Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

Bibi kortini kwa kudaiwa kumuua Mjukuu wake

0
0
 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, imeelezwa kuwa, mtoto Naomi John (7) alifanyiwa ukatili uliopitiliza na bibi yake uliopelekea kifo chake.

WP 2265 Ditectivu Sajenti Mgeni amedai hayo leo mbele ya Msajili Pamela Mazengo alipokuwa akitoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Esther Lyimo ambae anatuhumiwa kumuua mjuu wake Naomi John Machi 25, 2017.

Akiongozwa na Wakili Cecilia Mkonongo kutoa ushahidi wake, WP Mgeni amedai, Machi 25,2017 alipigiwa simu na mkuu wa upelelezi Mbagala ambae alimtaarifu juu ya tukio la mauaji maeneo ya Tuangoma Kigambo na kumtaka alifanyie kazi.

Amedai Machi 26, 2017 alipoingia ofisini alilichukua jalada hilo na kulisoma ndipo akagundua kuwa kuna washtakiwa watatu katika kesi hiyo ambao wote ni wanawake. 

Ameendelea kudai kuwa, baada ya kulisoma jalada lile alienda eneo la tukio huko Tuangoma akiwa ameongozana na mtoto wake Victoria pamoja na askari Aloyce, ambapo baada ya kufika tulipogonga wakatoka vijana wawili ndani mmoja alionekana kuwa na miaka 7 na mwingine 13 hadi 14.

"Niliwauliza mama yupo mtoto huyo wa miaka saba (jina limehifadhiwa) akasema hayupo, ameenda wapi? ameenda hospitali, na baba je hayupo pia, wakati namuhoji mtoto yule shingoni alionekana kuwa na alama, nikamuuliza tena akasema ameumia, nikamuuliza na hapa kifuani hakijubu kitu alionekana kama anaona aibu kuongea, lakini nilipoendelea kumuangalia nikamuona mkononi anakidonda na kichwani alikuwa amevimba.

Ameendelea kudai kuwa, nilipomuuliza akamjibu kuwa mama yake mdogo alimpiga na fimbo, akadai, akaamua kumfunua shati  ndipo alikuta mwili mzima mtoto anamajeraha na makovu yaani mwili mzima alionekana kama ngozi ya kenge.

" Nilipomuangalia yule mtoto nilibaini hata yule aliyekufa atakuwa amefanyiwa ukatili kama huyu isipokuwa huyu hajafa".Nilimjulisha afande Walelo akasema niendelee na upelelezi ila mtoto yule niliyemkuta na majeraha niende nae kituoni.

Ameendelea kudai kuwa, alipotoka pale,  alienda kwa majirani ambapo alimkuta jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi ambae alipomueleza kuwa Naomi amefariki alilia sana, ndipo yeye akafanya kazi ya kumbembeleza  kabla ya kumuhoji.

"Mwanahamisi alinieleza kuwa, wale walikuwa ni majirani na mara nyingi alikuwa akimuona Esther akimpiga Naomi, Naomi alikuwa mtoto mdogo lakini alikuwa anafanya kazi za mtu mkubwa, ambapo alienda na kumuuliza mbona watoto unawapiga sana ndipo hapo ukawa mwanzo wa uhasama akawa akimsalimia haitiki.

Nae Koplo Joyce akitoa ushahidi wake mahakamani hapo amedai aliitwa kwenda Hospitali ya Temeke baada kupata taarifa kuwa kuna mtoto amefikishwa pale hospitali  akiwa Katika hali ambayo siyo nzuri na kwamba Dk. aiyempokea alibaini kuwa mtoto yule alishakufa masaa kadhaa nyuma Ila waliompeleka wanadai kuwa ni mgonjwa na walipomkagua alikuwa na majeraha ambayo siyo ya kawaida.


Amedai, alipomuhoji mshtakiwa majeraha na makovu yaliyokutwa kwenye mwili wa marehemu yalisababishwa na nini alimjibu " Mimi huwa nampiga pale anapokosea kwa utukutu wake"  nilipowauliza watu aliofuatana nao kumpeleka mtoto Naomi hospitali Victoria na Jackline  vitendo vya ukatili alivyokuwa anafanyiwq huyo mtoto hawakuwa wakiviona? Walimwambia "tulikuwa tunaviona ila mama ni mkali sana hata ukiongea nae haelewi".

Kwa upande wake Inspekta Salma Sechenzo akitoa ushahidi wake alidai wakati anamchukua mshtakiwa maelezo ya onyo alikiri kumchapa mtoto Naomi na kumfinya mara kwa mara na kila mara alopokuwa akimpiga alikuwa akirejea maeneo yale yale yenye majeraha.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, (Ijumaa) Mtoto wa miaka tisa aliezeza mahakamani hapo jinsi mama yake mdogo, Esther Lymo (mshtakiwa) alivyowatesa hadi mwenzake Naomi John (9)akapoteza maisha.

