Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

EAC Secretariat urges Partner Statesto increase risk and crisis communication measures to keep out Ebola Viral Disease

$
0
0
The confirmation of a fatal Ebola case in the Ituri province of the Democratic Republic of Congo (DRC) further increases the risk for the East African Community (EAC) region of the outbreak crossing the borders. The Ituri province is only 70 km from the South Sudanese border and even closer to the Ugandan border. 

The first three cases of Ebola in the EAC region were diagnosed in Uganda in June 2019 and triggered strong response measures by the Ugandan government. 

Trade is vibrant between DRC and the EAC regionand can exacerbate the spread of the Ebola Virus Disease (EVD) due to the high mobility of people and goods. In the light of the Public Health Emergency of International Concern declared by the World Health Organization,) Dr Michael Katende, acting Head of Health at the EAC Secretariat urges the Partner States to strongly engage the communities in the border regions and traders and trade associations in risk and crisis communication measures. 

“This is particularly important, as most of the border line is porous and difficult to control” says Katende, “informal and formal traders need to know the risk and be able to take informed decisions to minimise it and to actively take precautions.”

EAC Partner States have put in place precautionary measures to stop the spread of EVD into the EAC region. This includes vaccinating frontline health workers, screening all travellers at points of entry including airports and training the first responders in case of an outbreak. However, these measures might not be sufficient. Dr Michael Katende, acting Head of Health at the EAC Secretariat was especially concerned about EVD spreading into South Sudan with its still rather weak health system.

The EAC Secretariat calls upon the Partner States to increase risk and crisis communication by involving community, religious and other leaders and the media in public awareness raising. At the same time, the Secretariat calls upon traders and trade associations and those travelling across the border with DRC to take extra precaution, as the EVD threat is real:

· All people crossing the border should cooperate with immigration, health and security officials who areconducting screening at the pointsof entry and should strictly follow their advice.

· Frontline health workers and members of the affected communitiesshould accept to be vaccinated against EVD for their own protection and to help prevent the further spread of EVD.

· People in the affected regions should avoid unnecessary ‘body to body’ contact as this is the main way of disease transmission.

· The public should be vigilant and immediately inform the nearest health workers when spot a person with signs of EVD which are: fever, severe headache, body weakness, fatigue, diarrhea, vomiting, and unexplained haemorrhage (bleeding or bruising) from various body outlets like the nose, ears and mouth. This is particularly important along the “green border” where no screening measures are in place.

GAVANA SHILATU ATEMBELEA MAGHALA YA UFUTA

$
0
0


Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Ndugu Emmanuel Shilatu ametembelea Maghala ya vyama vya msingi yanayopokea ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ya Mihambwe na Michenjele yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ili kujionea utaratibu unaotumika.

*"Kazi ya Serikali ni kuwasimamia, kuona mambo yanaenda vyema. Nimekuja kuwatembelea ili kuona changamoto zilizopo ili kuzitatua na pia kujiridhisha na utaratibu unaotumika. Kwa taarifa mlizonipatia mnakiri malipo yanaenda vyema kwa ufuta uliouzwa tayari. Kwa upande wa Mnunuzi ajitahidi sana kuja kuuchukua mzigo wake kwa wakati mara tu afanyapo malipo."* alisisitiza Gavana Shilatu. 

Wakulima wanaendelea kujitokeza kwa wingi kuleta ufuta ghalani na hadi sasa minada minne mikubwa imefanyika ya kuuza ufuta ambapo 60% ya makusanyo yote mpaka sasa yameshauzwa na Wakulima wameshalipwa fedha zao.

MWANAHABARI ASHEHEREKEA 'BESDEI' KWA KUWAPA ZAWADI AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
Mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo Radio Faraja FM Stereo iliyopo Shinyanga Mjini Josephine Charles, amesheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi kwa wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.


Tukio hilo limefanyika leo Julai 23, 2019 ambapo ni siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kadhaa hapa duniani, ambapo ametembelea kwenye wodi ya wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji, wodi ambayo na yeye alijifungua mtoto wake Desemba 23,2018 kwa njia hiyo Christian Alex ambaye ametimiza miezi saba sasa. 

Zawadi alizotoa kwa akina mama hao ni taulo za kike, sabuni za kufulia, kuogeshea watoto pamoja na poda, huku akitoa wito kwa wanawake kujenga utamaduni wa kuhudhuria kliniki mapema na kwa wakati pamoja na kujifungulia watoto wao kwenye huduma za kiafya mahali ambapo ni salama kuliko majumbani. 

“Nimeamua kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa kwenye wodi hii ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji, wodi ambayo na mimi nilijifungua mtoto wangu kwa njia hii, ili kutoa hamasa kwa akina mama kupenda kujifugulia kwenye vituo vya afya na kuweza kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi mkoani Shinyanga,” amesema Charles.

 “Nasema haya kwa sababu siku ambayo mimi nililazwa kwenye wodi hii kwa ajili ya kujifungua mtoto wangu, alikuja mama mmoja akiwa hoi ambapo alipohojiwa ili kuchukuliwa taarifa zake aligundulika hakuwahi hata siku moja kuhudhuria kliniki, na alipozidiwa ndipo akaona aje hospitali kupatiwa huduma kitendo ambacho ni hatari kwa maisha yake,”amesema Charles. 

"Pia natoa wito kwa watu wengine ambao wana nafasi wasiwe wanasheherekea siku zao za kuzaliwa kwa kufanya vitu vya anasa, bali wawe wanatumia fursa hiyo kusaidia watu ambao wana uhitaji ili na wao wasione kama jamii inayowazunguka imewatenga",ameongezaCharles.

 Nao baadhi ya wazazi waliojifungua watoto wao kwa njia hiyo ya upasauaji akiwemo Dotto Jumanne na Winfrida Joseph ambao ni wakazi wa mkoani Shinyanga, wameshukuru kupewa zawadi hizo huku wakipongeza huduma ambayo wanapatiwa hospitalini hapo, ambapo wameweza kujifungua watoto wao salama. 

