Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKUU WA MKOA WA PWANI.

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 24 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi zaidi ya 35 maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 123.

RC Makonda amesema katika siku tano ambazo mwenge umekimbizwa Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 35 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano.

Aidha RC Makonda amewashukuru wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kwa siku zote walizokuwa Dar es salaam na kuwapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa walioonesha tangu siku mwenge ulipowasili.

Itakumbukwa kuwa mwenge wa Uhuru uliwasili Dar es salaam Julai 19 ukitokea mkoa wa mjini Magharibi na leo umekabidhiwa Mkoa wa Pwani tayari kwa kuendelea na shughuli ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo mkoani humo.


MAKAMBA AKABIDHI OFISI KWA GEORGE SIMBACHAWENE

$
0
0
 Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akikabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.  
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene akimsindikiza Mhe. January Makamba mara baada ya kukamilika kwa hafla ya makabidhiano ya Ofisi katika Ofisi ndogo Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima.


Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya Ofisi: Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene (kulia) Mhe. January Makamba na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima.



KATIBU WA NEC (CCM) ORGANAIZESHENI AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI SUMBAWANGA MJINI

$
0
0
Leo tarehe 24/07/2019 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Organaizesheni ndg Pereira A. Silima ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa CCM Mikoa ya Katavi na Rukwa amekutana na viongozi wa dini zote katika Wilaya ya Sumbawanga mjini Mkoani Rukwa kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kuwakumbusha mchango wao katika ujenzi wa Taifa. 

Katika Mkutano huo, ndg Pereira amewaomba kuendelea kulinda na kutetea amani ya nchi kwa kuwa wao ndiyo walezi muhimu katika jambo hilo na kuwakumbusha umuhimu wa kufundisha vijana wanaopoteza maadili ili kuwarudisha katika maadili stahiki ya nchi yetu ya Tanzania. Pamoja na hayo, Viongozi hao wamepata nafasi ya kutoa ushauri, kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majawabu kutoka kwa viongozi wa Chama na Serikali waliohudhuria. 

Ndg Pereira amewaomba kuendelea kuhubiri na kusimamia Umoja katika jamii zao, kutobaguana wala kutengana kwani binadamu wote ni sawa kama ambavyo imani ya Chama Cha Mapinduzi inasema katika Katiba yake na mwisho amewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanazozifanya katika kutoa mchango wa kulijenga Taifa. 


Leo tarehe 24/07/2019 ndg Pereira anaendelea na ziara yake ambapo anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa Mashina, Matawi na Kata za CCM katika Wilaya ya Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa

UBA GROUP SETS TO PROJECT AFRICAN ENTREPRENEURS TO THE GLOBAL MARKET VIA ITS SECURED ECOMMERCE PLATFORM - ‘UBA MARKETPLACE’:

$
0
0


‘UBA Marketplace’ is a secure online marketplace that allows businesses (small and medium scale) have an online store where they can advertise and sell their products or services across the continent and beyond. The UBA Marketplace is owned and managed by United Bank for Africa, a leading Pan-African financial institution in Africa with over 12 million customers. The Marketplace offer businesses personalized e-commerce site with their own unique store name to showcase their goods online thereby reaching potential customers across the globe irrespective of their physical locations.

As part of the process of enhancing the business network of African entrepreneurs, UBA Group also organizes an annual gathering of the ‘UBA Marketplace’ registered merchants, vendors, customers and other stakeholders for a two day exhibition in Nigeria. This year’s event is scheduled to hold at the iconic Transcorp Hilton Hotel, in Nigeria’s capital city of Abuja on the 26th and 27th of July 2019 with the theme “Empowering African Entrepreneurs”. This Africa’s largest gathering of business owners and entrepreneurs, promises to be the ideal forum for the enhancement of Tanzanian entrepreneurs business connections as over 5,000 visitors and over 100 registered exhibitors across 20 African countries, plus top private and public sector players will be gracing this annual historical event.

The UBA Market is available https://www.ubagroup.com/nigeria/market-place-africa/


On UBA Marketplace, there are different ways to sell your products such as listing on the marketplace, offering deals or listing as an auction. The E-commerce platform features categories such as electronics, fashion, jewelry, health and beauty, groceries, household goods, perfumes and more.

To further advance the course of entrepreneurs in the continent, 3 African leaders on day 2 of the event, will be engaging an audience of 5,000 people and watched around the globe through TEF forum, courtesy of the founder of TEF, Tony O. Elumelu, the Group Chairman of UBA Plc.

There will be plenary sessions which will highlight entertainment and music industries. Likewise, fashion, a big cultural and revenue attraction on the continent, will be showcased with the designs of 10 leading African labels. The event will provide a unique opportunity to shop, eat, play, network and party at the Africa’s largest fair of entrepreneurs as the African renowned artist “Wizkid” will be leading others; Niniola, DJ Cuppy, DJ Neptune to provide live music concert.