Mtoto huyo alidai alikuwa akiishi Dar es Salaam na mama yake mdogo ambaye pia ni mama yake wa ubatizo pamoja dada zake.
"Tulikuwa tunaishi pamoja na Junior, dada Sia na Naomi, Namfahamu Naomi John tulikuwa tunakaa naye pale pale, lakini yeye amezikwa.
Wakili:Naomi yuko wapi.
Mtoto:Amezikwa alipigwa mpaka akafa.
Wakili; Alipigwa na nani.
Mtoto: Alipigwa na mama yule pale.
Wakili:Alifanya nini akapigwa.
Mtoto:Alimwaga maji yakasambaa nyumba nzima akaambiwa ayafute.
Wakili:Aliyafuta.
Mtoto:Alianza kuyafuta, alipofika akafika sehemu akagoma kuendelea kufuta.
Wakili;Alipokataa ikawaje.
Mtoto;Mama mdogo akaanza kumpiga na fimbo ya mpera, alimpiga... zilikuwa fimbo nyingi hadi ikabakia moja.
Wakili;Elezea ilivyokuwa.
Mtoto;Mamdogo alimng'ata mgongoni akamnyanyua juu kisha akamwachia, akamweka katika maji akamtoa na kumweka barazani, akamwagia chai ya moto.
"Naomi alipoachiwa alianguka chini, alikuwa kachoka, akamchukua akampeleka ndani, alimpeleka bafuni akamtoa akaenda kumlaza kitandani, akamwashia feni, Naomi alikuwa kachoka sana.
"Aliniita mamdogo akanituma dukani nikanunue unga wa kumkologea uji, niliporudi dukani nilimkuta Naomi anatoka povu puani.
"Mama alienda kununua dawa, aliporudi alimkuta Naomi kafariki,"alidai.
Wakili:Ulijuaje kama Naomi kafariki.
Mtoto: Nilijua sababu wakina dada niliwaona wanalia, wakamchukua Naomi wakampeleka hospitali.
Alidai alibaki nyumbani na Junior, akafika mjomba wake Hamza akampa hela akanunue soda lakini naye mwilini alikuwa na makovu yaliyotokana na kupigwa na mama mdogo.
"Askari walinichukua wakanipeleka hospitali, nilikaa hospitali kesho yake nikapelekwa Kituo cha kulelea watoto yatima, nikiwa hospitali madaktari walinidanganya kwamba Naomi hajafa ili nisilie, waliniambia nitamuona lakini sijamuona tena,"alidai na kuongeza kwamba alioneshwa kaburi la Naomi.
Alipotakiwa kueleza kaburi ni kitu gani alisema ni shimo 
Mtoto huyo alinalowekwa jeneza lililotengezwa kwa mbao.
Mtoto Naomi hakuwa anakosa mara zote, mama mdogo alikuwa akimpiga hata yeye na ubapa wa panga fupi na kumfinya kwa kutumia kucha na kisu cha kukatia ugali.
Shahidi huyo aliiinesha mahakama kovu katika mkono wake lililotokana na kupigwa na ubapa wa panga.


Aidha shahidi wa pili, Daktari kutoka Temeke, DK.Abdulkarim Aljabir alidai alimpokea Naomi baada ya kuletwa na mshtakiwa Esther Lymo akidai malaria ilipanda kichwani naye alipewa taarifa ndio akamfata na kumkimbiza hospitali.
"Nilimsaidia kumfungua mgongoni mgonjwa, alikuwa amelegea sana, nikamlaza katika kitanda na kuanza kumchunguza.

"Nilipomchunguza nilibaini baadhi ya vitu haviko sawa, mapigo ya moyo hayakuwepo, msukumo wa damu haukuwepo macho na mdomo vilikuwa wazi, mboni ya jicho ilitanuka, ishara hiyo ilinijulisha kwamba alifariki zaidi ya saa nne zilizopita.

"Tulipomchunguza zaidi na madaktari wenzangu tulibaini, kichwani kulikuwa na uvimbe mkubwa sio wa muda mrefu uliotokana na kuvilia kwa damu kwa sababu ya kupigwa na kitu kizito kisichokuwa na ncha.

"Mdomo wa Naomi ulikuwa unakosa meno matatu yaliyoondolewa bila kufuata utaratibu wa ung'oaji wa meno hali iliyosababisha majeraha kwenye vizi na ulimi.

"Kifuani kulikuwa na majeraha mapya na ya zamani, mkono wa kulia ulivunjika mara mbili, bega la kulia liliteguka, tumbo lilikuwa halina chakula kabisa zaidi ya gesi, sehemu za siri kote kote kulikuwa na michubuka, mapaja yote mawili yalikuwa na vidonda na alama za kuungua moto,"alidai.

