Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

PWANI YAANZA KUFANYIA KAZI MAAGIZO YA MKONGEA ",ALIYOYATOA KATIKA MIRADI ILIYOKUTWA NA DOSARI-NDIKILO

0
0
MWAMVUA MWINYI ,PWANI

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemkabidhi mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stephen Kebwe ambapo katika mkoa wa Pwani miradi minne iliingia dosari kwa kukataliwa kati ya miradi 95 yenye thamani ya sh.bilioni 40.436.

Kati ya miradi iliyokataliwa ni pamoja hospital ya wilaya ya Mafia ambayo ilitolewa kiasi cha sh.mil403.600 na ujenzi wa barabara ya KN52 Kilimahewa huko Mafia yenye thamani ya mil.22.336 ambayo kalavati na barabara haina ubora na uendelevu wa mradi wa maji huko Bweni .

Mradi mwingine ni wa maji Bokomnemela,Kibaha Vijijini, baada ya kubaini taratibu za ujenzi kukiukwa katika zege la juu lililotengewa kiasi cha sh.milioni 1.5.

Akitoa taarifa hiyo ,wakati akikabidhi mwenge huo Mkoani Morogoro agost 2 mwaka huu, eneo la mpakani mwa mikoa hiyo Bwawani , Ndikilo alisema wilaya ya Mafia,Kibaha na mkoa kijumla umepokea maelekezo na wanayafanyia kazi.Alifafanua tayari wamechukua hatua ya kuunda timu ya kufuatilia jambo hilo na ripoti itakabidhiwa kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).

"Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Pwani Julai 24 na kukimbizwa kwenye wilaya saba ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 imepitiwa yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 40.436.6:', Kati ya miradi hiyo miradi 61 imekaguliwa,17 ilipaswa kuwekwa jiwe la msingi,9 kuzinduliwa na 8 kufunguliwa "alieleza Ndikilo.

Ndikilo alisema ,miradi hiyo ni mizuri lakini imejitokeza dosari ndogo ambayo wanaichukulia ni funzo na taratibu zinafanyika ili kutimiza maagizo waliyotakiwa kuyatekeleza ."Nakupongeza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na timu yako, kwa kuwa makini kufuatilia thamani ya miradi na taarifa zake"" alisema Ndikilo.

Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea alitaka maelekezo aliyotoa yafanyiwe kazi.Pia ,Mkongea aliupongeza mkoa huo kwa ushirikiano biana ya chama na serikali pamoja na viongozi wote kuwa na ushirikiano na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi na baadhi ya halmashauri kuinua mapato yake.

Licha ya mwenge wa uhuru kukataa baadhi ya miradi pia kiongozi huyo wa mbio za mwenge alinusa ubadhilifu wa fedha, katika mradi wa maji Ikwiriri huko Rufiji ambao umejengwa na mamlaka ya maji safi Dar es salaam DAWASA kwa zaidi ya sh.bilioni 2.055.6.

WAZEE TUNDURU WAOMBA HUDUMA ZA UCHUNGUZI KARIBU NA MAKAZI YAO

0
0

Na Ripota wetu,Tunduru

BAADHI ya wazee wa Kijiji cha Amani kata ya Namasakata Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,wameiomba Serikali kuongeza kasi  kampeni ya uchunguzi wa  ugonjwa wa kifua kikuu  ambao umekuwa  tishio na kusababisha vifo vya watu wengi  hususani  wazee waishio vijijini.

Wakizungumza jana wakati wa kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa wakazi wa kijiji hicho, wazee hao wameomba wataalam wa Afya waendelee  na kampeni  ya kijiji hadi kijiji  kwani itasaidia kuibua watu wengi ambao wanashindwa kwenda Hospitali ya wilaya umbali wa km 20 kwa ajili ya vipimo pamoja  na tiba ya ugonjwa huo.

Hamis Rashid(65) na Ahamd  Majikita(70)  licha ya kuipongeza  Hospitali ya wilaya kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma  kuanzisha kampeni ya uchunguzi wa kifua kikuu kwa watoto na watu wazima.

Hata hivyo  walidai,  kuna haja ya wataalam hao kwenda katika maeneo yote hasa vijijini ambako kuna idadi kubwa ya watu wenye viashiria vya ugonjwa wa kifua kikuu lakini hawajapata vipimo wala tiba na wanaendelea kuteseka.

Ahmad Majikita alisema, tatizo linalochangia kukithiri kwa magonjwa  maeneo ya vijijini  ni hali duni ya kipato, kutokana na kukosa fedha za nauli, gharama za chakula na maradhi pindi wanapohitajika kwenda Hospitali ya wilaya Tunduru au katika vituo vya Afya kwa ajili ya kupata matibabu.

Alisema,kwa hiyo kama wataalam watafika kila kijiji  itasaidia wazee wengi kutambua hali ya Afya zao na kupata matibabu.

Alisema, maeneo ya vijijini wazee wengi wanapoteza maisha kwa kukosa vipimo na tiba sahihi kwani licha ya kuwepo kwa zahanati lakini tatizo  ni vifaa tiba kwa ajili ya vipimo, wataalam  na  baadhi ya dawa  ambazo zinapatakana katika hospitali ya wilaya Tunduru mjini na  katika vituo  vikubwa  vya Afya.

Kwa upande wake mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,serikali kupitia kitengo cha kifua kikuu katika Hospitali ya wilaya imeanza kuchukua hatua kwa kutembelea  vijijini kwa ajili ya kufanya  uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu sambamba na kuwaanzishia dawa wale watakabainika kuwa na vimelea vya maradhi hayo.

Kwa mujibu wa Kihongole,Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau wengine  kama shirika la MDH katika kutokomeza ugonjwa  huo ambao unatajwa ni miongoni mwa  ugonjwa hatari unaoongoza kuuwa watu wengi Ulimwenguni.

Alisema, ugonjwa wa kifua kikuu unatibika kwa mtu  kupata tiba sahihi, na makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni pamoja  na wazee,watoto walio chini ya miaka mitano na watu wanaoishi kwenye mazingira yenye mwanga hafifu na hata hewa  mzito.

Kihongole alitaja kundi lingine ni watumiaji dawa za Hospitali kwa muda mrefu bila kufuata ushauri wa  kitaalam na wale wenye magonjwa sugu na utapia mlo kwa watoto wadogo.

Dkt Kihongole ameshauri wananchi kwenda kufanyiwa vipimo vya afya zao mara kwa mara badala ya kukimbilia kununua dawa na kumeza au kusubiri hadi pale hali inapokuwa mbaya kwani ni hatari kwa usalama wao.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Amani kata ya Namasakata Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,wakimsikiliza mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wa Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole(hayupo pichani)wakati wa  zoezi la uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa wakazi wa kijiji hicho,hata hivyo wazee hao wameiomba Serikali kukiongezea nguvu kitengo cha kkifua kikuu na Ukoma ili wataalam wake waweze kufika maeneo mengi kwa ajili ya uchunguzi wa ugonjwa huo.

