Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

BORESHENI MAENEO YANAYOSABABISHA WANANCHI WAICHUKIE SERIKALI YAO- RAS SIMIYU

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini (hawako pichani)majadiliano hayo yanaendelea jijini Dodoma.
Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini yanayoendelea jijini Dodoma wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) aliyekuwa akizungumza na wataalamu hao juu ya kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.
Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini yanayoendelea jijini Dodoma wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) aliyekuwa akizungumza na wataalamu hao juu ya kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) akizungumza kitu na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (katikati) huku Dkt. James Jessy (kulia) muendeshaji wa majadiliano akiwasikiliza.
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) akizungumza kitu na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (katikati) huku Dkt. James Jessy (kulia) muendeshaji wa majadiliano akiwasikiliza.
………………….
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini amewataka wataalamu wanaoshiriki majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini kuangalia namna ya kuboresha maeneo ambayo yanawapa mamlaka watu walio katika nafasi za kuzuia uhalifu, ukamataji, uendeshaji wa mashtaka, utoaji adhabu na urekebishaji wa wahalifu kuacha vitendo vinavyowagonganisha wananchi na Serikali.
Bw. Sagini ameyasema hayo jlipokuwa akizungumza na wataalamu wanaoshiriki majadiliano ya pamoja ya kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai yanayoendelea jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo huo na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuona kwa pamoja namna ya kufanya maboresho katika Mfumo wa haki jinai nchini.
“Ndugu washiriki , niwaombe hapa muangalie maeneo yote yanayotoa mwanya kwa maafisa wanaohusika na uzuiaji wa uhalifu, ukamataji wahalifu, uendeshaji mashtaka, utoaji adhabu na urekebishaji wahalifu, vitendo hivi vinafanya wananchi waone kuwa hawatendewi haki na Seriakli yao na hivyo kusababisha wananchi kusigishana na Serikali yao kutokana na vitendo vinavyofanywa na maafisa wa Serikali katika maeneo hayo,” amesema.
Amesema uamuzi wa kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai ili uweze kuendana na nyakati zilizopo utawezesha kila mwananchi kupata haki yake pale anapostahili na hivyo kuondoa dhana ya kuoneana ambayo imeshamiri kwa wananchi.
Amesema anaamini kuwa maboresho katika mfumo huo yatawezesha watendaji katika maeneo husika kuondokana na tabia za mazoea ambazo zimekuwa kawaid kwa watendaji hao kuwaonea wananchi na hivyo kuwanyima haki.
Bw. Sagini pia ametaka washiriki kuangalia namna ya kuboresha maeneo ya uwezeshaji kwa watendaji wa serikali ili kupunguza vitendo mbadala kwa ajili ya kufanikisha utendaji wa kazi zao ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa program za mafunzo zitakazowafanya wahalifu wakiwa gerezani kupata ujuzi na utaalamu wa maeneo fulani na hivyo kuwa raia wema ambao hawako tayari kurejea magerezani pindi wanapokuwa wameachiliwa kutoka huko.
Amesema maeneo hayo yakizingatiwa yataimarisha Imani ya wanachi kwa serikali yao na hivyo kuona wako katika mikono salama huku wakiamini kuwa Serikali yao iko pamoja nao katika kuhakikisha wananchi wote wanapata haki.

NEWS ALERT: AZIM DEWJI ,WAANDISHI WATATU WANUSURIKA AJALINI

$
0
0
Na Sultani Kipingo wa Michuzi TV.

Mfanyabiashara maarufu nchini Azim Dewji na Waandishi Watatu wa vituo vya televisheni ya ITV,Chanel Ten na Azam TV wamepata ajali leo Julai 27,2019 majira ya asubuhi  baada ya gari lao kuacha  njia na kuingia vichakani kijiji cha Nyamwinywili,Rufiji mkoani Pwani.

Akiongea na Michuzi TV, Dewji, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shia Ithnaasheri, amesema anaendelea vyema na matibabu hospitalini hapo, huku akitoa shukurani kwa madaktari katika Hospitali ya Misheni ya Mchuki alikopatiwa matibabu ya awali, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. John Kiang’u Jingu  na Wasaidizi wake ambao amesema walikatisha safari ya kuelekea Rufiji ili kumfikisha hospitali hapo.

Dewji, ambaye aliwahi kuwa mfadhili wa simba miaka ya 1990, amewashukuru pia madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI kwa kile alichoeleza ni weledi wa hali ya juu kwa huduma bora alizopatiwa toka alipopelekwa hapo na anazoendelea kupatiwa.

“kwa kweli huduma za hapa Muhimbili hazina tofauti na huduma utazopata katika hospitali yoyote kubwa duniani”, amesema Dewji. “Kwa kweli nimeshangaa na nawashangaa wale ambao baada ya kupata matatizo hawaji hapa Muhimbili. Pako vizuri kwa kweli…”

Akielezea chanzo cha ajali, anasema tairi lilipasula na kusababisha dereva wake kuacha barabara na kuingia porini kabla ya kugonga mfereji na kusababisha gari kupaa juu na liliporudi ndipo yeye akaumia uti wa mgongo.

“Wengine wote walitoka salama. Kwa kweli ajali ni majaaliwa ya Allah. Tulikuwa tumebakiza dakika kama ishirini hivi kufika kwenye hafla ya kuweka jiwe la Msingi la Rufiji Hydro Power Project ndipo tukapatwa na kadhia hiyo”, amesema Dewji.

Amesema alikuwa ndani ya gari akiwa na wanahabari kadhaa ambao aliwapa lifti baada ya kuachwa na gari maalumu waliloandaliwa, na kuongeza kwamba anashuru wanahabari hao wote wako salama na waliendelea na safari kwenda kwenye eneo la sherehe.

