Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

BALOZI KAMALA AKUTANA NA UONGOZI WA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA GHENT - UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza na Viongozi wa Wanafunzi wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Ghent waliofika ofisini kwake leo Brussels kumweleza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kumuomba awasaidie kuzungumza na Mabalozi wa nchi za Afrika, Karibiani na Pacific ili kutafuta ufumbuzi.

NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE ILIYOKWAMA ARUSHA AIRPORT YAKWAMULIWA - TBC 1

BASI LA HOOD LAPATA AJALI MOROGORO

$
0
0
Mtu mmoja amekufa na wengine 27 kujeruhiwa baada ya basi la Hood Limited lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Arusha kupata ajali eneo la Melela Mvomero, Mkoani Morogoro.
Wakazi wakishuhudia basi la kampuni ya Hood lililopinduka jioni hii maeneo ya Doma,Morogoro. 

Upande wa chini wa basi la Hood 

Wakazi wa eneo la Doma nje kidogo ya mji wa Morogoro wakitafakari tukio kwa huzuni. Picha na Junior Matukuta

OKWI ATUA RASMI JIJINI DAR, APOKELEWA NA MASHABIKI KIBAO WA JANGWANI

$
0
0
Okwi akilakiwa kwa shangwe na mashabiki waliofika kumpokea mapema leo jioni.
 Okwi akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga waliofika uwanja wa ndege kumpokea  leo jioni jijini Dar es salaam
 Okwi akionesha namba yake ya mashambulizi siku ya jumamosi

HATIMAYE mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi ametua nchini leo majira ya saa tisa na nusu alasiri  na kupokelewa na viongozi wa Yanga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Okwi  ambaye amesajiliwa Yanga kwa miaka miwili na nusu kwa jumla ya dola 60,000 alitua nchini na ndege ya  shirika la Rwanda.
Mbali na viongozi hao wa Yanga ambao ni Abdallah Binkleb, Musa Katabalo na Seif Ahmed  'Magari' pia alilakiwa na wanachama wachache ambao walijitokeza uwanjani hapo kwa lengo la kushuhudia ujio  wake.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Okwi ambaye amezaliwa  Desemba 25, mwaka 1992  alisajiliwa Simba akitokea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la  dola za Kimarekani 40,000 alisema "Mimi ni mchezaji na mpira ni kazi yangu, nimekuja kuichezea Yanga na  nitaitumikia kwa mapenzi yangu yote, nimekuja kufanya kazi na si kuiangalia Simba, mkataba wangu na Simba  ulishaishaga.

Akizungumzia mechi ya Yanga na Simba itakayofanyika Jumamosi ijayo alisema "Mimi nipo fiti, nipo tayari  kucheza mechi ya Simba, nimejiandaa kikamilifu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ya mimi kucheza au  kutocheza ni kocha, kama atanipanga nitafurahi zaidi."alisema Okwi ambaye amejiunga kambini na wenzake jana  jioni kwenye hotel ya Protea iliyopo Oyesterbay jijjini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya  Nani Mtani Jembe Jumamosi.

Kuhusu utata wa usajili wake Yanga, Okwi alisema "Mimi hayo mambo siyajui, nimeyaacha mikononi mwa  viongozi wa Yanga ndio watakaomaliza hilo suala."alisema Okwi ambaye baada ya mkataba wake na Simba  kuisha Desemba mwaka jana aliongezewa mkataba wa miaka miwili na Simba kabla hajaanza kuutumikia  akahamia Etoile du Sahel ya Tunisia ambako aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 fedha ambazo Simba  wanazisotea  mpaka leo kwa kile walichoeleza kuwa Etoile haijawalipa.

