Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

SADC YAELEZA SABABU ZA TANZANIA KUPEWA NAFASI YA KUANDAA MKUTANO WA JUMUIYA HIYO MWEZI AUGUST,2019

$
0
0
Tanzania imepewa fursa ya kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kutokana na kutimiza vigezo vinavyohitajika na jumuiya hiyo ikiwemo uwepo wa demokrasia na utawala bora mbali na vigezo vingine kama vile mchango wa Tanzania katika ukombozi wa bara la Afrika pamoja na uwepo wa uenyekiti wa awamu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt Stagomena Tax muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa 21 wa kamati ya mawaziri kuhusu asasi ya siasa,ulinzi na usalama ya Jumuiya ya maendeleo kusini mwa bara la Afrika SADC kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mulungushi Lusaka nchini Zambia.

Amezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kukuza demokrasia na utawala bora kwa kuwa ndio nguzo muhimu za jumuiya hiyo na kwamba licha ya uchanga wa demokrasia katika ukanda huo nchi hizo zimeendelea kupiga hatua kubwa katika kuboresha demokrasia na utawala bora na Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozingatia uwepo wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama. 

Mkutano huo wa mawaziri wa asasi ya siasa,ulinzi na usalama ya Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC umeiridhishwa na ukuaji wa demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama kutokana na chaguzi zilizofanyika kwa haki,uhuru na Amani katika nchi takribani sita ikiwemo Afrika ya Kusini,Eswatini,Malawi,Madagascar pamoja na Jamhuri ya demokrasia ya Congo DRC.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema kumalizika kwa chaguzi katika nchi sita wanachama wa jumuiya hiyo kunaidhihirishia dunia namna ambavyo Ukanda wa Kusini mwa Afrika ukiyasimamia mambo yake yenyewe bila ya kuingiliwa na mataifa mengine,Afrika ina uwezo wa kuimarisha taasisi zake za demokrasia,utawala bora na haki jambo ambalo Tanzania inalisimamia kwa dhati na kwa umakini.

Ameongeza kuwa mkutano huo pia umejadili suala la maombi ya Burundi kuomba kujiunga na jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maombi ambayo yamekuwepo kwa takribani miaka mitatu sasa, na kutanabaisha kuwa Burundi imetekeleza kwa kiwango cha asilimia sabini masharti iliyotakiwa kuyatimiza ili kupata ridhaa ya kuwa mwanachama wa SADC na kwamba yale ya asilimia thelathini yaliyosalia,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na sekretarieti ya SADC na nchi nyingine wanachama zitaendelea kuisaidia Burundi ili iweze kuwa mwanachama jambo litakaloisaidia Burundi kuimarika kisiasa na kidemokrasia na kushiriki katika maendeleo ya Bara la Afrika.

Maazimio yote ya mkutano huo wa 21 wa kamati ya mawaziri kuhusu asasi ya siasa,ulinzi na usalama ya Jumuiya ya maendeleo kusini mwa bara la Afrika SADC sasa yatapelekwa katika mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utakaofanyika Dar es Salaam nchini Tanzania mwezi Augusti mwaka huu ili wakuu hao wan chi waweze kufanya maamuzi ya mwisho kwa ajili ya utekelezaji.

Aidha Prof. Palamagamba John Kabudi ameitumia fursa ya mkutano huo kumweleza Katibu Mkuu wa SADC Dkt Stagomeana Tax kuhusu maandalizi ya mkutano wa SADC utakaofanyika Dar Es Salaam Tanzania ambaye ameonekana kuridhika na maandalizi hayo huku akiwasisitiza watanzania kuitumia fursa ya ujio wa wakuu wa Nchi 16 kwa pamoja Tanzania kwa ajili ya kujipatia kipato kupitia furtsa mbalimbali za kibiashara zitakazojitokeza katika mkutano huo.


Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Sweden na Denmark waliyomaliza muda wa kazi nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi Tinguely zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi Jensen zawadi ya picha iliyochorwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen na Balozi Sweden Mhe. Florence Tinguely hapa nchini ambao wamemaliza muda wao wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen (wa pili kutoka kulia), Balozi Sweden Mhe. Florence Tinguely (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Petterson kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
Balozi wa Italy Mhe. Roberto Mengoni (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Charles Mbando wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
Balozi Sweden Mhe. Florence Tinguely naye alitoa neno la shukrani kwa ushirikiano alioupata wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa hapa nchini. ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na kuitangaza vyema Tanzania 
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen naye alishukuru kwa ushirikiano alioupata wakati wote katika kutekeleza majukumu yake akiwa hapa nchini. Hata hivyo hakusita kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na Rushwa pamoja na kujenga miundombinu mizuri hapa nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (katikati), kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Jestas Nyamanga wakiwasikiliza Balozi wa Sweden na Denmark (hawapo pichani) walipokuwa wakizungumza. 
Kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed naye akizungumza neno wakati wa hafla ya kuwaaga Mabalozi wa Sweden na Denmark (hawapo pichani) 

KIONGOZI WA MWENGE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA TENKI LA MAJI PUGU

$
0
0
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali ameweka jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa tanki na mfumo wa usambazaji maji katika maeneo ya Pugu, Gongo la Mboto, Pugu Station, Air Wing, Ukonga na Majohe.

Kiongozi huyo pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mgema kuhakikisha malighafi zote zinazotumika katika mradi wa maji Pugu yanafanyiwa vipimo kubaini ubora wake ili kuhakikisha mradi huo unakuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi huo ambao unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam DAWASA.

Mmradi huo umegharimu Sh. Bilioni 7.3 ambapo Mzee Mkongea amemshukuru Rais Magufuli kwa  kuhakikisha watu wanapata MajiSafi na salama.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa  mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huo unatekelezwa na mamlaka hiyo ikiwa ni katika jitihada za kuboresha huduma za maji kwenye maeneo yaliyokuwa hayana mtandao wa maji safi lengo ni kufikia asilimia 95 ya wakazi mnamo 2020.