MSIMU WA MAONESHO YA NANENANE 2019, PSSSF YAAHIDI KUTOA HUDUMA BORA NA ZENYE VIWANGO

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeahidi kutoa huduma bora na za uhakika wakati wa msimu huu wa maonesho ya Nanenane mwaka huu wa 2019 yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu na kwenye Kanda tatu za Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Mashariki.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bi. Rehema Mkamba ameyasema hayo leo Agosti 2, 2019 kwenye viwanja vya Nyakabidni nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
“Tunawahamisha sana wananchi na wanachama wetu kutembelea kwenye mabanda yetu katika maonesho haya yanayofanyika kitaifa hapa Nyakabindi, lakini pia Kikanda, na tuna Kanda ya Kaskazini maonesho yanafanyika jijini Arusha, Kanda ya Mashariki, mkoani Morogoro na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini maonesho yanafanyika jijini Mbeya.” Alifafanua Bi. Mkamba.
“Tunaamini kuwa maonesho ya nanenae hapa Nyakabindi na kwenye Kanda nilizotaja ni jukwaa zuri kwa Mfuko wa PSSSF ambao unahudumia watumishi wa Umma kukutana na wanachama wetu ambao taasisi nyingi za Umma zinashiriki katika maonesho hayo, hivyo nitoe wito kila wapatapo nafasi wapitie kwenye banda letu ili tuwahudumie kama ambavyo wangehudumiwa kwenye ofisi zetu zilizoenea kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.” Alisisitiza.
Katika mabanda yetu tunatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa za Pensheni ya Uzeeni, taarifa za Mafao ya kukosa Ajira, taarifa za Mafao ya Uzazi, taarifa za Dhamana ya Mikopo ya Nyumba, taarifa za Uwekezaji lakini pia wastaafu watapata fursa ya kuhakiki taarifa zao zoezi ambalo ni endelevu.” Alifafanua Bi. Mkamba.
Alisema PSSSF ni Mfuko ulioanzishwa mwaka mmoja uliopita baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF.
Mwananchi huyu (watatu kulia), akipatiwa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) alipotembelea banda namba 37 la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw.Mawazo Ngeraniza (kulia), akitoa elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa wanachama wa PSSSF waliotembeela banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama wa Mfuko alipotembelea banda la Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba akimfafanualia jambo mwanachama aliyefika kuhudumiwa.
Timu ya PSSSF iliyoweka kambi kwenye banda namba 37 la Mfuko huo mkabala na BoT kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimweleza mwananchi huyu (kushoto)kuhusu masuala ya hifadhi ya Jamii, alipotembeela banda la Mfuko kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Katikati ni Afisa Matekeelzo PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Mohammed Nyengi.
Afisa Matekelezo PSSSF Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Muhoni (kulia), akitayarisha taarifa za michango za Mwnaachama huyu kushoto, aliyetembeela banda la PSSSF viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimkabidhi mfuko wenye taarifa mbalimbali za PSSSF, mwanachama huyu aliyefika kujua taarifa za michango yake.
Mmoja wa wanachama waliotembela banda la PSSSF akiangalia taarifa za michango yake.
Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi.Linda Balati (kulia), akimfafanualia mwanachama huyu kuhusu hali ya michango yake.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Rehema Mkamba (katikati), akishirikiana na Afsia Matekelezo wa Mfuko huo, Bw. Charles Muhoni wakati akiandaa taarifa za michango za mwanachama wa Mfuko aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua hali ya michango yake.

NMC ARUSHA YAJA NA UNGA WA DONA BORA

0
0
Afisa mdhibiti ubora wa kiwanda cha NMC Ramadhan Dendegu akionyesha mfumo utakaotumika kiwandani hapo kuhakikisha ubora wa bidhaa itakayokuwa ikizalishwa kiwandani hapo.
Meneja wa kiwanda cha NMC Arusha, Kulwa Rwegasira akielezea ujio wa kiwanda kipya cha NMC kwa lengo la kuwanyanyua wakulima kwa kununua bidhaa zao pamoja na kuzalisha bidhaa bora kwa walaji.
Afisa udhibiti ubora uzalishaji wa kiwanda cha NMC akielezea waandishi wa habari ubora wa mashine za kiwanda hicho katika kudhibiti ubora wa bidhaa zitakazoanza kuzalishwa hivi karibuni. 



Na Seif Mangwangi, Michuzi blog, Arusha 

WAKULIMA wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wanatarajiwa kuondokana na adha ya masoko ya kuuzia mazao yao hususani mahindi na ngano kufuatia kiwanda cha NMC kilichopo jijini hapa kuanza uzalishaji hivi karibuni. 

Akizungumza kiwandani hapo leo, Meneja Mwendeshaji wa kiwanda hicho, Kulwa Rwegasira amesema NMC ambayo zamani ilijulikana kama ‘Monaban’ inatarajia kuanza kununua mazao ya wakulima wa kanda ya Kaskazini na kuzalisha bidhaa mpya ya unga wa dona utakaojulikana kwa jina la ‘Dona bora’.

Kiwanda hicho cha NMC kilichokuwa kikiendeshwa na mwekezaji, hivi sasa kinaendeshwa na Serikali kupitia bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko baada ya Serikali kukichukua kwa kile kinachodaiwa mwekezaji kushindwa kulipa kodi ya pango.

Rwegasira anasema kiwanda hicho kitakuwa kikizalisha aina hizo za unga kwa kutumia vigezo vya ubora wa kimataifa kwa kuwa mbali ya kusambazwa nchini pia utasambazwa kimataifa ikiwemo nchini Kenya. 

Anasema pia kiwanda hicho kiko kwenye matengenezo mbalimbali katika baadhi ya mashine zake ili kiweze kuzalisha unga wa ngano kwaajili ya kutengenezea bidhaa tofauti hususani vitafunwa. 

“Mbali ya kuzalisha dona bora pia tutaanza kuzalisha unga wa ngano ambao na wenyewe utakuwa unga bora tofauti na unga mwingine, lengo letu ni kuhakikisha mwananchi anapata bidhaa yenye ubora wa hali ya juu,”anasema.

Rwegasira anasema NMC pia inatoa huduma za mizani, kusafisha mazao ya wafanyabiashara na wakulima kwa bei nafuu, kukausha mahindi yanayokosa soko kutokana na kuwa na unyevunyevu, pamoja na kukodishia wafanyabiashara maghala ya kuhifadhia mazao.

Kwa upande wao maafisa udhibiti ubora kiwandani hapo Abdallah Dengedu na Jonathan Lunyemela wanasema wamejipanga kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na na bei nafuu ili kuleta tofauti katika soko.

ZANZIBAR WAENDELEA KUFAIDI MBEGU YA MPUNGA AINA YA SUPA C ILIYOBORESHWA KWA MIONZI

0
0
Wananchi wa Tanzania upande wa Zanzibar wameendelea kufaidika na mchele unaotokana na mbegu ya mpunga aina ya SUPA BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia Mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha bengu hizo . 

Mradi huo ulifadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) na kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) ili kuhakikisha mbegu hiyo inaboreshwa na kuwa yenye ubora wa hali ya juu. 

Akizungumza katika maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Nyakabindi, Wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu, Mtafiti Msaidizi wa mazao ya kilimo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar Bwana Hamza Hamid Hamza amesema kuwa mbegu hiyo ina ubora na huzalisha mpunga kwa wingi na kwa sasa ni chaguo la wakulima na wananchi wengi Kisiwani Zanzibar. 

Amesema mbegu aina ya SUPA BC, ina uwezo wa kuzalisha mpunga hadi kufikia tani 7 kwa hekta moja ambapo huchukua muda wa siku 130 mpaka kuvunwa kwake hali ambayo kwa sasa imewahamasisha wakulima wengi kulima aina hiyo ya mpunga visiwani humo. 

“Mchele unaotokana na mpunga wa mbegu ya SUPA BC ni mzuri, wenye harufu nzuri na wenye ladha tamu kwa walaji na wakulima wengi wanashawishika kupanda mbegu hiyo kwa wingi” alisema Hamza Hamid. 