A good number of Tanzanian entrepreneurs are poised to grace the trade fair and will be showcasing Tanzanian products and culture. With this event, UBA seeks to touch base with small business owners while positively affecting the lives of entrepreneurs doing business in its countries of operations and beyond’.

Furthermore, this Forum presents the largest single annual opportunity for entrepreneurs and policy makers to interact directly and all sessions at the Forum have private sector and public sector leaders anchored in panel discussions, master classes, and a dynamic pitching competition that will engage an audience of start-up entrepreneurs, development institutions and policymakers.


The Managing Director of UBA Tanzania, Usman Isiaka explained various benefits as to why the entrepreneurs should embrace this golden business opportunity: UBA Marketplace reach wider audience through Internet penetration with increasing number of internet users and online shoppers; it is cost effective as it offers an effective low cost channel for SMEs in Tanzania to drive sales online through new customer acquisition; it leverages on the support of a trusted bank with over 12 million customers; customers will be able to create their store url to share with their buyers (example: Omary.ubamarketplace.com) where “Omary” is the store name; ability of entrepreneurs to auto post their products on Facebook and sell them from own business page; secure transaction using one of the highest Secure Socket Layer Encryption on the platform with a payment gateway which is Payment Card Industry Data Security Standard (PCI DSS) compliant and reliable logistics managed by DHL.

As part of its initiative of supporting African entrepreneurs, UBA Group has developed a Young Entrepreneurs Finance (YEF) Scheme which is being rolled out in phases across our 20 presence countries in Africa. The product provides existing TEF Alumni and other African Entrepreneurs above 18 years with qualifying business plans, opportunity to get up to $50,000.00 loan with 6 months deferred interest.




UBA Bank Tanzania Managing Director Usman Isiaka speaks in Dar es Salaam today during an event to ECOMMERCE PLATFORM - ‘UBA MARKETPLACE’ which gives an opportunity to allow businesses (small and medium scale) have an online store where they can advertise and sell their products or services across the continent and beyond 

PSPTB yaandaa mafunzo kwa Wataalamu wa Ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za Serikali na binafsi

$
0
0
Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeaanda mafunzo ya Siku mbili kwa  wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi kuhusu upendeleo wa makundi maalumu kwenye sheria ya ununuzi wa umma.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye amesema serikali imeweka kifungu maalumu kinachozitaka taasisi nunuzi kutengeneza asilimia 30 ya ya bajeti zao za manunuzi kwenda kwa wanawake, Vijana,wazee na watu wenye ulemavu.

Bilabaye amesema, sheria hiyo inalenga kuwaandaa vijana ambao hawana ajira, wajiweke kwenye Makundi maalumu ili kujipatia kazi za ununuzi kutoka kwenye taasisi za umma.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi, wajumbe wa tenda za zabuni na taasisi za umma zilizotajwa na sheria (Special Group Supporting Entity) ili kuzijengea uwezo wanamna bora ya kuyaandaa makundi maalumu ili yaweze kushiriki kwenye zabuni.
 Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma ( PPAA), Hamis Tika  akitoa mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yanayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa na mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa PSPTB. Kulia ni Afisa Mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa PSPTB, Shamim Mdee.
 Baadhi ya washiriki wakichangia mada kwenye mafunzo kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka taasisi za serikali na binafsi waliofika kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

 Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi, wajumbe wa tenda za zabuni na taasisi za umma wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka Taasisi za serikali na binafsi, wajumbe wa tenda za zabuni na taasisi za umma wakiwa kwenye picha ya pamoja.

MCHEZA FILAMU WA MEXICO ATEMBELEA HIFADHI NNE ZA TAIFA

$
0
0
*Zimo Ngorongoro, Serengeti, Manyara na Tarangire

*Ni Leticia Calderon, aliyeigiza filamu ya ESMERALDA

MUIGIZAJI maarufu wa filamu kutoka Mexico, Bi. Leticia Calderon (51) amesifia rasilmali ya hifadhi za wanyama ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Muigizaji huyo ambaye amefanya kazi hiyo kwa miaka 36, na ameigiza sinema maarufu ya ESMERALDA, yuko nchini kwa mapumziko ya siku saba kwenye hifadhi za wanyama za ukanda wa Kaskazini.

Akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi, Bi. Calderon amesema amevutiwa na uzuri wa hifadhi za Tanzania na idadi kubwa ya wanyama aliowaona kwenye hifadhi za Taifa za Tarangire, Manyara na Ngorongoro.

“Kwa miaka mingi nilikuwa natamani sana kuja Tanzania kuona wanyama. Tuliyoyaona yametufurahisha mimi pamoja na wanangu. Nchi yenu ina uzuri wa kustaajabisha. Watu wenu ni wema na wakarimu,” alisema Bi. Calderon.

“Ninafurahi kwamba ndoto yangu imetimia. Tulienda Tarangire, Manyara na Ngorongoro ma sasa tunajiandaa kwenda Serengeti. Tulipokuwa Ngorongoro, tuliona simba wanne, majike wawili na madume wawili. Tumefurahi sana na nikirudi nyumbani, nitawaonyesha picha marafiki zangu na kuwaalika waje kutembelea Tanzania,” alisema.