"Mradi huu unatarajiwa kusambaza maji katika maeneo ya Pugu, Majohe, Gongo la mboto, Bangulo, Ukonga-Airwing, Kigogo na Buyuni/Chanika na maeneo jirani pia mradi utaendelea kupanuliwa kulingana na upatikanaji wa fedha", amesema

Ameongeza kuwa bomba Kuu litakuwa na uwezo wa kusafirisha kiwango cha maji kipatacho lita 2,880,000 kwa siku ambapo wakazi wapatao 450,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo pamoja na maunganisho mapya ya wateja zaidi ya 50,000 yatafanyika mara baada ya kukamilika kwa mradi. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akisoma risala wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uwekaji wa  jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto uliofanyika leo katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha namna  mradi wa ujenzi wa Tenki na Mfumo wa Usambazaji wa Maji Pugu-Gongolamboto utakavyofanya kwa Viongozi wa Mbio za mwenge mwaka 2019.

Prof. Kabudi apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa India, Mhe. Sanjiv Kohli. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. 
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Balozi mteule Sanjiv Kohli mara baada ya kupokea nakala zake 
Mazungumzo yakiendelea 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Mteule Mhe. Sanjiv Kohli mara baada ya kumalizaka kwa hafla hiyo

CHUO CHA KODI CHAWAHIMIZA WANAFUNZI KUJIUNGA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Chuo cha Kodi kimesema kuwa wahitimu wa kidato cha sita wajiunge na chuo hicho kwa kuwa mazingira ya chuo hicho ni rafiki kwa kusomea pamoja na wigo wa kazi kwa kujiajiri kuwa mpana kutokana kuwepo kwa mahitaji katika masuala ya forodha na kodi ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Chuo hicho Oliver Njunwa amesema chuo kimejipanga vyema katika udahili wa mwaka wa masomo 2019/2020.

Amesema wanatoa kozi za forodha na kodi katika maeneo mbalimbali kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya taaluma hiyo kadri siku zinavyokwenda.“Serikali pamoja na kampuni mbalimbali zinahitaji wataalam wa masuala ya forodha na kodi”.

Njunwa amesema katika maonesho ya vyuo vikuu wanafanya udahili moja kwa moja hivyo wanafunzi watumie fursa hiyo kutembelea na kutatua changamoto zao katika kufanya maombi ya udahili.

Aidha amesema idadi ya waombaji katika chuo hicho imezidi kuongezeka kutokana na wananchi kukifahamu Chuo cha Kodi pamoja na umuhimu wa taaluma ya kodi katika nchi yetu ambayo dira yake ya maendeleo ni kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

Kwa mujibu wa Njunwa, maonyesho haya yamewafanya wananchi wengi hususan wazazi na wanafunzi wengi wafahamu fursa zilizopo baada ya kuhitimu mafunzo ya forodha na kodi ambapo wanafunzi waliohitimu katika chuo hicho wanaweza kufanya kazi katika sekta mbalimbali huku wengine wakijiajiri.

Chuo kinahakikisha mwanafunzi anajengewa uelewa wa kitaaluma, uwezo wa kutenda kazi ili anapomaliza masomo aweze kufanya kazi kwa umahiri na weledi wa hali ya juu.

Pia tumejipanga katika utoaji wa mafunzo yenye bora ili kuweza kukidhi mahitaji ya watalaam katika masuala ya kodi pamoja na forodha kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya watalaam katika sekta hiyo.

Chuo cha Kodi kimesajiliwa na Baraza la Vyuo vya Elimu ya Ufundi na kupatiwa Ithbati ya kudumu kutoa mafunzo yafuatayo ambayo ni Astashahada ya Forodha ya Afrika Mashariki -East Africa Clearing and Freight Forwarding Practicing Certificate (CFFPC), Astashahada ya Forodha na Kodi- Techninican Basic Certificate in Customs and Tax Management (CCTM), Stashahada ya Forodha na Kodi - Diploma in Customs and Tax Management, Shahada ya Forodha na Kodi- Bachelor Degree in Customs and Tax Management- (BCTM).

Kozi nyingine ni:- Stashahada ya Uzamili ya Forodha na Kodi – Postgraduate Diploma in Tax, Shahada ya Uzamili ya Sheria na Usimamizi wa Kodi- Masters of Arts in Revenue Law and Administration (MARLA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha dare salaam na Chuo Kikuu cha Muenster cha Ujerumani.

Tunawashauri wanafunzi waendelee kutuma maombi yao kabla muda wa udahili kumalizika.
Afisa Udahili wa Chuo cha Kodi Paschal Gomba (kulia) akiwasaidia wanafanuzi kufanya udahili wanafunzi waliotembelea banda la chuo hicho katika maonesho ya 14 ya vyuo vikuu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Edwin Matemanga afisa udahili wa chuo cha kodi.
Afisa Udahili wa Chuo cha Kodi Paschal Gomba akitoa maelezo kwa wanafanuzi waliotembelea banda la chuo hicho katika maonesho ya 14 ya vyuo vikuu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
Afisa Mkuu Mawasiliano Chuo cha Kodi, Oliver Njunwa akimfafanulia mzazi aliyetembelea maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

WAZIRI MKUU AWAFUNDA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vitabu katika maktaba iliyokarabatiwa ya Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Same Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa Same Sekondari, Omari Pundugu, akielezea changamoto mafanikio na changamoto za shule hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi, baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019.

*************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawe na mipango ya kazi ambayo itaweza kupimika na kutoa matokeo.

“Kila mtumishi anapaswa awe na mpango kazi katika sekta yake na ni lazima aende kupima matokeo. Awamu hii, tunataka kuona matokeo ya kazi zenu.” Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Julai 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Same kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, mjini Same. 

“Watumishi mmeletwa kwenye wilaya hii ili muwahudumie wananchi. Tulioajiriwa, kazi yetu kubwa ni kuwatumikia wananchi bila ubaguzi wowote uwe ni wa kabila, itikadi au rangi.” 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao kwamba baada ya mchujo wa watumishi hewa, waliobakia wanapaswa kufanya kazi kwa bidii. “Fanyeni kazi kwa bidii, msimamo wa Serikali hii ni kwamba hatumvumilii mtumishi ambaye si mwajibikaji, ni mwizi, mzembe au anaomba rushwa. Serikali hii hatuna muda wa kujadili matatizo ya watumishi, tunamalizana hapo hapo,” amesema. 

Amewataka watumishi hao wasimamie utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo chama tawala. “Mtumishi angalia sekta yako inasema nini, ifanyie kazi. Kama ni maji, tafuta ni wapi yanapatikana, changanua zinahitajika shilingi ngapi, tafuta njia ya kupata hizo fedha ili wananchi wapate maji.” 

Kuhusu tabia ya kukaa ofisini, Waziri Mkuu amekemea tabia hiyo na kuwataka watumishi wote nchini waache tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kuwasikiliza wananchi. 

