Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KONGWA,MBANDE MKOANI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa nyama katika eneo la Mbande mkoani Dodoma mara baada ya kuzungumza nao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wa Mbande hawaonekani (pichani) katika Njiapanda ya Kongwa mara baada ya kusimama wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.
Wafanyabiashara pamoja na Wananchi wa Mbande mkoani Dodoma wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama na kuzungumza nao katika eneo hilo la Mbande.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza mziki kwenye gari wakati akiondoka eneo la Mbande mara baada ya kuwasalimia wananchi wa eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa nyama katika eneo la Mbande mkoani Dodoma mara baada ya kuzungumza nao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo Wamachinga katika eneo la Mbande mnadani wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.
Mfanyabiashara ndogondogo Lukas Chanzi akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza katika eneo hilo la mnadani Mbande mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo Wamachinga katika eneo la Mbande mnadani wakati akitokea Kongwa mkoani Dodoma.


MRADI KUUNGANISHA UMEME TANZANIA, KENYA KUTUMIA DOLA MILIONI 258.82

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

DOLA za Marekani milioni 258.82 zinatarajiwa kutumika katika mradi wa 
kuunganisha umeme kati ya nchi za Kenya na Tanzania ,ambapo mradi huo 
utahusisha ujenzi wa laini kubwa ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Singida kupitia Manyara na Arusha kwa upande wa Tanzania hadi Isinya kwa upande wa Kenya.

Akizungumza wakati wa makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi huo Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Arusha Herrin Mhina amesema mradi huo ni mkubwa na wa kimkakati wa Serikali na laini hiyo itakuwa na urefu wa kilometa 510.7.Kilometa 414.7ni kwa upande wa Tanzania yaani ya Singida na Namanga na kilometa 96 ni kwa upande wa kenya itakayo toka Namanga hadi Isinya.

Amesema kuwa ujenzi wa laini utahusisha pia upanuzi wa vituo vya kupooza 
umeme vya Dodoma na Singida pamoja ujenzi wa kituo kipya cha kupooza 
umeme chenye uwezo wa kilovolti 400 kinachojengwa Arusha katika kijiji cha Lemgur.

Aidha mradi huo utahusisha usambazaji wa umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji 22 vilivyopo kandokando ya mradi vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme wa msongo wa 33kV vikiwemo vijiji tisa vilivyopo ndani ya mkoa wa Arusha .

Mhina amesema malengo makuu ya mradi ni kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kwenye gridi ya taifa kufikia kiwango cha juu cha 2000MW .Pia mradi huo utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa bei nafuu kuelekea uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda.

"Pia mradi huu utawezesha nxhi moja kuweza kuuza umeme kwa nchi nyingine kwa bei nafuu pindi itakapotokea uhitaji hivyo kusaidia kukuza undugu na ushirikiano uliopo baina ya nchi ya kenya na Tanzania.

"mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo april 2020 ambapo gharama za mradi zimekadiriwa kuwa USD 258.82milioni kati ya hizo USD 214.93ni fedha za mkopo toka AfDB na JICA na USD 43.89 milioni zikiwa ni fedha kutoka ndani"amesema Mhina

Akizindua rasmi ujenzi wa mradi huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza Serikali ya kwa kuwaletea mradi huo kwani utachangia kuimarisha uwezo wa usambazaji wa umeme kwa wananchi na katika nchi zote mbili na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Pia zitasaidia kuondoa baadhi ya gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta mazito na gesi kwa kutumia umeme wa maji ambayo itasaidia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa.Amebainisha mradi huo umekuja na faida kwani umepita katika kijiji cha Lemgur na umewasaidia wananchi hao kupata umeme wa uhakika pia wananchi wa kijiji hicho watanufaika na barabara ambayo ni sehemu ya ujenzi wa kituo cha 
kupooza umeme.

Amwasihi wananchi kuacha nafasi ya kupitisha barabara na mitaro ili shughuli za maendeleo ziweze kuja kwa urahisi kwani kukiwa na barabara ni rahisi shughuli za maendeleo kufanyika kiurahisi .Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakandarasi hao kuwapatia vijana wa eneo hilo ajira kwani kuna 
vijana wengi wa eneo hilo wenye nguvu na weledi .

Kwa upande wake Mkandarasi wa mradi huo mkandarasi m/s Gopa kutoka 
International Enegy Consultant GmbH kutoka ujerumani amesema katika mradi huo changamoto inayowakabili ipo katika ujenzi wa barabara ambapo usanifu wa barabara ulilenga kuwa na barabara yenye viwango sawa na barabara za TARURA.

Ambazo zinaupana usiopungua mita 15 kutoka katika barabara hivyo kuwezesha kuwepo na mitaro ya maji ambayo sio muhimu tu kwakuilinda barabara balilakini pia kuzuia maji kufikakwenye makazi ya watu . 
 Mkandarasi wa mradi wa umeme wa Tanzania na Kenya akitoa maelezo Ya yajinsi mradi ulivyo,hapa alikuwa akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kuunganisha umeme kati ya kenya na nchi Tanzania
  Meneja wa shirika la umeme Tanzania mkoa wa Arusha  (Tanesco ) Herrin Mhina  Akitoa maelezo ya mradi mbele ya mgeni rasmi.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo  akibadilishana mawazo na mkandarasi wa mradi wa kuunganisha umeme kenya na Tanzania  mkandarasi m/s Gopa kutoka International Enegy Consultant GmbH kutoka ujerumani. 
  mkuu wa wilaya ya ArushaGabriel Daqarro akiongea katika uzinduzi huo 
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro akiongea katika uzinduzi huo wa mradi wa kuunganisha umeme kenya na Tanzania

KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAPAMBA MOTO, MAHAKAMA YAUKATAA MKATABA WA MAUZIANO YA KIWANJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MKATABA wa mauziano ya Kiwanja, uliotolewa na upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake umeshindikana kupokelewa mahakamani kwa kuwa haujakidhi matakwa ya kisheria.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 18, mwaka 2019 imekataa kupokea mkataba huo, usitumike kama kilelezo katika kesi hiyo kwa sababu haujakidhi matakwa ya sheria ya ushahidi.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba amesema upande wa utetezi umepinga mkataba huo usipokelewe mahakamani kama kielelezo 
kutokana na kukiuka sheria ya ushahidi kwani kwa mujibu wa sheria ya ushahidi, ili nyaraka ipokelewe mahakamani inatakiwa iwe halisi( Original) na sio nakala( copy).

"Kutokana na sababu hiyo, Mahakama hii inakataa kupokea nyaraka hiyo 
isitumike kama kielelezo katika kesi hii," amesema Hakimu Simba. Kesi hiyo 
imeahirishwa hadi Julai 31 mwaka huu itakapitajwa na Agosti Mosi na Agosti 6, itakapoendelea na kusikilizwa.

