Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live

HESLB sasa yawafuata wanafunzi JKT kuwapa elimu ya uombaji mikopo

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Jumatatu, Julai 15, 2019 imeanza kuendesha programu za elimu kuhusu uombaji mikopo kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka huu ambao wapo katika kambi 17 za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini kote.

Programu hizo ni muendelezo wa programu za elimu ya uombaji mikopo kwa usahihi ambazo HESLB iliziendesha mwezi April na Mei mwaka huu katika shule 119 za sekondari zilizopo kwenye mikoa 17 na kuwafikia wanafunzi 27,913 waliokua wanajiandaa na mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita iliyomalizika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza katika kambi ya JKT Ruvu Jumatatu, Julai 15, 2019 Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema lengo la programu hizo ni kuwawezesha wanafunzi kuomba mikopo kwa usahihi na hatimaye wenye sifa wapate mkopo na elimu ya juu.

“Kwa kushirkiana na wadau wetu, likiwemo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), tumedhamiria kuwafikia wahitaji wa mikopo pale walipo, ndiyo sababu tupo hapa na wenzetu wapo katika kambi nyingine kama 16 ... na ikumbukwe tuliendesha programu kama hizi katika shule ya sekondari Tanzania Bara na Zanzibar,” amesema Badru na kuongeza:

“Kwa mwaka 2019/2020, Serikali imeongeza bajeti ya fedha mikopo kutoka TZS 427.5 bilioni hadi TZS 450 bilioni zinazotarajia kuwanufaisha jumla ya wanufaika 125,000 wakiwemo wa mwaka wa kwanza zaidi ya 45,000. Mwaka huu wa masomo unaomalizika ambao TZS 427.5 bilioni zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 123,285 wakiwemo 41,345 wa mwaka wa  kwanza,” amesema Badru. 

Kambi hizo ni Bulombora, Kanembwa na Mtabila zilizopo mkoani Kigoma; Rwamkoma (Mara); Msange (Tabora); Nachingwea (Lindi); Mpwapwa na Makutupora (Dodoma); Mgambo na Maramba (Tanga). Nyingine ni Makuyuni (Arusha); Mafinga (Iringa); Mlale (Ruvuma); Itaka na Luwa (Songwe); na Milundikwa iliyopo mkoani Rukwa.  

Badru aliongeza kuwa uzoefu wa miaka iliyopita umeifanya HESLB kuandaa programu hizo ambazo alisema zimeonesha mafanikio makubwa kutokana na aina ya maswali yanayoulizwa.

“Tunawaeleza kuhusu nyaraka muhimu zinazotakiwa kuambatishwa, namna sahihi ya kuomba kwa kutumia mtandao wetu ambao upo wazi hadi Agosti 15 na tunaruhusu maswali kutoka kwao na kuyajibu papo hapo,” ameongeza.

Akizungumza baada ya mkutano huo, mwanafunzi Ngatowana Ndakwila Kiwanga ameishukuru Serikali na HESLB kwa kuandaa utaratibu wa kutembelea kambi za JKT na kuwaelimisha wanafunzi ili wawasilishe maombi kwa usahihi na hatimaye kutimiza ndoto zao za elimu.

“Mimi nimepata daraja la kwanza la pointi saba na nilikua nasoma HKL (Historia, Kiswahili na Kiingereza) na ingawa sijaomba hadi sasa, nitaomba na ninaamini nitapata mkopo na nitakua mwanasheria,” amesema Kiwanga, mwanafunzi mwenye ulemavu aliyemaliza kidato cha sita mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.

Kwa upande wake, akiongea katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Utoaji Mikopo wa HESLB Dkt. Veronika Nyahende amesema matarajio ya HESLB kwa mwaka huu ni kuona idadi ya wanafunzi wanaokosea kujaza fomu za maombi inapungua kwa kiasi kikubwa.

“Pamoja na elimu ya maelezo ya mdomo, tumewapa kitabu kidogo cha lugha ya kiswahili chenye maswali na majibu kuhusu utaratibu mzima wa uombaji mikopo kwa lugha nyepesi…tunawasihi wasome na kuzingatia maelezo yote muhimu,” amesema Dkt. Nyahende.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Jeshi hicho ambapo kambi hiyo yenye vijana takribani 3,000 wapo, Luteni Kanali Alex Malenda alishukuru utaratibu ulioandaliwa na kuongeza unastahili kupongezwa kwa kuwa utasaidia kupunguza muda unaotumika na wanafunzi kukamilisha maombi kwa kuwa wanakua hawajui mambo mengi.

HESLB ilianza kupokea maombi ya mkopo kwa njia ya mtandao tarehe 1 mwezi huu wa Julai na inatarajia kufunga tarehe 15 Agosti mwaka huu ili kuruhusu kazi ya uchambuzi wa maombi yaliyopokelewa na hatimaye kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa ifikapo mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Veronica Nyahende akizungumza na wanafunzi waliohitimu kidato cha sita walioko katika mafunzo ya JKT  Ruvu namna ya kuomba mkopo katika Bodi hiyo kwa ajili ya elimu ya Juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru akitoa Vitabu vya elimu kuhusu uombaji mikopo, ni Luteni Kanali Alex Malenda Katika Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita walioko katika mafunzo katika Kambi hiyo.



Chuo cha Mwalimu Nyerere chajinasibisha uwezo wake wa utoaji wa Elimu nchini

0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy kimesema  licha ya kufundisha kozi mbalimbali pia wanafundisha maadili.

Akizungumza na waandishi wa habari Katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Elimu ya Juu wa Chuo hicho Dkt.Philip Daninga amesema kuwa  Wanafunzi katika maonesho hayo kwani wanadahili hapo hapo .