Daktari alitaja sababu ya kifo cha Naomi ni majeraha kichwani, bakteria katika mwili wake kwa kiwango kikubwa kisichotibika na alipata maumivu makali yaliyosababisha kushindwa kustahmili. Kesi hiyo inaendelea kesho.

DC Ndejembi - Rais Magufuli anatekeleza kwa vitendo aliyoyaahidi 2015

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi (pichani kati) amesema vijana nchini wanapaswa kumuunga mkono Mhe Rais Dk John Magufuli kwa jinsi alivyowaamini kwenye nafasi mbalimbali za uongozi

DC Ndejembi amesema kwa miaka mingi ilikuepo dhana ya vijana kuonekana hawana uwezo wa kuongoza lakini Mhe Rais Magufuli katika Serikali yake ya awamu ya tano ameteua vijana wengi kwenye uongozi kuliko awamu nyingine zote.

Amesema kwa maendeleo ambayo Rais Magufuli ameyaleta ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne anapaswa kuungwa mkono na vijana na siyo kulalamika pembeni.

Ndejembi ambaye pia amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho kupitia Umoja wa Vijana pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi amewataka vijana kumuunga mkono Rais Magufuli na kumsaidia kwenye utendaji wake wa kazi katika kuwatumikia wananchi.

" Mhe Magufuli ndiye Rais wetu na ndiye Mwenyekiti wetu ndani ya Chama, mapinduzi ambayo ameyafanya kwenye Nchi hii yanapaswa kupongezwa kwa kiwango kikubwa sana.

" Leo hii chini ya Rais Magufuli Tanzania imepiga hatua kwenye sekta ya usafirishaji, tunajenga reli ya kisasa kiwango cha Kimataifa (SGR), usafiri wa anga ulikua umekufa lakini tunavyozungumza Ndege zinapishana angani kutua viwanja vya Afrika Kusini na India. Ni lazima tumuunge mkono Jemedari wetu huyu," Amesema DC Ndejembi.

Aidha ameongeza kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Magufuli Wilaya anayoiongoza ya Kongwa imeletewa zaidi ya Shilingi Bilioni sita kwa ajili ya miradi ya maji vijijini, mtandao wa barabara ya lami unaogharimu Bilioni tano pamoja na mradi wa maji Kongwa ambao kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kilitengwa kufanikisha mradi huo wenye lengo la kumtua Mama ndoo kichwani.

" Ninapoona mtu analalamika ninashangaa sana, ndani ya kipindi cha miaka minne yamefanyika mambo makubwa ambayo kwa muda mrefu yalishindikana, uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye nishati na umeme ambapo mradi mkubwa wa Stiglers unajengwa, umeme umefika hadi kijijini na kule kukatika katika kwa umeme migao ya mara kwa mara imekwama.

" Rais Magufuli ameimarisha miundombinu ya barabara Nchi nzima, lami imetandazwa kwenye kila barabara lengo, sekta ya afya imepiga hatua sana tunapozungumza hivi sasa vituo vya afya vinajengwa Nchi nzima, hakika Mhe Rais anastahili kupongezwa," amesema DC Ndejembi.

Amempongeza Rais Magufuli kwa kusimamia nidhamu kwa watumishi wa umma huku pia akiongoza mapambano dhidi ya rushwa na dawa za kulevya.

" Hakuna mtu asiyejua namna ambavyo ilikua ngumu kuzuia biashara ya dawa za kulevya, lakini chini ya Rais Magufuli dawa za kulevya zimetokomezwa na ameaokoa kundi kubwa la vijana ambalo lilikua limeangamia kwa utumiaji wa dawa za kulevya." Sisi vijana tulioamiwa na Mhe Rais tuna jukumu zito la kumsaidia kazi, kutekeleza Yale yote ambayo amekua akihitaji kuona Watanzania wanyonge wananufaika na Nchi yao lakini pia ndani ya Chama chetu cha CCM tuko imara chini ya Mwenyekiti wetu Dk John Magufuli, " Amesema DC Ndejembi.

Amewataka vijana na viongozi walioko ndani ya CCM kushikamana na kumuunga mkono Rais Magufuli ambaye tangu aingie madarakani ametekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi yake ya elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

MBUNGE KINGU AKAGUA UJENZI WA SHULE YA MSINGI BUNKU NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

0
0
 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana  Kitongoji cha Bunku kilichopo Kijiji cha Mayaha  Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Msingi na kuahidi kuendelea kusaidia ujenzi kwa kutoa mifuko ya saruji 120 na mabati.
 Burudani zikiendelea kwenye mkutano huo
 Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata hiyo Paul Hema akizungumza kwenye mkutano huo,






BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 22.07.2019

WAZIRI JENISTA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na waombolezaji wakati alipowaongoza katika Ibada na kuaga mwili wa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Richard Kalinga, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma, Julai 22, 2019. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mohammed Kiganja.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akitoa pole kwa familia ya mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Richard Kalinga, baada ya kuwaongoza waombolezaji katika Ibada ya kumwombea marehemu na kutoa heshima za mwisho, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma Julai 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UJENZI WA MAHANDAKI RELI YA KISASA - SGR WAANZA RASMI MKOANI MOROGORO

0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Atashasta Nditiye azindua rasmi uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki ‘tunnels’ yatakayopitisha reli ya Kisasa – SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro  hivi karibuni .

