Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WAAJIRI WANAOWANYIMA HAKI WANAWAKE LIKIZO YA UZAZI.

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna wa mwisho Kulia ni Mwakilishi kutoka UNICEF James.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia maelezo kuhusu huduma ya unyonyeshaji katika maeneo ya kazi kutoka Afisa kutoka Wizara ya Afya Bi Tufingene Malambugi wakati uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma.

……………………………………………………

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DOMOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuanza kuwachukulia hatua Waajiri wote ambao wanavunja Sheria kwa kugandamiza haki ya kupata likizo ya uzazi kwa wanawake pindi anapojifungua.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu ya “Wawezeshe wazazi kufanikisha unyonyeshaji”.

“Haki ya Mwanamke Kuzaa na kupata likizo ya uzazi ni haki yake ya asili, haitakiwi kuwekewa vikwazo au changamoto yoyote, kwahiyo nitoe wito kwa wanawake ambao wanafanya kazi, ni haki yako kupata likizo, asije mtu anakwambia anaijaza kazi yako kwakuwa umetoka likizo ya kujifungua, tuambie sisi, tutachukua hatua, na huyo Mwajiri tutamtangaza kuwa ni adui wa Wanawake na Watoto wa Tanzania “.Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha dawati la kutoa malalamiko litaloshughulikia kupigania na kutetea haki za wanawake kupata likizo ya uzazi, jambo litalosaidia kudhibiti tabia za baadhi ya Waajiri kukandamiza haki za wanawake baada ya kujifungua.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri chini ya miaka miwili wananyonyeshwa maziwa ya mama, hii inaonesha kuwa hali ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama imepungua ikilinganishwa na takwimu ya mwaka 2015/2016 ambayo ilikuwa ni asilimia 98.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi (ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa) ni asilimia 53 ikilinganishwa na asilimia 51 ya mwaka 2015/2016

Aliendelea kusema kuwa, idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 58 ikilinganishwa na asilimia 59 ya mwaka 2015/2016.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa Idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni 35%, huku kiwango kikionekana kuongezeka ikilinganishwa na asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, takwimu za utafiti wa hali ya lishe nchini za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa asilimia 31 ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa ikilinganishwa na asilimia 34 ya mwaka 2015/2016, huku sababu kubwa ya ikiwa ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto.

Naye Mwakilishi kutoka UNICEF Bw. James Gitau amesema kuwa, unyonyeshaji ni moja ya njia muhimu kuhakikisha Afya Bora kwa maisha ya mtoto, hivyo kutoa wito kwa wanahabari kuhakikisha wanapeleka Elimu kwa wananchi hususan wanawake kuhakikisha wanafahamu umuhimu wa kunyonyesha Watoto mfululizo miezi sita ya mwanzo,

Pia, Bw. James Gitau ametoa wito kwa Serikali kuongeza nguvu katika uhamasishaji juu ya umuhimu na haki ya Watoto kunyonyeshwa, amesema jambo hili litasaidia kuokoa watoto kupata magonjwa yanayotokana na kukosa virutubisho kutoka kwa maziwa ya mama.

TANZANIA YAPIGA HATUA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

$
0
0
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira akifanya utambulisho wa wageni walioshiriki mkutano wa mwaka wa mapitio na kutengeneza mpango kazi wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka wizara ya afya Dkt.Leonard Subi akiongea na vyombo vya habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Mratibu wa NTD Dkt.Upendo Mwingira akisalimiana na mgeni rasmi Dkt.Elias Kwesi.
Mgeni rasmi wa mkutano huo wa NTD ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Elias Kwesi akifungua mkutano huo ambao unawakilishwa na waratibu wa mpango huo kutoka mikoa mbalimbali,wadau wa ndani na nje ya nchi.
Kaimu Mwakilishi mkazi wa shirika la afya duniani(WHO)Dkt. Christine Musanhu akiongea kwenye mkutano huo.


Na.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia wizara ya afya imepiga hatua katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchi.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na Maafa wa Wizara hiyo, Dk. Elius Kwesi wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mapitio ya shuguli wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na mpango kazi wa mwaka.

Dkt.Kwesi alisema mkutano huo ni muhimu kwani watajadiliana na wadau hao kuona namna watakavyoshirikiana na Wizara hiyo kwa upande wa rasilimali fedha.

“Tuna pengo la rasilimali mbalimbali na tumewaita hapa Wadau kujadiliana nao Mpango kazi wetu na kuangalia namna gani watatusaidia kuziba pengo na kutakavyosaidiana kutekeleza,” alisema Dkt.Kwesi

Alisema tangu utekelezaji wa Mpango huo ulipoanza nchini umefanikiwa kupunguza magonjwa hayo kwa kiwango cha asilimia 80.

Awali Mkurugenzi wa huduma za Kinga wizarani hapo Dkt.Leonard Subi alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yasipodhibitiwa yatapelekea watu wengi kuugua siku zijazo kwani yana athari kubwa na kusababisha upofu na ulemavu kwa jamii.

“mfano ugonjwa wa kichocho kwa watoto huathiri ukuaji na wengine wanaweza kupata saratani katika maisha yao”.Alisema Dkt.Subi

Alisema wizara kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanya jitihada kubwa na hivyo kufanikiwa kudhibiti magonjwa hayo kwa kiwango kikubwa

“Wilaya ambazo zilikua zimeathirika sana na matende na mabusha miaka kumi iliyopita zilikua takribani 120 lakini hivi sasa zimebaki wilaya 24 ambazo bado tunaendelea na ugawaji kingatiba na trakoma kulikuwa na wilaya 71 na sasa zimebaki wilaya sita tu”.

Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele(NTD) Dkt.Upendo Mwingira amesema kwa upande wa kichocho na minyoo ya tumbo bado inahitajika kuendelea kuwakinga watoto na baadhi ya wilaya wanaendelea kugawa kingatiba za matende na mabusha pamoja na usubi.

Wawekezaji washauriwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za kazi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya kazi.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na wawekezaji wa Shamba la Katani la China State Farms lililopo Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Steven Kebwe akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipomtembelea katika ofisi yake Julai 31, 2019 kabla ya kutembelea maeneo ya kazi yaliyopo katika Mkoa huo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na Wafanyakazi wa Shamba la China State Farms lililopo Wilaya ya Kilosa alipofanya ziara ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoa wa Morogoro, Julai 31, 2019.
Baadhi ya Wafanyakazi wa shamba la China State Farms wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembelea shamba la China State Farms lililopo Wilayani Kilosa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kutokea kulia) akisikiliza kero kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Shamba hilo Bw. Azory Andrea kuhusu mikataba inayotolewa na mwekezaji wa shamba hilo.

