Na: Moshy Kiyungi,Tabora.
Mwaka huu 2019 imetimia miaka kumi tangu Michael Jackson alipoiaga dunia, Juni 25, 2009 nchini Marekani.
Alikuwa msanii mwenye vipaji vingi, aliyefahamika zaidi kwa jina bandia la kiheshima la ‘Mfalme wa Pop’Michael alipata mafanikio makubwa kwa muda wote pia alikuwa mmoja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika medani ya muziki.Michango yake katika muziki, fasheni, na hasa suala la kuanika hadharani maisha yake binafsi, vilimfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne.
Wasifu wa Michael Jackson unaonesha kuwa alizaliwa Agosti 29, 1958 huko Gary, Indiana, nchini Marekani.Alitokea katika familia ya wanamuziki ya Jackson Five.
Michael Jackson alifariki mnamo Juni 25, 2009 katika hospitali ya UCLA Medical Center, nchini Marekani, alokokuwa amelazwa.Wakati wa uhai wake aliwahi kusimulia kuhusu miaka yake ya awali, mara kadhaa ilisema kuwa baba yake alimlazimisha kufanya mazoezi mno ya kucheza na uimbaji.
Michael akiwa pamoja na ndugu zake, alipewa uongozi wa uimbaji kwa mara ya kwanza akiwa mwanachama mdogo katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964.
Alianza kazi ya usanii wa kujitegemea kunako mwaka wa 1971, ambapo allbamu yake ya mwaka 1982 iliyopewa jina la ‘Thriller’, imebaki kuwa ni yenye mauzo bora kwa muda wote.Mchango wa Michael Jackson katika utengenezaji wa muziki wa video, ulimuinua kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali ya kisanii zaidi.
Video zake za Billie Jean, Beat It na Thriller zilimfanya kuwa msanii Mmarekani mweusi wa kwanza kupata kupigiwa nyimbo zake sana kwenye MTV.Michael Jackson alipata umaarufu kwa baadhi ya mitindo alipokuwa akicheza muziki huo kama vile Robot na Moon Walk.
Mitindo ya muziki, sauti yake na zile Koregrafia, zimetambulika vizazi kwa vizazi, kirangi na hata katika mipaka ya kitamaduni.Michael alikuwa mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye Rock and Roll Hall of Fame.Mafanikio mengine yamejumlisha tuzo ya Guinness World Records (ikiwa ni pamoja Mburudishaji mwenye mafanikio kwa muda wote.
Nguli huyo alituzwa tuzo za Grammy 15 (ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award).Zingine ni pamoja na 26 American Music Awards akiwa kama msanii pekee ya kujitegemea, pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne, zaidi ya msanii mwingine yeyote.Single zake 17 zilishika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na nne alizopaa akiwa kama mwanachama wa Jackson 5.
Inakadiriwa Michael Jackson alifanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 duniani, yaliyomfanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi zao vilivyo kwa muda wote na haijawahi kutokea.Kuanzia katikati mwa miaka ya 1980 muonekano wa Michael Jackson ulikuwa unabadilika bila kificho.
Umbo la sura yake vilibadilika pia, madaktari wa upasuaji kadhaa walikisia ya kwamba, kunako miaka ya 1990, alipitia upasuaji kadhaa wa pua, kuinua paji la uso, kufanya midomo iwe myembaba, na upasuaji wa mfupashavu.
Michael Jackson alifanya upasuaji wa pua kwa mara ya kwanza baada ya kuvunja pua yake wakati anacheza mchezo wa hatari kunako mwaka wa 1979.Hata hivyo, upasuaji huo haukukamilika kisawasawa, alianza kulalamika ya kwamba upumuaji wake ni wa tabu, ungeathiri shughuli zake.
Michale akaelekezwa kwa Dk. Steven Hoefflin, ambaye alifanya upasuaji wa pua kwa mara ya pili mnamo mwaka wa 1981.Katherine Jackson alisema katika mahojiano kwamba Michael alipata madhila ya pua kwa makusudi hapo mara ya kwanza.
Yaelezwa kwamba Michael Jackson alifanya tena upasuaji wa pua kwa mara ya tatu na ya nne mnamo mwaka wa 1986.Mwamba huyo wa Pop, Michael Jackson aliandika katika wasifu wake mnamo 1988 Moonwalk, kwamba katika ongezeko la upasuaji wa pua, pia alipata kutengeneza kidimpo katika kidevu chake.
