Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Serikali ya Zanzibar yaanza utekelezaji wa uimarishaji wa Miundombinu katika Sekta ya Elimu

0
0
 Muonekano wa Jengo Jipya la Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Sekondari ta Kilindi linalojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
  Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Maalim Mohamed Nassor akitoa Taarifa ya ujenzi wa Mabara ya Sayansi Skuli ya Kilindi mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kukagua Ujenzi huo.
 Balozi Sdeif akiambatana na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullah akiangalia ujenzi wa Maabara ya Sayansi Skuli ya Sekonmdari ya Kilindi Mkoa wa Kusini Pemba.
 Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdulla akiishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazochukuwa za kusogeza maendeleo ndani ya Mkoa huo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kilindi na Vitongopji vyake baada ya kulikagua Jengo la Maabara ya Sayansi katika Skuli ya Kijiji hicho.
 Balozi Seif akizungumza na Viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa Miwili ya Pemba kwenye Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake Pemba kujadili zoezi la uhakiki wa kuyatambua mashamba na Eka za Serikali.
Balozi Seif akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi wa Kamati za ulinzi na Usalama za Mikoa Miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba hapo Ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chakle Pemba. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa msingi wa uimarishaji wa Miundombinu katika Sekta ya Elimu kwenye Fani ya Sayansi ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia yaliyopo Ulimwenguni.

Alisema utekelezaji huo umezingatia muelekeo wake katika Ujenzi wa Majengo 24 ya Maabara ya Sayansi { School Hurb } katika Visiwa vya Unguja na Pemba yatakayojikita na masomo ya Kemia, Fizikia na Biology.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo mwanzoni wa ziara yake ya Siku Nne Kisiwani Pemba kuangalia Miradi ya Maendeleo pamoja na ufuatiliaji wa Mashamba na Eka tatu tatu ambazo bado haliko kwenye Miliki ya Serikali.

Alisema wakati umefika kwa wanafunzi wa Skuli za Sekondari Unguja na Pemba kuchangamkia fursa hiyo ambayo katika siku za baadae itaweza kuziba pengo la upungufu wa Wataalamu wa Fani ya Sayansi hapa Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameridhika na kiwango kizuri cha Ujenzi kilichofikiwa na Wahandisi wa Majengo hayo Kampuni ya Kizalendo ya Salim Contructor na kuzitaka Kampuni nyengine zitakazopewa jukumu la ujenzi wa Majengo ya Serikali na Taasisi za Umma kuzingatia ubora wa kiwango kinachokubalika.

Akitoa Taarifa ya Ujenzi wa Maabara ya Sayansi ya Skuli ya Kilindi Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Nd. Mohamed Nassor alisema Maabara hiyo ni miongoni mwa Majengo 24 yanayoendelea kujengwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Nd. Mohamed alisema Maabara ya Sayansi {Shool Hurb} yameanzishwa kama vituo vya kutoa huduma katika masomo ya Sayansi likiwemo pia somo mama la Kingerezakwa Wanafunzi hasa waliko Vijijini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa fursa hizo.

Akitoa salamu Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema Wananchi wa Mkoa huo wanafurahia Maendeleo makubwa yanayopatikana chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.

Alisema huduma za Maji safi na salama, Umeme Bara bara za Lami pamoja na miundombinu ya Miradi ya Kiuchumi imekuwa ikileta matumaini ya kuongezeka kwa Kipato cha Wnanchi hao jambo ambali limestawisha Maisha yao ya kila siku.

Mh. Hemed alisema Wananchi wana kila sababu ya kujivunia maendeleo hayo makubwa yanayoonekana kila pembe katika dhana nzima ya Utekelezaji wa vitendo wa ahadi zilizotolewa na Serikali ikiwemo kuwasili kwa vifaa vya kutengenezea Miundombinu ya Mawasiliano Kisiwani Pemba.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana na Viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa Miwili ya Pemba katika Ukumbi wa Mikutano wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ulijadili na kutafakari hatua zilizochukuliwa na Taasisi mbali mbali Kisiwani Pemba zilizopewa jukumu la kufuatilia na kubaini Mashamba na Eka za Serikali ambazo kwa kipindi kirefu ziko mikononi mwa Watu.

Akitoa Taarifa ya zoezi hilo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo, Malisili, Mifugo na Uvuvi Pemba Nd. Sihaba Haji Vuai alisema Wizara hiyo imekabidhiwa Madaftari yenye takwimu za Mashamba na Eka za Serikali tokea Mwaka 20113.

Alisema vielelezo vilivyomo ndani ya Mabuku hayo Matatu vimeainisha uwepo wa Mashamba na Eka 2,438 Wilaya ya Mkoani, eka 2,299 Wilaya ya Chake chake na Ekari 2,273 Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Nd. Sihaba alisema Watendaji wa Wizara ya Kilimo ilianza zoezi la kuyafuatilia Mashamba na eka za Serikali katika maeneo mbali mbali kwa kushirikiana na Masheha wa Shehia zilizomo Shamba na Eka hizo.

Alisema zoezi hilo liliweza kubaini uwepo wa Eka 838 Wilaya ya Mkoani, eka 295 Wilaya ya Chake chake, eka 992 Wilaya ya Wete na eka831 katika Wilaya ya Micheweni.

Alifahamisha kwamba mashamba yote ya Serikali yaliyomo ndani ya mikono ya Watu yamekadiriwa kufikia 9,982, ambapo hadi sasa yaliyobainika hadi sasa ni mashamba 6,315 sawa na asilimia 63% ya mashamba yote Kisiwani Pemba.

Afisa mdhamini huyo wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugona Uvuvi Pemba alieleza kwamba uchambuzi wa mashamba na eka hizo umefafanua kwamba Mashamba 2016 yana miti ya Mikarafuu, mashamba 721 miti ya Minazi, 1,884 mazao mchanganyiko, 365 yameachwa muda mrefu, 600 yamegeuzwa kuwa Makaazi na 1200 mashamba yaliyofungishwa Mkataba.

Alisema Mashamba yapatayo Mia 732 yako kwenye utaratibu wa kutaka kugaiwa kwa Wananchi kwa shughuli za kuendeleza Kilimo ili kusaidia kunyanyua kipato chao kitakachokidhi maisha yao.

Nd. Sihaba alisema utayari mdogo wa baadhi ya Viongozi, Taasisi za Umma pamoja na Wananchi ndio unaopelekea baadhi ya Eka walizopewa Wananchi kwa shughuli za Kilimo kugezwa matumizi mengine jambo linalokwenda kinyume na malengo ya utolewaji wa Eka hizo mnamo Mwaka 1964.

Wakichangia Taarifa hiyo Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho walisema Viongozi wanaosimamia zoezi hilo lazima wawe tayari kufuatilia kwa kina mashamba hayo na kuondoa muhali unaopelekea kuzorotesha zoezi hilo muhimu.

Walisema ipo haja ya kufuatilia kwa kina kuanzia ngazi ya Mtaa, shehia hadi Jimbo ili kuibaini Mashamba na Eka ambazo hadi sasa ziko ndani ya mikoni ya baadhi ya Watu.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema zoezi hilo la kubaini mashamba na eka za Serikali zilizo mikononi mwa Watu halina lengo la kuwanyang’anya wale wanaoendelea kuzitumia badhi kinachofanyika ni utambuzi wa kujua mali za Serikali.

Balozi Seif alisema wapo baadhi ya Wananchi katika maeneo tofauti Nchini wanayashughulikia mashamba na Eka za Serikali na unapofika wakati wa mazao wao ndio wanaopewa nafasi ya kwanza kukodi hasa katika upande wa zao la Karafuu.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba Serikali haitasita kuchukuwa hatua za kunyang’anya Eka ya Serikali Mtu ye yote atakayebainika kuificha mali ya Serikali.

ALLY CHOKI ‘MZEE WA FARASI’ ASIYEKATA TAMAA.

