Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA HOSPITALI NA SHULE KUTOKA TAASISI YA HELPING HAND NA BENKI YA NMB

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaa mbalimbali vya hospitali vilivyotolewa na Taasisi ya Helping Hand na Taasisi ya Jamii Bora kwa ajili ya Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa, kwenye viwanja vya Zahanati ya Nandagala wilayani humo, Julai 28, 2019. Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jamii Bora, Yassir Salim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salum Tahir (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Helping Hand kuhusu vifaa mbalimbali vya hospitali alivyokabidhiw na Taasisi ya hiyo kwa ajili ya hospitali, zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa. Mahakabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo (wapili kulia) kuhusu kompyuta na madaftari kwa ajili ya shule wilayani Ruangwa pamoja na madirisha ya aluminium na milango kwa ajili zahanati ya Nandagala . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala Julai 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya hospitali kutoka Taasisisi ya Helping Hand vyenye thamani ya sh. Milioni 250 pamoja na madirisha ya aluminium, milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala, julai 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kupokea madirisha ya aluminium na milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala,Julai 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NGOs KANDA YA KASKAZINI ZAITWA KUJISAJILI

$
0
0
Msemaji wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Erasto Ching’oro (kushoto) pamoja na wakizungumza na vyombo vya habari kuhusu zoezi la uhuishaji Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kilimanjaro kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kilimanjaro Bi Hilda Lauo
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

***************

Na Mwandishi Wetu. Kilimanjaro

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Kanda ya Kasikazini yamehimizwa kujitokeza kwa wingi ikiwa ni mwendelezo wa uhuishaji wa Mashirika yaliyosajili awali kwenye chini ya Sheria nyingine lakini zinafanya kazi za kijamii hivyo kutakiwa kusajili kwa Sheria ya NGOs kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.3 ya Mwaka 2019.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mkoani Kilimanjaro Msemaji wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Erasto Ching’oro amesema zoezi hilo litafanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro kuanzia tarehe 29, July hadi tarehe 6 Augosti 2019 ili kutoa fursa kwa wadau wa Mashirika yaliyoko Mikoa ya Kasikazini kufanya usajili kwa haraka lakini ikiwa ni nia njema ya Serikali kupeleka huduma karibu na Wananchi.

Bw. Ching’oro ameongeza kuwa NGOs zote zinazofanya kazi za kijamii ambazo awali usajili wake ulifanyika katika Mamlaka nyingine kama RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na BRELA usajili wake utakuwa umefutwa kama zitashindwa kujisajili chini ya Sheria ya NGOs kama iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 katika kipindi cha miezi miezi miwili toka tarehe 01 Julai, 2019.

“Sheria inayataka Mashirika hayo kujisajili katika Sheria ya NGOs kwa kipindi cha miezi miwili hivyo huu ni wakati wa Mashirika kujitahimini yako wapi ili yaweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kipindi kilichotolewa na Sheria hii kupita.’’ Alisisitiza Bw. Ching’oro

Bw.Ching’oro amesema usajili huu unafanyika kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na kutoa wito kwa Mashirika yaliyopo katika Mikoa hiyo kufanya usajili huo akiongeza kuwa zoezi hili linafanyika bila malipo kwa Mashirika yanayouhisha usajili lakini Mashirika yanayojisajili mara ya kwanza yanatoa malipo kwa ajili ya huduma hiyo.

Aidha Msajili Msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro Bi Hilda Lauo ameyataka Mashirika Mkoani Kilimanjaro kuhakikisha yanashiriki usajili huu kwani baadhi ya Mashirika Mkoani humo yamekuwa yakitoa huduma za kijamii wakati yakiwa yamesajili katika Sheria nyingine.

“Kuna Mashirika hapa Mkoani yanatoa huduma za Mikopo kwa jamii lakini ukiongea nao wanakwambia tumesajili Brela wakati huduma wanazotoa ni za kijamii hivyo nivyema wafike kwa ajili ya kufanya usajili kwa mujibu wa sheria mpya” alisema Bi. Hilda.

Zoezi hili la usajili limeanza tangu tarehe 10 mwezi huu Jijini Dar es Salaam ambapo asilimia 80 ya NGOs zilizoko Kanda ya Mashiriki zimefanya usajili wake na zoezi la usajili linaendelea kwa kipindi cha miezi miwili kama ilivyo matakwa ya sheria. 

KUMEKUCHA USAJILI KANDA YA KASKAZINI

WAZIRI LUGOLA AMVUA MADARAKA MKUU WA USALAMA BARABARANI MKOA WA ARUSHA, ATOA ONYO KALI KWA MA-RTO MOROGORO NA MARA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiikagua
pikipiki katika Kituo cha Polisi Malinyi, Mkoani Morogoro, leo,
ambayo imepata ajali na kusababisha dereva wa pikipiki hiyo
kufariki dunia. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Majura
Kasike, na Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi, ASP Evaristi
Makalla. Majura kasika Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimpa
maelekezo Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Malinyi, Mkoani
Morogoro, SSP Ramadhan Fusi (kulia), wakati alipofanya ziara
Wilayani humo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza
katika mkutano wa hadhara na wananchi Wilayani Malinyi,
Mkoani Morogoro, leo. Lugola amemuondoa madarakani Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), na
kamwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara yake, kumchukulia hatua
za kisheria kwa kutokufuata maagizo anayoyatoa Waziri huyo
na kuyaita ni yakisiasa. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
*************

Na Felix Mwagara, MOHA-Malinyi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuondoa
madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa kosa la kuyapuuza
maagizo yake na kuyaita ya kisiasa.

Licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo, Waziri Lugola
amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, kumchukulia hatua
kali za kinidhamu RTO huyo ili iwe fundisho kwa matrafiki hao
wa mikoa nchini.

Lugola amesema RTO huyo ameshuhudia katika video ambayo
ilikua inasambaa mitandaoni akiwa katika mkutano jijini
Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na pia
kutokuyatekeleza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mji
wa Malinyi, Mkoani Morogoro, leo, Lugola amesema yeye hatoi
maagizo ya kisiasa bali anatoa maagizo yatakayomsaidia rais
kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na
umaskini na ajira.

“namuagiza katibu Mkuu achukue hatua za kinidhamu ikiwa ni
pamoja na kumuondoa u-RTO afanye shughuli zingine za
kipolisi, na maRTO ambao mkono wangu haujafika kwenu, na
wengine nimeanza kuwaona hamsimamii vizuri maagizo yangu,
wapo ambao wanaendelea na uonevu, wapo baadhi ya askari
wanaendelea kuchukua rushwa barabarani,” alisema Lugola.

Pia Waziri Lugola ametoa onyo kali kwa MaRTO Mikoa ya
Morogoro na Mara akiwataka wachukue fursa ya kujitathimini
katika utendaji wao kabla hajawachukulia hatua.

“Wapo baadhi ya askari waonevu, wanaendelea kuchukua
rushwa, wajitathimini, katika utendaji wao kabla sijawachukulia
hatua kali za kinidhamu,” alisema Lugola.

Lugola katika hotuba zake katika mikutano yake mbalimbali
alisema Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na haitaki
kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki
wasiokuwa waaminifu.

Lugola alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi nchini, kuwa
bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo
katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika
kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika
katika ajali.
“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini
kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo,
napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,”
alisema Lugola.

Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Malinyi na
Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani
zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya
mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa.

Pia Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari
Polisi hapa nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za
Jeshi, anasema kwa kufanya hilo kunaleta kero kwa madereva
na pia anayekamatwa anaweza akadhaniwa kuwa ni jambazi.

Lugola anaendelea na ziara yake mkoani Morogoro, na
anatarajia kumaliza ziara hiyo Wilaya ya Ulanga Mkoa humo
Julai 29, 2019.