“Watumishi wa umma msikae ofisini. Nendeni vijijini walau kwa siku nne za juma. Hizo mbili zinazobakia, zitumieni kuandaa taarifa. Nendeni huko ili wananchi wasipate usumbufu wa kuja hapa mjini kuwatafuta,” amesisitiza. 

“Mkuu wa Wilaya simamia zoezi la wakuu wa idara na wasaidizi wao kwenda vijijini. Wakienda vijijini ni lazima waonane na waheshimiwa madiwani, washirikiane kusikiliza kero na kutafuta majibu kwa wananchi. Huo ndiyo mshikamano wenyewe unaohitajika,” amesema. 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma watambue mipaka yao na wajenge mahusiano baina yao na wengine. Alitoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Moshi, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

“Kila mmoja lazima atambue mipaka yake na mamlaka baina yake na wengine. Hapa mko wateuliwa, waajiriwa na wachaguliwa. Kila mtu ana nafasi yake ya kuwatumikia wananchi.Aliwataka watumishi hao watambue falsafa ya Kiongozi mkuu wa nchi ambayo inahimiza uchapakazi. “Kwa hiyo tunaposema Hapa Kazi Tu, maana yake chapa kazi na tuone matokeo. Tunasisitiza kazi na tunataka kazi unayoifanya, itoe matokeo,” alisema.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA MAJI SAME

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Same Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



*Azivunja Jumuiya za watumiaji maji Hedaru

*Aagiza Katibu wa Jumuiya moja akamatwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Same, Mussa Msangi kwa kosa la kumdanganya kuhusu mradi wa maji aliouzindua leo katika kata ya Hedaru.

Amechukua uamuzi huo leo jioni (Ijumaa, Julai 19, 2019) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Hedaru mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Lengeni-Hedaru, wilayani Same.

Waziri Mkuu alibaini kuwepo kwa tatizo wananchi walipoanza kuzomea wakati zikitolewa salaam za utambulisho kwa viongozi alioambatana nao. Kabla hajahutubia, aliamua kumuita Mhandisi huyo aelezee ukweli wa madai ya wananchi kwamba maji yametoka leo kutokana na ujio wake.

"Eleza ni kwa nini nilipofungua maji, hayakuwa na presha ya kutosha na wewe umesema upatikanaji wa maji umefikia zaidi ya asilimia 80?"Alipoulizwa kwa mwezi wanakusanya kiasi gani cha fedha kutokana na mauzo ya maji hayo, Mhandisi Msangi alijibu kwa mwaka uliopita walikusanya sh. milioni saba tu.

"Haiwezekani kama maji yanatoka, wenye KAMATI wapate shilingi milioni saba. Ni ama maji hayatoki au wanakusanya hela na wanazila."

Alipoambiwa aelezee utendaji wa mradi huo wa maji na kama alikuwa akiufuatilia, alishindwa kutoa maelezo kamili, akidai kuwa leo maji yanatoka kidogo kwa sababu kuna hali ya mawingu. "Mbona kule ndani ulisema zile betri zinasaidia kuvuta maji na kubalance upatikanaji wa maji wakati hakuna jua la kutosha?" alihoji Waziri Mkuu. 

Waziri Mkuu aliamua kumuita mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji maji au Kiongozi mwingine yeyote aje atoe maelezo, lakini wote hawakuwepo kwenye mkutano huo. Ndipo akachukua uamuzi wa kuzivunja jumuiya hizo.

"Jumuiya zote za maji nazivunja kuanzia leo, na wahusika wote watafutwe na Jeshi la Polisi. Haiwezekani nipewe kazi ya kuzindua mradi ambao hauna maji," alisema Waziri Mkuu.

"Katibu Tawala wa Mkoa lete wakaguzi wa mahesabu kwenye huu mradi, pia leta Mhandisi mwingine asimamie huu mradi. Huyu arudishwe kwa Waziri wake," alisema.Waziri Mkuu pia alimwagiza Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Awesu abaki Hedaru na afuatilie utendaji wa mradi huo kisha ampe taarifa.

Wakati akimaliza kutoa maagizo hayo, Katibu wa Jumuiya ya watumiaji maji Hedaru-Masasi (HEWAUA), Bw. Francis Kazen Kiondo aliletwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi, lakini Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kituoni akatoe maelezo.

Taarifa zilizothibitishwa zimebainisha kuwa Kata ya Hedaru inazo Jumuiya tatu za watumiaji maji ambao ni Hedaru-Masasi, Lung wana na Mradi wa Kati. Wakazi wa Hedaru wanakadiriwa kufikia 20,000.

Ilibainika kwamba wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Hedaru-Masasi, Bw. Clement Ngoka aliamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa sababu ya upinzani aliokuwa akipata kwa viongozi wenzake ambao pia wanadaiwa kuwaunganishia maji baadhi ya watu hadi majumbani kwao na fedha zilizolipwa hazijulikani zilipoenda.

Awamu ya pili ya mradi wa maji alioenda kuuzindua Waziri Mkuu, inahusisha ujenzi wa chanzo cha maji katika korongo la mto Rangeni ambao ulikamilika Desemba 2018. Chanzo hicho cha mtiririko, kilitarajiwa kuzalisha lita 750,000 kwa siku ili kusaidia maji yanayozalishwa kwenye visima ambayo yana ujazo wa lita 7,500 kwa saa.

BENKI YA DUNIA YAIJENGEA TANZANIA UWEZO WA TATHMINI BAADA YA MAAFA

$
0
0

Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo  wa Utekelezaji wa Mipango ya  menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo  wa Utekelezaji wa Mipango ya  menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali  Jimmy Matamwe (Wa pili kulia), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Menejimenti ya Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania, Edward Anderson na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu, , wakati  wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji  wa Mpango wa  Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa  taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa  Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
***************

Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia  Ofisi ya Waziri  Mkuu,  Idara ya Menejimenti ya Maafa, imeendesha mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo,  jijini Arusha leo tarhe 19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa na wataalam wa kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na maendeleo.

“Mafunzo haya yatatusaidia kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa  kuwa na mfumo  wa pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika  kuendesha shughuli ya Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu binafsi, Taifa na Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza kuwa na mpango wa pamoja wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.

Matamwe ameendelea kufafanua kuwa kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa kurejesha  hali, utaalamu huo utaisaidia nchi yetu Tanzania kuwa na Takwimu za  urejeshaji hali  ambazo tutapata uwezo wa kurejesha hali itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.

