Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19,2019


UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAFANIKISHA HAFLA YA UZINDUZI WA SAFARI ZA AIR TANZANIA MUMBAI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwele akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa safari za  Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) katika mji wa Mumbai nchini India. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Bandra Kurla mjini Mumbai tarehe 18 Julai 2019
Waziri wa Elimu, Michezo na Ustawi wa Vijana wa India ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi rasmi wa safari za a Shirika la Ndege la Tanzania mjini Mumbai nae akizungumza kwenye hafla hiyo
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai nchini India
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania, Mhandisi Emmanuel Korosso nae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za Air Tanzania mjini Mumbai, India
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa tayari kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai, India
Mhe. Kamwele akiwa na Viongozi wengine kutoka Tanzania na India wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akikata keki maalum kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Ndege za Air Tanzania mjini Mumbai, India
Matukio mbalmbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Air Tanzania mjini Mumbai
Mhe. Waziri Kamwelwe akipokea Jarida la Travel ambalo ambalo huandika taarifa kuhusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi kwa ujumla
Mhe. Waziri Kamwelwe (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (wa tatu kushoto), viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na India pamoja na Marubani waliofamikisha ndege ya kwanza ya Air Tanzania kutua Mumbai kwa ajili ya safari za kibiashara 
Mhe. Balozi Luvanda katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki uzinduzi wa safari za ndege ya Air Tanzania mjini Mumbai. Kushoto ni Bw. Kheri Goloka, Afisa wa Ubalozi Mwandamizi.

MAVUNDE AZINDUA MAONESHO YA KWANZA YA TEHAMA NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akizungumza na Wageni waalikwa kutoka makampuni mbali mbali yaayojihusha na Tehama, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walisoma mambo ya Tehama na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  
 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa maonesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  

 Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akisaini mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri, Wizara ya Kazi Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh.Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbalibali walisoma mambo ya Tehama wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya kazi za Teheama nchini Tanzania yalioandaliwa na Huawei Tanzania  jijini Dar es Salaam jana.  

OSHA WATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO ZAIDI VIONGOZI ILI KUSIMAMIA USALAMA NA AFYA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0
Na Khadija seif, Michuzi tv

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Mh Christina Mndeme amewashauri wakuu wa 
taasisi mbalimbali kujua vizuri majukumu ya wakala wa usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA) ili waweze kuwasaidia 
wananchi kulinda usalama na afya wakiwa kazini.

Mndeme amesema hayo mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala wa 
Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) jijini Dar es salaam kujifunza 
mambo mbalimbali yanahohusu usalama na Afya kwa Wafanyakazi.

Akizungumza na Uongozi wa Wakala wa usalama na Afya Mahali Pa Kazi 
(OSHA) Jiji Dar es salama, Mkuu wa Mkoa huyo alisema Jukumu la Viongozi 
wa serikali ni Kuijua OSHA vizuri na kusimamia usalama na Afya sehemu ya 
kazi katika maeneo yao.

Alisema yeye kama kiongozi wa Mkoa wa Ruvuma pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, anapokea 
Malalamiko kwa watumishi toka sehemu mbalimbali za uzalishaji, hivyo 
Kuifahamu vizuri OSHA kutusaidia pia kushughulikia malalamiko yanayoletwa na Wafanyakazi wakiwa maeneo ya kazi.

Hivyo OSHA haina budi kuwajengea uwezo zaidi Viongozi ili waweze kusimamia vizuri usalama na afya kwa wafanyakazi.

Pia Mndeme amewashauri wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) kufungua Ofisi zaidi mikoani na kusogeza huduma hizo hadi ngazi ya wilaya jambo ambalo litasadiakufahamika zaidi kwa wananchi wengi na kuwasaidia wananchi walio wengi kwenye maeneo yao.

“Naipongeza serikali kwa kuanzisha OSHA, hivyo niwajibu wetu kuiunga 
mkono, kwani shughuli za OSHA zinagusa wananchi wote. Tunajukumu la 
kumsaidia Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Katika 
kutekeleza majukumu yake, serikali imefanya mengi kupitia serikali ya 
awamu ya tano, imeweze kujenga Hospital, kupeleka Umeme hadi Vijijini 
hivi sasa kupitia REA wananchi wengi wameweza kuingiziwa 
Umeme”alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa pamoja na wafanyakazi wa uwakala wa usalama na Afya Mahala pa kazi (OSHA) Mara baada ya kuwatembelea na kupatiwa elimu mbalimbali kuhusu usalama Mahala pa kazi pamoja na majukumu

WAZIRI LUGOLA KUYAFUTA KAMPUNI BINAFSI YA ULINZI YANAYOAJIRI VIKONGWE, ASKARI FEKI WASIOPITIA MAFUNZO, KULIPA MISHAHARA FINYU

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya Nansimo, Mwibara, Wilayani Bunda, Mara, leo, ambapo amesema Serikali itayafuta makampuni ya ulinzi binafsi nchini ambayo yanaajiri askari vikongwe, wasiokuwa na mafunzo ya askari wa akiba (mgambo) wala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na kutowalipa au kuwalipa mishahara midogo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isack Mahela. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya Chitengule, Mwibara, Wilayani Bunda, Mara, leo, wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Chitengule jimboni humo. Lugola aliwataka wananchi hao kufanya kazi kwa kujitolea na sio kuwa na Imani kula kila kitu kinafanywa na Serikali. Aliyevaa Kaunda suti ni ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Isack Mahela. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………………………………… 

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Serikali itayafuta makampuni ya ulinzi binafsi nchini ambayo yanaajiri askari vikongwe pamoja na wasiokuwa na mafunzo ya askari wa akiba (mgambo) wala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 

Lugola amesema Wizara yake haiwezi kucheza na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi kwa kuyaacha makampuni hayo yakiendelea kuajiri vikongwe ambao hawezi kushika silaha za moto na pia mara kwa mara wanasinzia kiasi kwamba muda wowote wanaweza wakanyang’anywa silaha na majambazi ambao wanazitafuta silaha kwa ajili ya kufanyia uhalifu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, leo, Lugola amesema kutokana na upungufu wa askari, Serikali iliruhusu kuwepo na makampuni binafsi ya ulinzi kwa ajili ya kusaidia masuala ya ulinzi na usalama nchini, lakini baadhi ya makampuni hayo yanavunja sheria kwa kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo yoyote, askari waliostaafu ambao wamechoka na hawawezi kufanya kazi hizo na pia wanalipwa mishahara midogo au kutokulipwa kabisa.

Amesema kwa miaka ya hivi karibuni Serikali imeendelea kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba kwa wale wanaopita katika Jeshi la Akiba ambao wanaitwa Mgambo, na wale wanaopitia katika Jeshi la Kujenga Taifa, maeneo hayo mawili yasaidie kuzalisha askari ambao watachukuliwa na Makampani ya Ulinzi ili waweze kufanya kazi kwasababu wanauzoefu wamefundishika, wanajua jinsi ya kubeba na kutumia silaha za moto, namna ya kufanya doria pamoja na kulinda mali na maisha ya wananchi. 