Kwa mujibu wa Hamza amesema kuwa mpunga huo una sifa nyingi ikiwemo urahisi katika kufikicha tofauti na mbegu nyingine nyingi za mpunga zilizozoeleka na kuwa mmea wake una urefu wa wastani na usioweza kuanguka baada ya kubeba mpunga ukiwa shambani hivyo hupelekea kubaki na mazao yote hadi wakati wa kuvuna pamoja na uwezo wa kutoa machipukizi mengi wakati wa ukuaji wake. 

Mbegu hiyo ilizinduliwa rasmi na Wizara ya Kilimo na Mifugo ya Zanzibar mwaka 2011 ambapo mpaka sasa inaendelea kulimwa kwa wingi visiwani humo. 

Mtaalamu huyo amesema kuwa teknolojia hii ya nyuklia kwa kutumia mionzi ya Gamma ikiendelea kutumika inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo hasa katika kutafiti wa mbegu mbali mbali za mazao hapa nchini. 

Bw. Hamza pia ameshauri kwamba kwa sasa kutokana na mbegu hiyo ya mpunga kutumika visiwani Zanzibar pekee , ni wakati muafaka sasa mbegu hiyo ikaanza pia kutumika pia katika eneo la Tanzania Bara. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Bi Zainab Terak akiwa ameshika mpunga uliotokana na mbegu ya aina ya Supa BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha mbegu hizo mradi ulioofadhiliwa na Shirika la nguvu za Atomiki la kimatifa (IAEA) kwa kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zanzibar (ZARI) .

MASAUNI APOKEA MSAADA WA VYEREHANI TISINI NA NNE KWA AJILI YA VIJANA VISIWANI ZANZIBAR

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea vyerehani kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (wapili kushoto), vilivyotolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza kuzitumia katika kujiinua kiuchumi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi mmoja wa wananchi cherehani zilizotolea na Taasisi ya Islamic Foundation,kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo , Arif Nahdi,vyerehani hivyo vimetolewa kwa ajili wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi
Wananchi Visiwani Zanzibar waliogawiwa vyerehani na Taasisi ya Islamic Foundation wakiwa wamesimama mbele yake baada ya kuruhusiwa kuchukua.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza baada ya kupokea vyerehani tisini na nne kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (aliyekaa kulia), vilivyotolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza kuzitumia katika kujiinua kiuchumi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
……………………………

Serikali kuzilinda Taasisi za Kidini

Serikali imesema itaendelea kuziunga mkono taasisi za kidini nchini ili ziweze kuleta maendeleo na kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni mdau muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kupokea msaada wa vyerehani Tisini na Nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne vilivyotolewa kwa taasisi ya TAYI inayojishughulisha na kuwaokoa vijana kutoka katika tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.

“Serikali tumekua tukipokea misaada mbalimbali kutoka katika taasisi za kidini nchini,wamekua wakisaidia visima vya maji,mashule na kubwa zaidi wanafundisha maadili ili taifa letu liwe na watu makini wanaoweza kuliletea maendeleo siku za usoni,kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani tunaahidi kuzilinda taasisi hizi ili ziweze kufanya shughuli zake bila kubughudhiwa” alisema Masauni.

Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa msaada huo wa vyerehani, Aref Nahdi amewaomba wananchi waliopokea mssada huo kwenda kuzitumia katika shughuli za ujasirimali akiamini watapata kipato zaidi endapo watazitumia vizuri.

“Nawaomba mkazitumie vizuri ili ziweze kuwaongezea kitu kwenye vipato vyenu,natoa wito msiende kuviuza kwani lengo lake ni kuwawezesha muwe na shughuli itakayowaingizia kipato na sisi kama taasisi tunaahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa wale wanafunzi ishirini wa kwanza watakaotaka kujifunza ushonaji ili waweze kuzitumia vizuri” alisema Nahdi
.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopokea misaada hiyo ya vyerehani wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa vyerehani hivyo huku waiwaomba wasichoke kuwasaidia mara kwa mara ili vijana wengi wawe na shughuli za kuzalisha kipato.

ZANZIBAR WAENDELEA KUFAIDI MBEGU YA MPUNGA AINA YA SUPA BC ILIYOBORESHWA KWA MIONZI

0
0
Wananchi wa Tanzania upande wa Zanzibar wameendelea kufaidika na mchele unaotokana na mbegu ya mpunga aina ya SUPA BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia Mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha bengu hizo . 

Mradi huo ulifadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) na kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) ili kuhakikisha mbegu hiyo inaboreshwa na kuwa yenye ubora wa hali ya juu. 

Akizungumza katika maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Nyakabindi, Wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu, Mtafiti Msaidizi wa mazao ya kilimo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar Bwana Hamza Hamid Hamza amesema kuwa mbegu hiyo ina ubora na huzalisha mpunga kwa wingi na kwa sasa ni chaguo la wakulima na wananchi wengi Kisiwani Zanzibar. 

Amesema mbegu aina ya SUPA BC, ina uwezo wa kuzalisha mpunga hadi kufikia tani 7 kwa hekta moja ambapo huchukua muda wa siku 130 mpaka kuvunwa kwake hali ambayo kwa sasa imewahamasisha wakulima wengi kulima aina hiyo ya mpunga visiwani humo. 

“Mchele unaotokana na mpunga wa mbegu ya SUPA BC ni mzuri, wenye harufu nzuri na wenye ladha tamu kwa walaji na wakulima wengi wanashawishika kupanda mbegu hiyo kwa wingi” alisema Hamza Hamid. 

Kwa mujibu wa Hamza amesema kuwa mpunga huo una sifa nyingi ikiwemo urahisi katika kufikicha tofauti na mbegu nyingine nyingi za mpunga zilizozoeleka na kuwa mmea wake una urefu wa wastani na usioweza kuanguka baada ya kubeba mpunga ukiwa shambani hivyo hupelekea kubaki na mazao yote hadi wakati wa kuvuna pamoja na uwezo wa kutoa machipukizi mengi wakati wa ukuaji wake. 

Mbegu hiyo ilizinduliwa rasmi na Wizara ya Kilimo na Mifugo ya Zanzibar mwaka 2011 ambapo mpaka sasa inaendelea kulimwa kwa wingi visiwani humo. 

Mtaalamu huyo amesema kuwa teknolojia hii ya nyuklia kwa kutumia mionzi ya Gamma ikiendelea kutumika inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo hasa katika kutafiti wa mbegu mbali mbali za mazao hapa nchini. 

Bw. Hamza pia ameshauri kwamba kwa sasa kutokana na mbegu hiyo ya mpunga kutumika visiwani Zanzibar pekee , ni wakati muafaka sasa mbegu hiyo ikaanza pia kutumika pia katika eneo la Tanzania Bara. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Bi Zainab Terak akiwa ameshika mpunga uliotokana na mbegu ya aina ya Supa BC iliyoboreshwa kwa Teknolojia ya Nyuklia kwa kutumia mionzi aina ya gamma iliyotumika kununurisha mbegu hizo mradi ulioofadhiliwa na Shirika la nguvu za Atomiki la kimatifa (IAEA) kwa kuratibiwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo (SUA) na Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zanzibar (ZARI) .


WAZIRI MWAKYEMBE AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUWEKA DARAJA NA SERIKALI

0
0
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe wakati akifungua semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
……………………………………………
Serikali imewataka wamiliki wa vyombo vya habari kujenga daraja baina yao na serikali na kuacha kushirikiana na balozi za nje au taasisi za nje katika kujadili maslahi ya nchi


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es salaam, kwenye semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Mwakyembe amesema vyombo vya habari visiwe na hofu ya kushirikiana na serikali kwani wanapaswa kuweka daraja kati yao na kuachana na kuwa karibu na balozi au taasisi za nje.Alisema wanatakiwa kutambua kuwa jambo lolote likifanyika nchini mtu wa kwanza awe serikali na siyo balozi za nje au taasisi za kimataifa.