0
0
Na: Moshy Kiyungi

Jina la Ally Choki siyo geni masikioni mwa washabiki na wapenzi wa muziki, anayetamba kwa kipindi kirefu Afrika Mashariki kupitia tungo nauimbaji wake.

Baada ya kuonesha vituko vingi kwenye kumbi mbalimbali,  baadhi ya washabiki wake walimpachika walimuita “Mzee wa Farasi” au “Mzee wa Kijiko”. Choki kila bendi aliyopita kupiga muziki, aondokapo huacha simanzi kubwa kwa wanamuziki wenziwe, washabiki na wapenzi wa muziki wa dansi.

Ni mwenye vipaji vingi vilivyojengeka kichwani mwake vikiwemo vya kutunga, kuimba pamoja na uongozi.

Historia yake katika muziki Choki iliieleza kwamba alianza muziki rasmi mwaka 1988, alipojiunga katika bendi ya Lola Africa. Baadaye akajiunga na bendi ya Mwenge Jazz iliyokuwa chini ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Hakudumu kwa kipindi  kwani baada ya miezi sita alihamia katika bendi ya Bantu Group iliyokuwa ikiongozwa na ‘Komandoo’ Hamza Kalala.

“Mwaka 1990 nikiwa Bantu na Hamza Kalala akiwa kiongozi tulitoa albamu ya Baba Jane. Mwaka 1991 nilitoka Bantu, nikajiunga na Legho Stars chini ya uongozi wa Tshimanga Kalala Assosa...” alisema Ally Choki

Safari ya kusaka mafanikio ilikuwa ikisababisha kwenda huku na kule ambapo huko Legho Stars, nako hakudumu sana akaamua kurudi katika bendi ya Bantu Group.

Choki alikuwa mithiri ya Kunguru kwani  huko nako hakukaa sana, akaenda kujiunga na  bendi ya Bendi ya MK Beat ‘Tukunyema’ iliyokuwa ikiongozwa na Shem Ibrahim Kalenga.

Mwaka 1992 alihamia katika bendi ya Washirika Stars ‘Watunjatanjata’ ambako walitoa albamu iliyopewa jina la Gubu la Wifi. Pale walikuwa na mwimbaji mahiri Adam Bakari ‘Sauti ya Zege’, mpapasaji Kinanda Abdul Salvado ‘Father kidevu’ na wengine wengi.


Katika harakati za kusaka maisha Ally Choki aliamua kuvuka mpaka wa nchi nakuingia  katika jiji la Nairobi, nchini Kenya mwaka 1994, ambako aliungana na wanamuziki wengine akiwemo Muumini Mwinjuma, wakaanzisha bendi yao ikiitwa Extra Kimwa mwaka 1998.

Ilipotimu mwaka  mwaka 1999, aliamua kurejea nchini  baada ya kupata taarifa kuwa mama yake mzazi kuwa alikuwa mgonjwa.

Ally akiwa hapa nchini aliamua kujiunga katika bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’  chini ya uongozi wa mkurugenzi Asha Baraka. Choki alikubali kujiunga na bendi  hiyo baada ya kupokea ushauri kwa mwanamuziki mwenzake Robert Hegga ‘Caterpillar’ ambaye walikuwa wote Nairobi.

Mwaka 2000 walitoa albamu iitwayo Jirani ilikuwa na nyimbo nyingi lakini Jirani ulikuwa utunzi wake yeye Choki.

Kama kuna kitu ambacho hawezi kukisahau wakati akiwa Twanga, ni pale wanamuziki wengi walihama bendi hiyo na kwenda kujiunga na bendi nyingine ya Chuchu Sound. Wengine wakatimkia katika bendi ya Mchinga Sound, akiwemo Adolf Mbinga mpiga solo.

Busara zake akazitumia kwa kumfuata mpiga solo mwingine Miraji Shakashia ‘Shaka Zulu’.

Shakashia naye hakudumu kwa kipindi kirefu akatimka, ndipo nafasi yake ilishikwa na Kassim Rashid ‘Kizunga’ aliyekuja kupiga gitaa la rhythm.

Baadae alipewa cheo kuwa kiongozi wa bendi na ndipo walipotengeneza albamu ya Fainali Uzeeni. Albamu hiyo ilifuatiwa na ile ya ‘Ukubwa Jiwe’ hatimae ‘Chuki Binafsi’.

Ally Choki alikuwa na kila sababu  za kujivunia akiwa hapo Twanga, kwa kuwa alikuwa akiongoza kwa kutunga nyimbo nyingi zilizovuma.

Baada ya kujipima uwezo wake, akanzisha bendi yake ya Extra Bongo mwaka 2003. Bendi hiyo ilikusanya wanamuziki wengi mahiri hapa nchini na kuweza kuwa tishio kwa bendi zingine hususan katika jiji la Dar es Salaam.

Choki aliweza kushirikiana kuima na baadhi ya wanamuziki akiwemo Muhidin Maali Gurumo, walipotoka na wimbo wa ‘Jirani’. Aidha alishirikiana na Ndanda Kossovo katika wimbo wa ‘Bea’.

Lakini kama wasemavyo waswahili “Penye riziki hapakosi fitina” ndivyo ilivyotokea kwa Ally Choki ambapo fitina ikatengenezwa  na wanamuziki wake wakanunuliwa akabaki  pasipo ‘mweupe’

Kutokana na hali hiyo, alilazimika kuiacha bendi yake na kwenda kujiunga katika bendi ya Mchinga. Huko nako hakudumu kwa kipindi kirefu, akarejea tena Twanga Pepeta.

Baadaye tena akajiunga na kundi zima la Tanzania One Theater lililokuwa likiongozwa na Kapteni mstaafu John Komba.

Akiwa ni mmoja wa viongozi wa TOT, Choki alifanikiwa kuipandisha chati bendi hiyo baada ya kuwaleta wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Alidumu na bendi hiyo ya TOT hadi mkataba wake ulipokwisha, akaamua kuifufua tena bendi yake ya Extra Bongo mwaka 2009.

 Ally Choki akizungumzia kisa cha sababu za kushuka kwa kiwango cha muziki wa dansi, Choki alikanusha kauli hiyo.

Alisema kwamba muziki wa dansi haujashuka kiwango isipokuwa vyombo vya habari vimeupa kisogo kwa kuangalia zaidi muziki wa Bongo Fleva, licha ya wao kuntoa nyimbo nzuri na hata video.

“Uongozi wa bendi za muziki ni mgumu ukilinganisha na mwanamuziki wa Bongo Fleva ambapo kiongozi hana wanamuziki wengi. Hata hivyo naamini kuna muda utafika muziki huu utakuwa juu…” alisema Ally Choki.

Choki akithamini mchango mkubwa wa wanamuziki waliomtangulia, alimuelezea marehemu Muhidin Maalim Gurumo, kuwa alikuwa mwalimu na mtu anayesikiliza ushauri.

Alisema kwamba yeye binafsi alifanya naye kazi nyingi zikiwapo zili walizotoa albamu yenye nyimbo zake tatu na za Gurumo tatu.

“Album hiyo ilifanya vizuri sana na tulipata fedha nyingi mpaka kila ninapokutana naye akawa anasema nakushukuru sana kijana….” Alisema Ally Choki.

Akielezea siri ya mafanikio yake , Choki alieleza kuwa yanatokana na yeye kufanya juhudi, kutokuvuta sigara wala kunywa pombe aliyoanchana nayo 1994.

Aidha amesema kwamba anamiliki nyumba, gari, mke na watoto sita.

Ikumbukwe kabla ya kuondoka African Star, alikwaruzana na mkurugenzi wake  Asha Baraka. Katika  purukushani hizo Choki alifika mbali kwa kutoa kiapo kibaya dhidi ya mkurugenizi wake  huyo.

Kwanza kitendo cha ASET kumpeleka mahakamani kumdai gari, pili ASET kukataa kurudisha pesa za Miraji Shakashia na tatu ni ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia pesa nyingi.

