Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

TANZANIA YANG'ARA KIMATAIFA MASHINDANO YA WAREMBO VIZIWI

0
0
*Washindi waishukuru Serikali kwa kuwashika mkono na kuishauri jamii kutowatenga watu wenye ulemavu

*BASATA yafurahishwa na ushindi, yahaidi ushirikiano zaidi

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KWA mara ya kwanza Tanzania imeshiriki katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya viziwi (Miss Deaf International) na mrembo Winfrida Bryson  kuongoza kwa kushika nafasi ya kwanza katika vipengele vya ubunifu wa mavazi, mitindo na utamaduni katika mashindano hayo ya urembo yaliyofanyika kuanzia Julai 7 hadi 15 mwaka huu huko mjini St.Petersburg nchini Urusi.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea walimbwende hao Naibu Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Juliana Shonza amesema kwamba Wizara imefurahishwa na ushindi huo ukizingatia ni mara ya kwanza wanashiriki mashindano ya kimataifa ya aina hiyo na amewapongeza washiriki hao kwa juhudi zao za kuonesha ubunifu na hatimaye kurudi na ushindi nyumbani.

"Tumefurahi kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania, Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na ninawahimiza wazazi ambao wana watoto wenye matatizo ya ulemavu wawawezeshe watoto na sio kuwafungia ndani, hii ni dalili njema na tunaamini watafika mbali zaidi hasa kama jamii tukionesha ushirikiano kwao" ameeleza Shonza.

Aidha Shonza amewaomba wadau mbalimbali kukitokeza ili kuweza kufadhili shughuli mbalimbali wanazozifanya na hiyo ni sambamba na kuwatumia katika matangazo mbalimbali ya kijamii.

Aidha amesema kuwa wazazi na wanajamii wasiwatenge watoto wenye aina yoyote ya ulemavu bali wawezeshe kile wanachokipenda ili kuleta matokeo yenye tija.

Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye walemavu Stella  Ikupa ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwashika mkono watu wenye ulemavu bila kujali tofauti zao na kuwaomba wadau wengi zaidi kujitokeza kushirikiana nao ili kupeleka taifa mbele zaidi.

Ikupa amewashukuru wazazi wa walimbwende hao kwa ushirikino walioonesha na kuwataka wazazi wengine wanaoishi na watoto wenye ulemavu kutowachukulia tofauti na watoto wengine katika malezi.

Pia katibu mtendaji mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza ameeleza kufurahisha na ushindi kutoka kwa walimbwende hao na kuahidi kushirikiana nao katika kila hatua ili kuzidi kupeperusha vyema bendera ya taifa.

"Ushindi huu wa Winfrida na   Grace sio wa kwao pekee bali wameitangaza nchi na limekuwa jambo jema zaidi kwa kuwa ni mara ya Kwanza Tanzania kushiriki katika mashinano hayo, Baraza litaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua" ameeleza Mngereza.

Aidha kituo hicho cha KISUVITA kimeishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii  kwa kugharamia warembo hao na mkuu wa msafara pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Wizara husika chini ya uongozi wa Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe na naibu Juliana Shonza.

Katika mashindano hayo Tanzania iliwakilishwa na warembo wawili ambapo Grace Mtui alishiriki mashindano hayo ya Urembo na kuwa kati ya washindi 10 bora huku Winfrida pamoja na ushindi huo pia alishika nafasi ya 10 kwenye mashindano hayo ya Urembo ya Kimataifa ya Viziwi (Miss Deaf International.) Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mrembo kutoka Botswana, wa pili Kenya na wa tatu Urusi.
 Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Baraza la sanaa la taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea walimbwende hao ambapo ameeleza kufurahishwa na ushindi huo ulioletwa nchini kwa mara ya kwanza na kuahidi kwamba  baraza litaendelea kushirikiana nao ili kupeperusha vyema bendera ya taifa, jijini Dar es Salaam.

 Washindi wa mashindano ya urembo ya kimataifa kwa viziwi Grace Mtui (kulia) na Winifrida Bryson (kushoto) wakiwa na viongozi waliokuja kuwalaki uwanjani hapo katikati ni Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza walioketi ni naibu Waziri wa Sanaa, habari na michezo Juliana Shonza (kushoto) na naibu waziri...
 Winifrida Bryson ambaye ni mshindi wa kwanza katika vipengele vya ubunifu wa mavazi, mitindo na utamaduni na mshindi wa kumi katika mashindano hayo ya urembo ya kimataifa kwa viziwi (Miss Deaf International) akiwa na viongozi waliokuja kumpokea ambapo kwa kutumia lugha ishara ameeleza kuwa wao kama walemavu wana nafasi ya kuleta mabadiliko katika jamii na amewataka walemavu kushirikiana zaidi, jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa Miss Deaf International wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi, ndugu na wanachama wa kituo Cha sanaa na utamaduni kwa viziwi nchini (KISUVITA), jijini Dar es Salaam.
Grace Mtui, mshindi wa kumi bora katika mashindano ya urembo ya  Miss Deaf International akizungumza kwa lugha ishara mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza kuwa mashindano hayo yamewapa uzoefu wa kutosha na ameishukuru serikali na Wizara inayowasimamia kwa kuwashika mkono jijini Dar es Salaam.

Wateja wa Mpesa sasa kuula zaidi Bahati nasibu ya Biko

0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar leo kuhusu Kampuni hiyo kuungana na kampuni ya Vodacom Tanzania kuhakikisha wachezaji wa mchezo huo wanatumia Mpesa kushinda zaidi kwa kuendeshwa droo maalum inayohusisha watumiaji wa Mpesa pekee,kushoto ni Mkuu wa Kitengo Cha Uzalishaji cha wateja wakubwa-Vodacom, Ali Z Ali na kulia na kulia ni Meneja Mauzo-Vodacom,Carolyn Lyimo

Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta akipeana mkono na Mkurugenzi Kitengo Cha biashara Arjuun Dhillon kuonesha msisitizo wa muungano wao kati ya BIKO na kampuni ya Vodacom Tanzania, kuhakikisha wachezaji wa mchezo huo wanatumia Mpesa kushinda zaidi kwa kuendeshwa droo maalum inayohusisha watumiaji wa Mpesa pekee.


Kampuni ya mchezo wa kubahatisha wa Biko, wameungana na Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania kwa kuhakikisha kwamba wachezaji wa mchezo huo wanaotumia Mpesa kushinda zaidi kwa kuendeshwa droo maalum inayohusisha watumiaji wa Mpesa pekee.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema droo hiyo ni tofauti na zile za kawaida zinazofanyika kila Jumatano na Jumapili kwa watumiaji wa mitandao yote nchini Tanzania, wakiwa na dhamira ya kupanua wigo wa ushindi kwa Watanzania wote, hususan wanaotumia Mpesa.

"Kwa kuendeshwa mchezo huu, sasa wigo wa ushindi umepanuka kutoka mara mbili hadi tatu, kama vile zawadi za papo kwa hapo, zawadi kubwa ya wiki ya Jumatano au jumapili, bila kusahau droo kubwa ya wachezaji pekee wa Mpesa ambao wao pekee watatafutwa mara baada ya kupata washindi wetu wa kawaida kutoka Biko.

"Tunadhani sasa kushinda Biko ni rahisi zaidi, ukizingatia kuwa droo zetu zote zinachagizwa na tumaini letu la kugawa zawadi za juu kwa Watanzania wetu, hivyo ukiacha wigo wa droo zetu za kawaida, bado upo ukumbi muhimu wa watumiaji wa Mpesa ambao wote watacheza kwa mfumo wa kawaida wa kutumia namba yetu ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu namba 2456,"alisema Mgeta.