Amesema kuwa Wanafunzi wakisoma hapo wanajengwa kimaadili na kufanya kuweza kujitambua katika maisha yao. Dkt.Daninga amesema wanakozi mbalimbali katika Chuo hicho ambapo vijana wanaweza kusoma kutokana na kuwa Mazingira rafiki ya kusoma.

Aidha amesema kuwa maonesho hayo ni fursa ya kuwafikia wanafunzi ikiwa kutoa taarifa mbalimbali za Chuo hicho. "Tumedhamiria kutoa elimu bora inayokwenda na Mazingira ikiwa ni pamoja kuwafanya vijana kuwa wabunifu"amesema Daninga.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy Jenipher Siriwa akitoa ubunifu wake wa Umeme wa Jua  katika mfumo wa kufuata Jua Katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy Mohamed Abushiri  akitoa maelezo namna alivyogundua kuzuia gesi kulipuka katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Elimu ya Juu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial Academy Philip Daninga akizungumza na waandishi habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Balozi Iddi atembelea eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali ya Zanzibar Dodoma

0
0
Na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi ameoneshwa na kutembelea eneo ambalo zitajengwa Ofisi za Serikali hiyo eneo la Mahoma Makulu Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Balozi Iddi ambaye aliambatana na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali, alishukuru Serikali kwa kupewa eneo hilo. 

Aliahidi kuwa SMZ itaaaza ujenzi wa Ofisi zake katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kama watapata fungu ujenzi utaanza mapema iwezekanavyo ili waweze kuhamia katika Makamo Makuu ya Nchi.
Katika ziara hiyo ujumbe huo kutoka Zanzibar ulipokelewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi, Samuel Mwashambwa hiyo na viongozi mbalimbali.

Balozi Seif alipata nafasi ya kutembelea pia eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba ambako zimejengwa Ofisi 25 za Serikali zikiwemo za Wizara mbalimbali na tayari watumishi wake wamehamia.
Akizungumza kuhusu eneo hilo Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe alisema eneo hilo lina ekari 30.

Alisema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza Serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi Julai 25, 2016 ulianzishwa mchakato wa kuhamisha watumishi.
 Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine alipowasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
 Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Mwashambwa, mara baada ya kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
 Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi alisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sifuni Msangi, mara baada ya kuwasili Mahona Makuu jijini Dodoma ambako alioneshwa eneo litakalojengwa Ofisi za Serikali hiyo.
 Makamuwa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi (mbele katikati) akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Joseph Sokoine (mwenye tai), kuangalia eneo lililotolewa kwa SMZ kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi zake Mahona Makulu jijini Dodoma.

Mratibu wa Mchakato wa Kuhamishia Serikali Dodoma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Meshack Bandawe (kushoto) akitoa maelezo kuhusu eneo lililotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TIA yashiriki maonesho ya Vyuo Vikuu

0
0
 Wanafunzi wakipata maelezo katika Banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) akipata maelezo katika banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MHANDISI KAMWELWE ATOA MIEZI MITATU KWA TEMESA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutopeleka magari ya Serikali kwenye karakana binafsi kwani Wakala unajitosheleza kwa kuwa na wataalamu  na vifaa vya kutosha.

Mhandisi Kamwelwe, amesisitiza kwa Wakala huo kuhakikisha  unatengeneza magari kwa bei nafuu na muda na mfupi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wao.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine alikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini hapo.

"Ninyi ni taasisi ya Serikali fanyeni vitu viwe nafuu na mtengeneze kwa viwango ili watu wafurahie huduma zenu", amesisitiza Waziri Mhandisi Kamwelwe.

Aidha,  ametoa wito kwa Wakala huo kutoa ushauri wa magari ya Serikali kwa umahiri na weledi na kutokubali kutengeneza magari ya Serikali endapo gari hilo litaonekana gharama yake  ni sawa na kununua gari nyingine.

Waziri Kamwelwe ameupongeza Wakala huo kwa kupunguza gharama za kutengeneza taa za barabarani ambazo zinatumia mfumo wa dakika. 

"Wakala umetumia kiasi cha shilingi milioni 150 katika kitengeneza taa hizo badala ya milioni 250 na tayari zimeanza kufungwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro" amesema Waziri Kamwelwe.

katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/20 Waziri Kamwelwe amefafanua kuwa Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua boti za uokoaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi katika visiwa vya Ukerewe (Ilugwa, Nafuba na Gana).

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TEMESA kwa Waziri huyo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Masele, amemueleza kuwa Wakala umejipanga kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 kuanzisha karakana katika ngazi za Wilaya ikiwemo Wilaya ya Kahama, Simanjiro, Same, na Chato lengo likiwa ni kupeleka huduma karibu na wateja hasa kwa walio mbali na karakana za mikoa.

Ameendelea kueleza kuwa hadi sasa Wakala umeshafanya uwekezaji wa shilingi bilioni 66 kwa ajili ya kununua vivuko 18 na hivyo kufanya kufikia jumla ya vivuko 31 na boti ndogo tano hapa nchini.

Kuhusu kukamilisha ujenzi wa vivuko  nchini Mhandisi Masele amesema kuwa tayari wakala umekamilisha ujenzi wa kivuko kipya cha MV Mwanza kinachotoa huduma eneo la kigongo-Busisi, ujenzi wa miundombinu katika kivuko cha Lindi Kitunda na inaendelea kukamilisha ujenzi wa Kivuko cha Kayenze- Bezi kitakachotoa huduma kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala Na.30 ya mwaka 1997 ikiwa na majukumu ya kufanya matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali, matengenezo ya usimikaji wa mifumo ya umeme, uendeshaji wa vivuko vya Serikali, utoaji huduma za ukodishaji wa mitambo ya Serikali, kufanya usanifu na usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa mitambo, umeme na elektroniki.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua vitendea kazi vya kisasa vilivyofungwa katika karakana ya MT. Depot iliyopo jijini Dar es Salaam inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakati alipofanya ziara ya kikazi katika karakana hiyo, mkoani humo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Masele, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuhusu taa za barabarani zinazotumia mfumo wa dakika zinazotengenezwa na Wakala huo katika karakana ya MT. Depot ya jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kikazi katika karakana hiyo, mkoani humo.
 Muonekano wa vyuma vinavyotumika katika utengenezaji wa taa za barabarani zinazotengenezwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme Arch. Edwin Nnunduma,  akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Lindi Wamshukuru Magufuli kwa MV Kitunda

