Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

Introducing "Nionyeshe" (Official Audio) by Q Chilla Ft. Harmonize


Introducing "My Boo Remix" (Official Video) by Harmonize FT. Q Chilla

StanChart CEO awarded “Best Leader - Banking, Tanzania 2019” by Global Brand Awards

$
0
0
Standard Chartered Bank’s Chief Executive Officer, Sanjay Rughani, has been awarded the “Best Leader-Banking, Tanzania 2019” Award by the Global Brand Awards.

Global Brands Awards were established with the aim of honoring excellence in performance and rewarding Companies and Individuals across different sectors. In addition to Company Awards, the Global Brand Awards aim to acknowledge key individuals who strive for fineness and reward their performance with the ultimate Global Recognition under the Leadership Awards Category.

Mr. Rughani was one of the few nominees, globally, who were selected for the Leadership Awards – Banking category.
To identify the nominees, and ultimately, the winner, an external research team was constituted by the Global Brands Awards Team to evaluate the nominees. Data was collected by the research team from different sources, including third party data providers, providing a robust leadership system.

Based on the thorough research that was conducted, Mr. Rughani has showcased excellence in the Leadership field in the Banking Sector in Tanzania thereby winning the Award.

On learning about the news, Mr. Rughani said, “I am humbled by this recognition and I attribute it to the people that I work with at Standard Chartered Bank Tanzania. I also attribute it to the rest of my counterparts in the banking sector with whom I work closely under the Tanzania Bankers Association umbrella. This is our Win and I thank them all.”

Mr. Rughani was appointed as the first Tanzanian CEO for Standard Chartered in Tanzania in January, 2016. He has worked for the Bank since 1999 and has held various key positions within the Bank which include heading the Bank’s Global Finance Shared Services in Chennai, heading Finance Operations and Change Management for the Africa Region, being an Executive Finance Director for Ghana and Area Chief Finance Officer for the Western Africa Region covering Ghana, Gambia, Sierra Leone and Cote d’Ivoire. He was also a Regional Finance Manager for Africa based out of London and an Executive Finance Director for the Bank in Tanzania.

In addition to his role as the CEO of Standard Chartered Bank in Tanzania, Mr. Rughani holds important governance representations which include being the Chairman of the CEO Roundtable in Tanzania, Vice Chairperson for Tanzania Bankers Association, A Director in the Board of the Tanzania Private Sector Foundation and a Non-Executive Director of the Association of Tanzanian Employers.

 Mr. Rughani is also the Vice Chairperson of the Professional Accountants in Business Committee (PAIBC) for International Federation of Accountants (IFAC).

The Global Brand Awards are organized by Global Brands Magazine, a leading Brands Magazine providing opinions and news related to various Brands across the world. This is the seventh edition of the Awards and the winning companies and individuals will be presented with their awards at an exclusive gala scheduled to take place next month.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA lA NMB,MKUTANO WA ALAT UNAOENDELEA JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipata maelezo ya huduma za kibenki kutoka kwa Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi alipotembelea kwenye banda la Benki ya NMB kwenye Mkutano wa ALAT unaoendelea jijini Mwanza. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo (Kushoto).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akimweleza Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB – Filbert Mponzi jinsi Serikali inavyothamini Benki ya NMB kama Benki ya Serikali alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye Mkutano wa ALAT unaoendelea jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo na Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Abraham Augustino.

SAKATA LA UTEKAJI WA MOHAMMED DEWJI, MAHAKAMA YATOA HATI YA KUKAMATWA KWA RAIA WANNE WA KIGENI

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kuwakamata raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wanaodaiwa kumteka nyara Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu MO.

Hati hiyo ya kukamatwa imetolewa dhidi ya washitakiwa Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi dhidi ya mshtakiwa Mousa Twaleb anayedaiwa kumteka mfanyabiashara huyo, leo Julai 23, 2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa na pia wameomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao wanatarajiwa kuunganishwa katika kesi hiyo.

Wakili wankyo amedai kuwa, washitakiwa hao wataunganishwa katika kesi hiyo kujibu mashitaka mawili ya  kumteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari na kuongoza genge la uhalifu.

Mshitakiwa Twaleb ambaye ni dereva taksi na Mkazi wa Tegeta, tayari alishafikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Shaidi.

Katika kesi hiyo, inadaiwa, Mei Mosi, 2018 na Oktoba 10, mwaka huo huo, katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg Afrika Kusini, kwa makusudi washitakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.

Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo Hoteli ya Colloseum katika wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

 Aidha, Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha kiasi cha sh. Milioni nane huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

Oktoba 11, mwaka jana majira ya alfajiri katika maeneo ya Hoteli ya Colloseum mfanyabiashara MO alitekwa nyara na watu wasiojulikana alipokuwa akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

MALINZI, MWESIGWA WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU, MMOJA AACHIWA HURU

$
0
0

Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi,  Katibu wake  Selestine Mwesigwa na wenzao wawili wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka  20 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Wengine waliokutwa na kesi ya kujibu ni  Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga,  na Karani Flora Rauya huku Meneja wa TFF, Mariam Zayumba akiachiwa huru.

Uamuzi huo umetolewa leo Julai 23,2019 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Maira Kasonde kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya uamuzi mdogo kuona kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Kasonde amesema, upande wa mashtaka ulileta mashahidi 15 na vielelezo tisa katika kuthibisha kesi hiyo.

Amesema katika mashtaka 30 waliyokuwa wakikabiliwa nayo, yapo pia mashtaka ya  matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Malinzi na Mwesigwa, shtaka la kula njama na kutoa nyaraka za uongo linalomkabili mshitakiwa Mwesigwa.

