Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

YANGA KUANZA NA WABOTSWANA, SIMBA MSUMBIJI MICHUANO YA CAF

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira Afrika CAF wametoa ratiba ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CCL) ambapo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Simba na Yanga zikipangiwa timu kutoka ukanda wa Jangwa la Sahara.

Mabingwa wa Tanzania Simba wataanzia ugenini dhidi ya timu ya UD do Songo ya Msumbiji kati ya tarehe 09/10/11 Agosti 2019 nchini Msumbiji.

Mshindi wa mchezo kati ya Simba na UD do Songo atacheza na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets ya Malawi na Platnumz ya Zimbabwe.

Wawakilishi wengine wa michuano hiyo Yanga wataanzia nyumbani dhidi ua Township Rollers mchezo utakaochezwa kati ya tarehe 09/10/11 Agosti 2019 na baadae kurudiana nao nchini Botswana.

Mshindi wa mchezo huo atamsubiri mshindi kati ya Green Mamba Eswatin na Zesco ya Zambia.Kwa upande wa wawakilishi kutoka Zanzibar, KMKM watarusha karata yao ya kwanza kwa Desportivo De 1 Agosto ya Angola na mshindi wa mchezo huo atamsubiri na Green Eagles ya Zambia dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Kwa kuanzia msimu wa mwaka 2019, CAF wameongeza timu kutoka Tanzania kwa upande wa Klabu Bingwa ni timu mbili na Shirikisho timu mbili

KUMEKUCHA SHEREHE ZA UREMBO WA ASILI NCHINI TANZANIA,KUFANYIKA JULAI 27 NA 28 LIFE PARK

0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KUMEKUCHA Sherehe za Siku ya Urembo wa asili Tanzania!ndivyo unavyoweza kuelezea sherehe hizo ambazo zinatarajia kufanyika Julai 27 na 28 mwaka huu.

Taarifa ya Mratibu na muandaaji wa sherehe hizo Antu Mandoza ni kwamba zitafanyika eneo la Life Park Mwenge-Dar es salaam na hakutakuwa na kiingilio.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

Mandoza amesema katika siku hiyo pia watawafundisha wanawake kutengeneza vipodozi vya asili na visivyo na kemikali na watatoa kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile watu wenye ulemavu kushiriki katika maonesho hayo bure.

"Mgeni rasmi atakuwa Juliana Shonza na kutakuwa na maonesho ya Wajasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zisizo na madhara kwa ngozi na nywele , urembo na wajasiriamali wengine watashiriki.Pia kutakuwa na upimaji wa kansa ya shingo ya uzazi na ya titi bure , pamoja na burudani ya muziki, fashion shows ya wasichana naturalist na watoto,"amesema.

Tamasha hilo linalofanyika kwa mara ya pili sasa ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Antu Mandoza @missmandoza lengo kubwa ni kusaidia jamii kuepukana na matumizi ya vipodozi hatarishi vinavyosababisha madhara makubwa kiafya kama vile Kansa na pia kuwapa wanawake hasa wasichana ujasiri wa kujiamini na kujipenda walivyo." Naomba kwa wale ambao wanahitaji ufafanua na maelezo mengine ya ziada tuwasiliane kupitia mawasiliano ya namba za simu 0783324787,"amesema Mandoza.

LORD JAGANATH annual event of RATH YATRA A SUCCESS

0
0
LORD JAGANATH annual event of RATH YATRA is celebrated for past 30 years in Dar Es Salaam to bless the people of TANZANIA for peace and harmony to prevail. 
This year, the event started from 9am to 12 noon today along Kisutu area in Dar es salaam where many religious believers as well as the  High Commissioner of India to Tanzania  Hon. Sanjiv Kohli and Deputy Mayor of Hon. Mussa Swedi Kafana Dar es salaam were  also present at the Shree Sanatan Dharma Sabha  SSDS, Hindu temple.
SSDS new Chairman Mr. Sujit Bhojak was happy that the celebrations not only were a success but also went on as planned and that all that attended left satisfied
This celebrations, which are conducted worldwide, originated from PURI in  INDIA.




Milioni 150 zagharamia Mkutano Mkuu wa ALAT kwa Miaka mitano Mwanza

0
0
Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi (Kushoto) akikabidhi mfano wa Hundi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa – Mh Gulamhafeez Mukadam ikiwa ni ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wa pili kushoto ni Mkuu wa KItengo cha Huduma za Serikali – NMB – Vicky Bishubo na Katibu Mkuu wa ALAT – Elirehema Kaaya. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa.
Mwenyekiti wa ALAT Taifa - Mh Gulamhafeez Mukadam akiondoka kwa mbwembwe na cheki ya mfano ya shilingi Milioni 150 aliyopewa na Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – filbert Mponzi kama ishara ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa unaotegemewa kuanza leo jijini Mwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – John Magufuli. Wanaoangalia ni Katibu Mkuu wa ALAT - Elirehema Kaaya wa pili na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT Mh Zaynab Vulu. NMB ndiye Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa ALAT Taifa. 


Benki ya NMB imesaidia Zaidi ya shilingi Milioni 150 kwaajili ya Mikutano Mikuu ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (ALAT) kwa miaka mitano mfululizo huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na serikali za mitaa nchini kutatua changamotoimbalimbali.

Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi aliyasema hayo juzijijini Mwanza wakati akikabidhi udhamini wa Benki hiyo kama mdhamini Mkuu wawa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT unaoanza leo katika Hoteli ya MalaikaBeach jijini Mwanza.

Mponzi alisema kuwa Benki hiyo inatambua mahusiano ya kibiashara yaliyopokati ya NMB na ALAT kupitia Zaidi ya halmashauri 180 ambapo Benki inashirianakukusanya mapato ya Serikali huku akisema kusema kuwa taasisi hiyo ni mmbiawa karibu na serikali, hivyo mahusiano ya NMB na ALAT yameanza mudamrefu uliopita.

“Tunaishukuru sekretariet ya Alat pamoja na wajumbe wote kwa kuendelea
kutoa ushirikiano, kufanya biashara pamoja na sisi kama benki tumekuwa
tukiendelea kuboresha huduma zetu ili kuweza kuhudumia serikali kuu
pamoja na serikali za mitaa,” alisema Mponzi.

“Tumepeleka huduma zetu nchi nzima huku tukizifikia Zaidi ya halmashauri 180tukiwahudumia katika Nyanja mbalimbali za kibenki kuanzia wafanyakazi,wafanyabiashara na wajasiliamari na pia madiwani nah ii inaonyesha utayariwetu wa kuhudumia Serikali za mitaa.” Alisema Mponzi.

Mwenyekiti wa ALAT taifa – Gulamhafeez Mukadam ameishukuru Benki ya NMBkwa kuonyesha kujali Serikali za mitaa na mchango wa mwaka huu unaonyeshadhamira na ushirikiano wa kweli kati ya taasisi mbili.

Mheshimiwa Mukadam aliongeza kuwa jamii za Serikali za mitaa na mamlaka zakebado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kushikwa mkono nataasisi kama NMB kwaajili ya kusaidiana kutatua changamoto hizo.

Aliiomba pia Benki ya NMB kuangalia namna ya kuangalia upya misaada yakeinayotolewa kwa jamii kupitia uwajibikaji kwa jamii (CSR) akiomba Benki kuanzakusaidia jambo ambalo mwisho linakuwa kubwa kuliko misaada midogo midogoambayo inaweza ikawa na mchango mdogo kwenye jamii.

Mukadam alitoa mfano wa misaada ya vifaa vya ujenzi mashuleni na
mahospitalini na kusema kuliko kusaidia vifaa vya kuezekea, ichukue mradi mzimakama ni ujenzi wa darasa mpaka unakamilika kwa manufaa ya jamii.

“Nafikiria Benki inaweza sasa ikabadiri muelekeo wake kuhusu misaada
mbalimbali kwa jamii, kwa kuhakikisha wanachukua mradi hata mmoja mkubwakwenye wilaya na kuhakikisha wanaukamilisha kwa usimamizi wao ambao utaletaile thamani halisi ya fedha wanazotoa.” Alisema.

Mjumbe wa Kamatiu Tendaji ya ALAT na Meya wa SUmbawanga – Justine
Malisawa aliishukuru Benki ya NMB kwa kuleta mfumo wa ukusanyaji mapato yahalmashauri kielektroniki na kuisifia kuwa imeleta mafanikio makubwa kwamapato ya Serikali kuongezeka tofauti na ilivyokuwa zamani hasa ndani ya miakahii mitatu.

Maneno ya Bwana Malisawa yaliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu waKisarawe na Mjumbe wa Kamati tendaji ya ALAT – Mh Zaynab Vuli huku akisemaBenki hiyo imejipambanua kwa kufika maeneo ambayo Benki zingine hazijafika.

Mh Vulu aliiomba Benki hiyo kupunguza riba na kutoa mikopo nafuu kwa wafanyabiashara wadogo hasa wale wanaofanya biashara zao vijijini ili kusaidiamaendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini.

MHE.AWESO AKAGUA MRADI WA MAJI HEDARU SAME MKOANI KILIMANJARO

0
0

Wananchi wakichota maji katika kituo cha kuchotea maji cha Mradi wa Maji Hedaru katika eneo la Hedaru B, wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiwa katika eneo lilipojengwa chanzo cha Mradi wa Maji Hedaru katika Kijiji cha Gundusine, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiwasikiliza wakazi wa Kijiji cha Gundusine katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akikagua moja ya kituo cha kuchotea maji cha Mradi wa Maji Hedaru katika mji wa Hedaru, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule wakati wakikagua Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Tenki jipya la kuhifadhi maji la Mradi wa Maji Hedaru, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.
……………………..
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekagua Mradi wa Maji Hedaru uliogahrimu Shilingi bilioni 1.7 kwenye Mji wa Hedaru kwa lengo la kujionea changamoto zinazoukabili, ikiwemo usimamizi wa mradi katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri Aweso amekagua vituo vyote vya maji vilivyojengwa kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi katika mradi huo na kukuta vyote vikitoa maji, lakini akabaini mambo yafuatayo:- 

Chanzo cha maji kutokuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya wananchi. 
Matumizi ya mfumo wa nishati ya jua baadala ya nishati ya umeme ambayo imefika kwenye mji huo. Usimamizi mbovu wa Kamati za Maji uliosababisha mradi kutojiendesha kwa faida. 

Mgawanyo wa maji usio na uwiano sahihi na kusababisha mgogoro kwa wananchi. 

