Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

DKT BASHIRU ATEMBELEA MKUTANO WA WATAALAMU WANAOJADILI MABORESHO YA MFUMO WA HAKI JINAI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Wataalam wanaoshiriki majadiliano ya kufanyia maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai nchini unaofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Wataalam wanaoshiriki majadiliano ya kufanyia maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai nchini unaofanyika jijini Dodoma.
Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa majadiliano yenye lengo la kufanyia maboresho sekta ndogo ya haki jinai nchini unaofanyika jijini Dodoma wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally (hayupo pichani ) alipokuwa akizungumza nao juu ya kazi hiyo wanayoifanya.
…………………..
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametembelea Mkutano wa Wataalam wanaoshiriki majadiliano ya kufanyia maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai nchini unaofanyika jijini Dodoma na kuwataka wataalamu hao kushughulikia maeneo yanayotoa mianya ya rushwa, urasimu na ubwetekaji kwa taasisi zinazohusika na mfumo wa haki jinai ili kupata mfumo sahihi unaotoa haki kwa wananchi.

Amesema kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai inapaswa kushirikisha taasisi zote zinazohusika na mfumo huo ikiwa ni pamoja na sheria zinazosimamia taasisi hizo ili kuziondoa katika mazingira ya ubwetekaji, urasimu na mazingira yanayotoa mianya ya rushwa.

“Huwezi kuwa na mfumo bora na thabiti wa utoaji haki nchini kama taasisi zinazosimamia na kutoa haki nchini zitakuwa zimebweteka, zina urasimu na kuwa na sheria ambazo zinatoa mianya ya rushwa, ni jukumu lenu kuangalia taasisi husika na sheria zao, na msipofanya hivyo hamuwezi kufikia lengo la kuwa na mfumo bora na thabiti utakaotoa haki kwa watu” amesema.

Amesema ni wazi kuwa taasisi nyingi zinazohusika na mfumo wa haki jinai nchini bado zinakabiliwa na kasoro hizo na kuongeza kuwa ili kuondokana nazo ni lazima taasisi zinazohusika ziondokane na vitu hivyo.

Amesema kama vitu hivyo visipozingatiwa lengo la kupata mfumo bora na thabiti wa utoaji haki kwa wananchi haliwezi kufikiwa na hivyo kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa haki kwa wananchi.
Amewataka Washiriki kuangalia maeneo yote ambayo yanatoa mwanya wa kufanyika kwa vitendo vya kijinai ambavyo ni vya kutengenezwa na hivyo kuwakosesha wananchi haki kwa kuwa wahusika wa taasisi hizo wana mianya hiyo.

“Muangalie maeneo yote ambayo yanawapa mianya watendaji katika taasisi husika kutengeneza vitendo vya kihalifu na kuwarushia wananchi ambao mwisho wa siku wanakuwa wamekoseshwa haki zao kutokana na kukabiliwa na vitendo hivyo vya kihalifu ambavyo ni vya kutengenezwa,” amesema.

Amesema kushamiri kwa vitendo hivyo kunafanya kuanguka kwa mfumo wa haki jinai nchini ambako pia kunamaanisha kwamba taasisi zinazohusika na mfumo huo pia zinakuwa zimefeli.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo jijini Dodoma alipotembelea mkutano wa Wataalam wanaoshiriki katika majadiliano ya kuboresha mfumo wa haki jinai jinai nchini ili iweze kuimarisha utoaji haki nchini kwa wote na kwa wakati.

Wataalam hao ambao ni kundi la pili wanapitia mnyororo wa haki jinai na kubainisha changamoto katika mfumo na kupendekeza hatua za namna ya kutatua changamoto hizo na hivyo kuwa na mfumo mpya wa haki jinai ambao utazingatia utoaji haki kwa wananchi..

MCHEZA FILAMU WA MEXICO ATEMBELEA HIFADHI NNE ZA TAIFA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Muigizaji wa Tamthilia maarufu ya ESMERALDA kutoka nchini Mexico, aliyekuja nchini kwa mapumziko ya siku saba na watoto wake, wakati Waziri Mkuu akiwa mkoani Arusha kwenye ziara ya kikazi. Julai 23.2019. Tokea kushoto ni watoto wa muigizaji huyo, Carlo Collado (14) na Luciano Collado (15).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wafanyakazi wa hoteli ya The Retreat at Ngorongoro iliyoko wilayani Karatu, wakati akiwa mkoani Arusha kwenye ziara ya kikazi. Julai 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
………………..

*Zimo Ngorongoro, Serengeti, Manyara na Tarangire
*Ni Leticia Calderon, aliyeigiza filamu ya ESMERALDA

MUIGIZAJI maarufu wa filamu kutoka Mexico, Bi. Leticia Calderon (51) amesifia rasilmali ya hifadhi za wanyama ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Muigizaji huyo ambaye amefanya kazi hiyo kwa miaka 36, na ameigiza sinema maarufu ya ESMERALDA, yuko nchini kwa mapumziko ya siku saba kwenye hifadhi za wanyama za ukanda wa Kaskazini.

Akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi, Bi. Calderon amesema amevutiwa na uzuri wa hifadhi za Tanzania na idadi kubwa ya wanyama aliowaona kwenye hifadhi za Taifa za Tarangire, Manyara na Ngorongoro.

“Kwa miaka mingi nilikuwa natamani sana kuja Tanzania kuona wanyama. Tuliyoyaona yametufurahisha mimi pamoja na wanangu. Nchi yenu ina uzuri wa kustaajabisha. Watu wenu ni wema na wakarimu,” alisema Bi. Calderon.

“Ninafurahi kwamba ndoto yangu imetimia. Tulienda Tarangire, Manyara na Ngorongoro ma sasa tunajiandaa kwenda Serengeti. Tulipokuwa Ngorongoro, tuliona simba wanne, majike wawili na madume wawili. Tumefurahi sana na nikirudi nyumbani, nitawaonyesha picha marafiki zangu na kuwaalika waje kutembelea Tanzania,” alisema.