Kwa upande wake Daktari wa wodi hiyo ya akina mama wanaojifungua kwa njia ya upasuaji Dkt. Amoni Amoni, alitoa wito kwa wadau wa afya mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wakina mama juu ya umuhimu wa kuhudhulia Klinik mapema na kwa wakati pamoja na kujifungua watoto kwenye huduma za kiafya. Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mwandishi wa habari kutoka kituo cha matangazo Radio Faraja Shinyanga Mjini Josephine Charles akizungumza nje ya wodi ya wazazi ambao wamejifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, mara baada ya kumaliza kutoa zawadi kwao ikiwa ni siku ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa leo Julai 23,2019. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mwandishi wa habari wa kituo cha matangazo Radio Faraja Shinyanga Mjini Josephine Charles (kwanza kushoto) akiwa na wanafamilia, waandishi wa habari wa Radio Faraja pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakifungua zawadi kwa ajili ya kuwapatia wazazi. Josephine Charles akitoa zawadi kwa wazazi ambao wamejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa, wodi ambayo na yeye alijifungua mtoto wake kwa njia hiyo ya upasuaji. Josephine akiendelea kutoa zawadi. Josephine akiendelea kutoa zawadi kwa akina mama waliojifungua watoto kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa njia ya upasuaji. Josephine akiendelea kutoa zawadi. Josephine akiendelea kutoa zawadi kwa akina mama walijifungua watoto wao kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga , ikiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa. Zawadi zikiendelea kutolewa. Josephine akiendelea kutoa zawadi huku akiwa amembeba mtoto wake Christian Alex ambaye alijifungua kwenye wodi hiyo kwa njia ya upasuaji. Josephine akitoa pia zawadi kwa wauguzi wa wodi ya wazazi wanaojifungua kwa njia ya upasuaji kwa kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wazazi wanajifungua salama na kupunguza vifo vya uzazi. Mzazi Dotto Jumanne akishukuru zawadi hizo ambazo zimetolewa na Josephine Charles katika siku yake ya kuzaliwa. Daktari wa wodi ya akina mama ambao wanajifungua wa njia ya upasuaji Dkt Amon Amoni, akitoa wito kwa akina mama kuhudhuria kliniki mapema na kwa wakati pamoja na kujifungulia kwenye huduma za kiafya, sabambamba na elimu itolewe zaidi kwa akina mama juu ya umuhimu wa kujifungulia kwenye huduma za afya mahali ambapo ni salama. Dkt. Justice Minofu mwenye shati jekundu akimpatia zawadi ya siku yake ya kuzaliwa Josephine Charles ambaye amefikisha miaka kadhaa hapa duniani na kumtakia maisha mema na marefu. Awali Josephine Charles akiwa na wafanyakazi wenzake wa Radio Faraja wakiwasili kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wazazi ikiwa ni siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.Kushoto ni Steve Kanyefu akifuatiwa na Joseph Edward. Josephine Charles akipiga picha na familia yake, waandishi wa Radio Faraja na wauguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ,katika wodi ya wazazi waojifungua kwa njia ya upasuaji wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wazazi hao. Josephine Charles akipiga picha ya pamoja na familia yake, waandishi wa Radio Faraja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ,katika wodi ya wazazi waojifungua kwa njia ya upasuaji wakati wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wazazi hao. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

BURUNDI YAFURAHIA MRADI WA RELI YA SGR NA BANDARI KAVU KWALA - RUVU

$
0
0
Serikali ya Burundi imeufurahia mradi mkubwa wa reli ya SGR unaoendelea kufanyika nchini pamoja na ujio wa bandari kavu iliyopo eneo la kwala , ambapo nchi jirani ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda, Congo , Malawi , Zambia zitanufaika na usafirishaji wa mizigo . 

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe katika ziara iliyofanyika hivi karibuni na viongozi kutoka Burundi kutembelea miundombinu ya ujenzi wa reli pamoja na bandari kwa dhumuni la kuboresha usafirishaji wa mizigo inayopitia nchini kuelekea nchi jirani . 

Waziri Kamwelwe alisema kuwa asilimia 90 ya mzigo wa Birundi unapita katika bandari ya Dar es Salaam , pia alielezea upakuaji wa mizigo kwa Bandari ya Dar es Salaam unaongezeka kwa kasi hivyo lazima kuwe na miundombinu ya kutosha kuboresha usafirishaji wa mizigo. 

“ Sasa mageti matatu ya Bandari ya Dar es Salaam yamekamilika , na mkandarasi amekwenda kwenye gati la nne “ alisema Mhandisi Kamwelwe 

Waziri Isaac Kamwelwe alisema kuwa Ujenzi wa miundombinu kama reli ya SGR na bandari kavu utaongeza maendeleo ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa usafirishaji wa mizigo kutoka kwenye meli na kuwekwa moja kwa moja kwenye treni na kushushiwa bandari kavu ili kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam. 

“Sasa hivi tunaendelea kujenga miundombinu ya umeme na maji na pia watu wa TTCL wameshaleta optic fiber kuhakikisha swala la mtandao lipo sawa , ili tusicheleweshe maendeleo ya nchi “ alisema Mhandisi Kamwelwe

Naye Waziri anaeshugulikia masuala ya mahusiano Africa Mashariki Ndahayo Isabelle aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanya miradi mikubwa pamoja na mipango iliyopo baina ya Tanzania na Burundi katika usafirishaji wa mizigo ,pia aliongezea kua juhudi zilizofanyika katika mradi mkubwa wa SGR ni hatua nzuri katika kuleta maendeleo ya nchi .

“ Naipongeza sana Tanzania kwa mradi huu mkubwa wa Reli ambao unafanyika kwa kutumia fedha zenu “ Alisema Ndahayo Isabelle.Isabelle Alisema kua licha ya mradi huo kuja kurahisisha usafirishaji na biashara pia utaleta fursa ya ajira kwa wananchi na kuleta maendeleo ya Tanzania na Burundi .

“Kokote kwenye miundombinu mizuri, maendeleo hufuata “ alisema Ndahayo Isabelle.Vilevile Isabelle ameipongeza sana nchi ya Tanzania kwa kuwa na utaratibu wa kuweka ulinzi pamoja na ofisi ya kodi katika bandari zake .

UJIO WA UJUMBE WA JIMBO LA ZHEJIANG NI FURSA YA SEKTA YA UTALII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UJUMBE kutoka Jimbo la Zhejiang nchini China, uko nchini kusaka fursa za uwezekezaji, ikiwamo kukutana na wafanyabiashara wakubwa na wadau wa sekta ya Utalii watakaoweza kushirikiana nao katika uwekezaji maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara kati ya wageni hao na wafanyabiashara wa hapa nchini na wadau mbalimbali, Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa ujio huu wa wageni ni moja ya fursa waliyoipata mwaka jana kwenye ziara ya ya utangazaji baada ya kwenda Nchini China na kuingia makubaliano na kampuni ya Touch Roaf

Mdachi amesema, kampuni hiyo iliwaahidi kuleta watalii 10,000 na katika kundi la kwanza la utalii 343 wameshafika nchini na watalii wengine watafika nchini muda wowote kwa kutumia shirika la ndege la Air Tanzania baada ya makubaliano kati ya Touch Road na ATCL.

Amesema, wanaandaa ziara nyingine ya utangazaji nchini China na watatembelea mikoa yote ili kuongeza fursa ya kutangaza sekta ya utalii hususani upande wa malazi.

PMwenyekiti wa ujumbe huo, Ge Huijun, alisema hatua hiyo inatokana na ushirikiano wa China na Tanzania, ambao umezidi kuimarishwa siku za hivi karibuni.

Alisema jimbo la Zhejiang lenye zaidi ya wakazi milioni 57 lina fursa nyingi za biashara na uwekezaji, lakini pia lina wakazi wengi wenye uwezo wa kuwekeza nje ambao nao wanahitaji kujua fursa zilizopo Tanzania.

Amesema, jimbo lake lina watu wengi ambao wana kipato cha kati na wanahitaji kutalii, wameona Tanzania kuna fursa za utalii na wameanzisha kampeni maalumu ya ‘Travel to Tanzania’ yenye uwezo wa kuleta hadi watalii milioni saba kwa mwaka.