Mara baada ya kukagua mradi huo, Naibu Waziri Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) kusimamia mradi huo katika kipindi cha mpito mpaka watakapo patikana viongozi wa kamati mpya itakayosimamia mradi.Pili, ameelekeza yafanyike mabadiliko ya mfumo wa nishati ya jua kwenda kwenye umeme.

Tatu, ameelekeza kitafutwe chanzo kipya cha uhakika kitakachokidhi mahitaji halisi ya wananchi.Nne, amewataka wataalam kutoka Bonde la Mto Pangani kufika na kutatua changamoto ya watumiaji maji.Tano, amesisitiza ushirikishwaji na elimu itolewe kwa wananchi katika uendeshaji wa mradi ili waweze kuwajibika katika maendeleo ya mradi.

Aidha, Naibu Waziri Aweso amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwashirikisha wananchi katika hatua zote za ujenzi wa miradi yote ya maji, waweze kuwa wasimamizi wazuri wa miradi itakayokuwa endelevu.

SERIKALI KUJENGA CHUO CHA VETA MINYUGHE WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida jana. 
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akilakiwa na wakina mama alipo kuwa amewasili kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiwasalimia wananchi alipokuwa amewasili kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Minyughe, Nelson Kiwesi, akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Minyughe, Samuel Daniel, akizungumza kwenye mkutano huo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amesema Serikali imetenga zaidi ya sh.bilioni

mbili kwa ajili ya kujenga Chuo cha Ufundi Veta cha kisasa katika Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kingu aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia Wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuzungumzia miradi ya maendeleo iliyofanyika kwenye kata hiyo na kujua changamoto zilizopo.

"Tuna bahati sana sisi Wanaminyughe kwani serikali yetu sikivu inayoongonzwa na Rais Dkt.John Magufuli inatuletea chuo cha Veta katika kata hii tunakila sababu ya kuichagua kwa kura nyingi mwakani" alisema Kingu.

Alisema ujenzi wa chuo hicho ukikamilika kitasaidia watoto wa wilaya hiyo na maeneo mengine wanao maliza elimu ya msingi na sekobdari kwenda kupata stadi mbalimbali za ufundi na kuweza kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa nchini.

Diwani wa Kata ya Minyughe Samuel Daniel alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na nchi nzima kwa ujumla.

Daniel alisema tayari wamekwisha tenga eneo la ekari 54 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambacho kitakuwa mkombozi kwa watoto wa kata hiyo na mkoa wa Singida.

BANDARI YA KISASA KUFUNGUA LANGO LA BIASHARA KATAVI

0
0

Sehemu ya Ziwa Tanganyika likionekana likiwa limetulia 
Sehemu ya eneo itakapojengwa Bandari ya Kisasa ya Karema wilayani Tanganyika
Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Katavi na watumishi wa serikali wakiwa na Balozi Silima katika ufukwe wa Ziwa Tanganyika

************* 

Na Mwandishi wetu, Katavi 

Mradi wa ujenzi wa bandari ya kisasa utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 65 katika kata ya Karema wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi utawezesha kufungua lango kuu la biashara kati ya mkoa huo na nchi jirani ya Kongo DRC kutokana na nchi hiyo kutegemea chakula kutoka mkoani katavi ambapo kwa sasa kinasafirishwa kwa kutumia majahazi 

Akizungumza na Wanahabari Katibu tarafa wa tarafa ya Karema Bi. Zawadi Mirambo,amesema kuwa tayari wametenga eneo la ukubwa wa mita 1000 kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo hivyo mita 500 ni kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo na mita nyingine 500 ni ziada itakayoendelezwa baadae ambapo wananchi waliopo katika eneo hilo wapo tayari kupisha mradi mara watakapolipwa fidia. 

Naye Afisa Tawala wa wilaya ya Tanganyika Bwana Reginald Mhango amesema tayari serikali imekwisha idhinisha kiasi cha shilingi bilioni 25 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo. 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Bw. Selemani Kakoso amesema bandari hiyo ya kisasa itaboresha uchumi wa watu wa Katavi na nchi kwa ujumla kutokana na upande wa Kongo Kusini kupokea kiasi kikubwa cha chakula kutoka mkoani Katavi. 

“Si Mahindi na Mchele tu hata Kitunguu wanachopikia Kongo kinatoka Katavi”. Amesema mbunge huyo. 

Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Bw. Pereira Silima ambaye pia ni mlezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Katavi amefika kukagua eneo itakapojengwa bandari hiyo ambapo amewataka viongozi kuwa makini katika usimamizi wa utoaji wa fidia kwa wananchi na usimamizi wa mradi wenyewe.

Maadhimisho miaka 80 ya TAG na miaka 10 ya Mpango Mkakati wa Mavuno 2009-2019 Yafanyika Jijini Arusha.

0
0


Umati wa watu uliojitokeza katika Ibada ya kuadhimisha miaka 80 ya Kanisa la TAG Tanzania iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Karume Jijini Arusha ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa.Picha na Habari na Vero Ignatus Michuzi Blog.