Kufuatia hali hiyo, Simba walipeleka malalamiko yao Fifa kuishtaki Etoile ambayo nayo ilipeleka malalamiko  ya Okwi kuwa ametoroka kwenye klabu hiyo, ambayo hata hivyo alidai alikalishwa benchi miezi mitatu bila  kuchezeshwa wala kulipwa mshahara wake kitu ambacho kilimfanya atimkia nchini kwao Uganda miezi  michache iliyopita na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), lilimuombea kibali mchezaji huyo Fifa ili ajiunge  na klabu ya Sports Clab Villa ili kulinda kiwango chake na Fifa ilimuidhinisha kuichezea klabu hiyo kwa muda   wa miezi sita suala lake likiwa linashugulikiwa na tayari ameichezea klabu hiyo kwa  miezi miwili.

Tayari Fufa wameiandikia Fifa barua kutaka ufafanuzi  wa usajili wa mchezaji huyo Yanga kwa vile alizuiwa  kucheza michuano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa vile  hajamaliza matatizo yake na Etoile du Sahel.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb alisema "Baada ya mechi ya Jumamosi  tutatoa ufafanuzi zaizi kuhusu usajili wa Okwi, sisi hatujakurupuka, tumemsajili kwa ajili aweze kutusaidia  kwenye mechi zetu za kimataifa, tunaenda kupeperusha bendera ya Tanzania hivyo Simba wawe wazalendo,  kumsajili Okwi ni kama kunogesha 'ice' kwenye keki, tunalenga kuhakikisha michuano ya klabu bingwa mwakani tunafika mbali.

Kauli ya Binkleb imekuja kukiwa kwa mahasimu wao Simba kunawaka moto kwa wanachama kumshinikiza  mwenyekiti wao Ismail Aden Rage kujiuzulu huku wakimtuhumu kutafuna dola laki tatu za mauzo ya Okwi kitu  ambacho Rage anakipinga vikali kwa kusema hajatafuna fedha hizo na kuweka ngumu kujiuzulu.

B-PESA-UnionPay zasaini mkataba wa ushirikiano

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Smart Banking Solutions (SBS) Bw. Gustav Vermaas (kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi Mkuu wa UnionPay International kanda ya Afrika na Mashariki na Kati, Li Zhixian, kama ishara ya maridhiano ya mkataba wa ushirikiano kati ya makampuni yao itakayowezesha kadi za B-PESA kukubalika katika vituo vyote vya UnionPay duniani kote.
Mwakilishi Mkuu wa UnionPay International kanda ya Afrika na Mashariki na Kati, Li Zhixian (kulia) akisaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Smart Banking Solutions (SBS) kupitia Kadi yake ya B-PESA, ambayo itatoa fursa kwa huduma hii mpya ya malipo ya kabla ya kutumia kadi ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki, kufanyika katika wigo mpana ndani na nje ya Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SBS Bw. Gustav Vermaas.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Smart Banking Solutions (SBS) Bw. Gustav Vermaas akisaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya UnionPay International ya China, makubaliano hayo itatoa fursa kwa huduma mpya ya malipo ya kabla ya kutumia kadi ya B-PESA -ya kielektroniki la daraja la juu inayotumia mfumo wa kibenki- kufanyika katika wigo mpana ndani na nje ya Tanzania. Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa UnionPay International kanda ya Afrika na Mashariki na Kati, Li Zhixian.

TAPSEA yaendesha mafunzo kwa Makatibu Muhtasi jijini Arusha

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Mh. John Mongella (wa pili kushoto walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya Makatibu Muhtasi wanaohudhuria Mafunzo ya Usimamizi wa Ofisi na Utawala (Advanced Office Management and Administration Skills) yaliyoandaliwa na Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),ambayo yanamalizika leo kwenye Hoteli ya Lush Garden,Jijini Arusha.Wa pili kulia kwa walioketi ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Pili Mpenda.
Baadhi ya Makatibu Muhtasi wanaohudhuria Mafunzo ya Usimamizi wa Ofisi na Utawala (Advanced Office Management and Administration Skills) yaliyoandaliwa na Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho,Pili Mpenda (wa pili kushoto kwa walioketi) ambayo yanamalizika leo kwenye Hoteli ya Lush Garden,Jijini Arusha.

ratiba kamili ya game ambazo Golden Bush itacheza weekend hii

$
0
0
Niseme wazi kwamba timu yetu iko kwenye maandilizi ya mwishomwisho kabisa kabla ya kuumana na watani wetu wa jadi, Wahenga Veterans, hii itakuwa na game number 566U itakayopigwa uwanja wa TP Tandale alimaarufu Nangwanda sijaona.