Bi. Calderon ambaye amefuatana na wanaye wawili Luciano Collado (15) na Carlo Collado (14) alisema wakimaliza mapumziko yao huko Serengeti watakwenda Masai-Mara kwa siku tatu na kisha wataelekea Paris, Ufaransa kumtembelea rafiki yake ambaye waliigiza filamu pamoja huko nyuma.

Bi. Calderon pia ameigiza tamthilia ndefu (soap operas) 29 katika jiji la Mexico City ambalo ni mji mkuu wa Mexico. Mbali ya Esmeralda, filamu nyingine maarufu ambazo ameigiza ni En Nombre del Amor (In the Name of Love); Amor Bravia (Valiat Love) na La Indomable (The Taming of the Shrew).

Waziri Mkuu alimshukuru mwanamama huyo na wanaye kwa kuichagua Tanzania kwa mapumziko yao na akawatakia heri katika safari yao ya mbugani.

Akizungumza na wafanyakazi wa hoteli ya The Retreat at Ngorongoro iliyoko Karatu ambako muigizaji huyo alikuwa amefikia, Waziri Mkuu aliwataka wafanyakazi wa hoteli hiyo na wengine walioko kwenye hifadhi za Taifa, wafanye kazi kwa bidii ili huduma zao ziwavutie watalii wengi zaidi.

“Tunampongeza mwenye hoteli kwa uwekezaji huu mkubwa lakini niwasihi wafanyakazi mchape kazi ili wageni wengi zaidi waweze kuvutiwa na huduma zenu,” alisema Waziri Mkuu.

“Sasa hivi tunapata watalii wengi na watu maarufu kama hawa, wamechagua kuja kupumzika Tanzania. Mheshimiwa Rais Magufuli ameshanunua ndege sita, nyingine mbili zinakuja, moja itawasili Oktoba, na nyingine Januari, mwakani. Na tayari kuna ndege tatu nyingine zimeagizwa. Lengo lake ni kuimarisha usafiri wa ndani kwa kutumia ndege,” alisema.

“Zamani ilikuwa ni vigumu sana kuja Tanzania moja kwa moja. Ili mtalii afike, ilibidi apitie nchi nyingine na huko akidakwa anaondokea hukohuko. Sasa hivi, akitoka kwao ataweza kuja Tanzania moja kwa moja, akitua KIA anakuja Karatu au Serengeti moja kwa moja,” alisema.

YANGA SC KUCHEZA NA KARIOBANGI SHARKS YA KENYA, SIKU YA MWANANCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Kuelekea Kilele cha Wiki ya wananchi Agosti 4 2019, Uongozi wa Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Kariobangi Sharks kutoka Nchini Kenya.

Mchezo huo maalumu unatarajiwa kupigwa kwenye kilele cha Siku ya Mwananchi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Makamu Mwenyekiti - Fredrick Mwakalebela amesema Wiki ya Mwananchi itaanza Julai 27 na kufanyika kwa uzinduzi ambapo itafanyika matukio mbalimbali ikiwemo kufanya shughuli mbalimbali za Kijamii pamoja na kuitangaza siku hiyo sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Mwakalebela amesema, wanacheza na Kariobang baada ya AS Vita ya DR Congo kuomba udhuru ya kuingiliwa na ratiba ya CAF baada ya kupokea barua hiyo wakafanya mazungumzo na Kariobang na kukubali kuja nchini kucheza mchezo huo wa kirafiki.

Kwa upande wa katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki hiyo ya Mwananchi, Deo Mutta alisema kuwa "Uzinduzi ya Wiki ya Mwananchi itaanza rasmi Julai 27, mwaka huu kwa baadhi ya wanachama wa Yanga kwenda Zanzibar kutembelea kaburi ya muhasisi wa Yanga, Abeid Amani Karume na baada ya hapo jioni tutacheza mchezo wa kirafiki wa wanachama.

Mutta ameeleza watarejea Dar siku inayofuata na kuanza kukusanya kijiji kwa kuanza kutembea na gari kubwa la wazi la GSM litakalokuwa na wasanii wa muziki na filamu.

"Gari hilo la wazi litaanzia safari zake Kutoka Makao Makuu ya Klabu na kupita Morocco, Mwenge, Bunju, Bagamoyo, Kiwangwa, Msata, Lugoba, Msoga na Mdaula na baadaye kwenda Morogoro na kurejea tena kwa kupitia njia ya Kimara naMbezi," alisema Mutta.

Awali Yanga walipanga kuadhimisha wiki ya mwananchi Julai 27 kutokana na muingiliano wa ratiba ya michuano ya kufuzu CHAN kati ya Tanzania na Kenya Julai 28 ratiba kubadilishwa na kuelekea Agosti 4 mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredirick Mwakalebela akitoa taarifa ya kubadilika kwa timu watakayocheza nayo mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4 mwaka huu baada ya timu ya awali As Vita kuomba udhuru kutokana na ratiba ya michuano ya kimataifa ya CAF iliyotoka mapema wiki hii.

Wakazi wa Dodoma Wafurahishwa Kuanza Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme Bonde la Mto Rufiji

MWENGE WA UHURU WATUA PWANI,KUTEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 40

$
0
0
.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mku wa Mkoa wa Pwani Muhandisi,Everist Ndikilo.(Picha na Emmanuel Massaka Mzichuzi Tv)
Mku wa Mkoa wa Pwani Muhandisi,Everist Ndikilo akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga.(Picha na Emmanuel Massaka Mzichuzi Tv)
Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga akizungumza na wananchi wa kata ya Mwandege waliojitokeza kuupokea mwenge wa uhuru leo.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally (katikati)akizungumza na wananchi kata ya Mwandege mkoa wa Pwani leo mara baada ya kufungua kiwanda cha kuchata samaki (ABAJUCO LTD) kulia Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga,na (kushoto)Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa waliojotokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally akiwa ameambatana na bviongozi mbalimbali wakikaguwa maenso mbalimbali ya kiwanda cha kuchata samaki (ABAJUCO LTD)

MBWAMAJI WAMPONGEZA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA KUFANIKISHA MRADI WA MAJI

$
0
0
Mkimbiza Mwenge akimtwisha na kumtua ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Gezaulole kama ishara ya kuzindua mradi wa maji Kisima cha Gezaulole. (Picha na Andrew Chale).