Naye Mkuu wa Kitengo Cha Uzalishaji Cha wateja wakubwa, Ali Z Ali, aliishukuru Biko kwa kuanzisha droo mahususi kwa ajili ya wateja wao wa Mpesa, akisema kuwa itaonyesha ni namna gani wametambua huduma nzuri kutoka Vodacom Tanzania.

"Vodacom kupitia Mpesa na wenzetu Biko tupo kwa ajili ya wateja wetu wote ambao sasa fursa za ushindi kwao ni pana zaidi, hivyo tunawaasa watumie fursa hii ili wajishindie zawadi kutoka Biko kila siku,"Alisema Ali.

Mbali na droo hiyo maalum ya Biko kwa wateja wa Mpesa, zawadi za papo kwa hapo zinaendelea kutoka kwa wachezaji wa Biko wa mitandao yote ya Tigopesa, Airtel Money, Halopesa na Mpesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku zawadi za papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi milioni moja, bila kusahau droo kubwa za wiki za Jumatano na Jumapili.

Waziri Jafo Azindua Shule Shinikizi Tabora

0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Waziri wa nchi Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa TAMISEMI, Suleiman Jafo amefanya uzinduzi wa kitaifa wa shule shikizi nchini, Akizindua shule hizo kitaifa katika wilaya za Nzega na Igunga mkoani Tabora ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la kimataifa DFID kupitia program ya EQUIPT

Waziri Jafo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi amepongeza mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri katika usimamizi wa miradi inayotekelezwa katika mikoa tisa hapa nchini na kueleza namna Serikali ilivyoridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha Shilingi bilioni Mia sita za program ya maboresho ya elimu nchini EQUIPT

Awali waziri Jafo pia alitembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ufugaji mbuzi katika shule ya Msingi Isimba na mradi wa ufugaji samaki katika shule ya Msingi Simbo ambayo inafadhiliwa na DFID

Nae Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema upatikanaji wa Shule hizi utasaidia kuongeza Ufahulu kwa wanafunzi kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni huku mwakilishi wa shirika la DFID Elizabeth Arthy akibainisha kuwa shirika hilo limetenga kiasi cha Shilingi bilioni Mia sita katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Pichani ni Waziri wa nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Akizungumza katika uzinduzi wa kitaifa wa shule Shikizi mkoani Tabora.

RC GAGUTI AZINDUA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARALIA KAGERA .

0
0

Picha ya Pamoja Mkuu wa Mkoa Kagera, Brig. Jen. Marco Gaguti pamoja na Wakuu wa Wilaya, wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya, watumishi wa Afya, watendaji kutoka Wizarani, Mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Zero maralia inawezekaana

Pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa Profesa Kamuzora, akitoa Maelezo machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kuzindua rasmi kampeni ya zero maralia inaanza na Mimi, katika ukumbi wa E.L.C.T Bukoba.
Pichani Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii, wazee jinsia na watoto Bi. Linda Makara akitoa shukrani zake kwa niaba ya Wizara, kwa Uongozi wa Mkoa juu ya utekelezaji wa masuala ya Afya Mkoani Kagera, katika Kikao cha Uzinduzi wa kampeni ya Zero maralia inaanza na Mimi.
Pichani Mwakilishi kutoka TAMISEMI Bwn. Kalidushi Charles nae akitoa shukrani zake kwa niaba ya Wizara jinsi Mkoa ulivyotekeleza na kusimamia masuala ya Afya ikiwemo ujenzi wa zahanati na Hospitali tatu za Wilaya.
Sehemu ya baadhi ya Viongozi wakiendelea kufuatilia Kikao maalumu cha uzinduzi wa Kampeni ya Zero maralia inaanza Mimi, katika ukumbi wa E.L.C.T Bukoba


Anaandika Abdullatif Yunus wa MichuziTV - Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amezindua rasmi Kampeni ya Kutokomeza maralia Mkoani Kagera itayoambatana na Ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi Shuleni inayobeba ujumbe wa "Zero maralia inaanza na Mimi"

Mapema Mhe. Gaguti akitoa salaam zake za ufunguzi amesema kitakwimu Mkoa wa Kagera, maambukizi ya ugonjwa wa Maralia kitakwimu ni asilimia 15.4 % ukilinganisha na asilimia 7% ya Maambukizi ya Maralia kitaifa, hivyo nakuongeza kuwa kama Mkoa juhudi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika kwani mwaka 2016 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 41% hivuyo kuwataka wasimamizi kuhakikisha maambukizi ya Maralia yanazidi kushuka zaidi.

Kampeni hiyo ambayo inaratibiwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera pamoja na Shirika la PSI chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na watoto, na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaaanza mara moja kwa kusambaza vyandarua shuleni, huku tahadhali ikitolewa juu ya matumizi ya vyandarua hivyo, na kwa yeyote ambaye atajaribu kukwamisha kampeni hiyo atakumbana na mkono wa sheria.

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA (TAEC) KUSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA MKOANI SIMIYU

0
0


Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), inatarajia kushiriki kwenye maadhimisho ya sherehe za kitaifa za Nane Nane kanda ya ziwa mashariki yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 28 Julai hadi 10 mwezi Agosti, 2019. 

Katika maadhimisho hayo, TAEC itaweza kuonesha shughuli mbali mbali zinazofanyika katika Tume ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi na wadau mbali mbali juu ya udhibiti na matumizi salama ya mionzi hapa nchini. 

Elimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwenye sekta za afya, kilimo, viwanda, mifugo, maji, lishe pamoja na ujenzi inatolewa. 

Wananchi wote wanakaribishwa ili kuweza kujipatia elimu bure kwa njia za maelezo, video fupi, vipeperushi na majarida ili kujiongezea uelewa juu ya majukumu yanayotekelezwa kisheria na TAEC katika Nyanja za udhibiti wa mionzi na uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia. 

Imetolewa na , 

Peter Ngamilo 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano 

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania

Vodacom Tanzania Foundation na Girl Effect kuwezesha watoto wakike nchini kupitia Tujibebe

0
0
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania imeungana na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect kuzindua ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19.

Huduma ya Tujibebe itawaunganisha vijana wenye uzoefu katika ujasiriamali kuwahamasisha vijana wengine na kusaidiana kutatua changamoto za maisha huku wakitimiza malengo yao. Maudhui ya tujibebe yanalenga katika kuwapa vijana wa kitanzania taarifa na rasilmali wanazohitaji kufanya maamuzi sahihi ya maisha yao – mafunzo ya kuboresha ujuzi wao, kuanzisha biashara na kusimamia fedha zao.

 Tujibebe itatumia tovuti pamoja na huduma za simu za IVR kutoa mafunzo kupitia simulizi ya sauti ambayo ni bure kabisa kupitia mtandao wa Vodacom.

Jukwaa la Tujibebe limezinduliwa rasmi na Mjumbe wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Simon Shayo na wadau mbali mbali wa sekta ya maendeleo, katika hafla iliyofanyika hoteli ya Golden Tulip. Wageni waalikwa walipata nafasi ya kusikia baadhi ya maudhui kutoka kwa watafiti wa Technology Enabled Girl Ambassadors (TEGAs) ambao ndio kiini cha taarifa na maudhui yaliyotumiwa kuhakikisha kwamba Tujibebe inakidhi mahitaji ya wasichana na vijana wa kitanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo Bw Shayo  alisema amefurahi kwamba makampuni mengi yanaungana ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unaongezeka na pia kuwawezesha vijana kiuchumi, alizipongeza taasisi za Vodacom Tanzania Foundation na Girl Effect kwa kuwekeza katika vumbuzi zinazosaidia kubadilisha maisha ya watu wengi.