Maandamano ya maandhimishonya mika 80 ya Kanisa la TAG na miaka 10 ya mpango mkakati wa mavuno 2009-2019
Maandamano yakiingia uwanjani kwaajili ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 80 ya Kanisa la Tanzania Asaemblies of God nchini Tanzania.
Maandamano yakiingia uwanja wa Shekh Amri Abeid Karume.
Wamishionari wa ww kanisa la TAG wakiwa katika maadhimisho ya miaka 80 ya Kanisa hilo .
Baadhibyavwachungaji wakiwa katika ibada ya kuadhimisha miaka 80 ya kanisa la TAG iliyofanyika kitaifa Jijini Arusha.
Baadhi ya wachungaji wakimuomba Mungu katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG leo Jijini Arusha.
Vijana wa CAS kama wanavyoonekana katika picha wakicheza kwa furaha katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa lao la TAG yaliyofanyika kitaifa Jijini.Arusha.
Umati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG tangia kuanzishwa kwake mwaka.1939 mkoani Mbeya.
Baadhi ya wamishionari wa Kanisa la TAG wakiwa katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa hilo yaliyofanyika Jijini Arusha katika uwanja wa makumbusho ya Sheikh Amri Abeid Karume leo.
Mass Preise Team wakiwa wanaimba katika maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa la TAG na Mpango utekelezaji wa mkakati wa mika 10 ya mavuno



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Maadhimisho ya miaka 80 ya TAG na miaka 10 ya mpango mkakati wa mavuno 2009-2019 yamefanyika jijii Arusha na kuhuduhriwa na viongozi mbalimbali wa dini na waumini wa kanisa hilo.

Dkt.Barnabas Mtokambaki ni Askofu mkuu wa Kanisa la TAG nchini Tanzania ambapo pia ni Rais wa kanisa hilo Afrika, Maadhimisho hayo Askofu mkuu wa amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Tanzania kwa kulipenda Kanisa hilo na kuwajali.

Mpango mkakati wa awamu ya kwanza ya mafanikio ya kanisa la TAG kwa mujibu wa Dkt.Mtokambali wameyapata katika miaka 10 ya mavuno kwani majimbo yameongezeka kutoka 10-69,makanisa 2,619-9,986,wachungaji 2,616-10,085,washirika kuongezeka 200,069-13,326,vyuo vya Biblia 4-8 ambapo Idara ya kujenga shule za sekondari na nyingine zitaanza kuandikisha wanafunzi mwezi Januari 2020.

Ameeleza changamoto kubwa waliyonayo ni eneo la kujenga ofisi kwani makao makuu ya kanisa hilo yaliyopoubungoba limekuwa na nafasi ni ndogo ukilinganisha na wingi wa idadi ya waumini waliopo hivyo wamemuomba Dkt.Magufuli kuwatazama upya na kuwapa eneo kwaajili ya ujenzi sambamba na kuondolewa kodi ya vifaa ambavyo vipo bandarini.

Vile vile Dkt.Mtokambali ameweza kukabidhi mifuko 1000 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwaajili ya kumalizia ujenzi katika shule zilizopo mkoani huko ambapo awali alishawahi kutoa mifuko mingine 5000 ya saruji.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamuhuri ya Tanzania ambapo amewakilishwa na waziri mkuu Kasimu Majaliwa ambapo amesema kuwa serikali imedhamiria kuwatumikia watanzania wote bila kujali dini wala siasa.

Amesemaserikalivya awamu ya tano itaendekea kudumisha umoja na ushirikiano na Taasisi za kidini Mungu katika utekelezaji wa majukumu yake yote wakati wanasheherehekea mpango mkakati wa mavuni ni vyema wakakumbuka mchango wa waanzilishi wote wa Kanisa hilo na kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi kufikia,walipo sasa.

Mhe.Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuendelea kuendelea kuimarisha kitengo chao cha kuinua miradi itakayowafaidisha na kuwainua kiuchumi.

Akijibu ombi la lililoletwa na Askofu mkuu wa Kanisa la TAG Dkt.Barnabas Mtokambali kuhusu eneo la kanisa lililopo Ubungo kitalu namba 434 G unamilikiwa na TTCL,Waziri Mkuu amesema ombi hilo limepokelewa na atalifanyia kazi.

Vile vile Mhe. Waziri Mkuu alitolea ufafanuzi kuhusiana na msamaha wa kodi kwa vifaaa na kusema kuna baadhi ya Taasisi za kidini zilitumia vibaya msamaha huo wa kodi ndiyo walisababisha eneo hilo kuwekewa sheria ila ameahidi swala hilo atalifikisha kwa Mhe.Rais wa Tanzania Dkt.Magufuli.

Serikali inaendelea kusimamia swala la Amani na utulivu sambamba na kudhibiti matukio yote yanayovunja Amani ambaposerikali inawategemea sana viongozi wa dini.

"Endeleeni kuliombea taifa na viongozi wake ili kuliombea taifa na viongozi wake mnajua fika kuwa Mhe.Rais anahitaji kuombewa sana na nyie viongozi wa dini" ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi"alisema Waziri Mkuu.

Amehitimisha kwa kusema kuwa Seririkali inaendekea kuliongoza taifa la Tanzania kwa kufuata miongozo mbalimbali kama Katiba na sheria katika katika kila nyanja na kwa maslalahi ya Taifa.Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Viongozi wa dini kichocheo cha usalama na Amani katika mkoa wa Arusha .