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Yohana Luhemeja akiwa kwenye eneo hilo la jengo la kisima.
…………………
Na Andrew Chale, Kigamboni
WANANCHI wa Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni wamempongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Yohana Luhemeja kwa juhudi zake za kusimamia maendeleo ikiwemo suala la upatikanaji wa maji safi na salama.

Wananchi hao wametoa pongeza hizo mapema jana Julai 23 wakati wa Mwenge wa Uhuru uliotembelea kukagua mradi huo ambao utasaidia wakazi zaidi ya 8000 Mtaa huo wa Mbwamaji, Somangila.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye tukio hilo la Mwenge wa uhuru uliotembelea kukagua mradi huo, Wananchi hao walieleza kuwa maendeleo hayana Chama na kwa hatua na juhudi za Mwenyekiti alizoahidi awali miaka kadhaa iliyopita zimeweza kutimia.

“Awali mradi huu ulikufa na hakukuwa na mtu mwenye kutaka kuonesha nia ya kuufufua, tunashukuru Mwenyekiti wa Serikali wetu licha ya kutoka upinzani alipoingia kushika nafasi hii alianza na suala la hiki kisima na kwa kushirikiana na kamati yake waliweza kuonesha juhudi na hatua zimechukuliwa na sasa kisima kimefufuliwa. Hizi ni juhudi kubwa tunawapongeza wote ikiwemo Dawasa na viongozi wa Halmashauri kwa pamoja kwa kumuunga mkono” alieleza Sagala Msumi mkazi wa Mbwamaji.

Nao baadhi ya Wanawake wa Mtaa huo akiwemo Ester Modest na Falhaty Mussa wameshukuru kwa hatua hiyo kwani kwa sasa kero ya maji itakuwa ni historia kwao ambapo walikuwa wakikumbwana na changamoto ya maji safi na salama ya matumizi ya nyumbani.

“Tumekuwa tukitumia maji ya visima ambavyo baadhi yake sio salama hivyo kukamilika kwa kisima hiki kitatusaidia sana tunamshukuru sana Mwenyekiti wetu na Kamati yake kwa ujumla”alieleza Bi. Ester Modest.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo Yohana Luhemeja ameeleza kuwa, mradi huo wa kisima hicho utaenda kusaidia Wananchi kwenye zaidi ya Kaya 8000 na kwa sasa tayari mabomba yanaendelea kutandikwa ardhini na mwezi Desemba mwaka huu maji yataanza rasmi.

“Kisima hiki ni cha muda mrefu na kwa sasa kimefufuliwa na kipo tayari kwa kuanza kazi kwani wananchi wameanza kusambaziwa mabomba pia mitaa mitatu itaenda kunufaika na maji haya kuanzia Mwezi Desemba mwaka huu” alisema Mwenyekiti huyo.

Yohana Luhemeja aliongeza kuwa: mradi huo wa kisima hicho awali ulikuwa wa Kijiji cha Gezaulole lakini ukafa na kubaki bustani pekee hata hivyo katika moja ya ahadi zake wakati wa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa aliahidi kufufua kisima hicho na kwa sasa ahadi imetimia huku akiwapongeza DAWASA

na Halmashauri ya Kigamboni kwa kuweza kumuunga mkono kwenye suala hilo la kukifufua na kwa sasa wananchi wa Gezaulole watapata maji ya uhakika.” Alimalizia Mwenyekiti huyo, Yohana Luhemeja.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru katika Wilaya hiyo ya Kigamboni umeweza kutembelea na kukagua miradi 5 yenye thamani ya Bilioni 14, ikiwemo kisima hicho cha Maji Gezaulole

HALMASHAURI YA GEITA MJINI YATOA MKOPO WA BILIONI 1.6 KWA VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU

$
0
0

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungmza kwenye mkutano kati ya wananchi na Mbunge kuhusu ahadi mbalimbali alizozitekeleza ikiwemo suala la utoaji mikopo wa shilingi bilioni 1.6 kwa vikundi mbalimbali wakiwemo vijana, wanawake na walemavu kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii kwenye mkutano uliofanyika katika kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita, Mhe.Mohamed Ali( wa pili kulia) pamoja na Diwani wa kata ya Ihanamiro, Joseph Lugaila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kabla Mhe. Kanyasu kuanza kuzungumza na wananchi wake katika kata ya Ihanamiro.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkuatano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza wakatik akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu ahadi alizozitekeleza kwa wananchi wake likiwemo suala la mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.
Baadhi ya Madiwani wa viti maalum walioshirki kwenye mkutano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza wakati akizungumza na wananchi wake katika kata ya Ihanamiro.
Baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza Mbunge wao wakati alipokuwa akizungyumza nao katika kata ya Ihanamiro.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita, Mohamed Ali akizungumza na wananchi wa kata ya Ihanamiro kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na utalii ambaye pia ni Mbunge wa Geita mjini kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.


Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa amekaa na wananchi wa kata ya Ihanamiro huku akiwa akiwa anazungumza nao kabla ya kikao cha ndani kuanza.
……………………….
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Halmashauri ya mji wa Geita hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu tayari imeshatoa mkopo wa Shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya wakinamama, vijana na walemavu kwa lengo la kutimiza adhima ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.
Amesema lengo la kutoa mkopo huo ni kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kuweza kuinua kipato cha wananchi kwa kunufaika na miradi mbalimbali na hatimae kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hayo ameyasema kwenye mkutano wakati akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi mbalimbali alizozitekeleza ikiwemo ya kutoa mkopo wa shilingi bilioni 1.6 kwa vikundi mbalimbali kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii katika mkutano huo uliofanyika katika kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita.
Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo miongoni mwa madiwani katika Halmashauri hiyo wameweza kutoa mkopo huo. Hata hivyo amesema kuwa mikopo hiyo itasaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi
Akizungumza katika mkutano huo,Mhe.Kanyasu amesema anajisika fahali ya kutoa mikopo hiyo kwa vikundi ikiwa ni moja ahadi alizozitimiza za kuhakikisha mwananchi wake wanajihusisha kwenye shughuli za kiuchumi ili kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa
Amesema kuwa kutokana na changamoto zilizoko katika taasisi za fedha, ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo serikali imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu.
Aidha amesema mikopo hiyo itawasaidia makundi hayo kuweza kuongeza mitaji na kutoa ajira ndani ya jamii.
Aidha, Mhe, Kanyasu amesema katika awamu ya pili ya utoaji mkopo wataongeza viwango vya mikopo kwenye vikundi ambapo kila kikundi kitakuwa na uwezo wa kukopeshwa hadi kufikia shilingi milioni 20 tofauti na ilivyokuwa awali
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Ihanamiro, Mhe. Joseph Lugaira amemueleza Mbunge huyo kuwa katika kata hiyo jumla ya vikundi 19 vimenufaika na mkopo huo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi.
Amesema vikundi hivyo vimekuwa vikifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo biashara pamoja na kilimo ambapo anaamini wataweza kupata faida pamoja na kurejesha mkopo huo na kukopa tena.
Naye Diwani wa viti maalum, Mhe. Suzana Mashala amewahimiza wanawake wasiogope kukopa kwani hawawezi kujiendeleza kiuchumi pasipo kukopa.
Vile vile, Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanawake waliokopa wajitahidi kurejesha mikopo hiyo mapema ili mikopo hiyo iweze kuwasaidia watu wengine lengo likiwa ni kuondokana na umasikini.
Kwa upande wake, Emalio Nyangabo ambaye ni kiongozi wa Kikundi cha Tuinuane, amesema walipokea mkopo ambao umewasaidia kuinuka kiuchumi, na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuachana na kujihususha na vitendo visivyofaa katika jamii
Naye, Godson Maduka ambaye ni miongoni mwa vijana walionufaika wa mkopo huo amesema mkopo huo umewasaidia vijana wengi kujiepusha kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na unywaji wa pombe kupita kiasi.

MLOGANZILA WAPATIWA MAFUNZO DHIDI YA MAJANGA YA MOTO.

$
0
0
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a
akielezea majanga ya moto yanavyotokea na namna ya kukabili.
Kamanda Shang’a akifundisha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa
kutumia blanket maalum ya kuzimia moto (fire blanket).
Kamanda Shang’a akielekeza namna ya kuzima moto kwa kutumia
kizimia moto aina ya poda kavu (dry powder fire extinguisher).
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mloganzila wakifanya zoezi
la kuzima moto mara baada ya kupatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi yamajanga ya moto.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene
(kushoto) akiwapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya motowatumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, kulia ni MkaguziMsaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a.
Watumishi wa Hospitali ya Mloganzila wakifuatilia mafunzo hayo.


Dar es salaam 24-07-2019

Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzoya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa lengo la kujikinga namajanga ya moto na kuhakikisha Tanzania inakua salama dhidi ya majanga yamoto.

Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo ni yanadharia na vitendo yametolewa na Jeshila Zimamoto na Uokoaji.Akizungumza katika mafunzo hayo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto naUokoaji Peter Mwambene amesema moja ya vitu vinavyomfanya mtu ashindwekupambana na moto ni uoga na kutokua na vifaa sahihi vya kupambana na motounapokua katika hatua za awali.

Hivyo mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa matumizi sahihi ya vifaa vya
kuzimia moto, kujua aina mbalimbali za moto na namna ya kukabili, kujua mbinuza kuzima moto pamoja na namna ya kujiokoa pindi moto unapotokea.
“Moto unapotokea mtu hushindwa kuukabili kutokana na uoga, unatakiwa ufanyeyafuatayo pindi unapogundua moto, piga king’ora, kengele au mayowe,ita Jeshi laZimamoto na Uokoaji kupitia namba 114, watu wasiojiweza wapewe kipaumbelekutoka eneo hatarishi, jaribu kuzima moto bila kuhatarisha usalama wako na watuwengine’’ amesema Mwambene.

Ametaja vyanzo vikuu vinavyoweza kusababisha majanga ya moto kuwa ni
matumizi ya vifaa vya umeme visivyokua na ubora, ajali, nguvu asilia (radi,
upepo,mkali, tetemeko la ardhi , milipuko ya Volkano).

BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha MUHAS wwakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwake ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana na Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe, wakwanza kushoto ni Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha MUHAS Prof. Said Aboud.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha MUHAS Prof. Eliangiringa Kaale, wakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwa Waziri Ummy ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na wamwisho ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Watumishi na Wanafunzi wa chuo cha MUHAS (hawapo kwenye picha) wakati alipofanya ziara ya kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho.
Wataalamu mbali mbali wa masuala ya tafiti pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakifuatilia hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika chuo cha MUHAS ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti

……………………………………………………

NA WAJMW-DSM
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo wakati wa kukagua na kufuatilia maendeleo ya ushirikiano kati ya nchi ya Ufaransa na Tanzania katika masuala ya utafiti mafunzo na utoaji wa huduma za Afya katika chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili.

Kwa kiasi kikubwa Waziri Ummy pamoja na Balozi huyo wameridhishwa kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wataalamu katika chuo hicho ikiwemo utafiti, mafunzo na utoaji wa huduma za afya.

“Binafsi tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na wataalamu wetu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, katika masuala ya utafiti tumeona kazi kubwa inayofanyika katika utafiti juu ya dawa za kuua wadudu”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema hakuna sheria nzuri za udhibiti wa dawa hizi nchini hivyo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Muhimbili na Serikali ya Ufaransa itaendelea kufanya utafiti na kuona jinsi gani itapunguza madhara ya utumiaji wa dawa za kuua wadudu kwa binadamu.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy amefurahi kuona ushirikiano ambao Serikali ya Ufaransa inaendelea kuutoa katika huduma za watu wenye tatizo la Seli nundu “Sickle Cell”.

