Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

RC HOMERA AZINDUA MRADI WA MAJI CHAMALENDI, KATAVI.

0
0
 Katika kutekeleza ilani ya CCM ya 2015/2020 ibara ya 53,54,55 na vifungu vyake..

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera tarehe 11.07.2019 amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Chamalendi kata ya Chamalendi Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe wilayani Mlele. 

Mradi huo wenye thamani ya Tsh 402,600,000/= umeshuhudiwa na mamia ya wananchi . Mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 10,000 Katika kata hiyo ya chamalendi.

Ikumbukwe kuwa, lengo la serikali inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni kufikisha maji mpaka kijiji cha mwamapuli na vijiji vya jirani.

Hata hivyo mkuu wa mkoa Mhe. Homera aliwaomba wananchi wa Kijiji cha Chamalendi na kata hiyo kwa ujumla kuendelea kumuombea Raisi Wetu awe na afya njema aendelee kuwatumikia vyema watanzania na wanakatavi wote kwa ujumla. 

Pamoja na hayo, RC Homera amempongeza waziri wa Maji Prof Makame Mnyaa Mbarawa kwa usimamizi wa karibu wa miradi ya maji mkoani Katavi na kupelekea kutekelezwa kwa asilimia zaidi ya 99%, hivyo amewaomba wananchi waendelee kumwombea afya njema Mhe Mbarawa pia.

Mwisho, Mkuu wa wilaya hiyo ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda amewataka wananchi hao kuutunza Mradi huo kwa kutumia vyema fedha za michango ya watumia maji ili mabomba yakiharibika waweze kukarabati na kuongeza vioski vingine vya kuchotea maji kutoka 20 na kuongeza vingine zaidi.

SERIKALI KUOKOA BILIONI 25 KIGOMA ZA KUZALISHA UMEME

0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,( katikati) akiwapa maelekezo wasimamizi wa mitambo ya kufua umeme katika kituo cha kuzalisha a umeme mkoani Kigoma.
Watendaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.( katikati) , alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha kuzalisha umeme, alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,( katikati) akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme mkoani Kigoma. 

……………………. 
Na Zuena Msuya Kigoma, 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema Serikali inatarajia kuokoa takribani shilingi bilioni 25 zinazotumika kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme katika Mkoa wa Kigoma kwa mwaka. 
Akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Kigoma , Julai 12, Mgalu alisema serikali itaokoa fedha hizo, baada ya kuunganisha mkoa huo katika gridi ya taifa na kuacha kutumia umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito. 

Alisema kuwa tayari ujenzi njia ya kusafirisha umeme kuunganisha Mkoa wa Kigoma katika gridi taifa umeanza ambapo itapita katika Wilaya ya Urambo mkoani Tabora,Nguruka, na Kidawe mkoani Kigoma. 
Vilevile aliweka wazi kuwa tayari ujenzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme katika njia hiyo ya kusafirisha umeme umeanza. 

“Serikali imekuwa ikitumia shilingi bilioni 25, kila mwaka kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme Kigoma, lakini imekuwa ikiuuza umeme huo kwa shilingi bilioni 10 tu, hii ni hasara, hivyo tunatekeleza mpango mathubiti wa kumaliza changamoto hii”,alisema Mgalu. 

Mradi huo ni wa kusafirisha umeme wa Kilovolti 132, na unatarajiwa kukamilika mwezi June 2020. Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa huo,Mgalu alisema mkoa huo unahitaji umeme zaidi, ila kwa sasa upo mpango wa kuongeza mitambo ya kufua umeme katika wilaya zenye mahitaji makubwa zaidi ikiwemo Wilaya ya Kasulu. 

Mitambo hiyo ni ile iliyozimwa katika mikoa ambayo ilikuwa inatumia mafuta mazito kufua umeme , ambapo kwa sasa tayari imeunganishwa katika gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito. 

Sambasamba na hilo, alitoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kuwa, ujenzi wa njia ya umeme ukikamilika uende sambasamba na uimarishaji wa upatikanaji wa huduma ya umeme. 

Pia kusitokee changamo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kwa lengo la kuwapatia huduma bora watumiaji katika kuendesha shughuli za uzalishaji. 

“ Tanesco katika mradi huu mjipange,mtimize azma ya serikali ya kuwapatia wananchi umeme wa kutosha na wa uhakika,wananchi wajue kweli wameingia kwenye gridi, siyo wanaingia kwenye gridi umeme unakatika hapana,nawapa tahadhari mapema,” alisisitiza Mgalu. 

Akiuzungumzia fursa za Mkoa wa Kigoma, Mgalu amesema, serikali imedhamiria kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa wenye viwanda na kuwavutia zaidi wawekezaji kwa kuwa mazingira yanaruhusu.