"Hata mimi nilipoteuliwa kuwa kiongozi mahali pa kwanza nilipokwenda kuripoti ni kwa viongozi wa dini na kuwaambia mimi ni kijana wenu naomva ushirikiano wenu na popote nitakapotetereka mnirekebishe"

Kanisa hilo la TAG lilianza kazi nchini mwaka 1939, Igale Mbeya,Askofu wa kwanza akiwa Emmanuel Lazaro,Mwanisongile,na awamu ya tatu Dkt.Barnabas Mtokambali, ambapo hivi sasa yapo makanisa 9,986, vyuo vya Biblia 8 vyuo vya kupanda makanisa ,shule za sekondari,vyuo vya ualimu ambavyo vinakaribia kukamilika,vituo vya Radio,vyuo vya ualimu,vituo vya Afya na vituo vya huduma za jamii kwa watoto yatima.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI IKULU DSM.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 22,2019

MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA WAZIRI SIMBACHAWENE, NAIBU WAZIRI BASHE

0
0
*Asema ana matumaini makubwa dhidi yao, hivyo wachape kazi
*Awambia anajua watapigwa vita sana lakini watamngulize Mungu

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kwa wakati.

Akizungumza baada ya Simbachawene na Bashe kula kiapo leo Julai 22 mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amewaambia kuwa wawe chachu ya kuhakikisha changamoto zilizopo zinapata ufumbuzi wa haraka.

Rais Magufuli wakati anamzungumzia Simbachawene amesema Wizara yake inahusika na masuala ya Muungano , hivyo akahakikishe anakuwa chachu ya kuuimarisha muungano na si kuwa chachu ya kuuvuruga.

Kuhusu eneo la mazingira Rais Magufuli amemwambia Waziri Simbachawene kuwa akahakikishe anaisimamia NEMC kuhakikisha vibali vinatoka kwa wakati, kwani kuna ucheleweshaji mkubwa wa vibali NEMC.

"Tunahitaji viwanda hivyo lazima vibali navyo vitoke kwa wakati na ikiwezekana viwanda viwe vinaanza halafu mambo ya vibali yanafuata baadae maana kumekuwa na tabia ya kucheleweshwa kwa vibali.

"Kwa hiyo nenda kasimamie hili , kaa na watalaamu wako kuhakikisha mnasimamia hili la vibali na mambo mengine muhimu.Pia hakikisha unasimamia na kutekeleza majukumu yako kwa wakati.

"Nakumbuka suala la katazo la mifuko ya plastiki nililizungumza kwa muda mrefu lakini hakulitekelewa hadi nilipoamua kutoa maagizo ya lazima ndipo likafanyika. Nenda kafanyie yale ambayo umeyaapa leo hii tena kwa wakati,"amesema Rais Magufuli wakat anatoa maelekezo kwa Simbachawene.

Wakati huo huo amesema kwenye eneo la mazingira kuna fedha nyingi zinaelekezwa huko lakini haziendani na uhalisia na kwamba kumekuwepo na miradi hewa akitoa mfano mradi wa upandaji mikoko Rufiji , hivyo amemtaka Simbachawene kwenda kusimamia vizuri eneo la mazingira.

Pia Rais Magufuli amesema siku za karibuni anajiandaa kufanya mazungumzo na wafugaji wote nchini ili kusikiliza changamoto zao,ili zipatiwe ufumbuzi.

Kuhusu Naibu Waziri Bashe,Rais Magufuli amesema kuwa amekuwa akimfuatilia bungeni na namna ambavyo amekuwa akichambua hoja na mijadaa inayohusu sekta ya kilimo.

"Nimekuwa nikikufuatilia sana unapozungumza bungeni, sasa yale uliyokuwa unayachambua nenda kayafanye kwa vitendo.Najua hutashindwa kutekeleza kwa vitendo.Pia natambua kuna changamoto nyingi katika eneo la kilimo na kutoa mfano kuwa Bodi ya sukari inafanya kazi nzuri sana lakini inapigwa vita sana.

"Nilikuwa nasubiri tu nione kama Waziri wa Kilimo ataivunja bodi lakini ana bahati hakufanya hivyo kwani angekiona cha mtema kuni.Lazima niseme ukweli, bodi inafanya kazi nzuri lakini kuna baadhi ya watu wanaipiga vita kwa maslahi yao binafsi,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua Wizara ya Kilimo ikisimamia vizuri italeta matumaini makubwa kwa wananchi huku akitumia nafasi hiyo anafahamu changamoto iliyopo katika zao la kahawa mkoani Kagera.

"Hata hivyo pamoja na Serikali kutoa maelekezo kuhusu bei ya kahawa, ninazo taarifa kuna wafanyabiashara wameanza kuwadaha wananchi, hao lazima washughulikiwe tena washughulikiwe kwa mkono mkubwa,"amesema.

Rais Magufuli amemtaka Bashe na Waziri wa Kilimo kushirikiana katika kutatua changamoto za sekta ya kilimo huku akitoa rai kuwa lazima wakulima wanufaike na kilimo chao kwa kulipwa fedha zao kwa wakati.

"Katika zao la pamba nako lazima Wizara hii isimame imara kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanapata fedha zao kwa wakati .Lazima tuhakikishe wakulima wanyonge wanasimamiwa vema na ukweli uliopo sekta ya kilimo imebeba matumaini ya wananchi walio wengi.Hivyo nenda mkashirikiane kuisimamia vizuri,"amesema Rais Magufuli.