“Nilienda kumsapoti Mheshimiwa Rais wetu na tutaendelea kumsapoti” alisema Azim na kuongezea: Tunamwombea kila siku Mungu amlinde na maadui wake ili aendelee kutuongoza kufikia Tanzania ya asali na maziwa ambayo imeshaanza kuonekana…”
Madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Misheni ya Mchuki wakimpatia Azim Dewji huduma alipofikishwa hapo baada ya kupata ajali 
Madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Misheni ya Mchuki wakiendelea kumpatia Azim Dewji huduma na uangalizi alipofikishwa hapo baada ya kupata ajali 
Azim Dewji akisubiri kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata rufaa katika hospitali ya Micheni ya Mchuki alikopatiwa huduma na uangalizi wa awali

MBUNGE MASABURI AWASIHI VIJANA KATIKA SUALA LA MAADILI NA NIDHAMU KWA VIONGOZI

$
0
0
MBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Janeth Masaburi  ameeleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya vijana  wataifa  kukosa  maadili kwa kuwanenea maneno yasiyo ya maadili  wazee na viongozi jambo ambalo limesababisha wazee kupata maradhi ya moyo ama msongo wa mawazo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Mbunge  Maburi , amesema  moja ya jambo linalochangia hilo ni pamoja na kukosa  upendo na maadili kutoka kwa wazazi wote wawili, kuiga mambo kutoka nchi za magharibi, wazazi kuwa dekeza watoto kupita kiasi, taama za haraka haraka na kutaka utukufu bila  kuwa na karama za mwenyezi Mungu, kukosa hofu ya Mungu, wazazi kutosimamia watoto katika misingi ya imani kwa kuwafundisha kuwa na upendo  na  kusamehe.

Aidha amewataka watanzani kuwa wamoja bila kugawanyika  katika kipindi hiki ambacho nchi inapiga hatua kimaendeleo na kusema kuwa katika miaka mitatu kuelekea minne ya utawala wa awamu ya tano  mwelekeo wa Rais Magufuli amekuwa mfano wa kuigwa kwani amejitolea kuwasaidia na kuwavusha watanzania kuwatoa katika zama za ujanja ujanja  (mission town) kuwa wachapa kazi.

Amesema kuwa miaka iliyopita  kulikuwa na shida kubwa katika upatikanaji wa huduma za maji, afya, elimu na ufisadi uliokithiri.

“Sisi sote tunao kula viapo kupitia vitabu vitakatifu Biblia na Quran tutambue kuwa viapo hivi vitatutafuna mbele za haki hivyo tusijidanganye  na kuwa jeuri kwa kuwa tuko hai tuanapumua  maslahi ya watu wa Mungu  ni ya kwanza kuliko nafsi zetu" ameeleza.

Amesema kuwa; "
 Rais Magufuli amekomesha ujangili, kaleta nidhamu kazini hasa katika ofisi za umma, heshima kwa wote hata mtaani tunaheshimiana, zamani ukimpeleka mtu Polisi baada ya kukutendea jambo baya  ubadilishiwa kesi wewe ndiyo unakuwa mshitakiwa" ameeleza.

Vilevile amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli iwepiga vita dawa za kulevya kwa nguvu zake zote na kuwaokoa  vijana walikuwa wanaharibika kila siku na wauza unga wakambilia nchi za nje.


Amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa jasiri wa kutetea wanachi na nchi yake kwa kupitia mikataba ya madini, na kusema kuwa chama cha Mapinduzi CCM kina hazina ya viongozi ambao  ni  mabalozi wa taifa.

“Tanzania yaleo siyo yajana na  CCM yaleo nibora kuliko  jana, Mwenyezi Mungu tunakuomba  mbariki rais wetu Dkt John Pombe Magufui  mpe ulinzi wako wote kwakuwa ana kutamka mbele ya mataifa  nawewe ulisema anaye nitamkana mbele ya mataifa, Magufuli amekutukuza mbele ya mataifa  kikasiku anaomba msaada  wako umlinde “Ameeleza.

WATU 12 KORTINI KWA KUKWEPA KULIPA KODI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
Watu 12 wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la  kukwepa kodi na kusababisha hasara ya zaidi ya sh. Milioni 100.7/-

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Janet Magoha amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Rose Kerandi, Ally Abdul, Geoffrey Kayanza, Anwar Rubeya,  Khalid Kigoma, Joseph Marcelo, Samir Hussein, Matiku Mgaya Iddi Bogaboga, Edward Maguri, Alex Sanga, Said suleman, Lali Mohamed na Hamidu Abu.
Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa, Siku na mahali pasipo julikana, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kukwepa kodi.

Katika shtaka la pili imedaiwa  February 21, 2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa walishindwa kulipa kodi ya sh. 100,739,873 ya mzigo wa ambao walikuwa wakiuingiza  nchini.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa, Siku na mahali hapo waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho cha fedha kwa nia ovu ya kutokulipa kodi ya bidhaa ya kontena la futi 40 lilolokuwa limebeba  mikoba.

Hata hivyo wakato wakisomewa mashtaka hayo, washtakiwa  Anwary Rubeya, Joseph Marcelo, Matiku Mgaya na Idd Bogobogo hawakuwepo mahakamani hapo na mahakama imetoa hati ya wa washtakiwa hao kukamatwa ili waweze kufika mahakamani hapo kujibu mashtaka yao.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu Uchumi na imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa utetezi, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGA MAFUNZO YA SABA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza maandamano kwa Wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam Luteni Jeneral Paul Peter Massao wakati wa Mahafali ya Saba ya Chuo Hicho leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifunga Mafunzo kwa Wahitimu wa Mahafali ya Saba wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akikmabidhi Cheti Zhao Zishun kutoka China ambae ni Mmoja kati ya Wahitimu wa Mafali ya Saba ya Chuio cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar Es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na na Viongozi na Wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Brigedia Gegeral Mbaraka Naziad Mkeremy wa JWTZ Mmoja kati ya Wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na CDF Mstaafu George Waitara walipokutana kwenye Mahafali ya Saba ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kumpongeza Mindi H. P. Kasiga Mmoja kati ya Wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Kunduchi Jijini Dar es salaam leo Julai 27, 2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI HASUNGA AAGIZA KUKAMATWA MFANYABIASHARA ALIYEUZA MBEGU FEKI WILAYANI MBOZI