Toka 1986 na kuendelea, alikuwa mteja wa kawaida wa Arnold Klein, mtaalamu wa magonjwa ya ngozi ambaye amebobea katika tiba ya sindano za ugonjwa ngozi, utaratibu wa utoaji wa tiba ya upodozi bila upasuaji.
Katika kitabu chake, Michael alidhania kuwa madailiko ya sura yake ni matokeo ya kubalehe, mpangalio mkali wa mlo wa kutokula nyama, upungufu wa uzito, badiliko katika mtindo wa nyewele na taa za jukwaani.
Lakini Michael Jackson alikana madai yaliyotolewa na baadhi ya watu kwamba alibadilisha macho yake.Mwaka 1990, kiwango chote cha upasuaji wa Jackson kilijadiliwa mno, hayo yalikaribia kusema kwamba mwimbaji huyo amepitia karibia taratibu kumi za upasuaji ya kubadili umbo lake.
Ilivyofika mwezi Juni 1992, gazeti la Daily Mirror liliweka picha nzima katika ukurasa wake wa mbele, likidai sura ya Michael Jackson, ambayo walielezea kama "sura mbaya isiyo na umbo zuri" kwa kufanya upasuaji wa sura.
Michael Jackson akalishtaki jarida hilo na mwaka wa 1998, wakakubaliana kuondoa kesi mahakamani na kuyamaliza nje ya mahakama.Mnamo mwaka wa 1993 alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia kwa mtoto, ingawa hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa dhidi yake.Michael Jackson aliwahi kufunga ndoa na Bi. Lisa Marie Presley, binti wa mwanamuziki Elvis Presley mnamo mwaka 1994.
Aidha alimuoa mwanamke mwingine Deborah Rowe mwaka 1996, ambaye alizaa naye watoto wawili wa mwanzo kati ya watatu.Baadaye mama huyo alitoboa siri ya ndoa yao na kuwaambia watoto wake kuwa Michael Jackson sio baba yao.Deborah Rowe aliyasema hayo wakati alipohojiwa kwa mara ya kwanza tangia kutangazwa kwa kifo cha Michael Jackson.
Alifunga ndoa na Michael Jackson na kupata watoto wawili Prince na Paris.
Deborah alifafanua kuwa watoto hao alizaa baada ya kupandikizwa mbegu za kiume za mwanaume asiyejulikana, aliyejitolea mbegu zake za kiume hospitalini.
Mwanamke huyo Deborah alikutana na Michael wakati alipokuwa akifanya kazi kwenye kliniki ya ngozi ya Beverly Hills, Marekani ambako Michael alikuwa akienda mara kwa mara kwa matibabu.
Rafiki wa zamani wa Michael Jackson ambaye pia alikuwa mtaalamu wa ngozi Arnold Klein, aliibuka na kusema kuwa mfalme huyo wa muziki wa Pop ulimwenguni Michael Jackson, hakuwa na uwezo wa kuzaa kutokana na kujeruhiwa mara mbili korodani zake.
Katika mahojiano yaliyorekodiwa na mtandao mmoja wa nchini Marekani, Paul Gohranson ambaye ni mtaalamu wa kuchua misuli na aliyewahi kuishi kimapenzi na Klein, amesema kuwa Jacko alipoteza uwezo wake wa kutengeneza mbegu za uzazi baada ya baba yake kumpiga korodani zake.
Gohranson alieleza kwamba hali hiyo ndiyo iliyopelekea rafiki yake wa zamani kujitolea mbegu zake ili kumwezesha Jacko kuwa baba.Alinukuliwa akimuuliza "Arnold kwanini Michael Jackson asitumie mbegu zake mwenyewe? alijibiwa kuwa Michael alikuwa hawezi kuzaa"
Akifafanua Arnold alisema kuwa Klein alimwambia na kumthibitishia mara mbili kuwa Michael Jackson aliwahi kumwambia kuwa alipigwa sehemu zake za siri mara mbili kwanza wakatia akiwa mtoto mdogo ambapo baba yake alimnyanyua mguu wake mmoja na kuanza kumpiga.Alisema kuwa Klein aliendelea kumueleza kuwa baba yake Michael hakudhamiria kumpiga sehemu zake hizo za siri wakati huo lakini ndiyo hivyo imetokea na ilimsababishia maumivu makali sana Michael.Mara ya pili ilikuwa pale Michael alipotoa albamu ya peke yake, kila mtu alimjia juu Jacko kuwa anapoteza sauti yake, mtazamo wake na huenda akaitia aibu familia ya Jackson.