“Lakini niendelee kusikitika, baadhi ya makampuni, tumeshuhudia, yanaendelea kuajiri askari ambao wamechoka, askari ambao wamestaafu kwa mujibu wa umri wao, kwa maana hawawezi kufanya kazi tena hizi za kiaskari, lakini wanaajiriwa tena katika makampuni haya ya ulinzi, lakini pia tumeshuhudia unashtukia tu asubuhi mwananchi uliyemuona jana mtaani, na unamjua kabisa huyu mtoto wa fulani, hana mafunzo yoyote ya askari wa akiba, hana mafunzi yoyote ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambapo vijana wanafundishwa uzalendo, uadilifu, lakini unamuona ghafla amebeba bunduki, amevaa sare za kampuni ya ulinzi, ana kirungu na anasema mimi nimepata ajira pale mjomba kanipeleka,” alisema Lugola.

Amesema yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na kupitia Jeshi la Polisi nchini, haiwezekani masuala ya ulinzi na usalama ukachezewa, ambapo Ulinzi unahitajhi watu wenye mafunzo, watu wakakamavu, watu ambao hawana maradhi, na pia unahitaji watu ambao wanaweza wakafukuzana na uhalifu lakini baadhi ya makampuni hayo yanaajiri watu ambao hawana sifa hizo.

Lugola alisema, kutokana na changamoto hiyo, Serikali inakaribia kukamilisha kuwepo na sheria ya makampuni hayo ya ulinzi, ambayo itasimamia vizuri makampuni yote nchini, na sheria hiyo itaenda kudhibiti pia masuala ya ajira askari hao.

“Unaona mzee anatoka kazini asubuhi na bunduki yake kachoka hatua ishirini tu ameona mti pale kuna kivuli anafika hapo anaanza kusinzia mzee wa watu na bunduki, hata yunifomu zenyewe hazimkai vizuri, kachokaa, eti huyo ni askari wa kampuni binafsi ya ulinzi, haiwezekani, silaha hizi zinahitaji umakini katika kubeba na katika kutumia, na wahalifu nao wanazitafuta silaha za namna hii, wakigundua mahala fulani kuna walioajiriwa ni wachofu, wapo hoi bin taabani hao ndio wanaonyang’anywa bunduki,” alisema Lugola.

Amesema amelielekeza Jeshi la Polisi, wahakikishe kuwa Makampuni hayo yanaajiri askari ambao wanasifa za kufanya kazi hiyo, pamoja na wahakikishe wanaajiri askari wenye sifa na kuwalipa askari hao vizuri, kwa kuwa baadhi ya wamiliki wa kampuni hizo wamekua wakiwatapeli, kutokuwalipa, na wengine wanakopwa na ofisi zao.

“Askari gani wanakopwa, hawalipwi, huyo ni askari wa namna gani, matokeo yake askari huyo ambaye ana dhana ya moto anaweza kushawishika akafanya matumizi ya silaha ambayo hayaruhusiwi, au mali za wananchi zikaporwa kwasababu huyo ameshakata tamaa, kwahiyo niwatake makapuni yote ya ulinzi ambao askari wao watanilalamikia mimi au watamlalamikia Inspekta jenerali wa polisi kwamba hawalipa askari wao, hatuwezi kukubali kuwa na askari wanaofanya shughuli za ulinzi na usalama ndani ya nchi hii ambao hawalipwi, nitahakikisha makampuni hayo nitayachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha yanafutwa kwenye madaftari ya makampuni ya ulinzi nchini,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola katika ziara anayoendelea nayo jimboni kwake, kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, pia aliwataka wananchi wa jimbo hilo, kufanya kazi kizaelendo kujenga miundombinu, na kutofikiria kazi za maendeleo zinafanywa na Serikali pekee.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI KUJADILI NAMNA BORA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA MWAKA 2019 – 2020

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akizungumza na Wakurungenzi wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo walipokutana kujadili maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka wa fedha 2019 – 2020.
Mkurungenzi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bw. Ally Msaki akielezea jambo kuhusu uwasilishwaji wa mpango kazi kwa kila taasisi wakati wa kikao kilichowakutanisha kujadili maeneo ya ushirikiano yanayoitaji utekelezaji wa pamoja.
Baadhi ya Wakurugenzi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la PSSSF, Jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba.
Sehemu ya wataalamu wa mipango na bajeti kutoka kwenye taasisi wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika, Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakisikiliza maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Urio akielezea jambo wakati wa kikao kilichowakutanisha kujadili maeneo ya ushirikiano yanayoitaji utekelezaji wa pamoja.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akiwasilisha taarifa ya malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo kwa mwaka 2019 – 2020.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akipitia taarifa ya malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi ya OSHA kwa mwaka 2019 – 2020, wakati wa kikao kilichowakutanisha kujadili na kukubaliana maeneo ya ushirikiano.
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Bezil Ewala akiwasilisha taarifa ya malengo mkakati na kazi zilizopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo kwa mwaka 2019 – 2020, wakati wa kikao hicho.PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO
OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………

NA MWANDISHI WETU

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe amekutana na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa lengo la kujadili kwa kina maeneo watakayo shirikiana kwa pamoja katika mpango kazi wa mwaka 2019 – 2020 na kutoa maelekezo juu ya namna bora ya kuhudumia wananchi kulingana na huduma zinazotolewa na taasisi hizo.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma, alisema kuwa Mwaka wa fedha 2019/2020 ni muhimu kukubaliana kwa pamoja maeneo ambayo yatatekelezwa kwa ushirikiano ili kuimarisha utendaji wa shughuli mbalimbali.

“Lengo kuu la kukutana kwetu hapa ni kuangalia utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwenye mpango kazi wa kila Taasisi katika mwaka huu wa fedha, na kubaini namna bora ya kutekeleza maeneo hayo kwa ufanisi,” alisema Massawe.

Katibu Mkuu aliongeza kuwa kupanga na kukubaliana maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa mpango kazi kutasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kazi na majukumu ya kila siku.“Ninapenda kuona tunakuwa mfano wa kuingwa kwa kujijengea mwenendo mzuri wa kushirikiana katika utendaji ili kufanikisha shughuli nyingi kwa wakati mmoja,” alisisitiza Massawe

Aidha, alitoa wito kwa wakuu hao kuzingatia suala la mawasiliano na uhusianao kwa wadau na wateja wanaowahudumia ikiwemo kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa kwa wakati.

Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda alieleza kuwa ushirikiano na taasisi nyingine na wizara ni fursa pekee itakayo wawezesha kutekeleza dhamira na mikakati waliyopanga ili kuleta maendeleo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema kuwa yapo maeneo mengi ya kushirikiana kwa pamoja na mpango kazi wa mwaka ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio yatakayo wasaidia kuwa na ushirikiano endelevu katika maeneo mbalimbali.

Kikao hicho kiliudhuriwa na Wakurugenzi na Wataalamu wa Mipango na Bajeti kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

WAZIRI MKUU: WEZI WA NONDO TANI 5 WASAKWE MARA MOJA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah awasake na kuwatia mbaroni watu waliohusika na wizi wa tani tano za nondo na kisha wakatoroka.