Kabla ya kukataliwa kwa kielelezo hicho, upande wa utetezi kupitia kwa Wakili , Semi Malimi, ulipinga nyaraka hiyo iliyotolewa na upande wa mashtaka, isipokelewe mahakamani hapo kwa sababu haikufuata sheria kwani nyaraka yoyote ambayo inatolewa mahakamani lazima iwe halisi na sio kopi.

Alidai kama inatolewa kopi basi yangekuwepo na mazingira fulani ya kutolewa kwa kopi na pia upande wa mashtaka hawajaeleza chochote kuhusu nyaraka halisi. Mpaka sasa mashahidi 20 wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa hao.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, makosa 19 kati ya hayo ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo 

alitenda kosa hilo kati ya Januari mwaka 2005 na Desemba mwaka 2015.
Inadaiwa mshitakiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya sh. bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa, huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, 
Leonard Aloys na Yasin Katera.

Rais Magufuli aagiza Wizara ya Sheria kupitia Magereza, aagiza kununuliwa ndege3 mpya na aagiza Askari Polisi warejeshwe kazini

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinavyohusika na masuala ya Mahakama kupita katika Magereza yote nchini ili kuchambua na kuwaondoa Mahabusu ambao hawastahili ama hawalazimiki kuwa Magerezani.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa Kongwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini hapo muda mfupi baada kutembelea eneo la maziko ya ukoo wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai (ambaye ni Mbunge wa Kongwa) na kuweka shada la maua katika kaburi la Baba yake Mzazi, Marehemu Yustino Ndugai.


Mhe. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku 2 tangu atembelee Gereza Kuu la Butimba Mkoani Mwanza na kujionea hali halisi ambapo amekuta Gereza hilo lenye uwezo wa kuchukua wafungwa na mahabusu 900 lina jumla ya wafungwa na mahabusu 1,925 wakiwemo mahabusu wenye makosa madogo yanayoweza kupata dhamana.


Amempongeza Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bw. Biswalo Mganga kwa kuchukua hatua mara moja ambapo ndani ya siku 2 amepitia Magereza ya Butimba, Bariadi, Mugumu, Tarime, Bunda na Kahama na kuwaachia Mahabusu zaidi ya 325 wakiwemo Askari Polisi waliokamatwa kwa kuhusika na utoroshaji wa dhahabu Mkoani Mwanza, na ameagiza Askari hao warejeshwe kazini.


“Siwezi kutawala nchi ya machozi, machozi haya yataniumiza, siwezi kutawala nchi ya watu wanaosikitika wapo kwenye unyonge na unyonge wao ni wa kuonewa”amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.


Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Kongwa kwa kuchapa kazi na kushirikiana vizuri na Mbunge wao katika maendeleo, na amemuelezea Mhe. Ndugai kuwa ni kiongozi mwenye mchango mkubwa kwa Taifa kutokana na kuliongoza Bunge kupitisha bajeti na Sheria mbalimbali zilizoiwezesha Serikali kutetea rasimali za Taifa, kuongeza ukusanyaji wa mapato na kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa na yenye manufaa kwa Watanzania wote.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Railway – SGR), kujenga mradi wa uzalishaji wa megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji, miradi ya maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa hospitali na vituo vya afya, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo, kutoa shilingi Bilioni 473 za mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi Bilioni 31 (2015/16) hadi shilingi Bilioni 270 hivi sasa.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema kutokana na mafanikio ya kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi Bilioni 850 (2015/16) hadi kufikia shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300 kwa mwezi hivi sasa, Serikali imeweza kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya 8 zikiwemo 6 zilizowasili nchini na kuanza kutoa huduma ndani na nje ya nchi, na kwamba tayari ameshatoa maelekezo ya kununuliwa kwa ndege zingine 3 (Airbus 2 na Bombardier 1) ili kupanua huduma za usafiri wa anga na kukuza utalii.

Ametoa wito kwa wananchi wa Kongwa kuendelea kuchapa kazi na kudumisha amani, na amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Manyara kwa kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji iliyokuwa ikisababisha mauaji.


Akizungumza katika Mkutano huo, Mhe. Ndugai amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa hatua yake ya kuhamishia Serikali katika Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma pamoja na kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Uwanja wa Ndege Msalato, barabara za lami za Jiji la Dodoma kilometa 110, kutoa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya mradi wa maji wa Kongwa, kujenga Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, vituo vya afya vya Ugogoni na Mlali na kujenga chuo cha ufundi.


Mhe. Ndugai amemuomba Mhe. Rais Magufuli kusaidia kujenga barabara ya lami ya Mbande – Kongwa- Mpwapwa hadi kuungana na Barabara Kuu ya Iringa – Dodoma, na kwa ombi lake la kusaidiwa ujenzi wa Shule ya Msingi Sagala iliyoezuliwa na Upepo, Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na ameendesha harambee iliyofanikisha kupatikana shilingi Milioni 6.5, mifuko 528 ya saruji na mabati 252.


Kuhusu maombi ya kupelekewa Kikosi cha Jeshi katika Wilaya ya Kongwa ambayo ina historia ya kuwa na kambi ya wapigania uhuru wa nchi nyingi za Afrika, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi hayo. 


Akiwa njiani kutoka Kongwa kwenda Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amesimama kuwasalimu wananchi wa Mbande Mnadani na Mbande Njiapanda ambao wamemshukuru kwa kupatiwa vitambulisho vya wajasiriamali vinavyowawezesha kufanya biashara bila bughudha, na amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge kumega eneo lililo chini ya Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) kando ya Mbande Njiapanda kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Mabasi, Kituo cha Polisi na Kituo kidogo cha afya, na kuhakikisha eneo la Mbande Mnadani linapatiwa maji na vyoo. Pia amechangia shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Polisi.

 

 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

18 Julai, 2019

MAHAKAMA YAAGIZA RAIA WA URUS ANAYETUHUMIWA KUINGILIA MAWASILIANO ,KUITIA NCHI HASARA ADAKWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imetoa amri ya 
kukamatwa raia mmoja wa Russia Vadim Burin ili afikishwe mahakamani hapo kujibu mashtaka nane yanayomkabili yakiwemo ya kuingilia mawasiliano ya kielectroniki na kuisababishia Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA hasara ya milioni 41.

Mshtakiwa Burin ambae pia ni mfanyabiashara anayeishi Morovania nchini humo anashtakiwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na Mtanzania, Msafiri Msayi aliyesomewa mashtaka yake pasipokuwepo na mshtakiwa namba moja (Burin) mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Salum Ally baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Monica Mbogo kuiomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo na mahakama ikaridhia.

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya Msayi, Wakili wa Serikali Batilda Mushi 
akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Burin na Msayi wanatuhumiwa kwa mashtaka nane,waliyoyatenda kati ya Mei, 15 hadi Juni 10 mwaka huu.

katika shtaka la kwanza, inadaiwa katika siku na tarehe zisizofahamika jijini Darces Salaam, washtakiwa walikula njama ya kutumia mtandao wa njia ya udanganyifu.Washtakiwa wandaiwa Mei 15, mwaka huu wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere waliingiza vifaa vya kieletroniki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo ni,one voice over internet protocol (VOIP) na Gateway model GOIP-8 yenye kumbukumbu namba GOIP8MCDRM17033127.