“kwa Mujibu wa Tafiti tuna jumla ya watu 200,000 nchini ambao wana tatizo la seli nundu na watoto ambao wanazaliwa ni 11,000 kwahiyo tumejadiliana na Serikali ya Ufaransa kuona ni jinsi gani tunaweza kuboresha huduma za ugunduzi ili tuweze kuwatambua mapema watoto pale wanapozaliwa na tatizo hili na kuhakikisha huduma za matibabu zinapatikana ikiwepo dawa ya kupunguza maumivu inapatikana”. Amesema Waziri Ummy.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Ummy amemuomba Balozi Frederic kushawishi makampuni makubwa ya kutengeneza dawa kutoka Ufaransa yaweze kusaidia katika kuzalisha dawa ya kupunguza maumivu ya Seli nundu inapatikana kwa Watanzania wengi.

Wakulima tumieni Mbegu Zinazohimili Mabadiliko Ya tabia ya nchi

$
0
0
Daniel Ulimboka ni Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya teknolojia za kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.
Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho za teknolojia ya kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.


Na Vero Ignatus,Arusha.

Mbegu bora za mahindi aina ya Tumbili 419 kutoka Kampuni ya Mbegu ya Seedco ni mbegu ambazo zinahimili mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamekua yakisababisha uhaba wa mvua katika maeneo mengi nchini hivyo kumsaidia mkulima kupata mavuno mengi licha ya mabadiliko hayo. 

Daniel Ulimboka ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Seedco, akizungumza katika Maonyesho ya kilimo Teknolojia yaliyofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tari Seliani ,alisema wamefanya utafiti nana wamekuja na mbegu bora ambazo zinahimili hali ya ukame licha ya uhaba wa mvua bado zinaleta mavuno ya kutosha kwa mkulima.

"Tuna mbegu aina ya tumbili 419 ambayo inafanya vizuri sana hasa katika kipindi hiki ambacho hakuna mvua za kutosha wakulima bado wamekua wakipata mavuno na kufurahia kilimo" Alisema Daniel

Melchiory Temu Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha aliwataka watafiti kubuni teknolojia zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili wakulima waweze kupata mazao badala ya kupata hasara kutokana na mabadiliko hayo ambayo yamekua yakileta athari na kusababisha kushuka kwa uzalishaji.

Aidha aliwataka Wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuwaletea manufaa wakulima na taifa kwa ujumla.Gerald Masila ni Mkurugenzi wa Baraza la Nafaka Afrika Mashariki alisema kuwa wanafanya juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko ili waweze kupata faida ya kilimo chao na kujikwamua kiuchumi.

Yasinta Pius na Leskar Mollel ni wakulima waliofika katika maonyesho hayo Mollel wameiomba wadau kuzifikisha teknolojia hizo maeneo ya vijijini ili ziweze kuwanufaisha wakulima.

TICTS DONATION AT ILELA SECONDARY SCHOOL, MLELE, KATAVI REGION

$
0
0
 Mr. Donald Talawa, TICTS Corporate Affairs Director handing over 1,200 bags of cement and 1,200 pieces of iron sheet worth Tshs 56 million to Mrs Rachel Kasanda Mlele District Commissioner, to assist with the construction of a girl's hostel at Ilela secondary school. The hostel is planned to accommodate 200 girls as the school is located 11 kilometers from Inyonga town in Mlele district, Katavi region and has a total of 485 students.
 Mr. Donald Talawa, TICTS Corporate Affairs Director, addressing the students Ilela secondary school after handing over a donation of 1,200 bags of cement and 1,200 pieces of iron sheets to assist with the construction of a girl's hostel which will accommodate 200 girls. On the right are Mrs. Rachel Kasanda Mlele district commissioner, and Mr. Alexius Kagunze, Mlele district executive director. On the left is Mr. Deus Bundala, Mlele district council chairman.
Ilela secondary school students, teachers, and parents looking on during the handover ceremony of 1,200 bags of cement and 1,200 pieces of iron sheet donated by TICTS to assist with the construction of a girls hostel. The donation which is worth Tshs 56 million was received on behalf of District government by Mrs. Rachel Kasanda, Mlele District Commissioner, Mr. Alexius Kagunze, Mlele District Executive Director and Mr. Deus Bundala, Mlele District Council Chairman.

Leo kwenye ICC ni Man United dhidi ya Tottenham Hotspurs.

$
0
0
 
Mchana wa leo katika mchuano ya ICC Manchester United wanakutana na wenzao wa Ligi ya Uingereza majogoo wa jiji la London, Tottenham Hotspur mashabiki wategemee pambano la aina yake aisee.
Dimba la Hongkou jijini Shanghai ambalo linaweza kuchukua mashabiki 33,000 ndilo litakalowajibika kuhodhi mtanange huo Alhamisi ya leo.

Japokuwa ni wazi kwamba timu hizi zitachezesha wachezaji wasiokuwa na uzoefu sana na wasio na majina makubwa, mashabiki wa soka nchini China wako tayari kushuhudia mchezo huo.
Timu hizi mbili zinaingia katika mechi hiyo zikiwa zimetoka kupata ushindi katika mechi zao za kwanza, Manchester United waliifunga Inter Milan 1-0 huko Singapore Jumamosi iliyopita, huku Harry Kane akiifungia Spurs goli kutoka katikati ya uwanja na kuwapa ushindi wa 3-2 dhidi ya mabingwa wa Serie A Juventus.

Dhidi ya Juventus kocha wa Spurs Mauricio aliwapa nafasi wachezaji kama golikipa Paulo Gazzaniga, beki Anthony Georgiou na Japhet Tanganga, sambamba na kiungo Olivier Skipp na mshambuliaji mwenye miaka 17 Tory Parrott ambao walianza kwenye kikosi cha kwanza.
Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alienda mbali zaidi, kwa kuanza mchezo dhidi ya Inter kwa mchanganyiko wa wachezaji wachanga na wale wenye uzoefu, na baadaye kuwabadilisha wachezaji wote 11 katika kipindi cha pili.

Kwa muda mwingi ni mchezaji aliyenunuliwa kwa dau la paundi Milioni 50 Aaron Wan-Bissaka ndiye aliyevutia zaidi kwa upande wa United, ambaye ndiye alikuwa nyota wa mchezo katika mechi yake ya tatu tu tangu ajiunge na United akitokea Crystal Palace.