MASAUNI ATEMBELEA KIWANDA CHA GEREZA BUTIMBA JIJINI MWANZA

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa mavazi ya kiraia), akiangalia nguo inayoshonwa na wafungwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara yake alipotembelea Kiwanda cha Gereza Butimba, jijini Mwanza 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia moja ya mashine inayotumika kutengenezea vikoi wakati wa ziara yake alipotembelea Kiwanda cha Gereza Butimba, jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WATUMISHI WA CHALIWASA WAASWA KUWA NA NIDHAMU NA LUGHA RAFIKI KWA WATEJA

0
0

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

BAADHI ya watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze, (CHALIWASA) wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameaswa kuwa na lugha rafiki na nidhamu kwa wateja wanapokwenda kwenye ofisi badala ya kutoa majibu yasiyoridha hali inayosababisha malalamiko .

Kauli ya Mhandisi Raymond imefuatia malalamiko kutoka kwa Abdallah Kipolelo, aliyelalamikia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHALIWASA kutokuwa na lugha nzuri, mara baada ya kupokea taarifa za utendaji wa kazi kutoka kwa wateja.

Mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA Mhandisi Honest Raymond, aliwaeleza watumishi watimize wajibu wa majukumu ya kazi na kufuata maadili ya kazi,wakati wa kikao cha kuwakumbusha majukumu yao kazini.

Kauli ya Mhandisi Raymond imefuatia malalamiko kutoka kwa Abdallah Kipolelo, aliyelalamikia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHALIWASA kutokuwa na lugha nzuri, mara baada ya kupokea taarifa za utendaji wa kazi kutoka kwa wateja.

“Sisi tunafundishwa namna ya kuwahudumia wateja, wao hawana somo kama hilo hivyo unapokutana na mteja anakuwa mkali, wewe jukumu lako ni kumtuliza, wakati mwingine anaweza kufikia hatua ya kukupiga ngumi inabidi mjue namna ya kuishi nao” alisema Mhandisi Raymond.

Kwa upande wake, Kipolelo alisem kuna wakati mtumishi anapokea simu ya upole kutoka kwa mteja akimjulisha kuwepo kwa uvujaji maji eneo alilopo, lakini utakuta kiongozi anajibu simu kwa ukali, hatua aliyodai kama ya udhalilishaji.

Akitoa mada katika kikao hicho, Elizabeth Eusebius ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii aliwaambia watumishi hao kuwa wameamua kutoa mafunzo hayo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendajikazi wa taasisi.

KATIBU MKUU WA TAGCO AWAPONGEZA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI

0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi amewapongeza Maafisa hao kwa kazi nzuri waliyofanya katika kipindi chote cha Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Aliyasema hayo mwishoni mwa maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2019 na kufikia kilele Julai 13, 2019.

“Kipekee kabisa nimefarijika sana kuona kazi kubwa mliyoifanya ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi za umma ama kupitia vyombo vya habari au kwa kuwaelimisha wananchi moja kwa moja.” Alisema Bw. Njaidi wakati alipokuwa akiwatembelea maafisa hao kwenye mabanda waliyokuwa wakiyasimamia katika viwanja hivyo maarufu kama Viwanja vya Sabasaba.

Bw. Njaidi ambaye alikuwa amefuatana na Mjumbe wa TAGCO, Bi. Lulu Mengele alisema. “Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu zinazifanywa na Serikali yao kupitia taasisi mbalimbali za Umma na kwa hili nimeliona mimi binafsi wakati nikiwa hapa lakini pia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.” Alisisitiza.

Alisema wananchi wanayo haki ya kujua jinsi serikali yao ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inavyowatumikia katika Nyanja mbalimbali kama vile huduma za kijamii zikiwemo, Afya, Elimu, Maji, ujenzi wa miundombinu ambao ndio unaotupeleka kwenye nchi ya uchumi wa kati.

Maonesho ya mwaka huu yalibeba kauli mbiu isemayo “"Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi, (wapili kushoto), akiwa na Meneja Msaidizi Uhusiano na Itigfaki, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina (watatu kushoto), Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (wane kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT. Bw. Lwaga Mwambande (wakwanza kushoto), wakati alipowatembelea kwenye banda la BoT, Mwishoni mwa maonesho hayo Julai 13, 2019.
Bw. Njaidi alizungumza na Afisa Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Luhende Singu, alipomtembela kwenye banda la NHIF Mwishoni mwa maonesho hayo.
Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (kulia), akizungumza na Bw.Luhende Singu, Afisa Mawasiliano NHIF.
Bw. Njaidi akisalimiana na fisa Mwandamizi wa Masiko na Uhusiano PSPTB, Bi. Shamim Ally Mdee huku Bi. Lulu Mengele akishuhudia.