Akiongea katika mafunzo hayo  kwa niaba ya Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Mtaalamu wa Mawasiliano Benki ya Dunia Edward Anderson amefafanua kuwa  Benki hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na  wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa wakati baada ya maafa kutokea.

“Tangu mwaka 2016 nilipofika hapa nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea  ikiwemo tetemeko la ardhi mkoani Kagera, na mafuriko katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016, hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na Mpango bora katika kurejesha hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo tayari katika kutekeleza hayo” Amesema Edward.

Aidha, washiriki wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa kurejesha hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji, mbinu za kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji hali, kuainisha hasara na athari  zitokanazo na maafa  .


Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia  tarehe  16 hadi 19 Julai, 2019,  liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa , kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,  kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

WANANCHI ARUMERU WAJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

$
0
0
Na Woinde Shizza  Michuzi Tv,Arusha
Mwitikio wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura jimbo la Arumemeru mashariki  upo vizuri , kwani Katika Kata Akheri,Kwarisambu, Poli wananchi wanajitokeza kwa wingi haswa vijana waliotimiza miaka 18 wanaojiandikisha kwa mara ya kwanza
 Hayo yanebainishwa na Afisa mwandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki Emmannuel Mkongo akizungumza na wandishi wa habari ,ambapo mwitikio wa  Kata hizo mwitikio ni mkubwa zaidi maeneo yenye mikusanyiko ya watu unaotokana na shughuli za kibiashara tofauti na maeneo ya pembezoni ambapo mwitikio ni mdogo.
Mkongo amesema hakuna changamoto iliyojitokeza ikaahiri zoezi  hilo hadi sasa kwani baadhi ya Mashine za Bvr  zilizo kuwa na itilafu na shindwa kuchapa  vitambulisho ilitatuliwa na wataalamu wa TEHAMA .
 "Nilipopita kukagua zoezi hili la uandikishaji  Kituo cha Kupigia kura chuo cha Mifugo Tengeru LITA  nilikuta BVR KIT haifanyi kazi  na kwa sasa wataalam wa TEHAMA mameshatatua na wananchi wanapata huduma"ameeleza Mkongo.
Mkongo ametoa rai kwa  Wananchi kuhifadhi vizuri vitambulisho vyao vya  Mpiga Kura  kwani wengi wao wanaokwenda kuboresha taarifa zao  imeoneka vitambulisho vyao vya awali kuharibika (vunjika) kutokana na kuvikali vikiwa mifukoni ,alibainisha  Kitambulisho cha mpiga kura ni kitambulisho muhimu kwani kinakupa haki ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Rais ,Mbunge na Diwani hivyo hamna budi kuvihifadhi vizuri.
Aidha Mkongo ametoa rai kwa wananchi ambao wanataka kurekebisha na  kuhamisha taarifa zao,kufuta taarifa zao, wanaotimiza umri wa  miaka 18 ifikapo tarehe 28 Mwezi Octoba 2019 na wenye miaka umri wa 18 ambao hawajajiandikisha kujitokeza na kujiandikisha na kupata vitambulisho vya Mpiga Kura kwani zoezi hilo litadumu kwa siku saba tu.
Afisa uandikishaji jimbo la Arumeru Mashariki ,ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo akifuatilia utendaji wa BVR KIT Operator Mbora Kweka ,katika kituo cha kupiga kura Mkwakirika Kata ya Poli
Ayob mbise akiweka alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura

TEWW Yajidhatiti Kuwakomboa Vijana Waliokosa Elimu katika Mfumo Rasmi

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bw. Timoth Anderson alitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la TEWW, juu ya sifa za kujiunga na Taasisi katika programu za Shahada, Stashahada na Astashahada , Katika Maonesho ya Vyuo vikuu Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yanafanyika toka 15-20 Julai 2019 
Afisa Udahili wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Bw. Justine Mbwamboakisisitiza jambo kwa mgeni alietembela banda la TEWW katika maonesho ya Vyuo Vikuu ambayo yanaendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. 
Mtumishi toka TEWW Bi. Felister Lyimo (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya ujazaji wafomu ya kujiunga na na TEWW, kwa mgeni alietembelea banda la Taasisi ya Elimu yaWatu Wazima, katika Maoneshoya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katikaviwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Umma na Shule Huria Bw. Placid Balige akiongea nawaandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna ambavyo Taasisi ya Elimu yaWatu Wazima (TEWW) inatekeleza mkakati wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania waliokosa elimu kupata Stadi za kazi, stadi za maisha na ujuzi wa Ujasiriamali ili kuwezesha Tanzania ya Viwanda kufikiwa. 

*************** 



Na Timoth Anderson – TEWW 

Taasisi ya elimu ya watu wazima (TEWW) imesema imeweka mkakati wa masomo wa kitaifa ambao utakwenda sambamba na Mpango Changamani kwa Vijana Walio Nje ya mfumo Rasmi wa Elimu maarufu kama ‘IPOSA’ ili kuwafikia Vijana wa kike na wa kiume ambao hawajawahi kwenda shule, wanafunzi walioacha shule za msingi, wanafunzi waliomaliza darasa la saba lakini hawajapata fursa ya kuendelea, wanafunzi waliohitimu masomo yao kupitia program ya MEMKWA, Wasichana walioacha shule kwa changamoto mbalimbali kama vile ujauzito na ndoa za utotoni Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Elimu kwa Umma Shule Huria, Bw. Placid Balige wakati alikuwa akizungumza na waandishi habari kwenye maonesho ya 14 ya Vyuo vya elimu ya juu sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. 

“Taarifa ya tathmin ya Mpango wa Elimu Changamani baada ya msingi (MECHAM) ya mwaka 2015,Utafiti uliofanywa na Wizara ya Elimu, Sayansi ya Teknolojia wa mwaka 2015 na taarifa ya takwimu ya Elimu ya msingi zinaonesha watoto wa kati ya miaka 14-17 wapatao 2,256,940 hawapo shule japokuwa ilibidi wawepo shule hivyo TEWW, Wizara yetu, wakaanza kuandaa mpango ambao hapana mtoto atakaeachwa kupewa elimu”.Amesema Balige. 