Bi. Calderon ambaye amefuatana na wanaye wawili Luciano Collado (15) na Carlo Collado (14) alisema wakimaliza mapumziko yao huko Serengeti watakwenda Masai-Mara kwa siku tatu na kisha wataelekea Paris, Ufaransa kumtembelea rafiki yake ambaye waliigiza filamu pamoja huko nyuma.

Bi. Calderon pia ameigiza tamthilia ndefu (soap operas) 29 katika jiji la Mexico City ambalo ni mji mkuu wa Mexico. Mbali ya Esmeralda, filamu nyingine maarufu ambazo ameigiza ni En Nombre del Amor (In the Name of Love); Amor Bravia (Valiat Love) na La Indomable (The Taming of the Shrew).

Waziri Mkuu alimshukuru mwanamama huyo na wanaye kwa kuichagua Tanzania kwa mapumziko yao na akawatakia heri katika safari yao ya mbugani.

Akizungumza na wafanyakazi wa hoteli ya The Retreat at Ngorongoro iliyoko Karatu ambako muigizaji huyo alikuwa amefikia, Waziri Mkuu aliwataka wafanyakazi wa hoteli hiyo na wengine walioko kwenye hifadhi za Taifa, wafanye kazi kwa bidii ili huduma zao ziwavutie watalii wengi zaidi.

“Tunampongeza mwenye hoteli kwa uwekezaji huu mkubwa lakini niwasihi wafanyakazi mchape kazi ili wageni wengi zaidi waweze kuvutiwa na huduma zenu,” alisema Waziri Mkuu.

“Sasa hivi tunapata watalii wengi na watu maarufu kama hawa, wamechagua kuja kupumzika Tanzania. Mheshimiwa Rais Magufuli ameshanunua ndege sita, nyingine mbili zinakuja, moja itawasili Oktoba, na nyingine Januari, mwakani. Na tayari kuna ndege tatu nyingine zimeagizwa. Lengo lake ni kuimarisha usafiri wa ndani kwa kutumia ndege,” alisema.

“Zamani ilikuwa ni vigumu sana kuja Tanzania moja kwa moja. Ili mtalii afike, ilibidi apitie nchi nyingine na huko akidakwa anaondokea hukohuko. Sasa hivi, akitoka kwao ataweza kuja Tanzania moja kwa moja, akitua KIA anakuja Karatu au Serengeti moja kwa moja,” alisema.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Muigizaji wa Tamthilia maarufu ya ESMERALDA kutoka nchini Mexico, aliyekuja nchini kwa mapumziko ya siku saba na watoto wake, wakati Waziri Mkuu akiwa mkoani Arusha kwenye ziara ya kikazi. Julai 23, 2019. Tokea kushoto ni watoto wa muigizaji huyo, Carlo Collado (14) na Luciano Collado (15). Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wafanyakazi wa hoteli ya The Retreat at Ngorongoro iliyoko wilayani Karatu, wakati akiwa mkoani Arusha kwenye ziara ya kikazi. Julai 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI UNAANZA KWAKO MWANANCHI- MZEE ALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali amesema kazi ya kutunza vyanzo vya maji sio ya serikali peke yake inaanza na wananchi wenyewe. Hayo ameyasema baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea chanzo cha maji Kulungu kinachopatikana kwenye Kijiji cha Mkwalia Kitumbo chenye uwezo wa kuzalisha maji Lita Milion 1.8 kwa siku.

Akitoa salamu za Mwenge, Mzee Mkongea amesema vyanzo vya maji vinatakiwa kutunzwa na wananchi wanatakiwa kuwa wa kwanza kwenye kuhakikisha wanavitunza kwa kuacha kufanya shughuli za kijamii pembezoni.

Mkongea amesema, ili vyanzo viweze kudumu na kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na cha baadae na kuendelea kutoa huduma ya maji safi,  wananchi hawana budi kupanda miti rafiki inayopenda maji na ufugaji wa nyuki.

Amesema, Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na utunzaji huu wa Chanzo cha Maji na amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa hatua kubwa waliyoifanya kwa kuzungushia uzio na kupanda miti wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wa Hlamashauri ya Mkuranga, Afisa Mazingira Herman Basisi amesema kuna vyanzo kumi na nne katika wilaya vinavyoendelea kutunzwa na kuhifadhiwa kwa kusimamia uoto wa asili usiharibike.

Amesema, kuanzia mwaka 2008 miti 500 ilipandwa aina ya michuja na mikorosho poro ambayo ni rafiki wa vyanzo vya maji ili kuitunza isivamiwe na shughuli za kibinadamu.