WACHIMBAJI MADINI WILAYA YA IKUNGI MKOANI SINGIGA WAOMBA WAWEKEZAJI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh. Elibariki Kingu (katikati) akiangalia usafishaji wa dhahabu kwa kutumia mashine duni ya Wachimbaji wa Kata ya Muhintiri alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea machimbo hayo yaliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh. Elibariki Kingu (katikati) akiangalia mawe yenye dhahabu akiwa na wachimbaji wadogo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh. Elibariki Kingu (kushoto) akiangalia mchanga wenye dhahabu baada ya kusafishwa.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mh. Elibariki Kingu (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa wachimbaji wadogo wakiwa eneo la machimbo.
Wachimbaji wadogo wakiwa eneo la machimbo na Mbunge wao.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WACHIMBAJI wadogo wa madini wa Muhintiri Mining Cooperative Society Ltd wamewaomba wawekezaji ambao watashirikiano nao kuchimba dhahabu katika kata hiyo.

Ombi hilo walilitoa jana wakati wakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu alipofanya ziara ya siku ya kutembelea mgodi wa uchimbaji wa madini uliopo Kata ya Muhintiri katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Akizungumza mbele ya Mbunge Kingu, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa wilaya hiyo, Selemani Dule alisema wanahitaji wawekezaji ambao watashirikiana nao katika kazi.

" Mheshimiwa Mbunge katika mgodi huu tunatumia zana duni za uchimbaji tunaomba ututafutie wawekezaji ambao watasaidia tuwe na uchimbaji wa kisasa" alisema Dule.Akizungumzia changamoto waliyonayo katika mgodi huo alisema ni uchimbaji holela ambapo walimuomba Kingu awasaidie kupata wataalamu kwa ajili ya kupima ili kuyabaini maeneo yenye dhahabu ili kuwarahisishia uchimbaji.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni mawe yenye dhahabu kuwa ndani ya mto Muhintiri ambao watu wa mazingira waliwashauri waupitishe eneo lingine ili wao waendelee na uchimbaji kwenye eneo hilo.

Mchimbaji mdogo wa eneo hilo Moses Mussa alisema changamoto kubwa waliyonayo ni kuondolewa na mtutu kwenye maeneo wanayoyagundua yana madini na kuchukuliwa na wakubwa ambao hakufafanua ni akina nani.

"Tukigundua madini yalipo wakubwa huwa wanakuja na askari polisi na kutuondoa kwa mtutu jambo ambalo linaturudisha nyuma kiuchumi" alisema Mussa.Baada ya kusikia changamoto hizo za wachimbaji hao Kingu aliwaahidi kuzifikisha kwa wahusika ili kuzitafutia ufumbuzi.

NAIBU SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AWAAGA MADAKTARI WA KICHINA ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Meneja wa kitengo cha maradhi yasioambukiza Omar Mwalim Omar akizungumza katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.
Mgeni Rasmi Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma akitoa hotuba kuhusiana na maradhi ya shingo ya kizazi katika hafla ya kuwaaga wafanyakazi 18 wa kichina waliokuwa katika Mradi wa awamu ya Pili ya Upimaji na utibabu wa Maradhi ya Shingo ya Kizazi hafla iliofanyika Katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Zanzibar.

******

Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 28/07/2019

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amesema Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Zanzibar umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kugundua maradhi mbali mbali ya akinamama na kupatiwa tiba

Amesema wananchi wengi walijitokeza na kufanyiwa uchunguzi huo na baadhi waliweza kugunduliwa na tatizo hilo.

Hayo aliyasema wakati wa kuwaanga na kuwatunuku vyeti Timu ya Madaktari kutoka jimbo la Jiangsu nchini China pamoja na Madaktari na Wauguzi wa ndani ambao wamemaliza mradi wa awamu ya pili wa kutoa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi Zanzibar.

Amesema wananchi waliofanyiwa uchunguzi katika zoezi hilo jumla ya watu 5181 walichunguzwa wagonjwa 72 wamegunduliwa wako katika saratani ya hatua ya awali 15 hatua ya kiwango cha juu ambao wametakiwa wapelekwe ocean road kwa kupatiwa mionzi na wagonjwa saba wamefanyiwa upasuaji na 27 wanahitaji kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya mnazi mmoja .

Waziri huyo alisema kupima afya ni jambo la muhimu kwa kila mmoja wetu kwani kunasaidia kugundulika kwa maradhi mapema na kupatiwa tiba na kupona kwa haraka .

Aidha alisema saratani ya shingo ya kizazi Tanzania inaongoza kuwa na idadi kubwa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki takwimu zinaonyesha kati ya watu elfu 35 hupata kensa ya shingo ya kizazi kwa kila mwaka kati ya hao asilimia 20 tu ndio hufika hospitali na kupatiwa matibabu.

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma amewataka wananchi kuzitumia fursa zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za uchunguzi wa afya katika maradhi mbali mbali ambayo zinatolewa na wataalamu katika Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja .

“Tunatakiwa kufanya uchunguzi wa kiafya hasa sisi akinamama tujichunguze saratani ya matiti ,chingo ya kizazi na hata Tenzi dume kwa akinababa ili tuweze kujigundua matatizo mapema kuliko maradhi mgonjwa yeshamuathiri “alisema Naibu Spika

Naibu huyo amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea huduma ya matibabu kwa lengo la kufanikisha Taifa lenye wananchi wenye afya bora .

Naibu Spika aliitaka timu hiyo kuendelee kutoa misaada yao ya huduma za kiafya kwa Serikali ya Zanzibar ili kuweza kuwapatia wafanyakazi wa afya ujuzi wa kitaalamu wa kuweza kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wao .

Nae Mkuu wa Kitengo cha Maradhi Yasiyoambukiza Omar Mwalim amesema shughuli za upimaji zimekwenda vizuri na madaktari na wauguzi wameweza kuengeza ujuzi wa kazi zao na kufikia malengo yaliyohitajiwa.

Aliitaka Wizara ya Afya kuvungua kitengo maalum cha uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ii kuweza kupungua tatizo hili na kuondoka kabisa .

Kwa upande wa Mratibu wa Madaktari kutoka China Jasmine Qi Xiaomin alisema uchunguzi wa maradhi ya saratani ya kizazi kutasaidia kuwafanya akinamama wawe na afya bora na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa .

Pia aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa mapokezi mazuri katika muda wote wa mwezi mmoja wa kutoa huduma kwa wananchi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja .

THE RUFIJI HYDROPOWER PROJECT

4% YA WANANCHI WAAMBUKIZWA VIRUSI VYA HOMA YA INI

$
0
0
Na WAMJW-DOM

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa miongoni mwa Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wameabukizwa Virusi vya Homa ya Ini aina ya B, hii ni kutokana na Takwimu za Ofisi ya Taifa wa Takwimu 206-2017.

Dkt. Alphonce Chandika amesema hayo leo wakati wa Siku ya Homa ya Ini Duniani ambayo, yenye kauli mbiu ya “Wekeza katika mapambano ya Homa ya Ini “ maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamini Mkapa.

“kati ya wachangiaji damu 307,835 takribani watu 13,613 sawa na asilimia 4.4 walikuwa na maambukizi ya homa ya ini kwa mujibu wa takwimu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)” alisema Dkt. Alphonce Chandika.

Dkt. Alphonce Chandika aliendelea kusema kuwa Mwaka 2017, kati ya wachangiaji damu 233,953 takribani watu 11,417 sawa na asilimia 4.9 walikuwa na maambukizi, aidha asilimia 0.5 ya wachangiaji damu walikuwa na maambukizi ya homa ya ini aina ya C kwa mwaka 2017 na asilimia 0.3 kwa mwaka 2018.

Aidha, Dkt. Alphonce Chandika alisisitiza juu ya kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya athari za ugonjwa wa Homa ya Ini katika jamii na kwa nchi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa Serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kama itawekeza nguvu kwenye kinga, ambacho kinachotumika kwenye matibabu dhidi ya ugonjwa huu wa homa ya ini.

Nae, Mkurugenzi msaidizi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba amesema kuwa huduma hii ya chanjo ya homa ya Ini imeanza kutolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa za Sokoture Mwanza,Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi Kilimanjaro, Hospitali ya Rufaa ya Geita, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Hospitali ya Muimbili, Moi, Ocean Road na vituo vyote vya mipakani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba, na Kulia ni mwakilishi wa WHO anaitwa Dr. Christine Chakanyuka Musanhu .
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akitembelea moja ya banda la kufanyia uchunguzi wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiwajulia hali baadhi ya watu waliojitokeza kufanya uchunguzi homa ya ini, katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya Dkt. Janneth Mghamba. 
Wadau mbali mbali wa Afya wakifuatilia kwa makini taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akiteta jambo na mwakilishi wa WHO Dkt. Christine Chakanyuka Musanhu wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika katika picha ya pamoja na Wadau pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakati wa maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

KUMBUKIZI YA ‘BANZA STONE’.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Mwanamuziki Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ alikuwa mahiri kwa utunzi pia uimbaji wake katika bendi mbalimbali alizowahi kuzifanyia kazi.