"Ni jukumu la mahakama kuangalia kama mshitakiwa ametajwa kwa namna yoyote katika mashitaka na ni upande wa mashitaka ambao wanatakiwa kuyathibitisha bila kuacha shaka yoyote mashtaka yote, katika ushahidi wote uliotolewa mahakamani dhidi ya shtala la kula njama, hakuna chembe ya ushahidi kwamba mshitakiwa Malinzi na Mwesigwa walikula njama kufanya makosa ya kughushi hivyo, ili kuthibitisha upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta vielelezo vya kuonesha namna njama zilivyofanyika kwa.mantiki hiyo mahakama inawaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu kwenye shtaka hilo."

RAIS MAGUFULI NA DKT. SHEIN KUIPAMBA WIKI YA VIWANDA KATIKA KUELEKEA MKUTANO MKUU WA SADC

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS Dkt. John Joseph Magufuli  na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar  Dkt. Ally Mohamed Shein wanategemewa kushiriki katika  wiki ya viwanda itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 5 hadi 9 mwaka huu ikiwa ni katika kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa SADC utakaofanyika nchini Agosti mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa mkutano huo ni fursa kubwa kwa watanzania wakiwa wanachama hasa katika kutumia fursa hiyo katika kutangaza huduma na bidhaa hasa za viwanda na utalii zinazopatika nchini kupitia mkutano huo.

Amesema kuwa Ufunguzi wa mkutano huo utafanyika Agosti 5 ambapo Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi na utafungwa Agosti 8 na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein na hiyo yote ni kutokana na uzito wa tukio hilo ambalo limebeba  faida kubwa kwa taifa na watanzania.

Bashungwa amesema kuwa "lazima tunufaike na mkutano huo tukiwa wanachama na ninawahimiza wenye viwanda wazidi kujitokeza kwa wingi zaidi, ninafurahi watanzania wanachangamkia fursa hii ambapo hadi sasa idadi ya washiriki waliojiandikisha wamefika 580 huku idadi ya watanzania ikiwa juu zaidi" ameeleza Bashungwa.

Aidha amesema kuwa wizara ya viwanda kwa kushirikiana na Wizara nyingine itaendelea kuhakikisha inawawezesha vijana ili kuweza kujenga uchumi wa viwanda unaowahusisha watu wa kada zote na kuahidi kusimamia vyema mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.

Mkutano huo wa 39 wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 17 na 18 ambapo wakuu wa nchi 16 watakutana na Rais Magufuli ambaye ni Makamu mwenyekiti wa umoja huo atakuwa mwenyekiti kwa muhula mmoja kwa kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa Namibia.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa ni sehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Shilingi Milioni 100 kutumika katika Miradi ya Jamii JAHIBU WMA

$
0
0
Baadhi ya madarasa yaliyofanyiwa ukarabati na Taasisi za Chemchem Association.
Kikao cha vikoba wananchi wa vilima vitatu kikiendekea
Madawati yametolewa na Kampuni ya Taasisi za Chemchem Association shule msingi Vilima vitatu.
Baadhi ya madarasa yaliyofanyiwa ukarabati na Taasisi za Chemchem Association ambapo kwa jumla yake yapo saba.Hayo madawati yametolewa shule msingi Vilima vitatu, na hiyo ndio shule iliyokarabatiwa na hapo kikao cha vikoba wananchi wa vilima vitatu

Na Vero Ignatus,Arusha

Zaidi ya sh 100 milioni imepangwa kuchangia miradi ya Maendeleo katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Wanyamapori( JUHIBU kutoka kwa Taasisi za Chemchem Association.

Taasisi hiyo ya JUHIBU, ilianzishwa mwaka 2003 ambapi inaundwa na vijiji vyaangawe,Mwada,Ngoley,Vilimavitatu,Minjingu,Kakoi,Olasiti,Manyara,Magala, na Maweni na ina ukubwa wa 283.

Walter Palangyo ni Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, amesema taasisi inachangia miradi hiyo kama sehemu ya wajibu wake kuchagia shughuli za Maendeleo ya jamii(SCR) mbali ya kodi na tozo nyingine zinazolipwa na Chemchem iliyowekeza shughuli za Utalii katika hifadhi hiyo.

Amesema taasisi hiyo, imekamilisha ukarabati wa majengo ya shule ya msingi vilima vitatu,ofisi mbili za walimu na sasa ipo kwenye mradi wa ujenzi wa vyoo ."katika shule hii, tumetumia kiasi cha sh 50 milioni, ili kuhakikisha wanafunzi katika shule hii wanapata elimu bora katika mazingira mazuri kwani tayari tumewapatia madawati 100 kwa ili kumaliza tatizo katika shule hii"alisema

Amesema taasisi hiyo pia imetoa kiasi cha sh 5 milioni ili kusaidia Vikoba katika baadhi ya vijiji katika eneo hilo, ikiwepo vikundi vya jamii ya wabarbeig ili kuweza kuwa na miradi ya maendeleo."Kuna kikundi cha Wicheda na Datoga vya jamii ya Kibarbeig ambavyo tumepatia kiasi cha sh 2.5 milioni ili kukuza mitaji yao"alisema

Alisema katika jamii hiyo, pia kumeanzishwa mradi wa maboma ya asili ambayo watalii wataweza kuwatembelea ."Mwaka huu pia tunaendelea na mradi wa kusomesha watoto katika jamii hii, katika chuo cha wanyamapori cha Mweka na chuo cha Ufundi (VETA) naa wengine tumewalipia ada za shule ya sekondari "alisema

Amesema pia kuna miradi ya maji, michezo na afya katika vijiji hivyo, hasa kutokana na fedha ambazo zinatokana na la ya utalii.