Chanzo cha maji Kulungu kinapeleka maji kwenye Tanki la Hospital lenye ujazo wa lita Laki moja na tisini na tano (195,000) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaa DAWASA wameanza ujenzi wa miundo mbinu ikiwamo kulaza mabomba na ujenzi wa tanki la maji la ujazo Lita Milioni 1.5

Pia, Mwenge wa Uhuru umezindua tanki la maji la ujazo wa lita laki moja (100,000) linalopatikana Mwanambaya litakalopokea maji kutoka kwenye chanzo cha Kulungu.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Mkongea Ali akipanda mti kwenye eneo la Chanzo cha maji Kulungu baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea eneo hilo leo Mkoa wa Pwani. Picha ya Chini akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga baada ya kupanda mti kwenye eneo hilo.

 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Mkongea Ali akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya Mkuranga Filberto Sanga baada ya  kutembekea chanzo cha Maji Kulungu Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2019 ulipotembelea kujionea uhifadhi wa vyanzo vya maji bila kuharibu uoto wa asili.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Mkongea Ali akiyagusa maji yanayotoka kwenye chanzo cha Maji Kulungu yanayotiririka kwa wingi.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Mkongea Ali akipokea taarifa ya uhifadhi wa chanzo cha maji Kulungu uliosomwa na Afisa Mazingira Herman Basisi(kulia) baada ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 kutembelea chanzo hicho leo Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Article 3

$
0
0
Na Mwandishi wetu- Sengerema, Mwanza
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) inaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa mpango wa elimu mbadala kwa wasichana na wanawake walio nje ya shule katika wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ili kuwajengea stadi za kuwawezesha kujitambua, kutambua mazingira yao na kuchukua hatua sahihi za kujikwamua kiuchumi.

Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa rasmi leo na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Ndugu Godwin Barongo.
Ndugu Barongo amefafanua kuwa, mpango huo umejikita katika maeneo matatu ya kujifunza ambayo ni stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), stadi za maisha na ujasiriamali zinazoendana na mahitaji ya jamii kwa sasa.

Aidha, ameeleza kuwa wasichana na wanawake hao watapata ujuzi wa kusindika karanga, matunda, mihogo, kutengeneza sabuni na batiki ili waweze kushiriki katika shughuli za kuwaingizia kipato hivyo kuboresha maisha yao na kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
Ameongeza kuwa, baada ya mafunzo, wasichana na wanawake hao wataunda na kusajili vikundi vyao ili kupata mikopo ya kujiendeleza inayotolewa na Halmashauri pamoja na asasi mbalimbali zilizojikita katika kukwamua kundi hilo.

Kaimu Mkurugenzi Barongo ameeleza kuwa elimu mbadala inaweza kubadili mtizamo na fikra za jamii juu ya mtoto wa kike kwa kumwezesha kuwa mtu mwenye mchango wa thamani katika maendeleo ya jamii.
Ndugu Barongo amewataka washiriki wa warsha hii kufatilia mafunzo hayo kwa umakini kwani yataweza pia kuwaongezea ujuzi na thamani katika utendaji wao kikazi.

Mpango wa Elimu mbadala unatekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Korea KOICA katika wilaya tatu za Sengerema, Ngorongoro na Kasulu. Mpango huu unalenga kuwafikia wasichana na wanawake 900 walio nje ya shule wenye umri kati ya miaka 14-24.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza,  Godwin Barongo, akifungua warsha ya Mafunzo ya Wawezeshaji wa mpango wa elimu kwa wasichana walio nje ya shule. Warsha hii ya siku nne imefunguliwa rasmi leo tarehe 23 Julai, 2019 na itaendelea hadi tarehe 26 Julai, 2019  ikilenga kuwajengea uwezo wawezeshaji wa mpango huu kuanzisha vituo vya mafunzo na kuendesha mafunzo kwa wasichana walio nje ya elimu rasmi katika wilaya ya Sengerema. Mradi huu unatekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kwa ufadhili wa Shirika la Korea KOICA katika wilaya tatu za Sengerema, Ngorongoro na Kasulu.
 Mwezeshaji wa mafunzo yakuwajengea uwezo  wakufunzi wa mpango wa kuwajengea uwezo wasichana walio nje ya mfumo  rasmi wa elimu katika wilaya ya Sengerema Bi. Leonia Kassamia akiwasilisha mada kwa wawezeshaji wa vituo vya mpango wa elimu mbadala ya wasichana walio nje ya shule, Warsha hii inalenga kuwajengea uwezo wawezeshaji wa mpango huu kuanzisha vituo vya mafunzo na kuendesha mafunzo.
 Washiriki wa warsha ya kujenga uwezo kwa wawezeshaji wa vituo vya mpango wa elimu mbadala ya wasichana walio nje ya shule wakiendelea kufuatilia maelekezo ya kuwajengea uwezo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Ndugu Godwin Barongo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kujenga uwezo kwa wawezeshaji wa vituo vya mpango wa elimu mbadala ya wasichana walio nje ya shule. (wa pili kutoka kushoto).