“Tuwe na uzalendo kwenye, nchi yetu kwani jata nchi za nje hazitanngazi mambo mabaya ya kwao lakini wenyewe wanashinikiza kutangaza yetu,” alisema Mwakyembe.Alisema hata gazeti likifungiwa au kupewa adhabu, wamiliki wanapaswa kuonana na waziri husika kwanza kuliko kukimbia kwa mabalozi au taasisi za nje.

Hata hivyo alisema hivi sasa hawezi kuzungumza na balozi yeyote wa nje ya nchi bila kuita waandishi wa habari wa hapa nchini.“Sidhani kama kutakuwa na jambo la siri ambalo watakuwa wanataka lisisikike na kuhitaji kuonana na mimi bila waandishi wa habari hivyo kuanzia sasa nitakukuwa nafanya hivyo,” alisema Mwakyembe.

Mmoja kati ya waandaaji wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Mac D, Deogratius Rweyunga alisema wanaendelea kufanya semina kama hizo ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari.“Tulikuwa tunawajengea uwezo zaidi waandishi wa habari za michezo pekee lakini sasa tunafanya pia mafunzo kama haya na waandishi wa habari zote kwa mikoa mbalimbali,” alisema Rweyunga.

Akielezea mada katika mafunzo hayo mwezeshaji Allan Lawa alisema waandishi wanapaswa kuandika suluhu ya matatizo ya jamii na kubadilika na kuachana na kuandika matukio pekee.“Tunapaswa kuzama kiundani kwa kuandika suluhu ya matatizo ili ajali, maradhi na mambo mengine na siyo kuandika tuu ajali inatokea sehemu kila mara au ugonjwa wa dengua unaua watu mikoa ya Dar es salaam na Tanga,” alisema Lawa.

Mmoja kati ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo, Joseph Lyimo kutoka kampuni ya Mwananchi, mkoani Manyara alisema amejengewa uwezo zaidi wa kuandika habari za changamoto na haki za binadamu.“Nimejifunza mambo mengi mno hasa nafasi na wajibu wa uandishi wa habari za haki za binadamu na suluhisho la matatizi ya jamii kupitia uandishi wa habari na siyo kuandika matukio pekee,” alisema Lyimo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe akisoma baadhi ya vifungu vya sheria ya Habari vilivyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakati akifungua semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC akizungumza kuhusu semina ya waandishi wa habari iliyowashirikisha waandiishi 59 wa mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Mkurugenzi wa kampuni ya MAC D ambayo ndiyo imeandaa semina hiyo kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bw. Deo Lweyunga akimshukuru Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wakati akuzungumza katika semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Mwezeshaji wa semina hiyo Allan Lawa akiwasilisha mada katika semina hiyo.
Felista Mauya Mkurugenzi Ujengaji Uwezo wa Uwajibikaji akiwasilisha mada ya haki za binadamu katika semina hiyo.
Picha zikionesha washiriki mbalimbali kutoka vyombo vya habari waliohudhuria katika semina hiyo.

NMB Kuwawezesha wakulima kisasa, Yadhamini Maonesho Ya Kitaifa Ya Nanenane Kwa Milioni 30

0
0

BENKI ya NMB imesema kuwa itahakikisha inaendeleza jitihada zake kwa wakulima za kuwawezesha kadri wanavyohitaji kulingana na mazao yao ili kuifanya sekta ya kilimo nchini kubeba uchumi wa nchi.

Mbali na hilo benki hiyo imesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikitangaza sekta ya wakulima na kuwasaidia wakulima kama ajenda yake kuu, kutokana na asilimia kubwa ya watanzania kutegemea sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse wakati akikabidhi kiasi cha sh. Milioni 30 na tisheti 300 kwa katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini kama udhamini wa benki hiyo kwenye maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) kitaifa yanayofanyikia Mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magese. Fedha hizo zitatumika kwenye maonesho ya NaneNane ya kitaifa. NMB ni wadhamini wa Maonyesho hayo ya kitaifa yanayolenga kutoa fursa kwa wakulima na Wafugaji



Magesse alisema kuwa benki hiyo imekuwa haifanyi kazi ya kutunza fedha za wateja wake tu, bali hata kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali za Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya na Biashara.

Alisema kuwa katika maonesho hayo benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inatoa elimu kwa wakulima, wafugaji, jinsi ya kulima kisasa na kitaalamu ikiwa pamoja na kuwaeleza jinsi gani benki hiyo inaweza kushiriki kwenye kilimo kwa kuwapatia mikopo.

“Kwenye maonesho ya mwaka huu ambayo yatakuwa bora zaidi, ushiriki wetu kama benki utakuwa mkubwa zaidi, na umelenga kuwasaida wakulima, tutakuwa na bidhaa za wafugaji wa ng’ombe, na wakulima wa mazao ya pamba, tumbaku na kahawa lakini hata Matrekta tutakuwa nayo,” alisema Magesse.

Aliwataka wakulima kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo hasa kwenye banda la NMB ili waweze kupata elimu itakayowafanya walime kisasa kwa kutumia teknoloJia na kuzalisha kwa tija.

Akiongea mara baada ya kupokea mchango huo Katibu Tawala huyo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake, ambapo alisema utawezesha kuboresha zaidi eneo la Nyakabindi ambako sherehe hizo zinafanyikia.

Sagini ameeleza kuwa Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia mambo mbalimbali katika mkoa wa Simiyu ikiwemo Elimu na Afya, huku akibainisha kuwa mchango huo utawezesha maonesho hayo kuwa bora zaidi.

“Kwa mchango huu NMB watakuwa kwenye wachangiaji wale wa pili kwa ukubwa, tunawashukuru sana kwa mchango wao na tuombe mahusiano yetu na wao yaendelee kuwa mazuri zaidi ya hapa,” alisema Sagini.


Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama bidhaa za mfanyabiashara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye Banda la NMB wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Machunda na Mkuu wa Idara wa Biashara kwa Serikali NMB Vicky Bishubo
Wananchi wakipata huduma mbalimbali kwenye banda la NMB, wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu walipotembelea banda hilo. NMB ni mmoja ya wadhamini wakuu wa maonesho hayo .

MUHUMBILI YAWAHAKIKISHIA WANANCHI KUENDELEA KUPATA HUDUMA KWA GHARAMA NAFUU

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imeendelea kuleta kuwahakikishi wananchi kupata huduma kwa garama nafuu ambapo sasa imeweza kuokoa kiasi cha shilingi 3.5 bilioni toka kuanza kutolewa kwa huduma ya upandikizaji wa figo Novemba 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Agosti 2,2019 Daktari bingwa na mkuu wa idara kitengo cha figo Dkt.Jackline Shoo amesema toka walipoanza kutoa huduma hiyo yabkupandikiza fiho, ayari wagonjwa 47 wamepatiwa huduma hiyo ambayo imegarimu kiasi cha shilingi 1.1 bilioni.

Amesema, kama wagonjwa wote 47 wangepelekwa nje ya nchi basi kwa mgonjwa mmoja ingegharimu takribani shilingi milioni 80 hadi 100 na kufanya jumla yake kuwa shilingi bilioni 4.7 kwa wagonjwa wote. Lakini kwa huduma hiyo zaidi ya asilmia 25 hadi 32 ya fedha inaokolewa.

Aidha Dkt. Shoo amesema, wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi wa figo lakini wengi wao hufika hospitalini hapo wakiwa wameshafikia hatua za mwisho kwani, kwa sasa tuna wagonjwa zaidi ya 300 ambao wanapatiwa huduma ya kusafishwa damu na karibu nusu yao wanahitaji huduma ya kupandikizwa figo.

