Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

MHANDISI MTIGUMWE AKERWA NA KUSUASUA KWA MRADI YA ERPP HUSUSANI KATIKA UJENZI WA MAGHALA

0
0



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

KATIBU mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amefanya ziara katika Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga-ERPP) unaotekelezwa katika Wilaya za Kilosa, Kilombero na Mvomero Mkoani Morogoro na kutorishwa na kasi ya wakandarasi katika ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia Mpunga.

Mradi wa ERPP unatekelezwa na Wizara ya Kilimo ukiwa na lengo la kuongeza tija katika uzalisha wa zao la Mpunga kwa kutoa mbegu bora za zao hilo, ukarabati wa skimu za umwagiliaji ujenzi wa Maghala pamoja na utafutaji wa masoko.

Aidha Mradi wa ERPP unatekelezwa katika Visiwa vya Zanzibar huku Tanzania Bara ukitekelezwa katika Maeneo matano ya Mkoa huo.

Akiwa katika ziara hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ametembelea ujenzi wa Maghala katika Kijiji cha Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ghala la Kijiji cha Msolo ujamaa Kilombero, Kijiji cha Njage Kilombero pamoja maghala ya Kijiji cha Kigugu na Mbogo katika Halmashauri ya Wilaya Mvomero.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa serikali haitosita kuwachukulia hatua wakandarasi hao kwa kuchewesha kazi wanazopatiwa pasina kuwa na sababu za msingi.Amesema kuwa hatua zitakazochuliwa ni pamoja kupeleka mapendekezo katika bodi za wakandarasi ili kampuni hizo ziweze kufutiwa usajili nchini kutokana na kutotimiza matakwa ya serikali katika ujenzi wa maghala hayo ikiwemo kutokukabidhi kazi kwa wakati pamoja na ujenzi chini ya Kiwango.

Akiwa katika Kijiji cha Mbogo Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo ametaka kuchunguzwa kwa Mkandarasi wa kampuni ya Skemu ya Mkoani Morogoro kutokana kuwa nyuma ya kazi tofauti na Mkataba wa kazi hiyo unavyoelekeza.

Amesema kuwa Mkandarasi huyo pia ameshindwa kuweka uzio mzuri katika eneo la ujenzi kutokana kutumia mabati mabovu hivyo kumtaka aubomoe kisha kujenga mwingine kama alivyoekezwa katika mkataba.

Awali Viongozi wanaosimami mradi huo katika Mkoa wa Morogoro walimueleza katibu Mkuu wa Kilimo kuwa Baadhi wa wakandarasi wamekuwa wazito katika ujenzi hali inayotia wasiwasi wa kushindwa kukabidhi kazi kwa wakati.

Nao Baadhi ya wananchi wakizungumza kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi huo na kueleza kuwa utakuwa chachu ya kuongeza uzalisha wa zao la Mpunga hali itakayofanya waweze kuongeza pato lao pamoja na kuchangia uchumi wa Taifa

kwa Upande wao wakandarasi hao wamesema kuwa awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali huku pia wakimuahidi katibu Mkuu huyo kukamilisha kazi kwa wakati na kiwango kinachotakiwa na serikali.

DC Ndejembi Aahidi kumaliza mgogoro uliodumu kwa miaka 13 ndani ya Siku 10

0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhe Deo Ndejembi amekutana na viongozi wa Kata ya Lenjuru na Kata ya Njoge ili kutatua mgogoro wa mipaka ambao umedumu kwa kipindi cha miaka 13.

Akizungumza baada ya mkutano aliofanya na viongozi wa pande zote mbili Mhe Ndejembi ameeleza kugundua kiini cha mgogoro huo ni maslahi binafsi ya watu ambapo ubavu mmoja unafanya eneo hilo kama malisho ya mifugo yao huku upande mwingine ukiwa umeuza maeneo yao kwa wakulima na hivyo kusababisha mgongano huo.

" Baada ya kusikiliza pande zote mbili nimegundua kuna mgongano wa kimaslahi baina yao, mwanzoni walikubaliana kwamba pande zote mbili zitumie eneo la mpaka kama malisho, hivyo nimetoa maelekezo kwamba kabla ya Julai 30 mwaka huu tukutane tena tukiwa na ramani ya Wilaya na Kata zote mbili ili tuweze kubainisha mpaka huo," amesema DC Ndejembi.

Aidha DC Ndejembi amesema watawapokonya mashamba wale wote waliogaiwa kinyume na taratibu na kuyarudisha kwenye Serikali ya Kijiji baina ya kubaini wapo baadhi ya watu waliogaiwa mashamba hayo kinyume na utaratibu.

" Wale ambao wanamiliki mashamba kinyume na utaratibu wajiandae kuyarudisha, Sheria no5 ya mwaka 1999 toleo la 2002 linasema wazi kwamba Kijiji mwisho wake kutoa ni ekari 50 lakini Kijiji hiki cha Njoge kimempa Mfanyabiashara mmoja mkubwa Ekari zaidi ya Ekari 1200 kinyume na utaratibu na eneo hilo wamemgawia kutoka kwenye eneo la malisho jambo linaloleta mgogoro huu," amesema DC Ndejembi.

DC Ndejembi amesema maamuzi yake kuhusu mgogoro huo yanaenda kwenye ramani ambayo inaonesha mpaka kati ya Kata ya Pandambili na Njoge kwa sababu Lenjuru ilizaliwa kutoka Kata ya Pandambili na Njoge haikuwahi kumegwa, hivyo maamuzi yake ni kwenda kwenye mpaka halisi kwa sababu ilipozaliwa Kata ya Lenjuru hakuna kilichobadilika zaidi ya mpaka uleule uliokuepo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza na viongozi wa Kata za Lenjuru na Njoge katika mkutano wa kutatua mgogoro wa mipaka baina ya Kata hizo mbili uliodumu kwa miaka 13
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi (katikati) akijadiliana jambo na viongozi wa Kata za Lenjuru na Njoge baada ya kumaliza nao mazungumzo yaliyolenga kutatua mgogoro baina yao uliodumu tangu mwaka 2006

Mbunge Ditopile amwaga mifuko 100 ya saruji UVCCM Ruvuma

0
0

Na Charles James, Michuzi TV

Mbunge wa Viti Maalumu Taifa anayewakilisha vijana, Mhe Mariam Ditopile amechangia mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Sita Kwa ajili ya kujenga Hosteli za Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoani Ruvuma.

Mhe Ditopile ametoa mifuko hiyo ya saruji wakati aliposhiriki shamrashamra za Ruvuma ya kijani na kutekeleza ombi la vijana wa Mkoa huo waliomuomba kutoa mchango wake kwa ajili ya Hostel hizo ambazo zitatumika kama kitega uchumi cha UVCCM mkoani humo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo ya Ruvuma ya kijani Mhe Ditopile amempongeza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma, Raymond Mhenga kwa maandalizi mazuri pamoja na uthubutu wao kama vijana wa ujenzi wa Hosteli hizo ambazo zitaimarisha uchumi wa Umoja huo.

" Nitumie fursa hii kuupongeza Uongozi wa UVCCM Ruvuma chini yake Comrade Mhenga, tunaposema uchumi wa kati ni pamoja na Umoja wa vijana, hivyo nimetoa mifuko hii 100 ya saruji ili kuhakikisha hostel hizi zinakamilika na kuwa sehemu ya kitega uchumi cha UVCCM.

" Mimi kama Mbunge naetokana na Umoja huu na kuwakilisha vijana nawaahidi ushirikiano na kuwa nanyi bega kwa bega, tupeane ushauri na kusaidiana kwa pamoja leo likiwa ni kumuunga mkono Mhe Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wetu, "amesema Mhe Ditopile.