Alisema kupitia kampeni hiyo ya kuwataka watu wao wasafiri na kuja Tanzania kutalii, mapokeo yamekuwa mazuri na katika safari za awali zimetimiza zaidi ya asilimia 80 ya matarajio yao.
Picha ya pamoja ya ujumbe kutoka Jimbo Zhejiang na wafanyabishara na wadau wa sekta ya utaliu baada ya kumalizika kwa kongamano. 
Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumzia fursa waliyoipata kwenye sekta ya utalii kutokana na ziara iliyofanywa mwaka jana nchini China na kufanikisha kuingia mkataba na kampuni ya Touch Road ga kuleta watalii 10,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza kwa niaba ya wafanyabishara na kuzungumzia fursa zinazopatikana nchini Tanzania na kuwakaribisha wawekezaji hao kutumia nafasi hiyo kuja nchini kuwekeza. Hayo aliyasema wakati wa Kongamano la wafanyabishara na ujumbe kutoka jimbo la Zhejiang.
Mwenyekiti wa Ujumbe wa Jimbo la Zhejiang Nchini China Ge Huijun akielezea madhumuni ya safari yao nchini Tanzania, hatua hiyo imetokana na ushirikiano kati ya nchi ya China na Tanzania ulioimarika siku za hivi karibuni
Mwenyekiti wa Bodi wa Utalii Nchini (TTB) Jaji Thomas Miayo akizungumza wakati wa Kongamano la wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utalii na ujio wa ujumbe kutoka jimbo la Zhejiang utakaoboresha sekta ya utalii nchini

MANGULA ATOA ONYO KWA WANA CCM

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akiimbiwa wimbo maalumu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akihutubia juzi wilayani Ikungi mkoani Singida katika mkutano wa kuwapongeza Wana CCM wa Jimbo la Singida Mashariki kwa ushindi aliopata mgombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mdogo, Miraji Mtaturu ambaye alipita bila ya kupingwa. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akivikwa Skafu baada ya kuwasili wilayani Ikungi kwa ajili ya mkutano huo. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akisaini kwenye kitabu cha wageni Ofisi ya CCM Wilaya ya Ikungi . Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akizungumza na Viongozi wa CCM Mkoa wa Singida . Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akimtuza mmoja wa wasanii waliokuwa wakitoa burudani nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Wana CCM wakiwa kwenye mkutano huo wakiimba wimbo wa Taifa
Mbunge Mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akishukuru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba akizungumza katika mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Mkoa wa Singida. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza.
Mke wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akisalimia. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Jane Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akizungumza. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akimbidhi mbunge huyo mteule Miraji Mtaturu ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/2020 ikiwa ni ishara ya kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo la Singida Mashariki.



Na Dotto Mwaibale, Singida

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo hayo yakiwa na wawakilishi.

Mangula alitoa onyo hilo mwanzoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wana CCM wilayani Ikungi mkoani Singida katika mkutano wa kuwapongeza WanaCCM wa Jimbo la Singida Mashariki kwa ushindi aliopata mgombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mdogo, Miraji Mtaturu ambaye alipita bila ya kupingwa.

" Natoa maelekezo kuwa mtu yeyote atakayebainika kuanza kujipenyeza kwenye majimbo kwa nia ya kuanza kufanya kampeni ya kuwania nafasi hizo za uongozi hatutamuonea huruma tunamchukulia hatua kali za kinidhamu" alisema Mangula.

Alisema katika majimbo hayo kuna wawakilishi ambao muda wao wa miaka mitano bado haujaisha hivyo waachwe watekeleze ilani ya chama hicho kwa kuwapelekea wananchi maendeleo.

Alisema mwana CCM mwenye nia ya kutaka nafasi hizo anatakiwa kusubiri muda utakapo fika na wanachotakiwa sasa ni kwenda kwa wananchi kutangaza kazi za maendeleo zilizofanywa na viongozi waliopo madarakani na si kuanza kuwania majimbo hayo 

Mangula alitoa maagizo kwa wana chama hicho kuwa pindi watakapo muona mtu yeyote ameanza kujipenyeza katika majimbo hayo watoe taarifa ili mtu huyo aweze kuchukuliwa hatua kali kupitia kamati ya maadili.Katika hatua nyingine Mangula alielezea umuhimu wa kutoa elimu ya mpiga kura ili kila mtu aweze kujua haki yake ya kikatiba ya kupiga kura.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita katika baadhi ya maeneo watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache kutokana nakutokuwepo kwa elimu hiyo hivyo kujikuta kiongozi akichakuguliwa kwa kura chache akitolea mfano katika Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambapo idadi ya wapiga kura walikuwa ni asilimia 22 kati ya watu 100.

"Kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu hii walau mgombea aweze kupata zaidi ya asilimia 40 kuliko kuwa chini ya hapo" alisema Mangula.

Alisema mapambio, chereko chereko na watu wengi katika mikutano ya kampeni hayawezi kuongeza idadi ya wapiga kura kama hakuna elimu hiyo ambapo aliongelea umuhimu wa mabalozi wa nyumba kumi katika upigaji wa kura kuwa ni watu muhimu sana kwa vile wanawajua watu wao na kuweza kuwahamasisha kwenda kupiga kura.

Mangula akitumia hafla hiyo kumkabidhi mbunge huyo mteule Miraji Mtaturu ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/2020 ikiwa ni ishara ya kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo la Singida Mashariki.

Mtaturu akitoa shukurani kwa wana CCM hao alisema atashirikiana nao kwa dhati na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa na maendeleo ambayo waliyakosa kwa kipindi cha miaka tisa kwa kile alichoeleza halikuwa na mbunge sahihi wa kuwatumikia na sasa Singida imekuwa ni ya kijani.

Naibu Waziri Shonza awataka waalimu wa Michezo kupata mafunzo katika Chuo cha Michezo Malya.

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro Julai 23,2019.




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) Julai 23,2019 wakati wa alipofungua wa mashindano ya mpira wa wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Yahya Hassan akizungumzia mafanikio ya mpira wa Wavu katika mkoa wa Morogoro wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira huo kitaifa yanayofanyika mkoani hapo yaliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kulia) Julai 23,2019.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Taifa (TAVA) Bw.Benedito Kambanyuma akitoa historia ya Shirikisho hilo pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mchezo wa Wavu wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira huo kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro yaliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza Julai 23,2019.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Morogoro,viongozi wa Shirikisho la mpira wa Wavu Tanzania pamoja na baadhi ya wachezaji mara baada ya kufungua mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro Julai 23,2019.