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA DHAHABU NA FEDHA ZILIZOKAMATWA NCHINI KENYA

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaidia kuhesabu vipande vya dhahabu huku akishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi aliyevipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa zilizokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kushuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa xzilizokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana kwa simu ya mkononi na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Jomo Kenyatta baada ya viongozi hao kushuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokewa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019. Kushoto ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akifuatiwa na Mhe Monica Juma. Kutoka kulia ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akifuatiwa na Profesa Kabudi na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali Mhe Biswalo Mgangha
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma baada ya kukabidhi Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019 PICHA NA IKULU

Serikali kutumia Rasilmali Watu wa Bahari wanaozalishwa nchini-Kwaadikwa

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Michuzi TV
Serikali imesema inaendelea  kujenga Miundumbinu mbalimbali ikiwemo vivuko ili kusaidia mabaharia wanaozalishwa nchini kuweza kutumika katika vivuko hivyo.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano- Ujenzi Elias Kwaandikwa wakati ya Maa kizungumza katika maadhimisho siku ya mabaharia Afrika yaliyofanyika katika Chuo cha Mabaharia Dar es Salaam (DMI) jijini Dar es Salaam.

Kwaandikwa amesema katika kuadhimisha siku ya mabaharia ni pamoja na kuangalia changamoto katika sekta katika vyombo vya Bahari.
Amesema Chuo kinazalisha wataalam wenye umahiri hivyo kinapunguzia serikali gharama ya kuchukua.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kuandikwa akipata Mkufuzi Msaidizi wa Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI) Elia Mahenge namna ya usalama katika Bahari katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Afrika yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Bahari Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kuandikwa akipata Mkufuzi Msaidizi wa Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam (DMI) Elia Mahenge namna ya usalama katika Bahari katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Afrika yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Bahari Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano-Ujenzi Elias Kuandikwa akipata maelezo kutoka Kwa Afisa Habari wa Wakala wa Meli nchini (TASAC) katika maadhimisho ya Siku Bahari Afrika yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Bahari Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kuandikwa akipata maelezo kutoka Kwa Mkufuzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam. Mhandisi Regina Mbilinyi kuhusiana na usalama katika Bahari namna ya kutumia bidhaa katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Afrika yaliyofanyika Viwanja vya Chuo cha Bahari Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kuandikwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Bahari Afrika yaliyofanyika Viwanja Chuo cha Bahari Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama cha Bahari Wanawake katika maadhimisho ya Siku ya Bahari Afrika.

WATANZANIA UINGEREZA WACHAGUA VIONGOZI WA JUMUIYA - ATUK

$
0
0
Hatimaye Watanzania Uingereza wamewachagua viongozi wa Jumuiya yetu ( Association of Tanzanians UK) yaani ATUK. Juni 2018 mkutano mkuu ulifanyika mjini Reading kufukuzia zoezi hili chini ya ulezi wa Balozi Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Mchecheto ulifukuzwa na wengi ila aliyewasha kiberiti alikuwa Joseph Warioba. Baada ya mwaka, siku nzima ya Mtanzania, Jumapili 30 Juni , 2019, ilitayarishwa na wanakamati wa ATUK – ambao baadhi walikuja kuwa viongozi wa Jumuiya. Hapa inaonyesha namna juhudi za Balozi kutuunganisha zilivyoambatanika na ari na hamasa za Watanzania.

Azma kuu ya Jumuiya hii si tu kukutanisha Watanzania kama sauti moja. Pia kuweka ngazi ya kusaidia , kujenga na kuwekeza nyumbani kutokea huku Majuu. Ni jambo la kuchangamkiwa sana. Watanzania toka sehemu mbalimbali za Uingereza walijieleza na kutafuta kura wakipigania nafasi za uenyekiti, katibu na mweka hazina na makaimu wao. Nusu ya kampeni hizi iliendelea mtndao wa WhatsApp na nusu ikakamilika ofisi za ubalozi wetu mtaa wa Bond Street, London, Jumapili 14 Julai, 2019. Uongozi mpya wa ATUK. Waliosimama nyuma. Toka kushoto, Mweka Hazina Msaidizi, Nelson Kampa, (Birmingham); Naibu Katibu, Frank Leo (Coventry), Mweka Hazina, Lucy Shigikile (London). Walioketi, toka kushoto,: Makamu Mwenyekiti, Zuhura Mkwawa (Leicester), Mwenyekiti , Martha Mpangile (London) na Katibu wake, Dk Imani Kondo... Kura ikipigwa ... Sam Mbogo mkazi Wales akijieleza kwa mintaarafu ya kupata kura  Toka kulia, Mwanahabari mkongwe na Mhariri wa The East African, Deo Kamuhanda, akiwa na Simon Mzuwanda (aliyepigania kijasiri wadhifa wa Uenyekiti na kushindwa ), Patricia Mpangala na Joe Wairoba, aliyefanya kazi kubwa kuisimamisha, ATUK.  Ukumbi umejazana Watanzania toka vitengo mbalimbali vya kisayansi, sanaa na akina mama wa TAWA.  Alex Masuguri mmmoja wa wasimamizi wakuu wa shughuli hii muhimu akitangaza matokeo. Wenzake ni kushoto, Batilda Tenga na kulia, Pauline Nzengula.  Mwenyekiti mpya, Martha Mpangile, ( pili kutoka kushoto) na Mweka Hazina , Lucy Shigikile (wa kwanza kulia ) wakipongezwa na kina mama wenzao. Picha na Habari za Freddy Macha 

