Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DSTV WAWATOA HOFU WATEJA WAO KATIKA MSIMU MPYA WA LIGI KUU

$
0
0


Na.Khadija seif, Michuzi tv 

KAMPUNI ya Multi Choice Tanzania kupitia King'amuzi Cha dstv wamewahakikishia mashabiki wa soka kuendelea kuwapatia mechi ya ligi kuu maarufu duniani kwa msimu mpya.

Ligi ambazo zitarushwa mubashara kwa lugha ya kiswahili ni Ligi kuu ya Uingereza(EPL), Italia (Serie A), Hispania (La Liga), Liga ya mapingwa Ulaya(UEFA) pamoja na makombe mengine maarufu.

Akizungumza na waandishi wahabari Mkuu wa Masoko wa Kampuni hiyo Ronald Shelukindo amesema pazia la msimu mpya litafunguliwa Agosti 2 kwa mtanange wa ngao ya jamii.

"Msimu huu tutaanza na Ligi ya ngao ya jamii Kati ya Liverpool na kigogo wa Ligi ya Uingereza Manchester City huu utakua mubashara kwa lugha ya nyumbani kiswahili," alisema Shelukindo

Akaongeza kuwa watangazaji wa msimu huu ni Salama Jabir, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge, Ibrahim Madoud, Abduli Liongo na Oscar Oscar pia kingamuzi cha DStv unaweza kuunganisha vifaa mbalimbali kama vile Simu, Tablet na Laptop.

Aidha uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadua wa soka, wachezaji wastaafu Sekolojo Chambua, Mohmed Hussein na Fikiri Magoso na wasanii mbalimbali Pierre Liquid, Romeo Jonsoni' Dj RJ' na Quickracka.
Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, Kauli Mbiu ya Msimu huu ni SOKA MWANZO MWISHO’
Afisa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bi. Shumbana Walwa akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam.
MMoja wa wachezaji wa zamani Sekilojo Chambua akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso na Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo pamoja na wafanyakazi wengine wakiwa meza kuu wakifurahia jambo katika hafla hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Bw. Jonson Mshana akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka.
Mmoja wa wachambuzi wa soka Ole Mjengwa akizungumza wakati hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka.

MWENYEKITI MSTAAFU WA CHAMA CHA SOKA SHINYANGA HAMIS MGEJA AMUOMBA WAZIRI MKUU KUITISHA MKUTANO WA WADAU WA MICHEZO

$
0
0
Na Ripota Wetu, Michuzi TV

MWENYEKITI mstaafu wa Chama cha soka Mkoa wa Shinyanga (Shirefa) Khamis Mgeja ambaye pia ni mdau mkubwa wa soka nchini amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuitisha mkutano wa wadau wa sekta ya michezo nchini ili kujadili changamoto na mstakabali wa maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa na watu walio wengi

Mgeja ambaye pia kada wa CCM ambaye kwa sasa amejikita katika sekta ya michezo hususani ile ya kukuza vipaji kwa vijana waliopo wilayani Kahama ameamua kumuomba Waziri Mkuu akiamini ni msikivu na mwanamichezo mzuri na kuongeza kama itampendeza na atakavyoona inafaa, afanye na yeye kuwaita wadau wa sekta ya michezo kama ambavyo amekuwa akifanya Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaita wadau wa sekta mbalimbali na kuzungmza nao ili kutatua changamoto na kutoa maelekezo.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kahama kuhusu mustakabali wa soka letu la Tanzania hasa katika mashindani mbalimbali ya kimataifa ambayo timu yetu ya taifa imeshiriki kuanzia ile ya chini ya miaka 17 pamoja na ile ya wakubwa ya Kombe la Mataifa ya Afrika sambamba na michuano hii ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

"Michezo kwa sasa ndio inachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi pamoja na kuona ajira kwa makundi makubwa ya vijana ambao kwa sasa ndio makundi makubwa ambayo yapo mitaani hayana ajira za kudumu na kupitia michezo wanaweza kujiajiri na kujipatia fedha zitakazo kuza maisha yao ya kila siku,"amesema Mgeja.

Amefafanua kuwa katika siku za hivi karibuni Rais Magufuli aliitisha mikutano kwa nyakati tofauti zikiwahusisha wadau kama vile wa madini na baadae wafanyabiashara, vikao hivyo vilikuwa na tija na mafanikio makubwa katika ujenzi wa Taifa. Baada ya wadau kupata nafasi ya kusema changamoto na mafanikio.

Aidha Mgeja amesema mkutano huo wa sekta ya michezo kama utaitishwa utatoa fursa ya wadau mbalimbali kutoa michango yao ya kimawazo na kujadili jinsi gani tutoke hapa tulipo kwenye aibu za mara kwa mara ili twende na kufika kwenye faraja hali ambayo tutapata wadau wengi na ikiwezekana wakawa na mawazo mazuri tofauti tofauti tukabadilishana mawazo na uzoefu na kufikia muafaka na kupanda daraja la michezo.

Hata hivyo Mgeja amewaomba Watanzania hasa wadau wa michezo wavute subira pamoja na kwamba tumeumia na tunaendelea kuumia baada ya matokeo ya mashindano ya watoto chini ya umri wa miaka 17 Afcon yaliyofanyika nchini kwetu na baadae Afcon ya wakubwa Misri hatuna sababu ya kutafuta mchawi wala kumtoa mtu kafara haitatusaidia chochote kuleta mabadiliko ya michezo na kama hatutajielekeza kuwekeza katika michezo Tanzania tutaendelea kuwa washiriki na wala shio washindani na tusitarajie kuvuna bila kupanda kama matunda pori.

"Hakuna njia ya mkato katika mafanikio yoyote yale bila kuwekeza katika soka na tatizo la watanzania tunataka matokeo mazuri kitu ambacho hakiwezekani hata ukitaka pepo lazima ufe kwanza.

“Msitake pepo bila kufa na inasikitisha tunataka maendeleo bila kuwekeza katika shule za mpira za watoto wadogo hapa nchini na hakuna njia nyingine yeyote ya kupata mafanikiom katika soka bila ya kuwea na shule za kufundisha watoto tangu wakiwa wadogo mapka wanapokuwea wakubwa na kusajiliwa na vilabu vingine”,amesema Mgeja.

Mgeja pia amewapongeza wachezaji na kocha wao Amunuke kwa pale walipofikia ni kweli vijana wetu uwezo wao ndipo ulipofikia katika mashindano ya Afcon na Misri ukweli utabaki pale pale. Ni kujidanganya kuwa tungeweza kufika kwenye robo fainali au nusu fainali na hatimaye fainali hayo yangekuwa maajabu makubwa ya dunia .

Amesema tumejifunza kuanzia Afcon ya watoto na wakubwa Misri tumeona wenzetu nchi zingine walivyowekeza kwa kiwango cha juu sana katika Academy Nchi kama Madagasca na Burundi na mfano wa kuigwa na sisi tujipange upya naimani tutafika pazuri penye faraja na sasa tumeingia katika mashindano ya Afcon ya wachezaji wa ndani na watanzania wanapenda kuona mabadiliko makubwa katika soka letu.

Amesema kuwa michezo kwa sasa hapa duniani ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kujenga afya za mwili na kama serikali itaongea na wadau mbalimbali kama ilivyo kwa sekta nyingine kunaweza kukaleta mabadiliko makubwa na hivyo kufanya nchi yetu kukua kwa kiwango cha juu katika sekta ya michezi kama ilivyo kwa nchini nyingine barani Afrika.

Mgeja pia amewapongeza ushirikiano mkubwa kama Taifa ulivyooneshwa katika mashindano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini na Afcon ya wakubwa tuliyoshiriki Misri. Ushirikiano wa pamoja wa hali na mali ukiongonzwa na Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais ,Waziri mkuu, Waziri wa michezo viongozi wa TFF.

Pia Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji Taifa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Wadhamini mbalimbali wasani na Watanzania wote kwa ushirikiano huu tuliouonesha tunaweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio kama walivyofanya nchi zingine Mfano Aljeria, Everycost, Cameroon, Nigeria, Misri, Tunisia na Senegal.

MKUU WA MAJESHI AWATAKA WANAJESHI KUFUATA MISINGI YA MAADILI YA JESHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKUU wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Wanajeshi ambao wanaendelea kutumikia taifa kufuata misingi na maadili ya Jeshi ili wanapomaliza muda wao wa kazi waagwe kwa heshima. 