$
0
0
Wakazi wa kijiji cha Weru 1 Kata ya Wasa wakicheza ngoma ya asili na mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Wakazi wa kijiji cha Weru 1 Kata ya Wasa wakisikiliza hotuba ya mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019.
Wakazi wa kijiji cha Iganduka Kata ya Wasa wakisikiliza hotuba ya mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mhr John Palingo kumkamata mfanyabiashara aliyewauzia wakulima mbegu feki katika wilaya hiyo hivyo kuathiri mavuno kwa wakulima.

Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano yake katika kijiji cha Isalalo, Wasa na Malolo vilivyopo katika kata ya Wasa kadhalika akiwa katika kijiji cha Msia, Weru 1 na Iganduka vilivyopo katika kata ya Msia.

Waziri huyo wa Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa kitendo cha mtu kuuza pembejeo feki ni cha uhujumu wa Kilimo na uchumi na kwamba serikali haiwezi kuvumilia hali hiyo."Katika hili namwagiza mkuu wa wilaya kumkamata msambazaji wa mbegu hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa" alisema Hasunga.

Kauli hiyo ameitoa kufuatia swali la mkulima mmoja mkazi wa Kijiji cha Malolo Ndg Isaya Nyondo ambaye alitaka kujua hatua zipi zinachukuliwa na serikali kufuatia kuuziwa mbegu feki na hivyo kufanya washindwe kuvuna mwaka huu.

Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuimarisha sekta ya Kilimo hivyo mfanyabiashara yeyote anayecheza na ufanisi wa wakulima atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

MPINA ASHIRIKI MAZISHI YA OFISA MFAWIDHI WA ULINZI WA RASILIMALI ZA UVUVI NA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU KANDA YA UKEREWE

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akishirikiana na waomboleza kubeba mwili wa Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Kupambana na Uvuvi Haramu Kanda ya Ukerewe, Marehemu Ibrahim Juma Njarari aliyezikwa wa kijijini kwake Kyangasaga wilayani Rorya mkoani Mara.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akiweka udongo kwenye kaburi la Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Kupambana na Uvuvi Haramu Kanda ya Ukerewe, Marehemu Ibrahim Juma Njarari aliyezikwa wa kijijini kwake Kyangasaga wilayani Rorya mkoani Mara.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akikabidhi Hati ya Ushujaa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Familia ya Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Kupambana na Uvuvi Haramu Kanda ya Ukerewe, Marehemu Ibrahim Juma Njarari aliyezikwa wa kijijini kwake Kyangasaga wilayani Rorya mkoani Mara.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akikabidhi Hati ya Ushujaa kwa Familia ya Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Kupambana na Uvuvi Haramu Kanda ya Ukerewe, Marehemu Ibrahim Juma Njarari aliyezikwa wa kijijini kwake Kyangasaga wilayani Rorya mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Samson Chacha na Mkurugenzi wa Uvuvi, Magesse Bulayi wakiweka udongo kwenye kaburi la Ofisa Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Kupambana na Uvuvi Haramu Kanda ya Ukerewe, Marehemu Ibrahim Juma Njarari aliyezikwa wa kijijini kwake Kyangasaga wilayani Rorya mkoani Mara.

Benki ya Exim Yashiriki Bonanza la Tanzania On Twitter (TOT Bonanza) Kwa Kuhamasisha Uchangiaji wa Damu

$
0
0
Meneja Masoko na Mahusiano ya jamii wa Benki ya Exim, Bw Abdulrahman Nkondo akichangia damu wakati wa Bonanza la kijamii linalofahamika kama Tanzania On Twitter (TOT Bonanza) lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Anaemuhudumia ni Afisa Mwandamizi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Bw Peter Chami.
Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama- Kanda ya Mashariki Bi Fatuma Mjungu (Kushoto) akimuhudumia mmoja wa washiriki wa Bonanza la kijamii linalofahamika kama Tanzania On Twitter (TOT Bonanza) Bi Irene Lyimo aliejitokeza kuchangia damu wakati wa Bonanza hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Plasco expands operations - launches the first state of the art pipe factory in East and Central Africa using ‘Weholite’ technology

$
0
0
Plasco Limited in Tanzania is the largest manufacturer of plastic pipes for water supply and sanitation in the country has launched a USD 4 million factory expansion using ‘Weholite’ technology, the first of its kind in East and Central Africa used to produce Structured Wall High Density Polyethylene (HDPE) pipes for Sewerage and Drainage, Manholes and Tanks for storm water retention and drinking/potable water. 

The company aims to provide modern water storage and sanitation solutions to the region through the use of this new technology that is now available in Tanzania and East Africa as a whole. The factory was inaugurated in Temeke, Dar es Salaam by the Minister of Industry and Trade, Innocent Bashungwa; other government official in attendance included the Deputy Permanent Minister of Water, Emmanuel Kolobelo. 

Speaking during the event, Hon. Bashungwa remarked on the company’s use of innovative technology to accelerate the progress of the pipe manufacturing industry in Tanzania. “The ministry applauds such innovations which directly contribute to catalysing industrial development and increases the competitiveness of our industries, locally and internationally. The factory expansion and its use of cutting-edge technology is a significant milestone in the revival of the industrial economy,” said Bashungwa. 

He added that the new technology will attract more investment and boost the economy of the country through exports. Bashungwa urged other industries to invest in innovative technology to boost the quality of their products to international standards. 