Scott McTominay alisema kwamba mlinzi huyo mwenye miaka 21 ameingia na kufiti vizuri kwenye kikosi cha United. “Yuko kama wachezaji ambao wamekuwepo hapa kwa muda mrefu, ni vizuri kuwa naye pia ni mchezaji mkubwa ambaye atakuwa wa muhimu sana kwenye timu yetu.
“Inachukua muda mrefu kwa mchezaji mpya kuzoea lakini huyu amezoa mara moja”

Mchezo huo utapigwa majira ya saa nane na nusu (8:30) Mchana wa leo huko Shanghai China. Kwa mashabiki wa soka nchini watautazama kupitia king’amuzi cha StarTimes kwenye chaneli ya ST World Football HD.

RAIS DKT MAGUFURI ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA MKOANI MOROGORO

WAZIRI HASUNGA AWAKUMBUSHA WANANCHI JIMBO LA VWAWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MKAAZI KWA AJILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Wakazi wa Kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakifatilia mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Ndg David Kafulila mara baada ya kuwasili mkoani humo kw aajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mhe Hasunga ametoa wito huo leo tarehe 24 Julai 2019 kwa wananchi wakati wa mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kijiji cha Ipapa, Ipanzya na Mpela katika kata ya Ipunga sambamba na vijiji vya Maronji, Shilanga na Hanseketwa vilivyopo katika kata ya Ihanda.

Alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuchagua wajumbe na wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa ni muhimu kwani ndio sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaowahusisha Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.Hivyo umuhimu wa wananchi kujiandikisha ni sehemu ya kufanya maamuzi ya viongozi watakaowawakilisha katika kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo ambazo kwa sehemu kubwa zimetajwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa barabara, Zahanati na upatikanaji wa maji, Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejikita katika dhamira ya utatuzi wa changamoto hizo kwa kipindi cha muda mfupi na malengo ya muda mrefu.

Mbele ya wananchi Mhe Hasunga amekiri kuwa kumekuwa na tatizo sugu na la muda mrefu kwenye sekta ya Kilimo la kuchlewa kwa pembejeo kuwafikia wakulima lakini tayari amekemea na kuagiza Taasisi zinazohusika kufikisha pembejeo kwa wakati.

Alisema kuwa Uongozi wa Taasisi itakayoshindwa kufikisha pembejeo kwa wakati na kukwamisha juhudi za serikali katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya wakulima utachukuliwa hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.

Kadhalika Mhe Hasunga amepiga marufuku kuzuia kwa kufunga mipaka ya biashara ya Mazao badala yake wananchi wametakiwa kuuza popote watakapo.

WANANCHI SINGIDA WANASEMA WAGOMBEA WA CCM WASIENDE KUFANYA KAMPENI WATAWACHAGUA TU

$
0
0
Wananchi wa Kijiji cha Mdughuyu Kata ya Kaugeri wilayani Ikungi mkoani Singida wakisukuma gari la Mbunge wao Elibariki Kingu wakati alipokuwa amewasili kijijini hapo jana kufanya mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mdughuyu iliyopo Kata ya Kaugeri wilayani Ikungi mkoani Singida wakati alipokuwa amewasili shuleni hapo jana kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo.Awali shule hiyo ilikuwa na madarasa mawili tu lakini sasa ina madarasa manne yaliyo jengwa kwa msaada wa mbunge huyo na Diwani.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akikagua ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Mdughuyu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akicheza pamoja na waimba kwaya wa Kijiji cha Mdughuyu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mdughuyu.
Wananchi wa Kijiji cha Mdughuyu wakiwa kwenye mkutano huo.
Wasanii wakitoa burudani
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimkabidhi fedha mmoja wa kiongozi wa Chadema aliyehamia CCM ili akanunue sare za chama.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimtwisha ndoo ya maji Mwanafunzi wa Kidato cha tatu wa Shule ya Sekondary ya Mwaru, Faidha Jumanne kutoka katika bomba lililo jengwa shuleni hapo kwa msaada wa mbunge huyo.
Watoto wa Kata ya Mwaru wakiwa wamepanda kwenye miti wakimsikiliza mbunge wao.
Diwani wa Kata ya Mwaru Iddi Makangale akihutubia.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Jimbo la Uchaguzi la Singida Magharibi wamesema wakati ukifika wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais, Mbunge na Madiwani wabaki nyumbani wasiende kufanya kampeni kwani wao watawachagua tu.

Wananchi hao waliyasema hayo kwa nyakati tofauti jana katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Elibariki Kingu yenye lengo la kuelezea kazi za miradi ya maendeleo zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongonzwa na Rais Dkt.John Magufuli na kusimamiwa na mbunge pamoja na madiwani.

"Mheshimiwa Mbunge wakati ukifika wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani mbaki nyumbani msije kufanya kampeni tutawachagua tu kwa kura nyingi kwani maendeleo mliyotuletea kwa miaka minne mliyokuwa madarakani ni makubwa mno" alisema mkazi mmoja wa Kijiji cha Mdughuyu Kata ya Kaugeri wilayani Ikungi mkoani Singida aliyejitambulisha kwa jina moja la Manyama.

Manyama alimwambia Kingu kwamba Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa ya kuwajengea barabara, shule na zahanati hivyo wanakila sababu ya kuwachagua wagombea watakao simamishwa kugombea nafasi za Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, Urais, Ubunge na Udiwani kupitia chama hicho.

Mkazi mwingine wa Kata ya Mwaru aliyejitambulisha kwa jina la Shija alisema wagombea wa CCM waondoe mashaka kabisa kwani watachaguliwa wote tena bila ya kuharibika kwa kura hata moja. Shija alisema Serikali inayoongonzwa na Rais Dkt.Johnn Magufuli imejibu maswali yao kwani imewapelekea maji, shule na zahanati vitu walivyokuwa wamevikosa kwa zaidi ya miaka 50.