Choki alisema kitendo cha ASET kumpeleka mahakamani kumdai gari ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana.

Kama Wahenga walivyonena kuwa “Wangombanao ndo hao wapatanao” Ally Choki baadaye alirejea tena bendi yake ya zamani ya African Star ‘Twanga Pepeta’.

Baadaye Ally Choki alikwenda jijini Mwanza akajiunga katika bendi ya Orchestra Kamanyola. Huko ameungana na watunzi na waimbaji wenzake mahiri akina Benno Villa Anthony na Mukumbule Lolembo ‘Parashi’.

Julai 2019, alisikika akiimba nyimbo katika bendi yake ya zamani iliyolea kwa kipindi kirefu ya African Stars  ‘Twanga Pepeta’

Mwandaaji wa makala anapatikana kwa namba: 0784331200 , 0736331200, 0713331200 na 0767331200

BUNDUKI MBILI AINA YA AK 47 NA MENO YA TEMBO MAWILI VYANASWA RUVUMA

0
0
 Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Simon Maigwa Marwa akionesha Bunduki mbili aina ya AK 47 kwa waandishi wa Habari zilizokamatwa katika kijiji cha Nambendo Songea vijijini ambazo zimeingizwa kutoka Nchi jirani ya MSUMBUJI ambapo watu wanne wanashikiliwa na kuhusiana na  tukio hilo.
Mkazi wa kijiji cha Nambendo tarafa ya Muhukuru Issa Millanzi akiwa na  meno mawili ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Ml 50 baada ya kukamatwa na Polisi kufuatia msako mkali unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma kuwasaka watu wanaojihusisha na matukio ya uharifu na ujangili katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo hasa maeneo yanayopakana na Nchi jirani ya MSUMBUJI,

NYBOMA MWAN'DIDO MWENYE SAUTI ISIYOCHUJA

0
0
Na Moshy Kiyungi
Nyboma Mwan'dido ni nguli katika muziki alianza kufaidi matunda ya jasho lake akiwa na umri wa miaka 18, kupitia tungo na sauti yake nyororo  katika uimbaji.

Amepiga muziki katika bendi nyingi akishirikiana na wanamuziki wakubwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tungo na sauti ya mwanamuziki huyo, haijachuja tangu akiwa kinda. Sauti yake inayoweza kulinganishwa na ya ndege aitwaye Churiku.

Mfano mdogo sauti yake imesikika akiimbisha wimbo wa Abisina, wakati akiwa katika bendi ya Orchestra Kamale, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwan’dido anazo talanta nyingi za utengenezaji muziki, utunzi na uimbaji wa nyimbo za muziki wa Soukous.

Alizaliwa nchini humo, na kujifunza kuiimba akiwa bado mdogo  wakati huo akiwa kijiji cha Nioki, kilicho umbali wa kilometa 200, Kaskazini Mashariki mwa jiji la Kinshasa, DRC.

Alipokuwa mwanafunzi wa shule, alijiunga na kwaya ya shule pamoja na ya Kanisa.

Baada ya wazazi wake kuhamia katika jiji la Kinshasa, wakati yeye akiwa bado mwanafunzi ya shule ya msingi, alijiunga katika bendi yake ya kwanza ya Baby National, kama mwimbaji wa kulipwa mwaka 1969, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18.

Baadaye Nyiboma alikwenda kujiunga katika bendi ya Negro Success. Alipiga muziki na bendi hiyo hadi pale kiongozi wao Bavon Marie-Marie Siongo alipofariki kwa ajali ya gari.

Bavon alikuwa mdogo wake Franco Makiadi, alifariki dunia Agosti 05, 1970, baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupata ajali.

Ajali hiyo ilitokana na wivu wa kimapenzi baada ya kutokea mzozo kati yake na  kaka yake Franco Luambo Makiadi,  akimtuhumu kwamba alikuwa anafanya mapenzi na rafiki yake wa kike aliyejulikana kwa jina la Lucy.

Mwan’dido aliingia mkataba na kampuni ya kurekodi ya Editions Veve, iliyokuwa ikimilikiwa na Kiamuangana Mateta Wazelambongo ‘Verckys’.

Verckys alikuwa mahiri kwa kurekodi muziki wa soukous, producer, mfadhili, mtunzi, mpulizaji wa saxophoni pia alikuwa kiongozi wa bendi yake ya Orchestra Veve katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire wakati huo)

Mwaka 1975 Nyboma Mwan’dido aliteuliwa kuwa kiongozi wa bendi ya Orchestra Kamale, iliyokuwa chini ya Editions Veve record label.

Kamale iliundwa na Verckys akiwatumia baadhi ya wanachama wa bendi ya Orchestra Lipua Lipua na Orchestra Kiam ambazo zilikuwa miongoni mwa bendi zilizoasisiwa chini ya lebo ya Veve, ya Verckys.

Bendi ya Kamale ilikuwa na watunzi na waimbaji mahiri akiwemo yaye Nyboma na Tshimanga Kalala Assosa, ambaye yupo nchini Tanzania, tangu miaka ya 1980, alipokuja na bendi ya Orchestra Fuka Fuka.

Hivi sasa Asossa ni kiongozi wa bendi ya Orchestra Bana Maquis ya jijini Dar es Salaam.

Wakati huo bendi ya Orchestra Kamale, walitoka na nyimbo kali zilizowakuna wapenzi na mashabiki wa muziki wa soukuos. Miongoni mwa nyimbo hizo ni Ngali, Masua, Andoya, Abisina, Bitota na nyingine nyingi.

Orchestra Kamale ilisambataika mwaka  1978, baada ya Tshimanga Kalala Assosa na Mulembu, walipoondoka kwenda kuunda bendi yao ya Fuka Fuka.

Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Orchestra Kamale waliobakia, wakabadili majina ya bendi ikaitwa Les Kamale, ikiiongozwa na Nyboma Mwanan’dido.

Miaka ya 1970, Les Kamale, ilikuwa maarufu kwa nyimbo kali za "Salanga" na "Afida na ngai."

Mwaka 1979 Nyboma alikwenda kufanya kazi ya muziki katika kundi ka African All-Stars nchini Togo, baada ya mwanzilishi wa kundi hilo Sam Mangwana kuondoka. 

Ilipotimu mwaka 1981, Nyboma alirekodi albam moja kali ya ‘Double Double’, akiwa katika bendi yake mpya ya Les Kamale Dynamiques Du Zaire.

Aidha mwaka 1983 hadi 1984, alirekodi albam nyingine tatu chini ya jina la Les Kamale Dynamiques Du Zaire.

Nyboma aliwahi kufanya kazi za muziki na wanamuziki wakubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akina Pepe Kalle akiwa na bendi yake ya Empire Bakuba, Koffi Olomide akiwa na wanamuziki wake wa Les Quatre Latin,  Etoiles, Bopol, Syran na Wuta Mayi.

Albam nyingi za Nyiboma Man’dido aliwashirikisha wanamuziki nguli wakiwemo akina Pepe Kalle, Madilu Systeme, Kamale, Lokassa Ya Mbongo na wengine wengi.

Aidha Pepe Kalle alimshirikisha Nyiboma Man’dido katika wimbo albamu ya Moyibi 1988.

Aidha aliimba  nyimbo za Lipwa Lipwa De Nyimboma na Stop Feu Rouge.

Baadhi ya albam alizotunga ama kushiriki kuimba alipokuwa katika bendi ni kama ya L’Orchestre Kamale iliyotoka mwaka 1977, Innovation vol. 6 na 7 alimshirikisha Bovi mwaka 1980.

Zingine ni Dede ambapo Nyboma, alimuita Lesale wakashirikiana kutengeneza wimbo. Mwaka 1982, akimshirikisha tena Pepe Kalle katika nyimbo za Lesale ya 1983 na Coeur a Coeur.