Waziri Mkuu afungua Mkutano Mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) alipomwakilisha Rais Magufuli,kwneye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza 23.7.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Selemani Jafo akizungumza kwenye mkutano mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa Benki ya NMB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo, Wakati na Kilimo wa Benki ya NMB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Meneja wa Mahusiano ya Serikali Benki ya NBC, William Kallaghe, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasikiliza watumishi wa Benki ya CRDB, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019.
 aziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati Benki ya CRDB (kulia), Boma Raballa, wakati akikagua mabanda, katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Abubakar Mukadam.

WANAWAKE WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UJENZI

$
0
0
Wito umetolewa kwa makandarasi wanawake kwenye mikoa ya Kanda za Magharibi na Nyanda za Juu Kusini kujitokeza na kuchangamkia fursa za miradi midogo inayojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani Kigoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga, ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mafunzo ya wiki mbili kwa makandarasi wanawake kutoka mikoa minne ya Kanda ya Magharibi na Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili kushiriki kwenye kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara hapa nchini.

"Wanawake msilale changamkieni fursa za hii miradi na msing'ang'anie tu kazi hizi za kufyeka nyasi na kuzibua mitaro kwenye madaraja bali mjitokeza hata kwenye kazi za ujenzi wa barabara", amesisitiza Mhe. Anga.

Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo ameongeza kuwa fursa za utekelezaji wa miradi midogo kwenye miradi mikubwa inayo nafasi kubwa ya kuwajengea uwezo wa kitaalam na kifedha wahandisi wanawake nchini hivyo ni wajibu wao kutumia nafasi hiyo sasa ambapo mkoa wa Kigoma unayo fursa ya utekelezaji wa miradi mingi ya ujenzi ambayo wakandarasi wengi wanaweza kujitokeza na kuifanya.

Mhe. Anga amesema kuwa bado makandarasi wengi wanawake mkoani Kigoma hawajajitokeza kwa wingi kushiriki kwenye miradi ya ujenzi fursa ambayo inawanyima kukua kimtaji na uwezo wa utekelezaji wa kazi na miradi mingi ya ujenzi.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma, amesema kuwa kwa sasa mkoa Kigoma unatekeleza mradi mkubwa wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 260 ambapo zipo kazi ambazo wakandarasi hao wanawake wanaweza kuzifanya.

Mhandisi Choma amesema kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Sera ya uwezeshaji wanawake kiuchumi imeweka mkakati wa kuwasaidia na kuwapa kipaumbele kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa chini ya Wizara hiyo. 

Awali Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji Wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Gladiness  Kitaly, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwapa ujuzi makandarasi hao wanawake kujua namna ya kuomba miradi ya barabara, taratibu za kujaza zabuni za maombi ya miradi, ufanisi wa teknolojia ya nguvu kazi katika kufanya matengenezo ya barabara katika maeneo ambayo yanatoa kipaumbele kwa wanawake.

Mafunzo hayo ya wiki mbili yameshirikisha wahandisi wanawake  kutoka katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora na wenyeji Kigoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga,  akifungua semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake makandarasi wa mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi. Mafunzo hayo yanafanyika katika Chuo cha Veta mkoani Kigoma.
 Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma, akizungumza na wanawake makandarasi kuhusu kuchangamkia fursa za kazi ya matengenezo ya barabara hasa kwa mkoa huo. Mafunzo hayo yamejumuisha wanawake makandarasi kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi.
 Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta  ya Ujenzi) Mhandisi Gladiness Kitaly, akizungumza na wanawake makandarasi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya zaidi ya wiki moja kwa ajili ya kuwajengea ufanisi katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara, mkoani Kigoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga,  akipokea asali kutoka mwanamke mkandarasi Bi. Rosemary Augen, ambaye pia anajishughulisha na biashara ndogondogo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananawake makandarasi yanayofanyika mkoani Kigoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga, akiwa katika picha ya pamoja na wanawake makandarasi kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi mara baada ya kufungua mafunzo ya makandarasi hao ya kuwajengea uwezo, mkoani Kigoma.
Meneja wa Kanda ya Kati ya Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB), Mhandisi David Msekeni, akifundisha namna ya taratibu za kujisajili kupitia bodi hiyo kwa wanawake makandarasi kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa na Katavi walioshiriki semina ya kuwajengea uwezo, mkoani Kigoma.

DC MURO APONGEZA CHUO CHA UHASIBU,AWAELIMISHA UMUHIMU WA KUSOMA

$
0
0
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv,Arusha 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amefurahishwa na kazi zinazofanywa na Chuo cha Uhasibu Arusha,amekiomba chuo hicho kuendelea kuwaandaa vijana kitaaluma na kivitendo ili kuja kupambana katika changamoto ya soko la ajira. 

Muro liyasema hayo chuoni hapo wakati akifunga maonyesho ya nadharia na vitendo ya kitaaluma yaliyoshirikisha shule 18 za sekondari mkoani hapa ambapo alitumia Muda huo kukipongeza na kukisifu chuo hicho kwa kutoa elimu mbalimbali pia kuwahamasisha vijana waliopo kidato cha nne kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu na kujiunga na elimu ya chuo .

Aidha alifafanua kuwa chuo hicho kimefanya ubunifu mkubwa wa kushirikisha vijana wa sekondari za mkoa wa Arusha kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho kwani kwakufanya hivyo wanawaandaa Vijana hao wa sekondari kwa ajili ya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu kwa baadaye. 