Speaking on behalf of the company, Alimiya Osman, the Chief Operating Officer, disclosed that the country will no longer need to import plastic pipes as the investment in new equipment meets the growing demand and aligns with local content policy. He added that the use of HDPE materials ensures that the pipes do not rust or corrode and adheres to international standards. 

“Since the start of the company’s operations in 1993, we remain committed to manufacturing and supplying quality, robust and leak proof plastic piping systems to our customers in Tanzania and neighbouring countries. The investment in new equipment supports the government’s efforts to develop critical infrastructure to improve water supply and sanitation systems that will improve the lives of Tanzanians throughout the country,” concluded Alimiya. 

As the country’s leading pipe manufacturer, Plasco Limited employs over 100 Tanzanians and supports the country’s industrialization drive and ambitions to become a middle-income economy by 2025. 

Minister of Industry and Trade Innocent Bashungwa launching Plasco Ltd extension factory that uses Weholite technology which is the first in Tanzania, East and Central Africa to produce plastic pipes. Dar es Salaam, today Third left is Plasco Ltd Chief Operating Officer, Alimiya Osman and Finland Ambassador for Tanzania, Ambassador Riitta Swan (Right).
Minister of Industry and Trade Innocent Bashungwa commending the technology and the quality of pipes produced by Plasco Ltd to during the launching ceremony of an extension factory that uses Weholite technology which is the first in Tanzania, East and Central Africa to produce plastic pipes, Dar es Salaam, today. Right is Plasco Ltd Chief Operating Officer, Alimiya Osman.


WAZIRI LUGOLA ATAKA VIONGOZI WA TAASISI ZAKE KUACHA KUWANYANYASA ASKARI, WATUMISHI RAIA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia)
akizungumza na askari na watumishi raia waliochini ya Wizara
yake, mjini Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro,
leo, akiwataka kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa. Pia
aliwataka viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuacha
tabia ya kuwanyanyasa watumishi, na pia wahakikishe
wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na
kulipwa fedha za likizo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),
akimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hassan Okello,
alipokua anatoa taarifa ya kikao cha askari na watumishi raia,
mjini Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, leo.
Lugola amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii bila
kukata tamaa. Pia aliwataka viongozi wa vyombo vya Ulinzi na
Usalama kuacha tabia ya kuwanyanyasa askari na watumishi
raia, na pia wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha
mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza
na askari na watumishi raia waliochini ya Wizara yake, mjini
Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro, leo, akiwataka
kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa. Pia aliwataka viongozi
wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuacha tabia ya
kuwanyanyasa watumishi, na pia wahakikishe wanawapandisha
vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za
likizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto),
akimsalimia Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Innocent
Magesa, wakati alipokuwa anawasili mjini Ifakara, leo kwa ajili
ya kufanya ziara ya kikazi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo,
James Ihunyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.

**************

Na Felix Mwagara, MOHA-Ifakara.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka
viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya
Wizara yake nchini, kuacha tabia ya kuwanyanyasa askari
waliochini yao na wahakikishe wanawapandisha vyeo,
wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo.

Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili
kupandishwa vyeo na kurekibishiwa mishahara, kwa kuwa
Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli askari hao wana haki kwa
mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi
wa Wizara yake, mjini Ifakara, Wilaya Kilombero, Mkoani
Morogoro, leo, Lugola alisema katika uongozi wake hataki
kusikia askari wananyanyaswa na kiongozi yeyote wa Taasisi
zake.

Lugola alisema, unyanyasaji, kutokupandisha vyeo, pamoja na
kulipwa fedha zao za likizo, changamoto hizo zinapunguza
nguvu ya utendaji kazi wa askari hao wanaofanya kazi ngumu.

Waziri Lugola aliongeza kuwa, alitoa agizo la askari
wanaostahili kupandishwa cheo, kurekebishiwa mishahara yao,
wanaodai kulipwa fedha za uhamisho pamoja na changamoto
mbalimbali zingine alizozielekeza.

“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara
yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini, lakini naamini kila kitu kinaenda vizuri na ahadi niliyoitoa
itakamilisha kwa wale askari ambao wanasifa watapewa vyeo
hivi karibuni,” Alisema Lugola.

Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi
ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli anatoa
mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna
upungufu mkubwa wa nyumba hizo.
“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la
ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali
inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,”
alisema Lugola.

Pia Lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari
wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na
atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi.

Lugola alisema jambo ambalo linamuumiza kichwa ni kuhusu
madai ya askari na watumishi wa wizara yake ambayo anasema
kama wafanyakazi hawatalipwa haki zao na utendaji wa kazi
utapungua.

Waziri Lugola yupo Mkoani Morogoro kikazi na tayari
amemaliza ziara yake Wilaya ya Kilombero, na anatarajia
kufanya ziara hiyo katika Wilaya za Malinyi na Ulanga Mkoani
humo.

WAZIRI MKUU AAGIZA WALIMU WAWILI WAPELEKWE NANGANGA KESHOKUTWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Nanganga wilayani Ruangwa, Julai 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Afisa Elimu wa Wilaya ya Ruangwa anayeshughulikia elimu ya msingi, Bw. Selemani Mrope atafute walimu wawili kutoka Ruangwa na kuwahamishia kata ya Nanganga mara moja.

“Lazima kuna walimu wamejazana pale Ruangwa mjini, leo tukitoka hapa nenda kaandike barua za uhamisho. Kesho Jumapili, wahusika wapewe barua zao na Jumatatu waje kuripoti hapa Nanganga,” amesema Waziri Mkuu na kuamsha shangwe miongoni mwa wakazi wa Nanganga.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2019) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nanganga, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi alipopita kuwasalimia wakazi hao.

Waziri Mkuu ambaye amewasili Lindi leo kwa mapumziko mafupi, alipokea taarifa ya shule ya msingi Nanganga ambayo ilionesha kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 237 ina walimu sita tu. Kati ya hao, wavulana ni 124 na wasichana ni 113.

