarifa za kidemokrasia, elimu, hali ya ulemavu, ajira, ukosefu wa ajira. 

Akifafanua zaidi, Dkt. Chuwa alisema sampuli ya utafiti huo katika ngazi ya kaya pia utahusisha maeneo ya kuhesabia yapatayo 200 yaliyo mkoani Dar es Salaam na kaya zilizochaguliwa zaidi ya 2,400 pamoja na ukusanyaji wa taarifa kutoka kwenye biashara zaidi ya 4,000 na matokeo ya utafiti huo yatawezesha upatikanaji wa taarifa za kitakwimu ambazo ni wakilishi katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

ZOEZI LA KUPIMA UTAYARI WA KUKABILI EBOLA LA ACHA ALAMA MKOANI KAGERA

$
0
0

Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti 2019. 
Mratibu wa zoezi hilo toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dharura na Maafa, Dkt. Faraja akiendelea na shughuli za uwezeshaji wa zoezi la kupima utayari wa kukabili wa ugonjwa wa Ebola kwa watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera, Agosti 2019. 
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kuvaa vifaa kinga kwa ajili ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti 2019. 
Afya wa Afya katika Kituo cha Afya Bunazi mkoani Kagera,akiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti 2019. 
Waratibu wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, wakiendelea kufafanua utekelezaji wa zoezi hilo kwa mtumishi wa Afya katika kituo cha Afya cha Bunazi, mkoani Kagera Agosti 2019. 
Watumishi wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa, Bukoba, mkoani Kagera,wakiendelea kufanya mazoezi ya namna ya kuvaa vifaa kinga kwa ajili ya kumhudumia mgonjwa anayehisiwa kuwa na maabukizi ya ugonjwa wa Ebola, katika hospitali hiyo Agosti 2019. 
Waratibu wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, wakiendelea kuelekeza namna ya kuvaa vifaa kinga kwa watumishi wa Afya katika kituo cha Afya cha Bunazi, mkoani Kagera Agosti 2019. 

****** 

Na. OWM, KAGERA 

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo, imefanikiwa kufanya zoezi la kupima utayari wa kukabili ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Kagera katika wilaya tatu za mkoa huo kwa kuhusisha watoa huduma za Afya katika wilaya hizo za Bukoba, Misenyi na Ngara. 

Zoezi hilo limefanikiwa kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo wakipatina, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kagera. 

Akiongea kuhusu kuhitimishwa kwa zoezi hilo jana tarehe 3 Agosti, 2019, mkoani Kagera, Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa, ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu, ameeleza kuwa watumishi wa sekta ya Afya katika maeneo yote ambayo zoezi hilo limefanyika wameweza kuimarishwa katika suala la uratibu hususani katika kuhakikisha kuwa rasilimali zote zinazohitajika pindi ikigundulika kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola zinapatikana kwa wakati na kwa kutosheleza mahitaji pamoja na kutumika kwa usahihi. 

Aidha, Mratibu wa zoezi hilo toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dharura na Maafa, Dkt. Faraja Msemwa amefafanua kuwa timu ya wataalamu wa sekta za Afya na Uratibu wa Shughuli za serikali, kutoka Wizarani, Idara na Mashirika ya Kimataifa, wamefanikiwa kuendesha zoezi hilo kwa watoa huduma wa Afya kwa wilaya tatu za mkoa huo hususan zilizopo mipakani. 

“Zoezi letu tumefanikiwa kulihitimisha mkoani hapa tayari kwa kufanya zoezi la kupima utayari wa kukabili ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma wa Afya kwa vituo vya Afya vya Nshambya, Kabyaile, Kabanga, Bunazi pamoja na Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Bukoba.Tunaamini kufanikiwa kufanya zoezi hili limeboresha utendeji wa watoa huduma hao katika kukabili ugonjwa wa Ebloa” alisema Dkt. Msemwa 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Marco Mbata amefafanua kuwa kufanyika kwa zoezi hilo mkoani humo kumewawezesha kujua maeneo gani ya kuboresha wakati wa ugonjwa wa Ebola na watumishi wameelewa kwa vitendo wapo tayari kukabili ugonjwa huo. 