 “Tujibebe inaonesha umuhimu wa taasisi binafsi na zile zisizofanya kazi kwa faida kuungana na kuhakikisha malengo endelevu ya maendeleo yanatimia, ninapenda kuzihamasisha taaisis nyingine nyingi Zaidi kuwa wabunifu katika maeneo yao na kuungana na taasisi zingine ili kubuni miradi ambayo itabadilisha maisha ya jamii zinazowazunguka,” aliongeza Shayo 

Serikali inafanya kazi na taasisi mbali mbali ikiwemo UNDP, USAID na Vodacom Tanzania Foundation katika masuala ya kuleta usawa na kuwawezesha wasichana, pia aliwapongeza Vodacom na Girl Effect kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo nchini. “Inabidi wote tushirikiane kuinua vijana wetu na hasa wasichana kwani wao ndio Tanzania ya baadae. Napenda kuwasihi wadau kuungana pamoja kutengeneza miradi kwa ajili ya kuwasaidia vijana wengi zaidi.” aliongeza Shayo.

“Sote tunafahamu kwamba teknolojia ya simu ina uwezo wa kubadilisha dunia, tunafuraha sana kuungana na Girl Effect, kupitia mtandao wetu ambapo tutaweza kuwafikia vijana wengi zaidi na kuwafanya wafikie malengo yao” alisema Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia.
Akielezea faida za jukwaa la Tujibebe katika kuleta mabadiliko katika maisha ya Vijana wa Kitanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Girl Effect, Jessica Posner Odede alisema maudhui ya tujibebe yametengenezwa kwa ajili ya kuwaunganisha vijana wote lakini lengo kubwa ni kubadilisha maisha ya wasichana watakaotumia elimu kutoka Tujibebe.

 “Mara nyingi vijana huwa na maswali mengi kuhusiana na kesho yao, na hawajui mahali pakupata majibu sahihi – kuanzia kuwa na ujuzi kwa ajili ya kupata kazi, jinsi ya kupata pesam na pia namna ya kutunza pesa hizo. Hapo zamani ilikuwa ni vigumu kwa wasichana kupata taaarifa hizi - leo tunazindua tujibebe ili wakiingia kwenye mtandao wapate elimu mtandaoni, sio tu wapakue mambo ya kufurahisha, bali pia waweze kupata mafunzo ambayo yanagusa maisha yao ya kila siku. Lengo letu kubwa ni kutumia tujibebe kuwaunganisha wasichana na huduma zinazowazunguka na kutengeneza mabadiliko ya kudumu.

Mwezi uliopita Vodacom Tanzania Foundation ilizindua mpango mkakati wa miaka mitatu 2019-2021 ambao umelenga kuleta maendeleo jumuishi katika afya, elimu na mazingira. Kimataifa Vodafone Foundation ni mbia wa Girl Effect katika kubuni miradi mbali mbali ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya simu.
 Mjumbe wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Simon Shayo akizungumza wakati wa  kuzindua ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi akizungumzia mchango wa Taasisi ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania inavyoshiriki kuinua watoto wa kike wakati wa uzinduzi wa Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia akizungumza kuhusu wabunge wanavyoishauri serikali kwenye ulinzi wa mtoto wa kike ili waweze kufikia malengo yao wakati wa uzinduzi wa ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect, Jessica Posner Odede akizungumza kuhusu namna taasisi hiyo ilivyojikita  kutoa huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 ijulikanayo kama ‘Tujibebe’.
Msheheleshaji Tulanana Bohela akifanya mahojiano na vijana waliofikiwa na  Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect kupitia ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.




Baadhi ya Viongozi, Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na vijana wakifuatilia uzinduzi wa ‘Tujibebe’ huduma mpya inayotoa elimu ya maisha kupitia simu ikiwalenga vijana waliopevuka wenye umri kati ya 15-19 iliyowezeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya kimataifa ya Girl Effect.


RAIS WA TUNISIA AFARIKI DUNIA

0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BENI Caid Essebsi ambaye ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Tunisia amefariki leo alfajiri akiwa na miaka 92 katika hospitali ya jeshi nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na kijana wa  Rais huyo Hafedh Caid ameeleza kuwa baba yake Essebsi amefariki dunia leo alfajiri na hiyo ni baada ya kulazwa mara kwa mara katika hospitali hiyo kuanzia mwisho wa mwezi Juni na hadi leo mambo hayakwenda sawa.

Kabla ya kushika nafasi hiyo Essebsi aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo waziri mkuu mwaka 2011 na baadaye kuwa Rais wa nchi hiyo.Pia amewahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2015 na hakutangaza nia ya kugombea nafasi ya kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu.

TAFRIJA MAALUM KWA WAANDISHI WA HABARI KUADHIMISHA MIAKA 70 YA TAIFA LA CHINA YAFANYIKA ZANZIBAR

0
0
Na Ali Issa,  Maelezo
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mshirika mkubwa wa kimaendeleo kwa Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Hayo yamesemwa huko Hoteli ya Verde na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Muhammed Salum katika sherehe za miaka 70 ya kuundwa kwa Jamuhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.

Amesema China ilikua ni nchi ya kwanza kuiunga mkono Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na ushirikiano huo umekuwa ukiendelea hadi hivi sasa.

Aliongeza kusema kuwa China imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar na kuiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, kilimo, utamaduni na michezo.

Alikumbusha juu ya ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Amanai na Mao tse Tung na kusaidia kuleta madaktari na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na ile ya Mkoani.

Aidha alisema wameweza kusaidia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar na miundo mbinu ya Barabara na huduma za mawasiliano kwa kuweka taa katika barabarani mbali mbali za Zanzibar.

Alisema uhusiano uliopo kati ya China na Tanzanzia ni wa kipekee kwani Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kiongozi pekee alieweza kukutana na Baba wa Taifa la China Marehemu Mao mjini Beijing mara nyingi zaidi kuliko kiongozi mwengine yoyote katika uhai wake.

Aidha Mkurugenzi huyo alilieleza kuwa China imekuwa ikitoa elimu kwa vijana wa Zanzibar katika fani tofauti na imekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.

Nae Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema kuwa Nchi yake imekuwa rafiki wa kweli na Tanzania na imekuwa mstari wa mbele kuongeza misaada yake kwa Taifa hilo na Afrika kwa Ujumla .

Aliongeza kuwa China inaendeleza juhudi za upatikanaji wa huduma za maji safi na salama mijini na vijijini kwa kuchimba visima vipya katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na kujenga matangi mapya ya kuhifadhia maji Saateni na Kilimani.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk,Juma Mohamed Salum akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (kulia)akimkabidhi zawadi ya Kitabu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum kushoto yake katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari mbalimbali katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum wakichukua chakula katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
 Waandishi wa Habari wakichukua chakula katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

Benki Ya NBC Yaahidi Ushirikiano Zaidi Na Mamlaka Za Serikali Za Mtaa.