Ameongeza kuwa, watoto walioingia katika ndoa na mimba za utotoni na kukatisha masomo yao wamepata mafanikio makubwa kwani TEWW kupitia miradi yake mbalimbali wamewafundisha stadi za maisha jambo lililopelekea kuwawezesha kujiajiri wenyewe hali ambayo itawawezesha wale wenye nia ya kurudi shuleni kwa mfumo rasmi kurudi kwakuwa wameshapewa stadi za maisha juu ya kukabiliana na mazingira yao. 

Aidha, Bw. Balige ameongeza kuwa , watoto hao wameweza kufungua maduka nakuweza kudhalisha bidhaa zao wenyewe ikiwemo kutengeneza sabuni, kusindikachakula jambo lililopelekea kupata mkopo wa asilimia 4 wa vijana unaotolewa naHalmashauri katika maeneo yao ili kuwakomboa vijana kiuchumi. 

“Tumeweza kuwafikia vijana 3000 katika mkoa wa Dodoma,Rukwa na Lindi ambao walipata ndoa za utotoni na kukatisha masomo yao kwa sasa wameweza hata kujiunga Vikundi na kuweza kupata mkopo wa Manispaa wa asilimia 10 unatolewa nchi nzima”. Amesema Balige. 

Aidha amesema, Taasisi hiyo ilianzishwa na Sheria ya Bunge Namba 12 ya Mwaka 1975 ambapo pamoja na majukumu mengine inatoa Mafunzo kuanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada katika eneo la Elimu ya Watu Wazima na Mafunzo Endelevu pamoja na Ustawi wa jamii kwa njia ya ana kwa ana na kwa njia ya masafa ili kuwaandaa wataalamu wa Elimu ya Watu Wazima hiyo ikiwa ni mtekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kwasababu ni mpango mahususi katika kuchagiza Tanzania ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA MWISHO YA USAJILI WA NGO’s KANDA YA MASHARIKI

$
0
0

Wanasheria kutoka Ofisi ya Msajili Bw. January Kitunsi (kushoto) na Denis Bashaka (wa pili kushoto) wakitoa huduma ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kwa wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi lililohitimishwa leo tarehe 19/07/2019 kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO’s Bw. Baraka Leonard (kushoto) akitoa huduma kwa wadau ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi lililohitimishwa leo tarehe 19/07/2019 kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Wadau kutoka Mashirika Yaiyo ya Kiserikali wakisubiri kupata huduma ya kusajili Taasisi zao chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kutoka katika Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi lililohitimishwa leo tarehe 19/07/2019 kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Huduma ya kusajili Taasisi chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kwa wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine na yanayojisajili kwa mara ya kwanza katika zoezi lililohitimishwa leo tarehe 19/07/2019 kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.

VIONGOZI WASTAAFU CHAMA NA SERIKALI WATAKIWA KUACHA KUINGILIA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI AWAMU YA TANO-MBUNGE SIMANJIRO

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Mbunge wa Simanjiro, na kada wa chama cha Mapinduzi ccm,James ole Milly amewataka viongozi wasitaafu serikalini na Chama kuacha kuingilia na kukosoa jitihada zinazofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi badala yake waunge mkono jitihada hizo zinazofanywa na rais John Magufuli katika kuliletea maendeleo taifa.

Milly ametoa Kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha, kufuatia kuibuka kwa baadhi ya viongozi wastaafu nchini kuanza kukosoa na kubeza jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli ambaye ameonyesha uzalendo mkubwa katika kulitumikia Taifa na wananchi wake.

Mbunge huyo amewataja baadhi ya wastaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba na Mzee Abdulrahman Kinana ambao hivi karibuni waliibuka na kuandika waraka wakitumia kivuli cha chama cha Mapinduzi, alidai viongozi hao wastaafu hawana mamlaka ya kufanya hivyo.

Alisema wastaafu hao Mzee Makamba na Kinana hawana uhalali wowote wa kukosoa na kuhoji mwelekeo wa CCM na serikali yake."Ukisoma kwa kina taarifa ya viongozi hawa wastaafu wa CCM utagundua kuwa walikuwa na nia ovu ya kuhujumu na kutokuwa na imani na uongozi wa Rais Magufuli" Alisema Milly.

Amesema taarifa hiyo ni Kuendeleza siasa za kudhalilisha na kuponda juhudi za mabadiliko chanya ya kisiasa ,Kijamii,kiuchumi na kiusalama yaliyoanzishwa na mwenyekiti wa CCM ,Rais Magufuli.

Milly alisema pamoja na kutounga Mkono kauli mbalimbali zinazoibuliwa na wanaharakati ,ila aliwataka Makamba na Kinana iwapo wanabaini shutuma zinazoelekezwa kwao si za msingi ,kukimbilia mahakamani na si kutumia kivuli cha CCM .

Aliwataka wananchi kuepuka kauli za kichochezi zinazoenezwa na wastaafu hao kwa kuwa zinalenga kuigawa CCM na serikali yake na kuwataka wananchi wamuunge mkono rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR),mradi wa Umeme wa maji ya mto Rufiji (Stickers Gorge ,Ununuzi wa ndege 8 na ufufuaji wa shirika la Ndege nchini (ATCL).

Aliwataka viongozi wasitaafu kumwacha huru rais Magufuli ili atekeleze ahadi alizozitoa kwa wananchi na kuepuka kumwingiza kwenye misukosuko na migogoro ya kisiasa

NIC WATOA MSAADA WA MABATI 300 KWA HALMASHAURI YA ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Shirika la Bima la Taifa(NIC) limekabidhi mabati 300 yenye thamani ya shilingi milioni nane laki moja kwa wilaya ya Arusha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu mkoani Arusha. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mkurugenzi wa Shirika hilo Sam Kamanga alisema kuwa mabati hayo yanathamani ya shilingi milioni 8.1 na kuongeza msaada huo ni moja kati ya misingi ya utawala bora ambayo serikali inahimiza. 

Kamanga ameeleza kuwa ni mara ya kwanza kutoa msaada kwa Mkoa wa Arusha na kusema kuongeza kuwa tayari wameshatoa msaada katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro na Mwanza. 

Kamanga ameongeza kuwa wanatarajia kuja na bima ya kilimo watakayoizindua katika maonesho ya Nanenane mwaka huu mkoani Simiyu ambayo amesema ina lengo la kumkomboa mkulima. 