…………………….
Na Shamimu Nyaki –WHUSM MOROGORO
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka waalimu wote wa michezo mbalimbali kujiunga na Chuo cha Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza ili kupata mafunzo ya muda mrefu na mfupi yanayotolewa chuoni hapo kwa lengo la kupata utaalamu mzuri wa kufundisha michezo hapa nchini.
Mhe.Shonza ameyasema hayo jana Mkoani Morogoro wakati alipofungua mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa ambapo amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na TAMISEMI zinashirikiana katika kukuza michezo hapa nchini ikiwemo kuhamasisha walimu wa michezo kuongeza ujuzi unaoendana na wakati katika kufundisha michezo.
“Wizara yetu kupitia Chuo cha Michezo Malya inatoa mafunzo ya cheti pamoja na astashahada kwa waalimu wa michezo na wanapomaliza wanakwenda kufundisha michezo katika shule zetu na kwa wanamichezo, hivyo nitoe rai kwa waamuzi pamoja na waalimu ambao hamjapata mafunzo hayo mjiunge na chuo hicho ili kupata ujuzi zaidi wa kufundisha michezo”alisema Mhe.Shonza.
Aidha Mhe.Shonza ameupongeza uongozi wa Shirikisho la mpira wa Wavu hapa nchini (TAVA) kwa jitihada kubwa uliofanya mpaka kufanikisha ushiriki wa timu za Taifa za Wavu wa ufukweni katika michuano ya Afrika iliyofanyika katika nchi za Kenya,Algeria,Misri pamoja na Cape verde ambapo zimeiletea heshima na kuitangaza vyema nchi.
Vilevile Mhe.Shonza ameihakikishia TAVA pamoja na Vyama vya Michezo vyote hapa nchini kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI kushiriki katika mashindano ya UMITASHUNTA NA UMISETA kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Bw.Benedito Kambanyuma amesema kuwa michuano ya klabu bingwa ya Taifa kwa wanaume na wanawake hufanyika kila mwaka tangu mwaka 2018 ambapo ilianzishwa ligi kupitia vyama vya Mikoa na washindi wanne wa kila mkoa hukutana katika michuano na kupata bingwa wa Taifa.
Bw.Kambanyuma ameongeza kuwa TAVA imeanzisha utaratibu wa kutambua vituo vyote vya timu za watoto ambazo zitasaidia kupatikana kwa vipaji vingi vya mchezo huo pamoja na kukuza kipato kwa wachezaji.
Naye Mchezaji wa kulipwa anayechezea nchini Rwanda Bw.Jackson Mmari ameeleza kuwa mchezo wa Wavu ni miongoni mwa michezo inayotoa ajira na kukuza kipato ambapo amewashauri vijana kujiunga na mchezo huo ili kupata ajira.
Mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili hapa nchini ambapo timu tisa ikiwemo Jeshi Stars wanaume na wanawake,Kigamboni wanawake,Dodoma Combine Wanaume,Star Girls na nyingine zitachuana kupata Klabu bingwa ya Taifa.

NDEGE ILIYOBEBA MADINI YA DHAHABU YA TANZANIA YALIYOKAMATWA KENYA YAWASILI NCHINI

$
0
0
 
Ndege maalum ya Jeshi la Kenya iliyobeba Dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa Kenya ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli atashuhudia makabidhiano hayo Ikulu Dar es Salaam kutoka kwa Mjumbe Malalum wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata.Picha na Ikulu

Watanzania changamkieni Fursa za Mkutano wa SADC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yatangaza uchaguzi mdogo wa Kata 13

$
0
0
Taarifa kwa umma iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Mbarouk Salim Mbarouk Mjini Babati, Mkoani Manyara leo (tarehe 24.07.2019) imesema kwamba fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya tarehe 29 Julai mpaka tarehe 03 Agosti 2019.

Jaji Mbarouk amesema kwamba uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 03 Agosti 2019 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Agosti 2019 mpaka tarehe 16 Agosti 2019.

Alizitaja kata zenye uchaguzi na halmashauri zake kwenye mabano kwamba ni pamoja na Laroi, Lemanyata na Likiding’a (Wilaya ya Arusha), Kimokouwa (Wilaya ya Longido), Kwembe (Manispaa ya Ubungo), Izigo (Wilaya ya Muleba), Mahida (Wilaya ya Rombo).

Nyingine ni pamoja na Makanya (Wilaya ya Same), Barikiwa (Wilaya ya Liwale), Kikeo (Wilaya ya Mvomero), Biro (Wilaya ya Malinyi), Myangayanga (Mji wa Mbinga) na Kapenta (Wilaya ya Sumbawanga).

Jaji Mbarouk amesema Tume imetangaza nafasi hizo kuwa wazi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata Kumi na tatu (13) zilizopo katika Halmashauri Kumi na moja (11) na Mikoa Nane (8) ya Tanzania Bara.

Amesema nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo Vifo, Kujiuzulu na Uamuzi wa Mahakama.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu Umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo Kumi na tatu (13),” Jaji Mbarouk alisema.

Kwa taarifa hiyo, Jaji Mbarouk amesema Tume inavialika Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika Uchaguzi huo.

“Tume inachukua fursa hii kuviasa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo,” alisema.

RAIS DKT MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UMEME RUFIJI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza na wanahabari kuwaelimisha juu ya uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa umeme wa Rufiji unaotarajiiwa kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli Julai 26, 2019. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wanahabari katika ofisi za Mkoa wa Morogoro kuwaelezea juu ya uzinduzi wa mradi wa Umeme wa Rufiji unaotarajia kuzinduliwa July 26, 2019 na Mheshimiwa Raise Dkt John Magufuli. Pembeni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe na kulia ni msemaji wa serikali Dkt Hassan Abas. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.  

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa kuzalisha na kufua umeme katika maporomoko ya maji ya Rufiji unaotarajiwa kuzalisha umeme wa mega wati 2115.

 Akizungumza na wanahabari mkoani Morogoro juu ya ujio wa Rais Dkt John Magufuli, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi linarajiwa kufanyika Julai 26 mwaka huu ambapo afafanua uwekaji wa jiwe hilo utakuwa chachu ya kuongeza kasi ya ujezi mradi huo ambao kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia kumi na tano kwa kipindi cha miezi nane. 

 Waziri Kalemani ameongeza kuwa miongoni mwa fursa za moja kwa moja ambazo zimepatika tangu kuanza kwa mradi huo ni pamoja na upatikanaji wa ajira kwa Watanzania sambamba na uwekaji wa umeme katika baadhi ya vijiji vya karibu na mradi kutoka katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. 

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Stephen Kebwe amewaomba wananchi kujitokeza na kuendelea kulinda wale watakaojitokeza kuhujumu miundo mbinu huku wakichangamkia fursa ya kuwekeza maeneo husika. "Niwaombe wakazi wa Mkoa wa Morogoro na Pwani tujitokeze kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa umeme utakaokuwa ni hisitoria ya pekee," amesema.

WAZIRI LUGOLA AONGOZA KIKAO CHA TUME YA UTUMISHI YA POLISI, UHAMIAJI NA MAGEREZA JIJINI DODOMA, LEO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Wajumbe  wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza wakati wa kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara jijini Dodoma, leo. 

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Polisi, Uhamiaji na Magereza katika kikao cha kujadili utendaji wa vyombo vilivyopo chini ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika Ukumbi wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuapisha Afisa Utumishi wa Wizara hiyo, Andrew Kiangi, kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo. Kulia (aliyekaa) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. 

Vijana wanaokwenda kwenye mashindano ya michezo Norway waagwa Dodoma

$
0
0

Na Charles James, MICHUZI TV

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na Taasisi binary katika kukuza na kuendelea vipaji vya watoto mashuleni ili kuinua sekta ya Michezo nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe Edward Mpogolo wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi wanne wa kituo cha Michezo cha Fountain Gate wanaokwenda nchini Norway kushiriki mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 10 hadi 19.