Kabla ya kifo chake baadhi ya watu walikuwa wakimzushia kifo mara kwa mara kuwa amefariki dunia.

Lakini uzushi huo ukageuka kuwa ukweli Julai 17, 2015, alipoiaga dunia akiwa nyumbani kwao Sinza jijini Dar es Salaam.

Julai 18, 2015, taratibu zote za dini ya Kiislamu zilifanywa, Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ akawekwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Banza Stone kabla ya kifo chake maradhi makali yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala, kutokana na ugonjwa wa saratani ya ubongo.Aliwahi kuwalalamikia mara kadhaa baadhi ya watu waliokuwa wakimzushia kifo, akisema anajisikia vibaya sana na si jambo jema kuzushiwa kifo.

Banza akizungumza kwa taabu alitamka kwamba alitamani apone ili arudi tena jukwaani, akisema kuwa maombi yao ni muhimu na msaada mkubwa kuliko kitu chochote.Wasifu wa Banza unaeleza kuwa alizaliwa katika hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam, Oktoba 20, 1972 akiwa ni mtoto wa tisa kati ya 11 katika familia yao.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na alifanikiwa kumaliza darasa la saba mwaka 1987. Banza baada ya kumaliza shule, alianza taratibu za kujihusisha na maswala ya muziki akiwa angali mdogo.Alijiunga katika muziki wa Hip Hop uliokuwa ukisikika katika redio.

Masanja aliwahi kunukuliwa akisema kuwa “…mara tu baada ya kumaliza elimu yangu ya msingi, nilianza kujihusishana muziki wa Hip Hop, enzi hizo tulikuwa tukisikia katika redio, pia tukienda dansi tunakuta nyimbo za wasanii kadhaa wa Hip Hop zikirindima.

Wakati huo nilikuwa na wenzangu kama kina K One na Scoz Man…” alisema Banza.Banza alieleza kuwa wakati huo ilikuwa vigumu sana kupata nafasi ya kutumbuiza eneo lolote lile kwani muziki huo hakukubalika.Alikumbuka mwishoni mwa mwaka 1989, walikuwa wakienda Coco Beach kuonesha vipaji vyao vya kuimba muziki wa Hip Hop.

Banza alitamka kuwa vijana wengi walionesha kuukubali muziki huo japo ilikuwa ngumu sana kueleweka mbele ya jamii kutokana na muziki huo wa Hip Hop kuonekana kama uhuni.“Tulikuwa na kazi kubwa ya ziada kufanya vile inavyotakiwa, lakini bahati haikuwa yetu wazazi walileta kipingamizi.

Hata hivyo tulionekana kama vijana wa kihuni….” anasikitika Banza Stone.
Japo alipenda sana muziki, wazazi wake waliweka pingamizi baada ya kuonekana muziki huo wa Hip Hop kuwa ni wa kihuni.

Mwaka 1990 akaamua kuanza mchakato mpya wa ‘kunengua’ muziki wa dansi, ambapo alikuwa akicheza kwenye harusi na kufanikiwa kupata fedha kidogo. 

Mwaka 1995 Banza alijiunga katika bendi iliyochini ya Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) ya Twanga Pepeta kabla ya kuchepukia katika bendi ya Extra Bongo iliyokuwa ikiongozwa na Alli Choki.

Banza alionesha kupevuka kifikra mwaka 2000, alipomua kwenda kupata mafunzo ya muziki sehemu tofauti ikiwemo Kituo cha Utamaduni cha Watu wa Korea.

Aidha alipokuwa katika bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), wanamuziki wake walipelekwa kuapata mafunzo hayo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo akiwemo yeye.

Baada ya kuhitimu alianza kuimba katika bendi mbalimbali zikiwamo za The Heart Strings, bendi za Twiga na Achigo, akiwa mpiga ngoma pamoja na Afri-Swez na zingine ndogo ndogo.

Katika bendi hizo zote hizo alikuwa akidumu kwa miezi kadhaa, kabla ya kuhamia katika bendi nyingine hadi alipoingia katika bendi ya The African Stars, “Wana Twanga Pepeta” akawa na ahuweni ya maisha.

Soko la Banza lilikuwa kubwa hivyo baada ya kuipaisha Twanga Pepeta kwa kiasi kikubwa, alichukuliwa kwenda kujiunga katika kundi la Tanzania One Theatre (TOT) “Wana Achimenengule”

Akiwa hapo alijulikana zaidi kwa jina la ‘Mwalimu wa Walimu’ japo nako hakukaa sana.Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ aliamua kuanzisha bendi yake iliyokuwa ikiitwa Bambino Sound.Kwa bahati mbaya bendi hiyo ilidumu kwa miezi kadhaa kabla ya kusambaratika kutokana na uongozi mbovu.

Banza aliwahi kuelezea kwamba katika kipindi cha miaka 23 tangu aanze muziki wa dansi rasmi, haikuwa rahisi kwake kupata mafanikio mazuri licha ya kuzunguka sana kutafuta maisha.Banza Stone alipitia zaidi ya bendi tisa ikiwemo Rufita Band.

Mwaka 2014, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Ramadhani ‘H-Baba’ alimshirikisha Banza kurekodi wimbo wake mpya wa ‘Sina Raha’.Kibao hicho kimo kwenye albamu mpya ya msanii huyo inayojulikana kwa jina la ‘Shika Hapa, Acha Hapa’.

Banza Stone hatunae tena hapa duniani, lakini ametuachia ujumbe mzito kutoka kupitia nyimbo zake ambazo bado zitamba.Baadhi ya nyimbo hizo ni za Mtaji wa Maskini, Kumekucha, Elimu ya Mjinga, Angurumapo Simba Mcheza nani na Falsafa ya Maisha.

Ramadhani Masanja alikuwa ‘msanii wa ukweli’ kwani alithubutu kuimba vibao kadhaa vya taarabu ukiwamo ‘Kuzaliwa mjini’ na ule wa ‘Play Boy’.
Banza alieleza jinsi alivyohangaika ili kufikia kuwa msanii mkubwa hadi kujulikana.Alisema alifanya subira ili kutimiza doto zake zilizokuja hatua kwa hatua.

Mwaka 1990 waliamua kuanza mchakato mwingine wa kunengua akiwa na wenzake wakicheza hususan kwenye harusi mbalimbali, wakaweza kupata fedha kiasi.Banza alifafanua kuwa walikuwa wakifanya maonesho kwa muda mrefu kidogo na wakati huo walikuwa wakicheza kwa kufuatisha nyimbo za wanamuziki kutoka nje, kama wa Michael Jackson na wengine.

“Mwaka 1995 niliingia Twanga Pepeta, wakati huo bendi hiyo ilikuwa bado changa sana, tulianza kwa kutoa albamu ya “Kisa Cha Mpemba”

Bendi hiyo ikaendelea kukua zaidi kimuziki mpaka kufikia katika hatua ya kuwa bendi bora ya muziki wa dansi nchini mwishoni mwa miaka ya 1990…” alitamka Banza.Ramadhan Masanja kuna kipindi alivuma mno kwa wimbo wa Kumekucha, uliokuwa wa kwanza kutunga na kurekodi studio mwaka huohuo.

Alisema hapo ndipo safari ya muziki ilipoanza, aliamua kuendelea na shule ya muziki baadae mwaka 2000, ili kuongeza ujuzi na maarifa katika kazi yake.Baadae aliicha bendi ya Twanga na kutimkia katika bendi Tanzania One Theater (TOT Plus) ambako nyota yake ilizidi kung’ara.
Akiwa TOT Plus, alishirikiana na wakali wengine wakiwepo Abdul Misambano, Papii Kocha na wengine wengi waliosababisha kuwepo upinzani mkubwa wa kimuziki dhidi ya Twanga Pepeta.