Pamoja na maelekezo ambayo ameyatoa kwa mawaziri hao, Rais Magufuli amesema anajua baada ya kuwaapisha kwenye nafasi hizo watapigwa vita sana lakini wakamtangulize Mungu ili kuyashinda majaribu."Najua mtapigwa vita sana lakini kafanyeni kazi tu."
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.Simba Chawene  pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe 

WAZIRI MKUU AZINDUA KITUO CHA HUDUMA ZA UTALII WILAYANI KARATU

0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa bwana Francis Theodosia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Julai 21.2019. ( 
………………… 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao. 

“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili. Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema. 

Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la polisi kwa ajili ya patrol ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha. 

Waziri Mkuu alizindua kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido). 

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.” 

Aliwataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi. 

Pia aliwashukuru viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu. Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20. 

“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema. 

Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi ya 10 yamesimamishwa njiani. 

“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo, akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke juani wakati mwenye makosa ni dreva?” 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata hukohuko,” alisema. 

Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini.

NAIBU WAZIRI BASHE AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA KILIMO

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

NAIBU Waziri wa Kilimo amesema anafahamu changamoto zilizpo kwenye sekta ya kilimo, hivyo atashirikiana na Waziri wa Kilimo kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

Bashe ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kula kiapo mbele ya Rais Magufuli ambapo amesema kuwa anaifahamu sana sekta ya kilimo kutokana na Spika kumteua kuwa mjumbe katika kamati.

"Wanyonge katika nchi hii wako katika eneo la kilimo na anafahamu changamoto zilizopo kwenye sekta ya kilimo na sasa nitakwenda kushirikiana na viongozi wengine kutatua changamoto.

"Nitatumia kila aina ya uwezo wangu kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kilimo,"amesema Bashe na kuongeza sekta ya kilimo imebeba sehemu kubwa ya wananchi ambao wanategemea kilimo, hivyo lazima sekta hiyo isimamiwe vizuri.

WATOTO WA KIKE MSIKUBALI KUDANGANYWA – WAZIRI MKUU

0
0


*Awaonya vijana, wazee wanaotaka kuwaoa, asema miaka 30 jela ni yao 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watoto wa kike wasikubali kudanganywa na wanaume na badala yake wakazanie masomo hadi wahitimu elimu ya juu. 

“Wasichana wote mliopo hapa, mwanaume yeyote akikufuatafuata mwambie usinusumbue; mwambie niache nisome. Kamwe msikubali kudanganyika, someni hadi mmalize Chuo Kikuu,” alisema. 

Ametoa wito huo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wakazi wa wilaya za Same na Mwanga akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. 

Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ziara ya siku nne mkoani humo, amewaonya vijana na wazee ambao wana tabia ya kuweka mahusiano ya kimapenzi na watoto wa kike kwamba waache mara moja la sivyo wataishia jela. 

“Wanaume msisahau kwamba mtoto wa mwenzio ni wako. Nataka niwakumbushe kuwa ukimuona mtoto wa kike, muache. Huyo ni moto wa kuotea mbali. Ukimchumbia, ukimuoa, au kumpa mimba mtoto wa kike, ujue kuwa miaka 30 jela ni yako.” 

“Serikali ya awamu ya tano, imeamua kuwekeza kwa mtoto wa kike, kwa hiyo tunataka watoto wa kike wakianza shule ya awali, wasome shule ya msingi, waende sekondari hadi wamalize Chuo Kikuu,” alisisitiza.

NDUGU LUBINGA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI GEITA

0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,Mkuu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Geita,Ndugu Ngemela Lubinga ameanza ziara ya kikazi Mkoani Geita na amewasili wilaya ya Bukombe na kupokelewa na viongozi wote wa Mkoa wa Geita wa Chama na Serikali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Ndg.Dotto Biteko. 

Lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha uingizaji wa wanachama kwa njia ya kielekroniki na kubaini changamoto za uingizaji wa wanachama kwa njia ya mfumo huo,pamoja na kukagua uhai wa chama na Jumuiya zake na atafika katika kila wilaya pamoja na kata na kuzungumza na viongozi wa ngazi ya matawi na mashina pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. 
Wakati huo huo alipata nafasi ya kuzungumza na kamati ya Siasa ya Wilaya ambapo alipokea taarifa fupi ya kazi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake pamoja na hilo akawaambia “ninyi viongozi wa wilaya mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha viongozi wa kata,shina na matawi wanashikamana na kuwa wamoja na kuwaheshimu tunaowaongoza”. 

Ndugu Ngemela Lubinga amewaambia viongozi hao kuwa dhamana waliyonayo ni kubwa hivyo waitumie vyema kuhakikisha wanakwenda kwa wananchi kuwaelezea mambo yote makubwa yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili wajue kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM maana Watanzania wengi ni waungwana sana. 

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Geita Ndugu.Iddi Kassim Iddi alipata nafasi ya kukabidhi ahadi yake ya jezi kwa timu nne za mpira alizokuwa ameahidi vijana wa Bukombe mbele ya mlezi huyo.

Makamu wa Rais kufungua maonyesho ya Nanenane Simiyu

0
0
Kwa kutambua mchango wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kuinua uchumi wa Tanzania, Wakuu wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kwa kushirikiana na Mawaziri wenye dhamana ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wanawakaribisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wadau wengine kwenye maonesho na maadhimisho ya sikukuu ya Nanenane Kitaifa yatakayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 28/07/2019 na kilele chake kuwa tarehe 08/08/2019.