Alitoa agizo hilo jana jioni, (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na wafanyakazi na wananchi mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi, katika kata ya Ngangamfumuni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi za siku nne, alisema mradi huo ni maalum kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na Halmashauri.

“Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 9 za kuanzia mradi huu lakini inasikitisha kuona kwamba wanaMoshi mnahujumu kwa kuiba vifaa vya ujenzi. Ninazo taaarifa kuwa hapa zimeibiwa tani tano za nondo na zimeshakamatwa.”

“Ni aibu, ni aibu kwa wana-Moshi. Ninyi wenyewe mnauhujumu huu mradi. Manispaa iweke utaratibu wa ulinzi ili vifaa vingine visipotee zaidi. Mkuu wa Wilaya chukua hatua ya kuwafuatilia wote waliohusika,” alisema.

Kupitia maswali aliyouliza, Waziri Mkuu alibaini kuwa walinzi wawili waliokuwepo siku ya tukio walitoroka ndipo akaamua kumwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa, awasake na kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ujenzi wa stendi hiyo kubwa unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China akishirikiana na wakandarasi wasaidizi watano na unatarajiwa kukamilika Januari 2021. Hadi kukamilika, ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 28.8.

Ikikamilika, stendi hiyo ambayo itakuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka. Kati ya hayo, mabasi 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kukamatwa kwa watu watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na wizi wa tani tano za nondo katika eneo la ujenzi wa stendi hiyo lililopo Ngangamfumuni.

“Hawa watu tumewakamata jana jioni, na kati ya walinzi waliotoroka, tumemkamata mmoja wao tayari akiwemo mkazi wa Rau, Daudi Audifasi mwenye miaka 48 ambaye anadaiwa kutoboa ukuta wa uzio kwa chini, na kukutwa na nondo nyumbani kwake ambako ni mita 10 kutoka eneo la tukio.”

Amesema tukio hilo, lilitokea Julai 6, mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi ambapo walinzi wa eneo hilo ambao ni Maxshield company walitoroka baada ya tukio hilo. Kamanda Issah alithibitisha kwamba nondo hizo zimekamatwa na ziko polisi.

DULLA MAKABILA ASHUSHA UJUMBE MZITO KWA WASANII WA SINGELI,

$
0
0
Na.Khadija Seif, Michuzi tv

AMBER rutty na Mumewe wote peponi,Salam akikuchukia huvuki boda, ni miongoni mwa vionjo vinavyopatikana kwenye wimbo mpya wa Mkali wa Muziki wa Singeli nchini Abdallah Omari a.k.a Dulla Makabila unaoitwa "Waongo" akitoa ujumbe kwa Mashabiki kuwa kuna stori zingine ni uongo tu waache imani potofu.

Makabila ni Msanii ambae amekuwa akifanya vyema kwa upande wa Muziki huo kwa sasa nchini.Pia ameweka wazi sababu zinazomfanya Muziki wake usishuke kiwango kwa Mashabiki zake na uendelee kuishi.

Makabila amesema zipo sababu nyingi ila kuwa kwake nadhifu hasa kwenye swala la Mavazi kumeendelea kumpatia maadili mengi likiwemo la mmoja wa wasanii waliochaguliwa kutumbuiza kwenye Tamasha la Wasafi Muleba mwaka huu linalotarajiwa kufanyika julai 19 mwaka huu.

"Wasanii wengi wa Singeli hawajipendi,wachafu wanavaa Mavazi ya kihunihuni ndio sababu hata wadau ,taasisi na waandaaji wa Matamasha imekua ngumu kuwaita wafanye kazi nao ,"

Pia ameeleza kuwa kwa sasa yeye ndio Mkali na mfalme wa Muziki wa Singeli kutokana na utofauti wake na Muziki wake na waimbaji wengine wa Singeli.

"Asilimia kubwa wanaimba mashairi ya matusi ambayo my hawezi kusikiliza Muziki ambao ujumbe wake sio mzuri na hauna maana ila Mimi nimebobea kwenye kuburudisha na kuelimisha kama wimbo wangu mpya unaoitwa "Waongo" ambao nimejaribu kufafanua zaidi kuhusu watu wenye imani potofu kuhusu vitu mbalimbali kuwa waache imani hizo,"

Pia ametoa shukrani kwa Msanii wa Muziki wa kufokafoka (HIP HOP) country boy kutokana na kushirikiana nae bega kwa bega katika kuboresha kazi zake za kisanaa hasa upande wa Mavazi

Matukio Katika Picha Ziara ya Naibu Waziri Subira Mgalu Ukaguzi Miradi ya REA Mkoani Kigoma

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akionyesha kifaa maalum cha kuunganishia umeme kwenye nyumba ambazo hazijawekewa mfumo wa kusambazia umeme kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo mkoa wa Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme kwenye moja ya saluni ya mteja aliyeunganishiwa umeme katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijiji vya wilaya za Kibondo, Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Loyce Burra Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (wapili kulia) akisikiliza maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Loyce Burra (kuulia) mara baada ya kuwasha umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Nyange na Saluni ya mkazi wa kijiji hicho wakati ziara yake ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini mkoani Kigoma inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mabamba,Mektrida Ngugwa. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akisikiliza maelezo ya Mkandarasi wa Usambazaji Umeme katika vijiji vya Wilaya za Kasulu, Buhigwe na Uvinza Kampuni ya CCCE – ETERN wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vijiji vilivyopo katika Mpango wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza (REA III) mkoani Kigoma hivi karibuni. Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa, Mtabira 825 KJ kilichopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Meja Peter Lyanga akizungumza walipotembelewa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu kwa lengo la kujionea maendeleo ya usambazaji umeme katika Kikosi hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kibondo vijiji 40, Kakonko vijiji 29, Buhigwe 21, Kasulu 12 Uvinza 10 na Kigoma vijijini 17. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na vijana wa program ya hiari wa Jeshi la Kujenga Taifa alipotembelea Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa, Mtabira 825 KJ kilichopo Kasulu mkoani Kigoma kwa lengo la kujionea maendeleo ya usambazaji umeme katika Kikosi hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Shunga na Lugoma wilayani Kasulu wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akifurahia jambo mara baada ya kuzindua zoezi la kuwasha umeme katika baadhi ya nyumba za wananchi wa mtaa wa Ruhita wilayani Kasulu wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji umeme vijijini mkoani Kigoma hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Wapili kutoka kulia ni Meneja Mradi wa Usambazaji Umeme Vijini Mkoa wa Kigoma toka REA. Mhandisi, Oscar Benedict Migani. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme akiwasha umeme katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mardi wa usambazaji umeme vijijini mkoani humo hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akiwasha umeme akiwasha umeme katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mardi wa usambazaji umeme vijijini mkoani humo hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo Mbunge wa Jimbo la Manyovu -Buhigwe mkoani Kigoma, Mhe. Albert Obama akimshukuru Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (katikati) kwa niaba ya Serikali kutokana na hatua za kusambaza umeme katika vijiji vya wilaya ya Buhigwe wakati wa ziara ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayauma. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akimkabidhi kifaa maalum cha kuunganishia umeme kwenye nyumba ambazo hazijawekewa mfumo wa kusambazia umeme kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA), mkazi wa Kijiji cha Nyankoroko wilayani Buhigwe, Bibi. Melenia Kutegwa wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji hicho hivi karibuni. Naibu Waziri Mgalu alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambapo jumla ya vijiji 129 vinasambaziwa umeme mkoani humo. Kifaa hicho kinatolewa bure kwa watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza, wajane ili waweze kumudu gharama za kuunganisha umeme katika makazi yao. Sehemu ya mtandao wa usambazaji nyaya za umeme kama zinavyoonekana katika Mtaa wa Ruhita uliopo katika Halmashauri ya Mji wa kasulu mkoani Kigoma. Moja ya nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Ruhita, Kasulu mkoani Kigoma ikiwa imeunganishiwa umeme kupitia Mradi wa Usambazaji Umeme Vijini Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza ambapo jumla ya vijiji 129 vinaunganishiwa umeme kupitia mpango huo.