Mabeyo amesema hayo wakati wa hafla ya kuwaaga Majenerali 9 ambao wamestaafu utumishi wa Jeshini ambapo amesema mwanajeshi ili apewe heshima anatakiwa awe na nidhamu awapo kazini. 

Amesema Majenerali hao ambao wamestaafu kwa muda wa miaka mitatu wataendelea kuwa washauri katika jeshi la akiba. "Ambao bado wapo makazini wajitaidi kuwa na nidhamu ili wakati wanastaafu wapewe heshima kama hii ya leo,”amesema .

“mwanajeshi akistaafu uagwa kiheshima pindi anapostaafu tofauti na ukifukuzwa uwezi kupewa heshima”
Nao Baadhi ya Majenerali ambao wamestaafu waliwataka wanajeshi ambao wamebaki kuitumikia nchi kwa moyo mmoja. 

Joyce Kabatiambaye ni mmoja wa Majenerali hao aliwahasa wazazi na walezi kuacha dhana potofu kuwa watoto wa jinsia ya kike awawezi kuwa wanajeshi. Dk.Denis Janga ameelza katika kipindi chake cha utumishi wa jeshi alikua Daktari na alishiriki Vita vya Uganda hivyo aliwahasa wananchi kulinda amani iliyopo na kuepukana na migogoro kwa vita si nzuri
"Niliyoyashuhudia wakati wa ile vita sitaki kuona yanatokea maana watu walipata shida sana "amesema

Aidha wanajeshi hao wastaafu wamemshukuru mwenyezi mungu kwa kuwasaidia kumaliza kipindi chao salama na kupata heshima ya kuagwa kwa Amani.Wanajeshi walioagwa ni P6693 Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor mstaafu, P3726 Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi mstaafu, P3649 Meja Jenerali Denis Raphael Janga mstaafu, P7696 Brigedia Jenerali Zoma Mathic Kongo mstaafu, 

P7833 Brigedia Jenerali Nicodems Elias Mwangela mstaafu, P6090 Brigedia Jenerali Charo Hussein Yateri mstaafu, P8019 Brigedia Jenerali Raymond Kusirie Mwanga mstaafu, P8023 Brigedia Jenerali Juma Hidaya Mwinula mstaafu na PW 0131 Brigedia Jenerali Joyce Luli Kabati mstaafu.
 Mameja Jenerali, kutoka (kushoto) Gaudence Milanzi, Issa Suleiman na Denis Raphael, wakitoa heshima wakati wa gwaride maalumu la kuwaaga baada ya kustaafu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Kambi ya Twalipo, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanajeshi waliostaafu na kuagwa kwa heshima leo kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye kambi ya Twalipo, Jijini Dar es Salaam
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Issa Suleiman Nassor wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofnayika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, akimkabidhi kitambulisho cha kustaafu kazi, Meja Jenerali, Joyce Kabati wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.
 Gwaride la heshima kwa wastaafu wakati wa hafla ya kuwaaga Mameja Jenerali na Mabrigedia Jenerali , iliyofanyika katika Kambi ya Twalipo Dar es Salaam.

WAKAZI WA TANGA KUPATA HUDUMA ZA DHARURA NA MAHUTUTI KATIKA HOSPITALI YA BOMBO

$
0
0
Na Emmanuel Malegi-WAJMW-Tanga

Wakazi wa Jiji la Tanga sasa wataanza kupata huduma za uhakika za dharura pamoja na huduma za wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo).

Huduma hizo zimefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati ziara yake ya siku mbili mkoani humo huku akiwahakikishia wananchi wa Tanga kutolazimika kupewa rufaa kwa ajili ya kufuata huduma hizo Muhimbili na KCMC.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kuboresha huduma za afya katika Hospitali za mikoa kwa kujenga jengo la huduma za dharura lililogharimu Tsh. Milioni 211.6 na jingo la kuwahudumia wagonjwa mahututi Tsh. Milioni 350 katika kipindi cha mwaka 2018/19”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kuanzishwa kwa huduma hizo za dharura na mahututi zitatatua changamoto zilizokuwepo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/19 Serikali iliipatia Hospitali hiyo ya Mkoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Oksijeni (Oxygen Implantation).

Aidha, Waziri Ummy amesema kuanzishwa kwa huduma za dharura na mahututi zinategemewa kupunguza vifo vitokanavyo na dharura kwa asilimia 50, huku akiongeza kuwa Serikali inatarajia kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kwa asilimia 100 Hospitalini hapo, kutengeneza lifti katika wodi ya Galanos, kujenga kituo cha uchunguzi na vipimo pamoja na kujenga jengo la tiba shufaa kwa wateja walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Pamoja na hayo Waziri Ummy ameishukuru taasisi ya ABBOTT chini ya makamu wake wa Rais Bw. Andy Wilson kwa kusaidia ukarabati wa jengo la huduma za dharura kwa wagonjwa pia Waziri amewashukuru Wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kwa kuchangia kuboresha huduma za afya katika Hospitali hiyo.

Kwa upande Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi huduma za Kinga Dkt. Leonard Subi amesema uzinduzi huo wa huduma za dharura na chumba cha wagonjwa mahututi ni katika utekelezaji wa mkakati wa Wizara ya Afya kuhakikisha huduma hizo zinapatikana katika Hospitali zote za rufaa nchini. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa chumba cha wagonjwa mahututi wakati alipotembelea chumba hicho baada ya uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta na Makamu wa Rais wa Taasisi ya ABBOTT Bw. Andy Wilson wakati wa uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea jambo wakati wa uzinduzi wa huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga mapema leo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw. Thobias Mwilapa.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Kushoto) akioneshwa kifaa cha kusaidia mapigo ya moyo na Daktari bingwa wa huduma za dharura Dkt. Juma Ramadhan wakati Waziri alipozindua huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Bombo mkoani Tanga.

 

MKURUGENZI HOTELI YA KITALII IMPALA, NAURA JIJINI ARUSHA WASHIKILIWA POLISI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

MKURUGENZI wa Hoteli ya Kitalii Impala na Naura za jijini Arusha Randy Mrema na msaidizi wake wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kosa kuwanyanyasa na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake wapatao 180 katika kipindi cha miezi mitatu mfululizo.

Mrema na msaidizi wake Joram Lemanya walikamatwa mchana wa leo baada ya kuitwa na maofisa wa idara ya kazi ofisini na baadae kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi jijini hapa wanakoshikiliwa hadi sasa.

Kabla ya kutiwa nguvuni kwa Mkurugenzi huyo maofisa wa Idara ya kazi pamoja na maofisa wa Uhamiaji walivamia hotel ya Impala na kuwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi wawili ambao ni raia wa Kenya wanaodaiwa kufanyakazi kinyume na taratibu za nchi katika hotel ya Naura na Impala.

Akizungumzia tukio hilo Ofisa Idara ya Kazi mkoani hapa Wilfred Mdumi alithibitisha kushikiliwa kwa Mkurugenzi huyo kwa madai ya kukiuka makubaliano ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wake katika kipindi cha miezi mitatu, Mei Juni na Julai kiasi kinachofikia zaidi ya Sh.milioni 120.

Amesema Mkurugenzi huyo amekuwa akiahidi kupitia vikao mbalimbali kuhusiana na madai hayo kikiwemo kikao na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqar lakini wameshindwa kutekeleza ahadi wanazozitoa huku wafanyakazi wakiendelea kuteseka kwa kukosa mshahara.

Ameongeza amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kisheria ili wafanyakazi hao waweze kupata haki yao na wanatarajia kumfikisha mahakamani baada ya jalada kurejea kutoka kwa mwanasheria wa Serikali.

Kwa mujibu wa Mdumi Mkurugenzi huyo anadai changamoto za kibiashara zinazotokana na mgogoro wa kifamilia zinapelekea kuhujumiana kibiashara jambo linalosababisha kukosa wateja katika hoteli ya Impala na Naura na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi.

Baadhi ya wafanyakazi hao wamedai kunyanyaswa na kudharauliwa na Mkurugenzi huyo na wala hataki mawasiliano yoyote juu yao jambo lililowalazimu kuandika barua za malalamiko kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na ofisi ya idara ya kazi kutaka kujua hatima ya madai ya mishahara yao ya miezi mitatu.