“Tunashukuru vifaa tunavyo vya kutumia wakati wa kujikinga iwapo atatokea mgonjwa wa Ebola, hivyo kupitia zoezi hili tumeongeza uelewa wa kujikinga wenyewe, kuwakiknga watu walio karibu na mgonjwa pamoja na jamii nzima. Tumeweza kujifunza jinsi ya kumpokea mgonjwa, kuchukua vipimo hakika zoezi hili limetujenga ” alisisitiza Mbata. 

Naye Mratibu wa Vituo vya Mipakani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Remedius Kakuru amebainisha kuwa kupitia zoezi hilo limeimarisha utendaji wa maafisa Afya wa mipakani kwa kuzingatia kuwa tayari serikali imenunua vifaa vya kisasa muhimu vinavyo hitajika kwa ajili ya utambuzi wa abiria mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ikiwemo Vipima joto la mwili “themo scanners”.Vifaa hivyo vyenye uwezo wa kupima joto la mwili la abiria wanao pita katika mipaka ya Tanzania vina uwezo wa kupima joto la mwili kwa kuwa ndiyo kiashiria kikuu kimojawapo kwa mgonjwa mwenye maabukizi ya Ebola . 

Kwa upande wake Afisa anayeshughulika na Magonjwa ya Mlipuko kutoka Shirika la Afya Duniani, hapa nchini, Anthony Kazoka alieleza kuwa Shirika la Afya Duniani linaendelea kushirikiana na serikalai ya Tanzania katika kulinda Afya za watu wake kwa kutoa utaalamu katika zoezi hilo kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimo hatarini kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Hivyo kwa kufanyika zoezi hilo kwa mafanikio kutasaidia Tanzania kuwa salama na kuwa chanzo cha kuiweka Dunia salama kwa kutambua maabukizi ya ugonjwa huo mapema iwapo yatatokea. 

Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa ya mipakani ukiwemo mkoa wa Kagera. Mkoa huo ambao unapakana na nchi ya Uganda ambayo inapakana na DRC lakini pia imekuwa na wagonjwa kadhaa wa Ebola. 

Zoezi hilo linaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ambao ni WHO, FAO, USAID, HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu. Zoezi hilo limefanyika kwa muda wa wiki moja ambapo limekamilika tarehe 3 Agosti mwaka 2019, kwa kufanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya mkoani wa Kagera.

Ocean Road yavuka lengo kambi maalum uchunguzi homa ya ini

$
0
0
NA MWANDISHI MAALUM - ORCI 

TAASISI ya Saratani Ocean Road (ORCI) imefanikiwa kuvuka lengo walikojiwekea kuwachunguza watu 1000 kujua iwapo wana maambukizi ya virusi vya homa ya ini, katika kambi maalum ya uchunguzi iliyofanyika Julai 27 hadi 31, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo leo kueleza tathmini ya kambi hiyo iliyofanyika hospitalini hapo kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kinga ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa amesema mwitikio wa watu kujitokeza kuchunguzwa afya zao ulikuwa mzuri.

"Tulipanga kuwachunguza watu 1000 katika siku hizo tano, tumefanikiwa kuwachunguza watu 1197, kati ya hao 49 tumewagundua tayari wana maambukizi ya homa ya ini," amesema.

Amesema watu hao waliokutwa na maambukizi wanaendelea kufanyiwa vipimo zaidi ili waweze kupangiwa aina ya matibabu wanayostahili.

"Mtu akichunguzwa kwa kipimo cha kwanza Screening test, akigundulika ana maambukizi anapimwa tena kwa vipimo vya ziada Confirmatory test, tunaangalia hatua ambayo ugonjwa upo ili tuweze kumpangia matibabu anayostahili," amesema. 