"Hapa kuna wanasayansi, uchumi, watu wa mapambo na upishi wa keki hii yote ni lengo la chuo kuwawezesha vijana ili wakimaliza masomo wasitoke na elimu ya darasani tu bali kwenda kuwa wajasiriamali ili waendeshe maisha yao. "alifafanua Muro

Alitumia mda huo kuwahasa wanafunzi hao kuwa makini katika swala zima la kusoma na kutilia manani masomo kwani katika soko la ajira la kipindi hiki ili uweze kushinda nalo lazima uwe na elimu ya kutosha ya natharia na vitendo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka Alisema kuwa chuo hicho kitaendelea kutoa elimu bora ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na ujuzi wa kuendesha maisha yao baada ya masomo. 

"Kila kozi anayosoma mwanafunzi anapewa kazi mbalimbali ili ajue kwa vitendo kwani lengo letu nikutoa wajasiriamali pia huko waendako wakaweze kupata ajira na kujiajiri kwani soko la ajira kwa sasa ni changamoto kubwa "aliongeza Profesa Sedoyeka. 

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaacha vijana wao au watoto wao kuchagua masomo ambayo wanayataka wenyewe kuyachukua na sio kuwachagulia kombi,aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao chuoni hapo kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayoendana na soko la Ajira. 

"chuoni kwetu pia tunatoa ushauri ni masomo gani mwanafunzi achukue ili aendane na soko la ajira iwe anataka kuajiriwa au anataka kujiajiri hivyo wazazi walete watoto wao ili wapatiwe ushauri mzuri"alifafanua Profesa Sedoyeka

Kwa upande wake mmoja ya mwanafunzi alieshiriki maonyesho Hayo Bundalla Bachia kushukuru na kusema maonyesho hayo yamewasaidia kwani yanawapa fursa ya kujifunza kivitendo masomo wanayofundishwa darasani

Alibainisha kuwa maonyesho hayo yamewatengenezea uzoefu na ujuzi kwani wamekutana na wanachuo wanaosoma fani mbalimbali hivyo wanatarajia kujiunga nazo mara baada ya kidato cha nne na hiyo inawapa hamasa ya kufikia Elimu ya juu.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro katikati akimkabithi kapteni wa timu ya mpira wa miguu kutoka Shule ya sekondari mara baada ya kushinda katika michezo iliyoandaliwa na Chuo cha uhasibu Arusha,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka .

MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI MKOANI PWANI AMEZITAKA HALMASHAURI KUFUATA UTARATIBU WA MANUNUZI NA FEDHA

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI
MKAGUZI wa hesabu za serikali mkoani Pwani, Hamis Juma amewataka wakuu wa idara ,maofisa ununuzi na wakuu wa vitengo ikiwemo cha fedha ,kuhakikisha wanafuata utaratibu wa manunuzi,fedha na sheria zilizowekwa ili kuondokana na kutofungwa kwa baadhi ya hoja na hati chafu.

Aidha amewataka ,kila mmoja asimame katika nafasi yake kusoma sheria zinazomuongoza katika idara yake.

Akizungumza katika baraza maalum la madiwani,huko Kibiti lililohusu kujadili taarifa za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Juma alieleza halmashauri ya Kibiti ni moja ya halmashauri tisa mkoani hapo ambazo zilikuwa na hoja za miaka ya nyuma na hoja za mwaka husika 2017/2018.
 Alisema, halmashauri nyingi zimekuwa na hoja zisizofungwa kutokana na kutofuata taratibu na ukaguzi waliouweka.

Juma alifafanua kwamba, pia kutokuwa na ushirikiano baina ya halmashauri, watendaji na madiwani inasababisha utekelezaji wa kufunga hoja kukwama.

"Kumekuwepo na changamoto ya kiutendaji katika raslimali watu na fedha na kusimamia miradi ya maendeleo":Hivyo basi wakurugenzi na watendaji katika halmashauri zote tisa simamieni ili sheria,kanuni na taratibu zifuatwe kwa lengo la kusaidia mkaguzi akipita kusiwepo na dosari"alifafanua Juma.
Nae katibu tawala wa mkoa wa Pwani, Theresia Mmbando alisema ,watendaji wafuatilie na wawe wasimamizi na wazingatie sheria,kanuni na taratibu kwani ni suala la msingi katika utendaji kazi wao.

Alisema katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo fedha zinazokuwa hazijatumika wahakikishe wanatumia kwa mwaka husika na kwa makusudi yaliyolengwa.

Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti ,Alvera Ndabagoye alisema kuwa wataendelea kufanya kazi kulingana na sheria,kanuni pamoja na kusimamia fedha za maendeleo zitumike kwa maslahi ya jamii.

MWANZO MWISHO KESI YA MALINZI, MWESIGWA, WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU.

$
0
0

Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi, Katibu wake Selestine Mwesigwa na wenzao wawili wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 20 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Wengine waliokutwa na kesi ya kujibu ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, na Karani Flora Rauya huku Meneja wa TFF, Mariam Zayumba akiachiwa huru.

Uamuzi huo umetolewa leo Julai 23,2019 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Maira Kasonde kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya uamuzi mdogo kuona kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Kasonde amesema, upande wa mashtaka ulileta mashahidi 15 na vielelezo tisa katika kuthibisha kesi hiyo.

Amesema katika mashtaka 30 waliyokuwa wakikabiliwa nayo, yapo pia mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Malinzi na Mwesigwa, shtaka la kula njama na kutoa nyaraka za uongo linalomkabili mshitakiwa Mwesigwa.

"Ni jukumu la mahakama kuangalia kama mshitakiwa ametajwa kwa namna yoyote katika mashitaka na ni upande wa mashitaka ambao wanatakiwa kuyathibitisha bila kuacha shaka yoyote mashtaka yote, katika ushahidi wote uliotolewa mahakamani dhidi ya shtala la kula njama,hakuna chembe ya ushahidi kwamba mshitakiwa Malinzi na Mwesigwa walikula njama kufanya makosa ya kughushi hivyo, ili kuthibitisha upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta vielelezo vya kuonesha namna njama zilivyofanyika kwa.mantiki hiyo mahakama inawaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu kwenye shtaka hilo."