CMSA yafungua Shindano la Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzai wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezindua Shindano la Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzi wa Vikuu pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama amesema Shindano hilo ni kuwajengea uwezo wa Wanafunzi wa elimu ya juu kuwajengea uwezo katika Masoko ya Mitaji ikiwa ni pamoja kufanya sekta hiyo kutambulika na watanzania.

Amesema uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka wa miaka mitano 2018/2019 hadi 2020/ 2023 ikwa ni dhamira ya serikali kuendeleza sekta ya Masoko na Mitaji kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.

Mkama amesema mkakati mwingine ni kuongeza uelewa na ushiriki katika Masoko ya Mitaji kwa lengo la kupanua wigo kwa wsshiriki hao kujenga uwezo wa watendaji katika sekta hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema mamlaka inatekeleza mikakati kwa njia mbalimbali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa Umma na kwa makundi mengine akiwemo Shindano kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.

Wawekezaji na wsshiriki wa Shindano katika Masoko ya Mitaji wanahitaji kupata uelewa wa kutosha kuhusu Masoko ya Mitaji na namna ya kushiriki hatua umuhimu ya kuwawezesha kulinda masilahi yao na kufanya uwekezaji huo kuwa endelevu.

Amesema elimu ya Masoko ya Mitaji inawezesha pia kundi la Wanafunzi kuepuka kushiriki fursa za uwekezaji za kitapeli na udanganyifu ambapo siku za usoni kumekuwa na wimbi kwa vijana kulagaiwa na kushiriki.

Mkama amesema tangu waaze mashindano kumekuwa na mwitikio kwa wanafunzi wa Vyuo kushiriki.Amesema 2015/2016 washiriki walitaka 2000 lakini walipata washiriki 7,500 na 2016/2017 lengo ilikuwa 7000 wakapata washiriki 7,901,2017/2018 lengo lake ilikuwa 10,000 wakapata 15,004 na mwaka huu ni kupata washiriki 16,000.

Amesema washindi watapelekwa katika nchi mbalimbali katika kujifunza namna wanavyoendesha sekta hiyo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akizungumza wakati uzinduzi wa Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu   pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu nchini lilofanyika katika mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu lilofanyika katika mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Adela Niko akizungumza namna alivyojipanga katika kushiriki Shindano la Masoko ya Mitaji
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Dustan Komba akitoa matarajio yake katika Shindano la Masoko ya Mitaji

Naibu Waziri Aweso Aahidi Kumaliza Changamoto ya Maji Kondoa, Atoa Maelekezo kwa TAKUKURU

$
0
0

Na Charles James,Michuzi TV

Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema Wizara yake itashirikiana na TAKUKURU ili kujiridhisha katika utekelezaji mradi wa Maji katika kijiji cha Masange Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Aweso ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo alipofanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa Maji kijiji cha Masange uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni 433 baada ya kupewa majibu yasiyojitosheleza na Mkandarasi wa Mradi huo.

“Haiwezekani tukauziwa mbuzi kwenye gunia,lazima kukagua na kujionea,baada ya kupewa majibu ya kusuasua hivyo TAKUKURU tutashirikiana nao kubaini ubadhilifu,na mkandarasi asilipwe mpaka tufanye uchunguzi tujiridhishe''amesema Aweso

Hali hiyo imekuja baada ya Mkandarasi wa mradi huo wa Maji kampuni ya Best One kwa kushirikiana na wataalam wa sekta ya Maji wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kutoa majibu yasiyoridhisha kuhusu matumizi ya fedha zilizotumika katika mradi huo .

Akijibu kero ya wananchi hao kuhusu Maji Mhe Aweso amepiga simu mbele ya wananchi kwa wataalamu wa Wizara kuulizia taratibu za upatikanaji wa Gari la kuchimba visima katika kijiji hicho ambapo ameahidi kuchimbwa visima viwili kwenye Kijiji hicho ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Katika kujiridhisha na mradi huo Mhe Aweso alilazimika kupanda kwenye mlima ambao chanzo cha maji kinapatikana ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto Na kuahidi kuzimaliza ili wananchi wa Masange waweze kupata maji na kwenda sawa na kauli mbiu ya kumtua mama ndoo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji amesema yupo tayari kufanya kazi hata saa sita usiku na walichomwagiza wananchi wake ni kutatua kero ya Maji .

Dkt.Kijaji amesema kuwa wananchi wa Mtaa wa Masange wamesema adha kubwa inayowakabili ni maji hivyo ni vyema serikali ikafanya mchakato haraka kutatua kero hiyo.

Awali ,akisoma taarifa ya Mradi wa Maji wa Masange mbele ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso,Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji vijijini[RUWASA]Wilaya ya Kondoa Mhandisi Falaura Seleman Kikusa amesema mradi wa Maji Masange ulianza tangu tarehe 15,Disemba,2014 na kuzinduliwa rasmi tarehe 13,Septemba ,2016 kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru huku ukigharimu zaidi ya Tsh.Milioni 433 .

Aidha amebainisha kuwa muda wa utekelezaji wa Mradi huo kwa mujibu wa Mkataba ni kipindi cha miezi mine kuanzia tarehe 15,Disemba,2014,hadi 15,Machi,2015 hivyo kutokana na changamoto mbalimbali hususan kuchelewa kwa malipo ya madai ya mkandarasi,mradi uliongezewa muda wa utekelezaji na kukamilika rasmi mnamo tarehe 7,Juni,2018.

Mhandisi Kikusa ameendelea kufafanua kuwa upatikanaji wa Maji katika kijiji cha Masange haukidhi mahitaji halisi ya maji kwa wakazi wa kijiji hicho kwani huduma ya maji imekuwa ikipatikana kwa mgao kwa vitongoji kwa masaa manne hadi matano.

Amesema chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo unatokana na changamoto kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa wakazi pamoja na kukua kwa mji wa Masange ,Uwezo wa chanzo cha Maji [lita 119,577.6 kwa siku]kuwa mdogo ikilinganisha na mahitaji halisi ya Maji ya sasa [zaidi ya lita 141,560 kwa siku] na changamoto nyingine ni usimamizi usio mzuri kutoka kwa timu ya mhandisi.