0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepewa pongezi na Wakazi wa Mkoa wa Lindi kwa kuwaletea huduma ya kivuko cha MV Kitunda kinachofanya safari zake kutoka Lindi kwenda ng’ambo ya pili katika eneo la Kitunda.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni wakati Maafisa Habari wa Idara ya Habari – MAELEZO walipotembelea eneo la feri ambapo kivuko hicho kinafanyia kazi ili kujionea utendaji kazi wa kivuko hicho.
Mfanyabiashara na mkazi wa Kitunda, Yusuph Yahya amesema kuwa kabla ya kivuko hicho biashara zilikuwa ngumu kwa sababu uvushaji wa mizigo haukuwa rahisi pia gharama na muda uliokuwa ukitumika kuvusha mizigo hiyo ni kubwa hivyo muda mwingine wafanyabiashara walikuwa wanapata hasara kutokana na mizigo yao kuharibikia njiani wakati wa usafirishaji.

“Kwa kweli tunamshukuru sana Rais wetu Magufuli kwa kutuletea kivuko hiki kwani mwanzoni tulikuwa tunatumia usafiri wa boti ndogo ndogo hata magari ilikuwa shida kuyavusha lakini kwa sasa usafiri ni salama biashara zimekuwa zikifanyika kwa urahisi hata gharama za usafirishaji zimeshuka, zamani mzigo mdogo tu unasafirsha zaidi ya shilingi 2000 hadi 3000 lakini sasahivi tunavusha mzigo mdogo kuazia shilingi 1000,” alisema Yahya.

Naye Mkazi wa Manispaa ya Lindi, Shakira Nandonde amesema kuwa kivuko hicho kimewaondolea adha ya usafiri hasa kwa wanawake, watoto na walemavu kwa sababu boti zilikuwa zikipaki mbali na nchi kavu hivyo ilikuwa ni changamoto kuufikia usafiri huo pia kwa wagonjwa ilikuwa changamoto kuwatoa Kitunda kuwaleta Lindi Mjini ambako ndio kuna matibabu makubwa.

Mkazi mwingine wa Kitunda, Said Omary ameishukuru Serikali kwa ujio wa kivuko hicho kwani kimepunguza gharama za usafiri kutoka shilingi 500 malipo ya usafiri wa boti mpaka shilingi 300 kwa usafiri wa kivuko pia kivuko hicho kimesaidia kupanua mji wa Kitunda kwani kwa sasa watu wameanza kujenga na wengine wameanza kulima katika maeneo hayo.

“Sina cha kusema zaidi ya kuipongeza Serikali na Rais wetu Magufuli ila tunaomba muda uliowekwa wa mwisho saa 12 jioni kwa siku uongezwe ili shughuli zingine ziendelee pia tunaomba kivuko hiki kizidi kuboreshwa ili usafiri uwe wa uhakika,” alisema Omary.
Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 50 kimeanza kufanya kazi Machi,2018, kinabeba abiria 100, magari madogo 6 pamoja na magari makubwa mawili kwa kila safari moja na kwa siku kivuko hicho kinakadiriwa kubeba abiria wasiopungua 900.
Kivuko cha MV Kitunda kinachofanya kazi kati ya kuvusha watu kutoka Lindi mjini hadi Kitunda kikiwa na uwezo wa wa kubeba mizigo tani 50, abiria 100, magari madogo 6 makubwa mawili inakadiriwa kwa siku kinabeba abiri 900. Kabla ya uwepo wa Kivuko hiki wakazi wa Kitunda walikuwa wanatumia mitumbwi kuvuka upande wa pili. Kivuko hiki kimepelekwa Mkoani Lindi kikitokea Tanga kwa amelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni kutatua kero ya wakazi wa Kitunda na maeneo mengine ya Lindi.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu: Wanafunzi 128,285 kunufaika mikopo ya elimu ya Juu

0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imepanga kutoa mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 450 kwa wanafunz 128,285 katika mwaka wa masomo 2019/2020.

Akizungumza na waandishi Habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Habari Mwandamizi  wa Bodi hiyo Veneranda Malima amesema kuwa kati ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza watakuwa 45,000.

Amesema mwaka wa bajeti  2018/2019 bajeti iliyokuwa imepangwa ilikuwa ni sh.Bilioni  427.7 kwa kusomesha wanafunzi 123,000, kati yao wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa 41885.

Malima amesema kuwa kuna ongezeko kubwa na kutaka wanafunzi wafuate taratibu za Uombaji wa mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Amesema wako katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na kujibu changamoto za wanafunzi katika Uombaji wa mikopo hiyo.

Aidha amesema kwa walionufaika na mikopo  urejeshaji umezidi kuongezeka na kutaka kuendelea kurejesha kwa ajili ya kunufaisha wengine.
 Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Veneranda Malima akizungumza na waandishi habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Afisa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kuhusiana na Uombaji wa mikopo ya elimu ya Juu katika Bodi hiyo katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo kutoka Kwa maafisa Bodi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

CHINA KUENDELEA KUIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA SEKTA YA AFYA

0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
BALOZI mdogo wa Jamhuri ya watu wa China Xie Xiuowu amesema nchi yake itaendeleza azma yake ya kuisaidia Zanzibar katika nyanja tofauti ikiwemosekta ya afya ikiwa ni juhudi zake za kukuza uhusiano miongoni mwa nchi hizo mbili.