Hakimu Kasonde amesema, katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, washtakiwa Malinzi na Mwesigwa wamekutwa na kesi ya kujibu kwani upande wa mashitaka walitengeneza kesi dhidi yao hivyo wanapaswa kujitetea.

Mshtakiwa Mwesigwa pia atatakiwa kujitetea katika shitaka la kutoa nyaraka ya uongo ya maazimio ya kamati tendaji ya Juni 5, 2016 kwa lengo la kuonesha kuwa kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka Edgar Masoud kwenda kwa Mwanga.

Katika shtaka la tano hadi 14 la kughushi yanayomkabili Malinzi na Rauya, ushahidi ulionesha kuwa nyaraka iliyoghushiwa ambayo ni risiti ilitengenezwa na shahidi namba 10 ambaye ni Hellena Mihayo kwa kufuata maelekezo toka kwa Mkurugenzi wa Fedha.

Kwa upande wa mshitakiwa Rauya yeye anatakiwa kujitetea katika shitaka moja la kughushi risiti namba 00746 kwani ndiye aliyetengeneza nyaraka hiyo na hakuna ushiriki wa Malinzi katika mashitaka hayo.

Aidha, katika shitaka la saba mahakama imewaona washitakiwa kuwa hawana kesi ya kujibu kwani hakuna ushahidi unaowaunganisha na kesi hiyo.

Pia Hakimu Kasonde amesema katika kosa la kughushi la tisa, hati ya mashitaka inaonesha Malinzi na Rauya walighushi risiti namba 00870 ya Sh milioni 50 wakati kitabu cha risiti hiyo kinaonesha ni Sh milioni tano huku katika shtaka la 11, hati ya mashitaka inaonesha risiti 00947 iliyoghushiwa ni USD 10,000 lakini uhalisia ni USD 1000.

Ameongeza kuwa, mashitaka ya 15 hadi 26 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu yanayomkabili Malinzi mahakama imemuona kuwa ana kesi ya kujibu na kumtaka kujitetea.

"Katika mashitaka ya 27 na 28 ya utakatishaji fedha yanamkabili Malinzi hivyo, atatakiwa kujitetea na katika mashitaka ya 29 na 30 ya utakatishaji fedha yanawakabili Mwesigwa na Mwanga mahakama inawaona na kesi ya kujibu hivyo mtatakiwa kujitetea," alisema Hakimu Kasonde.

Baada ya kusomewa hayo, mawakili wa utetezi wakiongozwa na Abrahamu Sembuji, Kashinde Thabiti wamedai wateja wao watajitetea chini ya kiapo na kuleta mashahidi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.

Balozi Seif akagua mashamba ya Serikali

$
0
0
 Muonekano wa Shamba la Serikali la Makuwe liliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba ambalo Mwaka 2017 limekodishwa Mikarafuu yake kwa gharama ya shilingi Milioni 290,000,000/-.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea na kukagua Mashamba ya Serikali yaliyomo ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Mkuu wa Idara ya Misitu na Mali zisizorejesheka Kisiwani Pemba Nd. Said Juma Hamad Kushoto akitoa maelezo ya mazingira yaliyopo ya Mashamba ya Serikali Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Baadhi ya Wananchi na Wakulima wa Vijiji vya Finya na Makuwe waliojitokeza kumlaki Balozi Seif aliyefika katika Vijiji hivyo kukagua Mashamba ya Serikali.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa maagizo ya utafutwaji wa Mashamba ya Serikali wakati alipofanya ziara ya kuyakagua Mashamba ya Serikali ya Finya na Makuwe Kisiwani Pemba.
 Naibu Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Shamata Shaame Khamis akitoa ushauri wa namna ya kusafishwa Mashamba ya Serikali kwa kutumia Vikosi vya SMZ. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa maamuzi mara baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa Mashamba yake yote yaliyomo katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.

Alisema maamuzi hayo pamoja na mambo mengine yatazingatia pia kuwapa Wananchi ili wayaendeleze kwa kilimo hasa yale yaliyokosa usimamizi na kuyaendeleza kwa muda mrefu na kusababisha uzalishaji mdogo wa mazao pamoja na Karafuu.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiendelea na ziara yake ya Siku Nne Kisiwani Pemba akikagua Mashamba yanayomilikiwa na Serikali yaliyomo ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema umefika wakati Mashamba ya Serikali yawe na uwezo kamili wa uzalishaji kama yalivyo ya Watu Binafsi na pale inaposhindikana kukosa huduma za usafishaji ni vyema ukaandaliwa utaratibu na Taasisi zinazohusika kuwapa Wananchi wale wenye nia ya kuyaendeleza kwa Kilimo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuridhia Wizara ya Kilimo , Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar kuandaa utaratibu wa kutoa Ajira kwa Vijana ili yasafishwe Mashamba yote ya Serikali ambayo hukaa muda mrefu na kupoteza Uzalishaji.

Balozi Seif alifahamisha kwamba mbali ya usafishaji wa Mashamba hayo utakaoongeza Mapato ya Taifa lakini kwa upande mwengine fursa hiyo itatoa ajira kwa Vijana watakaokuwa tayari kufanya kazi hiyo ya Kizalendo ya kuokoa Uchumi wa Taifa.

Aliushauri Uongozi wa Wizara ya Kilimo mbali ya kufanya Uhakikishi utakaoongozwa na Wakuu wa Wilaya wa kuyatambua Mashamba ya Serikali katika Wilaya mbali mbali lakini wakazingatia kuwahakiki Wananchi waliyojitolea kuyasafisha Baadhi ya Mashamba hayo bila ya kushurutishwa.