Jamaa akiendelea kusimulia mkasa huo akasema baada ya Michael kumaliza kumwambi yote hayo, machozi yalikuwa yakimtoka na hayo aliyaeleza baada ya kufanyiwa vitendo hivyo alisema Klein.Hata hivyo baba yake Michael Joe Jackson, alikanusha kwamba aliwahi kupiga mtoto wake huyo kiasi hicho wakati wa utoto wake.
Familia ya Michael kwa muda mrefu ilikuwa ikilalamikiwa kwa ukatili dhidi ya mwanamuziki huyo hasa katika kipindi ambacho ilikuwa ikisimamia kazi za Jackson 5.Katika utetezi wake mzee Joe aliwahi kusikika akisema kuwa hakuwahi kuwa kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto wake hao wakoseapo.
Kwenye mahojiano yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa toka gerezani kwa kuhusishwa na kifo cha Michael Jackson, Dokta Conrad Murray alielezea kwenye mahojiano aliyofanya na The Mail kwamba, Michael hakuwa baba wa mtoto wake hata mmoja.
Nguli huyo Michael aliathiriwa na madawa kiasi cha kufikia hatua ya kuhitajika kuwa anavaa condom sababu mkojo ulikuwa unatoka wenyewe kwenye uume wake.Naamini aliamka na kuamua kufanya aliyozoea kufanya, akajidunga sindano haraka ambayo ilisababisha kumpeleka kwenye hali iliyomfika.
Michael Jackson alikuwa kwenye majanga mwishoni mwa maisha yake, akiwa na msongo wa kimawazo aliyekata tamaa japokuwa Dokta Muraay alijaribu kumlinda ila mwisho wa siku niliangushwa naye.
Jackson alikuwa ameingia kwenye matatizo ya kuathirika kiakili na kimwili kutokana na ziara yake ya London.’’ Alisema Dokta Conrad Murray.
Kifo cha Michael Jackson kilitokana na kuzidisha kiasi cha dawa wakati anajiandaa na ziara ya tamasha lake la This Is It. Tamasha ambalo lilitakiwa lianze katikati ya mwaka 2009, ikaripotiwa kwamba alitumia dawa aina ya Propofol na Afisa uchunguzi wa vifo wa Wilaya ya Los Angeles walielezwa kuwa kifo chake ni uuaji wa binadamu, na mashtaka yanakwenda kwa daktari wake binafsi kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Kifo hicho cha Michael kiliamsha mihemko ya huzuni na huduma ya ukumbusho wake uliofanywa hadharani ulitangazwa ulitazamwa na maelfu ya watu moja kwa moja duniani.Mbabe huyo katika mambo ya sanaa Michael Jackson katika siku zake za mwisho kabla kifo chake, alikuwa akijua mambo yote yatakayomtokea.
Hii ni kwa mujibu wa dada yake La Tonya, ambaye aliamua kufunua mambo hadharani. Akiadai kuwa kaka yake hakufa kwa kifo cha kawaida na kwamba palikuwa na mapango kamambe wa kuondosha uhai wake.
Kwa mujibu wa La Tonya mfalme huyo wa Pop, aliyekuwa maarufu kwa jina la WackoJacko, alimuambia kwamba lazima atauawa kutokana na muziki wake.La Toya ambaye pia ni msanii maarufu alidai alimuambia Wacko Jacko kuwa “Watu wanakuingilia mpaka katika maisha yako, angalia mumo unavyoishi, ni lazima ujidhibiti hasa katika fedha zako. Wale wanaokufadhili, mapato yako na kila kitu kinachokuhuhusu.
Alidai kwamba baada ya kumwambia hivyo,Michael Jackson alimtazama na mwisho akamwambia “La Toya ,mimi nakwenda kuuawa na hasa kutokana na muziki na mali ninazozimiliki…”La Tonya alidai Wacko alikuwa anaogopa mno kuhusu maisha yake na akimshutumu Dk.Tohme Tohme ambaye ndiye aliyekuwa anamsimamia katika kuchangia kwa kiasi kikubwa kifo chake.