LUGOLA AAGIZA POLISI KUWASAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO KUTEKWA, KUPOTEA KWA WATU NCHINI

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, leo, katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi hao pamoja na kujadili miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo. Pia Waziri Lugola alilitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafunguliwa mashtaka wanaosambaza taarifa za uongo, na za kutengeneza matukio ya utekaji na kupotea watu ambayo yanachafua taswira ya Serikali. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akiandika swali la Mkazi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Mnyaga Semba, alipokuwa anamuuliza Waziri kuhusu matukio ya kupotea na kutekwa watu nchini. Waziri Lugola ambaye alifanya Mkutano wa hadhara katika Mji huo, kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi hao pamoja na kujadili miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo. Lugola alilitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafunguliwa mashtaka wanaosambaza taarifa za uongo, na za kutengeneza matukio ya utekaji na kupotea watu ambayo yanachafua taswira ya Serikali. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, leo, katika Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi hao pamoja na kujadili miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo. Pia Waziri Lugola alilitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafunguliwa mashtaka wanaosambaza taarifa za uongo, na za kutengeneza matukio ya utekaji na kupotea watu ambayo yanachafua taswira ya Serikali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
………………….. 

Na Mwandishi Wetu, Mwibara (MOHA) .

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafunguliwa mashtaka wanaosambaza taarifa za uongo, ambazo zinatengenezwa kuhusu matukio ya utekaji na kupotea watu wakiwa na lengo la kuichafua taswira ya Serikali. 

Lugola amesema baadhi ya watu hao ambao wana nia mbaya ya nchi, wanakaa mitandaoni kuanzia asubuhi hadi jioni wakizusha matukio hayo machafu wakiwa na lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa kuichonganisha Serikali Rais Dkt. John Magufuli na wananchi wake, ambayo inaendelea kufanya kazi nzuri kwa kuiletea nchi maendeleo kwa kasi zaidi. 

Waziri Lugola ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alipokuwa anajibu maswali mbalimbali ya wananchi wa Mji Mdogo wa Kisorya, Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo mmoja wa wananchi hao alimuuliza Waziri huyo kuhusu Wizara yake imejipangaje kuyasambaratisha matukio ya utekaji, kupotea watu hususani tukio la kupotea kwa mwandishi wa habari. 

“Lazima tuwe na uchungu na taifa hili, taarifa hizi zinazoripotiwa na watu kupotea ama kutekwa zipo katika makundi mawili, moja ni taarifa za uongo, za kutengeneza, wakiwa na lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa, wakiropoka hovyo, na miongoni mwa watu hao wanaodaiwa kutekwa ama kupotea, wengine tumewabaini wanajiteka wenyewe, wanajipoteza wenyewe, na kuna wengine wameshafikishwa mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo kuwa wametekwa, au kupotea,” alisema Lugola na kuongeza; 
“Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kuna watu wanatunga matukio ya uongo, wanatengeneza matukio ya kutekwa na kupotea, ndugu zangu Watanzania, taarifa hizi zinaweza kuigawa taifa, kusababisha machafuko na kusababisha taharuki katika jamii.” 

Lugola pia amesema, kuna baadhi ya taarifa za kweli na Serikali inakubali yapo matukio ya mtu kuweza kupotea au kutekwa, na hata kutoonekana katika familia yake, hiyo haipingwi na Serikali inakubali yapo, lakini pia wapo ambao wanakua kweli wamepotea ama kutekwa, serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Polisi, limekua likiendelea kuwatafuta watu hao, na wakati linapoendelea kuwatafuta Jeshi linahitaji pia taarifa za wananchi kuwezesha kuwapata watu hao. 

“Ndugu wananchi, pia kuna taarifa za upotoshaji kwa watu wanaodaiwa kupotea au kutekwa kweli, lakini wengine wanasambaza taarifa za uongo, tumekuwa tukishuhudia katika baadhi ya migodi ya madini, wakitatafuta utajiri, lakini majumbani kwao walishafanya mpaka matanga wakiamini ndugu yao alishafiriki kwa kutekwa au kupotea, kumbe anatafuta utajiri machimboni,” alisema Lugola. 

Alisema Serikali yoyote duniani ambayo imechukua dhamana ya kuwalinda wananchi wake halafu Serikali hiyo hiyo igeuke kuwateka na kuwaua, Serikali ya namna hiyo haipo duniani. 

“Naelekeza Jeshi la Polisi, kwa wale ambao wanatunga maneno ya uongo na kuchonganisha Serikali na wananchi, muwasake popote walipo, muwakamate na muwafikishe katika vyombo vya sheria,” alisema Lugola. 
Lugola alijibu swali hilo la kuhusu utekaji na upoteaji wa watu baada ya Mkazi wa Kisorya, Mnyaga Semba alipokuwa anataka kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na matukio hayo. 