0
0

Benki ya NBC imeahaidi kuendelea kutoa huduma bora zenye ubunifu kwa Mamlaka za serikali ya mtaa hapa nchini ili kuongeza tija na ufanisi zaidi kwa mamlaka hizo.

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa NBC, Bw William Kallaghe wakati akizungumza kwenye kwenye Mkutano wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza hivi karibuni.

Alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uwepo wa benki hiyo hapa nchini, imewekeza katika huduma mbalimbali za kifedha ambazo zimeleta tija kubwa kwa mamlaka hizo na taifa kwa ujumla.

“Katika kipindi chote hicho NBC tumefanikiwa kutoa suluhisho ya kiubunifu kupitia huduma za kielectroniki kwa Halmashauri za Wilaya na Manispaa katika ukusanyaji wa mapato sambamba na huduma za malipo zinazoboresha usahihi katika uendeshaji akaunti’’ alisema.

Alibainisha kuwa uwezo huo umeimarishwa zaidi kufuata mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroniki (GePG),Mtandao wa NBC Wakala, Mfumo wa makusanyo wa POS pamoja na makusanyo kupitia simu za mikononi.

Kwa mujibu wa Bw Kallaghe, huduma za kielektroniki za malipo na ukusanyaji wa mapato zinazotolewa na benki ya NBC kwa mamlaka hizo zimeongeza ufanisi katika malipo na ukusanyaji wa mapato kwa mamlaka hizo na hivyo kurahisisha usahihi katika uendeshaji wa akaunti zao.

“Matawi ya NBC yamewezeshwa kwa nyanja zote katika kufanikisha mahitaji yote ya kifedha kwa Halmashauri na Mamlaka zote za serikali ya mitaa,’’ alibainisha huku akiongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha mamlaka hizo zinatoa huduma bora na za kisasa sambamba na kujiongezea mapato.


Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma kutoka Benki ya NBC, Bi. Noelina Kivaria akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Anaeshudia ni Mwenyekiti wa Alat Taifa, Gulamhafeez Mukadam (kushoto). Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipata maelezo ya huduma za kibenki kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa NBC, Bw William Kallaghe alipotembelea kwenye banda la benki hiyo kwenye Mkutano wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Kibenki cha Taasisi za Sekta ya Umma, Bi. Noelina Kivaria. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisoma moja ya machapisho ya huduma za kibenki ya Benki ya NBC alipotembelea kwenye banda la benki hiyo kwenye Mkutano wa Mkuu wa 35 wa Mwaka wa Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Kushoto ni Meneja Mahusiano ya Kiserikali wa Benki ya NBC, Bw William Kallaghe pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

Wazazi wakingia kifua Mwalimu Mkuu Mtoni Kijichi

0
0
WAZAZI wa shule Shule ya Msingi, Mtoni Kijichi, iiyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam,  wameadhimia kumuita Mbunge, Mkuu wa Wilaya na Meya kwenye wa Temeke, kwenye kikao kinachotarajiwa kufanyika Jumamosi kwa lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo kushushwa cheo kwa aliyekuwa Mwalimu Mkuu Wa shule hiyo, Evelyne Munisi.

Amesema mkutano huo umeadhimia kuwaita viongozi hao ili kuja kutatua mgogoro uliopo ndani ya shule ya Msingi Mtoni Kijichi baina ya Kamati ya Wazazi, Mwalimu na diwani wa kijichi.

Amesema, diwani wa Kijichi, Eliasa Mtarawanje pia anidaiwa kuwatishia wazazi wa shule hiyo kupitia kwa Katibu wa Kamati ya Wazazi, Mathias Balijuza kuwa endapo watafanya mkutano shuleni hapo, atawafunga.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika hivi karibuni shuleni hapo katika chumba cha darasa la VII A, Bulijuza amesema kuwa alitishiwa kufungwa na diwani huyo, baada ya kutaka  kuwatangazia wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, wawaambie wazazi wao waje kwenye kikao.


"Alinitishia, Balijuza nitakufunga, nitakufunga wewe unataka kuleta fujo kwenye eneo la shule, angalia nitakufunga, picha hiyo ilinichanganya ikabidi niwapatie wazazi taarifa ya mkutano kupitia ujumbe wa simu" amesema Balijuza.

Amesema, kufuatia tishio hilo, baadhi ya wazazi walihofia kufika kwenye kikao hicho kwa sababu mimi nilikwenda kutoa taarifa kwa niaba ya wazazi wote,"

Naye  Mwenyekiti wa Mtaa wa Butiama, Kata ya Kijichi, Haji Mgaya amesema amepata mualiko kupitia Kamati ya Shule kwa ajili ya kwenda kuangalia mchakato mzima wa elimu bure, lakini alipofika katika mkutano huo alikutana na changamoto nyingi ikiwemo ya Mwalimu Mkuu kushushwa cheo na madarasa yanayotumikaga kufanyia mikutano yamefungwa.

" Niwatoe hofu wazazi, sisi na Kamati ya wazazi tunasimamia sheria, hakuna taasisi yoyote ya kipolisi inayoweza kufanya jambo kinyume na taratibu na sisi tupo kwenye miongozo ndiyo maana tunaalika watu wenye sifa kuja kutoa maamuzi

Kuhusiana na kufungwa kwa milango la madarasa, Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Twaha Kifunde alisema madarasa hayo yalifungwa kama kawaida na walinzi, kwa sababu hakukuwa na mkutano rasmi shuleni hapo na mtu wa kwanza kutangaza mkutano ni Mwalimu Mkuu.

"Hakuna aliyeniambia nimfungulie vyumba vya madarasa nikakataa na hii taarifa ya kuwa mimi nipewa maelekezo na diwani ya kukataza mkutano usifanyike shuleni hapa si za kweli, kwa sababu kuna utaratibu wa kufanya mikutano," alisema Mwalimu Kifunde

Naye Diwani Mtarawanje akijibu tuhuma hizo alisema hayo ni mambo ya kisiasa  na kututaka tuachanenayo, kwa sababu yeye anasimamia Serikali kutokuchangisha wazazi michango ya shule kwa sababu, Serikali inatoa elimu bure.

"Haya mambo sitaki kuyasikia, sisi tunasimamia Serikali kutokuchangisha michango, mambo ya kupigiana pigiana simu sio, waache na tuhuma zao.Tuhuma zao zingine ni zipi? achana nazo hizo habari, mambo ya kisiasa hayo achana nayo," alisema Diwani Mtarawanje

Hayo yote yametokana na  kikao cha wazazi kilichokaa kupitisha maadhimio kuwa kila mzazi mwenye mtoto wa darasa la sababu achangie Sh 8,000 kwa ajili ya masomo ya ziada, ambapo badae Mwalimu Munisi alishushwa daraja na kuwa Mwalimu wa kawaida kwa madai kuwa yeye ndiye alichangisha michango h

Amesema mchanganuo wa fedha hiyo ni kwamba , Sh 10,000 ni ya chakula cha mchana kwa wanafunzi hao, ambapo sahani ya chakula kwa siku ni sh 500 na Sh 5000 iliyobaki ni kwa ajili ya gharama ya uchapishaji wa mitihani ya masomo matano ambayo yatakuwa yanafanyika kila jumamosi ya wiki.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATAKA MABORESHO YA HAKI JINAI YAJENGE NA SIO KUKOMOA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainabu Chaula ataka Haki Jinai itengeneze katika kujenga na sio kukomoana ili kuwa na jamii bora yenye kufuata misingi ya haki.