“Shule hii ina madarasa nane likiwemo darasa la awali, masomo yanayofundishwa ni tisa, mkibaki na walimu hawa sita, mzigo unakuwa mkubwa kwa walimu hawa waliopo. Afisa Elimu tafuta wawili walimu waje hapa Jumatatu, na Mkurugenzi wa Halmashauri atakupa gari ya kuwahamishia hapa,” amesema. Shule ya msingi Nanganga, iliyoko kata ya Nanganga, iko umbali wa km. 59 kutoka Ruangwa mjini.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa Ruangwa, amewataka wakazi wa kata hiyo wafikirie kuanza ujenzi wa shule ya sekondari yao ya kata ili kuwapunguzia safari wanafunzi wa kijiji hicho ambao kwa sasa wanalazimika kwenda kusoma Nangumbu, iliyoko umbali wa km. 10.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, Serikali imetoa sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ambayo yakikamilika walimu watapata ofisi pia.Amesisitiza kwamba fedha hizo zitumike kujenga madarasa manne ambapo walimu pia watapata ofisi moja. 

Pia amemwambia diwani wa kata ya Chinongwe, Bibi Maki Camillius kwamba katika bajeti ya mwaka huu, kata hiyo itapatiwa sh. milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za walimu katika shule ya sekondari ya kata ya Chinongwe.

Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Amiri Musa Kambona alisema madarasa mawili na ofisi moja ya walimu vilibomoka mwaka 2014 kutokana na mvua na upepo mkali na kusababisha upungufu wa madarsa na ofisi.

Akielezea changamoto nyingnea za shule hiyo, Mwalimu Kambona alisema shule ina upungufu wa nyumba moja ya walimu, darasa moja, matundu mawili ya vyoo vya walimu, ofisi moja ya walimu na kukosekana kwa chanzo cha maji safi na salama kwa matumizi ya wanafunzi na walimu.

Anne Makinda awaasa madiwani wanawake kuwajibika

$
0
0
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina ya kujenga uwezo viongozi wanawake wa serikali za Mitaa (WASEMI).


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amewataka wabunge na Mdiwani wa vitimaalum nchini kusimamia kikamilifu rasilimali za umma ili ziwanufaishe wananchi wote.

Akizungumza Jijini Mwanza katika semina ya kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wa serikali za Mitaa (WASEMI) iliyoandaliwa na shirika la TGNP Mtandao, Makinda alisema kwamba, mchango wa wabunge na madiwani wa viti maalum umekuwa hauonekani vizuri au kutambuliwa na jamii kutokana na wao wenyewe kuwa na hofu au kutokujiamini kitu ambacho kimechangia kuwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea mbele.

“tatizo letu sisi viongozi Wanawake, tunajenga hofu, tunaogopa sana kujitokeza na kuwajibika vizuri kwa wananchi, eti kwa sababu ni viti maalum. Sisi tulianzia pia viti maalum , lakini tulipata nafasi ya kwenda jimboni kwasababu tulijiamini, tuliwajibika kikamilifu na tulihangakikisha uwezo wetu unaonekana na kila mmoja. Jitokeze, kwa wananchi, watumikie kwa uadilifu na watakuona na kutambua mchango wako” alisema Makinda

Makinda amewaasa wanawake viongozi wa serikali za Mitaa, kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma za jamii kwenye halmashauri zao na kuhakikisha kila kinachofanyika kwenye halmashauri wanakielewa vizuri na kutoa taarifa kwa wananchi wote.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake viongozi wa serikali za Mitaa (WASEMI), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Kibena Kingo, alisema kwamba WASEMI itahakikisha wenyeviti wa halmshauri wanawake wanaonesha mfano bora wa utendaji uliotukuka kwenye halmashauri zao hasa kutokomeza rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na kuhakikisha kila senti iliyopangwa kwajaili ya kuboresha maisha ya wananchi inatumika vizuri.

“Niwaombe ndugu zangu, viongozi wanawake wa halmshauri pamoja na madiwani, sisi wanawake tumeaiminiwa tukapewa nafasi, tusimamie vizuri rasilimali za halmshauri zetu, tujenga mtandao wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, tutenge bajeti nzuri inayozingatia usawa wa kijinsia na kuboresha maisha ya wananchi wote bila ubaguzi” alisema Bi. Kingo

Mkutano huu ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa TGNP Mtandao na WASEMI ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Serikali za Mitaa ALAT Gulamhafeez Mukadam, na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Bi. Anjelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza. 

Tanzani ina Halmshauri 185, ambapo kati ya hizo, wanawake wanaoongoza Halmshauri ni watano pekee ambazo ni halmashauri za Biharamulo, Hai, Mwanga, Morogoro na Gairo. Ambao wamekubaliana kuhakikisha wanaweka hitoria ya kuwa halmashauri za mfano kwa maendeleo na zenye kuzingatia usawa wa kijinsia katika Nyanja za uongozi na mipango.
Mwenyekiti wa Umoja wa Serikali za Mitaa ALAT Gulamhafeez Mukadamika akitoa neno katika semina iliyofanyika jijini Mwanza ya kuwajengea uwezo viongozi wanawake wa serikali za mitaa.
Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Bi. Anjelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza akiongea na washiriki wa semina hiyo.

SERIKALI YAZINDUA MKAKATI KABAMBE KUDHIBITI MBU NA WADUDU WADHURIFU

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 28,2019

DAWASA WACHOCHEA UJENZI MRADI UMEME KWA KUPELEKA MAJI KUTOKA MTO RUFIJI

$
0
0
Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es salaam (DAWASA) wameweza kuwa moja ya chachu ya mradi wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji (Stiegler's Gorge) kwa Kukarabati mradi wa maji uliojengwa miaka ya 1970.

Mradi huo wa maji ni kwa ajili ya kutoa huduma katika kambi ya ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa Rufiji Mkoani Pwani ambao utakamilika Juni 2022 na kuzalisha megawati 2,115 baada ya kujenga miundo mbinu ya maji.