“Mbunge wangu, wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, nataka nijue kundi linaloteka watu, kushambulia watu, na pia jambo hili tena limezuka juzi Waziri wetu wa Mambo ya Nje alipokuwa anahojiwa tukasikia jambo la mwandishi wa habari, Azory mara kazikwa mara hivi, naomba kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na jambo hili?,” alisema Semba. 

Aidha, Lugola alizungumzia kuhusu uhalifu katika ziwa Victoria, ambapo wananchi wananyang’anywa mashine, nyavu na samaki na wahalifu hao, kuwasababnishia wananchi umaskini, alilitaka Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu hao kwa kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo hayo ya ziwa kwa lengo la kudhibiti uhalifu huo. 

Pia Waziri huyo, alilitaka Jeshi hilo kutowasumbua waendesha bodaboda kwa kuwakamata hovyo barabarani na bodaboda hizo kuzihifadhi vituo vya polisi huku wamiliki wa vyombo hivyo wakiteseka kuzipata. “Bodaboda akifanya makosa mpigeni faini, na apewe muda wa siku saba kulipa faini hiyo kama inavyokua katika faini za magari. Na nilishasema, bodaboda ambazo zinapaswa kuwepo kituoni ni za aina tatu tuu, ambazo zilizoshiriki uhalifu, zilizookotwa na zilizopata ajali, ndizo nilizoagiza ziwepo kituoni,” alisema Lugola.

ZIARA YA MAFUNZO 5S-KAIZEN KWA WAGENI KUTOKA WIZARA YA AFYA NA WATUMISHI YA BANGLADESH

0
0
Muuguzi Mkuu – Hospital ya Rufaa ya Mkoa- Amana,Beauty Mwambebule akitoa maelezo kwa wageni kutoka nchi ya Bangladesh namna mfumo wa KAIZEN unavyofanya kazi katika Hospital hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
Mratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa kutoka Wizara ya Afya -Idara ya Tiba -Kitengo cha Uratibu wa Hospitali za Rufaa za Mikoa,Dkt. Angelina Clarisa Sijaona (kushoto) akiwa na wageni kutoka nchi ya Bangladesh akiwaonesha mambo mbalimbali yanayo tumika kwenye mfumo wa KAIZEN katika Hospital Amana jijini Dar es Salaam. 
Wangeni kutoka Bangladesh wakiwa katika Hospital ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja ya maofisa kutoka wizara ya afya,hospitali ya rufaa ya mkoa Amana pamoja na wageni kutoka Bangladesh baada ya kutembelea hospitali ya Amana 
………………….. 

Na.WAMJW,Dsm
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mradi wa Kuimarisha Hospitali za Rufaa za Mikoa (RRHMP) katika kuendelea kuziwezesha Hospitali za Rufaa za Mikoa ilipanga kukaribisha wageni kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika ili kubadilishana uwezo katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini. 

Kulingana na mpango kazi wa mwaka huu, Mradi ukishirikiana na Wizara ya Afya ulitarajia kupokea wageni kutoka Wizara ya Afya na watumishi wa sekta hiyo kutoka nchini Ghana (7) na Bangladesh (7) kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM pamoja na wawakilishi wa JICA wawili kutoka kila nchi. Pamoja na hao, tulitegemea kupokea watumishi wa Afya 14 kutoka nchi za kiafrika zikiwemo Uganda, Kenya, Malawi, Liberia, Siera Leoni, Sudan, Zambia, Zimbabwe na Benin. 

Tayari wageni wote hawa waliishafika na kupata mafunzo kutoka haya. 
Wiki hii, tumewapokea wageni kutoka Katika Wizara ya Afya na watumishi 7 wa sekta na wawakilishi wawili wa JICA-Bangladesh. Wageni hawa watakuwepo hapa nchini kwa wiki moja Katika kipindi hicho watapata mafunzo ya KAIZEN na leo wametembelea Hospitali za Rufaa ya Mkoa Amana na kesho wanategemewa kutembelea Hospitali za Taifa Muhimbili. 

Lengo la ziara hii ni kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa 5S-KAIZEN-TQM katika hospitali zetu kwa ajili ya kujifunza na kuiga mazuri ya kujifunza watakaporejea nchini kwao. Aidha, Timu zetu zinategemewa kupata nafasi ya kupata uzoefu kutoka kwa nchi zinazotutembelea. 

Falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inalenga kuboresha mazingira ya kutoa huduma za afya na kukidhi mahitaji ya wateja wetu, wale wa ndani na wa nje. 