Jumla ya Mahandaki 4 yenye jumla ya urefu wa Kilometa 2.6 yanatarajiwa kujengwa katika Mradi wa SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa ambapo handaki refu zaidi nchini linatarajiwa kujengwa likiwa na urefu wa Kilometa 1.031 sambamba na mahandaki mengine matatu ambayo yote kwa pamoja yataunganishwa na madaraja makubwa ili kuepusha athari za mafuriko ya mto mkondoa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mbunge wa Kilosa, Menejimenti na Wafanyakazi wa TRC na Yapi Merkezi, wanahabari pamoja na wananchi wa wilaya ya Kikosa katika Milima ya Kilosa mkoani Morogoro. 

Waziri Nditiye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kwa Usimamizi mzuri wa Miradi na kuwataka waendelee kuchapa kazi ili kuleta tija na mtokeo mazuri katika utoaji huduma bora za usafiri wa reli.

Aidha Naibu Waziri amewashukuru wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano wanaoonesha kwa wakandarasi na TRC, pia amewatoa hofu wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kuwa endapo serikali itahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi, mwenye eneo atalipwa fidia pamoja na stahiki nyingine anazostahili kulipwa.

“Napenda niwahakikishie watanzania, kwa Yule amabaye tutamfuata kwenye eneo lake tutamlipa fidia yake” Amesema Mhe. Atashasta

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa ameongeza kuwa uthaminishaji wa ardhi ili kukabidhi maeneo yaliyobaki wa mkandarasi unaendelea na majedwali ya fidia yanafanyiwa kazi.
  Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano,Mh. Atashasta Nditiye akikata utepe jana julai 22,2019 kuashiria kuanza rasmi kazi ya uchorongaji  milima kwa mara ya kwanza Shirika la Reli Tanzania kwa ajili ya mahandaki ambayo watatumia kupitisha reli ya kisasa-SGR kwa kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa Morogoro- Makutupora katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano,Mh. Atashasta Nditiye akipewa maelezo baada ya kukata utepe jana julai 22,2019 kuashiria kuanza rasmi kazi ya uchorongaji  milima kwa mara ya kwanza Shirika la Reli Tanzania kwa ajili ya mahandaki ambayo watatumia kupitisha reli ya kisasa-SGR kwa kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa Morogoro- Makutupora katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Muonekano rasmi uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki ‘tunnels’ yatakayopitisha reli ya Kisasa – SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro 

WAZIRI MKUU: TUMIENI FURSA ZA UTALII KUBORESHA MAISHA YENU

0
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Julai 21, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa bwana Francis Theodosia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao.

“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili. Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la polisi kwa ajili ya patrol ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.


Waziri Mkuu alizindua kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido). 

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.” 

Aliwataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi. 

Pia aliwashukuru viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu. Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20. 

“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema. 

Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi ya 10 yamesimamishwa njiani. 

“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo, akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke juani wakati mwenye makosa ni dreva?” 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata hukohuko,” alisema. 


Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini.