Mhe Mpogolo amesema wao kama Serikali ya Wilaya ya Dodoma wanathamini mchango mkubwa unaofanywa na Fountain Gate katika kukuza michezo kwa vijana wadogo ambao watakuja kuwa msaada mkubwa kwa Taifa Siku zijazo.

" Sisi kama Wilaya ya Dodoma tunajivunia kazi kubwa sana inayofanywa na wenzetu wa Fountain Gate, wamekua na mchango usiyotiliwa shaka katika ujenzi wa mchezo. Ni lazima kama Wilaya tuwaunge mkono na tayari tumeshawapa eneo kubwa zaidi kwa ajili ya kujenga akademi kubwa yenye kubeba vijana wengi zaidi.

" Chini ya Rais Magufuli kila mtu amejionea namna ambavyo Serikali imewekeza nguvu kubwa kwenye michezo, na hii ni kwa sababu tunaamini sekta hii inatoa ajira kwa kundi kubwa la vijana lakini ni sekta ambayo inatumika kutangaza Nchi yetu," amesema Mhe Mpogolo.

Aidha DAS Mpogolo amewataka vijana hao wanaokwenda kushiriki mashindano hayo kutumia fursa hiyo kutangaza Nchi pamoja na vivutio vinavyopatikana ikiwemo Mbuga za Wanyama na Mlima Kilimanjaro.

Amewataka kuonesha uzalendo, nidhamu na kutokata tamaa wanapokua kwenye mashindano yao kwani watanzania wako nyuma yao wakiwaombea ili wafanye vizuri na kuiletea Nchi sifa.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Fountain Gate, Japhet Makau ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa namna ambavyo imekua ikiwapa sapoti pamoja katika kuhakikisha vijana wenye vipaji wanalelewa katika mazingira yenye kukuza vipaji vyao.

Wanafunzi waliochaguliwa kushiriki michezo michuano hiyo ni Abiel Renatus Tarimo, Enos Boniface Semela, Brown Vicent Meshack na Abduraziz Beberwa Ahmed na wataambatana na mwalimu mlezi kutoka Fountain Gate Dodoma Sekondari, Lespicius Mwelinde France.

Nafasi hii ni muhimu kwa vijana kuonyesha vipaji vyao na inaweza kuwawezesha kupata 'scholarship' kwenye shule za nje ambazo zinaendeleza soka la vijana.Vijana hawa kutoka Fountain Gate Academy wataungana na vijana wa kituo cha Magnet cha jijini Dar es Salaam kuunda Timu ya Tanzania.

Norway CUP ni mashindano makubwa ya vijana yanayoongoza duniani kwa kuwaleta vijana kutoka pande zote za dunia pamoja. Hadi sasa nchi Zaidi ya 127 duniani na maelfu ya vijana wamepata nafasi ya kishiriki mashindano haya.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Edward Mpogolo akiwa na vijana wa Taasisi ya Fountain Gate wanaoelekea Nchini Norway kushiriki mashindano ya vijana chini ya miaka 19 na miaka 10.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanne wa Taasisi ya Fountain Gate wanaoelekea Nchini Norway kushiriki mashindano ya vijana.

NDALICHAKO: NIMERIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI WA SHULE ALIYOSOMA BABA WA TAIFA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amekagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa shule ya msingi Mwisenge na kuridhishwa na kasi na ubora wa kazi ya ukarabati inayoendelea ambao umefikia asilimia 60.

Ukarabati wa Shule ya Mwisenge ambayo alisoma baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ulianza kufanyika baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuitembelea na kuagiza ikarabatiwe na kujengewa ukuta.

Akizungumza akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo mradi huo amesema ameridhishwa na kasi hiyo ya ujenzi huo ambao unahusisha ukarabati wa majengo ya kale, ukarabati wa madarasa, mabweni, ujenzi wa madarasa na mabweni mapya, ujenzi wa uzio kuzunguka shule hiyo, ukarabati wa mnara wa kumbukumbu pamoja na uboreshajii wa mazingira ya nje. 

Mradi huo unaogharimu kiasi cha sh Milioni 706 ambazo zimetolewa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia unatarajiwa ulianza Mwezi April na utakamilika na kukabidhiwa mwezi Septemba mwaka huu.

“Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa mpaka sasa na viwango vya ujenzi wa madarasa na mabweni nao ni imara, hata ujenzi wa ukuta unafanyika vizuri, kuta za mabweni ni ndefu na zitawafanya watoto wakiwa ndani wapate hewa vizuri”alisema Profesa Ndalichako.

Shule hiyo awali ilikuwa haina ukuta kabisa hali ambayo ilisababisha mazingira kuwa hatarishi kwa watoto hasa wenje ulemavu wa Ngozi. Ukuta huo umeshajengwa kuzunguka shule yote.

Katika hatua ingine ilionekana ukarabati wa baadhi ya majengo ya kihistoria katika shule hiyo ambapo moja ya jengo linalengwa kuwa zahanati itakayotumika kwa ajili ya wanafunzi umesimama. Akitoa taarifa ya ujenzi Mkuu wa Shule hiyo.... amesema majengo hayo yalisimama kutokana na Idara ya Mambo ya Kale kutowasilisha maoendejezo yao baafa ya kufanya tathmini.

Waziri Ndalichako amewataka watalaam hao kufika mara moja ili kutoa muongozo unaohitajika kuwezesha kukamilisha ukarabati wa majengo hayo kwa wakati.

“Ni vizuri ndugu zetu wa Mambo ya Kale wafike mara moja ili kutoa muongoza wa namna bora wa kufanya ukarabati wa majengo haya ya kihistoria yanapaswa kukarabatiwa kuwezesha ujenzi huo kukamilika mapema kuwezesha wanafunzi kupata fursa ya kuyatumia, kwani kuendelea kuchelewesha taarifa hiyo ni kukwamisha utekelezaji wa mradi.

Prof. Ndalichako amesema lengo la wizara ni kuona shule hiyo inakamilika mapema ili kutimiza maagizo aliyoyatoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jonh Pombe Magufuli ya kutaka shule hiyo ikarabatiwe iwe na hadhi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuweka kumbukumbu nzuri ya shule aliyosoma.

Ndalichako ameshauri wajitahidi hiyo ikamilike mapema ikiwezekana kabla ya tarehe 14 Oktoba, siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa ili iwe sehemu ya maadhimisho hayo.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Musoma , Dkt. Vicent Anney alimweleza waziri kuwa baadhi ya majengo hayajakamilika kutokana na kusimamishwa kwa ukarabati wa majengo hayo ya kihisitoria katika shule hiyo na Ofisi ya Mambo ya Kale yenye jukumu la kutoa muongozo wa namna gani ukarabati unapaswa kufanywa, ingawa toka kusimamishwa wataalam hao bado hawajafika kutoa maelekezo yeyote yale na tayari wameshawaandikia barua ya kuwakumbusha.
 
“Lengo letu ni kuhakikisha ifikapo Oktaba 30 ukarabati huu uwe yamekamilika kabisa, lakini changamoto iliyopo sasa ni kukwama kwa ukarabati wa baadhi ya majengo ya kihistoria ambayo wenzetu wa mambo ya kale waliagiza ukarabati wake usimame mpaka watakapofika na kutoa maelekezo ya namna gani ufanyike lakini mpaka sasa hakuna mtaalam yeyote aliyefika pamoja na kuwaandikia barua, Amesema Dkt. Anney.