Amesema kambi hiyo ilifanykma ili kuenda sambamba na kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo 'Tafuta mamilioni ya watu wenye maambukizi ya homa ya ini wasiojulikana'

Amesema kambi hiyo uchunguzi ilifanyika bila malipo na kwamba baada ya kuhitimika huduma za uchunguzi zinaendelea katika utaratibu wa kawaida wa kila siku hospitalini hapo, kwa watu kuchangia gharama.

MKUTANO MKUU WA SADC WAIVA, WANAWAKE NA VIJANA FURSA NJE KUONESHA GUNDUZI ZAO

$
0
0



*Mwito watolewa kwa wafanyabiashara kujitokeza na kutangaza bidhaa zao


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambao utatanguliwa na wiki ya viwanda itakayoanza kesho kwa kuzinduliwa rasmi na Rais Dkt. John Joseph Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutengeneza masoko na kupata oda kutoka nchi 16 zinazoshiriki mkutano huo.

Akizungumza katika kilele cha siku ya wanahabari leo jijini humo Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa mkutano huo ni fursa kwa watanzania hasa wafanyabiashara katika kutangaza bidhaa zao, kupata ujuzi mpya na kutafuta masoko.

"Niwaombe wananchi watumie fursa hii adhimu katika kutangaza bidhaa zao, kupokea oda, kubadilishana na kupokea ujuzi kutoka kwa wageni pamoja na kujenga ushirikiano wa hali ya juu na wageni wetu, na mmeona hata uzito uliopewa na viongozi wetu Rais Magufuli atazindua wiki ya viwanda kesho na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein atafunga wiki ya viwanda Agosti 8 hivyo tuwaunge mkono" ameeleza Mhandisi Manyanya.

Kuhusiana na idadi ya wananchi waliojiandikisha kushiriki katika maonesho hayo Mhandisi Manyanya ameeleza kuwa zaidi ya watu 2000 wamejiandikisha huku wengi wakiwa wazawa hali inayoashiria watanzania wamekubali mabadikiko na kasi ya maendeleo yanayoongozwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

"Hadi kufikia jana idadi ya washiriki waliojiandikisha ilifikia 2000, huku wazawa wakiwa zaidi ya 700 na watakaoonesha bidhaa mbalimbali wakifikia zaidi ya 900. Kwa hali hii tunategemea matokeo chanja na maendeleo kupitia mkutano wa 39 wa SADC" Ameeleza.

Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kuendeleza desturi ya ukarimu na uzalendo katika kipindi chote Cha mkutano ili kuweza kuendelea kupeperusha vyema bendera ya amani ya nchi yetu.

Vilevile kaimu Mkurugenzi wa mipango wa sekta ya viwanda na ushindani Dkt. barani Afrika Dkt. Johansein Rutaihwa amesema kuwa malengo ya wiki ya viwanda ni pamoja na kutoa elimu ya uelewa kuhusu mpango wa maendeleo hasa maendeleo ya viwanda uliogawanya katika vipindi vitatu ambavyo ni ule wa mwaka 2015/2020, 2021/2050 na ule 2051/2063 mikataba ambayo iliidhinishwa mwezi Machi mwaka 2015.

Amesema kuwa wiki ya viwanda imelenga kuleta ushirikiano pamoja na kutengeneza mnyororo katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na kubwa kuliko nikuwashirikisha wanawake na vijana katika sekta ya viwanda kwa kuwapa fursa za kuonesha gunduzi zao.