BONDIA AFARIKI BAADA YA PAMBANO LAKE KUISHA

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Bondia kutoka nchini Urusi, Maxim Dadashev amefariki dunia katika Hospitali ya UM Prince George, Maryland, United States baada ya pambano lake na Bondia, Subriel Matias katika pambano lao lililomalizika kwenye raundi ya 11 siku ya Ijumaa Julai 20, 2019.

Imeelezwa kuwa Bondia huyo alipata majeraha katika kichwa chake, pamoja na kuvuja damu katika Ubongo wake.

Dadashev amefariki akiwa na umri wa miaka 28 akiwa ameshinda mapambano 13 tangu aanze mchezo wa ngumi.

Siku ya pambano lake hilo, Dadashev alishindwa kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya Mkufunzi wake, Buddy McGirt kuona hali yakushangaza katika Afya yake.

Shirikisho la Ngumi nchini Urushi limesema kuwa litafanya uchunguzi kuhusu Kifo cha Bondia huyo.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo , Umar Kremlev amesema huenda kukawa na upuuzwaji, ameongeza kuwa tumempoteza Maxim Dadashev. Ni kijana yetu mdogo sana, "Tupo tayari kumsaidia pamoja familia yake ikiwa na masuala ya kifedha"

MHANDISI AHUKUMIWA MIAKA MIWILI KWA KUUA BILA KUKUSUDIA

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji imemuhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani Mhandisi wa kampuni ya Best World Engineering, Novat Kaberwa, baada ya kukiri kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake, baada ya kurudi nyumbani saa tatu usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, huku akirudi akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoacha mume wake nyumbani.

Hukumu hiyo imesomwa leo Julai 24, na Msajili, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa ni kweli alimuua mke wake bila kukusudia.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, msajili Mazengo amesema,  amezingatia hoja zilizotolewa na mawakili wa utetezi kuwa mshtakiwa ameweza kuipunguzia gharama ma usumbufu  Mahakama kwa kukiri kosa na pia amezingatia mazingira ya tukio yalivyotokea, hivyo mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Mapema, Wakili wa utetezi, Venance Victor akishirikiana na Hashimu Mziray na Neema Kalabuha, waliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wao kwa sababu hilo ndiyo kosa lake la kwanza na pia ana watoto wawili ambao hawana mtu wa kuwaangalia.

Victor amedai mteja wao amekaa mahabusu tangu Julai 15, 2016, na kwa kipindi chote hicho, cha zaidi ya miaka mitatu amejifunza na amebadilika, ambapo hadi sasa hakuna kosa lolote alilolitenda akiwa gerezani na amebadilika na pia anajutia alichokitenda.


Aidha, wakili huyo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake huyo kwani amesomeshwa na Serikali mchepuo ya sayansi na bado serikali inamuhitaji aweze kukamilisha miradi ambayo alipewa na serikali.

" Kumbukumbu zinaonesha mshtakiwa pamoja na kampuni yake ya Best World Engineering ilikuwa imepewa mradi wa kurekebisha barabara ya Mikumi na Kilosa, hadi sasa Serikali imeshindwa kutekeleza kwa wakati kwa sababu mshtakiwa yupo ndani,"amedai Victor.

Wakili huyo, katika kumtetea mshtakiwa aliongeza kudai kuwa, katika tukio hilo hakuna silaha yoyote iliyotumika kuonesha alifanya kitendo hicho kwa kudhamilia na pia ukizingatia marehemu hakufia eneo la  tukio, alifia hospitali.

Naye wakili, Neema aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wao huyo kwani  watoto wawili mmoja ana miaka 19 na mwingine 11 alionao  hawana mtu wa kuwasaidia kwa sababu tayari wameshampoteza mama yao, tunaomba mshtakiwa arudi nyumbani kwake ili awatunze watoto wake wasijione yatima.

Mapema, wakili wa Serikali, Justus Ndibalema alimsomea mshtakiwa kosa la  lake linalomkabili akidai kuwa mshtakiwa alikuwa anaishi na mke wake Clara maeneo ya Keko mwanga wilayani Temeke jijini Darbes Salaam, na kwamba Januari 13,2016 majira ya jioni Clara alitembelewa na dada yake Veronika Munishi nyumbani kwake .

Amedai, akiwa hapo, Clara  alimfahamisha dada yake huyo kuwa mume wake Kaberwa majira ya mchana alimpiga wakati huo mshtakiwa hayupo hapo nyumbani.