Kamishina Msaidizi wa Kazi, Bi. Rehema Moyo akitoa ufafanuzi kuhusu mkataba wa kazi wa Bw. Azory Andrea (hayupo pichani) alipowasilisha tatizo lake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea hilo la China State Farms, Wilayani Kilosa Julai 31, 2019.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiangaalia katani iliyoanikwa, wakati alipotembelea shamba hilo lililopo wilayani Kilosa. Kushoto anayetoa maelekezo ni Meneja wa Rasilimali watu na Fedha Bw. Athumani Migeto. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Meneja Rasilimali Watu wa Shamba la China State Farms Bw. Athumani  Migeto (kulia) alipotembelea sehemu ya mitambo ya uzalishaji. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi.

Muonekano wa Nyumba zilizojengwa na Uongozi wa Shamba la China State Farms kwa ajili ya wafanyakazi wa shamba hilo.

***********

Hayo ameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Shamba la Katani la China State Farms lililopo wilayani Kilosa ikiwa ni ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika shamba hilo alieleza kuwa wawekezaji wakiwa kama waajiri lazima wahakikishe wanafuata sheria za kazi katika maeneo yao ya uzalishaji kwa kuzingatia masuala ya msingi ya wafanyakazi ili waweze kuzalisha kwa tija na kuwahamasisha kufanya kazi zao kwa juhudi.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kuboresha mazingira ya biashara ambayo yamekua yakivutia zaidi wawekezaji, hivyo sera nzuri zilizopo nchini zimekuwa chachu kwa wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu,” alisema Mhagama

Alieleza pia, endapo wawekezaji watafuata miongozo ya kisheria katika masuala ya kazi na ajira yatawarahisishia utendaji wao wa kazi.

Akitolea mfano kuhusu masuala ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi, likizo ya uzazi kwa wanawake, uwazi wa mikataba ya ajira, uhuru wa mfanyakazi kujiunga na chama cha wafanyakazi, haki ya kupatiwa vitendea kazi na maslahi ya wafanyakazi ni baadhi ya vitu vya msingi ambavyo mwekezaji inabidi atoe kwa mfanyakazi wake kwa kuzingatia taratibu na sheria.

Hata hivyo aliongezea kuwa ushirikiano na vyama vya wafanyakazi ni jambo la muhimu kwa kuwa vimekuwa vikitetea masuala ya wafanyakazi ambayo yamekuwa yakijitokeza katika maeneo yao ya kazi, pamoja na kuwa na mkataba wa hali bora za wafanyakazi baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Sambamba na hilo Mheshimiwa Mhagama alitoa maagizo kwa timu ya wataalamu ambao aliambatana nayo kutoka Idara ya Kazi, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Tume ya Usuluhisi na Uamuzi pamoja na Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuendelea kutoa elimu kwa umma hususan wafanyakazi ili watambue sheria za kazi na namna taasisi hizo zinaweza kuwasaidia katika kupata ufumbuzi wa masuala yao ya kazi.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa pongezi vilevile kwa wawekezaji wa Shamba la Katani la China State Farms kwa kuwajali wafanyakazi wao ikiwa na kuwajengea nyumba bora za kuishi wafanyakazi wao.

“Nimpongeze mwekezaji kwa kuona umuhimu wa kuwajengea makazi wafanyakazi ambayo yatamaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa nyumba na umbali ambao wafanyakazi wamekua wakitumia kwenda kazini,” alisema Mhagama

Pia, alitumi muda huo kuwahamasisha wafanyakazi kutumia muda wao wa ziada katika mashamba yao binafsi na kujiunga kwenye mashamba ya ushirika yatakayo wawezesha kupata soko la uhakika kutoka kwa mwekezaji huyo ili waweze kuimarika kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi alisema kuwa Sheria za kazi zimekuwa zikitoa mwongozo mzuri kwa wawekezaji katika kuimarisha shughuli zao za uzalishaji, kutoa ajira pamoja na kuchangia kwenye mapato ya nchi.

Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho Bw. Majuto Chitema alitoa pongezi zake kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusifu juhudi alizonazo katika kuboresha na kuwajengea mazingira wezeshi wawekezaji, kwani serikali yake imeweza mstari wa mbele kuweka sera, miongozo, kanuni na sheria ambazo zimekuwa haziwabani wawekezaji.

Miongoni mwa Wafanyakazi wa China Estate Farms Bw. Azory Andrea alisema kuwa Serikali iendelee kuangalia namna ya kuwa kuwasimamia wawekezaji waliopo nchini ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za kazi.

Kabla ya ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata taarifa ya maeneo aliyoandaliwa kutembelea katika ziara yake mkoani hapo.

PICHA YA MWAKA: RAIS DKT. MAGUFULI APIGA PICHA WAPIGA PICHA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha picha alizowapiga wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa ndani ya ndege ye ATCL ya Dreamliner iliyotua kutoka 

Mumbai  wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019



SHILATU AHIMIZA UJENZI KWA WANANCHI KUJITOLEA

$
0
0


Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewahimiza Wananchi kushiriki ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa ili kuchochea maendeleo zaidi kwenye jamii zao.

Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye mkutano wa baina ya uongozi wa shule ya Msingi Chilindu iliyopo Kijiji cha Kichangani kata ya Mkoreha na Wazazi ambao ulikuwa na malengo ya Kujadili hali ya taaluma pamoja na uibuaji miradi ya maendeleo shuleni hapo.

Gavana Shilatu aliwasisitizia Wazazi kuhakikisha wanajitolea kuiboresha miundombinu ya shuleni ambapo waliridhia kwa kuchangia ujenzi wa vyoo kwanza vijengwe na baadae wataelekeza nguvu kwenye ujenzi wa Madarasa na nyumba za Waalimu na kusisitiza kila Mzazi kutimiza maazimio ya pamoja.

“Ni lazima tuelewane, kile ambacho kimetoka kama azimio hapa ni wajibu kila Mtu hapa kutimiza wajibu wake kutekeleza. Kikubwa tujiletee maendeleo yetu.” Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu pia aliwasisitizia Wazazi kukemea vikali tabia ya mimba shuleni (ambayo imepungua sana kwa sasa) pamoja na utoro shuleni ambao upo wa rejareja ili Watoto waanze na kumaliza shule ipasavyo kwani Elimu ni bure inatolewa.

Kupitia kikao hicho fedha zilianza kuchangwa na Wazazi hapo hapo ambapo uongozi wa shule ndio ulipokea michango hiyo huku Wazazi wakionyesha kufurahishwa na kitendo cha wao kushirikishwa.