Nae Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma, Raymond Mhenga amempongeza Mhe Ditopile kwa kazi kubwa anayofanya katika kuwatumikia Watanzania Nchi nzima hasa vijana na kumuomba kuendelea kushirikiana na Umoja huo katika kila kujenga Tanzania yenye uchumi wa kati.
 Mbunge wa Viti Maalum Taifa anayewakilisha Vijana, Mhe Mariam Ditopile akikabidhi mifuko ya Saruji aliyoitoa kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoani Ruvuma kwa ajili ya ujenzi wa Kitega Uchumi cha Umoja huo.
 Mifuko ya Saruji yenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Sita iliyotolewa na Mh Mariam Ditopile kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM mkoani Ruvuma kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli ambayo itatumika kama kitega uchumi cha Umoja huo.
Sehemu ya Wanachama na Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria shamrashamra hizo za Ruvuma ya Kijani zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM ambapo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Mariam Ditopile alitoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Hostel

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA UFUNGUZI WA RELI YA TANGA - MOSHI/ KILIMANJARO

0
0


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe . Kassim Majaliwa amefanya ufunguzi wa njia ya reli ya Tanga mpaka Moshi / Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika mjini Moshi , Kilimanjaro Julai 20, 2019, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wa vyama pamoja na wa dini.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amelipongeza Shirika la Reli Tanzania -TRC kwa Kurejesha njia ya Tanga-Moshi ambayo takribani zaidi ya miaka 12 ilikuwa haifanyi kazi. Waziri Mkuu amesema kuwa mafanikio haya ni utekelezaji wa sera ya kitaifa na Mkakati wa Nchi kuinua sekta mbalimbali za kimkakati ili inchi ya Tanzania ifikie Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri mkuu aliongeza kuwa juhudi na kujitoa kulikofanyika kurejesha njia ya reli kuanzia Dar es Salaam hadi Tanga na kisha kuelekea Moshi ,Kilimanjaro ni uamuzi wa busara uliokuja kwa wakati na unaoshamirisha azima yetu ya kuchochea ukuaji wa uchumi lakini na kuyabadili maisha ya wananchi kupitia huduma bora za usafiri na uchukuzi .

“ Kamwe hatuwezi kufikia hadhi hiyo muhimu kiuchumi bila kuwa na miundombinu imara ikiwemo ya reli “ amesema Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania inapakana na nchi zaidi ya tano ambazo zinategemea sana miundombinu ya nchi ya Tanzania ya usafirishaji na uchukuzi ndani ya nchi ili kupitisha bidhaa. Pia aligusia juu ya mradi mkubwa wa kihistoria wa SGR unaoendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Mokutopola na kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano imewekeza takribani Shilingi Bilioni 7.2 fedha za walipa kodi kutekeleza mradi huo .

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha pia amepongeza bodi na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania katika ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya ufufuaji wa Shirika na njia mbalimbali za reli zilizokufa kwa miaka mingi hapa nchini. Hata hivyo Naibu Waziri ametoa rai kwa wafanyazi wa Shirika la Reli na watanzania kwa ujumla kuwa walizi wa miundombinu ya reli ambayo ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa nchi yetu.

“TRC limepewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia uhuishaji na utendaji wa shirika pamoja na kuboresha huduma za reli “ amesema Mhe . Nditiye .

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania ndugu Masanja Kungu Kadogosa ametoa Shukrani za dhati kwa Waziri Mkuu kuitikia wito wa ufunguzi wa reli hiyo ya Tanga hadi Moshi / Kilimanjaro ulioambatana na uzinduzi wa safari za treni za mizigo kutoka bandari za Dar es Salaam na Tanga kuelekea Moshi Kilimanjaro. Ndugu Kadogosa aliwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Reli kwa uzalendo na juhudi kubwa walizofanya katika mradi wa ufufuaji wa njia ya reli kutoka Tanga hadi Moshi.

“Timu ya kutekeleza mradi huu ilijumuisha wafanyakazi wapatao 525 kutoka TRC , kati ya hao vibarua ni 466, wahandisi 12 na mafundi wa reli na nyanja nyingine 47 “ amesema Ndugu Masanja Kungu Kadogosa.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu alibainisha kua juhudi za Serikali na kujituma kwa wafanyakazi wa TRC kutafungua fursa mpya katika usafirishaji na uchukuzi katika ukanda wa Kilimanjaro ambapo historia inaonesha 12 iliyopita Shirika lilikuwa na uwezo wa kusafirisha mazao mbalimbali tani elfu 70 kwa mwaka kutoka Tanga, tani Laki moja za mbolea kwa mwaka na maharage mabehewa 144 kwa mwaka.

“ Ningependa kuihakikishia serikali kuwa Shirika la Reli Tanzania litaendelea kusimamia miradi yote ya kuboresha huduma za Shirika, utendaji na miundombinu kwa kasi na ubunifu unaopaswa ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano” alizungumza Mkurugenzi Mkuu.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019.
Muonekano wa Treni ya Mizigo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Wananchi wa Moshi, wakipokea treni ya mizigo kwa furaha kubwa, wakati ikiwasili tokea Tanga, Julai 20.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwapungia mikono wananchi waliyofika kushuhudia uzinduzi wa treni ya mizigo katika reli ya Kaskazini uliyofanyika katika stesheni ya reli Moshi, Julai 20.2019.

WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA MAJI WA SAME-MWANGA- KOROGWE

0
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Kiongozi wa Mradi, Richard Magwizi, wakati akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. Katikati ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Mwanga, katika ukumbi wa Green Bird, wilayani hapo, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, wakati alipowasili kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) na kuongea na wananchi, katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine za kusukumia maji, kwenye mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chanzo cha maji, katika mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

…………………………………………………. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ulioko Kirya, wilayani Mwanga, na kukagua hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo. 

Waziri Mkuu amekagua ujenzi huo jana (Jumamosi, Julai 20, 2019) na kutoa maelekezo kadhaa ili kuharakisha ujenzi wa mradi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa. 

Akizungumza na wakazi wa Kirya, Nyumba ya Mungu na vijiji vilivyo jirani na eneo la mradi, Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kutoa fedha hatua kwa hatua ili kukamilisha mradi huo. 

Waziri Mkuu amewataka wakazi hao waache kutumia uvuvi haramu na badala yake, wavue samaki kwa kutumia njia halali. “Bwawa la Nyumba ya Mungu linagusa wilaya tatu za Mwanga, Simanjiro na Moshi Vijijini. Ninataka Serikali za wilaya husika zisimamie jambo hilo,” alisisitiza. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Pauline Nkwama amsimamie Afisa Elimu wa Wilaya hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi, Bibi Mariana Mgonja na kuhakikisha kuwa anawahamishia walimu kwenye shule mbili za Kirya ambazo zilikuwa na walimu wawili wakati zina wanafunzi zaidi ya 400 kila moja. 

“Afisa Elimu Mkoa hakikisha Afisa Elimu wa elimu ya msingi katika wilaya hii anahamisha walimu kutoka pale mjini na kuwaleta huku ili huku vijijini kuwe na walimu sita katika kila shule. Kesho Jumapili (leo) andika barua za uhamisho, Jumatatu wapewe ili Jumanne waje kuripoti huku,” alisema. 

Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga, Bw. Zephrin Lubuva awatafutie gari walimu watakaohamishiwa huko ili wafike mapema. 