Mkutano huo wa Jumuiya ya Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ulifanyika nchini mwaka 2003 ambapo Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa alihudumu nafasi ya uenyekiti kwa mwaka 2003/2004 na mwaka huu Rais Magufuli atapokea kijiti hicho kutoka kwa Rais wa Namibia Hage Geingob na atahudumu nafasi ya uenyekiti kwa muhula mmoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za kikanda na mikutano ya kisekta ikiwemo afya na elimu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO HUSSEIN BASHE ATEMBELEA BANDA LA BENKI KUU YA TANZANIA BoT MAONESHO YA NANENANE KITAIFA VIWANJA VYA NYAKABINDI, SIMIYU

$
0
0

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (aliyenyoosha mikono), akizungumza wakati alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenye maonesho ya nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. Maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu ya "Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa nchi yamefunguliwa rasmi Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na yatafikia kilele Agosti 8, 2019.
Mhe. Bashe (kulia), akisindikizwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Meneja wa Idara ya Uhusioano wa Umma na Itifaki, (BoT), Bi. Zalia Mbeo (katikati), wakayti akitoka kwenye banda hilo baada ya kulitembeekla.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, (kulia), akisainin kitabu cha wageni huku akisikilizwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT Bw. Lwaga Mwambande (kushoto).
Mhe. Bashe akiuliza maswali ili kupata ufafanuzi kutoka kwa watumishi wa BoT alipotembelea banda la taasisi hiyo inayosimamia masuala ya kifedha hapa nchini. (Picha:Innocent Mmari-BoT).

WCF MBIONI KUANZISHA MFUMO WA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI KUWASILISHA MADAI YA FIDIA KIMTANDAO

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), hivi karibuni uko mbioni, kuanzisha mfumo wa waajiri na wafanyakazi kuwasilisha madai ya Fidia kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anselim Peter ameyasema hayo jana kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Bw.Peter alisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kusogeza karibu huduma za Mfuko kwa wateja wadau wake na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kupata fursa ya kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi kuhusu shughuli za Mfuko ambazo ni kulipa Fidia, utaratibu gani wa kufuata ili kuwasilisha madai kabla ya kulipwa Fidia.
"Pia katika banda la WCF hapa Nyakabindi, wataalamu wetu watatoa elimu kuhusu Mfuko, kusajiliwa, kuwafahamisha taratibu za michango, kuwafahamisha taratibu za madai ya fidia na pia kupokea maoni ya wadau kuhusu Mfuko. Lakini pia tunatoa huduma kwa vitendo jinsi wanavyoweza kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi wake kwenye orodha iliyoko WCF, kuprinti cheti, na pia kulipa michango ofisini kwako.” Alifafanua Bw. Peter.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko huo kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa kujenga kiwanda cha kutengenza vifaa tiba Huu ni utekelezaji kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuanzisha na kuimarisha viwanda ambavyo vitaipeleka nchi kafika uchumi wa Kati.
"Nishukuru na kutambua mchango mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba na WCF kwa ujumla kwa sababu ni partner (Mshirika) Mkubwa kwenye mipango yetu ya ujenzi wa kiwanda cha Vifaa tiba." Alisema Mhe. Mtaka.
Alisema uongozi wa Mkoa walishirikiana na WCF katika hatua mbalimbali za kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda hicho ambapo tayari site clearance imeshafanyika na kwamba hivi sasa wizara iko katika nafasi nzuri ya kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga kiwanda hicho.
"Kwetu sisi kama mkoa WCF imetoa ushirikiano mkubwa katika mipango yetu ya kushiriki katika uchumi wa viwanda wametoa ushirikiano mkubwa." Alisema Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (watatu kushoto), akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter (katikati) na Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, wakati alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Simiyu 
 Afisa Uhusiano Mwandamizi WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia) akitoa elimu ya Fidia kwa wafanyakazi
 Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa elimu hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akisalimiana na mama huyu aliyefika banda la WCF kupata elimu ya Fidia kwa wafanyakazi


TANZANIA YALAANI MAUAJI YA WATU WASIO NA HATIA MAREKANI

Utapeli kwa kutumia simu za mkononi waendelea kudhibitiwa.