 Itakumbukwa kwamba mwaka jana mechi kama hii wenzetu walishinda kwa goli za jioni sana, kwakutambua hilo walimu wetu akina Madaraka Selemani wamefanya kazi ya ziada kwa kurekebisha baadhi makosa na vilevile kucheza mechi nyingi sana za kirafiki ikiwa ni pamoja na kuvuka maji hadi visiwani tulipowapiga KMKM 2-1.

Tarehe
Muda
Mechi No
Uwanja
mechi Na
21/12/2013
0800am
564U
Staki Shali
Staki shali Veterans
22/12/2013
0430pm
565H
Nagwanda Sijaona a k a TP
Kilwa Veterans
28/12/2013
0430pm
566U
Nagwanda Sijaona a k a TP
Wahenga Veterans

Timu iko sawasawa kutoa burudani kwa wapenzi wetu karibuni sana.

Pamoja na maandilizi hayo tunapenda kuwafahamisha kwamba Golden Bush tumemchukua bwana Jonas Afumwisye kuwa bounsa wetu hasa pale tunapocheza game nzito hasa zenye upinzani kama Wahenga.

Asanteni
Onesmo

Balozi Seif Ali Idd apokea mchango wa sh. Mil. 15 kutoka kwa mwenyekiti wa Yanga,Yussuf Manji

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya maadhimisho ya Kitaifa akipokea fedha taslim Shilingi Milioni 15,000,000/- kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Bwana Yussuf Manji kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group ambae pia ni Mwenyekiti wa Kalabu ya Soka ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yussuf Manji mara baada ya kupokea mchango wa mfanyabiasra huyo nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa (Zanzibar) amepokea mchango wa fedha kutoka  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yussuf Manji ili kusaidia kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.

Bwana Manji ambae alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ushiriki wa Timu yake ya Yanga katika mashindano ya Mapinduzi Cup alikabidhi mchango huo nyumbani kwa Balozi Seif Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Alisema Kampuni yake pamoja na Timu yake imehamasika kutoa mchango huo wa Shilingi Milioni  Kumi na Tano { 15,000,000/- } kufuatia umuhimu wa Tanzania  kukabiliwa na sherehe hizo kubwa  za maadhimisho ya Nusu karne ya mapinduzi ya Zanzibar.

Akipokea mchango huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimpongeza  Bwana Yussuf Manji kwa uamuzi wa Taasisi zake kuona umuhimu wa kusaidia sherehe hizo zilizokabiliwa na masuala mengi kutokana na umuhimu wake kihistoria.

Balozi Seif alimuhakikishia Kiongozi  huyo wa Quality Group na Timu ya Soka ya Yanga pamoja na wananchi wote kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano iko katika utaratibu wa kukamilisha maandalizi ya mwisho ya maadhimisho hayo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

20/12/2013.

KASEBA,ALIBABA KUPIMA UZITO FRIENDS CORNER HOTEL KESHO

$
0
0

Mabondia jafet kaseba wa jijini Dar es salaam na Alibaba Ramadhan wa arusha wanategemea kupima afya na uzito kesho jumamosi ya tarehe 21 decemba 2013 saa nne asubuhi katika ukumbi wa friends corner hotel ambapo ndipo hapohapo pambano lao litafanyikia siku inayofuata ya jumapili tarehe 22/12/2013 kuanzia saa kumi jioni


Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya  BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya karage suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu  Fadhili awadh[tiger]  katika uzito wa wealter[66kgs] pambano la raundi kumi, nao wanategemea kupima hiyo kesho



kizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa  mabondia wanaotegemea kupima ni mbaruk heri mabae  atapima kwa ajili ya kuzipiga na lusekelo daudi ,Issa omar nampepeche na Hassan kiwale’moro best’, Zumba kukwe na Jacob maganga, Adam Yahaya na Harman shekivuli, jocky hamis na mbena rajab, Ernest Bujiku na Shah kasim, shaban bodykitongoji na mwinyi mzengela, shaban manjoly na  kasim chuma.