Amechukua hatua hiyo, baada ya kuelelezwa na mbunge wa jimno hilo, Profesa Jumanne Maghembe kwamba katika eneo hilo kuna shule mbili ambazo zina walimu wawili wakati kuna madarasa nane, yaani la awali moja na ya msingi saba, na wanafunzi zaidi ya 400. Alizitaja shule hizo kuwa ni Kiti cha Mungu na Emangulai. 

Mapema, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, msimamizi wa mradi huo Mhandisi Richard Magwizi alimweleza Waziri Mkuu kwamba Serikali inatekeleza mradi huo ili kuondoa kero ya maji inayowakabili wakazi wa miji ya Same na Mwanga na vijiji 38 vilivyo katika eneo la mradi. 

Alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kunufaisha wananchi 438,931 katika Wilaya za Same (246,793), Mwanga (177,085) na Korogwe (15,053). Alisema mradi huo umegawanywa katika awamu mbili za utekelezaji na unakadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 300. 

“Awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa maji safi na kusambaza maji kwa wakazi wa Mji wa Same na Mji wa Mwanga na vijiji 9 vilivyo kandokando ya chanzo cha maji ambapo awamu ya pili itahusisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji katika vijiji 29,” alisema. 

Akielezea changamoto zinazowakabili, Mhandisi huyo alisema wana changamoto ya kuchelewa kwa malipo ya mkandarasi kutokana na uwiano wa uchangiaji ambapo Serikali inagharimia asilimia 50.18. “Malipo yanapochelewa, yanaathiri kasi ya utekelezaji,” alisema.

Shilingi milioni 700 kujenga Madarasa 100 Mwanza, Morogoro na Dodoma

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara akizindua mojawapo kati ya madarasa manne ya elimu ya awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa katika wilaya za Misungwi na Ukerewe mkoani Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Magaka, wilayani Misungwi jana. 
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Children in Crossfire bwana Craig Ferla ambaye aliwezesha kukamilika kujengwa kwa madarasa 4 kati ya 30 yanayojengwa mkoani Mwanza akizungumza kabla ya Naibu Waziri kuzindua mojawapo ya madarasa hayo katika kijiji cha Magaka jana. 
Picha za nje na ndani kuonyesha mandhari ya madarasa yanayojengwa kwa ushirikiano baina ya shirika la Children in Crossfire na Serikali kama linavyoonekana. Jumla ya Madarasa 100 ya aina hii yatajengwa katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma 

………………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mwanza 

Serikali imelipongeza shirika lisilo la kiserikali la children in Crossfire kwa mkakati wake wa kujenga madarasa ya elimu ya awali 100 katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 
Pongezi hizo zimetolewa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara katika kijiji cha Magaka, wilayani Misungwi wakati akizindua mojawapo kati ya madarasa manne ya elimu ya awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa katika wilaya za Misungwi na Ukerewe mkoani Mwanza. 

Mhe.Waitara amesema kuwa kujengwa kwa madarasa hayo ya awali kutachochea ari ya watoto wanaojiunga na elimu ya awali kupenda kusoma na hivyo kupunguza utoro katika maeneo yanakojengwa madarasa hayo. 
Mhe.Waitara ameongeza kuwa kama madarasa yenyewe yanayojengwa ni kama hayo aliyozindua anatumaini kuwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, na Dodoma itakuja kuongoza kitaaluma katika miaka ijayo.
 
“Kama madarasa yenyewe ni yale tunaamini mikoa ya Mwanza katika wilaya za Misungwi na Ukerewe, pamoja na mikoa ya Dodoma na Morogoro inapaswa kuja kuongoza kwa taaluma ambayo wanaipata, na tunaamini kuwa watoto wataokuja kusoma katika madarasa haya watakuwa na uwezo mkubwa wa kimasomo,” amesema. 

Amesema madarasa hayo ni ya mfano kwani siyo tu yanaongea, bali pia yanacheka na kutabasamu kwani kona zote za madarasa hayo zimesheheni zana mbalimbali za kujifunzia zinazomuwezesha mtoto siyo tu ajifunze kwa urahisi bali pia apende shule kutokana na kuwa na rangi za kuvutia. 
“Hili darasa kama mlivyoona, nimekutana na madarasa yanayoongea lakini hili darasa linaongea, kutikisika na kucheka, na tabasamu linaongezeka,” amesema na kuongeza: 

“Sasa nilikuwa napiga picha ya madarasa yanayoongea ambayo niliwahi kuonyeshwa pamoja na haya hapa, hongereni sana haya yametia fora.” 
Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa sera ya mafunzo ya elimu ya mwaka 2014, Naibu Waziri amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la watoto wanaojiunga na elimu ya awali kutoka milioni moja mwaka 2015 hadi watoto milioni moja na nusu mwaka 2016. 
Aidha Mhe.Waitara ameziagiza halmashauri kuhakikisha kuwa kila zinapojenga shule za msingi pia zinapaswa kuweka bajeti kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya awali. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Children in Crossfire bwana Craig Ferla amesema kuwa shirika hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo limepanga kutumia shilingi milioni mia 700 kwa ajili ya kujenga madarasa 100 ya aina hiyo katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma. 

Naye Mratibu wa mafunzo ya elimu ya awali kutoka shirika hilo bwana Davis Gisuka amesema kuwa mbali na kujenga madarasa hayo pia shirika lake linawezesha kufanyika kwa mafunzo maalum kwa walimu wa shule za awali za serikali ili waweze kumudu kuwapatia elimu watoto wanaowafundisha kupitia mbinu mbalimbali za mafunzo ikiwemo matumizi ya zana rahisi za kufundishia zinazotengenezwa na walimu hao katika shule zao.

VIJIJI VYOTE VITAKAVYOPITIWA NA MRADI WA KUUNGANISHA UMEME TANZANIA NA KENYA KUPATIWA UMEME

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

MRADI wa ujenzi wa njia za kusafirisha Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 inayoanzia Singida na kupitia Babati nakuja mkoa wa Arusha hadi Namanga utanufaisha vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na mradi huo na havina umeme Kwani Serikali imeahidi kuvitapatiwa umeme. 

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga wakati akikagua mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,ambapo amebainisha kuwa kwa nchi yetu huo ni mradi mkubwa na ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2016 ambapo mradi wa kwanza kama huo ulianza kutekelezwa ulianzia Dodoma kuja hadi Singida ila pia ulipelekwa hadi Shinyanga na sasa utaanzia Singida na utapita mkooani Arusha hadi Namanga na kisha kuvuka upande wa nchi ya Kenya. 

Ameema miradi hiyo inayohusu njia ya kusafirisha Umeme kwa kilovolti 400 ni mradi wa kwanza kutekelezwa katika nchi yetu ambapo awali njia za kusafirisha umeme za juu kabisa kwa Tanzania zilikuwa kilvolti 220 lakini kutokana na uhitaji wa umeme katika nchi yetu pamoja na vile ambavyo Rais Magufuli alivyoelekeza tunatakiwa kuwa na viwanda na nchi yetu kuwa katika uchumi wa kati, 

Ambapo ameelekeza kwamba kunatakiwa kuwa na meme wa kutosha na wa uhakika na wa bei nafuu, hivyo ni lazima kuwepo na vyanzo vya umeme wa uhakika.

"Navyanzo hivyo tunavyo na tukianza na kile cha Rufiji ambapo kinazalisha megawatt 2115 lakini pia tunamiradi mingine ya Misumo, Kinyerezi na yote ni yakuzalisha umeme na imeshakamilika ,sasa kazi kubwa ya njia hizi za umeme nikusafirisha umeme huu kutoka katika hivi vyanzo vya umeme na unasafirishwa kwa ajili ya kwenda mikoani kwa watumiaji.