Banza alitua TOT Plus 1999 chini ya ukurugenzi wa Kapteni John Komba ambaye alimchukua mwimbaji huyo ili kuliimarisha kundi hilo liweze kupambana na Twanga Pepeta.Wakati huo ndipo Banza alipotoa ‘rap’ mpya wa ‘Uliona wapi Tingatinga likaenda kwenye starehe’ kikiwa ni kijembe kwa rafiki yake wa karibu Ally Choki ambaye wakati huo alikuwa Twanga Pepeta.

Kuna siku Choki katika uzinduzi wa moja ya albamu, aliingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee akiwa juu ya Kijiko au Tingatinga.Mbali ya rap hiyo akiwa TOT, Banza pia alitunga vibao kama Elimu ya Mjinga ni Majungu, Mtaji wa Maskini Nguvu zake mwenyewe, Angurumapo na Simba sehemu ya pili.

Mwaka huohuo Banza alirejea katika bendi ya African Stars ‘Wana Twanga Pepeta’ ambako alikutana na Alli Choki pamoja Luiza Mbutu chini ya uongozi wa mkurugenzi Asha Baraka, ilipoedelea kupata umaarufu mkubwa zaidi.

Nyimbo za Angurumapo Simba, Kisa cha Mpemba, Mtaji wa maskini, Elimu ya Mjinga, Mtu na Pesa zake na nyingine nyingi zilizovuma na kuipa umaarufu bendi hiyo ni kielelezo halisi cha uwezo aliokuwa nao marehemu Banza Stone.Hakika kifo chake kilileta simanzi kubwa kwenye tasnia hiyo.

Huko Africana Stars Banza Stone alijulikana zaidi kwa jina la ‘Mwalimu wa Walimu’ japo hakukaa kwa muda mrefu katika bendi hiyo.Baadae mwanamuziki huyo aliondoka TOT Plus na kwenda kuanzisha kundi lake la Bambino Sound.Akiwa na bendi hiyo, alitoka na kibao cha ‘Mimi niseme na wewe Useme nani atamsikiliza mwenzie?

“Bendi yangu ilikuwa inaitwa Bambino Sound, ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa tu, lakini ilivunjika kutokana na kutokuwa na uongozi mzuri, haikuwa na mtu makini hilo ndilo liliangusha bendi hii, hatimae nikarudi tena African Stars Band. Baadaye nilienda Extra Bongo…” alisema Banza katika mahojiano wakati wa uhai wake.

Bendi hiyo haikudumu kwa kipindi kirefu, ikafa.

Banza Stone alikuwa , mtunzi, mwimbaji na rapa wa muziki huo nchini. Pia alianika idadi ya bendi alizopitia katika kipindi cha miaka 23 tangu aanze muziki wa dansi rasmi.Aliweka wazi kwamba alipita kupiga muziki katika bendi zaidi ya bendi tisa, katika harakati zake za za muziki.

Banza aliwahi kutunga na kuimba nyimbo akiwa katika bendi ya Twanga Chipolopolo na Rufita Jazz kabla ya kujiunga na Extra Bongo, inayoongozwa na Ally Choki.

Akiwa na Extra Bongo, Banza alikuwa akitamba na kibao chake kinachojulikana kwa jina la ‘Falsafa ya Maisha’. Pia alikuwa akiimba nyimbo alizowahi kutamba nazo katika bendi mbalimbali.

Mwaka 2003 Banza alikuwa miongoni mwa wanamuziki watatu nguli nchini, wengine Ally Choky na Muumini Mwinjuma, walioibuka na zing zong yao iliyoandaliwa na Mohamed Mpakanjia (sasa marehemu).

Mwaka mmoja baadae alirejea tena Twanga Pepeta na kuibuka na kitu kikali kilichojulikana kama ‘Mtu Pesa’.Kabla hakijapoa, akiachia tena kibao cha ‘Hujafa hujasifiwa’, ambacho alisema alitunga baada ya mara kadhaa kuzushiwa kifo.Nguli huyo alisema kuwa alikwisha rekodi vibao kadhaa alivyoimba kwa mtindo wa Hip Hop, kati ya hizo upo wimbo alioutengeneza akiwa na Chid Benz miaka miwili iliyopita ambao hakufanikiwa kuutoa.

“Nina wimbo ambao haujatoka, lakini nimesha achia wimbo mmoja Mshenga, niliorekodi na Man Dojo na Domo Kaya ambao haukufanikiwa kufanya vizuri katika chati za muziki wa kizazi kipya…” alitamka Masanja Banza Stone.

Wimbo mwingine aliorekodi ni Sema unachotaka, aliouimba akishirikiana na Godzilla ambao alipanga kuupeleka redioni mwaka huo.

Marehemu Banza atakumbukwa kwa mengi kutokana na umahiri wake wa kutunga na kuimba na kutunga nyimbo ambazo ‘ziliwabamba’ mashabiki wa muziki huo na kujikuta akiwa kipenzi cha watu wengi wa muziki wa dansi.

Msanii mwenzake aliyefanya nae kwa ukaribu, Ally Choki alisema kuwa Banza Stone alikuwa na kipaji cha kipekee na alikuwa chachu kubwa ya kukua kwa muziki wa dansi tangu alipojitumbukiza kwenye tasnia hiyo 1991 akianzia kama mnenguaji kwenye kundi la Sinza Stars.

Alikiri kuwa kuna kipindi Banza aliwahi kuwa mpinzani wake mkubwa wa kwenye ushindani katika muziki, licha ya kuvutiwa na uimbaji wake.
Hali hiyo Choki alilazimika kufanya mazoezi ya ziada ili aweze kuhimili ushindani kutoka kwa mkali huyo ambaye nyota yake imezimika ghafla.
Banza aliwahi kuimba vibao kadhaa vya taarabu ukiwamo Kuzaliwa Mjini na ule wa Play Boy.

Licha ya kuwa msanii bora wa muziki wa dansi Banza Stone alisema, “…nashindwa kukua zaidi katika muziki kutokana na maradhi yanayonisumbua, muda mwingi ninakuwa kitandani, hivyo nashindwa kuendelea vizuri katika kazi zangu, kipindi cha hivi karibuni nilipumzika muziki kwa miezi kadhaa lakini Mungu mkubwa kwani hivi sasa ninaendelea vizuri…”

Banza baada ya kupata ahuweni alitarajia kurejea tena katika bendi yake aliyokuwa akiitumikia ya Extra Bongo na kufanya mambo makubwa zaidi.
“Natarajia kufanya kazi ambayo mashabiki watafurahia, tumeshazindua albamu ya ‘Mtenda Akitendewa’ na ‘Kinachosubiriwa’ hivi sasa ni kazi mpya, tayari nina vibao kadhaa ambavyo vitatoka mapema mwaka huu...” alisema Banza Stone.

Ni dhahiri kwamba Banza Stone ameacha alama katika muziki wa dansi hapa nchini kupitia nyimbo zake zitakazoendelea kuishi na kuwa kumbukumbu na elimu kwa jamii.Kabla ya kulazwa hospitalini Banza tayari alikuwa amekwisha kata tama ya kuishi kwa vile aliwahi kuota ndoto kuwa mwisho wake wa kuishi duniani umekaribia.

Alieleza kwamba aliota ndoto anakufa na ameoneshwa jinsi kifo chake kwamba ataugua ghafla na kufariki dunia.Nyota huyo alisema kufuatia ‘maono’ hayo, ameanza kutunga nyimbo ambazo zingezungumzia historia ya maisha yake.“Ni kweli naona mwisho wangu umekaribia, nimeoneshwa ndotoni, inawezekana ni mpango wa Mungu ili nitengeneze maisha, nimeshaanza kuandaa albamu itakayohusu historia ya maisha yangu…” alisema Banza

Stone. Alizidi kusema kwa masikitiko kuwa baada ya ndoto hiyo amekosa raha ya kuishi tena na hajui yupo katika ulimwengu upi, kwani anafikiria maisha ya ulimwengu mwingine atakaoelekea.Banza alisema kwamba ndani ya moyo wake ana siri nzito ambayo angeitoa kwenye moja ya nyimbo zake hizo.