Ameyasema hayo alipotembelea kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai kinachoendelea Jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo wa haki jinai nchini na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuona kwa pamoja namna ya kufanya maboresho katika Mfumo wa haki jinai nchini.

“Haki Jinai itengeneze katika kujenga na sio kukomoana” amesema na kuongeza kuwa sehemu kubwa ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu haki zao na hivyo kusababisha kukosa haki hizo na pale wanapofanikiwa kuzijua hawazipati kwa sababu anayetoa haki ni mbabe.

Hivyo akasisitiza elimu ya haki jinai isambae kwenye jamii kupitia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya redio na Runinga  na njia nyingine mbalimbali ambazo zitakuza uelewa kwa jamii ili kuwawezesha kudai haki zao pale zinapokiukwa.

Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa nchi yetu ina mambo mengi mazuri ambayo jamii haiyajui ikiwemo suala zima la Haki Jinai na hivyo kusababisha ukiukwaji wa haki za msingi kwa jamii.

Mfumo wa Haki Jinai unafanyiwa maboresho katika maeneo ya Kisera, kisheria na kiorganizasheni ili kuufanya mfumo huo kuweza kuakisi changamoto za maendeleo zilizopo na zijazo. Aidha, ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kukutanisha wadau mbalimbali ili kufanya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainabu Chaula akiongea na kikosi kazi kinachofanya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Patience Ntwina na kulia ni Mkurugenzi kitengo cha Ugavi na Manunuzi Ndg. David Mwangosi.
Washiriki wa kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainabu Chaula (hayupo pichani), alipotembelea kikosi kazi hicho kinachoendelea na maboresho jijini Dodoma.

MKONGEA AKEMEA KILIMO CHA BANGI NA MADAWA YA KULEVYA

0
0

 NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ali amekemea kilimo cha bangi kwani kinaharibu mazingira na kuweka rehani maisha na afya ya watumiaji ambapo asilimia kubwa ni nguvu kazi ya Taifa ambayo ni kundi la vijana.

Ameeleza,licha ya hayo serikali inaendelea kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo,milungi,cocaine,heroine, bangi pamoja na kudhibiti mianya ya wauzaji wa madawa hayo ili kuokoa nguvu kazi hiyo ambayo inaangamia siku hadi siku.

Hayo aliyasema wakati mbio za mwenge wa uhuru Jaribu Mpakani, kata ya Mjawa wilayani Kibiti mkoani Pwani.
 Mkongea alieleza Taifa letu bado kuna matumizi ya madawa ya kulevya hivyo tushirikiane kudhibiti na kupambana na janga hilo .

"Chakusikitisha vijana hawa wanaita bangi kwa majina mengi kama vile misuba,cha Arusha,jani,ganja,msokoto,Bob Marley na Jamaica lakini ukweli unabaki pale pale bangi ni bangi tu, vijana tubadilike tupambane na janga hili na tujiingize katika shughuli za kujenga Taifa kuchapa kazi"alisisitiza Mkongea.

Hata hivyo, Mkongea aliwaasa vijana kuacha kuvuta bangi ,kujidunga sindano za madawa ya kulevya kwakuwa wanakuwa hatarini kupata ugonjwa wa ukimwi,moyo,ini,mapafu na hatimae kifo.

Akizungumzia suala la Ukimwi, mkimbiza mwenge kitaifa huyo alisema ugonjwa huo bado ni hatari jamii ijilinde na kuwa waaminifu.

"Watanzania takriban milioni 1.4 wanaishi na VVU ,maambukizi mapya kila mwaka ni watu 81,000 tuendelee kujikinga na kuwa na tahadhari na maambukizi mapya"alibainisha .

Mkongea alieleza, mkoa wa Njombe unaoongoza kwa maambulizi nchini kwa asilimia 11.4,Iringa asilimia 11.3,Mbeya asilimia 9.3,Mwanza asilimia 7.2 na Kagera 6.5 huku kitaifa ikiwa asilimia 4.7.

Kwa upande wake ,mkuu wa wilaya ya Kibiti ,GulamKifu alisema ,mwenge wa uhuru ukiwa Kibiti utapitia miradi 13 yenye gharama ya bilioni 2.59.

Alieleza katika miradi hiyo ,mradi mmoja utafunguliwa,mmoja utazinduliwa,miradi mitatu itawekwa jiwe la msingi na mingine nane itatembelewa.

Nae mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, ambae pia ni naibu waziri wa nishati Subira Mgalu aliwahamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli za uwekaji jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa umeme Stigo wilayani Rufiji,itakayofanyika Julai 26 mwaka huu.

Aliwaambia wananchi hao baada ya mradi huo kukamilika maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme yatanufaika na mradi huo .

CHUO KIKUU HURIA YARUDISHA PROGRAMU YA MSINGI KWA WANAFUNZI WALIOKOSA SIFA ZA UDAHILI.

0
0
Na Khadija seif, Michuzi tv

KUFIKIA uchumi wa viwanda kati pamoja na viwanda 2025 vyuo vikuu havina budi, lazima kuzalisha na kutengeneza wataalam wengi wasomi kutokea hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Makamu Mkuu wa chuo kikuu huria nchini Pro. Elifas Bisanda amesema kwa sasa wanafunzi wajikite kwenye masomo ambayo yataleta manufaa kwa mustakabali wa nchi kwa ujumla hasa masomo ya sayansi.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa chuo hicho kitatoa programu ya msingi ili kumuwezesha mwanafunzi kuwa na sifa za kuendelea na elimu ya juu.

"Kumekuwepo kwa changamoto tulizokumbana kutokana na Tume ya vyuo vikuu kufunga programu hiyo kwa muda wa miaka miwili kutokuwepo kwa program hiyo ya msingi (FOUNDATION COURSE) kwa wanafunzi ambao kimsingi walikosa sifa za kuendelea kwa masomo na kulazimika kurudi mtaani na kukatisha ndoto zao,"

Aidha, Bisanda amefafanua sifa za wanafunzi ambao wanaotakiwa kufanya udahili ni kwa wale ambao watakua wamefanya vizuri katika ngazi ya Astashada pamoja na wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na kufaulu marks wanazohitaji ambazo ni nne zinazohesabiwa kwenye masomo mawili.

" Ni programu inayowaongezea maarifa wanafunzi ili kufikia kiwango Cha kujiunga na elimu ya juu, na sio programu rahisi Kama watu wanavyoitafsiri kwani wengi wao wamekua wakirudia mara kwa mara ili kupata sifa stahiki,"

Pia amebainisha kuwa programu hiyo ina masomo 14 ambapo masomo ambayo mawanafunzi inamlazimu kuyasoma masomo ya mazingira,tehama na Mawasiliano ili kumuandaa kulingana na ufaulu wake.

" Chuo chetu kinamuwezesha mwanafunzi kusoma mwenyewe kwa Mfumo wa tehama na kwa kutumia vitabu ambavyo vimechapishwa kwa moduli na kuendelea kusoma au kompyuta mpakato na simu janja wanaweza kupata mada zote ,"

Pia ametoa wito kwa wanafunzi wanaotaka kufanya udahili chuoni hapo kutokata tamaa kutokana na kukosa sifa na waanze na programu hiyo ya msingi na kumuwezesha kuendelea na elimu ya juu.
Makamu Mkuu wa chuo kikuu huria nchini Pro.Elias Bisanda akitolea ufafanuzi changamoto walizokua wakikumbana nazo wanafunzi walioachishwa masomo kutokana na kufutwa kwa programu ya msingi (FOUNDATION COURSE) na tume ya vyuo vikuu nchini.