Hata hivyo mkandarasi wa mradi hadi kufikia sasa alishalipwa kiasi cha sh.347,421,000 kati ya gharama 433,288,548 na zilizobaki kwa mujibu ya makubaliano ya mkataba ni Tsh.120,609,648.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Juma Aweso akiwa ameambatana na Wananchi wa Kijiji cha Masange wilayani Kondoa wakati akipandisha Mlima Masange ambao ndipo lilipo Tanki na Chanzo cha Maji kijijini hapo
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masange ilayani Kondoa alipofika kuzungumza nao na kutatua kero ya maji iliyokua ikiwakabili. 
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Ashantu Kijaji akieleza changamoto ya maji inayowakabili wananchi wake wa eneo la Masange, Kondoa mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akipanda juu ya Tanki la Maji ambalo linatumika kugawa maji kwa Wanaanchi wa Kijiji cha Masange wilayani Kondoa.

SERIKALI KUANZA KUSAJILI HATI ZA ARDHI NDANI YA MKOA HUSIKA

$
0
0

Na Charles James, Michuzi TV,Dodoma

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amesema serikali itaanza kusajili nyaraka na hati milki za ardhi ndani ya mkoa husika, badala ya utaratibu wa mwanzo wa kusajiliwa ndani ya kanda zilizokuwa zimetengwa lengo ni kupunguza ucheleweshaji wa usajili wa nyaraka hizo na kuepusha usumbufu wa wananchi.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akifungua, mkutano wa wataalamu wa sekta ya ardhi na wakurugenzi na makatibu tawala wa mikoa, wanaokutana jijini Dodoma, kutathmini malengo ya sekta hiyo, sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu hao namna bora ya ufanyaji kazi na namna ya kutatua changamoto zilizopo.

Amesema wamekusudia kuhamisha ofisi za kusajili nyaraka za ardhi kutoka katika kanda, na kuzirudisha ndani ya mikoa husika, ili kurahisisha zoezi hilo, na upatikanaji wa nyaraka hizo kwa wakati, na tayari wakuu wa mikoa wameridhia na kutoa majengo yatakayotumika kama ofisi za wizara za usajili ndani ya mikoa.

“Nataka hatimiliki zote zitolewe na kusajiliwa mikoani kwani watu wamekuwa wakipoteza muda na gharama nyingi za usafiriki kufuatilia hati hivyo hatuwatendei haki hawa wananchi wanyonge kwa kuwatwisha mzigo wa gharama”amesema Lukuvi.

Na katika kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata huduma stahiki, amepiga marufuku wakuu wa idara za ardhi kupokea tozo ambazo hazistahili, pamoja na utumiaji wa madalali ndani ya ofisi za umma.

Amesema kuwa wananchi hivi sasa wamekuwa wakipatashida kupata hatimiliki zao za maeneo kutokana ofisi nyingi kuwepo katika maeneo ya kanda pekee yake.Pia amesema yupo mbioni kuandaa kanzi data ya matapeli wa ardhi na kuiweka katika tuvuti ya wizara ya ardhi ili wananchi wawajue na kujiepusha nao ili wasitapeliwe ardhi zao na watu hao na hata muogopa mtu yeyote.

Waziri Lukuvi pia amesema kuwa haitakuwa na maana kwa serikali kama itaendelea kuwapa mzigo wa gharama wanachi wake wakati wa ufuatiliaji wa hati miliki za maeneo yao na ndio maana wakaja na mpango huu.

“Tunataka kuwasaidia wananchi kupata hati miliki za maeneo yao huku gharama wanazozitumia ni nyingi leo hii unakuta mtu anatoka Kigoma anakuja Tabora, kufuata hati lakini tofauti na nauli anatumia siku saba hadi kumi kukamilisha zoezi hilo”, amesema

Mbali na hilo amewaonya watumishi wa idara za ardhi nchini kuacha tabia ya kupandisha bei ya maeneo pamoja na gharama za upimaji kwa madai kuwa wanajiongezea mapato ya ndani.Amesema bei ya viwanja lazima ziwe kwamujibu wa sheria zilizowekwa na siyo kila mtu kujipangia bei zake ambazo zinageuka kuwa kero kwa wananchi na kubaki kumilikiwa na wachache wenye uwezo wa kifedha.

Amemtaka katibu mkuu wa wizara hiyo Doroth Wanyika, kuhakikisha anapanga safu ya wakuu wa idara haraka watakao kwenda kufanya kazi katika ofisi za wilaya na ofisi za mipango miji na orodha hiyo ipite mikononi mwake kabla ya wahusika kupewa barua za uteuzi.

Vilevile amesema wataanza kutumia tehama katika kurasimisha ardhi na wameanza katika mkoa wa Dar es saalam na unafanya kazi kwa kasi sana na kuanzia mwakani zoezi hilo litakuwa la Tanzania nzima.

Amebainisha kuwa baada ya mkutano huo wataanza utaratibu wa kuwapisha kiapo cha maadili kwa watumishi wote kuanzia ngazi ya wizara hadi ngazi za chini ili kuhakikisha kila mtu katika kitengo chake anafanya kazi kwa uadilifu mkubwa kuleta mabadiliko chanya ndani ya wizara hiyo.

Katibu mkuu wa wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Doroth Mwanyika amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kufahamiana na kuleta mapinduzi katika sekta ya ardhi nchini.Amesema lengo jingine ni kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikisababisha kudolola kwa shughuli za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la kiwanja kimoja kumilikishwa kwa mtu zaidi ya mmoja.
 WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, 
Sehemu ya Makatibu Tawala, Wakurugenzi na Wataalamu wa Ardhi wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Mhe William Lukuvi katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma

CHUO CHA KODI CHAWAHIMIZA WANAFUNZI KUJIUNGA

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Chuo cha Kodi kimesema kuwa wahitimu wa kidato cha sita wajiunge na chuo hicho kwa  kuwa mazingira ya chuo hicho ni rafiki kwa kusomea pamoja na wigo wa kazi kwa kujiajiri kuwa mpana kutokana kuwepo kwa mahitaji katika masuala ya forodha na kodi ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Chuo hicho Oliver Njunwa amesema chuo kimejipanga vyema katika udahili wa mwaka wa masomo 2019/2020.

Amesema wanatoa kozi za forodha na kodi katika maeneo mbalimbali kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya taaluma hiyo kadri siku zinavyokwenda.

“Serikali pamoja na kampuni mbalimbali zinahitaji wataalam wa masuala ya forodha na kodi”.

Njunwa amesema katika maonesho ya vyuo vikuu wanafanya udahili moja kwa moja hivyo wanafunzi watumie fursa hiyo kutembelea na kutatua changamoto zao katika kufanya maombi ya udahili.

Aidha amesema idadi ya waombaji katika chuo hicho imezidi kuongezeka kutokana na wananchi kukifahamu Chuo cha Kodi pamoja na umuhimu wa taaluma ya kodi katika nchi yetu ambayo dira yake ya maendeleo ni kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.



Kwa mujibu wa Njunwa, maonyesho haya yamewafanya wananchi wengi  hususan wazazi na wanafunzi wengi wafahamu fursa zilizopo baada ya kuhitimu mafunzo ya forodha na kodi ambapo wanafunzi waliohitimu katika chuo hicho wanaweza kufanya kazi katika sekta mbalimbali huku wengine wakijiajiri.