ZOEZI LA USAJILI WA NGO's ZILIZOSAJILIWA WALI KATIKA SHERIA NYINGINE WAENDELEA KWA KANDI YA KATI DODOMA


PROF.MKENDA:TAMASHA LA URITHI FESTIVAL KUFANYIKA PAMOJA NA JAMAFEST MWAKA HUU

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (kulia) akitoa tamko la kuridhia kuunganishwa kwa Tamasha la Urithi Festival kwa mwaka kufanyika pamoja na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika (JAMAFEST) mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (kushoto) wakati wa kikao kilichofanyika leo jijini Arusha, kujadili namna ya matamasha haya yanaweza kuunganishwa kwa sababu yote yana dhana moja ya kutangaza Utalii wa Kiutamaduni na tarehe za maadhimisho ziko sawa mwezi Septemba 21- 28 jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (kushoto) akitoa shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (kulia) baada ya kuridhia kuunganishwa kwa Tamasha la Urithi Festival kwa mwaka huu kufanyika pamoja na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika (JAMAFEST) katika kikao cha makubabaliano kilichofanyika jijini Arusha leo cha kushirikiana kuadhimisha Tamasha la Urithi kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Jamafest Tanzania Bibi.Joyce Fissoo akitoa ufafanuzi wa kuwepo kwa takribani programu kumi na moja za Kiutamaduni katika Tamasha la JAMAFEST katika kikao cha ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuandaa Tamasha la Urithi Festival kilichofanyika leo Jijini Arusha. 
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Urithi Festival Prof.Martin Mhando akiwapongeza makatibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo baada ya kuridhia kuungana na kufanya pamoja Tamasha la Urithi Festival katika kipindi cha maadhimisho ya Tamasha la JAMAFEST litakalofanyika jijini Dar es Salaam, katika kikao kilichofanyika jijini Arusha leo,kwani kushirikiana kwa mwaka huu kutasaidia kuongeza ubunifu kwa Tamasha la Urithi Festival mwakani,kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Jamafest Tanzania Bibi.Joyce Fissoo. 
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (watatu kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Maandalizi ya Tamasha la Urithi Festival na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika (JAMAFEST) mara baada ya kikao cha maridhiano ya kuunganisha matamsha hayo kufanyika pamoja kwa mwaka huu kutokana na matamasha hayo kuwa na dhana moja ya kutangaza utalii wa Kiutamaduni na kuwa katika ratiba moja ya tarehe za maadhimisho. 
………………… 
Na Anitha Jonas – WHUSM 
Arusha. 
Tamasha la Urithi Festival kwa mwaka huu kufanyika pamoja na Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika (JAMAFEST) jijini Dar es Salaam. 

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda alipokuwa akifanya kikao cha pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi kuzungumza namna ya Wizara hizo zitakavyoweza kuungana kuandaa Tamasha la Urithi kama ilivyokuwa imeagizwa na Waziri Mkuu. 

“Kwa mwaka huu itakuwa vyema kuyaunganisha matamasha haya mawili kwani yote yana lengo moja la kutangaza Utalii wa Kiutamaduni, na tarehe za uendeshwaji wa matamasha hayo zipo sawa” Prof.Mkenda. 

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Prof.Mkenda alisema kwa sasa sekta ya utalii inataka kuongeza wigo zaidi na kutangaza utalii kwa Kiutamaduni ikiwemo Vyakula vya Asili,Ngoma,Mila na Desturi za Makabila mbalimbali, lengo ikiwa ni kuonyesha ulimwengu utajiri wa Utamaduni uliyopo Tanzania,kama nchi za wenzetu wa India na China wanavyofanya. 

Halikadhalika kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuridhia matamasha hayo kuunganishwa kwani lengo ni moja la kutangaza sekta ya Utalii wa Utamaduni wa Taifa. 

Pamoja na hayo Bibi.Mlawi aliendelea kufafanua kuwa Tamasha la JAMAFEST huandaliwa na kila baada ya miaka miwili na kwa mwaka huu Tanzania ndiyo mwenyeji na wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ndiyo mwenye jukumu la kuandaa tamasha hilo kwa sasa kama wizara yenye dhamana ya Utamaduni. 

“Tamasha hili la JAMAFEST ni kubwa na tunatarajia kuwa na washiriki zaidi ya elfu moja kutoka nchi za wanachama wa Jumuiya, katika tamasha hili kutakuwa na matukio mbalimbali ambayo yataongeza chachu kwa Sanaa za Ufundi,Maigizo ya Jukwaani,ziara ya kutembelea vivutio vya Utalii,ambapo kila nchi wanachama itateua mtu mmoja wa kwenda kutembelea vivutio hivyo,” alisema Bibi.Mlawi. 

Halikadhalika tamasha hilo linauwezo wa kutengeneza jukwa zuri ambalo litatangaza filamu za kiutalii za taifa kupitia shindano la Serengeti Film Festival ambalo nalo litafanyika wakati huo. 

Naye mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Urithi Festival Prof.Martin Mhando alisema kuunganishwa kwa matamasha haya mawili kutusaidia zaidi kutangaza utalii wa Utamaduni na pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa sekta ya utalii itapata fursa ya kunadi bidhaa za Kiutamaduni ikiwemo vinyago na michoro mbalimbali. 

Halikadhali naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Jamafest Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alisema tamasha hilo litakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo maonyesho ya vyakula vya asili kutoka nchi wanachama,Sanaa za Ufundi,Mashindano ya Michezo ya Jadi na Maonyesho ya Mavazi ya Kiutamaduni.

DC CHAMWINO AWATAKA MAKOCHA WA TIMU ZA TAIFA KUFIKA VIJIJINI

0
0

NA Charles James, MICHUZI TV

MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga amesema kuna haja ya walimu wa timu za Taifa kuangalia vipaji ambavyo vinapatikana maeneo ya vijijini.

Hayo ameyatoa wakati akifunga mashindano ya Buchimwe Cup yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Buigiri ambapo mchezo wa fainali ulizikutanisha timu za Buigiri Mission na Songambele.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema vijijini kumekuwa na vipaji vya hali ya juu lakini anakosekana mtu wa kuwashika mkono hivyo akawaomba walimu wa timu za Taifa kuifika katika maeneo hayo.

