Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

WANANCHI SINGIDA WATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MBUNGE WAO

0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akivikwa shada la maua baada ya kuwasili Kijiji cha Kitandaa kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara wilayani Ikungi mkoani Singida jana. Mbunge Kingu alifanya mikutano miwili katika kijiji hicho na makao makuu ya Kata ya Mtunduru.
Wakina mama wa Kijiji cha Kitandaa wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea Kijiji cha Kitandaa.
Mbunge Kingu akisalimiana na wazee wa Kata ya Mtunduru baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mkutano.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzì (UVCCM) wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Ikungi, Himid Tweve, akiimbisha wimbo wa viongozi wamechachamaa.
Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpakii akizungumza.
Wanawake wa Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akihutubia kwenye mkutano huo wa Kata ya Mtunduru.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale, Singida

DIWANI wa Kata ya Mtunduru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Ramadhani Mpakii amesema jitihada zinazofanywa na Mbunge wao Elibariki Kingu za kuwapelekea miradi ya maendeleo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa Jimbo la Singida Magharibi.

Akizungumza kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge huyo katika vijiji vya Kitandaa na Mtunduru Mpakii alisema haijawahi kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.

" Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye ni msikivu na amejitahidi sana kutuletea maendeleo katika Kata yetu ebu tumuache aendelee kututumikia kwa kipindi kingine kwanza umri wake bado ni mdogo " alisema Mpakii.

Alisema katika kata hiyo ameweza kujenga shule, zahanati, na sasa amewaletea mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh.milioni 405 ambao utasambaza maji kwenye vijiji vyote vya kata hiyo.

Mpakii aliongeza kuwa tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais Dkt.John Magufuli na Mbunge huyo ya kuwapelekea miradi hiyo itawarahisishia upatikanaji wa kupata kura nyingi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mtaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

" Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya" alisema Mpakii.

Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwa wananchi wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita ndani ya jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji 24 huku mchakato wa kupata umeme wa REA ukiendelea na kuwa amepata fedha zaidi ya sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Sekondari ya Mtunduru.

Wakati huo huo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji, ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo hayo yakiwa na wawakilishi.

DKT. MWANJELWA AAGIZA KUONDOLEWA KWA MRATIBU WA TASAF MKOA WA KAGERA

0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameagiza kuondolewa kwa Bw. Efraz Mkama katika nafasi ya Uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Kagera kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 

Dkt. Mwanjelwa ametoa maagizo hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustin Kamuzora baada ya kutembelea walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Bukoba kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji. 

Naibu Waziri huyo, amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unapaswa kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambayo ina dhamira ya dhati ya kuziwezesha kaya maskini kuboresha maisha. 

Dkt. Mwanjelwa ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mratibu huyo wa TASAF Mkoa wa Kagera na hivyo kutaka nafasi hiyo apewe mtumishi mwingine ambaye ana vigezo na uwezo wa kutekeleza maagizo ya Serikali kikamilifu kupitia utaratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa ufanisi zaidi. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa ameridhishwa na mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika nyanja za elimu, afya, uzalishaji mali na ujenzi wa nyumba unaofanywa na walengwa wa mpango huo mkoani Kagera. 

“Nimejionea namna wanufaika wanavyotumia rukuzu wanayoipata kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba bora za kuishi, kujishughulisha na kilimo, ufugaji na kugharamia mahitaji muhimu ya elimu na afya,” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza. 

Dkt. Mwanjelwa amesema, kwa kutambua mchango wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali imeamua kutekeleza sehemu ya pili ya Mpango huo ambayo itatilia mkazo zaidi kwa walengwa kufanya kazi katika miradi itakayoibuliwa kwenye maeneo yao na kupata ujira kama njia mojawapo ya kuijiongezea kipato. 

Akizungumzia suala la kutotekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika baadhi ya maeneo, Naibu Waziri huyo amesema, Serikali imeamua kutekeleza Mpango huo katika maeneo yote nchini ili kuwafikia wananchi wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na umaskini. 

Dkt. Mwanjelwa yuko mkoani Kagera katika ziara ya kikazi kujionea utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma katika Halmashauri zote za mkoa huo. 

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) YASISITIZA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUKATA BIMA YA KILIMO

0
0
Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akitoa ufafanuzi kuhusiana na Bima ya Kilimo katika maonyesho ya 26 Kanda ya kaskazini Njiro Mkoani Arusha.
Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA:amesisitiza wakulima wanaodai malipo ya Bima wafike banda la TIRA kwaajili ya msaada zaidi
Meneja wa TIRA kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akisisitiza kwajambo mteja kama anavyoonekana katika picha,kushoto kwake ni Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA 





Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA imepitisha na kutoa mwongozo wa Bima ya kilimo ikiwa na maana ya kusisitiza wananchi ambao wanajihusisha na kilimo kwenda katika maonyesho ya 88 ili waweze kupatiwa huduma ili kukinga kilimo chao na mifugo yao .

Eliezer Rweikiza ni Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini amesema kuwa yapo makampuni ambayo ni mahususi kwa huduma hiyo na siyo makampuni yote yanatoa huduma ya kilimo na mifugo .

Amesema hivi karibuni Mamlaka hiyo imeendesha mafunzo kwenye vikundi takribani 50vinavyojumuisha VICOBA,SACOS,AMCOS, pamoja na wajasiriyamali ambao wamejipanga kujieleza jinsi ya kupata hizo huduma za kilimo

Ameainisha vijiji ambavyo wametoa elimu kwa ujumla kwa mkoa wa Tanga Mjini vipo 10.Muheza 12,Korogwe 11,Babati 6,na Hanang 8.

Rweikiza mesema huduma hizo zimekuwa zikutolewa zaidi ya miaka mitano nyuma ila kwa sasa zinakuwa na vitu ambavyo vimeboreshwa zaidi kwani zipo huduma hadi kwa wakulima wadogo

Rweikiza amesema kuwa mkulima anapokata bima ya kilimo inamkinga na majanga kwani mkulima akipata hasara anafidiwa na kampuni husika vilevile mkulima anakuwa amekinga uchumi wake hakiti nje ya ulingo unabakia palepale

Kahiyo hii bima ni muhimu sana kwa wote wanaolima kilimo kikubwa au kilimo kidogo ,yote haijalishi huduma ya bima ipo inahusika ,kwahiyo tunawataka sana wananchi hasa kanda ya kaskazini wakate bima ya Kilimo na Mifugo 

Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA amesema kuwa katika msimu huo wa nanenane watashughulika na malalamiko ya wananchi amabapo wanayadai makampuni mbalimbali ya bima ambapo madai yao hayaja shughulikiwa hadi sasa,na kuwasaidia namna gani wanaweza kulipwa madai yao yale yanayolipika.

Sambamba na hayo amesema kuwa watashughulika namna ya kutoa ushauri kwa kwa watu ambao wanahitaji kusajili makampuni yao katika kufanya shughuli za Bima,kwa maana ya wale wanaohitaji kufanya udalalali,Mawakala,sambamba na wale wanaotaka kufanya kazi ya ukadiriaji hasara za Kibima

Amesema kuwa miongozi mwa kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa masoko ya Bima linakuwa linaendeshwa kwa uhuru,wazi, faida kwa watu amabao ni wanufaika katika shughuli za Bima.