Chuo kinahakikisha mwanafunzi anajengewa uelewa wa kitaaluma, uwezo wa kutenda kazi ili anapomaliza masomo aweze kufanya kazi kwa umahiri na weledi wa hali ya juu.

Pia tumejipanga  katika utoaji wa mafunzo yenye bora ili kuweza kukidhi mahitaji ya watalaam katika masuala ya kodi pamoja na forodha kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya watalaam katika sekta hiyo.

Chuo cha Kodi kimesajiliwa na Baraza la Vyuo vya Elimu ya Ufundi na kupatiwa Ithbati ya kudumu kutoa mafunzo yafuatayo ambayo ni Astashahada ya Forodha ya Afrika Mashariki -East Africa Clearing and Freight Forwarding Practicing Certificate (CFFPC),  Astashahada ya Forodha na Kodi- Techninican Basic Certificate in Customs and Tax Management (CCTM), Stashahada ya Forodha na Kodi - Diploma in Customs and Tax Management, Shahada ya Forodha na Kodi- Bachelor Degree in Customs and Tax Management- (BCTM).

Kozi nyingine ni:- Stashahada ya Uzamili ya Forodha na Kodi – Postgraduate Diploma in Tax, Shahada ya Uzamili ya Sheria na Usimamizi wa Kodi- Masters of Arts in Revenue Law and  Administration (MARLA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha dare salaam na Chuo Kikuu cha Muenster cha Ujerumani.

Tunawashauri wanafunzi waendelee kutuma maombi yao kabla muda wa udahili kumalizika.
 Afisa Udahili wa Chuo cha Kodi Paschal Gomba (kulia) akiwasaidia wanafanuzi kufanya udahili wanafunzi waliotembelea banda la chuo hicho katika maonesho ya 14 ya vyuo vikuu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Edwin Matemanga afisa udahili wa chuo cha kodi.
 Afisa Udahili wa Chuo cha Kodi Paschal Gomba akitoa maelezo kwa wanafanuzi waliotembelea banda la chuo hicho katika maonesho ya 14 ya vyuo vikuu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
Afisa Mkuu Mawasiliano Chuo cha Kodi, Oliver Njunwa akimfafanulia mzazi aliyetembelea maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Tanzania wahitajika kuwekeza katika afya na elimu ya vijana wake–Ripoti ya Benki ya Dunia

$
0
0
 Tanzania imetakiwa kuwekeza kwa haraka katika elimu na afya za watu wake hasa vijana kama itataka kuimarisha rasilimali watu kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kauli hiyo imo katika toleo jipya la jarida la Uchumi la Benki ya Dunia.
Imeelezwa kuwa katika miaka ya karibuni Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya binadamu ambapo imeweza kupunguza idadi ya vifo kwa watoto chini ya miaka mitano, kuongeza miaka ya wanafunzi kuwa shule kwa vijana wake na kuimarisha umri wa uhai kwa watu wazima.
Hata hivyo takwimu za urari wa uzalishaji wa binadamu yaani Human Capital Index (HCI) ya 0.40 inamaananisha kuwa watoto wanaozaliwa leo nchini Tanzania wanaweza kufikia asilimia 40 tu ya pato wanaloweza kulipata wakiwa na afya njema na elimu.
“Utajiri nchini Tanzania umeongezeka kwa asilimia 45 toka mwaka 1995 na haya ni mafanikio makubwa, lakini pia idadi ya watu imeendelea kuongezeka, na hivyo kupungua kwa pato halisi na hivyo kukosa uendelevu,” anasema  Bella Bird, Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Tanzania.
“Ili nchi iwe na ukuaji endelevu, inahitaji kuwekeza kwa watu wake, kwani raslimali watu ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile.” 
Benki ya Dunia ilizindua HCI Oktoba 2018, kama mradi mpya wa kushawishi mataifa kuwekeza zaidi kwa wananchi wake.
Urari huo unaangalia vipengele vitano vyenye kuonesha kipato cha baadae: uhai wa watoto baada ya miaka mitano; Wastani wa miaka inayokamilishwa na  vijana kujipatia elimu; Ubora wa elimu katika shule;ni kwa miaka mingapi watu watafanyakazi, kama kipimo cha uhai wa mtu mzima utapitiliza miaka 60 na kuzuia udumavu kwa vijana na watoto. 
“Kuna mambo mengi kwa Tanzania na mataifa mengine kujifunza kutoka katika nchi zilizofanikiwa katika urari huo ( HCI ) nchi za Singapore, Korea Kusini, Japan, na Hong Kong.
Mataifa haya mafanikio yake yameelezwa kutokana na kuwekeza zaidi katika vijana, wakizingatia zaidi elimu na maendeleo ya utaalamu katika ngazi zote za makuzi yao,” anasema Quentin Wodon, Mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia na Mwandishi mwenza wa  toleo la 12 la uchumi wa Tanzania.
Kwa kuangalia kiwango chake cha maendeleo, Tanzania haifanyi vyema miaka ya kijana kuwa shuleni na kuna hatari ya watoto chini ya miaka 5 kudumaa.
Ripoti zinaonesha pia  urari mbaya wa mapato kijinsia inakwamisha kuongeza ubora wa raslimali watu na hivyo pato la utajiri.
Ili kukabiliana na vikwazo vinavyozuia maendeleo ya raslimali watu, serikali imeshauriwa kuimarisha uwekezaji katika maeneo mengi kwa kutumia nguvu yake yote na kutoa huduma bora.
Pia mkazo umetakiwa kuwekwa kwa makundi yenye shaka hasa wasichana wanaokua na kwa kuangalia maeneo ambayo yapo nyuma.
Pia wametaka muda wa wanawake kufanyakazi wasizolipwa kama utunzaji wa familia upunguzwe, kwa kusambaza wajibu huo ili kuwawezesha kufanya kazi zaidi zinazowalipa.
Pia kuwapa nafasi zaidi wanawake kumiliki mali za kufanyia uzalishaji, kuangalia hali ya soko na mifumo ya kitaasisi inazuia fursa kwa wanawake.
Jarida hilo la sasa linaloelezea hali za uchumi pia limetoa maoteo ya hali ya uchumi kwa miaka michache ijayo. Kuangalia changamoto za mazingira ya nje ya biashara na uwekezaji kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku ikitambulika kwamba kwa Tanzania hali inakuwa bora zaidi.
Hata hivyo taarifa hiyo imesema ukuaji huo utategemea utekelezaji wa mabadiliko katika sera. 
Pia hatua za serikali kuboresha mazingira biashara na kifedha ikiwamo kupunguza tozo, kurejesha fedha kwa wananchi hasa za kodi na kuweka kipaumbele kwa miradi ya uwekezaji inayolenga kuleta maendeleo na yenye fedha tayari za kumalizia miradi kwa wakati uliopangwa.

 Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la jarida la Uchumi la Benki ya Dunia iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kuhusu maono ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati kufikia mwaka wa 2025 na inawekezana kuhakikisha kuwa maono yanafikiwa kwa kuboresha huduma zetu za afya na miundombinu wakati wa uzinduzi wa wa toleo jipya la 12 la jarida la uchumi wa Tanzania la Benki ya Dunia katika hafla iliyofanyika  kwenye Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia na Mwandishi mwenza wa toleo la 12 la uchumi wa Tanzania, Quentin Wodon akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa wa toleo jipya la 12 la jarida la uchumi wa Tanzania la Benki ya Dunia katika hafla iliyofanyika  kwenye Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa uzinduzi wa wa toleo jipya la 12 la jarida la uchumi wa Tanzania la Benki ya Dunia katika hafla iliyofanyika  kwenye Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. 
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. William Ole Nasha akizungumzia juhudi za serikali katika kuboresha elimu ya Tanzania wakati wa uzinduzi wa wa toleo jipya la 12 la jarida la uchumi wa Tanzania la Benki ya Dunia katika hafla iliyofanyika  kwenye Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wadau wa masuala ya uchumi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali nchini walioshiriki hafla ya uzinduzi wa wa toleo jipya la 12 la jarida la uchumi wa Tanzania la Benki ya Dunia iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.


LUKUVI ATANGAZA KUANZISHWA OFISI ZA ARDHI KILA MKOA

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema Wizara yake itaanzisha ofisi mpya za ardhi katika kila mikoa ili kuboresha utoaji huduma za ardhi nchini.

Lukuvi alisema hayo jana wakati akifungua Mkutano wa siku tatu wa Wataalamu wa Sekta ya Ardhi nchini unahudhuriwa pia na Makatibu Tawala wa mikoa pamoja na Wakurugenzi wa halmashauri unaoendelea katika jiji la Dodoma.

Alisema, kutokana na mabadiliko hayo sasa huduma zote za ardhi zilizokuwa zikitolewa katika ofisi za ardhi za kanda sasa zitatolewa mkoani na wananchi hawatahangaika tena kufuata hati au kusajili kiwanja katika ofisi za Kanda.

Kwa mujibu wa Lukuvi, katika kila mkoa kutakuwa na Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Mkoa sambamba na Mpima na Mthamini wa mkoa lengo likiwa kuondoa kero kwa wananchi waliokuwa wakipata shida ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za ardhi.

Pia Lukuvi alisema Wakuu wa Idara za Ardhi katika kila wilaya watapangwa upya kulingana na sifa na kufafanua kuwa suala Mkuu wa Idara kuwa na taaluma ya Afisa Nyuki au Misitu sasa halitakuwepo tena na wakuu hao watakuwa chini ya Wakurugenzi wa Halmashauri na kuhudhuria vikao vya menejimenti.

Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia alipiga marufuku Maafisa Ardhi kujishughulisha na kazi binafsi zinazoendana na kazi walizoajiriwa nazo na kubainisha kuwa kufanya hivyo ni kutumia muda wa serikali kwa kazi binafsi.

Vile vile, Lukuvi alibainisha kuwa Wizara yake itaanzisha Kanzidata ya matapeli wa ardhi na kuwataka wananachi wanaowafahamu matapeli wote wa ardhi kumtumia majina ili awafuatilie na kuweka majina yao hadharani.

Katika kile kinachooneka kusikia kilio cha wananchi kuhusiana na gharama kubwa ya uuzaji viwanja, Lukuvi alizitaka halmashauri kuwa na bei ekekezi ya viwanja pamoja na upimaji mashamba kwa kuwa sasa hivi kumekuwa na gharama kubwa inayowafanya wananchi wa hali ya chini kushindwa kumudu gharama.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alieleza kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi za Ardhi za Kanda lakini bado malengo ya kuwaondolea kero wananchi katika eneo hilo haijafikiwa.

Aliwataka Watendaji wa Sekta ya Ardhi nchini kuzingatia suala la huduma kwa mteja wakati wa utendaji kazi wao wa kila siku ili kuwaondolea kero wananchi wanaohitaji huduma za ardhi.

Aidha, aliwaonya washiriki wa mkutano huo ambao ni Maafisa Ardhi, Maafisa Mipango Miji na Wapima kuwa Uafisa Ardhi Mteule wa eneo lolote unaweza kukoma iwapo Afisa huyo hatatenda kazi yake vizuri ya kuwahudumia wananchi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Wataalamu wa Sekta ya Ardhi katika mkutano wa Wadau wa Sekta hiyo unaofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Center jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Wataalamu wa Sekta ya Ardhi katika mkutano wa Wadau wa Sekta hiyo unaofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Center jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wataalamu wa Sekta ya Ardhi unaofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma Convention Center jijini Dodoma.
 Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa wakiwa katika Mkutano wa Wataalamu wa Sekta ya Ardhi unaofanyika kaika ukumbi wa Dodoma Convention Center jijini Dodoma jana. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

BENKI YA DUNIA YAIJENGEA TANZANIA UWEZO WA TATHMINI BAADA YA MAAFA

$
0
0
Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia  Ofisi ya Waziri  Mkuu,  Idara ya Menejimenti ya Maafa, imeendesha mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo,  jijini Arusha leo tarhe 19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa na wataalam wa kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na maendeleo.

“Mafunzo haya yatatusaidia kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa  kuwa na mfumo  wa pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika  kuendesha shughuli ya Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu binafsi, Taifa na Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza kuwa na mpango wa pamoja wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.

Matamwe ameendelea kufafanua kuwa kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa kurejesha  hali, utaalamu huo utaisaidia nchi yetu Tanzania kuwa na Takwimu za  urejeshaji hali  ambazo tutapata uwezo wa kurejesha hali itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.

Akiongea katika mafunzo hayo  kwa niaba ya Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Mtaalamu wa Mawasiliano Benki ya Dunia Edward Anderson amefafanua kuwa  Benki hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na  wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa wakati baada ya maafa kutokea.

“Tangu mwaka 2016 nilipofika hapa nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea  ikiwemo tetemeko la ardhi mkoani Kagera, na mafuriko katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016, hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na Mpango bora katika kurejesha hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo tayari katika kutekeleza hayo” Amesema Edward.

Aidha, washiriki wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa kurejesha hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji, mbinu za kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji hali, kuainisha hasara na athari  zitokanazo na maafa  .

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia  tarehe  16 hadi 19 Julai, 2019,  liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa , kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na  Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo  kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa,  kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
 Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo  wa Utekelezaji wa Mipango ya  menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
 Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo  wa Utekelezaji wa Mipango ya  menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
 Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali  Jimmy Matamwe (Wa pili kulia), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Menejimenti ya Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania, Edward Anderson na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu, , wakati  wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji  wa Mpango wa  Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa  taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha.

 
Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa  Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.

DC KIGAMBONI AWATAKA WANANCHI KUTOYAKUMBATIA MATATIZO YA FAMILIA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole alipofika kutoa pole na kuzungumza na wananchi hao, na amewataka wananchi  kuwa makini na kuishi kwa tahadhari leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wa kata ya Gezaulole waliojitokeza katika kikao hicho, leo jijini Dar es Salaam.
 Nyumba iliyofanyika tukio la mauaji na kuchomwa moto kwa bi. Naomi Orest Marijani huko Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam.