"Na mradi wa Rufiji ukikamilika tutajenga njia yakusafirisha umeme kutoka Rufiji kupita Chalinze mpaka Dodoma na ukishafika Dodoma utaunganishwa na hii njia .Tunafahamu hii njia kwa nchi yetu ni muhimu sana maana inaunganisha mitandao ya umeme ya nchi za Kenya ,Ethiopia mpaka huko Sudan.Pia itaunganisha na mitandao ya umeme upande wa Kusini ambapo upande huo itaunganisha Zambia, Namibia, Afrika Kusini, Angola mpaka nchini Congo,"amefafanua Luoga

Amesema mradi huo unafaida nyingi ikiwemo kuwa na umeme wa kutosha katika nchi yetu,pia utatuunganisha na nchi za jirani na tutakuwa na uwezo wa kuuza umeme katika nchi hizo za jirani na kwamba nchi yetu itakapo kuwa na umeme wa kutosha tutakuwa na nafasi na uwezo wa kuuza umeme huu nchi za nje kama Kenya ,Zambia mpaka Ethiopia.

"Na mradi huu ni wamanufaa sana kwetu ukiacha tu katika suala la uchumi wa vijana lakini pia utatusaidia kupata mapato kutokana na kuuza kwa umeme katika nchi za nje,"amesema.Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili wakandarasi hao wasipate changamoto.Pia wawe tayari kupokea umeme kwani vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo watapatiwa umeme.

Kwa upande wake Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye, amefafanua mradi huo wanaamini utakamilika kwa wakati kama ambavyo wamekubaliana na wakandarasi ambao tayari wapo kazini na vifaa vyote muhimu vimefika na kazi ya kusimika nguzo imeanza.

Amesema Tanzania imebarikiwa kwai itakuwa na sehemu tatu za mradi huo ambapo ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa wakati sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya ambapo kuna kituo kimoja kinachoitwa Isinya.

Amesema kwa upande wao watakwenda vizuri kwani kila kipande cha ujenzi wa mradi kuna mkandarasi wake na kila mmoja yupo hatua mbalimbali za ujenzi."Kupitia watalaam wetu tumekuwa tukifuatilia hatua kwa hatua na wakati huo huo wapo watalaamu wengine ambao nao wanafanya kazi hiyo hiyo kuhakikisha kila kinachofanyika kimezingatia mahitaji na vigezo vya viwango vya ubora,"amesema Mhandisi Kigadye.

Amesema kuwa mradi huo wa njia ya umeme ya Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, unatarajiwa kukamilika Aprili mwaka 2020 na anaamini mradi huo utakapo kamilika nchi yetu itaingia kwenye biashara ya umeme na hakutakuwa na tatizo la umeme tena.
Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye,akitoa maelezo ya kotii cha kupoozeshea Umeme cha Legur wakati Kamishna wa Umeme alipofanya ziara. 
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiuliza Jambo wakati alipikuwa akikagua ujenzi wa nradi wa kukagua Umeme uliopo katika Kijiji cha Legur
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akiuliza Jambo wakati alipikuwa akikagua ujenzi wa nradi wa kukagua Umeme uliopo katika Kijiji cha Legur

ALICHOKISEMA JANUARI MAKAMBA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMUONDOA NAFASI YA UWAZIRI

0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

ALIYEKUWA Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano na Mazingira Januari Makamba amemua kuvunja ukimya baada tu ya Rais Dk.John Magufuli kumuondoa kwenye baraza lake la mawaziri.

Mapema asubuhi ya leo Rais Magufuli ametangaza kumtengua Januari Makamba katika nafasi hiyo na kuteua Mbunge wa Jimbo la Kibakwe George Simbachawene kushika nafasi hiyo huku Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Hivyo baada ya uamuzi huo Januari Makamba kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hivi " Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa.Nitasema siku zijazo."

Katika maelezo yake hayo Januari Makamba ameamua kuambatanisha na picha yake akiwa na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Kwa kukumbusha tu taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Julai 21 ,mwaka 2019 ilisema Rais Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira .Simbachawene anachukua nafasi ya Januari Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.Bashe anachukua nafasi hiyo iliyokuwa awali inashikiliwa na Innocent Bashungwa ambaye siku za karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

TUKIO ZIMA LA KUIPOKEA TRENI YA MIZIGO HAPA MOSHI,MACHOZI YAFURAHA YATAWALA,JPM APONGEZWA SANA

NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI ABDALLAH ULEGA AGOMA KUWEKA JIWE MSINGI ZAHANATI YA MWANDEGE, KISA...

0
0
NAIBU Waziri wa  Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amegoma kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Mwandege iliyopo Mkuranga mkoani Pwani kutokana na paa lililoezekwa kuwa chini ya kiwango.

Akizungumza na wananchi wa Mwandege wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga Ulega amesema kuwa jengo hilo tayari linahitilafu kwasababu bati zote zinakutu.

"Kwa kweli mtanisamehe sitaweka jiwe la msingi, wenyewe mmekiri hapa katika risala yenu mapungufu ya paa hapa nawaagiza rekebisheni mapungufu yaliyojitokeza ili wananchi hawa wapate haki yao ya huduma,"amesema Ulega.

Aidha Ulega amesema atamuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filibeto Sanga na timu yake yote ya kamati ya ulinzi na usalama kufika eneo la Zahaati ili kufanyia uchunguzi kufahamu nani au kitu gani kilijitokeza mpaka kufikia bati kuwa na kutu.

Ulega amesema ili kulinda haki ya wananchi wa Mwandege ni lazima jambo hilo lichunguzwe na wale wote waliofanya ubabaishaji na kubainika wamehujumu ujenzi huo,hatua kali zichukuiwe dhidi yao sambamba na kulipa bati hizo.

Hata hivyo amesisitiza  uchunguzi ukibaini kwamba kumetokea kasoro ya bahati mbaya basi wa mwandikie barua,na yeye atakuwa tayari kugharamia bati zote 250 zinazohitajika kwa ajili ya ukarabati na ikitokea vinginevyo wahusika watalipa.

"Ninavyojua jengo kila linavyo fika hatua moja ya ujenzi lazima likaguliwe,sasa sijui ilikuwaje jengo hili likaezekwa,lazima wataalamu watuambie haliyehusika na hao majina walifanyaje mpaka ikafika hivi,"amesema

Sambamba na hilo Ulega pia amebainisha  mpaka sasa Serikali  imeshachangia kiasi cha Sh milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kohelo amesema mhandisi kutoka halmashauri alishakuja na kueleza kuwa hitilafu hiyo sio ya bahati mbaya bali ni la makusudi yaliyofanywa na wahusika kwa aslahi yao binafsi.

Adha Kohelo amessema mtaalamu huyo pia alishauri kubadilishwa kwa mbao zilizotumika kuezekea paa hilo kwani haziimili uzito wa kwakuwa nyembamba.

Hata hivyo amesema mpaka sasa zaidi ya milioni kumi na nne zinahitajika ili kuweza kuezeka jengo hilo.
 Muonekano wa Mabati ya Zahanati hiyo aliyogoma kuweka  jiwe la msingi kwa kutoridhishwa na ujenzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akikabidhi mifuko ya Saruji 50 kwa viongozi wa  kata ya Mwandege kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa shule ya msingi  Lugwadu jana.Picha na (Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mkutano ukiendelea.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akiweka Howe la msingi katika shule ya ya msingi Lugwadu ambapo alikabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya shule ya msingi  Lugwadu jana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandege ambapo aligoma kuweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo  kwa kutoridhishwa na ujenzi.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DK. KIJAJI ASHAURI WATANZANIA KUICHUKULIA BIMA KAMA HITAJI MUHIMU

0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema umefika wakati kwa Watanzania kuchukulia bima kama hitaji muhimu na kujifunza aina mbalimbali za bidhaa za bima zilizopo sokoni ili wazitumie kujikinga.