DAWASA wameweza kufanikisha hilo kwa kujenga mfumo wa maji kutoka kwenye chanzo cha Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) na kulaza mabomba yaliyopeleka maji kwenye matanki.

Mradi huo wa kufua umeme umewekewa jiwe la msingi na Rais Dkt John Pombe Magufuli jana ambapo kukamilika kwake kutachochea ukuaji wa uchumi.

Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo zimefanyika kando ya eneo litakapojengwa bwawa la maji na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nishati wa Misri Mhe. Dkt. Mohamed Shaker, Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Tanzania, Wabunge, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali.

Kwa upande wa DAWASA, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema watatumia fursa ya bwawa hilo kwa kuangalia namna ya kujenga mtambo na kuanza kuzalisha maji kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi.

Amesema, lengo la DAWASA ni kuleta maji kutoka maporomoko ya Stieglers Gorge na mchakato huo tayari umeanza ikiwemo kuunda timu ya wahandisi wa mradi kufanya usanifu ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wake huku fedha zitakazotumika zikiwa ni za ndani na utekelezaji wa mradi huo mkubwa utasaidia kuondoa ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani na kuifanya Dar es Salaam kuwa salama zaidi kwa matumizi ya maji safi na salama.

Mradi wa maji kutoka maporomoko ya Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) umesimamiwa na DAWASA na kugharimu kiasi cha Milioni 604.9 na umekamilika Mwezi Agosti mwaka jana ukiwa na uwezo kuzalisha maji lita 209,000( laki mbili na elfu tisa) kwa ajili ya matumizi ya kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji wa megawati 2115.

Mradi huo wa maji utawasaidia wakandarasi kuwa na miundo mbinu wezeshi itakayowapatia maji muda wote wa matumizi yao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanusi mkubwa na kusaidia mradi wa ujenzi la bwawa la kufua umeme kukamilika kwa wakati.

DAWASA walikarabati miundo mbinu iliyokuwa chakavu ikiwemo ukarabati wa eneo la chanzo pamoja na ufungaji wa pampu moja mpya itakayokuwa na uwezo wa kuchota maji mtoni kiasi cha lita 2.41 kwa sekunde, ulazaji wa mabomba ya kusambazia maji na urefu wa Km 1463 kutoka mahali maji yanapopatikana ambapo mradi huo wa maji utapeleka maji kwenye matanki makubwa mawili.

Katika ukarabati huo pia waliweza kuhusisha bomba la kusafirishia maji (GS pipe) kipenyo cha nchi 3, ujenzi wa bomba jipya la plastic(HDPE) la kusafirishia majighafi kutoka mto Rufiji hafi kwenye tanki na kituo cha kusafisha maji, ukarabati wa kituo cha kusafisha maji, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji, ujenzi wa bomba la kusafirishia maji, ukarabati wa matanki mawili ya zamani ya lita 12,500 na 22,500 na ufungaji wa dira za maji , air valve 4 na gate valve 4.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la Kufua umeme na watatumia fursa ya bwawa hilo kwa kuangalia namna ya kujenga mtambo na kuanza kuzalisha maji kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi.

MAGUFULI AMEFANYA MENGI, ASIYEONA MWAMBIE AFUMBUE MACHO-KHERI JAMES

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.

Vijana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Kagera, wametakiwa kueleza kazi nzuri na kubwa iliyofanywa Nchi nzima na Uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Kagera ikiwa miongoni na kwamba hizi sio zama za propaganda.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Kheri James wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kagera ya Kijani mapema Julai 27, katika viwanja vya Hamugembe ndani ya Manispaa ya Bukoba, katika sherehe za Uzinduzi wa mkakati wa Kagera ya Kijani, zilizohudhuliwa na Wananchi, wanaharakati, makada na Viongozi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Kagera.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Kagera, katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi juu ya mambo makubwa yaliyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, Ndg. Kheri amesema Mhe.Rais Magufuli Amefanya mambo mengi kila sehemu ambayo mengi hayakuwezekana kwa kipindi cha nyuma lakini sasa yanaonekana dhahiri na kwa asiyeona basi afungue macho, kwani mambo makubwa yanakuja.

"Leo Vijana wote, akina mama wote, walemavu wote wana haki ya kupata fedha kutoka halmashauri zao, na fedha hizi zimefutiwa riba.......fungua macho" amesema Ndg. Kheri 

Katika sherehe hizo Ndg. Kheri amepokea zaidi ya Vijana 50 walojiunga na CCM wakitokea vyama mbali mbali, waliokiri utendaji wa Dkt. John Pombe Magufuli, huku wajumbe, makada na wawakilishi wa CCM katika nyadhifa mbalimbali wameonesha utayari wa kutaka kufanya vizuri zaidi katika chaguzi ndogo zijazo za serikali za mitaa kwa kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinaibuka na ushindi mnono lilikiwa hasa ndilo lengo la Mkakati wa Kagera ya Kijani.

Hayo yanajiri wakati ambapo Taifa linajiandaa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, ikiwa kwa Kagera baadhi ya mitaa katika Wilaya inaongozwa na Vyama vya upinzani, huku Maandalizi zaidi yakielekezwa katika Jimbo la Bukoba Mjini linaloongozwa na Upinzani pia.
 Pichani Ni Mwenyekiti wa Vijana CCM Taifa, Ndg. Kheri James akihutubia umati uliofurika katika sherehe za Uzinduzi wa Kagera ya Kijani, Mjini Bukoba.

