Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

NDUGU WA MTANZANIA ALIYEFIA AFRIKA KUSINI WANATAFUTWA

$
0
0
 Watanzania waishio Johannesburg wanawatafuta ndugu, rafiki au jamaa wa Shiraz Abeid Juma (pichani), ambaye sasa ni marehemu. Shiraz alifariki wiki hii na kuzikwa siku ya Jumanne huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Marehemu alifika Afrika Kusini akitokea eneo la Mpendae kule Zanzibar kama nyaraka alizoacha zinavyoonyesha. Namba za simu zilizokuwa kwenye vitabu vya marehemu hazipatikani. Kwa yoyote mwenye kumfahamu marehemu, tafadhali wasiliana na Abdallah Hussein +27 71 216 8505.



MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA

$
0
0
Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu  akisoma historia ya marehemu Mteming'ombe huku naibu katibu mkuu  CCM Bara Bw Mwigulu Nchemba akionyesha kufuta machozi
Mjane  wa Mteming'ombe akiweka maua
Mzee Mteming'ombe akiweka shada la maua
Naibu katibu mkuu CCM Bara  Mwigulu Nchemba  akiongoza  waombolezaji kuweka shaba la maua  katika kaburi la aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa marehemu Emanuel Mteming'ombe leo katika makaburi ya RC Rujewa Mbarali Mbeya
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  akiweka shada la maua
mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr Ishengoma  akiweka  shada la maua
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TCRA YAWAFUNDA WAANDAAJI WA VIPINDI NA WATANGAZAJI WA REDIO KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi, Injinia Magreth Munyagi amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha watangazaji kuhusu kufuata maudhui yaliyokusudiwa yanayoelimisha na kuburudisha jamii na kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Kushoto ni Mgeni rasmi wa Warsha hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha, na kulia ni mjumbe wa Bodi ya TCRA, Bw. Joseph Mapunda

Mgeni rasmi wa Warsha hiyo, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amesema kukiuka kwa maadili katika baadhi ya vituo vya utangazaji kunatokana na wamiliki kuwaajiri wafanyakazi wasiokuwa na taaluma ya Utangazaji. Kushoto ni mjumbe wa Bodi ya TCRA Bw. Walter Bgoya.


Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo.

TANZANIAN CONJOINED TWINS SUCCESSFULLY SEPARATED AT TAIL END OF THEIR SPINES AT APOLLO HOSPITA,L CHENNAI, INDIA

$
0
0
Ericana and Eluidi with their Mother Grace 

Mwakyusa before separation surgery


The conjoined Tanzanian twin boys, Ericana and Eluidi Mwakyusa, who were referred to Apollo Children Hospital in Chennai, India for surgery by Ministry of Health and Social Welfare, Tanzania on June, 2013, now sleep in separate hospital beds in the Pediatric Critical Care Unit of Apollo Hospital’s Vanagaram facility after successful major separation surgery which was done on 16th December, 2013.

They are able to do so after nine months, thanks to the efforts of 20 surgeons and an equal number of hospital staffs of Apollo hospital Chennai who made this happened.

These types of Conjoined twins, though rarely encountered, are seen in one in 200,000 deliveries. However, more than 60% of them are stillborn while 35% of the remaining die within a few days or months of birth due to various causes. Conjoined twins can be joined at the chest, abdomen, back, buttock and head. Fusion at the buttocks (Pygopagus) is very rare and accounts for less than 17% of all conjoined twins.

 Live born Pygopagus twins are usually female in sex while male pygopagus twins are extremely rare. Till now in medical literature, only 30 sets of Pygopagus twins have been reported out of which 26 were female and only four were male.
 The nine-month-old pygopagus twins boy (conjoined at the end of the spine), were born at Kasumulu in Kyela, Mbeya Region. The twins’ spines were fused at the base, and they shared a single anus and rectum.

The twins were referred to Muhimbili National Hospital in Dar es Salaam, which in turn sought help from the Government through the Ministry of Health and Social Welfare (MOHSW), which then  the MOHSW, referred the twins to Apollo Children’s hospital in Chennai India for further evaluation and management.

KAMANDA WA FFU UGHAIBUNI RAS MAKUNJA USO-KWA-USO NA ANKAL LEO, WAPEANA ZAWADI...