Alisema misaada wanayoitoa inaongozwa na dhamira njema hasa kwa watu wenye mahitaji ili kuona nao wanaendelea kufurahia maisha yao ya kila siku.

Balozi Xie aliyasema hayo katika hafla ya kuwaaga madaktari wa China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha madaktari wapya ambao nao watahudumu katika sekta ya afya Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Alikumbusha kuwa Jamhuri ya Watu wa China ilianzisha utaratibu wa kuleta madaktari Zanzibar tokea mwaka 1964 na utaratibu huo unaendelezwa na kuimarishwa zaidi hadi sasa.

Alisema kwa sasa wanatekeleza mradi wa kupambana na kichocho, saratani ya shingo ya kizazi na kuwajengea uwezo watendaji katika sekta ya tofauti ili kuimarisha uhusiano kati ya Zanzibar na China.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed alisema uhusiano wa China na Zanzibar unaendelea kuimarika siku hadi siku na kuiomba China ifikirie namna ya kuwafanya madaktari hao kutumia muda wa miaka miwili Zanzibar badala ya mmoja ili kutoa huduma zaidi.

Alisema kupitia uhusiano huo China imeweza kuimarisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo hospital ya Abdalla Mzee kisiwani Pemba.

Aidha aliongeza kuwa wataalam wanaokuja kutoka China husaidia pia huwaongezea ujuzi wananchi na madakri wa Zanzibar kupitia programu mbali mbali ikiwemo za televisheni na hospitalini.

Waziri Hamad aliwashukuru kupitia mradi wa kupambana na maradhi ya kichocho ambapo dola za Marekani Milioni 5 walizotoa zitasaidia kupambana na maradhi ya Kichocho Zanzibar.

Alisema pesa hizo pia zitatumika katika programu ya miaka mitano ya kupambana na maradhi ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi kwa wanawake wa Zanzibar.

“Kiujumla misaada wanayoitoa ndugu zetu hawa ni mingi sana na hawajawahi kutuwekea masharti yanayotubana, tunashirikiana nao vyema tofauti na misaada ya nchi nyingine”, alibainisha Waziri Hamad.

Aidha Hamad aliwasifia madaktari hao kwa nidhamu ya kazi ambayo inapaswa kuigwa na madaktari wazalendo ikiwemo ya kuwahi kazini mapema bila ya malalamiko yoyote.

“Hili la nidhamu ya kazi kwa kweli sisi kama Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tunapaswa tuige. Wanawahi kazini na kuondoka kwa wakati na husikii wakipewa lawama na wananchi wanaowahudumia”, alisema Waziri Hamad.

Kuhusu timu ya madaktari wapya, Waziri Hamad alisema waliokuja ni wataalamu zaidi ambao pia watatumika kutoa elimu katika ngazi za vyuo vikuu vya Zanzibar.

Akitoa salamu za shukran kwa niaba ya wenzake Mkuu wa madakrari waliomaliza muda wao Dk.Zhang Zhen ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ukarimu wao waliouonesha katika kipindi chote cha kuhudumia wananchi Zanzibar.

Alisifia mazingira safi ya visiwa vya bahari ya Hindi ikiwemo Zanzibar ambavyo vitaendelea kubaki katika kumbukumbu zake.

Nae Kiongozi wa timu mpya ya madaktari hao Dk. Yang Xiaodong aliahidi kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na weledi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
 Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu msitari wa pili waliokaa na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kushoto kwake wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Madaktari wnaomaliza muda wao wa mwaka mmoja kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
 Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu katikati na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kushoto kwake, wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya Madaktari wapya kutoka China ambao watakuwa wakifanya kazi ya kuhudumia wagonjwa kwa kipindi cha mwaka mmoja Zanzibar.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid akibadilishana mawazo na Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu wakati wa hafla ya kuwaaga Madaktari wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha madaktari wapya kuhudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
 Balozi mdogo wa China Xie Xiuowu akitoa hotuba yake katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari kutoka China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha Madaktari wapya watakaohudumia wananchi kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
 Waziri wa Afya Hamad Rashid akitoa hotuba yake katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari kutoka China wanaomaliza muda wao na kuwakaribisha Madaktari wapya watakaohudumia wananchi kwa kipindi cha Mwaka mmoja. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wa kutoka China waliomaliza muda wao wa kuhudumu katika sekta ya Afya Zanzibar akitoa neno la shukran katika hafla maalum ya kuagwa kwao na kukaribishwa kwa Madaktari wapya. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar
 Kiongozi wa Timu ya Madaktari wapya kutoka China Dkt.Yang Xiaodong akitoa nasaha zake katika hafla ya kuagwa na kukaribishwa kwa madaktari hao ambao watahudumu Zanzibar katikakipindi cha mwaka mmoja.
Baadhi ya Madaktari wa kutoka China waliohudhuria katika Hafla maalum ya kuwaaga Madaktari wanaomaliza muda wao na kukaribishwa kwa Madtari wapya watakaotoa huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji na Kichocho. Hafla hiyo ilifanyika Ubalozi mdogo wa China mjini Zanzibar Picha na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

KUBORESHWA KWA MIUNDOMBINU SKIMU ZA UMWAGILIAJI KWAPAISHA BAJETI YA HALMASHAURI MVOMERO MKOANI MOROGORO.

0
0

Na Ripota, Michuzi TV-Morogoro

HALMASHAURI ya Wilaya Mvomero mkoani Morogoro imesema asilimia 30 kati ya asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri hiyo inategemea mazao ya kilimo na hasa cha umwagiliaji.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Florent Kyombo mbele ya Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Marco Ndonde.