Dk.Kijaji amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na madawati 40 vyenye thamani ya jumla ya Sh.milioni 49 kwa Shule ya Msingi Lusangi iliyopo wilayani Kondoa,yaliyojengwa kwa msaada wa kampuni ya bima ya Sanlum, ambayo ndiyo mtoaji mkubwa wa bima barani Afrika.

“ Huduma ya bima inahitajika sana ili kuwawezesha watu kujikinga na majanga yasiyotabirika ya siku za usoni,” amesema Dk. Kijaji, na kuongeza ishara iliyoonyeshwa na kampuni ya Sanlam ya kurudisha sehemu ya faida yake kusaidia miradi ya jamii ichukuliwe kama ishara ya namna gani bima ni muhimu kwa uhakika wa maisha.

Amesema ni vema Watanzania wakapata elimu ya kutoa kuhusu masuala ya bima na faida zake ambazo kimsingi ni nyingi na zinamanufaa makubwa,hivyo ni wakati muafaka kwa jamii kutambua na kuona umuhimu wa uwepo wa bima.

Hata hivyo akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda – Afrika Mashariki wa Sanlam Pan-Afrika, Julius Magabe, amesema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi ya jamii nchini Tanzania.

“ Naomba nichukue fursa hii kuwahakikishia kuwa Sanlam tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii,"amesema Magabe, na kufafanua kampuni hiyo mwaka jana wa 2018 imesherehekea kutimiza miaka 100 tangu kuanziswha kwake na kwamba iko thabiti katika kurejesha sehemu ya faida yake kusaidia jamii.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lusangi, Josephine Paul amesema shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madarasa, kwa kuwa madarasa matano yaliyokuwepo kabla hayakuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi ambayo ni 348.

“Kutokana na mradi huu kukamilika, utakuwa umepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa na oofoso ya walimu uliokuwepo,” amesema Mwalim mkuu huyo.

Wakati huo huo uongozi wa Sanlam umesema wamefurahishwa na namna ambavyo fedha walizotoa kufanikisha ujenzi huo zimetumika kwa uadilifu mkubwa na kwamba wamethibutisha walivyowaamifu kwani Sh.milioni 2.7 hazijatumika kutokana na kupungua kwa gharama za vifaa vya ujenzi.Hata hivyo fedha hizo sasa zimeelekezwa zitumike kujenga vyoo vya wanafunzi wa kike na wakiume.

“ Sisi Sanlam hatujawahi kushuhudia mradi tunaoufadhili ukisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu kiasi hiki,” amesema Magabe, ambayo kampuni anayotumikia ina matawi ndani ya nchi 38 barani Africa, huku huduma zake zikiwa zimesambaa mabara ya Amerika, Asia na Australia.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, Mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), DK. Mussa Juma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakifungua pazia la jiwe la msingi kuzindua madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam yenye thamani ya shilingi milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo iliyopo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, nkoani Dodoma. Kutoka Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Stella Rutaguza(kulia).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima Sanlam kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe wakishikana mikono baada ya kufungua pazia la jiwe la msingi katika uzinduzi wa madarasa mawili na ofisi ya walimu ya Shule ya Msingi Lusangi yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bima ya Sanlam kwa thamani ya shilingi Milioni 49. Uzinduzi huo ulifanyika shuleni hapo tarafa ya Pahi, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life, Khamis Suleiman , Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA), Dk. Mussa Juma (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya kati, Stella Rutaguza (kulia).

GAGUTI APIGA MARUFUKU ULANGUZI WA KAHAWA, UKIKUTWA NI MAHAKAMANI.

0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amepiga marufuku wale wote wanofanya biashara ya ununuzi wa kahawa kwa wakulima bila kufuata Mfumo rasmi, ambao kawafananisha watu hao wahujumu na Kangomba, mapema Julai 21, 2019 wakati akizungumza na Wenyeviti wa vyama Ushirika, Wakulima na watendaji wa Serikali Wilayani Karagwe.

Mhe. Gaguti Amesema kuwa hakuna mtu yeyote au mfanyabiashara yeyote mwenye mamlaka ya kununua kahawa kwa Mkulima, biashara hii inafanywa kati ya Msimamizi (Serikali) na Mkulima pekee na sivinginevyo hivyo nakutoa wito wale wanaolenga kwenda kwa wakulima kulangula Kahawa kwa bei pungufu na hata wale wanaokwenda kuwazuia wakulima hao wasinunue kahawa watachukuliwa hatua za kisheria.

"Hakuna MTU ataruhusiwa kwenda Kwa Mkulima akanunue kahawa, hicho kitu hakiruhusiwi na kwa atayekutwa au kukamatwa akifanya hivyo ni kufungwa kamba na moja kwa moja ni mahakamani " amesema Mhe. Gaguti.

Aidha ameongeza kuwa zipo taarifa za moja ya kampuni ambayo imeagiza mawakala huko vijijini kwa ajili ya kufanya hujuma ya kahawa kwa kununua kahawa kwa mfumo usio rasmi ambapo ameagiza jeshi la polisi Mkoani Kagera kuhakikisha watu hao wanakamatwa Mara moja kwani tayari wanajulikana.

Haya yanajiri wakati ambapo Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tayari wapo mkoani Kagera kueneza elimu ya Mfumo Jumuishi, mfumo huo wa malipo wenye lengo la kumnufaisha Mkulima ikiwa ni pamoja na Mkulima kulipwa malipo yake kwa njia za Kibenki ambapo pia watafika katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa. 

Awali Kabla ya Mhe. Gaguti kuongea na Wakulima, Watendaji wa Vijiji pamoja na Wenyeviti wa Vyama vya Ushirika, amefanya ziara ya kutembelea viwanda vya kukoboa kahawa Vya Karim Amri na kujionea jinsi Kiwanda hicho kilivyojipanga vyema kwa ajili ya msimu huu mpya wa kahawa, kwa kuongeza mashine mpya zenye uwezo wa kukoboa kahawa nyingi kwa muda mfupi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti akimsaidia kibarua kuchambua kahawa safi na kuhakikisha haibaki na mawe wala uchafu, tayari kuuzwa kiwandani, pembeni ni Mkuu wa Wilaya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimj na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Godfrey Mheluka.
Pichani Wakulima, watendaji, na wenyeviti wa vyama vya Ushirika vya Wilaya za Karagwe na Kyerwa wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa Kagera (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kuwasikiliza katika kufanikisha msimu mpya wa kahawa
Pichani ni Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoa hotuba yake wakati alipokutana na kuzungumza na Wakulima, Watendaji na Wenyeviti wa Vyama vya Ushirika Wilayani Karagwe.
Pichani ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kukoboa kahawa cha Karim, Bwn. Karim Amri akitoa ufafanuzi juu utaratibu wa kusafisha na kukoboa kahawa kwa Mhe. Gaguti alipofika kiwandani kwake Omgakorongo Karagwe.