GAGUTI AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA -VITA YA KAGERA .

0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa MichuziTV - Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, ameongoza maafisa, askari wa Kikosi Na. 21 KJ, wananchi katika maadhimisho ya miaka 40 ya mashujaa Wa Vita ya Kagera, ambayo yamefanyika katika shamba la mashujaa Kaboya, Julai 25, 2019.

Katika Salaam zake Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewashukuru askari kwa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kujitolea damu, huku akiwakumbusha askari hao juu ya majukumu yao ya ulinzi wa amani na mipaka ya Nchi yetu. Sambamba na hilo amewataka askari pamoja na majirani kuliona eneo la Kaboya na umuhimu wake kwa kulitunza na kulifanya la kihistoria akilifananisha na Eneo la Hijja kiimani, na kuahidi kuweka Nyumba ya kumbukumbu na historia ya Kikosi Na. 21KJ katika ushiriki wa Vita ya Kagera.

Vita ya Kagera ilianza mwaka 1978 Oktoba wakati ambapo Rais wa Uganda wakati huo Idd Amin Dada alipovamia ardhi ya Tanzania Mkoani Kagera eneo la Mtukula, eneo lenye Kilomita 1852, baada ya kuharibu Mali za wananchi, kuua wananchi, kuvunja daraja la Kyaka na kisha kubomoa Kanisa, na hapo ndipo Amir Jeshi wa Tanzania wakati huo Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na majeshi ya Tanzania yakiongozwa na Marehemu Jenerali Twalipo mnamo Novemba 1978 waliamua kutangaza vita ya Kagera iliyokusudia kumuondoa Idd Amin.

Katika Vita hiyo iliyomalizika Julai 1979 ilisababisha vifo vya askari wapatao 619, huku askari waislam wakiwa 258 na wakristo wakiwa 461. Mpaka sasa Mkoa wa Kagera umejiimarisha na kuendelea kuimalika kiulinzi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa mipaka ya Nchi, na usalam wa Raia na Mali zao chini ya Vikosi vya ulinzi na Usalama.
 Pichani Mnara wa mashujaa uliopo katika shamba la mashujaa Kaboya, walipozikwa askari waliofariki katika vita ya Kagera mnamo mwaka 1978-79.
 Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa Kagera akipata Maelezo kuhusu masalia ya zana za kivita zilizotumika kumuondoa Nduli IDD Amin na majeshi yake, wakati alipofika Katika  shamba la mashujaa Kaboya Julai 25, 2019.
 Pichani Brigedia Jenerali Gaguti akitoa heshima katika kaburi la Askari wa kwanza Kupoteza maisha katika Vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Vita ya Kagera.
 Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akiweka Ngao na Mkuki Katika mnara wa mashujaa waliokufa katika vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya Miaka 40 ya Vita ya Kagera.
 Pichani ni Luteni Kanali Sadala Twalibu Kapungu Kamanda wa Kikosi 21 KJ, akiweka shada la maua katika mnara wa mashujaa waliokufa katika vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya kumbukumbu ya Vita hiyo.
 Pichani ni Askari wa Gwaride kutoka kikosi cha 21 KJ wakiwa katika gwaride la heshima katika shamba la mashujaa Kaboya, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 Vita ya Kagera.
 Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha 21 KJ, kabla ya ukaguzi wa gwaride hilo na kisha kutembelea makaburi ya mashujaa Wa vita ya Kagera.
 Pichani Ni Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti pamoja na Kamanda wa Kikosi Na. 21 KJ Luteni Kanali Sadala Kapungu, wakiingia katika shamba la mashujaa Kaboya, walipolala askari waliopoteza maisha wakati wa Vita ya Kagera.
Sehemu ya Baadhi ya Askari, Wananchi, majirani na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kaboya, wakiendelea kumsikiliza Mgeni Rasmi wakati wa maadhimisho ya Miaka 40 ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Kagera.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI MAPINGAMIZI YA CHADEMA,YAPOKEA VIELELEZO VILIVYOPINGWA UPANDE WA UTETEZI TEPU MBILI

0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu  imetupilia mbali mapingamizi ya Chadema na kupokea kielelezo cha Kamera ya kurekodi video na Tepu mbili kilichopingwa Mahakamani hapo na upande wa Utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.

Uamuzi huo umetolewa leo Julai 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba amesema, Kifungu cha 18 cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki kimeweka vigezo vya upokeaji wa vielelezo vya eletroniki ambavyo shahidi namba sita Koplo Charles alikidhi vigezo hivyo na kuongeza kuwa, ushahidi wake umekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwenye kifungu hicho hivyo kwa muktadha huo mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi yanatupiliwa mbali.
 "Mahakama imeyatupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi,  Kamera hiyo imepokelewa kama kielelezo namba nne na zile tape mbili kama kielelezo namba tano, " amesema Simba

Julai 11, mwaka huu  Wakili Kibatala alipinga kupokelewa kwa vielelezo hivyo vilivyotolewa na shahidi wa sita wa upande wa mashtaka kwa kudai kuwa ushahidi wa kieletroniki hauwezi kupokelewa mahakamani mpaka kuwepo kwa kiapo mahususi juu ya utoaji wa vielelezo hivyo kwa mujibu wa sheria fungu la 18 na 19 ya ushahidi wa kieleketroniki.

Dk Zainab alijibu hoja hizo Julai 12, mwaka huu kwa kuieleza Mahakama kuwa aina ya utunzaji vielelezo vilivyowasilishwa na Shahidi wao ulikuwa mzuri kama yalivyo matakwa ya kisheria.
Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018, Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu  Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi,  Wakili wa Serikali Mkuu , Dk. Zainab Mango na Wakili wa Serikali Mwandamizi  Wankyo Simon.

Pia Upande wa utetezi uliwakilishwa na  Wakili Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu Chadema  Dk.Vicent Mashinji, John Mnyika Naibu Katibu Mkuu (Chadema)-Bara na Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar.

Wengine ni Ester Matiko Mhadhini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Tarime Mjini, Halima Mdee Mwenyekiti wa (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini, na Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la kula njama na uchochezi

DC Ikungi aapishwa, aahidi kushirikiana na wananchi wake

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli kufuatia .Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
 Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo vitendea kazi leo Ofisini kwake,mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli.Mh Edward alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Mh Edward Mpogolo akitia saini kiapo chake mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singinda Mh Dkt.Rehema Nchimbi.



Na Charles James, MICHUZI TV

MKUU mpya wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Bw Edward Mpogolo ameapishwa leo rasmi kuanza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya hiyo, kuchukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Miraji Mtaturu ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu jana, uteuzi wa Bwana Mpogolo ulianza rasmi jana Julai 24, 2019, kuwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi Rehema Nchimbi, Mpogolo ameahidi kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya  Wilaya katika  kuhakikisha inakuwa na maendeleo sambamba na kusimamia kikamilifu  makusanyo  ili kuinua uchumi wa eneo hilo.

“Ninamskuru Rais Dk,John Magufuli kwa kuniteua,ninaahidi kuwa sitamwangusha ,nitahakikisha ninashirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri yangu ya Ikungi ili kuhakikisha tunafikia malengo ya makusanyo katia Wilaya yetu”amesema Mpogolo.

Ameahidi kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili kuhakikisha wanatumikia wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa wao ndio wawakilishi wa Rais katika eneo hilo.