Dkt. Anney ameishukuru wizara kwa kuipatia Wilaya ya Musoma fedha za kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea ikiwemo shilingi milioni 152 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za udhibiti ubora wa shule, ukarabati wa shule ya sekondari ya ufundi musoma ambayo imewekewa mitambo pamoja na vifaa vya kufundishia iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.2.

WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR (ZFDA) WAPIGA MARUFUKU CHOKLET NA JUISI

$
0
0
Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula Mohamed Shadhili Shauri akielezea jitihada wanazochukuwa kuhakikisha bidhaa hiyo inatoka sokoni.
Muandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali katika Mkutano huo.Picha na Makame Mshenga


Na Faki Mjaka

Wazazi na Walenzi nchini wametakiwa kuepuka kuwanunulia Watoto wao bidhaa aina ya Choklet zilizotengenezwa mfano wa Bomba ya Sindano kutokana na kuingizwa nchi kimagendo bila kuthibitishwa ubora na usala wake kwa watumiaji.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula (ZFDA) Dr. Khamis Ali Omar wakati akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar kuhusu uwepo wa bidhaa hiyo katika Soko.

Amesema Muingizaji wa Bidhaa hizo hakupita katika Ofisi yake hivyo bidhaa hizo bado hajizasajiliwa wala kupita katika Maabara yao kujulikana ubora na usalama wake.

Aidha Dk. Khamis ameongeza kuwa ZFDA kwa kushirkiana na vyombo vingine vya uchunguzi wanaendelea kumtafuta Mfanyabishara aliyeziingiza bidhaa hizo nchini kinyume na sheria na akipatikana atapelekwa katika vyombo vya Sheria.

“Jukumu la ZFDA kwa sasa ni kuziondoa katika Soko kutokana na kutokidhi vigezo wakati huo huo kwa kushirikiana na vyombo vingine tunamtafuta Mfanyabiashara huyo ili tumpeleke katika vyombo vya kisheria”

Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha usajili wa bidhaa kutoka ZFDA Khadija Ali Sheha amesema bidhaa hiyo siyo halisi kwa vile haioneshi hata Kampuni au Kiwanda kilichotumika kutengeneza bidhaa hiyo.

Amesema katika Vifungashio vya Bidhaa hiyo imeandikwa inatoka nchini China lakini hakuna maelezo ya ziada kuelezea Kiwanda kilichotumika na Jimbo husika nchini China ili kufuatilia zaidi.

Kuhusu kifungashio chake amesema bidhaa hiyo inamlaghai mtoto na hivyo zinaweza kupelekea athari kubwa kwa watoto siku za mbele.

“Kifungashio kinamlaghai mtoto lakini kinaweza pia kuwapelekea Watoto waweze hata kutumia Mabomba ya Sindano ya kawaida kutia maji au juisi wakaanza kutumia na mwisho kupata maambukizi mbalimbali” Alisema Khadija.

Kutokana na hali hiyo tayari Wakala unaendelea na zoezi la kuzichuguza bidhaa hizo katika maeneo tofauti ili zisiwepo katika Soko.

Mohamed Shadhil Shauri Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula ZFDA amesema tayari wamekagua maduka 25 ya mjini na zoezi litaendelea maeneo mbali mbali ya mijini na Vijijini.

Amesema kuna uwezekano wa bidhaa hizo kupitia katika Bandari bubu au kupitia katika Vituo vya forodha bila kufahamika vyema hasa kwa wale Wafanyabiashara wanaochanganya bidhaa tofauti katika Kontena moja.

Jumla ya Maboksi 24 yenye Choklet zipatazo 600 tayari yamekamatwa katika Maduka mbali mbali ili kuondolewa katika Soko.

Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) umeanzishwa chini ya sheria No.2 ya mwaka 2006 na marekebisho yake ya no. 3 ya mwaka 2017 ambapo jukumu lake ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa katika soko zipo katika hali ya ubora na usalama kwa ajili ya matumizi.

WAZALISHAJI MBEGU WAKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha.

Wazalishaji wa mbegu nchini wameanza mkakati wa kuzalisha mbegu zinazoweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,ili kuhimili hali ya ukame na kuleta mazao mengi hivyo kumsaidia mkulima kupata uhakika wa chakula na kipato.

Akizungumza katika Maonesho ya kilimo Teknolojia yaliyofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tari Seliani ,Meneja Mauzo wa Kampuni ya Seedco Daniel Ulimboka alisema kuwa kwa sasa wamefanya utafiti na kuja na mbegu bora ambazo zinahimili hali ya ukame licha ya uhaba wa mvua bado zinaleta mavuno ya kutosha kwa mkulima.

"Tuna mbegu aina ya tumbili 419 ambayo inafanya vizuri sana hasa katika kipindi hiki ambacho hakuna mvua za kutosha wakulima bado wamekua wakipata mavuno na kufurahia kilimo" Alisema Daniel

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha aliwataka watafiti kubuni teknolojia zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili wakulima waweze kupata mazao badala ya kupata hasara kutokana na mabadiliko hayo ambayo yamekua yakileta athari na kusababisha kushuka kwa uzalishaji.

Aidha aliwataka Wakulima kuondokana na kilimo cha mazoea ili waweze kufanya kilimo chenye tija na kuwaletea manufaa wakulima na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Baraza la Nafaka Afrika Mashariki Gerald Masila alisema kuwa wanafanya juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko ili waweze kupata faida ya kilimo chao na kujikwamua kiuchumi.
 Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya teknolojia za  kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.Picha na Woinde Shizza ,Arusha .
Meneja Muzo wa kampuni ya Mbegu ya Seedco Daniel Ulimboka  akifafanua juu ya mbegu za tikiti zinazozalishwa na kampuni hiyo katika maonyesho za  teknolojia ya kilimo yaliyofanyika katika eneo la kituo cha Utafiti wa kilimo cha Tari Seliani na kuandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki.Picha na Woinde Shizza ,Arusha .

TIC KUUTMIA MKUTAO WA SADC KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZIPO NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KITUO Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kitahakikisha kinatumia kikamilifu Mkutano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kutangaza fursa za uwekezaji zilizpo nchini hasa kwa kuzingatia soko la jumuiya hilo ni kubwa.

Akizungumza leo Julai 24 ,2019 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geofrey Mwambe amesema kuwa kituo hicho kinatambua umuhimu wa mkutano wa SADC na fursa zilizopo, hivyo wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutangaza fursa za uwekezaji.

"SADC ni eneo kubwa la soko na Tanzania tunayo nafasi ya kulitumia vizuri.Tunafahamu tulianza na SADC iliyokuwa na lengo la kuokomboa nchi za Kusini mwa Afrika na baadae tukawa na SADC ambayo imejikita kuzungumzia maendeleo.