NEC KUANZA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

0
0
Baadhi ya viongozi wa dini, , viongozi wa asasi zisizosa Kiserikali na wawakilishi wa vijna , wanawake na watu wenye ulemavu wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.Baadhi ya viongozi wa dini, , viongozi wa asasi zisizosa Kiserikali na wawakilishi wa vijna , wanawake na watu wenye ulemavu wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.

Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi,(kulia) Mratibu wa Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu, Bw. Maganga Simon

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja viongozi wa dini mkoani Simiyu mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani humo, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.

*************

Na Stella Kalinga, Simiyu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Simiyu kuanzia Julai 31, 2019 hadi Agosti 06, 2019.

Akifungua mkutano wa wadau wa Uchaguzi mkoani Simiyu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema Tume imekamilisha maandalizi ya uboreshaji daftari ambayo ni pamoja na kuhakiki vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi ya vifaa vya uboreshaji daftari, mkakati wa elimu kwa mpiga kura na uzinduzi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema uboreshaji huu hautawahusisha wapiga kura wote walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 bali utawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza miaka 18, wale ambao watatimmiza.umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ambao wamehama katika maeneo ya awali ya uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika

Katika hatua nyingine Jaji Kaijage ametoa rai kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kuboresha taarifa zao, huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa, kuzingatia sheria za uchaguzi na kanuni zake katika zoezi hili la uboreshaji na maelekezo kwa Vyama vya Siasa kuhusu uboreshaji.

Kwa upande wake Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando amesema Tume imefanya uhakiki wa vituo vya uandikishaji ambavyo vimeongezeka kutoka 36,549 mwaka 2015 hadi 37,407 mwaka 2018 (Tanzania Bara), upande wa Tanzania Zanzibar vimeongezeka kutoka 380 mwaka 2015 hadi 407 mwaka 2018; huku akifafanua kuwa katika uandishaji huu kila Kijiji au Mtaa utakuwa na angalau Kituo kimoja cha kujiandikisha.

Naye Mratibu wa Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu, Bw. Maganga Simon amesema mkoa umejiandaa vizuri ili kufanikisha zoezi ambapo wananchi wenye sifa zaidi ya 700,000 wanatarajia kuandikishwa katika daftari hilo huku akiwasisitiza viongozi wote mkoani hapo kuwahamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kujiandikisha.

“Mkoa wetu ni mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka2019, tutatumia fursa hiyo kuhamasisha, kutakuwa na bango kubwa litakaloonesha kuwa kuanza Julai 31 hadi Agosti 6 2019 mkoa wetu utashiriki kikamilifu kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Simiyu tumejipanga kufanikisha zoezi hili ambalo linasimamiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi” alisema

Akizungumza kwa niaba ya watu wenye ulemavu, Katibu wa Chama cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Alex Benson amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kuwapa fursa watu wenye ulemavu kuwania nafasi mbalimbali, huku akisisitiza wasimamizi kupewa mafunzo ya lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano na watu wenye ulemavu pindi wanapoenda kujiandikisha na kupiga kura.

Naye Dora Stephano kutoka katika ASASI za kiraia amesema Tume ione uwezekano wa kuongeza ushirikishwaji wa asasi za kiraia nyingi zaidi, ili kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa wapiga kura juu ya masuala mbalimbali ya uandikishaji na uchaguzi.

Mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Simiyu, umewahusisha Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Viongozi wa Vyama vya siasa Viongozi wa dini, wawakilishi wa watu wenye ulemavu, wawakilishi wa vijana, wawakilishi wa wanawake, wawakilishi wa asasi za kiraia, watendaji wa Tume na waandishi wa habari.

WAZIRI MKUU ALIPONGEZA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea ngao kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli, kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Barnabas Mtokambali, kwenye maadhimisho ya miaka 80 ya kanisa hilo, yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Julai 21.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

***********

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God kwa kuthamini na kutambua kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

“Baba Askofu Mtokambali umenifurahisha kwa takwimu ulizozitaja hapa za miradi mikubwa ambayo inatekelezwa na Serikali hii. Kuna wengine hawapendi kusikia mambo kama haya, hongera sana,” amesema.

Ametoa pongezi hizo leo mchana (Jumapili, Julai 21, 2019) wakati akizungumza na maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika maadhimisho ya miaka 80 ya TAG hapa nchini yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, amesema ameguswa na jinsi kanisa hilo linavyomtambua Mheshimiwa Rais na wasaidizi wake na kuthamini juhudi za Serikali. 

“Serikali hii imedhamiria kuwatumikia Watanzania wote bila kujali dini zenu, rangi wala itikadi za kisiasa. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kumtegemea Mungu pasipo shaka yoyote.”

Pia amewapongeza viongozi wa kanisa hilo kwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chote cha miaka 80. “Pia nikupongeze Baba Askofu kwa kuchangia mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari hapa Arusha. Natambua kwamba ulishachangia mifuko mingine 500, asante sana.”

Alilishukuru kanisa hilo kwa kuendesha maombi maalum kwa ajili ya Taifa yaliyoongozwa na Mchg. Titus Mkama. “Niliguswa sana wakati maombi ya Taifa yalipokuwa yakiendelea. Mchungaji aligusia masuala ya muhimu kwa Taifa hili.”

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na maelfu ya washirika waliohudhuria maadhimisho hayo, Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kulipenda na kulijali kanisa hilo.

Alimpongeza Rais Magufuli kwa miradi mikubwa ya maendeleo anayoisimamia kama vile umeme wa Stiegler’s Gorge, reli ya SGR, ununuzi wa ndege, ujenzi wa hospitali mpya 67 za wilaya, ujenzi wa vituo vya afya 370 na ununuzi wa dawa za hospitali.

“Nina umri wa kutosha lakini katika miaka yangu yote hii, sijawahi kuona hospitali 67 zikijengwa kwa pamoja. Tena, mwaka huu wa fedha mmetenga hela kwa ajili ya ujenzi wa hospitali nyingine 27. Hongera sana kwa ujasiri huo,” alisema Dkt. Mtokambali. 

Maadhimisho ya miaka 80 ya TAG yameenda sambamba na hitimisho la miaka 10 ya Mpango Mkakati wa mavuno.

Ripoti nyeti Stiegler’s yazinduliwa,Yapangua hoja potofu za UNESCO, WWF kuhusu uamuzi wa Rais Dk. Magufuli

0
0

TIMU ya wataalamu bingwa watano wa kitanzania waliobobea katika masuala ya uhifadhi, mazingira na uchumi, juzi ilizindua ripoti yake ya utafiti wa kitalaamu kuhusu faida na madhara ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Mto Rufiji, unaofahamika zaidi kama Stiegler’s Gorge Hydropower Project.

Ripoti hiyo imezinduliwa zikiwa zimesalia takriban siku saba kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na Kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Misri,inayofahamika kwa jina la Arab Contractors.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Hotel ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, kiongozi wa timu hiyo wa wataalamu, Saleh Pamba alisema utafiti wao ulilenga kuangalia madhara na faida za ujenzi wa mradi baada ya mashirika mawili ya umoja wa mataifa kujitokeza hadharani kupinga azma ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, kuutekeleza.

Pamoja na Pamba, wataalamu wengine katika timu hiyo ni Dk. Abubakar Rajab, Abdulkarim Shah, Dk. Magnus Ngoile na Dk. Thomas Kashililah.Pamba aliyataja mashirika ya umoja wa mataifa yaliyojitokeza kuupinga mradi huo na kusambaza taarifa zake duniani kote zikieleza athari zitakazojitokeza iwapo utatekelezwa kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF).