"tumeamua kuileta bima ya kilimo kwasababu wakulima wengi wamekua wanaingia katika kilimo na wakilima na kupata hasara wengine wanakata tamaa wengine wanakufa kwasababu ya presha ya kupata hasara hivyo ndio maana tumeleta msaada huu"alisema Kamanga

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro alilishukuru shirika hilo kwa msaada kwakuwa utasaidia katika maandalizi ya uhitaji wa sekta ya elimu na kuziomba wizara nyingine kuitikia maombi waliyoomba. 

Alisema kuwa tangu serikali ya awamu ya nne itangaze elimu bure kumekuwepo na muamko wa wanafunzi na wazazi kupeleka watoto shule hivyo itawasaidia katika kuwekeza madarasa ya vyoo na nyumba za walimu 
Mkurugenzi wa Shirika hilo Sam Kamanga watatu kulia akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro mabati 300.
mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro akimkabidhi mkurugenzi wa jiji la Arusha dr Maulid Madeni mabati yaliotolewa na shirika la bima ya Taifa (NIC) mara baada yakukabidhiwa na shirika hilo.

UHASIBU WAPONGEZWA KWA KUANDAA TAMASHA LINALOWAFANYA WANAFUNZI KUONGEZA UJUZI WALIOKUWA AWANA AWALI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

Wanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule mbali mbali jijini Arusha wamepongeza chuo cha uhasibu kwa kuandaa tamasha ambalo limewafanya kuweza kuongeza ujuzi waliokuwa hawana awali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa maonyesho ya Taaluma kwanye chuo cha uhasibu wanafunzi hao wamepata fursa ya kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo kutambua na kuwa na uwelewa kuchagua kozi zitakazo wafaa katika elimu ya juu .

Wamesema kwamba maonyesho hayo yamewatengenezea uzoefu na ujuzi kwani wamekutana na wananchuo wanao soma fani mbali mbali hivyo wanataraji kujiunga nazo mara baada ya kidato cha nne na hiyo imewapa hamasa ya kufikia elimu ya juu

Baadhi ya wanachuo wa chuo cha uhasibu wanaoshiriki maonyesho hayo wanaelezea Faida ya maonesho hayo ni kujitangaza kwa jamii kutambua masomo mbali mbali yanayo tolewa kwa wanafunzi na jinsi gani yanawasaidia kujiajiri nwenyewe

moja wa wakufunzi chuoni bundalla bachia hapo katika maonyesho hayo ameleza kwamba kumekua na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi wa secondary kutembelea mabanda na kujifunza mambo mbali mbali kutoka kwao

Akitembelea tamasha hilo waziri wa elimu na mafunzo ya Amali serikali ya mapinduzi ya Zanzibari Riziki Pembe Juma alisema ni fursa nzuri maana wanafunzi wanatumia zaidi katika tamasha hili kufanya mafunzo ya vitendo.

Alisema kuwa matamasha haya yatasaidia wanafunzi hawa kwani watabadilishana uzoefu wa aina mbalimbali ,pamoja na ujuzi wa aina mbalimbali ,pia maonyesho hayanasaidia wanafunzi hawa kupata muda wa kuonyesha kile ambacho wanajifunza hivyo ni jambo jema sana chuo hichi wamefanya.

Kwa vile ni mara ya kwanza kufanya basi waendelee kufanya mara kwa mara na wasishirikishe shule za serikali tu bali washirikishe na shule za binafsi uli wabadilishane uzoefu,lengo letu la serikali ni kuona vijana wetu wanajifunza na kujiajiri hapo baadae"alisema Riziki

Alitoa wito kwa vyuo vingine kuiga mfumo huu kwani ni mzuri unasaidia wanafunzi kujifunza mambo mbalimbali.
mmoja ya mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Arusha bundalla bachia akiongea na waandishi wa habari juu ya faida za tamasha hilo 
Daktari kutoka hospitali ya NIC akimpima mmoja wa wanafunzi aliuzuria katika tamasha hilo ambapo hospitali ya nic imetoa huduma ya upimaji sukari na presha .
Waziri wa elimu na mafunzo ya Amali serikali ya mapinduzi ya Zanzibari Riziki Pembe Juma wa pili kulia akiangalia baadhi ya vitu vinalivyoletwa na wanafunzi katika maonyesho yaliondaliwa na wanavyuo yanayofanyika ndani ya viwanja vya chuo cha uhasibu Arusha

MAHAKAMA YA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA KIMATAIFA YA UPATANISHI ILI KUWEZESHA MIGOGORO KUSIKILIZWA KWA NJIA YA UPATANISHI

$
0
0

Na Magreth Kinabo

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma amesema Mahakama ya Tanzania iko tayari kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Upatanishi ‘International Chamber of Commerce’ (ICC) ili kuwezesha Mahakama kusikiliza migogoro kwa njia ya mfumo wa upatanishi( Abitration).

Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu, ofisini kwake jijini Dar es Salaam ,wakati alipofanya mazungumzo na ujumbe watu watano kutoka taasisi hiyo, uliongozwa na Makamu wa Rais wa taasisi hiyo, Profesa . Dkt. Mohamed Wahab.

Awali Makamu huyo wa taasisi hiyo alisema wamefika hapa nchini ili kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu, Profesa Juma kushirikiana Mahakama ya Tanzania kuiwezesha kusikiliza migogoro kwa njia ya mfumo wa upatanishi.

Profesa, Dkt. Wahab aliongeza kwamba tayari nchi nyingine zimeruhusu Mahakama, imeruhusu mfumo huo kutumika na umeonyesha kufanikiwa, ambapo alitolewa mfano nchi ya Afrika Kusini na Mauritania, hivyo wangependa kuona na Tanzania inatumia mfumo huo na taasisi hiyo itatoa mafunzo kwa majaji.

“Ni tunaiomba Tanzania kutengeneza kanuni ili kuwezesha mfumo huo wa upatanishi kuweza kufanya kazi katika Mahakama za Tanzania.Jaji Mkuu alisema yuko tayari kuwezesha mfumo huo kuanza kutumika nchini kwa kuwa ni muhimu na utawezesha migororo kusikilizwa haraka.

“Tuna sheria ya Upatanishi, ni sheria ya zamani hivyo kuna haja ya kuihuisha ili iendane na mahitaji ya sasa,” alisema Profesa Juma.

Alisema Mahakama inatumia njia ya upatanishi ndani ya kesi za madai, lakini haujaweza kufanya kazi vizuri kwa sababu ya kutoeleweka ipasavyo miongoni mwa wadaawa.Hivyo aliongeza kwamba ni vizuri majaji na mawakili wakapatiwa mafunzo juu ya masuala hayo. Profesa Juma aliutaka ujumbe huo kuandaa andiko na kuhusu mfumo huo na kuonyesha mapendekezo yao.