"Hii ni mara ya kumi toka tulipoanza rasmi Novemba 2017 kutoa huduma hii, na kwa hatua ya leo wagonjwa wanne ambao wamepandikizwa figo akiwemo mtoto wa miaka tisa wanaruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea na maisha yao ya kawaida Ila wanapaswa kuzingatia kutumia dawa kwani wagonjwa wote wanaopandikizwa na wale wanaotoa figo watatakiwa kuishi kwa masharti na kutumia dawa katika maisha yao yote", amesema Dkt Shoo.

Aidha Dkt Shoo alisema kuhusiana na garama za matibabu, wale wanaotumia bima zinalipia,lakini walioko kwenye msamaha wanapewa msamaha na ambao hawana uwezo kabisa hospital inagaramia

Kwa upande wake, Daktari bingwa wa figo Onesmo Kissanga amesema kila mwezi wamekuwa wakipokea wagonjwa takribani 20 wanaohitaji huduma maalum ikiwemo upandikizaji wa figo na kila wiki watoto 15 wamekuwa wakipokelewa wakiwemo watatu wanaotakiwa kupandikizwa figo au huduma maalum ya kusafishwa damu.

Alisema sababu ya kupokea idadi hiyo ya wagonjwa ni kutokana na changamoto ya elimu katika jamii kuhusiana na ugonjwa huo.Akizunguma kuhusu mtu anayepaswa kuchangia figo dkt Kissanga amesema anaetakiwa kufanya hivyo ni umchangia ndugu wa damu baada ya kufanyiwa vipimo na kuonekana kuwa vinafaa.

Naye, Mary Michael anayeishi Tanga ambae amemtolea figo mwanae Othniel Kimaro amesema ameamua kumtolea figo mwanae kufuatia hali yake ilikuwa siyo nzuri na kwamba alikuwa akipitia changamoto mbali mbali, lakini aliposhauriana na madaktari niliamua kumtolea mtoto wangu figo.

"Nililazwa hapa toka Alhamisi mtoto wangu akiwa na hali mbaya sana lakini baada ya kufanyiwa upandikizaji jumapili hivi sasa hana shida tena, mimi na mwanangu wote tunaendelea vizuri" ameongeza.

Mama huyo amewataka Watanzania kutoogopa kuchangia figo kwa ndugu zao wenye matatizo ya figo kwani kufanya hivyo wataokoa maisha ya ndugu zao kwani haina maadhara yoyote kwa kuwa huduma zinazotolewa hospitali hapo ni nzuri.Gasper Mbeka ambaye pia amepatiwa huduma hiyo, ameishauri serikali kuangalia namna ya kuweka utaratibu kwa ndugu wanofika kwa ajili ya kuwatolea ndugu zao figo kupatiwa husuma hiyo katika sehemu moja badala ya kuambiwa nenda Ocean road mara Agakhan kitendo kinachowafanya kushindwa kuwa wavumilivu na hats kifikia kuondoka.

Wagonjwa wengine waliofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa leo ni pamoja na Ramadhani Ongoa.
 Wataalam wa MNH wakiwa katika picha ya pamoja na wagonjwa waliopandikizwa figo na baadhi ya wachangiaji.
 Wagonjwa waliopandikizwa figo wakiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Shoo kabla ya kurejea nyumbani leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Jacqueline Shoo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya upandikizaji figo ambayo ilianza Novemba, 2017.
Mkazi wa Tanga, Merry Michael akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu afya ya mtoto wake, Othniel Kimaro baada kupandikizwa figo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).  Mtoto huyo amechangiwa figo na mama yake, Bi. Merry Michael.

MFANYAKAZI KAMPUNI TIGO, WENZAKE WANNE KORTINI KWA MAKOSA SABA LIKIWEMO LA UTAKATISHAJI FEDHA

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MFANYAKAZI wa Kampuni ya Simu ya Tigo Babati Hamis Singa (30) na wenzake wanne wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka saba likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh.milioni 26.

Washitakiwa wengine ni Jailos Joseph(33), makazi wa Arusha, Singa Mananga (32) mkazi wa Babati, Japhet Mkumbo (33) mkazi wa Babati na Omary Abdalah (33) mkazi wa Arushà.

Hamis ambaye ni raia wa Burundi na wenzake hao walipandishwa kizimbani mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ally Salim na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon.

Akisoma mashitaka hayo, Wakiki Simon alidai kati ya Januari na Julai mwaka huu katika sehemu tofauti Mkoa wa Manyara na Babati, washitakiwa wote walikula njama ya kutenda kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa katika kipindi hicho na maeneo hayo, washitakiwa hao kwa ulaghai walijipatia Sh. 26, 432, 441 kupitia miamala ya wateja wa kampuni ya Vodacom na Airtel.

Siomon alidai katika kipindi hicho, washitakiwa hao walisambaza taarifa za uongo kupitia ujumbe wa maandisi usomekao 'tuma pesa kwa namba hii ' kwa lengo la kuudanganya umma wa Watanzania.

Katika shitaka lingine washitakiwa hao wanadaiwa kusambaza ujumbe ambao haujaombwa kupitia laini zao za simu za mkononi ambazo wamezisajiri kwa majina ya watu wengine. Pia wanadaiwa kusambaza ujumbe huo kwalengo la kujipatia fedha.

Mshitakiwa Hamisi pia anadaiwa akiwa mwajiriwa wa Tigo Babati, aliingilia taarifa za miamala ya fedha za mawakala wa Tigo kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Shitaka lingine, washitakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh. 26,432,441 wakati wakijua zilitokana na kosa la jinai ambalo ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwani Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi na imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapotajwa tena. Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilka.

TCRA YAENDELEA KUTOA ELIMU MAONESHO YA NANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

0
0
*Yahamasisha usajili laini za simu kwa alama za vidole

Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani Kanda ya Mashariki (TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Mashariki watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano pamoja uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.

Mhandisi Odiero amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.

Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba na kufanya watu wengine kuona muda uliopangwa ulikuwa hautoshi.

“Muda uliowekwa ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu hizo. 

Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalilbali za amawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akiwa katimu picha ya pamoja na timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Christopher John akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mwananchi akisaini kitabu wakati alipotembelea banda la TCRA kanda ya Mashariki katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Wananchi wakipata huduma katika banda la NIDA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Baadhi ya watoa huduma za Simu katika Banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.

KAILIMA ATOA AGIZO KWA JESHI LA POLISI,ATAKA JAMII IPEWE ELIMU YA DHAMANA

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Central (OCS), Kidwadi Karinga (Wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Watatu kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo Cha Kushughulikia Malalamiko, Rabikira Mushi wakiwa katika Kituo Kkuu (Central) kilichopo Wilaya ya Dodoma Mjini wakiwa kwenye ziara ya Kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Wa pili kulia), Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dodoma (RCO), Pipi Kayumba (Wa tatu kushoto), na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, Rabikira Mushi wakiwa katika kituo cha Polisi Nkuhungu kilichopo Wilaya ya Dodoma Mjini wakikagua kitabu cha taarifa za Polisi (RB) walipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani kailima, (Wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Central (OCS), Kidwadi Karinga (Wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamuhanga (Wa tatu kushoto), wakimsikiliza mwananchi aliyekuwa akisubiri huduma katika Kituo Kikuu cha Polisi, Wilaya ya Dodoma Mjini wakati viongozi wao walipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (Katikati), akitoa maelekezo kwa viongozi wa Polisi na watendaji wakuu wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko baada ya kukamilisha ziara ya kikazi Kituo cha Polisi Chang’ombe, Wilaya ya Dodoma Mjini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
…………………..

Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuboresha mazingira ya huduma wanazotoa kwa wananchi.

Alisema ni wajibu wa jeshi hilo kutoa elimu kwa jamii iweze kufahamu hatua za kufuata pindi wanapotaka kuwawekea dhamana ndugu zao waliopo katika vituo vya polisi.Kailima aliyasema hayo hayo jana alipofanya ziara ya kutembelea vituo vinne vya polisi mkoani Dodoma.

Lengo la ziara hiyo iliyoandaliwa na Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko Ndani ya Wizara hiyo ni kuangalia utendaji kazi wa jeshi hilo juu ya huduma wanazotoa kwa wananchi.Vituo alivyotembelea ni vile vilivyopo katika Wilaya ya Dodoma Mjini ambavyo ni Kituo Kikuu (Central), Chang’ombe, Nkuhungu na Kikosi cha Usalama Barabarani.

Katika ziara hiyo, Kailima aliambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamuhanga pamoja na Maafisa wengine wa kitengo hicho.

Akiwa kwenye kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kailima alikuta idadi kubwa ya watu waliokuwa na shida mbalimbali, alitumia fursa hiyo kuzungumza nao na kuwataka waeleze kero zao.Baada ya kuzungumza na wananchi, Kailima aliushauri uongozi wa kituo hicho kuweka mazingira mazuri ya kutoa huduma ili kuondoa mrundikano wa wananchi nje, ndani ya kituo.
“Wekeni mazingira mazuri ya mwananchi mmoja kuhudumiwa na askari mmoja kutokana na idadi ya askari ambao watakuwa zamu ili kupunguza msongamano,” alishauri.

Aliongeza kuwa; “Toeni elimu inayohusu dhamana kwa jamii ili wananchi wajipange kabla ya kuja kituoni, unakuta watu wengi wanakuja kuwawekea dhamana ndugu zao bila kujua taratibu hivyo kusababisha wajazane kituoni bila sababu,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, Pipi Kayumba, alisema katika utendaji kazi wake, kila siku anapita kituoni hapo ili kuonana na wananchi anaowakuta kituoni, kusikiliza shida zao.Alishauri ili jeshi hilo liweze kuboresha huduma zake, kuwepo vituo vya polisi katika njia zote za kuingia jijini Dodoma kwani jiji hilo limekuwa kubwa, idadi ya watu imeongezeka.

“Kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu, hata utoaji huduma nao umekuwa mkubwa, kuanzishwa kwa vituo hivyo litakuwa jambo jema kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla,” alisema.Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga alishauri Mkuu wa Kituo hicho, Kidwadi Karinga, aweke mkakati wa kuondoa malalamiko ya wananchi kwenye kituo hicho.

Kailima aliendelea na ziara yake kwenye Kituo cha Kikosi cha Usalama Barabarani, kuzungumza na wananchi waliodai kuna mtu ambaye si askari alikuwa akitoa taarifa ya upotevu wa mali (loss report).Mtu huyo alikuwa akitoa taarifa hiyo nje ya kituo hicho kwa gharama kubwa wakati gharama halisi ni sh. 500 tu, hulipwa kwa utaratibu uliowekwa na kupewa lisiti.
Kailima alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa lengo la ziara hiyo ni kujionea mazingira ya kazi za askari kwa jamii ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

Alimpongeza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Nuru Selemani kwa kutekeleza agizo la Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola juu ya kuziondoa pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.

“Wasisitize askari wako waache kuomba na kupokea rushwa, kutobambika kesi kwa wananchi, askari kutumia lugha nzuri, kuelimisha wananchi wanapofanya kosa, kutoa elimu katika redio namna ya kuvuka kwenye zebra, kutoa taarifa kuhusu hali ya mji kila siku,” alisisitiza Kailima.

Aliwataka askari wa Usalama Barabarani wafanye operation kubwa mara moja kwa mwezi ili kufanya wepesi wa kukusanya maduhuli ya serikali, kutimiza wajibu wao wawapo kazini na wanaokwenda tofauti wachukuliwe hatua stahiki.

Alisisitiza suala la usalama hasa kipindi hiki ambacho kuna ugeni wa Mkutano wa SADC kuanzia Agosti 5, mwaka huu, hivyo kama chombo cha usalama wamuunge mkono Rais Dkt. John Magufuli.Pia Kailima alitembelea Kituo cha Chang’ombe kinachohudumia kata tatu za Chamwino, Chang’ombe na Chinangali ambapo hali ya usalama si nzuri kutokana na matukio ya wizi, unyang’anyi.

Matukio hayo yamelifanya jeshi hilo kufanya msako mkali na tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.Kailima aliushaurio uongozi wa kituo hicho na askari kuitumia jamii au serikali za mitaa ili kupata taarifa za wahalifu.

Mkuu wa kituo hicho, Emanuel Mawi, alisema kuna doria inafanyika maeneo mbalimbali, pia wanashirikiana na jamii, changamoto waliyonayo ni udogo wa kituo ambacho kinahudumia eneo kubwa.Akiwa kwenye Kituo cha Nkuhunga, Kailima aliambiwa kituo hicho kinahudumia kata mbili za Nkuhungu na Kizota.

Akiwa kituoni hapo, Kialima aliambiwa kituo hakilazi mahabusu ambao hupelekwa Kituo Kikuu (Central).Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, Kayumba alisema changamoto waliyonayo ni uchache wa magari kwa ajili ya doria za kila siku.

Kailima aliwapongeza Kayumba na Karinga kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga, alimshukuru Kailima na kumuahidi kuwa, watatekeleza maelekezo yote aliyotoa katika ziara hiyo ili kuboresha utendaji kazi.

MBUNGE DITOPILE AMPONGEZA RAIS DKT.MAGUFULI KWA KUZIDI KUONDOA KERO ZA USAFIRI

0
0

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana, Mhe Mariam Ditopile amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa niaba ya vijana nchini kwa kuzidi kuondoa kero za usafiri.Mhe Ditopile ametoa kauli hiyo baada ya jana Rais Magufuli kuzindua jengo la tatu (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema jengo hilo limeongeza hadhi ya uwanja huo na kwenda sawa na Uwekezaji ambao umekua ukifanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

” Tumeingiza ndege za kutosha na tunaendelea na Ujenzi mpya na ukarabati/upanuzi wa viwanja vya ndege, hii inaonesha jinsi gani Serikali yetu imejipanga katika kukuza uchumi wetu kupitia usafiri wa anga lakini pia uwezo wa ndege zetu kutua katika viwanja vikubwa vya kimataifa kunaongeza soko la watalii nchini,” amesema Mhe Ditopile.

Kuhusu usafiri wa Nchi kavu, Mbunge huyo amesema kuna barabara za kutosha na zenye ubora kwa zaidi ya asilimia 95 Nchi nzima na zimeunganishwa na mtandao wa lami.

” Ujenzi wa reli ya mwendo kasi/Treni ya umeme (SGR) unaendelea kwa kasi kubwa, Serikali inaenda kuwekeza ktk reli ya TAZARA*kwa kuboresha miundombinu pamoja na injini na mabehewa ya kutosha na ya kisasa kwa kushirikiana na wabia wenzetu jirani zetu wa Zambia,” amesema Mhe Ditopile.

Aidha amempongeza Rais Magufuli kwa namna anavyoendelea kukarabati vivuko na meli mbalimbali pamoja na kupanua na kuongeza bandari kavu.
” Kwa haya maendeleo makubwa yanayofanywa na Jemedari wetu Rais Magufuli hakika kunatupa deni kubwa sisi wasaidizi wake kuhakikisha tunawatumikia wananchi wanyonge kama ambavyo yeye mwenyewe Mhe Rais anafanya kwa vitendo,” amesema Mhe Ditopile.