Ametoa wito kwa wakazi wa kanda ya kaskazini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo kwani wamegundua ya kwamba uwelewa wa bima bado haujawa mkubwa hivyo wananchi watembelee banda la TIRA sambamba na mabanda mengine yanayojihusisha na shughuli za bima katika mtaa wa Bima.

Maonyesho hayo ni ya 26 yaKilimo na sherehe za nanenane yanayoendelea Themi Njiro Mkoani Arusha yamebeba kauli mbiu isemayo: Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi

TEKNOLOJIA YA NYUKLIA KUWA MKOMBOZI KWENYE UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA MAZAO NA MIFUGO

0
0
Simon Mdoe Mtafiti mwandamizi wa teknolojia ya Nyuklia akiwa katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha.
Simon Mdoe Mtafiti Mwandamizi wa teknolojia ya Nyuklia akimpatia mteja elimu ya teknolojia ya nyuklia katika kilimo mteja Gadiel Kitomari alipotembembelea banda hilo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha
Peter Ngamilo ni mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAEC akimpatia mteja elimu ya teknolojia ya nyuklia katika kilimo mteja Gadiel Kitomari alipotembembelea banda hilo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha


Na Vero Ignatus, Arusha

TUME ya Nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) imefanikiwa kupata matokeo chanya ya utafiti wa mbegu ya mpunga ya Super Bc kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya kununurisha vinasaba (viasili)vya mbegu hizo
na kupelekea mavuno mengi zaidi visiwani Zanzibar.

Simon Mdoe ni Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya Nyuklia, na Michuzi Blog kwenye maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini amesema utafiti huo ulioanza 2009 umefanikisha matokeo chanya mara saba zaidi kwa mavuno ya mbegu ya mpunga ya Super Bc huko visiwani Zanzibar ikilinganishwa na awali.

Amesema TAEC kwa kushirikiana na shirika la mbegu la Zanzibar, ZARI na pamoja na chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ilianza utafiti wa mbegu hiyo ambapo walinunurisha kupitisha mionzi kitaalamu kwenye mbegu) ambayo ilibadilisha viasili (vinasaba) na kuwa bora zaidi kuweza kuzalisha mara saba ya mazao yaliyokuwa yakizalishwaawali.

“Utafiti wetu tulichukua mbegu za mmea wa mpunga na kupitisha miale ya nyuklia kwa hatua sita, huku kila hatua moja tukihamishia mbegu shambani na kupata matokeo tofauti, mara ya mwisho tulipata matokeo mazuri zaidi kuliko hatua nyingine tano na kugundua kuwa na mavuno yamefikia mara saba ya kawaida ya mbegu hizo kama mkulima anavuna magunia 19 kama ambavyo imezoeleka kwa mbegu za zamani na alipotumia mbegu zetu alipata gunia 80 za mpunga.alisema Mdoe

Mtafiti huyo amesema baada ya matokeo ya utafiti walishirikisha mashirika ambayo pia yalialika maduka ya mbegu visiwani Zanzibar na kuwapelekea wakulima ambao walipata matokeo hayohayo mazuri mara saba zaidi
tofauti na awali kabla ya utafiti.

Mdoe amesema pia matokeo mengine ya utafiti na kuboreshwa kwa mbegu kupitia mionzi ya nuklia yamebaini kuongezekana kwa ladha ya mchele uliotokana na mpunga wa Super Bc, pamoja na harufu nzuri kwa walaji.

“Alisema pia matokeo ya tafiti yameonyesha mbegu hiyo kutoshambuliwa
na wadudu wakati wa kuota na ukuaji wake”alisema Mdoe
Mtafiti huyo alisema TAEC kwa kushirikiana na Chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA) wanaendelea na utafiti ili kununurisha mbegu nyingine za mpunga, zaidi ya Super Bc kwa kuzingatia hali ya hewa na maeneotofauti ya Nchi na aina ya udongo ili kupata tija itokanayo na mavuno mengi kwa ustawi wa Uchumi wa Nchi.

Mdoe amesema utafiti wa kununurisha mbegu hizo unafanyika kwenye kituo cha utafiti cha Ilonga Mkoani Morogoro na katika kituo cha Mati kilichopo eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Tafiti nyingine kama hizo za mbegu za Mahindi na shairi zinazofanyika katika Kituo cha utafiti wa mbegu za Kilimo cha SELIAN, Arusha ambazo ununurishaji umeshafanyika na tayari mbegu hizo ziko kwenye hatua za mpando wa awali ambapo hatua yenye ubora wa juu utakapofikia tamati, zitasambazwa kupitia njia zilizofanyika Zanzibar kwa wakulima ili kuongeza mavuno na kukuza uchumi wa wakulima na Taifa kwa pamoja.

Amesema TAEC/(TAHA)kwa pamoja wako kwenye upembuzi yakinifu ili kuona namna ya kununurisha mboga mboga,matunda na maua ili kuhifadhika kwa muda mrefu na unaofaa pindi bidhaa inapokuwa sokoni kwa muda ili isiharibike kwa urahisi kwani uzoefu unaonyesha asilimia 40 ya matunda na mboga ,boga huharibika kwa kuoza kutokana kukosa teknolojia kama hiyo ya mionzi.

Amesema tafiti nyingine zinafanyika kwenye mbegu za wanyama kama N’gombe kwa njia ya uhamilishaji kwa kushirikiana na Tasisi ya mifugo ya uhamilishaji iliyopo Usa ya (NIC) ili kupata mifugo bora inayokidhi viwango vya ndani na nje kwa nyama bora.

Peter Ngamilo ni mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAEC ambapo amesema shirika hilo lina matarajio ya kuwa na mtambo wa kuzalisha vyanzo vya mionzi (Linear Acceletor)vinavyotumika kwenye matibabu, viwanda,

kilimo na utafiti (Radioisotopes)

Aidha TAEC ina matarajio ya kuanzisha mradi wenye kutumia teknolojia ya nuklia katika kufanya tafiti mbalimbali (Nuclear Research Reactor)Zenye manufaa kwa Nchia ambapo Mtambo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na viwanda vya madawa ya tiba ya saratani pamoja na kutumika kama nyenzo ya kufundishia katika taasisi za elimu ya juu na
utafiti.

Tume ya nguvu ya Atomiki (Tanzania Atomic Energy ommission)ilianzishwa kwa sheria ya Bunge no 7 ya Mwaka 2003, awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya taifa ya mionzi iliyoanzisha kwa sheria ya bunge no 5 Mwaka 1983 ambapo ina majukumu ya kuthibiti matumizi ya mionzi salama Nchini, kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojiaya Nyuklia na kufanya utafiti.