“Yaani mawazo yangu hayapo hapa, sijui niko dunia gani, nimekata tamaa, ninauona mwisho wa maisha yangu upo karibu lakini siogopi, natamani kufa kwa sababu ni lazima nitakufa hata nikiishi miaka mingapi…” alisema Banza.Mwaka 2014, Nyota huyo aliugua kwa muda na kulazwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Habari za mara kwa mara zilikuwa zikizushwa kuwa amefariki dunia, lakini siku yake ilipowadia, Julai 17, 2015 Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ akaaga dunia.Julai 17, 2019, Banza Stone atatimiza miaka minne tangu aiage dunia.

Mungu uiweke roho yake pahala pema peponi, Amina.

WAZIRI BITEKO APOKEA RIPOTI YA KAMATI TEULE YA USULUISHI WA MIGOGORO YA MIPAKA WACHIMBAJI WADOGO NA TML

$
0
0



Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akizungumza katika mkutano wa Kupokea Ripoti kutoka kwenye kamati iliyoundwa na Waziri wa Madini Dotto Boteko leo Mirerani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Teule iliyoundwa kwaajilivya kutatua migogoro kati ya TML na wachimbaji wadogo Mhandisi Hamis Kamando.

Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto kwake Katibu mkuu wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila kimsikiliza Meneja wa Mgodi wa Tanzanite Afrika Wilfred Mushi a(liyevaa shati jeupe)


Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexanda Mnyeti akizungumza katika mkutano wa Kupokea Ripoti kutoka kwenye kamati iliyoundwa na Waziri wa Madini Dotto Boteko leo Mirerani.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexanda Mnyeti akisalimiana na Mkurugenzi wa kampuni ya TML Hussein Gonga.

Waziri wa Madini Dotto Boteko akipokea maelekezo kuhusu ujenzi wa Kituo cha ukaguzi wa madini kilichopo Mirerani Mkoani Manyara.

Picha ya jengo la Kituo cha kukagulia madini kikiwa katika hatua za mwisho kumalizika kama kinavyoonekana.Picha zote na Vero Ignatus Michuzi Blog.







Na.Vero Ignatus,Manyara.

WAZIRI wa Madini Mhe.Dotto Bitteko amefuta jumla ya leseni zaidi ya elfu 12 ambapo kati ya leseni 33 elfu zilikuwa zimepewa hati za makosa kwa kutokulipa kodi ya leseni ya mwaka huku kampuni ya TanzaiteOne wanadaiwa dola 98 ambapo kodi hiyo inatosha inatosha kufuta leseni ya uchimbaji

Akipokea ripoti ya migogoro ya mipaka kati ya wachimbaji wadogo na Tanzanite One iliyopo Merereni Mkoani Mnyara ambapo kamati hiyo ilibaini makosa 13 ambapo kamati hiyo ni ya tisa kati ya kamati 8 zaawali ambazo zilichunguza mgogoro huo.

Amewataka baadhi ya watu kutokujipa haki kwani yeye kama waziri mwenye dhamana anapimwa kutokana na utendaji wake wa kazi ,hivyo amewataka kupunguza maneno yasiyokuwa na maana ila waacheni watu wafanye kazi kwa ufasaha.

"Hivi leo tuna uparesheni ya watu wanao uza madini kwenye masoko ya nje, mimi haijalishi kuwa wewe ni ndugu yangu au shemaeji yangu, kwani miongoni mwao yup mmoja shemeji yangu,lakini mie ninamwambia kuwa atarudi wakati utaratibu wa serikali ukikamilika"Alisema Biteko

Aliahidi kukaa na kamati yake haraka iwezekanavyo kutoa majibu ya taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiteua ya kuchunguza mgogoro huo uliodumu kwa kipindi kirefu.Hata hivyo amewataka waajiri wa wachimbaji wadogo (Apolo) kuwapa stahiki zao kwani muda wa nguvu zao utakapokwisha wao wanabaki bila ya kuwa na thamani yeyote kwa familia na badala yake kuwa mizigo kwaserikali hapo baadae.

Naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo ameipongeza kamati kwa kazi nzuri waliyoifanya huku akioma radhi kwa sintofahamu ambayoilijitokeza
kati ya mbunge Olemilya na Mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo awali walionyesha kuzozana wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo.

Awali akiwasilisha taarifa ya kamati mwenyekiti wa kamati hiyo Mhandisi Hamisi Kamando alisema wamebaini makosa 13 ikiwemo la TanzaniteOne kuwa na leseni ya uchimbaji wa madini ya viwandani huku

wakichimba madini ya vito kinyume cha sheria na kuongeza kuwa leseni hiyo ndio chanzo cha migogoro kwani wamebaini kufanya kazi kwenye kitalu B kwa zaidi ya mita 50 eneo ambalo siyo lao.Mbali na hilo kamati imependekeza mkataba kati ya TanzaniteOne na STAMICO uvunjwe na leseni yake ifutwe kwani ndio chanzo cha migogorona kwamba inafanya kazi kinyume cha sheria.

Watu 1000 kuchunguzwa homa ya ini Ocean Road

$
0
0

NA MWANDISHI MAALUM - ORCI

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), imepanga kuwachunguza virusi vya homa ya ini watu wapatao 1,000 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani.

ORCI imetenga siku tano kuanzia Julai 27 (jana) hadi kufikia Julai 31, mwaka huu ambapo uchunguzi utafanyika bila malipo.

Hayo yameelezwa leo hospitalini hapo na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Huduma za Saratani ORCI, Crispin Kahesa alipozungumza na waandishi wa habari.

"Kwa siku ambazo si za maadhimisho huwa tunatoza kiasi cha Sh. 10,000 kuchunguza, tumefanya bila malipo ili kuenda sambamba na na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo 'Finding the Missing millions'  (Wekeza kwenye mapambano dhidi ya homa ya ini," amesema.

Dk. Kahesa amesema kwa siku ya jana na leo tayari watu zaidi ya 150 wamejitokeza kuchunguzwa iwapo wana maambukizi ya virusi hivyo au la!

"Kwa upande wa watu wazima umekuwa mkubwa kwa kundi la wanawake kuliko wanaume na kwa kundi la vijana uwiano umekuwa sawa huku ikielezwa kwamba wengi waliojitokeza ni wale waliozaliwa kuanzia 1990 na kuendelea," amesema.

Dk. Kahesa ambaye pia ni bingwa wa Kinga ya magonjwa ya saratani ORCI amesema kati ya watu hao zaidi ya 150 waliojitokeza sita walikutwa wana maambukizi.

Dr. Kahesa amesema sambamba na utoaji hudumu ya uchunguzi na chanjo ya Homa ya ini unaoendelea kutolewa katika taasisi ya Ocean road huduma hii pia inatolewa Kwa watumishi katika maeneo yao ya kazi ikiratibiwa Na ORCI kwa maombi maalumu.

Amesema kwa namna ambavyo jamii imepata mwamko kuhusu umuhimu wa kuchunguzwa iwapo wana maambukizi ya ugonjwa, wapo baadhi ya wazazi ambao waliambatana na watoto wao ili nao wachunguzwe.

"Wamekuja na watoto wa umri wa mwaka mmoja, miwili wakiomba nao wachunguzwe, hawakuwa na uelewa kwamba watoto waliozaliwa kuanzia 2002 hadi sasa tayari walishapatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa huu.

"Hivyo, pamoja na kufanya uchunguzi tumetoa pia elimu, kwamba wanaostahili kuchunguzwa ni wale ambao walizaliwa kuanzia 2002 kurudi miaka ya nyuma," amesema.

Amewasihi watanzania kuzitumia vema siku zilizobakia kwa kuhakikisha wanajitokeza kuchunguzwa afya zao.

"Hadi kufikia Julai 31, mwaka huu tunakusudia kuwachunguza watu 1,000, ikiwa mtu anakutwa hana maambukizi atahitajika kupata chanjo tatu kukingwa.