Pia MAC ADR383F10048B10, 383F10048B11,8channel, one VOIP Gateway S/N 8M2ARMV51800553, MAC adress 383F105CBD6, 383F1005CBD7, Eight 
channel, one VOIP Gateway S/N SMB32T18110540, MAC address 
383F1005108,388F1005DE09 bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa bila uhalali wowote walisimika mifumo ya kieletroniki bila kuwa na leseni ya TCRA. Katika shtaka la nne, imedaiwa, kati ya Mei 15 na Juni 10,mwaka huko Sea Cliff, Masaki, Wilaya Kinondoni, washtakiwa walitumia vifaa vya mawasiliano vya kieletroniki ambavyo waliviunganisha kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano bila kuwa na kibali cha TCRA. 

Katika shtaka la tano, washtakiwa wandaiwa siku na mahali hapo, waliendesha mtambo wa mawasiliano kwa lengo la kupokea na kutoa mawasiliano ya kimataifa bila kuwa na leseni.

Aidha kwa lengo la kukwepa kodi, washtakiwa wanadaiwa kukwepa malipo 
ambayo yanatolewa katika huduma ya kutoa mawasiliano ya kimataifa ambapo bila kujali walisambaza mawasiliano hayo kwa kuunganisha mawasiliano ya kimataifa huku pia washtakiwa hao wanadaiwa kutumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa, ambapo za halotel zilikuwa 173 na Vodacom zilikuwa 37. 

Katika shtaka la mwisho, washtakiwa wanatuhumiwa kuisababishia Serikali na TCRA hasara ya Sh.milioni 41.7. Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya 

kusikiliza shauri hilo na kesi imeahirishwa hadi Agosti Mosi, mwaka huu.

WATUMIAJI WA ZIWA VIKTORIA KUNUFAIKA NA UBORESHAJI WA UTOAJI WA TAHADHARI ZA HALI MBAYA YA HEWA

$
0
0
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa mpango maalumu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Victoria.

Mpango huo umebainishwa leo Julai 18, 2019 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘HIGH impact Weather lAke sYstem (HIGHWAY)’ uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Darves Salaam.

‘Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kuongeza ufanisi wa uandaaji na usambazaji kwa wakati wa taarifa za hali ya hewa hususani taarifa za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Victoria" amebainisha Dkt. Chang’a.

Ameongeza kuwa, wadau wa mradi huu wakiwemo wataalam kutoka TMA watakaa kwa pamoja na kufanyia maboresho taarifa zinazotolewa na Mamlaka na hivyo kufanikisha utoaji wa huduma bora zaidi zitakazoweza kusaidia serikali katika jitihada za kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinachangia katika kufanikisha mikakati na jitihada za nchi kufikia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda , ‘

Mapema katika ufunguzi, huo Rita Roberts mtaalam wa mradi kutoka ‘National Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ alifafanua kuwa mradi huo utasaidia Kanda ya Afrika Mashariki kupitia taasisi zake za hali ya hewa kufanikisha utoaji endelevu wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati pamoja na kuongeza kiwango cha usahihi na uhakika kwa taarifa za hali ya hewa na hivyo kupunguza athari za vifo na upotevu wa mali.

Mradi huu unahusisha Taasisi za Hali ya Hewa za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na ‘National Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ kutoka Marekani, Taasis ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UKMet Office) kwa ufadhili wa ‘Department for International Development (DFID)’ ya Uingereza.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KUWEKA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UGOJWA WA KIFUA KIKUU (TB)

$
0
0

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwakaribisha Viongozi wa Dini kwa ajili ya Kongamano la kujadili namna Viongozi hao wanavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB)  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na  Ugojwa wa Kifua Kikuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mtadao huo Mhe. Oscar Mkasa.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Dini wakati wa Kongamano la kujadili namna Viongozi hao wanavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB)  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na  Ugojwa wa Kifua Kikuu,  Mhe. Oscar Mkasa akizungumza wakati wa Kongamano hilo lililowahusiha Viongozi wa Kidini ili  kujadili namna wanavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB).
 Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ugojwa wa Kifua Kikuu na Ukoma, Bw. Dues Kamara akiwasilisha mada  wakati wa Kongamano la kujadili namna Viongozi wa Kidini wanavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB)  katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
 Mwekahazina wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na  Ugojwa wa Kifua Kikuu,  Mhe. Kimirembe Lwota  akizungumza wakati wa Kongamano hilo lililowahusiha Viongozi wa Kidini ili  kujadili namna wanavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB).
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, (katikati ya waliokaa) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini, Wabunge  wa Mtandao kupambana na TB na wadau katika mapambano dhidi ya TB    wakati wa Kongamano la kujadili namna Viongozi wa Dini wanavyoweza kuwasaidia katika mapambano dhidi ya Ugojwa wa Kifua Kikuu (TB)  lilofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia waliokaa ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na  Ugojwa wa Kifua Kikuu,  Mhe. Oscar Mkasa, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Thaddeus Ruwa’ichi, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum na Makamu wa Rais wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kassala.PICHA NA BUNGE

China kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya afya

$
0
0

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 15.07.2019
BALOZI mdogo wa Jamhuri ya watu wa China Xie Xiuowu amesema nchi yake itaendeleza azma yake ya kuisaidia Zanzibar katika nyanja tofauti ikiwemosekta ya afya ikiwa ni juhudi zake za kukuza uhusiano miongoni mwa nchi hizo mbili.
Alisema misaada wanayoitoa inaongozwa na dhamira njema hasa kwa watu wenye mahitaji ili kuona nao wanaendelea kufurahia maisha yao ya kila siku.
Balozi Xie aliyasema hayo katika hafla ya kuwaaga madaktari wa China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha madaktari wapya ambao nao watahudumu katika sekta ya afya Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Alikumbusha kuwa Jamhuri ya Watu wa China ilianzisha utaratibu wa kuleta madaktari Zanzibar tokea mwaka 1964 na utaratibu huo unaendelezwa na kuimarishwa zaidi hadi sasa.
Alisema kwa sasa wanatekeleza mradi wa kupambana na kichocho, saratani ya shingo ya kizazi na kuwajengea uwezo watendaji katika sekta ya tofauti ili kuimarisha uhusiano kati ya Zanzibar na China.
Kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed alisema uhusiano wa China na Zanzibar unaendelea kuimarika siku hadi siku na kuiomba China ifikirie namna ya kuwafanya madaktari hao kutumia muda wa miaka miwili Zanzibar badala ya mmoja ili kutoa huduma zaidi.
Alisema kupitia uhusiano huo China imeweza kuimarisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo hospital ya Abdalla Mzee kisiwani Pemba.
Aidha aliongeza kuwa wataalam wanaokuja kutoka China husaidia pia huwaongezea ujuzi wananchi na madakri wa Zanzibar kupitia programu mbali mbali ikiwemo za televisheni na hospitalini.
Waziri Hamad aliwashukuru kupitia mradi wa kupambana na maradhi ya kichocho ambapo dola za Marekani Milioni 5 walizotoa zitasaidia kupambana na maradhi ya Kichocho Zanzibar.
Alisema pesa hizo pia zitatumika katika programu ya miaka mitano ya kupambana na maradhi ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi kwa wanawake wa Zanzibar.
“Kiujumla misaada wanayoitoa ndugu zetu hawa ni mingi sana na hawajawahi kutuwekea masharti yanayotubana, tunashirikiana nao vyema tofauti na misaada ya nchi nyingine”, alibainisha Waziri Hamad.
Aidha Hamad aliwasifia madaktari hao kwa nidhamu ya kazi ambayo inapaswa kuigwa na madaktari wazalendo ikiwemo ya kuwahi kazini mapema bila ya malalamiko yoyote.
“Hili la nidhamu ya kazi kwa kweli sisi kama Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tunapaswa tuige. Wanawahi kazini na kuondoka kwa wakati na husikii wakipewa lawama na wananchi wanaowahudumia”, alisema Waziri Hamad.
Kuhusu timu ya madaktari wapya, Waziri Hamad alisema waliokuja ni wataalamu zaidi ambao pia watatumika kutoa elimu katika ngazi za vyuo vikuu vya Zanzibar.
Akitoa salamu za shukran kwa niaba ya wenzake Mkuu wa madakrari waliomaliza muda wao Dk.Zhang Zhen ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ukarimu wao waliouonesha katika kipindi chote cha kuhudumia wananchi Zanzibar.
Alisifia mazingira safi ya visiwa vya bahari ya Hindi ikiwemo Zanzibar ambavyo vitaendelea kubaki katika kumbukumbu zake.
Nae Kiongozi wa timu mpya ya madaktari hao Dk. Yang Xiaodong aliahidi kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na weledi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid akibadilishana mawazo na Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu wakati wa hafla ya kuwaaga Madaktari wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha madaktari wapya kuhudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu akitoa hotuba yake katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari kutoka China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha Madaktari wapya watakaohudumia wananchi kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid akitoa hotuba yake katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari kutoka China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha Madaktari wapya watakaohudumia wananchi kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa kutoka China waliomaliza muda wao wa kuhudumu katika sekta ya Afya Zanzibar akitoa neno la shukran katika hafla maalum ya kuagwa kwao na kukaribishwa kwa Madaktari wapya. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
Kiongozi wa Timu ya Madaktari wapya kutoka China Dkt.Yang Xiaodong akitoa nasaha zake katika hafla ya kuagwa na kukaribishwa kwa madaktari hao ambao watahudumu Zanzibar katikakipindi cha mwaka mmoja.
Baadhi ya Madaktari wa kutoka China waliohudhuria katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wanaomaliza muda wao na kukaribishwa kwa Madtari wapya watakaotoa huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji na Kichocho. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu msitari wa pili waliokaa na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kushoto kwake wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Madaktari wnaomaliza muda wao wa mwaka mmoja kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu katikati na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kushoto kwake, wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Madaktari wapya kutoka China ambao watakuwa wakifanya kazi ya kuhudumia wagonjwa kwa kipindi cha mwaka mmoja Zanzibar. Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 


WAGONJWA WA MOYO 26 WAFANYIWA UPASUAJI WA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI YA SIKU 14 KWENYE TAASISI YA JKCI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpata zawadi muuguzi wa chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutoka shirika la CardioStart International la nchini Marekani Anasi Griffin wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalamu kutoka shirika hilo ambao kwa kushirikiana na JKC wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la CardioStart International la nchini Marekani wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya siku 14 inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 26 wakiwemo watoto 13 na watu wazima 13 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Daktari wa chumba cha uangalizi maalum kwa watoto kutoka shirika la CardioStart International la nchini Marekani Barbara Ferdman akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wataalamu kutoka shirika hilo ambao kwa kushirikiana na JKC wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima.(PICHA NA JKCI)

NA MWANDISHI MAALUM

WAGONJWA 26 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya siku 14 inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Waliofanyiwa upasuaji ni watoto 13 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu, mishipa ya damu ya moyo na valvu kutofanya kazi vizuri na watu wazima 13 ambao wamefanyiwa upasuaji wa kubadilishwa valvu moja hadi tatu ambazo hazikuwa zinafanya kazi vizuri na kupandikizwa mishipa ya damu ya moyo (Coronary artery bypass grafting - CABG).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji Dkt. Anjela Muhozya alisema matibabu hayo yanafanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la CardioStart International la nchini Marekani.

Dkt. Anjela ambaye pia ni daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) alisema katika kambi hiyo walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 40 kati ya hao watoto 20 na watu wazima 20 , hadi sasa wameweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 26 ambao hali zao zinaendelea vizuri na wengine wamesharuhusiwa kutoka ICU na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuanza mazoezi pamoja na kuendelea na matibabu mengine. 

“Katika watoto tuliowafanyia upasuaji, mtoto mmoja alikuwa na tatizo kubwa la valvu zake tatu kutokufanya kazi vizuri, leo hii tunamfanyia upasuaji na kumwekea valvu nyingine tatu”. 

“Kuwepo kwa kambi hii kumesaidia kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa waliohitaji matibabu ya utaalamu wa hali ya juu kufanyiwa upasuaji wakiwa hapa nyumbani pia kubadilishana ujuzi wa kazi kati yetu na wenyeji kwani katika kambi hizi huwa tunajifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wageni ambao wanakuja kufanya kazi na sisi”, alisema Dkt. Anjela.

Kwa upande wake Kasilda Koka ambaye binti wake amefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo aliishukuru Serikali na wafanyakazi wa JKCI kwa kumpokea binti yake na kumfanyia upasuaji huku akitibiwa kwa kutumia bima ya afya.

“Mwaka 1999 wakati huduma za upasuaji wa moyo hazikuwepo hapa nchini nilimpeleka mwanangu ambaye alikuwa na tundu katika moyo kutibiwa nchini India ambako nilitumia gharama kubwa” . 

“Hivi sasa binti yangu alikuwa na shida ya valvu moja kutofanya kazi vizuri ameweza kufanyiwa upasuaji hapa nchini na kuwekewa valvu nyingine kama mnavyomuona anaendelea vizuri”, alisema Kasilda.

BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT 2019

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja wa Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB –Boma Labala (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 150 kwa ajili ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT – 2019 utakaofanyika jijini Mwamza, kwa mwenyekiti wa ALAT taifa Mheshimiwa Gulamhafeez Mukadam. Kushoto ni Maneja Mwandamizi waBiashara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB Suzana Shuma na kulia ni Mheshimiwa Zainab Vullu, Muwakilishi wa Wabunge ALAT.
Benki ya CRDB imekabidhi hundi ya mfano ya shilingi Milioni 150 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa 35 wa ALAT taifa unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 22 Julai hadi 24 jijini Mwanza.

 Fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 500 kati yao wakiwa mameya, kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 185, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 500.

 Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Goldcrest jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Boma Labala alisema kuwa Benki ya CRDB inathamini sana mchango wa Serikali za mitaa hususan halmashauri katika ustawi wa uchumi na maendeleo ya Taifa. 

“Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa ALAT katika kuchochea maendeleo ya taifa letu, pasi na shaka hiki ni chombo kinachounganisha pamoja mamlaka na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya Serikali za Mitaa hapa nchini ambapo ndio hasa wanamgusa Mtanzania katika ngazi ya chini. Hii ndio sababu kubwa iliyotufanya sisi kuwa tayari kushiriki mkutano huu, kwa kuamini kuwa mikakati na maazimio yanayofikiwa hapa leo yatakwenda kuongeza kasi maendeleo ya taifa letu na kuwagusa watanzania walio wengi”. 

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhefeez Mukadam alisema kuwa taasisi yao inathamini sana udhamini huo wa Benki ya CRDB kwani kwa kiasi kikubwa utachangia gharama za uendeshaji wa mkutano huo muhimu. Mheshimiwa Mukadam alisema kuwa Benki ya CRDB imekuwa mdau mkubwa wa Serikali za mitaa kwa kuendelea kutoa huduma za kifedha kwa halmashauri zaidi ya 60 nchini na mikopo kwa halmashauri hizo na wafanyakazi wake. “CRDB ni mdau wetu muhimu sana na tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono” alisema.

Maandalizi ya Maonesho ya Utalii Karibu Kusini Yashika Kasi

TAMASHA LA WASAFI KUZINDULIWA MULEBA KAGERA.

$
0
0

Na Abdulatif Yunus, Michuzi TV, Bukoba

Hatimaye Msanii nguli nchini Diamond Platinum akiambatana na Wasanii wenzake ambao wapo chini ya Kampuni (Lebal) ya WASAFI wawasili mkoani Kagera na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti tayari kwa uzinduzi wa Tamasha kubwa la (WASAFI FESTIVAL) Wilayani Muleba Julai 19, 2019.

Mara baada ya kuwasili ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa Gaguti  alimpongeza Diamond na uongozi wa WASAFI kwa kuamua Tamasha la Wasafi lianzie katika Mkoa wa Kagera pia kushirikiana na TACAIDS kuhakikisha wanawahamasisha vijana kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI, kutumia kinga pia kutumia dawa kwa wale ambao tayari wameambukizwa na VVU>

“Mkoa wa Kagera ni mkoa wa kimkakati ni rahisi sana kwenda Kigali, Kampala na Buumbura kutokea hapa Bukoba kuliko kwenda Singida hapa ni karibu sana na nchi jirani kwa hiyo kuleta WASAFI FESTIVAL pia nchi jirani zinanufaika kwa wapenda burudani kuja kuona wasanii wakubwa hapa kwetu Kagera” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wasanii hao kushiriki katika wiki ya uwekezaji Kagera ambayo inatarajia kuanza Agosti 12 hadi 17, 2019 na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Naye Msanii Diamond Platinum alimshukuru Mkuu wa Mkoa Gaguti kwa kukubali kuwapokea pia kuonesha ushirikiano katika mkoa wake wa Kagera. Diamond alisema kuwa yeye na wasanii wenzake ni vijana na wanajua ni namna gani ya kuongea na vijana wenzao kwa kuwahamasisha kujikinga na maambukizi mapya ya Virus vya UKIMWI na ndiyo maana wanashirikiana na TACAIDS kutoa elimu hiyo.

Said Fella Meneja wa Msanii Diamond alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa mapokezi lakini pia alisema kuwa kuleta Tamasha la Wasafi Mkoani Kagera ni fursa kwa vijana Bodaboda, mama lishe, wamiliki wa Hoteli na wafanyabiashara mbalimbali. “Sisi timu yetu tumekuja zaidi ya watu mia moja kwahiyo ni fursa hiyo.” Aliongeza Said Fella.

Msanii Diamond Plutnum amewasili mkoani Kagera Julai 18, 2019 na ameambatana na wasanii wenzake Rayvany, Malomboso, Queen Darlin, Rubi, Dulla Makabira, na wengineo na Tamasha la WASAFI linatarajiwa kuzinduliwa rasmi nchini Wilayani Muleba Ijumaa Julai 19, 2019

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KONGWA MKOANI DODOMA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Kongwa mara baada ya kuwasili wakati akitokea Chamwino mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa kidini wakati akiondoka katika eneo la Makaburi ya Ukoo wa Ndugai katika eneo hilo la Kongwa mara baada ya kuweka shada la maua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kongwa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili wakati akitokea Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anazungumza na Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa Job Yustino Ndugai wakati akitoka kuweka shada la maua katika kaburi la Baba mzazi wa Spika Mzee Yustino Ndugai katika eneo la Malalo ya ukoo wa Ndugai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika eneo la Makaburi ya Ukoo wa Ndugai mara baada ya sala fupi iliyofanyika katika eneo hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kongwa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili wakati akitokea Chamwino mkoani Dodoma.

Sehemu ya Wananchi wa Kongwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kongwa mkoani Dodoma mara baada ya kuwasili wakati akitokea Chamwino mkoani Dodoma.
Sehemu ya Wananchi wa Kongwa wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi  la Baba mzazi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai katika eneo la Makaburi ya Ukoo wa Ndugai yaliyopo Chimotolo Kongwa mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU



MAFIA YAJIPANGA KUINUA PATO NA UCHUMI KUPITIA ZAO LA KIBIASHARA LA NAZI NA MWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

WILAYA ya Mafia ,mkoani Pwani imejipanga kuinua uchumi wake kwa kutumia zao la kibiashara la nazi na Mwani ambayo kwa sasa yananunuliwa kwa bei ya chini na kuwakandamiza wakulima wa mazao hayo.

Aidha halmashauri ya wilaya hiyo, imetoa jumla ya sh.milion 68.758 ikiwa ni mkopo kwa vijana ,wanawake na walemavu kwa mwaka 2018/2019.

Mkuu wa wilaya ya Mafia,Shaibu Nnduma akizungumza na madiwani pamoja na baadhi ya viongozi wa ofisi ya mkoa wa Pwani alieleza, fedha hizo ni mikopo ambayo watarudisha bila riba.

"Fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri ambapo imegawiwa kwa vikundi 12 kutoka kila kata zilizopo katika halmashauri hiyo"alifafanua Nnduma.

Hata hivyo Nnduma alisema, Mafia ni wilaya inayozalisha nazi kwa kiwango kikubwa tani 35,000 kila mwaka na kulikuwa hakuna kiwanda ila maamuzi ya kuanzisha kiwanda cha kusindika mafuta kitasaidia.

"Nazi zinauzwa hadi sh.100-150 na wakati mwingine zinaokotwa tuu chini hivyo uanzishaji wa kiwanda utainua soko hilo"alisisitiza Nnduma.