WAZIRI LUGOLA AONGOZA KIKAO CHA TUME YA UTUMISHI YA POLISI, UHAMIAJI NA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

0
0

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akizungumza katika Kikao cha Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo katika Wizara hiyo. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


MKUU WA MAJESHI AWATAKA WANAJESHI KUFUATA MISINGI YA MAADILI YA JESHI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKUU wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Wanajeshi ambao wanaendelea kutumikia taifa kufuata misingi na maadili ya Jeshi ili wanapomaliza muda wao wa kazi waagwe kwa heshima. 

Mabeyo amesema hayo wakati wa hafla ya kuwaaga Majenerali 9 ambao wamestaafu utumishi wa Jeshini ambapo amesema mwanajeshi ili apewe heshima anatakiwa awe na nidhamu awapo kazini. 

Amesema Majenerali hao ambao wamestaafu kwa muda wa miaka mitatu wataendelea kuwa washauri katika jeshi la akiba. "Ambao bado wapo makazini wajitaidi kuwa na nidhamu ili wakati wanastaafu wapewe heshima kama hii ya leo,”amesema .

“mwanajeshi akistaafu uagwa kiheshima pindi anapostaafu tofauti na ukifukuzwa uwezi kupewa heshima”
Nao Baadhi ya Majenerali ambao wamestaafu waliwataka wanajeshi ambao wamebaki kuitumikia nchi kwa moyo mmoja. 

Joyce Kabatiambaye ni mmoja wa Majenerali hao aliwahasa wazazi na walezi kuacha dhana potofu kuwa watoto wa jinsia ya kike awawezi kuwa wanajeshi. Dk.Denis Janga ameelza katika kipindi chake cha utumishi wa jeshi alikua Daktari na alishiriki Vita vya Uganda hivyo aliwahasa wananchi kulinda amani iliyopo na kuepukana na migogoro kwa vita si nzuri
"Niliyoyashuhudia wakati wa ile vita sitaki kuona yanatokea maana watu walipata shida sana "amesema

Aidha wanajeshi hao wastaafu wamemshukuru mwenyezi mungu kwa kuwasaidia kumaliza kipindi chao salama na kupata heshima ya kuagwa kwa Amani.Wanajeshi walioagwa ni P6693 Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor mstaafu, P3726 Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi mstaafu, P3649 Meja Jenerali Denis Raphael Janga mstaafu, P7696 Brigedia Jenerali Zoma Mathic Kongo mstaafu, 

P7833 Brigedia Jenerali Nicodems Elias Mwangela mstaafu, P6090 Brigedia Jenerali Charo Hussein Yateri mstaafu, P8019 Brigedia Jenerali Raymond Kusirie Mwanga mstaafu, P8023 Brigedia Jenerali Juma Hidaya Mwinula mstaafu na PW 0131 Brigedia Jenerali Joyce Luli Kabati mstaafu.
 Mameja Jenerali, kutoka (kushoto) Gaudence Milanzi, Issa Suleiman na Denis Raphael, wakitoa heshima wakati wa gwaride maalumu la kuwaaga baada ya kustaafu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Kambi ya Twalipo, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanajeshi waliostaafu na kuagwa kwa heshima leo kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye kambi ya Twalipo, Jijini Dar es Salaam
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Issa Suleiman Nassor wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofnayika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Joyce Kabati wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 Gwaride la heshima kwa wastaafu wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.

ULAJI RANGI TANO ZA MBOGAMBOGA ,MATUNDA NA VIUNGO KINGA YA MAGONJWA MBALIMBALI

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Watanzania wametakiwa kula Rangi tano za mbogamboga ,matunda na viungo kwani vitu hivi vinasaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga na maradhi mbalimbali yanayoshambulia binadamu. 

Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa lishe kutoka taasisi ya kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA) Evarsta kimario,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ya maonesho ya nanenane yanayofanyika Ndani ya viwanja vya Themi vilivyopo Njiro jijini hapa ambapo alifafanua kuwa Rangi tano za Mbogamboga zinafaida nyingi sana katika mwili wa binadamu

Alieleza kuwa watanzania wengi wamekuwa hawana tabia wala mazoea ya kutumia matunda ya Rangi hizi tano kitu ambacho Kinasababisha hatari kubwa ya kupata magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.

"Kila tunda au mboga inafaida yake mwilini na Faida za ulaji wa Rangi tano za mbogamboga nikitoa mfano ,matunda , mbogamboga na viungo vyenye Rangi nyeupe au kahawia hizi zinakemikali za asili zinazoitwa flovonoids, Fructans ,allyl sulphides na allicim na hivi vingi vinapatikana kwa wingi kwenye kitunguu Swaumu ,kemikali hizi huinarisha Afya ya mifupa ,mzunguko wa damu mwilini,hususa ni mfumo wa umengenyaji chakula huondoa sumu mwilini na hupambana na virusi ,bakiteri na fangasi na hii huepusha miili yetu isipate magonjwa ya moyo na saratani" alisema Kimario

Aliwataka watanzania kujenga mzoea ya kula mbogamboga na matunda angalau moja katika kila mlo ambao wanaula kwakufanya hivi kutawasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama kisukari ,kansa,tezi dume ,pia alibainisha kuwa ulaji wa vitu hivi unasaidia pia kuimarisha mifupa,kuongeza king a mwilini pia inasaidia kuimarisha ngozi isizeeke mapema 

Kwa upande wake Meneja masoko wa Taha Wilibarti Mdete alisema kuwa aliwataka wananchi hususa ni wakulima kutembelea banda lao la Taha lililopo katika viwanja vya nanenane Themi Njiro kupata Elimu zaidi kuhusiana na Kilimo cha mbogamboga pamoja na matunda kwani ni kizuri na kinanufaisha wengi.

Alisema kuwa ndio msingi wa maisha ya binadamu na kwa Mtanzania, tunaambiwa daima kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, kikiwa kinachangia asilimia kubwa ya pato la taifa na pia kilimo ni mwajiri kwa takribani asilimia 70 ya Watanzania.

Aidha aliwataka Wakulima nchini Tanzania kulima kilimo cha biashara kwa mfumo wa kilimo hai ambapo mbolea na dawa za kunyunyizia zitumike za asili badala ya zile za kisasa ili kuondokana na lishe hatarishi kwa afya ya walaji na pia kujiongezea kipato.

Akiongelea maonyesho hayo Mwenyekiti halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya alipotembelea maonyesho hayo alizitaka halmashauri zinazoshiriki mashindano hayo pamoja na Taso kanda ya kaskazini kutumia nguvu kubwa kuyatangaza maonyesho hayo pamoja na kuwahamasisha wakulima na watanzania kutembembelea maonyesho haya na kujionea na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu kilimo na biashara.

Aidha Aliwataka wakulima kutenga bajeti yakuandaa maonyesho haya ya nane nane,ili yaboreke zaidi na wakulima waweze kujifunza zaidi mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa.