Kwa ujumla wake, falsafa ya 5S-KAIZEN-TQM hii inarahisha kazi, inahakikisha usalama kwa wateja wa ndani na nje na inapunguza upotevu wa rasilimali, napunguza makosa na inapunguza gharama za uendeshaji. 
Kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa ambayo wanaitimia falsafa hii wameweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora, kuongeza katika mapato na wafanyakazi kufurahia mazingira yao ya kazi. 

Ni falsafa inayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali pamoja na viwandani.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANA CCM WILAYA ZA KIGOMA MJINI NA KIGOMA VIJIJINI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM wa wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma, Julai 14, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Serukamba wakati aliopowasili kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma kuzungumza na Viongozi wa CCM kutoka wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini, Juni 14, 2019. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako.
Baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya za Kigoma Mjini na Kigoma Vijijini wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma, Julai 14, 2019.

RAIA wa Burundi waishtaki nchi yao mahakama ya Afrika mashariki.

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

RAIA 19 wa Nchi ya Burundi wamefungua kesi katika mahakama ya Afrika mashariki dhidi ya serikali yao kupinga vitendo vya unyanyasaji wa haki za binadamu unaoendelea Nchini humo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mara baada ya kusajiriwa kwa kesi yao, baadhi ya mawakili kutoka chama cha wanasheria Afrika (PALU) wanaosimamia kesi hiyo,Evelyn Chijorira kutoka nchini Zimbabwe, alisema kuwa, wananchi hao kutoka Taifa la Burundi wamefungua shauri la haki ya Ardhi lenye namba 16/2019 katika mahakama hiyo.

Wakili huyo alisema kuwa, mwaka jana serikali ya Burundi iliwashtaki mahakamani wananchi wake wapatao 32 waliokuwa wakipinga Rais wa Burundi kushika madaraka kwa awamu ya tatu , lakini cha kushangaza kabla ya kesi hiyo kumalizika walisikia Ardhi yao,Nyumba zimetaifishwa na serikali ya Burundi.

"Tumekuja hapa katika mahakama ya Afrika mashariki kuwakilisha wananchi 19 wa Burundi kufungua kesi dhidi ya serikali yao wakilalamikia manyanyaso na kupokonywa Ardhi na Nyumba zao na serikali ya Burundi" Alisema

Aliongeza kuwa, mwaka jana kulitokea vurugu kwa wananchi kupinga rais wa nchi hiyo kujiongezea muda wa madaraka kwa awamu ya tatu jambo lililopelekea baashi yao kukamatwa na wengine kuikimbia nchi yao na kukimbilia mafichoni katika nchi mbalimbali.

Hata hivyo wakiwa nchi za Ng'ambo walisikia Ardhi zao na Nyumba vimechukuliwa na serikali ya Burundi jambo ambalo limewalazimu kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kudai haki zao na kupinga manyanyaso yanayotokea dhidi ya raia na nchi ya Burundi ikiweni kunyimwa Uhuru wa kujieleza, hali ambayo imechangia baadhi yao kuikimbia nchi yao.

"Ktokana na unyanyasaji huo kati ya wananchi hao 32 wananchi 19 wamekuja kufungua kesi katika mahakama hii ili kudai haki zao za kunyanganywa ardhi, nyumba na kutopewa Uhuru wa kujieleza. "alisema Wakili huyo.

Naye Wakili mwingine,anayewatetea walalamikaji hao Gustave Niyonzima kutoka Burundi alisema kuwa, yeye na mawakili wenzake wanne ambao wanawatetea wananchi hao 19 wa Burundi wamefungua kesi hiyo wakiwa na matumaini ya kupata haki kwa wananchi hao.

Alisema kuwa, wanaiomba mahakama hiyo iweze kusaidia watu wa Burundi wapate haki zao kutokana na kunyanganywa ardhi yao, nyumba na hata kunyimwa Uhuru wa kuzungumza wakati hiyo ni haki ya kila mmoja.

"Tunamatumaini makubwa na hii mahakama kuwa haki itatendeka ili raia wa Burundi waweze kupata amani na uhuru na hatimaye kuweza kumiliki mali zao. "alisema Wakili Niyonzima.

Kwa mujibu wa Mawakili hao kesi hiyo itapangiwa siku rasimi ya kuanza kusikilizwa baada ya upande wa serikali ya Burundi kujulishwa.