Akielezea zao la mwani alibainisha, Jibondo na Chole soko lipo Zanzibar na Dar es salaam wanauza bei chini sh 300 kwa kilo ,wakulima wanalalamika hivyo ukiwekwa mfumo mzuri wa kuiuza utaongeza pato la wakulima hao.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Pwani ,(RAS)Theresia Mmbando aliipongeza halmashauri hiyo kwa kusimamia vyanzo vya mapato na kutenga asilimia zinazopaswa kusaidia wanawake,vijana na walemavu.

Theresia aliyataka makundi yanayopatiwa mkopo huo kuutumia vizuri kwa kuzalisha na sio kuingia tamaa ya kula hela ama kufanya matumizi mabaya ya fedha.

WAZIRI BASHUNGWA AZIVALIA NJUGA KERO ZA KARIAKOO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Michuzi TV 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa Leo amefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa kariakoo na kuhaidi kutatua kero sugu zinazozoletesha biashara katika soko Hilo.

Waziri Bashungwa amesema Wizara yake ipo tayari kushughulikia na kero hizo ikiwemo swala la tozo zisizo za lazima kwa wafanyabiashara na changamoto wanazokutana nazo kutoka kwa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na Bandari.

"Kwa hakika nimesikia kero zenu kwa hatua ya Kwanza nimezungumza na kamishna wa TRA ndugu yangu amekubali kufanya mkutano na nyie kesho saa nane pia katika mkutano huo atakuwepo kiongozi kutoka mamlaka ya Bandari nchini" Amesema Bashungwa.

Hata hivyo waziri Bashungwa aliwataka wafanyabiashara hao kulinda Viwanda vya ndani kwa kuuza bidhaa zinazopatikana hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutekeleza sera ya Viwanda inayosimamiwa na Rais Magufuli.

Waziri Bashungwa aliwashukuru wafanyabiashara hao kwa kunitokeza na kuzungumza mambo ambayo yanahitaji lengo la kujenga uchumi wetu kwa kufanya Kariakoo kuwa Hub ya Afrika Mashariki.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akionyesha kitabu Cha Blue Print ambacho kinaeleza namna serikali ya awamu ya tano imejipanga kuweka mazingira Bora ya kufanya biashara na uwekezaji.
 Wafanyabiashara waliofika katika ukumbi wa anatoglo kumsikiliza Waziri Bashungwa kama wanavyoonekana katika picha.
Washiriki wakimsikiliza kwa makini waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa katika mkutano wa wafanyabiashara.


WADAU WA MAZIWA KUPITIA SHERIA YA MAZIWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

Wadau was sekta ya Maziwa nchini wamekutana jijini Dar es Salaam leo kujadili na kupitia sheria ya Maziwa sura 262 ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo Kaimu Msajili wa bodi ya Maziwa nchini, Dkt. Sophia Mlote Amesema sheria Ina miaka 15 tangu ianze kutumika mwaka 2004 na kanuni zake ni za mwaka 2007 na 2012.

Amesema Tasnia ya Maziwa imekua na mabadiliko mbalimbali na mambo mengi yamejitokeza ambayo ni ya msingi katika uendelezaji wa Tasnia ya Maziwa ambayo yanahitaji usimamizi wa kisheria.

" Kwa kutekeleza lengo la  mkutano huu la kupitia sheria na kanuni zake kikamilifu na kutoa michango yetu tutaweza kuboresha usimamizi wa tasnia ya Maziwa ili kuiwezesha kusimamiwa ipasavyo" Amesema  

Ametaja kuwa maeneo yatakayopitiwa na marekebisho haya ni sheria ya Maziwa Na.8 Sura 262 ya mwaka 2004 , kanuni ya uuzaji wa Maziwa na bidhaa zake nje na ndani ya Nchi  ya mwaka 2012,usimamiaji wa madaraja ya Maziwa ghafi ya mwaka 2007.

Amesema kanuni ya usafirishaji wa Maziwa ghafi nayo inapitiwa,kanuni ya majukumu na kazi A wakaguzi ya mwaka 2007.
Alimaliza kwa kwa kusema majukumu ya bodi ya Maziwa kwa mujibu wa sura 262 ya mwaka 2004 ni kusimamia nankuendeleza uzalishaji ,usindikaji na uuzaji wa Maziwa.
 Kaimu Msajili wa bodi ya Maziwa nchini,Dkt.Sophia Mlote akizungumza na wadau wa Maziwa nchini wakati wa mkutano Maalum was kufanya mapitio ya sheria ya Maziwa katika ukumbi wa Mvuvi House jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakimsikiliza kwa makini Kaimu Msajili wa Maziwa nchini DKt.Sophia Mlote
Mwanasheria wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Irine Lukindo akifafanua juu ya sherianya zamani na marekebisho yake kifungu kwa kifungu.

KUFIKIA JULAI 30 WAKULIMA WOTE WATAKUWA WAMELIPWA FEDHA ZA PAMBA- WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mzani wa kupimia Pamba mara baada ya kuwasili katika kijiji na kata ya Nyamigota Halmashauri ya Mji wa Katoro kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu kwenye zao la Pamba wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, Jana tarehe 18 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua kiwanda cha kuchakata pamba kilichotelekezwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Shinyanga (SHIRECU) kilichopo Wilayani Mbogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, Jana tarehe 18 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kutoa ufafanuzi kuhusu zao la Pamba mara baada ya kuwasili katika kijiji na kata ya Msasa, wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, Jana tarehe 18 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko kabla ya kuzungumza na wakazi wa Kijiji cha Namparahala kilichopo katika kata ya Busonzo katika wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wakati wa mkutano wa hadhara kutoa ufafanuzi kuhusu zao la Pamba, Jana tarehe 18 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo mbele ya kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ya Mbogwe wakati akitoa ufafanuzi kuhusu zao la Pamba, wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, Jana tarehe 18 Julai 2019.




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Geita


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa hadi kufikia Julai 30, 2019 wakulima wote wa Pamba nchini watakuwa wamelipwa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya sintofahamu kuhusiana na suala ununuzi wa zao hilo baada ya kutangazwa kwa bei elekezi ambayo ni sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Alisema kuwa miongoni mwa changamoto za wanunuzi ni dhamana ya serikali katika taasisi za kifedha. Ambapo tayari serikali imeridhia kuwadhamini ili kununua zao hilo.

Waziri Hasunga ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Julai 2019 wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika Wilaya ya Mbogwe, Bukombe na Geita wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali imeamua kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba kutokana na kusuasua kwa soko lake kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.

Wakati huo huo Mhe Hasunga aliwasihi wakulima wa zao hilo la pamba na wakulima wa mazao mengine nchini wahakikishe mara baada ya kuuza mazao yao wanatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo watakazozitumia katika msimu ujao.