Nyimboma alishirikiana vyema na Pepe Kalle kwenye albam za Moyibi mwaka 1988, Anicet  ya mwaka 1994 na Bandona.

Nyiboma Man’dido bado anendelea na shughuli za muziki akiwa nchini Uingereza ambako ndiko ameweka makazi yake.

Muandaaji wa makala hii anapatikana kwa namba: 0713331200, 0784331200, 0736331200 na 0767331200.

NAIBU WAZIRI BASHE ATUA WIZARANI, WAZIRI WA KILIMO AGAWA MAJUKUMU

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu. Kulia kwake ni Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) na kushoto kwake ni Mhe Omary Mgumba. (PIcha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu. Kulia kwake ni Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Julai 2019 ameongoza kikao kazi cha uongozi wa juu wa Wizara ya Kilimo ili kutoa taswira ya muelekeo wa Wizara hiyo.

Kikao hicho kilichotuama kwa masaa kadhaa katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mhe Hasunga, kimehudhuriwa pia Naibu Maziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) na Mhe Hussein Bashe kadhalika katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Katika kikao hicho Waziri Hasunga amewataka Naibu Mawaziri hao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli akiwa na muktadha wa kuimarisha uchumi wa wananchi kadhalika maendeleo kwa ujumla wake.

Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga ametoa taswira ya muelekeo wa wizara hiyo katika mipango ya muda mfupi na muda mrefu ili kuwa na weledi na utendaji uliotukuka katika utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.

Rais Magufuli amemteua Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akishika nafasi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ambaye sasa ni waziri wa Viwanda na Biashara.

Moja ya mambo aliyoyabainisha Mhe Hasunga ni pamoja na haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla. 

“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo na tayari tupo katika hatua za mwisho, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesema

Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.

Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto na Tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Kadhalika ameeleza kuhusu usajili wa wakulima wa mazao yote na ambapo Bodi hizo ziliagizwa kuwapatia vitambulisho kwa ajili ya kuwatambua wakulima hao na wanapofanyika kazi zao ili iwe rahisi kuwahuduma.

Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga ametaja umuhimu wa Wizara ya Kilimo kuanzisha Bima ya Mazao itakayokuwa suluhisho kwa wakulima nchini ambao kwa muda mrefu wamekosa utetezi pindi wanapopatwa na majanga kutokana na uchache wa mvua ama vinginevyo, jambo linalopelekea kukoseka kwa mazao ya kutosha.

MAELEZO ,XINHUA Wasaini Mkataba Kuimarisha Ushirikiano.

0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi Kulia, na Mhariri Mkuu wa shirika la Xinhua Tanzania Si Sibo Li Kushoto, wakisaini mkataba wa Ushirikiano ,  waliosimama kutoka kulia  ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, Katikati ni Bw.He Ping Mhariri Mkuu wa Xinhua na mjumbe wa Kamati Kuu ya  Chama cha CPC na Kushoto Wang Ke balozi wa China nchini Tanzania, wakishuhudia tukio hilo. (Picha na Idara ya Habari MAELEZO)

 Kutoka Kushoto Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, Mhariri Mkuu wa Xinhua na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha CPC He Ping, Dkt.Hassan Abbassi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, pamoja na Si Sibo Li Mhariri Mkuu wa Xinhua Tanzania , wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini makubaliano Jijiji Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari MAELEZO)


Na Mwandishi Wetu-MAELEZO. 

Ofisi ya Idara ya Habari MAELEZO chini ya Wizara ya Habari Utanaduni Sanaa na Michezo, imesaini Mkataba wa Ushirikiano kati yake na Shirika la Habari la Serikali ya China Xinhua ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na China ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Tse Tung. 

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mkataba huo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alisema ushirikiano wa Tanzania na China umekuwepo kwa miaka mingi katika Nyanja mbalimbali na sasa nchi hizo zimekua kama ndugu. 

Waziri Mwakyembe alisema yapo mambo mengi yalioacha alama kwenye ushirikiano wa kindugu kati ya China na Tanzania, ikiwemo reli ya Tazara pamoja na uwanja mkubwa wa Taifa Jijini Dar es Salaam pamoja na majengo mbalimbali makubwa. 

“Nafurahi kuona leo wenzetu wa Idara ya Habari Maelezo wanatiliana saini mkataba wa ushirikiano kati yao na Xinhua, hii inadhihirisha kukomaa kwa urafiki kati ya Tanzania na China na imeongeza wigo wa maeneo ambayo nchi hizi mbili zinashirikiana” Alisema Waziri Mwakyembe. 

Alisema licha ya kwamba kuna mashirika ya Habari ya China ambayo yanafanya kazi hapa nchini kama CCTV,CGTN, XNHUA pamoja na baadhi ya magazeti, ushirikiano mpya uliosainiwa kati ya Xinhua na Idara ya Habari Maelezo utaimarisha zaidi sekta ya habari hapa nchini , na pia utasaidia kubadilishana uzoefu katika masuala ya habari na mawasiliano kwa ujumla. 

Kwa upande wake mhariri Mkuu wa Shirika la Xinhua ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ukombozi cha watu wa China CPC Bwana He Ping, alisema amekuja Tanzania kuimarisha uhusiano wa kindugu ulioasisiwa na waanzilishi wa mataifa haya mawili, na pia kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Idara ya Habari Maelezo na shirika la Habari la Xinhua. 

Alisema tangu mwaka 1969 Xinhua imekua ikileta wanahabari wake kufanya kazi hapa nchini, lakini ushirikiano mahsusi kama ulioanzishwa kati ya Shirika hilo na Idara ya Habari, utasaidia katika upatikanaji wa habari nyingi za maendeleo kwani nchi yake inahangaika usiku na mchana kuendelea kuwaletea wananachi wake maendeleo. 

“Lengo letu kama taasisi ya Serikali ni moja tu kuhakikisha kwamba habari tunazoandika na kusambaza zinachangia katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kujikita hasa katika habari za maendeleo, hili linatakiwa kusisitizwa sana kwani katika miaka 40 iliyopita China ilikua ni nchi inayoendelea lakini kwa sasa imepiga hatua kubwa za maendeleo duniani” Alisema Bwana Ping. 

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi, alisema habari ni maendeleo na ushirikiano huo ulioanzishwa utaendelea kuleta chachu ya maendeleo baina ya Tanzania na China hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa. 

“Sisi tuko tayari kuwapa habari za kina na zenye takwimu sahihi ili mtusaidie kuieleza dunia kwamba Tanzania sasa tunapiga hatua, kama mlivyofanya mageuzi makubwa ya kiuchumi huko China na sisi tunajitahidi kuhakikisha tunakua Taifa lenye maendeleo makubwa na lenye nguvu kiuchumi” Alisema Dkt Abbasi. 

Mkataba uliosainiwa kati ya Idara ya Habari MAELEZO na Shirika la Xinhua una lengo la kuimarisha uhusiano katika kubadilishana habari na taarifa mbalimbali, kupitia magazeti na majarida lakini pia kupitia mitandao ya kijamii. 

Aidha katika Ushirikiano huo Idara ya Habari Maelezo italisaidia shirika la Xinhua katika kupanga na kufanya mahojiano na viongozi wa serikali, Taasisi na wakala mbalimbali pamoja na kuwawezesha waandishi wa Shirika hilo kufanya kazi zao kwa wepesi zaidi hapa nchini. 

Katika mkataba huo wa ushirikiano Idara ya habari pia itawasaidia waandishi wa habari wa Xinhua katika kupata vibali vya kufanyia kazi hapa nchini pamoja na kuwapatia vitambulisho vya wanahabari (Press cards). 

Kwa upande wa shirikala Xinhua watasaidia kwenye kutafiti,kuandika na kutoa habari ambazo zinaisaidia Serikali kupitia Ofisi ya Msenaji Mkuu, pia watahakikisha habari wanazotoa zinz viwango vinavyokubalika na Idara ya Habari, pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha wanahabari (press Center) Jijini Dodoma. 