Ufunguzi rasmi wa Maonesho hayo utafanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan siku ya tarehe 01/08/2019. Kaulimbiu ya Nanenane mwaka huu ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.

Wakati wa maadhimisho hayo, tarehe 03/08/2019 itakuwa siku ya “Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP ll)” Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasimu Majaliwa Majaliwa, siku ambayo wananchi watajenga uelewa zaidi kuhusu utekelejazi wa “Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili’

Mgeni Rasmi siku ya kilele ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kutakuwa pia na mafunzo ya nadharia na vitendo kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi ili kuongeza uzalishaji na tija. Sambamba na hiyo kutakuwa na kongamano kuhusu namna bora ya kuendesha kilimo biashara, teknolojia mpya, masoko na mitaji.

KARIBUNI KANDA YA ZIWA MASHARIKI ili kuona fursa mbalimbali zitakazomwezesha mwananchi kuinua uchumi wake binafsi na Taifa kwa ujumla

KAULI YA WAZIRI SIMBACHAWENE KWA RAIS MAGUFULI BAADA YA KULA KIAPO

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene amesema anamshukuru Rais John Magufuli kwa kumianini tena na kumpa nafasi tena nafasi ya kuwa Waziri kwenye Serikali yake.

Akizungumza baada ya kuapishwa leo Julai 22,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam Waziri Simbachawene amesisitiza kuwa "Kwa heshima kubwa mimi na familia yangu tunakushukuru sana, kwa kuniamini na kunipa nafasi tena.

"Rais wangu nafahamu nini maana ya kula kiapo ,ni kuahidi kuendelea kuviamini viapo vyote na kuvitunza hadi uzeeni kwanu.Leo kiapo ambacho nimeapa ni cha tano kwangu,"amesema Waziri Simbachawene.

Kuhusu nafasi yake baada uteuzi wa Rais na kisha kula kiapo, amesema anafahamu kuwa nchi yetu inayo matatizo makubwa katika mazingira na kuna fedha nyingi ambazo zinaingia kwa ajili ya eneo la mazingira lakini hazitumiki kama inavyotakiwa.

"Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, hivyo najua changamoto zilizopo katika eneo la mazingira na fedha ambazo zinaingia nchini kwa ajili ya mazingira lakini zinatumika kinyume na malengo ya hizo fedha.Hili nitalisimamia na kuhakikisha fedha za mazingira zinatumika kwa ajili ya mazingira yetu na si vinginevyo,"amesema.

Waziri Simbachawene amesema anafahamu kuwa kuna uharibifu mkubwa wa mazingira katika jami yetu." Nikuhakikishe Rais , kwa kumsaidia Makamu wa Rais kwenye ofisi yake, pamoja na wengine nitakaowakuta ofisini nitashirikiana nao na kutoa mawazo yangu ili kuokoa mazingira."

Amefafanua kuwa suala la mazingira linaweza kuzungumzwa kwa aina tofauti, kwani mazingira kimataifa na mazingira kitaifa.Hivyo atajitahidi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Pia amesema anafahamu analo jukumu kwenye eneo la Muungano na katika eneo hilo atajitajidi kadri ya uwezo wake na hasa kwa kuzingatia yeye ni Mwanasheria na Wakili atatumia kila aina ya maarifa yake kuhakikisha muungano unaendelea kuwa imara.

WAZIRI MKUU: TUMIENI FURSA ZA UTALII KUBORESHA MAISHA YENU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Bashay, wilayani Karatu watumie fursa zinazojitokeza kwenye sekta ya utalii kuboresha maisha yao.

“Tumieni fursa ya uwepo wa eneo hili. Halmashauri wakishajenga vizimba vya biashara, leteni bidhaa zenu kama vile picha za tingatinga, mapambo, vinyago na vyakula vya asili ili watalii wakija hapa wapate huduma kutoka kwenu,” alisema.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vituo vya polisi vya kupunguza changamoto kwa magari ya utalii barabarani na kukabidhi gari la polisi kwa ajili ya patrol ya watalii katika eneo la Bashay, wilayani Karatu, mkoani Arusha.


Waziri Mkuu alizindua kituo cha kutolea huduma za usalama kwa watalii wilayani Karatu ikiwa ni ishara ya kuwakilisha vituo vingine vitatu vinavyoendelea kujengwa mkoani Arusha katika maeneo ya Kikatiti (Arumeru), Makuyuni (Monduli) na Engikaret (Longido). 

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi hao wawalinde watalii ili waitangaze vema nchi ya Tanzania pindi wakirudi makwao. “Ili kukuza na kutangaza utalii, tunapaswa tuwe na mapenzi mema kwa watalii lakini kikubwa zaidi ni usalama wao.” 

Aliwataka wakazi hao waendelee kuiamini Serikali ya awamu ya tano na waendelee kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili apate nguvu ya kuleta maendeleo zaidi. 

Pia aliwashukuru viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators (TATO) kwa kuchangia ujenzi wa vituo hivyo na kutoa gari jipya la polisi kwa ajili kituo hicho cha Karatu. Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililogharimu dola za Marekani 45,000, limepewa namba za usajili za PT 4190. 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa Bashay waliohudhuria hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ujenzi wa vituo hivyo umetokana na malalamiko aliyopokea kwamba watalii wakitoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi kufika Karatu wanakuwa wamesimamishwa njiani zaidi ya mara 20. 