Maonesho haya ya nane nane ni 26 ambapo kwa kanda ya kaskazini yanafanyika Mkoani Arusha katika viwanja vya Themi Njiro Ndani ya Jiji la Arusha na mikoa inayoshiriki kutoka kanda ya kaskazini ni Manyara,Kilimanjaro ,Tanga pamoja na mwenyeji Mkoa wa Arusha ambapo kauli mbiu ni yake inasema kilimo ,mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
 kwanza kushoto bwana shamba wa Taha wa kwanza kushoto Magembe Sugwa akimuelekeza  mmoja wa mkulima alietembelea banda lao Bjarne Laustsen (mzungu) namna Taha wanavyofanya kazi  katika banda lao lililopo ndani  ya  maonyesho ya nanenane  kwa kanda ya kaskazini ambayo yanafanyika katika viwanja vya  Taso vilivyopo Njiro  jijini Arusha . 
Mtaalamu wa lishe kutoka taasisi ya kilimo cha mbogamboga na matunda (TAHA) Evarsta kimario akiongea na waandishi katika maonyesho ya nanenane ambayo kwa Kanda ya kaskazini yanafanyika jijini Arusha.

Vyama 18 na wagombea 60 wajitokeza kuchukua Fomu za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata 13

0
0
TumeyaTaifa ya Uchaguzi iliutangazia Umma kuhusu Uchaguzi Mdogowa Udiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 17 Agosti mwaka 2019,kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Na. 292.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, Utoaji wa Fomu za wagombea ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 03 Agosti, 2019 na Uteuzi wa wagombea kufanyi katarehe 03 Agosti, 2019.
Hadi kufikia leo tarehe 02 Agosti, 2019 saa 10:00 jioni jumla ya wagombea 60 kutoka vyama vya siasa 18 wamechukua fomu za uteuzi.Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea waliochukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).
Imetolewa leo tarehe 02 Agosti, 2019 na
 Hussein Makame
AFISA HABARI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


BENKI YA CRDB YAJIKITA KUINUA KILIMO, WADAU MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LAO NANE NANE 2019

0
0
Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB anayehusika na Mikopo ya Kilimo, Maregesi Shaaban (kushoto) akimuelezea jambo Mkurugenzi wa Kampuni ya NSAGALI ambaye pia ni Mteja wa Benki ya CRDB Mkoani Simiyu, Emmanuel Silanga (wa pili kulia) aliyetembelea banda la Benki hiyo katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya NSAGALI ambaye pia ni Mteja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Silanga (katikati) akimuuliza jambo Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Bariadi, Felix Kisenha wakati alipotembelea banda la Benki hiyo katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu, Charles Madata akipokea maelekeo ya namna wakulima wanavyonufaika na mikopo ya pembejeo kutoka kwa Afisa wa Benki ya CRDB Dennis Dodo alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa wa Benki ya CRDB, Gelorida Samuel akimuhudumia mmoja wa wateja waliotembelea banda la Benki hiyo katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa wa Benki ya CRDB, Daniel Nyamuvugwa akimsikiliza mmoja wa wateja waliotembelea banda la Benki hiyo katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Afisa wa Benki ya CRDB, Mary Makunda akimuunganisha mteja na huduma ya SimBanking katika banda la Benki hiyo wakati wa maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Sehemu ya Wateja wa Benki ya CRDB wakipatiwa maelezo ya namna ya matumizi ya Matrekta yanayokopeshwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya ETC Agro, wakati wa maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Bariadi, Felix Kisenha akimfungua akaunti ya Mtoto (Junior Jumbo) mmoja wa wateja waliotembelea banda la Benki hiyo wakati wa maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.





PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA BARAZA LA KILIMO NA WADAU WAKE KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO

0
0
 Mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania kutoka Karatu Mkoani Arusha Bi Tarsila John akitoa maelekezo kwa mteja wake ya namna ya kutumia Mifuko y kuhifadhia Nafaka na Dawa za kuhifadhia nafaka, Bi Tarsila yuko katika maonyesho ya NaneNane kuelezea  ubora wa mifuko hiyo.

 Mwenyekiti wa Umoja wa wauza pembejeo wilayani kilombero mkoani morogoro ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania Bw John Bosco Zakaria Mvunjapori akitoa maelezo  kuhusu pembejeo za kilimo.

Mkazi wa Pawaga Mkaoni Iringa Bw. Twalibu Ubwa akifafanua jambo kwa wateja wake kuhusu bidhaa ya mchele, Ubwa ni mwanachama wa Baraza la Kilimo Tanzania na yuko katika maonyesho hayo kuelezea namna wanavyoshiriki katika uongezaji thamani katika zao la Mpunga.

 Muonekano wa Banda la Baraza la Kilimo Tanzania katika Viwanja vya Mwl. Julias Nyerere Mkaoni Morogoro, ambapo Baraza limekuwa likishiriki kila mwaka maonyesho ya wakulima NaneNane, Fika katika banda lao ili uweze kupata taarifa sahihi kuhusu sekta ya Kilimo na mchango wake katika uchumi wanchi.


Bi Zaibab Mahenge kutoka Mafinga akiwa katika Banda la Baraza la Kilimo Tanzania akifafanua jambo kwa mteja wake aliyetaka kujua zaidi kuhusu bidhaa ya unga wa lishe inayozalishwa na Bi zainab ambayo inamchanganyo wa Unga wa Dona,Soya, Mbegu za Maboga, Ulezi na Mchele.



LUKUVI AMREJESHEA ENEO LAKE BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU BAADA YA KULIHANGAIKIA KWA MIAKA 20

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemrejeshea eneo lake lililoko Jangwani Beach wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam Brigedia Jenerali Mstaafu Francis Mbena kufuatia kuhangaika kwa miaka 20 kulirejesha eneo alilodhulumiwa.

Akizungumza wakati akimkabidhi hati ya kiwanja chake leo eno la Mbezi Beach Dar es Salaam Lukuvi alisema, Brigedia Mstaafu Mbena alitaka kudhulumiwa eneo lake na Idan Mongi aliyeuziwa eneo hilo na John Rwechungura.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kiwanja hicho chenye ukubwa wa takriban mita za mraba 2000 hati yake iligushiwa na baadaye kiwanja hicho kuuzwa kwa Mongi ambapo alieleza mnunuzi huyo alitapeliwa kwa kuwa kiwanja kilikuwa kimefutwa.

Lukuvi alitoa onyo kwa wanasheria kuacha tabia ya kuchelewesha kesi kwa kutowaeleza ukweli wateja wao iwapo kesi wanayoishughulikia hawezi kushinda na kufafanua kuwa ni bora wanasheria wakawaeleza ukweli kuhusiana na mwenendo wa kesi wanazoziendesha kuhusina na masuala ya ardhi.

Aidha, amewataka wananchi wanaotaka kununua viwanja kufanya utafiti katika ofisi ya Msajili wa Hati Wizarani kwa lengo la kujiridhisha umiliki wa muuzaji wa eneo husika.

Kwa upande wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mbena amefurahishwa na uamuzi uliofanywa na Lukuvi wa kumpatia hati yake aliyoihangaikia kwa miaka 20 na kueleza kuwa eneo hilo limekuwa likimtesa sana kwa kuendesha kesi kwa muda mrefu na kutumia fedha yake ya pensheni kuendeshea kesi.

Mbena alisema eneo hilo alilipata mwaka 1988 Oktoba 3 na kuingia katika mgogoro baina yake na watu wanaodai kulimiki kuanzia mwaka 1999ambapo kesi ilianzia Baraza la Ardhi na Nyumba na kufikia Mahakama Kuu amapo iliisha mwaka jana Julai na Mbena kushinda.