“Waje na hapa kwetu Chamwino kuna vipaji vya hali ya juu naamini hata wale Algeria waliochukua AFCON kupitia vipaji hivi ninavyoviona hapa wasingeweza kutufunga,”amesema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi ambaye ndie muandaaji wa mashindano hayo amesema ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ya Michezo wilayani humo ili kukuza vipaji vya vijana kwani Michezo imekua ni ajira kubwa iliyobadilisha maisha ya vijana wengi.

" Mhe DC tunakushukuru sana kwa kufika pamoja na kufanikisha mashindano haya bado tunakabiliwa haswa na uhaba wa viwanja pamoja na vifaa vya Michezo, tuwaombe Serikali kuwekeza Kwa nguvu pia huku vijijini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi," amesema Mhe Yindi.

Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa,Joel Mwaka (CCM),Buigiri Mission waliibuka na ushindi wa Penalti 3-1 dhidi ya Songambele mara baada ya dakika 90 timu hizo kutoka sare ya kutofungana.

Jina la mashindano hayo,Buchimwe ni muunganiko wa herufi za mwanzo za vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Buigiri ambavyo ni Chinangali 11,Buigiri na Mwegamile.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Vumilia Nyamoga akimkabidhi Kombe Nahodha wa Timu ta Buigiri Mission baada ya kutwaa taji la mashindano ya Buchimwe,

 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Vumilia Nyamoga akikagua kikosi cha Timu ya Songambele kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya Buchimwe Cup

WAZIRI MPINA AWAPIGA NYUNDO NZITO WANAOKULA NJAMA ZA KUMHUJUMU RAIS MAGUFULI

0
0
Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Charles Mazuri (katikati) akimpokea Kiongozi maarufu wa CHADEMA Jimbo la Kisesa, Chekinorisi baada ya kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi. Kushoto ni Mbunge wa Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
Mbunge wa Kisesa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa jimbo hilo katika mkutano uliofanyika Kata ya Tindabuligi.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi jimboni Kisesa kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM na mwelekeo ya Serikali ya awamu ya tano.
Wananchi wa Jimbo la Kisesa wakimpokea Mbunge wao, Luhaga Mpina wakati akiwasili uwanja wa mkutano katika Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi kuwaelezea wananchi juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano.
Wananchi wa Jimbo la Kisesa wakisalimiana na Mbunge wao Luhaga Mpina wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi


Na Mwandishi Wetu, Simiyu 

MBUNGE wa Jimbo la Kisesa (CCM) Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina amewashukia baadhi ya watu waliowahi kupewa nyadhifa za juu serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi kuendesha mikakati na kula njama za kutaka kumuondoa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye ajenda kuu ya kuwahudumia wananchi na kutaka taifa lijadili mambo ya watu binafsi.

Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jimbo la Kisesa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi na kuhudhuriwa na wananchi wote wa jimbo hilo, Mpina amesema watanzania wanaimani kubwa na Serikali ya awamu ya tano na kwamba mikakati na njama hizo kamwe hazitafanikiwa.

Mpina amesema viongozi hao hao waliowahi kupewa nafasi za juu ndani ya CCM na Serikali lakini watanzania walishuhudia usimamizi dhaifu wa shughuli za chama na kusababisha makundi makubwa ya viongozi na wanachama kuhamia vyama vya upinzani na kuisababishia CCM na Serikali kuchukiwa na wananchi.

Mpina amesema baada ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. Magufuli kufanikiwa kusuka upya mifumo, kufumua mikataba na sheria mbalimbali na kuongeza udhibiti na usimamizi wa rasilimali za nchi pamoja na kupambana na rushwa kwa vitendo na kukomesha mambo machafu yaliyokuwa yanaumiza wananchi ndio wanaibuka watu wachache kutoa waraka na kutaka kuwahamisha wananchi kwenye ajenda kuu ya maendeleo ili wajadili mambo binafsi kwa masilahi yao.

“Walanguzi na wala rushwa waliokuwa wanaiba fedha za taifa hili wamedhibitiwa, mishahara hewa ililipwa miaka nenda rudi viongozi wakawa wanaimba mishahara hewa kana kwamba hakuna mtu aliyetakiwa kuchukua hatua leo Mheshimiwa John Pombe Magufuli amekuja mishahara hewa yote imekuwa historia” alisema Mpina.

Pia amesema Rais Magufuli amerekebisha mifumo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya madini hali iliyowezesha Serikali kuwa na hisa kwenye migodi hiyo ambapo sasa Serikali inapata mabilioni ya fedha kutoka kwenye madini, rasilimali zetu zilikuwa zinaibwa kana kwamba hakuwepo mtu wa kuchukua hatua.