Nae Mtanzania aishie Canada kareem kutch  atapima na  Tata boy kwa ajili ya pambano la kimataifa la mchezo wa kickboxing la raund tano, Mabondia wote wameshawasili Dar es salaam, wakati Alibaba Ramadhan wa Arusha na Jacob maganga wa Tanga wamefikia katika hotel ya valley view wakati kareem kutch yupo Durban hotel kariakoo wapo vema na wenye furaha kwa mapambano yao

NANI MKALI KATI YA MSONDO NA SIKINDE??

MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

WATAKIWA KUACHA KULIMA KANDO MWA HIFADHI

$
0
0
Na Denis Mlowe.Aliyekuwa Arusha
WANANCHI  wa wanaozunguka   hifadhi   ya  Taifa ya Ziwa Manyara iliyoko mkoani Arusha wametakiwa kulinda hifadhi hiyo kwa kuachana na kulima katika vyanzo vya maji na maeneo yanayoizunguka hifadhi hiyo.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa TANAPA Dk.Ezekiel Dembe hivi karibuni wakati akizungumza na  wanahabari mkoa wa Iringa ambao  walikuwa katika ziara ya mafunzo ya kutangaza utalii katika  Hifadhi za Kaskazini.
Alisema kuna hatari kubwa ya  Ziwa Manyara kukauka zaidi kutokana na wananchi kuendelea kulima na kupelekea ziwa kujaa tope kutokana na kilimo hicho cha pembezoni.

Dk.Dembe alisema kutokana na kisichozingatia uhifadhi wa Ziwa Manyara baadhi ya ofisi za hifadhi  hiyo zimeharibika vibaya kutokana na mafuliko hivyo Tanapa wana mpango wa kutafuta  eneo  jingine ili kujenga ofisi  hizo.
Akizungumzia ubovu  wa  miundo  mbinu katika hifadhi za Taifa alisema kuwa  TANAPA  wapo katika mkakati kuboresha miundo mbinu  hiyo ili kuvutia  zaidi watalii wanaofika katika  hifadhi  hizo kuendelea kupitika kwa urahisi kwa mwaka


Akielezea kuhusu hifadhi ya Taifa Ruaha iliyoko Iringa kutangazwa kama ilivyo hifadhi za Kaskazini Dk. Dembe, alisema kuwa hivi  sasa mkakati umewekwa wa kuelekeza nguvu ya kuitangaza hifadhi hiyo  ili kuvutia watalii  zaidi  japo alisema  changamoto  kubwa ni upatikanaji wa mafuta  ya Ndege ambazo zinaleta  watalii ambao  hulazimika kujaza mafuta Dodoma .
“Hata  hivyotumeanza mkakati wa kuhakikisha hifadhi ya Katavi na Ruaha katika viwanja wa ndege  vilivyopo  huko kunakuwa na mafuta ya ndege  kupunguza gharama ambazo watalii wanatumia kwa sasa” alisema Dk. Dembe 
Alisema TANAPA wako katika mchakato wa kutafuta  wawekezaji wa kujenga  Hotel za kisasa katika hifadhi ya Ruaha ili kuvutia  watalii wengi zaidi.
Kuhusu  usalama wa watalii alisema kuwa  TANAPA wamejipanga  kuweka usalama mzuri wa watalii ili ni pamoja na kuanzisha ulinzi wa askari  watakaofanya kazi ya kulinda  watalii pekee.