Akihutubia katika mikutano iliyofanyika Mdughuyu na Kata ya Mwaru Kingu alisema miradi hiyo yote inafanyika baada ya Rais kuzuia matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi."Kwa kweli ninyi Wasukuma mnajua kuzaa mmetuletea huyu mwanaume Magufuli anafanya makubwa sana hapa nchini tuzidi kumuombea" alisema Kingu.

Kingu aliwaambia wananchi hao kuwa sasa wasubiri kupata umeme wa REA ambao tayari Serikali imetenga fedha za kuwawekea katika vijiji vyao kwa gharama ya sh.27,000 tu.Diwani wa Kata ya Mwaru Iddi Makangale alisema kazi inayofanywa na Rais Magufuli na Kingu ni ya kutukuka kwani inaonekana na wananchi wa kata hiyo wameiona kupitia miradi ya maendeleo iliyofanyika ndio maana wanasema wataichagua CCM kwa kura nyingi.

Katika mikutano hiyo baadhi ya wananchi waliokuwa ni wanachama wa Chadema pamoja na viongozi wao walijiunga CCM.

HASUNGA ATETA NA MADEREVA WA MALORI MKOANI SONGWE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikabidhi mchango wake kwa Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe Ndg Deogratius Agripa tarehe 24 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga leo tarehe 24 Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na madereva wa Malori mkoani Songwe ili kubaini changamoto zinazowakabili.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi katika eneo la Vwawa mkoani Songwe Mhe Hasunga amewahakikishia madereva hao kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga vyema katika ujenzi wa miundombinu ili kuimarisha usafirishaji.

Alisema kuwa serikali inaendelea na mpango wake wa uboreshaji wa miundombinu zikiwemo barabara kubwa na ndogo ili kuongeza ufanisi wa magari yanayotumia barabara hizo kumaliza safari zao katika hali ya usalama.

Kadhalika madereva hao wamempongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Vwawa kwa kuteuliwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa waziri katika sekta muhimu ya kilimo hapa nchini kwani jambo hilo limeongeza heshima.

Walisema kuwa imani iliyoonyeshwa na Rais Magufuli kwa wananchi wa Vwawa na Mkoa wa Songwe kwa ujumla ni matokeo ya imani ya wananchi hao waliyoionyesha kwa mbunge huyo baada ya kumchagua kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 2015.

Mhe Hasunga ameahidi kushirikiana na chama hicho cha madereva ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Sherehe Siku ya Urembo wa asili Tanzania

$
0
0


Sherehe za Siku ya Urembo wa asili Tanzania mwaka huu kufanyika wikiendi hii Jumamosi na jumapili July 27 & 28 Life Park Mwenge-Dar es salaam , HAKUNA KIINGILIO

Kutatolewa mafunzo ya kutengeneza vipodozi vya asili na visivyo na kemikali Bure

Kutakua na upimaji saratani ya titi na elimu ya kansa aina mbalimbali Bure.

Habari njema ni kuwa tutatoa kipaumbele kwa Wanawake Wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile Walemavu kushiriki katika maonesho hayo , watapewa banda bure la kuonesha kazi zao , pamoja na Wajasiriamali vijana.

Upande Burudani sasa, tutakua nae Malkia wa mipasho Bi khadija Kopa pamoja na mwimbaji Aneth Kushaba. Tutakua na appearance ya watu maarufu mbali mbali kama Mwasiti , Dina Marious , Grace matata, Rose ndauka na mchekeshaji Jaymond watakapata nafasi ya kuongea , itakuwepo fashion show kutoka kwa wasichana naturalist na watoto.

Mgeni rasmi atarajiwa kuwa Mh. Juliana shonza Naibu waziri wa Habari utamaduni sanaa na michezo.
kutakuwa na maonesho ya Wajasiriamali mbali mbali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zisizo na madhara kwa ngozi na nywele , Urembo , vyakula, michezo ya watoto , wauza vitabu na wajasiriamali wengine wengi watakuwepo.

Tamasha Hili linalofanyika kwa mara ya pili sasa limeandaliwa na kuratibiwa na Bi. Antu Mandoza Lengo ni kusaidia Jamii kuepukana na matumizi ya vipodozi hatarishi vinavyosababisha madhara makubwa kiafya kama vile Saratani na pia kuwapa Wanawake hasa Wasichana ujasiri wa kujiamini na kujipenda walivyo kwa manufaa ya kiafya na zaidi ya yote kuinua Wajasiriamali wadogo.

Wasichana 300 watakaofika wa kwanza watapata zawadi za pakiti za Pedi za Belle bure .

Jipende, Jiamini, Jithamini na jikubali vile ulivyo , kwani Urembo wa asili sio ushamba, nywele za Asili sio ushamba.

Kwa mawasiliano zaidi piga No: 0783324787 au 0655258737

Siku ya Urembo wa asili Tanzania Imeletwa kwenu Kwa udhamini wa Fern marketing , global piblishers, KUAMBIANA investment ,Life Park, Millard 
ayo, SnS na Efm

TCRA yaendelea na kampeni ya utoaji Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole Kilwa,mkoani Lindi

$
0
0
Wakazi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi ya TCRA Mabel Masasi amesema ni fursa kwa wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano. Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Masasi amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA."TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Masasi.
Wananchi wakipata huduma katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Wananchi wakipata huduma katika Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa huduma kwa mwananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Wananchi wakipata elimu katika Banda la TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika enoo la Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi.
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akizungumza  na Wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa alama vidole

NI MRADI WA UMEME WA MTO RUFIJI SIYO STIEGLER’S – WAZIRI KALEMANI

$
0
0
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Morogoro, kuhusu maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, unaotarajiwa kufanyika Julai 26, 2019.
 Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na waandishi wa habari wa Morogoro (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya hafla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji, unaotarajiwa kufanyika Julai 26, 2019.
 Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akikagua maandalizi hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, unaotarajiwa kufanyika Julai 26, 2019.