Naye Idan Mongi aliyetapeliwa kiwanja hicho alieleza kuwa kiwanja alichotapeliwa kina historia ndefu ambapo kabla yeye kukinunua kilipitia kwa wamiliki wengine watatu na kubainisha kuwa yeye alikinunua kwa John Rwechungura mwaka 2009.

Alisema kuwa, anamkabidhi eneo lake Brigedia Mstaafu Mbena kwa moyo mmoja na hatabomoa nyumba na ukuta aliojenga na ameomba kuhamisha vitu vyake ndani ya miezi mitatu.

Lukuvi alisema, kutokana na uungwana aliounesha Idan Mongi Wizara itamzawadia kiwanja katika eneo la Pemba na Mnazi Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kuishi tu.

WATUMISHI HANDENI WAONYWA KUHUSU FEDHA ZA MIRADI

0
0
KATIBU Tawala wa wilaya ya Handeni Mwalimu Boniface Maiga akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu katika vijiji nane vya halmashauri ya wilaya hiyo uliokwenda sambamba na mkutano wa wadau uliofanyika Kata ya Mkata ambapo mradi huo unaendeshwa na asasi ya Tree of Hope chini ya ufadhili wa Foundation for civil Society (FCS) kulia ni Diwani wa Kata ya Mkata akifuatiwa na Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane Goodluck Malilo
Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane wilaya ya Handeni Goodluck Malilo akizungumza
Mwezeshaji Wakili Richard Vicent akisisitiza jambo
Sehemu ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya washiriki wakifuatilia matukio mbalimbali
Mmoja wa washiriki akichangia
Mmoja wa washiriki akijitambulisha
Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane wilaya ya Handeni Goodluck Malilo kushoto akiteta jambo na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mwalimu Boniface Maiga mara baada ya kufungua

WATUMISHI wa Halmashauri wilayani Handeni mkoani Tanga wameonywa kuacha kufanya vitendo vya ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao kwani zitawatokea puani.

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mwalimu Boniface Maiga wakati wa utambulisho wa mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu katika vijiji nane vya halmashauri ya wilaya hiyo.

Utambulisho huo ulikwenda sambamba na mkutano wa wadau uliofanyika Kata ya Mkata ambapo mradi huo unaendeshwa na asasi ya Tree of hope chini ya ufadhili wa Foundation for civil Society (FCS).

Alisema kwamba sio ambao watabainika wamehusika kwenye kufanya ubadhirifu wakifanya uchunguzi na wakibaini wamehusika watawashughulikia kwa mujibu wa sheria na hakuna ambaye atasalimika

Katibu Tawala huyo ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema kwamba hawatakuwa tayari kuona fedha zinazopelekwa kwenye maeneo yao na serikali huku zikihujumiwa hivyo watakuwa wakali kwa kuhakikisha wahusika wanashughulikiwa.

“Niwaonye watumishi ambao mnaofanya ubadhirifu kwenye miradi inayotelekezwa kwenye maeneo yenu acheni tabia hiyo mara moja kwani hatutawavumilia na hili niseme kwamba fedha ya serikali hailiwi ni moto hivyo watakaobainika watashughulikiwa “Alisema.

Hata hivyo alisema kwamba wilaya hiyo imepokea milioni 362.5 kutoka Serikalini kwa ajili ya ukamilishaji na umaliziaji wa vyumba vya madarasa 29 vya shule ya msingi wilayani humo.

Fedha hizo zilitolewa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ambaye amepania kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.

Alisema kwamba bado ujenzi unaendelea kwa sehemu mbalimbali na haitafikia mwezi Agosti majengo hayo yatakuwa yamekamilika na hivyo kuondokana na changamoto zilizopo.

“Lakini pia niwapongeze Asasi ya Tree of hope kwa maana maeneo mradi huo umefanya kazi kuna mabadiliko makubwa ya uwazi na uwajibika lakini pia hata utoro umepungua kwa asilimia kubwa hivyo mradi huo umekuwa chachu kubwa sana kwa jamii “Alisema.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo wa wadau Mratibu wa Mradi wa Kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu kwenye vijiji nane Goodluck Malilo alisema kwamba mradi huo rasmi kutekelzwa na Asasi ya Tree of hope katika wilaya hiyo mwezi Agosti mwaka 2017 hdi Mwezi Julai 2018.

Alisema kwamba mradi huo ulikuwa ukitekelezwa kwenye vijiji vinne vya Halmashauri ya Handeni ambazo ni Michungwani (Kata ya Segera), Kwedizinga (Kata ya Kwedizinga), Kabuku Nje (Kata ya Kabuku) na Komsanga (kata ya Mgambo) chini ya ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society.

Malilo alisema baada ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza na kuonekana mafanikio makubwa asasi hiyo iliongezewa muda wa ufadhili kwa kipindi cha miezi mitano kuanzia Novemba mwaka 2018 hadi mwezi Machi 2019 ili kuendeleza kutatua changamoto za elimu katika vijiji hivyo.

Alisema kutokana na mafanikio ya mradi huo kuwa endelevu na yenye tija katika sekta ya elimu waliomba ufadhili kutoka Shirika la Foundation for Civil Society ili kutanua wigo wa maeneo ya utekelezaji kutoka vijiji vinne had inane ambapo walikubaliwa huku wakiongeza vijiji vya Mjani Mapana (Kabuku ndani),Hoza(Komkonga),Kitumbi (Kitumbi) na Mkata Mashariki (Mkata).

Hata hivyo alisema kwamba mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane kuanzia mwezi Julai 2019 hadi February 2020 huku akieleza shughuli za mradi zitakazotekelezwa katika vipindi viwili vya miezi minne minne .

Alisema shughuli hizo ni pamoja na mikutano ya wadau wa elimu,uundaji wa kamati za wananchi za uhamasishaji na ufuatiliaji uwajibikaji ,mafunzo ya utawala bora,midahalo ya wadau wa elimu,uhamasishaji uwajibikaji jamii na mamlaka husika katika kuboresha elimu ikiwemo utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi vya uelimishaji ikifuatiwa na ziara za ufuatiliaji na tathimini katika maeneo ya mradi.

NIC YAZINDUA MPANGO WA BIMA YA MAZAO KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE, SIMIYU

0
0
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akipokea mpango wa Bima ya mazao ambao utaanza kutumika kwa wakulima wa zao la Pamba kwa mkoa wa Simiyu na Kahawa katika Mkoa wa Kagera, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye, leo Agosti 3, 2019 wakati akiuzindua, katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akishuhudia.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (kushoto) akizindua rasmi mpango wa Bima ya mazao ambao utaanza kutumika kwa wakulima wa zao la Pamba kwa mkoa wa Simiyu na Kahawa katika Mkoa wa Kagera, leo Agosti 3, 2019 katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye. 
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akionyesha mpango wa Bima ya mazao ambao utaanza kutumika kwa wakulima wa zao la Pamba kwa mkoa wa Simiyu na Kahawa katika Mkoa wa Kagera, aliouzindua leo Agosti 3, 2019 katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye. 
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza baada ya kuzindua rasmi mpango wa Bima ya mazao ambao utaanza kutumika kwa wakulima wa zao la Pamba kwa mkoa wa Simiyu na Kahawa katika Mkoa wa Kagera, leo Agosti 3, 2019 katika maonyesho ya 26 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane 2019), yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Picha ya Pamoja.