Wakurugenzi hao wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kwa lengo la kuangalia shughuli za kilimo cha umwagiliaji kinachotokana na skimu zilizopo wilayani humo ikiwa ni jitihada za Serikali kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

Akifafanua zaidi Kyombo amesema mchango wa kipato kinachotokana na kilimo cha umwagiliaji kwa halmashauri ni mkubwa na asilimia 33 ya bajeti ya halmashauri inategemea mazao ya kilimo na kati hizo 30 ni mazao ya umwagiliaji.

"Hivyo tukiona skimu zinaendelezwa katika Wilaya yetu na zinafanya kazi kwa ufanisi tunaamini wananchi wetu watavuna sana na maana yake hata kwa halmashauri tunatajia mapato ya fedha za bajeti kuongezeka.

"Hivyo kupitia fedha hizo halmashauri itajenga madarasa, zahanati, itaboresha miundombinu pamoja na kuendeleza miradi mingine ya maendeleo kwa ajili ya wananchi,"amesema Kyombo.

Pia amesema kuimarika kwa miundombinu kumekuwa kukiongeza mzunguko wa fedha, kwani sehemu kubwa ya kipato cha wananchi kinategemea kilimo na mifumo. "Hivyo wananchi wakivuna utaona mzunguko wa fedha unaongezeka na shughuli za uchumi zinachangamka ikiwemo watu kwenda minadani."

Akizungumzia skimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Kyombo amesema kuna skimu 11 lakini zinazofanya kazi ni chache kwani nyingine bado hazijaendelezwa. 

"Ukiangalia hata maeneo yaliyowekwa miundombinu ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa eneo la Skimu. Hata hivyo kupitia skimu hizo chache ukweli ni kwamba faida zake ni nyingi sana kwani kwa sasa uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka na hiyo maana yake pato la mwananchi nalo limeongezeka,"amesema Kyombo.

Amesisitiza kutokana na kuboreshwa kwa skimu hizo wakulima wa zao la mpunga wanavuna kati ya gunia 40 hadi gunia 50 kwa ekari moja wakati huko nyuma kabla ya skimu walikuwa wnavuna kati ya gunia 10 hadi 15 tu.

"Kuptia skimu ambazo tunazo , uzalishaji wa zao la mpunga umeongezeka.Pia imetoa fursa ya ajira kwa vijana, wanawake na wanaume na kubwa zaidi kila mmoja anaweza kujikwamua kiuchumi."Hivyo Halmashauri tumeendelea kuwa na mikakati ya kuomba fedha ili skiku ambazo bado hazijaendelezwa nazo ziendelezwe.Kwa Dakawa tunayo skimu kubwa sana ambayo uwepo wapo umefanya kuwe kunazalishwaa mpunga kwa wingi sana,"amesema Kyombo.

Pia amesema kwa halmashauri yao nao wamejipanga ili kuwa na Skimu ambayo wanaamini itasaidia kuongeza mapato na kuwa chachu kwa wakulima wa mpunga huku akitoa rai kuwa wananchi wanalo jukumu la kuhakikisha skimu ambazo miundombinu yake imeendelezwa inalindwa.Wakati huo huo ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuendeleza skimu zilizopo Mvomero kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi kuziendeleza ikiwemo skimu ya Dakawa.

Pia amesema kuna skimu nyingi ambazo nazo miundombinu yake ipo hatua mbalimbali ya kuendelezwa na ni matumaini yao zitakapokamilika zitasaidia kuongeza upatikanaji wa mazao ya kilimo."Wananchi wamehamasika sana kutokokana na uwepo wa skimu hizi.Tunafahamu skimu kongwe zote nazo zipo kwenye mchakato wa kuendelezwa ikiwemo skimu ya Mkenge ambayo imeshawekewa banio na itaanza kutumika siku za karibuni,"amesema Kyombo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akifafanua jambo ofisini kwake mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde, Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (hawapo pichani),kuhusu Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo akisoma moja ya kitabu (nyenzo) kinachohusu Skimu ya mwagiliaji,alichokabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (pichani kulia) kwa ajili ya kuendelea kuimarisha Skimu ya Umwagiliaji Wilayani humo,mkoani Morogoro.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Wataalamu wapo katika wilaya hiyo ya Mvomero kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata baada ya ukarabati mkubwa wa miundombinu kufanyika katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24.
Pichani kulia Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda wakiwa na Wataalamu pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu Maendeleo na mafanikio waliyoyapata kufuatia ukarabati mkubwa wa miundombinu uliofanywa katika shamba la Ushirika la Wakulima Wadogowadogo Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa (UWAWADA),Wilayani humo,ambapo ukarabati wa miundominu hiyo umefadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani kupitia Shirika la Misaada la USAID-Tanzania,aidha gharama za ufadhili huo wa Ukarabati wa Miundombinu hiyo ya shamba imegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24. 
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu -Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Senzia Maeda akiomba taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu Skimu ya Umwagiliaji katika Wilaya ya Mvomero inavyofanya kazi na mafanikio yake mpaka sasa.
Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bwa.Marco Ndonde (kushoto) pamoja na Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero,Mhe.Florent Kyombo kuhusu maendeleo na mafanikio ya Skimu ya Umwagiliaji wilayani humo.

Naibu Waziri Aweso awataka Mameneja wa RUWASA kutomuangusha Rais Magufuli

0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amewataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa Wakala wa Majisafi, Usafi na Mazingira Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanaondoa changamoto za Maji katika maeneo yao.

Mhe Aweso ameyasema hayo wakati alipokutana na Mameneja hao jijini Dodoma ambapo amesema kwa sasa Wizara hiyo imeunda kitengo cha usanifu ambacho kitasaidia katika kuangalia upya usanifu, mikataba na gharama zinazowekwa na wakandarasi kabla ya ujenzi wa miradi.

Amewataka Mameneja hao kutumia weledi na taaluma zao kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani na kuwataka kuacha mambo ya hovyo yaliyokuepo awali.