Na Veronica Simba – Pwani
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amewasihi watanzania kuwa wazalendo kwa kuacha kuuita mradi wa kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mto Rufiji kwa jina la Stiegler’s badala yake wauite kwa jina lake halisi la kizalendo.
Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti jana, Julai 24, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro na baadaye akiwa Rufiji mkoani Pwani mara baada ya kutembelea na kukagua maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo, unaotarajiwa kufanywa na Rais John Pombe Magufuli, kesho, Julai 26.
“Jina halisi ni Mradi wa Umeme wa Rufiji na siyo Stiegler’s kama ambavyo wengi wamekuwa wakiuita. Nawasihi watanzania kuenzi jina la utaifa la Rufiji,” alisisitiza Waziri.
Akizungumza katika maeneo hayo tajwa, Dkt. Kalemani alisema utekelezaji wa mradi husika, utaweka mazingira sahihi, yanayotabirika na imara katika kujenga uchumi wa viwanda.
Akifafanua, alisema hiyo ni kutokana na Sera na Dira ya Taifa ya kujenga uchumi wa viwanda, lakini pia kuinua maisha ya watanzania kutoka kima cha chini kwenda kima cha kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema, lengo kubwa la mradi husika; pamoja na mambo mengine, ni kuzalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu.
“Tumpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa umahiri mkubwa wa utekelezaji wa mradi huu. Kwa niaba ya Wizara ya Nishati, nataka kuwahakikishia watanzania kuwa mradi huu utatekelezeka kwa wakati na upo uwezekano wa kuokoa walau mwezi mmoja wa ukamilishaji wake kimkataba.”
Akizungumzia manufaa makubwa mengine ya mradi, alisema ni pamoja na ajira ambapo alieleza kuwa hadi sasa watanzania 600 wameajiriwa kwa shughuli za awali za ujenzi. Aliongeza kuwa, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia 6,000 na zaidi pindi mradi utakapofikia katika kilele cha ujenzi wake.
Waziri alieleza manufaa mengine kuwa ni uunganishaji wau meme katika maeneo yaliyo jirani na mradi ambapo alisema jumla ya vijiji 22 vya mikoa ya Morogoro na Pwani tayari vimeshanufaika na kwamba vijiji vingine 37 vya mikoa hiyo vitapatiwa umeme baada ya kujenga miundombinu ya kuusafirisha.
Vilevile alitaja manufaa mengine kuwa ni pamoja na kuwezesha kilimo cha umwagiliaji, uvuvi pamoja na kuwezesha uhifadhi wa mazingira kutokana na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya mkaa yanayosababisha ukatwaji wa miti.
Aliwaasa wananchi kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea eneo la mradi ili kujionea na kujifunza, kabla watalii kutoka nchi mbalimbali duniani hawajaanza kuja kutalii eneo hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe alimpongeza Waziri wa Nishati kwa jitihada ambazo Wizara imeendelea kufanya katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji.
Alisema mradi utaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro kama yalivyoelezwa na Waziri lakini pia akamhakikishia Dkt. Kalemani kuwa suala la ulinzi na usalama katika eneo la mradi limezingatiwa kwa uzito wa aina yake.
“Tumeongeza idadi ya askari Polisi ili kudhibiti kikamilifu tukio lolote la kihalifu endapo litajitokeza. Hata hivyo, hadi sasa hatujapata shida yoyote ya kiusalama,” alisema.
Mkutano wa Waziri na waandishi wa habari ulihudhuriwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt Hassan Abbas pamoja na wataalamu mbalimbali wa Wizara na TANESCO.

SHULE YA WATU WENYE ULEMAVU NA MAHITAJI MAALUMU YAJENGWA WILAYANI ARUMERU

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Zaidi ya shilingi bilion 2.8 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya secondary ya elimu maalumu katika eneo la chuo cha Patandi kilichopo Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya miundombinu wilayani Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mh, Jery Muro amesema kuwa fursa hiyo ni ya kwanza hapa nchini ambapo italeta manufaa kwa watu wenye mahitaji maalumu

Amesema kuwa licha ya kusaidia kitaleta kielelezo cha kuhakikisha watoto wenye ulemavu watapewa mtazamo mpya wa elimu kwa kuokoa watoto wenye changamoto na mahitaji maalumu kutoka sehemu mbalimbali 

Aidha ameseama kila mwezi serikali inatoa bilioni 23 kwa wastani kwa ajili ya ujenzi wa elimu na kugharamia sera ya elimu bure hapa nchini 

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya mahitaji maalumu Patandi Mwl. Janeth Molel ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kuwajali watu wenye mahitaji maalumu hasa kupitia elimu kwani hii itasaidia kupunguza ongezeko la watoto wa mtaani na hatiamye kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda

Amsesema kuwa,kwa sasa yamekamilika madarasa manane 8 na itachukua wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari wameshapata waalimu 5 kwa ajili ya kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itakuwa shule ya mfano hapa Tanzania.

Amewataka wazazi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu bali watumie fursa iliyojitokeza katika kuhakikisha wanawapatia elimu ambayo itawasaidia katika kujenga msingi mzuri wa maisha

Kwa upande wake mbunge wa Arumereru Mashariki John, Danielson Palanjo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha elimu inapewa kipaombele hasa kwa watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwa nao wana uwezo wa kulitumikia taifa

Amesema huduma ya elimu katika ambayo imeletwa wilayani hapo, italeta manuafaa kwa jamii na kuwa mfano kwa huiduma ambazo kila mtu atazifaidi kwa kuwa itakuwa tegemezi kwa kila mwananchi

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Bw. Emanuel Mkongo amesema wao kama halmashauri bwanasubiri kukabidhiwa madarasa na pia watahakikisha kila kitu kimekamilika ili kuweza kuruhusu wanafunzi kuingia madarasani ambapo nao wana mchango mkun=bwa katika kuhakikisha wanaungana na serikali kuendeleza watu wenye mahitaji maalumu 

Hata hivyo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na wanafunzi 120 wenye mahitaji maalumu bila ubaguzi na watapata huduma mabalimbali kulingana na uwezo wao 
Muonekano wa Bwalo la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu linalojengwa katika Shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi, Arumeru mkoani Arusha
Muonekano wa Jengo la Utawala la Shule ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo cha Ualimu Patandi.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images