ZAIDI YA BILIONI SITA ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA MAPANDA.

0
0
Diwani wa kata Mapanda Obadia Kalenge akielezea jinsi gani walivyotumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni




NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

Zaidi ya bilioni sita zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu,afya na utamaduni katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.

Akizungumza na blog hii diwani wa kata hiyo Obadia Kalenge alisema kuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo kwaushirkiano wa serikali,wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo katika kata hiyo.

“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni mchanga na mawe tu,mfano shule ya Kihansi pekee yake ina miradi inayogharimu kiasi cha shilingi milioni mia sita themanini na nane na laki tano hivyo nina shule saba na jumla ya shilingi milioni mia nane na sitini zimetumika kuleta maendeleo kwenye elimu katika kata yangu ya Mapanda” alisema Kalenge

Kalenge alisema kuwa katika sekta ya afya amefanikisha uwepo wa CTC kuwepo kwenye kata hiyo na kuanza kujenga jingo la wodi ya akina mama na watoto na kuendelea na ujenzi wa kituo cha afya na kata ya hiyo inavijiji vitano hivyo kila kijiji kina zahanati ambayo imekuwa ikasidia kuta huduma ya afya kwa wananchi wa kata hiyo.

“Mwaka jana wakati wa bajeti nilijenga hoja kwenye baraza la madiwani kwa kuomba kujengewa kituo cha afya ambapo halmashauri walinikubaria ombi langu na kuhakikisha mwisho mwa 2019 kituo hicho cha afya kinakuwa kimeanza kufanya kazi” alisema Kalenge

Kila zahanati kuna mganga na nesi na kuongeza kila zahanati zilizopo katika kata hiyo kuna pikipiki ambazo zimekuwa zikisaidia katika usafiri wa hapa na pale kutokana na mazingira ya kata hiyo hivyo usafiri wa pikpiki umekuwa ukirahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa afya wa kata hiyo.

Aidha Kalenge alisema kuwa swala la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo kuharibika mara kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo laki kuna barabara ya kutoka Chogo hadi Isipi kwa mara ya kwanza ndio imetengenezwa kwa mara ya kwanza toka kuumbwa kwa dunia.

“Ili kurahisisha maendeleo lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano mkubwa na mbunge wa jimbola Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa tumefanikiwa kutatua kero hiyo kwa kiasi chake” alisema Kalenge

Kalenge alisema kuwa tatizo la maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

DKT SHEIN AWATAKA WAHADHIRI NA WATAALAMU WA VYUO VIKUU KUTUMIA MITAALA ISIYOLETA ATHARI KWA WANAFUNZI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein amewataka Wahadhiri na Wataalamu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu kuhakikisha kwamba Mitaala wanayoitumia katika kufundishia Taaluma ya Dini haitaleta athari kwa wanafunzi ndani ya mfumo wa Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yaliyopo hivi sasa Duniani.

Alisema Uislamu haukatazi Waumini wake kujifunza Elimu ya Dunia lakini kinachopaswa kuzingatiwa zaidi na Wahadhiri na Wataalamu hao ni kufuata Sheria na Miongozo ya Uislamu kwa vile Dini yenyewe tayari imeshakamilika katika nyanja zote kwa ajili ya kutekelezwa na Wanaadamu.

Dr. Ali Mohamed Shein alisema hayo katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiufungua Mkutano wa Tatu wa Siku mbili wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu unaofanyika katika Hoteli ya Madinat Al – Bahr iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema Mwanafunzi wa Chuo Kikuu anapaswa kujengewa mazingira sahihi ya Mfumo wa Kisasa yatakayomuwezesha kushajiika na kujifunza masomo ya Sayansi, Ufundi na Ustawi wa Jamii ili atakapomaliza awe kiungo na maendeleo katka Umma unaomzunguuka.

Dr. Shein alisema Vyuo vya Kiislamu katika kipindi hichi cha utandawazi vina kazi kubwa kwa Wataalamu wake kufanya Utafiti wa kina katika masuala ya Ustawi na sayansi utakaowawezesha kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili Waumini wa Dini hiyo.

“ Vyuo Vikuu vya Kiislamu vichukuwe jukumu la kuieneza elimu ya DSini ya Kiislamu sambamba na kujenga hoja za kujibu itikadi zisizo sahili zinazotolewa dhidi ya Dini hiyo”. Alisema Dr. Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alieleza kwamba ufundishaji wa sasa ni vyema ukazingatia matumizi ya Tekonojia ya Habari na Mawasiliano ambayo inamuharakisha Mwanafunzi kujifunza kwa haraka Quran Tukufu na Mafundisho ya Kiongozi wa Dini hiyo Mtume Muhammad {SAW}.

Alisema Teknolojia hiyo ya kisasa ya Habari na Mawasiliano ni rahisi kwa vile Mwanafunzi anayeamua kutumia mfumo huo ana uwezo wa kutafuta kumbukumbu za Vitabu anavyovihitaji katika mafunzo yake zikiwemo pia tafiti za Wahadhiri tofauti.

Dr. Ali Mohamed Shein ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Sumait chukwani kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani.

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na aliushukuru pia Uongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Vyuo Vikuu vya Kiislamu {IIIT} kwa uamuzi wake wa Mkutano huo wa Tatu kuufanyia Visiwani Zanzibar.

Mapema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Simait Chukwani Profesa Amran Rasli alisema Zanzibar imepata Heshima kubwa kutokana na kufanyika kwa Mkutano huo wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani ikitanguliwa na ile iliyofanyika Morogoro na Uganda.

Profesa Amran alisema hii ni fursa ya pekee kwa Wahadhiri na Wataalamu wa Zanzibar kuitumia nafasi ya uwepo wa Mkutano huo kuchota fikra kutokana na kuwasilishwa kwa Mada na Tfiti 50 kutoka kwa wenzao wa Mataifa shiriki katika Mkutano huo.

Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Mtandao waMawasiliano ya Kiislamu {IIIT} Profesa Omar Kasule alisema lengo la kuanzishwa kwa Taasisi yao ni kujikita zaidi katika kutoa Elimu sahihi katika Umma wa Kiislamu.

Profesa Omar alisema Wataalamu wanaelewa na kufahamu fika kwamba Elimu ndio inayosogeza maendeleo mahali popote pale Duniani iwe kwa Taifa na hata Jamii za kawaida.

Akimkaribisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya Ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amnali Zanzibar Mh. Simai Mohammed Said alisema hadhara hiyo itasaidia kuleta mashirikiano baina ya Wahadhiri na Wasomi mbali mbali.