Wafanyakazi hao wameenda mbali zaidi kwa kudai Mkurugenzi wao amekuwa na matumizi mabaya ya fedha ambapo amekuwa akiendekeza kununua viwanja ,nyumba na kufungua hoteli yake binafsi na kushindwa kuwajali wafanyakazi wake wanaomwingizia kipato.

Wafanyakazi hao wamemwomba Waziri mwenye dhamana kuwasaidia ili kuweza kulipwa madai yao ya mishahara kwani kwa muda mrefu wanateseka na kushindwa kutunza familia zao na wengine kufukuzwa kwenye nyumba walizopanga.

Kabla ya tukio hilo Randy na Joram hivi karibuni walikamatwa na askari wa kikosi maalumu cha kuzuia dawa za kulevya wakihusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya na kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam chini ya ulinzi mkali walikoshikiliwa kwa wiki moja kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Hotel hiyo ya Impala ,Naura na Ngurdoto ni Mali ya baba yao Marehemu Bilionea,Melau Mrema aliyefariki mwaka 2017 nchini Afrika Kusini alikokuwa amelazwa ,ambapo marehemu aliacha wosia kuwa mali zote zisimamiwe na mtoto wake mkubwa Joan Mrema.

Marehemu Mrema aliyekuwa na wake zaidi ya wanne ,Mama yake na Randy aliungana na dada yake na marehemu Mrema(Shangazi) na kuamua kukimbilia mahakamani kumpinga Joani na kufanikiwa kumpindua .

Hata hivyo uamuzi wa Mahakama ulimpa mamlaka Randy kuwa msimamizi na Mkurugenzi mpya wa hotel ya Impala na Naura huku Joan akiachiwa hotel ya Ngurdoto na baadhi ya miradi mingine yakiwemo magari ya kusafirisha watalii.

Hata hivyo Joan ameonesha uwezo mkubwa wa kusimamia mali za marehemu baba yake na kufanikisha kuwalipa mishahara wafanyakazi wa Ngurdoto kwa wakati huku akifungua miradi mingine ikiwemo kuanzisha ofisi mpya ya utalii.

MICHUZI TV: NIDA YAWAKUMBUSHA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI ILI KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA

DKT. MWANJELWA ATEMBELEA MKOA WA KAGERA KUKAGUA MIRADI YA TASAF.

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (hawapo pichani) katika Manispaa ya Bukoba wakati wa ziara ya kikazi yenye kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.

 Baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipowatembelea kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. 

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikaribishwa na mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Manispaa ya Bukoba, Bibi Irene Mgongo katika nyumba aliyoijenga baada ya kupata ruzuku ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na moja ya kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Manispaa ya Bukoba.

 Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Manispaa ya Bukoba, Bibi Irene Mgongo akimuonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) shamba analolima kwa kutumia ruzuku ya TASAF ili kujiongezea kipato.




DKT. MWANJELWA AWAFUNDA WALENGWA WA TASAF MKOANI KAGERA.

Na Estom Sanga- Kagera. 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Dokta Mary Mwanjelwa amewahimiza Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kuthamini mchango huo wa serikali kwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kunufaika zaidi na kuboresha maisha yao. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti mwanzoni mwa ziara yake ya mkoani Kagera ambako amekutana na Walengwa wa TASAF na Watumishi wa Umma ,Dr. Mwanjelwa amesema Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanapaswa kutumia vizuri fursa hiyo adhimu waliyoipata ili waweze kuendelea kunufaika nayo kwa ukamilifu. 

Naibu Waziri huyo wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amesema utekelezaji wa Mpango huo ni miongoni mwa Mikakati ya Serikali ya kukabiliana na kero ya umaskini kwa Wananchi na hivyo akawahimiza kuitumia fursa hiyo kwa kuanzisha miradi ya kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao na taifa kwa jumla. 

Aidha Dr. Mwanjelwa amepongeza mafanikio yaliyoanza kuonekana kwa Walengwa wa TASAF kuanza kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba,kuanzisha miradi ya kilimo, ufugaji na kukuza sekta ya elimu na afya ambayo amesema kwa kiwango kikubwa zimesaidia kukuza uwezo wa kuendesha maisha yao. 

Akizungumzia suala la baadhi ya vijiji kutojumuishwa kwenye Mpango, Dr, Mwanjelwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli ameagiza vijiji vyote vyenye Wananchi wanaostahili kujumuishwa kwenye Mpango huo vipewe fursa hi katika sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio waliyoanza kupata Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Bukoba tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango huo hususani katika nyanja za elimu, afya, uzalishaji mali na uboreshaji wa makazi yaa. 

“Nimejionea namna walengwa wa TASAF mnavyotumia rukuzu mnayopata kuboresha maisha yenu hilo ni jambo zuri kwani mnaunga mkono nia njema ya serikali ya Awamu ya Tano kwa vitendo,” Amesisitiza Dkt. Mwanjelwa. 

Amesema, kwa kutambua mchango wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika maendeleo ya wananchi, Serikali imeamua kuendelea kuutekeleza Mpango huo katika sehemu ya pili ambapo mkazo utawekwa zaidi katika miradi itakayowawezesha Walengwa kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kupata ujira kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato. 

Akizungumzia suala la baadhi ya maeneo kutonufaika na huduma za Mpango huo , Naibu Waziri huyo amesema, Serikali imeamua kuwa katika sehemu ya pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni maeneo yote nchini ambako wananchi watakidhi vigezo wajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo. 

“ Serikali hii haibagui wananchi wake, hivyo wale wote ambao watakidhi vigezo vya kuweko kwenye Mpango watapata fursa hiyo ili waweze kuitumia katika kuboresha maisha yao” Amefafanua Dkt Mwanjelwa. 

Dkt. Mwanjelwa yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi kujionea utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma katika Halmashauri zote za mkoa huo. 

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo takribani Kaya za Walengwa zipatazo Milioni MOJA na LAKI MOJA zimenufaika na huduma za Mpango huo katika sehemu yake ya Kwanza iliyoanza kutekelezwa mwaka 2012 kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba.

DK. BASHIRU: NI MARUFUKU WAJUMBE WA MASHINA (MABALOZI) KUKAA FOLENI KATIKA OFISI ZOTE ZA SERIKALI NA CHAMA

$
0
0
Katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Mwanza, leo Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally amefika wilayani Magu, ambapo katika vikao vitatu tofauti amesisitiza mabalozi nchi nzima kutokupanga foleni katika ofisi yeyote ya Serikali ama ya CCM.

Akiambatana na viongozi wa chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Ndg. Anthony Diallo, Katibu Mkuu amekutana na wanachama, mabalozi, na wajumbe wa halmashauri kuu za kata zote na matawi yote wilayani Magu katika vikao vitatu tofauti.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, mabalozi nchi nzima hawatakiwi kukaa foleni katika ofisi yoyote ya serikali na chama, kuanzia ofisi za watendaji wa mitaa, watendaji wa kata, wakuu wilaya, wakurugenzi, wakuu wa mikoa mpaka ofisi za wizara yoyote nchini, kwa sababu mabalozi ndio watu wanaofanya kazi kuliko kiongozi yeyote, kwa kuhangaika na changamoto za mwananchi mmoja mmoja katika eneo lake, bila ya mshahara na wanajitolea wakati wote.

“Nitoe rai kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi nchi nzima kwa viongozi wa serikali na Chama, wakuu wilaya na mikoa, wakurugenzi wote wa Halmashauri nchi nzima, makatibu wa wilaya na mikoa nchi nzima, hawa viongozi wetu wajumbe wa mashina ni marufuku kukaa foleni kwenye ofisi zenu, hawa ni viongozi na wamebeba watu nyuma yao, wanapokuja ofisini wanakuja kueleza hisia, changamoto, na ushauri wa watu wao 
wanaowaongoza. Kiongozi yeyote atakaye wadharau mabalozi wetu huyo hatufai ndani ya Chama na serikali hii ya CCM.” 