" Katika ziara zangu zote katika maeneo mbalimbali nimekua mkali sana kwa wahandisi na wakandarasi, baadhi ya wataalamu wametuangusha kwa kutumia miradi kujipatia fedha, nimejionea mwenyewe miradi mingi wakishindwa kuimaliza kwa wakati. Wakandarasi hawa hatuwezi kuwavumilia hata kidogo.

" Mhe Rais ametuamini sana katika nafasi hizi tulizoteuliwa, ni jukumu letu kumsaidia kazi na kutumia taaluma zetu kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo vijijini inafikiwa kwa asilimia 85 au zaidi ifikapo mwaka 2020," amesema Mhe Aweso.

Amewataka Mameneja hao kutosubiri Waziri au Katibu Mkuu kufika katika maeneo yao ya kazi na kuwaonesha changamoto badala yake waunde mikakati ya kuwawezesha kufikia maeneo yenye changamoto ya Maji ili waweze kuitatua.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo amesema malengo ya Wizara hiyo ni kuongeza upatikanaji wa Maji kufikia asilimia 84 kutoka asilimia 64 kwa maeneo ya Vijijini, lakini pia wakifikia asilimia 95 kutoka asilimia 84 kwa maeneo ya Mjini.

" Tumekua tukiwekeza sana kwenye miradi mipya lakini kama tukiongeza nguvu na kumaliza miradi ambayo imekwishaanza na kuanza kufanya basi tungekua mbali sana hivyo katika bajeti zetu lazima tupange bajeti zetu Katika kukarabati miradi ya zamani.

" Mhe Naibu Waziri kazi kubwa na ya haraka kufanywa na RUWASA ni kujenga imani kubwa kwa Mhe Rais na Wananchi, na imani hiyo itajengwa na wahandisi hawa kwa kuhakikisha miradi ya wananchi inafanya kazi lakini kubwa zaidi ni kumaliza tatizo la Maji," amesema Prof Mkumbo.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akizungumza na Mameneja wa RUWASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo akitoa neno katika kikao cha Mameneja wa RUWASA kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.
 Mameneja wa RUWASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma walipokutana na Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso (katikati) akiwa Katika picha ya Pamoja na watendaji wa Wizara hiyo na Mameneja wa RUWASA kwa ngazi za Mikoa na Wilaya jijini Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA PAMOJA NA MELI YA MV BUTIAMA KATIKA ENEO LA BANDARI YA MWANZA SOUTH

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tuta la Sehemu inapojengwa Chelezo kubwa yenye uzito wa Tani 4000 kwa ajili ya Ujenzi wa Meli mpya kubwa na ya kisasa itakayohudumu katika Ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenda Bukoba, Kisumu(Kenya) na Jinja nchini Uganda.
  Meli ya MV Victoria inayotoa huduma katika Ziwa Victoria ikiwa katika ukarabati mkubwa. Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa tatu na Mashine Engine zake mpya zinatarajiwa kuwasili hivi karibuni.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo katika eneo la tuta la ujenzi wa  Chelezo ya kujengea Meli hio kubwa na ya kisasa.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Meli ya MV Victoria ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa katika eneo la Bandari ya Mwanza South.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Bandari ya Mwanza pamoja na Wabeba mizigo Makuli kuhusu ujenzi wa Meli hizo. PICHA NA IKULU

Uzinduzi wa duka la jipya la Vodacom mkoani Arusha

0
0



Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo (kulia) na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen wakizindua duka la Vodacom litakalowahudumia wateja eneo la Kwamrombo jijini Arusha, wa tatu kushoto ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia), Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (wa pili kulia), mdau wa Vodacom Bakari Fungo na mkewe wakifurahi baada ya kuzindua duka la Vodacom litakalowahudumia wateja eneo la Kwamrombo jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Brigita Stephen(kulia) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akimsikiliza Mkuu Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kushoto) wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha, kulia ni mdau wa Vodacom Bakari Fungo.


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akifungua chupa ya Champagne wakati wa uzinduzi wa duka la Vodacom eneo la Kwamrombo jijini Arusha, wa pili kulia ni mdau wa duka hilo Bakari Fungo na kushoto ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen.


RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAFUNGWA KATIKA GEREZA LA BUTIMBA JIJINI MWANZA

0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafungwa, Mahabusu, pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Butimba mkoani Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Gereza Kuu la Butimba mara baada ya kuzungumza na wafungwa Mahabusu, pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Butimba mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi fedha mmoja wa Afisa Mwandamizi wa Magereza ACP Shaku Umuya Umba kwa ajili ya kununulia ngombe watatu na magunia ya mchele 15 ili Wafungwa, Mahubusu na Askari hao wapike na kula pamoja. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliokusanyika katika eneo la Butimba Kona na Mkuyuni wakati akitokea Gereza la Butimba.

Baadhi ya Wananchi waliokusanyika katika eneo la Butimba Kona na Mkuyuni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia. PICHA NA IKULU

Mrema atangaza kumaliza muda wake bodi ya Parole

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

BODI ya Taifa ya Parole imeiomba Serikali kuiongezea fedha za uendeshaji wa shughuli zake, ili waweze kukidhi  mahitaji ya utendaji wa kazi wa mikoa na Taifa kwa sababu fedha zinazotengwa na bajeti hazitoshelezi katika  utendaji wa kazi zao.

Aidha, imeshauri Waziri wa Mambo ya Ndani, kuyafanyia kazi majalada yanayowasilishwa na bodi hiyo kutoka magereza mbalimbali kwani bila kufanya hivyo baadhi ya wafungwa wanaotakiwa kunufaika kumaliza vifungo wakiwa ndani.

Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Augustine Mrema ambae amemaliza muda wake leo Julai 16,2019, ameyasema hayo nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi za parole kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai, 2016 hadi Julai 15,2019

Amesema, bajeti finyu imepelekea ukosefu wa vitendea kazi vya kuweza kuwafikisha maeneo mbali mbali hasa katika magereza ili kuzungumza na wafungwa.