“Sisi hatuna shida ya kuchangia maana fedha zinatumika kwa ajili ya maendeleo yetu, kikubwa tupeane ushirikiano kama hivi leo kwa hatua zote.” Alisikika mmoja wa Wazazi kikaoni hapo.

Kikao hicho kilihudhuliwa pia na Mtendaji Kata Mkoreha, Watendaji Vijiji, uongozi na kamati ya shuleni hapo.

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU KIJIJINI KWAKE MSOGA

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru ulipowasili kijijini kwake Msoga wilayani Bagamoyo wakati ukikimbizwa katika mkoa wa Pwani
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kiongozi wa mbio za  Mwenge wa Uhuru ulipowasili kijijini kwake Msoga wakati ukikimbizwa katika mkoa wa Pwani

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiwa katika sherehe za kuupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili kijijini kwake Msoga wakati ukikimbizwa katika mkoa wa Pwani

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete na wakiwa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru ulipowasili kijijini kwake Msoga wakati ukikimbizwa katika mkoa wa Pwani 
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa akihutubia wananchi Mwenge wa Uhuru ulipowasili kijijini Msoga

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA LAWAKARIBISHA WATANZANIA KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE SIMIYU

$
0
0
Naibu waziri wa Kilimo, Omary Mgumba (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakati alipotembelea Bando lao kwenye Maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. NIC inanatarajia kutazindua rasmi bima ya kilimo mahususi kwa ajili ya kulinda uharibifu wa mazao yaliyopo shambani.

bofya alama ya play kuona.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akipokea mfuko wa NIC kutoka kwa Bwana Maleku, wakati alipotembelea Bando lao kwenye Maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. 

MISS UTALII KUCHELE, NCHI ZAIDI YA 100 KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWA KUTANGAZA UTALII

$
0
0

*BASATA yaibariki bodi mpya na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BODI maalumu itakayosimamia mashindano ya urembo, utalii na utamaduni maarufu kama Miss Toursim Tanzania imezinduliwa rasmi jana  jijini Dar es Salaam na hiyo ni kufuatia kushindwa kwa usimamizi wa mashindano hayo kupitia taasisi iliyokuwa inasimamia mashindano hayo hali iliyopelekea kurekebishwa kwa mfumo wa mashindano hayo kwa kuimarisha usimamizi wa mashindano pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.

Akizungumza mara baada ya kuizindua bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa baraza la sanaa la taifa (BASATA) Vivian Shalua amepongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.

Shalua amesema kuwa mwaka 2013 baraza hilo ilitoa muda wa wasimamizi wa mashindano hayo kujichunguza na kuboresha mashindano na wanaamini bodi hiyo itafanyavizuri zaidi kwa kuwa wamekuwa wakishirikisha baraza la sanaa kwa kila hatua na katika vikao vyao wamedhamiria kutangaza vivutio vya nchi kitaifa na kimataifa na kuwaomba wadhamini kujitokeza ili kuweza kudhamini mashindano hayo.

Kwa upande wake Rais na mwenyekiti wa bodi hiyo Gideon Chipungahelo amesema kwamba baada ya kutathimini na kupanga mikakati kuhusiana na mashindano hayo wamekuja na nguvu mpya kwa kuandaa shindano la kitaifa la miss utalii Tanzania kwa kuhusisha zaidi ya nchi 100 duniani pamoja na washiriki watakaowakilisha Tanzania kupitia kanda maalumu za ushiriki.

Chipungahelo amesema kuwa bodi inayosimamia mashindano hayo ipo imara na yataendeshwa kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu kwa malengo ya kulitangaza taifa kupitia utalii, utamaduni pamoja na mila za kitanzania.

Vilevile amewashauri wasanii na wadau wa Sanaa kuwatumia wataalamu kutoka BASATA ili waweze kufahamu namna bora za uendeshaji wa shughuli za sanaa kote nchini.

Mchakato wa mashindano hayo ya urembo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti na utahusisha kanda nane katika Mikoa yote nchini na kubeba kauli mbiu ya, "Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa- Utalii mi Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa-"
Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akimshukuru Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua mara baada ya kumaliza kikao chao na kupatikana kwa bodi mpya ya shindano hilo na kuitangaza rasmi mbele ya Waandishi wa Habari,jana jijini Dar.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mikakati mipya ya shindano hilo,mara baada ya kutangazwa bodi mpya ya shindano hilo,huku wakishirikiana bega kwa bega na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)

Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),mara baada ya kuizindua bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania,ambapo pia alipongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.
Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA katika meza kuu,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.


Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano mpya wa shindano hilo mara baada ya kuzinduliwa upya na Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwashukuru wanahabari (hawapo pichani) na Wadau mbalimbali waliojitokeza kushuhudia tukio hilo adhimu,kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA


NMB yauza Hati Fungani za Bil.83.3/-

$
0
0








Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NMB – Filbert Mponzi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna.


Afisa Mkuu wa Fedha, Ruth Zaipuna akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wateja wadogo na wakati (Chief Retail Banking), Filbert Mponzi na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha (Head, Global Markets Treasury department), Gladness Deogratius.

***********

BENKI ya NMB, imetangaza matokeo ya mauzo ya toleo la tatu laprogramu ya hati fungani ya benki hiyo, ambako imekusanya Sh. Bilioni83.3 sawa na asilimia 333 ya mauzo yaliyotarajiwa awali ya Sh. Bilioni 25.Mauzo ya toleo la tatu la hati fungani ya NMB yalifunguliwa Juni 10 na kufungwa Julai 8, mwaka huu, ambako kipindi hicho cha miezi miwili,kilikuja baada ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA),kutoa idhini ya mauzo hayo.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza matokeo hayo, iliyofanyika jijiniDar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha , Ruth Zaipuna, alisema waokama benki wanajivunia kiwango hicho cha mauzo, kinachothibitishaimani ya wananchi na jamii kwa benki yake.

Zaipuna alibainisha kuwa, tayari NMB imeyapokea na kuyakubali maombiyote na kwamba waombaji wote wa manunuzi ya hati funganiwametaarifiwa na kwamba leo Agosti 2, wanaorodhesha hati funganizote, kabla ya wanunuzi kukabidhiwa vyeti mwezi mmoja ujao.

Alifafanua ya kwamba, mauzo hayo ya kiwango cha juu kulikowalivyotarajia, yanaiongezea benki nguvu ya kiuchumi katika kufanikishautoaji wa mikopo kwa wateja wao na kwamba mchakato mzimaumeshirikisha zaidi ya matawi 200 kote nchini.