"Kupata chanjo atachangia gharama kiasi cha Sh. 10,000, chanjo ya pili atarudi baada ya mwezi mmoja na ya tatu ni baada ya miezi sita," amesema.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Huduma za Saratani ORCI, Crispin Kahesa

CCM SHINYANGA YAONYA KUWEKA WAGOMBEA WASIOKUBALIKA,YAZINDUA KISHAPU YA KIJANI.

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amezindua rasmi kampeni ya 'Kishapu ya Kijani', huku akionya viongozi na wanachama wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwezi Oktoba mwaka huu kutopitisha wagombea wasio na sifa.


Uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Kishapu umefanyika leo Julai 28, 2019 katika kata ya Maganzo kwenye Uwanja wa michezo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, wilaya na mkoa , wanachama, wananchi wakiongozwa na mbunge wa jimbo a Kishapu Suleiman Nchambi.


Mlolwa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi amesema lengo la Kampeni ya Kijani ni kuhakikisha kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2020, wagombea wote wa CCM wanashinda kwa kishindo na kutowapatia hata kiti kimoja wapinzani.


Amebainisha kuwa ili adhma hiyo ipate kutimia ni marufuku viongozi wa CCM pamoja na wanachama kupitisha wagombea watakaowania viti vya uongozi kwenye chaguzi hizo, ambao watakuwa hawana sifa na wasiokubalika kwa wananchi, bali wapitishe wagombea wenye vigezo ambao watarahisisha uchaguzi na hatimaye kupita bila ya kupingwa.

“Tunaposema kampeni ya kijani maana yake ni kushinda viti vyote vya ugombea kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani, na kutowapa nafasi wapinzani sababu CCM ndiyo chama pekee ambacho kinaleta ukombozi kwa wananchi, nadhani mnaona nyie wenyewe mambo anayo yafanya Rais wetu Dkt. John Magufuli,”amesema Mlolwa.

“Hivyo ili tupate kushinda viti vyote vya uongozi ni lazima tupitishe wagombea wote ambao wana sifa na kukubalika kwa wananchi, na siyo kupitisha tu watu ambao hawana vigezo wana maskendo machafu huko kwa wananchi kisa tu wana pesa, nawasihi msipitishe watu wa namna hiyo watatuangusha,”ameongeza.

Katika hatua nyingine alionya makundi ndani ya chama katika kuelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi, na kuwataka wawe kitu kimoja katika kuendeleza mapambano ili waweze kupata ushindi wa kishindo, na baada ya hapo, pale penye mapungufu ndipo wakae kuyamaliza na kusameheana.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kishapu Suleimani Nchambi, alimtoa wasiwasi mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga, kuwa jimbo hilo hakuna mgombea wa upinzani ambaye atashinda kwenye chaguzi zote, kwani wananchi wana imani na CCM kutokana na kuwatekelezea maendeleo yakiwamo maji safi na salama kutoka ziwa Victoria.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilayani Kishapu Joseph Kwilasa, amewataka vijana kutotumika kuvuruga amani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka ujao, bali wajiandikishe kwa wingi na kupiga kura kwa kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo ambao wanatoka CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizindua kampeni ya "Kishapu ya Kijani" na kuonya kuweka wagombea wasio na sifa wala kutokubalika kwa wananchi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Shinyanga Barack Shemahonge, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kishapu ya Kijani.Amewataka vijana kutofanya makosa bali wachague wagombea wote wa CCM, na pia wajiunge kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo na kujipatia kipato kuliko kusubili kutumika kwenye uchaguzi na kupewa vitu vidogo.


Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe. Suleiman Nchambi akisalimia wananchi na wanachama wa CCM wilayani humo kabla ya kutoa salamu zake kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe. Suleiman Nchambi akizungumza na wananchi wa jimbo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani, na kuelezea kuwa serikali ya CCM haina mpinzani kwenye chaguzi zote zijazo kwani wametekeleza sehemu kubwa ya ilani ya uchaguzi kwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi ikiwamo kuwaletea maji ya Ziwa Victoria wananchi wa Kishapu. 


Diwani wa Kata ya Maganzo wilayani Kishapu Mbalu Kidiga, akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake ambapo amesema kuwa kwenye chaguzi zote zijazo CCM itashinda kwa kishindo na hatimaye kuifanya Kishapu kuwa ya kijani.
Afisa mazingira kutoka mgodi wa Almasi Mwadui Prisca John, akipongeza kampeni ya Kishapu ya Kijani na kuwataka siyo kupata ushindi tu bali hata kijani hiyo waielekeze kwenye kupanda Miti na kuondoa hali ya jangwa wilayani humo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilayani Kishapu Joseph Kwilasa, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani.Amewaasa vijana kuacha kutumika kwenye kipindi cha uchaguzi, bali wajiandikishe kwa wingi na kwenda kupigia kura wagombea wa CCM ambao ndiyo watawaletea maendeleo. Awali mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akisalimia wananchi na wanachama wa CCM kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa kwenye uzinduzi wa Kishapu ya Kijani na kupewa maagizo ya kupigia kura wagombea wote wa CCM Pamoja na kupitisha wagombea wenye sifa pale watakapokuwa wakipiga kura za maoni. Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa wamebeba mabango kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kishapu ya Kijani, wakitoa ujumbe kwenye Kata ya Mwadui Luhumbo ambayo inatawaliwa na viongozi kutoka CHADEMA. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa wamebeba mabango kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kishapu ya Kijani, wakitoa ujumbe kwenye Kata ya Mwadui Luhumbo ambayo inatawaliwa na viongozi kutoka CHADEMA. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu na baadhi ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Wanachama wa CCM wilayani Kishapu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Burudani za ngoma zikinogesha uzinduzi wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Burudani za ngoma zikiendelea kunogesha uzinduzi huo wa kampeni ya Kishapu ya Kijani. Awali mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi mwenye Shati la njano akicheza ngoma wakati akimsubiri mgeni Rasmi mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa kuja kuzindua kampeni ya Kishapu ya Kijani, na wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Maganzo Mbalu Kidigi. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungwa Skafu mara baada ya kuwasili kwenye Kata ya Maganzo wilayani Kishapu tayari kwa kuzindua Kampeni ya Kishapu ya Kijani. Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi katikati akiwa na mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa wa kwanza kulia wakielekea kwenye tukio la uzinduzi wa Kishapu ya Kijani. Maandamano yakielekea kwenye eneo la uzinduzi wa Kishapu ya Kijani. Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi (kushoto) akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa,Mwenyekiti wa CCM Wilayani Kishapu Shija Ntelezu sambamba na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Barack Shemahonge, wakisali mara baada ya kuhitimisha uzinduzi wa Kishapu ya Kijani.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

TAIFA STARS YABANWA MBAVU UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Tanzania (Taifa Stars) kimeshindwa kufanya vyema kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu ya kutokufungana na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars'.

Mchezo huo wa kufuzu michuano ya wachezaji wa ndani CHAN umefanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa kwa kuzikutanisha timu hizo.

Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije amesema mchezo ulikuwa ni mzuri kuna mapungufu ameyaona ila atakaa na wachezaji kuweza kuyafanyia kazi.

"Tutaenda kufanyia kazi mapungufu yaliyojitojeza na kwenda kusaka ushindi katika michezo wa marudiano nchini Kenya na kushindwa kupata matokeo leo haimaanishi tutashindwa kufuzu," amesema Ndayiragije.

Katika mchezo wa leo, Taifa Stars imeshindwa kupata matokeo katika mchezo wa leo na Kocha amesema anaamini lengo la vijana wake ni kupambana kwenye mchezo wa marudiano.

Sasa Stars italazimika kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Kenya Agosti 4.




Yanga wapiga tafu Hospitali ya M/nyamala.

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Michuzi tv

YANGA Tawi la nguvu ya Buku lenye makazi yake Mwananyamala leo wamekabidhi rasmi wodi ya wanaume no. 5 baada ya kuifanyia ukarabati wa ndani na nje ya wodi kwa takribani wiki moja sasa.

Ukarabati huo umefanyika ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya Wananchi inatarajiwa kuadhimishwa na Klabu ya Yanga Jumapili ya Agosti 4,2019.

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya makabidhiano Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura aliwapongeza Wanayanga tawi la Nguvu ya Buku kwa fikra za msaada walioufikiria na fundisho tosha kwa wengine.