$
0
0
 Ankal akimkabidhi zawadi ya Krismasi  na kadi Kamanda wa FFU Ughaibuni The Ngoma Africa Band ya Ujeruman, Ras Ephraim Makunja, a.k.a Field Marshal wa jamii ya Annunaki walipokutana leo katikati ya jiji la Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya faragha ya saa moja katika kiota cha Break Point cha mjini. Katika mazungumzo yao waliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza undugu uliopo baina ya Globu ya Jamii na FFU Ughaibuni, na kupanga tarehe ambazo The Ngoma Africa Band itakuwa huru kuja kufanya maonesho kadhaa nchini Tanzania.
 Ras Makunja anarivenji kwa kumkabidhi Ankal zawadi ya moja ta T-Shirt kibao alizomletea zikiwa na logo ya Globu ya Jamii.
 Ankal akimshukuru Ras Makunja kwa zawadi hiyo mwanana
Ras Makunja akiwa na mjomba wake akijiondoa eneo la tukio taratibu huku kakumbatia zawadi yake ya Krismasi na kadi. Meno yote arobaini yako nje kwani hakutegemea kupata heshima hii. Picha kwa hisanio ya mpiga picha wa The Ngoma Africa Band aliyeongozana naye katika ziara hii ya mapumziko jijini Dar es salaam. Mara ya mwisho kufika Bongo kwa Ras Makunja ilikuwa miaka sita iliyopita, na ameshangazwa na mabadiliko na maendeleo makubwa aliyotaona kila mahali, kuanzia nyumbani kwake mtaa wa Aggrey ambako mbavu za mbwa yao imeshajengwa bonge la Ghorofa, nusura apotee, na huko kwake Segerea ambako anasema kuna lami mpaka jikoni....

Article 3

$
0
0

AIESEC University of Dar es Salaam, is a local branch of AIESEC, an international leadership development organization which runs a global exchange program, entirely driven by students and recent graduates. 
 AIESEC was established over 60 years ago and is present in over 1700 Universities in over 124 countries across the world. What's more, since its foundation, AIESEC has been entirely youth-led. This means every single year, new leadership teams are elected from the membership at every level of the international association.


This means we have over 1,000,000 alumni who've been through an 'AIESEC Experience' many of whom have gone on to do incredible things. Our alumni include leaders within business, global politicians and even a Nobel Peace Laureate. 
 The organization works towards the vision of “peace and fulfillment of humankind’s potential.” The main channel to do this is by providing young students the opportunity to experience living and working in a different culture to understand and appreciate diversity, whilst developing both personally and professionally. 
 AIESEC in Tanzania has sent out more than 300 students in the last 15 years since establishment. These students have worked as volunteers and professionals in over 124 countries worldwide. Students who embark on an exchange with us have a multicultural experience (Global Mindset), self development (they gain skills and competencies that are useful for their career life) and become more social responsible. 
 So, if there are university or college students in Dar es Salaam who want to experience a 6 week volunteering program abroad, or bachelor graduates who want to work abroad, please contact us. Warm Regards, 
Anthony P. 

TAARIFA TOKA TFF LEO DESEMBA 201, 2013

SHAMRASHAMRA YA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA SOPHIA KESSY


BREAKING NYUUUZZZZZZ: Moto wawaka bungeni - mawaziri Nchimbi, Nahodha, Kagasheki na Mathayo waenguliwa

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi  Kagasheki amejiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma hivi sasa. Habari zaidi kwa kirefu zitakuja baadaye.
Hii inatokana na Operesheni Tokomeza iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini. 
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo kuuawa, kupigwa na uporaji.
Operesheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa).
Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, naye pia amegoma jiuzulu baada ya kutoa utetezi wake mrefu. Amedai pia kuwa ameonewa.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki zichukuliwa. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa ameutaja kuwa ni  muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya kuongea na Rais.  mkuu wa nchi ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika awajibike.
Amesema Rais ameshauri
 kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe  James Lembeli (pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa  Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa.
Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu  waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba  kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.
Spika Mhe. Anne Msekwa ameahirisha Bunge (saa tatu na dakika nne usiku huu) hadi saa tatu kesho asubuhi. 

 Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein Afungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu Zanzibar

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Hassan Mshinda,Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania,wakati alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Alex Maharindo, wa Kampuni ya  BR-Solution,ambayo inashuhulika na utoaji wa Taarifa kwa watumiaji wa simu za mikononi, wakati   alipotembelea maonesho katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,
  Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof, Idrisa A.Rai,alipokuwa akitoa salamu zake wakati wa Kongamano la Utafiti na Ubunifu,lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia pichani).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,kulifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua Kongamano la Utafiti na Ubunifu, katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,(wa kwanza kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa,( SUZA), Prof, Idrisa A.Rai, (kushoto) ni Dk.Hassan Mshinda,Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia  Tanzania,akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed,
Baadhi ya wadau mbali mbali walioshiriki katika Kongamano la Utafiti na Ubunifu,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) akitoa hutuba yake wakati alipolifungua leo katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.Picha na Ramadhan Othaman-IKULU-Zanzibar

MAMA REGINA LOWASSA ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akishiriki kuhudumia chakula watoto wenye ulemavu  katika Kituo cha Huduma ya Walemavu kinachomilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki jijini Arusha kilichopo Monduli wakati alipokwenda kushiriki nao Ibada ya X-Mass pamoja na kuzungumza na kula nao chakula cha mchana.

MKOA WA SIMIYU WAPATA MPANGO WA KUJIANDAA KUKABILI MAAFA MKOANI SHINYANGA OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA KUTOA

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Pascal Mabiti akimhakikishia  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba jinsi mkoa huo utakavyo tekeleza Mpango Wa Kujiandaa Kukabili Maafa katika mkoa wa  Simiyu, wakati wa uzinduzi wa mpango huo jana.

 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Pascal Mabiti akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi  Mpango Wa Kujiandaa Kukabili Maafa katika wilaya hiyo, wakati wa uzinduzi wa mpango huo  Wilayani Bariad jana (kulia) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Pascal Mabiti (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka mkoa wa Simiyu mara baada ya uzinduzi  jana Mpango Wa Kujiandaa Kukabili Maafa katika mkoa wa  Simiyu (wan ne toka kushoto) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Lut Jen (Mst) Sylivester Rioba.

mdau Khalid Ubwe Rubama alamba nondozzzzz

$
0
0

Mdau Khalid Ubwe Rubama akifurahia na familia yake baada ya kulamba nondozzzz ya Masters ya Utawala Chuo Kikuu cha Mzumbe University , Dar es salaam Campus, jana. Khalid ni mmoja wa wadau wakuu wa Globu ya Jamii ambaye mchango wake wa mawazo umekuwa na faida sana katika kuendeleza Libeneke. Hongera sana Khalid!

Bondia Alibaba wa Kilimanjaro atamba kumpiga Kaseba kwa KO

$
0
0
Bondia Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro (shoto) akizungumza na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Bondia Japhet Kaseba litakalo fanyika kesho.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

BONDIA Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro ametamba kumpiga kwa Knock out (KO) bondia Japheth Kaseba wa jijini Dar es Salaam.

Alibaba alitoa kauli hiyo jana muda mfupi kabla ya kupanda gari kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya shughuli ya kupima afya na uzito itakayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner leo saa 4 kuelekea mpambano wao wa kesho.

Akizungumza kwa kujiamini Alibaba amesema amaefanya maandalizi ya kutosha na yuko tayari kuwashangazza mashabiki wa mchezo huo watako jitokeza katika kushuhudia mpambano huo hiyo kesho.

Pambano hilo linalofanyika kwa uratibu Ibrahim Kamwe wa Kampuni ya Bigright Promotions ya Dar es Salaam kwa kivuli cha PST, litasindikizwa na mengine sita likiwemo la Karage Suba na Fadhili Awadh ‘Tiger’ katika uzani wa welter kg 66 watakaozichapa kwa raundi kumi.

Akizungumzia pambano hilo la kesho, Kamwe amesema wengine watakaopima uzito leo ni Mbarouk Heri atakayezichapa dhidi ya Lusekelo Daudi na Issa Omar Nampepeche ataoneshana kazi na Hassan Kiwale ‘Moro Best.’

Naye Zumba Kukwe atazichapa na Jacob Maganga; Adam Yahya vs Harman Shekivuli, Jocky Hamis v Mbena Rajab, Ernest Bujiku na Shah Kasim, Shaban Kitongoji v Mwinyi Mzengela, Shaban Manjoly v Kassim Chuma.