 Pichani Ndg. Kheri James M/kiti UVCCM Taifa akimshukuru Bi. Joan Kataraiya kwa ahadi ya Shilingi Milioni Moja ya Ukarabati wa Jengo la CCM Wilaya, katika harambee iliyofanywa na Kiongozi huyo.
 Pichani ni wafuasi wa vyama vya upinzani waliorejea na wengine kujiunga na CCM rasmi baada ya kuridhika na utendaji kazi wa Awamu ya Tano.
 Pichani Ndg. Kheri James M/kiti wa UVCCM Taifa akikabidhiwa kadi na bendera za wanachama wapya waliojiunga na CCM katika sherehe za uzinduzi wa Kagera ya Kijani.
 Pichani Ndg. Joani Kataraiya akikabidhi bendera 400 kwa M/kiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri James lengo likiwa kwenda kuongeza hamasa katika Chaguzi zijazo.
Kagera ya Kijani Tukutane Kaziini

Wanawake washauriwa kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya vipodozi

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha.

WANAWAKE wameshauriwa kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya vipodozi vilivyoidhinishwa na mamlaka za kiserikali ili kuepukana na magonjwa hatari ya ngozi yanayotokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari kwa afya za watumiaji.

Ushauri huo umetolewa na Dk.Irene Shayo wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Ecollagen inayotengenezwa na kampuni ya Oriflame ya nchini Sweden .Bidhaa hiyo ni vipodozi vilivyotengenezwa kwa viambata asilia kama mimea na matunda na havina kemikali za viwandani.

“Bado kuna kiwango cha juu cha matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatarishi kwa afya ngozi miongoni mwa wasishana, wanawake na hata vijana wa kiume wa Tanzania, hivyo juhudi kubwa zinahitajika kuwaelimisha madhara ya matumizi ya vipodozi hivyo hatarishi”alisema Dk.Shayo.

“Wengi wanatumia vipodozi hivi kutokana na upatikanaji na bei zake kuwa rahisi, lakini madhara yake ni makubwa sana na ni chanzo cha maradhi hatari kama kansa ya ngozi na kuharibika kwa ngozi ndani ya kipindi cha muda mfupi”aliongeza Daktari huyo.

Alisema tafiti mbalimbali zilizofanywa na Madaktari na Wataalamu wabobezi wa vipodozi na afya ya ngozi umethibitisha kuwa kemikali hizo hatari hundoa seli za ngozi zinazoitwa Melanin ambazo ndizo zinazomfanya binadamu kuwa na rangi nyeusi.

“Kemikali hizo huondoa seli za Melanin ambazo ndiyo zinazolinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua na hata moshi wa viwandani kwahiyo inakuwa rahisi kwa mtumiaji kushambuliwa na maradhi kama kansa ya ngozi”aliongeza Dk.Shayo.

Madhara mengine kwa watumiaji kwa mujibu wa Daktari huyo kwa wanawake wanaotumia vipodozi vyenye kemikali (mkorogo) ni pamoja na uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo,ugumba na maradhi ya figo.

Utafiti uliofanywa na Profesa Msaidizi Kelly Lewis wa Chuo Kikuu cha Georgia Atlanta cha nchini Marekani kitengo cha Sosholojia nchini Tanznia kati ya mwaka 2000 hadi 2012 unaonyesha kuwa asilimia 30 ya wanawake kati ya milioni 23 nchini ambayo ni sawa na wanawake milioni 6 wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari.

Kwa upande wake mmoja wa maaifisa masoko wa kampuni hiyo ya Oriflame Maribel Mwenda alisema kampuni hiyo imekuja na mfumo wa mauzo wa moja kwa moja (networking marketing) biashara ya mtandao kwa lengo la kuzuia watu wasiowaaminifu kunakili (fake) biadhaa zao na kuziingiza sokoni.

“Kupitia mfumo huu watumiaji au wateja wanapata fursa tatu, kupendeza,kupata faida na kupata ajira na kipato cha uhakika kutokana na faida inayopatikana katika mauzo”alisema.

Naye Suzan Mlay ambaye ni Mkurugenzi mwenye hadhi ya Juu (Senior Gold Director) wa kampuni hiyo ya Oriflame alisema vipodozi vya Ecollagen vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa zaidi isiyo madhara kwa watumiaji wa jinsia zote na hupunguza “uzee” katika ngozi kwa asilimia 49.

“Bidhaa zetu zimegawanyika katika makundi manne ya manukato ya kike na kiume,ya kulinda ngozi,(skin care),bidhaa za urembo wa rangi na kabla ya mteja kutumia hupewa kwanza ushauri wa kitaaalamu kwa kulingana na muonekano na afya ya ngozi yake”alisema.

Kampuni ya Oriflame ni ilianzishwa nchini Sweden miaka 50 iliyopita na ni kati ya makampuni makubwa yanayoongoza kwa utengenezaji na biashara ya vipodozi duniani ikisambaza biadhaa zake zake katika nchi zaidi ya 65 duniani

SHONZA ASHIRIKI TAMASHA LA UREMBO WA ASILI

$
0
0
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe . Juliana Shonza (katikati) akipata maelezo ya vipodozi visivyokuwa na kemikali vilivyotengenezwa na wajasiriamali wa Tanzania wakati wa Tamasha la Urembo wa Asili lililofanyika jana Julai 27/2019 katika viwanja vya Life Park Jijini Dar es Salaam.

UVCCM YAWATAKA WANACHAMA WA CCM KUHAMASIKA NA KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT MAGUFULI ZA KUJENGA NCHI

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary Kubecha akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa shina la Chama cha hicho wetulopo eneo la Mwembe radu, Mwembe Yanga Wilayani Temeke.


 Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa  Japhary Kubecha akisoma jumbe zilizoandikwa kwenye shina hilo la Mwembe radu,Wilayani Temeke.

 Mjumbe wa Halmashauri kuu Japhary Kubecha akizungumza mbele ya wanaCCM waliojitokeza katika Uzinduzi wa shina la Mamboleo Lililopo Sandari,Wilayani Temeke.

 Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary Kubecha akivishwa kitambaa shingoni na vijana chipukizi wa Chama hicho wakati akizindua shina lililopo ndani ya Kata ya Sandari Wilayani Temeke leo .picha na Mpiga picha wetu.