$
0
0
Matapeli wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya Tigo Pesa inayotolewa na kampuni hiyo ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati kiukweli sio waajiriwa wa Tigo.

 Matapeli hao utumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadae wamezitumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Hawa watu wana mbinu mbalimbali, tukitolea mfano, kuna ambao watakupigia wakisema aidha wamekutumia hela kimakosa, au anakupigia kutoka makao makuu ya kampuni ya simu husika na angependa utatue tatizo ambalo mteja amelalamikia.

Tulipata nafasi ya kumuhoji wakala mmoja, kwa jina la Amos Chirwa kutoka Kijichi, ambae alisema, " kwa kweli matapeli ni wengi, na kila siku wanabuni njia tofauti tofauti ili waweze kutuibia sisi mawakala au wateja".

"Mimi kama wakala, ambae nina uzoefu wa miaka 6 sasa, ningependa kuwashauri watanzania kwa ujumla, kwamba usimpe mtu namba yako ya siri, au taarifa binafsi hata kama amejitambulisha kama mfanyakazi wa kampuni za simu kama Vodacom, Airtel, Tigo au Zantel". Alimalizia kwa kusema.

Mtandao huu ungependa pia kuwaasa watanzania kutojishirikisha na masuala ya kiuhalifu hususan katika masuala ya simu za mkononi kwani serikali ina mkono mrefu.

WANANCHI WA KIJIJI CHA MPETU MKOANI SINGIDA WAMPONGEZA MBUNGE KINGU

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akihutubia Wananchi wa Kijiji cha Mpetu katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akiwa na viongozi wa Kata ya Muhintiri mbele ya gari lenye mtambo wa kuchimba maji katika Kijiji cha Mpetu. Maji yaliyopatikana katika kijiji hicho yatakuwa yanatoka lita 11,000 kwa saa.
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea.
Mchungaji Josephat Michael wa Kanisa la Pentecoste F.P.C.T. la Kijiji cha Mpetu akiuombea mkutano huo.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Muhintiri, Bahati Mkungile akiwatambulisha wataalamu waliopo katika kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzì (CCM) wa kata hiyo, Maliko Deu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpetu, Yona Hongoa akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Muhintiri, Peter Lyimo akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wana CCM wa Kijiji cha Mpetu wakiwa wamembeba, Shabani Ramadhani aliyehamia chama hicho kutoka Chadema.
Jonatha Nkhundi aliyehamia CCM kutoka Chadema akizungumza.
Wanakwaya ya Huruma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Muhintiri wakitoa burudani.




Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kijiji cha Mpetu Kata ya Muhintiri wilayani Ikungi mkoani Singida wamempongeza Mbunge wao wa Singida Magharibi, Eribariki Kingu kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya katika jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali.

Hayo yalibainishwa jana na mkazi wa kijiji hicho, Yona Hongoa katika mkutano wa hadhara aliouandaa mbunge huyo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwahamasisha 

kujitokeza kwa wingi kujiandika katika daftari la kudumu la mpiga kura na kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata ushindi kwenye chaguzi zake kuanzia wa viongozi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.

"Kwa kweli tunampongeza mbunge wetu kwa kazi kubwa anayoifanya katika jimbo letu kwani tangu kijiji chetu kianzishwe hatukuwahi kuwa na maji lakini amefanikisha kutuletea ikiwemo ujenzi wa shule, Zahanati pamoja na barabara" alisema Hongoa.

Diwani wa Kata ya Muhintiri, Peter Lyimo akizungumza katika mkutano huo alisema katika utekelezaji wa ilani ya CCM, Mbunge huyo ameweza kuchangia fedha nyingi kutoka mfukoni mwake na mfuko wa jimbo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

" Kwa kazi hii kubwa anayoifanya mbunge hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya" alisema Lyimo.

Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji na kuwa kazi hiyo inaendelea jimboni humo.

Kingu alisema kuna zaidi ya sh.milioni 300 zimeelekezwa kutekeleza mradi wa maji katika kijiji hicho.