Pia ameahidi kwenda kuisimamia  Katiba ya Nchi pamoja na Ilani ya Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi  katika  kuwatumikia   wananchi atakaowaongoza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema  Mkuu wa Wilaya ndio msimamizi mkuu wa Kamati ya ulinzi na usalama na ndio msimamizi mkuu wa shughuli za maendeleo katika eneo husika na kumtaka kwenda kusimamia  vyema miradi ya Serikali inayotekelezwa Wilayani humo.

“Mkuu wa Wilaya yeye ni msimamizi mkuu na muwakilishi wa Rais katika Wilaya na ndio mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama na ukasimamie miradi yote inayotekelezwa Wilayani humo” amesema Dtk Rehema.

Hata hivyo amemwambia kuwa Wilaya ya Ikungi inamiradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kwenye malengo ikiwemo miradi ya visima 28 vilivyokusudiwa kukamilishwa .

Aidha Dk.Nchimbi amesema upande wa Singida magharibi wana miradi ya visima 13 na Singida mashariki visima 15 .

Amebanisha malengo mengine yaliyowekwa kwa Wilaya hiyo kuwa ni kilimo cha zao la michikichi ekari 200 pamoja na kilimo cha zao la korosho.

RC MAKONDA AENDELEA KUTIMIZA AHADI YA UFADHILI WA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 KUTOKA FAMILIA DUNI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 25 amepokea zaidi ya Shilingi Milioni 23 kutoka kwa wadau ambao wameguswa na kampeni aliyoanzisha ya ufadhili wa matibabu ya upasuaji moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye hali duni.

Miongoni mwa Wadau waliomuunga Mkono RC Makonda ni Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Sylvester Koka ambae amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 10 kwaajili ya matibabu ya watoto 5 huku Mkurugenzi wa Dorka Catering Bi. Dorothy Kansolele akichangia milioni 6 na mkurugenzi wa kampuni ya Abe Professional Sound Bw. Abraham Ngomko akichangia Milioni 6 kwaajili ya matibabu ya watoto 3.

Akipokea fedha hizo RC Makonda amezikabidhi kwa uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kueleza kuwa zitasaidia kugharamia zaidi ya Watoto10 kwenye upasuaji wa awamu ya pili.

Aidha RC Makonda amewashukuru wadau wote wanaondelea kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya watoto ambao wangeweza kupoteza maisha kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Kwa upande wao wadau waliokabidhi fedha hizo wameeleza kuwa wataendelea kuunga mkono zoezi hilo kwa kuongeza fedha nyingine kwakuwa wanaamini kampeni aliyoanzisha RC Makonda ni njema na linapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha ya watoto.

Itakumbukwa kuwa RC Makonda alitoa ahadi ya kufadhili matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 60 kwa muda wa miezi sita ambapo kila mwezi watatibiwa watoto10 na hadi sasa tayari amefanikisha matibabu ya watoto 30 kati ya 60 alioahidi.

WAZIRI MKUU ATAKA RUVUMA IONDOE VIKWAZO VYA UWEKEZAJI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo na kuondoa vikwazo vyote ili kuvutia wawekezaji zaidi.

“Mkoa wa Ruvuma kama ilivyo mikoa mingine, unazo fursa ambazo zikiendelezwa, zitaleta tija na kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Nitoe rai kwa mkoa uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo sambamba na kuondoa vikwazo vyovyote vya uwekezaji na biashara ili kuvutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje,” amesema.

Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Julai 25, 2019) wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji mkoani Ruvuma linaloendelea kwenye uwanja wa Majimaji, Manispaa ya Songea. Pia amezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo.

Amesema katika ustawi wa uchumi, nchi nyingi hapa duniani zimeweza kukuza uchumi wao kupitia ujenzi wa viwanda na zikafanikiwa kupunguza umasikini katika jamii zao. Amezitaja nchi hizo kuwa ni Marekani, China, Japani, Korea ya Kusini na Ujerumani.

“Tunapaswa kuiga kutoka wa wenzetu. Ndiyo maana Tanzania pia tunahamasisha ujenzi wa viwanda kuanzia ngazi ya vijiji mpaka mikoa ili tulete mageuzi ya kiuchumi yatakayowezesha upatikanaji wa ajira na hatimaye kuondoa umaskini,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza:

“Kongamano hili ambalo kaulimbiu yake ni “Ruvuma itavuma kwa uchumi wa viwanda, wekeza sasa,” imelenga kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo mkoani humu, na  inajipambanua vema na kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo 2025.”

Amesema mchango wa sekta ya viwanda kiuchumi na kijamii nchini ni pamoja na kuongeza pato la Taifa na kupandisha hali ya maisha ya wananchi; kusaidia nchi isiyumbe kiuchumi ikizingatiwa kuwa viwanda vingi havitegemei hali ya hewa kama kilimo; kuboresha urari wa biashara (improve balance of trade) kwa sababu tija yake ni kubwa na hasa zikiuzwa bidhaa nyingi nje ya nchi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Amezitaja faida nyingine kuwa ni kuchangia maendeleo ya sekta nyingine kama za kilimo, uvuvi, elimu na madini; kutengeneza ajira kwa wananchi; kuchagiza na kuharakisha maendeleo ya teknolojia na rasilimali watu na kuwezesha matumizi mazuri ya maliasili zilizopo kwa faida zaidi.

Nyingine ni kuleta uhakika wa soko la mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini kwa sababu hutumika kama malighafi na kuwepo kwa uhakika wa kuingiza fedha za kigeni nchini kupitia mauzo ya bidhaa nje ambapo husaidia kuagiza mitambo, malighafi na bidhaa nyingine ambazo hazizalishwi nchini.

Mapema, akitoa salamu kwa niaba mabalozi wengine, Mwakilishi wa Balozi wa China, Bw. Xian Bing alisema ana uhakika kuwa kongamano hilo litafanikiwa kuleta mabadiliko mkoani humo kwa sababu wana bidii ya kazi.

“Ninaahidi kuleta wawekezaji kutoka China kwa sababu tunataka waje kuleta teknolojia mpya, wafanye kazi pamoja na Watanzania na wawafundishe teknolojia hizo mpya. Tunataka hapa Ruvuma iwe model (mfano) kwa mikoa mingine,” alisema.

Akielezea kwa kifupi kuhusu mwongozo uliozinduliwa na Waziri Mkuu, mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Hoseana Lunogelo alisema walitumia mfumo shirikishi ili kupata mwongozo unahusisha wawekezaji wa ndani.