Dk. Bashiru amesisitiza.
“Wajumbe wa mashina ni watu muhimu sana na wamekuwa wakifanya kazi hizi ngumu kwa uzalendo wao pasipo malipo ya mshahara, wanajitoa wakati wote kusaidia watu, wanajua changamoto za mwananchi mmoja mmoja na wakati mwingine hawalali kwa ajili ya shida za watu wanaowaongoza, wanafanya yote haya kwa kujitolea na uzalendo kwa nchi yetu, sitaki nisikie wanawekwa foleni katika ofisi yoyote ya umma, hata ofisini kwangu nikisikia balozi amekuja kutaka kuongea na mimi ni lazima nimpe kipaumbele kwa sababu najua hawa ndio wanaishi na watu.” Katibu Mkuu amefafanua.

Katika vikao hivo Dk. Bashiru amepata fursa ya kusikiliza kero za wananchi, ambapo wananchi wameonesha kuwa na hamu kubwa ya kusikilizwa kero zao za muda mrefu na kutopata wasaa wa kukutana na viongozo wa maeneo yao, kuelezwa na kufafanuliwa mambo mbalimbali yanayohusi changamoto zao.

Katika hatua hiyo Dk. Bashiru ameendelea kukazia maelekezo ya Mh. Rais John Pombe Magufuli kuwataka viongozi wote kuanzia ngazi za msingi mpaka taifa kutenga muda katika maeneo yao kuwa karibu na wananchi, kuwasikiliza kero zao, na kuwapatia ufafanua kwa kuzingatia hali halisi kama afanyavyo Rais mara kwa mara apatapo muda ofisini au akiwa ziarani, kama alivyofanya kwa wachimbaji wadogo, wafanyabiashara n.k.
“Kila mmoja katika eneo lake la uongozi asikilize watu, atoe ufafanuzi juu ya masuala yanayowatatiza wananchi, awe karibu na wananchi.

 Hatuwezi kumuachia Mh. Rais aendeshe nchi hii peke yake wakati ametupatia mamlaka ya kutenda na kusaidia watu.” Katibu Mkuu amesisitiza.

Akiwa wilayani Magu Katibu Mkuu ameweka jiwe la msingi la na kushiriki ujenzi wa Hosteli za CCM na kukagua mradi wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ambapo amewaongezea ng’ombe mmoja ili kuimarisha mradi utakao wezeshe shughuli za Chama na Jumuiya.Ziara ya leo wilayani Magu ni muendelezo wa kutekeleza jukumu la viongozi wa CCM kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU WANAPOWASILISHA TAARIFA ZA KIUTUMISHI OFISI YA RAIS UTUMISHI KUEPUKA MALALAMIKO YA WATUMISHI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya Watumishi wa Umma mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof.Faustin Kamuzora akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Watumishi wa Umma mkoani Kagera chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
…………………….

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka waajiri nchini kuhakikisha wanazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu wanapowasilisha taarifa za kiutumishi ili kuepuka malalamiko yanahusu stahili mbalimbali za kiutumishi.

Dkt. Mwanjelwa ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuzungumza na Watumishi wa Umma mkoani humo kuhimiza uwajibikaji.
Dkt. Mwanjelwa amesema zoezi la kusafisha taarifa za watumishi limeibua kero kwa baadhi ya watumishi kutokana na waajiri kutozingatia maadili wanapowasilisha taarifa za kiutumishi.

“Awali baadhi ya waajiri waliwasilisha taarifa za watumishi zisizo sahihi hali iliyosababisha baadhi ya watumishi hao kupewa stahili ambazo si halali na matokeo yake wakati wa zoezi la kusafisha taarifa wamekuwa wakibainika kutostahili na hatimaye watumishi hao kuona kama wameonewa,” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Ameongeza kuwa, mtumishi wa umma anakamilika kwa kuwa na tabia njema, nidhamu ya kazi, mwenendo mzuri, weledi na ubunifu, hivyo ni vema kila mtumishi akazingatia hilo ili awe na manufaa kwa umma na tija kiutendaji.

Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha utumishi wa umma unakaa sawa, kama mtumishi anapaswa kupata haki yake, atapata na kama hastahili aachwe badala ya kupendelewa,” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa yuko mkoani Kagera katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma katika Halmashauri zote za mkoa huo.

BRELA KUTOA LESENI ZA BIASHARA DARAJA A KWA WASAFIRISHAJI WA MAZAO NA MIFUGO NJE YA NCHI KWENYE MAONYESHO YA NANE NANE

$
0
0
Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo kulia akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda lao kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu
NAIBU Waziri wa Viwanda Mhandisi Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) mara baada ya kutembelea banda lao
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) wamesema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje.

Hayo yalisemwa na Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu.

Alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja dhima ya kujenga uchumi wa viwanda.
Suzana alisema hivyo vyote vinaenda sambamba na uwezeshaji biashara huku akieleza lengo kubwa la mfumo ni kuhakikisha wakulima na wazalishaji wa bidhaa nchi wanapata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje .

“Kwa mfano mtu anataka kusafirisha bidhaa kupeleka Ulaya ,ni rahisi sana kupata taarifa hizi katika mfumo wa trade facilitation information module ambapo hapo awali haikuwepo kabisa”Alisema

Alieleza kwamba wanataka wakulima,wafanyabishara wapate taarifa moja kwa moja kutoka mkoani Simiyu katika viwanja vya nane nane.

Aidha alisema kwa mkoa huo wafugaji wengi hivyo wafugaji ni wengi hivyo ukitaka kujua taarifa zinazohusu vibali na leseni mbalimbali katika kupeleka mifugo yake katika soko la nje ni rahisi kwasababu taarifa zipo ambazo zitamuwezesha kujua nini anahitaji, kwa gharama gani, itachukua muda gani, aendee taasisi gani na iko wapi.

Aliongeza kwamba kwa mantiki hiyo mfumo huu ni mwarobaini wa tatizo la taarifa za kibiashara katika upatikanaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini huku wakiwakaribisha wananchi kufika kwenye banda lao kupata huduma hizo.

“Lakini pia BRELA tunatoa leseni za kundi A kama zilivyoainishwa katika sheria Leseni za Biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake…. Leseni za kundi A ni zipi, ni zile leseni zinazotolewa kwa biashara zenye mlengo wa kitaifa, kimataifa na zenye usimamizi maalum, biashara hizi ni kama usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi na biashara za usimamizi maalum kama za madini, benki na zingine kama hizo.

Awali akizungumza Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela suzana Senso amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje (internatinal market) .

Hivyo bas mkulima / mfanyabiashara akifika BRELA anapata taarifa za kibishara zaidi katika biashara za kimataifa,asajili kampuni au jina la biashara na anapata leseni itakayomuwezesha kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi.

Hata hivyo alisemwa kwamba kwa matiki hiyo sasa Brela ni one stop shop mfanyabiashara akifika hapa anapata kila kitu kitakachomuwezesha kwenda kufanya biashara duniani.

Naye kwa upande wake Eliabu Rwabiyago ambaye ni Afisa kutoka Brela amesema wakala pia ina kitengo cha kuwezesha biashara (trade facilitation section) ambacho kimejikita katika uwezeshaji biashara.

Alisema kwa sasa wakala huo unaandaa portal inayoitwa trade facilitation information module , portal ambayo itajikita katika kutoa taarifa za kibiashara nchini.

Alisema kwasababu wafanyabiashara wengi nchini na nje ya nchi wanataka kufanyabiashara lakini taarifa za kibiashara kwa maana ya vibali na leseni mbalimbali zinazohitajika zinapatikanaje na kwa muda gani hivyo kwa mtandao hayo maswali yote yamejibiwa.

Alieleza kwamba kukamilika na kutumika kwa mfumo huu kutakuwa na faida nyingi sana katika uwezeshaji wa biashara ikiwemo kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za umma, kuiongeza ushirikiano baina ya ofisi za umma na wafanyabiashara maana kwa kutumia mfumo watakuwa wanaweza kaundika maoni na maswali yao kujibiwa moja kwa moja,

Alisisitiza pia kwamba pia mfumo huu unatumika kama promotional tool kwa maana bidhaa ambazo tunataka ziende duniani kirahisi zinawekwa katika mfumo na wafanyabiashara wanazipata kirahisi, kupunguza gharama za ufanyaji wa biashara na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla.