*Awataka wananchi kuhoji matatizo ya ndugu na watu wao wa karibu na kutoruhusu kukumbatia matatizo.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TUKIO la kupotea kwa bi. Naomi Orest Marijani au Sandra (36) na baadaye kugundulika ameuawa, kuchomwa moto na kuzikwa na mume wake Khamis Ruwongo (38), wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole Wilaya ya Kigamboni wametakiwa kuchukua tukio hilo kama funzo na kuwa makini kwa kutoyakumbatia matatizo yao hasa ya kifamilia.

Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri ameeleza kusikitishwa na tukio la kupotea kwa Naomi na baadaye kugundulika ameuwawa na mume wake.

Sarah amesema kuwa haki itatendeka na kuonekana na kuwaasa wananchi hasa vijana kudhibiti  siasa zisizo na msingi na kuelekeza matukio hayo kwa wanaowaita watu wasiojulikana.

Pia amewashukuru sana ndugu wa Naomi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa zilizosaidia katika uchunguzi na kuwaomba viongozi wa dini kutumia majukwaa ya dini katika kuhimiza amani na upendo katika familia.

Amesema kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea na uchunguzi na tukio hilo ambalo si la kuigwa na si la kitanzania na wala sio tukio la kujifunza kabisa.

Amesema vyombo vya ulinzi vimelaani vikali tukio hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ipo makini na kila afanyaye tukio la namna hiyo kwa namna yoyote ile atafahamika na kueleza kuwa matukio yoyote ya kiharifu yanayosukwa kokote yatamulikwa kwa kuwa vyombo vya ulinzi vipo makini.

Aidha amesema kuwa Kama Kuna mitandao inayoshiriki katika kufanya hayo, ambapo amekemea vikali na kusema kuwa hayo yote yatafika mwisho na amewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika tukioh hilo na ya namna hiyo. 

Na amewashauri wanawake kutokumbatia matatizo ya kifamilia pamoja  na kutodharau mambo wanayosikia kwa majirani na watu wao wa karibu na tukio hilo liwe fundisho na kuishi kwa tahadhari.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kizani amesema kuwa msiba huo ni mkubwa na wanaishukuru serikali, Waziri wa mambo ya nje na mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano hadi tukio hilo likafikia kwenye hatua hiyo.

Vilevile Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando ametoa pole na kuelezwa kusikitishwa na tukio hilo la kusikitishwa na kusema kutumia wasaa huo kueleza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unakaribia na kuwashauri wanakijii kuchagua watu sahihi watakaoweza kuwatumikia wananchi.

Amesema kuwa tarehe 23 mwezi mtaa wa Kinzani utapitiwa na Mwenge wa uhuru kwa kufungua mradi wa maji na kuwataka wananchi wa Kinzani kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufurahia huduma ya maji kwa mitaa mitatu.

WAZIRI MKUU AWAFUNDA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
*Ataka wawe na mipango kazi, asema Serikali inapima matokeo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawe na mipango ya kazi ambayo itaweza kupimika na kutoa matokeo.

“Kila mtumishi anapaswa awe na mpango kazi katika sekta yake na ni lazima aende kupima matokeo. Awamu hii, tunataka kuona matokeo ya kazi zenu." 

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Julai 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Same kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, mjini Same. 

“Watumishi mmeletwa kwenye wilaya hii ili muwahudumie wananchi. Tulioajiriwa, kazi yetu kubwa ni kuwatumikia wananchi bila ubaguzi wowote uwe ni wa kabila, itikadi au rangi.” 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao kwamba baada ya mchujo wa watumishi hewa, waliobakia wanapaswa kufanya kazi kwa bidii. 

"Fanyeni kazi kwa bidii, msimamo wa Serikali hii ni kwamba hatumvumilii mtumishi ambaye si mwajibikaji, ni mwizi, mzembe au anaomba rushwa. Serikali hii hatuna muda wa kujadili matatizo ya watumishi, tunamalizana hapo hapo," amesema. 

Amewataka watumishi hao wasimamie utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo chama tawala. 

"Mtumishi angalia sekta yako inasema nini, ifanyie kazi. Kama ni maji, tafuta ni wapi yanapatikana, changanua zinahitajika shilingi ngapi, tafuta njia ya kupata hizo fedha ili wananchi wapate maji." 

Kuhusu tabia ya kukaa ofisini, Waziri Mkuu amekemea tabia hiyo na kuwataka watumishi wote nchini waache tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kuwasikiliza wananchi. 

"Watumishi wa umma msikae ofisini. Nendeni vijijini walau kwa siku nne za juma. Hizo mbili zinazobakia, zitumieni kuandaa taarifa. Nendeni huko ili wananchi wasipate usumbufu wa kuja hapa mjini kuwatafuta," amesisitiza. 

"Mkuu wa Wilaya simamia zoezi la wakuu wa idara na wasaidizi wao kwenda vijijini. Wakienda vijijini ni lazima waonane na waheshimiwa madiwani, washirikiane kusikiliza kero na kutafuta majibu kwa wananchi. Huo ndiyo mshikamano wenyewe unaohitajika," amesema. 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma watambue mipaka yao na wajenge mahusiano baina yao na wengine. 

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Moshi, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

"Kila mmoja lazima atambue mipaka yake na mamlaka baina yake na wengine. Hapa mko wateuliwa, waajiriwa na wachaguliwa. Kila mtu ana nafasi yake ya kuwatumikia wananchi.

Aliwataka watumishi hao watambue falsafa ya Kiongozi mkuu wa nchi ambayo inahimiza uchapakazi. “Kwa hiyo tunaposema Hapa Kazi Tu, maana yake chapa kazi na tuone matokeo. Tunasisitiza kazi na tunataka kazi unayoifanya, itoe matokeo,” alisema. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na Viongozi na Watumishi wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, katika ukumbi wa Halmashauri Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua darasa lililokarabatiwa la Shule Kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua maabara katika Shule Kongwe ya Same Sekondari, kabla ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia darasa lililokarabatiwa la Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia vitabu katika maktaba iliyokarabatiwa ya Shule Kongwe ya Same Sekondari, katika mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe mkoani Kilimanjaro, Julai 19.2019. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Same Sekondari Hoza Mgonja.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Same Sekondari mara baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa Same Sekondari, Omari Pundugu, akielezea changamoto mafanikio na changamoto za shule hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa shule hiyo kongwe, iliyoko wilayani Same katika mkoa wa Kilimanjaro, Julai 19.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi, baada ya kuzindua mradi wa ukarabati wa shule kongwe ya Same Sekondari, mkoani Kilimanjaro Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).   

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wahudumu wa ndege iliyomchukua baada ya kuteremka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam asubuhi leo Ijumaa Julai 19, 2019 akitokea jijini Dodoma. PICHA NA IKULU

CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU TCU NA KUFANYA UDAHILI PAOHAPO

$
0
0
Karani udahili  kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, Veronica Kazimoto(kulia) akimfanyia mmoja wa wanafunzi waliofika katika Banda la chuo hicho kudahiliwa katika maonesho hayo.
Mhadhiri msaidizi wa Idara ya ustawi wa jamii Peter Mgave akitoa maelekezo ya kozi mbalimbali kwenye Banda la chuo hicho katika maonesho ya vyuo vikuu Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.


Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images