SPIKA AKABIDHIWA RIPOTI YA MGOGORO WA BOMBA LA GESI KUTOKA MTWARA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea ripoti ya kamati maalum ya Spika kutoka kwa Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani aliyoiunda Mwezi Mei, 2013 kuchunguza mgogoro wa ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni wajumbe wa Kamati hiyo Mhe. Said Nkumba, Mhe. Cecilia Pareso na Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo  Bi. Nesta Kawamala. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Mzumbe University (Dar es salaam campus) 12th graduation ceremony held today

$
0
0
 Mzumbe University Vice Chancellor, Prof. Joseph Kuzilwa (centre) with the varsity’s Deputy Vice Chancellor, Academics, Prof. Josephat Itika (second left) and Acting Chancellor, Prof. Daniel Mkude (right) during the Mzumbe University's  12th  graduation ceremony, Dar es Salaam campus, held today.  In the left  background is Mr. Ludovick Utoh who is the President of Mzumbe University Convocation.

 Mzumbe University Vice Chancellor, Prof. Joseph Kuzilwa (centre) with the varsity’s Deputy Vice Chancellor, Academics, Prof. Josephat Itika (second left) and Acting Chancellor, Prof. Daniel Mkude (right) during the Mzumbe University's 12th  graduation ceremony, Dar es Salaam campus, held today.  In left background is Mr. Ludovick Utoh who is the President of Mzumbe University Convocation.
 Some of the graduands at the Mzumbe University 12 graduation ceremony, Dar es Salaam campus which took place in Dar es Salaam yesterday.  A total of 1225 graduands grouped in eight different programs were conferred their masters’ degree.

Some of the graduands at the Mzumbe University 12 graduation ceremony, Dar es Salaam campus which took place in Dar es Salaam yesterday.  A total of 1225 graduands grouped in eight different programs were conferred their masters’ degree. 

KUTOKA MAKTABA: PAN AFRICAN FOOTBALL CLUB

$
0
0
Kikosi cha Pan African mwaka 1988. Wenye kujua majina yao msaada tutani tafadhali...

Sikinde yajichimbia Bagamoyo kuikabili Msondo Krisimasi

$
0
0

HOMA ya pambano la watani wa jadi katika muziki wa dansi nchini kati ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' na Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' litakalofanyika siku ya Krismasi imeanza kupanda kwa bendi hizo kujificha kambini na huku wakipigana vijembe.


Bendi hizo kongwe nchini zinatarajiwa kuonyeshana kazi katika onyesho litakalofanyika kwenye viwanja wa TCC Club Chang'ombe, Temeke Dar es Salaam katika kunogesha sikukuu hiyo ya Krismasi.


Katika kuonyesha wamelipania pambano hilo bendi ya Sikinde tayari imeiendea Msondo wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kuweka kambi yao na wamewatahadharisha 'mahasimu' wao hao wasije wakatoa visingizio baada ya kugaragazwa kwenye onyesho hilo.
"Sisi tumeamua kuweka kambi yetu mjini Bagamoyo ambako tutatua viwanja vya TCC kutokea huko ili kuisambaratisha Msondo, na tunataka wajipange sawasawa ili wasije wakatoa visingizio tena kwa maana kama vyombo vipya bendi zote imepewa na Konyagi," Katibu wa Sikinde, Hamis Milambo alisema.
Milambo alisema mashabiki wa dansi wajitokeze kwa wingi kushuhudia namna gani wanavyowachachafya wapinzani wao hao, ikizingatiwa hawajakutana kwa muda tangu mwaka jana.
Upande wa Msondo kupitia Meneja wao, Said Kibiriti, alisema hawana haja ya kutaja mahali kambi yao ilipo isipokuwa wamejiandaa kuwatoa nishai wapinzani wao siku ya onyesho hilo litakaloanza saa nane mchana.
"Sisi hatuna mchecheto wowote na mpambano huo, tunaendelea kujifua kimya kimya mahali ambapo siwezi kupataja kwa sasa," alisema Kibiriti.
Naye muimbaji anayekuja juu wa bendi hiyo ya Msondo alitokea Sikinde, Athuman Kambi, alisema amejipanga kuonyesha umahiri wake katika mpambano huo baada ya kufanya hivyo wakati akiwa Sikinde dhidi ya Msondo kwenye ukumbi wa Diamond na kuwawehusha mashabiki wa muziki wa dansi nchini.
"Najua watu watataka kuona nafanya kitu gani dhidi ya bendi yangu ya zamani iliyonitangaza vyema, wasiwe na hofu waje Desemba 25 waone nini nitakachofanya TCC Club Chang'ombe," alisema Kambi.
Mpambano huo wa Sikinde na Msondo umeandaliwa na kampuni ya Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, Integrated Communications, CXC Africa na Salute5 na Michuzi Blog.