Alisema uhakiki huo uwaandalie Wanachi hao njia na namna ya kuandika Maombi na kuyapeleka Serikalini kupitia kwa Masheha na Wilaya zao yatakayotoa utaratibu wa kumilikishwa katika matumizi yake kama ilivyofanywa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mara baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Akitoa ushauri wa kunawirishwa kwa Mashamba ya Serikali, Naibu Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Shamata Shaame Khamis alisema ni vyema vikatumiwa Vikosi vya SMZ wakiwemo Watu wa Chuo cha Mafunzo katika usafishaji wa Mashamba hayo.

Mh. Shamata alisema hatua hiyo ya dharura inaweza kusaidia kipindi hichi cha mpito kuelekea mafuno ya Msimu wa Vuli ambao hutegemea kuzalisha mazao mengi haza lile la Uchumi wa Taifa la Karafuu.

Alisema Vikosi cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na mambo mengine ya Ulinzi lakini pia vina utaratibu wa kushiriki kwenye shughuli za Kijamii na Kitaifa pale inapotokeza kuwepo kwa mahitaji hayo.

Mapema Mkuu wa Idara ya Misitu na Mali zisizorejesheka Kisiwani Pemba Nd. Said Juma Hamad alisema yapo Mashamba Sita yanayomilikiwa na Serikali Kisiwani pemba ambayo hayako katika hali ya kuridhisha kutokana na ushughulikiaji mdogo.

Nd. Said alitolea mfano Shamba la Makuwe pekee linalotegemewa na Serikali kwa mapato Makubwa lenye ukubwa wa Ekari 200 likiwa na Wafanyakazi Watano tu wanaolihudumia.

Alisema Shamba hilo lililosheheni zaidi miti ya Mikarafuu na Minazi limefanyiwa usafi Mnamo Mwaka 2016 kukodishwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 290,000,000/- katika kipindi cha Msimu wa Vuli mnamo Mwaka uliofuatia wa 2017.

Mkuu huyo wa Idara ya Misitu na Mali zisizorejesheka Pemba alifahamisha kwamba Minazi iliyomo ndani ya Shamba la Makuwe nazi zake hutumika kuoteshea Miche kwenye Vitalu vya Wizara ya Kilimo na baadhae kugaiwa kwa Wakulima.

Naye Afisa Mdhamini wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC} Kisiwani Pemba Ndugu Abdullah Ali Ussi alisema Shirika hilo limefurahishwa na utaratibu uliobuniwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuyafuatilia kwa uhakiki na utambuzi Mashamba yake yote.

Nd. Abdullah alisema kutokana na kutoshughulikiwa kwa mashamba ya Serikali ambayo ndio yenye uwezo wa kuzalisha zao la Karafuu kwa wingi kumesababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo katika Miaka ya karibuni na kufika Tani 8,500 wakati miaka ya nyuma uzalishaji ulifikia hadi Tani 16,000.

Akitoa ufafanuzi wa Mashamba ya Serikali Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bibi Maryam Abdallah Saadala alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba njia pekee ya kuyaokoa Mashamba ya Serikali na kupatikana ajira za Muda kwa Watu watakaosafisha Mashamba hao.

Bibi Maryam alisema Mashamba Sita yaliyopo Kisiwa cha Pemba yanaweza kuwa katika mazingira bora iwapo Serikali kupitia Taasisi inayosimamia Utumishi wa Umma itaridhia kutoa baraka za upatikanaji wa Vijana watakaoajiriwa kwa muda kufanya kazi hiyo muhimu.

Alisema mfumo huu unaweza kutumika kwa muda pale inapotokea dharura ya kutaka kusafishwa Mashamba hayo hasa ule wakati unaofuatia baada ya Msimu wa Mvua Kubwa hapa Nchini.

Akiambatana na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata wasaa wa kuyakagua Mashamba ya Serikali yaliyo chini ya Wizara ya Kilimo, Maliasilini. Mifdugo ya Uvuvi yaliyopo katika Vijiji vya Finya na Makuwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.

MSAMA AWAHIMIZA WAFANYABIASHARA KUCHANGAMKIA FURSA MKUTANO WA SADC

$
0
0
  Na.Khadija seif, Michuzi tv.

WAFANYABIASHARA wametakiwa kuona kama tunu na kuupa kipaumbele Mkutano
kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart Alex Msama amesema Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi mbalimbali.

"Mkutano huo wa 39 unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo hivyo ni fursa pekee kufanyika ndani ya ardhi ya Tanzania na tutaweza kuongeza pato la taifa katika kila sekta hapa nchini,"

Aidha, Msama amesema mbali na kuongeza pato la taifa kupitia sekta mbalimbali bali pia tutaweza kupata fursa ya kufanya biashara mbalimbali ikiwemo mahoteli,vyakula pamoja na usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia wageni watakaokuwepo nchini katika Mkutano huo.

"Ni wakati wa wafanyabiashara wenzangu kuzikimbilia fursa kwa kipindi hicho wageni watakapowasili kwenye Mkutano huo ambapo Rais wetu John Pombe Magufuli amekishika kijiti Cha kuendesha Mkutano huo akiwa kama Mwenyeji ,"

Pia Msama amesema kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ya Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna ambae ataweza kumuangusha chini Rais huyo ifikapo 202o katika uchaguzi Mkuu.

"Katika kipindi chote alichokua Madarakani Rais Magufuli ameboresha kila sekta kuanzia elimu,usafiri,ajira, pamoja na Miundombinu mbalimbali na kwa wiki hii tunategemea kupokea umeme wa Rufiji ikiwa ni ishara tosha ya kuendelea kupokea wawekezaji kwa wingi bila kuwepo kwa kikwazo cha kukosa na kukatisha shughuli za uzalishaji viwandani kwa wawekezaji wetu,"
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni na Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Ofisini kwake,jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujio wa mkutano mkubwa wa SADC.