“Uvuvi haramu kila kona samaki walikuwa hakuna Taifa lenye maziwa makubwa kuliko nchi yoyote Afrika na Dunia Taifa lenye bahari samaki tunanunua za kutoka nje Mh. Magufuli akasema uvuvi haramu hapana Mpina nenda pale kakomeshe uvuvi haramu, uvuvi haramu umekoma nchi hii wananchi wanakula samaki wengi na wakubwa kila sehemu na mauzo ya nje yameongeka ”alisema Mpina

Mpina amesema mambo mengine makubwa yaliyosimamiwa na Rais Magufuli ni pamoja na kudhibiti utoroshaji fedha nje ya nchi, biashara ya dawa za kulevya, matumizi ya pombe za viroba, utoroshaji magogo nje ya nchi, uingizaji holela wa bidhaa toka nje na kuua viwanda vya ndani, mikopo ya serikali, matumizi holela ya fedha za umma yote yameshughulikiwa na Serikali ya awamu ya tano.

“Sasa wengine wanaanza kujitokeza na mawaraka yao wataendelea kuyasoma wenyewe watanzania wako bize na maendeleo hawahitaji waraka hatuhitaji waraka sisi, sisi tunahitaji umeme wa uhakika, sisi tunahitaji elimu bora na maji, sisi tunahitaji soko na bei nzuri ya pamba, sisi tunahitaji malisho ya mifugo, sisi tunahitaji usafirishaji wa uhakika treni, ndege, barabara, madaraja na viwanda, sisi tunahitaji hospitali nzuri, tunahitaji dhuluma zote dhidi ya wananchi zikomeshwe, mambo hayo Mhe. Magufuli amekuwa akishughulika nayo kufa na kupona.. sisi hatuhitaji waraka…..waraka wakasome wao na familia zao “alisema Mpina na kuungwa mkono na wananchi.

Amesema mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake Tanzania haita msahau na Wana CCM hawatamsahau kwa juhudi kubwa alizofanya za kuweka mifumo imara ndani ya Serikali na CCM.

“Kama ni kwenye chama nani katika historia ya nchi yetu aliyeweza kufanya kama Mh. John Pombe Magufuli nani katika utawala ambaye ameweza kurudisha wabunge 10, madiwani 200 na halmashauri 4 kutoka upinzani na kujiunga na CCM, huyo ndiye Mhe. John Pombe Magufuli Rais wa wanyonge na hata wagombea wenyewe wa urais kukimbia vyama vyao na kujiunga na CCM rekodi hii haijawahi kuvunjwa na kiongozi yoyote ” alisema Mpina.

Hivyo akawataka watanzania wote waendelee kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli ndani ya CCM ndani ya Serikali ili aendelee kupambania maendeleo ya watanzania na kwamba mambo mengi yaliyoshindikana yanatekelezwa katika kipindi chake cha Serikali ya awamu ya tano.

Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi amewahakikishia wafugaji na wavuvi wote nchini kuwa wako kwenye mikono salama na kwamba Serikali ya Rais Dk. Magufuli iko macho na iko kazini muda wote kushughulikia changamoto zao ili ufugaji na uvuvi uwe na tija na kuleta masilahi makubwa kwa taifa.

Akisoma risala ya wananchi wa Jimbo la Kisesa, Diwani wa Kata ya Tindabuligi, Antony Maghembe alisema wananchi wa jimbo hilo wanamuunga mkono Dk. Magufuli na kumshukuru na kumpongeza kwa kazi kubwa ya kupambania maendeleo ya watanzania, kukomesha dhuluma na kwamba kazi anayoifanya ina Baraka za Mungu na Baraka za wananchi wote.

HIVI NDIVYO UJENZI MAHANDAKI RELI YA KISASA ULIVYOZINDULIWA

RAIS DKT.MAGUFULI AAGIZA MKURUGENZI MKUU TPDC KUREJESHWA KAZINI

DC KISARAWE ATOA NENO KUFUATIA KUNASWA KWA MTUHUMIWA ALIYEKUWA AKITUMIA JINA LAKE KWA UTAPELI

0
0
Kipekee naomba nimshukuru Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz kupitia Kitengo cha CYBER CRIME kwa kufanikisha kumnasa mtuhumiwa wa utapeli ambae amekua akijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Amefungua ukurasa Facebook kwa jina langu na kudanganya watu kuwa ninatoa mikopo Kwa njia ya Saccos / Viccoba na hivyo wamtumie fedha Huyu Mtuhumiwa kwenye picha kupitia namba 0713924045 jina lake ni Abdalah Mbanjo ya kuomba mikopo na akiba ya asilimia kumi ya mikopo wanayoomba.

Kwa mara nyingine napenda kuijulisha jamii kwamba sina taasisi yoyote ile inayotoa mikopo na watoe taarifa kituo chochote cha polisi iwapo mtu yoyote au taasisi yoyote itatumia jina langu au ofisi ya DC wa Kisarawe kujipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya mtuhumiwa huyu kutiwa nguvuni ilibainika kuwa yapo makundi mengine mengi ambayo yanatumia jina langu kujipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu.