“Pamoja na kwamba mtalipwa fedha nzuri iliyopangwa na serikali ya shilingi 1200 lakini nawakumbusha kuwa serikali sasa haitawakopesha pembejeo hivyo ni vyema mkatenga fedha ili kununua pembejeo hizo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga alisema Serikali itahakikisha inaendelea kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa masoko kwa mazao yao na hivyo kujiongezea tija.Pia, alisema mbali na kutafuta masoko, Serikali imedhamiria kufufua viwanda mbalimbali vya nguo hapa nchini ili kuwawezesha wakulima wa zao la pamba kuwa na soko la uhakika. 

“Kuhusu suala la maghala tunatambua tatizo hilo na tutahakikisha tunayaboresha ili pamba iweze kuhifadhiwa katika mazingira bora” Alisema
Akizungumzia kuhusu changamoto ya viuatilifu, Waziri Hasunga alisema Serikali itahakikisha vinapatikana kwa kuzingatia eneo husika ili kuweza kudhibiti wadudu waharibufu.

Sambamba na hayo Mhe Hasunga ametoa miezi miwili kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Shinyanga (SHIRECU) kuhakikisha kuwa kinafufua kiwanda cha kuchakata Pamba Kilichopo katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na kufikia mwaka 2020 kianze kufanya kazi.

BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 150 KUDHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT 2019

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja wa Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB –Boma Labala (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 150 kwa ajili yaUdhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT – 2019 kwa mwenyekiti wa ALAT taifa Mheshimiwa Gulamhafeez Mukadam. Kushoto ni Maneja Mwandamizi waBiashara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB Suzana Shuma na kulia ni Mheshimiwa Zainab Vullu, Muwakilishi wa Wabunge ALAT.

………………..

Benki ya CRDB imekabidhi hundi ya mfano ya shilingi Milioni 150 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa 35 wa ALAT taifa unaotarajia kufanyika kuanzia tarehe 22 Julai hadi 24 jijini Mwanza.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 500 kati yao wakiwa mameya, kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 185, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 500. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Goldcrest jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Boma Labala alisema kuwa Benki ya CRDB inathamini sana mchango wa Serikali za mitaa hususan halmashauri katika ustawi wa uchumi na maendeleo ya Taifa. 

“Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa ALAT katika kuchochea maendeleo ya taifa letu, pasi na shaka hiki ni chombo kinachounganisha pamoja mamlaka na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya Serikali za Mitaa hapa nchini ambapo ndio hasa wanamgusa Mtanzania katika ngazi ya chini. Hii ndio sababu kubwa iliyotufanya sisi kuwa tayari kushiriki mkutano huu, kwa kuamini kuwa mikakati na maazimio yanayofikiwa hapa leo yatakwenda kuongeza kasi maendeleo ya taifa letu na kuwagusa watanzania walio wengi”. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhefeez Mukadam alisema kuwa taasisi yao inathamini sana udhamini huo wa Benki ya CRDB kwani kwa kiasi kikubwa utachangia gharama za uendeshaji wa mkutano huo muhimu. Mheshimiwa Mukadam alisema kuwa Benki ya CRDB imekuwa mdau mkubwa wa Serikali za mitaa kwa kuendelea kutoa huduma za kifedha kwa halmashauri zaidi ya 60 nchini na mikopo kwa halmashauri hizo na wafanyakazi wake. “CRDB ni mdau wetu muhimu sana na tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono” alisema.

MABASI MENGINE MAWILI YAKAMATWA YAKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 85

$
0
0
Katika muendelezo wa operesheni ya ukaguzi wa Mabasi na Malori Mkoani Arusha iliyoanza tarehe 09.07.2019, leo tarehe 18.07.2019 muda wa mchana huko katika maeneo Kona ya Engaruka – Mto wa Mbu, Wilaya ya Monduli Katika barabara inayoelekea Loliondo mabasi mawili moja la Kampuni ya Coastal Line na lingine la Kampuni ya Loliondo yalikamatwa yakiwa yamezidisha Abiria zaidi ya 85. 

Akiongea na Waandishi wa Habari Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP)Joseph Bukombe amesema basi la kampuni ya Coastal Line lenye namba za usajili T. 447 ADR lilikamatwa likiwa na abiria 87, ambapo abiria 22 walikua wamezidi katika basi hilo badala ya 65 ambao ndio uwezo wa gari. Basi la Kampuni ya Loliondo lenye namba za usajili T. 919 BRA lilikamatwa likiwa na abiria 66 badala ya abiria 60 ambapo abiria 6 walikuwa wamezidi. 

Amesema saivi madereva na makondakta wa mabasi wamebuni mbinu nyingine ambapo wakati wa ukaguzi kabla ya kutoka stendi ya mabasi wanakua wamebeba levo siti, lakini wakiwa njiani hasa wakishavuka vituo vya ukaguzi wanaamua kubeba abiria wengi zaidi. 

Aliendelea kusema saivi wameamua kufanya operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali bila ya ubaguzi nje kabisa ya mji kwa lengo hasa la kuwakamata wote wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa hasa wenye tabia ya kubeba abiria zaidi na kuendesha magari yakiwa mabovu. 

“Leo tumeamua kufanya ukaguzi nje kabisa ya mji, ka mnavyoona tupo huku maeneo ya Mto wa Mbu na tumeyakuta mabasi haya yakiwa yamezidisha abiria.Tunaendelea kuwataka wamiliki pamoja na madereva wote kuzingatia masharti ya leseni zao kwani tutaendelea kuwachukulia hatua kali”. alisema RTO Bukombe. 

Aidha ameendelea kutoa wito kwa Wamiliki wa vyombo vya usafiri hasa mabasi kuwasimamia madereva na Makondakta ili kuepukana na usumbufu wa mara kwa mara utakaojitokeza. Ameongeza kuwa endapo watawasimamia vizuri watafuata sheria zote za barabarani zilizowekwa . Pia amewataka kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara. 

Madereva na Makondakta wa mabasi hayo walikamatwa kwa ajili ya mahojiano na kisha walipewa dhamana ili waweze kuwafikisha abiria sehemu wanazoelekea na baadaye wametakiwa kurudi kituo cha Polisi kwa hatua zaidi za kisheria. Aidha abiria waliozidi katika mabasi hayo walirudishiwa nauli zao. 

Toka Habari Ofisi ya Kamanda – Arusha

NCHI 100 KUSHIRIKI SHINDANO LA KIMATAIFA LA MISS UTALII TANZANIA (MISS TOURISM Tanzania INTERNATIONAL)

$
0
0
Washiriki zaidi ya 100, wenye mataji ya kitaifa kutoka nchi 100 duniani kote watashiriki shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019 / 2020,litakalo fanyika Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2020. 