WAZIRI MKUU AZIONYA HALMASHAURI ZILIZOLEGA MAKUSANYO YA KODI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na washiriki katika mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), uliyofanyika katika ukumbi wa Malaika, jijini Mwanza, alipomwakimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo, Julai 23.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezionya Halmashauri za Wilaya na Manispaa zilizoshindwa kufikisha malengo ya makusanyo ya kodi na kuzitaka zijitathmini ni kwa nini hazijafikisha malengo hayo.

“Kuna Halmashauri zimetajwa hapa kwamba hazijafikisha malengo ya makusanyo ya ndani. Fanyeni tathmini, ni kwa nini hamjafikia malengo na mhakikishe kuwa mwakani hamji kutajwa tena kwenye mkutano kama huu,” alisema. Halmashauri hizo ni Kakonko, Buhigwe, Madaba, Kigoma, Momba na Songea.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumanne, Julai 23, 2019) wakati akizungumza na washiriki wapatao 700 ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) unaoendelea jijini Mwanza.

Waziri Mkuu ambaye amefungua mkutano huo wa siku tatu kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka washiriki wa mkutano ambao ni Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Majiji, Miji na Manispaa, wasimamie makusanyo ya mapato kupitia vyanzo vyao ili waweze kupanga mipango ya maendeleo. “Lengo la Serikali ni kuwezesha kila Halmashauri zijitegemee kwa asilimia 80-100 ifikapo 2025,” amesema.

“Katika makusanyo hayo, hakikisheni kuwa mnatenga asilimia 40 kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Na hili ni tatizo kwa Halmashauri nyingi zikiwemo zile kubwa. Ukifuatilia kwa makini huoni miradi inayogusa maisha ya wananchi wa kawaida.”

“Ukichukulia Dar es Salaam au Arusha ambao wanakusanya kati ya shilingi bilioni tano na 10, ni mradi gani wa thamani kubwa uliojengwa kwa kutumia fedha zenu za ndani, ukiacha hii mikubwa ya stendi za mabasi au barabara za lami ambayo inajengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu?” alihoji.

“Hivi kuna Halmashauri ambayo imejenga kituo cha afya cha kisasa kwa kutumia fedha zake za makusanyo? Afadhali hawa wa Dodoma ambao wameanza kujenga stendi ya mabasi na hoteli mbili za kitega uchumi,” amesema.

“Uamuzi wa Mheshimiwa Rais Magufuli wa kukusanya fedha zote na kuziweka kwenye chanzo kimoja ulitokana na study ya muda mrefu iliyofanyika na kubaini kuwa fedha zinazokusanywa haziendi kwenye miradi inayogusa wananchi. Niwasihi sana, fanyeni miradi ambayo kila Mtanzania angependa kuiona kwenye Mamlaka zenu za Serikali za Mitaa,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali iliamua kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa ALAT, Bw. Abraham Shamumoyo kwa sababu ya utendaji mbovu.

“Kuna maamuzi alikuwa akiyafanya bila kuishirikisha Kamatai ya Utendaji. Kuna mikataba ilikuwa ikifanyika na mingine inahusisha hadi mataifa ya nje. Kuna fedha zilitolewa, zikawekwa kwenye akaunti binafsi na siyo akaunti ya ALAT,” amesema.

Amesema ALAT ni taasisi kubwa ya Serikali ambayo inahitaji kuheshimiwa, na siyo ya kuancha iendeshwe na mtu mmoja kama atakavyo. “ALAT ni taasisi kubwana Serikali inaitegemea. Niwahakikishie kuwa Mheshimiwa Rais, anawathamini, anawapenda na anataka mchape kazi kuisaidia Serikali yenu,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bw. Suleiman Jafo alisema Serikali inajivunia ujenzi wa shule za sekondari za kata ambazo mwaka huu zimefanya vizuri kwenye mitihani ya kuhitimu kidato cha sita.

“Kati ya shule bora 100, shule 64 ni za Serikali na kazi ya shule hizo 64, shule 54 ni za kata. Na kwenye matokeo ya masomo ya sanaa, kati wanafuzi bora 10 wa kiume, wanafunzi saba wanatoka kwenye shule za kata,” alisema.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imewekeza sana kwenye sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari na ukarabati wa shule kongwe za sekondari.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kutenga sh. bilioni 268.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi 38 ya kimkakati kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kama vile ujenzi wa masoko, machinjio na stendi za mabasi.

STIEGLER’S GORGE HYDROPOWER PROJECT: REASONS BEHIND THE PROJECT, ITS FAR REACHING BENEFITS

Rais Dkt Magufuli mgeni rasmi Ufunguzi wa Maonesho Wiki ya Viwanda nchi za SADC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mageni rasmi katika ufunguzi wa maonensho ya wiki ya Viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5, 2019 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa ya maonesho ya wiki hiyo yatakaofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kukuza ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza masoko kwa nchi wanachama. 

“ Tayari washiriki 580 wameshajiandikisha kushiriki maonesho hayo na matarajio yakiwa washirki zaidi ya 1000 kutoka katika nchi wanachama wa SADC na tunachoangalia kwa sasa ni namna maonesho ya wiki ya viwanda yatakavyowanufaisha Watanzania kwani hii ni fursa ya wazalishaji wetu na wamiliki wa viwanda kutangaza bidhaa zao na kupanua wigo wa masoko katika nchi wanachama “ Alisisitiza Mhe Bashungwa 

Akifafanua Mhe Bashungwa amesema kuwa amani na mshikamano uliopo hapa nchini ni msingi wa maendeleo ya sekta ya viwanda na sekta mbalimbali hapa nchini hali inachangia kukuza ustawi wa wananchi na kujenga uchumi jumuishi. 