Utiaji saini wa mkataba huo wa ushirikiano, ulifanywa na Dkt.Hassan Abbasi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali na Bwana Si Sibo Li ambaye ni mhariri Mkuu wa shirika la Xinhua hapa nchini. 

Hafla ya utiaji saini mkataba huo wa ushirikiano, ulihudhuriwa pia na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wawakilishi wa Xinhua kutoka Nairobi Kenya, wawakilishi kutoka Makao Makuu China, wawakilishi wa Idara ya habari Maelezo, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamona na mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO MAKANDARASI WADOGO

0
0
Serikali imesema itawajengea uwezo makandarasi wadogo wanaotumia teknolojia ya nguvukazi (Labor Based Technology) katika ujenzi na ukarabati  wa matengenezo ya barabara, madaraja na majengo ili kuhakikisha kuwa wanapata fursa zaidi za kushiriki na kushindana katika kazi zilizotengwa mahsusi kwa ajili makandarasi hao.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, kwenye kongamano la uhamasishaji na uanzishwaji wa umoja  wa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengenezo ya barabara uliofanyika mkoani Mbeya katika Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI) na kuhudhuriwa na wakandarasi wadogo wadogo zaidi ya 150.

Arch. Mwakalinga, alisema kuwa Wizara kupitia taasisi zake zinazotekeleza miradi ya ujenzi itaendelea kutumia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhakikisha kazi zilizoainishwa kwenye miradi ya ujenzi ikiwemo ukarabati  na matengenezo ya barabara, madaraja na majengo zinafanywa na makandarasi  hao.

"Wizara imeteua timu ya wataalam kupitia nyaraka mbalimbali za miradi ya ujenzi ili kuhakikisha asilimia 30 ya fedha zinazolipwa kwenye mikataba mbalimbali ya ujenzi zinaelekezwa kwa makandarasi wanaotumia teknolojia ya nguvu kazi", alisema Mwakalinga. 

Aliongeza kuwa upitiaji utafanyika kwa haraka chini ya wataalam hao ambapo anaamini watafanya kazi hiyo vizuri ili kubainisha vigezo ambavyo makandarasi hao wamekuwa wakivilalamikia kila siku katika utekelezaji wa kazi zao ili vifanyiwe kazi.

Aidha Arch. Mwakalinga, alibainisha kuwa Serikali inatambua makandarasi hao ni chachu kubwa katika kutatua tatizo la ajira kwa wananchi hususani maeneo ya vijijini kwani mara nyingi wakandarasi hao hutumia vifaa na vibarua wanaopatikana katika eneo la mradi. 

"Mbali na kuongeza ajira na kuimarisha usafiri hususani maeneo ya vijijini, serikali inaelewa fika mnachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kwa kodi mnayolipa kupitia kazi mnazozifanya" alisisitiza Mwakalinga.

Alisema ni jukumu la wakandarasi hao kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuwa na sauti moja katika kufuatilia fursa mbalimbali na maslahi yao na kupata ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazowakabili. 

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu huyo Mkurugenzi wa Barabara, Mhandisi Rogatius Mativila, alisema madhumuni ya kikao kazi hicho ni kujadili kwa pamoja masuala muhimu katika Sekta ya Ujenzi ili kuendeleza na kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Nguvukazi katika kutekeleza matengenezo ya barabara, madaraja na majengo bila kusahau sekta nyingine nchini. 

Akiongea kwa niaba ya makandarasi hao, Bi Aurelia Mtui, alitoa shukrani za dhati kwa Serikali kwani amekuwa kwenye taaluma hiyo kwa miaka 18 na kwa mara ya kwanza wamekutana na Katibu Mkuu  wa Sekta ya Ujenzi kuzungumzia changamoto zao na kuomba maazimio waliyokubaliana katika kikao hicho yafanyiwe kazi. 

Serikali ilianzisha mpango wa kuendeleza matumizi ya teknolojia ya Nguvukazi tangu mwaka 2004 na kulingana na takwimu zilizopo hadi kufikia mwezi Juni 2019 jumla ya Makandarasi 267 walikuwa wamesajiliwa na bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) katika madaraja ya kutumia teknolojia ya nguvukazi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akifungua kongamano la uhamasishaji na uanzishwaji wa umoja  wa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengenezo ya barabara lililofanyika katika Chuo cha Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI) mkoani Mbeya.
 Mshiriki wa kikao kazi cha Makandarasi wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvukazi katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara, Bw. Ambakisye Mwakipesile, akiwasilisha hoja zake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) katika kongamano lililofanyika katika Chuo cha ATTI Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya na kushirikisha wakandarasi hao kutoka nchi nzima.
 Mkandarasi Boniface Mambya, akitoa maoni yake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) wakati wa kongamano la umoja kwa makandarasi na vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika Ujenzi ukarabati wa Matengezo ya barabara lililofanyika katika chuo ATTI, Mkoani Mbeya.
Washiriki wa kongamano la uhamasishwaji wa uanzishwaji wa umoja wa makandarasi na Vikundi vinavyotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi, ukarabati wa matengezo ya barabara wakipitia baadhi ya makabrasha na kumsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch.Elius Mwakalinga (hayupo pichani) lililofanyika katika Chuo cha ATTI, Mkoani Mbeya.

SERIKALI YARIDHISHWA KASI YA UJENZI MRADI WA KUUNGANISHA UMEME TANZANIA NA KENYA

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi TV,Arusha

SERIKALI imesema imeridhishwa na kasi ya wakandarasi wanaojenga mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa kilovolti 400 inayopita Singida, Babati, Arusha hadi Namanga kwani unaenda mbio na mpaka sasa ujenzi umefanyika umekamilika kwa asilimia 51.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400.Ziara hiyo ilihusisha kukagua njia ya umeme ya Namanga ,kituo cha kupoozea umeme 
cha Legur kilichopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru na njia za kusafirishia umeme zilizopo katika halmashauri ya Babati Vijijini katika kijiji cha Nagwa .

Amebainisha kuwa kazi zinazofanywa na wakandarasi waliopewa miradi hiyo ameridhishwa nazo kwani hadi sasa wameshafanya kazi kwa asilimia 51 na hivyo kubakisha asilimia 49 na anaamini kwa kasi wakandasi hao wanayoendelea nayo watakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa. "Mradi huu unatakiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa Serikali Aprili 2020".

Ameongeza kuwa "Nimepita na kuangalia hatua iliyofikiwa katika mradi huu wa njia ya usafirishaji wa umeme ambao miundombinu yake itaunganishwa katika vyanzo vya uzalishaji umeme.Nia ya ziara hii ni kuangalia tumefikia wapi hadi sasa hivi na kunachangamoto zipi zinazoukabili ili kama zipo Serikali itatue haraka na kazi iendelee." 

Pia amesema katika mradi huo kuna Lot T5 ambayo ya kwanza inaanzia Singira mpaka Babati na Lot T2 ya pili inaanzia Singida hadi Arusha na Lot T3 ya tatu inaanzia Arusha mpaka Namanga ,Lot T4 inausisha ujenzi wa vituo vya kupooza umeme ambapo kimoja kiko kisongo na kingine kitakuwepo pale Singida na Lot T5 itahusisha kusambaza umeme katika vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi huo.

Amesema kulingana na kasi ambayo wakandaras hao wanaendanayo kunauwezekano mkubwa wa mradi huu kukamilika kabla ya ratiba iliyopangwa au utakamilika kwa wakati .“ Serikali tumewaagiza wakandarasi hawa wafanye kazi kila siku,wakandarasi wawatumie vijana wetu katika kazi zote kazi ambazo zinaitaji elimu na hata zile ambazo hazihitaji elimu na katika suala hili nawapongeza wakandarasi maana wametii maelekezo.

"Wameajiri vijana zaidi ya 400 ambao wanatoka katika vijiji ambavyo miradi imepita kuanzia pale ulipoanzia Namanga hadi Singida.Pia tumewataka wakandarasi washirikiane na jamii zinazozunguka 
miradi hii ili kusiwepo na changamoto,"amesema.