Ujumbe huo umekuwepo nchini tangu Julai 17 na Julai 19 , mwaka huu na umefanya mazungumza na ujumbe wa Tanzania kuhusu masuala ya upatanishi ndani nan je ya, ikiwemo Siku ya Upatanishi iliyofanyika kwenye hoteli ya Slipway, Dar es Salaam Julai 18,mwaka huu na utakuja tena mwakani.

SHILATU AWASHUPALIA WAKANDARASI

$
0
0
Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Tabia ya Wakandarasi kuchelewa kukabidhi kazi kwa wakati na kwa ubora haitakubalika kwenye miradi ya ujenzi ya Serikali. 

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Ndugu Emmanuel Shilatu wakati alipotembelea kufuatilia maendeleo ya miradi ya ujenzi wa umaliziwaji wa maboma ya Madarasa kufuatia Serikali kutoa fedha za kukamilisha ujenzi huo na kuweka na Madawati. 

Akizungumza na Mwandishi wetu, Gavana Shilatu alisisitiza uzembe wowote wa kukabidhi kazi kwa wakati na kwa ubora hautavumilika. 
“Kwanza kabisa tunamshukuru Rais Magufuli kutoa fedha za kumalizia maboma nchi nzima. Kila nilipopita kwenye miradi ya shule zote nimewasisitiza Wakandarasi kuheshimu mkataba, kuheshimu BOQ, kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya pesa. Nimewaambia ndani ya siku 5 kuanzia sasa miradi yote iwe imekamilika ipasavyo, nitaenda tena kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yangu yote niliyoyatoa.” alisisitiza Gavana Shilatu. 

Tarafa ya Mihambwe imebahatika kupata fedha Tsh. Milioni 42.5 kukamilisha maboma ya madarasa matatu yaliyopo shule za Msingi za Misufini, Mmalala na Ngongolo.

MAKAMU WA PILI WA RAIS AFUNGUA TAMASHA 24 LA UTAMADUNI WA MZANZIBARI

$
0
0

Na Mwashungi Tahir,Maelezo 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi aliwataka vijana kuacha kuvutika na desturi za kigeni kwa kuacha mila zao kwani kunaweza kusababishia ukiukwaji wa maadili kwa Taifa la Wazanzibar. 
Wito huo aliutoa huko katika Uwanja wa Kumbu Kumbuwa Mapinduzi Square wakati alipokuwa akifungua Tamasha la 24 la Utamaduni wa Mzanzibar na kuwataka vijana waendeleze silka , tamaduni na mila za Kizanzibar ili jamii isipotee. 

Alisema Vijana hawafuati mfumo halisi wa maisha uliowakuza na hatimaye wamekuwa wahanga wa kuiga, kukumbatia na kufuata tamaduni ambazo kimfumo haziendani na mazingira pamoja na mfumo mzima wa maisha ya Wazanzibar. 

Hivyo alisema wakati umewadia kuacha utamaduni wa kigeni na kila siku tujivunie mambo ya Wazanzibar na kuwa na mikakati mbali mbali itayosaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuenzi kulinda na kuendeleza utamaduni wa Zanzibar. 

Pia alieleza kwamba tukiendelea kuadhimisha tamasha hili jamii ina wajibu wa kujiuliza na kupata jibu la pamoja kwa kiasi kipi matamasha haya yananandaliwa katika visiwa vya Unguja na Pemba na kuweza kubeba dhima na kusaidia ukuzaji na uendelezaji wa mfumo wa utamaduni na sanaa katika jamii ya Zanzibar. 

Vile vile alikemea matendo maovu ambayo yanakosa uadilifu na kusababisha kuzaa chuki , mifarakano, visasi baina ya familia na kuhatarisha mshikamano wa kijamii ambao husababisha uvunjifu na amani, kutia aibu Taifa na watu wake . 

Aliiomba jamii kuiunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika vitendo vua udhalilishaji kwa kuacha muhali au kuoneana haya jamii ijitokeze kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria hatimae sheria ichukuwe mkondo wake tukishirikiana kwa pamoja tunaweza na kuondosha madawa ya kulevya ili tupate vijana walio bora katika nguvu kazi. 

“naomba vijana wajiepushe na madawa ya kulevya ili Taifa lipate vijana walio imara na kupatikana Taifa lililo bora”,alisema Balozi Seif. 
Nae Waziri wa Vijana , Utamaduni, Sanaa na Michezo Ali Abeid Karume alisema Tamasha la Mzanzibar tutalienzi kwa lengo la kukuza mila silka na utamaduni ili jamii waweze kujua mambo ya visiwa hivi na kizazi kiendelee kujua mambo ya nchi yao yakiwemo mambo ya asili . 

Alisema tamasha hili mwaka ujao linatimiza miaka 25 ambalo litakuwa linaingia robo karne hivyo amewataka wananchi kutarajia tamasha kuwa kubwa zaidi . 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud alitoa rai kwa Wizara ya Vijana , Utamaduni , Sanaa na Michezo kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ianze mitaala ili watoto waanze wakiwa wadogo kufundishwa mambo ya utamaduni ili usipoitee. 
Alisema dhamira kubwa ya tamasha hili ni kutunza utamaduni , utu mila na silka za kizanzibar . 

Kauli mbiu ya tamasha hili ni”Utamaduni ni Ngao na ustawi wa jamii yetu” .

ALGERIA MABINGWA WA AFCON 2019

$
0
0
Timu ya Taifa ya Algeria imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mataifa huru Afrika AFCON baada ya kuifunga Senegal kwa goli 1-0.

Algeria wanabeba ubingwa huo kwa mara ya pili baada ya miaka 29 toka ilivyochukua kwa mara ya kwanza huku Senegal akiwa hajalibeba hata moja.

Mchezo huo ulianza na kasi ilichukua dakika 2 kwa Algeria kuandika goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Baghdad Bounedjah baada ya kupiga mpira na kumgonga beki wa Senegal na kupoteza mwelekeo wa mpira.

Mchezo ulikuwa na kasi kubwa, Senegal wakisaka goli la kusawazisha huku Algeria wakitaka kupata uhakika zaidi wa ushindi kwa kupata goli.