Aidha, bondia mwingine wa Tanzania anayeishi nchini Canada, Kareem Kutch, atacheza na Tata Boy kwa pambano la kimataifa la Kickboxing la raund tano.

BONDIA LULU KAYAGE AJIFUA KUMKABILI Mariam Abdallah DESEMBA 25

$
0
0
Bondia Lulu Kayage kushoto aki oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Kayage anajiandaa na mpambano wake na Mariam Abdallah utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner hotel wakisindikiza mpambano wa Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani 
Bondia Lulu Kayage kushoto aki oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamisi Belege wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Ilala Kayage anajiandaa na mpambano wake na Mariam Abdallah utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner hotel wakisindikiza mpambano wa Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani.

Picha na Habari na  Super D
Akizungumzia mpambano huo Lulu Kayage amesema kuwa: "Mimi nafanya mazoezi mwaka mzima niwe na mechi niwe sina mechi. Hivyo nipo fiti wakati wowote kucheza mpambano huo kwani mimi kwa sasa ndie nataraji kuwa bingwa kwa upande wa wanawake.

"Hivyo wanawake wanaoweza kuhimili vishindo vya mchezo wa masumbwi wajitokeze ili kuleta changamoto ya mchezo huo unaopendwa na watu wengi duniani wakiwemo wanawake.

"Unajua mimi naiga staili ya Leila Ali ambaye alikuwa bingwa wa mchezo wa masumbwi duniani na mpaka sasa amestaafu bado ana heshimika hivyo nataka nifate nyayo zake hivyo naomba mashabiki wengi wajitokeze waje kutuunga mkono na kututia moyo wa kuendelea kuupenda mchezo wa masumbwi", Alisema Lulu.



Naibu waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dk Seif Rashid afunga kambi ya watoto ya Ariel 2013 Kilimanjaro

$
0
0
 Mgeni rasmi katika siku ya ufungaji wa kambi ya watoto iliyofanyika mjini Moshi naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii ,Dk Seif Rashid akimlisha keki mmoja wa watoto waliokuwa katika kambi hiyo kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita.
 Mgeni rasmi katika siku ya ufungaji wa kambi ya watoto iliyofanyika mjini Moshi ,naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii ,Dk Seif Rashid akitoa zawadi ya vifaa vya shule kwa mmoja wa watoto walioshiriki kambi hiyo kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita.
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii ,Dk Seif Rashid akitoa hotuba yake kwa watoto walioshiriki kambi hiyo kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita.
 Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii ,Dk Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na walezi wao.
Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii,Dk Seif Rashid akicheza na watoto wakati wa  kufunga kambi ya watoto iliyofanyika Uhuru hotel mjini Moshi. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

TAARIFA RASMI YA DKT. REGINALD A. MENGI MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED YENYE KUJIBU MAELEZO YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA MUHONGO KUHUSU HODHI YA VITALU

$
0
0
Dkt. Reginal Mengi
---
Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania. Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.

Ningependa kuwaeleza Watanzania 
wenzangu yafuatayo: BOFYA HAPA

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA KUHUSU TATHMINI YA MATATIZO YALIYOTOKANA NA OPARESHENI TOKOMEZA

NANI KUWA MTANI JEMBE,KATI YA SIMBA NA YANGA UWANJA WA TAIFA LEO??

$
0
0
 Mashabiki wa Timu ya Yanga wakishangikia kwa shangwe hivi sasa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya kukutana kwa Timu mbili kubwa hapa nchini ambazo ni Simba na Yanga.Mtanange huu wa leo ni wa Kumsaka Mtaji Jembe kati ya Timu hizo mbili. Watu mbali mbali ambao ni wapenzi wa soka bado wanazidi kuingia uwanjani hivi sasa.Timu ya Globu ya Jamii iko Uwanjani hapa hivi sasa na itakuwa ikikuletea matukio kedekede yanaendelea kuanzia sasa mpaka mwisho wa mchezo huu.
 Mashabiki wa Timu ya Simba nao hawako nyuma kwenye kuisapoti timu yao.
 Hadi hivi sasa hali ya Mashabiki uwanjani hapa iko namna hii kwa upande wa Yanga.
Na kwa Upande wa Mashabiki wa Simba Mambo yako namna hii.
Hii ndio LineUp ya leo kama inavyosomeka hapa.

SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA TOKA GLOBAL PUMLISHERS

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images