Mh. Simai alisema ushirikiano huo wa Kitaaluma katika masuala zaidi ya Dini ya Kiislamu utaongeza upeo wa uelewano katika kuendeleza mbele Dini ya Kiislam katika maeneo tofauti Duniani.

Mkutano huo wa Tatu wa wa Siku Mbili wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani umeshirikisha Wahadhiri, Wataalamu na Wasomi wa Vyuo Vikuu kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki, Afrika Magharibi pamoja na Mashariki mwa Bara la Asia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein hapo Hoteli ya Manidat Al – Bahr Mbweni. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Simait Chukwani Profesa Amran Rasli akiwakaribisha Zanzibar Washiriki wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Manidat Al – Bahr Mbweni.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Mtandao waMawasiliano ya Kiislamu {IIIT} Profesa Omar Kasule akielezea lengo la Taasisi yake katika kuimarisha Elimu ya Dini katika Mfumo wa Kisasa.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Mtandao waMawasiliano ya Kiislamu {IIIT} Profesa Omar Kasule Kushoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Simait Chukwani Profesa Amran Rasli wakibadilishana hati za Mkata wa ushirikiano baada ya kutia saini mbele ya Mgeni rasmi Balozi Seif.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amnali Zanzibar Mh. Simai Mohammed Said akimkaribisha Balozi Seif kuufungua Mkutano huo wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu vinavyoshiriki Mkutano wa Tatu wa Vyuo hivyo Shein hapo Hoteli ya Manidat Al – Bahr Mbweni.Picha na – OMPR – ZNZ.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Simai Mohamed Said Kulia akimuongoza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuelekea kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Manidat Al – Bahr kuufungua Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani.

WAZIRI UMMY AKABIDHI MASHINE YA UPULIZIAJI DAWA ZA KUDHIBITI WADUDU MKOANI TANGA

0
0
Viongozi wa Jiji la Tanga wakifurahia makabidhiano ya Mashine ya upuliziaji dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Tangamano jijini humo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), Mkurugenzi wa kinga wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Subi (wa kwanza kushoto) wakiwa pamoja na Mabwana Afya wa Jijini Tanga wanaotekeleza mkakati wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu mkoani humo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Bw. Mustafa Mhina wakiangalia jinsi mashine ya upuliziaji inavyofanya kazi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa afya wa jiji la Tanga jinsi wanavyowanasa mbu kwa ajili ya kuwafanyia tafiti mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashine ya upuliziaji dawa za kuangamiza wadudu wadhurifu iliyofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mashine ya kupulizia dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akiongelea mkakati wa wizara hiyo wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu ambao utatekelezwa nchi nzima, hapo ni katika makabidhiano ya mashine ya kupulizia dawa za kudhibiti wadudu wadhurifu yakiyofanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.



Na Emmanuel Malegi-WAJMW, Tanga

Jiji la Tanga limekua la pili kupata mashine za kupulizia dawa za kuua mbu na wadudu wadhurifu waenezao magonjwa mbalimbali ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI katika kudhibiti wadudu hao.

Akikabidhi mashine hiyo kwa uongozi wa Jiji la Tanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema mkakati huo ni wa miaka mitano (2019-2024) na unalenga kuhakikisha mbu na wadudu wadhurifu wanadhibitiwa kwa njia ya utengamano na ameiomba jamii ishiriki kikamilifu katika kupambana na wadudu hao.

“Wizara yangu imeagiza mashine nane za kisasa(foggig mashine) zenye uwezo mkubwa wa kupulizia na zinabebwa na magari na kupuliza eneo kubwa kwa wakati mmoja, hivyo naomba jamii ihakikishe inashiriki kikamilifu katika kupambana na wadudu hawa dhurifu”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa ni vema mikoa ikawekeza katika maeneo ya msingi am bayo ni pamoja na ushiriki wa jamii, sekta binafsi na wadau kushiriki katika kudhibiti wadudu kwa njia shirikishi zinazolenga kuharibu mazalia ya wadudu. Mikoa kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mbu na wadudu wadhurifu katika ngazi zote na kupanga njia madhubuti za udhibiti wa wadudu hao.

Waziri Ummy amesema katika kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa, Wizara ya afya kwa kushirikiana na TAMISEMI imetoa maagizo kwa kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote ziweze kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya utekelezaji wa udhibiti wa mbu na wadudu wadhurifu ambayo itakua mtaa kwa mtaa, Halmashauri kuhakikisha zinaishirikisha jamii katika ngazi zote za mapambano haya ya mbu na wadudu wadhurifu.

Pia Waziri Ummy amezitaka Halmashauri kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkakati huu katika kipindi cha mwaka mmoja na kutoa taarifa ya mafanikio, changamoto na mipango ya Halmashauri katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na kununua mashine za upuliziaji (Fogging Machine) angalau moja katika kipindi cha kufikia Januari 2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambae ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw. Thobias Mwilapa amemshukuru Waziri Ummy na Wizara ya Afya kwa ujumla kwa kuupatia mkoa huo mashine hiyo ambayo itasaidia katika utekelezaji wa mkakati wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu ambao wanaeneza magonjwa huku akiitaja Tanga kushika namba mbili kitaifa kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue baada ya Dar Es Salaam.

MAJALIWA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA SHIRIKA LA MAWASILIANO TANZANIA (TTCL)

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo wa simu wa zamani wakati alipotembelea makumbusho ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) iliyopo kwenye jengo la EXTELECOMS HOUSE jijini Dar es salaam, Agosti 3, 2019. Kushoto kwake ni Nibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba na Kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa TTCL, Laibu Leonard.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA PAMBA,AZITAKA BENKI ZIWAHUDUMIE WANUNUZI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mkutano kwa njia ya video na Wakuu wa Mikoa inayolima Pamba ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Kagera, Singida na Tabora akiwa jijini Dar es salaam, Agosti 3, 2019. Mkutano huo pia ulimjumuisha, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, Maofisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Mabenki, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU ATAKA BENKI ZIWAHUDUMIE WANUNUZI WA PAMBA KESHO JUMAPILI

*Nia yake ni wakulima waanze kulipwa Jumatatu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki zilizoko kwenye mikoa inayolima pamba zihakikishe kuwa kesho Jumapili zinatoa huduma kwa wateja ili wanunuzi wa pamba wakamilishe taratibu za mikopo.

“Kesho mabenki yanayotoa huduma Jumapili ni vema yafanye kazi, ili wanunuzi wa pamba waje wakamilishe taratibu zote za makaratasi na Jumatatu wapate hela ya kuanzia kazi. Hata mkifunga saa 6 mchana, wao wabakie hadi saa 10 ili mradi wakamilishe taratibu zote,” amesema.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumamosi, Agosti 3, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa nane inayolima pamba ya Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, Singida na Taborapamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB.

Waziri Mkuu amesema kikao kilichofanyika jana (Ijumaa, Agosti 2, 2019) baina ya Benki Kuu, wanunuzi wa pamba na wamiliki wa mabenki kimeafiki kuanza kutoa mikopo kwa wanunuzi ili waanze kununua pamba kuanzia keshokutwa (Jumatatu, Agosti 4, 2019). 