"Ukiitaza historia yetu, Tanzania ni mwanzilishi wa SADC iliyokuwa na CC mbili na baadae nchi zilizmo kwenye jumuiya hiyo zikaingia kwenye SADC yenye C moja.Kwetu sisi mkutano wa SADC kufanyika nchini tutatumia nafasi hiyo kujitangaza kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,"amesema Mwambe.
 Amesisitiza kupitia mkutano wa SADC unaotarajia kufanya Agosti mwaka huu wanaimini kutaibuka fursa mpya hasa kwa kuzingatia ni mkutano mkubwa na wenye kukutanisha idadi kubwa ya wananchi wa jumuiya hiyo.

Amefafanua kuwa jumuiya hiyo ya SADC ina watu milioni 450 ambalo ni soko kubwa na Tanzania inayo nafasi ya kutosha kuitumia kwa ajili ya kufanya maendeleo yake kupitia uwekezaji huku akifafanua kupitia jumuiya hiyo kuna mambo mengi ambayo nchi wanachama wamekubaliana na yanatoa nafasi kwa nchi hizo kutumia soko lililpo kufanya biashara.

Mwambe amesema kwa bahati nzuri ambayo Tanzania imepita kwani, kupitia mkutano huo Rais Dk.John Magufuli atakabidhiwa Uenyekiti wa SADC na hivyo ni fursa nzuri itakayoiwezesha nchi kutumia nafasi hiyo kujiimairisha kwenye soko la biashara kwa nchi wanachama.

Wakati huo huo Mwambe amezungmzia Kongamano la kimataifa la zao la korosho ambalo lilifanyika mkoani Mtwara ambapo amefafanua kongamano hilo limeleta tija kubwa na anaamini linakwenda kusaidia katika kuongeza thamani ya korosho nchini.

Mwambe amesema kuwa zaidi ya washiriki 400 wamahudhuria wakiwamo wageni 100 kutoka mataifa 23 duniani baada ya kongamano hilo wengi wao wameonesha nia ya kuwekeza katika zao la korosho,"amesema na kuongeza kuwa mikoa inayolima zao la korosho ya Mtwara,Lindi, Pwani na Ruvuma iko tayari kupokea wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika kuinua zao la korosho.

Ametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya uwekezaji yawe yanaandaliwa mapema kwa kupimwa na kuwekwa michoro ili muwekezaji akipatikana iwe rahisi kuanza uwekezaji.
Kwa upande mwingine Mwambe ametoa rai kwa watanzania kuwekeza kwani wakiamua wanaweza na kikubwa ambacho wanatakiwa kukifanya ni kuunganisha nguvu ya pamoja.

CLIMATE ACTION NETWORK YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MATUMIZI YA NISHATI JADIDIFU, MBINU ZA KUONGEZA CHAKULA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

TAASISI ya Action Network Tanzania inayojihusisha na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi imewakuwakutanisha wadau wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani kwa lengo la kutafuta mbinu ambazo zitachochea matumizi ya nishati jadidifu na mbinu za kuweza kupatikana chakula cha kutosha.

Wadau hao wamekutana wilayani Bagamoyo ambapo pamoja na mambo mengine wametumia mafunzo maalumu ambayo yameandaliwa na Climate Action Network Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na wametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina mbinu ambazo watazitumia kuhamasisha jamii katika matumizi ya nishat ijadidifu.

Pia wameeleza kuwa, kuna kila sababu ya kuhakikisha kunakuwa na elimu ya kutosha kwa jamii katika kueleza umuhimu wa kutumia nishati mbadala na kutafuta mbinu zitakazosaidia upatikanaji wa chakula cha kutosha huku wakiiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupata sera ambayo itajikita katika kuisimamia na kuindeleza nishati jadidifu nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa majadiliano hayo, Meneja Rasilimali na Ukutanishi Jophillen Bejumula amesema kuwa wana imani kuwa baada ya kukutana na wadau hao kwa majadiliano wanaamini watatoka na mbinu mbadala na kuangalia mbinu gani zitafaa na Serikali isaidie wapi katika kuwasaidia wavuvi, wakulima na wafugaji ikiwa ni sehemu ya makati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Pia amesema kuwa Chalinze na Bagamoyo wananchi wengi wanajishughulisha na kilimo, uvuvi na ufugaji na ni miongoni mwa maeneo ambayo mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha athari kwa namna moja au nyingine.Hivyo kupitia majadiliano hayo watatoka na mbinu za kukabiliana na mabadiliko hayo ikiwemo ya kutumia nishati jadidifu na kuongeza uzalishaji wa chakula.

Wakati huo huo amesema kupitia majadiliano hayo wanajaribu kuonesha changamoto zilizopo katika kuitumia nishati jadidifu na katika hilo wanaona iko haja ya kuwa na mkakati madhubuti kuendeleza matumizi ya nishati jadidifu pamoja na malengo ya muda mrefu.

Bejumula amesema kupitia majadiliano hayo pia wamekumbushwa wajibu wao huku akieleza kwamba Climate Action Network Tanzania wapo katika kuipitia upya sera ya nishati iliyopo na kisha wataandaa majadiliano mazuri na ujumbe wake utawasilishwa Wizara ya Nishati.

"Tunatarajia kuona uwepo na mkakati wa muendelezo wa kuendeleza nishati jadidifu.Tunao ushirikiano mzuri na wakaribu na viongozi wa ngazi za juu Serikali, wamekuwa wakitoa maelekezo nasi tunayafanyia kazi, na tutaendelea kuwasikiliza.Hata hivyo tunadhani ni vema kukawa na sera inayohusu kuendeleza nishati jadidifu nchini Tanzania,"amesema.

Kwa upande wake mmoja ya watoa mada kwenye majadiliano hayo , Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Marian Dk.Brown Gwambene amesema kikubwa ambacho wamekifanya ni kuwasiliza zaidi wadau ambao ndio walengwa na kupitia wao wameibua mambo mapya na hivyo kwa pamoja sasa watakuwa na uelewa wa namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mmoja wa washiriki katika majadiliano hayo Mtafiti na Mhadhiri mstaafu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Hilda Kiwasila amesema umefika wakati wa kuwa na mikakati endelevu katika eneo la nishati jadidifu na kufafanua kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikiwekeza katika nishati jadidifu lakini tatizo ni kwenye usimamiaji na uendelezaji.

Mshiriki mwingine wa majadiliano hayo kutoka jamii ya wafugaji Monica Sambingu amesema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sana jamii ya wafugaji na kupitia majadiliano hayo atakuwa mabolozi wa kuhamasisha jamii yake kushiriki kukabiliana na athari za mabadiliko hayo ikiwa pamoja na kuhakikisha hakuna uharibifu wa mazingira.
 Yanasia Nguma kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi Bagamoyo akizungumza wakati wa majadiliano hayo
 Meneja Rasilimali na Ukutanishi kutoka Taasisi ya Climate Action  Network Tanzania Jophillene Bejimula akifafanua jambo kuhusu lengo la kuwakutanisha wadau kujadili kuhusu matumizi ya nishati jadidifu pamoja na mbinu mpya katika kuongeza uzalishaji chakula
 Mshiriki kutoka jamii ya wafugaji Monica Sambingo akitoa maoni yake kwenye baraza la majadiliano lililoandaliwa na Taasisi ya Climate Action Network Tanzania ili kujadili mabadiliko ya tabianchi
 Washiri wakifuatilia majadiliano wakati wa semina maalum iliyowakutanisha wadau wa kada mbalimbali katika Wilaya ya Chalinze na Bagamoyo kujadili athari za mabadiliko ya tabianchi
 Washiriki wakifuatilia majadiliano yaliyohusu kutafuta mbinu mpya za kuongeza uzalishaji chakula na utumiaji wa nishati jadidifu kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi
Baadhi ya washiriki wa majadiliano yaliyohusu kuangalia mbinu mpya zitakazosaidia kuongeza upatikanaji wa chakula na matumizi endelevu ya nishati jadidifu .Majadiliano hayo yamefanyika kwa kuwashirikisha wadau kutoka Chalinze na Bagamaoyo na  yameandaliwa na taasisi ya Climate Action Netwrok Tanzania.