Baada ya hapo Clara na Veronika walienda dukani kununua mafuta ya kupikia wakati wanarudi nyumbani walimkuta mshtakiwa amerudi  nyumbani ndipo ugomvi ulianza  baina yao ambapo wakati ugomvi ukiendelea Veronika alifanikiwa kukimbia wakati mshtakiwa akiendelea kumpiga mdogo wake Clara huku akimburuza na kumtoa nje ya geti ndipo marehemu akapiga kelele na majirani wakaja.

Kabelwa alipowaona majirani hao alikimbia ambapo walimchukua Clara na kumpeleka kituo cha Polisi na baadaye walimkimbiza katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Aliendelea kueleza kuwa, hali ya Clara iliendelea kuwa mbaya na ilipofika Januari 14,2016 alifariki na mwili wake ulipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai kuwa, Januari 18,2016 uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanyika na ripoti ilionyesha sababu ya kifo chake damu ilivia tumboni.

Ilidaiwa kuwa, Januari 15,2016 Kabelwa alikamatwa eneo la Kilosa mkoani Morogoro na kuletwa kituo cha Polisi Chang'ombe.
Mhandisi wa kampuni ya Best World, Nivat Kaberwa akitolewa mahakamani tayari kwa kwenda kuanza kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukiri shtaka la kumuua mke wake

WATU 14 KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAKOSA YA MTANDAO, UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WATU 14  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kusambaza ujumbe usiohitajika kwenye mitandaoni pamoja na utakatishaji fedha.

Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo jana ni David Simon, Michael Joseph, Omary Rajabu, Ramadhani Issah, Adolph Martine, Martine Maiko, Ajuaye Gerald.

Wengine ni Adam Christopher, Frank Magazi, Mathias Godfrey, Joseph Mabruck, John Mwambusa, Hamza Hassan , Amosi Mazwile.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Nancy Mushumbusi amedai mbele ya Hakimu Mwandamizi, Hamza Wanjahz kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2017 na Mei 31, mwaka huu, katika maeneo ya Sumbawanga mkoani Ruvuma na maeneo mengine tofauti ya Tanzania washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia washtakiwa kwa makusudi huku wakijua walisambaza taarifa za uongo kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia kompyuta kwa lengo la kudanganya umma.

Aidha, washitakiwa kwa pamoja walipanga kusambaza ujumbe usiohitajika kwenye mitandao  kwa njia ya kompyuta huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Katika shtaka la nne, washtakiwa wanadaiwa kujihusisha katika muamala unaohusu fedha taslimu  Sh. Milioni 11 wakati wakijua fedha hizo ni mazao ya kosa la jinai la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchum.

Wakili Mushumbusi alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo aliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu

MZEE MKONGEA AWASHUKIA WATENDAJI WA CHINI AMBAO WAMEKUWA WAKIHUJUMU MIRADI YA MAJ

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Mzee Mkongea Ali amewashukia baadhi ya watendaji wa chini ambao wamekuwa wakihujumu ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji huku akielekeza mtendaji atakaebainika kushiriki katika hujuma hizo awajibishwe.

Amewaagiza wakuu wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani ,kuwashukia wazima wazima watendaji wa aina hiyo wasiwaonee huruma .

Akizungumza katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani ,ukitokea jijini Dar es salaam ,Ali alisema haiwezekani serikali itekeleze mipango mizuri ili kuboresha sekta ya maji kisha atokee mtendaji wa chini kukwamisha juhudi hizo.

“Washukieni wazimawazima, Rais dk.John Magufuli alivyoingia madarakani aliahidi kutekeleza kuboresha sekta hiyo na kuleta maendeleo,na ana fanyakazi nzuri sasa watendaji wa chini wanaosuasua wana maana gani!!tushirikiane kuonyesha jitihada zinazofanywa na serikali”alieleza Ali.

Ali alielezea maji ni haki ya kila mtu, vyanzo vya maji vitunzwe kwa maslahi ya jamii.Pia kiongozi huyo za mwenge,aliwataka wananchi kushiriki katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vitongoji.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akipokea mwenge wa uhuru alisema ,ukiwa mkoani hapo utakimbizwa kwenye wilaya saba ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 itapitiwa yenye thamani ya zaidi ya sh.Bilioni 40.436.6, kati ya miradi hiyo miradi 61 itakaguliwa,17 itawekwa jiwe la msingi,9 itazinduliwa na 8 itafunguliwa.

Akizungumzia sekta ya maji, Ndikilo alibainisha kuwa asilimia 52 ya watu mkoani humo wanapata huduma ya maji safi na salama na wanaopata maji watu 790,000 sawa na asilimia 67 ya wakazi wote milioni 1.2.

Wakati huo huo ,mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema ,mwenge huo utatembelea miradi nane yenye thamani ya bilioni 5.177.
Mwenge wa Uhuru upo mkoani Pwani ukiwa ni mkoa wa 21 tangu ulipozinduliwa mkoani Njombe .