Kitaifa fainali hizo zitaanzia katika ngazi za kanda maalum za Miss Utalii Tanzania, zitakazo shirikisha washindi wa mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani, ambayo imegawanywa katika kanda maalum nane za mashindano haya. Kanda hizo na mikoa yake katika mabano ni Miss Utalii Kanda ya Kaskazini “Miss Tourism Northern Zone” (Manyara, Arusha, na Kilimanjaro), Miss Utalii Kanda ya Kusini “Miss Tourism Southern Zone“ Ruvuma, Lindi, Mtwara, na Morogoro),Miss Utalii Kanda ya Pwani ya Kiswahili “Miss Tourism Swahili Coast Zone” (Coast, Dar es Salaam and Tanga),Miss Utalii Kanda ya Magharibi “Miss Tourism Western Zone” (Kigoma, Tabora and Katavi),Miss Utalii Kanda ya Ziwa “Miss Tourism Lake Zone” (Kagera, Mwanza, Mara, Geita na Simiyu), Miss Utalii Kanda ya Kati “Miss Tourism Central Zone” (Dodoma, Singida, na Shinyanga, Miss Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini “Miss Tourism Southern Highlands” (Mbeya, Rukwa, Iringa, na Njombe), Miss Utalii Kanda ya Mashiriki “Miss Tourism Eastern Zone” (Unguja and Pemba). 

Nchi zote duniani zitakazo shiriki katika shindano hili, zita wakilishwa na warembo wenye mataji ya mshindi 1 au 2 au 3 katika moja ya shindano la kitaifa la nchi husika. Ambapo washiriki wa nje watawania taji la Miss Tourism Tanzania International, na washiriki wa ndani watawania taji la Miss Tourism Tanzania. Mshindi wa taji la Miss Tourism Tanzania International, majukumu yake itakuwa ni ya kimataifa ya kutangaza na kuhamasisha utalii, uwekezaji na utamaduni wa Tanzania kimataifa ,huku mshindi wa taji la Miss Utalii Tanzania ,atakuwa na jukumu la kitaifa la kuhamasisha na kutangaza utalii, mazingira,uwekezaji,huduma za Misitu, Wanyamapori na utamaduni kila mwaka. 

Fainali hizo za kimataifa za Miss Utalii Tanzania, zitakuwa ni tukio kubwa la Utalii na kitamaduni duniani, litaonyeshwa na kurushwa mbashara (LIVE) duniani kote kupitia Televisheni na mitandao ya kijamii, na kutazamwa na zaidi ya watazamaji 750 milioni duniani kote. Wakati wa shindano hili inatarajiwa, zaidi ya wageni 1500 toka nje watakuja nchini kushudiwa fainali hizi, wakiwemo wapenzi wa mashindano ya urembo wa kitalii, waandishi wa habari wa kimataifa, Ndugu na jamaa wa washiriki, watu mbalimbali mashuhuri duniani n.k. 

Washiriki kutoka kila nchi watambatana na waandishi wa wa habari za Televisheni, Mitandao ya kijamii na magazeti ya nchi anayo toka, lakini pia Ndugu jamaa na marafiki. Wakiwa kambini nchini, washiriki wote wakiambatana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa wata tembelea vivutio mbalimbali vya utalii, utamaduni, uwekezaji, mazingira, huduma za misitu, Wanyama pori, maeneo ya wadhamini na ya vipaumbele vya nchi na serikali huku wakipiga picha za Televisheni,Filamu,Magazeti,Majarida na Matangazo. 

Kufanyika kwa shindano hili la kimataifa nchini ni Matokeo ya mageuzi na mapinduzi ya tuliyo fanya ya sanaa ya urembo nchini, ambapo sasa nchi itanufaika kwa kuwatumia washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani kama bango la kujitangaza , lakini pia ni fulsa kwa Tanzania kama nchi, na wafanya biashara kama wadhamini kujitangaza kimataifa na kitaifa kitalii, kitamaduni, kiwekezaji, kiuchumi na kijamii, kupitia washiriki na matangazo mbashara ya Televisheni, Mitandao ya kijamii na machapisho mbalimbali. Lakini hii itakuwa ni fulsa pia kwa nchi, wafanya biashara na wajasiriamali wa Tanzania kufanya mauzo ya bidhaa zao, lakini pia kupenya na kupanua Masoko ya bidhaa zao kitaifa na kimataifa, kwani washiriki na wageni wote wakiwa nchini watatumia huduma na bidhaa za Tanzania kwa Mahitaji yao ya kila siku kwa muda wote watakapo kuwapo nchini. Katika hatua za awali tayari washiriki kutoka nchi mbalimbali za Ulaya, Amerika, Asia, Afrika, Canada na India zimethibitisha kushiriki fainali hizi za kimataifa za Miss Utalii Tanzania ,ambazo zitakuwa zina fanyika kila mwaka nchini. 

Shindano la Miss Utalii Tanzania limeruhusiwa kufanyika tena nchini ,baada ya kufunguliwa na BASATA 22,Januari 2019,baada ya kusitishwa kwa muda baada ya tathmini ya mwaka 2013, kwa lengo la kuboresha zaidi mfumo wa uongozi na wa mashindano, kutoka kwenye mfumo wa kiimla kuja kwenye mfumo mpya wa sasa wa kitaasisi. 

Shindano hili ambalo kwa mfumo mpya sasa linakuwa ni la kimataifa, lina baki kuwa ndilo shindano pekee nchini lenye mafanikio makubwa hasa kimataifa. Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa ndilo shindano la kwanza nchini kabla na baada ya kutwaa taji la dunia, ambapo Miss Utalii Tanzania 2004, Witness Manwingi alitwaa taji la kihistoria la Dunia la Miss Tourism World 2005 – Africa katika fainali za dunia zilizo fanyika Harare Zimbabwe 25-2-2005. Miss Utalii Tanzania ndilo shindano pekee nchini, ambalo limetwaa mataji katika mashindano yote ya Dunia na kimataifa tuliyo shiriki, ambapo hadi sasa tunashikilia mataji 5 ya dunia na kimataifa. 

Mafanikio makubwa zaidi ni pale tulipo andika historia kwa Tanzania kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Tourism World 2006,fainali ambazo zilifanyika nchini 11-3-2006 Ubungo Plaza Dar Es Salaam, na kushirikisha nchi 119 duniani, huku fainali hizo zikirushwa LIVE Duniani kote kupitia Televisheni, na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 duniani kote. 

Tafiti mbalimbali duniani zimethibitisha kwamba katika mashindano ya urembo, nchi wenyeji wa shindano ndio hunufaika kwa kuwatumia washiriki kutoka nchi mbalimbali kama mabango ya kutangaza nchi mwenyeji, na kuacha nchi shiriki bila faida yoyote ya kimantiki ya kwenda kushiriki au kutuma wawakilishi. Tuna amini wakati sasa umefika, tena wakati sahihi kwa Tanzania na watanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazo nufaika kwa kuwa wenyeji wa mashindano na matukio ya kimataifa ya sanaa ya urembo na mitindo,ikiwa ni tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii,Michezo,Utamaduni,Wanyamapori,Mazingira,Uwekezaji na Mambo ya Nje. 

Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha – Utamaduni ni Uhai wa Taifa (Miss Tourism Tanzania The Symbol of National Heritage – Tourism is Life – Culture is Living).
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images