Alisema Wambura, msaada wa kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa Historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja.Leo mmefanya Tawi la Nguvu ya Buku tunaomba wajitokeze na wengine.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano Mwananyamala ambako Tawi hilo linapatikana aliwapongeza sana Tawi la Nguvu ya Buku kwa kitendo cha Kijamii walichokifanya na hakika yeye kama mshabiki wa upande wa pili wamejifunza kitu ambacho kinastahili kuigwa na Mwananchi yeyote anayejitambua.

Aidha, Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha aliwapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano huohuo siku zote.

Mwisho Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Lyagala alisema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu.

MWENGE WA UHURU WAKATAA BAADHI YA MIRADI MAFIA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali amesita kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi mitatu wilayani Mafia ,mkoani Pwani na kutoa wiki mbili kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza miradi hiyo ,thamani yake halisi na matumizi kisha apelekewe taarifa .

Miradi hiyo ni pamoja na hospital ya wilaya ambayo ilitolewa kiasi cha sh.mil 403.600 .

Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya KN52 Kilimahewa yenye thamani ya mil.22.336 ambayo kalavati na barabara haina ubora pamoja na uendelevu wa mradi wa maji huko Bweni ambako kero za wananchi hazijafanyiwa kazi kipindi kirefu .

Akielezea juu ya hali hiyo iliyojitokeza ,Mkongea alisema endapo kutabainika kuna ubabaishaji juu ya miradi hiyo basi hatua za kisheria zitachukuliwa.

"Tunapitia miradi hii,tunakagua sio tuu kupitia ila ni kujiridhisha ,hivyo basi TAKUKURU na mkuu wa wilaya fuatilieni suala hili kwa kina ,ili kama kutabainika hakuna ubadhilifu mkuu wa wilaya ataifungua miradi hiyo hapo baadae"alifafanua Mkongea.

Nae mkuu wa wilaya ya Mafia ,Shaibu Nnduma alipokea maelekezo na maagizo waliyopatiwa .Alisema ,jumla ya miradi nane yenye thamani zaidi ya bilioni sita imepitiwa na mwenge wa Uhuru lakini miradi mitatu ndio imewaletea mushkeri.

Mwenge huo baada ya kumaliza mbio zake wilayani Mafia Julai 27 ,umekabidhiwa wilayani Kisarawe na kupokelewa na mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo Julai 28 na kukimbizwa umbali wa km153.1 .

Akielezea kuhusu miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru ,Jokate alieleza miradi mitatu imewekwa jiwe la msingi,minne imekaguliwa na miwili imezinduliwa huku ikiwa imegharimu kiasi cha sh. bilioni 11.97 .#


TIMU YA RIADHA YA BENKI YA CRDB YANOGESHA BAGAMOYO MARATHON

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanaounda timu ya Riadha ya "CRDB Bank Jogging" wakiwa katika picha ya pamoja na medali zao walizoshinda katika katika Bagamoyo Historical Marathon, iliyofanyima Julai 28, 2019, Bagamoyo mkoani Pwani.








































WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA SHAMBA LA KATANI LA HASSAN SISAL ESTATE

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu akizungumza na wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate lililopo Makanya, Wilayani Same alipotembelea shamba hilo kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alifanyaziara Mkoani Kilimanjaro. 
Meneja Mshauri wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate, Bw. Ndekirwa Nnyari (Kushoto) akitoa maelezo kuhusu shamba hilo na masuala ya wafanyakazi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara katika shamba hilo Julai 27, 2019. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara katika shamba hilo kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alifanyaziara Mkoani Kilimanjaro. 
Sehemu ya Wataalamu walioambana na Mhe. Waziri na wafanyakazi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara katika shamba hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mwinyi Mkuu wakati wa ziara yake Wilayani Same katika Shamba la katani la Hassan Sisal Estate. 
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Large Mature akifafanua jambo kuhusu uwasilishaji wa michango ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihakiki malipo ya wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate alipokuwa akioneshwa na Meneja Mkuu wa Unique Consultance Bw. Edwin David (Kulia) . Afisa Kazi Mfawidhi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mwinyi Mkuu (katikati). 
Mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate Bw. Salum Issa akimwelezea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani), changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji kazi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza kero kutoka kwa mfanyakazi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate, alipofanya ziara kwenye shamba hilo Julai 26, 2019 kwa lengo la kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Rosemery Staki (kulia), alipofanya ziara Wilayani huo kwa lengo la kufuatia maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Meneja Mshauri wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate, Bw. Ndekirwa Nnyari (katikati) akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa Shamba la katani la Hassan Sisal Estate. 

*************** 

Na; Mwandishi Wetu 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametoa maagizo kwa viongozi wa Shamba la Katani la Hassan Sisal Estate kuhakikisha wanatatua migogoro na wafanyakazi pamoja na kusimamia haki zao ipasavyo. 

Waziri Mhagama ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Same alipofanya ziara katika Shamba la Hassan Sisal Estate ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu masuala ya kazi aliyoyatoa Julai 20, 2019 alipotembelea shamba hilo lililopo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Same. 

Akizungumza na wafanyakazi pamoja na viongozi wa shamba hilo, alieleza kuwa waajiri wanatakiwa kutekeleza matakwa yote ya Sheria za ajira na mahusiano kazini kwa kuzingatia miongozo na kanuni ambayo inasimamia haki za msingi kwa wafanyakazi. 

“Tunataka kuona ninyi kama waajiri mnakuwa na vikao vyenye tija na wafanyakazi katika kuleta suluhu ya masuala mbalimbali ya kazi,” alisema Mhagama 

Aliongeza kuwa Kampuni mbili zilizopo katika shamba hilo yaani Unique Consultancy na UPAMI kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wafanyakazi hao, ikiwemo kuwasilisha michango kwa wakati kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Pamoja na hayo alishauri pia kampuni hizo kuwaweka wazi wafanyakazi kuhusu mikataba yao. 

“Malalamiko na Manung’uniko ya wafanyakazi ni mengi, mnatakiwa kukaa na kujadili pamoja namna bora ya kutatua matatizo yao yanayojitokeza hususani kwenye mikataba,” alisema Mhagama. 

Katika hatua hiyo, Mhe. Mhagama alimuagiza Meneja wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA), kufanya kanguzi za mara kwa mara katika shamba hilo na kuangalia kama wafanyakazi wanakabidhiwa vifaa vya kujinginga na madhara kazini (Protective gears) kwa wakati, pamoja na kusimamia zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi hao. 

Pia, alitoa maelekezo kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kilimanjaro, kukabidhi kadi za uwanachama kwa wafanyakazi wa shamba hilo la Hassan Sisal Estate na kufuatilia uwasilishaji wa michango yao kutoka kwa waajiri wao. 

Sambamba na hilo, Waziri Mhagama ametaka Afisa Kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro kutembelea shamba hilo na maeneo mengine mbalimbali katika mkoa huo ili kuelimisha wafanyakazi sheria mbalimbali za kazi na ajira zitakazo wawezesha kutambua haki zao za msingi. 

Aidha, Waziri Mhagama alitoa maelekezo juu ya uwepo wa vyama vya wafanyakazi kwenye mashamba yote ya katani yaliyopo nchini, vitakavyosadia kuongeza tija na ufanisi katika shughuli mbalimbali za utendaji kazi. 

Pamoja na hayo, Mheshimiwa Mhagama aliwataka viongozi wa shamba hilo kuendelea kusimamia vizuri maslahi ya wafanyakazi wao ili waweze kutekeleza majukumu ya kila siku wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. 

Naye, Meneja Mshauri wa Shamba hilo, Bw. Ndekirwa Nnyari aliahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa ikiwemo kuwa na majadiliano ya mara kwa mara na wafanyakazi kwa itakayowapa munufaa ya pamoja. 

Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Victor Luvena amesema kuwa watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri kwa kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaoshindwa kutekeleza. 

Pia mmoja wa Wafanyakazi wa Shamba hilo, Bi. Cheshi Juma alisema kuwa ujio wa Waziri na wataalamu alioambatana nao utasaidia kuondoa kero za wafanyakazi na kujenga mahusiano mazuri na waajiri wao. 