“Mwongozo huu umezingatia Dira ya Taifa ya 2025 katika kutimiza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya uchumi na viwanda, tumeshirikisha wananchi wa mkoa wa Ruvuma ili wasibakie kuwa watazamaji,” alisema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa China Tanzania, Bwana Xian Ding, wakati alipoipongeza Serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji,yaliyofanyika katika Mkoa wa Ruvuma, Julai 25.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Ruvuma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma. Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje John Ndumbalo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amebeba mkaa wa mawe, wakati akikagua mabanda kwenye banda la TANCOAL, katika  maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na kulia ni Mkuu wa Jiolojia TANCOAL.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mkaa wa mawe, uliyotengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na wajasiriamali wa kikundi cha Mbalawala Women Group, wakati akikagua mabanda kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019. Tokea kulia ni Meneja wa Fedha wa kikundi hicho, Esta Silas na Msimamizi wa Mradi, Hajra Yakub.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Mbinga Coffee Curing Company, kabla ya kufungua maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, akiangalia na vikundi vya ngoma, kwenye maonesho ya viwanda na kongamano la uwekezaji mkoani Ruvuma, Julai 25.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

PUMA ENERGY TANZANIA YAAHIDI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI NCHINI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI

0
0
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (wa pili kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni nne kwa mshindi wa kwanza wa shindano la michoro ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka 2019, Alphonce Philipo wa shule ya msingi Jenerali Musuguri, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah,akisoma taarifa katika utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah,akifurahia jambo na wanafunzi (hawapo pichani) wakati akisoma taarifa inayohusu utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mratibu wa mafunzo ya Elimu ya usalama barabarani kutoka Amend Bi.Neema Swai,akiongea wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mwalimu wa shule ya Msingi ya General Musuguri,Beatrice Chidumizi,akitoa pongeza kwa Puma Energy wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Afisa Elimu Msingi jiji la Dodoma,Joseph Mabeyo,akitoa shukrani kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde (wa pili kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, waandaaji wa shindano, Dominic Dhanah, wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mwalimu wa shule ya msingi Kaloleni Bi.Edina Kagulumbega,akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Sehemu ya Wanafunzi kutoka shule za msingi wakifuatilia hafla ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Baadhi ya walimu wakifuatilia utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Wanafunzi wakiimba wimbo maalumu wa unaoelezea umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Mmoja wa wanafunzi waliopata elimu ya mafunzo ya usalama barabarani akionesha mfano wa mwanafunzi aliyepata ajali kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Wakiangalia michoro ya usalama barabarani iliyochorwa na wanafunzi kutoka shule tano za msingi katika jiji la Dodoma kabla ya kumtangaza mshindi wa shindano la Michoro ya Usalama Barabarani kwa mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Puma Energy Tanzania hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini Dodoma .
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la michoro ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mwaka 2019, hafla ambayo imefanyika jijini Dodoma.

......................

*Ni katika mkakati wake wa kukomesha ajali nchini, wanafunzi Dodoma wanufaika

*Naibu Waziri Mavunde awapongeza, asema ni kampuni ya mfano...atoa maombi maalum

Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Dodoma

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imesema itaendelea kutoa elimu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa shule za msingi mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wake wa kupunguza ajali nchini.

Pamoja na ahadi hiyo kampuni hiyo imetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi zaidi ya 4500 katika shule tano za msingi katika Jiji la Dodoma kwa mwaka huu wa 2019 huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu hiyo na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wanafunzi wengi zaidi ambao watakuwa mabalozi kwa wengine.

Akizungumza leo Julai 25 jijini Dodoma mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Vijana Athony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema programu hiyo ya mwezi mmoja kwa Dodoma ilihusisha mafunzo ya usalama barabarani kwa walimu 15 na wanafunzi 4500, katika shule tano.

Amefafanua kulikuwa na shindano la uchoraji wa michoro inayo hamsisha usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni iliyozinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa huku wanafunzi 100,000 wakiwa wamepatiwa mafunzo katika mikoa ya Dar-es-salaam, Geita, Ruvuma na Dodoma.

“Puma Energy Tanzania imeamua kuja jijini Dodoma kwa sababu ya ukuaji wa haraka wa jiji hili ambapo shughuli za kijamii na ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha usalama wa watoto wanapokwenda shuleni na kurudi nyumbani,",amesema Dhanah na kuongeza “Hadi sasa tumeweza kufundisha wanafunzi zaidi ya 4500 wa shule tano za msingi zilizopo jiji la Dodoma".

Dhahana amesema mafunzo hayo ya usalama barabarani na uchoraji alama za barabarani ni kipaumbele kwa lengo la kuwapa uelewa watoto hususani wa shule za msingi juu ya namna bora ya matumizi ya barabara.Alibainisha lengo ni kuwafanya watoto kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara ili kuongeza uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa Watanzania.

“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima. Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya watanzania,” amebainisha.Akieleza zaidi amesema unzo hayo yametolewa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Amend ambapo elimu hiyo pia imetolewa kwa walimu 15 wa shule hizo.

Awa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amesema Puma Energy Tanzania ni kampuni iliyoamua kutoa elimu ya usalama barabara nchini huku akitoa ombi kwa kampuni hiyo kufundisha walimu hizo ili wakifundisha masomo ya kawaida wawe pia wanataka na elimu ya usalama.

Amesema kwa kufanya hivyo inasaidia kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani huku akifafanua Serikali itaendelea kuweka alama za usalama barabarani ili kuondoa changamoto za ajali.Amesema kuwa kutokea kwa elimu hiyo kwa Jiji la Dodoma kunakwenda kutengeneza jamii yenye mabalozi wazuri katika kutoa elimu ya usalama barabarani huku akieleza Dodoma ni ya pili kwa mtandao wa barabara za lamo,hivyo ni muhimu elimu hiyo kuendelea kutolewa.

"Nimesikia ombi la walimu na wanafunzi la kuhitaji alama za barabarani, hivyo Serikali itaendelea kuweka alama hizo.Pia nimezungumza na wenzetu wa Puma wamekubali kupaka rangi za usalama barabarani na wataanza na shule tano ambazo zimepatiwa elimu hii ya usalama barabarani,"amesema Mavunde

Wakati huo huo walimu wakuu katika shule za msingi katika Jiji la Dodoma wametoa ombi la kuweka alama za barabarani na hasa alama za pundamilia au matuta ili kuhakikisha wanafunzi wanapovuka wanakuwa salama kwani barabara nyingi hazina alama hizo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi General Musuguri Beatrice Chidumizi amesema changamoto iliyopo kwenye eneo la shule yao ni kukosekana kwa matuta au alama za barabarani, hivyo wanalazimika kumuweka mtu wa kuvusha wanafunzi ambaye analipwa fedha.

"Changamoto kubwa iliyopo katika shule yetu ni barabara yetu kutokuwa na matuta na alama za pundamilia,hivyo tunaomba tuwekewe alama za barabarani kwa ajili ya usalama wa wanafunzi wetu.Tunaishukuru Puma kwani imetusaidia sana kuwajengea uelewa wanafunzi wetu na sasa wanafahamu cha kufanya wanaoutaka kuvuka barabara.

"Tunaamini kupitia mafunzo haya tutapunguza ajali kwa watoto wetu na watumiaji wengine wa barabara zetu,"alisema Mwalimu Chidumizi na kuongeza kuwa umefika wakati kwa elimu hiyo kuendelea kutokea kwa Jiji la Dodoma hasa kwa kuzingatia Dodoma inakuwa kwa kasi kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.

RAIA WA HUNGARY AFIKISHWA KORTINI DAR, KISA AKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

0
0


Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

RAIA wa Hungary Akos Berger (28), amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu  250  aina ya Amphetamine.

Berger amefikishwa mahakamani hapo leo Juali 25,2019 na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai,  Julai 19 mwaka huu, eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu  Kasonde alimtaka mshitakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa za kulevya, usipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP

Upande wa mashitaka umedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka na kesi iliahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa.

Wakati huo huo, Wafanyabiashara wawili wa jijini Dar es Salaam wamefikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilogramu 21.67.

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala amewataja washitakiwa hao kuwa ni Ramadhan Gumbo (25) mkazi wa Ilala na Fahad Salehe (24).

Makakala amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Julai 13, mwaka huu maeneo ya Mbezi wilayani Kinondoni, walisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Hakimu Shaidi amewataka washitakiwa kutojibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images