Amesema kazi ya kununua pamba ikianza, ilipwe kwanza iliyokusanywa ili ianze kusombwa na iweze kupisha nafasi kwa pamba mpya itakayoendelea kununuliwa na kupelekwa kwenye maghala.

Amemtaka pia Mwenyekiti wa Wanunuzi, Bw. Christopher Gachuma ahakikishe anaweka ufuatiliaji ili kujua kujua ni kiasi gani cha pamba kimenunuliwa kutoka kwa nani na wapi. “Endeleeni na uratibu wa ununuzi mjue nani amenunua nini, wapi na kwa gharama ipi.”

Pia amewataka wataalamu wa Wizara wa Kilimo waende mikoani, watu wa mabenki na Benki Kuu washirikiane na taasisi ambata kama Bodi ya Pamba, Tume ya Ushirika na AMCOS ziratibu vizuri kila mwananchi anayepeleka pamba na wahakikishe analipwa.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wanunuzi wa pamba na wafanyabiashara wote wajenge viwanda hapa nchini ili kupata suluhisho la kudumu la soko la pamba. “Natoa wito kwa wafanyabiashara nchini wajenge viwanda vya kusokota nyuzi na kutengeneza nguo.

Amesema hivi sasa nchini, kuna viwanda viwili tu vya kusokota nyuzi ambapo kimoja kiko Dar es Salaam na kingine kiko Shinyanga ambavyo uwezo wake ni mdogo. “Leo tumenunua pamba lakini tutaanza kupata changamoto ya usafirishaji wa kuipelekea nje ya nchi kuiuza. Tukiwa na viwanda hapa ndani, tatizo la soko halitakuwepo.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabenki, Bw. Abdulmajjid Nsekela, aliwahakikishia wakuu wa mikoa yote na wanunuzi waliokuwa wakishiriki mkutano huo kutoka kwenye mikoa yao kwamba fedha itapatikana kuanzia Jumatatu (keshokutwa).

“Napenda kuwahakikishia kuwa kwenye kikao cha jana, benki zote zimeridhia kwamba zitatoa mikopo kwa wanunuzi. Tulikubaliana kwamba wanunzi wote walioomba mikopo waje haraka kuchukua fedha zao, waliopata lakini wakawa hawajachukua mikopo waje pia kuchukua.

“Mabenki yako tayari kutoa fedha hizo, na tutasimamia ili kuhakikisha fedha zinatolewa kwa wakati na wanunuzi wanapata hela,” alisema mbele ya Waziri Mkuu.

Naye Mwenyekiti wa Wanunuzi wa Pamba, Bw. Christopher Gachuma alisema wanunuzi wako tayari kununua pamba ili itoke mikononi mwa wakulima iende kwa ginners (wenye vinu vya kuchambua pamba.

“Kuanzia wiki ijayo, tutajitahidi kununua pamba kwa haraka na kwenye maeneo yasiyo na wanunuzi tutakutana na kujipanga ili tuwafiie wote. Ila kwenye mikoa ya pembezoni kama Katavi, ambako hakuna ginneries, tunaomba upendeleo maalum sababu ya umbali uliopo.”

Naye Waziri wa Kilimo, Bw. Japhet Hasunga amesisitiza kuwa wanunuzi wanaoenda kununua pamba wilaya za Meatu, Igunga na Singida wawe makini na wapeleke kwenye ginneries maalum za kuchambua mbegu na siyo za kusindika mafuta.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi (OR-TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo ameiomba Benki Kuu ya Tanzania (BoT) isimamie kwa karibu makubaliano ya kikao cha jana ili utekelezaji wake uende kwa haraka zaidi.

“Ningeshauri Mwenyekiti wa Wanunuzi afuatilie wafanyabiashara wake, ili wakipata hiyo fedha, waende wakatimize malengo yaliyokusudiwa. Na Wakuu wa Mikoa mkutane na wanunuzi wa mikoa yenu kila baada ya siku mbili, ili muweze kubaini kwa haraka changamoto zinazowapata na kuzisuluhisha kwa haraka,” alisema.

RC MAKONDA AWAPA ULAJI WACHONGA VINYAGO NA WACHORAJI PICHA, AWAKABIDHI SEHEMU YA KUUZA BIDHAA KWA WAGENI ZAIDI YA 1,000 KUTOKA SADC.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza kuwa ifikapo August 06 atafunga Barabara zinazozunguka Chuo cha IFM zenye ukubwa wa Mita 700 ili eneo hilo litumiwe na Wachonga vinyago, Wachoraji wa picha na watengeneza Shanga kuuza bidhaa wanazozalisha kwa 
ndani ya siku 15 za ugeni wa viongozi wa Jumuiya ya SADC.

RC Makonda amesema kwakuwa eneo hilo lipo jirani na Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere unapofanyika mkutano huo itakuwa rahisi kwa wageni kutembelea wafanyabiashara hao na kununua bidhaa mbalimbali zinazatengenezwa kwa umahiri na ubunifu mkubwa ikiwemo Vinyago, Picha za kuchora, Shanga na Vinyago jambo litakalosaidia pia kutangaza utalii wa Tanzania.

Aidha RC Makonda amesema eneo hilo pia litakuwa na ulinzi wa kutosha na litafungwa Taa za kisasa ili kuhakikisha wageni wafika na kununua bidhaa muda wowote kwa kipindi chote cha mkutano wa Jumuiya ya SADC jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa wauzaji na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo RC Makonda amesema ni vyema Wananchi wakauchukulia Ugeni huu wa Viongozi zaidi ya 16 wa Jumuiya ya SADC kama sehemu ya fursa ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.

MATUKIO KATIKA PICHA ZOEZI LA USAJILI NGOs KANDA YA KASKAZINI MKOANI KILIMANJARO

0
0
Msajili na Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao (kulia) akifafanua jambo kwa mdau wa NGO aliyefika kuhuisha usajili wa Shirika lake kwa Kanda ya Kaskazini katika zoezi la usajili linaofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioanza tarehe 29/07 hadi tarehe 06/08/2019.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Faki Shaweji(kulia) akitoa ufafanuzi wa kisheria kwa wadau wa NGO aliyefika kuhuisha usajili wa Shirika lake kwa Kanda ya Kaskazini katika zoezi la usajili linaofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioanza tarehe 29/07 hadi tarehe 06/08/2019.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Idda Kombe (kushoto) akitoa ufafanuzi wa kisheria kwa wadau wa NGO aliyefika kuhuisha usajili wa Shirika lake kwa Kanda ya Kaskazini katika zoezi la usajili linaofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mpaka ulioanza tarehe 29/07 hadi tarehe 06/08/2019.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Timoth Mgonja (kulia) akitoa huduma ya usajili kwa wadau wa NGO aliyefika kuhuisha usajili wa Shirika lake kwa Kanda ya Kaskazini unaofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioanza tarehe 29/07 hadi tarehe 06/08/2019.
Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO wakitoa huduma katika zoezi la kuhuisha usajili wa Shirika lake kwa Kanda ya Kaskazini katika zoezi la usajili linaofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ulioanza tarehe 29/07 hadi tarehe 06/08/2019.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images