“Tulijiuliza hawa watalii wamekuja kutalii, wanataka kupumzika, sasa ni kwa nini wasumbuliwe kiasi hicho? Tuliamua kuanzisha vituo vya aina hii, ili watalii wafanyiwe ukaguzi kwenye check-points maalum,” alisema. 

Aliomba Jeshi la Polisi liwapange barabarani askari ambao ni weledi na wana uelewa wa masuala ya utalii na kutolea mfano wa wiki iliyopita ambapo alikuwa akitokea mjini kwenda Karatu na kukuta magari ya watalii zaidi ya 10 yamesimamishwa njiani. 

“Niliona baadhi yao wakiwa wamelala kwenye magari kwa uchovu, nilipowauliza wamekalishwa kwa muda gani, walisema ni kwa zaidi ya dakika 45. Nilipomuuliza askari aliyewasimamisha ni kwa nini anafanya hivyo, akanijibu kwamba dereva amemjibu vibaya. Hivi ni kwa nini watalii wateseke juani wakati mwenye makosa ni dreva?” 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa TATO, Bw. Henry Kimaro aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya za kupambana na ujangili na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini. “Tumeona hivi karibuni watalii wengine kutoka Israel, China na sasa ndege yetu imeanza kwenda India kuwafuata hukohuko,” alisema. 


Alisema wameanza na vituo hivyo vinne mkoani Arusha lakini tatizo hilo liko maeneo mengi nchini na wao hawawezi kufika nchi nzima kutoa huduma kama hiyo. Hivyo, alimuomba Waziri Mkuu awahimize Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao zinajihusisha na sekta ya utalii, waige mfano wa wilaya ya Karatu ili kuhakikisha usalama wa watalii wawapo nchini.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati alipofungua kituo cha huduma za utalii, katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Julai 21, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua kituo cha huduma za utalii, kilichopo katika Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia kituo kidogo cha Polisi kilichopo katika kituo cha huduma za utalii, wilayani Karatu, kabla ya kukifungua rasmi, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipewa maelezo na Mrakibu wa Polisi Joseph Bukombe, ndani ya kituo kidogo cha Polisi, kilichopo katika kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019. Tokea kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua gari jipya la Polisi, lililokabidhiwa kwa ajili ya kuwahudumia watalii, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi gari jipya la Polisi, litakalotumika kwa ajili ya kuhudumia watalii, kwa Kaimu RPC Mkoa wa Arusha James Manyara, kwenye kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kuzindua rasmi  kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mke wa Bwana Joseph Erro, Bibi Evalina Madawe, ambaye amejitolea kiwanja kilichotumika kujengea kituo cha huduma za utalii wilayani Karatu, katika Mkoa wa Arusha, Julai 21.2019. Kulia ni mtoto wa bwana Francis Theodosia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA BAJETI YA MAENDELEO SEKTA YA KILIMO

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Serikali imeshauriwa kuona umuhimu wa kuongeza bajeti ya maendeleo katika sekta ya kilimo kutoka asilimia 2 ya sasa kukidhi azimio la Malabo na Maputo linalizitaka serikali kutenga asilimia 10 kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza mchango wa sekta hiyo kuchangia katika pato la taifa na usalama wa chakula.

Pia imepongezwa kwa dhati kwa mikakati yake na jitihada kubwa katika kuendeleza na kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini katika kufikia azma ya mapinduzi ya viwanda.

Katika hatua za awali kutekeleza azma hiyo serikali imefuta na kupunguza ada na tozo 54 zinazotozwa na wizara idara na taasisi zinazojitegemea ili kuondoa kero na urasimu kwa wafanyabiashara na kuboresha mazingira ya biashara.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha wakati akichambua bajeti ya serikali hususani kwenye sekta ya kilimo Mwenyekiti wa baraza la taifa la kilimo ,Jackline Mkindi ambaye pia ni Mkurugenzi wa TAHA alisema kuwa kwa misingi hiyo ukuaji wa uchumi umekuwa kwa asilimia 7.0 mwaka 2018 kulinganishwa na mwaka 2017 kwa asilimia 6.3.

Amesema kuwa pato la taifa limefikia trillion 129.4 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na shilingi trillion 118 mwaka 2017 na kilimo kinachangia katika pato la taifa asilimia 28.2 hivyo uwekezaji mkubwa unahitajika

Kwa mujibu wa Mkindi uboreshaji wa mazingira mazuri ya kilimo biashara katika kuimarisha mazingira mazuri ya kilimo nchini hotuba hiyo ya waziri wa kilimo imeonyesha kuwekeza nguvu zaidi mpango kazi wa kuboresha mazingira ya biashara katika sekta ya kilimo ili mazingira yawe rafiki na na yenye gharama nafuu.
Mwenyekiti wa baraza la Taifa la kilimo ambaye pia ni Mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkindi akizungumza na waandishi wa habari

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA SIMBACHAWENE NA BASHE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. George Simbachawena kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela akiwalisha viapo vya maadili ya viongozi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene na Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo, baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. Hussein Bashe baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe. George Simbachawena baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene na Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na viongozi waandamizi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene na Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na viongozi wakuu wa vyombo vy ulinzi na Usalama katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene na Mhe. Hussein Bashe Naibu Waziri wa Kilimo baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akijiandaa kundoka mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Julai 22, 2019 PICHA NA IKULU.
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images