“NMB inatoa shukrani za dhati kwa taasisi zote zilizofanikisha uuzwaji watoleo la tatu la hati fungani ya NMB, ikiwemo CMSA, Soko la Hisa la Dar esSalaam (DSE), Mshauri Kiongozi wa NMB, Stanbic Bank Tanzania Ltd naDalali Mfadhili wa NMB, Orbit Securities Company Ltd,” alisema Zaipuna.

Hati fungani ni aina ya uwekezaji, ambao unamuwezesha mteja kuwekezapesa katika taasisi (hasa shirika la kibiashara au Serikali), kwa kuikopeshafedha kwa muda maalum na kwa riba isiyobadilika. Riba ya hati funganiza NMB kwa mwaka ni asilimia 10.

Mteja anaponunua Hati Fungani ya NMB, anakuwa ameikopesha benkifedha zake, ambako NMB inaahidi kurejesha fedha zake (msingi) katika kipindi maalum cha ukomavu. Kuanzia muda uliowekeza hadi muda waukomavu ambao unakuwa miaka mitatu.

Bonge la Mnada wa mali za Ubalozi wa Marekani, Uholanzi, Uingereza na Denmark.

WABUNIFU KUENDELEZWA ILI KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA: PROFESA NDALICHAKO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

SERIKALI imesema kupitia mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

Itahakikisha inatumia kamati mbalimbali za SADC kuwasaidia wabunifu katika Sayansi na teknolojia ili waweze kufanya tafiti zenye kuleta tija na kutatua changamoto za jamii nchini

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo Agosti Mosi, jijini Dar es Salaam, katika kilele cha maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Amesema, zipo kamati mbali mbali za mawaziri wa sayansi na teknolojia pamoja na ubunifu ambapo wamepanga mipango ya kuendeleza ubunifu na kwamba wanaangalia na kuweza kuwatambua wabunifu kwa kuwaendeleza.

Ameongeza kuwa serikali imeweka mipango na taratibu madhubuti za kuwatambua wanasayansi na wabunifu hasa kipindi hiki ambacho jumuiya hii inaingia katika Mapinduzi ya Viwanda na kufanya wabunifu kuwa ni watu wa muhimu na kuongeza kuwa, maonesho hayo ya TYS, yanaashiria kuwa elimu inayotolewa inakidhi na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za jamii hasa katika masomo ya Sayansi.

"Nimefurahi kuona miradi inayoonyeshwa imeongezeka kutoka 81 na hadi 95 ambayo ni mafanikio makubwa kwa sekta hii..."Najivunia kuona kuwa idadi ya wasichana imezidi kuongezeka kwani mwaka huu wasichana 88 waliojitokeza kushiriki maonesho haya ni sawa na asilimia 46," amesema Ndalichako.

Pia amewapongeza wasichana wanaozidi kujitokeza katika mambo ya sayansi Teknolojia na ubunifu kwani zamani masomo ya Sayansi hayakupendwa na wasichana lakini katika kipindi hiki mwamko umekuwa mkubwa kutokana na jitihada za walimu kuhamasisha Sayansi mashuleni.

Profesa Ndalichako pia amewaomba walimu kuwafundisha wanafunzi kufanya tafiti ambazo zitasaidia ukuaji wa uchumi hasa katika Mapinduzi manne ya Viwanda kwani hata tafiti zilizofanyika kwa mwaka huu zimekuwa na kiwango bora na zenye kulenga kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Amos Nundu amesema kwa muda mfupi vijana kupitia YST wamefanya tafiti zinazoonesha kutatua changamoto za jamii.

"Mifumo huu ni mzuri kwa kuwa umeweza kujenga vijana wadogo wenye uwezo wa kufanya tafiti zenye weledi zinazosaidia kuchangia ukuaji wa taifa," alisema Dk. Nundu.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa mfuko wa kusaidia ubunifu Tanzania (HDIF) Joseph Manirakiza amesema, wao kama wadau wa ubunifu nchini,

wamekiwa wakiiunga mkono YST kwa miaka 4 sasa. "Sisi HDIF tunafanya hivi kwa sababu tunaamini katika mchango wa ubunifu kwa maendeleo ya nchi yoyote, na ukianza kuwajenga vijana wakiwa wadogo una uwezekano mkubwa wa kuja kuwa na wanasayansi, wagunduzi na wabunifu wengi wazuri mbeleni", amesema Manirakiza

Katika maonesho hayo Washindi walikabidhiwa vikombe na medali ambapo mshindi wa Kwanza ilikuwa ni shule ya Sekondari ya Chief dodo ya mkoani Manyara ikifuatiwa na shule ya Sekondari Kisimiri na Iliboru.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wandau mbalimbali wa elimu leo Agosti Mosi katika kilele cha maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Joyce Ndalichako akiwakabidhi zawadi washindi wa YST 2019
Mkurugenzi Mkazi wa mfuko wa kusaidia ubunifu Tanzania (HDIF) Joseph Manirakiza akikabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo ya human development innovation katika kilele cha maonesho ya Young Scientists Tanzania,leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo yab Ufundi,Prof Joyce Ndalichako akipata maelezo mafupi kutoka kwa wanafunzi walioshili maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 
Mtaalamu wa mambo ya Mahusiano kutoka HDIF, Hannah Mwandoloma akifafanua jambo kwa wanafunzi katika maonesho hayo. 
Mtafiti Msaidizi wa Ubongo Kids, Timothy Sambwe, akifafanua jambo kwa wanafunzi waliotembelea banda la HDIF kujua jinsi katuni za mbali mbali za masomo maarufu kama ubongo kids zinavyobuniwa. Ni katika maonesho ya wabunifu chipukizi yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam 
Mtaalamu wa mambo ya Mahusiano kutoka HDIF, Hannah Mwandoloma akifafanua jambo kwa wanafunzi katika maonesho hayo. 
Mtafiti Msaidizi wa Ubongo Kids, Timothy Sambwe, akifafanua jambo kwa wanafunzi waliotembelea banda la HDIF kujua jinsi katuni za mbali mbali za masomo maarufu kama ubongo kids zinavyobuniwa. Ni katika maonesho ya wabunifu chipukizi yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam 

WFP wasafirisha shehena ya mzigo kwa kutumia MV. Umoja kwenda Uganda

$
0
0
Meli ya mizigo ya MV Umoja iliyobeba mabehewa ya treni yenye shehena ya mzigo wa Shirika la Programu ya Chakula Duniani (World Food Program-WFP) kutoka Mwanza kwenda Uganda iliwasili bandari ya Portbell, Uganda tarehe 31 Julai 2019.

Katika Halfa ya mapokezi ya meli hiyo, Serikali ya Uganda iliwakilishwa na Waziri wa Nchi-Uchukuzi, Mhe. General Katumba Wamala na kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Dkt. Aziz Mlima alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.

Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam hadi Kampala.

Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa kutumia njia hii wameokoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 2.


Ujumbe uliosafiri na meli ya MV Umoja iliyobeba mabehewa hayo yenye mizigo ya WFP ulijumuisha Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa; Mkurugenzi wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Johnson Kisaka ambao waliambatana na Mkurugenzi wa WFP-Tanzania, Bw. Michael 



Meli ya MV. Umoja iliyobeba shehena ya mzigo, mali ya WFP kutoka Dar Es Salaam ikiwasili katika Bandari ya Port Bell jijini Kampala tarehe 31 Julai 2019.

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima akitoa neno wakati wa hafla ya mapokezi ya meli ya Mv. Umoja jijini Kampala, Uganda.


Balozi Mlima akiongea na wanahabari kuhusu zoezi hilo.

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZAVA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mmoja wa Wafanyakazi wa Kiwanda cha Mazava Bi. Sophia Lyimo (kushoto) anayehusika na uzalishaji akimwelezwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama namna wanavyotengeneza nguo katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wa kiwanda cha Mazava alipowasili Mkoani Morogoro kwa lengo la kutembelea maeneo ya kazi.
Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchukya akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye taasisi OSHA (waliokaa msatri wa mbele) wakisikiliza ufafanuzi kuhusu masuala ya Kazi kutoka kwa Waziri wa Nchi, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), alipofanya ziara kwenye kiwanda hicho.
Meneja wa Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Rose Meattu akilelezea jambo kuhusu makusanyo ya michango ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoa wa Morogoro.
Katibu wa TUICO, Mkoa wa Morogoro Bw. Mgasa Timola akielezea kuhusu masuala ya wafanyakazi waliojiunga na chama hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana na viongozi wa kiwanda cha Mazava alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro. Kushoto ni Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava upande wa Uzalishaji Bw. Bernald Makau, (katikati) Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchukya na Bw. Nicolaus Ngowi Katibu wa TIPAWU Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia nguo zinazozalishwa katika kiwanda cha Mazava, alipotembelea kiwanda hicho. Kulia ni Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha Mazava upande wa Uzalishaji Bw. Bernald Makau akitoa maelezo.
Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Mazava, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza changamoto na kero wanazokumbana nazo wafanyakazi katika Kiwanda cha Mazava kutoka kwa Bw. Mrisho Tugulu (kulia), alipotembelea kiwanda hicho kujionea utendaji kazi.Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wafanyakazi wa Mazava wakati wa ziara yake alipotembelea kiwanda hicho mkoani Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuuanayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Mazava kilichopo Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kutembelea Maeneo ya Kaz iJulai 31, 2019.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

SERIKALI IMETOA MILIONI 100 KUJENGA BWENI LA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM HALMASHAURI YA MJI GEITA

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akicheza na watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha Watoto wenye mahitaji maalum cha shule ya msingi Mbugani, Waziri huyo yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya Elimu

Moja ya majengo hayo


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum katika kituo Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum (Hawapo Pichani) baada ya kukagua ujenzi wa bweni la Kituo cha Watoto wenye mahitaji Maalum cha Shule ya msingi Mbugani iliyopo mkoani Geita.

………………………………………………………..

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kisasa la wanafunzi katika kituo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mbugani iliyopo katika halmashauri ya Mji Geita.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara mkoani Geita ambapo amesema fedha hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu nchini.

Ole Nasha amesema serikali ya Awamu ya Tano inatambua umuhimu wa kuwajengea fursa na mazingira mazuri ya kusoma watoto wenye mahitaji maalum na ndio maana imeweka mkazo katika kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu wa kutosha, vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vitabu ili kuwawezesha kusoma bila vikwazo vyovyote kutokana na changamoto zao za kimaumbile.

“Kwa miaka mingi jamii nyingi zimekuwa zikiwatenga watoto wenye mahitaji maalim, lakini kwa sasa nashukuru tumeendelea kuwawezesha kupata haki yao ya Elimu kama walivyo watoto wengine na kwamba wanaweza kuwa na changamoto za kimaumbile lakini ubinadamu wao upo palepale amesema Waziri Ole Nasha.

Amewataka wanafunzi hao wenye mahitaji maalum kutokatishwa tamaa na changamoto walizonazo za kimaumbile kwani serikali imewawekea mazingira ya kuwawezesha kufika mbali zaidi katika Elimu na kuwataka kuendelea kutumia fursa hizo za kielimu ili kutengeneza maisha yao ya baadaye.

“Wanafunzi, mtu hawezi kujua kipaji chako ni kipi lakini serikali inakupa fursa ya kuonyesha kipaji chako, Mhe Rais ametambua uwezo mkubwa wa watu wenye mahitaji maalum na ndio maana siku hizi tunae Naibu Waziri anayeshughulika na watu wenye mahitaji maalum ambaye naye ana changmoto ya ulemavu,” amesema Naibu Waziri.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mbugani Edwicka Ndunguru amemweleza Naibu Waziri kuwa kituo hicho kilijengwa kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata haki ya kielimu katika mazingira wezeshi na kuwapa fursa wengi zaidi wenye mahitaji maalum wanaoishi mbali na shule zinazotoa elimu maalum kupata elimu.

Amesema mafanikio ya kuwepo kwa vituo vya watoto wenye mahitaji maalum mbali na kuwawezesha kupata haki yao ya kielimu, pia imewasaidia kujifunza ujuzi mbalimbali, jamii imetambua nakuthamini umuhimu wa wanafunzi wenye mahitaji maaluma kupata Elimu na wengine kufanikiwa kupata kazi katika maeneo mbalimbali.

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapomaliza hapa wanakua na ujuzi katika fani za ushonaji, ufumaji na useremala, fani hizi zimewezesha baadhi kuajiriwa katika maeneo mbalimbali na wengine kujiajiri amesemu mwalimu Ndunguru.

Kituo hicho chenye vitengo vinne vyenye jumla ya wanafunzi 143 ambavyo ni vitengo vya ulemavu wa akili, Viziwi, ulemavu wa viungo na ulemavu wa macho, mbali ya kuhudumia wanafunzi hao wenye uwezo wa kufika shuleni lakini pia vinahudumia watoto 38 wenye ulemavu wa kiwango cha juu ambao hawawezi kufika shuleni.

SERIKALI YAPONGEZWA MFUMO WA GePG

$
0
0
Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu

Mwandishi Mashughuli wa Vitabu nchini kikiwemo cha “Mabala The Farm”, Bw. Richard Mabala, ameipongeza Serikali kwa kubuni mfumo wa kielektroniki wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali- GePG kwa kuwa unasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma na kuweka uwazi wa mapato na matumizi.