" Bodi ya Parole  inaomba pikipiki 30 ambazo zitagawiwa kwa Mikoa yote Tanzania bara ili maafisa wa Parole waweze kutekeleza majukumu yao vizuri," amesema

Pia wameiomba vyama visivyo vya kiserikali, taasisi mbali mbali na watu wenye mapenzi mema kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuwarekebisha wafungwa na kusaidia bodi za parole ili wafungwa wanapoachiwa huru na kurudi kwenye familia zao wawe wamerekebeshika.

Amesema, bodi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi chote hicho cha miaka mitatu lichabya changamoto kadhaa zilizojitokeza ambazo ziko nje ya uwezo wa bodi hiyo.
Aidha, Mrema amemshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kumpa nafasi hiyo, akisema katika miaka mitatu wafungwa  742 kati yao 720 walipendekezwa  na 648 waliachiliwa kwa msamaha wa Parole.

Amesema, wafungwa wote walioachiliwa kwa mpango wa Parole hakuna hata mmoja aliyevunja masharti na kurudishwa  gerezani, kujihusisha au kuhusishwa  na vitendo vya uhalifu.

Akijibu swali iwapo atateuliwa tena na Rais kwa nafasi hiyo atakubali, amesema "yeye ni nani mpaka amkatalie Rais" amesema Mrema

Rais wa Misri kizimbani kwa tuhuma za kutorosha madini

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
RAIA wa Misri Hany Ahmed (27) amefikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutorosha madini aina ya diamond  yenye thamani zaidi ya Sh. Milioni 12.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba,  Wakili wa Serikali Wankyo Simon amedai,  Julai 10, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wilaya ya Ilala jijini  Dar es Salaam.

Imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa  alikutwa akisafirisha madini ya diamond yenye uzito wa carats 11:12 ambayo yana thamani ya Dora za Kimarekani 5,238 sawa na Sh. 12,050,131bila ya kuwa na kibali. 

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na  kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 30, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa, mshtakiwa amerudishwa rumande. 


Robert Lowassa na Stephanie Kaaya walivyomeremeta jijini Arusha, Watu mashuhuri wahudhuria harusi yao

0
0
Bwana harusi Robert Lowassa akimvisha pete Mkewe Stephanie Kaaya wakati wakifunga ndoa yao  takatifu mwishoni mwa wiki iliyoisha katika Kanisa la KKKT Jijini Arusha, na kufuatiwa na sherehe baab'kubwa katika Bustani ya Kiringa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Kidini na watu wengi mashuhuri. Robert  ni Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
Bwana harusi Robert Lowassa akivishwa pete ya ndoa na Mkewe Stephanie Kaaya wakati wakifunga ndoa yao  takatifu mwishoni mwa wiki iliyoisha katika Kanisa la KKKT Jijini Arusha,

Maharusi wakiwa na familia zao. Wa tatu kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ambaye ni Baba wa Bwana harusi na watatu kushoto ni Mama wa Bwana Harusi, Mama Regina Lowassa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwapongeza maharusi wanati wa sherehe yao iliyofanyika, katika Bustani ya Kiringa, Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa wakati alipofika kwenye sherehe ya harusi ya kijana wake, Robert Lowassa .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa wakati alipofika kwenye sherehe ya harusi ya kijana wake, Robert Lowassa .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwapongeza maharusi wanati wa sherehe yao iliyofanyika, katika Bustani ya Kiringa, Jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Biashara na Viwanda, Amina Salum Ali akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa wakati alipofika kwenye sherehe ya harusi ya kijana wake, Robert Lowassa .
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa wakati alipofika kwenye sherehe ya harusi ya kijana wake, Robert Lowassa.

Mmoja wa Wanasiasa Wakongwe na Rafiki Mkubwa wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Rostam Aziz akilipowasili kwenye sherehe hiyo.







WATATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUJIFANYA MAOFISA WA TAKUKURU

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MKUU wa Kitengo cha Mauzo cha Ramada Hoteli, William Mgatta (36) wenzake wawili,   wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo shtaka la kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kushawishi rushwa ya Sh milioni 300.

Mbali na Mgatta washitakiwa wengine ni wafanyabiashara Mohammed Abdallah (25) na Daniel Ileme (35) ambao wote kwa pamoja  wamesomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mmbando.

Hati ya mashtaka imesomwa na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Aneth Mavika  imedai kati ya Mei Mosi na  Juni 10, mwaka huu, katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Arusha, mshitakiwa Abdallah na Ileme wakiwa wafanyabiashara na mshitakiwa Mgatta akiwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo cha Ramada hoteli walishawishi rushwa ya Sh milioni 300.

Amedai kuwa, alishawishi rushwa hiyo kutoka kwa Francis Matunda kama kishawishi ili wasimchukulie hatua za kisheria kwa kukataa kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha Sh bilioni moja wanayomdai.

Imeendelea kudaiwa kuwa katika tarehe tofauti katika eneo lisilotambulika jijini Dar es Salaam na Arusha washitakiwa Abdallah, Ileme na Mgatta walikula njama ya kutenda kosa la kujifanya ni watumishi wa umma.

Wakili Mavika ameendelea kudai kuwa, katika shtaka la tatu, imedaiwa, Juni 10, mwaka huu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam na Arusha washtakiwa kwa pamoja  walijifanya ni watumishi wa Takukuru kitu ambacho walijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, upande wa mashtaka umedai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hawana pingamizi la dhamana endapo washitakiwa watatimiza masharti.

Akiwasomea masharti ya dhamana, Hakimu Mmbando amemtaka kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika wenye barua halali na vitambulisho ambao pia wametakiwa kuwalisilisha mahakamani hapo fedha taslimu Sh milioni 50 au hati ya mali isiyohamishika  yenye thamani ya fedha hiyo na kusaini bodi ya Sh milioni 50.