SPIKA NDUGAI AIPIGIA CHAPUO UTALII WA FUKWE ZA PWANI YA BAHARI YA HINDI

0
0
Na Dennis Buyekwa,MAELEZO-DAR ES SALAAM

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa wito kwa Serikali kuendeleza utalii wa Pwani ya Bahari ya Hindi, hatua itakayosaidia kuchochea ukuaji wa utalii nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana alhamisi (Agosti Mosi, 2019), Ndugai alisema Tanzania ina kila sababu ya kuendeleza fukwe hizo kutokana na ukweli kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi za fukwe na bahari zilizo bora kuliko nchi yoyote ndani ya bara la Afrika.

Spika Ndugai aliongeza kuwa uendelezaji wa fukwe hizo utasaidia nchi kwa kiasi kikubwa kupiga hatua na kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Sisi hapa Tanzania tuna pwani ya bahari nzuri zaidi kuliko pwani zingine popote pale Afrika, hizi ni hifadhi za mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kuanzia Pangani mpaka Mtwara ambazo hazijatumika vizuri.” Alisema Spika Ndugai

Aidha Spika Ndugai aliongeza fukwe hizo zikitumika vizuri zitasaidia kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kuoanishwa vizuri kwa utalii wa pwani na ule wa bara na hivyo kuifanya sekta ya utalii kuongeza wigo mwingine wa mtandao wa mapato nchini.

Akizitaja sababu zilizopelekea utalii kutoonekana vizuri, Spika Ndugai alisema moja ya sababu kubwa inayochangia sekta ya utalii kutokufanyika vizuri ni kwa kuwa utalii wa fukwe za bahari bado uko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Aidha katika kuonyesha umuhimu wa kuendeleza fukwe hizo, Ndugai aliyataja maeneo ya Mombasa, Lamu na Malindi nchini Kenya kama maeneo ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendeleza fukwe katika Pwani zao, ambapo zimesaidia kuchochea ongezeko la watalii katika maeneo hayo.

“Kwenye Pwani zao kwa sasa kuna utalii maarufu unaofanyika baharini, unaofahamika kama ‘Marine Parks tourism’, ndio maana ukiangalia Pwani yao imejaa hotel, na sisi hapa kwetu tukitumia fukwe zetu vizuri tunaweza kuwa na utalii mzuri zaidi wa namna hii utakaosaidia kuongeza idadi ya watalii nchini”. Alisema Spika Ndugai.

Pia Spika Ndugai alimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua kuipandisha hadhi iliyokuwa sehemu ya pori la akiba la Selous Game Reserve’ kuwa hifadhi kamili itakayojulikana kama Hifadhi ya Taifa ya Nyerere au ‘Nyerere National Park’.

Akizungumzia kuhusu suala hilo Rais Magufuli alisema pendekezo la kuendeleza fukwe za pwani ya Bahari ya Hindi ni moja ya vipaumbele vya Serikali kwa sasa, na kumuagiza Waziri Mkuu , Kasim Majaliwa kuangalia jinsi ya kuendeleza fukwe zote kuanzia Moa hadi Msimbati.

HAMORNIZE AMTUMIA UJUMBE MZITO RAIS MAGUFULI ...ASEMA UTAMFIKIA TU

0
0
MSANII marufu nchini Tanzania katika muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva ambaye kwa sasa yuko kwenye ubora wake Rajab Abdull Kahali a.k.a Harmonize amemuandikia ujumbe mzito Rais Dk.John Magufuli.

Katika ujumbe huo Harmonize ameandika hivi ; kipaji na umaarufu ni tunu ambayo Mungu humpatia amtakaye kwasababu maalum!!! 

Kwa lugha nyingine , ni sauti yenye mamlaka ya peke ambayo hupendwa na kushabikiwa na wengi yaani watoto, kwa watu wazima, wanawake kwa wanaume. Hakuna awezaye kujipa umaarufu au kujipa bila matakwa yake Mungu Baba...!!!

Nitakuwa mpumbavu sana endapo nitaliona jambo baya na kupitia sauti hii au tunu hii ambayo Mungu kanijaalia nikalifumbia macho tena hata M/Mungu anaweza Kanijalia Nikalifumbia Macho Tena Hata M/Mungu Anaweninyang'anya maana hatokuwa na faida tena!!!!

Lakini nitakuwa mpumbavu zaidi nikiliona jambo jema hasa linalogusa watu waliosababisha mimi leo hii naitwa Harmonize eti nilifumbie macho kwa kuingiwa na hofu ya aina yoyote ile...!!!!

Kiukweli nitakuwa sijaitende haki ile sauti yenye mamlaka na ushawishi niliyo tunukiwa tena sio kwa unjanja wangu...!!!!

Naomba niseme kwa heshima na taadhima nikiwa kama Mtanzania Mzalendo niliyezaliwa Mtwara naipongeza Saaaana Serikali ya Awamu ya Tano (5).

Pia nichukue fursa hii kuzishukuru Serikali za Awamu zote....!!!! Tukufu zilizopita kwa misingi mizuri ambayo tunajivunia sisi na vizazi vijavyo...!!

Tamanio langu ujumbe huu utakufikia na kukuongezea nguvu ya kutujali zaidi wanyonge na kupambana kwa niaba ya Taifa letu tukufu....!!!!! 

Kwako Mhe.John Pombe Magufuli #TanzaniaKwanza #JESHI #KONDEGANG4EVERYBODY #WCB4LIFE

WAZIRI WA AFYA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA KIVUNGE WILAYA YA KASKAZINI “A’

0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa taarifa kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kuhusu utaratibu wa kuingia kazini (shifti) kwa Wafanyakazi wa hospitali hiyo.Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma akizungumza na Wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja juu ya kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa ufanisi,kushoto ni Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed.Mkurugenzi Tiba kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt. Juma Salum Mbwana akiwahimiza Wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kufanya kazi zao inavyotakiwa (kulia) – Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed.Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakifatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed huko katika Hospitali hiyo.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
……………………
Na Mwashungi Tahir,Maelezo
WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohamed amewaagiza Viongozi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge kuingia kazini kwa zamu (Shifti) kama ilivyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja ili wananchi waweze kupatiwa huduma muda wote wanapozihitaji.
Amesema agizo hilo linapaswa kutekelezwa ifikapo Jumaatatu wiki ijayo ili kuhakikisha Afya za wananchi zinaimarishwa kwa kupatiwa matibabu muda muafaka.
Wito huo ameutoa katika Hospital ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A, kuhusu malalamiko yanayotolewa na Wananchi kwa kukosa huduma kwa wakati.
Amesema utaratibu wa Shifti utaondosha malalamiko yaliyojitokeza na itaweza kutambulikana kila mfanyakazi utendaji wake wa kazi.
Aidha amesema utaratibu wa Shifti utasaidia pia kutekeleza kanuni na sheria za uajiri kwa mpango maalum unaotakiwa.
“Huu ni mpango rasmi wa Serikali utakaoanza wiki ijayo tunaanza kwa Hospitali ya Kivunge, utakwenda na Makunduchi na nyengine zinafuatia,”alisema Waziri Hamad.
Aidha alisema Hospital ya Kivunge ni ya Wilaya ambayo imetangazwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein hivyo wafanyakazi wanapaswa kuwajibika kikamilifu ili kukidhi haja ya Wananchi.
Waziri Hamad amewataka Wafanyakazi hao kutumia lugha nzuri katika kuwahudumia wagonjwa kwani lugha nzuri huwapa faraja na kuwajengea sifa hata Madaktari wanaotoa huduma.
Aidha amewakumbusha wafanyakazi kuheshimu majukumu yao na sheria ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kuchelewa kazini na kufika mapema ili huduma zipatikane kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Utumishi wa Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma alisema kwa upande wa utumishi Serikali imejitahidi kuwasomesha ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati.
Hivyo amewaasa wafanyakazi waache kujipangia wenyewe kufanya kazi kwani Sheria ya utumishi inamtaka mfanyakazi afanye kazi kwa masaa manane na siyo kama wanavyotaka wao.