Vodacom yatoa mafunzo namna ya kulipia mafuta kwa M Pesa

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu, Vodacom Tanzania leo imeendesha mafunzo kwa watumishi wa kituo cha mafuta cha OilCom kilichopo kwenye makutano ya barabara ya Libya na Morogoro kuhusu huduma ya kulipia kwa njia ya M-pesa. 
M-pesa na OilCom walizindua huduma inayowawezesha wateja wao kulipia kwa njia ya M-pesa wanapopata huduma kwenye vituo vya OilCom vya TMJ Msasani, Kipawa na Libya. “Tunawapatia mafunzo wateja na watumishi kwenye vituo hivi ili kila mmoja aweze kunufuika na kile tunachowapatia kupitia M-pesa. 
"Tunafurahi kuona huduma hii imepokelewa vizuri na inatumika bila ya shida yoyote.”Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Salum Mwalim. 
“Lengo letu kuu ni kujua mandeleo ya huduma yetu ni jinsi gani inatumika hapa, tumekuja kupata maoni ya wauzaji pamoja na wateja wao pia kuwaelekeza pale wanapokwama. Hatutaki yale tuliyokubaliana siku ya ubia yaishie kwenye vyombo vya habari, tunataka kupata maoni ya wateja wetu moja kwa moja ili tuwasaidie.” Alisema Salum Salum
Aliongeze kuwa kutembelea kunawasaidia sana wateja wao na hata kuwaondelea wasiwasi juu ya huduma ya M-Pesa na kwamba watafanya hivyo kwenye vituo vyote vya OilCom ambapo huduma ya M-pesa inapatikana. 
Akizungumza kituoni hapo Meneja wa IT wa kampuni ya OiCom Abubakar Mohamed amesema huduma hiyo iliyozinduliwa wiki tatu zilizopita yayari imeshakubalika kwa wateja na kwamba wameifurahia kw akuwa inawaondolea usumbufu wateja wao. 
"Tumefurahi sana na inakwenda vizuri. Mipango inaendelea kuahkikisha vituo vyote vya OilCom vya jijini Dar es salaam vinawezeshwa kufanya malipo kwa njia ya M-pesa.”Alisema
Amesema wateja wateja wa OilCom hawana sababu yoyote ya kutoitumia njia ya M-pesa kufanya malipo kwenye vituo ambavyo tayari vimeshawezeshwa na kwamba kampuni yake imejiapnga kisawasawa kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake. 
Esmail Abdulrahaman ni mmoja wa wateja waliofika kujaza mafuta kituoni hapo, kwa upande wake yeye amesema “Huduma hii ini nzuri na inaleta urahisi sana ni vema tunajua uwepo wake na hakuna shak inatushaiwhsi kuitumia ili kuondoa usmbufu na utegemezi kwenye njia moja tu ya malipo ya fedha taslimu.” 
Kwa upande wake Mahmud Mohammed lisema kuwa yeye ni mteja mzuri sana wa mafuta ya kituo cha Oilcom na kudhihirisha kuwa huduma hii imemletea faraja kubwa sana kwani kwa sasa hatokuwa akibeba fedha nyingi badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na kufanya mizunguko yake akiwa na uhakika kwa kuweka mafuta kwenye gari lake. 
Hivi karibuni kampuni ya Vodacom Tanzania na Oilcom ziliingia ubia ambapo wateja wa pande zote mbili wamewezeshwa kulipia mafuta kwa kupitia huduma ya M-Pesa popote kwenye vituo vya kampuni hiyo ya mafuta. 
Kwa kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam na kituo cha mafuta cha TMJ Msasani kikiwa cha kwanza kuunganishwa na huduma hiyo huku vingine viwili vimefatia kisha huduma hiyo kusambaa nchi nzima palipo na huduma ya M-Pesa na vituo vya mafuta vya Oilcom.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimjulisha Mahmud Mohamed aliyefika kujaza mafuta kwenye kituo cha OilCom kilichopo kwenye makutano ya barabara ya Libya na Morogoro jijini Dra es salaam kuhusu kuwepo kwa huduma ya malipo kwa njia ya M-pesa kituoni hapo. Kushoto ni Meneja wa IT wa kampuni hiyo ya mafuta Abubaka Mohammed. Huduma ya malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya OilCom vya TMJ Msasani na Kipawa.
 Meneja wa IT wa Kampuni ya OilCom Abubakar Mohamed akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa kituo cha OilCom kilichopo kwenye makutano ya Barabara ya Libya na Morogoro.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na kulia ni Meneja Msaidizi wa kituo hicho Hussein Ahmed.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiwapa mafunzo wahudumu wa kituo cha mafuta cha OilCom kilichpo katika makutano ya barabara ya Libya na Morogoro jijini Dar es salaam juu ya namna ya wateja wanaojaza mafuta kituoni hapo wanavyoweza kulipia kwa njia ya M-pesa. Huduma ya malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya OilCom vya TMJ Msasani na Kipawa.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akionge na Mteja wa OilCom Esmail Abdulrahaman kuhusu kuzinduliwa kwa huduma ya malipo kwa M-pesa kwenye vituo vya OilCom Msasani TSJ, Makutano ya barabara ya Libya na Morogoro na Kipawa jijini Dar es salaam. Kulia ni mtumishi wa OilCom Ala Mohammed.