Kwa upande wake Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hao ikiwa ni pamoja na kuwasadia kazi mbalimbali za ujenzi.

Pia Serikali imewahaidi wakandarasi hao kuwasaida katika masuala mbalimbali ikiwemo wakati wa vitu kutoa vifaa vya ujenzi bandarini ili wakamilishe mradi huo kwa wakati na kwamba mradi huo utakamapokamilika utachochea maendeleo katika nchi yetu. 
Muendesha mashine ya kuchanganya sege kutoka kampuni ya ukandarasi ya Booygues , Dominic Heriman akimuonyesha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga jinsi wanavyochanganya sege kwa kutumia komputa wakati katibu alipofanya ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 hapo ni ndani ya store yard ya Lot T2 iliopo katika kijiji cha Nanja . 

 Meneja wa mradi  kutoka kampuni ya Booygues Energies &services Potier Mathiew  akitoa maelekezo kwa  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye pamoja na viongozi mbalimbali wa Tanesco wakiwemo wakandarasi wakati walipotembelea moja ya shimo lililopo tayari kwa ajili ya kusimamisha mnara. 
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi

IN MEMORY OF ABEL YANGA

0
0
Today we are counting four years since that sad morning of July 22, 2015, when our beloved Abel answered the call of his Creator. 
God took him,  it was his will as he always picks the best of flowers from his Garden. Abel, you slipped like water between fingers, but that was God's will. Though we do not see you in flesh anymore, in our hearts you live forever.
You are deeply missed by your parents Mzee Charles Yanga and 
Mama Lucy Yanga,  your young brothers and sisters, in-laws,  relatives, and friends. We will cherish the memories you left till we meet again. Amen.
Attachments area

WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE RASMI OFISI NDOGO YA MAKAMU WA RAIS DAR ES SALAAAM

0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Mhe. GHeorge Boniface Simbachawene akisaini kitabu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi alipowasili Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli JIjini Dar es salaam leo Julai 22,2019 mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo Ikulu Jijini Dar es salaam.
 Naibu hi Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima  (kushoto) akimkaribisha Waziri wa NcOfisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene (katikati) katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene akikaribishwa na Bi. Elizabeth Mtiganzi katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam mara baada ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Boniface Simbachawene akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo Dar es Salaam, mara baada ya kuwa kuapishwa Ikulu Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mhe. Simbachawene amewataka watendaji hao kushirikiana kwa pamoja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

USHAURI WA BURE WA BALOZI MSTAAFU PATRICK TSERE KWA WASTAAFU

WAZIRI SIMBACHAWENE AWASILI OFISINI, APOKELEWA NA MAKAMU WA RAIS

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Boniface  Simbachawene alipowasili Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Julai 22,2019 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira George Boniface Simbachawene akisaini kitabu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi alipowasili Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli JIjini Dar es salaam leo Julai 22, 2019 mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo Ikulu Jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wafugaji wa jamii ya kibarbeig Babati kunufaika la utalii

0
0
Mkurugenzi wa Chemchem Nicolas Negri akipokea zawadi kutoka kwa akina mama wa jamii ya kibarbeig kutokana na kuwezeshwa vikundi vyao.
Wanawake wa jamii ya kibarbeig wakiwa kwenye kikao cha vikoba baada ya kupatiwa mkopo na Taasisi ya Chemchem.




Mwandishi wetu,Babati.

WAFUGAJI jamii ya Kibarbeig wilayani Babati, mkoa wa Manyara wanatarajiwa kuanza kunufaika zaidi na Utalii baada ya kuanzishwa vituo vya kuvutia watalii katika maeneo yao.

Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya Chemchem association, Walter Palangyo amesema,Taasisi hiyo iliyowekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, kupitia hoteli za Kitalii za Chemchem imejipanga kuboresha maisha ya jamii hiyo ili inufaike zaidi na Utalii.

Anasema jamii hii iliyopo katika kijiji cha Vilima vitatu, imewezeshwa kupitia vikundi vyao vya Vikoba na itajengewa maboma ya kitalii ambayo yatakuwa yakitembelewa na watalii ambayo watalipa fedha.

"kuna kikundi cha Wicheda ba na Datoga vya jamii ya kibarbeig ambavyo tumepatia kiasi cha sh 2.5 milioni ili kukuza mitaji yao na kuweza kufanya shughuli za kijasiriamali ikiwepo kuuza vitu vya asili kwa watalii "anasema

Kamishna wa uhifadhi wa Mamlaka ya wanyamapori(TAWA),Dk James Wakibara anasema jamii zilizopo eneo hilo la hifadhi ya jamii,linaweza kunufaika sana na Utalii kama wakizitumia fursa zilizopo.

" mwaka jana hifadhi hii imeingiza zaidi ya sh 1.2 bilion hivyo mnaweza kunufaika zaidi kama mkiendelea kuhifadhi eneo hili na kutumia fursa zavutalii zilizopo"amesema.

Naibu Waziri Shonza Atembelea Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bi. Ingiaedi Mduma (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea programu hiyo kujionea shughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bi. Ingiaedi Mduma (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea programu hiyo kujionea shughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam, kushoto Afisa wa Programu hiyo Mayzuhura Simba.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akifafanua jambo kwa watumishi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea programu hiyo kujionea shughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Christopher Mhongole (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea programu hiyo kujionea shughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akiangalia moja ya kitabu chenye picha mbalimbali za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kujioneashughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mratibu wa Programu hiyo Bi. Ingiaedi Mduma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akiangalia maendeleo ya ukarabati wa majengo ya Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea programu hiyo kujionea shughuli mbambali za utendaji kazi wa programu hiyo mapema hii leo Julai 22, 2019 Jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – DSM.

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA UHIFADHI WA CHANZO MAJI KIZINGA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali amezindua mradi wa uhifadhi wa chanzo cha Maji wa mtambo Mtoni kwa kupanda miti aina ya mitomondo na kuweka jiwe la msingi.

Mbio za Mwenge zimetembelea chanzo cha maji cha Mtoni kilichoanza uzalishaji wa maji mwaka 1950 ukiwa na uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha ujazo wa lita 7000 hadi 9000 kwa siku.

Kiongozi wa Mbio hizo Mzee Mkongea Ali ameridhishwa na mkakati uliowekwa wa Kulinda vyanzo vya maji kwa kupanda miti na kuwataka wananchi kushirikiana kwa pamoja kuvitunza na kuvilinda.

Amesema, wananchi wanapotunza vyanzo vya maji vinasadia katika kupata maji safi na salama kwa wingi na lengo la Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli inalenga katika kumtua mama ndoo kichwani.

Mzee Mkongea, ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa uhifadhu chanzo cha maji cha Mtoni Mashine ya maji na kushiriki upandaji wa miti pembezoni mwa mto.

Akisoma taarifa fupi ya mradi huo, Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka DAWASA Modester Mushi amesema, chanzo cha Mto Kizinga kilianza kupunguza uwezo wa uzalishaji wa maji hadi kufikia wastani wa mita 2700 kwa siku kutokana na kukithiri kwa shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya mto.

Amesema, wameendelea na juhudi za upandaji wa miti aina ya mitomondo ili kulinda na kuhifadhi chanzo hicho na kufikia Mwaka 2019 miti 10146 imepandwa, pamoja na jitihada za kukutana na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ya mto wanaofanya shughuli za kilimo katika hifadhi ya mto.

"Mpango huu maalumu wa kuhifadhi chanzo cha maji kwa kupanda miti umeleta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji maji kutoka mita za ujazo 2,700 kwa siku mwaka 2015 hafi kufikia mita za ujazo 7,200 kwa sasa," amesema Modester.