Alibainisha hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Alisema kuwa Mfumo wa GePG unamanufaa kwa Serikali na wananchi, kutokana na uwazi uliopo lakini pia makusanyo kufika kwa wakati katika maeneo husika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na mengine.

“Mfumo huo utanisaidia malipo ya kodi ya majengo na kodi nyingine kwa kuwa unaondoa urasimu wa kwenda katika ofisi mbalimbali kwa ajili ya malipo na pia unaokoa muda kwa kuwa ni rahisi kuutumia kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Bw. Mabala.

Mwandishi huyo wa Vitabu ametoa wito kwa wadau, ikiwemo Serikali kuhamasisha matumizi ya Simu zenye uwezo wa kutumia mfumo wa GePG, hasa katika maeneo ya vijijini ambako idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wakulima wanapatikana.

Tanzania inaidadi kubwa ya vijana ambao wanauwezo wa kutumia mfumo wa kielektroniki katika malipo ya Serikali ukilinganisha na wazee, hivyo umekuja wakati mwafaka na utakua na nafasi kubwa ya kuchochea maendeleleo ya kiuchumi.

Bw. Mabala amesema kuwa, Mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika Mipango ya Serikali ukilinganisha na awali ambapo mfumo huo haukuwepo hivyo uwepo wa GePG utaongeza ufanisi kiutendaji na kuharakisha maendeleo kulingana na ushindani uliopo katika nyanja mbalimbali duniani hasa katika mifumo ya teknolojia.

Kwa upande wao wanafunzi wa Sekondari ya Biashara iliyopo Bariadi Mkoani Simiyu, wameipongeza Serikali kwa kutumia mfumo wa kisasa wa GePG, hivyo elimu waliyoipata katika maonesho ya Nanenane wataipeleka kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka ili waweze kuitumia katika malipo ya Serikali.
Mwaandishi Mashughuri wa Vitabu Nchini Tanzania, Bw. Richard Mabala (kushoto), akipata maelezo kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki- GePG, kutoka kwa mtaalam wa mfumo huo wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Stella Nguma, alipotembelea katika banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane eneo la Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto), wakitoa elimu ya masuala ya Bajeti, Sera, Pensheni na Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki- GePG, katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Wanafunzi wa Kidato cha Tatu kutoka Sekondari ya Biashara Mkoani Simiyu, Happiness Gwalugwa na Elen Mhuly, wakipata maelezo kuhusu Masuala ya Bajeti kutoka kwa Mtaalamu wa Bajeti Bw. Asajile Mwaipopo, walipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mwaandishi Mashughuri wa Vitabu Nchini Tanzania Bw. Richard Mabala (kushoto), akipata maelezo ya masuala ya Bajeti kutoka kwa Mtaalamu wa Bajeti Bw. Asajile Mwaipopo, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkazi wa Bariadi Mkoani Simiyu Bi. Mariamu Ezekieli, akielezwa namna bajeti inavyoandaliwa na umuhimu wake kwa wakulima, kutoka kwa mtaalamu wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Asajile Mwaipopo, alipotembelea banda la Wizara hiyo, katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 
Muonekano wa Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. (Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango- Simiyu).

TANZANIA NA ZIMBABWE ZASAINI HATI 5 ZA MAKUBALIANO YA PAMOJA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) na Waziri wa mambo ya Nje wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo wakisaini hati za makubaliano ya pamoja (MoU) katika Nyanja mbalimbali. Tukio hilo limefanyika Harare,Zimbabwe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) na Waziri wa mambo ya wanawake,Jinsia na Maendeleo ya Jamii Mhe. Sithembiso Gile Nyoni wakisaini hati za makubaliano ya pamoja (MoU) katika Nyanja ya jinsia na kuwawezesha wanawake  Tukio hilo limefanyika Harare,Zimbabwe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) na Waziri wa mambo ya Nje wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo wakisaini hati za makubaliano ya pamoja (MoU) wakionesha kwa furaha hati za makubaliano ya pamoja (MoU) kati ya Tanzania na Zimbabwe mara bade ya kusaini hati hizo. Tokio hilo limefanyika Harare,Zimbabwe.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe (JPCC). Mkutano huo umefanyika Harare,Zimbabwe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) na Waziri wa mambo ya Nje wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo,wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe judoka Tanzania na Zimbabwe mara bade ya kumalizika Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe. Mkutano huoumefanyika Harare,Zimbabwe




SERIKALI YATENGA MILIONI 360 ZA MAJI KATA YA IHANJA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ihanja wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge Kingu akikagua ujenzi wa matundu ya choo katika Shule ya Sekondari ya Masinda ambapo pia alikagua ujenzi wa madarasa ya shule hiyo na Shule ya Msingi ya Mpangwe.
Mbunge Kingu akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Masinda.
Wasanii wa Kikundi cha Nkunguli wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
Mbunge Kingu akicheza sanjari na wasanii wa Kikundi cha Mshikamano.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ihanja, Juma Ntandu akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mbunge Kingu akimkabidhi kadi ya CCM Mzee, Abrahaman Moja aliyehamia chama hicho kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedi Madai akitoa taarifa ya miradi ya maendeleo iliyofanyika katika kata hiyo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

SERIKALI imetenga sh.milioni 360 kwa ajili ya kupeleka maji Kata ya Ihanja iliyopo Wilayani Ikungi mkoani Singida.

Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu wakati akiwahutubia wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara ambao ulikuwa na lengo la kuelezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika eneo hilo pamoja na kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

"Serikali imetupa sh.milioni 360 kwa ajili ya kutuwekea maji katika kata hii ambapo pia tutayafikisha vijiji vya jirani" alisema Kingu.Kingu alisema hivi sasa kazi inayofanyika ni usanifu wa mradi huo na wakati wowote itaanza kujengwa miundombinu kwa ajili ya kusambaza maji hayo kwenda kwa wananchi.

Alisema katika kata hiyo Serikali imeweza kujenga madaraja saba yaliyopo barabara ya kwenda Kata ya Ndulu, Kituo cha Afya cha kisasa na sasa wanataka kuongeza kujenga madarasa mengine na hosteli katika Shule ya Sekondari ya Masinda ili iwe na kidato cha tano na sita kama itakavyo kuwa katika Tarafa ya Sepuka.

Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi na kuwa katika jimbo hilo kuna miradi mikubwa ya maji 24.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa.

Kingu aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo baada ya kukamilika na kueleza kuwa itakuwa haina maana miradi iliyogharamiwa na serikali kwa fedha nyingi ikaachwa iharibike.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Ihanja, Obedy Madai, alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na kusema miradi yote iliyofanyika katika kata hiyo thamani yake inaweza kufika sh.bilioni moja.