Mpaka sasa BRELA wameweza kuweka taarifa ya bidhaa 26 za kupeleka nje ya nchi (export) na 13 za kuingiza ndani ya nchi (import)

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MOROGORO

$
0
0

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia bustani ya Mboga alipotembelea banda la Halmashauri ya Morogoro wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa hotupa wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere Agosti 1, 2019 Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Steven Kebwe akizungumza na washiriki pamoja na wakazi wa Morogoro waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane katika Mkoa huo.
Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya washiriki wa Maonesho hayo na wananchi wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa maonesho ya Nanenane 2019.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Morogoro Bi. Theofora Madilu akielezea huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea banda la benki hiyo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Steven Kebwe.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitazama aina ya mtama alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo katika maonesho hayo ya Nanenane.
Kaimu Afisa Kilimo kutoka kwenye Banda la Halmashauri ya Morogoro, Bi. Happifania Matafu akimfafanulia Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama aina ya tangawizi zinazozalishwa katika Mkoa huo, alipotembelea banda hilo.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia akiangalia shamba dogo la mbaazi alipotembela banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo.

Waziri Mwakyembe akutana na kufanya mazungumzo na mjumbe toka Ligi ya Hispania

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya wakati Mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe na kujadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana ili kuinua soka la Tanzania.
Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe mikakati ya Shirikisho la nchi yake katika kuisadia Tanzania kufanya vizuri katika mchezo wa soka.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi nchini, Boniface Wambura (kushoto) akifafanua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) mikakati mbalimbali waliyofikia na Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (hayupo pichani) wakati mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akiagana na Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (kushoto) mara baada ya kumaliza kujadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana ili kuinua soka laTanzania.Picha na WHUSM-Dar es Salaam.

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU BAJAJ, BODABODA KULIPISHWA FAINI PAPO KWA PAPO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza
na mamia ya Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodadoda Mkoa
wa Kilimanjaro, katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa CCM,
Mjini Moshi, Mkoani humo, leo. Amewapiga marufuku Polisi wa
Usalama Barabarani nchini kuwalipisha faini waendesha bajaj
na bodaboda papo kwa papo wanapofanya makosa barabarani
na kutaka wapewe siku saba kama ilivyokuwa kwa magari.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto)
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira
alipokua anazungumza na mamia ya Wamiliki na Waendesha
Bajaj na Bodadoda Mkoa wa Kilimanjaro, katika Ukumbi wa
CCM, Mjini Moshi, Mkoani humo, leo. Lugola amewapiga
marufuku Polisi wa Usalama Barabarani nchini kuwalipisha faini
waendesha bajaj na bodaboda papo kwa papo wanapofanya
makosa barabarani na kutaka wapewe siku saba kama
ilivyokuwa kwa magari. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza
na mamia ya Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodadoda Mkoa
wa Kilimanjaro, katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa CCM,
Mjini Moshi, Mkoani humo, leo. Amewapiga marufuku Polisi wa
Usalama Barabarani nchini kuwalipisha faini waendesha bajaj
na bodaboda papo kwa papo wanapofanya makosa barabarani
na kutaka wapewe siku saba kama ilivyokuwa kwa magari.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mmiliki wa Bajaj Mjini Moshi, akimuuliza swali Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani),
wakati wa Mkutano wa kutatua changamoto zinazowakabili
wamiliki na waendesha bajaj na bodaboda Mkoani Kilimanjaro.
Mkutano huo uliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa huo
na kumwalika Waziri Lugola kwa lengo la kuja kuzungumza
katika mkutano huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.

Naibu Waziri Kwandikwa Akagua Miundombinu ya Ujenzi Mkoani Ruvuma

$
0
0
Kazi ya ujenzi wa barabara ya Lusitu- Mawengi km 50 inayojengwa kwa zege ikiendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Itoni-Ludewa-Manda km 211.4.
Mhandisi mshauri wa ujenzi wa barabara ya Lusitu- Mawengi km 50 ambayo ni sehemu ya barabara ya Itoni-Ludewa-Manda km 211.4 Moon Dong Ryeol akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akisambaza zege alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Lusitu- Mawengi km 50 wilayani Ludewa mkoani Njombe.Muonekano wa barabara ya Lusitu- Mawengi km 50 inayojengwa kwa zege ambayo ni sehemu ya barabara ya Itoni-Ludewa-Manda km 211.4 mkoani Njombe.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa pamoja na wataalam wake wakifurahia kupita juu ya blanketi lililofunika barabara ya Lusitu- Mawengi km 50 inayojengwa kwa zege katika kijiji cha Mselesele Wilayani Ludewa.Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akikagua daraja la Mkenda katika mto Ruvuma, daraja hilo linaunganisha nchi za Tanzania na Msumbiji na linatarajiwa kujengwa sambamba na barabara ya Lukuyufusi-Mkenda km 124, kulia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Bw, Porleto Mgema na katikati ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma Eng. Razak Alinanuswe.Muonekano wa daraja la Mkenda mkoani Ruvuma daraja hilo linaunganisha nchi za Tanzania na Msumbiji kupitia mto Ruvuma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akitoa maelekezo kwa mhandisi mshauri wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Songea Eng, Deo Mugishangwe (kulia) na mkuu wa Wilaya ya Songea Bw, Porleto Mgema (kushoto), alipokagua ukarabati wa uwanja huo.

SERIKALI IMETOA MILIONI 100 KUJENGA BWENI LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM HALMASHAURI YA MJI GEITA

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kisasa la wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mbugani iliyopo katika halmashauri ya Mji Geita.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara mkoani Geita ambapo amesema fedha hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu nchini.

Ole Nasha amesema serikali ya Awamu ya Tano inatambua umuhimu wa kuwajengea fursa na mazingira mazuri ya kusoma watoto wenye mahitaji maalum na ndio maana imeweka mkazo katika kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu wa kutosha, vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vitabu ili kuwawezesha kusoma bila vikwazo vyovyote kutokana na changamoto zao za kimaumbile.

“Kwa miaka mingi jamii nyingi zimekuwa zikiwatenga watoto wenye mahitaji maalim, lakini kwa sasa nashukuru tumeendelea kuwawezesha kupata haki yao ya Elimu kama walivyo watoto wengine na kwamba wanaweza kuwa na changamoto za kimaumbile lakini ubinadamu wao upo palepale amesema Waziri Ole Nasha.

Amewataka wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kutokatishwa tamaa na changamoto walizonazo za kimaumbile kwani serikali imewawekea mazingira ya kuwawezesha kufika mbali zaidi katika Elimu na kuwataka kuendelea kutumia fursa hizo za kielimu ili kutengeneza maisha yao ya baadaye.

"Wanafunzi, mtu hawezi kujua kipaji chako ni kipi lakini serikali inakupa fursa ya kuonyesha kipaji chako, Mhe Rais ametambua uwezo mkubwa wa watu wenye mahitaji maalum na ndio maana siku hizi tunae Naibu Waziri anayeshughulika na watu wenye mahitaji maalum ambaye naye ana changmoto ya ulemavu," amesema Naibu Waziri.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mbugani Edwicka Ndunguru amemweleza Naibu Waziri kuwa kituo hicho kilijengwa kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata haki ya kielimu katika mazingira wezeshi na kuwapa fursa wengi zaidi wenye mahitaji maalum wanaoishi mbali na shule zinazotoa elimu maalum kupata elimu.

Amesema mafanikio ya kuwepo kwa vituo vya watoto wenye mahitaji maalum mbali na kuwawezesha kupata haki yao ya kielimu, pia imewasaidia kujifunza ujuzi mbalimbali, jamii imetambua nakuthamini umuhimu wa wanafunzi wenye mahitaji maaluma kupata Elimu na wengine kufanikiwa kupata kazi katika maeneo mbalimbali.

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapomaliza hapa wanakua na ujuzi katika fani za ushonaji, ufumaji na useremala, fani hizi zimewezesha baadhi kuajiriwa katika maeneo mbalimbali na wengine kujiajiri amesemu mwalimu Ndunguru. 

Kituo hicho chenye vitengo vinne vyenye jumla ya wanafunzi 143 ambavyo ni vitengo vya ulemavu wa akili, Viziwi, ulemavu wa viungo na ulemavu wa macho, mbali ya kuhudumia wanafunzi hao wenye uwezo wa kufika shuleni lakini pia vinahudumia watoto 38 wenye ulemavu wa kiwango cha juu ambao hawawezi kufika shuleni.
 Sehemu ya bweni lilojengwa na serikali katika Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mbugani iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum katika kituo Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.
Baadhi ya wanafunzi wa kituo cha Elimu Maalum katika shule ya msingi Mbugani wakicheza ngoma mbele ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha aliyefanya ziara katika kituo hicho kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum (Hawapo Pichani)  baada ya kukagua ujenzi wa bweni la Kituo cha Watoto wenye mahitaji Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.