Washitakiwa wameshindwa kutimiza masharti hayo na wamerudishwa rumande. kesi imeahirishwa hadi Julai 30, mwaka huu kwa kutajwa.

WATAALAMU WA AFYA TOENI ELIMU SAHIHI YA AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE, KUTOKIMBILIA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Gabriel Daqarro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ya Afya ya mama na mtoto yenye jina la "JIONGEZE TUEAVUSHE SALAMA" lengo kuu likiwa ni kutokomeza vifo vya mama mjamzito pamoja na mtoto.

Na Lucas Myovela, Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqarro leo Jully 16, 2019 amezindua rasmi kampeni ya ya Afya ya mama na mtoto yenye jina la "JIONGEZE TUEAVUSHE SALAMA" lengo kuu likiwa ni kutokomeza vifo vya mama mjamzito pamoja na mtoto.

Awali kampeni hii ya JIONGEZE TUWAVUSHE  SALAMA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan June 6, 2018 na badae ilizinduliwa kimkoa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo April 16 mwaka.

Katika uzinduzi huo wa Afya ya mama na mtoto Dc Daqarro ameonya vikali juu ya uzembe wa watumishi wa serikali katika vituo vya Afya katika jiji la Arusha kwa kuwa wazembe wakati wa hutoaji wa huduma kwa wanawake wajawazito na kutoa maelekezo kwa uongozi wa Afya jiji la Arusha kuweza kutoa elimu ya mwanamke kujifungua kwa njia ya kawaida na kuacha kujifungua kwa upasuaji.
"Mpaka sasa wasichana wengi wanao anza uzazi huwa hawapendi kupata uchingu wa  uzazi wao kazi yao kubwa wakiona siku za kujifungua zimefika anaenda kwa dactari anamwambia chana hapa." alisema  Dc Daqarro.

Aidha pia Daqarro aliwataka wataalamu wa Afya wote kujitagidi kadri ya ujuzi wao ili kuondoa vifo vya mama na mtoto kaktika jiji la Arusha,viongozi wa dini kukemea mimba za utoto na kwa wakuu wa mila kuacha imani potofu kwani kwa kila mmoja kufanya majukumu yake kutasaidia zaidi kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Nae kwa upande wake Dactari mkuu wa mkoa wa Arusha Welson Sichalwe ameeleza kuwa kwa mwaka jana vifo vya mama na mtoto vilivyo tokea ni 116 katika uzazi hai 7000 na huku watoto 10 katika uzazi hai 1000 na kueleza yote haya yanatokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo lishe duni.
Pia Dr Welesnon amebainisha kuwa katika awamu hii ya tano ya Docta John Pombe Magufuli imeendelea kupamba na kuboresha secta ya Afya na kufanya mkoa wa Arusha kuwa na wastani wa akiba ya azina ya madawa kwa 97% ya dawa zote na kuwa na viyuo vya Afya 12 na zahanati 1 hivi vyote vimeghalimua zaidi ya bilioni 16 za kitanzania.

Aidha pia katika uzinduzi huo wa kampeni ya kuzuia vigo vya mama na mtoto katika wilaya ya Arusha mjini maafisa tarafa wameweza kusaini mikataba ya kuwa mabolozi na waelimisha jamii kwa kupinga vifo vya mama na mtoto katika tarafa zao,Pia uzinduzi huo uliweza kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,vyama vya siasa,viongozi wa dini pamoja na taasisi mbali mbali za kijamii.

KAMPUNI INAYODAIWA KUMPIGA MISS SHINYANGA YAFUNGIWA NA BASATA

0
0
Baraza la Sanaa la Taifa BASATA limeisimamisha Kampuni ya Makumbusho Entertaintment pamoja na viongozi wake kujishughulisha na shughuli yoyote ya masuala ya sanaa na burudani.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza ikieleza kuwa wakiwa kama wasimamizi wa shughuli za sanaa nchini na kupokea kwa masikitiko taarifq za unyanyasaji wa Kijinsia uliofanywa na kampuni hiyo dhidi ya mmoja wa washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2019.

Tukio hilo la udhalilishwaji kwa mlimbwende Nicole Emmanuel lilifanyika Julai 6 mwaka huu Mkoani Shinyanga. BASATA imetoa wito kwa wasanii, wadau na waandaaji wa shughuli za sanaa nchini kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili kulind, kuthamini na kuikuza sanaa yetu nchini.

Inadaiwa kuwa Nicole amedai kupigwa na kuchaniwa nguo hadharani na waandaji wa mashindano hayo wa Kampuni ya  Burudani ya Makumbusho Entertainment mjini Shinyanga wakati akidai fedha zake nauli shilingi 70,000/=  akiwa na mshiriki mwenzake wa shindano hilo aitwaye Agnes Masunga walipofika kwenye hoteli hiyo(kambi waliyokuwa wanaitumia) ili kudai nauli zao.

Waandaji wa Shindano hilo wanaotuhumiwa kumpiga na kumdhalilisha binti huyo ni Meneja Mkuu wa Makumbusho Entertainment,George Foda na Mkurugenzi wa Makumbusho Entertainment Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) mkoa wa Shinyanga.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YAKAGUA UKARABATI MKUBWA WA MIUNDOMBINU SKIMU ZA UMWAGILIAJI DAKAWA-MOROGORO,YARIDHISWA NA MATOKEO.

0
0

Pichani wa pili kulia,Kaimu Mkurugenzi Tume ya Umwagiliaji Bwa.Marco Ndonde akimsikiliza Mwenyekiti wa Ushirika Wakulima Wadogowadogo  Kilimo cha Umwagiliaji Mpunga Dakawa,Mvomero mkoani Morogoro Bwa.Thomas Kakema alipokuwa akimuonesha namna Miundombinu ya Skimu za Umwagiliaji zilivyoboreshwa katika shamba hilo la Ushirika.
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live




Latest Images