MBOZI SASA YAKUNA VICHWA JUU YA NAMNA YA KUPUNGUZA TAKA MJINI

0
0
Mwananchi huyu akiendesha shughuli za uchimbaji kokoto kwenye Mlima Mbozi, eneo linalopendekezwa kuwekwa Dampo la taka zinazozalishwa katika Miji ya Vwawa na Mlowo.
Bwawa la Mbozi lililopo katikati ya mwamba wa jiwe linaloendelea kutumika kutengeneza kokote kwaajili ya miradi ya Barabara kwenye mkoa wa Songwe. Wananchi wanatumia fursa ya bwawa hilo kufanya shughuli za uvuvi na unyweshaji wa mifugo.
Timu ya wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakijadiliana jambo katika moja ya maeneo yanayopendekezwa kuwa Dampo katika Halmashauri hiyo.
Wataalamu wa Halmashauri ya Mbozi wakiangalia bwawa la maji ya mvua pamoja na chemichemi linalotokana na kuchimbwa kwa tabaka la juu la mwamba wa kokoto ambao ulitumika kwenye ujenzi wa barabara miaka ya 80. 
…………………… 

Na Danny Tweve Mbozi .

Timu ya wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi wamefanya ukaguzi wa maeneo kadhaa kwaajili ili kutambua eneo linalofaa kuhamishia dampo la taka baada ya lililokuwepo kuwa eneo la mji kutokana na kasi ya ukuaji wa mji wa Vwawa inayotokana na kuwepo kwa makao makuu ya mkoa. 

Maeneo kadhaa yaliyobainishwa kwenye mapendekezo yametembelewa na wataalamu na hatimaye mapendekezo yake kuwasilishwa kwenye mamlaka za juu za Halmashauri kwa maamuzi. 

Miongoni mwa maeneo hayo ni eneo la mlima Mbozi na Karasha ambayo kwa pamoja yalibainishwa na timu hiyo huku yakitolewa ushauri kulingana na athari za maingira zilizopo kwa kila eneo. Kasi ya ukuaji miji inayoenda sambamba na uzalishaji taka mijini ni moja ya changamoto kubwa zinazozikabili mamlaka za serikali za mitaa ambazo ndiyo zinazopanga maeneo hayo. 

Hata hivyo changamoto ya vifaa vya usafirishaji taka na mitambo ya kuhifadhia, ni miongoni mwa maeneo ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi hasa hapa nchini licha ya maeneo machache ya miji kufanikiwa kununua vifaa hivyo. 

Mbozi ni moja ya maeneo yenye uhaba wa magari ya kuzolea taka na hata vifaa vya kuhifadhia na katika kutambua hilo. “mkakati wa halmashauri ni kutafuta wadau itakaoshirikiana nao hasa katika kuzirejesha taka kwaajili ya matumizi (recycling and re-use) ambapo baadhi ya bidhaa kama mbolea, mazuria na mapambo yanaweza kutengezwa kupitia taka” anadokeza mkurugenzi wake Bi Halima Mpita.

MBUNGE VITI MAALUM FAHARIA ATOA VIFAA VYA SH.MILIONI 15

0
0
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari (kulia),akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Magomeni Ndugu Khadija Rajab Pazi (kushoto). MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Shomari Khamis akimkabidhi Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee Kiti Kimoja na Meza Moja vya Ofisi.BAADHI ya Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini, kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja.MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja Bi.Ghanima Sheha akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Mkoa huo,huko katika Ukumbi wa Mkoa wa Mjini ulioopo Amani Unguja. 

………………….. 
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari,amekabidhi Vifaa mbali mbali vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 15 kwa Majimbo yote ya UWT ndani ya Mkoa huo. 
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti 451,Meza Moja ya Ofisi na Mashine Moja ya kutengenezea Chaki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkoa juhudi za Ujasiliamali za Akina Mama wa Mkoa huo. 
Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo Mbunge huyo Mhe.Faharia amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020. 
Mhe.Faharia ameeleza kuwa akina Mama wa UWT ndani ya Mkoa huo pamoja na majukumu ya kisiasa waliyokuwa nayo bado wanatakiwa kujiajiri wenyewe kupitia ujasiriamali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia katika harakati hizo za kujiajiri wenyewe. 
Pamoja na hayo alitoa Wito kwa Wanawake wa rika mbali mbali ndani ya Mkoa wa Mjini kushiriki kaiunga Mkoa CCM ili ishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020. 
Katika hafla hiyo Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo ambao ni Mhe.Mgeni Hassan Juma aliahidi kutoa Mashine mbili za Photocopy kwa UWT Wilaya ya Amani na Mjini huku Mhe.Saada Ramadhan amekabidhi Mifuko Mitano ya Jipusamu kwa ajili ya kutengenezea chaki na kuahidi shilingi Milioni Moja kwa kila jimbo la UWT. 
Wakizungumza kwa wakati tofauti Makatibu wa UWT wa Majimbo yote yaliyomo katika Mkoa huo, wameahidi Vifaa hivyo kuvitunza na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi yaliyokusudiwa. 
Awali akifungua Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndugu Ghanima Sheha,amesema Kikao hicho kitajadili masuala mbali mbali ya kiutendaji na kutoa maelekezo ya kiutendaji juu ya ufanikishaji wa majukumu mbali mbali ya UWT na CCM kwa ujumla.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI LUSHOTO MKOANI TANGA