Kwa sasa chanzo cha Mtoni kinahudumia wakazi 480,978 kikiongezeka kutoka 280,000 na lengo ni kuongeza watumiaji wa maji kufikia 751, 978 na idadi hii itafikiwa baada ya kupeleka maji katika tanki la Mbagala kukamilika.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji cha Mto Kizinga na kuunga mkono mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kupanda miti baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akisoma taarifa fupi ya mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya kutembelea chanzo hicho.

 Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akikabidhi taarifa fupi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo cha Mto Kizinga leo Jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akipanda mti pembezoni mwa Mto Kizinga ikiwa ni katika kuunga mkono uhifadhi wa vyanzo vya maji baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mazingira Modester Mushi akitoa maelezo ya chanzo cha uzalishaji maji kutoka Mto Kizinga kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali baada ya mwenge wa uhuru kutembelea chanzo hicho leo Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI JENISTA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na waombolezaji wakati alipowaongoza katika Ibada na kuaga mwili wa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Richard Kalinga, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma, Julai 22, 2019. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mohammed Kiganja.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akitoa pole kwa familia ya mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Richard Kalinga, baada ya kuwaongoza waombolezaji katika Ibada ya kumwombea marehemu na kutoa heshima za mwisho, nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma Julai 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAOSOMA NJE WATAKIWA KUACHA KUPIGA DILI NCHI ZA WATU

0
0
Kaimu Mkuu was Chuo Cha Mtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda akizungumza , wakati akiwaaga wanafunzi watano kati ya 80 wa Stadhahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Komputa, wanaoenda nchini India kwa ajili ya kumalizia mwaka wa mwisho
Mkuu wa Chuo chaMtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda, akitoa neno la mwisho kwa Wanafunzi wanaosafiri.
Mwanafunzi wa Kike aliyepata nafasi ya kwenda India kusoma Masomo ya Uhandisi wa Kompyuta ,Sky Karoli akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mwanafunzi wa Kiume George Temu aakifafanua kwa Waandishi wa habari umuhimu wa kwenda kusoma India.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

WANAFUNZI wanaopata ufadhili wa kwenda kusoma nje ya nchi, wametakiwa kujiepusha na shughuli za kufanya vibarua katika nchi za watu kwa lengo la kujipatia kipato na badala yake wazingatie kile kilichowapeleka.

Wito huo umetolewa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda, wakati akiwaaga wanafunzi watano kati ya 80 wa Stadhahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Komputa, wanaoenda nchini India kwa ajili ya kumalizia mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa lengo la kuwaongezea ufanisi katika taaluma hiyo.

Alisema kila mwaka chuo hicho kimekuwa kikiwapeleka wanafunzi wote wa mwaka wa mwisho ngazi ya Stadhahada na Shahada wa Uhandisi wa Sanyasi ya Komputa nchini India kwa ajili ya kumalizia masomo yao ili wapate uzoefu wa kuendana na teknolojia ya masomo hayo.

"Nina waasa, chuo kinawapeleka India kwa ajili ya kupata elimu, kuongeza taaluma ili kuwa wahitimu mnaoendana na teknolojia ya Sayansi ya Komputa, acheni kwenda kufanya kazi za vibarua, acheni kwenda kufanya uhuni na mambo ambayo hayaendani na kilichowapeleka kazi yenu iwe kusoma na mrejee nchini mkiwa mmepata elimu na si vinginevyo," alisema Prof. Ngalinda.

Alisema kumekuwapo na tabia za vijana wanaokwenda katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya masomo kujihusisha na vitendo visivyo na maadili na matokeo yake kuharibu mipango yao na malengo tayariwa.

Aidha, alisema chuo hicho kinazingatia ubora wa elimu wanayotoa na ndio sababu wamekuwa wakipeleka wanafunzi nje ya nchi ili kuwapatia elimu inayoendana na ukuaji wa teknolojia na kukidhi matakwa ya soko la ajira nchini.

"Gharama za masomo wanayolipia ndizo zinazotumika kuwapeleka India kwa ajili ya kumalizia masomo yao na si kwamba tunawatoza fedha nyingine. Huu ni mkakati wa chuo kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo bora na wala hakuna haja ya kusafiri kuifata mataifa mengine kwa sababu tunakidhi mahitaji yote," alisema.

Kwa upande wa wanafunzi wanaokwenda nchini India, Sky Karoli, mbali na kuushukuru uongozi wa chuo hicho kwa kuwawezesha kupata uzoefu kutoka chuo cha nchini India alisema ni fursa nzuri kwao.Alisema wanaamini watapata elimu iliyo bora itakayo wawezesha kuwa wahitimu wanaoweza kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii.

Naye George Temu, alisema wanaenda kujifunza namna nchi nyingine zilivyopiga hatua katika ukuaji wa teknolojia ili kupata elimu itakayowawezesha kuifanyia kazi wakirudi nchini.

KAMILISHENI USAJILI KWA KIPINDI CHA MIEZI MWILI –MSAJILI NGOs

0
0

 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akizungumza na vyombo vya habari kuhusu usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGOs zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
 Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. January Kitunsi (kushoto) akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Denis Bashaka(kushoto)akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini yanayofanya kazi za kijamii ambazo awali usajili wake ulifanyika katika Mamlaka nyingine kama RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na BRELA usajili wake utakuwa umefutwa kama zitashindwa kujisajili chini ya Sheria ya NGO's kama iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 katika kipindi cha miezi miezi miwili toka tarehe 01 Julai, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao ameyataka Mashirika hayo kutekeleza matakwa ya Sheria hiyo kwa mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa zoezi linaloendelea la usajili Jijini Dodoma linalenga Mashirika hayo.

“Sheria inayataka Mashirika hayo kujisajili katika Sheria ya NGO's kwa kipindi cha miezi miwili hivyo huu ni wakati wa Mashirika kujitahimini yako wapi ili yaweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kipindi kilichotolewa na Sheria hii kupita.” Aliongeza Bi. Mayao.

Bi. Mayao amesema usajili huo kwa awamu hii unafanyika kwa mikoa ya Kanda ya Kati Tabora, Singida, Kigoma na Dodoma na kutoa wito kwa Mashirika yaliyopo katika Mikoa hiyo kufanya usajili huo akiongeza kuwa zoezi hili linafanyika bila malipo kwa Mashirika yanayouhisha usajili lakini Mashirika yanayojisajili mara ya kwanza yanatoa malipo kwa ajili ya huduma hiyo.

Bi. Mayao ameyataka Mashirika kusajili pia kwa njia ya mtandao kwani fomu za kujaza zinapatikana kwenye Website ya Msajili ambapo mtu anayetaka kusajili atajaza fomu hiyo lakini pia kuwasilisha Katiba dogo ikiwemo sifa za viongozi wa Shirika pamoja na eneo la utekelezaji au kusudio la shughuli za kazi za shirika.

Aidha Mwakilishi wa Msajili wa Jumuiya za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw.Thomas Sanila amesema kuwa Ofisi ya Msajili wa Jumuiya inashiriki usajili huo kuangalia kama kuna mkanganyiko wowote utakaojitokeza na kufuatilia kama shuguli zinazofanywa na Shirika husika zinaendana na Sheria na taratibu za Nchi.

Bi. Khadija Omari kutoka Taasisi ya Tuvuke Wote iliyoko Jijini Dodoma ameyataka Mashirika kujitokeza kwa wingi akisifu taratibu za usajili kuwa ni za haraka tofauti na alivyofikiria kwani ametumia takribani nusu saa kukamilisha zoezi la usajili.

Zoezi hili la usajili limeanza tangu tarehe 10 mwezi huu Jijini Dar es Salaam ambapo asilimia 80 ya NGO's zilizoko Kanda ya Mashiriki zimefanya usajili wake na zoezi la usajili linaendelea kwa kipindi cha miezi miwili kama ilivyo elekezwa katika marekebisho ya Sheria Na. 3 ya mwaka 2019.