NHIF ARUSHA YATOA HUDUMA ZA VIPIMO NA USHAURI WA AFYA BURE VIWANJA VYA NANENANE

$
0
0
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Miraj Kisile(kulia) akizungumza na mmoja wa wananchi waliofika katika banda hilo kwenye maonesho ya Nanenane Njiro jijini Arusha.
Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la NHIF kwenye uwanja wa maonesho ya Nanenane jijini Arusha akipewa ushauri baada ya kupima afya bure.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Miraj Kisile(kulia) akizungumza na wananchi waliotembelea maonesho ya Nanenane na kufika katika banda hilo kwaajili ya kufahamu shughuli za mfuko huo na kupima afya bure.
Mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la NHIF kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane mkoa wa Arusha akifurahia maelezo yanayohusu sekta ya afya.





Wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kupata huduma za ushauri na kupima afya bure kwenye maonesho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi maarufu Nanenane viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha.

MWINYI ZAHERA ATARAJIA MAKUBWA KWA TIMU YAKE MSIMU HUU

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA mkuu wa Timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema kwa msimu huu ameweza kusajili wale wachezaji aliowataka hususani katika safu ya ushambuliaji.

Zahera amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Kariobang Sharks uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.

Amesema, anaanini kuelekea msimu ujao wa 2019/20 kikosi chake kitakuwa ni bora zaidi ya msimu uliopita na watakuwa kwenye mwendo wa mchakamchaka kwani hakuna mchezaji atakayekuwa anatembea uwanjani. 
Zahera amesema ushindani msimu ujao ni mkubwa naye amejipanga kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani mkubwa msimu ujao.

"Nimefurahi kuona mashabiki wengi wamejitokeza leo uwanja wa Taifa, hichi ni kitu ambacho tulikikosa msimu uliopita hivyo msimu ujao waendelee kujitokeza kwa wingi."Kazi yetu msimu ujao itakuwa ni kote kwani hatuna mchezaji atakayekuwa anatembea wote wanakimbia mwanzo mwisho," amesema.

Kwenye mchezo huo, Kariobangi Sharks waliweza kutangulia kwa kufunga bao dakika ya 48 kupitia kwa Patrick Otieno na baada ya dakika tisa, Yanga wanasawazisha kwa mkwaju wa Penati kupitia kwa Patrick Sibomana dakika ya 57.

Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa na Ushindani mkali kwa kila timu kutafuta matokeo, Yanga wametengeneza nafasi nyingi kupitia kwa Patrick Sibomana ambaye amekuwa ni moto wa kuotea mbali kipindi cha kwanza akicheza vizuri na mshambuliaji kutoka Namibia Sadney Urikhob.

Kabla ya mchezo huo kulitanguliwa na mechi kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva, Maveteran wa Yanga na Maveteran wa Pamba.Pia, walitumia siku ya leo kutambulisha wachezaji wao wapya waliosajiliwa msimu huu pamoja na jezi zao.

Mashabiki wa Yanga waliweza kujitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kubeba watu 60,000.ni kama wote uwanja wa Taifa leo kwenye kilele cha Mwanachi.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Farouk Shikhalo, Moustafa Selemani, Muhaeami Issa ‘Marcelo’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohammed Issa ‘Banka’/ Mrisho Ngassa dk65, Sadney Urikhob/ David Molinga ‘Falcao’ dk87, Juma Balinya/ Maybin Kalengo dk82 na Patrick Siebomana.

Kariobangi Sharks: Brian Bwire, Eric Juma/David Simiyu dk82, Samuel Qlwande, Kyara Amani, Nixon Omandi, Yidah Sven, Shaphan Oyugi/James Mazembe dk59, Harrison Mwendwa, Patrick Otieno/ Julius Masaba dk54/Peter Oudo dk88, Patrick Nguyi na Erick Kapato.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images