Faida za maonesho hayo ni pamoja na kukuza masoko, kuongeza na kupanua wigo wa uwekezaji katika sekta ya viwanda na pia kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi wanachama kupitia jukwaa la biashara litakalozinduliwa wakati wa wiki ya Viwanda. 

Aidha, Mhe Bashungwa amesema kuwa Tanzania kuwa mwanachama SADC na katika Jumuiya mbalimbali ni fursa ya wananchi kuongeza uzalishaji wenye tija unaolenga kukuza sekta ya Viwanda. 

Wiki ya viwanda itahitimishwa kwa washiriki kutembelea maeneo ya Viwanda jijini Dar es Salaam, ikiwemo eneo la ukanda maalum wa uwekezaji na kujionea utekelezaji wa shughuli za uzalishaji zinavyoendeshwa. 

Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika itafanyika kuanzia Julai 5 hadi 8 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 na 18 Jijini humo. 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za
maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo yaKusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi waKimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa nisehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

MWENGE WA UHURU 2019 WADHAMIRIA KUBORESHA SEKTA YA MAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MBIO za Mwenge wa Uhuru kiaifa 2019 zinazoongozwa na Mzee Mkongea Ali zimetembelea Kisima cha Gezaulole kilichojengwa mwishoni mwa miaka ya sabini kinachokarabatiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA.

Kisima cha Gezaulole kilisimama kufanya kazi mwaka 2010kutokana na kharibika mkwa pampu npamoja na ukarabati wa mabomba ambapo mwaka 2018 Manispaa ya Kigamboni iliomba uongozi wa DAWASA kufufua mradi huu ili utoe huduma ya maji kwa wananchi.

Mzee Mkongea amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji ili waweze kunufaika na miradi ya maji ya jamii ambapo katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitafa mwaka huu zimekusaidia kuoresha sekta ya maji pamoja na ushirikishwai wa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amewaonya wakandarasi wanaojenga miradi chini ya kiwango na wengine kuchelewa kuimaliza kwa wakati na kuwa suala hilo halitafumbiwa macho na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mkongea amesema, kuanzia mwaka 2006 hadi 2018 miradi 1659 imekamilika, na lengo la serikali kufikia 2020 wakazi wa vijijini asilimia 85 wanapata maji safi na salama na mijini kwa asilimia 95, ameongeza kwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 miradi 124 imekamilika kwa upande wa mijini na na kuna miradi mingine mikubwa inaendelea kutekelezwa chini ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mkongea ameweza kutembelea miradi mbalimbali ya DAWASA na wameridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo inayoongozwa naMhandisi Cyprian Luhemeja.

Akisoma taarifa fupi, Msimamizi wa mradi huo kutoka DAWASA Mhandisi Lilian Masilago amesema kuwa kisima kilichopo Gezaulole kina uwezo wa kuzalisha Lita za ujazo 24,000 kwa saa na miundo mbinu mingine iliyopo ni pamoja na matanki mawili yenye ujazo wa Lia 90,000 na lita 60,000.

Lilian amesema, kisima hiki kipo chini ya Manispaa ya Kigamboni na kimegharimu zaidi ya Milion 154 zilizotumika kwa mfumo wa Force Account kutoka DAWASA na Milion 3 kutoka Halmashauri kwa ajili ya ufufuaji wa Bustani.

“Mradi wa Kisima cha Gezaulole unatarajia kuhudumia wananchi takribani 8000 katika maeneo ya Gezaulole, Mbwa maji na Kibugumo na kufufuliwa kwa mradi huu ni katika kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye ndiye aliyeanzisha huduma hii ya majia pamoja na bustani ya Gezaulole wakati wa uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa,”amesema Lilian.

Aidha ameeleza changamoto mbalimbali katika mradi huo ikiwamo uvamizi wa eneo la tanki katika Mtaa wa Kizani ambapo tayari Halmashauri inalifanyia kazi.
 Msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Lilian  Masilago   akisoma taarifa  fupi ya mradi wa Kisima cha maji Gezaulole Kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali , kisima  hicho kitatoa huduma kwa wananchi 8000 baada ya kukamilika kwa ukarabati baaada ya kuharibika kwa pampu mwaka 2010.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akimtwisha mama ndoo kichwani baada ya kutembelea Tanki la maji lililopo eneo la Kizani linalopokea maji kutoka kwenye kisima cha Gezaulole.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akipanda mti kama kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere  katika Bustani ya Gezaulole wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 ilipotembelea mradi wa Kisima cha maji cha Gezaulole.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akizungumza na wananchi wa eneo la Kizani lilipo tenki la maji  wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 ilipotembelea mradi wa Kisima cha maji cha Gezaulole  
 Msimamizi wa Miradi ya Maji ya Jamii ww Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Charles Makoye akitoa maelezo ya Kisima cha Gezaulole kwa Kiongozi wa Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Ali Mkongea baada kutembelea leo.

Kisima cha Maji cha urefu wa Mita 24 na pampu iliyofanyiwa ukarabati na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka DAWASA.



OHOOOOOO....AJALI

$
0
0
Gari aina ya Rav4  imepiga mweleka na kuingia mtaroni  eneo la Mbezi barabra ya Morogoro   jijini Dar as Salaam leo, chanzo cha ajali hiyo hakikufahamika mara moja (Picha na Emmanuel Massaka Michuzi Tv)
Break Down likiwa tayari kwa kulinyanyua gari hilo toka mtaroni.







Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images