Alisema hoja za upinzani huo dhidi ya uamuzi wa Rais Dk. Magufuli zilizosambazwa duniani kote kwa njia ya maandishi kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kabla ya kubebwa na baadhi ya wapinzani wa maendeleo wa ndani ya Tanzania zilianza kujenga taswira mbaya dhidi ya mradi wenyewe na Rais Magufuli ambaye aliapa kuutekeleza.

“UNESCO na WWF walitushtua sana baada ya kusoma maandiko yao yaliyokuwa yakipinga mradi wa Stiegler’s, waliandika hoja nyingi zilizokuwa zikipinga uamuzi wa rais kutekeleza ujenzi wa mradi huo wakitaka jumuiya ya kimataifa ipaze sauti kwa pamoja ili usitekelezwe. Sisi tulishtuka kwa sababu hizo hoja zao nyingine zilikuwa haziingii akili lakini nyingine zilikuwa zinafikirisha.

“Tukaona kama wasomi wa kitanzania ni wajibu wetu kujiridhisha ili kama kuna hizo hatari walizozianisha tuishauri serikali ifanye vinginevyo, tumefanya utafiti wa kina kweli kweli, tumegusa kila kipengele walichopigia kelele lakini sasa ajabu tulichogundua ni kwamba kelele zote za hao wazungu ni uongo mtupu. Wanatishwa na kasi ya Rais Dk. Magufuli kuliletea maendeleo taifa letu,” alisema Pamba.

Alisema, haina shaka hata kidogo kuwa mataifa ya Magharibi yanajaribu kutumia kisingizio kuwa Hifadhi ya Selous ambayo inatambulika kama eneo la urithi wa dunia na mahali unapojengwa mradi wa Stiegler’s, serikali imekusudia kupaharibu lakini ukweli ni kwamba hofu kubwa ya Magharibi ni kasi ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa kati na kujitoa kwenye utegemezi wa mataifa hayo na taasisi zake za misaada.

Pamba alisema katika utafiti wao wamebaini kuwa eneo la hifadhi la Selous litakalotumika kujenga mradi ni asimilia mbili tu ya kilomita za mraba 50,000 hivyo sehemu kubwa ya hifadhi haitaguswa na kwamba hata eneo ambalo mradi utatekezwa halitaathirika na uharibifu wa mazingira au kuhatarisha ustawi a wanyama.

“Kama UNESCO na WWF wana wasomi wasiokuwa na uwezo wa kufanya utafiti wa kiwango kile basi tafiti zao hasipaswi kupewa kipaumbele hata siku moja. Lakini sisi katika utafiti wetu tulibaini kuwa hawa jamaa ajenda yao ni kuhakikisha Tanzania haifikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025.

“Umeme wa Stiegler’s utawezesha kukua haraka kwa sekta za viwanda, madini, uendeshaji wa treni za kisasa ya umeme, upatikanaji wa umeme vijijini na wafanyabiashara wadogo watakuwa na uhakika wa kupata umeme wa bei nafuu, uchumi wetu utapaa kwa kasi ya ajabu.

“Ripoti yetu hii ambayo tunaitoa kwenu waandishi wa habari nendeni mkaisome na mtakubaliana na sisi kuwa uamuzi wa ujenzi wa mradi huo ulifikiwa miaka 60 na 70 huko lakini uamuzi wa kuifanya Selous kuwa eneo la urithi wa duniani ulichukuliwa mwaka 1982. Hizi taasisi za kimataifa zilikuwa na taarifa kuhusu uamuzi wetu huo.

“Sasa katika hoja zao za sasa wanasema ujenzi wa mradi huo utahatarisha hali ya usalama na utasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, siyo kweli hata kidogo. Sisi tumebaini katika utafiti kuwa utekeklezaji wa mradi utalinda mazingira na tumefafanua vizuri sana katika ripoti kuwa hali ya usalama itamaarika mno kwa sababu kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika eneo zima la mradi hivyo hata wawindaji haramu hawatasogolea huko.

“Hawa wazungu wanasema wakati wa utekelezaji wa mradi kutakuwa na kelele na uchafuzi wa hewa, hoja za kitoto kabisa kwa sababu sisi katika uchunguzi wetu tumebaini kuwa kabla ya mradi kuanza kutekelezwa, hivi sasa kuna viwanja vya ndege vidogo, hizi Airstrips 38 na kati za hizo 33 zinafanya kazi kila uchao kusafirisha watalii, hapo hawaoni kelele hizo za ndege kupaa na kutua.

“Sasa utafiti hupingwa kwa utafiti, ripoti ya utafiti wetu tumeiweka mezani kama wao wanayo yao mpya ya utafiti wa kweli kweli siyo ya kuchafua nchi au rais nao waiweke mezani. Wapeni watanzania ripoti yetu wajue kuwa mradi huu una manufaa makubwa kwa nchi yetu na hawa wazungu lengo lao tusiutekeleze ili tuendelee kuwategemea wao.

“Kwetu sisi tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti za ujenzi wa vyanzo vipya vya uzalishaji umeme wa uhakika ili iepuka kushindwa kufikia malengo ya kuwa taifa lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.“Pia Tanzania inapaswa kuwa na vyanzo vipya vya umeme wa uhakika ili kuepuka hatari ya maeneo ya misitu kugeuka jangwa na kuepuka athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, alisema Pamba.

Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutaepusha uteketezwaji wa kilimota za mraba 412,000 za misitu kila mwaka kwa ajili ya shughuli za kibinadamu na hivyo kuongeza ustawi wa maeneo ya uoto wa asili na mapori mengi zaidi.
Mmoja wa TIMU ya wataalamu bingwa watano wa kitanzania waliobobea katika masuala ya uhifadhi, mazingira na uchumi,Saleh pamba

WAZIRI LUGOLA, ZUNGU WAFANYA OPERESHENI KUWASAKA MATEJA BONDE LA JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM, RPC ILALA APEWA AGIZO ZITO

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (kulia), wakiwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu katika Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Zuberi Chembera, alipompigia simu afike katika eneo la Bonde la Msimbazi, kuongeza kasi ya kuwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanatuhumiwa kufanya matukio ya ukabaji, na upora wa mali za watu mbalimbali katika eneo hilo. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (wapili kulia), wakiwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu katika Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 



Na Felix Mwagara, MOHA. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam. 

Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia katika maeneo ya vijiwe vyao. 

Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera, kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo. 

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa. 

“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani, kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au mchana. Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi wao ni mateja ambao wanatumia dawa za kulevya. 

Kwa upande wake Mbunge Zunge, ambaye ndio alimwita Waziri huyo kutembelea eneo hilo kuona kero kubwa awanazopata wananchi wake, alisema wahalifu hao hawatoki pekee katika Jimbo lake, bali wengi wao wanatoka maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam. 

“Wenyeji wa eneo hili ni wachache, wengi wanatoka mitaa mbalimbali ya hapa Dar es Salaam ikiwemo Temeke na kwingineko, hivyo mheshimiwa Waziri tunajua utendaji wako, tunakuomba hii kero inatuumiza sana, wananchi wanakosa amani kutokana na uwepo mkubwa wa wahalifu hawa,’ alisema Zungu. 

Waziri Lugola alisema Dkt John Magufuli anawataka wananchi wake waishi kwa amani na utulifu, yeye Waziri hatakubali kuona matukio hayo ya baibu yakishika kasi mitaani. Aliwataka Makamanda wa Polisi nchini kuwasaka wahalifu muda wowote si mpaka yeye atoe agizo au atembeleee.

MAKAMU WA RAIS KUWASILI JIJINI DAR KIKAZI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Kizito Malongo kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati Makamu wa Rais akielekea Dar Es Salaam kikazi.