“Tumehamasika sana kuona Serikali yetu ipo pamoja nasi katika kutetea maslahi ya wafanyakazi na kushughulikia kero tulizokuwa tukikabiliana nazo katika maeneo ya kazi,” alisema Cheshi

UTOMVU NI DHAHABU NYINGINE INAYOPATIKANA SHAMBA LA SAO HILL.

$
0
0
Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo akitoa maelezo jinsi gani wanavyovuna utomvu kwa baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita wakishangaa jinsi miti inavyoweza kutoa mabilioni ya fedha baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo
Moja kati ya maeneo ya Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Watanzania kuanza kunufaika na zao la miti kutokana na uvunaji wa utomvu kutoka kwenye miti ya kupandwa iliyopo kwenye Shamba la Sao Hill lililopo Mufindi mkoani Iringa kwa kuiliingizia taifa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa kupindi cha miaka miwili ya majaribio.

Hiyo imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.

Akitoa ufafanuzi mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema kuwa Shamba la Miti Sao Hill wameanziasha mradi mpya wa kuvuna utomvu ambao umekuwa unatengenezewa gundi kwa ajili ya kutumika kwenye bidhaa mbalimbali kulinga na mahitaji ya wahusika.

“Tumeanza kugema utomvu kwenye miti mikubwa kwa kuwa tupo kwenye majaribia lakini wataalamu wamesema kuwa ukianza kugema utomvu mti ukiwa na umri mdogo basi utagemwa kwa muda mrefu na kuleta faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla, na kumbukeni kuwa hapa mti haukatwe unaendelea kustawi tu” alisema Mbwambo

Mbwambo alisema kuwa takwimu za dunia zinaonyesha kuwa inawezekana utomvu ukawa unalipa zaidi ya zao la miti hivyo utafiti ukimalizika yawezekana wakulima wa miti wakahamia kwenye uvumaji wa utomvu.

“Kwa takwimu hizo sio muda faida kubwa itakuja kwa wananchi na serikali kwa ujumla maana inaonyesha dhahili kuwa utomvu unalipa sana kuliko mbao hiyo watafiti waliopo hapa katika shamba la Sao Hill ukizaa matunda basi utahamia kwa wakulima wa miti” alisema Mbwambo 

Mbwambo alisema kuwa miti milioni tatu kila mwaka ndio inatumika katika uvunaji wa utomvu na hakuna eneo maalum ambao limetengwa kwa ajili ya kuvuna bali wametoa maeneo ambayo yanamiti ambayo inatarajiwa kuvunwa baada ya miaka miwili ijayo

“Shamba hili la Sao Hill ni kubwa sana linakaribia kuwa na hekta laki moja na elfu hamsini na nne hivyo sio rahisi kufanya majaribio shamba lote hiyo tumetoa eneo ambalo miti yake inatarajiwa kuvunwa baada ya miaka miwili” alisema Mbwambo 

Mbwambo alisema kuwa soko la utomvu duniani kwa sasa linategemee kutoka nchi China hivyo soko lipo huko na kampuni ya AATY Limited ya kichini inavyovuna hapa katika shamba la Sao Hill na ni kampuni kubwa kuliko zote dunia za uvunaji wa utomvu duniani.

Akizungumza kwenye eneo la tukio mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa wamejifunza kitu kipya ambacho hawakuwahi kukifikiria katika maisha yao kuwa uvunaji au ugemaji wa utomvu unalipa kwa namna hiyo.

“Navyo sema kuwa sasa tumegundua dhahabu ya kijani namaanisha hivi,utomvu unaigiza fedha nyingi tumeana hapa mkurugenzi katueleza hivyo ni lazima tuchukue swala hili kwa umuhimu stahili ili hata kweli kwetu Chato tutalifanya kwa umakini mno” alisema Msafiri


Shamba la Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980 na shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira na shamba hilo ni miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na wizara ya maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

MBUNGE CHUMI:MAMILIONI YA FEDHA YATUMIKA KWENYE MIRADI MAENDELEO YA JIMBO LA MAFINGA MJINI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akiongea kwenye mkutano wa jimbo akiwaeleza wapiga kura wake kwa namna gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kama alivyoahidi wakati wa kumba kura kwa wananchi waliompa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Daudi Yassini akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Mufindi wakati wa upokea taarifa ya utelezaji ya Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi wakati alipokuwa akiwasilisha mambo aliyoyafanya katika jimbo hilo kwa miaka mitatu aliyopo madarakani



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wa jimbo la mafinga mjini wamenufaika na matunda ya miaka mitatu madarakani ya mbunge Cosato Chumi kwa ktekeleza ahadi zake kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 kwa ujenzi wa Kituo cha afya cha Ihongole, ujenzi wa Madarasa, mabweni na maabara katika shule za Sekondari za Changarawe, Ihongole na JJ Mungai,kushughulikia swala la maji na kufikisha umeme katika Vijiji vyote kumi na moja. 

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo Chumi alisema kuwa miradi ya Maendeleo katika Jimbo hilo ni pamoja na ujenzi wa jengo la kisasa la Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambalo liko katika hatua za mwisho, ujenzi wa matanki ya maji katika Vijiji vya Maduma, Bumilayinga, Kinyanambo na Changarawe ambako ujenzi wa tanki la ujazo wa lita milioni moja unaendelea.

“Bado kuna changamoto katika baadhi ya maeneo lakini yapo mengi yaliyofanyika ambayo ni wajibu wetu kuyasema tena wazi wazi na kuwaelewesha wananchi kwa kuwa yanaonekana kwa macho na kuwaambia kuwa changamoto zitatuliwa kulingana na muda wake hawezi kutatua changamoto zote kwa pamoja” alisema Chumi

Chumi alisema kuwa alipokuwa anaingia madarakani Mafinga hatukuwa na gari la uhakika la kubebea wagonjwa lakini kwa kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake amefanikisha upatikanaji wa magari matatu ya kubebea wagonjwa (ambulance), vitanda na ultrasounds machine ambayo inasaidia katika kuchunguza magonjwa ya kina mama Wajawazito

“wajibu wa kila mwanachama wa CCM kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi wote mwananchi wa jimbo la mafinga atambue kazi kubwa inayofanywa jimboni hapo au kwenye majimbo mengine” alisema Chumi

Aidha Chumi alisema kuwa kuna watu ambao kazi yao ni kubeza na kuwapotosha wananchi kazi zinazofanywa na serikali ya CCM,Sasa waelezeni wananchi kuwa ili kuongeza mapato ambayo yatatusaidia kujenga barabara zetu, umeme kufika kila Kitongoji ndio maana Rais Magufuli akaamua kununua ndege ili watalii wengi watembelee mbuga zetu na sisi tupate fedha

“kukaa kimya na kutoeleza na kutafsri faida kubwa ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya tano,nawaambia ndugu zangu kazi kubwa inafanyika lakini bila sisi wana-CCM kueleza umma wa watanzania, basi ni Sawa na bule au kutupa jiwe gizani bila kujua litamkuta nani” alisema Chumi

Chumi amesema kuwa wapo wanaobeza kwa kuwaambia wananchi kuwa miradi ya ujenzi wa Reli na ununuzi wa ndege haina tija wakati miradi hiyo inaenda kuchochea ukuaji wa biashara na sekta binafsi kwa ujumla.

“Anakuja mtu anakuambia Wewe treni ya umeme utapanda lini, na Wewe mwana CCM unakaa kimya, hiyo sio Sawa, mueleze wazi wazi kuwa ili tupate fedha, tunajenga reli ya kisasa ambayo itatumika kusafirisha mizigo kwenda nchi za jirani ambazo hazina Bandari, na sisi tutapata fedha ambazo zitagharamia elimu ya watoto wetu, tutajenga barabara za lami, Tutafikisha umeme kila kona ya Mafinga na nchi yote, tutapata maji ya uhakika” alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daudi Yasini alimpongeza mbunge huyo kwa kazi aliyoifanya ambayo inaonekana tofauti na kuwa na mbunge wa maneno maneno bila kazi kunekana.

JARIDA LA MRADI WA UMEME WA MAJI RUFIJI

Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images