MAUZO YA TOLEO LA TATU LA HATIFUNGANI ZA BENKI YA NMB YAWEKA HISTORIA KATIKA MAENDELEO YA MASOKO YA MITAJI

$
0
0
*CMSA yapeleka ujumbe kwa benki za biashara, wananchi kutumia fursa, DSE yagusia mafanikio ya NMB 

Ripota Wetu, Michuzi TV

OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Nicodemus Mkama ametoa mwito kwa benki za biashara pamoja na benki za wananchi kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ikiwemo kuuza hatifungani kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika soko la hisa ili kuongeza mitaji yao.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni muhimu kwani itasaidia utekelezaji wa agizo la Serikali kwa benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha ili kujiendesha kibiashara.

Mkama ameyasema hayo leo Agosti 2,2019 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa toleo la tatu la hatifungani ya Benki ya NMB katika Soko la Hisa Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mauzo ya toleo la tatu la hatifungani ya benki ya NMB yameweka historia kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini.

"Kwani mauzo haya yamekuwa na idadi na thamani kubwa kuliko mauzo yote ya hatifungani yaliyowahi kufanyika hapa nchini, ambapo jumla ya wawekezaji 2,264 wameweza kushiriki .Kati ya wawekezaji hao ,wawekezaji 2,253 ni wawekezaji wadogo sawa na asilimia 99.5 wakati wawekezaji 11 ni kampuni.

"Hatua hii ni muhimu kwani imewapatia fursa wawekezaji wadogo wadogo ambao ndio idadi kubwa ya wananchi kuwekeza katika masoko ya mitaji kupitia hatifunfani hii.Aidha kati ya wawekezaji hao , wawekezaji 1,381 wanatoka nje ya Jiji la Dar es Salaam , sawa na asilimia 61 ya wawekezaji wote.Idadi hii inajumuisha wawekezaji kutoka mikoa ya kanda zote nchini,"amesema.

Ameongeza kupitia mauzo hayo , masoko ya mitaji yamefanikiwa kupata wawekezaji wapya, ambapo kati ya wawekezaji 2,264, wawekezaji wapya ni 1,358, sawa na asilimia 60.Hatua hiyo ni muhimu kwani imeongeza idadi ya wawekezaji katika masoko ya mitaji na kuchangia utekelezaji wa mpango jumuishi wa huduma za kifedha hapa nchini.

"Fedha zilizopatikana kupitia mauzo hayo toleo hili zitatumika kugharamia shughuli za maendeleo ya benki ya NMB , ikiwa pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa kampuni ndogo na za kati za ujasiriamali pamoja na wawekezaji wadogo wadogo yenye lengo la kukuza na kuendeleza ujasiriamali nchini.

"Hatua hii ni muhimu kwani inatarajiwa kuwa na matokeo chanya katika ukuaji wa sekta binafsi na uchumi wa nchi kwa ujumla na hivyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuinua wananchi wenye kipato kidogo.Tunashukuru sana benki ya NMB kwa mikakati hii ya kuunga juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano,"amesema Mkama.

Pia amesema uorodheshwaji wa toleo la tatu la hatifungani ya NMB katika soko la hisa unawapatia fursa wawekezaji kuuza hatifungani zao pale wanapohitaji fedha kwa ajili ya matumizi mengine , kujua thamani halisi ya hatifungani zao na kuwapatia fursa wawekezaji wapya kununua hatifungani hizo ambapo wawekezaji hao hupata riba kama faida itokanayo na uwekezaji huo.

Mkama ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wadau wote wa masoko ya mitaji kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana katika kutekeleza mikakati ya kuendeleza masoko ya mitaji nchini ikiwemo kuleta bidhaa mpya katika masoko hayo ambazo zitaweza kuorodheshwa katika soko la hisa ili pamoja na mambo mengine kuwapatia wawekezaji taarifa mbalimbali kuhusu bidhaa hizo ikiwemo bei kwa namna iliyo wazi.

Kwa upande wake Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema "Leo tupo hapa kwa ajili ya tukio muhimu la kuorodheshwa hatifungani ya NMB ambayo tulipata idhini ya kuuza kwa wananchi yenye thamani ya Sh. bilioni 25.

"Leo hii tunafurahi kuwa hapa na wenzetu wa soko la hisa Dar es Salaam na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) kuorodhesha rasmi kwa asilimia 100 fedha zote tulizozipata kutokana na mauzo ya hatifungani ya NMB.Mauzo ya toleo la tatu la hatifungani ya benki ya NMB yalifunguliwa Juni 10 ,2019 na kufungwa Julai 8 ,2019 ambapo benki ya NMB ilifanikiwa kukusanya Sh.bilioni 83.3 ikilinganishwa na Sh.bilioni 25 zilizotarajiwa kukusanywa,"amesema.

Zaipuni amefafanua kwa taarifa tu hatifungani hiyo imepokea maombi 2264, kati ya maombi hayo ni maombi 14 tu ndio yamepita kwa madalali wa soko la hisa , maombi mengine 2250 wameyapokea kupitia matawi ya NMB na kwamba hilo ni jambo la kujivunia wao kama benki.

"Hii ni mara ya kwanza kwa hati fungani kupata mafanikio makubwa namna hii katika historia ya masoko ya mitaji nchini, hii inadhihirisha imani kubwa ya wawekezaji waliyonayo kwetu.Tunawashukuru Watanzania kwa kutuamini na kutuweka kuwa benki namba moja kwenye masoko ya mitaji,"amesema na kuongeza kwa niaba ya menejimenti ya NMB anatoa shukrani za dhati kwa taasisi zote zilizofanikisha uuzwaji wa toleo la tatu la hatifungani ya NMB.

Wakati huo huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) Moremi Marwa amesema anawapongeza NMB kwa mafanikio ya hali ya juu ambayo yamepatikana na ndio yamesababisha kuwepo kwa shughuli hiyo ya leo ya uoredheshwaji wa hatifungani ya NMB baada ya kuuzwa katika mnada wa awali ikiwa ni sehemu ya programu ya uuzaji wa hatifungani za benki hiyo ikiwa na thaman ya Sh.bilioni 200.