“Huyu alikuwa anajifanya mshauri wa kibiashara wa Michael Jackson, akafukuza watu wangu muhimu zaidi ambao walikuwa na Michael Jackson kwa muda mrefu…” Alitamka La Tonya.Mwanadada huyo alisema kuwa dunia itaendelea kumkumbuka Michael Jackson.
Historia ya Michael Jackson inaeleza kuwa kutokana na umahiri wake wa kuimba na kucheza, alipewa heshima ya kuwa Mfamle wa Pop.Aliingizwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness kama mmja wa wanamziki wanaopendwa.
Alianza kuonesha cheche zake katika muziki akiwa mdogo kabisa pale alipoungana na ndugu zake na kuunda kundi la The Jackson 5, kabla hawajalibalisha jina na kuliita Jackosons mwaka 1964.Lakini miaka saba abaadaye aliamua kujiondoa katika kundi hilo, akaanza kupiga muziki peke yake.
Miaka ya 1980, Wacko Jacko akaja kuwa maaruru zaidi katika muziki hasa alipoibuka na Video za nyimbo zake za Beat It, Bile Jean na Thriller amabzo zilichangia kwa kiasi kikubwa kwa Televisheni mpya iliyokuwa imeanzishwa ya MTV.
Video nyingine kama Black or White na Scream zikaibeba MTV kiuifanya iendelee kung’ara zaid katika miaka ya 1990.
Album yake ya Thriller iliyotoka mwaka 1982, ndiyo iliyouza nakala nyingi mno kuliko nyingine zote, huku zile za Off the Wall (1979), Bad (1985), Dangerous,(1991) na History (1990) nazo pia ziilingiza mauzo makubwa duniani.
Wacko Jacko wakati wa uhai wake alitwaa mamia ya tuzo na kumfanya kuwa mmoja kati ya wasanii waliopata tuzo nyingi katika historia ya muziki. Pia alijulikana kwa jinsi alivyokuwa akisaidia jamii huku akiwa ametoa msaada kwa zaidi asasi 39.
Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, Wacko Jacko pia alichangia mamillioni ya dola kwa asasi mbalimbali zinazohusika na watoto. Michael Jackson alizunguuka katika hospitali nyingi mno kwa ajili ya kuwatembelea watoto.
Jacko mara nyingi alipokuwa akifanya zaira zake hizo, alipomaliza ni lazima alikuwa akiwauliza madaktari na wauguzi ni kitu gani walicho kuwa wanakihitaji kutoka kwake, akiambiwa vitu vya gharama kubwa, yeye alitimiza.
Mnamo mwaka 1993 alikumbwa na kashfa ya ngono na watoto, lakini kesi iliyofunguliwa ikamalizwa nje ya mahakama huku mwaka mwaka 2005, pia alikumbana na kesi nyingine kama hizo.
Aidha Kampuni ya Sony Music Entertainment ilisaini mkatataba wa milioni 250, ili iwe haki ya kusambaza haki zake mpaka 2017. Wacko Jacko alikuwa amejiandaa kufanya shoo moja kubwa kubwa iliyokuwa imepewa jina la This is It.Machael Jackson alikuwa mtoto wa nne kati ya kumi ambao ni Wamerekani wenye asili ya Afrika. Aliishi na ndugu zake katika nyumba moja ndogo ya vyumba vitatu iliyokuwa katika eneo la viwanda katika Jimbo la Chicago, nchini Marekani.
Mama yake Katherine Esther Scruse ni muumini mzuri wa mashahidi wa Yehova.Baba yake Joseph Walter ‘Joe’ Jackson, alikuwa mfanyakazi wa kwenye kiwanda cha chuma.Lakini pia alikuwa na bendi iliyokuwa ikijulikana kwa jia la The Falcon, ambayo alikuwa ikipiga katika mtindo wqa R&B.
Wacko Jacko alikuwa na dada watatu ambao ni Rbbie, La Toya na Janet huku wanaume wakiwa watano amabao ni akina Jackie, Tito, Jaremaine, Marlon, Randy na Kaka yake Brando, aliyekufa muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake.
Michael Jackson alikuwa na msuguano katika uhusiano yake na baba yake, huku baba akidai alikuwa akitimiza majukumu yake kama mzazi.
Japokuwa ilikuwa imeripotiwa kudhalilishwa kwake wakati akiwa mtoto kwa miaka kadhaa, yeye binafsi alizungumza kinagaubaga kuhusu hilo katika mahojiano yake ya mwaka wa 1993 na Oprah Winfrey.