IKUPA AITAKA MANISPAA YA ILALA KUUNDA KAMATI YA UTENDAJI KAZI

$
0
0
NAIBU WAZIRI wanchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge ,kazi ajira na Wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa, ameitaka Manispaa ya Ilala ,kuharakisha kuunda kamati ili kurahisi utendaji kazi kutoka katika ngazi za mitaa na Wilaya. 

Mhe. Ikupa ametoa kauli hiyo alipokutana na walemavu Wilayani Ilala akiwa katika ziara yake ya kukutana na walemavu ambapo alisema zimeundwa Ilala bado ikonyuma katiaka kuunda kamati hizo kwani mpaka sasa imeunda kamati 27 kati ya kata 36 na mitaa 76 kati ya mitaa 156. 

“Fanyeni juhudi kubwa katika kuunda hizi kamati zinaumuhimu mkubwa zitasaidia kuanzia huko chini kupata takwimu na siyo tu kwamba ziundwe bali zifanye kazi “ 

Aidha ameikumbusha Manispaa hiyo kutoa mafuta chupa moja kila baada ya miezi mitatu kwa watu wenye Ualbino, na kuagiza mikokopo ya asilimia mbili kwa walemavu iendelee kutolewa kwa utaratibu uliowekwa badala ya kupewa kikundi fulani ili kiwagawie wengine. 

‘’Tayari tumesha weka kanunu za utoaji mikopo hii ,suala la kusema kipewe kikundi fulani haliwezekani mimi ni mkweli nakwa wale mlichukua mikopo ya Bajaji mlitaka mpunguziwe rejesho nimezunguza na mkurugenzi amesema inawezekana mtakutana naye ili mliweke sawa’’Alisema Ikupa 

Pia alitoa rai kwa mkoa wa Dar es salaam ,kuviunga mkono vikundi vya wenye ulemavu wanao tengeza vifaa saidizi badala ya kuendelea kununua kutoka nje na kusema kuwa hata Rais Magufuli anasisitiza watanzania tupende vya kwetu ili kuendeleza viwanda vya ndani. 

Ikupa alisisitiza matumizi ya Lugha ya alama pale mikutano inapofanyika na pia katika mikutano ya kampeni za Serikali za mitaa ili kusaidia kundi hilo kumfahamu mtu anaye mpigia kura , pia akaagiza kurekebishwa miundo mbinu ya majengo kwa kwaajili ya walemavu hasa yale ya zamani yafanyiwe ukarabati. 

Alisema Serikali kupita Ofisi ya Waziri mkuu imeendelea kuhakikisha kwa huduma kwa watu wenye ulemavu zinaendelea kuboreshwa na Wizara mbali mbali zimeendelea kutekeleza na yameundwa madawati katika kila wizara na ofisi yake imeanza taratibu za kupata takwimu za wenye ulemavu kupitia mitaa ili serikali iweze kupanga bajeti kusaidia wenye ulemavu. 

‘’Serikali pia tumeajiri watu wenye ulemavu wasiyo ona ,tumeajiri walimu 60 ,kwa hiyo tunapo sema sekta binafs iajiri watu wenye ulemavu sisi lazima tuwe mfano” 

Pamoja na hayo Naibu huyo, amewapongeza watu wenye ulemavu kwa kuendelea kuwa watulivu na kusema kuwa matatizo ya na malalamiko yao kuhusu kuvamiwa na watu wengine katika sehemu zao za kazi ya kuendesha bajaji zitafanyiwa kazi na Manispaa kwa na kusema kuwa itafanika operesheni kubwa ya kuwaondoa watu wanao fanya kazi hizo katika maeneo ya walemavu bila utaratibu. 

Kwa upande wao watu wenyeulemavu walio pata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo pamoja na kumpongeza Naibu waziri , wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuwajali walemavu na kuwapatia mikopo ya asilimia mbili , kuwawekea waziri anaye shughulikia masuala yao jambo ambalo limewafanya kujisikia nao kama binadamu wengine. 

“Hapo kipindi chanyuma, Mlemavu alizaraulika , alikuwa omba omba ,mchafu asiyekuwa na mwelekeo hata hapakuwa na hata Benk moja ambayo inaweza kumkopesha fedha leo Serikali ya awamu yatano imetthamini sana Mhe Naibu waziri tupelekee pongezi zetu kwa Rais wetu mwambie tuna mpenda “ Alisema Henry Chacha.

PROFESA JAY KUUPAMBA USIKU WA KUMSAKA MISS KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha 

Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Mbilinyi (Prof Jay ) anatarajiwa kutumbuiza katika shindano la kumsaka mlibwende wa kanda ya Kaskazini linalotarajiwa kufanyika July 27 Karina ukumbi wa Naura Spring Jijini hapa. 

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa mkurugenzi wa kampuni ya kismat promotion media Ltd , ambaye pia ni Mkurugenzi wa mashindano haya Mary Mollel Alisema kuwa jumla ya warembo 12 waliotoka katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambayo ni Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara wanatarajiwa kuminyana katika usiku huo. 

Alibainisha kuwa mbali na Profesa Jay  kutoa burudani, Pia kutakuwa na wasanii mbalimbali kutoka Kanda ya Kaskazini zikiwemo ,burudani kutoka katika vikundi vya ngoma Za asili. 

Ikiongea na warembo hao afisa Utamaduni jiji la Arusha Benson Maneno aliwataka warembo hao kujiandikisha Katika daftari la kudumu la kupiga kura kwani kwa kutokufanya hivyo watapoteza haki yao ya msingi ya kupiga Kura. 

"pia napenda kuwasihi muwe na hekima na heshima na nithamu pia pindi mnapokuwa katika kambi zenu, muheshimu Jamii inayowazunguka pamoja na viongozi wanaowafundisha ,napia napenda kuwaasa muwe natabia Mjema maana nyie nimfano wa kuigwa katika Jamii naweza sema nikioo cha jamii "Alisema Maneno 

Kwa wake mrembo wa kanda ya Kaskazini anaeachia muda wake Teddy Mkenda Alisema mashindano haya yamemsaidia mambo mengi ikiwemo kuvijua vituo mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini. 

Hata hivyo aliwataka warembo hao kujiamini na kutumia taaluma yao na urembo huo kusaidia Jamii inayowazunguka, huku akiwataka kujitaidi ili waweze kuleta taji la miss Tanzania ndani kanda ya Kaskazini.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images