OLE NASHA: SERIKALI HAITAMVUMILIA MTENDAJI YEYOTE ATAKAYEHUJUMU FEDHA ZA UJENZI WA OFISI ZA UTHIBITI UBORA WA SHULE

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameagiza watendaji wa idara ya uthibiti ubora wa shule kusimamia kwa makini miradi ya ujenzi wa ofisi za Uthibiti ubora wa shule pamoja na fedha zinazotumwa kwa ajili ya ujenzi huo katika Halmashauri za wilaya mbalimbali nchini.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema hayo mkoani Geita wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya Elimu inayotekelezwa mkoani humo, ambapo amesema serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayehujumu ama kutumia vibaya fedha hizo zilizotolewa na wizara kwa ajili ya kujenga ofisi hizo.

Amesema miradi ya ujenzi wa ofisi hizo ni muhimu sana kwa wizara kwani ili kuwa na maendeleo katika sekta ya elimu lazima kuwa na wadhibiti ubora wa shule mahiri, wenye uwezo wa kukagua shule na wenye vitendea kazi vya kuwezesha kufanya kazi katika mazingira sahihi.

“Kama tunataka kuwa na maendeleo katika sekta ya Elimu lazima kuwe na usimamizi thabiti na ndio maana tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha tumeboresha idara ya uthibiti ubora kwa kuhuisha mfumo kutoka kuwa ukaguzi na kuwa uthibiti kwa maana kwamba unashirikisha kila mtu katika hatua zote,” amesema Ole Nasha.

Ole Nasha amesisitiza kuwa haiwezekani kufanya kazi ya uthibiti ubora wa shule kama hakuna ofisi, vitendea kazi ikiwemo magari na ndio maana kila Afisa Elimu wa Kata kwa nchini nzima alipewa pikipiki ya kumwezesha kufanya kazi. Serikali pia ilitoa magari 45 kwa wilaya mbalimbali na sasa halmashauri zipatazo 100 zinajengewa ofisi za uthibiti ubora.

Naibu Waziri Ole Nasha amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ofisi hizo, Wizara itapeleka vifaa vyote muhimu kwenye ofisi hizo ili kurahisisha kuchakata taarifa zote za elimu kutoka maeneo yote ya nchini kwa lengo la kurahisha huduma za kielimu.

Aidha, Waziri Ole Nasha amesema ameridhishwa na usimamizi na matumizi ya fedha za ujenzi wa ofisi za uthibiti ubora Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha Mikoa ya Geita, Mwanza na Mara ambayo kwa ujumla inajengewa ofisi 15 zenye thamani zaidi ya bilioni 2.28.

Katika ziara hiyo Waziri Ole Nasha amekagua majengo ya uthibiti ubora wa shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Halmashauri ya mji wa Geita. Ole Nasha pia amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni mawili na vyoo katika shule ya sekondari Mwatulole ambayo inatarajiwa kuanzisha kidato cha tano hivi karibuni.

Shule nyingine aliyotembelea ni shule ya sekondari ya Wasichana Nyankumbu ambapo ametembelea chumba cha kompyuta na ameahidi kupeleka kompyuta 50 shuleni hapo ili kuongeza ari ya kujifunza.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka alimweleza Naibu Waziri kuwa ameshirikiana na watendaji wengine kufanikisha ujenzi ambao uko kwenye hatua ya ukamilishaji na kuahidi kuwa ataendelea kusimamia ili jengo hilo likamilike kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwatulole s alipofikia  shuleni hapo kukagua  maendeleo ya ujenzi wa mabweni mawili pamoja na madarasa unaotekelezwa na wizara ya Elimu.

Muonekana wa jengo la ofisi za uthibiti ubora wa shule ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita huku ujenzi ukiendelea. Jengo hili ni moja ya majengo ya ofisi za wathibiti bora kati ya matano yanayoendelea kujengwa katika Mkoa wa Geita.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiangalia baadhi ya vitabu katika maktaba ya shule ya wasichana ya sekondari Nyankumbu alipofikia  shuleni hapo kukagua  chumba chs kompyuta, waziri Ole Nasha yupo Mkoani Geita kwa ziara ya Kikazi


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita (Hawapo Pichani) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo ambapo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa ofisi hizo.

TENKLOLOJIA YA NYUKLIA KUWA MKOMBOZI KWENYE UZALISHAJI WA MBEGU BORA ZA MAZAO NA MIFUGO

$
0
0
Simon Mdoe Mtafiti mwandamizi wa teknolojia ya Nyuklia akiwa katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha.
Simon Mdoe Mtafiti Mwandamizi wa teknolojia ya Nyuklia akimpatia mteja elimu ya teknolojia ya nyuklia katika kilimo mteja Gadiel Kitomari alipotembembelea banda hilo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha
Peter Ngamilo ni mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAEC akimpatia mteja elimu ya teknolojia ya nyuklia katika kilimo mteja Gadiel Kitomari alipotembembelea banda hilo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini Themi Njiro Mkoani Arusha


Na Vero Ignatus, Arusha

TUME ya Nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) imefanikiwa kupata matokeo chanya ya utafiti wa mbegu ya mpunga ya Super Bc kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya kununurisha vinasaba (viasili)vya mbegu hizo
na kupelekea mavuno mengi zaidi visiwani Zanzibar.

Simon Mdoe ni Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya Nyuklia, na Michuzi Blog kwenye maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini amesema utafiti huo ulioanza 2009 umefanikisha matokeo chanya mara saba zaidi kwa mavuno ya mbegu ya mpunga ya Super Bc huko visiwani Zanzibar ikilinganishwa na awali.

Amesema TAEC kwa kushirikiana na shirika la mbegu la Zanzibar, ZARI na pamoja na chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ilianza utafiti wa mbegu hiyo ambapo walinunurisha kupitisha mionzi kitaalamu kwenye mbegu) ambayo ilibadilisha viasili (vinasaba) na kuwa bora zaidi kuweza kuzalisha mara saba ya mazao yaliyokuwa yakizalishwaawali.

“Utafiti wetu tulichukua mbegu za mmea wa mpunga na kupitisha miale ya nyuklia kwa hatua sita, huku kila hatua moja tukihamishia mbegu shambani na kupata matokeo tofauti, mara ya mwisho tulipata matokeo mazuri zaidi kuliko hatua nyingine tano na kugundua kuwa na mavuno yamefikia mara saba ya kawaida ya mbegu hizo kama mkulima anavuna magunia 19 kama ambavyo imezoeleka kwa mbegu za zamani na alipotumia mbegu zetu alipata gunia 80 za mpunga.alisema Mdoe

Mtafiti huyo amesema baada ya matokeo ya utafiti walishirikisha mashirika ambayo pia yalialika maduka ya mbegu visiwani Zanzibar na kuwapelekea wakulima ambao walipata matokeo hayohayo mazuri mara saba zaidi
tofauti na awali kabla ya utafiti.

Mdoe amesema pia matokeo mengine ya utafiti na kuboreshwa kwa mbegu kupitia mionzi ya nuklia yamebaini kuongezekana kwa ladha ya mchele uliotokana na mpunga wa Super Bc, pamoja na harufu nzuri kwa walaji.

“Alisema pia matokeo ya tafiti yameonyesha mbegu hiyo kutoshambuliwa
na wadudu wakati wa kuota na ukuaji wake”alisema Mdoe
Mtafiti huyo alisema TAEC kwa kushirikiana na Chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA) wanaendelea na utafiti ili kununurisha mbegu nyingine za mpunga, zaidi ya Super Bc kwa kuzingatia hali ya hewa na maeneotofauti ya Nchi na aina ya udongo ili kupata tija itokanayo na mavuno mengi kwa ustawi wa Uchumi wa Nchi.

Mdoe amesema utafiti wa kununurisha mbegu hizo unafanyika kwenye kituo cha utafiti cha Ilonga Mkoani Morogoro na katika kituo cha Mati kilichopo eneo la Uyole Jijini Mbeya.