MSANII HARMONIZE KUMSHIKA MKONO Q CHILLAH KWENYE KAZI ZAKE

0
0
MSANII wa Bongofleva Rajab a.k.a Harmonize amesema ifike wakati wasanii watambue na waheshimu jitihada za wakongwe na waasisi wa Muziki .

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam leo. Harmonize amesema anatambua mchango wa wakongwe wa Muziki wa Bongofleva na kuwataja Q chillah,Ay,Mwana fa,Ferouz na wengine wengi kuwa ndio moja wa funguo zilizowafanya wasanii wengi kutamani kuingia kwenye kiwanda cha Muziki.

"Wachache sana wenye kutambua juhudi za wakongwe hawa ambapo nchi za nje wasanii wa zamani wamekua wakipewa kipaumbele na kuheshimiwa mfano mzuri Msanii 2 face idibia kutoka nchi ya Nigeria anaheshimiwa sana na wasanii ambao ni chipukizi na wanaofanya vizuri kwa sasa lakini hapa kwetu imekua nadra wakongwe kupewa thamani yao,"

Hata hivyo Harmonize ameamua kutangaza rasmi kurudi kwa Mkongwe wa Bongofleva Abubakar katwila a.k.a Qchillah na kutangaza kazi zake mpya tatu ambazo ameshirikiana na kwenye album yake.

"Wakati nilipokua najifunza kuimba nilikua namtazama chillah kama mfano wa kuigwa na nimepita kwenye nyayo zake kutokana na kipaji chake kuanzia utunzi wake na sauti yake ya kipekee ambayo bado ipo vizuri,"

Aidha, mbali na Harmonize kutangaza rasmi kurudi kwa msanii q chillah pia ameamua kumpatia gari aina ya porte kama zawadi kwake itakayomuwezesha kufanya Safari zake za kimuziki.

"Wakati nampigia chillah aje studio tutengeneze nyimbo kwa ajili ya album yake alisema mdogo wangu nikija utanilipia bodaboda binafsi nilijisikia vibaya kutokana na yeye ni Msanii mkubwa sana na hakustahili kuwa kwenye Hali duni kiasi hicho ndio maana nimeamua kumzawadia gari,"

Kwa upande Mkongwe huyo Q chillah amesema anatambua mchango wa Harmonize kwani ni wachache sana wanaojitoa kwa watu na kuwa na moyo wa kuwasaidia wengine.

Hata hivyo amehaidi kufanya kazi na kurudi kwa kasi zaidi na kuwataka mashabiki wasubiri album yake mpya na nyimbo ambazo amemshirikisha harmonize.

WAZIRI MKUU AAGIZA ENEO LA MNARA WA ZINJATHROPOUS LIBORESHWE

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isimamie uboreshaji wa eneo la mnara wa Zinjathropus ili paweze kuvutia zaidi.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Julai 22, 2019) wakati akizungumza na wananchi na viongozi waliohudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjathropus Bosei, eneo la bonde la Olduvai, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Maadhimisho hayo yamefanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na uzinduzi wa makumbusho ya Dkt. Mary Leakey. Mnara wa Zinjathropus na Homo habilis umejengwa kwenye hifadhi ya Ngorongoro karibu na njia panda ya kuelekea bonde la Olduvai. 

"Kwenye mnara wa Zinjathropus na Homo habilis pasiachwe kama palivyo. Pajengwe seng'eng'e kuzunguka eneo lile lakini pia paweke kibanda cha mlinzi ambaye pia atakuwa anatoa taarifa kwa wageni wanaopita hapo.”

"Mtafute vijana kadhaa ambao ni wenyeji wa eneo hili, wafundishwe historia kamili kisha wapewe ajira hizo. Kibanda kikijengwa kwa juu kiwe na vioo ili anayelinda aweze kuona pande zote na pia muweze kumkinga na vumbi na upepo mkali wa eneo lile."

Waziri Mkuu pia alitembelea korongo la Frida Leakey, (mahali ambapo zinjathropous aligunduliwa) na kupata maelezo juu ya kugunduliwa kwa fuvu la mtu wa kale duniani yapata miaka milioni mbili iliyopita.

Akigusia kuhusu uhifadhi wa eneo hilo, Waziri Mkuu alisema nako pia pajengwe kibanda cha mlinzi mwenye uwezo wa kutoa taarifa kwa watalii na akasisitiza pia ajira hizo ziwahusu wenyeji wa eneo hilo. 

"Kwenye korongo la Frida, pawekwe bango lenye maelezo ya Kiswahili, nako pia wapatikane vijana sita au nane, waeleweshwe hiyo historia, wakifuzu, Wizara iwawezeshe, wapangiane zamu ya kushinda hapo. Pia pajengwe kibanda cha wageni kupumzikia wakifika eneo hilo.

Kuhusu makumbusho ya Dkt. Leakey, Waziri Mkuu alisema makumbusho hayo ni lulu kwa Taifa. "Ninawapongeza viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Ngorongoro kwa kuendeleza na kutunza makumbusho haya."

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah alisema kwa sasa dunia inatambua kuwa chimbuko la binadamu ni Afrika. “Hata kama tunatofautiana sura na rangi, watu wote duniani wana asili ya Afrika. “Kwetu sisi Tanzania, tunaadhimisha uvumbuzi huu kwa sababu fuvu la Zinjanthropus ni alama na nembo ya Tanzania na dunia.”

Alisema maadhimisho hayo yataendelea kwa kufanya maonesho ya fuvu la Zinjanthropus boisei na malikale zingine katika mikoa sita ya Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, Mtwara na Dodoma.

Alisema wizara yake imebaini fursa zilizopo kwenye sekta ya urithi wa utamaduni yaani malikale au utamaduni tuli (static cultural heritage) na utamaduni hai (dynamic culture) ili  kuvutia watilii na hivyo kuongeza idadi yao na kuwafanya waongeze muda wa kukaa nchini (length of stay) na hatimaye kuongeza pato la Taifa litokanalo na utalii. 

“Wizara yangu imeanza kuiboresha na kuendeleza sekta ya malikale na urithi wa utamaduni ili izalishe mazao ya utalii na kuvutia watalii kwa kuhamisha vituo vya Idara ya Mambo ya Kale na kuvipeleka TANAPA, TAWA, NCAA, TFS na Makumbusho ya Taifa ili viendelezwe na kuwa vivutio vya utalii.

“Pia tumehamishia Makumbusho ya Taifa kazi zote za uhifadhi wa urithi wa utamaduni tuli au malikale na kuanzisha tamasha la urithi wa utamaduni wa Mtanzania (Urithi Festival: Celebrating Our Heritage).  Tamasha hili litasherehekewa Septemba, kila mwaka.

Naye Balozi wa Marekani hapa nchini, Dk. Inmi Patterson ameipongeza Serikali kwa kukuza na kuendeleza utalii wa kitamaduni. 

Pia alisifu utajiri wa rasilmali misitu na wa nyama ambao Tanzania imejaliwa kuwa nao. "Uamuzi wa Rais Magufuli wa kuanzisha hifadhi ya Burigi, unazidi kunogesha sifa ya Tanzania katika suala la hifadhi za maliasili na utalii na katika kukuza urithi na utajiri wa nchi," alisema kwa Kiswahili fasaha.

Alisema maadhimisho hayo ni siku muhimu kwake kwani yamewakutanisha watu wa kaliba tofauti wakiwemo wanasiasa, wanasayansi, maprofesa kutoka Uingereza, Marekani na Ujerumani, wanafunzi kutoka shule za Tanzania na wenyeji wa Ngorongoro.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wakati alipotembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Marekani Tanzania, Dkt. Inmi Patterson, baada kutembelea mnara wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), uliyopo katika bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei). Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei), katika eneo alipo gunduliwa binadamu huyo wa kale na Dkt. Mary Leakey, kwenye bonde la Olduvai-Ngorongoro, Julai 22.2019, kabla ya kufungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus Boisei. Tokea kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabula.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati  akifungua maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale (Zinjanthropus Boisei). 







Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images