Na yote tumeshafahamu yalipo. Nalishukuru Jeshi la Polisi Kwa kuwa wamejipanga kuwasaka popote walipo nchini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na wote wanaotumia jina langu vibaya kwenye mitandao tutawachukulia hatua kali.

Mwisho ila sio kwa umuhimu Namshukuru na Kumpongeza IGP Sirro kwa kuwa na jeshi la polisi makini lenye kufanya kazi kwa weledi.- Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Mtuhumiwa  Abdalah Mbanjo 


Wananchi Lindi Wanufaika na Kivuko cha MV Kitunda


HAPA KAZI TU BY NGOMA AFRIKA BAND FROM GERMANY

SENSEI RUMADHA FUNDI AZIDI KUPAA KATIKA KARATE MTINDO WA GOJU RYU, AFUZU DARAJA LA TANO WAKATI WA SEMINA YA MA-SENSEI WA DUNIA NZIMA HUKO AUSTRIA

0
0
Kiongozi mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania Sensei Rumadha Fundi akipokea chetu cha ufauru wa GO DAN (mkanda mweusi daraja la tano) toka kwa Sensei Kancho Miyazato, Mkuu wa karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu Duniani.
Sensei Rumadha anakuwa anakuwa Mtanzania wa Kwanza kufika ngazi ya juu yenye uthibitisho toka makao makuu ya Jundokan Goju Ryu Karate do huko Okinawa, Japan. 
Sensei Rumadha anakuwa  Mtanzania wa Kwanza kufika ngazi ya juu yenye uthibitisho toka makao makuu ya Jundokan Goju Ryu Karate do.
Hivi karibuni Sensei Rumadha alikuwepo nchini ambako baada ya kuendesha mafunzo kwa wanafunzi waandamizi aliwapandisha vyeo wanafunzi kadhaa katika Dojo lake la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania.
Kiongozi mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania Sensei Rumadha Fundi akipokea chetu cha ufauru wa GO DAN (mkanda mweusi daraja la tano) toka kwa Sensei Kancho Miyazato, Mkuu wa karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu Duniani huko Vienna, Austria, wakati wa semina ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki.
 Kiongozi mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania Sensei Rumadha Fundi akiwa na cheti cha ufauru wa GO DAN (mkanda mweusi daraja la tano) alichopokea toka kwa Sensei Kancho Miyazato  Mkuu wa karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu Duniani (wa pili kulia) huko Vienna, Austria, wakati wa semina ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki.


 
 Kiongozi mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania Sensei Rumadha Fundi akiwa mazoezini na ma-Sensei wenzake toka sehemu mbalimbali duniani  baada ya kutunukiwa cheti cha ufauru wa GO DAN (mkanda mweusi daraja la tano) toka kwa Sensei Kancho Miyazato wakati wa semina yao huko Vinenna, Austria, mwishoni mwa wiki



Kiongozi mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Goju Ryu Karate Tanzania Sensei Rumadha Fundi (kushoto kati) akiwa katika picha ya pamoja na ma-Sensei wenzake toka sehemu mbalimbali duniani  baada ya kupokea cheti cha ufauru wa GO DAN (mkanda mweusi daraja la tano) toka kwa Sensei Kancho Miyazato wakati wa semina yao huko Vinenna, Austria, mwishoni mwa wiki

WAZIRI MKUU AAGIZA ENEO LA MNARA WA ZINJATHROPOUS LIBORESHWE

MWENYEKITI WA BARAZA LA USHAURI LA BUNGE LA ZHEJIANG, CHINA ATEMBELEA BUNGE LA TANZANIA

0
0
 Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza kwa niaba ya Mhe. Spika na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Zhejiang  lilopo nchini China, Mhe. GE  Huijun na Ujumbe wake Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Zhejiang  lilopo nchini China, Mhe. GE  Huijun akimuelezea jambo Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati wa kikao katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Zhejiang  lilopo nchini China, Mhe. GE  Huijun na Ujumbe wake Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Zhejiang  lilopo nchini China, Mhe. GE  Huijun na Ujumbe wake Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu ( wanne kutoka kulia) katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Zhejiang  lilopo nchini China, Mhe. GE  Huijun (wanne kutoka kushoto) wengine katika picha ni wasaadizi wa Viongozi hao. PICHA ZA BUNGE

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la jimbo la Zhejiang nchini China

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wafanyabiashara katika jimbo la Zhejiang, China jimbo embalo ni la nne kwa uchumi miongoni mwa majimbo ya China.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiendelea kuzungumza na Mhe. Bi. GE Huijun pamoja na ujumbe alioambatana nao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Bi. GE Huijun ambaye alionekana kuifurahia sana.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images