Tafiti nyingine kama hizo za mbegu za Mahindi na shairi zinazofanyika katika Kituo cha utafiti wa mbegu za Kilimo cha SELIAN, Arusha ambazo ununurishaji umeshafanyika na tayari mbegu hizo ziko kwenye hatua za mpando wa awali ambapo hatua yenye ubora wa juu utakapofikia tamati, zitasambazwa kupitia njia zilizofanyika Zanzibar kwa wakulima ili kuongeza mavuno na kukuza uchumi wa wakulima na Taifa kwa pamoja.

Amesema TAEC/(TAHA)kwa pamoja wako kwenye upembuzi yakinifu ili kuona namna ya kununurisha mboga mboga,matunda na maua ili kuhifadhika kwa muda mrefu na unaofaa pindi bidhaa inapokuwa sokoni kwa muda ili isiharibike kwa urahisi kwani uzoefu unaonyesha asilimia 40 ya matunda na mboga ,boga huharibika kwa kuoza kutokana kukosa teknolojia kama hiyo ya mionzi.

Amesema tafiti nyingine zinafanyika kwenye mbegu za wanyama kama N’gombe kwa njia ya uhamilishaji kwa kushirikiana na Tasisi ya mifugo ya uhamilishaji iliyopo Usa ya (NIC) ili kupata mifugo bora inayokidhi viwango vya ndani na nje kwa nyama bora.

Peter Ngamilo ni mkuu wa kitengo cha Mawasiliano TAEC ambapo amesema shirika hilo lina matarajio ya kuwa na mtambo wa kuzalisha vyanzo vya mionzi (Linear Acceletor)vinavyotumika kwenye matibabu, viwanda,

kilimo na utafiti (Radioisotopes)

Aidha TAEC ina matarajio ya kuanzisha mradi wenye kutumia teknolojia ya nuklia katika kufanya tafiti mbalimbali (Nuclear Research Reactor)Zenye manufaa kwa Nchia ambapo Mtambo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na viwanda vya madawa ya tiba ya saratani pamoja na kutumika kama nyenzo ya kufundishia katika taasisi za elimu ya juu na
utafiti.

Tume ya nguvu ya Atomiki (Tanzania Atomic Energy ommission)ilianzishwa kwa sheria ya Bunge no 7 ya Mwaka 2003, awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya taifa ya mionzi iliyoanzisha kwa sheria ya bunge no 5 Mwaka 1983 ambapo ina majukumu ya kuthibiti matumizi ya mionzi salama Nchini, kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojiaya Nyuklia na kufanya utafiti.

MBUNGE YOSEPHER KUFIKISHA KILIO CHA WANANCHI WA KIJIJI CHA UPARE MUHEZA WIZARA YA AFYA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba kushoto akichukua kero za wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge huyo
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba kushoto akisalimiana na wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao wakati wa ziara yake

UKOSEFU wa Huduma za Afya kwenye Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga kumepelekea Mbunge wa Viti Maalumu mkoa huo (Chadema) Yosepher Komba kujitwisha mzigo huo na sasa anakusudia kwenda Wizara ya Afya ili kufikisha kilio hicho.

Hatua ya Mbunge huyo inatokana na kilio cha wananchi hao ambao walieleza kwamba idadi yao ni wakazi zaidi ya 600 wakati wa ziara yake wakieleza tatizo la kukosa zahanati na kulazimika kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Teule.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kusikiliza kilio hicho alisema kwamba sheria ya Wizara ya Afya kila Kijiji kinapaswa kuwa na Zahanati hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha kijiji hicho kinapatiwa huduma ya afya ili kuweza kunusuru afya za wananchi wa maeneo hayo hasa kinamama na watoto.

Mbunge huyo alisema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo atakwenda kukutana na Waziri Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ili kumueleza tatizo hilo kwani haiwezekani zaidi ya wananchi 600 katika kijiji hiki wanakosa huduma ya afya hii ni hatari kwa ustawa wa afya zao.

Alisema anashangazwa na viongozi wa Serikali wanaofanya ziara katika maeneo mbalimbali ya wilaya na wanajua tatizo hilo la kutokuwepo kwa huduma hiyo ya afya huku hakuna hatua zozote ziznazochukuliwa ili kuwasaidia wananchi hao.

Alisema ni jukumu la viongozi kutenda haki katika nyanja zote ili kutenda usawa wa huduma za kijamii na kuweka mazingira rafiki ya afya kwa wananchi hao kuliko kusubiria athari zitokee na kuanza kutafuta chanzo.

Awali wakizungumzia hali wananchi wa maeneo hayo alisema wanalazimika kutembea zaidi ya km 12 kuelekea Wilayani Muheza kupata huduma bora ya afya jambo ambalo linahatarisha maisha yao.

Mmoja wa wananchi hao Frednand Francis alisema ipo haja kwa Serikali kupitia Wizara yake kuwahurumia wananchi hao katika suala zima la afya ambayo ndio msingi wa maisha ya mwanadamu.

Francis alisema ni kitu cha ajabu kuona kijiji hicho kilichokuwa na wakazi zaidi ya 600 huku kikosa huduma hiyo ya afya jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao na watoto ambao ndio msingi wa Taifa lijalo.

Hata hivyo alimuomba kuwasaidia kufikisha kilio hicho kwa Waziri mwenye dhama juu ya hali mbaya kukosa huduma ya afya jambo ambalo ambalo linaweza kuleta madhara baadae kutokana na wananchi wengi kuathirika na maradhi.

AGAPE YAHITIMISHA MRADI ELIMU AFYA YA UZAZI NA UJINSIA KATA YA USANDA

$
0
0
Shirika lisilo la kiserikali la AGAPE AIDS CONTROL PROGRAM la Mkoani Shinyanga, limehitimisha Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana ambao ulikuwa unatekelezwa katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambao ulilenga kutokomeza masuala ya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.


Kikao cha kuhitimisha mradi huo wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana, kimefanyika leo Agosti 2,2019 katika shule ya Msingi Shingita iliyopo kwenye kata ya Usanda, na kuhudhuriwa na mtendaji wa kata, mratibu elimu kata, Afisa maendeleo, wenyeviti wa vitongoji, viongozi wa kidini, wazee wa kimila, pamoja na waelemishaji rika. Utekelezaji wa mradi huo wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia ulianza mwaka (2017) na kuhitimishwa June 30 mwaka huu (2019), ambapo Shirika la AGAPE lilikuwa likiutekeleza kwenye kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Sida la nchini Sweden kupitia Save the Children. =

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mradi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola ,amewaasa viongozi wote wa kata hiyo ya Usanda,wakiwemo wazee wa kimila na waelemishaji rika, kuyaendeleza mapambano ya kupinga ukatili ndani ya jamii zikiwemo mimba na ndoa za utotoni. 

Amesema licha ya AGAPE kuhitimisha mradi huo kwa awamu ya kwanza isiwe ndiyo mwisho wa kuendeleza mapambano ya kupinga ukatili pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, ambapo kila mtu anapaswa awajibike kwa nafasi yake ikiwemo na viongozi kuendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia mikutano mbalimbali na kutomeza matukio hayo. “Sisi AGAPE leo tumekuja kuhitimisha rasmi mradi wetu wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kwenye kata hii ya Usanda, ambao ulilenga kutokomeza masuala ya ukatili wa kijinsia, zikiwamo mimba na ndoa za utotoni,”amesema Myola. 

“Hivyo kutokana na sisi kuhitimisha mradi wetu huu, tunaomba na nyie sasa viongozi wa Kata hii ya usanda mkiwemo viongozi wa kidini,wazee wa kimila, wenyeviti wa vitongoji na waelimishaji rika, muendeleze mapambano haya ili msirudi kule mlikotoka, ambapo awali kata hii ilikuwa ikiongoza kwa mimba na ndoa za utotoni,”ameongeza Myola. Pia amewataka wazazi na walezi kwenye kata hiyo , wawekeze watoto wao kwenye elimu na kuacha kuthamini mifugo, na kuozesha watoto wao ndoa za utotoni, ambapo pindi watakapohitimu masomo yao na kupata kazi nzuri, watakuja kuwasaidia baadae, pamoja na kuwanunulia hiyo mifugo ambayo wanaitaka.