  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala kushoto akiwa sambamba na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Japhary aliyevaa kofia meza kuu pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo Kata na Matawi..

 Burudani
Katibu wa Kata ya Sandari wa Jumuiya ya Vijana Mrisho Kamba akizungumza mbele ya wanaCCM katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Kata hiyo  ya Sandari Wilayani Temeke.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Kata Sandari  kushoto akiwa pamoja na Mjumbe wa Halmashauri kuu Japhary Kubecha wakisubiri kuzungumza na waandishi wa Habari  moja ya ofisi za Chama Kata ya Sandari Temeke Dar Es Salaam.



MJUMBE wa Halmashauri kuu Taifa kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Jafaphary Kubecha amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kuhamasika na kuendelea kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt.John Magufuli ya kuijenga Tanzania.

Amesema tangu amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu mapema mwaka huu kupitia Jumuiya ya vijana amefanya ziara katika mikoa kadhaa na Wilaya zake ameshuhudia wanaCCM wakiwa na hamasa kubwa .

Kubecha ameyasema hayo Jijini Dar Es Salaam leo akiwa katika kazi maalum ya kufungua mashina ya Chama hicho yaliyopo ndani ya Kata ya Sandari Wilayani Temeke.

"Nawahamasisha wanaccm popote walipo kuendelea kuunga mkono kazi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt Magufuli Mimi tangu nimechaguliwa katika nafasi hii nimeshafanya ziara mikoani na kwakweli wananchi na wanaCCM wanahamsika sana ." amesema Kubecha

Pia katika hatua nyingine amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao unatarajia kufanyika mwaka huu na uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020.

Akizungumza wakati akizindua mashina hayo amewataka wanachama wa Chama chake kuenzi matawi hayo na kamwe wasigeuze kuwa sehemu ya vijiwe vya kukutania.

"Nawaomba mashina haya yawe chachu ya kujenga umoja miongoni mwenu na kufanya kazi za kuimarisha chama chetu na msitumie matawi haya kama sehemu ya kupigia stori na vijiwe vya kufanya mambo yasio stahili.

Pia akizungumzia changamoto iliyojiyokeza ndani ya chama juu ya walaka ulioandikwa na wazee wa Chama hicho ambao pia wamewahi kuwa viongozi wakuu watendaji amesema walaka huo hauna mashiko.

Amesema wazee hao wanajua utaratibu wa Chama na si kuandika walaka ambao mwisho wasiku wanaposti kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii jambo ambalo si sahihi.

" Chama hiki kina utaratibu wake na kwa bahati nzuri wote tunajua hivyo walaka huo kwasababu haujapita kwenye utaratibu wa kichama upita kwenye mitandao basi hatuwezi kufanyia kazi jambo ambalo limepitishwa huko."amesema Kubecha.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Sandari Mrisho Kamba amewataka Vijana wa chama cha Mapinduzi CCM kujipanga vema kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mtaa na huku wakiendelea kuyazungumzia mazuri yanayofanywa na Mwenyekiti wao wa Chama Taifa na Rais Dkt John Magufuli.

Pia amewataka Jeshi la Polisi kutoa kibari kwa vijana hao wa Chama kushughulika na watu ambao wanasema maneno ya hovyo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli.

"Ndugu mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Ndugu Kubecha tunaomba tufikishie salamu kwa mh Rais wetu .kwamba tupo tayari kuwashughulikia watu ambao hawaoni kazi anayofanya katika nchi hii na kwamba Polisi wawaache wawafunze adabu." Amesema Kamba

CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO YA KUKUZA NA KUSIMAMIA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI.

$
0
0
Mwakilishi kutoka CEED Bw. Fred Laiser akiongea na wanahabari (hawapo pichani)


Bi. Elizabeth Swai mjasiliamali wa biashara ya kuku akichangia moja ya mada.


Bw. Robin Zimbakov kutokea nchini Macedonia akichangia moja ya mada.

Baadhi ya Wajasiriamali waliohudhuria

Kituo cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), yawakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa mazao ya kilimo na usindikizaji vyakula katika hafla iliyolenga kutoa mafunzo ya usimamizi, maarifa ya biashara, utayari wa uwekezaji na fursa za mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari,mwakilishi kutoka CEED bwana Fred Laiser amesema lengo la hafla hii ni kutoa elimu kuhusu usimamizi wa biashara zao na kuwakutanisha wajasirimali kutoka ndani na nje ya nchi ili kujifunza mengi zaidi.

“Sisi CEED kazi yetu ni kuwainua wajasiriamali mbali mbali nchini hasa wa mazao ya kilimo pamoja na mifugo.Leo tupo hapa kwa ajili ya kuwapa elimu ya usimamizi wa biashara zao hasa zinapokuwa kubwa kwasababu biashara inapokuwa kubwa changamoto nazo zinaongezeka”,Alisema Fred.

Kwa upande wa washiriki kutoka Tanzania, Bi Elizabeth Swai mjasiliamali wa biashara ya kuku amesema amefurahia kupata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa kimataifa ambayo yatamuwezesha kuendeleza biashara yake.

“Kuwa mjasiriamali kuna changamoto mbalimbali, hasa kipindi ambacho biashara yako inakua changamoto zinakuwa ngumu zaidi. Kama mjasiriamali ni muhimu sana kujibadilisha kila wakati ili kutoa huduma bora au bidhaa bora kushindina katika soko”. Elizabeth Swai.

Hafla hiyo imeudhuriwa na wafanyabiashara takribani 40 kutoka kona mbalimbali kutoka ndani na nje Tanzania akiwemo mfanyabishara wa kimataifa mwenye mafanikio makubwa bwana Robin Zimbakov ambaye aliezea safari yake ya ujasirimali, changamoto alizokutanazo hadi biashara yake kusimama.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images