Mpaka mapumziko Algeria walienda vyumbani wakiwa kifua mbele. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na washambuliaji wa Senegal kushindwa kutumia nafasi walizozipata.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Algeria wanatwaa ubingwa kwa mara ya pili baada ya muda mrefu.

Mchezaji Ismael Benaccer wa Algeria amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa AFCON mwaka huu huku Mlindamlango wa Algeria Rais Mbolhi ndiyo Golikipa bora wa AFCON.

Algeria wamefanikiwa kuruhusu nyavu zao kutikishwa mara 2 dhidi ya Nigeria mchezo uliomalizika kwa ushindi wa 2-1 na ule wa Ivory Coast 1-1 ulioamuliwa kwa mikwaju ya penati na wakifunga jumla ya 13.

AZAM FC WATINGA FAINALI YA KAGAME CUP

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Azam FC imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Kagame kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuwaondosha kwa mikwaju ya penati As Maniema Union ya DR Congo.

Mchezo huo uliokuwa wa kasi na ushindani, ilichukua dakika 120 kuweza kupatikana kwa mshindi atakayeenda kucheza na KCCA ya Uganda kwenye mchezo wa fainali.

Azam ambao ndio mabingwa watetezi wakiwa wamelichukua mara mbili mfululizo watacheza fainali ya nne kihistoria siku ya Jumapili.

Katika Mikwaju ya Penati, Azam walifanikiwa kufunga penati 5-4 kufuatia dakika 120 kumalizika kwa suluhu. 

Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo mara mbili mfululizo, watacheza fainali hiyo dhidi ya KCCA ya Uganda Jumapili hii.

MILIONI 85/- ZA MIZANI KATIKA JIJI LA ARUSHA ZALIWA NA WATUMISHI WASIO WAAMINIFU,MHASIBU AKIMBIA,WAWILI WAKAMATWA

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha.

IMEELEZWA kuwa zaidi ya Sh.milioni 85 zimepotea kwa mwezi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokana na baadhi ya wafanyakazi wa Serikali , ambao wamekuwa wakichukua fedha za ushuru wa mizani na kufisadi fedha hizo kwa kuziweka mifukoni mwao badala ya kuzipeleka serikalini .

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Maulid Madeni wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kushutukiza katika mizani ya kupimia magari makubwa iliopo eneo la Morombo jiji hapa.

Amesema baadhi ya wafanyakazi wa mizani hiyo wakiongozwa na mmoja wa wahasibu wa halmashauri ya jiji(akamtaja jina) wamehujumu uchumi wa serikali ya awamu ya tano kwa kujaza mifuko yao na kuacha kujaza mifuko kwa Serikali ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli.

"Kiwango cha ukusanyaji wa mapato kwa sehemu husika ni milioni 2.4 kwa siku na kwa mwezi ni kama sh.milioni 85 kwa mwaka ni kama sh.bilioni 1.2 , sasa kwa maana hiyo kwa mwezi halmashauri inapata milioni mbili laki nane tu mafisadi hawa ambao ni huyu muhasibu pamoja na wakusanya ushuru wanatia mifukoni mwao milioni 85 ,sasa milioni hizo 85 mara miezi 12 ni sh.bilioni 1.2,hii haikubaliki,"amesema Madeni

Aidha amesema kuwa muhasibu huyu amekimbia na haonekani mara baada ya kugundua wametambua mchezo wake,na hivyo Serikali itamtafuta popote alipo maana nyumbani kwake hayupo ,kazini hajatokea na simu zake hazipatikani.

"Popote tutakapomkuta tutamkamata na kumpeleka Polisi ili sheria zifuate mkondo wake ,pia tunapenda kumwambia ajisalimishe yeye mwenyewe kituo kikuu cha polisi Arusha ili atoe maelezo hizo sh.bilioni 1.2 zinapotea namna gani.Muhasibu huyu ndio alikuwa amewapanga wapokea ushuru hawa wa mizani ya Morombo na walikuwa wanampelekea fedha,"amesema.

Amesema kuwa taarifa hizo wamezipata kutokana na mfumo wa mashine za kieletroniki ambazo wanazitumia ambapo alitoa mfano juzi Julai 18 zilikusanywa fedha ndogo sana ambazo ni Sh.540,000 lakini kwenye mfumo wa mapato wa kielotroniki unaonyesha kuna shilingi laki moja na kumi tu.Hii inamaanisha wakusanyaji wenyewe wanaiba na wakimpelekea pia mhasibu naye anaiba na anaingiza kiwango anachakitaka kwa hiyo tulipata taarifa tukasema lazima tuende tukafanye ukaguzi na tuje kuwakamata lakini kwa bahati mbaya mhasibu huyu alijua na akakimbia,"amefafanua. 

Ametoa onyo kwa wafanyakazi wote wenye tabia hii kwani pindi watakapo mpata fisadi au mhujumu uchumi anaeshibisha mifuko yake badala ya kufikisha fedha za Serikali salama,hata kama mdogo kiasi gani watamfikisha katika vyombo vya sheria maana serikali hii haipo tayari kulea wahujumu uchumi na mafisadi

Kwa upande wake Mchumi wa Jiji la Arusha Anna Mwambele amesema kwa sasa hivi katika Jiji la Arusha wamejipanga kufanya ufatiliaji wa mara kwa mara katika vyanzo vya mapato ,ili kubaini iwapo kuna vyanzo vinahujumiwa.

Ameongeza kuwa tangu waanze kufatilia wamebaini fedha nyingi sana zimepotea, hivyo kuamua kufanya zabuni mbalimbali na kuamua kuwapa wenzao wa Suma JKT ili kuweza kukusanya hayo mapoto.

Na kuziba mianya mbalimbali ya upotevu wa mapato,ili fedha zinazopatika ziwezeshe jiji la Arusha kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi mengine mbalimbali katika Jiji la Arusha na pia kuweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ambapo alisema kwa mwaka huu 2019/2020 wanamalengo ya kukusanya bilioni ishini pointi saba . 

Katika ziara hiyo wakusanya ushuru wa mizani wawili ambao ni Agness Loishie MA Thobias Julius wamekamatwa na kufikishwa kituoni kikuu cha Polisi huku mhasibu wa Jiji la Arusha yeye amekimbia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Maulid Madeni akiuliza Jambo wakati alipofanya ziara ya kushutukiza katika mizani ya kupimia magari makubwa iliopo eneo la Morombo jiji hapa.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images