Kwa upande wa Mkurugenzi tiba wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Juma Salum Mbwana aliwataka kujirekebisha na kufanya kazi kwa bidii na kuepukana na kuwajibishwa kwa barua au onyo kwani kunaharibu utendaji wako wa kazi.

SHILOLE ALIA NA WAANDAAJI WA WASAFI FESTIVAL

0
0

Na.Khadija seif, Michuzi tv

MSANII wa kike wa Bongofleva pamoja na Bongomovie kwa pamoja Zuwena Mohammed a.k.a shilole amikiri wazi kushuka kwa soko la Muziki kwa kipindi hiki.

Akizungumza kwenye vyombo vya habari hivi karibuni ,Shilole amesema kwa sasa anakumbana na changamoto ya kutotoa ngoma mpya kutokana na kutokuwepo kwa mpangilio mzuri sokoni kwani kila Msanii anatoa ngoma mpya kiasi kwamba inapelekea mashabiki kutoweza kutegea sikio nyimbo ipi na kupata wasaa wakuburudika.

"Imekua changamoto mpaka kwa watayarishaji (producer) kuchanganya vionjo na kuvirudia rudia kwa nyimbo zaidi ya moja,"

Hata hivyo shilole amewatolea uvivu waandaaji wa tamasha la wasafi kutokana na kubagua baadhi ya wasanii kutokuwepo kwenye tamasha hilo tangu lianze kwa mwaka huu.

"Wajaribu kuwa sawa na kufata utaratibu kama waandaaji wa Matamasha mengine walivokua wakifanya hasa katika kuchagua wasanii watakaotumbuiza kwenye jukwaa lao pindi wanaposafiri mikoani kwani kwa sasa soko la Muziki limekua pana sana na wasanii chipukizi ni wengi na wanafanya vizuri sana,"

Aidha amesema kundi la lebo ya wasafi wamekua wakijipendelea wao wenyewe kutokana na uwezo waliokua nao hivyo amewashauri kusaidia na wasanii wengine kujiinua kimuziki na kutambulika ndani na nje ya nchi Kama wasanii waliomo kwenye kundi hilo Rayvan,lavalava, Harmonize pamoja na Mbosso ambae amekua akipewa ushirikiano mkubwa kutoka kwenye lebo hiyo.

WADAU WA NGOs WAITIKIA USAJILI KANDA YA KASKAZIN

0
0
Wanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) wakitoa ushauri wa kisheria kwa baadhi ya wadau wa NGOs waliofika kwenye dawati la Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kukamilisha maombi ya usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa mashirika hayo linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
Afisa Maendeleo ya Jamie mkoa wa Kilimanjaro Bi. Hilda Lauwo Adios Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Victor Rugarabamu wakitoa ushauri kwa baadhi ya wadau wa NGOs waliofika kwenye dawati la Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kukamilisha maombi ya usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa mashirika hayo linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
Wasajili wasaidizi kutoka Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Usajili wa Asasai za Kiraia) na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini, RITA wakishiriki huduma ya pamoja ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya wadau wa NGOs waliofika kwenye dawati kukamilisha usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa mashirika hayo linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW


…………………………………..

Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambao awali walijisajili chini ya Sheria nyingine, wameendelea kuiitikia zoezi la usajili wa asasi zao katika siku ya tano ya usajili huo unaofanyika katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na vyombo vya habari leo mkoani Kilimanjaro Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Erasto Ching’oro ameeleza kuwa idadi ya wadau wanaofika kupata huduma ya usajili wa mashirika ya kijamii imepanda kutoka wastani wa mashirika 20 kwa siku katika siku mbili za kwanza hadi mashirika 35 katika siku ya tano likiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 75 ya wadau wanaofika kuhuisha usajili wao kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 3 ya mwaka 2019.


Bw. Erasto ameongeza kuwa, walengwa wakuu wa Usajili unaoendelea ni Mashirika naTaasisi zinayofanya kazi za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya jamii, ambao awali walisajiliwa chini ya Sheria nyingine ikiwemo Sheria ya Vyama Sura 337, Sheria ya Udhamini Sura 375, na Sheria ya Makapuni Sura 212/213, kama zilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria Namba 3 ya mwaka 2019, na sasa wanapashwa kusajiliwa chini ya Sheria stahiki ikiwemo Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2019.

“Sheria hii inazitaka Mashirika yote zilizojisajili chini ya Sheria nyinginezo kuhakikisha kuwa zimekamilisha uhamisho wao ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia siku ya tarehe 1 Julai, 2019 ili kuendelea kupata haki na hadhi ya kuendesha shughuli za katika jamii kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni. Alisisitiza Bw.Erasto

Ameongeza kuwa mafanikio yaliyongeza mwitikio wa wananchi ni juhudi zinazofanywa na Ofisi za Wasajili wa Mamlaka husika katika kuwajengea uelewa chanya kuhusu nia njema ya Serikali katika uendeshaji wa zoezi hili ambao unalenga kukuza mchango wa Mashirika hayo katika maendeleo na ustawi wa Watanzania.

Aidha Bw. Erasto ameongeza kuwa zoezi la kuhuisha usajili wa mashirika yanayofanya kazi za kijamii na kiuchumi katika ngazi ya jamii, wilaya, mkoa na Taifa linaumuhimu kwani litawezesha kuwa na matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa kuwa na mtawanyiko wenye uwiano wa afua mbalimbali katika kuhudumia jamii, jamii itahamasishwa kuchangia maendeleo yao, itakuza ajira na weledi wa miradi na pia kukuza uwazi na uwajibikaji katika ngazi mbalimbali.

Usajili huu unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa takwa la kisheria linaloelekeza Mashirika na Taasisi zote zinazofanya kazi za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananachi kuhakikisha kuwa yamekamilisha usajili wake chini ya Sheria Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa mabadiliko chini ya Sheria Namba 3 ya mwaka 2019.

Kwa Kanda ya kaskazini zoezi hili la uhuishaji usajili limeanza tarehe 29 Julai 2019 na litahitimishwa tarehe 6 Agosti, 2019 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na linaendeshwa kwa utaratibu wa Kituo cha pamoja cha usajili ambacho kinajumuisha Msajili kutoka BRELA, RITA, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara kuu Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kutoa huduma katika sehemu moja na kuepuka urasimu.

TCRA YAENDELEA KUTOA ELIMU MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

0
0
*Yahamasisha usajili laini za simu kwa alama za vidole

Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani Kanda ya Mashariki (TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Mashariki watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano pamoja uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro, amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.

Mhandisi Odiero amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.

Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba na kufanya watu wengine kuona muda uliopangwa ulikuwa hautoshi.

“Muda uliowekwa ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu hizo. 

Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalilbali za amawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (wane kutoka kushoto) akiwa katimu picha ya pamoja na timu ya TCRA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Christopher John akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Mwananchi akisaini kitabu wakati alipotembelea banda la TCRA kanda ya Mashariki katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Wananchi wakipata huduma katika banda la NIDA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Baadhi ya watoa huduma za Simu katika Banda la TCRA katika maonesho Nane Nane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images