"Hatifungani ambayo tunairodhesha ni toleo la tatu katika programu hiyo ya Sh.bilioni 200.Katika hatufungani hii NMB walitarajia kupata Sh.bilioni 25 lakini makusanyo ambayo wameyapata ni mara tatu zaidi. Hivyo mafanikio hayo ni jambo kubwa na sio tu kwa NMB bali kwa wote walioko kwenye masoko ya mitaji na dhamana pamoja na sekta ya fedha kwa ujumla,"amesema. 
  OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama akigonga kengele mbele ya Waandishi wa habari na Wageni waalikwa  kuashiria kufungua uuzaji wa Hisa,wakati wa hafla fupi ya kuorodheshwa kwa toleo la tatu la hatifungani ya Benki ya NMB katika Soko la Hisa Dar es Salaam,iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.Pichani anaefuata ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) Moremi Marwa ,Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna,Mwenyekiti wa Bodi benki ya NMB,Prof. Joseph Semboja na kushoto ni Ofisa wa Soko la Hisa Dar es Salaam,Emmanuel Nyalali.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media.
 OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari wakiwemo wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani). waliofika kwenye hafla fupi ya kuorodheshwa kwa toleo la tatu la hatifungani ya Benki ya NMB katika Soko la Hisa Dar es Salaam, ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mauzo ya toleo la tatu la hatifungani ya benki ya NMB yameweka historia kubwa katika maendeleo ya masoko ya mitaji hapa nchini.
 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna akizungumza mbele ya Waandishi wa habari wakiwemo wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika kwenye hafla fupi ya kuorodheshwa kwa toleo la tatu la hatifungani ya Benki ya NMB katika Soko la Hisa Dar es Salaam,  "Leo hii tunafurahi kuwa hapa na wenzetu wa soko la hisa Dar es Salaam na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) kuorodhesha rasmi kwa asilimia 100 fedha zote tulizozipata kutokana na mauzo ya hatifungani ya NMB,amesema.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) Moremi Marwa akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari na Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaa.Marwa amewapongeza NMB kwa mafanikio makubwa waliyoyapata 
"Hatifungani ambayo tunairodhesha ni toleo la tatu katika programu hiyo ya Sh.bilioni 200.Katika hatufungani hii NMB walitarajia kupata Sh.bilioni 25 lakini makusanyo ambayo wameyapata ni mara tatu zaidi. Hivyo mafanikio hayo ni jambo kubwa na sio tu kwa NMB bali kwa wote walioko kwenye masoko ya mitaji na dhamana pamoja na sekta ya fedha kwa ujumla,"amesema.
 Wageni waalikwa mbalimbali  wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla fupi ya kuorodheshwa kwa toleo la tatu la hatifungani ya Benki ya NMB katika Soko la Hisa Dar es Salaam,Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar. 
 Picha ya pamoja.

Serikali, PS.3 Wapongezwa Misungwi

$
0
0
Maafisa kutoka Sekta ya Afya na Mipango kwenye Halmashauri ya Misungwi wakiwa katika zoezi la uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa iMES.
Wataalam katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wakijadiliana wakati wa zoezi la majaribio la uingizaji wa taarifa za sekta mbalimbali kwenye mfumo wa iMES.
************

Na. Atley Kuni

Watendaji katika Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza wamepongeza juhudi zilizochukuliwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI pamoja na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma nchini PS.3, kufuatia kukamilisha uundwaji wa mfumo jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathimini (integrated Monitoring and Evaluation System- iMES)ambao utawezesha kupata taarifa na takwimu katoka jukwaa moja.

Pongezi hizo zimekuja wakati huu ambao Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwakushirikiana na Wizara za kiseta pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini USAID, kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma nchini kukamilisha utengenezaji wa mfumo wa iMES ambao unalengo lakutatua tatizo la upatikanaji wa taarifa na takwimu kwaajili yakufanya maamuzi kwenye mipango ya maendeleo.

Akiongea wakati wa Majaribio ya Mfumo huo, Mwalimu Meshack Chaula, ambaye amekuwa kwenye dawati la takwimu katika Halmashauri ya Misungwi kwa kipindi cha Mwaka mmoja, amesema hapo awali walikuwa na kasoro ndogo ndogo za kimfumo hasa kutokana na kutokuwepo kwa jukwaa moja ambalo lingekuwezesha kuona takwimu zakutoka sekta nyingine lakini sasa iMES imekuja kutoa suluhu.

“Lazima tukiri kuwa, Serikali inafanya kazi nzuri na katika hili tunajionea kazi kubwa katika mifumo mbalimbali, sote tunajua tatizo la taarifa na takwimu katika nchi yetu, mfano mdogo ni hapa katika Halmashauri yetu tuliletewa fedha za kukamilisha maboma ya vyumba vya madarasa mawili kwa kila shule, lakini katika ile orodha iliyokwenda ngazi za juu zilikuwepo shule mbili hazikuwa na sifa za vyumba viwili, suala hili lilitokana na kutokuwa na dashboard moja ya taarifa, alisema Chaula.

Mbali na kupongeza, wataalam hao wanaiona iMES kuwa Mfumo utakao mrahisishia mtumaji wa taarifa pindi zinapo hitajika muda wowote, kutokana na kwamba ni web Based system.

“Kwa iMES, unaweza kutuma taarifa hata ukiwa njiani ili mradi uwe na kifurushi cha mtandao kwenye kishkwambi au simu janja yako” anasema Chaula na kusisitiza kuwa, kuna wakati mtu anaombwa taarifa akiwa hajajiandaa, hivyo baadhi ya taarifa zikawa zinatumwa bila usahihi kutokana kuwa na vyanzo tofauti tofauti lakini kwakuwa sasa taarifa zote zitapatikana kwenye jukwa moja ni imani yetu kukinzana kwa takwimu hakutakuwepo.

Kwa upande wake, Katibu wa Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi bibi Swaiba Ngulugulu pamoja na kupongeza, yeye ameelekeza maombi yake kwa watengenezaji juu ya taarifa za mfumo wa DHIS-2 na mifumo mingine kama FFARS na Epicor kuvutwa katika mfumo wa iMES ili kuondoa kujirudiarudia kwa ujazaji wa takwimu, alisema Swaiba.

“Tutafarijika kuona takwimu za Mifumo mingine zinavutwa moja kwa moja kwakuwa mambo mengi tunayo yajaza ni yale yale tu, mfano taarifa za fedha, taarifa watumishi, kwakutaja kwa uchache.” alihitimisha Swaiba. 

Mkoa wa Mwanza na Halmashauri zake za Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, zimekuwa Halmashari za mwanzo kabisa kuanza kuutumia mfumo ambapo jumla ya watumiaji 63 kutoka sekta tofauti tofauti wamewezeshwa kuanza kuutumia mfumo wa iMES.

WATUMISHI WA BUNGE WACHAGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI BUNGENI

$
0
0
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Ndg. John Mchenya akiongea na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia jambo kwa makini Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).
Mtumishi wa Ofisi ya Bunge Ndg. Frank Ngonyani akichangia jambo mbele ya kikao cha Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images