Alikunja uso kwa huzuni wakati anazungumzia mateso aliyokuwa ana pata kutoka katika mikono ya baba yake mzazi. Aliamini ya kwamba ameyakosa maisha yake ya utotoni kwa miaka kadhaa, akikubaliana na hali ya kwamba alikuwa akilia mara kwa mara hasusan kwa kufuatia upweke aliokuwa nao.
Walisema ya kwamba walikuwa wakinyanyasika sana kimwili na kihisia na baba yao.Katika moja ya mabishano makali ambayo baadaye yalikumbushiwa na Baba yake mzee Joseph, aliwahi kumning'iniza Michael miguu juu kichwa chini huku akimshika mguu mmoja tu na kumchapa vibiko kwa mkono wake na kumpiga vibako vya matakoni.
Mzee huyo alikuwa na kawaida ya kuwachukua vijana na kuwatupa ukutani.
Usiku mmoja wakati Michael Jackson kalala, baba yake mzee Joseph alipanda hadi chumbani kwa mwanae kwa kupitia dirilisha la bafuni, huku akiwa amevaa kinyago cha kutisha. Akaingia chumbani Michael akanza kupiga ukelele wa nguvu.
Mzee huyo alisema eti alitaka kuwafundisha watoto zake wasiache dirisha wazi wakati wanaenda kulala. Kwa miaka kadhaa baada ya hapo, Michael Jackson alikuwa akisumbuliwa na ndoto za kutisha za jinamizi likija kumchukua chumbani kwake, mwanzoni mwa miaka ya 1980
Mwaka wa 2003, baba yake alikiri kwamba alikuwa akimchapa viboko sana Michael Jackson wakati yu mtoto.
Michael Jackson alikuwa binadamu wa kwanza kukosa usingizi kamili kwa siku 60, wataalamu walibaini. Daktari wake binafsi wa Michael Jackson, Conrad Murray alikuwa akimpa dawa za kutuliza maumvu kwa miezi miwili mfululizo kila siku hali iliyopelekea mwili kuchoka kila wakati.
Inaelezwa kwamba dawa hizo zina kawaida ya kumyima mtu usingizi na zinaweza kumfamfanya kupoteza fahamu.Daktari bingwa na mtaalamu wa magonjwa ya kichwa, Charles Czeisler alisema kuwa Michael Jackson huenda alifariki aidha kwa sabababu ya kukosa usingizi muda mrefu, au kwa kuumia kwa muda mrefu dawa za kutuliza maumivu alizokuwa akipewa na Murray.
Siku chache kabla ya kifo chake, ilielezwa kuwa hakuweza kucheza japo kidogo au hata kukumbuka baadhi ya maneno kwenye nyimbo zake.Wakati fulani katika miaka ya 1990, ilionekana ya kwamba Michael Jackson alikuwa tegemezi kubwa la madawa mbalimbali, hasa dawa za kuua maumivu na vipoozeo vikalivikali ambapo afya yake ikaanza kuyumba waziwazi.
Wakati uchuguzi unaendelea, hali ya Jackson ilishughulikiwa na Stan Katz, mtaalamu wa masuala ya akili.Kwa mujibu wa Randy Taraborrelli, uchunguzi uliofanywa na Katz ulionesha Jackson akili yake imerudi kama mtoto mwenye miaka kumi.
Baadhi ya wataalamu wa tiba walithubutu kusema hadharani kwamba wanaamini mwimbaji huyo pia alikuwa na matatizo ya akili ya kujiona kama watu wengine wanamuona si yeye kutaka mwonekano wa mtu mwingine.
Hali ya kisaikolojia ambapo msumbuliwa hana wazo au uwezo wa kufikiria taswira yake jinsi watu wanavyochukulia.Michael Jackson alienda kujiswafi mwaka wa 1993 kwa msaada wa Elizabeth Taylor na Elton John, lakini ulevi wa dawa ulibaki palepale.
Wacko Jacko alikuwa hapendi kabisa kulizungumzia hilo, lakini pindi tu anapolisema, alikuwa na huzuni sana na kusema ya kwamba angetapika kabla ya kukutana na baba yake.
Mungu aiweke pahala pema peponi, Amina.
Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkuwa wa mitandao.
Mwaandaji anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200,0736331200 na 0713331200.
Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.