WAKONGWE WA UTANGAZAJI USO KWA USO UZINDUZI WA REDIO KICHEKO MJINI MOSHI

0
0
Dk. Heavenlight Kavishe, Mmiliki wa Redio Kicheko Live akizungumza jambo na kuwakaribisha wageni waalikwa malimbali waliofika kwenye hafla hiyo inayoendelea hivi sasa mjini humo,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mhe.Anna Mghwira
 HOMECOMING : Wakongwe wa utangazaji wamekutana kwenye uzinduzi wa Redio Kicheko, katika Manispaa ya Moshi. Kutoka kushoto ni Jacob Tesha, mtangazaji wa zamani wa RTD, Joseph Mapunda aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya TSN, inayochapisha Magazeti ya Serikali ya Daily News/Sunday News, Salim Mbonde, mtangazaji wa zamani wa RTD, Thadayo Ringo, mtangazaji wa zamani wa Radio Habari Njema ya Moshi ambaye ni afisa mwandamizi wa TCRA, na Abdul Ngarawa, mtangazaji wa zamani wa RTD. Radio hii mpya inamilikiwa na mfanyabiashara wa mjini Moshi, Dk. Heavenlight Kavishe (PhD) - Industrial Engineering. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira, anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU UWEPO WA DAWA MPYA YA ASILI INAYOTIBU SARATANI YA TEZI DUME

BENKI YA CRDB KUWANEEMESHA WAJASIRIAMALI WAMACHINGA

0
0

Wajasiriamali Wamachinga sasa kuanza kunufaika na mikopo ya kidijitali kutoka Benki ya CRDB kufuatia urasimishwaji wa kundi hilo uliofanywa na Serikali nchi nzima kupitia vitambulisho vya ujasirimali.

Akizungumza kuhusiana na fursa hiyo wakati wa Semina ya Wajasiriamali kwa Mkoa wa Morogoro iliyofunguliwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe Steven, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema huduma hiyo ya mikopo ambayo itapatikana kupitia mfumo wa SimAccount inalenga katika kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo nchini kukuza biashara zao.

“Mikopo hii itakuwa ikipatikana kwa mfumo wa kidijitali kupitia huduma yetu ya SimAccount, hii itawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka zaidi kupitia simu zao za mkononi bila kutembelea tawini. Tunafanya hivi tukijua uhitaji wa mikopo kwa kundi hili la wateja ni mkubwa na mara nyingi wamekuwa na uhitaji wa haraka,” alisema Ndugu Nsekela.

Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imekuwa ikitoa kipaumbele kwa kundi la wajasiriamali katika mpango mkakati wake wa biashara ambapo benki imekuwa ikibuni huduma na bidhaa maalum kwa ajili ya kundi hilo ikiwemo mikopo. “Kwa mwaka jana pekee tumefanikiwa kutoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 421.58 kwa wateja wetu wajasiriamali”, aliongezea Ndugu Nsekela.

Dkt. Kebwe ameipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo akisema hatua hiyo itasaidia kutimiza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwawezesha wajasiriamali wamachinga nchini kupiga hatua katika biashara zao ikiwa ni mkakati wa kuwainua kiuchumi kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati.

Dkt. Kebwe alitumia fursa hiyo pia kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya kilimo nchini kupitia bidhaa yake ya FahariKilimo.

Dkt. Kebwe aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara waliohudhuria katika semina hiyo kuchangamkia fursa ya mikopo ya kilimo inayotolewa na Benki ya CRDB, huku akieleza kuwa mkoa wa Morogoro unafursa kubwa ya kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo hususani kilimo cha miwa, mpunga, pamba, korosho na kahawa.

Mbali ya kupata mafunzo juu ya fursa mbalimbali za ukuzaji biashara kupitia huduma na bidhaa mbalimbali za Benki ya CRDB, Wajasiriamali hao pia walipata fursa ya kutoa maoni juu ya uboreshwaji wa huduma.

Hivi karibuni Benki ya CRDB imetoa kiasi cha dola za kimarekani 60,000 kudhamini tafiti ya kampuni bora 100 ikijikita katika kipengele cha wajasirimali ambacho ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kuchochea makampuni hayo kufanya vizuri zaidi.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akisaliamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019. Katikati ni  Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga. 
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipoingia katika ukumbi tayari kwa Semina ya Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, katika hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Mkuuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven akitoa hotuba yake wakati akifungua Semina maalum kwa Wajasiriamali iliyoandaliwa na Benki ya CRDB, , katika ukumbi wa hoteli ya Nasheera, Mkoani Morogoro, Julai 13, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro, Julai 13, 2019. 
Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Pascal Kianga akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro juu ya furs mbalimbali zinazotolewa na bench hiyo kwa wafanyabiashara katika Semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Nashera,


























































WATAALAM WA MADINI YA DHAHABU NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR) WAKUTANA ARUSHA

0
0
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wamekutana Jijini Arusha ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu madini hayo kwa maslahi mapana ya nchi hizo.