MHE HASUNGA AANZA ZIARA YA UKAGUZI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO JIMBONI VWAWA MKOANI SONGWE

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akifundisha somo la Hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019, (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza ulazima wa wanafunzi kusoma kwa bidii wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Iyula akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019. Mwingine Pichani ni Mwalimu Mkuu wa shule huyo Ndg Barnaba Mahembe.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa.

Akiwa katika kata ya Iyula Mhe Hasunga amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Iyula ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kujikwamua katika wimbi la ujinga kadhalika kiuchumi.

Waziri Hasunga amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa mshikamano na usimamizi madhubuti wa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa ambavyo vimefikia katika hatua nzuri ya kuanza kutumika.

“Mna bahati sana kusoma katika shule ambayo imetoa waziri wa kilimo hivyo ili kuwa na viongozi wengi katika Taifa hili mnapaswa kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika Takwimu za mkoa wetu” Alisema Mhe Hasunga

Pamoja na kuchangia shughuli za maendeleo katika jimbo hilo la Vwawa lakini pia amewataka wanafunzi hao kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuimarisha elimu na imeanza na utoaji wa elimu bure kuanzia ngazi ya awali mpaka sekondari.

Alisema kuwa lengo la Rais Magufuli kuruhusu elimu kuwa bure ni kutaka kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa urahisi kwa wanafunzi wote nchini ili hata wale waliokosa fursa kutokana na kipato duni cha wazazi waweze kuelimika na kuwa msaada katika familia zao na Taifa kwa ujumla.

Mhe Hasunga amesema kuwa pamoja na vitabu kuwasaidia wanafunzi kuelimika lakini wazazi na walimu ni sehemu ya uimara wa mafanikio ya wanafunzi katika ufaulu wao.

“Mimi nawapongeza sana ninyi wanafunzi kwani mna bahati kubwa kusoma katika kata zenu mnazoishi maana sisi wakati tunasoma tulikuwa tukienda umbali mrefu kutafuta elimu jambo ambalo lilikuwa likitukatisha tamaa ya kusoma” Alikaririwa Mhe hasunga

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga atakuwa na ziara ya siku tano katika jimbo hilo ambapo pamoja na mambo mengine atashirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo.

Wadau Waipongeza Serikali Maandalizi ya Mkutano wa SADC

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Serikali ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.

Katika kikao hicho wadau waliahidi kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha maandalizi ya montano huo.Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akieleza hatua ziizofikiwa katika maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019. 
Wadau wa Sekta binafsi na Serikali wakimsikiliza kwa makini, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani) alipokuwa akiongea.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu akichangia jambo katika kikao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye akizungumza 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wakiwasikiliza wadau walipokuwa wakizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness Kayola (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Caroline Chipeta wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha Sekta Binafsi na Serikali
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Bw. Abbas Tarimba naye akichangia mada katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bw. Albert Jonkergouw naye akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Juu na chini sehemu ya wadau kutoka Sekta Binafsi wakichangia mada kwenye Mkutano huo. 
Dkt. Mnyepe akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo.

Rais Magufuli amteua Bw. Edward Mpogolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida

JEZI YA YANGA MSIMU WA 2019/20 KUZINDULIWA RASMI KWENYE WIKI YA MWANANCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

UONGOZI wa Klabu ya Yanga Yanga kupitia Kamati za Utendaji na Hamasa kwa pamoja zimetangaza siku ya kuzinduliwa kwa jezi ya msimu wa 2019/20.

Hayo yamewekqa bayana leo na Katibu wa Hamasa wa Yanga Deo Mutta kutokana na wananchi kutaka kufahamu msimu ujao timu yao watavaa jezi gani.Mutta ameeleza kuwa aina ya jezi zitakazotumika msimu wa 2019/20 zitazinduliwa rasmi Wakati wa Wiki ya Mwananchi tarehe 01 Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa, anatoa tahadhari kwa umma kwani mpaka sasa hakuna Jezi ya aina yoyote ambayo imeshatangazwa kwenye Chombo cha aina yoyote ile kwa hadi sasa hivyo wanayanga Wote Epukeni kabisa kununua Jezi au kifaa cha aina yoyote chenye Nembo ya Yanga kwakuwa muuzaji na mnunuaji wote niwahujumu wa mali za Yanga Kisheria.

Aidha, Mutta amesema Klabu tayari ilishamtangaza Msambazaji aliyekasimiwa dhamana hii kisheria kupitia Zabuni ambaye ni kampuni ya GSM.

Mutta amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuepuka kushiriki kuihujumu nembo ya klabu yao kwa kununua bidhaa feki na kuikosesha Klabu mapato.
Katibu wa Hamasa wa Klabu ya Yanga Deo Mutta akielezea uzinduzi wa jezi za msimu wa 2019/20 utakaofanyika Agosti 01 mwaka huu na kuwatahadharisha wanachama kuacha kushiriki kuihujumu nembo ya Klabu.

JE UNAFAHAMU KUHUSU SADC

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images