WAZIRI LUGOLA AIPONGEZA JKT UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA, JIJINI DA ES SALAAM, ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA KASI YA UMEME

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiwafafanulia jambo,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) na
Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali
Charles Mbuge (kulia) wakati Waziri huyo alipokua anakagua ujenzi wa
nyumba zaa askari Magereza, zinazojengwa na JKT, Ukonga, jijini Dar es
Salaam. Lugola ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
nyumba hizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali
Charles Mbuge (kulia), akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (katikati), jinsi ujenzi wa nyumba za askari Magereza
ukiendelea, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Lugola ameridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob
Kingu (wapili kushoto), akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola (kushoto), wakati viongozi hao walipofanya ziara
Ukonga kuangalia ujenzi wa nyumba za askari Magereza ulipofikia. Lugola
ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo.
Watatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, na
kulia ni Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenerali Charles Mbuge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya nyumba za askari Magereza zinazojengwa na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam. Ujenzi huo umefikia asilimia 70.
Na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara katika eno hilo akiwa na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, wote wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa
ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (kushoto) akimsalimia
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakati Waziri
huyo alipokua anawasili katika mradi wa ujenzi wa nyumba za askari
magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam, leo. Lugola ameridhishwa na kasi
ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

************

Na Felix Mwagara, MOHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema ameridhishwa
na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari magereza
unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam.

Waziri Lugola amesema Jeshi hilo linastahili pongezi kutokana na kasi ya
ujenzi wa nyumba hizo ambao umefikia asilimia 70 kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi huo, Lugola
amesema, atazungumza na Rais John Magufuli ili aweze kutoa kiasi cha
fedha kilichobaki kwa ajili ya kukamilisha asilimia thelathini zilizobaki ili
mradi huo ukamilike.

Lugola amesema, Jeshi la Kujenga Taifa lilikabidhiwa mradi huo zaidi ya
miezi miwili iliyopita kutoka kwa Wakala wa Majengo (TBA) kufuatia agizo
Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuonekana kusuasua kwake.

Waziri Lugola amesema, amefurahia kuona ujenzi huo ukiendelea vema na
kwa kasi kubwa na kuwapongeza askari hao kwa kazi kubwa wanayoifanya
na kusisitiza kuwa anataka kuona zaidi kauli ya Mkuu wa Ujenzi huo
akisema Jeshi halishindwi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob
Kingu, alisema amefurahishwa na kasi hiyo, na ana uhakika JKT ipo vizuri
na matumaini yake makubwa ujenzi huo utakamilika hivi karibuni.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, amesema
kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha jumla ya familia 172 za askari
Magereza kuishi eneo katika makazi hayo huku ujenzi huo ukikadiriwa
mpaka sasa kutumia zaidi ya shilingi bilioni.

SHUBILA STATON ANYAKUA TAJI LA MISS MOROGORO 2019

0
0

Miss Morogoro 2019 Shubila Staton akipungia mkono wageni waalikwa walifika katika shindano la kumsaka mlimbwende wa mjini kasoro bahari Morogoro mara baada ya kutangazwa.
Miss Morogoro 2019 Shubila Staton atoa machozi ya furaha baada ya kutangazwa kubeba taji hilo. Pembeni yake kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga, Miss Morogoro namba mbili Moureen Kaaya na kulia ni muandaaji wa mashindano hayo Farida Fujo. 
Wadhamini wa shindano hili, DSTV wakitoa zawadi kwa washindi wa tatu wa Miss Morogoro 2019.
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo akitoa neno la nasaha kwa washiriki na shukrani kwa wageni waliofika katika shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro July 20, 2019.
Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda (picha ya juu kulia) akitangaza mshindi. Picha ya chini ni warembo Moureen Kaaya aliyenyakuwa nafasi ya pili akiwa ameshikana mikono na Shubila wakati wakingoja kutangazwa kwa mshindi. 
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo akiwa na msemaji wa timu ya Simba Haji Manara ambaye nae aliungana katika hafla hiyo. 
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo (katikati) akiwa na Msimamizi wa Mshindano hayo Martini Kadinda (kulia) na kushoto ni Msanii wa bongo movie Irene Uwoya. 
Wasimamizi wa shindano la Miss Morogoro 2019 wakiwa katika picha ya pamoja. 
Msanii Christian Bella akitoa burudani. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. 

Mbio za kumtafuta Miss Morogoro 2019 zimefikia tamati alfajili ya leo ambapo mrembo Shubila Staton ameibuka kidedea kwa kuwaangusha warembo wenzake 12 na kupata nafasi ya kuwakilisha mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Miss Tanzania. 

Akimtangaza mshindi huyo msimamizi wa mashindano hayo Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda alianza kwa kutangaza walioingia sita bora na baade tatu kumalizia mshindi. Katika shindano hilo warembo hao walipanda jukwaani na kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo vazi la Ubunifu, vazi la jioni, navazi la ufukweni ambapo mlimbende Shubila Staton kushika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Moureen Kaaya na nafasi ya tatu ameshinda Veronica Royal. 

Akitoa neno mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga amewashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kulifanya la wazi na haki na linaloletea heshima katika mkoa. "Binafsi nimefurahishwa na waandaaji kwa kuendelea kuuletea heshima mkoa wetu kwa mwaka wa pili mfululizo," amesema. Kwa upande wake muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo amewashukuru wakazi wa Morogoro kwa kuendelea kuwaamini kwa miaka miwili mfululizo jambo linalowapa heshima ya pekee.

 Mashindano yaliyoandaliwa na Nyumbani Park ambao ni wamiliki wa kiwanja cha burudani cha Samaki Spot kilichopo mjini Morogoro yalikuwa na ushindani mkubwa kwa vile yalikuwa na warembo wenye viwango. Ni usiku ulipambwa na burudani za aina yake kutoka kwa wasanii Barnaba, Christian Bella na watu mashughuli nchini akiwemo Irene Uwoya, mama Dangote, Ndama mtoto wa ng'ombe, msanii Steve Nyerere huku shauku kubwa ya mashabiki wa sekta ya urembo mkoani Morogoro ni kushudia nani anatwaa taji la miss Morogoro mwaka 2019 kati ya walimbwende 12 walioshiriki shindano hilo.

Azam Fc yautema Ubingwa wa Kagame kwa KCCA ya Uganda

0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Timu ya KCCA imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Kagame Cup baada ya kuifunga Azam Fc mchezo uliomalizika kwa ushindi wa goli 1-0.

Mchezo huo wa fainali ulichezwa majira ya saa 11 jioni kwa saa za Rwanda na Saa 12 jioni kwa saa za Tanzania.Azam waliokuwa mabingwa watetezi walikubali kuuvua ubingwa huo walioushikilia kwa miaka miwili mfululizo. 
Kwa upande wa KCCA wanalichukua Kombe la Kagame kwa mara ya pili baada ya miaka 41 kupita toka walivyolichukua kwa mara ya kwanza.

Kocha wa Azam Etienne Ndayiragije amewapongeza KCCA kwa kuweza kushinda mchezo huo na kuchukua ubingwa na mpira ni mchezo wa makosa walipata nafasi wakashindwa kuzitumia KCCA walipata na wakaandika goli lililowapa ubingwa.

Ndayiragije amesema, timu yake imecheza vizuri na anawapongeza kwa hatua walioyofikia kwani siku zote mshindi ni mmoja.

Azam wamecheza fainali ya tatu mfululizo na kufanikiwa kulichukua kombe hilo mara mbili.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images