MABADILIKO YA TABIANCHI YANA MADHARA YA MALI NA UHAI WA BINADAMU - YUNA

$
0
0
DSC_1209
Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), Dr. Lwidiko Edward, akizungumza na vijana kutoka Asasi mbalimbali hapa nchini juu ya ushiriki wa vijana katika mkutano uliopita wa COP 19 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi UNESCO jijini Dar es Salaam. 

KUBALI KIPAJI CHA MTOTO WAKO, TUKUTANE LEDGER PLAZA BAHARI BEACH TAREHE 25, 26 NA 27 DESEMBA 2013

Japan hands over Maternity and Surgical wing to Moyo Safi wa Maria Health centre in Dar es salaam

$
0
0
On 18th December, 2013, the Handing Over Ceremony for “The Project for Expansion of Moyo Safi wa Maria Health Centre in Kinondoni Municipality, Dar es Salaam Region” was held at Moyo Safi wa Maria Health Centre. 
The Government of Japan, in response to the request by Franciscan Sisters of the Immaculate Heart of Mary Missionary Society Tanzania, extended a grant aid of US dollars 172,592 for the project in the Japanese Fiscal Year 2012, under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP). 
The Handing Over Ceremony was attended by: H.E. Masaki Okada - Ambassador of Japan to the United Republic of Tanzania H.E. Francisco Monticello Padilla - Apostolic Nuncio to the United Republic of Tanzania 
The Government of Japan has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the GGHSP scheme since 1991.
Part of the expanded Maternity and Surgical wing of the Moyo Safi wa Maria Health centre in Dar es salaam
 H.E. Masaki Okada - Ambassador of Japan to the United Republic of Tanzania watches as children entertain during the handing over ceremony
 H.E. Masaki Okada - Ambassador of Japan to the United Republic of Tanzania makes his speech
Part of the guests during the ceremony
The newly expanded and equipped  surgical room at the centre
The newly expanded maternity wing
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images