Mkutano huo wa siku mbili ulifunguliwa jana Machi 27, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambapo alisisitiza kuwa Nchi Wanachama wa ICGLR wanao wajibu wa pamoja kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa manufaa ya wanachama wote.

Gambo alizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo ni uvunaji haramu wa madini, utoroshwaji wa madini, uharibifu wa mazingira, ukosefu wa teknolojia na baadhi ya Nchi kuwa na changamoto za Kiusalama.

Hata hivyo alisema changamoto hizo zisiwe sababu ya kurudi nyuma badala yake juhudi za pamoja, mshikamano wa dhati unahitajika ili kukabiliana na changamoto hizo na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa maslahi mapana ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Nchi Wanachama ni Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo (Kinshasa), Congo (Brazzaville), Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan Kaskazini, Uganda na Zambia.

Tanzania imekuwa Mwanachama rasmi wa ICGLR Mwaka 2008 na tangu wakati huo imeendelea kutekeleza malengo ya mpango wa ICGLR ili kufanikisha udhibiti wa uvunaji haramu wa madini na kuhakikisha manufaa ya pamoja ya rasilimali husika yanapatikana.
Baadhi ya Waratibu wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Demokrasia na Utawala Bora- ICGLR, Balozi Ambeyi Ligabo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkutano, Service Julie kutoka Congo
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano
Mwenyekiti wa mkutano, Service Julie kutoka Congo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.
Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma akimwakilisha Kamishna wa Madini, Prof. Shukran Manya na Mhandisi Fadhili Kitivai (kutoka Wizara ya Madini).
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha.

Tupate wasaa wa kumsikiliza mzalendo, Kanali Mstaafu Haruna Ramadhani

NEMC LATOA UFAFANUZI KUHUSU KELELE CHAFUZI

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ZILIZOANDIKWA KWENYE MAGAZETI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU UWEPO WA DAWA MPYA YA ASILI INAYOTIBU SARATANI YA TEZI DUME

0
0
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ilianzishwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 23 ya mwaka 1979. NIMR ni taasisi chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Taasisi hii pamoja na kufanya utafiti, inaratibu, inakuza na kusimamia tafiti za afya zinazofanyika nchini na kukuza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo.

NIMR ina idara ya tafiti za tiba asili ambayo jukumu lake ni kufanya utafiti juu ya dawa za miti-shamba, ambazo nyingine zimekuwa zinatumika miaka mingi na bibi na babu zetu. Idara ya tafiti ya dawa asilia mwaka huu iliiwakilisha NIMR kwenye maonesho ya Sabasaba katika banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Lengo la kushiriki katika maonesho haya ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya zinazofanyika NIMR. Waandishi wa habari walimhoji mtafiti wa NIMR katika banda la COSTECH na wameripoti kwamba NIMR imegundua dawa ya kutibu saratani ya tezi dume. Kutokana na uzito wa suala hili na kuzingatia mateso ya wagonjwa wenye tezi dume NIMR ingependa kufafanua na kurekebisha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Ni kweli kwamba moja ya dawa za miti-shamba ambazo NIMR imetengeneza imeonesha dalili ya kupunguza uvimbe kwa wagonjwa wenye tatizo la kuvimba tezi dume. Dawa hii haijaonesha uwezo wa kutibu saratani ya tezi dume. Dawa hii bado iko katika hatua ya uchunguzi wa kitafiti. Lengo letu la kushiriki katika maonesho ya Sabasaba lilikuwa ni kuonesha ubunifu katika tafiti za afya.

Baadaye kama tafiti hizo zitakuwa na matokeo mazuri zinaweza kutumika baada ya kufuata hatua za kisheria za usajili. Tunaomba radhi kwa wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na ripoti hiyo iliyokuwa inasambaa.

Taarifa imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
3 Barabara ya Barack Obama
S.L.P. 9653, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2121400; Barua pepe: dg_office@nimr.or.tz

SERIKALI,BUZWAGI KUSHIRIKIANA KULINDA ULINZI NA USALAMA KAHAMA

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza wakati   Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akipokea zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu kutoka kw Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo  wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akionesha zawadi ya kitabu cha kuhifadhia kumbukumbu alichopokea  kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ,Arthur Mgongo(kushoto),  wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi , Arthur Mgongo (kulia) wakati  Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kahama ilipotembelea mgodi huo  ikiwa ni ziara ya kuimarisha Ulinzi katika wilaya hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya Nchi
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images