Naye mtendaji wa kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, amelipongeza Shirika hilo la AGAPE kwa kupeleka mradi huo katani humo, ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni. Kwa upande wake mratibu elimu kata ya Usanda Sospeter Kasonta, amesema Shirika hilo la Agape limesaidia kupunguza tatizo la mimba kwa wanafunzi, ambapo mwaka (2016) kulikuwa na mimba 21, (2017) 16, (2018) mimba nne (4), na mwaka huu mpaka sasa kuna mimba moja tu ya sekondari. TAZAMA PICHA HAPA CHINI Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akizungumza kwenye kikao cha kuhitimisha Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola,akizungumza kwenye kikao hicho na kuwataka viongozi wa kata ya Usanda, mtendaji wa kata, maendeleo, viongozi wa dini, kimila,vitongoji na waelimishaji rika, na kuwataka waendeleze mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni, licha AGAPE kusitisha mradi wao kwenye kata hiyo. Prosper Ndaiga kutoka Shirika la AGAPE akimwakilisha Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Lucy Maganga ,akielezea namna mradi huo ulivyofanya kazi kwenye kata hiyo ya Usanda na hatimaye kupunguza matukio ya ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni. Mtendaji wa kata ya Usanda Emmanuel Maduhu, akipongeza Shirika la Agape kwa kupeleka Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana, ambao umesaidia kupunguza matukio ya ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni. Afisa Maendeleo kata ya Usanda Halima Tendega, akielezea Shirika hilo la AGAPE namna lilivyosaidia kupunguza matukio ya ukatili zikiwamo mimba na ndoa za utotoni tofauti na hapo awali hali ilikuwa mbaya. Mratibu Elimu kata ya Usanda Sospeter Kasonta, akipongeza Shirika la AGAPE kwa kupunguza matukio ya ukatili, ukiwemo utoro mashuleni, mimba na ndoa za utotoni, huku akitoa na ushahidi kwa takwimu, ambapo mwaka 2016 kulikuwa na mimba 21, (2017) 16, )2018) nne na )2019) mimba moja. Mwenyekiti wa kitongoji cha Manyada Daudi Michael, akielezea namna Shirika la Agape lilivyosaidia kuifumbua jamii juu ya matukio ya ukatili na kupinga mimba na ndoa za utotoni, ambapo wao wameshapiga marufuku wanafunzi kucheza shoo kwenye maharusi. Geofrey Maganga ambaye ni muelimishaji rika kutoka kitongoji cha Mwagala, naye akielezea namna jamii ilivyobadilika mara baada ya kupata elimu kutoka kwenye Shirika la Agape, na kuanza kusomesha watoto wao hasa wa kike. Mzee wa kimila Shija Kulwa, akielezea namna Shirika hilo la Agape lilivyosadia kubadili mitazamo jamii na kuachana na masuala ya mila na desturi kandamizi ambazo zilikuwa zikisababisha kuendelea kuwepo masuala ya ukatili ndani ya jamii pamoja na kuozesha watoto ndoa za utotoni. Muelimishaji rika kutoka kitongoji cha Mwagala Mary John akielezea namna jamii ilivyobadilika mara baada ya kupewa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape. Mchungaji kutoka Kanisa la AICT Usanda Lameck Makungu, akielezea namna Shirika la Agape lilivyosaidia kuikoa jamii, ambapo wao kama viongozi wa kidini walipokuwa wakipinga matukio hayo ya ndani ya jamii, waumini walikuwa wakihama madhehebu kwa sababu ya kugusa maslahi yao. Viongozi kutoka kata ya Usanda, wakiwemo wa vitongoji, afisa maendeleo, mtendaji, mratibu elimu pamoja na viongozi wa kidini, kimila, na waelimishaji rika, wakiwa kwenye kikao cha Shirika la Agape cha kuhitimisha mradi wao wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwenye kaya hiyo. Picha zote naa Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

WAKULIMA WENGI HAPA NCHINI HAWANA TAALUMA YA UNYUNYUZIAJI WA VIUATILIFU-TPRI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha.

Imebainika kuwa wakulima wengi hapa nchini hawana taaluma ya kutosha ya kanuni za teknolojia ya unyunyiziaji wa viuatilifu hali inayopelekea viuatilifu hivyo kutofanya Kazi jinsi inavyotakiwa ,kitu kinachofanya wakulima hao kulalamikia viuatilifu hivyo nivibofu na havifanyi kazi 

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa kitengo cha unyunyuziaji wa viuatilifu vya kuulia wadudu kutoka TPRI Julius Mkenda wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya nane nane vilivyopo Themi njiro jijini hapa, ambayo kwa mikoa ya Kanda ya kaskazini yanafanyika mkoani hapa.

Alibainisha kuwa wamepokea malalamiko mengi kutoka kwa wakulima kuwa viuatilifu hivyo vya kuulia wadudu havifanyi Kazi na walipofanya uchunguzi waligundua kuwa tatizo halipo katika viatilifu Bali tatizo lipo kwa wakulima kwani hawana Elimu ya kutosha ya namna yakunyunyuzia viuatilifu hivyo.

"Tumepata malalamiko sehemu nyingi ikiwemo kwenye Korosho ,Pamba ,mbogamboga na maeneo mengine mengi ambayo tumekuwa tukiusika na wakulima na katika Utafiti tuliofanya na ufatiliaji tulioufanya tuligundua kuwa tatizo kubwa la wakulima ni kutonyunyiza viuatilifu kwanamna ambayo inavyotakiwa " alisema Mkenda

Alibainisha kuwa kutokana na kugundua tatizo hilo wao kama TPRI wameamua kuzunguka nchi nzima na kutoka mafunzo kwa wataalamu wa Kilimo ,maafisa Kilimo,wafanyabiadhara wa viuatilifu na wasambazaji wa viuatilifu pamoja na wakulima na pia wamewajengea uwezo wa ufahamu wa kanuni sahihi za unyunyuziaji wa viuatilifu ,pamoja na kuwafundisha kanuni na ufahamu wa uelewa wa matumizi sahihi ya vinyunyizi vinavyotumika katika kunyunyiza viuatilifu .

"Kuna vivyunyizi na vinyunyizo kwa hivyo wakulima wengi hawajui matumizi vinyunyizi yaani vile vitundu na tumekuwa tukiwafundisha kwasababu ,kinyunyunyizo hiki ndicho kinachotengeneza aina ya matone yanayo muangamiza kisumbufu yaani mdudu na kila mdudu ana aina ya matone yanayo muangamiza ,na tunatoa hii taaluma ili kuweza kuhakikisha wakulima wanafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu visumbufu" alibainisha Mkenda 

Kwa upande wake mtafiti mwandamizi wa visumbufu na viuatilifu Maneno Chidege alisema kuwa kwa sasa hivi kuna aina tatu ya vishambulizi ambayo vinasumbua sana wakulima ,kimoja wapo ya vishambulizi na visumbufu hicho ni viwavijeshi vya maize ambayo viliingia hapa nchini mwaka 2017 na huyu mdudu akuwepo hapa nchini naali sema mdudu huyu amevamia nchi huyu ni mdudu vamizi ,pia kuna mungine anaitwa kantangaze huyu akiwa anashambulia nyanya sana wote hawa wameingia hapa nchini kwani awali hawakuwepo ,na hadi sasa wamefanya Utafiti na wamegundua dawa , namna ya kuwathibiti wadudu hawa ambapo alibainisha kuwa njia pekee ya kuwaangamiza wadudu hawa ni pamoja na kuzingatia kanuni za mafunzo wanazopewa,pamoja na kuachana na tabia ya mazoea pia watumie taaluma mpya wanayopewa kwani watapata mafanikio

Aidha aliwataka wakulima kutopiga dawa holela bila kupata ushauri wa bwana shamba au wao wenyewe watafiti maana wanapopiga dawa holela kwanza wanamtengenezea mdudu usugu ,pili watakuwa wanamaliza fedha zao bure bila kupata mafanikio wala manufaa yoyote, pia inaweza isishambulie,pia utakuwa umeumiza mazingira ya kwenye udongo maana kila mdudu ana sumu ambayo inamzibiti.
Mkuu wa kitengo cha unyunyuziaji wa viuatilifu vya kuulia wadudu kutoka TPRI Julius Mkenda akitoa maelekezo kwa wakulima waliotembelea banda LA TPRI hawapo pichani kupata Elimu. 
Mtafiti mwandamizi wa visumbufu na viuatilifu Maneno Chidege akielezea aina za wadudu wanaosumbua wakulima 
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images